You are on page 1of 3

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA UCHUKUZI

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA


Simu ya Mdomo: +255 22 2460735/2460706
Nukushi: +255 22 2460735/2460700
Baruapepe: met@meteo.go.tz
Tovuti: www.meteo.go.tz

S. L. P 3056,
DAR ES SALAAM.

Unapojibu Tafadhali Nakili:


Kumb. Na. TMA/1622

29 Oktoba, 2015

YAH: TAARIFA YA HALI YA MWENENDO WA MIFUMO YA HALI YA HEWA


NA MVUA ZA MSIMU WA VULI 2015
UTANGULIZI
Taarifa hii inatoa tathmini ya mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na msimu wa mvua za
vuli kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka pamoja na mvua za
msimu kwa maeneo yanayopata msimu moja wa mvua kwa mwaka katika kipindi cha
Novemba- Desemba 2015.
MIFUMO YA HALI YA HEWA
Kuendelea kuongezeka kwa joto katika maeneo ya Bahari ya Pasifiki kunaonesha kuimarika
kwa El-Nino katika Bahari ya Pasifiki kama ilivyoelezwa katika taarifa ya Mamlaka
iliyotolewa mapema mwezi Septemba, 2015. Hata hivyo, mifumo mingine ya hali ya hewa
ikiwemo mwitikio wa mfumo ya hali ya hewa katika Bahari ya Hindi imekuwa na mchango
hasi kinyume na ilivyotarajiwa katika mwenendo wa mvua za Vuli nchini katika kipindi cha
mwezi Oktoba, 2015 na kusababisha vipindi virefu vya upungufu wa mvua katika Mikoa ya
Morogoro, Pwani na Dar es Salaam.
Hata hivyo mifumo ya hali ya hewa katika Bahari ya Hindi katika ukanda wa Afrika
Mashariki na ukanda wa pwani ya Angola katika Bahari ya Atlantiki imenza na inaendelea
kuimarika. Kuimarika kwa mifumo hii kunatarajiwa kusababisha kunyesha kwa mvua katika
maeneo mengi kama zilivyotabiriwa katika kipindi cha mwezi Novemba-Disemba 2015.
Kwa upande mwingine, mpaka sasa baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Ukanda wa Ziwa
Viktoria yameendelea kupata mvua za wastani katika kipindi cha mwezi Oktoba, 2015.

MVUA KWA MWEZI NOVEMBA HADI DISEMBA 2015


Maeneo ya Ukanda wa Ziwa Viktoria, Kanda ya Magharibi na Nyanda za juu kaskazini
Mashariki yanatarajiwa kupata mvua za juu ya wastani katika kipindi cha mwezi Novemba
hadi Disemba 2015, pamoja na vipindi vifupi vya mvua kubwa. Kwa ujumla mwelekeo wa
mvua bado ni kama ulivyotolewa mapema tarehe 2 Septemba 2015.

Maeneo yanayopata mvua mara moja kwa mwaka Mikoa ya Dodoma, Singinda, Ruvuma,
Lindi, Mtwara, Songea, Mbeya, Iringa, Njombe, Tabora, Kigoma Rukwa na Katavi mvua
zinatarajiwa kuanza kati ya wiki ya pili na ya nne ya mwezi Novemba, 2015. Ambapo mvua
hizo zimeanza kujiimarisha katika mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi na zinatarajiwa
kusambaa katika maeneo mengine mwezi huu wa Novemba 2015. Hata hivyo, Wilaya za
Kondoa, Kongwa na Singida Vijijini katika mikoa ya Dodoma na Singida zinatarajiwa pia
kupata vipindi vya mvua mapema mwanzoni mwa mwezi Novemba, 2015.

USHAURI
Mamlaka ya Hali ya Hewa inawashauri watumiaji wa taarifa za hali ya hewa ikiwa ni
pamoja na wakulima, wafugaji, Mamlaka za Wanyamapori, Mamlaka za Maji na Afya
waendelee kutafuta, kupata na kufuata ushauri wa wataalamu katika sekta husika katika
kutekeleza

mipango

inayoweza

kuathiriwa

na

mwelekeo

wa

hali

ya

hewa

iliyotabiriwa.Tahadhari zilizotolewa na Mamlaka sambamba na taarifa hii ya mrejeo


ziendelee kuzingatiwa .

VYOMBO VYA HABARI


Vyombo vya habari vinashauriwa kufuatilia, kupata na kusambaza taarifa sahihi za
mienendo ya hali ya hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na kutumia
wataalam wa sekta husika katika kuandaa na kufikisha taarifa za masuala mtambuka ya hali
ya hewa kwa jamii. Aidha, jamii nayo inashauriwa kufuatilia na kuzingatia taarifa sahihi za
hali ya hewa na mirejeo yake.

Mwelekeo wa mvua uliotolewa hapa umezingatia zaidi viashiria vya mvua katika kipindi cha
msimu(miezi mitatu) na hali ya mvua katika maeneo makubwa. Hivyo, viashiria
vinavyochangia mwenendo wa mifumo ya mvua na mabadiliko ya muda mfupi katika
maeneo madogo utazingatiwa katika

uchambuzi wa utabiri wa muda wa kati na mfupi.

Watumiaji wa taarifa za utabiri huu wanashauriwa pia kufuatilia tabiri za saa 24, siku 10
pamoja na wa mwezi kama zinavyotolewa na Mamlaka ya hali ya Hewa Tanzania.
Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania Itaendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo ya hali
ya hewa na kutoa taarifa za mwelekeo wa mvua nchini.
Dkt. Ladislaus B. Changa
KAIMU MKURUGENZI MKUU

You might also like