You are on page 1of 4

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
OFISI YA MKUU WA MKOA ARUSHA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo katika
utaratibu wake aliojiwekea wakutembelea Wilaya zote za Mkoa huu
amekamilisha ziara ya kikazi ya SIKU TANO aliyoifanya katika Wilaya ya
Longido kuanzia tarehe 24 -28/10/2016. Lengo ni kujitambulisha kwa
wananchi, kufahamu changamoto na kuzitafutia ufumbuzi, kuona fursa
zilizopo, kushiriki pamoja shughuli za maendeleo na kukagua miradi ya
Maendeleo.
Mhe.Gambo alitembelea Tarafa zote nne za Longido, Enduimet,
Kitumbeine pamoja na Engarenaibor kwenye Kata za GelaiLumbwa,
GelaiMerugoi, Kitumbeine, Engarenaibor, Matale, Tingatinga, Olmolog,
Sinya, Namanga, pamoja na Kata ya Longido. Pia alifanya mikutano ya
hadhara na wananchi wa Vijiji na vitongoji vipatavyo kumi na tano.
Vilevile, Mkuu wa Mkoa alitembelea eneo la mpaka wa Tanzania na Kenya
(Normans Land) na aliweza kukutana na wafanyakazi wa Taasisi za
Serikali zinazotoa huduma eneo la mpakani pamoja na wafanyakazi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Longido.
Kupitia ziara hiyo ya kazi Mhe.Gambo alibaini na kutoa maelekezo katika
maeneo yafuatayo:
i.
Mtandao wa Barabara Barabara ya Esokonoi yenye urefu wa
Km 25 iliyofunguliwa na kujengwa na wananchi kwa kutumia zana
za asili iingizwe kwenye mtandao wa barabara za Halmashauri na
kutengewa Fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi ili kuunga mkono
jitihada za wananchi. Pia aliwajulisha wananchi kuwa barabara ya
Namanga Sinya Elerai imepandishwa hadhi kuwa barabara
ya Mkoa kupitia kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa cha tarehe
22/10/2016; Aliwataka Halmashauri kukamilisha haraka miradi ya
Barabara iliyopo ili kuwaondolea kero wananchi.
ii.

Afya ya Jamii na uboreshaji wa miundombinu ya Afya


Wananchi walilalamikia upungufu wa dawa vituoni pamoja na
1

huduma za afya kupatikana mbali na makazi yao. Rc Gambo


alisema Serikali ya Wilaya lazima ianze ujenzi wa Vituo vya Afya
kwenye Kata za Kitumbeine na Namanga ili kuwasogezea
wananchi huduma na ukizingatia wananchi wa Namanga huenda
kutibiwa Kenya kutokana na kukosekana kwa huduma hii; Ujenzi
wa Kituo cha Afya Namanga ufanyike kwenye eneo ilipokuwa
Kambi ya Mkandarasi Namanga na kwa kuanza nachangia Bati
100 pamoja na mifuko ya saruji 100 nahitaji ujenzi huo uanze
mara moja.
Aliongeza kuwa Idara ya Afya iendelee kutoa elimu na
kuhamasisha wananchi kuendelea kujiunga na mfuko wa Afya ya
Jamii (CHF) ili kupunguza changamoto ya uhaba wa dawa na
watumishi wasio waadilifu waache mara moja tabia ya wizi wa
dawa kwani huleta madhara makubwa kwa wananchi wanyonge.
iii.

Elimu Msingi na Sekondari - Walimu wanaofanya kazi katika


Halmashauri ya Longido walisema wanaidai Serikali zaidi Tsh
Million 250 za malimbikizo yasiyo kuwa ya mishahara,
mishahara ya mwanzo pamoja na nauli. Kutokana na hilo, RC
Gambo aliahidi kufuatilia kwa karibu ili madeni hayo yaweze
kulipwa haraka iwezekanavyo.

iv.

Upatikanaji wa Maji Iliripotiwa kuwa changamoto kubwa kwa


wananchi wa Longido na upatikanaji wa maji. Kutokana na hali
hiyo RC Gambo aliagiza kuletewa taarifa ya miradi ambayo
haijakamilika kutokana na Fedha kutowasilishwa kwa wakati ili
aweze kufuatilia Fedha hizo Wizarani pia alisisitiza mradi mkubwa
wa maji utakaogharimu Bilioni 13 uanze kutekelezwa mara moja.
Mradi huo utaanzia Mto Simba (Siha) hadi vijiji vya
Longido, Ollepes, Orbombo, Engikarate mpaka Ranchi na
ukikamilika upatikanaji wa maji utaongezeka hadi kufikia
asilimia 80.

v.

Nidhamu kwa Watumishi Rc Gambo alisema Nakuagiza


katibu Tawala Mkoa kumuandikia barua Katibu Mkuu Tamisemi ili
awarudishe aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Longido
Bw. Julius Challya na Eng. Edwin Rwezaura waje kujibu
tuhuma za matumizi mabaya ya Fedha za mradi wa maji
uliogharimu zaidi ya Tsh Mil 400.
2

Wafanyakazi wa mpakani acheni kupokea rushwa, inaonekana


vitendo vya rushwa, urasimu na ubadhirifu vimekithiri hapa
Namanga hakika sisi kama Serikali hatutasita kuwachukulia hatua
wale wote watakaobainika kupokea na kutoa rushwa au
kushirikiana na wahalifu kuhujumu mapato ya Serikali kwa namna
yeyote ile tutamshughulikia pasipo kujali nafasi yake.
vi.

Uwekezaji Kutokana na wingi wa mifugo katika Wilaya ya


Longido RC Gambo alishauri Halmashauri kuangalia uwezekano
wa kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda vya Nyama na maziwa
pia Viwanda vya kusaga nafaka ili kusitisha biashara
inayoendelea sasa ya kusafirisha mazao ya nafaka ambapo
inaweza kupelekea baa la njaa kwa wananchi; Uwekezaji huu
utasaidia kuongeza mnyororo wa thamani pamoja na kuongeza
ajira.

vii.

Ukuaji wa mji Namanga Kutokana na ongezeko la Idadi ya


watu kumekuwa na uhitaji mkubwa wa huduma za kijamii katika
eneo la Namanga hivyo Mkuu wa Mkoa ameagiza uongozi wa
Wilaya kupitia madai ya wananchi wake ya kutaka kuanzishwa
kwa Mamlaka ya Mji mdogo katika eneo hilo na kuchukua hatua
stahiki.

viii.

Ajira kwa Vijana Mkuu wa Mkoa aliahidi kutoa boda boda


kumi kwa vijana wanaofanya shughuli hizo katika Wilaya
ya Longido, na kuangalia uwezekano wa kuongeza pikipiki hizo
kwa kadiri atakavyoridhishwa na utendaji kazi wao lengo ni
kuwajengea uwezo na kuinua pato la Vijana. Pia aliwaagiza
Halimashauri kuhakikisha 10% ya mapato yao inawafikia vijana
na kina mama kama Serikali ilivyoelekeza.

ix.

Kuchangia miradi ya Maendeleo Kupitia ziara hiyo Mkuu


wa Mkoa wa Arusha alichangia Mifuko ya saruji 580,
Mabati 856, mbao 466, madawati 100 pamoja na mchango
wa Fedha zaidi ya Tsh Mil 1.5 pia aliungwa mkono na
Umoja wa waendesha Noah za Arusha Namanga kwa
kuchangia mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ukamilishaji wa
ujenzi unaondelea wa madarasa, zahanati, vituo vya afya,
madaraja pamoja na barabara.

Mkuu wa Mkoa alihitimisha ziara yake kwa kuwataka Viongozi na


wataalam kuendelea kujipanga namna gani ya kuwatumikia wananchi
kwa uadilifu na kujitoa ili kupunguza malalamiko.
Hakikisheni mnawatembelea wananchi vijijini, kusikiliza na kujibu hoja,
mtatue changamoto zinazowakabili na kuwafariji katika harakati zao za
kujitafutia kipato na kuleta maendeleo Alisisitiza RC Gambo.
Imetolewa na:

Nteghenjwa Hosseah
Afisa Habari

You might also like