You are on page 1of 1

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Kitalu Na. 8, Mtaa wa Luthuli


S.L.P 2643, DAR ES SALAAM
Simu: +255 22 2135747/8; 2137125; 2135222
Faksi: +255 22 2111281
Barua Pepe: chragg@chragg.go.tz
Tovuti: www.chragg.go.tz
Agosti 26, 2016

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesikitishwa na
matamshi ya Mhe. Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
yanayokiuka misingi ya utawala bora aliyoyatoa tarehe 25 Agosti, 2016 wakati
wa kuaga miili ya askari Polisi watatu waliouawa Mbande, Mkoani Dar es
Salaam.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Bahame Tom Nyanduga, leo
(Agosti 26, 2016) Mhe. Makonda ametumiwa barua ya wito inayomtaka afike
makao makuu ya Tume mtaa wa Luthuli, tarehe 30 Agosti, 2016 ili kujadili kile
Tume ilichokiona kuwa ni kejeli kwa Tume pamoja na jumuiya yote ya watetezi
wa haki za binadamu.
Aidha, Tume imeona kuwa maagizo aliyoyatoa Mkuu huyo wa Mkoa kwa Jeshi
la Polisi hayana msingi wa kisheria na hayako ndani ya mamlaka ya Mkuu wa
Mkoa.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 6(1)(f) na (i) pia Kifungu cha 27(1) na (2) (a) vya
Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Sura Na. 391 ya
Sheria za Tanzania 2002, THBUB ina mamlaka ya kuchunguza mwenendo wa
mtu au taasisi yoyote kuhusiana na utendaji wa kazi zake zinapokiuka mipaka
ya madaraka yake, ili kuchukua hatua za kurekebisha ukiukwaji huo.
Imetolewa na:
(SIGNED)
Idara ya Elimu kwa Umma na Mafunzo
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
Agosti 26, 2016

Page 1 of 1

You might also like