You are on page 1of 4

Yesu si Mungu, Paulo ana kesi ya kujibu

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Dotto C. Rangimoto, Sep 25, 2016.

"Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, MTU ambaye nimewaambia iliyo kweli, niliyoisikia kwa Mungu.
Ibrahimu hakufanya hivyo."

Yohana 8:40

Katika andiko hilo YESU kwa kinywa chake yeye mwenyewe amejiita kuwa ni "MTU". Kama kuna mtu
ana ushahidi wowote katika biblia YESU akijiita MUNGU, basi nami hapo nitaamini kuwa YESU Mungu.

Hata hivyo, mnaweza kusema pia, kuwa YESU alikuwa Mungu na Pia alikuwa mtu. Hata hivyo tukitazama
sifa mbalimbali za mungu kama zilivyo tajwa au ainishwa na biblia, utaona hata kiduchu YESU hana sifa
hizo.

Mathalani.

"Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo
amenena, hatalifikiliza.."

Hesabu 23:19

Tumeona katika Yohana 8:40 Yesu akijiita Mtu, na hapa katika hesabu tunaambiwa Mungu si mtu, sasa
wewe unayemuita Yesu Mungu umepata wapi?

NANI KAFUNDISHA YESU NI MUNGU?

"tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi
wetu; "

Tito 2:13

Hayo maneno katika kitabu cha Tito, kimsingi ni barua ya kimisionari aliyo andika Paulo kwa watu wa
Tito, kama tuonavyo katika barua hiyo, pamoja na mambo mengine Paulo anawaambia watu wa Tito
kuwa Yesu ni Mungu Mkuu, maneno haya ya Paulo yanakwenda kinyume kabisa na maneno ga Yesu
mwenyewe aliyo yasema katika Yohana 8:40 lakini kinyume kabisa na mafundisho ya kinabii kutoka
katika kitabu cha Hesabu 23:19.

YESU ANASEMAJE KUHUSU PAULO?


Awali ya yote Paulo hakuwahi kuwa mwanafunzi wa Yesu na hakuwahi kumuona Yesu Kristo. Yesu kabla
hajapaa kwenda mbinguni aliwahi kusema maneno haya.

"Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa. Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja
atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada. Na hayo watawatenda kwa sababu
hawakumjua Baba wala mimi"

Yohana 16:1-3

Hapa Yesu anatabiri kuwa wanafunzi wake watakuja kuuliwa, anatabiri wakristo na wafuasi wa kanisa
lake watakuja kuuliwa, na akasisitiza huyo atajaye wauwa wanafunzi wake hamjui yeye wala
Baba(Mungu)

Nani huyo aliyeua wanafunzi wa Yesu? Jawabu ni Sauli ambaye ni Paulo.

"Lakini Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu,
akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii,
waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu."

Matendo 9:1-3

Kwa hivyo Mtu aliyetajwa na Yesu katika injili ya Yohana 16:1-3 kuwa atawaua wanafunzi wa Yesu si
mwingine Paulo, na katika kitabu cha matendo tunaoneshwa ukatili wa Paulo kwa wanafunzi wa Yesu.
Hata hivyo, Bwana Yesu anaendelea na utabiri wake juu ya Paulo katika aya hii.

"Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji
tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo
uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo"

Yohana 8:44

Katika aya hiyo Bwana Yesu anasema huyo Paulo si kwamba ni muuaji tu, lakini pia mtu muongo sana.
Na uongo mkubwa alio ufanya Paulo ni pale aliposema kakutana na Yesu na kisha akajifanya kipofu.

"Hata alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka
mbinguni. Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi? Akasema, U nani
wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe. Lakini simama, uingie mjini, nawe
utaambiwa yakupasayo kutenda"

Matendo 9:3-7

Baaada ya Paulo kuwaua sana wanafunzi wa Yesu na kuwatesa sana ili waache mafunzo ya Yesu, lakini
wanafunzi wa Yesu waligoma na walikataa katakata kuachana na mafunzo Yasu. Pia naomba mjue,
mafunzo ya Yesu yalikuwa mwiba kwa serikali(Dola ya Rumi) na Paulo alikuwa anatumiwa na serikali
katika kuhakikisha wanafunzi wa Yesu wanaachana na ukristo/uyaudi.

Pamoja na juhudi hizo za Paulo lakini alishindwa, hivyo njia aliyo amua kuitumia si nyingine bali ni
kujiunga na wanafunzi wa kristo. Na ili aaminike ndipo hapo alipotengeneza stori ya kumuona Yesu na
maagizo ya upofu, lakini kubwa zaidi alimnunua Anania ili msaidie kufanikisha lengo lake. Kwa kumtumia
Anania na kwa kudanganya kwake kuwa kamuona Yesu, wanafunzi wa Yesu walimkubali.

Na hapo ndipo Paulo alipoanza kuyachakua mafunzo ya Yesu, na ndio maana ukristo wa sasa si ule alio
ufundisha Yesu.

YESU NA MFARISAYO.

"Ewe FARISAYO KIPOFU, safisha kwanza ndani ya kikombe, ili nje yake nayo ipate kuwa safi. Ole wenu,
waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa
nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote."

Mathayo 26:23

Paulo msomi mkubwa alikuwa Farisayo, lakini Yesu alisema nini juu mafarisayo? Kama tulivyo ona, Yesu
anawaona mafarisayo kama vipofu, lakini kubwa katika andiko hili Yesu anamtabiri pia Paulo na maigizo
yake ya upofu.

"Paulo alipotambua ya kuwa sehemu moja ni Masadukayo, na sehemu ya pili ni Mafarisayo, akapaza
sauti yake katika ile baraza, Ndugu zangu, mimi ni Farisayo mwana wa Farisayo; mimi ninahukumiwa
kwa ajili ya tumaini la ufufuo wa wafu"

Matendo 23:6

Kwanza Paulo amekiri kwa kinywa chake kuwa yeye ni farisayo. Lakini hiyo haitoshi Paulo alijitia upofu
aso kuwa nao.

"Sauli akainuka katika nchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; wakamshika mkono
wakamleta mpaka Dameski. Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi."

Matendo 9:8-9

Katika aya hizi tunaona kuwa Paulo amekiri kuwa Farisayo lakini pia tunaona Paul yuko katika maigizo ya
upofu. Yote haya mawili yanakamilisha unabii wa Yesu pale aliposema

"Ewe farisayo kipofu.."

Mathayo 26:23

Katika aya hizo inatajwa sifa kuu au tabia kubwa ya Mafarisayo, na ambayo imethibiti(ilitimia) kwa
Paulo. Sifa hiyo si nyingine bali UNAFIKI.

Paulo alikuwa mnafiki, yaani alijifanya muumini wa mafundisho Yesu ili mradi apate kuwapotosha
wanafunzi wa Yesu, na hili kwakweli kafanikiwa sababu hakuna hata kanisa moja ambalo linafuata
mafunzo ya asili ya Yesu. Kila kanisa lina kituko chake.

MWISHO.

Kwa kifupi huku nikizingatia maelezo yangu yote ya huko juu, kuwa YESU SI MUNGU, lakini
hakumaanishi kuwa hakuna wanao muita au wanao amini Yesu Mungu. La kuzingatia kama tukiambiwa
kauli ipi ya kushika kati ya YESU mwenyewe na ya Paulo kwa vyovyote vile tunatakiwa kushika kauli ya
Yesu.

Kauli zote za Paulo ambazo hazipingani na za Yesu, kauli hizo tutazifuata, lakini kauli yoyote ya Paulo
inayo pingana na Yesu, kauli ya Paulo itapuuzwa na kuanguka, alafu watu wote wanatakiwa wafuate
kauli ya Yesu.

Hakuna kauli ya Yesu anayo alijiita Mungu, lakini zipo nyingi akijiita Mtu au mwana wa adamu. Na siku
zote alijitafautisha na Mungu. Yesu anakata mzizi wa fitina katika andiko hili.

"Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma"
Yohana 17:3

Nasema YESU SI MUNGU, na Paulo ana kesi ya kujibu kwa kudanganya ulimwengu, na kwa kuharibu
mafundisho ya Yesu na kubwa zaidi kwa kuwatesa na kuwaua wanafunzi wa Yesu na wafuasi wake.

Katika kuendeleza urongo wa Paulo, watu wameambukizwa urongo, sasa wanatusambazia picha na
sanamu za wacheza sinema na kisha wanataka tuziheshimu kama Yesu, kweli watu wanaangamia kwa
kukosa maarifa.

TUJADILI!

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)


Call/whatspp 0622845394 Morogoro.

You might also like