You are on page 1of 12

HABARI

HabariZA
za
NISHATI
nishati&MADINI
&madini

NewsBulletin
UMEME
Wabunge
http://www.mem.go.tz

Toleo
No.90
51
Toleo No.

LimesambazwaLimesambazwa
kwa Taasisi nakwa
Idara
zote
Taasisi
naMEM
Idara zote MEM Tarehe
- 23-29 Januari , 2015
Oktoba 23 - 29, 2015

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA RASMI BODI


YA TANESCO -Uk2
Mitambo ya kuzalisha umeme Kinyerezi I

waongezeka
Gridi ya Taifa

Waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA

Waziri wa Nishati
na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo

Naibu Waziri wa Nishati na


Madini, anayeshughulikia
Madini Stephen Masele

Naibu Waziri wa Nishati na


Madini anayeshughulikia
Nishati, Charles Kitwanga

Somahabari Uk.2

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,


Mhandisi Felchesmi
Mramba

Mkurugenzi Mkuu wa
REA, Dk. Lutengano
Mwakahesya

Serikali kukomesha uchimbaji, uuzaji haramu madini

JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo wa Msimbati-Uk4

Soma
habari
Uk. 2

Ofisi ya M awasiliano Serik alini inapokea habari za matukio mbalimbali


kwa ajili ya News Bullettin hii ya Wizar a ya Nishati na Madini
Ofisi ya Mawasiliano Serik alini inapokea habari za matukio mbalimbali
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
kwa
ajili ya
News
Bullettin
hiiGhorofa
na Jarida
la(MEM)
Wizar
a yapepe:
Nishati
na Madini
au Fika
Ofisi
ya Mawasiliano
ya Tano
Barua
badra77@yahoo.com
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: badra77@yahoo.com

Habari za nishati/madini

Megawati 35
zaongezwa
Kinyerezi I
Zuena Msuya na
Nuru Mwasampeta

hirika la Umeme Tanzania


(Tanesco) limewasha mtambo
mwingine wenye uwezo
wa kuzalisha umeme wa
kiasi cha Megawati 35 na
hivyo kufikisha jumla ya Megawati
70 zinazozalishwa kutokana na gesi

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

asilia inayotoka Madimba hadi kituo


cha kufua umeme cha Kinyerezi I
jijini Dar es salaam. Megawati 35 za
awali ziliwashwa mnamo tarehe 17
Septemba, 2015.
Akizungumza kituoni hapo Meneja
mradi wa Kinyerezi I, Mhandisi
John Mageni amesema mtambo huo
umewashwa ili kuendelea kuimarisha
upatikanaji wa huduma ya umeme
nchini kwa kuwa hivi sasa vyanzo
vya maji vinavyotegemewa kuzalisha
umeme vimeanza kukauka kutokana
na ukame.
Huduma ya umeme itaendelea
kuimarika kwani sasa tunawasha
mtambo namba 3 baada ya kukamilika
kwa kuufanyia majaribio yote na
kuridhika nayo kwamba uko tayari
kuanza kazi ya uzalishaji wa umeme na
hivyo kuongeza kiwango cha umeme
unaoingia katika gridi ya taifa, alisema
Mageni
Aliongeza kuwa kwa sasa mkoa

wa Dar es Salaam unapata umeme wa


uhakika baada ya kuwasha ule mtambo
wa kwanza wa megawati 35, hivyo
zoezi la kuwasha mitambo iliyosalia ili
kufikisha Megawati 150 litaendelea ili
kuimarisha huduma ya upatikanaji wa
umeme nchini nzima.
Alisema pindi mitambo yote
itakapowashwa katika kituo hicho
itakuwa na uwezo wa kuzalisha
umeme kiasi cha megawati 150,
ambazo zimeanza kuingizwa katika
gridi ya taifa.
Kituo cha Kinyerezi 1 kilizinduliwa
tarehe 13 Oktoba, 2015 na Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ambaye
aliitaka Tanesco kuongeza kasi ya
kuzalisha umeme unaotosheleza
mahitaji ya Watanzania.
Mitambo miwili kati ya minne
inayokamilisha Kinyerezi 1 imewashwa
na miwili iliyosalia itaendelea
kuwashwa kadri siku zinavyoendelea.

Serikali kukomesha uchimbaji, uuzaji haramu madini


Mohamed Saif na
Clinton Ndyetabula

meelezwa kwamba Serikali


imejizatiti katika kuhakikisha
inakomesha uchimbaji na uuzaji
haramu wa rasilimali ya madini
yaliyopo nchini kwa manufaa ya
sasa na ya vizazi vijavyo.
Hayo yameelezwa hivi karibuni
na Kamishna Msaidizi wa Madini
sehemu ya Leseni, Mhandisi John
Nayopa kwa niaba ya Kamishna wa
Madini wakati wa ufunguzi wa warsha
kuhusu utekelezaji wa mpango wa
kupambana na uchimbaji haramu
wa rasilimali kwa nchi za Ukanda wa
Maziwa Makuu (ICGLR) ujulikanao
kama ICGLR Regional Initiative
Against Illegal Exploitation of Natural
Resources (RINR).
Mhandisi Nayopa alisema lengo
la warsha hiyo ni kufafanua hatua ya
utekelezaji wa mpango wa RINR kwa
kuzingatia mazingira ya Tanzania;
kuongeza uelewa wa wadau kuhusu

mpango wa RINR, na kuandaa


mpango kazi sahihi ikiwa ni pamoja
na mkakati wa utekelezaji wa RINR
nchini.
Alisema Tanzania ni miongoni
mwa nchi 12 za Ukanda wa Maziwa
Makuu (ICGLR) ambazo zimeridhia
itifaki zenye lengo la kuimarisha amani,
utulivu, demokrasia na utawala bora
kwenye nchi husika.
Alisema Wakuu wa Nchi 11
za Jumuiya ya Nchi za Ukanda
wa Maziwa Makuu (ICGLR)
walikutana jijini Dar es Salaam
mwezi Oktoba, 2014 na kukubaliana
kwa pamoja kuimarisha maendeleo,
usalama na utulivu jambo ambalo
anasema linathibitisha dhamira yao
ya kubadilisha ukanda wa Maziwa
Makuu kuwa na amani endelevu kwa
mataifa hayo na kwa wananchi wake,
ikiwemo utulivu wa kisiasa na kijamii
na ukuaji wa maendeleo ya pamoja.
Mhandisi
Nayopa
alisema
makubaliano hayo yanaitwa Tamko
la Dar es Salaam, la Mwaka 2014

Kamishna Msaidizi wa Madini, Sehemu ya Leseni, Mhandisi


John Nayopa katika picha ya pamoja na washiriki wa
warsha. Wa kwanza kushoto waliokaa ni Mkurugenzi wa
Utawala na Rasilimali Watu Mrimia Mchomvu na wa kwanza
kulia ni Mwakilishi kutoka PAC, Stephen Turyahikayo.

Washiriki wa warsha wakifuatilia uwasilishaji mada kuhusu


utekelezaji wa mpango wa kupambana na uchimbaji
haramu wa rasilimali kwa nchi za Ukanda wa Maziwa
Makuu (ICGLR) ujulikanao kama ICGLR Regional Initiative
Against Illegal Exploitation of Natural Resources (RINR).

ambayo yanajulikana kama The Dar es


Salaam Declaration of 2014.
Ili kufanikisha hili, nchi za ICGLR
zilisaini makubaliano ambayo yalizaa
itifaki mbalimbali na miongoni mwake
ni itifaki ya kupambana na uchimbaji
haramu wa madini, alisema Mhandisi
Nayopa.
Alisema kwamba mojawapo ya
changamoto kuu kwenye baadhi
ya nchi za ICGLR ni kukithiri kwa
uchimbaji haramu wa madini jambo
ambalo
linatumika
kuchochea
migogoro na pia ni chanzo cha fedha
kwa wababe wa kivita.
Mhandisi Nayopa alisema Tanzania
imejaaliwa rasilimali nyingi ambazo
zinapasa kuleta maendeleo endelevu
kwa jamii na Taifa kwa ujumla ikiwa ni
pamoja na kukuza uchumi utakaoleta
mabadiliko chanya.
Licha ya mafanikio ambayo
Tanzania imekuwa nayo katika kuvutia
uwekezaji mkubwa katika Sekta ya
Madini na katika kurasimisha idadi

kubwa ya wachimbaji wadogo, bado


inakabiliwa na changamoto lukuki,
alisema.
Alisema kupitia Mpango huo wa
RINR, Serikali inatarajia matokeo
makubwa yenye tija katika kupambana
na uchimbaji haramu wa madini
yaliyopo nchini. Lengo letu na
matarajio yetu ni kwamba faida
zitokanazo na uchimbaji madini
zitaongezeka maradufu na hivyo
jamii kwa ujumla kunufaika, alisema
Mhandisi Nayopa.
Warsha hiyo ya siku mbili
imehudhuriwa na Kamishna Wasaidizi
wa Madini kutoka Kanda mbalimbali,
watumishi wa Wizara ya Nishati
na Madini hususan kutoka Idara ya
Madini, wawakilishi kutoka Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, kutoka Wizara ya Mambo
ya Ndani, wawakilishi wa wachimbaji
wadogo na washirika wa Maendeleo
wa Canada wajulikanao kama
Partnership Africa Canada (PAC).

NewsBulletin

Habari za nishati/madini

http://www.mem.go.tz

MEM

Tahariri
Na Badra Masoud

Makubwa yamefanyika
sekta ya Nishati

Wengi tutakumbuka wakati Rais wa Awamu ya Nne Mhe. Dk.


Jakaya Mrisho Kikwete alipoingia madarakani mwishoni mwa mwaka
2005 nchi yetu ilikuwa katika mgawo wa umeme na hadi ilipoingia
mwaka 2006 mgawo huo wa umeme uliendelea kuwa mkali.
Mgawo huo ulitokana na kukauka kwa Mabwawa ambayo
yanatumika kuzalisha umeme ambayo kwa kipindi hicho ndiyo yalikuwa
chanzo kikubwa na pekee cha kuzalisha umeme.
Baadhi ya watafiti na wana mazingira walieleza kwamba kukauka
kwa mabwawa hayo kunatokana na sababu kubwa mbili ambazo ni
mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kilimo kinachofanywa na baadhi
ya watu katika vyanzo vya maji (upstream) ambapo huchepusha maji na
kushindwa kufuata mkondo wake.
Kutokana na mgawo huo wa umeme Serikali hiyo ya Awanu ya
Nne kupitia Wizara ya Nishati na Madini iliamua kuchukua hatua za
makusudi na madhubuti kuanza kukabiliana na hali hiyo ya mgawo
na kipaumbele kikiwa ni kujenga mitambo ya kuzalisha umeme kwa
kutumia nishati mbadala hususan gesi asilia.
Serikali iliruhusu Kampuni binafsi kuchimba gesi na kusafirisha
pamoja na kuwauzia Makampuni binafsi, viwanda na TANESCO ili
TANESCO nayo iweze kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia.
Ilipofika mwaka 2008 Serikali ilikamilisha ujenzi wa mtambo wa
kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia wa Ubungo I wenye uwezo
wa kuzalisha Megawati 102.
Mwaka 2009 mtambo mwingine ulikamilika wa Tegeta wenye
uwezo wa kuzalisha Megawati 45 na mwaka 2012 Serikali ilizundua
mtambo wa Ubungo II (Megawati 105). Mitambo yote hiyo inazalisha
umeme kwa kutumia gesi asilia na inamilikiwa na Serikali kwa asilimia
mia moja.
Serikali pia ilijenga mitambo mingine ya kuzalisha umeme kwa
kutumia gesi asilia ya Mtwara (Megawati 18) na Somangafungu mkoani
Lindi (Megawati 7.5).
Ili kuwa na umeme wa uhakika katika gridi ya taifa kwenye mikoa
ya Kanda ya Ziwa, Serikali ilijenga pia mtambo mwingine wa kuzalisha
umeme kwa kutumia mafuta mazito wenye uwezo wa kuzalisha
Megawati 60 uliopo Nyakato, Mwanza.
Kutokana na gesi asilia kugundulika kwa wingi katika mikoa ya
Kusini mwa Tanzania yaani Lindi na Mtwara, Serikali iliamua kujenga
bomba kubwa la gesi kutoka Mtwara na Lindi pamoja na mitambo ya
kuchakata ambapo gesi hiyo inazalisha na kusafirishwa hadi kwenye
mitambo ya kuzalisha umeme kwani gesi inayozalishwa na kuuzwa na
watu binafsi haitoshelezi katika kuzalisha umeme.
Aidha, kutokana na bomba la gesi kujengwa na mitambo yake,
Serikali iliona ni busara kujenga mtambo wa Kinyerezi I wenye uwezo
wa kuzalisha Megawati 150.
Mitambo yote ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia
iliyojengwa na Serikali tangu mwaka 2008 hadi sasa 2015 imefikia jumla
ya Megawati 484.5 ya umeme wote unaozalishwa na mitambo hiyo ya
Serikali kupitia TANESCO. Hayo ni mafanikio makubwa katika sekta
ya Nishati katika kipindi cha Serikali ya Awanu ya Nne.
Pamoja na kwamba Serikali ya Awanu ya Nne inaondoka
madarakani mwishoni mwa mwaka huu lakini imeacha misingi mizuri
na jitihada kubwa za kuendelea kuboresha sekta ya nishati hususan
katika kuzalisha umeme.
Ni ukweli ulio wazi kwamba kukamilika kwa mtambo wa Kinyerezi
I ndiyo mwanzo wa kuanza kwa ujenzi wa mitambo mingine ya
kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia ya Kinyerezi II, Kinyerezi
III na Kinyerezi IV kwani zipo kila dalili za kuandaa na kuendelea kwa
ujenzi huo kuwapo kwa eneo lenyewe ambapo mitambo hiyo itajengwa
na wahusika wameshaanza kazi.
Hivyo tuna kila sababu ya kuipongeza Serikali ya Awanu ya Nne
inayoongozwa na Mhe. Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kwamba
imefanya juhudi kubwa katika kuhakikisha kwamba upatikanaji wa
umeme unaongezeka ili Taifa la Tanzania litakapofika mwaka 2025 liwe
ni taifa la uchumi wa kati na mafaniko hayo yote yatatokana na kuwapo
kwa umeme wa kutosha na wa uhakika.
Hii ni dhahiri kwamba maendeleo ya nchi yoyote duniani yanatokana
na upatikanaji wa umeme wa uhakika hivyo lazima wote tutambue
kwamba bila umeme hakuna maendeleo hivyo, umeme ni maendeleo.

Tuzungumzie Gesi Asilia

urasa hii inakupa fursa ya


kuongeza uelewa kuhusu
masuala yanayohusu sekta
ndogo ya gesi nchini.
Yaliyoandikwa katika kurasa
hii ni baadhi tu ya maswali ambayo yamekuwa
yakiwatatiza wananchi.
Gesi asilia ni nini?
Gesi asilia ni mchanganyiko wa molekuli
nyepesi za Carbon na Hydrogen mfano
methane (CH4), Ethane (C2H6). Gesi asilia
inatokana na kuoza kwa mata ogania (organic
matter) kama vile uozo wa masalia ya mimea
na wanyama miaka mingi iliyopita.

Ni kiasi gani cha gesi asilia


kimegunduliwa hapa nchini?
Kiasi cha gesi asilia kilichogunduliwa hadi
hivi sasa ni futi za ujazo trilioni 55.08 (Gas
initially in place- kabla ya kuhakikiwa kiasi
kamili kinachoweza kuvunwa). Kati ya hizo,
futi za ujazo trilioni 47.08 ni kutoka vitalu vya
kina kirefu cha bahari na futi za ujazo trilioni 8
ni kutoka vitalu vya nchi kavu.
Kwanini gesi asilia imepelekwa jijini Dar
es Salaam na sio kubaki kwenye Mikoa
ya Lindi na Mtwara?
Kwanza kabisa, kujenga miundombinu
hiyo kuliangaliwa uhitaji mkubwa wa gesi
asilia ulipo nchini, kama viwanda, kuzalisha
umeme na kadhalika.
Pili, uwepo wa miundombinu ya bomba

la gesi kwenda Dar es Salaam, hainyimi


fursa kwa Mikoa ya Kusini kutonufaika na
gesi asilia. Ikumbukwe kuwa mwaka 2006
kulijengwa Kituo cha kuzalisha umeme kwa
Mikoa ya Lindi na Mtwara ambapo kituo
hicho kinatumia gesi inayozalishwa Mnazi
Bay, Mkoani Mtwara. Vilevile, miundombinu
hiyo kwenda Dar es Salaam imejengwa
kitaalam kuruhusu kutoa gesi asilia kwenda
kila sehemu soko litakakopatikana. Mfano, ni
uwepo wa kiwanda cha Saruji cha Dangote
Mkoani Mtwara ambacho kinatarajiwa
kutumia gesi asilia.
Je, kuna ukweli gani kwamba
makampuni ya mafuta na gesi a
silia yaliyogundua gesi katika kina kirefu
cha bahari yameshaanza kuvuna gesi asilia
na kusafirisha nchi za nje?
Hapana, makampuni ambayo mpaka
sasa yamefanikiwa kufanya ugunduzi wa gesi
asilia katika tafiti za mafuta na gesi kwenye
kina kirefu cha bahari ni BG, Statoil na
washirika wake. Kwa sasa makampuni haya
kwa kushirikiana na Serikali yapo kwenye
mazungumzo ya kutafuta eneo la kujenga
mradi wa kubadili gesi kuwa kimiminika
LNG (Liquefied Natural Gas). Mradi huu
utasaidia upatikanaji wa nishati ya gesi nchini,
pamoja na kuuza gesi asilia nchi za nje na
kuingizia Serikali fedha za kigeni ili kuchochea
ukuaji wa uchumi. Kwa sasa hakuna uuzwaji
wowote unaofanywa na Meli kwenda nje ya
nchi.

Mitambo ya kuchakata Gesi Asilia, Madimba Mtwara


KWA HABARI PIGA SIMU
kitengo cha mawasiliano

TEL-2110490
FAX-2110389
MOB-0732999263
Bodi ya uhariri
Mhariri Mkuu: Badra Masoud
Msanifu: Lucas Gordon
Waandishi: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson
Mwase Teresia Mhagama, Mohamed Saif, Rhoda James ,
Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya

Five
Pillars of
Reforms
increase efficiency
Quality delivery
of goods/service
satisfAction of
the client
satisfaction of
business partners
satisfAction of
shareholders

Habari za nishati/madini

TUMEWEZA

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliachim Maswi akiwa na wanafunzi waliopata ufadhili
wa masomo kupitia Wizara ya Nishati na Madini kusoma Shahada za Uzamili na Uzamivu katika
masuala ya mafuta na gesi nchini China.Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali
Watu Lusius Mwenda na wa tatu kulia ni Kamishna Msadizi anayeshughulikia Maendeleo ya
Nishati, James Andilile, mwaka 2015.

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (wa tano kulia) na Balozi
wa Brazili nchini Fransisco, Carlos Luiz (wa tatu kulia) katika picha ya pamoja na Wanafunzi 15
waliohitimu mafunzo ya lugha ya Kireno. Wanafunzi 7 kati yao walipata ufadhili wa kusoma masuala
ya mafuta na gesi katika ngazi za Shahada ya Uzamili na Uzamivu nchini Brazil mwezi Machi,
mwaka 2015.

Waziri wa Nishati
na Madini George
Simbachawene (kulia)
akizungumza na
wanafunzi 22 waliopata
Ufadhili wa Masomo
kupitia Serikali ya
Watu wa China kusoma
Shahada za Uzamili
na Uzamivu kuhusu
masuala ya mafuta
na gesi nchini China.
Hafla ya kuwakabidhi
nyaraka za masomo
ilifanyika mwezi Agosti,
2015

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

UFADHILI WA
MASOMO

Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene


(kushoto) akimkabidhi mmoja wa wanafunzi nyaraka za
masomo kwenda nchini China. Anayeshuhudia katikati
ni Kamishna Msadizi anayeshughulikia maendeleo ya
nishati, James Andilile, Agosti 5, 2015.

Watanzania waliopata ufadhili wa masomo nchini China


mwaka 2014, katika ngazi ya shahada ya uzamili na uzamivu
katika fani ya mafuta na gesi wakiwa katika picha ya
pamoja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo (aliyekaa) na Katibu Mkuu Wizara ya
Nishati na Madini, Eliakim Maswi (wa nne kutoka kushoto
mstari wa nyuma) pamoja na watendaji wengine wa Wizara
ya Nishati na Madini mara baada ya kuagwa rasmi katika
Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini.Wengine
katika picha (mstari wa mbele) ni Kamishna Msadizi Nishati
anayeshughulikia Umeme, Mhandisi Innocent Luoga (wa
kwanza kulia), Kamishna wa Madini, Mhandisi Paul Masanja
(wa pili kulia), Kaimu Mkurugenzi Utawala Bi. Caroline
Musika (wa kwanza kushoto).

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

TUMEWEZA

Habari za nishati/madini

UTOAJI
RUZUKU

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Pinda akikabidhi hundi za mikopo kwa wachimbaji wadogo. Mwaka 2013 Serikali ilianza
utaratibu wa kutoa mikopo ya masharti nafuu na ruzuku kwa wachimbaji wadogo kupitia Benki ya Maendeleo ya TIB. Hundi za awamu ya kwanza za ruzuku hiyo
zenye jumla ya Dola za Marekani 537,000 sawa na shilingi milioni 880.68 zilikabidhiwa mwezi Aprili, 2014 na Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Pinda kwa miradi 11.
Mjasiriamali anayejihusisha
na biashara ya vito vya
madini kwa kukata, kusanifu
na kuuza, Susie Kennedy
kutoka Arusha, akipokea
mkataba kutoka kwa Waziri
wa Nishati na Madini, George
Simbachawene wakati wa
mafunzo kwa waliopata
ruzuku awamu ya pili ya
kuendeleza uchimbaji madini
mdogo. Wengine pichani
kutoka Kushoto ni Kamishna
Msaidizi wa Madini, Sehemu
ya Leseni, Mhandisi John
Nayopa, Mkurugenzi wa
Usimamizi wa Fedha za
Serikali kutoka Benki ya
Maendeleo ya TIB, Prisca
Changa na Rais wa Shirikisho
la Vyama vya Wachimbaji
Madini Tanzania (FEMATA),
John Bina. Mafunzo hayo ya
siku mbili yalifanyika mjini
Dodoma Oktoba 7 na 8, 2015.

Waziri wa Nishati
na Madini, George
Simbachawene (wa pili
kutoka kulia waliokaa)
akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya
wachimbaji madini wadogo
kutoka Kanda ya Kaskazini
waliopata ruzuku awamu
ya pili kwa ajili ya
kuendeleza uchimbaji
madini mdogo.Ruzuku
ya awamu ya pili ya kiasi
cha shilingi bilioni 7.2
ilitolewa kwa vikundi 111
vya wachimbaji wadogo na
watoa huduma mbalimbali
katika sekta ya madini.

Habari za nishati/madini

MAKALA

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Sera ya Madini ni Mkombozi wa Wanawake wachimbaji?


>>> Mjomba Hussein
atoa ushahidi
Na Veronica Simba

ivi karibuni, Wizara


ya Nishati na Madini
iliendesha
mafunzo
maalum kwa wachimbaji
madini ambao miradi yao
ilichaguliwa kupata ruzuku ya Serikali
kwa ajili ya kuendeleza uchimbaji
mdogo.
Miradi iliyochaguliwa kwa ajili
ya kupata ruzuku ilikuwa ya aina
mbalimbali na pia ilihusu jinsia zote.
Miradi hiyo ni pamoja na ile ya
uchimbaji madini, utoaji wa huduma
za kiufundi, uchenjuaji madini, usanifu
wa vito na pia huduma za mama lishe
migodini.
Mafunzo
hayo
yalilenga
kuwawezesha wachimbaji madini
wadogo nchini kuendeleza shughuli zao
kwa tija na yalihitimishwa kwa utoaji
mikataba ya wachimbaji madini wadogo
waliopata ruzuku kutoka Serikalini
awamu ya pili.
Mambo mbalimbali yalijadiliwa na
washiriki wa mafunzo hayo ambapo
baadhi ya washiriki waliipongeza
Serikali kwa kuwashirikisha wanawake
kwa upana zaidi katika uwezeshaji wa
shughuli za uchimbaji mdogo.
Kufuatia pongezi hizo, nilitamani
pia kupata mtazamo wa washiriki
wa semina ikiwa Sera ya Madini ni
Mkombozi wa wanawake wachimbaji
wa madini kwa kuwa kundi hili ni
mhimili wa maendeleo ya jamii yoyote.
Katika kutafuta jibu la swali hilo,
nilizungumza na wadau mbalimbali,
na hususan wanawake wawili kutoka
Merelani, waliojitambulisha kama Pili
Hussein na Susie Kennedy.
Nilivutiwa kuzungumza kwa kirefu
na Pili Hussein ambae ni mama wa
Mchimbaji madini
mdogo, Pili Hussein
maarufu kama Mjomba
Husein akipokea
mkataba kutoka kwa
Waziri wa Nishati
na Madini, George
Simbachawene wakati
wa mafunzo kwa
waliopata ruzuku awamu
ya pili ya kuendeleza
uchimbaji madini
mdogo. Wengine
pichani kutoka Kushoto
ni Kamishna Msaidizi
wa Madini, Sehemu ya
Leseni, Mhandisi John
Nayopa, Mkurugenzi wa
Usimamizi wa Fedha za
Serikali kutoka Benki
ya Maendeleo ya TIB,
Prisca Changa na Rais
wa Shirikisho la Vyama
vya Wachimbaji Madini
Tanzania (FEMATA),
John Bina. Mafunzo
hayo ya siku mbili
yalifanyika mjini Dodoma
Oktoba 7 na 8, 2015.

makamo, na alikuwa na historia ya


pekee katika uchimbaji wa madini ya
Tanzanite tokea mwaka 1988 katika
eneo la Merelani, Mkoani Manyara.
Pili anasema wakati akianza
shughuli za uchimbaji, jamii kwa wakati
huo iliichukulia shughuli hiyo kuwa ya
wanaume pekee hivyo yeye alilazimika
kujificha kwa kivuli cha mwanaume
akitumia jina la bandia la Mjomba
Hussein.
Nililazimika kuiaminisha jamii
iliyonizunguka katika kazi zangu kuwa
mimi ni mwanaume na siyo mwanamke
ili niweze kukubalika kufanya kazi hiyo,
anasema mama huyo.
Anasema alilazimika kuchanganyika
na wanaume katika mambo mbalimbali
ikiwa ni pamoja na kuvaa mavazi ya
kiume muda wote, kuvuta sigara, na
mambo mengine kadhaa ambayo ni
aghalabu kwa mwanamke kufanya.
Hata jina la Mjomba Hussein lilianza
wakati huo, anasema Pili.
Pili au Mjomba Hussein,
anawakilisha
wanawake
katika
jamii yetu ambao kwa muda mrefu
wamekuwa wakikatishwa tamaa
kutokana na mitazamo hasi ya baadhi ya
watu hivyo kushindwa kufanya shughuli
za kimaendeleo kwa dhana kuwa kazi
hizo zinafaa kufanywa na wanaume tu.
Aidha, kutokana na Sera za miaka
ya nyuma, hasa wakati wa ukoloni
kutotambua rasmi uchimbaji mdogo,
suala la ubaguzi wa jinsia lilikuwa na
nguvu zaidi kwa kuwa uchimbaji ambao
ulionekana kuwa haramu ulihitaji
wanaume wenye kuweza kupambana
na Serikali ilipobidi.
Ni jambo la kutia faraja kuwa Serikali
imekuwa ikipambana na mitazamo
na dhana hizo potofu zilizojengeka
kwa muda mrefu katika jamii yetu

Baadhi ya akina mama ambao ni wachimbaji wadogo wa madini


mkoani Shinyanga wakiwa katika semina kuhusu mfumo mpya wa
huduma za utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online
Mining Cadastre Transactional Portal OMCTP). Kutoka Kushoto
ni Amina Mtoro, Hafsa Issa, Halima Mohamed, Khadija Salum na
Nusura Juma. Semina hiyo ilifanyika hivi karibuni mjini Shinyanga.

kwa kuwajengea mazingira wezeshi


wanawake ili waweze kufanya kazi
mbalimbali za kujiletea maendeleo
pasipo kuwa na hofu ya aina yoyote.
Wizara ya Nishati na Madini
mathalani, imekuwa ikifanya jitihada
za kuwawezesha wanawake kushiriki
katika shughuli mbalimbali zinazohusu
sekta husika ikiwa ni pamoja na
uchimbaji mdogo wa madini.
Katika awamu hii ya pili ya utoaji
ruzuku, Serikali imepanua zaidi wigo
ambapo imetenga takribani Shilingi
za Kitanzania bilioni 7.2 kwa vikundi
111 vya wachimbaji wadogo na watoa
huduma mbalimbali katika sekta ya
uchimbaji madini mdogo ukilinganisha
na Dola za Marekani 500,000 sawa na
takribani Shilingi za Kitanzania bilioni
moja zilizotolewa kwa waombaji 11
katika awamu ya kwanza.
Kwa mujibu wa Kamishna Msaidizi
wa Madini, Sehemu ya Leseni, Mhandisi
John Nayopa, utoaji ruzuku katika
awamu ya pili umehusisha wachimbaji
wadogo pamoja na watoaji huduma

mbalimbali katika sekta husika tofauti


na ilivyokuwa katika awamu ya kwanza
iliyofanyika katika Mwaka wa Fedha
2013/14 ambapo Wizara iliwalenga
wachimbaji madini wadogo pekee.
Mhandisi Nayopa anafafanua zaidi
kuwa, watoa huduma katika uchimbaji
madini mdogo walionufaika na ruzuku
awamu ya pili ni pamoja na vikundi
vya wanawake wanaotoa huduma ya
chakula, kushona nguo kwa wachimbaji
madini na wale wanaojishughulisha na
uongezaji thamani madini, hasa ukataji
na uchongaji madini ya vito.
Aidha, Waziri wa Nishati na Madini,
George Simbachawene wakati akifunga
mafunzo kwa wachimbaji wadogo mjini
Dodoma hivi karibuni aliwapongeza
wachimbaji madini wanawake waliopata
ruzuku awamu ya kwanza na kueleza
kuwa wameonesha mfano mzuri kwa
kutumia vizuri fedha walizopatiwa na
hivyo kuongeza tija kwenye kazi zao.
Alitoa mfano wa mmoja wa
walionufaika na awamu hiyo kuwa ni
kampuni ijulikanayo kama Precision
Dcor inayomilikiwa na mwanamke na
inajishughulisha na uchimbaji wa madini
ya ujenzi yanayoitwa, Tanga stone.
Simbachawene aliwaasa wanawake
wachimbaji kuendelea kufanya kazi
kwa bidii na kuwa mfano wa kuigwa.
Natarajia pia katika awamu hii
wanawake wataendelea kuwa mfano
wa kuigwa. Dhana ya akina mama
wakisaidiwa ni sawa na kusaidia jamii
kubwa, inajitokeza hapa, alisema
Waziri.
Wakati huu ambapo Serikali
imebainisha kwamba Wizara inaendelea
kuweka mikakati mingi ili kuendeleza
wachimbaji wadogo, ni fursa nzuri kwa
wanawake kujitokeza kwa wingi na
kufanya kazi za uchimbaji madini au
utoaji huduma katika sekta husika ili
waweze kunufaika ipasavyo.
Bila shaka Sera ya Madini ni
mkombozi kwa wanawake hawa na
wengine ambao watachangamkia
fursa zilizopo kwenye sekta ya madini.
Shime wanawake wachimbaji, tuendelee
kuonyesha mfano kwa kuisaidia Serikali
kutimiza azma ya kuhakikisha sekta
ya madini inachangia kwa asilimia 10
katika Pato la Taifa ifikapo mwaka 2025.

NewsBulletin

Habari za nishati/madini

http://www.mem.go.tz

MIRADI YA GESI
ASILIA, 2015

TUMEWEZA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete


akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Kituo cha Kuchakata Gesi
Asilia cha Madimba. Kulia kwake ni Waziri wa Nishati na Madini,
George Simbachawene akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,
Halima Dendegu. Kushoto kwake ni Mke wa Rais, Mama Salma
Kikwete. Wengine ni Viongozi mbalimbali wa Kitaifa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete


(katikati) akikagua Kituo cha Kuchakata Gesi Asilia cha Madimba
wakati wa uzinduzi wa mradi wa miundombinu ya kusafirisha na
kuchakata gesi asilia. Kushoto kwake ni Waziri wa Nishati na Madini,
George Simbachawene akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC,
Dkt James Mataragio. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,
Halima Dendegu akifuatiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Kikwete akipewa


maelezo na Meneja Mitambo ya Kuchakata Gesi Asilia, Mhandisi Sultan
Pwaga (aliyenyoosha mikono) kuhusu Mradi wa Kuchakata Gesi Asilia
wa Madimba. Wengine katika picha ni viongozi mbalimbali wa Kitaifa
waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Mradi.

Mtambo wa Kuchakata Gesi Asilia wa Madimba,


Mkoani Mtwara

Habari za nishati/madini

8
Tulipotoka Tulipofika

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Kituo cha Kuchakata Gesi


cha Madimba, chenye uwezo
wa kusafisha Gesi kiasi
cha futi za ujazo Milioni 210
kwa siku, Gesi husafirishwa
kwenda kituoni hapo kwa
njia ya bomba.

1.

Bomba la gesi katika hatua za awali za ujenzi

2.

Mafundi wakifanya kazi ya kuziba maeneo yaliyokuwa


na hitilafu katika bomba la kusafirisha gesi kutoka
Mtwara hadi Dar es Salaam.

3.

Baadhi ya nyumba za Wafanyakazi wa Kituo cha


Kuchataka Gesi Asilia Madimba, Mtwara.

4.

Bomba la gesi likiwekwa chini ya ardhi.

5.

Meli ya Discover Americas 83 ikichoronga visima katika


Kitalu N0.2 kwenye kina kirefu cha maji katika Bahari ya
Hindi.

NewsBulletin

Habari za nishati/madini

http://www.mem.go.tz

TUMEWEZA

MRADI MKUBWA
UMEME WA GESI ASILIA

PICHA 1 na 2: Mitambo ya Kufua Umeme ya Kinyerezi I,


kutokana na Gesi Asilia kutoka Madimba- Mtwara yenye
uwezo wa kuzalisha Megawati 150 za umeme. Mradi wa
Kinyerezi I unaomilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 kupitia
Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), umegharimu kiasi dola
za Kimarekani milioni 183 sawa na shilingi za Tanzania
Bilioni 400. Ujenzi wa Miundombinu ya kusafirisha, kusafisha
na kuzalisha umeme wa Gesi Asilia ulizinduliwa mwaka 2012
na Rais Jakaya Kikwete

AWALI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete akiwa


katika eneo lilipo lango la kuingia katika Mitambo ya Kufua umeme ya
Kinyerezi I, wakati akikagua mitambo hiyo wakati wa uzinduzi wa mitambo
hiyo uliofanyika Oktoba 13, 2015.

AWALI

PICHA 3 na 4: Mitambo ya kufua umeme eneo la Kinyerezi


I, ikiwa katika hatua mbalimbali wakati wa ujenzi wake.

he Government of Tanzania, in
creating
an
enabling
environment for foreign and local
investments, formulated the Mineral Policy
of 1997; enacted the Mining Act of 1998
and major reforms in the mining fiscal
regime which contained generous tax
incentives aimed at attracting both local
and foreign investors in the mining
sector.The measures resulted into
increased large scale exploration and
mining
activities,
including
the
establishment of 7 large scale gold mines
between 1998 and 2009.
However, the Government could not
effectively realize the expected benefits
due to inadequate expertise and
ineffective monitoring of mining
operations. In order to address this
situation, the Government, among other
measures it reviewed the mineral policy,
mining legislation and strengthened

institutional administration. As part of


institutional arrangements, the Tanzania
Minerals Audit Agency (TMAA) was
established in 2009. The Agency is
mandated to monitor and audit large,
medium and small scale mining operations
in order to ensure maximization of
Government benefits from the mining
industry,
thereby
enhancing
socio-economic development.
Key functions of the Agency include
monitoring and auditing of quality and
quantity of minerals produced and
exported by large, medium and small scale
miners in order to facilitate collection of
payable royalty; auditing of revenue
generated, capital investment and
operating expenditure of the large and
medium scale mines for the purpose of
gathering taxable information and
providing the same to the Tanzania
Revenue Authority (TRA) and other

TMAA Chief Executive officer Engineer Dominic Rwekaza talking to reporters


at one of the agency's public awareness seminars

relevant authorities; and monitoring and


auditing environmental management,
environmental budget and expenditure for
progressive rehabilitation and mine
closure.
Since its establishment TMAA has recorded
remarkable achievements as a result of
effective monitoring and auditing of
mining operations in the country. Key
achievements include:

Payments of Corporate Income Tax


(CIT) amounting to USD 419 million
by major mines for the period
covering year 2009 to September
2015. No CIT was paid before TMAA
establishment.

Facilitation of inputs to district


councils hosting mining companies
to enable them with the collection of
Local Service Levy which has
amounted to USD 5.4 million for the
period covering year 2009 to
September 2015.

Royalty payments on building


materials and industrial minerals
whereby strategic audits of such
minerals conducted by the Agency in
collaboration with Zonal/Regional
Mines Offices, enabled the
Government to collect a total of TZS
11.7 billion from medium and small
scale miners for the period covering
June 2011 to September 2015. These
audits which are conducted through
the use of Mineral Sales Vouchers
cover various regions in the country
and are expected to include almost
all regions. Current regions being
covered include Arusha, Coast. Dar es
Salaam, Dodoma, Geita, Iringa,
Kagera, Katavi, Kilimanjaro, Lindi,
Manyara,
Mbeya,
Morogoro,
Mwanza, Mtwara, Rukwa, Ruvuma,
Simiyu, Singida and Tanga.

Royalty payments on gold produced


by mineral processors using vat
leaching technology in Geita, Mbeya
and Mwanza regions. Monitoring of
such activities which is conducted in
collaboration with Mines Offices has
enabled the Government to collect a
total of TZS 5.9 billion for the period

Despite the above achievements, the


Agency continues to work tirelessly in
order to ensure that the mining industry in
Tanzania benefits both the Government
and the mining companies in a win-win
situation. In realizing this, the Agency will
continue to strengthen its monitoring and
auditing of mining operations to meet
Governments expectations and the public
at large.

medium and some small scale


miners.
The Agencys laboratory in Dar es
Salaam, which is equipped with state
of the art equipment and highly
trained personnel, was accredited
with ISO/IEC 17025: 2005 in March
2015 by SADCAS, Botswana (an
international accreditation body for
Eastern and Southern Africa). TMAA
Laboratory offers a wide range of
quality services of mineral analyses at
competitive prices to all stakeholders
in the mineral sector.

Aerial view of one of the mining areas in Tanzania.

covering July 2012 to September


2015. Future monitoring will involve
other regions like Shinyanga and
Singida where such activities take
place.
The Agencys special desks at major
airports (Julius Nyerere International
Airport, Kilimanjaro International
Airport and Mwanza Airport) through
collaboration with other Government
enforcing institutions, intercepted 78
incidents of illegal mineral smuggling
between July 2012 and September
2015. These incidents involved
minerals worth USD 10 million. Some
of the minerals were confiscated after
court hearings and convicts were
fined according to the provisions
under the Mining Act of 2010.
Regarding
environmental
compliance at mining sites,
environmental audits conducted by
TMAA have contributed to a
tremendous
improvement
in
environmental compliance by large,

Minerals Auditing in Tanzania at a Glance

10
Habari za nishati/madini
http://www.mem.go.tz

NewsBulletin

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Habari za nishati/madini

11

12

Habari za nishati/madini

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA


MINISTRY OF ENERGY AND MINERALS

Kwa wadau wa sekta za Nishati na Madini, tembelea kurasa mpya za Wizara kwenye Mitandao
ya Kijamii ya Twitter na Facebook kwa anuani ya Nishati na Madini Karibu tuhabarishane na
tujadili kuhusu sekta za Nishati na Madini kwa maendeleo ya Watanzania wote.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

You might also like