You are on page 1of 19

Usalafi usiwagawe Wanasunnah - Uk 9

huwatoa watu gizani


Mwana mageuzi nguli

Sheikh Al-Amin mazrui: katika Uislamu - Uk 7


ISSN 5618 - N0. 009 BEi: Sh800/- KSH80/- Ush1,200/-

21 shaaban 1436, Jumatatu, juni 8 - 14, 2015

www.islamicftz.org

muswada wa habari

Waislam wadai marekebisho


Hijab, uarabu
vyamnyima
kitambulisho
cha taifa
Na Mwandishi Wetu

ke wa Sheikh mmoja
mashuhuri wa kisunnah
hapa jijini Dar es Salaam
amenyimwa kitambulisho cha uraia kwa kuhisiwa kuwa sio
raia kwa sababu ya asili yake ya uarabu.
Mama huyo ambaye ni mtanzania
halisi alinyimwa kitambulisho yeye na
mtoto wake mmoja huku maafisa wa
Mamlaka ya Vitambulisho ya Taifa
(NIDA) wakimwambia itabidi aanze
mchakato upya.
Mama huyo ambaye asili yake ni
Tanga aliambiwa na afisa mmoja wa
NIDA kuwa kita- inaendelea Uk 5

Masheikh 7 wa uamsho watupwa selo ya adhabu

Uk. 3

Head office, Lumumba Street, Opp: Viwanja vya Mnazi Mmoja, P. O Box 779 Dar es Salaam, Tanzania
Tell: 255 22 2182482/ 255 222184419, Fax: 255 22 2181424, E-mail: info@Binslum.com

21 Shaaban 1436, jumatatu Juni 8 - 14, 2015

habari / tangazo

www.islamicftz.org

Yatima walelewe majumbani - Mkuu MUM


M
NA MWANDISHI WETU

kuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro (MUM), Hajat


Mwantumu Malale ametaka
Waislamu waendelee na utaratibu wa zamani wa kulea yatima majumbani
chini ya usimamizi wa ndugu wa karibu, jambo ambalo litawasaidia kutohisi uyatima wao.
Hajat Malale ametoa wito huo, hivi karibuni alipokuwa akizungumza katika kongamano lililofanyika ukumbi wa DIT, jijini Dar
es salaam, lililoandaliwa na taasisi ya Wanawake wa Kiislamu inayojishughulisha na
kusaidia kuboresha maisha ya watoto yatima
wa majumbani (TAQWA).
Hajat Malale alikuwa ni mgeni rasmi kati-

ka kongamano hilo, ambapo alihimiza Waislamu kushiriki katika mpango wa kusaidia


watoto yatima wa majumbani unaoendeshwa
na taasisi hiyo.
Mpango wa kusaidia watoto wa mitaani
walio majumbani ulianzishwa mwaka 2011,
mwaka ambao taasisi hiyo pia ilianzishwa.
Katika mpango huo, TAQWA ilipita majumbani kuwasajili watoto na kuanza kuwasaidia
kielimu na kiafya, wakiwa wanalelewa na
jamaa zao.
Baada ya kuwasajili watoto hao, TAQWA
inatafuta mdhamini ambaye atakuwa anatoa
shilingi 55,000 kila mwezi kwa ajili ya kumhudumia mtoto mpaka amalize elimu ya
msingi, huku fedha hizo zikitumika kumlipia
ada, kununulia sare za shule, chakula, vitabu

TOLEO MAALUM:
Gazeti lako la Imaan, Ijumaa ya Juni 12,
2015 litachapisha toleo maalum la Mwezi
Mtukufu wa Ramadhan litakalochambua
mafundisho na masuala mbali mbali
kuhusiana na Ramadhan.
Ili kufanikisha
toleo hilo maalum, tunakaribisha ushiriki
wa watu binafsi, taasisi, kampuni, balozi na
misikiti
mbalimbali
kwa kutoa
makala na matangazo.

Kwa mawasiliano zaidi, tupigie:


0786 779 669, 0778 559 944
Email: imaanmedia3@gmail.com

na vifaa vingine vya shule.


Hajat Malale alisema: Unaweza
kuona kumchangia mtoto yatima
55,000 ni nyingi, lakini mbona mnatoa fedha nyingi kuchangia kitchen
party na send off na kununua nguo za
gharama bila kukumbuka kuwa hiyo
hela ukimpa yatima futari au kumsomesha ni amali yako itakayokuokoa
kesho akhera.
Naye Mkurugenzi wa TAQWA,
Dr.Salha Mohammed, alisema uchunguzi uliofanywa na taasisi yake unaonesha kuwa, watoto yatima wanaolelewa vituoni wanaathirika kisaikolojia na kujiona kama wapo jela
ya watoto, kwa sababu hawapati
mapenzi ya mama, kwani mama mmoja anayeendesha kituo hicho hawezi
kuhudumia na kuonesha mapenzi kwa

watoto wengi. Akizungumzia mafanikio ya taasisi tangu TAQWA ianzishwe,


Hajat Salha alisema, walianza na wadhamini 11 mwaka 2011, lakini mpaka
sasa wameongezeka hadi 68 wakihudumia watoto 108. Pia alisema,
TAQWA inatarajia kuanzisha mpango
wa kuwadhamini watoto yatima walioko sekondari.
Kwa upande wake Ukhti Khadija
Ally amesema, Quran na Sunnah za
Mtume zimehimiza kulea yatima
akinukuu Quran (93:9).
Tukumbuke Mtume wetu Muhammad alikuwa yatima baada ya kufiwa na baba na mama yake katika
umri mdogo, na hakuwahi kulelewa
kwenye kituo, na ndio maana tunahimiza watoto yatima tuwalee majumbani mwetu. Alisema Ukhti Khadija.

Gazeti jipya la kiislamu lazinduliwa

Na Khalid Omary
yombo vya habari vya Kiislam
vimezidi kuongezeka baada ya
kuzinduliwa kwa gazeti jipya la
Iqra, (Hoja kwanza), Ijumaa iliyopita katika msikiti wa Mtambani, Kinondoni jijini Dar es salaam.
Wakizungumza katika uzinduzi huo
Imam wa msikiti wa Mtambani, Sheikh
Suleiman Abdallah aliishukuru bodi ya Iqra
Media kwa kufanya uzinduzi katika msikiti
wake na kusema, kwa sasa Waislam wataendelea kupata habari na elimu kupitia vyombo vya Kiislam vinavyoongezeka kwa kasi.
Tulikuwa na kilio katika suala la elimu,
tunafurahi tumepiga hatua kubwa kwa
kuzinduliwa kwa gazeti hili (Iqra). Tunatumai tutapata elimu kubwa, alisema Sheikh
Abdallah.
Naye, Mwenyekiti wa bodi ya Iqra Media, Bilal Abdul-aziz amewataka Waislam

waweze kuviunga mkono vyombo vya Kiislam, kwani hakuna asiyekuwa Muislam
atakaeweza kutoa msaada zaidi ya wao
wenyewe.
Abul-aziz alisema: Vyombo vya habari
vya Kiislam vimekuwa na muamko
mkubwa hasa baada ya kujitokeza kwa redio Imaan, tunahitaji ushirikiano kutoka
kwa Waislam ili tuweze kufika mbali.
Kwa upande wake, Sheikh Nurdin Kishk,
mdau mwingine wa gazeti hilo, amewataka
Waislam wasome fani ya habari, kwa sababu wengi wa wanaosoma fani hiyo si Waislam na ndiyo maana Uislam unachafuliwa
na vyombo vya habari ulimwenguni.
Gazeti la Iqra linatolewa na Iqra Media,
litakuwa likitoka kila Ijumaa kwa bei ya
shilingi 800 likisheheni habari na makala
za dini ya Kiislam na jamii kwa ujumla zinazoandaliwa na masheikh mbalimbali pamoja na wanahabari wenye uzoefu.

Amiri wa Vijana Knjaro ahimiza kujiandikisha kupiga kura

Na bahati chume
miri wa Jukwaa la Vijana wa Kiislamu Mkoa wa Kilimanjaro, Abdalah Muhammed amewakumbusha Waislamu Mkoani Kilimanjaro kujitokeza kwa wingi kujiandisha
kwenye daftari la kudumu la wapiga kura
pindi muda utakapo wadia.
Akizungumza na waandishi wa habari,

nyakati za swala

Muhammed alisema ili vijana wapate frusa


ya kupiga kura na kuchagua viongozi katika
uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba
mwaka huu wa madiwani, wabunge na rais
ni lazima kujiandikisha katika daftari kama
wapiga kura. Alisema Waislamu wamekuwa wakipuuza jambo hilo na kwamba
hiyo ni hatari kwani wanapoteza haki zao
kama watanzania.
08 juni - 14 juni, 2015

Na. MJI ALFAJR DHUHUR ASR MAGHARIB


1
DAR ES SALAAM
11:16
6:22
9:44 12:15
2 ZANZIBAR
11:15
6:22
9:45 12:16
3 TANGA
11:17
6:26
9:49 12:22
4
MOROGORO
11:27
6:40
9:52 12:22
5
MTWARA
11:23
6:23
9:42 12:09
6 ARUSHA
11:22
6:35
10:00 12:34
7
DODOMA
11:27
6:35
9:58 12:29
8
MBEYA
11:43
6:47
10:08 12:37
9 KIGOMA
11:50
6:59
10:22 12:55
10
MWANZA
11:34
6:48
10:12 12:47
11 KAGERA
11:46
6:57
10:20 12:53
12 TABORA
11:39
6:48
10:11 12:43
13
SHINYANGA
11:36
6:47
10:11 12:45
14
SINGIDA
11:33
6:41
10:04 12:36
15
IRINGA
11:36
6:39
9:59 12:28

ISHA
1:25
1:26
1:32
1:32
1:20
1:44
1:39
1:47
2:05
1:57
2:03
1:53
1:55
1:46
1:38

21 Shaaban 1436, jumatatu Juni 8 - 14, 2015

habari

www.islamicftz.org

Masheikh 7 wa uamsho watupwa selo ya adhabu


Baadhi ya
viongozi na
wafuasi wa
Uamsho wakiwa
mahakamani.

NA MWANDISHI WETU

ongozi wa gereza la Segerea umeamuru watuhumiwa saba (7) wa ugaidi


wa Jumuiya ya Uamsho
na Mihadhara ya Kiislam ya Zanzibar (JUMIKI) kutupwa katika mahabusu maalum ya adhabu kwa kosa
la kugoma kula.
Uamuzi wa kuwapeleka watuhumiwa hao selo maalum ya adhabu
ulichukuliwa na uongozi wa gereza
hilo baada ya pande hizo mbili
kushindwa kuafikiana katika mkutano ulioandaliwa ili kupata suluhu
ya mgomo wa kula, ambao masheikh
hao waliuanza wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa Ally Mbaruku,
Katibu wa Kamati ya Maafa, Shura
ya Maimamu (T), katika kikao hicho, maaafisa wa gereza hilo walijaribu kuwashawishi masheikh hao

kuacha mgomo wakiwahakikishia


kuwa madai yao yanaendelea kushughulikiwa, lakini masheikh hao walikataa.
Kwa mujibu wa Mbaruku, ambaye aliwatembelea masheikh hao
huko gererani na kuonana na Sheikh
Farid Hadi siku ya Ijumaa, alisema
masheikh waliwaambia viongozi wa
magereza kuwa, hawaoni dalili za
madai yao kushughulikiwa na
kwamba msimamo wao wa kuendelea kugoma upo pale.

Hapo ndipo uongozi wa magereza ulipoamua kuwapeleka selo ya


adhabu, ambapo Sheikh Farid Hadi
na Mselem Ally wamewataka Waislam kuzidisha dua kuwaombea
masheikh hao.
Gazeti la Imaan lilipowatafuta
mawakili wa masheikh hao, Abdallah Juma, Abdulfatah Ali na Abubakar Salum walithibitisha kusikia
taarifa hizo kupitia njia ya ujumbe
mfupi na kwamba wanatarajia kulifuatilia suala hilo na kulitolea ufa-

fanuzi wake baada


ya kuonana na wateja wao siku ya
Jumatatu ya Juni 8 katika mahakama ya kisutu ambako kesi yao itatajwa tena.
Naye, Mkuu wa Gereza la Segelea,
Afande Kiyangi Abdallah, alipopigiwa hakuwa tayari kutoa ushirikiano
uliotarajiwa, akidai kuwa yeye si
msemaji wa Jeshi hilo.
Akizungumzia sakata hilo katika
mtazamo wa kisheria, wakili wa kujitegemea Juma Nassoro alisema,

kitendo cha kususia kula na kunywa


ni jitihada za masheikh hao kuonesha
hisia zao kwa ulimwengu juu ya vitendo
wanavyofanyiwa na kwamba ni njia nzuri
ya kufikisha ujumbe ili hatua ziweze
kuchukuliwa.

kitendo cha masheikh hao kugoma


kula na kunywa kisheria si makosa
ambayo unaweza kuhojiwa mahakamani.
Wakili Juma Nassoro aliongeza
kuwa, kitendo cha kususia kula na
kunywa ni jitihada za masheikh hao
kuonesha hisia zao kwa ulimwengu
juu ya vitendo wanavyofanyiwa na
kwamba ni njia nzuri ya kufikisha
ujumbe ili hatua ziweze kuchukuliwa.
Kugoma kula na kunywa si kosa
kisheria, ni haki ya mtu kujieleza juu
ya matatizo yanayowasumbua huko
gerezani. Ni kama wanaonesha hisia
zao kwa ulimwengu juu ya uonevu
wanaofanyiwa ili hatua ziweze kuchukuliwa , Wakili Nassoro alisema.
Hata hivyo, wakili huyo alisema
kwa taratibu na kanuni za uendeshaji za magereza, kugoma kula na
kunywa inaweza kuwa ni kosa na
kwamba adhabu yake huenda mtu
akabadilishiwa gereza, lakini hawezi
kushitakiwa mahakamani.
Masheikh wa uamsho walianza
mgomo wa pili wa kususia kula na
kunywa katikati ya wiki iliyopita
wakishinikiza madai yao kwa serikali yapatiwe ufumbuzi mapema ili
kuondokana na adha wanayoipata.
Masheikh hao wamekuwa wakilalaamika kesi yao kupigwa danadana, ambapo mpaka sasa tayari
masheikh wapatao 23 wameshakaa
gerezani takriban mwaka mmoja
bila ya kesi zao kupiga hatua ya maana.
Waislamu hao pia wanapinga
kushtakiwa upande wa Tanzania
bara, wakati makosa yao yalitendeka
katika ardhi ya Zanzibar. Wanadai
kesi hiyo irudishwe Zanzibar, kwani
Zanzibar ni nchi ambayo ina mahakama, magereza kama ilivyo Bara.
Mbali na madai hayo, pia
masheikh hao wanadai kutaka
kukutana na wanasheria wakuu wa
Tanzania bara na Zanzibar ili kusikilizwa kilio chao, hadi sasa madai
hayajatimizwa. Pia masheikh hao
wamelalamikia mateso wanayoyapata gerezani, ambapo wiki iliyopita
walimwandikia Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kumuomba awasaidie.

Waislam nao wadai marekebisho muswada wa habari


KHALID OMARY NA
SELEMANI MAGALI

aislam nchini wameitaka serikali kuacha


kubana uhuru wa kutoa na kupokea habari
kwa kutunga sheria kali zinazokandamiza uhuru huo, hususan katika
kipindi hiki cha kuelekea kwenye
uchaguzi mkuu.
Masheikh na wamiliki wa vyombo vya habari vya Kiislam wameliambia gazeti hili kuwa, muswada
wa Sheria ya Vyombo vya Habari wa
2015 ni kandamizi na unapingana
na Katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania pamoja na mafundisho
ya Mtume Muhammad (Rehma na

amani ziwe juu yake).


Mwenyekiti wa taasisi ya The Islamic Foundation inayomiliki vyombo vya habari vya gazeti Imaan,
radio na Tv Imaan, Aref Nahdi,
amesema mswada huo unabana
haki za msingi za raia za kutoa,
kupokea na kusambaza taarifa
pamoja na kuingilia sera za ndani za
vyombo mbalimbali vya habari.
Nahdi alisema, vyombo vya
habari vya Kiislam vitaathirika zaidi
kwa sababu pamoja na kuzingatia
sheria za nchi, vinatoa habari kwa
misingi ya dini ya Mwenyezi Mungu
na mafundisho ya Mtume Muhammad (Rehma na amani ziwe juu
yake), na si vinginevyo.
Nahdi alikuwa akirejea ibara ya

14(b)(iv) ya mswada huo inayotaka


vyombo vya habari vya utangazaji
(runinga na radio), kujiunga na
kituo cha runinga cha taifa na kile
cha radio kwa ajili ya taarifa ya
habari kila siku ifikapo saa 2 usiku.
Nahdi alisema: Vyombo vyetu
sisi Waislam vinazingatia maadili
maalum kwa mujibu maagizo ya Allah. Akitoa mfano, alisema ni haramu na mwiko mkubwa kwa vyombo
vya habari vya Kiislam kuonesha
watu wamevaa hovyo, sherehe za
ngoma, matangazo ya pombe na
riba.
Kwetu vitu hivyo ni haramu.
Muswada huu utatuletea madhara
na ni kinyume na dini yetu, na kama
ukipita utatunyima haki yetu ya

msingi ya kikatiba ya kuabudu, aliongeza Nahdi.


Kwa upande wake, Msemaji wa
Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, Sheikh Rajab Katimba alisema, serikali inataka kurudisha nyuma maendeleo na kuipeleka Tanzania miaka ya 70 na 80 ambako vyombo pekee vya habari vilikuwa ni
vya serikali, chama tawala na jumuiya zake.
Sheikh Katimba alisema: Vyombo vya habari katika kipindi kama
hiki ni lazima viachwe huru vifanye
kazi yake na kwamba kuwadhibiti
wanahabari ni kinyume na kanuni
za kidemokrasia.
Naye mchambuzi wa masuala ya
siasa katika Shirika la Utangazaji la

Uingereza, (BBC) Sheikh Muhammad Issa, amepinga muswada huo


kwa sababu unafinya uhuru wa kujieleza kama Katiba ya Jamhuri ya
Muungano inavyoelekeza.
Mchambuzi huyo aliongeza kwa
kusema, kupitishwa kwa muswada
huo kutaleta mgongano mkubwa
wa kisera miongoni mwa vyombo
vya habari kutokana na ukweli kuwa
kila chombo kina utaratibu wake wa
uendeshaji.
Katika hatua nyingine Sheikh
Issa ametoa wito kwa Serikali kuwa
sikivu pale wadau wanapoibua hoja
za kukosoa miswada ya sheria badala ya kupuuzia kwani hali hiyo inaweza kupelekea uvunjifu wa amani.

21 Shaaban 1436, jumatatu Juni 8 - 14, 2015

www.islamicftz.org

tujikumbushe
NA YUSUFU AHMADI

arehemu Bibi Titi Mohammed


anatajwa kuwa miongoni mwa
watu waliokorofishana vikali na
Mwalimu Julius Nyerere, Rais wa
kwanza wa Tanzania, kuhusiana na suala la Jumuiya ya Waislamu ya Afrika Mashariki
(EAMWS).
Inaelezwa kuwa katika miaka ya 1960 kulizuka mgogoro mkubwa miongoni mwa Waislamu na kuhusisha baadhi ya vyombo vya serikali. Mgogoro huo ulitokana na kampeni iliyoanzishwa kipindi hicho ya kuivunja Jumuiya
ya EAMWS. Bibi Titi yeye alikuwa ni Makamu
wa Rais wa Jumuiya hiyo. (Rejea: Maisha na
Nyakati za Abdulwahid Sykes 1998 kilichoandikwa na Mohammed Said).
Mgogoro huo unatajwa kuanza mara baada
ya kijana mmoja aliyejulikana kama Adam
Nasibu, mwalimu wa shule ya msingi na aliyekuwa Katibu wa EAMWS kule Bukoba kutangaza maandamano kwenda kwenye ofisi ya
chama cha TANU ya mkoa huo kumuunga
mkono Mwalimu Nyerere na sera yake mpya
ya Ujamaa iliyokuwemo kwenye Azimio la
Arusha.
Inadaiwa kuwa, Nasibu alisema sera mpya
ya Ujamaa ni sawa na mafundisho ya Quran
Tukufu na kwenda mbali zaidi kwa kutoa
miongozo kwa viongozi wa Kiislamu wa Bukoba kufafanua Azimio la Arusha. Ni huyu
ndiye aliyeongoza kampeni ya kuivunja
EAMWS.
Katika kampeni hiyo, vyombo vya habari
vya chama cha TANU na vile vya serikali, redio
na magazeti, vilitumika kuishambulia
EAMWS kwa kutumia baadhi ya Waislamu.
Hoja kubwa iliyotumika kuishambulia
EAMWS na kudai ifutwe ni uwepo wa Aga
Khan kama mlezi wa jumuiya hiyo.
Inaaminika kuwa moja kati ya watu walioshiriki katika kueneza propaganda hizo dhidi
ya EAMWS ni rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa akitumia gazeti la Nationalist,
ambapo aliandika chanya habari yoyote ya
Adam Nasibu. Ikulu ilikuwa kimya wakati
haya yakifanyika.
Kutokana na EAMWS kupitia misukosuko
mingi inaelezwa kuwa Makamu wa Rais wa
EAMWS hapa nchini, Bibi Titi Mohammed
akishirikiana na Rais wake, Tewa Said Tewa,
wakakusanya nguvu zao ili kuiokoa jumuiya
hiyo.
Katika mzozo huo, marehemu Bibi Titi Mohammed alisimama thabiti kutetea uhai wa
EAMWS. Katika kikao kimoja Bibi Titi alimkosoa vikali mwalimu Nyerere kwa kile alichodai alikuwa anachangia kuiua jumuiya hiyo
iliyokuwa muhimu kwa maendeleo ya Waisla-

Bibi Titi, Nyerere


walipokorofishana
kwa ajili ya EAMWS

mu Afrika Mashariki (rejea kitabu hicho hicho


cha Mohammed Said).
Bibi Titi aliwahi kutoa maneno makali katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya TANU
baada ya wanakamati wawili, Selemani Kitundu na Rajab Diwani, kuomba imjadili Aga
Khan na nafasi yake kama mlezi wa EAMWS.
Kitundu na Diwani walidai kuwa wana
habari Aga Khan anataka kuitawala Tanganyika kupitia Waislamu na EAMWS. Kwa ajili hii

basi wakapendekeza EAMWS ifungiwe. Nyerere aliwaunga mkono, lakini Bibi Titi akasimama kishujaa dhidi yao.
Biti Titi aliwaambia Diwani, Kitundu na
Nyerere hakuna kati yao aliyekuwa na haki ya
kuifungia EAMWS, kwani taasisi hiyo ilikuwepo kabla ya TANU ikitoa huduma kwa Waislamu, na kuongeza kuwa, kama walikuwepo
watu ndani ya EAMWS walikuwa wanakwenda kinyume na sheria basi wapelekwe mahakamani na sheria ichukue mkondo wake.
Inasemekana hasira zilipanda na kukawa
na kutoleana maneno kati ya Bibi Titi na Nyerere. Bibi Titi akamwambia Nyerere yeye hamuogopi yeyote ila Allah. Haya ni kwa mujibu
wa kitabu Maisha na Nyakati za Abdulwahid
Sykes - 1998 cha Mohammed Saidi.
Inadaiwa kuanzia hapo Mwalimu Nyerere
akajenga chuki dhidi ya Bibi Titi Muhammed
na mwaka 1965, yeye na Tewa Said Tewa wakapoteza viti vyao vya ubunge, hali ambayo inaaminika Mwalimu Nyerere alihusika pakubwa.
Hali hiyo haikumkatisha tamaa marehemu
Bibi Titi na mwenzake Tewa Said, kwani mwaka 1968, wakati njama za kuiua EAMWS zikiendelea kushika kasi, walimfuata Mwalimu
Nyerere ili kuonesha masikitiko yao ya namna
radio ya Serikali na magazeti ya TANU yalivyokuwa yakiishambulia jumuiya hiyo ya Kiislamu.

Inaaminika kuwa moja kati ya watu


walioshiriki katika kueneza propaganda
hizo dhidi ya EAMWS ni rais wa awamu ya
tatu, Benjamin Mkapa akitumia gazeti la
Nationalist, ambapo aliandika chanya
habari yoyote ya Adam Nasibu. Ikulu
ilikuwa kimya wakati haya yakifanyika.

Wakati Bibi Titi na wenzake wakimtahadharisha Nyerere kwa kuacha vyombo vya serikali kuchochea mgogoro ndani ya EAMWS,
Nyerere aliwachukulia akina Bibi Titi kama
maadui na kuwaambia uso kwa uso Mmeamua kunipiga vita, jiandaeni. (Rejea kitabu cha
Historia ya Kuhuisha Uislamu Tanzania kilichoandikwa na Islamic Propagation Centre).
Vita dhidi ya EAMWS ilinoga zaidi baada
ya Makamu wa Rais wa Tanzania, Abeid Amani Karume, kukiita chombo hicho kuwa ni cha
kinyonyaji. Ikikabiliwa na mashambulizi kutoka kila upande, hatimaye mnamo mwaka 1968
EAMWS ilipigwa marufuku kwa amri ya Nyerere na mali zake zote kukabidhiwa BAKWATA iliyoundwa na serikali, ambayo imekuwa
ikidai siku zote kuwa haina dini. Tangu hapo
BAKWATA imeendelea kuwapo na kuwa
chanzo cha madhila na udhalili wa Waislamu
Tanzania.
Katika kumuelezea Bibi Titi, katika makala
yake aliyoiita, Biti Titi Mohammed and The
Historical Context of the Time in Tanzania iliyotoka katika Awaaz Magazine toleo 3, juzuu
ya 11; Joseph Lwannia alimsifu kuwa alikuwa
Muislamu mwenye muono, kiongozi shupavu,
mwenye muelekeo uliodhahiri na aliyejali
mustakabali wa nchi yake, huku akiwa mfuasi
wa demokrasia yenye ladha ya ubepari.
Mwandishi huyo anaendelea kuandika
kuwa, tofauti za kiimani na kisiasa baina ya
Mwalimu Nyerere aliyekuwa mfuasi mkubwa
wa Ukatoliki na Ujamaa, na Bibi Titi mfuasi
wa Uislamu zilileta mapambano makubwa
katika chama cha TANU na hivyo kutishia
kukigawa chama.
Bibi Titi kupotea katika ramani ya Tanzania:
Mwaka 1969 Bibi Titi Mohammed
alikamatwa na mwaka uliofuata alifikishwa
mahakamani kwa madai ya kupanga njama ya
kutaka kuipindua serikali ya Mwalimu Nyerere
kwa kushirikiana na wenzake sita, akiwemo
Michael Kamaliza aliyekuwa Waziri wa Ulinzi.
Katika kesi hiyo, Bibi Titi alikuwa ni mwanamke pekee na hatimaye alipatikana na hatia
na kuhukumiwa kifungo cha maisha. Mwaka
1972 alipata msamaha wa rais Julius Nyerere.
Baada ya kutolewa jela, Bibi Titi Mohammed
aliishi maisha ya upweke. Mume wake alimtelekeza wakati wa kesi, huku marafiki zake
wengi wakimkimbia.
Mnamo mwaka wa 1991, wakati Tanzania
ikisherekea miaka 30 ya uhuru, Bibi Titi alitajwa kwenye makaratasi ya chama tawala kama
Shujaa wa kike aliyepigania uhuru wa Tanganyika. Na Novemba 5,
2000 Bibi Titi Mohammed alifariki katika
hospitali ya Net Care Hospital mjini Johannesburg ambapo alikuwa akitibiwa.

kutoka misikitini
Uislam. Alisema, ulimwengu wa sasa unakua kwa
kutegemea vyombo vya habari, kwani vinaweza
kufanya uongo kuwa kweli na kweli kuwa uongo, na
hata kama Mtume angekuwepo angetumia njia ya
vyombo vya habari kufikisha ujumbe wa Mwenyezi
Mungu. Sheikh Kishk aliongeza kuwa, kwa sasa
vyombo vya habari ndio silaha muhimu ya kuendeleza jambo lako na kama hutoitumia vizuri silaha
hiyo utakuwa ni mwenye kupata hasara. (KHALID
OMARY)

Kishk aviasa vyombo


vya habari vya Kiislam

Waislamu wazidishe dua kwa


yanayowasibu: Sheikh Wangara

Vyombo vya habari vya Kiislam vimetakiwa kuwa nyenzo ya kwanza ya kuuendeleza na
kuutangaza Uislam na sio kuwa chanzo cha malumbano miongoni mwao.
Hayo yalisemwa na Sheikh Nurdin Kishk wakati akitoa khutba ya swala ya Ijumaa katika
msikiti wa Mtambani uliopo Kinondoni jijini Dar es salaam. Sheikh Kishk alisema, endapo
kama vyombo vya Kiislam vitatumika katika njia hiyo, basi Uislam utasonga mbele. Hata
hivyo, badala ya kuutangaza Uislam, vyombo hivyo vimekuwa viwanja vya kuushambulia

Waislamu nchini wamehimizwa kuzidisha dua


kutokana na matatizo yanayowasibu, kwani kumuomba Allah ni ibada kubwa na miongoni mwa
sifa za mitume (amani iwe juu yao) na wema
waliotangulia.
Nasaha hizo zimetolewa na Sheikh Abuu Mussa

Wangara katika khutba ya ibada ya swala ya


ijumaa iliyoswaliwa msikiti wa Mtoro, Kariakoo,
jijini Dar es salaam, na akabainisha tatizo kubwa
lililopo katika umma wa Waislam ni kutotenga
muda kwa ajili ya kufanya maombi kwa Allah.
Sheikh Wangara amewataka Waislam kujilazimisha kuwa wanyenyekevu wanapoomba dua
ili kuzitakasa ibada zao, kwani mja mwenye akili
ni yule anayejitahadharisha na siku ya kukutana
na mola wake (Siku ya Qiyama) akinukuu aya za
Quran : Na ukipata faragha,fanya juhudi(94:7).
Na mola wako mlezi ndio mshughulikie(94:8).
Akifafanua madhila yanayowakumba Waislam, Sheikh Wangara amesema,kwa miaka 25
sasa Waislam wamekuwa na madai kadha wa
kadha kwa serikali, yakiwemo kupatiwa mahakama ya kadhi, lakini pia Tanzania kujiunga na
Shirikisho la nchi za Kiislam Ulimwenguni bila
mafanikio, hivyo kuwataka Waislam kuutumia
mwezi mtukufu wa Ramadhan kumlilia Allah ili
awatatulie matatizo hayo. (YUSUPH AMIN)

21 Shaaban 1436, jumatatu Juni 8 - 14, 2015

habari / tangazo

www.islamicftz.org

Uamsho waendeleza
daawah Segerea
Mwingine aliyesilimishwa asimulia
Alikuwa Gift Robert, sasa ni Issa Robert
Na Mwandishi wetu

asheikh wa Jumuiya ya Uamsho wanaotuhumiwa katika


kesi ya ugaidi wanaendeleza
daawah ndani ya gereza la
Segerea, ambapo mmoja kati ya waliosilimu Issa Kaiya Robert (22) ambaye kwa
sasa ameachiwa huru amesimulia kuhusu
harakati za masheikh hao.
Simulizi ya Robert inakuja takriban
wiki mbili tu baada ya kijana mwingine,
Nassor Emmanuel Malaja, kutoa ushuhuda katika Kongamano lililofanyika msikiti
wa Kichangani juu ya kazi nzuri ya
daawah ya masheikh hao.
Akizungumza na gazeti la Imaan, Issa
amesema, anajisikia faraja kuingia katika
nuru ya Uislam, kwani dini hiyo ni ya kweli.
Akifafanua daawah inayofanywa na
masheikh wa Uamsho, Issa amesema
masheikh hao wamekuwa wakifanya
juhudi kubwa ya kuwaingiza watu kwenye
nuru ya Uislam kupitia tabia na mawaidha mema kila wapatapo nafasi, licha ya
kunyimwa fursa na kubanwa na uongozi

wa gereza.
Hata hivyo, kwa uwezo wa Allah
masheikh hao wamekuwa wakitumia
muda mfupi kufikisha ujumbe wa dini ya
Kiislamu na kupata kundi kubwa la watu
wanaosilimu, ambapo kwa mujibu wa kijana Nassor aliyesilimu majuma kadhaa
yaliyopita, mpaka sasa wameshasilimisha
zaidi ya watu 15, wakiwemo watu wazima,
vijana na watoto.
Hata hivyo, Nassor alisema, mara nyingi wanaosilimu wanachukiwa na wenzao.
Watu wengi wanaosilimu huitwa majina
mabaya na kuhusishwa na tuhuma za
ugaidi na vile vile kunyimwa fursa ya kufanya ibada ya swala, alibainisha Nassor.
Akielezea sababu za kusilimu kwake,
kijana Issa Robert amesema, ukarimu na
ustaarabu uliooneshwa na masheikh kwa
mwezi mmoja aliokuwa mahabusu ulipelekea kutaka kuifahamu dini hiyo kiundani.
Alisema, baada ya kuvutiwa na tabia
nzuri za masheikh hao aliwafuata na
wakamlingania kwa njia ya kuoanisha vitabu vya Quran na Biblia, na hapo ndipo
alipogundua ukweli.

Issa Kaiya Robert.

Hijab, uarabu vyamnyima


kitambulisho cha taifa
mbulisho
chaka na cha mwanawe vimekwama na kwamba sasa anapaswa kujaza fomu upya.
Mama huyo na mwanawe
walipitia michakato yote
mwaka 2013 pamoja na
mumewe ikiwemo kujaza
fomu, kuwasilisha vyeti vyake,
kuwasilisha kitambulisho cha
mpiga kura, kuchukuliwa
alama za vidole, kupigwa
picha na hata kurekebisha
maelezo yaliyokuwapo katika
fomu.
Akiongea na gazeti hili,
mume wa mama huyo, ambaye yeye alishapata kitambulisho chake licha ya kuanza
mchakato huo pamoja, ameliambia gazeti la Imaan kuwa
ameshutushwa na uamuzi
huo wa NIDA.
Walimwambia mke wangu uraia wako unatiliwa shaka
kwa hiyo hutopewa kitambulisho chako hadi uraia wako na
wanao uhakikiwe na kujaza
fomu upya, Sheikh huyo aliliambia Imaan. Kadhia hiyo
pia imemkuta mfanyakazi wa
ndani wa familia hiyo ambaye
yeye anafanana na wasomali
na huvaa hijab.
Naye mwanamke
mwingine wa kiislamu
mwenye asili ya Kondoa alidai
inatoka Uk 1

alipokwenda kuchukua kitambulishao chake aliulizwa,


mbona anaonekana kama
msomali, swali ambalo lilimshangaza kwani maelezo yake
yote alishayatoa na walikuwa
nayo. Mwanamke huyo alidai
kwamba hawakuacha kumhoji mpaka alipowaeleza
kwamba yeye ni kutoka kabila
la Wasi kutoka Kondoa ndipo
wakampatia kitambulisho
chake.
Wanawake wote hawa
wawili walikuwa wamejipamba kwa mavazi ya staha
kamili ya hijabu ya kiislamu.
Hali hii ya Watanzania
Waislamu wenye asili ya kiarabu kutiliwa shaka uraia
wao zinakuja wakati raia wengine wakihudumiwa pasina
kutiliwa shaka jambo ambalo
linaonesha kukosekana kwa
usawa na ni hatari kwa usalama wa taifa.
Kumbe watu wa kutiliwa
shaka ni Waislamu tu, basi
adui akikusudia ubaya kwa
nchi yetu anachotakiwa kufanya ni kutojipamba kwa
mavazi wala muonekano wa
kiislamu, Sheikh huyo alilalamika.
Sheikh huyo aliongeza kwa
kusema: Maswali ambayo
Waislamu tunajiuliza, hivi

Mtanzania ni nani? Ni yule


mweusi tii kama mkaa? Kuna
haja gani kumnyima mtu haki
yake kwa mashaka tu?
Dosari hizi za kutilia shaka
watu kwa kuwa na ngozi nyeupe zimeripotiwa maeneo
maeneo yote ya Tanzania ambako zoezi hili limekwishaendeshwa au linaendelea kuendeshwa hususan
mikoa ya Waislamu wengi
ikiwemo Tanga, Zanzibar,
Morogoro na Pwani na kupelekea baadhi ya watu kuhisi
kuna hujuma na udini dhidi
ya Waislamu. Huko Lindi na
Mtwara hali ni hiyo hiyo
kwani ni maeneo ya waislamu
wengi.
Zoezi la kuandikisha watu
kwa limekwishafanyika katika mikoa ya Dar es Salaam,
Pwani, Lindi, Mtwara, Morogoro, Tanga na Visiwani
Zanzibar ambapo watu zaidi
ya mioni 6.1 wamekwishaandikishwa hadi sasa.

Afyais natural
source of sweet
drinking water
from underground stream
which is blended
with essential
minerals to support and aid perfect metabolism.

WATERCOM LIMITED
P.o. Box 20409, Plot N.4005, Kisarawe11 area
Temeke,Daresalaam, Tanzania
www.watercomtz.com, E-mail:info@watercomtz.com

21 Shaaban 1436, jumatatu Juni 8 - 14, 2015

hutolewa na kuchapishwa

tahariri / uchambuzi

The Islamic Foundation,P.O.Box 6011 Morogoro, Tanzania,E-mail: imaanmedia3@gmail.com


mhariri mtendaji: 0715 559 944, Mhariri: 0786 779 669, afisa masoko: 0785 500 502
TOVUTI: www.islamicftz.org

Vyombo vya habari viwe faraja kwa umma wa kiislamu

wishoni mwa juma lililopita umma wa waislamu wa Tanzania ulipata mgeni katika sekta
ya habari baada ya ujio wa gazeti
jipya la Iqra hatua inayofanya idadi
ya vyombo vya habari vya kiislamu
kwa upande wa magazeti kufikia zaidi ya matano (5) ukijumuisha yale ya
awali ambayo ni Annur,Alhudaa,Kisiwa na Imaan.Hiyo ni hatua ya kupongezwa na ni faraja kwa
umma wa kiislamu.
Kama inavyofahamika suala la
upashaji habari ni moja kati ya nyenzo muhimu katika kukabiliana na
propaganda chafu halikadhalika
ubunifu wa ajenda hasi zinazolenga
kuuchafua uislamu ambazo zimekuwepo tangu na tangu tokea enzi za
manabii na mitume.
Ukilinganisha na vyombo visivyo
vya kiislamu hali ya mambo haiko
tofauti sana hata katika vyombo vya

habari vya kiislamu kwani misingi ya


falsafa na maadili ya tasnia ya habari
hivi leo imejikita katika mizizi ya
itikadi na falsafa za magharibi ambazo lengo lake ni kuangazia soko
zaidi kuliko maslahi ya umma hali iliyodumu tangia kuanzishwa tasnia
ya uandishi wa habari (press) mnamo karne ya 15 na mwanzoni mwa
karne ya 16.
Lakini tukiwa kama
waislamu,tunapaswa kujenga
mshikamano ili kufanikisha lengo la
kuwepo kwetu hapa dunia kwani Allah Taala ametutaka kufanya hivyo,
Na shikamaneni kwa Kamba ya
Mwenyezi Mungu nyote pamoja,
wala msifarikiane. Na kumbukeni
neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu
yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa
nyinyi maadui naye akaziunganisha
nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa
ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa
shimo la Moto, naye akakuokoeni

nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu


anakubainishieni Ishara zake ili
mpate kuongoka(Quran 3:103).
Hata hivyo tunaporejea historia
ya kuanzishwa vyombo vya habari
kwa kiasi kikubwa utaona kulikuwa
na malengo hasi,ingawa manufaa
yake kwa sasa ni makubwa hususan
kwa jamii ya waslamu kwani imerahisisha ufanisi na utekelezaji wa
mambo kadha wa kadha.
Kwa umoja wetu kama waislamu
tunapaswa kutumia neema hizi za
vyombo vya habari katika misingi ya
dini iliyoainishwa ikiwemo,kuripoti
jambo lililochunguzwa,kuripoti bila
kutawaliwa na hisia binafsi,kuripoti
bila kulazimisha mawazo na fikra
binafsi,kuripoti bila kujali nani atasoma au nani hatasoma kazi
yako,kuripoti bila kujali nani atafurahi na nani atachukia na kuripoti
pande zote mbili sawasawa (Balancing). Kwa mfano inawezekana kwa

idadi ya vyombo vyote vya habari


vilivyopo sasa kwa upande wa
televisheni,radio na magazeti kuwa
na nafasi kubwa ya kufanya mapinduzi katika kupigania na kutetea
haki za waislamu,lakini si hivyo tu
bali pia kuielimisha na kuionya jamii
juu ya hofu ya Allah subhanahu
Wataala tofauti na ilivyo sasa kwa
baadhi ya vyombo hivyo kuwa kinyume na malengo yaliyokusudiwa
hivyo kukosa utofauti na vyombo
vingine.
Pia ni vema wamiliki wa vyombo
vya habari vya kiislamu pamoja na
watendaji wake kwa ujumla kuweka
kando itikadi za kimadhehebu
,kuepuka migongano na mifarakano
katika mambo yasiyo na tija na dini
yetu badala yake kuchukua fursa
hiyo kuwa na kauli moja katika kuyaendea mambo ya dini yetu na dunia
kwa ujumla.
Tunashauri vyombo hivi vya

habari kuwa na umoja wenye nguvu


kuanzia wamiliki wake, wahariri na
wanahabari ili kuweza kujenga sauti
moja inayofanana ya kuwapasha
habari waislamu.
Chombo kama jukwaa la wahariri
wa vyombo vya habari vya kiislamu,
bodi ya wamiliki wa vyombo vya
habari vya kiislamu vingeweza kuundwa ili kuwaunganisha pamoja
wadau katika sekta hii muhimu.
Tumalizizie kwa kusema,ili kuwepo maana ya vyombo vingi vya
habari vya kiislamu hapana budi
kuwa kitu kimoja ili kufanikisha
ajenda zetu.Katika kulifanikisha hilo
ni jukumu letu kubuni wazo la uanzishwaji wa jukwaa la wahariri kwa
vyombo vya habari vya kiislamu ili
kuweka mkazo katika nia ya pamoja
ya kuujenga umma wa waislamu hususan katika wakati huu ambao jamii
ya waislamu inakabiliwa na vita ya
fikra na propaganda.

nasaha za wiki

kweli kwamba kosa


moja ambalo watanzania tutalifanya katika
kipindi hiki linaweza
kutugharimu kwa miaka mitano
au kumi ijayo unafanya zoezi linaloendelea Dodoma la mchakato
wa uteuzi wa mgombea wa urais
wa CCM kuwa muhimu sana.
Watanzania tumeona na tunaendelea kushuhudia wimbi
kubwa la wanaowania nafasi ya
kurithi mikoba ya Jakaya Mrisho
Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiendelea
kujitokeza katika viwanja vya
Chimwaga kuchukua fomu za
kuomba kupeperusha bendera ya
CCM.
Mpaka Ijumaa iliyopita, wagombea 15 walishajitokeza kwenda
Dodoma kuchukua fomu hizo,
baadhi kwa mbwembwe na wengine kimya kimya.
Miongoni mwa waliokwisha
kuchukua fomu ni pamoja na
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dk Gharib Bilal; Waziri wa nchi Ofisi ya
Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark
Mwandosya; Waziri wa Kilimo,
Chakula na Ushirika, Stephen
Wassira.
Wengine waliochukua fomu ni
Balozi wa Umoja wa Afrika (AU)
huko Marekani, Amina Salum Ali
na Mbunge wa Bunge la Afrika
Mashariki, watoto wa marais waliopita wa taifa la Tanzania; Charles
Makongoro Nyerere na Balozi Ali
Karume, mawaziri wawili wa zamani wa nishati na madini, Prof.
Sospeter Muhongo na Wiliam
Ngeleja, mawaziri wakuu
wastaafu, Fredrick Sumaye na Edward Lowasa.
Makada wengine ambao wameonesha dhamira yao ya kutaka
kuwatumikia watanzania ni Amos

SELEMANI MAGALI

Kosa moja litagharimu


maendeleo yetu miaka 5
Siyantemi, Waziri wa Kilimo
Chakula na Ushirika Steven Wasira, Naibu Waziri wa Fedha,
Mwigulu Nchemba na Waziri wa
Uchukuzi, Samuel Sitta na Dk Titus Kamani.
Kujitokeza kwa makada wengi
kutaka kugombea nafasi hiyo kumeibua mijadala mingi miongoni
mwa jamii. Tukubaliane kuwa
mwitikio mkubwa wa makada wa
chama tawala kujitokeza katika
mbio za kuwania urais kuna faida
na hasara zake. Kuna uwezekano
wa kupata kiongozi mbaya au
mzuri.
Hasara na faida zimezalisha
kambi mbili katika mjadala wa
aidha wingi wa wagombea ni jambo zuri au baya.
Kuna wanaosema wagombea
wengi hiyo ni ishara mbaya kwa
mustakabali wa taifa kwa sababu
katika mtifuano na mkanganyiko
huo ni rahisi watu kuchanganyiki-

wa na kuishia kuchagua mtu ambaye atakatisha tamaa zaidi wananchi ambao tayari wanaonekana wamekata tamaa na wamepoteza matumaini kutokana na
changamoto za maisha.
Kundi hili linaamini kuwa inawezekana hatua ya uchujaji
itakuwa ngumu kiasi kwamba
maamuzi magumu itabidi yafanyike ili kukinusuru chama kisigawanyike.
Maamuzi magumu ni kama
yale ya 2010 ambapo iliamriwa
nafasi ya uspika ikamatwe na
mwanamke. Maamuzi magumu
ya namna hii sio muda wote
yanaweza kuwa mazuri na yanaweza kuacha wagombea wazuri.
Pia, ugumu wa kupata kiongozi
mzuri unaweza kutokana na ghilba
ya baadhi ya wagombea ambao
tayari baadhi yao inasemekana
wameanza kununua watu ili wa
washangilie na kuonekana kuwa

wanapendwa na kukubalika.
Wagombea wa aina hii, inasemekana, wameanza kununua hata
wanahabari. Ingawa ushahidi sina,
waswahili wanasema lisemwalo
lipo na kama halipo laja.
Lakini wapo pia watu wanaoona utitiri huu wa wagombea kama
jambo zuri, na ni ishara njema kwa
awamu ijayo.
Walio na matumaini kutokana
na utitiri wa wagombea wanaamini katika demokrasia, ambapo wagombea wengi inamaanisha una idadi kubwa ya watu ambao utapata fursa ya kuwapima na
kuchagua mgombea mzuri.
Katika orodha ya wana CCM
waliojitokeza kuna maprofesa,
madaktari, vijana, wazee, matajiri
na masikini, wenye uzoefu na
wachanga, wanadiplomasia na
kadhalika.
Ni mgombea mwenye elimu,
uzoefu na falsafa gani ataweza kuli-

Kujitokeza kwa makada wengi kutaka


kugombea nafasi hiyo kumeibua mijadala
mingi miongoni mwa jamii. Tukubaliane
kuwa mwitikio mkubwa wa makada wa
chama tawala kujitokeza katika mbio
za kuwania urais kuna faida na hasara
zake. Kuna uwezekano wa kupata
kiongozi mbaya au mzuri.

vusha taifa ndio swali la msingi


ambalo tukipata jawabu sahihi
watanzania tutakuwa tumeula.
Ukiwaangalia wale wote ambao
wamejitokeza na wale ambao wanatajwa kutaka kujitokeza kujiunga na mbio hizo za kuelekea ikulu,
unaweza kuhisi kabisa kuwa kuna
watu wenye uwezo, ujasiri na nia
ya dhati ya kutaka kuwapigania
wananchi.
Kwa upande wangu nadhani
kuwepo kwa utitiri wa makada kujitokeza kuchukua fomu ni hatua
ya kupongezwa, kwani inaonesha
namna chama tawala kilivyo na
utajiri wa watu wanaojiamini
kuwa wanaweza kuwavusha watanzania.
Changamoto iliyopo ni kwa wanachama wa chama tawala kuwasikiliza na kuwachuja vizuri viongozi hawa na kisha kuchagua
mtu ambaye anaweza kukabiliana
na matatizo lukuki yanayoikabili
nchi yetu kwa sasa, huku rushwa,
ufisadi na kukosekana haki na uadilifu (hususan kwa wanajamii
Waislam) ikiongoza orodha hiyo.
Kwa hiyo basi, hoja kamwe sio
wimbi la wagombea wengi pale
Chimwaga, lakini ni namna wananachi wanavyoweza kufaidika
kutokana mwamko wa kidemokrasia wa wingi wa wagombea hao waliojitokeza kwa kupata kiongozi safi.
Nasaha zangu kwa viongozi
wenye dhamana ya kuchuja wagombea, watumie uzalendo na
busara katika kuteua mgombea
mwenye sifa zisizo na shaka.
Nasaha hizi pia ziende kwa muungano wa UKAWA na vyama
vingine vya upinzani vinavyopanga
kusimamisha mgombea urais
mwaka huu. Kosa moja litagharimu maendeleo yetu miaka mitano

21 Shaaban 1436, jumatatu Juni 8 - 14, 2015

www.islamicftz.org

NA YUSUFU AHMADI

heikh Al Amin ni bahari ya kina kirefu!


Utazama...!Ukizuka
utatoka na kitu kidogo
tu!. Hayo ni maneno ya Marehemu AbdulKadir Said Al-Maamry
alipoulizwa na Sayyid Ghalib At
Tameemi kuhusu maisha ya
Sheikh Al Amin Ali Mazrui.
Sayyid Ghalib At Tameemi
ambaye aliandika kitabu alichokiita, Maisha ya Sheikh Al Amin
Ali Mazrui (1891 1947), anamuelezea Sheikh Al Amin kama
mwanazuoni ambaye amekuwa
kimbilio la utafiti wa wasomi wengi, wanasayansi na watafiti
mbalimbali ulimwenguni kwa
miaka mingi.
Umaarufu wa Sheikh Al
Amin unatokana na nafasi yake
kama mwanamageuzi wa Kiislamu Afrika Mashariki aliyejitahidi
kubadili mitazamo katika baadhi
ya mambo yaliyoonekana kuwa
hayastahili kufanywa na Waislamu na kuhimiza mambo muhimu
ambayo Waislamu hawakuwa
wakiyafanya.
Si ajabu basi kuwa, mwanawe,
Prof Ali Mazrui, msomi maarufu
duniani wa fani ya historia, anamuelezea Sheikh Al Amin kama: ...
mmoja kati ya wasomi wakubwa
wa Afrika ya Mashariki aliyekuwa
ulamaa, mwandishi, mhariri wa
magazeti, hodari wa mashairi,
mwanaharakati, aliyeanzisha harakati za mageuzi na muelekeo
mpya.

Sheikh Al-Amin ni nani?


heikh Al-Amin Ali Mazrui ambae alikuwa mtoto
wa Sheikh Ali Bin Abdallah Mazrui alizaliwa
Januari 27, 1891 katika mji wa
Mombasa nchini Kenya. Baba
yake, Ali bin Abdallah Mazrui alifariki akiwa na miaka 4 tu.
Baada ya kifo cha baba yake,
Sheikh Al Amin alilelewa na
mjomba wake, Sheikh Suleiman
bin Ali bin Hamisi Mazrui.
Inaelezwa kuwa wakati wa kukata
roho, Sheikh Ali Mazrui alimkabidhi Sheikh Suleiman awe mlezi wa
mwanae kwa kumwambia: Nakukabidhi mwanangu leo unirudishie mwenyewe kesho akhera.
Maneno hayo ya Sheikh Ali
Mazrui yananasibishwa na
maneno ya Allah (52: 21): Na walio amini na dhuriya zao wakawafuata kwa Imani tutawakutanisha nao dhuriya zao, na wala hatutawapunja hata kidogo katika vitendo vyao. Kila mtu lazima atapata alicho kichuma.
Sheikh Mazrui alijifunza dini
ya Kiislamu chini ya mlezi wake,
Sheikh Suleiman aliyekuwa Kadhi
Mkuu wa Kenya enzi za Utawala
wa Muingereza.
Katika safari yake ya kusaka
elimu ya dini ya Kiislamu, Sheikh
Al-Amin pia alifika visiwani Zanzibar, ambapo alisoma kwa
masheikh mashuhuri, wakiwemo
Sheikh Sayyid Ahmad Bin Sumayt
na Sheikh Abdalah Bakathir.
Pamoja na mambo mengine,
Sheikh Al-Amin anasifika kwa
uhodari katika utunzi wa mashairi,

Sheikh Al-Amin mazrui

Mwana mageuzi nguli katika Uislamu


jaji na msomi mahiri wa dini ya
Kiislamu kuwahi kutokea katika
ukanda wa Afrika mashariki.
Miongoni mwa maulamaa
mashuhuri ambao Sheikh
Al-Amin aliwafuatilia
kiundani mafundisho yao
ni Sheikh Ibn Taymiyya
na Sheikh Muhammad
Abdu.
Utumishi wa
Sheikh Al-Amin
waka
1910,
Sheikh
A l Amin alianza kazi
kama Katibu wa Kadhi wa Mombasa
mpaka mwaka 1919
ambapo aliamua
kuachana na cheo hicho na kuwa mwalimu
wa somo la kiarabu katika
shule ya kiarabu ya Mombasa.
Lakini mwaka 1921 alirejea
tena katika nafasi ya ukatibu wa
Kadhi wa Mombasa mpaka mwaka 1932 alipofanikiwa kushika nafasi ya Kadhi wa Mji wa Mombasa
na mwaka 1937 akafanikiwa kuwa
Kadhi Mkuu wa Kenya.

Mageuzi katika dini


atika utafiti wake bwana Randall L. Powels
uliobeba kichwa cha
habari,Sheikh AlAmin B. Ali Mazrui and Islamic
modernism in East Africa, 18751947 alioufanya kwa lengo la kutathmini mchango wa Sheikh AlAmin katika maendeleo ya dini ya
Kiislamu, anamtaja Sheikh huyo
kama mtu muhimu hapa Afrika
Mashariki aliyeleta mapinduzi
makubwa katika dini hiyo.
Miongoni mwa mapinduzi
makubwa aliyoyaleta Sheikh AlAmin ni kuwahimiza Waislamu
kufanya kazi zingine tofauti na za
dini tu, akisisitiza kuwa dini ya Kiislamu haijamkataza muumini
kuacha kushiriki katika shughuli
za dunia.
Moja ya harakati za Sheikh Alamin ni kutaka mabadiliko katika
Uislamu kuhusu walimu kujihusisha na uganga na kupiga ramli,
waislamu kushiriki mambo ya

ngoma (beni)
na pia
uzushi kuhusu mambo ya sherehe
za Maulid.(Kitabu cha Sheikh Alamin-Kutizamia, uk 10)
Kwa maneno mengine, Sheikh
Al-Amin ni muasisi wa harakati za
kisunnah Afrika Mashariki ndiyo
maana wanafunzi wake kama
Sheikh Abdallah Saleh Farsy walikuja kuendeleza harakati hizo.
Lakini tofauti na masheikh
wengi wa kisunnah leo, Sheikh AlAmin hakujiona tofauti na waislamu wengine hata kama walikuwa
wakiyafanya yale aliyokuwa akiyapinga kwa mujibu wa Quran na
Sunnah. Kuhusiana na elimu ya
kimagharibi (Western education),
Sheikh Al-Amin aliwahimiza
Waislamu kujifunza elimu ya sayansi na teknolojia ya Magharibi ili
waweze kupata maendeleo huku
akisema kuwa, dini ya Kiislamu ni
dini ya kisayansi na inayotumia
tafakuri (Rationality).
Katika kuonesha kuwa ndani
ya Uislamu kuna mambo ya kisayansi, Sheikh Al-Amin alitolea
mfano wa nchi ya Misri iliyokuwa
ya kiislamu ambapo Waislamu
waliweza kufanya mapinduzi
makubwa katika maendeleo ya

dunia kwenye nyanja za hesabu za


aljebra, unajimu, kemia, tiba
(medicine), na falsafa (philosophy).
Katika kusisitiza juu ya
suala hilo, Sheikh AlAmin aliwataka Waislamu kusoma vitabu
vya nchi za Magharibi kwa hoja kuwa
maarifa yaliyomo
humo baadhi
yakeyamechukuliwa kutoka katika mafundisho
ya dini ya Kiislamu.
Na ili kuweza
kufikia lengo hilo
la watu kupata
elimu, Sheikh AlAmin alihimiza
ujenzi wa shule za
kisasa. Kadhalika, pia
alihimiza watu wajenge hospitali, maktaba, waunde silaha za kisasa
na wafanye biashara.
Katika kuleta mapinduzi zaidi katika dini ya Kiislamu, Sheikh
Al-Amin alipinga kwa jitihada
zake zote mila potovu, yakiwemo
matumizi ya madawa kutoka kwa
waganga wa jadi kwa hoja kuwa
suala hilo si sahihi katika mafundisho ya dini ya Kiislamu.
Badala yake aliwataka Waumini
wa dini ya Kiislamu kuhakikisha
wana achana na mila potovu na
kushikamana na mafundisho sahihi ya dini ya Kiislamu.
Kutokana na kuenea zaidi kwa
mawazo ya nchi za Magharibi katika pwani ya Afrika Mashariki na
hivyo kuathiri mafundisho ya dini
ya Kiislamu, Sheikh Al-Amin aliwahimiza Waislamu kushikamana na kuyapinga mawazo hatari
ya nchi za Magharibi.
Pia Sheikh akishirikiana na
mlezi wake, Sheikh Suleiman alipambana na wakoloni na vituko
vyao mpaka wakoloni wakasalimu
amri na wakawaheshimu. Baba
yake naye alipambana na Sayyid
Barghash mpaka akafungwa jela
na mtawala huyo.
Kuanzisha vyombo vya habari
Katika malengo yake ya kuuamsha umma wa Kiislamu kuifahamu zaidi dini yao, mwaka 19301931, Sheikh Al-Amini alianzisha

Ukiachia mbali kutumia magazeti katika


kuhakikisha Uislamu unaimarika
katika mji wa Mombasa, Sheikh Al-Amin
alianzisha Jeshi la Upotovu (Going
astray Army) dhidi ya ushawishi mbaya wa
chini kwa chini uliokuwa ukifanywa na
jeshi la Uokovu (Salvation Army).

gazeti lake la lugha ya kiswahili lililojulikana kama Sahifa na kufuatiwa na gazeti jingine lililojulikana kama Al-Islah hapo mwaka
1932. Magazeti yote hayo mawili
yalikuwa yakichapisha habari zilizokuwa na lengo la kuufanya
umma kupokea mawazo mapya
ya kimaendeleo katika elimu huku
yakisisitiza watu kufuata misingi
sahihi ya Kiislamu.
Ukiachia mbali kutumia magazeti katika kuhakikisha Uislamu
unaimarika katika mji wa Mombasa, Sheikh Al-Amin alianzisha
Jeshi la Upotovu (Going astray
Army) dhidi ya ushawishi mbaya
wa chini kwa chini uliokuwa ukifanywa na jeshi la Uokovu (Salvation Army).
Maandishi na wanafunzi wake
heikh Al-Amin aliandika
vitabu vingi vya dini ya
Kiislamu katika lugha ya
kiswahili na kiarabu,
ikiwemo kutafsiri Suratul AlBaqara, Suratul Al- Imran na Suratul An-Nisaa. Pia alikuwa akiandika makala katika jarida la AlManar la Chuo Kikuu cha AlAzhar cha nchini Misri.
Katika uhai wake, Sheikh AlAmin alifundisha wanafunzi wengi, ambao baadhi yao walitoa
mchango mkubwa katika maendeleo ya dini ya Kiislamu. Baadhi
ya wanafunzi wake wakubwa ni
pamoja na Sheikh Muhammad
Kassim na Sheikh Abdullah Saleh
Al-farsy, ambao wote wamewahi
kushika nafasi ya Kadhi Mkuu wa
Kenya. Mwanafunzi wake
mwingine mahiri ni Maalim
Ghazali ambae nae alianzisha Madrasa ya Ghazali iliyokuja kujulikana kama Shule ya msingi ya
Mbaraki huko Kenya.
Sheikh Al-Amin atakumbukwa
kwa utabiri wake aliouita khatari
nyeusi uliosema: Jamaa wa bara
watazitupa fagio na kuwa mabwana kwa sababu ya elimu na vitabu,
na sisi tulio mabwana leo ndio tutakaotupa vitabu tukaokota fagio.
Sheikh Al-Amin pia alikuwa
mtetezi mkubwa wa elimu ya wanawake, ambayo haikuwa ikitolewa kwa kiasi kikubwa kwao na
alizihimiza familia nyingi kuwafunza elimu mabinti zao.
Sheikh Al-Amin alifariki dunia
mwaka 1947 baada ya kuugua kifua kikuu kwa muda mrefu. Siku
aliyokata roho, Sheikh Al-Amin
alimuuliza mkewe, sasa ni saa
ngapi? Akajibiwa ni alasiri.
Akamwambia mkewe mkubwa,
Bi Swafia bint Suleiman, amtawadhishe. Kisha, akainuliwa, akasali.
Akatoa salamu kumaliza swala.
Punde, Allah akachukua roho yake
akiwa amezungukwa na wakeze
wawili, wanawe na wanafunzi
wake.
Allah amrehemu

21 Shaaban 1436, jumatatu Juni 8 - 14, 2015

www.islamicftz.org

Kutoka katika Quran na Sunnah

iki iliyopita katika


mfululizo wetu wa
makala za Kutoka
katika Quran na
Sunnah tuliishilia pale Utubah alipolazimika kuuziba mdomo wa
Mtume ili asiendelee aliposoma
aya inayosema;
Wakikengeuka, basi sema (ee
Muhammad) Nakuhadharisheni
swaaiqah (mngurumo angamizi)
mfano wa swaaiqah ya kina Aad
na Thamuwd. Utubah alimwambia Mtume: Acha ewe Muhammad, tafadhali usiendelee.
Utubah aliporudi kwa watu
wake aliwaambia: Enyi watu
wangu naomba mnitii kwa siku ya
leo tu na mniasi katika siku nyingine zijazo. Naapa kwa hakika
nimesikia kutoka kwa Muhammad maneno ambayo sijawahi
kusikia mfano wake katu.
Mu a c h e n i m t u h u y u n a
mjitenge nae, nawaapia hatoacha
analofanya, muachieni waarabu
wengine, ikiwa atawashinda basi
utukufu wake ni utukufu wenu, na
cheo chake ni cheo chenu, yaani
mtapata utukufu kwa utukufu
wake na nguvu kwa nguvu zake, na
ufalme wake utakuwa ufalme
wenu.

Na Selemani Magali

ituo cha Sheria na Haki


za Binadamu (LHRC)
kimejizolea umaarufu
mkubwa katika ardhi ya
Tanzania kutokana na kazi yake ya
kuhakikisha haki na usawa wa raia
unaheshimiwa kwa kiwango cha
hali ya juu.
Kituo hiki kimejipambanua kwa
umma kama watetezi wa haki za
kiraia katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. Pia
wamesimama kidete kutetea haki
za makundi maalum huku wakitoa
elimu ya uraia na kuleta mabadiliko
chanya katika jamii.
Hivi karibuni taasisi hiyo isiyo ya
kiserikali ilizindua taarifa yake juu
ya hali ya haki za binadamu kwa
kipindi cha mwaka 2014 ambayo ilionesha hali ya haki za binadamu
nchini bado ni tete na kwamba
makundi mbalimbali kama ya
wazee, wanawake, watoto na watu
wenye ulemavu wameendelea kunyanyasika katika nchi yao. Taarifa
hiyo kwa umma iliibua hisia tofauti
miongoni mwa jamii, huku Waislamu wakiikosoa vikali na kukosoa
utendaji kazi wa kituo hicho ambacho wanakituhumu kwa ubaguzi
na kushindwa kutetea Waislamu.
Masheikh wamesema, kituo hicho kimekuwa kikipiga kimya ukiukaji wa haki za binadamu unapofanyika dhidi ya Waislamu, lakini
kimekuwa mstari wa mbele kusemea makundi mengine ya kijamii.
Akizungumza na gazeti la Imaan, Kaimu Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu,
Sheikh Rajabu Katimba alielezea

Na sheikh Tawakkal Juma

Mafunzo kutoka katika kisa cha Utubah


Na kama hao waarabu wengine
watamshinda, basi mtakuwa
mmeepushwa shari zake kwa
mikono ya watu wengine.
Watu waliomtuma Utubah wakasema: Hakika umeanza kumili
(kuegemea) kwa Muhammad na
jambo lako limekuajabisha na
umeacha ibada za masanamu za
watu wako. Utubah akawaambia: Maneno niliyosikia kutoka
kwa Muhammad sio uchawi wala
mashairi. Nimemsikia akisoma:
Wakikengeuka, basi sema (ee Muhammad) Nakuhadharisheni
swaaiqah (mungurumo angamizi)
mfano wa swaaiqah ya kina Aad
na Thamuwd. Nikamsihi aache na
nyinyi mnajua fika kuwa Muhammad asemapo kitu huwa hasemi
uongo, nikaogopa isije adhabu
ikakuteremkieni.
Mpenzi msomaji tunachojifunza katika kisa hiki ni kuwa, Quran
iko juu na itaendelea kuwa juu, na
wenye Quran wako juu na wataendelea kuwa juu. Kama wako
chini kuna mahali walikosea au
hawajatimiza vigezo na masharti.

Ushindi hauteremki kutoka katika ombwe wala hauji bila kutarajiwa. Kushinda au kushindwa
kupo na kunatawaliwa na kanuni
na njia ambazo zimenukuliwa na
Allah katika Quran ili waumini
waweze kuzijua kwa yakini, elimu
ya uhakika na kwa upeo mkubwa
zaidi. Kanuni hizi hazibadiliki kwa
kiasi kikubwa.
Allah anasema yafuatayo kuhusu kanuni hizi: Kabla yenu
zimepita nyendo nyingi; basi tembeeni katika ulimwengu muangalie vipi ulikuwa mwisho wa wanaokanusha (3: 137).
Na pia, Hii ni ada ya Allah iliyokuwa kwa wale waliopita zamani.
Wala hutapata mabadiliko katika
ada ya Allah (33: 62). Na Anasema tena Allah aliyetukuka: Huo
ndio mwendo wa Allah uliokwishapita zamani, wala hutapata
mabadiliko katika mwendo wa Allah (48: 23).
Kupotoka katika njia iliyonyooka na kusahau ujumbe wetu
ni moja kati ya sababu kubwa zinazotufanya Waislamu tushindwe.

Waislamu sasa hivi wameshindwa


kutofautisha baina ya adui na
rafiki na hawajui mikakati na njama za adui dhidi yao na mikakati
yao sahihi dhidi ya adui yao.
Hivyo, umma wa Kiislamu
hautoweza kushinda dhidi ya adui
yake hadi masharti fulani yatimizwe. Kama kweli ikiwa Waislamu wanataka kushinda ni lazima
wayafanyie kazi masharti hayo.
Nyakati za ushindi ama kushindwa
zinabadilishana mikono kutegemea kanuni hizo.
Allah anasema: Kama yamekupateni majeraha, basi na hao
watu wengine yamewapata majeraha mfano wa haya. Na siku za
namna hii tunaweletea watu kwa
zamu ili Allah awapambanue walioamini na awateuwe miongoni
mwenu mashahidi. Na Allah hawapendi madhalimu (3: 140).
Imani ya kweli yenye nguvu ni
sharti muhimu kwa Waislamu kuwashinda makafiri. Ikiwa Waislamu ni wakweli na waumini wa
kiuhakika, basi wataweza kuwashinda maadui zao kila wakati

na lau kama Waislamu hawataweza kuwa juu ya adui yao, basi


itakuwa Waislamu ndio wenye
matatizo kiimani.
Waumini ndio walengwa wa
kupata ushindi, kama Allah anavyomwambia Mtume wake: Na
wakitaka kukukhadaa basi Allah
atakutosheleza. Kwani Yeye ndiye
aliyekuunga mkono kwa nusura
yake na kwa waumini. Na akaziunga nyoyo zao. Na lau wewe ungelitoa vyote viliomo duniani usingeliweza kuziunga nyoyo zao, lakini Allah ndiye aliyewaunganisha (8: 62 63).
Wakati mwingine Allah anawatumia malaika ili wawasaidie waumini kama alivyosema: Mola
wako Mlezi alipowafunulia malaika: Hakika Mimi ni pamoja nanyi,
basi watieni nguvu walioamini.
Nitatia woga katika nyoyo za waliokufuru (8: 12).
Allah anasema tena: Kisha Allah akateremsha utulivu wake juu
ya mtume wake na juu ya waumini. Na Akateremsha majeshi
ambayo hamkuyaona, na akawaadhibu wale waliokufuru. Na hayo
ndiyo malipo ya makafiri (9: 26).
Itaendelea

Miaka 20 ya LHRC:

Masheikh Walalamikia ubaguzi


masikitiko yake juu ya tabia hiyo ya
LHRC ya kuwatenga Waislamu.
Sheikh Katimba alisema, wanaushahidi wa hujuma mbalimbali
ambazo zilifanywa na Serikali dhidi
ya Waislamu, lakini kituo hicho licha ya kuwa na taarifa walisita
walau kutoa matamko ya kulaani,
kama wanavyofanya katika matukio mengine ya uvunjwaji wa haki
za binadamu. Sheikh Katimba
amesema, ukimya wa LHRC unaweza kutafsirika kama mpango
maalum unaolenga kukandamiza
jamii ya Kiislamu.
Baadhi ya kadhia za uonevu na
ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu zilizowakumba Waislamu,
kwa mujibu wa Sheikh Katimba ni
pamoja na Sheikh Issa Ponda kuhojiwa wakati yupo kitandani na jeraha bichi la risasi.
Tukio lingine ni la viongozi wa
Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara
ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI)
kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji
na kikatili vilivyokiuka haki za bidanamu. Matukio haya yote yalipita
bila taasisi hiyo kukemea na kuwatetea masheikh hao.
Katimba alisema, baadhi ya
masheikh wa JUMIKI wamewahi
kuhojiwa wakiwa uchi, walipigwa
kipigo cha mwizi, waliingiliwa kinyume cha maumbile, pamoja na

kushindiliwa jiti sehemu za siri.


Sheikh Katimba ameongeza
kusema kuwa, hata ripoti ya hali ya
haki za binadamu hapa nchini ambayo imezinduliwa hivi karibuni ilishindwa kuonyesha ukatili huo unaofanywa na watekelezaji wa sheria,
jambo linalojenga hofu miongoni
mwa Waislamu juu ya uadilifu wa
kituo hicho.
Katimba alisema, Sheikh
anayedaiwa kufanyiwa udhalilishaji
na jeshi la polisi ambaye pia aliithibitishia Mahakama ya Kisutu
juu ya udhalilishwaji huo ni mtu
mzima mwenye wake watatu na
watoto wanane, na kuongeza kuwa,
kitendo cha uzalilishaji alichofanyiwa kilipaswa kukemewa kwa vikali,
lakini kwa mshangao mkubwa
hakuna mwanaharakati wa LHRC
aliyeguswa na tukio hilo.
Naye, Amir wa Baraza la Vijana
wa Kiislamu Tanzania, Sheikh
Shabaan Mapeyo ameitaka taasisi
hiyo kujitathmini kupitia miaka 20
wanayoazimisha, ili wapime kama
kweli malengo yao yamekamilika.
Mapeyo alikishutumu kituo hicho akisema, viongozi wake wamekuwa wakitupilia mbali matatizo
yanayoigusa jamii ya Kiislamu na
hivyo basi wajitathmni kama wanatenda haki na uadilifu katika jamii
na kisha wajirekebishe.

Mapeyo alisema, kutokana na


mfululizo wa matukio ya kiuonevu
yanayotokea dhidi ya viongozi wa
Kiislamu ni dhahiri kingekuwa ni
kituo cha kupigania haki za raia
wote, wangeingilia kati na kutoa
matamko ya kulaani. Hatujui kwa
nini wanakuwa wazito kwa matukio
yanayowagusa Waislamu, alihoji
Mapeyo na kuongeza: Wakati
kituo hicho kinasherehekea kutimiza miaka 20 ya kupigania haki na
usawa wa raia katika ardhi ya Tanzania, Waislamu wamekuwa wakisikitishwa na utendaji wao.
Mapeyo alisema, kutopata taarifa ya matukio hayo hakiwezi kuwa
hoja ya kujifichia, kwani matukio
mengi yamekuwa yakitagazwa katika vyombo vya habari na kujadiiwa bungeni .
WANACHOSEMA KITUO CHA
SHERIA
Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na haki za
Binadamu Dr. Helen Kijo-Bisimba
amekiri kuwepo kwa changamoto
hiyo, ambayo amesema, kwa muda
mrefu wanahangaika namna ya kuweza kuitatua.
Dr. Kijo-Bisimba alisema, Waislamu wamekuwa na mtazamo hasi
juu ya Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu na wengi wao wame-

kuwa wakiamini kuwa kituo hakina


msaada juu ya matukio yanayowagusa moja kwa moja Waislamu.
Akifafanua kwa nini taasisi yake
imekuwa inashutumiwa juu ya
utendaji kazi wake, Dr. Kijo-Bisimba alisema, kwanza, jamii lazima ifahamu kuwa taasisi yake haifanyi kazi kwa jicho la dini, bali imekuwa ikimulika haki ya raia yeyote
yule bila kujali anatoka kundi gani.
Ndugu yangu mwandishi, sisi
kituo tunajitahidi sana kuhakikisha
tunatoa huduma zetu kwa yeyote
yule mwenye mahitaji, hoja ya
kwamba tumekuwa kimya kwa
masuala ya Waislamu kwetu haina
mashiko, kwani tunahudumia jamii
yote bila kujali dini wala kabila, alisema Kijo-Bisimba.
Dr. Bisimba ameendelea kusema
kuwa, taasisi yake ilitumia rasilimali
zake mwaka 1998 kuingilia sakata
la Mwembechai, lakini suala lile liliisha bila mafanikio kutokana na
Waislamu kushindwa kutoa ushirikiano wa kutosha.
Akizungumzia mafanikio ambayo taasisi yake imeyapata kwa
kipindi hicho cha miaka 20, Dr. Kijo-Bisimba alisema, wamefanikiwa
kuinua uelewa miongoni mwa
jamii, ambapo mpaka sasa Watanzania wanaweza kuinuka na kudai
haki zao wakiona zinapindishwa.

21 Shaaban 1436, jumatatu Juni 8 - 14, 2015

www.islamicftz.org

ncha ya kalamu
Sheikh Muhammad Issa

Usalafi usiwagawe Wanasunnah

salaam alaykum ndugu


katika imani. Nimelazimika kuandika makala
haya kutokana na hali
miongoni mwa wanasunnah Tanzania ili kutekeleza mafundisho ya
Quran: Kumbusha huenda ukumbusho ukafaa. Atakumbushika
mwenye kumuogopa (Allah). Na
atajitenga nao (ukumbusho)
muovu (87:9-11).
Tunashuhudia masheikh wakongwe wa kisunnah wanakufurishwa na kuitwa majahili.
Masheikh vijana wanawakosea
adabu masheikh wenye umri
mkubwa kinyume na adabu za
kielimu na hadith ya Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake): Si
miongoni mwetu asiyewaonea
huruma wadogo wetu na asiyewaheshimu wakubwa wetu
(Muslim).
Kibaya zaidi, wanasunnah
Tanzania wametikisika kiasi
kwamba ni vigumu kuwaleta
pamoja kwa maslahi ya harakati
za kisunnah, huku wapinzani wao
wakiwapiga vita.
Hata tofauti za kimtazamo wa
kielimu tu zinatosha kumtoa
sheikh katika safu ya wanasunnah
na kumuingiza katika upotevu,
huku wakijua penye hitilafu
miongoni mwa wanawazuoni,
msimamo wa mmoja haulazimishwi kwa wengine.
Mambo haya yanayotokea sasa
hivi katika safu za wanasunnah

Tanzania hayakuweko miaka


michache nyuma, bali yamelipuka baada ya vita ya kwanza na ya
pili ya Ghuba, ambapo wanasunnah walianza kukufurishana.
Mtafaruku wa sasa miongoni
mwa wanasunnah haukuwepo
kabla ya harakati za kisalafi kushika kasi, kwani wanasunnah wa
mwanzo, kama Sheikh Al Amin
Maftah, Sheikh Abdallah Saleh
Farsy, Sheikh Jabir Yusuf Katura,
na Sheikh Juma Poli hawakujitambulisha kama masalafi, bali Answar Sunnah na wakatambuliwa
hivyo.
Si kwamba masheikh hawa
hawakuujua usalafi au waliupinga. Walifanya hivyo kwa kuwa
ndilo lililokuwa jina mashuhuri
wakati huo duniani, huku wakisimamia njia ya salafi kwa kauli na
matendo yao kiasi alichowajaalia
Allah Taala. Wako waliotiwa mis-

ukosuko, wakafungwa magerezani, wakapigwa na hata kuathirika


kiuchumi.
Hatimaye wanafunzi au wanafunzi wa wanafunzi wa
masheikh wa kisunnah wakaenda
kusoma nje na kukuta vuguvugu
la masalafi. Waliporejea nchini,
ikawa kama usalafi unaingia.
Vijana wakaja na ari kubwa ya
kuufikisha usalafi walivyouelewa.
Bahati mbaya ni kwamba ufikishaji umekuwa ni kwa mtindo
wa sisi na wao na hivyo kuwagawa wanasunnah.
Kwa nini kubaguana?
Usalafi si jina tu, bali ni manhaj
(njia) ya kuutekeleza Uislamu,
ndiyo maana utasikia huyu hafuati Manhaj Salafiyyah kwa maana
hafuati mwenendo wa wema waliotangulia. Kama usalafi ni njia,
kwa nini wanasunnah ambao
wote wanajinasibu kufuata njia

hiyo wabaguane?
Sababu kubwa ni baadhi ya
wanasunnah kuwaona wengine si
masalafi wa kweli, hata kuthubutu kuwaita watu wa bida na
kuwakufurisha (Mungu atuepushe) kwa kuwa tu wanatofautiana nao mitazamo.
Ni wazi masalafi wa zama hizi
kama zamani wanatofautiana katika jinsi ya kuziendea dalili za
kisharia. Masheikh wakubwa wa
kisalafi duniani wanatofautiana,
lakini hawakufurishani.
Uelewa wetu wa usalafi unajumuisha masuala mengi ya msingi
ambayo hayapewi kipaumbele na
makundi ya kisalafi ya leo,
ikiwemo msimamo kuhusu masuala ya kisasa ambayo watu wema
waliotangulia (Salaf Swaalih)
wenyewe hawakukumbana nayo.
Mambo hayo ni kama kupiga
picha, uraia na kujinasibu kwa

Mtafaruku wa sasa miongoni mwa


wanasunnah haukuwepo kabla ya
harakati za kisalafi kushika kasi, kwani
wanasunnah wa mwanzo, kama Sheikh
Al Amin Maftah, Sheikh Abdallah Saleh
Farsy, Sheikh Jabir Yusuf Katura, na
Sheikh Juma Poli hawakujitambulisha
kama masalafi, bali Answar Sunnah na
wakatambuliwa hivyo.

utaifa, kusajili taasisi, kuanzisha


na kujiunga na vyama vya kisiasa,
kugombea nafasi za kisiasa na kupiga kura, kuweka fedha benki,
kusoma elimu za fani za kidunia
na kadhalika.
Masuala haya yametolewa fataawa mbalimbali ambazo ni ijtihaadi za wanawazuoni wa kisalafi
wa leo, hata hivyo kamwe haziwezi kuwa ndio msimamo wa Salaf
Swaalih wa karne tatu njema kwa
sababu wao hawakukumbana
nayo. Kadhalika, hauwezi kuwa
msimamo wa masalafi wote leo.
Jambo jingine lenye athari
kubwa kwa Waislamu ni msimamo wa baadhi ya masalafi kupiga
vita Waislamu kusomea fani
mbalimbali katika shule na vyuo
vikuu kwa madai kuwa hiyo si
elimu ya muhimu, kama msimamo wa Boko Haram, Nigeria. Matokeo yake, wanafunzi wa Kiislamu ikiwemo wanaosomea udaktari wanaacha masomo na kukosesha umma wataalamu.
Hata hivyo, masalafi hao wanaopinga kusomea udaktari, wanapoumwa nao pia huenda kutibiwa na madaktari makafiri katika hospitali za makafiri kwa zana
zilizotengenezwa na makafiri.
Ukiuliza kwa nini wanaenda,
utaambiwa hiyo ni dharura.
Kama kutibiwa katika hospitali
zisizo za Kiislamu ni dharura kwa
nini kusoma elimu ya udaktari pia
isiwe dharu- inaendelea Uk 14

21 Shaaban 1436, jumatatu Juni 8 - 14, 2015

makala maalum

10

www.islamicftz.org

21 Shaaban 1436, jumatatu Juni 8 - 14, 2015

11

www.islamicftz.org

makala maalum
NA IDDI JENGO

hukran za dhati anastahiki


Mwenyezi Mungu na rehma na
amani zimuendee Mtume wake
Muhammad. Katika makala
yetu ya leo tutajadili kwa pamoja dhana ya
maandalizi ikiwa ni mada mahsusi tunapokaribia kuingia katika mwezi mtukufu
wa Ramadhani.
Makala yetu itakuwa na dhamira
kubwa mbili, moja kuelezea umuhimu wa
maandalizi katika jambo lolote na pili
kuangalia maandalilizi stahiki kwa ajili ya
Ramadhani.
Kila binadamu anahitaji mafanikio katika maisha na katika kila jambo lake, iwe
kitaaluma, kisiasa, kiimani, kiuchumi au
lolote lile. Kutafuta mafanikio imekuwa
ndio kiu ya walimwengu mpaka baadhi ya
watu wanatumia njia haramu.
Lakini kiujumla, maandalizi ndio kiini
cha mafanikio ambayo mwanadamu anahitaji kuyapata., yawe ya binafsi au ya kijamii. Katika zama zetu mafanikio
hupimwa kwa vipimo tofauti. Wapo wanao pima kwa kuangalia kiwango cha utajiri, idadi ya watoto, uzuri wa mke au
mume, nyumba nzuri n.k.
Kimsingi mafanikio ndio kipimo cha
utu wa mwanadamu anayejitambua.
Hivyo basi, kwa kuwa msingi wa mafanikio ni maandalizi, hebu tuone nini maana
ya maandalizi na umuhimu wake.
Maandalizi ni matayarisho rasmi anayoyafanya mtu au jumuiya fulani kabla ya
kuliendea jambo ili kupata ufanisi.
Kimsingi yapo maandalizi ya muda mrefu,
na pili ni maandalizi ya muda mfupi.
Aina ya maandalizi hutegemea uzito na
uelewa juu ya jambo linalokusudiwa kufanywa. Kukosa uelewa ni jambo la hatari
sana ambalo hupelekea maandalizi duni.
Masiku machache yanayokuja umma
wa Kiislam unaelekea katika ibada
adhimu na nzito ya swaumu ya mwezi
mtukufu wa Ramadhani, tukio la kila
mwaka la utekelezaji wa nguzo ya tatu ya
Uislam, lilikuwapo tangu ilipofaradhishwa swaumu na ambalo litaendelea kuwapo mpaka mwisho wa ulimwengu huu.
Ramadhan ni katika kambi maalum za
mafunzo zinazofunguliwa kila mwaka, kisha zinafungwa. Kutokana na Ramadhan,
mwenye kutaka kupata faida hupata faida
ndani yake na hula hasara mwenye kutaka
kula hasara.
Ramadhan ni chuo maalum cha mafunzo tulichowekewa na Mola wetu
Mtukufu kwa ajili ya kupata mafunzo
maalum kwa ulimwengu mzima.
Mafunzo hayo ni mafunzo ya kipindi
cha siku ishirini na tisa au thelathini tu,
haizidi na kila siku mlango mmoja unafungwa. Kwa hivyo anayetaka kuwahi na
awahi.
Kambi hii maalum ya mafunzo ni rasmi kwa umma wa Kiislam na inatupasa
kuukaribisha mwezi huu kwa shauku na
moyo mkunjufu, kwani ndani yake mna
kheri nyingi sana, na Allah husamehe
madhambi kama tukiepuka yale
makubwa.
Kutokana na manufaa mengi yaliyomo
ndani ya mwezi huu, Mtume wetu mtukufu (Rehma na amani ziwe juu yake)
alikuwa akiusubiri kwa hamu kubwa.
Huyu ni Mtume wa Allah (Rehma na
amani zimshukie) aliyekwisha samehewa
madhambi yake yaliyotangulia na yale
yaliyofuatia. Mtume aliyekabidhiwa funguo zote za hazina za ardhini.

Dhana ya maandalizi kuelekea Ramadhan

Mtume (Rehma na amani ziwe juu


yake) alikuwa mara unapoingia mwezi
huu akiikaza barabara nguo yake ya chini
(saruni) na nyakati za usiku akiwaamsha
watu wake ili wajishughulishe na ibada na
hii ni kwa sababu alikuwa akiujua vizuri
utukufu wa Mola wake na alikuwa akiitambua vizuri zawadi aliyowatayarishia waja
wake wanaoshindana katika kufanya
mema ndani ya mwezi huu.
Imepokelewa kuwa maswahaba (Mungu awaridhie) walikuwa wakimuomba
Mola wao kabla ya Ramadhan kwa miezi
sita ili awawafikishe kuufikia mwezi huu,
na baada ya kumalizika mwezi wa Ramadhan walikuwa wakiendelea kumuomba

Allah kwa muda wa miezi sita mingine ili


azikubali amali zao njema walizofanya
ndani yake na ili awaghufirie madhambi
yao.
Mwezi mtukufu wa Ramadhan ni
mwezi ambao ni hifadhi na kinga nzito ya
kumuepusha mja na adhabu kali ya moto.
Atakayefunga siku moja katika mwezi huo
akitaraji kupata radhi za Allah Taala na
ikiwa hiyo itakuwa ndio siku ya mwisho ya
maisha yake, basi ataingia peponi.
Swaumu ya mwezi wa Ramadhan ni
miongoni mwa nguzo za Uislam na ndani
yake kunapatikana usiku mtakatifu ambao
ni bora kuliko miezi elfu moja.
Katika mwezi huu, milango ya pepo

huwa wazi, milango ya moto hufungwa na


mashetani hufungwa minyororo.
Pamoja na kufahamu fadhila zote hizo
zinazopatikana ndani ya mfungo wa Ramadhani, moja ya jambo la hatari kwa zama
zetu ni kuibuka mambo mabaya ambayo
yanaelekea kuwa mazoea yanayopendwa na
kupata wafuasi wa kutosha, hususan katika
umma Kiislamu.
Hatari ya mambo hayo ni pale yanapoambatanishwa kama kianzio katika
kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Yaani, badala ya watu kujiandaa kwa mambo mema ya kheri kama kuanza kujifunza
kuhusu swaumu na masharti yake, kujizoesha kufunga swaumu za Sunnah, zikiwemo

za Jumatatu na Alhamisi na masiku meupe.


Kutoa sadaka kwa masikini ili nao wapate maandalizi mazuri ya mwezi huo wenye
baraka, na mema mengine ambayo yanapendeza kwa aliyetuumba; kinyume chake
kumekuwa kuna wengi wenye majina ya
Kiislam ambao huukaribisha mwezi huu
mtukufu kwa kila aina ya maasi kwa jina la
vunja jungu kama ijulikanavyo katika maeneo mengi Tanzania.
Jambo hilo sio tu halipo katika dini yetu
hii safi na tukufu, bali pia ni jambo ambalo
haliwezi kufanywa na Muislam mwenye
imani na khofu ya Mola wake na ndio maana tukawaita hao wayafanyao hayo kuwa ni
Waislam jina.

Katika siku za mwisho ya mwezi wa


Shaaban, hususan mkesha wa kuamkia Ramadhan, watu hao hukusanyana na kufanya sherehe kwa kusikiliza nyimbo na kucheza muziki, kunywa pombe ambayo kama
vile kisasi, na kujihusisha na uzinzi kwa
kuwa wanaogopa kufanya hayo Ramadhan.
Wale wavuta sigara ambao kidogo wanachelea kuvuta katika mwezi wa Ramadhan nao zitavutwa kwa mfululizo, huku
wala unga nao wakikomoa kokeini na heroini bila kusahau wanaoenda pikniki kutumbua maraha.
Watu wanaofanya mambo hayo wanamkebehi Mwenyezi Mungu na kumfanya

yeye Allah kuwa ni Mungu wa Ramadhan


tu! Hawa wamemfanya Mwenyezi Mungu
kuwa hana thamani katika miezi kumi na
moja iliyobaki.
Kinyume na hao niliowataja hapo juu,
wapo wengine ambao wanaukaribisha
mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa kununua mikeka ya kuswalia pamoja na kanzu na kofia, huku misikiti ikianza kusheheni
hadi inakuwa kero badala ya furaha kwa
wale wenye kudumisha swala za jamaakwa
miezi yote ya mwaka, kwani hata nafasi za
mbele walizozoea kuzipata huwa ni adimu.
Hizi ni tabia nzuri na zinapaswa kudumishwa hata baada ya Ramadhan.
Kwa upande wa wakina dada ambao

Ramadhan ni
katika kambi
maalum za
mafunzo
zinazo
funguliwa
kila mwaka,
kisha
zinafungwa.
Kutokana na
Ramadhan,
mwenye
kutaka
kupata faida
hupata faida
ndani yake na
hula hasara
mwenye
kutaka kula
hasara.
walikuwa hawajui hata kuvaa hijabu, basi
utawaona wanaanza kununua mitandio ya
kujitanda huku soko la kanga nalo likikua.
Wale wanaojitahidi zaidi hununua baibui.
Ndani ya baadhi ya nyumba za Waislam
utaanza kusikia Quran zikisomwa kwenye
redio na runinga na miziki ikipungua.
Hayo yote yanafanyika kama heshima
na taadhima kwa mwezi huu. Ila walichoghafilika ndugu zetu hawa, ni kuwa
uelewa huo unamaanisha kuwa katika
miezi iliyobaki hawapaswi kufanya hayo.
Ina maana kwamba, uwepo wa Mungu,
uwezo wake, nguvu zake na amri zake hazina uzito wowote ila Ramadhan tu. Nayo ni
dhana potofu. Mungu atuepushe nayo.
Ijulikane kuwa ni wajibu wa kila mwanajamii linapoonekana jambo lolote ovu
na baya kulizuia, kulikemea au kulikasirikia, ingawa hili la mwisho la kukasirika tu
ni katika udhaifu wa imani.
Alah Taala anasema:Na waumini wanaume na waumini wanawake wao kwa
wao ni marafiki walinzi. Huamrisha mema
na hukataza maovu, na hushika swalah, na
hutoa zakaah, na humtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Hao Mwenyezi Mungu atawarehemu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mtukufu, Mwenye nguvu, Mwenye
hekima (9: 71).
Vile vile hadith kutoka kwa Mtume
wetu mpenzi (Rehma na amani ziwe juu
yake) iliyosimuliwa na AbuSaiyd AlKhudriy(Radhi za Allah zimshukie)ambaye amesema:Nilimsikia Mtume(Rehma na amani zimshukie)amesema:
Yeyote yule atakayeona kitendo kiovu
basi akiondoe (akibadilishe) kwa mkono
wake, ikiwa hawezi basi kwa ulimi wake
(alikemee au kukataza), na ikiwa hawezi
basi kwa moyo wake (achukie) na huo
(yaani kuona baya na kunyamaza) ni udhaifu wa Imani(Muslim).
Jengokeya5@gmail.com 0714 135 201

21 Shaaban 1436, jumatatu Juni 8 - 14, 2015

12

www.islamicftz.org

afya yako

Mlinganiaji

Pazi Mwinyimvua

MLO BORA
KWA MFUNGAJI
SWAUMU YA
RAMADHAN 2

SHEIKH MUHAMMAD ISSA

Laana ya Allah kwa


kutokufanyika
kazi ya daawah

iki iliyopita tulijifunza kuwa, kutafuta


elimu kuhusu maswala ya chakula na
lishe sio uzungu, bali ni katika mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu.
Wajibu wa kuitafuta elimu hiyo
unakuwa mkubwa zaidi wakati wa
mfungo wa mwezi mtukufu wa
Ramadhan, unaotarajiwa kuanza
wiki ijayo Mola akipenda.
Hivyo, Waislamu lazima wajipinde kuitafuta elimu ya mlo unaofaa kwa futari na daku katika
kipindi cha mwezi wa Ramadhan
ili tuweze kuzitekeleza aya zifuatazo kwa ukamilifu: Enyi mlioamini
kuleni vizuri tulivyokuruzukuni,
na Mumshukuru Mwenyezi Mungu, ikiwa mnamuabudu yeye peke
yake (Quran: 2:172).
Aya nyingine ni ile isemayo: Na
kuleni katika vile alivyokuruzukuni Mwenyezi Mungu vilivyo vizuri
na halali na mcheni Mwenyezi
Mungu ambaye nyinyi mnamwamini (Quran: 5: 88).
Zaidi ya hayo, kujifundisha
elimu ya mlo unaofaa wa futari na
daku kutatuwezesha kufikia lengo
la ujenzi na uimarishaji wa afya ya
miili yetu kwa kupitia swaumu
kama tulivyohimizwa na Mtume
Muhammad (Rehma na amani
ziwe juu yake) katika hadith
ifuatayo: Fungeni mtapata siha
(afya).
Ili mtu awe na nguvu na afya
katika mwezi wa Ramadhan na
baada ya hapo, lazima azingatie
uchaguzi wa vyakula. Mtu ajitahidi
kula chakula kutoka mafungu
makuu yafuatayo: (a) mkate na
nafaka (b) maziwa, nyama, samaki, kuku, maharage, (c) matunda na (d) mboga za majani.
Mlo katika mwezi wa Ramadhan usitofautiane sana na milo ya
nje ya Ramadhan. Mlo katika
mwezi wa Ramadhan uwe wa hali
ya kawaida, sio wa kifahari sana.
Vyakula vinaweza kugawanywa
katika makundi makuu mawili
kwa kigezo cha muda wake wa kukaa tumboni. Kundi la kwanza ni
vyakula vinavyo chukua muda
mfupi, saa 3 mpaka 4 kusagwa.
Mfano wa vyakula hivyo ni kama
ndizi, viazi na vyakula vitamu
(mfano: tende, matunda).
Mtume Muhammad (Rehma
na amani ziwe juu yake)
ametuhimiza sana tufuturu kwa
kutumia tende. Kama umekosa
tende, tumia maji. Baada ya kufuturu, kula mlo wako, lakini uzingatie yanayoelezwa katika makala
hizi. Tende ina sukari aina ya glucose kwa wingi ambayo hutumika
kwa urahisi mwilini.
Kundi la pili la vyakula kwa kigezo cha muda wa kukaa tumboni

ni vyakula vinavyokaa tumboni


kwa muda mrefu (kiasi cha saa 5
mpaka 8). Mfano wa vyakula hivi
ni nafaka na mbegu ngano, shahiri, mtama, mahindi, mchele na
maharage.
Vyakula kama hivi viliwe kama
daku au usiku sana kwa wale wanaoshindwa kuamka na kula daku.
Vyakula hivi vitawapa nguvu ya
kuhimili mikiki mikiki ya swaumu
mchana na pia wataweza kumudu
majukumu mengine ya kazi za
mchana.
yakula vya kukaanga,
vyilivyotiwa viungo vingi na vyenye sukari na
chumvi nyingi ni hatari
kwa afya, kwani husababisha kiungulia, gesi tumboni na uzito
mkubwa. Mboga za majani na matunda ni muhimu sana ili kupunguza gesi tumboni, hasa kwa
mfungaji.
Vilevile, ni muhimu sana
kunywa maji safi na salama ya kutosha usiku wote wa Ramadhan ili
kupunguza hatari ya mwili kukaa
muda mrefu bila maji ya kutosha.
Maji huondoa sumu kutoka katika
mwili.
Hata hivyo, sio vizuri mtu
kunywa chai au kahawa wakati wa
kula mlo wa daku. Hii ni kwa sababu chai au kahawa hutengeneza
mkojo mwingi, hivyo maji na
madini yatapotea kwa njia ya mkojo kunapo kucha.
Vilivile, milo yote wakati wa Ramadhan isiwe na chumvi nyingi

kwa sababu mchana utakuwa na


kiu sana na utapoteza maji kwa
njia ya mkojo.
Ndizi ni nzuri kwa futari kama
tulivyosema hapo juu, hata hivyo
ndizi zinaweza kusababisha mlaji
kukosa choo kikubwa. Ili kuepuka
hilo, ni bora ndizi ziliwe na mboga
za majani na matunda kama papai.
Zaidi ya hayo hakuna haja ya
kula sana wakati wa kufuturu, mlo
wa usiku au mlo wa daku. Tabia ya
kula sana ni kinyume cha mafundisho ya Quran na Sunna.
Quran inasema ......Na kuleni
(vizuri) na kunyweni (vizuri). Lakini msipite kiasi tu. Hakika yeye
(Mwenyezi Mungu) hawapendi
wapitao kiasi (7:31).
Pia, ukila sana wakati wa Ramadhan (na miezi mingine pia)
mwili utashindwa kukitumia
chakula kilichohifadhiwa. Mtu akiwa amefunga mwili wake unatumia chakula kilichohifadhiwa
kama mafuta mwilini mwako.
Mchana wa swaumu unakuwa na
nguvu za kufanya kazi na unakuwa
na afya imara.
Mafuta ya ziada yanapotumika
wakati huu wa swaumu, mwili
unanusurika na maradhi mengi
ikiwemo moyo, presha, uzito
mkubwa, kiharusi na kansa.
Na hapa ndipo tunapopata yakini ya ukweli wa maneno ya
Mtume Muhammad (Rehma na
amani ziwe juu yake): Fungeni
mtapata afya.

Ili mtu awe na nguvu na


afya katika mwezi wa
Ramadhan na baada ya hapo,
lazima azingatie uchaguzi
wa vyakula. Mtu ajitahidi
kula chakula kutoka
mafungu makuu yafuatayo:
(a) mkate na nafaka (b)
maziwa, nyama, samaki, kuku,
maharage, (c) matunda na (d)
mboga za majani.

uonesha uzito wa
wajibu wa kufanya
kazi ya dawah kwa
Waislamu, Allah
ametahadharisha wasioifanya
kazi hii kupata laana kama alivyosema katika Quran; Hakika wale wafichao yale tuliyoyateremsha katika ubainifu, baada ya kuyabainisha kwa watu
katika kitabu, hao ndio waliolaaniwa na Allah na wamelaaniwa na kila chenye kulaani
(2:159).
Na maana ya laana ni kufukuzwa au kuwekwa mbali na
rehma za Allah (Subhaanahuu
wa taala). Matokeo ya kuwekwa
mbali na rehma za Allah ni kudhihiri kwa maovu na uharibifu
katika bara na baharini.
Mtume (Rehma na amani
ziwe juu yake) akaweka wazi
uzito wa kosa la kutokufanyika
dawah; Yeyote afichaye elimu
ambayo Allah hunufaisha watu
kwao katika mambo ya dini, Allah atamfunga makongwa ya
moto siku ya Qiyama (Ibn Majah).
Kuwa na Ilmu juu ya Uislamu kisha usiifikishe kwa wanadamu ni sawa na kuificha
elimu hiyo. Hivyo, mtu mwenye
elimu anawajibika kuifikisha
kwa watu kwa kufanya kazi ya
dawah.
Ni Waislamu wangapi wanaishi na wanadamu wenzao
nyumba moja, wanafanya kazi
nao ofisi moja, wanauza nao
soko moja kisha wasiwafikishie
ujumbe wa Allah, lakini wakawafikishia mambo waliyoyaona
katika runinga zao, au waliyoyasoma katika magazeti au
kusikia katika radio zao yasiyokuwa na manufaa nao? Kufanya hivyo ni sawa na kuificha
elimu ya Allah kwa viumbe
wake, ni khiyana ambayo Allah
huilipa kwa kumlaani mtendaji
(Allah atukinge na laana).
Nguzo za dawah:
Nguzo za dawah ni tatu:
Ujumbe unaolinganiwa, Mlinganiaji (Daai) na wenye kulinganiwa. Kila moja kati ya nguzo
hizi ina sifa zake, masharti yake
na malengo yake.
Ili kufanya kazi ya dawah
ipasavyo yampasa mwenye kutaka kuifanya kazi ya dawah
kuwa na elimu ya kutosha
kuhusu kila nguzo ya dawah.
Lengo la kazi ya dawah ni
kueneza mafundisho ya Uislamu kama yalivyofikishwa na
Mtume Muhammad (Rehma
na amani ziwe juu yake) ili dini

ya Allah iwe juu na dini za wale


waliokufuru ziwe chini.
Kama ni kuwalingania
Waislamu, lengo ni kusahihisha uelewa wao kuhusu mambo mbali mbali ya Uislamu,
ikiwemo itikadi (aqidah), kupiga vita ushirikina na kupiga vita
mambo ya uzushi (bida).
Mwana dawah akifanya
hivyo, ataonekana mgeni katika
jamii ya leo, siyo tu kwa wasio
Waislamu, bali hata kwa Waislamu wenzake. Mtume Muhammad (Rehma na amani
ziwe juu yake) alisema; Uislamu ulianza mgeni na utakuja
kurejea mgeni kama ulivyoanza. Basi hongera kwa watakaokuwa wageni.
Alipoulizwa Ee Mtume wa
Allah, hao wageni ni nani? Akajibu, Ni wale watakaokuwa
wanatengeneza pindi watu wanapoharibu (dini) (Tirmidhy).
Lengo la dawah limeelezwa
katika Suurat An-Nahl
(16:125): Na ita watu katika
njia ya Mola wako. Njia ya Allah ni Uislamu kwa mujibu wa
Quran na Sunnah.
Kwa hiyo inampasa mwenye
kutaka kufanya kazi ya dawah
ajiandae kwa elimu ili akifikisha basi iwe kwa mujibu wa
Quran na Sunnah, tena kwa
ufahamu wa wema waliotangulia.
Akielezea zaidi aya tuliyoitaja hapo juu, Sheikh Ibn Baaz
(Allah amrehemu) anasema:
Njia ya Allah, Mwenye nguvu,
Mtukufu, ni kujisalimisha
kwake, ni njia iliyonyooka, ni
dini ya Allah ambayo kwayo aliwatuma mitume.
Kwa hiyo hii ndiyo ambayo
watu walinganiwe kuiendea, si
madhehebu ya mtu fulani au
fikra za yeyote Njia ya Allah ni
ile ambayo Quran na Sunnah
sahihi za Mtume wa Allah zinamuelekeza mtu.
Ni lazima kwa wafanyao
kazi ya dawah katika Uislamu
kuwaita watu kwenye Uislamu
kamili na siyo kuibua mitafaruku miongoni mwa Waislamu, wala wasiwe wafuatao mitazamo ya watu (madhehebu)
kibubusa, wala kabila, wala
sheikh, wala kiongozi.
Bali lengo lake liwe kuthibitisha na kufafanua haki na
kuwakinaisha watu kuhusu
haki hiyo, hata kama kufanya
hivyo kutapingana na mtazamo
wa fulani na fulani (Min
Aqwaali Samaahat Shaykh Abdallah ibn Abdilaziz Fiy
Dawah, uk. 33-35).

21 Shaaban 1436, jumatatu Juni 8 - 14, 2015

13

www.islamicftz.org

uchumi na biashara
JAMAL ISSA

moja ya
kanuni ya
msingi ya
mfumo wa
fedha wa
Kiislamu
ni kuunga
nisha
fedha na
rasilimali
au bidhaa
badala ya
kufanya
fedha
yenyewe
kuwa
bidhaa.

hukrani na
utukufu ni
wake Mfalme
wa mbingu na
ardhi aliye pekee,
mwenye kustahiki
kuabudiwa kwa haki.
Sala na salam zimfikie
Mtume aliye msifika,
mjumbe wa Allah na rehma kwa walimwengu
wote. Kisha salam kwa
wanaofuata muongozo.
Ndugu mpenzi msomaji na mfuatiliaji wa
safu hii juu ya uchumi
na biashara katika mtizamo wa Kiislamu karibu tena kwa mara nyingine katika mfululizo
wa makala zetu.
Katika makala zetu
za matoleo yaliyopita

Ijarah: Mkataba wa
kukodishana kwa
malipo ya kodi
tulidurusu aina mbalimbali za ushirika, ikiwa ni
namna ya kufanya biashara na kuwezesha
kujenga uchumi usiojikita katika riba na
wenye kuzingatia

Dkt Idris
Rashid,
mkurugenzi wa
benki ya
Amana.

maadili. Katika makala yetu hii


ya leo, pia tutatizama namna
nyingine ya kufanya biashara
bila riba na kuzingatia maadili.
Napenda kusisitiza kuwa,
moja ya kanuni ya msingi ya
mfumo wa fedha wa Kiislamu

ni kuunganisha fedha na rasilimali au bidhaa badala ya kufanya fedha yenyewe kuwa bidhaa.
Namna nyingine ya kufanya
biashara katika utaratibu wa
Kiislamu inaitwa Ijarah.
Ijarah ni mkataba wa kukodisha rasilimali fulani kama vile
gari au nyumba kwa malipo ya
kodi, ambapo anaye kodisha
hubakia kuwa mmiliki na
anayekodi hunufaika kwa matumizi ya rasilimali hiyo. Anayekodisha anatakiwa amiliki
kwanza rasilimali hiyo kwa kuinunua au kujenga au kwa namna nyingine inayokubalika
kisharia kabla ya kukodisha.
Pia atawajibika kuihudumia
kwa huduma zinazostahiki kwa
nafasi yake kama mmiliki. Kwa
upande mwingine, anayekodi
anatakiwa kuitumia rasilimali

hiyo kwa matumizi yaliyokubaliwa katika mkataba na kuitunza.


Mkataba huu pia huweza
kutumiwa na taasisi za kifedha
katika kuwawezesha wateja
wake ambao wanahitaji rasilimali fulani katika biashara zao
au matumizi mengine.
Taasisi ya fedha kama benki
inaweza kununua rasilimali Fulani, kisha kuwakodisha wateja
wake kwa kipindi maalum, na
hivyo kunufaika na kodi ambayo ni njia mbadala ya pato la
benki lisilo tokana na riba.
Lakini taasisi za fedha nyingi
kama benki ni kiungo baina ya
wanaoweka akiba na wanaowekeza. Hivyo basi, taasisi
hizo zinatakiwa zisiwe mshirika
wa kudumu au kujishughulisha
katika miradi mingi ya kudumu
ambayo itaifanya ishindwe kufanya kazi yake kuu.
Hivyo, kama ilivyo kwenye
ushirika (Mushaarakah) ambapo kunakuwa na ushirika wa
kupungua mpaka benki inajitoa
katika umiliki, kadhalika katika
Ijarah benki inaweza kuhamisha umiliki baada ya mkataba
kuisha. In sha Allah tutadurusu
hilo katika makala ijayo.
jakham@rocketmail.com
+255713 996 031

Watu maarufu wasiokuwa Waislamu wasemavyo kuhusu Uislamu


Michael H. Hart,
Mwansayansi wa
anga za juu (Astrophysists) Mmarekani, muasisi wa mpango wa vitabu katika
mtandao (eBooks)

My choice of Muhammad to lead the list of the worlds


most influential persons may surprise some readers
and may be questioned by others, but he was the only man
in history who was supremely successful on both the religious and secular level
Tafsiri: Uchaguzi wangu kumchagua Muhammad kuongoza orodha ya watu muhimu zaidi
duniani unaweza kuwashangaza baadhi ya wasomaji na kuhojiwa na wengine, lakini alikuwa
mtu pekee katika historia aliyefanikiwa sana katika kiwango cha dini na dunia. (Michael H.
Hart, The 100:A Ranking of the Most Influential Persons in History)

21 Shaaban 1436, jumatatu Juni 8 - 14, 2015

14

www.islamicftz.org

Muda, uchache na wingi wa hedhi


Swali: aliulizwa Sheikh Muhamad bin Ibrahim Alu Sheikh
Allah amrehemu: Ni upi muda wa
hedhi?
Jawabu: Uchache wa hedhi ni
usiku na mchana, na wingi wake
ni siku kumi na tano. Lakini kauli
yenye nguvu zaidi inaeleza kuwa
hedhi haina muda maalum wa
wingi wala uchache, kwani hakuna ushahidi wa wazi katika hilo.
Na hili ndio chaguo la Sheikh Taqiyyud din (Allah amrehemu)
[Fatawa warasailu Sheikh Muhamad bin Ibrahim Alu Sheikh
2/97].
Je kiwango cha chini na cha
juu cha hedhi kinatambulika?
Swali: Aliulizwa Sheikh Muhamad bin Swaleh Al-uthaymin
(Allah amrehemu): Je kiwango
cha chini na cha juu cha hedhi kinatambulika kwa masiku?
Jawabu: Kwa kauli sahihi,
wingi wa hedhi au uchache haufahamiki kwa masiku. Allah anasema katika Quran: Na wanakuuliza juu ya hedhi. Waambie, huo
ni uchafu. Basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi. Wala
msiwaingilie mpaka wataharike
(2: 222). Allah hajaweka zuwio
ukomo kwa siku maalum,
isipokuwa zuwio ukomo
limewekwa kwa kutwaharika.

Na hapa ndipo tulipofahamu


kuwa sababu ya hukumu ni kuwepo au kutokuwepo kwa hedhi.
Wakati wowote itakapopatikana
hedhi, hukumu itathibiti, na
wakati wowote atakapotwaharika
hukumu itatoweka.
Ama suala la umri, kikomo na
muda halina ushahidi, pamoja na
kuwa kidharura ni jambo linalohitajia ufafanuzi. Na lau kama suala
la umri kikomo au muda lingethibiti kisharia, lingebainishwa katika Quran na Sunnah za Mtume.
Na kwa kulizingatia hilo, damu
yoyote atakayoithibitisha mwanamke kuwa ni hedhi, basi hiyo ni
hedhi, bila ya kuikadiria na muda
maalum. Isipokuwa kama damu
itaendelea kwa mwanamke na bila
ya kukatika, au itakatika kwa
muda mchache, kiasi cha siku au
siku mbili katika mwezi, hapo itahesabika kama damu ya ujusi.
(Fatawa na rasailu za sheikh ibn
Uthaimin 4/271).
Hedhi baada ya miaka 50
Swali: Aliulizwa Sheikh Muhamad bin Ibrahim Alu Sheikh
(Allah amrehemu): Ni ipi hukumu ya hedhi baada ya miaka 50?
Jawabu: Kauli sahihi ni kuwa
hedhi haifungwi kwa miaka hamsini. Isipokuwa muda wowote
damu ikiendelea kutoka, kwa sifa
na mpangilio wake, hiyo ni hedhi.

ALI (r.a) ANAVYOWAZUNGUMZIA


ABUBAKAR,
UMAR NA UTHMAAN (r.a):

inatoka Uk 9
ra? Sasa inapotokea wanawazuoni wa kisalafi wa
leo wakatofautiana, kwa nini baadhi
wachukue misimamo ya kuwakufurisha wengine kwa mambo yanayohitaji ijtihaadi za wanawazuoni?
Tatizo kubwa ni kujitakasa nafsi
zetu (Tazkiyatu-nnafsi) kunakopelekea kuwaona wengine si masalafi wa
kweli au hata si masalafi kabisa.
Tatizo jingine, ni kujikita katika
kufukua mabaya ya wengine (Al jarh
wat-tadiyl) kiasi kwamba hakuna
aliyesalimika sasa. Badala ya kujikita
katika kuzitakasa nafsi zetu dhidi ya
makosa yetu wenyewe twajikuta
tukitakasa nafsi zetu na makundi
yetu dhidi ya wengine.
Tatizo letu jingine, ni kuwachukulia Waislamu ambao bado hawajashika mwenendo wa kisalafi
kama makafiri. Mtazamo huu unazalisha kibri na kujiona (Al-ujub),

Ama hedhi ikipoteza mpangilio damu ya hedhi kwa nyanja zote.[


baada ya umri huo, haitozingatiAl-maj-muatulkamilahlimualwa kuwa ni hedhi, bali itazinlafaati Sheikh Ibn Saad 7/98].
gatiwa kuwa ni damu ya ujusi.
Na neno la Bi Aisha (Allah
Mwanamke ana miaka
amridhie): Mwanamke
hamsini na mbili,
atakapofikisha miaka
ndani ya kiasi cha
hamsini hutoka kwenye
siku tatu, humjia
ukomo wa hedhi
damu kwa
(Ahmad). Habari
nguvu
ya Bi Aisha inaaS w a l i : Alshiria wingi wa
iulizwa
Sheikh
fat-wa kwa
ukomo wa heAbdul Aziz
mwanamke
dhi huwa kabin Baz:
tika umri
Kunamwawa kiislam
huu, au imetanamke ana
sheikh Shabani Mussa
jwa kwa kuchunumri wa miaka
ga misingi ya
52. Ndani ya siku
kisharia, kwani kiatatu, hutokwa na
sili masuala yanayodamu kwa nguvu,
husu aina mbalimbali za
na siku zinazosalia kadamu ni ya kimaumbile
tika mwezi damu hutokama hakuna dalili inayka kwa wastani. Je damu
oitoa katika kundi la damu.
hii inazingatiwa kuwa ni
(Fatawa na rasailu za Sheikh
damu ya hedhi, hasa ikizinMuhamad bin Ibrahim 2/96).
gatiwa yeye ana umri zaidi ya
miaka 50 na tukizingatia baadhi
Ikipatikana damu kwa vigya wakati damu humjia baada ya
ezo baada ya miaka 70
mwezi, miezi miwili, au miezi mitatu. Je ataswali faradhi wakati
Swali: Aliulizwa Sheikh Ab- damu inamtoka? Na je ataswali
dur Rahmani Assaadiy (Allah swala za sunna na zile swala za
amrehemu): Mwanamke ana- usiku?
pofikisha umri wa miaka sabini na
Jawabu: Mwanamke kama
damu yake ikaendelea katika ka- huyu anatakiwa aizingatie damu
waida yake, je ataketi?
hii iliyompata kuwa ni damu ya
Jawabu: Mwanamke aliye- ujusi kwa umri wake na kukosa
fikisha umri wa miaka 70 na damu kwake mpangilio. Hali halisi inayhaijasita na inaendelea kumtoka, ofahamika kutoka kwa Bi Aisha,
mwanamke huyo atasimama kuwa mwanamke akifikisha umri
kuendelea na ibada kwani sahihi wa miaka 50, damu ya hedhi huni kuwa, hedhi haina ukomo kwa katika na hukoma kupata mimba.
mtu mwenye umri mdogo au umri Kupata damu bila ya mpangillio,
mkubwa, na kihukumu hii ni na umri wake ni dalili ya kuwa

Mwanamke mmoja zaidi


ya miaka 50 hupata hedhi
kwa utaratibu uliozoeleka
na mwingine hupata kwa
utaratibu usiozoeleka
Swali: Aliulizwa Sheikh Muhamad bin Swaleh Al-uthaimin
(Allah amrehemu): Kuna mwanamke ana miaka zaidi ya 50 na
hupata hedhi kwa utaratibu uliozoeleka na kuna mwingine hupata
hedhi kwa utaratibu usiozoeleka,
isipokuwa huona rangi ya manjano au hudhurungi?
Jawabu: Mwanamke anayepata hedhi katika utaratibu uliozoeka, kwa kauli sahihi ya wanazuoni, damu yake itakuwa ni
damu ya hedhi kwa sababu hakuna umri kikomo katika suala la hedhi. Na kwa hivyo, damu yake itachukuwa hukumu maarufu za
damu ya hedhi, ataacha kuswali,
kufunga, kukutana na mumewe
na atalazimika kuoga na kulipa
funga nk.

Kutoka kwa Khalid Al-ahmara alisema, Aliulizwa Abdillahi


ibn Hassan (Radhi za Allah ziwe juu yake) kuhusu Abu Bakr
na Umar (Radhi za Allah ziwe juu yao) akasema: Allah awape
amani na asimpe amani yule asiyewapa wawili hao amani
(Sherh Usuuli Itiqaad Ahlu s-Sunnah, Mjalada wa 7 uk. 1381).

Usalafi usiwagawe Wanasunnah


hususan kwa vijana wa kisalafi ambao hawajakomaa kielimu, hali iliyosababisha kuwa mahiri katika kukosoa makosa ya wengine na kutumia
muda mwingi kuwatafuta wenye
kukosea kuliko kutafuta elimu ya
kujua yaliyo sahihi katika usalafi.
Utakuta kijana mbichi katika usalafi akihifadhi majina ya
masheikhwapotofu alioambiwa
kuwa hawa hawako katika manhaj
ya salaf na orodha ya masheikh wa
kisalafi wanaokubalika. Huu ni msiba mkubwa. Tatizo jingine, ni utii
wa moja kwa moja kwa masheikh
wakubwa ambao hututolea fataawa.
Yaani akisema sheikh ndiyo basi.
Uislamu haufundishi utii wa moja
kwa moja kwa binadamu mwingine

hiyo si hedhi na analazimika


kuswali na damu hiyo itahesabika
kama damu ya ujusi ambayo
haimziwii kuswali wala kufunga,
wala haimzuwii mume wake kumuingilia. Kwa kauli sahihi zaidi
za wanazuoni, analazimika kutawadha katika kila swala na atajihifadhi kwa pamba, au kwa namna
nyingine, kama alivyosema
Mtume kwa mwanamke mwenye
damu ya ujusi: Tawadha kwenye
kila swala. (Imepokewa na
Bukhari) (Kitabu fataawad
Daawah cha sheikh Ibn Baz
2/72).

ila kwa mitume tu. Lakini leo inaibuka misimamo mikali ya tasubi si
za kimadhehebu, bali kwa masheikh
tuwapendao. Hata mtu apewe hoja
yenye mashiko, hakiuki msimamo
wa sheikh wake.
Kibaya zaidi usalafi huu wa sasa
umeshachukua msimamo wa kitaifa, huku baadhi wakifuata wanawazuoni wa Saudia, wengine wa Yemen
nk. Tofauti za kisiasa za nchi za Kiislamu zimeingia hata kwenye misimamo ya kisalafi ya leo.
Jambo jingine, ni hili la masalafi
wa leo kunyamaza kimya kuhusu
watawala. Sheikh Ibn Taymiyyah aliwakosoa sana watawala, kinyume
na masalafi wa leo walioshupalia kukosoa masheikh wa kisunnah tu.

Imekuwa kama alama ya usalafi


ni kunyamaza hadi baadhi ya watawala wanawaona masalafi kama
masufi tu, wasiojishughulisha na
dunia inayowazunguka.
Ndugu katika imani, tukumbuke
kwamba, harakati za makundi ya
kisalafi kama harakati nyingine za
kibinadamu hazikosi upungufu na
hata makosa. HiIi haifanyi usalafi
uwe jambo baya. Kukosea ndio ukamilifu wa ubinadamu.
Makosa ya makundi ya kisalafi si
makosa yaManhaj Salafiyyah, bali
ni makosa ya binadamu wanaotumika kama nyenzo ya kufikisha
manhaj hiyo. Ushahidi ni kuwepo
mitazamo mbalimbali ya kisalafi; na
bila shaka hakuna kundi lenye hati-

miliki ya usahihi mia kwa mia.


Harakati za kisalafi zina mengi
mazuri si tu kwa Waislamu, bali wanadamu wote, lakini makosa hayawezi kukosekana. Je haiwezekani
kufifisha tofauti zetu na kuacha kushambuliana, ili tuelekeze nguvu
zetu kwenye mambo ya msingi kwa
maslahi ya Uislamu?
Kama masalafi hawatahisi chochote ndani ya mioyo juu ya madhila
yanayowafika Waislamu ingawa ni
watu wa bida, na badala yake kufurahia, ni taswira gani ya usalafi tunaijenga kwa Waislamu?
Masalafi wanao mchango
mkubwa katika kusahihisha itikadi
potofu, lakini ni vema tuelewe peke
yetu hatuwezi kujitosheleza kwa kila
kitu; na umma unahitaji kufikishiwa. Tutawezaje kufikisha kwa watu
ambao daima twawaona hawafai
kutukaribia au sisi kuwakaribia?

21 Shaaban 1436, jumatatu Juni 8 - 14, 2015

15

www.islamicftz.org

Kuelekea uchaguzi 2015

NA YUSUFU AHMADI

akati fulani,
Tanzania ilitaka
kujiunga na
taasisi ya kiislamu ya kimataifa ya OIC, jambo ambalo lilipelekea kampeni kali ya kuzuia jambo hilo
kutoka kwa makanisa. Hili ni
suala la uhusiano wa kimataifa ambalo kama Waislamu
tunapaswa kuwahoji wagombea mbalimbali wa nafasi
za urais wanaojitokeza hivi
sasa.
Katika nchi zilizoendelea,
moja ya mambo muhimu
ambayo wapiga kura wengi
wanayaangalia wanapowapima wagombea waliojitokeza
kuwania nafasi kubwa kama
ya urais au uwaziri mkuu
huwa ni sera zake kuelekea
mataifa ya nje (Foreign policies).
Wengi wa wapiga kura na
wachambuzi humtathmini
kwa kina mgombea na sera
zake jinsi atakavyoshirikiana
na mataifa ya nje, na pia
atakavyokabiliana na
changamoto mbali mbali zilioko nje ya taifa lao ili mradi
tu wanaona zinaathiri maendeleo yao.
Japo kila nchi huwa na
sera zake maalum za nje zilizoandikwa kama ilivyo hapa
nchini kwetu, ila kwa baadhi
ya nchi kubwa za wenzetu,
mgombea nae huwa ananadi
sera zake kuelekea mataifa ya
kigeni.
Mfano, wakati Rais wa
Marekani Barack Obama
anawania nafasi hiyo kwa
mara ya kwanza, moja ya sera
zake kuelekea mataifa ya nje
ilikuwa ni kurejesha uhusiano ulioharibika baina ya
taifa lake na ulimwengu wa
Kiislam.
Jambo ambalo alilifanya
muda mfupi mara baada ya
kushika nafasi ya Urais kwa
kwenda nchini Misri katika
chuo kikuu cha Al-Azhar na
kuhutubia mataifa ya ulimwengu wa Kiislam, japo
maneno ya hotuba hiyo na
matendo ya nchi yake ni sawa
na bure.
Hivyo ndivyo ilivyo desturi
ya wagombea wa mataifa
hayo, kwani bila kueleza kwa
ufasaha sera zako kuelekea
mataifa ya kigeni itakuwa
vigumu sana kushinda nafasi
kubwa kama ya Rais, kwani
sera hizo zina nafasi yake katika maendeleo.
Tuje hapa nchini kwetu,
kwa sasa watanzania wanaendelea kushuhudia
mbwembwe, vituko na vim-

Stephen Wassira

Dkt Mohammed Gharib Bilal

Edward Lowassa

Dkt John Magufuli

Frederick Sumaye

Balozi Ali Karume

Watangaza nia
watuambie na
sera zao za Nje
bwanga vya watangaza nia ya
kugombea nafasi adhimu na
kubwa katika Urais kutoka
Chama cha Mapinduzi
(CCM).
Kila mtangaza nia amejaribu kusema kile atakachowafanyia watanzania endapo atapitishwa na chama
chake na kisha kupigiwa kura
katika uchaguzi mkuu wa
hapo Octoba 25 mwaka huu
na kushinda.
Yapo mengi ambayo
yamesemwa na watangaza
nia hao katika sera zao mbali
mbali, lengo likiwa ni kuushawishi umma wa Tanzania
uwapigie kura .
Lakini kwa bahati mbaya
au vinginevyo, takriban watangaza nia hao hakuna hata
mmoja aliewaelezea watan-

Lakini kwa
bahati mbaya
au vinginevyo,
takriban
watangaza
nia hao
hakuna
hata mmoja
aliewaelezea
watanzania
sera zake
kuelekea
mataifa ya
kigeni.

zania sera zake kuelekea


mataifa ya kigeni.
Kama nilivyoeleza hapo
juu, sera hizi kwa wenzetu ni
muhimu sana, kwani zinabainisha namna gani taifa
lao litakavyo kuwa na muingiliano na mataifa ya nje katika nyanja mbali mbali.
Na kwa dunia ya sasa iliyo
katika mfumo wa kibepari
unaosimamiwa na nchi za
Magharibi, huwezi ukazungumzia na kuandaa mikakati ya jinsi ya kuzitatua
changamoto za nchini kwako bila kuwa na mikakati ya
namna ya kushughulikia
masuala mengine yalioko
nje ya taifa lako.
Mfano, katika hawa watangaza nia wetu, yupo mgombea mmoja amesikika ak-

isema yeye ataendesha nchi


katika misingi ya ujamaa,
japo hautakuwa sawa na ule
wa Mwalimu Nyerere.
Ila katika maelezo yake
juu ya sera hiyo, mtangaza
nia huyo hajawaambia watanzania jinsi atakavyoweza
kupambana na wanakidedea wa ubepari katika sera
zake kuelekea mataifa hayo
ya magharibi.
Inafahamika wazi kwa
dunia ya sasa kujitangaza
wewe ni mjamaa hiyo tayari
ni vita tosha, je, kajiandaa
vipi dhidi ya hilo?
Mwingine anasema
kuwa, atalifanya taifa hili
liwe la viwanda na uchumi
wa kati, ukiangalia mikakati
atakayotumia inajionesha
kabisa ni ya ndani ya nchi tu,
pasina kuonesha mikakati
ya nje.
Nae huyu ilibidi awaambie Watanzania, ni mikakati
ipi ameandaa dhidi ya
mataifa ya kigeni ili kuhakikisha anadhibiti ongezeko
la bidhaa kutoka nchi za nje
ambazo kwa kiasi kikubwa
ndio zimechangia kuua viwanda anavyovililia yeye.
Leo, hii hata vijiti vya kuchokonolea meno (Toothpick) katika maeneo mbali
mbali ya nchi yetu vinatoka
nchini China wakati nchi
yetu ina misitu y akutosha,
je, sera zake ni zipi katika kukabiliana na hili janga.
Siku za hivi karibuni, tumekuwa tukimsikia Rais

Mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa akilalamika


na kuwaasa viongozi wa Afrika kuwa makini na mkataba wa ushirikianao wa kiuchumi (EPA) ulioandaliwa
na wazungu kuwa ni wakinyonyaji kutokana na yaliyomo ndani yake.
Hapa watanzania hawana budi kuwauliza watangaza nia hao, mambo kama
haya ya mikataba wanayajua
vema, na kama ndio sera zao
zinasema nini kuhusiana na
mambo hayo kutoka kwa
wenzetu wa huko ughaibuni
ambao kwa kiasi kikubwa
wana athari katika maendeleo yetu.
Huyo alikuwa ni wa viwanda, mwingine yeye
anasema ataendesha nchi
kwa kutumia gesi tu ya Mtwara, hapa alitakiwa
awaambie watanzania ni
sera gani kuelekea mataifa
ya nje zitakazomsaidia kukabiliana na mashirika
makubwa duniani ya kibiashara (Multinational corporations) ambayo nayo
yamekuwa yakilalamikiwa
kunyonya rasilimali za nchi
m a s i k i n i , Ta n z a n i a
ikiwemo.
Watanzania lazima
waelewe kuwa kwa ulimwengu wa sasa ulioko katika
mfumo wa utandawazi huwezi ukampima mgombea
wa nafasi kubwa ya Urais
kwa kuangalia sera zake za
ndani tu.

21 Shaaban 1436, jumatatu Juni 8 - 14, 2015

makala

16

www.islamicftz.org

Wanahabari
wa Kiislamu
tufuatilie
siasa za nchi
NA KHALID OMARY

yombo vya habari hapa


nchini vimekuwa na
mchango mkubwa katika
kuihudumia jamii kwa kutoa habari mbali mbali zinazoelimisha, kuburudisha na kuhabarisha, ingawa kumekuwa na mbinu nyingi za
kudhoofisha harakati zinazofanywa
na vyombo hivyo.
Kwa hapa nchini, vipo vyombo
mbali mbali vya habari vya kidini na
visivyo vya kidini. Lengo langu ni kuvizungumzia hivi vya kidini, huKuwa katika susan vya Kiislamu, wamiliki na
waendeshaji wake kwa ujumla.
chombo
Kabla sijaingia kwenye
cha Kiislam maudhui
ya makala, hadi sasa,
haimaanishi kuna vyombo vya habari vya Kiislamu ikiwemo redio, magazeti
tuwe
runinga visivyozidi 20, idadi
tunafuatilia na
ambayo ni ndogo ukilinganisha
mambo ya
na vile vya Kikristo.
Katika utafiti wangu mdogo
Uislam
nilioufanya, hasa baada ya mipekee,
jadala mikubwa ya sheria
kwani yapo mbalimbali zinazoathiri fani ya
mambo mengi habari hivi karibuni, baadhi ya
wamiliki ama waendeshaji wa
yanayo
vyombo vya Kiislamu walizunguka
ishindwa kunipa ushirikiano,
jamii ambayo jambo ambalo linaonesha hawafuatilii masuala ya siasa na ya
nayo ni
kijamii.
muhimu
Miswada na sheria hizi
mbalimbali zinagusa wadau wa
katika
moja kwa moja, wakmaisha yetu habari
iwemo wamiliki na waandishi,
ya kila siku hivyo ilitegemewa viongozi
hawa wa vyombo vyetu vya Kiislamu wangekuwa na uelewa wa kutosha kuhusiana na sheria hizo.
Sheria ambazo zinaweza kuathiri
vyombo vya habari zilizopitishwa hivi
karibuni ni pamoja na ile ya makosa
ya mtandao na ile ya takwimu.
Kadhalika, mswada mwingine
ambao huenda ukajadiliwa na kupitishwa hivi karibuni ni ule wa huduma
za vyombo va Habari.
Muswada wa Huduma za Vyombo
vya Habari una mambo yanayowahusu wamiliki wa vyombo vya habari,
waandishi wa habari pamoja na wale
wanaofanya kazi za uandishi kwa
kuchangia kuandika makala kwenye
magazeti.
Lakini katika muswada wote wa
sheria hiyo mambo kadhaa yaliweza
kuvuta na kugonga vichwa vya habari
nchini.
Moja kati ya hayo ni kutoka kwenye

Pichani juu
ni uzinduzi
wa gazeti
jipya la
Kiislamu
(IQRA)
uliofanyika
wiki
iliyopita
katika
msikiti wa
Mtambani
jijini Dar es
Salaam.
Chini,
mhariri wa
redio
Imaan,
Kassim
Lyimo
akiwa
katika moja
ya semina
za mafunzo
ya ndani
kwa
watendaji
Imaan
Media.

kipengele cha 14 (b)(iv) kinachoelekeza chombo chochote


cha habari binafsi kujiunga na
shirika la umma kwa ajili ya
taarifa ya habari ya kila siku ya
saa mbili usiku.
Ni kweli kuwa sio lazima
uwe mwandishi au mtangazaji
ndiyo uwe mmiliki au muendeshaji wa chombo chochote cha
habari kiwe cha Kiislamu au
kisicho kuwa cha Kiislamu, lakini kwa kuwa unaendesha
chombo cha habari nawe unatakiwa ufuatilie masuala ya kihabari, ikiwemo sheria zinazoathiri habari.
Miongoni mwa niliozungumza nao kwa ajili ya kupata
mawazo yao juu ya muswada
huo alikiri kuwa hafahamu
chochote kuhusu muswada
huo.
Haishangazi kuwa ukimuuliza mwanahabari au
mwendeshaji wa chombo cha
habari cha Kiislamu kuhusu
mambo yanayoendelea bungeni ambayo yana athari kwa
Uislamu asijue chochote, huku
akisahau kuwa haya yanayotekelezwa leo ambayo tunayalalamikia ni matokeo ya sera

zilizopangwa jana.
Inawezekana kama
kungekuwa na chombo kimoja
kinachowaunganisha waendeshaji wa vyombo vya habari vya
Kiislamu kusingekuwa na sintofahamu kama hii.
Hii ni kwa sababu dini ya
Uislamu ina mafundisho yake
ambayo hayaendani na mifumo ya uendeshaji wa vyombo
visivyo vya Kiislamu kwa sababu mbali mbali.
Kwa mfano, vyombo vya Kiislamu haviwezi kutoa picha
inayoonesha maumbile ya
mwanamke katika hali yoyote
ila awe amejisitiri.
Moja ya mambo ambayo
yanaonyesha kuwa baadhi wamiliki ama waendeshaji wa vyombo vyetu vya Kiislamu hawapo makini katika kazi zao na
kusahau kuwa hiyo ni taaluma
nyeti kabisa hapa ulimweguni
ni lile nililokutana nalo katika
kituo kimoja cha redio.
Nilipotembelea chumba
chao cha habari wakati wakiandaa taarifa ya habari ya
mchana, nilikuta watangazaji
na waandishi waliokuwepo
wakinakili habari kutoka

kwenye magazeti mabalimbali


ya kila siku na kuzigeuza katika
mfumo utakaoweza kusomwa
kama taarifa ya habari ya
kwenye redio.
Hali ile ilinistaajabisha na
kuniacha nikiwa nimepigwa
na butwaa na kujiuliza maswali
mengi huku nikikosa majibu.
Kwakweli jambo hilo linakiuka misingi ya habari, halikupaswa kutendwa na chombo
hicho cha Kiislamu. Au ndio
rasilimali fedha za kutuma
waandishi kutafuta habari
hamna? Kwa hali hii tutafika?
Waislamu wote tuliomo katika fani hii ya habari, pamoja
na wale ambao ni wachangiaji
katika vyombo vyetu ni wajibu
wetu kufuatilia matukio
mbalimbali ya kisiasa na kijamii, kwani hii ndio kazi yetu
ya msingi.
Na utafiti wetu uwe wa asili
(original) sio wa kunakili utafiti
wa waandishi wenzetu, tena
kwa mambo ya nchini mwetu.
Kuwa katika chombo cha Kiislam haimaanishi tuwe tunafuatilia mambo ya Uislam pekee,
kwani yapo mambo mengi yanayoizunguka jamii ambayo
nayo ni muhimu katika maisha
yetu ya kila siku. Waislamu hatuishi katika kisiwa. Matukio
mbalimbali yanayotokea katika nchi yanaathari kwa Uislam
na Waislam.
Na ijulikane vilevile kuwa
sio watu wa habari pekee wanaotakiwa kufuatilia mambo
yanayotokea duniani, bali pia
ni haki na wajibu wa Waislam
wote kwa ujumla, hususan katika karne hii ambapo kila raia
amekuwa mwanahabari.
Shukran kwa vifaa vya kisasa vya mawasiliano na katiba
inayohakikishia raia haki za
msingi, ikiwemo ya kujieleza.
Inasemwa njia pekee ya
kumshambulia adui yako ni
umjue kwanza.Sasa kama
hatufuatilii mambo tutawezaje
kumkabili adui yetu? Bila
utafiti huna haki ya kusema.

21 Shaaban 1436, jumatatu Juni 8 - 14, 2015

makala ya kimataifa

www.islamicftz.org

indi kifo kikikaribia na wagonjwa


mahututi wanapopitia maumivu
yasiyovumilika, wajibu wa
daktari unapaswa kubadilika kutoka kuponya hadi
kuondoa maumivu, kwa
kumsaidia kufa kama anavyotaka mgonjwa. Hili si
suala la uhai dhidi ya kifo,
bali ni kuamua jinsi ya
kufa, na kimsingi si uamuzi
wa daktari, ni uamuzi wa
mgonjwa - Dkt. Marcia
Angell.
Huyo ni daktari wa asasi
iitwayo Die with Dignity
ya huko Marekani akielezea kampeni inayoendelea duniani ya kutaka
madaktari waruhusiwe kukatisha uhai wa wagonjwa
wao wanapoamua kutaka
kufa kuepuka maumivu ya
maradhi. Dkt. Angell
alinukuliwa akisema:
Watu wanastahiki nafasi
ya kuchagua mwishoni
mwa uhai wao na madaktari wanapaswa kuruhusiwa kuwasaidia wagonjwa
kupata huduma ya mwisho
wa uhai waitakayo.
Dkt. Angell anapigania
kutungwa sheria ambazo
zitajulikana kama Death
with Dignity laws, yaani
sheria za kufa kwa heshim a . Hi i m a a n a y a k e
mgonjwa kuendelea
kuteseka kwa maumivu
hadi kifo ni kufa pasina
heshima. Inadaiwa
kwamba, daktari kulazimika kumpa mgonjwa dawa
ya kumuua ili kukatisha
maumivu yake ni jambo
gumu, kwa hiyo wagonjwa
wawekewe njia ambazo
wao wenyewe watajihudumia (self service) wanapoamua kufa, ili daktari asijihisi mkosaji kwa kumsaidia mgonjwa kujiua.
Harakati za haki ya
kufa zimepamba moto
nchini Marekani, Afrika ya
Kusini na Ulaya. Baadhi ya
majimbo kama vile Origon,
Washington na Vermont
yalishapitisha sheria za
kufa kwa heshima na wagonjwa wanaotaka kuamua
namna ya kufa huhamia
jimboni humo.

17

Madaktari wanapogeuka wauaji

Btittany Maynard
mwenye umri wa miaka 29
aliamua kuhamia Origon
na kujihudumia vidonge
vya barbiturates alivyopewa na daktari wake na
akafa. Kabla ya kuzuka
kampeni hizi, hilo lingeitwa kosa la kumsaidia mtu
kujiua. Lakini sasa si kosa
tena, bali haki ya mgonjwa
ambayo inapaswa
kulindwa.
In a d a i w a kw a m b a ,
mgonjwa kupewa dawa za
kujiua si kosa, kwa sababu
ni uamuzi wake mwenyewe,
na uamuzi wa mtu juu ya
mwili wake ni jambo lililoruhusiwa kikatiba.
uran inakataza
mtu kujiua pale
Allah Taala aliposema Na
wala msiziue nafsi zenu,
hakika Allah ni mwenye
huruma kwenu (4:29).
Katika hadith ya Mtume
(Rehma na amani ziwe juu

ssala alaykum msomaji


wa safu ya Tovuti za
Kiislamu,ni jumatatu
nyingine tunakutana
tena hivyo hatuna budi
kumshukuru Yule ambaye aliyeumba mbingu na ardhi bila ya
nguzo yoyote naye ni Mwenyezi
Mungu mwingi wa rehma
mwenye kurehemu.
muumba Hii leo tutataiangazia tovuti kongwe ya Islam
qa,com,ambayo ilianzishwa na
Seikh Muhammad Al Munajjid
mnamo mwaka 1997.Hii ni tovuti
ambayo imejikusanyia wasomaji
wengi ulimwenguni kote kutokana na kutumia lugha zaidi ya

Huko nyuma,
madakatari
walikuwa
wapingaji
wakubwa
wa kusaidia
wagonjwa
kujiua.
Jumuiya ya
madaktari
nchini
Marekani
iliwahi
kutoa tamko:
Daktari
kumsaidia
mgonjwa
kujiua ni
kinyume na
wajibu wake,
ambao ni
kumsaidia
mgonjwa
kupona.

kumi katika ufikishaji


dini ya Mwenyezi
Mungu.
Tovuti hii imejikita
kwenye fatawa mbalimbali
na kujibu maswali ambayo
Waislamu wengi yamekuwa
yakiwatatanisha.Kama jina
la ytovuti lenyewe lilivyo Islam qa likimaanisha maswali
na majibu juu ya Waislamu.
Katika utoaji wa huduma
hiyo wameigawa tovuti katika makundi tofauti tofauti
ambayo yatakuwezesha kusoma kile unacho kihitaji kwa
urahisi na ufasaha zaidi,makundi
hayo yanaeleza mada zilizopo

yake) kuhusu madhambi ya


aina saba yenye kuangamiza akataja; ...na kuuwa
nafsi ambayo Allah ameiharamisha ila kwa haki
(Bukhari Na. 2615, Muslim
Na. 145).
Huko nyuma, madakatari walikuwa wapingaji
wakubwa wa kusaidia wagonjwa kujiua. Jumuiya ya
madaktari nchini Marekani
iliwahi kutoa tamko: Daktari kumsaidia mgonjwa
kujiua ni kinyume na wajibu wake, ambao ni kumsaidia mgonjwa kupona.
Lakini kwa mujibu wa
uchunguzi uliofanyika huko
Ulaya na Marekani kwa kuwahoji madaktari 21,000,
asilimia 58 kati yao waliunga mkono utoaji wa huduma ya kuwasadia wagonjwa
kujiua, kwa mujibu wa
gazeti la The Atlantic la
Marekani.
Majimbo zaidi nchini
Marekani yanaelekea au

TOVUTI ZA

Na Khalid Omary
ndani yake. Miongoni mwa mada
hizo ni historia ya Uislam, Malengo makuu ya Imaan katika

yako katika hatua mbali


mbali za kutunga sheria kuruhusu wagonjwa kusaidiwa kujiua. Wagonjwa wa
baadhi ya magonjwa yanayochukua muda mrefu hadi
mtu kufa kama vile kansa
na ukimwi wanapigania
haki ya kujiua.
Nchini Afrika ya Kusini,
kampeni hii imekolea siku
za hivi karibuni chini ya
kauli mbiu My Life, My
Choice, yaani Uhai wangu,
Chaguo langu. Katika taarifa yao kwa vyombo vya
habari, Die with Dignity SA
wanasema: Tunaamini
kwamba, wananchi wa Afrika ya Kusini wanaotaabika kwa maumivu ya mwishoni mwa uhai wao wananyimwa haki yao kinyume cha sheria.
Hata hivyo, Waziri wa
Afya wa Afrika ya Kusini,
Aaron Motsoaledi, anapinga madai ya sheria ya kuruhusu wagonjwa kusaidi-

kipengele hicho kinazungumzia madhumuni ya Imaan lakini pia kipo


kipengele,namna ya kuishi
na familia yako kwa kufuata misin gi ya Quran na
Sunna za Mtume Muhammad (Rehma na amani
ziwe juu yake).
Vipengele vingine vinavyopatikna ni kile kinacho
wahusu wanawake wa kislamu na namna yao ya kuishi, demokrasia na uislamu
huku ikitoa rejea za namna
masahaba walivyokuwa
wakiishi katika dhana hii ya
demokrasia bila kusahau huwa

wa kufa. Waziri alisema:


Madaktari si Mungu, akiwa
na maana haki ya kuamua
mtu afe au asife ni ya Mungu pekee.
Akipinga suala hilo,
Waziri huyo alisema, kutoa
ruhusa kwa madaktari kuwasaidia wagonjwa kujiua
kutatoa mwanya wa familia
kupanga njama za kuwaua
wazazi au jamaa zao kwa
kutaka kurithi mali zao au
hata kulipwa pesa za bima
za maisha walizokata.
Huu ni msiba mwingine
baada ya ule wa ndoa za jinsia moja kuhalalishwa na
mataifa ya magharibi. Yote
haya yanaashiria mwisho
wa ustaarabu wa magharibi
umekaribia. Imamu,
mshairi maarufu, Ahmad
Shawqiy (Allah amrehemu),
alisema: Hakika mataifa
h u b a k i a k u w e p o kw a
maadili mema, iwapo
maadili yao yakitoweka na
wao pia watatoweka.

wanatoa ushauri juu ya jambo


ambalo litakuwa linajutatiza.
Vilevile ukitembelea wavuti
huu utaweza kusoma vitabu
nmbalimbali vya dini ya Uislamu
kuhusu dini lakini pia vipo vilivyoandika Uislamu na maisha ya
kidunia pamoja na masuala ya
sayansi ambavyo vitaweza kukusaidia katika kuongeza maarifa
yako. Unaweza kutembelea kupitia www.Islam-qa. Hayo ndio
machache ya tovuti hiyo niliyoweza kukuandalia katika wiki
hii,tukutane wiki ijayo panapo
majaaliwa.
0683110006

21 Shaaban 1436, jumatatu Juni 8 - 14, 2015

18

www.islamicftz.org

Kagimu Mk. (Science teacher) 0752 224 550

GET READY FOR ENGLISH PAPER:


Choose the correct answer:

1. Rachael and I in the compound before


the visitors arrived.
(a) were playing (b) play (c) plays (d) were playing
(e) were play
2.If she .. We would see her beautiful dress.
(a) Came (b) come (c) would come (d) will come (e)
had come
3. They were dancing in the classroom.
(a) Saw (b) see (c) sea (d) seen (e) sewn
4. Maryam . Food for the family now .
(a) cooks (b)cook (c) cooked (d) has cooked (e)
cooking.
5. Neither Nasser nor Khalid
brave enough to kill the lion.
(a) am (b) can (c) are (d) were (e)was
6. We shall .. all children of God.
(a) be (b) his (c) was (d) are (e) is
7. Grade seven pupils are looking forward to
.. for their national examinations.
(a) sit (b) seat (c) sitting (d) seating (e) will sit
8. Alot of maize in Iringa next year.
(a) was produced (b) produce (c) will be produced
(d) produces (e) produced.
9.There . Be an East African
tour in December 2015.
(a) are (b) will (c) will be (d) will have (e) will be
10. She a pen before the teachers asked
for it.
(a) hidden (b) hide (c) hid (d) had hidden (e) has
hidden
11.He managed .. the snake by
hands.
(a) kill (b) killed (c) to kill (d) to killed (e) to killing.
12.I usually .before I go to bed .
(a) prays (b) praying (c) pray (d) are praying (e) are
pray.
13. Where . They gone ?
(a) is (b) has (c) has (d) was (e) have
14. Tanzanians will be for presidency towards the end of the year.
(a) Vote (b) voted (c) voting (d) votes (e) votting

15. A few weeks ago our school .. by the


minister of education.
(a) was visited (b) visited (c) was visiting (d) visiting (d) had visited

SECTION B: GRAMMAR:

16. That is the place .. Bata


shoes are made.
(a) who (b) which (c) where (d) whose (e) whom
17. Ali is one of .. Pupils in his
school.
(a) Best (b) Better (c) Better than (d) the best (e)
good
18. Tanzania is .. the East African
countries.
( a) Either (b) among (c) between (d) at (e) as
19. Boys girls need to have
some time to rest .
(a) as well as (b) as well (c) also.. but (d) more
than
20.The place .. we sat was very wet .
(a) were (b) where (c) which (d) on (e) while.
21. A good driver always drives

(a) careful (b) carefully (c) very care (d) care (e)
cares
22. Ramadhani is .. than Juma.
(a) Active (b) activier (c) more activist (d) more
active (e) the most active
23. They help us whenever we get
stuck,..?
(a) Arent they (b) do they (c) dont they (d) arent
us (e) werent they.
24. T hat car belongs to them. It is
..
(a) Theirs (b) theirs (c) they are (d) theres (e)
theres
25.Anita is fond .. Playing in
class.
(a) for (b) of (c) about (d) with (e) to
26. The teacher roared angrily, .
Were making noise?
(a) Why (b) which (c) when (d) who (e) whom
27. Mwalimu Julius kambarage Nyerere was

.. Honest man.
(a) the (b) a (c) an (d) some (e) any.
28. He is as as a bee.
(a) Dangerous (b) brave (c) coward (d) cunning (e)
busy.

SECTION C: COMPOSITION:

Re- arranges these sentences to make a meaningful


story. Use the letters A-J:
29. who was also the first prime minister of Tanganyika .
30. This beautiful country was also under Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere as its first president.
31. 1961 was the time for the British to let Tanganyika, be independent.
32. In 1984 he resigned and let Hon. Ali Hassan
mwinyi be in power from 1985 to 1995.
33. After being given full power, he managed to
unite Tanganyika and Zanzibar in 1964.
34. Hon.Ali Hassan Mwinyi passed the relay stick
to Hon Benjamin William mkapa.
35. From that union a beautiful country was born .
36. Currently, Tanzania is a peaceful country shining under the leadership of Hon. Jakaya Mrisho
Kikwete.
37. Handed over the country to the late Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere in 1962.
38.Sir, Richard Turnbull, the last British governor
in Tanganyika.

ANSWERS FOR GET READY SCIENCE


DIGEST AS ON MAY 25, 2015
1. A
2. B
3. C
4. C
5. C
6. B
7. B
8. B
9. C
10. A

11. C
12. B
13. A
14. B
15. B
16. C
17. D
18. B
19. C
20. D

21. B
22. B
23. B
24. C
25. B
26. B
27. B
28. C
29. A
30. B

31.C
32. C
33. B
34. B
35.B
36.B
37.C
38.B
39.A
40.C

41.A
42.D
43.C
44.B
45.B
46.C
47.C
48.D
49.C
50.B

kona ya watoto

ZAHRA EBRAHIM

i Sumaiya (Radhi za Allah ziwe juu yake) na familia yake ni miongoni


mwa watu wachache wa
kwanza kuukubali Uislamu. Yeye
na familia yake walipitia mateso
mengi mikononi mwa makafiri
ambao walikuwa wakiwalazimisha
kuacha Uislamu.
Licha ya umri wake, Sumaiya
(Radhi za Allah ziwe juu yake) alisimama kidete katika njia ya haki na
alikuwa mvumilivu hata pale
makafiri walipomkokota yeye na
mumewe, Yasir, na mwanawe Am-

Sumaiya (Radhi za Allah ziwe juu yake)

mar (Radhi za Allah ziwe juu yao)


katika mchanga wa moto wa jangwani na kuwapiga mawe.
Mtume Muhammad (Rehma
na amani ziwe juu yake) aliwaambia kuweni wavumilivu na aliwaahidi pepo.
Sumaiya (Radhi za Allah ziwe
juu yake) alifariki kutokana na
mateso, na hivyo basi kuwa mwan-

amke wa kwanza kufa shahidi tangu Mtume Muhammad (Rehma


na amani ziwe juu yake) alipoanza
kuita watu katika dini ya haki, Uislamu.
Baada ya vifo vya wazazi wake
wote wawili, Ammar (Radhi za Allah ziwe juu yake) alipendwa sana
na Mtume Muhammad (Rehma
na amani ziwe juu yake). Kila

Mtume Muhammad (Rehma na


amani ziwe juu yake) alipozungumza kuhusu familia ya Sumaiya
(Radhi za Allah ziwe juu yake)
alikuwa akiisifia.
Zoezi:
Mtume Muhammad (Rehma
na amani ziwe juu yake) aliwaahidi nini familia ya Yasir?

Ni nani mtoto wa Sumaiya (Radhi za Allah ziwe juu yake)?


Kwa nini makafiri waliwatesa
Sumaiya na familia yake (Radhi
za Allah ziwe juu yake)?
Soma Surat Arrahman na
Surat Al-Waaqiah (pamoja
na maana) na elezea kuhusu
pepo kwa maneno yako mwenyewe.

21 Shaaban 1436, jumatatu Juni 8 - 14, 2015

watoto / tangazo

www.islamicftz.org

vipindi Radio imaan


Wakati

Muda

11:00 .11:05

05 min

11:05 .11:30

3
4

19

vipindi TV imaan
Kipindi

S/No:

Wakati
TIME

Adhana ya Alfajir

06:00 06:20

20MINSheikh:
NYIRADI ZA ASUBUHI

RECOR

25 min

Dua

06:20 06:35

15MINSheikh:
NASAHA ZA ASUBUHI

RECOR

11:30 .12:00

30 min

Nyiradi za asubuhi

12:00 .01:00

1 hr

06:35 06:45

10MINSheikh:i.Twaha
KILMA KIZURI

RECOR

01:00 .01:20

20 min

07:00 07:20

20MINSheikh:
DIRA YA HABARI

01:20 .04:00

3 hrs 40 min

07:20 07:30

10MIN

CHACHU YA DIRA

LIVE

04:00 .05:00

1 hr

07:30 08:00

30MIN

SUHUFA ZA MAGAZETI

LIVE

05:00 .05:05

05 min

Mukhtasar wa dira

10

08:00 10:00

2HR

MADA NYETI

LIVE

05:05 .06:00

55 min

Salaam za asubuhi

11

10:00 11:00

1HR

USALAMA BARABARANI

MARU

10

06:00 .06:45

45 min

Ulimwengu wa Kiislaam

13

11:04 11:35

31MIN

MAWAIDHA

RECOR

11

06:45 . 06:50

05 min

Adhana ya Dhuhr

14

11:35 12:00

25MIN

BULUGHULMARAM

RECOR

12

06:50 .07:20

30 min

Tarjuma

18

12:14 12:24

RECOR

13

07:20 .08:00

40 min

Mimbar zetu

20

12:26 12:56

10MINSheikh:
ENGLISH LECTURE

30 MIN

14

08:00 .09:00

1 hr

Mawaidha

22

13:00 13:13

13MINSheikhENGLISH
Nassor LECTURE
Bachu

RECOR

15

09:00 .09:20

20 min

Dira ya habari/matangazo25

14:00 14:45

45MIN

RECOR

16

09:20 09:45

25 min

Tauhiid

26

14:46 14:50

17

09:45 .09:50

05 min

Adhana ya al-asr

27

18

09:50 .10:20

30 min

Tarjuma

29

19

10:20 .11:00

40 min

Kalima

20

11:00 .11:20

20 min

Dira ya habari/

21

11:20 .12:00

40 min

Nasaha za washairi

22

12:00 .12:30

30 min

Adhkarul masaa

23

12:30 .12:35

05 min

Adhana ya Magharib

24

12:35 .01:00

25 min

Qur aan Tukufu

25

01:00 .01:45

45 min

Nasaha marudio

26

01:45 .01:50

05 min

Adhana ya Ishaa

27

01:50 .02:20

30 min

Qur aan Tukufu

28

02:20 .03:00

40 min

Mafundisho ya Qur aan

29

03:00 .03:20

20 min

Dira ya habari/

30

03:20 .04:20

1 hr

31

04:20 .05:00

40 min

32

05:00 .06:00

33

06:00 .11:00

Nasaha za asubhi
Dira ya habari/
Majlis ya tv Imaan
Tafsir ya Qur aan

Muda
DURATION

Kipindi
PROGRAM

ST

RECOR

Sheikh Mselem Ally

Ust:Ally Ajran
Sheikh:

NAFASI YA MWANAMKE
KUTOKA SHULENI

RECOR
Hasan

RECOR

14:50 15:50

4MINSheikhPROMO
Mohammed Nduli
1 HRSheikh:
UISLAM NA TIBA

15:52 16:22

30MINSheikh:
BUSATI LA KISWAHILI

RECOR

31

16:24 16:55

30MINSheikhQUR'AN

RECOR

S/No:

TIME

35

17:11 17:33

37

17:45 18:00

38

DURATION

MARU

PROGRAM

STATU

Ly
30MIN
SIMULIZI ZA BIBI ZAINAB Kasim
RECOR
Sheikh Mishari

15MIN

ANNASHEED

RECOR

18:00 18:20

20MIN

NYIRADI ZA JION

RECOR

39

18:20 18:40

20MIN

DUA + ADHANA

RECOR

40

18:40 18:57

17MIN

FAHAMU USIYO YAJUA

RECOR

42

19:00 19:30

30MIN

MAWAIDHA

RECOR

44

19:31 20:04

33MIN

MAWAIDHA

RECOR

47

20:10 20:32

22MIN

ALINGANIWE

RECOR

Kipindi maalum

50

20:40 - 21:10

30 MIN

SUHUFA ZA MAGAZETI

MARU

Mawaidha

51

21:10 - 23:10

1 hr

Familia

52

23:15 - 23:30

5 hrs

Usiku wa Qur aan

54

23:30 06:00

Sheikh:
Sheikh:
Sheikh

Sheikh:
Sheikh:

Ust:Othmaan Thabit

2HRSSheikh:
MADA NYETI

MARU

15 MIN
KABLA HUJALALA
Baba Kiruwasha
6:30HRS
USIKU WA QURAN
Sheikh:

RECOR
LIVE

Mwanza

105.6 Mhz

Kigoma

Arusha

104.5 Mhz

Tabora
101.6 Mhz
92.5 Mhz

90.8 Mhz

Dodoma

104.5 Mhz

Moro

102 Mhz

104.5 Mhz
Dsm

Masafa ya Imaan FM
1
2
3
4
5
6

Daresalaam
Morogoro
Arusha
Mwanza
Kigoma
Tabora

104.5 Mhz
96.3 Mhz
90.8 Mhz
105.6 Mhz
92.5 Mhz
101.6 Mhz

7
8
9
10
11
12

Mbeya
Dodoma
Ruvuma
Mtwara
Zanzibar
Pemba

90.3 Mhz
102 Mhz
94.2 Mhz
90.9 Mhz
104.5 Mhz
104.5 Mhz

Mbeya

104.5 Mhz

104.5 Mhz

104.5 Mhz

Ruvuma
Mtwara
94.2 Mhz

90.9 Mhz

21 Shaaban 1436, jumatatu Juni 8 - 14, 2015

20

Wanahabari
www.islamicftz.org
wa Kiislamu
tufuatilie
siasa za
nchi

Uk 16
21 Shaaban 1436, jumatatu Juni 8 - 14, 2015

Ansaar Sunnah
si dhehebu jipya
kama wasiojua
wanavyo
ambiwa, kwa
sababu kila
imam katika
maimam wanne
wa Ahlusunnah
wal Jamaaa
walikubaliana
katika kufuata
sunnah katika
kuyaendea
masuala yote
ya dini ya
Kiislam.

YUSUPH AMIN

nsaar Sunnah, jina hili


limekuwa likisikika
kwa miongo kadhaa
sasa kwa walio wengi,
lakini maana sahihi ya jina hili ni
ipi? Answaaru Sunnah ni watetezi
wa sunnah za Mtume (Rehma na
amani ya Allah ziwe juu yake).
Sunnah ni kitendo, neno au
jambo alilolifanya Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) au aliloliona linafanywa kisha kulinyamazia, ambapo mambo hayo
yote Waislamu wanapaswa
kuyafanya kwa kuzingatia usahihi
wake.
Mtume Muhammad (Rehma
na amani ziwe juu yake) amesema: Hakika dini ni nyepesi, hatoitia uzito mtu dini ila itamshinda
(Bukhari). Kwa mujibu wa hadith
hii, ni wazi kwamba masuala kadha wa kadha ya dini ya Kiislam
kama vile kuziendea hukumu za
sheria katika mambo ya kijamii
hutegemea Quran na Sunnah
(hadith).
Utaratibu wa kuzinusuru Sunnah za Mtume ndio ulikuwa
mwenendo wa waja wema waliotangulia. Kwa mfano ukirejea
kitabu kiitwacho kitabu Arrisala,
Imam Shafii (Allah amrehemu)
alikuwa akiitwa: Naaswiru sunnah wa Qaamiul bidai yaani
mtetezi wa sunnah za Mtume na
mwenye kuvunjavunja bida.
Lakini hivi leo wako Waislam
wanaolichukia jina Answaaru
Sunnah. Neno Ansaar ni wingi
wa neno la kiarabu Naaswiru,
yaani mwenye kunusuru.
Kwa hiyo, Waislam wanaojinasibu na Imam Shafii (Mungu amrehemu) wangepaswa kuwa Answaru Sunnah, lakini kinyume
chake wako wanaowapinga na
hata kuwapa majina mabaya
kama vile Wahabiya, watu wa
bida na kadhalika.
Kwa hiyo, Ansaar Sunnah si
dhehebu jipya kama wasiojua wanavyoambiwa, kwa sababu kila
imam katika maimam wanne wa
Ahlusunnah wal Jamaaa walikubaliana katika kufuata sunnah katika kuyaendea masuala yote ya
dini ya Kiislam.
Kauli za maimam hao zinasema inapothibiti hadith ya Mtume
basi hayo ndiyo madhehebu yangu (Imamu Shafii) na pia wakasema mnapoona kauli yangu imekwenda kinyume na kauli ya
Mtume wacheni kauli yangu,
mfuate ya Mtume (Imam Abu
Hanifa).
Kwa muda mrefu baada ya
karne tatu njema kupita, sunnah
za Mtume hazikuwa zinaeleweka
vilivyo, na si hivyo tu, bali watu
hata hadith za uwongo walizifuata

BASUTA

Taasisi inayoongoza harakati za Sunnah


wakihisi kuwa ni za kweli.
Sababu hizo zilipelekea vijana
wa Kiislam waliosoma elimu ya
dini na kuelimika kuona haja ya
kuzinusuru sunnah za Mtume
(Rehma na amani ziwe juu yake).
Katika eneo la Afrika Mashariki, hususan nchi ya Kenya walijitokeza maimam kadhaa waliojitahidi kuzihuisha sunnah za Mtume
na pia kupambana na bidaa kama
vile Imam Sheikh Ali Mazrui, ambapo ushahidi wake upo katika
kitabu chake kinachoitwa Hidaayatul-atfaali.
Pia, Sheikh Abdallah Saleh Alfarsy aliwahi kuandika vitabu
mbalimbali vinavyopinga bida na
kuibua ukweli, hali iliyopelekea
kuibuka malumbano na mijadala
baina ya Waislamu.

Ushabiki wa madhehebu na
ujima ni miongoni mwa mambo
yanayotajwa kusababisha tofauti
(Ikhtlafu) kwa umma wa Waislam
ulimwenguni, japokuwa waanzilis h i w a m a d h e h e b u h ay o
hawakupitiwa na hali hii.
Pia, imeibainika kuwa, tofauti
zinazojitokeza zinatokana na baadhi ya Waislam kuacha kutumia
dalili za Quran na Sunnah katika
kuyaendea mambo, badala yake
kutumia fikra na utashi zaidi au
kufuata kauli za masheikh pasina
dalili.
Uelewa tofauti kuhusu sunnah
baina ya Waislam na watu kujiingiza katika utungaji wa hadith za
uwongo ni baadhi ya changamoto
zilizopelekea wanazuoni wa dini
ya Kiislam Tanzania kuanzisha

jumuiya mbali mbali za Ansaar


Sunnah.
Baada ya kuona haja ya kuunganisha jumuiya hizi za Ansaar
Sunnah, Baraza Kuu la Jumuiya
za Ansaar Sunnah (BASUTA)
likaanzishwa mnamo mwezi Agosti 2007 katika mkutano uliofanyika Kibaha mkoani Pwani, likiwa
kama Baraza elekezi la wana Sunnah wote nchini, kwa lengo la kuziunganisha jumuiya za kisunnah
chini ya uongozi mmoja.
Sheikh Kombo Ali Fundi, ambaye ni Mhitimu wa Chuo Kikuu
cha Madina, ni Amir wa baraza
hilo nchini Tanzania.
Katika mahojiano yake na
gazeti la Imaan amesema, watu
wanaonusuru Sunnah za Mtume
ni lazima wajisalimishe katika

kupokea sharia kwa kutanguliza


Quran na Sunnah kuliko akili, na
pia mapenzi yao yawe kwa ajili ya
Allah, na kuchukia kwao kuwe ni
kwa ajili ya Allah.
Aidha, Sheikh Kombo amebainisha baadhi ya sifa za watu wa
Sunnah kuwa ni pamoja na kuyaendea mambo ya dini katika hali
ya uadilifu, kati kwa kati bila ya
kupindukia mipaka, kuwa na
subra katika kauli na daawa, kuwa
na pupa ya umoja na mshikamano, kuwaita watu kwenye hilo
na kupiga vita utengano.
Sifa nyingine ni kutokuwa na
Imam mkuu ambaye watu wote
watachukua maneno yake yote au
kuiga vitendo vyake vyote ila
Mtume (Rehma na amani ziwe
juu yake).
Kujiepusha na mizozo katika
dini, kuwapa heshima wema waliotangulia, na kuitakidi kuwa
mwendo wao ni sahihi, kwani wao
ni watu wa karne bora zilizosifiwa
na Mtume (Rehma na amani ziwe
juu yake).
Kuhusiana na masuala ya
itikadi, Sheikh Kombo amesema,
watu wa Sunnah hawana budi
kuafikiana katika mambo ya aqida na katika kumtegemea Allah
pamoja na kufuata sababu za maisha na kujikita katika Ucha Mungu.
Malengo ya Basuta
Moja ya lengo kuu la Basuta ni
kuwakilisha wanasunnah wote
wa Tanzania katika majukwaa ya
kitaifa na kimataifa.
Pia Basuta imejikita katika
kuziunga mkono juhudi za wanazuoni wa kisunnah na jumuiya
shirika zinazofanya kazi ya kuwaongoza watu wa kada mbalimbali kwa misingi ya Quran na
Sunnah sahihi za Mtume Muhammad (Rehma na amani ya Allah ziwe juu yake).

hutolewa na kuchapishwa na The Islamic Foundation, P.O.Box 6011 Morogoro, Tanzania E-mail: imaanmedia3@gmail.com

You might also like