You are on page 1of 2

Na Teresia Mhagama na Asteria Muhozya

Katibu Mkuu mpya na Naibu Katibu Mkuu walioteuliwa kuiongoza


Wizara ya Nishati na Madini wameanza majukumu yao na
kusisitiza watumishi wa Wizara na Taasisi zake kuzingatia Uadilifu,
Ubunifu, Uwajibikaji, na Uwazi katika utekelezaji wa majukumu
yao ya kila siku.
Wakizungumza na wajumbe wa menejimenti ya Wizara ya Nishati
na Madini, viongozi hao walisisitiza baadhi ya masuala yatakuwa
kipaumbele kuwa ni uwepo wa umeme wa uhakika na bei nafuu ili
wananchi watumie nishati hiyo kujiletea maendeleo na kukuza
uchumi wa nchi.
Vipaumbele vingine ni kuongeza mchango wa sekta madini katika
pato la Taifa, uwepo wa kiwanda cha kusindika gesi asilia, na suala
la uwezeshaji wazawa (Local Content) katika sekta za Nishati na
Madini.
Vilevile, vipaumbele vingine ni kuhakikisha kuwa wachimbaji
wadogo wanasaidiwa katika masuala ya fedha na utaalam na
kuboresha mazingira na maslahi ya wafanyakazi.
Katibu Mkuu, Mhandisi Omari Chambo, pamoja na kumshukuru
aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim
Maswi kwa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa, alitoa
wito wa ushirikiano kati ya uongozi huo mpya na wafanyakazi.
Naye, Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Paul Masanja pamoja na
kuainisha vipaumbele mbalimbali vya utekelezaji amemshukuru
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete
kwa kumteua kushika nafasi hiyo na kueleza kuwa, imetokana na
kuridhika na utendaji wake wa kazi wakati aliposhika nyadhifa
mbalimbali ikiwemo kuwa Kamishna wa Madini nchini.

Alitoa wito kwa wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini kutoa


ushirikiano kwa uongozi huo ili kwa pamoja waweze kukabiliana na
changamoto mbalimbali zinazojitokeza katka uendelezaji wa sekta
za Nishati na Madini.
Kabla ya kukabidhi nyaraka za makabidhiano, aliyekuwa Katibu
Mkuu wa Nishati na Madini, Eliakim Maswi ambaye ameteuliwa
kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, aliwashukuru
watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini kwa ushirikiano
waliompa wakati wa kipindi cha uongozi wake na kuwaasa kufanya
kazi kwa bidii na kutoa ushirikiano kwa uongozi mpya.
Vilevile, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Ngosi Mwihava
ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji,
aliwaasa Watumishi kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana,
kuzingatia taratibu, sheria na kanuni, kuzingatia muda na
kuimarisha mawasiliano.
Kabla ya kushika nyadhifa hizi Katibu Mkuu, Mhandisi Omari
Chambo alikuwa Katibu Tawala mkoa wa Manyara na Naibu Katibu
Mkuu, Mhandisi Paul Masanja alikuwa Kamishna wa Madini
nchini.

You might also like