You are on page 1of 4

O u r R e f:

NSSF Waterfront 7th Floor, Sokoine Drive, P.O. Box 14154, Dar es Salaam.

Tel: +255 22 2127410,


Fax: +255 22 2127411,
E-mail: info@sumatraccc.go.tz

Website:

www.sumatraccc.go.tz;

HALI YA USAFIRI KIPINDI CHA SIKUKUU ZA KRISMAS 2015


NA MWAKA MPYA 2016.
Ndugu wanahabari,
Kila kipindi cha mwisho wa mwaka, hasa mwezi wa Desemba,
Watanzania wengi wanasafiri kurudi nyumbani kwao kwa ajili ya
kuungana na jamaa zao kusherehekea sikukuu za Krismass na
mapumziko ya mwisho wa mwaka. Utamaduni huu unakua kwa kasi na
unachangia kusukuma maendeleo ya vijiji wanakotoka.
Ndugu wana habari,
Kutokana na wingi wa abiria hao, kila mwaka mahitaji ya usafiri kwa
kipindi hicho yanazidi kuwa makubwa kuliko huduma ya usafiri uliopo.
Kutokana na hali hiyo, baadhi ya watoa huduma ambao sio waaminifu
huchukulia kipindi hicho kama njia ya kuvuna zaidi kutoka kwa
watumiaji kinyume na masharti ya leseni zao. Aidha, kutokana na
mahitaji makubwa ya usafiri, baadhi ya abiria hukubali wenyewe kulipa
zaidi kusudi wapate kusafiri.

Ndugu wanahabari
Kutokana na hali hiyo, Baraza linachukua fursa hii kuwakumbusha
wamiliki wa mabasi yaendayo mikoani kupitia umoja wao (TABOA)
kufuata masharti ya leseni zao na kutoza nauli zilizoidhinishwa na
SUMATRA. Aidha, Baraza linatoa wito kwa wamiliki wote wa Mabasi
kuwahimiza wafanyakazi wao wanaokata tiketi katika vituo mbali mbali
nchini kuwa waaminifu kwa waajiri wao na wateja wao.
Ndugu wana habari,
Baraza linatoa wito kwa watu wote wanaotarajia kusafiri kipindi cha
mwisho wa mwaka kufanya maandalizi ya safari zao mapema ikiwa ni
pamoja na kufanya booking na/au kukata tiketi zao mapema ili
kuepukana na matatizo ya kulanguliwa tiketi..
Aidha, Baraza linatoa wito kwa abiria wote kutonunua tiketi za

safari zao kutoka kwa wapiga debe au vishoka katika eneo


la kituo cha mabasi cha Ubungo au vituo vingine nchini
kote.
Ndugu wana habari,
Baadhi ya abiria wanalalamika kwamba baadhi ya watoa huduma,
wakiongozwa na nia ovu, huwa wanawakatalia abiria wasifanye bookings
zao

mapema.

Kuwakatalia

abiria

kufanya

booking

mapema,

kunasababisha abiria kurundikana vituoni siku za safari bila sababu


yoyote na hivyo kutoa mwanya kwa wapiga debe na vishoka kuwalaghai
abiria hao. Tunaomba Abiria watakaokataliwa kufanya bookings zao
mapema mwaka huu kutoa taarifa kwetu au kwa Mamlaka ya SUMATRA
kwa hatua zaidi.
Ndugu wana habari,

Baraza la SUMATRA linatoa wito kwa abiria wote kuhakikisha


wanasafiri kwa tiketi yenye jina lako na iliyoandikwa kiwango sahihi cha
nauli uliyolipa. Baadhi ya abiria wanakubali kienyeji tu, analipa elfu 70
anapewa risti ya elfu 50. Abiria wa namna hii huwa ndio wa kwanza
kulalamikia mamlaka za SUMATRA na Jeshi la Polisi kitengo cha
usalama barabarani. Tunawasihi sana abiria kuwa makini na kutoa
taarifa na ushirikiano kwa mamlaka husika iwapo vitendo vya namna
hiyo vitajitokeza mwaka huu. Tunatoa wito kwa TABOA kuwa makini na
wafanyakazi wao kutojihusisha na vitendo vya namna hiyo kwani
ikigundulika tiketi za kampuni husika zinalanguliwa, mwenye kampuni
atawajibishwa.
Ndugu wana habari,
Tangia mwaka jana, Baraza limeanzisha vilabu vya watumiaji katika
shule za misingi na sekondari chini ya dhana ya kuelimisha watumiaji
vijana (empowering young consumers). Tunafurahi kuwajulisha kwamba
program hii imefanikiwa vizuri sana na baada ya miaka kumi ijayo
tutakuwa na jamii tofauti na ya sasa juu ya utambuzi wa haki na wajibu
wao. Program hii inaendeshwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga,
Arusha, Mwanza, Kagera, Kigoma, Mbeya na Mtwara. Program hii
inashirikisha jumla ya shule 41 (shule za msingi 18 na sekondari 23).
Katika program hii tunazaidi ya wanafunzi 2000 ambao ni wanavilabu
wa Baraza la SUMATRA.
Mwisho, Baraza la SUMATRA linatoa wito kwa TABOA kuhakikisha
madereva wao wanaendesha magari kwa mwendo unaokubalika. Kuna
taarifa kuwa kipindi cha Krismas mabasi mengi huenda mwendo wa kasi
kusudi wageuze siku hiyo hiyo kwa ajili ya kutengeneza fedha zaidi.
Jambo hili huatarisha usalama wa abiria. Tutangulize usalama wa abiria
na fedha iwe baadaye. Biashara inabidi iendelee hata baada ya Xmass
na Mwaka mpya.

Baraza linawatakia heri ya Xmass na heri ya Mwaka mpya 2016


.............................
Dr. Oscar Kikoyo
Katibu Mtendaji,
Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa Nchi Kavu na
Majini,

Council Members:- Ms. Regina L. Bieda (Chairperson), Mr. George M.M. Makuke,
Mr. Manyama M. Kanyere, Mr. Ebenezer S. Mshana, Ms. Lydia N. Ngwale, Mr. Said
H. Putta, Mr. Hassani R. Mnyone

You might also like