You are on page 1of 2

1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS, IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425

OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK
OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

SALAAM ZA MHE. JOHN POMBE MAGUFULI, RAIS WA JAMHURI YA


MUUNGANO WA TANZANIA, KWA WANANCHI KATIKA KUMBUKUMBU
YA MIAKA 54 YA UHURU, TAREHE 09 DESEMBA, 2015.

Namshukuru Mwenyezi Mungu aliyeiwezesha nchi yetu kutimiza miaka


54 ya uhuru kwa salama na amani. Namshukuru Mungu pia kwa
kuniwezesha kuiona siku hii nikiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania. Napenda kuchukua fursa hii, kuwapongeza Watanzania
wenzangu kwa Taifa letu kutimiza 54 ya Uhuru tarehe 09 Desemba, 2015.
Napenda kuwahakikishia kwamba, kama ilivyokuwa kwa Serikali za
awamu zilizopita, Serikali ya Awamu ya Tano itafanya kila lililo ndani ya
uwezo wake kuhakikisha kwamba Uhuru, Amani na Umoja na wa Taifa
letu hauchezewi na mtu, kikundi au Taifa lolote.

Tutaendelea

kudumisha Uhuru wetu na Mapinduzi ya Zanzibar, tunu ambazo ni


msingi wa Muungano wetu na Utanzania wetu.

Tofauti

na

ilivyozoeleka

tumeamua

mwaka

huu

kusherekea

kumbukumbu hizi kwa kufanya kazi,. Wakati tunapata Uhuru Taifa letu
lilikuwa likiongozwa na kauli mbiu ya UHURU NA KAZI. Kauli hii
ilikuwa na lengo la kuamusha moyo na uzalendo wa kufanya kazi
miongoni mwa Watanzania kwa kutambua kuwa uhuru wetu
hautakuwa na maana kama hatutafanya kazi kwa juhudi na maarifa ili
kujenga Taifa linalojitegemea. Watanzania katika miaka ile waliitikia
wito huo kwa kufanya kazi za kuwaongezea kipato na za kujitolea katika

kuunga mkono juhudi za Serikali za kuwaletea maendeleo. Katika miaka


ya hivi karibuni moyo na uzalendo wa kufanya kazi miongoni mwetu
umepungua sana. Kwa sababu hiyo, niliamua kutumia siku ya
kumbukumbu za uhuru wetu mwaka huu kukumbushana na kutekeleza
kwa vitendo kauli mbiu ya UHURU NA KAZI kwa kufanya kazi
hususan ya usafi wa mazingira. Madhimisho ya Uhuru mwakani
yatasherehekewa kama kawaida.

Nawapongeza viongozi wa Mikoa na Wilaya na wa Taasisi za umma na


binafsi

na

mashirika

yasiyo

ya

kiserikali

yaliyojitokeza

katika

kuhakikisha kuwa zoezi la usafi wa mazingira linafanikiwa.

Napenda kutoa wito kwa Halmashauri zote nchini kuhakikisha


zinaweka mifumo na taratibu thabiti zitakazowezesha usafi wa miji yetu
kuwa endelevu. Viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri waache
visingizio, uwezo na mamlaka ya kuhakikisha kwamba usafi katika miji
yao unadumishwa wanao. Uwezo wa utendaji wao utapimwa pia
kutokana na hali ya usafi wa miji yao.

Naomba wananchi tushirikiane katika kuhakikisha kuwa nyumba na


mazingira ya nyumba zetu yanakuwa safi na maji ya kunywa katika
maeneo ambayo hayawekwi dawa yanachemshwa. Aidha, wananchi
wajizuie kutupa taka ovyo na viongozi wa Serikali za mitaa, vijiji na
vitongoji wahakikishe kwamba kila nyumba inakuwa na choo.
Tutashinda vita dhidi ya maradhi kama kipindupindu ikiwa sote
tutazingatia kanuni za afya. Kila mtu atimize wajibu wake.

Mwalimu alisema Uhuru na Kazi na mimi nasema Hapa Kazi Tu.

You might also like