You are on page 1of 19

China yalazimisha Waislamu kuuza nguruwe, pombe - Uk 15

huwatoa watu gizani

Sheikh Nassoro Bachu:


ISSN 5618 - N0. 005 BEi: Sh800/- KSH80/- Ush1,200/-

Mhadhiri maarufu
Afrika Mashariki Uk 7
21 Rajab 1436, Jumatatu, mei11 - 17, 2015

Maandamano

ya Waislamu

www.islamicftz.org

Sheikh Ponda
atoweka Moro

Uk 3

Maandalizi yaiva

Tamko la mwisho lasubiriwa

Vituo vya
kuandikisha
wapiga kura
vyawekwa
makanisani

Head office, Lumumba Street, Opp: Viwanja vya Mnazi Mmoja, P. O Box 779 Dar es Salaam, Tanzania
Tell: 255 22 2182482/ 255 222184419, Fax: 255 22 2181424, E-mail: info@Binslum.com

Uk 5

21 Rajab 1436, jumatatu Mei 11 - 17, 2015

habari

www.islamicftz.org

Walimu wa madrasa wafunguka


Wataka elimu ya dini ithaminiwe
NA WAANDISHI WETU

icha ya kiwango kidogo


cha ada kinachotozwa
katika madrasa nyingi
zilizopo katika jiji la
Dar es Salaam, bado wazazi
wengi wamekuwa wazito kuwahimiza watoto wao kutafuta
elimu ya dini.
Kadhalika, uchunguzi wa
gazeti la Imaan umeonyesha

kuwa wazazi wengi hawalipi ada


za masomo za watoto wao, kutokana na kutothamani elimu hiyo
sawa na wanavyothamini shule.
Waandishi wetu waliotembelea madrasa wamegundua kuwa
kiwango cha ada katika madrasa
nyingi jijini Dar es Salam ni kati
ya Tsh. 1,000 hadi Tsh. 5,000
kwa mwezi, lakini walimu wa
madrasa waliozungumza na
gazeti la Imaan wamesema wa-

zazi wengi wamekuwa hawalipi


ada hiyo.
Miongoni mwa madrasa
walizozitembelea, ni pamoja na
Nurul-Islamiyyah na Azhari zilizopo kata ya Mabibo, Tul-Tarbiyyah iliyopo Kigogo na Istiqaamah ya Magomeni, ambazo
zote hutoza ada isiyozidi Tsh.
3,000 kwa mwezi.
Hata hivyo, walimu wa madrasa hizo wamesema wanafun-

zi wengi walioandikishwa hawahudhurii


madrasa ipasavyo na wazazi wengi hawalipi ada. Ustadh Hussein Dilunga,
mwalimu wa madrasa ya Nurul-Islamiyyah iliyopo mtaa wa jitegemee, Mabibo
amesema, mahudhurio hafifu na kutolipa ada kunasababishwa na mwamko
mdogo wa wazazi pamoja na ratiba za
shule ambazo hazitoi fursa ya muda kwa
watoto kwenda madrasa.
Ustadhi Dilunga, ambaye ameanza
kufundisha madrasa toka mwaka 1988
alisema, kuzuka kwa elimu ya ziada muda
wa jioni (tuition) inazuia watoto wa Kiislamu hususani wale walioanza sekondari
kuhudhuria madrasa. Zamani vijana
walikuwa wanarudi kutoka shuleni saa
nane, wanapata riziki huko majumbani,
kisha baadae wanakwenda madrasa kufundishwa dini, lakini siku hizi muda huo
haupo kabisa, alisema Dilunga akionesha namna vijana wa Kiislamu wanavyokosa fursa ya kujifunza dini yao kutokana na mfumo wa kielimu uliopo.
Hakuna ulazima wa kusoma masomo ya ziada. Enzi zetu tulikuwa tunasoma
ndani ya masaa manane na tulifaulu, vipi
leo ionekane mtoto hawezi kufaulu bila ya
masomo ya ziada, Dilunga alihoji.

Akielezea sababu za mahudhurio


mabovu, Ustadh huyo amesema, wazazi
hawaoni umuhimu wa kuhimiza watoto
wao kusoma elimu ya dini kwa sababu
wanaamini elimu ya dini haitawapatia
vijana wao ajira na kipato.
Naye Ustadh Omari Jokoo wa Madrasat Istiqama anasema, kuna hatari kubwa
ya kizazi cha Waislamu wa sasa kupotea
na kuingia katika majanga makubwa
kutokana na kushindwa kujifunza dini
yao. Ustadh Jokoo anaamini wazazi na
jamii ya Kiislamu kwa ujumla haitoi ushirikiano wa kutosha kwa walimu, na hivyo
walimu hao wanakumbana na changamoto zinazorudisha nyuma maendeleo
ya elimu.
Katika madrasa, mafundisho ya fiqhi,
quran, tabia, tajwid, tawhid, tafsiri ya
quran, na sira ya Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) yanafundishwa. Katika
hali hii, lazima uwe na walimu wasiopungua watatu, ambao wote wana mahitaji
yao ya kimaisha, wanahitaji kulipwa. Bila
ushirikiano wa wazazi, ni vigumu kwa
kweli kuendesha madrasa, alisema Ustadh Jokoo.
Kwa upande wa madrasa za nje ya jiji
la Dar es salaam, hali ni mbaya zaidi. Ustadh Omari Kinumbi anayefundisha madrasa Daiyya Islamiyya wal Jihad iliyopo
kata ya masaki, tarafa ya Sungwi, katika
wilaya ya Kisarawe amesema, walimu wa
vijijini wanapata tabu kubwa katika
utekelezaji wa jukumu lao la ufundishaji
wa madrasa.

Dhi Nureyn, Al Muntada

wasaidia wagonjwa wa moyo


NA KHALID OMARY

aasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation yenye makao makuu mkoani Iringa kwa kushirikiana na taasisi ya Al
Muntada Islamic Trust ya nchini
Uingereza imefanikisha zoezi la kutibu watoto
wenye magonjwa ya moyo bila ya kuwafanyia
upasuaji kwa kuziba matundu yaliyopo kwenye
moyo kwa kutumia kifaa maalum kiitwacho
Cathlet.
Tiba hiyo inafanyika kwa mara ya kwanza
hapa nchini kupitia idara ya tiba ya upasuaji wa
moyo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kushirikiana na madaktari bingwa kutoka hospitali ya Prince Sultan Cardiac iliyopo katika jiji la
Riyadh nchini Saudi Arabia.
Zoezi hilo ambalo lilianza Jumamosi iliyopita litakuwa ni la siku tisa hadi Ijumaa ya wiki hii.
Muasisi na Mwenyekiti wa taasisi ya Dhi

Afyais natural
source of sweet
drinking water
from underground stream
which is blended
with essential
minerals to support and aid perfect metabolism.

Nureyn, Sheikh Said Abri, amewahimiza wananchi kutumia fursa hiyo, kwa kuwapeleka watoto wao kupata matibabu hayo yanayotolewa
bure.
Hakika ni furaha kutoa matumaini mapya
kwa watoto hawa wenye ugonjwa wa moyo, na
ni furaha zaidi kwa mzazi ambaye atamuona
mtoto wake, kipenzi chake, anazaliwa upya na
kuaga machungu ya maradhi yaliyokuwa
yakimsumbua, amesema Sheikh Said Abri.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa hospitali ya
Taifa ya Muhimbili, Dk. Hussen Kidanto alisema, huu ni mwaka mzuri kwa upande wa tiba
kwa Tanzania.
Hadi kufikia mwezi April mwaka huu jumla
ya wagonjwa 453 wamefanyiwa upasuaji wa
moyo na wagonjwa 110 wamefanyiwa uchunguzi wa mishipa ya damu na utaratibu wa kushirikiana na wataalam kutoka nje ya nchi tutauendeleza, ameeleza Dk. Kidanto.

nyakati za swala

WATERCOM LIMITED
P.o. Box 20409, Plot N.4005, Kisarawe11 area
Temeke,Daresalaam, Tanzania
www.watercomtz.com, E-mail:info@watercomtz.com

Na.
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15

MJI
DAR ES SALAAM(6.75 S, 39.25 E)
ZANZIBAR(6.17 S, 39.25 E)
TANGA(5 S, 38.25 E)
MOROGORO(8 S, 37 E)
MTWARA(10.67 S, 39 E)
ARUSHA(3 S, 36 E)
DODOMA(6 S, 36 E)
MBEYA(8.5 S, 33 E)
KIGOMA(5 S, 30 E)
MWANZA(2.75 S, 32.75 E)
KAGERA(4.66 S, 30.67 E)
TABORA(5.5 S, 32.83 E)
SHINYANGA(3.75 S, 33 E)
SINGIDA(5.5 S, 34.5 E)
IRINGA(9 S, 35 E)

FAJR
5:13
5:12
5:15
5:23
5:18
5:21
5:25
5:40
5:48
5:34
5:44
5:37
5:34
5:30
5:32

DHUHUR
12:20
12:23
12:24
12:29
12:21
12:33
12:33
12:45
12:57
12:46
12:54
12:46
12:45
12:39
12:37

ASR
3:42
3:42
3:46
3:50
3:41
3:56
3:55
4:06
4:19
4:09
4:17
4:08
4:07
4:01
3:58

MAGHARIB
6:15
6:15
6:21
6:22
6:10
6:32
6:29
6:37
6:54
6:46
6:52
6:42
6:44
6:35
6:29

ISHAA
7:23
7:24
7:29
7:30
7:19
7:40
7:37
7:46
8:02
7:54
8:00
7:50
7:52
7:43
7:37

21 Rajab 1436, jumatatu Mei 11 - 17, 2015

habari

www.islamicftz.org

Maandamano ya Waislamu
Waislamu
wakiwa katika
moja ya
mikusanyiko. (na
mpiga picha wetu)

NA WAANDISHI WETU

kiwa zimebaki siku chache kabla


ya maandamano makubwa ya
kushinikiza Serikali kutekeleza
madai ya Waislamu, Serikali imeshauriwa kutumia busara ili kuepusha
madhara yanayoweza kutokea kutokana na mgogoro huo.
Ushauri huo umetolewa na waumini wa dini ya Kiislamu waliozungumza na timu ya gazeti la Imaan iliyopitia misikiti 10 ya jijini Dar es Salaam
ili kukusanya maoni juu maandalizi ya
maandamano hayo.
Waislamu wengi waliohojiwa, hususan vijana, wamesema kama Serikali
haitafanyia kazi madai yao, ni wazi
maandamano hayo hayaepukiki.
Sisi tumeshajipanga na kuhamasishana kujitokeza kwa wingi kufanya
maandamano ya amani kuelezea hisia
zetu, Halfani Abdallah, muumini katika msikiti wa Idrissa, Kariakoo ameliambia Imaan na kuongeza: Tunawasikiliza viongozi wetu kwa sasa. Tu-

Na Mwandishi Wetu

aharuki ilitanda mwishoni mwa wiki iliyopita juu


ya hali na usalama wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh
Ponda Issa Ponda baada ya kuibuka
kwa taarifa za kuhamishwa kutoka
Morogoro na kupelekwa kusikojulikana.
Hata hivyo, baada ya taarifa za
mkanganyiko kutoka mamlaka za
magereza baadae ilithibitika kuwa
Sheikh Ponda amehamishiwa
Ukonga, ingawa sababu halisi bado
hazijajulikana.

naamini kimya cha Serikali ni ishara ya


kutupuuza.
Msimamo huo wa Waislamu umekuja kufuatia Mwenyekiti wa Jumuiya
na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh
Musa Kundecha kutangaza kufanyika
kwa maandamano nchi nzima May 15
mwaka huu, iwapo madai ya Waislamu
hayatopatiwa ufumbuzi.
Madai muhimu zaidi ya Waislamu
kwa sasa ni pamoja na kuachiliwa kwa
dhamana kwa viongozi wa Kiislamu
walio magerezani, kusimamishwa kwa
zoezi la kamata kamata ya uonevu,
ikiwemo kuwaachia masheikh, walimu
na wanafunzi wa madrasa wanaoshikiliwa, na kushughulikiwa kwa suala la mahakama ya kadhi.
Hata hivyo, suala ambalo lililogusa
hisia za Waislamu wengi ni ufungaji
holela wa madrasa na kamata kamata
ya waumini wa dini ya Kiislamu.
Uchunguzi wa gazeti Imaan umebaini kuwa kutokana na kadhia ya madrasa iliyoendeshwa na jeshi la Polisi,
Waislamu wameingiwa na hofu na

wanajihisi kama si raia halali wa nchi


hii, hali iliyopelekea kadhia hiyo kuwa
gumzo katika mikusanyiko mbalimbali ya wananchi, hususan Waislamu.
Hili sasa ni suala la kufa na kupona.
Uhai na ustawi wa Waislamu na Uislamu unategemea jinsi tutakavyojitokeza
kuibana Serikali ili ishughulikie suala
hili, Mzee Hassan wa msikiti wa Tungi,
Temeke alisema.

Yapo mambo ya kufunika kombe


mwanaharamu apite, lakini sio hili.
Ukicheza na mbwa utaingia nae
msikitini, alitahadharisha.
Suala jingine lililoamsha hasira za
Waislamu ni kunyimwa dhamana kwa
viongozi wa Kiislamu walioko magerezani, wakihoji iweje Askofu Josephat
Gwajima awe nje kwa dhamana, lakini
viongozi wa Kiislamu wanaozea mage-

Msimamo huo wa Waislamu


umekuja kufuatia
Mwenyekiti wa Jumuiya na
Taasisi za Kiislamu nchini,
Sheikh Musa Kundecha
kutangaza kufanyika
kwa maandamano nchi
nzima May 15 mwaka huu,
iwapo madai ya Waislamu
hayatopatiwa ufumbuzi

3
reza, huku wakifanyiwa vitendo vya
kudhalilishwa?
Hamisi Kilongole wa msikiti wa
Chihota, Tandika alihoji: Au ni umati
wa watu waliojitokeza kumuunga
mkono Gwajima ndio ulioitisha Serikali? Nasi tutajitokeza Ijumaa, huenda
Serikali itaelewa uchungu wetu.
Kilongole pia aliasa Serikali itoe
kibali cha maandamano hayo, kwani
lengo si kufanya vurugu bali kuelezea
hisia zao.
Waislamu hao walisema, si haki
hata kidogo kuendelea kuwashikilia viongozi wa Kiislamu huku sheria inatoa
mwanya kwao kupatiwa dhamana
hizo.
Leo hii ni miaka miwili sasa Sheikh
Ponda yuko gerezani, tena akiwa ni
mgonjwa. Cha ajabu hapatiwi dhamana kisa Mkurugenzi Wa Mashtaka
nchini hataki, hiyo sio haki hata kidogo, amelieleza Imaan, mmoja wa viongozi waandamizi wa Baraza la Vijana
wa Kiislamu nchini, akiongea na
mwandishi katika msikiti wa
Kichangani, Magomeni.
Kiongozi huyo, akiongea kwa hisia,
alisema, huenda hayo yanatokea kutokana na vijana wa Kiislamu kutokuonesha hisia zao juu ya mambo yanayojitokeza nchini.
Waislamu wengi walioongea na
waandishi wa gazeti la Imaan walidai
kuwa Serikali kwa muda mrefu imekuwa haiyatili manani madai yao, jambo ambalo wamesema, linajenga taswira ya wao kubaguliwa.
Madai ya Waislamu hapa nchini
yanapopelekwa Serikalini ni nadra
sana kufanyiwa kazi, hapa dhana iliopo
ni kuwa Waislamu ni wakorofi tu, jambo ambalo si sahihi, Maneno Saidi wa
Buguruni amelalamika.
Kuhusiana na suala la Mahakama
ya kadhi, Waislamu hao wamesema,
Serikali imepuuza suala hilo kwa
muda.
Mmoja wa waumini, mkazi wa
Kibaha, mkoa wa Pwani alisema, Waislamu wamedai mahakama ya kadhi
kwa muda mrefu ila hawapewi bila
sababu za msingi, hali inayoonesha
kuwa bila kibali cha maaskofu Waislamu wa Tanzania hawawezi kupata haki
zao.
Mahakama hiyo iliingizwa katika
ilani ya chama cha Mapinduzi (CCM)
mwaka 2005, kuwa kikiingia madarakani kitawapatia Waislamu mahakama hiyo, lakini hadi leo kimeshindwa
kufanya hivyo.
Wakati hayo yakijiri, viongozi wa
Kiislamu walipotafutwa na gazeti hili
kuzungumzia mustakabali wa madai
yao na uwepo wa maandamano hayo,
Sheikh Rajabu Katimba alisema: Sina
cha kueleza kwa sasa, tulishamaliza,
kwani hukupata tamko letu? Wakati
muafaka ukifika tutazungumza.

Sheikh Ponda atoweka Moro


Uthibitisho kutoka kwa mke wa
Sheikh Ponda, Khadija Ahmad, jioni ya siku ya Jumamosi kuwa alionana na Sheikh Ponda na kuzungumza nae katika gereza la Ukonga
zilituliza kidogo nyoyo za Waislamu.
Kwa mujibu wa Khadija, baada
ya jana yake kuzungushwa na
maafisa wa gereza, Jumamosi aliomba kuonana na Mkuu wa Gereza
la Ukonga ambaye alimruhusu kuo-

nana na mumewe.
Khadija aliliambia gazeti la Imaan kuwa Jeshi la Magereza
lilimwambia mumewe amehamishiwa Dar es Salaam kwa usalama
wake kwa sababu katika gereza la
Morogoro kuna mgogoro wa
wakulima na wafugaji.
Mwanzo wa kadhia:
Taarifa zilizosambaa awali na
kusababisha taharuki kubwa zilianza siku ya Ijumaa baada ya wakili

wa Sheikh Ponda, Juma Nassoro,


familia yake na viongozi wa Kiislamu kugundua kuwa Sheikh Ponda
alihamishwa kutoka Morogoro
kimya kimya.
Baada ya kugundua hilo, wakili
Nassoro aliliambia gazeti la Imaan
kuwa wana wasiwasi mkubwa
kuhusu alipo na usalama wa Sheikh
Ponda baada ya kutokuwepo taarifa
rasmi za kuhamishwa kutoka Morogoro.

Tulipata habari kwamba Sheikh


Ponda hayuko tena Morogoro. Sisi
kama mawakili wake hatukujulishwa kuhusu kuhamishwa kwake na
wapi anakopelekwa ili tuweze kufuatilia hali yake kama tulivyokuwa
tukifanya tangu awekwe ndani.
Tulipojaribu kufuatilia ni wapi
anaweza kuwa amepelekwa, tulipata fununu kwamba huenda yuko gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam,
UK 5
alisema wakili Nassoro.

21 Rajab 1436, jumatatu Mei 11 - 17, 2015

www.islamicftz.org

tujikumbushe

Rajab, Mwezi wa Kumbukizi - 2


Vita vya kukomboa Jerusalem vilianza ndani ya Rajab
Ilipiganwa zaidi ya miaka 100
NA MWANDISHI WETU

adaraka yakachukuliwa na
mwanae, Nuuru d-Din
Zink ambaye naye alipambana na wapiganaji wa
crusade lakini hakufaulu kuwashinda.
Hapo ndipo, hatimaye, Allah akamuinua kiongozi mpya kuja kuzikomboa ardhi za Waislamu, naye ni Salahud-Din
Al-Ayyubiy au kifupi Saladin. Endelea
na kisa hiki cha kusisimua:
Katika kipindi hiki, Misri ilikuwa
chini ya dola ya mashia Fatmiyyin (The
Fatimid Dynasty). Watawala wa kishia
walikuwa wakishirikiana na wapiganaji
wa crusade waliozikalia ardhi za Waislamu.
Pamoja na kushirikiana nao, mwaka
1160 ma-crusaders wakaivamia Misri
kujaribu kuiteka. Nuuru d-Din Zink
akatuma jeshi kwenda kuwahami ndugu zake Waislamu. Kiongozi wa jeshi
hili alikuwa Jemadari Mkurdi, Shirkuh
huku Salahud-Din Al-Ayyubiy, mpwa
wa Shirkuh, akiwa miongoni mwa wapiganaji.
Shirkuh na jeshi lake wakafanikiwa
kuwashinda ma-crusaders na kuikomboa Misri, lakini akafariki kwa homa ya
matumbo muda mfupi baadae. Mpwa
wake Salahud-Din Al-Ayyubiy akashika
hatamu za uongozi wa jeshi hilo la Waislamu. Na huo ukawa mwisho wa utawala wa mashia Fatmiyyin Misri.
Hivi ndivyo Allah alivyomuinua
mkombozi wa ardhi takatifu Baitull
Muqaddas, Salahud-Din Al-Ayyubiy,
Mkurdi ambaye hata hakuwa mwarabu, kuonesha kwamba Uislamu si dini
ya Waarabu kama makafiri wanavyopenda ifahamike.
Lakini ni nani huyu Salahud-Din AlAyyubiy? Alikuwa kijana wa miaka 36
wakati akishika hatamu za kuiongoza
Misri, ikiwa sehemu ya dola ya Kiislamu
ikiongozwa na Wakurdi.
Wanahistoria Waislamu na makafiri
wanamuelezea kama mtu mnyenyekevu asiyependa makuu. Hakujali kuhusu
anasa za dunia kama wafanyavyo watu
wenye madaraka kama yake. Azma yake
kubwa ilikuwa ni kuzikomboa ardhi za
Waislamu kutoka mikononi mwa
makafiri.

Inasemekana Salahud-Din Al-Ayyubiy alikuwa hacheki na daima akiwa


na uso usio na furaha. Alipoulizwa kwa
nini yuko hivyo, alijibu: Nitawezaje
kucheka wakati Masjid al-Aqsa iko
mikononi mwa wana msalaba?. Wako
wapi leo watawala wa nchi za Kiislamu
wenye haiba, azma, na malengo kama
ya Salahud-Din Al-Ayyubiy? Inasemekana washauri wake walilazimika kuficha kiasi fulani cha dhahabu kama akiba yake kwa kuwa laiti angeiona mali
hiyo angeitumia katika maandalizi ya
wanajeshi tayari kuwakabili maadui.
Watu walikuwa wakisema alikuwa
hajionei huruma, lakini akiwahurumia
wengine.
Kwa sifa hizi, wako waliomlinganisha Salahud-Din Al-Ayyubiy na makhalifa wanne waongofu wa Kiislamu, ingawa hawezi kufikia daraja yao kwa
sababu wale walikuwa maswahaba wa
Mtume wa Allah (Rehma na amani
ziwe juu yake).
Mara baada ya Salahud-Din Al-Ayyubiy kushika hatamu za Misri, watu
walitegemea kwamba patazuka mvutano wa kugombea madaraka kati yake
na Nuuru d-Din Zink.
Salahud-Din Al-Ayyubiy aliliepusha
hili, na akasisitiza kwamba, yeye ni mtumishi mtiifu kwa Zink na lengo lao ni
moja, kuwashinda wana Msalaba. Uko
wapi moyo kama huu kwa viongozi wa
Kiislamu hivi leo?
Mwaka 1174 Miladia, Nuuru d-Din
Zink alifariki na kumuacha SalahudDin Al-Ayyubiy akiwa mtawala wa dola
mpya ya Kiislamu iliyotangaa tokea
Misri hadi Syria, na kwa hali hiyo akawa
amewazunguka wana msalaba (crusaders) nchini Palestina.
Kazi ya kwanza ya Salahud-Din AlAyyubiy baada ya kuwa mtawala mkuu
ilikuwa ni kuhakikisha kwamba Waislamu wameungana na wameandaliwa
vya kutosha kuwashambulia wana

msalaba.
Lakini, kwanza alilazimika kushughulikia masalia ya mashia Fatmiyyin
walioleta chokochoko kwa lengo la kutaka kuiteka tena Misri. Kulikuwa na
kundi likiitwa Hashaashiiyn (wazungu
wakaitamka kama Assassins) ambalo
mbinu yao kubwa ilikuwa ni kuendesha
mauaji ya siri (assassinations) ya viongozi Waislamu na hata wana msalaba.
Hili hatimaye lilishindwa.
Maandalizi ya Waislamu yalichukua
miaka kadhaa. Hadi kufikia mwaka
1180 Miladia, Salahud-Din Al-Ayyubiy
alikuwa amefanikiwa kuunganisha
nguvu za Waislamu tayari kuikomboa
ardhi takatifu ya Baitul Muqaddas (Jerusalem).
Wakati huo wana msalaba (crusaders) walikuwa wameparaganyika, hawana uongozi mmoja na wakitofautiana wao kwa wao. Hii ndiyo hali waliyokuwa nayo Waislamu wakati walipopoteza ardhi zao kwa wana msalaba hao
miaka 80 nyuma.
Mwaka 1182 Salahud-Din Al-Ayyubiy alivuka kutoka Misri kwenda ardhi
zilizokaliwa na wana msalaba na kuanza
mashambulizi dhidi ya wana msalaba
wa Franks ambao asili yao ni Ujerumani. Tukumbuke hawa ndio waliomuua
Imaad ad-Din Zengi.
Mpinzani mkubwa mwenye nguvu
na katili katika wana msalaba alikuwa
ni Reynald wa Chatillon, mmoja wa
kikosi cha wapiganaji waliojulikana
kama Knight Templers. Hawa ndio
waliokuja kuanzisha Umasonia duniani
chini ya misingi ya Hashaashiin.
Huyu Reynald wa Chatillon alikuwa
akiwavamia Waislamu katika ardhi zilizokaliwa na wana msalaba na kuwaua
na kushambulia misafara iliyokuwa ikienda Makka kwa ajili ya ibada ya hijja.
Reynald hata alitishia kuishambulia
miji ya Makka na Madina.
Salahud-Din Al-Ayyubiy hakuvu-

milia vitendo hivi dhidi ya Waislamu na


akaapa kumwadhibu Reynald kwa
mikono yake mwenyewe. Hili lilitimia
katika vita vilivyopiganwa Hittin, kaskazini mwa Israeli ya leo, mwaka 1187.
Wana msalaba walileta jeshi lao
kubwa la wapiganaji 20,000 kutoka Jerusalem kwa ajili ya vita hivi vya Hittin.
Jeshi la Salahud-Din Al-Ayyubiy liliwakabili lilikwa na wapiganaji 30,000.
Wana msalaba wakipigana kwa staili
ya Ulaya walisonga mbele wakiwa
wametanguliza wapiganaji waliovalia
mavazi ya chuma, lakini walikabiliwa na
uhaba mkubwa wa maji ya kunywa.
Hadi mapigano yanaanza, wapiganaji wa msalaba walikuwa hawana nguvu ya kusimama mbele ya Waislamu
kwa kiu na kuelemewa na mavazi mazito ya chuma. Kwa muda mfupi vita
vikamalizika kwa ushindi kwa jeshi la
Waislamu, lilifanikiwa hadi kumteka
Reynald.
Salahud-Din Al-Ayyubiy aliwapa
msamaha mateka wote, lakini kama alivyoahidi alimuua Reynald kwa mikono
yake mwenyewe, malipo stahiki kwa
mtu aliyewatesa na kuwaua Waislamu
kwa chuki kubwa.
Baada ya jeshi hilo kubwa la wana
msalaba kuteketezwa, Salahud-Din AlAyyubiy akasonga mbele na wapiganaji
Waislamu kuelekea Baitul Muqaddas
ambayo kwa wakati huo haikuwa na ulinzi madhubuti.
Oktoba 2, 1187 Miladia sawa na
mwezi Rajab mwaka 583 Hijriyyah,
Salahud-Din Al-Ayyubiy aliingia na
kuiteka Jerusalem ikiwa ni miaka 88,
miezi 2 na siku 17 tangu itekwe na wana
msalaba. Kama Mtume (Rehma na
amani ziwe juu yake) alivyowafanyia
watu wa Makka, uungwana wa Salahud-Din Al-Ayyubiy ulionekana kutokana na jinsi alivyowafanyia Wakristo
wa Jerusalem.
Miaka 88 nyuma ya hapo, Wakristo
wana msalaba toka Ulaya walipoiteka
Jerusalem, waliwaua wakazi wote Waislamu na Wayahudi mpaka inasemekana mitaa ya mji huo ilitiririka damu iliyofikia kiwiko cha mguu.(Wikipaedia,

Hivi ndivyo Allah alivyomuinua mkombozi wa


ardhi takatifu Baitull Muqaddas, sAlahud-Din AlAyyubiy, Mkurdi ambaye hata hakuwa mwarabu,
kuonesha kwamba Uislamu si dini ya Waarabu
kama makafiri wanavyopenda ifahamike

History of Jerusalem During the Middle


Ages).
Waislamu waliposhinda, SalahudDin Al-Ayyubiy aliwaruhusu wana
msalaba kujikomboa kwa kulipa kiasi
kidogo cha pesa kama fidia na wale wasiomiliki kiasi hicho aliwaruhusu waondoke pasina kulipa. Uungwana ulioje
kwa mshindi wa vita kuwatendea wema
aliowashinda tena waliowaua ndugu
zao hapo kabla?
Waislamu kuiteka Jerusalem
kuliamsha ari ya vita vya tatu na vya
mwisho vya msalaba kati ya Wakristo
wa Ulaya dhidi ya Waislamu. Wapiganaji wana msalaba walianza kuwasili
ardhi takatifu mwaka 1189, miaka miwili tu baada ya ushindi wa Waislamu.
Kiongozi wa jeshi hili la wana msalaba alikuwa Mfalme wa Uingereza, Richard the Lion Heart (Richard mwenye
moyo wa Simba). Baada ya mapigano
kadhaa kati ya majeshi ya Richard na
majeshi ya Salahud-Din Al-Ayyubiy
yakilinda ardhi takatifu, wana msalaba
walilazimika kurudi Ulaya mikono
mitupu wakiiacha Jerusalem mikononi
mwa Waislamu.
Katika moja ya mapigano SalahudDin Al-Ayyubiy alingamua kuwa farasi
wa Mfalme Richard alikuwa ameuawa.
Kwa kutambua kwamba jemadari wa
vita zama hizo hawezi kupiganisha jeshi
bila kuwa na farasi, Salahud-Din AlAyyubiy alimpelekea farasi.
Kwa kitendo hiki, wema wa SalahudDin Al-Ayyubiy umebaki kama simulizi
za mfano (legend) miongoni mwa watu
wa Ulaya hadi leo, na ingawa alikuwa
adui yao, wanamheshimu sana kwa
ukarimu wake hata kwa maadui zake.
Uongozi wa Salahud-Din Al-Ayyubiy na kujitolea kwake muhanga kwa
ajili ya dini kulifungua ukurasa mpya wa
umoja wa Waislamu.
Hata baada ya kufa kwake mnamo
mwaka 1193 Miladia, dola ya Kiislamu
aliyoiasisi ambayo ilipewa jina la Dola ya
Ayubi (Ayyubid Dynasty) na baadaye
Dola ya al-Amaalika (Mamluks) iliendelea kupambana na uvamizi wa wana
msalaba kwa muda mrefu.
Ardhi takatifu ya Jerusalem na Palestina zilibaki mikononi mwa Waislamu
hadi mwaka 1917 Miladia zilipotekwa
na jeshi la Waingereza katika Vita Kuu
ya Kwanza ya Dunia kwa hadaa ya
Waingereza walipowarubuni Waarabu
wawasaidie vitani. Ardhi hizi sasa zinakaliwa kimabavu na Israeli.
Tunapoyatafakari matukio ya kihistoria yaliyotokea ndani ya mwezi wa Rajab, hatupaswi kabisa kusahau kuwa
kilichonusuru Uislamu wakati ule wa
uvamizi wa wana msalaba ni umoja wao
na ucha Mungu wa viongozi wao kama
Salahud-Din Al-Ayyubiy (Allah amrehemu).

kutoka misikitini

Waislamu wahimizwa kushikamana na itikadi


Waislamu nchini wamehimizwa kushikamana na itikadi sahihi ya dini ya Kiislamu, kwani
kufanya hivyo kutawaepusha na misukosuko ya kimaisha na Allah (Subhanaahu Wataallah) atakuwa pamoja nao. Akihutubia mamia ya Waislamu wakati wa swala ya Ijumaa,
hivi karibuni, katika msikiti wa Umar Bin Khatwaab uliopo mtaa wa Jangwani, Dar es
salaam, Sheikh Abuu Musa amewaasa Waislamu kushikamana na njia sahihi ya Uislamu,
kwani hakuna mafanikio pasipo kufanya hivyo. Alisema, ili wanadamu wasalimike na madhila ya dunia hawana budi kushikamana na aqida sahihi, na kwamba fitna zitokanazo na
umiliki wa mali, watoto na madaraka zisiwadanganye, kwani hiyo ni mitihani kutoka kwa
Allah ambayo huitoa katika mambo ya kheri na shari. (MWANDISHI WETU)

Imam Tungi atahadharisha


Serikali

Waislamu watakiwa kumuiga


Mtume kwa vitendo

Serikali imetakiwa kuacha mara moja zoezi


linaloendelea la kufungia madrasa katika maeneo mbalimbali ya nchi, kwani kufanya hivyo
ni kuwanyima watoto haki yao ya elimu na
kuiangamiza dini ya Uislamu.
Hayo yalisemwa Ijumaa iliyopita, na Sheikh
Hussen Ismail, wakati akitoa khutba ya swala ya
Ijumaa katika msikiti wa Tungi, Temeke jijini Dar
es Salaam.
Sheikh Ismail alisema, sababu wanazozitoa za
kuzifungia madrasa hazina mashiko kwa sababu
serikali haijawahi kutoa muongozo wa kusajili
na kuendesha madrasa, na kusema kama suala
la mazingira mabovu ya madrasa, bado hawana
hoja, kwani zipo shule za serikali nazo hazina
mazingira mazuri. (KHALID OMARY)

Waislamu nchini wametakiwa kumuiga Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) kwa vitendo kwa kuwa
yeye ni mwalimu wa dini ya Uislamu.
Wito huo umetolewa na Sheikh Muhammad
Mujahid katika ibada ya swala ya Ijumaa iliyoswaliwa
katika msikiti wa Umar bin Khatwab uliopo mtaa
wa Jangwani jijini Dar e salaam na akaonya kuwa ili
amali ihesabiwe kuwa ibada haina budi kutekelezwa
kwa mujibu wa alivyofundisha Mtume. Sheikh Mujahid alisema jamii ya Waislamu inapaswa kujiepusha
na ibada zisizothibiti katika dini, kwani kufanya hivyo
kunapelekea mtu kuandikiwa madhambi mbele ya Allah . Aidha, aIiwakumbusha Waislamu kufanya ibada
kwa kutegemea malipo kwa Allah katika mwezi huu
wa Rajab sanjari na kujiepusha kufanya maasi, kwani
kufanya hivyo ni kujidhulumu nafsi na pia ni makosa
makubwa . (YUSUPH AMIN)

21 Rajab 1436, jumatatu Mei 11 - 17, 2015

habari

www.islamicftz.org

Vituo vya kuandikisha wapiga


kura vyawekwa makanisani
Waangalizi
kutoka
Mtandao
wa Asasi za
Kiraia wa
Kuangalia
Chaguzi
Tanzania
(TACCEO)
unaoratibiwa
na Kituo
cha Sheria
na Haki za
Binadamu
(LHRC)
wamesema,
waliweza
kushuhudia
vituo vya
uandikishaji
vikiwa
kwenye
makanisa
mkoani
Njombe

Mwenyekiti wa Tume
ya Taifa ya Uchaguzi,
Jaji Mstaafu Damian
Lubuva.

NA SELEMANI MAGALI

aislamu wameelezea hofu


ya kutengwa katika zoezi
la uandikishwaji wa wapiga kura kwa mfumo wa
kielektroniki huko mikoani kutokana na
baadhi ya vituo vya kuandikia kuwekwa
makanisani.
Hofu ya Waislamu imekuja kufuatia
taarifa ya waangalizi wa zoezi hilo kuwa
baadhi ya makanisa yamegeuzwa kuwa
vituo vya kuandikisha wapiga kura, jam-

inatoka UK 2

Wakili Nassoro
aliongeza: Tulikwenda Ukonga ili
kuongea nae atuambie kwa nini alihamishwa kutoka Morogoro kuletwa Dar es Salaam, na kwa nini apelekwe gereza la wafungwa (Ukonga)
na sio la mahabusu, lakini tuliambiwa hayupo Ukonga.
Tulipofika gerezani hapo tulionesha vitambulisho vyetu na
watu wa mapokezi waliingia ndani,
waliporudi walituambia Sheikh
Ponda hayuko pale, Wakili Nassoro
aliliambia gazeti la Imaan.
Kwa mujibu wa wakili Nassoro,
majibu ya Jeshi la Magereza ya siku
ya Ijumaa yaliongeza taharuki juu
ya hali ya Sheikh Ponda, hususan
ukizingatia kuwa huko nyuma Jeshi
la Magereza limekuwa likiwapa
ushirikiano mzuri tu kila walipotaka kuonana naye.

bo ambalo linakwaza uhuru Waislamu


kufika maeneo hayo na kuandikishwa
kutokana na msimamo wa kiimani.
Mmoja wa wananchi, Ustadh Mohammed Hamisi wa Kinondoni, jijini
Dar es Salaam amesema: Hili jambo
limetushtusha sana. Tunashukuru limeibuliwa mapema na waangalizi. Serikali iondoe hivyo vituo mara moja,
vinginevyo Serikali itaingia katika
mgogoro mwingine na Waislamu.
Waangalizi kutoka Mtandao wa Asasi
za Kiraia wa Kuangalia Chaguzi Tanza-

nia (TACCEO) unaoratibiwa na Kituo


cha Sheria na Haki za Binadamu
(LHRC) wamesema, waliweza kushuhudia vituo vya uandikishaji vikiwa kwenye
makanisa mkoani Njombe.
Baadhi ya makanisa ambayo yalikuwa
na vituo vya kupiga kura ni pamoja na
Kanisa la Lutherani Ilembula na Kanisa
la Pentekoste Ufwala, yote yakiwa Wilaya
ya Njombe. Jingine ni Kanisa la Kristo
Is o l w a y a , l i l i l o p o w i l a y a y a
Wangingombe.
Akizungumza na waandishi wa

Sheikh Ponda atoweka


Wakili Nassoro alisema,
hawakujua mabadiliko yale yana
maana gani, kwani mazingira yalionesha kuwa Sheikh yuko pale
Ukonga lakini hawakuwa na taarifa
rasmi na wahusika walikanusha
kuwa hayuko pale.
Ilitutia wasi wasi, wakili Nassoro aliliambia gazeti la Imaan siku
ya Jumamosi (juzi).
Katika hali ya kushangaza zaidi
katika kadhia hii, ndugu wa Sheikh
Ponda walipofika gereza la Ukonga
siku ya Ijumaa kumpelekea chakula
na mahitaji mengine, chakula
kilipokelewa lakini hawakuruhusiwa kumuona.

Kutojulikana alipo Sheikh Ponda


kuliwachanganya pia viongozi wa
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
nchini, ambapo kupitia kwa Msemaji wake, Sheikh Rajab Katiba,
walielezea kuwa wameshtushwa na
tukio hilo.
Hatujui sheikh aliko na hali hii
inatuchanganya sana, inaelekea lolote linaweza kutokea kwa Sheikh
wetu. Wahusika inabidi wawe wazi,
Waislamu tunataka kujua Sheikh
Ponda yuko wapi, maana katika historia ya nchi hii watu wamewahi
kupotea katika mazingira ya kutatanisha, alisema Katimba.

Mashataka ya Sheikh Ponda:


Sheikh Ponda awali alikuwa
ameshtakiwa kwa kuvamia kiwanja
cha Markaz Changombe jijini Dar
es Salaam baada ya Bakwata waliokabidhiwa mali za iliyokuwa Jumuiya iliyovunjwa ya Waislamu wa
Afrika ya Mashariki (EAMWS) kuwauzia wafanyabiashara kinyume
na taratibu za kusimamia mali za
waqfu.
Kesi hiyo iliyokuwa imefunguliwa mahakama ya Kisutu jijini Dar
es Salaam ilimalizika kwa Sheikh
Ponda kufungwa kifungo cha nje
cha mwaka mmoja.
Wakati akishughulikia rufaa ya

5
habari ofisini kwake, Mwenyekiti TACCEO, Martina Kabisama, amekiri kuwepo hali hiyo na kudai kuwa serikali imekiuka jukumu lake kwa kuruhusu vituo
hivyo kuwekwa kanisani.
Alisema, uwepo wa vituo hivyo katika
makanisa ni kasoro kubwa inayohitaji
kufanyiwa marekebisho, vinginevyo
kunaweza kukasababisha kundi kubwa
la waumini wa dini nyingine kuachwa
bila kuandikishwa, hivyo kuwanyima
haki yao ya msingi .
Kabisama ameongeza kuwa, kuweka
vituo hivyo makanisani kunaweza kuwazuia watu wengi wakiwemo hata Wakristo ambao kwa namna moja ama nyingine
hawapendi kufika katika makanisa hayo
kutokana na sababu wanazozifahamu.
Nadhani kuna haja ya kurekebisha
kasoro hizi, kuacha makanisa au nyumba
nyingine za ibada kutumika kama vituo
vya kuandikishwa wapiga kura si sahihi,
kwani waumini wa dini nyingine
watashindwa kushiriki kutokana na
woga au kuwa na imani tofauti, alieleza
Kabisama.
Ukiacha kasoro hiyo Kabisama
ametaja kasoro zingine ambazo zimebainika katika zoezi hilo kuwa ni pamoja
na mwitikio mdogo wa wananchi katika
vituo vya kuandikishwa kwa kile alichokitaja kuwepo elimu ndogo ya wapiga kura
inayotolewa juu ya umuhimu wa zoezi
hilo.
Amesema, ili kukabiliana na changamoto hizo tume ya taifa ya uchaguzi inapaswa kuongeza idadi ya asasi za kiraia ili
zitoe elimu hiyo na kuwavutia wananchi
walio wengi kujitokeza kujiandikisha.
Katika wilaya ya Ruangwa siku tatu
za mwanzo watu wachache walijitokeza
na hata kituo cha Kitandi Gulioni April
27, 2015 tulishuhudia watu 44 peke yake
wakiandikishwa, alisema Kabisama.
Pia ametaja kasoro nyingine katika
zoezi hilo kuwa ni pamoja na zoezi kupitiliza muda wake hadi kufikia saa sita,
watu kuandikishwa bila kuchukuliwa
alama za vidole, zoezi kushindwa kufanyika kwa wakati kutokana na kukosekana kwa mashine za kuandikishia (BVR)
na kundi kubwa la watu kutoandikishwa
kutokana muda kumalizika.
Kufuatia hali hiyo wameishauri tume
ya taifa ya uchaguzi kuboresha mchakato
wa zoezi hilo na pia serikali itimize wajibu wake wa kuipa fedha tume.
Zoezi la kuandikisha wapiga kura kwa
mfumo wa kielektroniki (Biometric voters registration-BVR) ulianza rasmi Febuari 23, 2015 katika Halmashauri ya
Mji wa Makambako mkoani Njombe kisha kuendelea katika mikoa ya Lindi,
Mtwara, Ruvuma na Iringa.

kesi yake na huku akitumikia kifungo hicho cha nje, Sheikh Ponda alikwenda mjini Morogoro mwaka
2013 kuhudhuria sherehe za Idul
Adhha ambako nusura apoteze
maisha baada ya kupigwa risasi.
Wakati akipatiwa matibabu ya
majeraha ya risasi Hospitali ya Taifa
Muhimbili, Sheikh Ponda alitiwa
pingu na kafunguliwa mashitaka
Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro akituhumiwa kuvunja
masharti ya kifungo chake cha nje,
kesi ambayo ilikuwa inaendelea
hadi sasa.
Wakati kesi ya Morogoro ikiunguruma, Sheikh Ponda alishinda
rufani yake Mahakama ya Kisutu,
na siyo tu kuachiwa huru, bali pia
kuruhusiwa kuwashitaki waliouza
mali ya waqfu ya Waislamu
Changombe Markaz.

15 Rajab 1436, jumatatu May 4 - 10, 2015

hutolewa na kuchapishwa
The Islamic Foundation,P.O.Box 6011 Morogoro, Tanzania,E-mail: imaanmedia3@gmail.com
mhariri mtendaji: 0715 559 944, Mhariri: 0786 779 669, afisa masoko: 0785 500 502
TOVUTI: www.islamicftz.org

tahariri / uchambuzi

Tusaidiane katika maafa ya mvua


T

angu wiki iliyopita


kumekuwa na mfululizo wa mvua nyingi
zinazoendelea kunyesha katika msimu huu wa mvua
za masika ambazo zimeleta
maafa makubwa kwa wananchi
katika mikoa ya Dar es Salaam,
Mtwara, Lindi, Tanga, Pwani,
Kagera, Zanzibar na maeneo
mengine ya nchi.
Ni kweli mvua ni neema
kutoka kwa Mwenyezi Mungu,
lakini zinapozidi zinaweza kusababisha maafa. Kutokana na
mvua hizo maafa mengi yamejitokeza. Watu zaidi ya nane (8)
waliarifiwa kufariki Dar es Salaam, huku familia zaidi ya 500
zikipoteza makazi au mali zao
kuharibika. Kadhalika, miundombinu ya barabara na ma-

daraja nayo imeathirika.


Watabiri wanatuambia
kuwa mvua hizo zinatarajiwa
kuendelea kunyesha hadi
mwisho wa mwezi huu, na kwa
sababu hiyo basi, tunapaswa
kuchukua tahadhari. Ni kutochukua tahadhari ndio
kumepelekea matatizo haya
kujitokeza kila msimu na
kuathiri hata maeneo ambayo
yamepimwa.
Hata hivyo, huu si wakati wa
kulaumiana bali kusaidiana, na
ndio maana sisi, gazeti la Imaan tunawaasa Waislamu na
wananchi wote kwa ujumla kusaidiana katika maeneo yetu ya
makazi pale miongoni mwetu
tunapofikwa na maafa katika
kipindi hiki cha mvua.
Mwenyezi Mungu anasema:

Na saidianeni katika wema na


uchamngu. Wala msisaidiane
katika dhambi na uadui. Na
mcheni Mwenyezi Mungu.
Hakika Mwenyezi Mungu ni
mkali wa kuadhibu (5:2).
Inaelezwa pia kuwa Uislamu ni kama mwili mmoja,
kikiumwa kiungo kimoja
vilivyobaki pia huathirika. Pia
Mtume (Rehma na amani ziwe
juu yake) amesema Muislamu
ndugu yake Muislamu.
Kutokana na ushahidi huo,
ni wazi kuwa tunao wajibu kwa
kila mmoja wetu kumsaidia
mwenzake mwenye tatizo. Sisi
tunaamini kuwa wakati Serikali ikijipanga kuwasaidia
waathirika wa maafa haya yanayoendelea; sisi wenyewe katika maeneo yetu tuna wajibu

wa kuwahami ndugu, jamaa na


majirani kwanza tatizo linapotokea kabla Serikali haijakuja.
Tunapenda pia kuwashauri
wananchi wanaoishi mabondeni kuhama kwenye maeneo
hayo ili kuondokana na adha
hizi za mafuriko na uharibifu
wa mali za kila mwaka. Serikali
yenyewe pia ina wajibu wa kuwawezesha watanzania wenzetu hawa kwa kuwatafutia
maeneo mengine, hususan
wale ambao hawajawahi
kupatiwa viwanja hivyo hapo
kabla. Kwa upande wa Serikali,
tunaishauri ijifunze kutokana
na maafa haya, hususan upande wa miundo mbinu. Miundo mbinu bora ni ile ambayo
inaweza kutusitiri katika vipindi vyote, kiangazi na masika.

Kwa hali tunayoiona sasa ni


wazi kuwa miundombinu yetu
haijawa rafiki. Katika jiji la Dar
es Salaam, ushahidi wa ubovu
wa miundo mbinu uko dhahiri
kupitia foleni, mahandaki
makubwa na mafuriko yanayosababisha foleni ndefu.
Kama tulivyotangulia kusema, mvua ni neema ya
Mwenyezi Mungu na jamii inapaswa kuelewa kuwa yote yanayojitokeza ni makadirio yake
Muumba, hivyo tulichukulie
janga hili kama ni sehemu ya
maisha ya mwanadamu, kwani
Mola wetu hutahini waja wake
katika mambo ya kheri na
shari.
Tunamuomba Allah atusitiri
kwa haya na mengineyo. Amiin.

nasaha za wiki

angu vita vianze huko


Yemen ukifwatilia sehemu
kubwa ya habari zinazoandikwa na waandishi
wetu katika vyombo vyetu vya Kiislamu nchini Tanzania utagundua
kuwa ipo haja ya vyombo vyetu
kuwa makini zaidi katika kuripoti
swala hili.
Namna vinavyoripoti inatia shaka kama kweli vimefanya utafiti wa
kutosha juu ya kadhia hii, maana
vimekuwa vikiulaumu na kuushutumu upande mmoja tu wa mgogoro
huo pasina kutueleza chochote
kuhusu upande wa pili.
Unapofwatilia vyombo hivi,
waandishi wake wanatuaminisha
kuwa Saudi Arabia imekurupuka
kiwazimu wazimu na kuingia Yemen kuanza kuuwa watu kiholela na
kuharibu miundombinu ya nchi
hiyo na hivyo ndio upande pekee wa
mgogoro unaopaswa kubebeshwa
mzigo wa lawama.
Ukweli ni kwamba vita vya Yemen si vya leo, vilianza muda mrefu,
lakini wakati huo wahusika walikuwa ni Wahouth na Serikali ya Ali
Abdallah Saleh, huku Serikali ya
Saudi Arabia ikiwa msuluhishi wao.
Kwa sasa vita vimepanuka sana.
Sababu za kupanuka vita hii ni tatu;
Ushiriki wa askari waasi wanaomuunga mkono rais aliyeondolewa
madarakani kwa nguvu ya umma,
Ali Abadallah Saleh, Uwepo wa
askari watiifu kwa Rais Abdo Rabou
Mansour na kujiingiza nchi ya Iran
kwa kuwapatia silaha wanamgambo waasi wa Kihouth.
Awali ugomvi wa Yemen ulikuwa
ni kupinga muungano na kutoridhika kwa Wahouth na siasa ya ndani na nje ya Rais Ali Abdallah Saleh.
Taarifa za mitandaoni zinaone-

SHEIKH ABDALLAH BAWAZIR

Vita vya Yemen, vyombo vyetu


vinapaswa kuwa makini zaidi

sha kuwa, mmoja kati ya viongozi


wa Wahouth, Badruddin Al-houth
ni mshirika mkubwa wa serikali ya
Iran, na kupitia ushirika huo, mwaka 2009 Iran ilianza kupeleka shehena za silaha kwa Wahouth kwa
njia ya siri.
Na baada ya Ali Abdalah saleh
kuondolewa madarakani kwa nguvu ya umma, Urais wa nchi hiyo
ukashikwa na Abdo Rabboh Mansour Hadi. Ali Abdallah Saleh hakuridhika na uamuzi huo.
Ali Abdallah Saleh alianza har-

akati za chini kwa chini na kufanikiwa kuunganisha wanajeshi wanaomuunga mkono na wale wana
mgambo wa Kihouth waliokuwa
maadui zake wakati wa utawala
wake.
Lengo la Ali Abdallah Saleh na
genge hili ni kuiondoa Serikali halali
ya Abdo Rabboh Mansour madarakani kwa mtutu wa bunduki.
Ikumbukwe, jeshi la serikali tawala lilidhoofishwa kwa ndani na
halikuwa na nguvu tena ya kuweza
kupambana na makundi ya waasi

na hatimae Rais Abdo Rabboh


Mansour akatimuliwa na kukimbilia nchi jirani.
Ni kukosa uadilifu kuilaumu
Saudi Arabia pekee katika balaa hii
ya vita vya Yemen bila ya kusoma
kikamilifu sababu za vita hivi na wahusika wakuu walioisababisha.
Anayestahiki lawama kubwa katika vita ya Yemen ni Ali Abdallah
Saleh aliyesababisha fitna hii, na wa
pili ni Iran kwa kujiingiza katika
mzozo wa Yemen ambao hausiki
nao kwa ndewe wala sikio.

Ukweli ni kwamba vita vya Yemen si vya leo,


vilianza muda mrefu, lakini wakati huo
wahusika walikuwa ni Wahouth na Serikali
ya Ali Abdallah Saleh

Katika kipindi hiki cha vita, silaha zote walizonazo Wahouth wanapata kutoka Iran.
Wahouth ni waasi na kila mtu
analijua hilo. Sasa ni kwa nini tuibebeshe Saudi Arabia peke yake lawama hii? Kwani ni lipi lengo la Iran
na Houth katika sakata hili kama si
kutaka kueneza Ushia na kuchochea
vita vya kiitikadi? Nini lengo la Iran
kama si kutaka kuleta vita baina ya
Waarabu na Wafursi?
Au nini lengo la Iran kama si kutaka kuchochea ugaidi na kuleta vita
vya Wayemen kwa Wayemen ili hatimae Iran kidogo kidogo ipate nafasi ya kuidhibiti Saudi Arabia na
nchi za ghuba kwa kila upande, na
hatimae kufikia lengo la kujitanua
kidini, kisiasa na kiuchumi?
Nimalizie nasaha zangu kwa
kueleza sababu tano zilizoipelekea
Saudia Arabia na nchi za ghuba kuingia katika vita hii.
Mosi, hatari ya kujisogeza kwa
Iran kwenye mipaka ya nchi za ghuba. Pili, kuimarika kwa ushawishi
wa Iran kusini mwa ghuba ya Uarabuni.
Tatu, Wahouth kwenda kinyume
na makubalianao ya Novemba 2011
ya nchi za Kiarabu, kwa kuchukua
hatua ya kuipindua Serikali iliyo
madarakani kwa nguvu ya mtutu
wa bunduki.
Sababu ya nne ni kulinda maslahi ya nchi za ghuba yaliyo katika ardhi ya Yemen na tano, kuikwamua
Bab al- Mandab kutoka kwenye
udhibiti wa Wahouth, kwani kimkakati hili ni eneo nyeti kwa usalama
wa mataifa ya ghuba na ndio njia
kuu ya meli za mizigo na mafuta na
maslahi mengine ya kiuchumi.
0773 215 898

21 Rajab 1436, jumatatu Mei 11 - 17, 2015

hazina yetu

www.islamicftz.org

NA YUSUFU AHMADI

Akifafanua hilo, Sheikh Yussuf


anasema: Hatukuwahi kumsikia
akisema siasa ni haramu. Yeye
mwenyewe alikuwa anasema,
Mtume Muhammad (Rehma na
amani ziwe juu yake) alikuwa ni
mwanasiasa.
Hata hivyo Sheikh Bachu alipinga siasa za kijahili(kijinga) za kuuana na kubaguana.
Sheikh Yussuf anaongeza,
Sheikh Bachu alikwepa kuchukua
upande wowote kisiasa na kuwabagua watu, lengo likiwa ni kufikisha ujumbe wa Uislamu kwa watu
wote.
Kuhusu elimu ya kisekula,
Sheikh Bachu alihimiza watu wasome ikiwezekana hadi vyuo vikuu.
Na hapa tulipo ni moja ya skuli
zake alizozijenga ili watu wasome
elimu ya kisekula, anasema Sheikh
Yussuf.

hana iliojengeka kwa


wengi ni kuwa uwezo wa
kuzungumzia masuala
ya kitaalamu unatokana
na elimu kubwa ya kisekula.
Lakini wapo baadhi ya watu
hawakusoma sana elimu ya kisekula lakini Allah amewabariki ufahamu mkubwa katika kuzungumzia
fani mbalimbali.
Miongoni mwa hao ni Sheikh
mashuhuri Afrika Mashariki na
Kati, aliyekonga nyoyo za waumini
wengi wa dini ya Kiislamu, mwenye
ufasaha wa kuzungumza na kushawishi, Marehemu Nassoro Bachu.
Sheikh Hamisi Yussuf, mwanafunzi wa Sheikh Bachu amesema Sheikh Bachu aliishia darasa la
saba, licha ya uwezo mkubwa wa
akili na ufahamu aliokuwa nao katika masomo.
Up e o n a u f a h a m u w a k e
mkubwa wa akili unadhihirika
kutokana na uwezo wake wa kuzungumzia fani mbalimbali,
ikiwemo fani ya elimu ya viumbe
(biology) na jiografia kwa umahiri
mkubwa sana.
Akizungumzia historia ya
mwalimu wake huyo, Sheikh Yussuf alisema, Sheikh Bachu alizaliwa mwaka 1951 katika eneo la
Fuoni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Baada ya kuhitimu darasa la
saba, Sheikh Bachu hakuendelea
na elimu ya kisekula kutokana na
vikwazo mbalimbali, ingawa watu
waliomfahamu enzi hizo wanasema alikuwa hodari sana darasani.
Kwa watu ambao walisoma
nae walikuwa wanasema nafasi ya
Sheikh Bachu darasani ilikuwa
mtu wa kwanza na wa pili tu, alisema Sheikh Yussuf.
Vikwazo vinavyotajwa kumzuia
Sheikh Bachu kuendelea na masomo vilitokana na mambo mbali
mbali ya kijamii, ikiwemo ubaguzi
wa rangi,anasema Sheikh Yussuf
ambaye anaamini Sheikh Bachu
alifelishwa kutokana na kuwa na
asili ya Uhindi.
Kwa upande wa elimu ya dini,
Sheikh Bachu alipata elimu yake
visiwani Zanzibar na hakuwahi
kwenda nje ya visiwa hivyo kwa
ajili ya kusoma.

Kuteuliwa kuwa Amir:


Marehemu Sheikh Nassoro Bachu ambae alibobea katika fani ya
tafsiri ya Quran aliteuliwa kuwa
Amir wa Masjid Sunna akimrithi
mwalimu wake Sheikh Said Tumba ambaye alistaafu uongozi.
Baada ya Sheikh Tumba kustaafu, alifwatwa na Mzee Othmani,
Ally na Mzee Mwinyi na kumuomba ateue miongoni mwa wanafunzi
wake kiongozi (Amir) wa kuendeleza Masjid Sunna.
Sheikh Tumba ambaye alipitia
misukosuko mingi kutoka Serikalini alipendekeza Sheikh Bachu
awe Amir kuanzia mwaka huo,
1979.
Kwa mujibu wa Sheikh Yussuf,
kustaafu kwa Sheikh Tumba kulichangiwa na Serikali, enzi za utawala wa Rais Aboud Jumbe,mwaka
1978, ambapo alimfungia kufanya
shughuli za uongozi na daawa.
Kufungiwa kwa Sheikh Tumba
kulitokana na mahubiri yake yaliozungumzia masuala tata ya mwandamo wa mwezi, maulid, na usomaji hitma.
Misukosuko toka Serikalini:
Baada ya Sheikh Bachu kuchukua mikoba ya mwalimu wake
Sheikh Tumba, naye alipitia misu-

Sheikh Bachu
Yungali hai miongoni mwa Waislamu
Mawaidha yake bado yanufaisha wengi
kosuko kama mwalimu wake.
Alipokea vitisho kutoka Serikalini na kwa baadhi ya makadhi wa
Zanzibar waliotamani kumfungia
shughuli zake.
Kadhi wa wakati ule ambae sitamtaja jina alimuita Sheikh Bachu zaidi ya mara tatu ofisini kwake
akimtisha na kumpa changamoto
asome na atafsiri Quran mbele
yake kama yeye ni Sheikh kweli,
amesimulia Sheikh Yussuf.
Kwa mujibu wa maelezo ya
Sheikh Yussuf, mahubiri ya mare-

hemu Sheikh Bachu ambaye


alikuwa na misimamo isiotetereka
yaliinyima usingizi Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar na hivyo
mara kadhaa alijikuta mikononi
mwa jeshi la polisi, japo hakuwahi
kushtakiwa wala kufungwa.
Wakati ule Zanzibar haikuwa
na mfumo wa vyama vingi vya siasa, hivyo yeye ndio alionekana
kama chama cha upinzani na adui
mkubwa wa Serikali, kwa kuwa
alikuwa akisema ukweli, Sheikh
Yussuf alifafanua.

Akitoa mfano, anasema, Sheikh


Bachu aliwahi kutoa darsa kuhusu
umuhimu wa waajiri kuwatendea
vizuri wafanyakazi wao. Ilikuwa ni
kipindi cha kuelekea uchaguzi na
hivyo akaonekana mbaya na kupata misukokusuko ya Serikali.
Sheikh Nassoro Bachu na Siasa:
Miongoni mwa vitu ambavyo
Marehemu Sheikh Nassoro Bachu
na wanafunzi wake walijiepusha
navyo ni siasa za kijahili (kijinga)
na kibaguzi.

Sheikh Bachu hakuwa mbinafsi wa elimu yake,


aligawana elimu na wanafunzi na Waislamu
kwa ujumla kupitia darsa na mawaidha yake.

Urithi wake hapa duniani:


Marehemu Sheikh Bachu atakumbukwa kwa kuanzisha darsa
za akina mama visiwani Zanzibar
ili kuwainua kielimu.
Sheikh Bachu alianzisha darsa
za akina mama na kuziendeleza.
Wakati ule wanawake wa Kiislamu
hawakuwa na fursa nyingi za kusoma dini yao, anasimulia Sheikh
Yussuf.
Sheikh Yussuf anasema, Bachu
alisaidia sana wanawake kusoma,
na baadhi ya walionufaika leo hii ni
walimu katika vyuo vikuu mbali
mbali vya kawaida na madrasa.
Kadhalika, Sheikh Yussuf alisema, miongoni mwa mambo ya kukumbukwa kwa Sheikh Bachu ni
pamoja na ushiriki wake katika kutoa elimu ya uvaaji hijab visiwani
Zanzibar, mpango ambao ulifanikiwa sana.
Katika uandishi, marehemu
Sheikh Nassoro Bachu kwa ushirikiano na wanafunzi wake waliandika kitabu cha Muandamo wa
mwezi.
Pia, Sheikh Bachu hakuwa
mbinafsi wa elimu yake, aligawana
elimu na wanafunzi na Waislamu
kwa ujumla kupitia darsa na mawaidha yake.
Wanafunzi wa Sheikh Bachu
wametawanyika kila mahali dunia
nzima, ikiwemo nchi za Kimagharibi na Saudi Arabia. Miongoni
mwa wanafunzi wake mashuhuri
ni Sheikh Mselem Ally, Said Gwiji,
Chichi na Hamadi Nassoro.
Kuugua na kifo chake:
Mwaka 2004 katika mwezi wa
Ramadhani akiwa katika darsa
zake msikiti wa Raha Leo, Visiwani, Sheikh Bachu alipatwa na
maradhi.
Kwa mujibu wa Sheikh Yussuf,
Sheikh Bachu alijiwa na kitu kisicho cha kawaida wakiwa darasani
hapo, ambapo walishangaa na
kuhisi Sheikh alipata stroke (mshtuko).
Sheikh Yussuf anasema, kuanzia hapo hadi mauti yanamkuta
marehemu Nassoro Bachu hakufundisha tena darsa kubwa
isipokuwa zile ndogo ndogo za nyumbani tu.
Sheikh Bachu alifariki Febuari
13, 2013 katika eneo la Chukwani,
Zanzibar kwa ndugu yake - Abdallah Bachu na kuzikwa eneo la
Donge. Sheikh Bachu aliacha wake
watatu na watoto 15.
Tunamuomba Allah Subhaanahu Wataallah amrehemu Sheikh
Nassoro Bachu, amsamehe pale alipokosea na ailaze roho yake mahali pema peponi.

21 Rajab 1436, jumatatu Mei 11 - 17, 2015

www.islamicftz.org

Kutoka katika Quran na Sunnah

akati wasomi
wakubwa na mabingwa wa sayansi wanashangazwa na
namna Quran inavyorandana na
tafiti mbalimbali za kisayansi, hebu
tuangalie walau maandiko kidogo
ya vitabu vingine vya kidini ambavyo
baadhi ya wasomi walidai eti ndiko
Muhammad alikonakili Quran
vinavyosema juu ya mambo ya
kisayansi.
Katika Mambo ya Walawi, 11:123, Biblia inataja sifa za wanyama
mbalimbali wanaoliwa na wale ambao hawaruhusiwi kuliwa.
Mambo ya Walawi 11:20 inasema hivi: Tena vyote vitambaavyo
vyenye mabawa viendavyo kwa miguu minne, hivi ni machukizo
kwenu. Katika Biblia ya Kiingereza
vitambaavyo vyenye mabawa viendavyo kwa miguu minne, vimetajwa kama flying insects that walk
on all fours.
Hapa Biblia inakataza kula
wadudu au insects wenye miguu
minne. Haijapatapo kutokea tangu
dunia kuumbwa hadi leo kuonekana au kuwepo mdudu au insect
mwenye miguu minne!
Kwa mantiki hii, ni jambo mu-

sheikh Tawakkal Juma

Quran, Biblia na sayansi


hali na linalotia wasiwasi ufunuo
ueleze watu wasile kitu ambacho
hakijawahi kutokea, kwa sababu ni
rahisi kwa mfano, kwa wanasayansi
kulipinga hilo, maana wanatuambia kuwa katika wadudu, mdudu
mdogo sana ana miguu sita, wala
hapajawahi kutokea mdudu
mwenye miguu minne. Hivyo Mungu anawakataza watu wasile kitu
ambacho hakiko au hajawahi
kukiumba!
Mfano mwingine, ni kile kifungu
kinachoeleza sababu ya kuumbwa
kwa upinde wa mvua au rainbow.
Ukisoma Biblia katika kitabu cha
Mwanzo 9:9-17 utaona Biblia
inaeleza kuwa upinde wa mvua
umeumbwa na Muumba ili umkumbushe apunguze mvua
inapokuwa kubwa ili isije ikazidi na
kuleta maafa kama yale yaliyotokea
wakati wa Nabii Nuh! Hivi ni kweli
Mungu ni msahaulifu kiasi ahitaji
kukumbushwa?
Ukweli ni kuwa upinde wa mvua
hauna uhusiano na kuzidi au kupungua kwa mvua, bali ni mambo

ya kupinda na kuakisiwa kwa


mwanga reflection and refraction of
light! Hivi ndivyo wanasayansi wanavyoeleza na ndiyo maana upinde
wa mvua huonekana mchana!
Ndani ya Quran kuna sura maalum inayoitwa Suratu Maryam
yenye aya 98 ambayo pamoja na
maudhui nyingine inazungumzia
na kutegua kitendawili cha Bikira
Maria na mwanawe Issa au Yesu, kitendawili cha utatu mtakatifu na
kuwa Yesu ni Nabii miongoni mwa
Manabii wa Allah, si Mungu wala si
Mwana wa Mungu na siku ya Qiyama atawakataa wale waliokuwa
wakimwita Mungu au Mwana wa
Mungu.
Kisa cha namna alivyozaliwa
Yesu kinatajwa wazi katika sura hii
ya 19 kuanzia aya ya 16 hadi 33. Kisha aya tatu zinazofuatia; yaani ya
34, 35, na 36 zikasema hivi:
Huyu ndiye Issa mwana wa
Maryam. Hii ndiyo kauli ya haki
ambayo (Wakristo) wanaifanyia
shaka. Haiwi kwa Allah Kufanya
mtoto; Ametakasika, Anapolitaka

jambo basi Huliambia kuwa; nalo


likawa. Na hakika Allah ni Mola
wangu na Mola wenu. Basi muabuduni. Hii ni njia iliyonyooka.
Nawaomba wakristo waisome
sura hii ya Quran kisha walinganishe na yale yaliyomo katika Biblia
kuhusiana na kuzaliwa kwa Yesu.
Bila shaka watastaajabu kama alivyokuwa akiistaajabu rafiki yangu
mmoja niliyekuwa nikisoma naye
kidato cha tano na sita nilipokuwa
nikimsomea sura hii. Kila siku alitaka niirejee rejee huku akiniuliza kwa
mshangao mkubwa kuwa, kweli
haya yametajwa ndani ya Quran?!!!
Quran ni chimbuko la elimu
mbalimbali na kwa hakika ni nuru
yenye kumuongoza mwanadamu
katika maisha ya hapa duniani na
akhera.
Katika kitabu chake; A Concise
Reply to Christianity, A Muslim
View, ukurasa wa 38, Gary Miller,
raia wa Canada na mwanamahesabu aliyekuwa mfanyakazi wa Kanisani na mtangazaji, ambaye alisilimu, ameiita Quran: The Amazing

Quran, yaani Quran Yenye Kustaajabisha au Kushangaza.


Katika maelezo yake anasema
kuwa, Quran haiwashangazi Waislamu tu, bali hata wasiokuwa Waislamu inawashangaza sana.
Anaeleza kuwa, jambo moja ambalohuwashangazasanawasiokuwa
Waislamu ni pale wanapoisoma
Quran huikuta tofauti na walivyokuwa wakitarajia; dhana yao ni
kuwa wanaposoma Quran wanasoma kitabu cha zamani kilichokuja
karne 14 zilizopita, tena jangwani.
Kwa hiyo matarajio yao ni kukuta kimekaa kijangwa jangwa! Mara
wanapoifungua na kuanza kuisoma
wanakuta inazungumzia bahari na
hata vilivyomo ndani ya bahari.
Mara wanakuta ndani mambo
hata ya sasa kabisa kama mabadiliko ya tabia nchi au global warming
nk. Wanakuta pia inazungumzia
sayari, jua, mwezi, nk.
Ndani ya Quran kuna elimu au
sayansi mbalimbali. Juhudi
mbalimbali, tafiti na gunduzi zinazoonyesha ukweli wa Quran kisayansi, ni kazi ndogo sana kulingana
na maajabu mbalimbali ya kitabu
hichi kitukufu, ambacho maajabu
yake hayaishi wala hayataisha.

mlinganiaji
Sheikh Muhammad Duwaysh
Mambo ya msingi kwa
khatwibu wa Ijumaa
Ilipoishia: Khatwibu aelewe
kwamba kuna kundi la Waislamu
hawajihusishi na matukio mbali
mbali yanayouhusu umma na
wala hawajali. Kundi hili linahitaji kuzinduliwa ili wajue nini kinaendelea katika kadhia za Waislamu. Mtu wa karibu nao zaidi
ambaye watu hawa wanaweza
kumtegemea ni khatwibu wa ijumaa
Sita, kuoanisha mada na waswaliji: Khatwibu atoe mada ambayo inaendana na wanaoswali
katika msikiti wake. Kwa mfano,
iwapo waumini wengi katika
msikiti husika ni wageni, kutoa
mada ambayo itakuwa inahusu
matatizo ya jamii ya mahala hapo
si sawa.
Na vile vile msikiti ambao
huswaliwa na wanafunzi wengi si
hekima kutoa khutba inayohusu
matatizo ya ndoa kwa sababu wanafunzi wengi watakuwa hawajaoa.
Kwa hiyo ni wajibu wa khatwibu kuelewa vilivyo hali za waswaliji katika msikiti wake na achague
mada ya khutba inayoendana na
hali zao na yale wanayoyahitajia.
Saba, kuwa na elimu ya kutosha kuhusu khutba: Khatwibu wa
ijumaa aepuke kufupisha mada
kwa sentensi fupi fupi pasina kufafanua watu waelewe. Vile vile

Mpaka tutakapofaidika na Khutba za Ijumaa - 4

asilete ufahamu au fikra zake bali


aegemeze khutba yake katika dalili
za kisharia katika Quran na Sun-

na na kauli za wanawazuoni na
ahakikishe kwamba msikilizaji wa
khutba anakinai kwa maelezo yake

na ananufaika.
Nane, kuelezea kwa kina:
Khatwibu awe na ujuzi wa kutosha na sahihi kuhusu mada aitoayo. Ujuzi wake utokane na
utafutaji (bahthi) wake katika
Quran na hadith za Mtume zilizo
sahihi na wala asitumie hadith
dhaifu (Dhuafaau) au za kutunga
(Mawdhuu).
Kwa hiyo ni wajibu wa khatwibu ajue jinsi ya kuthibitisha hadith
sahihi katika vitabu vya hadith za
Mtume (Rehma na amani ziwe
juu yake) au ajipambe na yale yaliyosemwa na wanawazuoni kuhusu
daraja ya kila hadith anayotaka
kuitumia katika khutba.
Tisa, kuepuka tetesi: haitakikani khatwibu kurukia tetesi
azisikiazo mtaani au katika vyombo vya habari na kuegemeza au
kusheheneza khutba yake na
khabari hizo pasina kuthibitisha
na kubaini ili kujua uhakika wake.
Kumi, masuala ya kitaalamu:
Khatwibu anaweza kuzungumzia
kuhusu masuala ya utabibu au
fani yoyote makhsusi. Mtu anapozungumzia jambo ambalo si fani
yake, aweza kukosea sana. Kwa
hiyo khatwibu afanye juhudi kujua habari hizo kwa kina kutoka
kwa watu wa fani husika kuepuka
kusema maneno ya kushangaza
kwa watu ikawa fedheha kwake.

Kumi na moja, kunasibisha


mada na matukio, mahali na
wakati: Khatwibu anaweza akazungumzia fadhila za kudiriki
Laylatul Qadr usiku wa thelathini
wa Ramadhan, jambo ambalo
halipo. Au panaweza kutokea
tukio kubwa nchini, mjini au kijijini na waswaliji wakakaa kusubiri
khutba itazungumziaje tukio hilo
ili wajue msimamo wa kisharia
ukoje, na wasisikie kitu. Mifano
hii ni kuonesha umuhimu wa
khatwibu kunasibisha mada na
matukio, mahali au wakati.
Kumi na mbili, mada juu ya
jambo moja: Haitakikani kwa
khutba kuchanganya mambo
mengi, kiasi kwamba msikilizaji
asijue khutba imezungumzia nini
haswa. Si vema khutba kusheheni
kila kitu kinachomjia khatwibu
kichwani kuhusu matatizo ya
umma, hadi akamchanganya
msikilizaji wa khutba.
Ni vizuri khutba ikawa juu ya
maudhui moja muhimu
inayoendana na mahali, wakati na
matukio katika wiki na isheheni
hoja na ufafanuzi wa kisharia kwa
dalili kutoka katika Quran, sunna
na kauli za wanawazuoni na mifano hai katika jamii juu ya maudhui hiyo.
Itaendelea toleo lijalo.

21 Rajab 1436, jumatatu Mei 11 - 17, 2015

www.islamicftz.org

ncha ya kalamu
Sheikh Muhammad Issa

Wahamiaji wa Kiafrika wakiwa kwenye boti kuelekea Ulaya.

atika ukuta mmoja


mjini Beghazi, Libya kuna maandishi;
Get Free or Die
Trying, yaani,Kuwa huru au
kufa ukijaribu.Hii ndiyo kauli
mbiu ya wale waitwao wahamiaji haramu kutoka Afrika
kwenda Ulaya. Na kweli wengi
wanafika huko wanakotaka kufika-Ulaya, lakini wengine wengi hufa njiani.
Kiongozi wa Chama cha Upinzani, UKIP cha nchini Uingereza, Nigel Farage, alipoulizwa
nani wa kulaumiwa kwa wimbi
hili la wahamiaji haramu lililoikumba Ulaya? Alijibu:
Kwa kweli ni vitendo vya
nchi za Ulaya vilivyosababisha
tatizo hili, ni ulimbukeni wa
Sarkozy na Cameron kuipiga
mabomu Libya na kuisambaratisha kabisa.
Huu ni mtazamo mmoja wa
tatizo la wahamiaji haramu kutoka
Afrika kwenda Ulaya, ambapo wengi maisha yao hupotea kwa kufa maji
baharini katika mitumbwi iliyosheheni watu wakiimba - Kuwa huru
au kufa ukijaribu.
Bajeti za kugharamia huduma za
uokoaji na za kibinadamu zimeongezeka kwa majeshi ya baharini ya
Malta, Italia, Ugiriki na Hispania.
Hivi sasa Bunge la Ulaya linajadili hatua za kuchukua, ambapo maazimio kumi (10) yamepitishwa kukabili hali hiyo, ikiwemo hatua za
kijeshi za kuharibu mitumbwi inayotumika kuvushia wahamiaji.
Lakini wahamiaji hawa walikuwepo kabla hata ya Libya kuvamiwa.
Ni busara basi kujiuliza sababu za
wimbi hili, uhuru upi wahamiaji wanaoutafuta huko Ulaya na nani alaumiwe?
Katika kitabu, The Immigration
Invasion: How Third World Immigration Is Destroying First World,
mwandishi Arthur Kemp anaandika: Ulimwengu wa tatu ni matokeo
ya (matendo) watu wa ulimwengu
wa tatu.
Kwa maneno mengine, ni Afrika
yenyewe inayostahili kujilaumu kwa
wimbi hili la wahamiaji haramu au
kwa usahihi tuwaite wakimbizi,
kwani kuhama gani huku anakohama mhamaji mpaka kuhiari hata
kufa?
Kwa upande wake mwandishi
Walter Rodney, katika kitabu chake,
How Europe Underdeveloped Africa, anadai kwamba, mataifa
makubwa yakiwemo yale ya Ulaya
ndiyo sababu ya hali ya umasikini wa
kutupwa barani Afrika na kwingineko katika nchi za ulimwengu wa
tatu.

Wahamiaji
haramu au
wakimbizi?
Hapa, tunaona kila upande unautupia lawama upande mwingine.
Lakini swali la msingi ni je, wimbi
hili la wakimbizi kutoka Afrika
kwenda Ulaya linasababishwa na
uduni wa maendeleo?
Mbona hatukuwahi kuona hali
kama hii miaka kadhaa nyuma na
uduni wa maendeleo ukiwa upo katika nchi hizi? Ni lazima kuna jambo
la ziada kando na uduni wa maendeleo au hali ya maisha.
Katika kitabu Migration and
Globalization: Challenges and Perspectives for the Research Infrastructure, Klaus F. Zimmermann anasema: Watu huhama kwa nia ya
kuboresha hali zao za kiuchumi, kujihakikishia mazingira salama zaidi
kuishi, kuungana na familia zao au
kukimbia mateso katika nchi zao za
asili.
Zimmermann anatupa fikra nyingine, kwamba inawezekana kabisa
hawa wanaoitwa wahamiaji haramu si wahamiaji bali ni wakimbizi.
ipo wanachokikimbia hali ngumu ya maisha,
kukosekana usalama na
mateso katika nchi zao.
Ni wazi hawaendi Ulaya kuungana
na ndugu zao.
Hili la kuboresha hali zao za maisha haliwezi kuwa kweli, kwa sababu
hali ngumu za maisha kwa Waafrika
zilikuwepo hata kabla ujio wa wakoloni. Kipindi hicho, hawakujazana
katika mitumbwi kukikabili kifo ili

kufika Ulaya.
Waafrika waliendelea kukabili
mazingira yao duni kama watu wengine kwa sababu chambilecho cha
waswahili mtu kwao.
Tofauti ni kwamba, walikuwa
wakiishi katika hali ya usalama na
amani, pasipo kuwepo mateso wala
khofu kutoka kwa watawala, wala
magenge ya wauaji na makundi ya
waasi yenye kupigania madaraka
katika nchi nyingi za Afrika kwa
mtutu wa bunduki baada ya
kushindwa katika uchaguzi wa kidemokrasia ya kimagharibi.
Nchi nyingi za Afrika baada ya
uhuru zilitawaliwa na wazawa waliosomeshwa katika mfumo wa elimu
wa kimagharibi.
Mfumo huu haukuwa na lengo la
kumuelimisha mwanafunzi kuja
kuitumikia Afrika, bali kuwa nyenzo
ya kuingiza watu katika Ukristo na
kuwaandaa kuwa watumishi wa tawala za kikoloni.
Mfumo huu wa elimu ulizalisha
wasomi butu, wasiojua jinsi ya kuvitumia vipawa vyao kukabiliana na
mabeberu wa nchi za magharibi.
Wengi wa wasomi hawa walihitimu
katika nchi hizo hizo za Ulaya na kurudi kuja kuzitawala nchi zao.
Jinsi wasomi hawa wanavyotawala utadhani walichosomea ni
kuiba mali ya umma, kuuza kwa bei
chee rasilimali za Afrika kwa
wawekezaji wa nchi za kimagharibi
na kuwakandamiza Waafrika wen-

zao.
Waafrika hatukuishia hapa,bali
tawala za kidikteta zilizowekwa madarakani na wamagharibi zikaikumba Afrika.
Naam, ubadhirifu wa mali ya
umma, ufisadi, usimamizi mbovu
wa rasilimali za mataifa ya Afrika
na rushwa ni miongoni mwa sababu zinazopelekea wimbi la wahamiaji haramu kwenda Ulaya.
Kugombea madaraka ni chanzo kingine, kwa kuwa kinasababisha ukabila, ukandamizaji wa
makundi dhaifu katika jamii na
machafuko ya kivita katika nchi
nyingi za Afrika.
Jambo moja la kufahamu hapa
ni kwamba, katika nchi za Afrika
zenye kukumbwa na machafuko
na ukosefu mkubwa wa usalama
na amani ni nchi za magaharibi na
kaskazini. Nchi za Chad, Niger,
Gambia, Senegal, Bukina Faso, Afrika ya Kati, Guinea, Mauritania
na Mali.
Matokeo ya machafuko katika
nchi hizo ni kukosekana amani na
usalama katika bara la Afrika, hivyo
watu wanakimbia kutafuta palipo
na usalama na amani.
Kwa kuwa katika nchi za Afrika
hakuna nchi isiyo na migogoro yake
ya ndani, chaguo jepesi linakuwa
Ulaya, ulimwengu wa kwanza, penye
maisha ya raha na amani, ingawa
wengi wakifika huko wamejikuta
wakiishi maisha ya dhiki kubwa.
Lakini, wakimbizi hawa pia wanatoka nchi za mashariki ya kati
zenye machafuko na vita, zikiwemo;
Uturuki, Syria, Iraq, Afghanistan,
Eritrea na Yemen.
Kwa hiyo sababu moja kuu ya
wimbi hili la wakimbizi kwenda
Ulaya ni ukosefu wa usalama,
mateso na vita kati nchi wanapotoka
wakimbizi.
Kwa kiasi fulani maneno ya
mwandishi Athur Kemp yana ukweli ndani yake, sisi wenyewe Waafrika na serikali zetu ndiyo wa kulaumiwa kwa tatizo hili la wakimbizi
kutoka Afrika kwenda Ulaya.
Lakini kwa kiasi kikubwa pia
Ulaya na Marekani zinahusika. Tukumbuke maneno ya Nigel Farage
kuhusu hatua ya Ulaya kuisambaratisha Libya.
Marekani na washirika wake wanatuhumiwa kutengeneza makundi
ya kigaidi kufanikisha lengo lao la
kubadili tawala wasizozitaka kuelekea mfumo mpya wa dunia New

ubadhirifu wa mali ya umma, ufisadi,


usimamizi mbovu wa rasilimali za mataifa
ya Afrika na rushwa ni miongoni mwa
sababu zinazopelekea wimbi la wahamiaji
haramu kwenda Ulaya

world Order.
Wamasonia wanaamini kuwa
Order comes from Chaos yaani
mpangilio au nidhamu huja kutokana na mparaganyiko. Dunia ilianza
kwa Chaos waliyoiita Big Bhang!
Mlipuko mkuu. Baada ya mlipuko
(chaos) ndiyo tukapata nidhamu ya
sayari, ikiwemo dunia tunayoishi
penye mazingira ya nidhamu (Order).
Kwa hiyo katika kutengeneza
mfumo mpya wa ulimwengu,
Wamarekani na washirika wake
wameunda Al-Qaeda,ISIS, An-nusra, Boko Haram, Al-Shabaab n.k.
Na sisi Waafrika tumeunda Seleka, Anti-Balaka, Mungiki n.k. matokeo ya makundi haya ni vita,
mauaji, mateso na kupelekea vichocheo vikubwa vya wakimbizi.
Kwa upande mwingine, kuna
magenge ya wavushaji wakimbizi
hawa yanayojitengenezea mabilioni
ya fedha.
Watu hawa hufanikiwa kwa
sababu nchi zetu zimeoza kwa
rushwa, kwa hiyo wanachofanya ni
kuwalipa maafisa wa uhamiaji mipakani kuvusha mizigo yao. Hawa
wanaitwa human traffickers au
wasafirishaji wa binadamu.
Mwaka 2011 pekee, zaidi ya wasafirishaji 9,000 nchini Uturuki walijilimbikizia Dola za Kimarekani milioni 303 sawa na Shilingi za Kitanzania 575,700,000,000 (Trilioni
5.75).
kwa hiyo hili si tatizo la wakimbizi
tu, lakini pia ni tatizo la biashara ya
binadamu kinyume na sheria za kimataifa.
Kwa hili Waafrika si wa kulaumiwa peke yao, bali pia magenge ya wazungu yanayowezesha kuwavusha
wakimbizi kutoka Afrika kwenda
Ulaya. Bila magenge haya tatizo hili
la wahamiaji haramu kwenda
Ulaya lisingekuwepo.
Suluhisho si kulaumiana, bali
kutafuta jinsi ya kuzuia sababu za
Waafrika kukimbia na kwenda
Ulaya.
Inaonekana sababu hizi ziko
ndani yetu, ndani ya nchi zetu. Serikali za Afrika zitende haki kwa raia
wake, zisimamie rasilimali vizuri, zijenge mazingira ya uwazi na uwajibikaji kwa viongozi.
Waafrika wa makundi mbali
mbali tuondoe fikra za kibaguzi
kama zinavyotokea huko Afrika ya
Kusini, hali ambayo inasababisha
ukosefu wa usalama na amani. Chuki za kidini kama zilivyotokea Afrika
ya Kati na kupelekea mauaji ya raia,
na zinavyoanza kutokea hapa Tanzania, ni sababu tosha ya kuzalisha
wakimbizi wa kesho kwenda Ulaya.
Tukumbuke kuwa tusipochukua
hatua muwafaka kwa wakati muwafaka, kila mmoja wetu ni mkimbizi
mtarajiwa.

10

21 Rajab 1436, jumatatu Mei 11 - 17, 2015

makala maalum

www.islamicftz.org

21 Rajab 1436, jumatatu Mei 11 - 17, 2015

11

www.islamicftz.org

makala maalum

MGOGORO SAUDIA NA IRAN: SIASA AU DINI?

Mashia walenga kuteka


Makka, Madina Wadai
Karbala ni bora kuliko Makka!

Mfalme Sulayman
wa Saudia

NA ABUU MAYSARA

iaka 35 ya mapinduzi ya Iran


ya mwaka 1979 imeibua
mengi katika umma wa Kiislamu. Badala ya kujikita katika kuleta mabadiliko (transformation)
yanayolenga kuimarisha imani, tawhidi
na maadili ya Waislamu, mapinduzi ya
Iran yamechukua sura ya kisiasa na kimapambano zaidi (reactionary).
Katika kipindi hiki, ulimwengu wa Kiislamu umeshuhudia vita vya wenyewe
kwa wenyewe kati ya Iraq na Iran, Syria,
ISIS na Iraq, Yemen na kwingineko,
kama ulivyoshuhudia pia vita mbili za
Ghuba kati ya Marekani na washirika wake dhidi ya Iraq chini ya
Saddam Hussein.
Mapinduzi ya Iran pia yameibua upya mitazamo inayokinzana kati ya Shia na Sunni
na kupelekea makundi haya
kupigana huko Syria, Iraq na
Yemen.
Miji mitakatifu ya Waislamu, Makka na Madina
Ilisukwasukwa na hadi kukatokea mauaji. Misikiti
maeneo mbalimbali ililipuliwa kwa mabomu na
m a e l f u y a Wa i s l a m u
kupoteza uhai.
Wako wanaoangalia
mvutano unaoendelea
kati ya Saudia na dola za
Kisunni kwa upande
mmoja na Iran kwa upande mwingine kama ni
masuala ya kisiasa tu na
kushindana kuhusu
udhibiti wa mashariki
ya kati.
Ki ukweli, kinachoendelea ni zaidi ya
siasa. Ni mvutano wa
kiitikadi kati ya Shia
wakiongozwa na Iran
na Ahlu Sunna wal
Jamaa, Saudia ikitangulia mbele
kutokana na kuwa
wenyeji

wa mahujaji na hivyo wasimamizi wa


Makka na Madina.
Kuupuuza ukweli huu ni kujidanganya na kuruhusu propaganda za itikadi
moja kuipiku nyingine. Hii ni vita kati ya
u-Shia na u-Sunni.
Iwe haipendezi kusema hivi au inapendeza, huu ndio ukweli na lazima usemwe wazi Waislamu na walimwengu
wajue.
arekani kuunga mkono Saudia na washirika wake kushambulia ma-Houthi walioipindua Serikali ya Yemen ya
Rais Abdul Rabb Mansuri Hadi kunatafsiriwa kuwa Saudia inamtumikia
Mmarekani.
Lakini Marekani ana kila sababu za
kufanya hivyo; kwanza, kama mshirika
mkubwa wa Saudia kibiashara na pili,
kuhalalisha kitendo chake mwenyewe
cha kuchukua hatua za kuvamia na kupiga nchi nyingine pasina kibali cha UN.
Ikiwa ushirika kati ya Saudia na
Marekani kibiashara ni dhambi, kuna
nchi katika dunia ya leo itasalimika na
dhambi hii? Iran yenyewe ni mshirika
mkubwa wa China na Urusi kibiashara,
kijeshi, kiteknolojia na hata kidiplomasia. Nani asiyejua ukweli huu. Kwa nini
isemwe Saudia tu?
Kwa kuwa Saudia na washirika wake
wa dola za Kisunni wanafanya mashambulizi Yemen pasina kupata kibali cha
UN, Marekani inachekelea kwa sababu
sasa ikichukua hatua mithili ya hizi zilizochukuliwa na Saudia na washirika
wake ni nani tena atainyooyesha kidole
kuwa inajifanya polisi wa dunia?
Tukirudi kwenye mada, je kinachotokea kati ya Saudia na Iran ni mgogoro
wa kisiasa au kidini? Msingi wa mgogoro
kati ya Saudia na Iran ni tofauti za kiitikadi kati ya u-Shia na u-Sunni, msingi
ambao umejengwa katika dhana nzima
ya al-Imaamiyyah au uimamu/uongozi.
Mashia wanaamini kwamba uimamu
au uongozi wa Waislamu kufuatia kufariki Mtume Muhammad (Rehma na
amani ziwe juu yake) ulipaswa kuchukuliwa na kizazi cha Mtume, wakati Ahlu
Sunnah wal Jamaa wakiamini kwamba
yeyote mwenye sifa za uongozi katika
maswahaba alifaa kuchukua uongozi wa
Waislamu.
Kwa mujibu wa ma-Shia, Makka na
Madina zinapaswa kuwa chini ya
uongozi wao, kwani wao ndio viongozi stahiki wa Waislamu
dunia nzima. Huu ndio msingi
mkubwa wa vita vya maneno
kati ya Iran na Saudia.
Historia ya uhusiano wa

sasa kati ya Saudia na Iran inaanzia miaka takriban 90 iliyopita, ambapo mnamo 1925 Iran ilikuwa ikiongozwa na
ufalme wa Shah na Saudia ikiongozwa
na ufalme wa ukoo wa Saud.
Kufuatia mapinduzi ya Iran ya mwaka
1979, utawala wa kishia ulinyakua madaraka nchini humo na kufunga mlango
wa uongozi wa kifalme, huku ukifungua
mlango wa uimamu wa kishia.
Kwa upande wa Saudia, ukiachilia
mabadiliko machache ya mwaka 2005
katika mambo ya kisiasa, nchi hiyo imebaki chini ya utawala wa kifalme unaoongozwa na ukoo wa Saud, lakini ukitoa nafasi ya maulamaa wa Kisunni
kuongoza masuala ya kidini.
Uhusiano kati ya Saudia na Iran unaweza kutazamwa katika ngwe (phase)
mbili, Kabla ya mapinduzi ya Iran (mwaka 1929-1979) na baada ya mapinduzi ya
Iran (1979 hadi sasa).

Ngwe ya kwanza: 1929 -1979


husiano kati ya Saudia na Iran
ya leo ulianza mwaka 1929
kwa mkataba uliojulikana
kama Saudia-Iran Friendship
Treaty Mkataba wa Urafiki kati ya Saudia na Iran. Katika mkataba huo, Iran ilitambua rasmi dola ya Saudia.
Hadi kufikia miaka ya 1960, nchi hizi
mbili majirani zilikuwa zikijishughulisha zaidi na kujenga miundo mbinu yao
ya ndani. Kutoka 1929 hadi 1968 matukio mengi yalitokea katika medani ya
kimataifa yaliyoathiri siasa za nje za
mataifa hayo mawili.
Vita vya pili vya dunia, kuundwa kwa
taifa la Israeli, vita kati ya Waarabu na
Israeli na vita baridi ni miongoni mwa
matukio makuu yaliyojiri katika kipindi
hiki.
Iran na Saudia, kila moja ilikuwa na
sera tofauti na yenzake katika matukio
haya. Kuhusu Vita ya Pili ya Dunia, Iran
ilishambuliwa na Urusi na Uingereza
zikilenga kudhibiti mafuta yake, ingawa
Iran haikuwa inaunga mkono upande
wowote katika vita hiyo.
Mfalme wa Iran, Raza Shah akalazimika amwachie kiti cha ufalme mwanae, Muhammad Raza Shah kwa mkandamizo wa mataifa ya kigeni.
Saudia kwa upande wake, nayo kama
Iran, mwanzo wa Vita haikuwa inaunga
mkono upande wowote. Kwa kuwa Saudia haikushambuliwa na mataifa ya kigeni, baada ya vita ikaibuka ikiwa imara
kuliko ufalme wa Iran.
Mwaka 1955, mkataba ulioitwa The
Baghdad Pact ulisainiwa kati ya Uingereza na nchi tano za mashariki ya kati,

ikiwemo Iran.
Nyingine zilikuwa Jordan, Uturuki,
Iraq na Pakistan. Saudi Arabia ilihofia
mkataba huu wa kusaidiana kiulinzi uliowaleta Waingereza karibu na dola za Bani
Haashimu (waliokuwa watawala wa
Makka na Madina kabla ya utawala wa
Saud). Kwa hiyo Iran na Saudia zikaanza
kutofautiana.
Mgogoro kati ya Waisraeli na Waarabu
uliifanya Iran itofautiane na Saudia.
Wakati mataifa ya kiarabu yakipigana na
Israeli katika vita ya mwaka 1956, Iran
ilikuwa na uhusiano kamili wa kibalozi
na Israeli.
Mwaka 1975, Mfalme Faisal wa Saudia
aliuawa. Khalid akashika hatamu za uongozi. Kwa upande wa Iran, sera za Shah
Muhammad Reza Shah zilizojulikana
kama Shahs white revolution zilikuwa
zikikasirisha wa-Iran na kupelekea
ufalme wa Pahlavi kupinduliwa mwaka
1979.

Ngwe ya Pili (1979 hadi sasa)


ufuatia mapinduzi ya mwaka
1979, Jamhuri ya Kiislamu ya
Iran iliundwa chini ya itikadi
ya ushia, ikiwa na sera mpya
kisiasa, kidini, kieneo na kimataifa.
Ni sera hizi mpya za Iran chini ya Ayatollah Khomein zilizoifanya Saudia na
Iran kuwa wapinzani wakubwa Mashariki ya Kati.
Tayari dola hizi mbili zikawa zimesimikwa katika itikadi mbili za kidini zinazokinzana. Iran ikiongozwa na itikadi ya
ushia, isiyomtambua Khalifa Abu Bakar,
Umar na Uthman na yenye chuki na maswahaba kadhaa wa Mtume, na Saudia
ikiongozwa na itikadi ya Ahlu Sunnah wal
Jamaa.
Kuanzia hapo, yote yanayotokea kati
ya Iran na Saudia ni muendelezo tu wa tofauti za kiitikadi ambazo huchukua sura
ya kisiasa. Malumbano ya kidini kati ya
Mashia na Ahlu Sunnah yakaibuka upya
tena kwa nguvu zaidi.
Tofauti na ilivyokuwa karne kadhaa
nyuma; kwa sasa, Mashia wanatumia
mbinu ya wagawe uwatawale wakiwataka Waislamu wa Ahlu Sunna wajitenge
na Mawahabi wanaoongozwa na waSaudia.
Mgogoro wa msingi wa kidini kati ya
Saudia na Iran unahusu uongozi Nani
anastahiki kuongoza Waislamu duniani?
Nani anastahiki kuongoza ibada ya hijja
na usimamizi wa misikiti miwili mitakatifu ya Makka na Madina?
Kwa mujibu wa Mashia, utawala wa
Saudia haustahiki kuongoza miji miwili
mitakatifu ya Makka na Madina. Wanad-

Kwa mujibu wa ma-Shia, Makka na


Madina zinapaswa kuwa chini ya
uongozi wao, kwani wao ndio viongozi
stahiki wa Waislamu dunia nzima.
Huu ndio msingi mkubwa wa vita vya
maneno kati ya Iran na Saudia.

ai utawala huo unapaswa kufukuzwa


kutoka katika ardhi takatifu na badala
yake kuwe na kamati ya kimataifa ya kusimamia miji ya Makka na Madina.
Wito huu ulitolewa mara ya kwanza
mwaka 1926 huko Lucknow, India ambako Waislamu dunia nzima walitakiwa
kuungana na kuwafukuza watawala wa
Saudia kutoka Hijaz. (Oriente Moderno
6 91926): 310, 513-14, 610).
Wito huu ukapamba moto tena baada
ya mapinduzi ya Iran kufuatia mauaji ya
mahujaji 402 mwaka 1986 yaliyochochewa na mipango ya wa-Iran ambao
waliandaa maandamano ya mahujaji yaliyopelekea mapambano na polisi.
Ayatollah Khomein alitoa kauli akisema: Hawa mawahabi muflisi wa maadili
na wasio wachaMungu ni kama jambia
ambalo daima limeutoboa moyo wa
Waislamu kutokea nyuma.
Ayatollah Khomein akaenda mbali zaidi kwa kusema: Makka iko chini ya
mikono ya genge la walioritadi (Khomeini, Radio Tehran, 3 Agosti 1987, BBC,
5 Agosti 1987).
Kilichofuatia ni kuharibika zaidi kwa
mahusiano kati ya Saudia na Iran. Kufuatia kampeni kubwa ya Iran dhidi ya Saudia dunia nzima, Saudia ililazimika kuitisha mkutano mjini Makka Oktoba 1987
uliofunguliwa na Mfalme Fahd ambapo
wawakilishi wa Waislamu kutoka nchi
134 walihudhuria.
Mwezi mmoja baadae, Iran ikaitisha
mkutano wa kimataifa uliohudhuriwa na
wawakilishi kutoka nchi 36 duniani.
Kauli mbiu ya mkutano huo ilikuwa ni
Kulinda Utakatifu na Usalama wa Msikiti Mtakatifu.
Akizungumzia mkutano huo, Rais wa
Iran wa wakati huo, Hashim Rafsanjani,
alinukuliwa akitoa wito wa kukombolewa Makka na kuanzishwa kwa baraza la kimataifa la Waislamu litakaloitawala Makka kama mji huru. (Rafsanjani,
Radio Tehran, 26 Novemba 1987, FBIS,
28 Novemba 1987).
Ayatollah Husayn Ali Montazeri, alipokutana na waalikwa alisema: Utawala wa Saud ni genge la mawakala wa majasusi wa Kiingereza kutoka (eneo) la
Najd ambao hawaiheshimu nyumba ya
Allah, wala wageni wa Allah.
Kisha Ayatollah Husayn akatoa undani wa malengo ya Iran kwa Saudia akisema:
Kama ambavyo Jerusalem itakavyokombolewa kutoka makucha ya wavamizi wa Israeli, hivyo hivyo Makka na
Madina zitakombolewa kutoka katika
makucha ya Saud (Kauli ya Montazeri,
Radio Tehran, 27 Novemba 1987, FBIS,
29 Novemba 1987).
Msomaji utakumbuka madai ya maadui wa Ahlu Sunna kudai kuwa harakati
za kisunna ziliasisiwa na Sheikh Muhammad ibn Abdilwahab aliyetokea Najd na
kwamba eti alifundishwa na jasusi wa Kiingereza Mr. Humphrey. Hizi ni propaganda za mashia walizozieneza duniani.
Watawala wa Iran wakaenda mbali zaidi kwa kudai kuwa watawala wa ukoo wa
Saud unaotawala Saudi Arabia si Waarabu bali ni Wayahudi.
Haya ni madai ya muda mrefu ya

Mashia wa Iran kama yalivyonukuliwa katika Nasir al-Said,Tarikh Al Saud, vol. 1 ([Beirut]: Ittihad shab al-jazira al-arabiyya, n.d.): 392-403.
Msomaji, pima mwenyewe maneno ya chuki
kama haya yalivyoweza kuharibu uhusiano baina
ya Saudia na Iran. Serikali ya Saudia Arabia ilijibu
mapigo kwa kwanza, kupiga marufuku maandamano ya mahujaji wakati wa hijja.
Pili, Saudia ilipunguza idadi ya mahujaji kutoka Iran kutoka 150,000 kwa mwaka (idadi kubwa
zaidi kuliko nchi yoyote ile) hadi 45,000 tu.
Saudia ilifanya hivyo ikitambua kuwa kwa kupunguzwa idadi ya mahujaji wao Iran itasusia kuleta mahujaji, hivyo kuepuka kurudiwa kwa tukio
kama lile la mwaka 1987.
Kwa muda wote wa mgogoro huu wa mahujaji,
Saudia ilikuwa haijavunja uhusiano na Iran,
pamoja na ubalozi wake kuvamiwa na kundi la
watu wenye hasira na kuuawa kwa afisa wake wa
ubalozi.
Aprili 1988, Saudi Arabia ikakata rasmi uhusiano wake na Iran, isiwezekane kabisa kwa wa
Iran kupata visa za hijja.
Kama ilivyotazamiwa, Iran ilisusia hija mwaka
1988, mwaka ambao pia Ayatollah Khomeini alifariki. Iran iliendelea kususa hadi mwaka 1989.
Pamoja na kutokuwapo mahujaji wa Iran, milipuko miwili ilitokea mjini Makkah mwaka huo
(1989) na kuua mahujaji wawili.
Polisi wa Saudia waliwatia nguvuni zaidi ya mahujaji 30 wa kishia kutoka Kuwait na mwezi Septemba mwaka huo watu 16 kati ya hao wakauawa
hadharani kwa kosa hilo.
Ingawa walikiri kutumwa na maafisa wa ubalozi wa Iran huko Kuwait, Serikali ya Saudia
haikusema lolote kuhusu Iran kwa kukosa ushahidi madhubuti.
Mwaka 1990, wabunge 140 wa bunge la Iran
wakaandika barua ya wazi kwa Saudia wakiweka
masharti ya mahujaji wa Iran kurejea tena.
Miongoni mwa masharti hayo ni Saudia kuomba radhi, ilipe fidia damu za mahujaji wa Iran waliokufa mwaka 1987 na pia ikubali idadi ya mahujaji 150,000 kama awali na waruhusiwe kufanya
maandamano ya kuwalaani washirikina.
Saudi Arabia ilikataa masharti yote hayo, na
hivyo kususia huku kukaendelea kwa mwaka wa
tatu. Wakati wa msimu wa hijja, Ayatollah Ali
Khamenei akasema:
Makka iko salama kwa washauri wa Marekani
na wamiliki wa makampuni ya mafuta, lakini
haiko salama kwa Waislamu wenyewe (Ujumbe
wa Khamenei kwa mahujaji, Radio Tehran, 28
Juni 1990, FBIS, 2 Julai 1990).

Kiongozi wa kidini
Iran - Ali Khamenei

21 Rajab 1436, jumatatu Mei 11 - 17, 2015

12

www.islamicftz.org

Je hutenguka udhu wa
mtu anayemuosha mwanawe najisi?

Swali: Aliulizwa Sheikh Muhamad bin Swaleh Al-uthaimin,


Allah amrehemu: Mwanamke aliye na udhu anapomchambisha
mwanawe hulazimika kutawadha?
J a w a b u : Mwanamke
anayemuosha mwanawe wa
kike au wa kiume na akagusa
utupu halazimiki kutawadha,
bali analazimika kuikosha
mikono yake tu kwa sababu
kugusa utupu bila ya shauku
hakuwajibishi udhu, na inavyofahamika mwanamke anayewachambisha watoto wake
hawezi kuwa na fikra za ashiki
akilini mwake.
Kwa maana hiyo, mwanamke akimchambisha mwanawe wa kike au wa kiume
ataosha tu mikono yake kwa
najisi iliyomsibu, wala hawajibiki kutawadha. [Fataawa
na Rasailu za Sheikh Swaleh
bin Uthaimin 4/203].

Je kumgusa mwanamke wa kando


kunachangua
udhu?

S w a l i : Iliulizwa
Kamati ya Kudumu ya
Fat-waa, je kumgusa au
kumpa mkono mwanam-

Ukiyatizama baadhi ya maswali ya wiki hii, na ya toleo lililopita ni kama


yanafanana kwa kiasi fulani, lakini kwa sababu ya nyongeza zilizomo na
majibu tofauti kutoka kwa wanazuoni, tumeona tuyalete kama yalivyo kwa
lengo la kukuongezea faida. Karibu ndugu msomaji.
ke wa kando (ajnabiy) kunatengua
udhu (Wakati tunafahamu
kumpa mkono mwanamke wa
kando ni haramu), kwani tumekuta baadhi ya hadith
kwenye vitabu vya fiqhi zinazoashiria kuwa kumgusa
mwanamke wa kando
hakutengui udhu, na kugusa
kunakozungumzwa wala
hakujafafanuliwa. Je huu
ujumla umewekewa ukomo
kwa kinachoruhusiwa
kuguswa
k w a
mwanamke au
la?

Jawabu: Kauli sahihi miongoni mwa kauli za wanazuoni ni


kuwa, kamwe kumgusa na kumpa
mkono mwanamke hakutengui
udhu, sawa akiwa ni mwanamke
wa kando, mke au mahram, kwani
asili ni kubaki na udhu mpaka
ithibiti kutoka katika sharia kinachofahamisha kuchangua, na hilo
halijathibiti katika hadith sahihi.
Ama kugusa kuliko ndani ya
neno la Allah:
Enyi mlioamini! Mnaposimama ili mkasali basi osheni nyuso
zenu na mikono yenu, mpaka
kwenye neno lake, Na mkiwa
wagonjwa au mmo safarini, au
mmoja wenu ametoka chooni au
mmeingiliana na wanawake, na
hamkupata maji, basi kusudieni
udongo ulio safi na kupaka nyuso zenu na mikono yenu; muradi wa (kugusa) kwa kauli sahihi miongoni mwa kauli za

wanazuoni ni jimai (kuingiliana).


[Fataawa Laj-natud Daimah
5/268].

Je kuwatazama wanawake na wanaume


walio uchi kunaharibu
udhu?

Swali: Iliulizwa Kamati ya Kudumu ya Fat-waa: Je udhu unachanguka kwa sababu ya kuwatazama wanawake na wanaume walio
u c h i ? Na j e u d h u w a m t u
huchanguka kwa kuangalia utupu
wake?
Jawabu: Hauchanguki udhu
wa mtu aliyetawadha kwa sababu
ya kuwatazama wanawake na wanaume walio uchi, wala kwa kujiangalia yeye mwenyewe, kwani
hakuna ushahidi katika suala hili.
[Lajnatud Daimah 5/270].

Je huchanguka udhu wa

fat-wa kwa mwanamke wa kiislam


sheikh Shabani Mussa

mkunga anayefanya kazi


ya kuzalisha?

Swali: Iliulizwa Kamati ya Kudumu ya Fat-waa, je mkunga hutakiwa kuoga au udhu unamtosha?
Jawabu: Mkunga hawajibiki
kuoga au kutawadha kwa sababu
ya kusimamia taratibu za uzazi wa
mjamzito, isipokuwa mkunga anapotaka kuswali huwajibika kuiosha najisi iliyoingia kwenye nguo
au mwili wake.
Lakini mkunga hutenguka
udhu endapo atagusa utupu wa
mjamzito wakati wa kuzaa. [Fatawa laj-natud Daimah 5/316].

Je malai ya nywele na
rangi ya mdomo inatengua udhu?

Swali: Aliulizwa Sheikh Muhamad bin Swaleh Uthaimin Allah amrehemu: Je mwanamke kutumia cream ya nywele na rangi
ya mdomo (lipstic) kunachangua
udhu?
Jawabu: Mwanamke kujipaka cream au mafuta ya aina yoyote
hakutengui udhu, na hata funga
haiharibiki. Isipokuwa katika
funga, kama lipstic itakuwa na
ladha, na kama hiyo ladha ya lip
stick itakuwa inapenya tumboni
kwake, hapo isitumike.[Fataawa
na Rasailu za Sheikh ibn Uthaimin
4/201].

afya yako
Pazi Mwinyimvua

Maradhi mengi yanayomkabili


mwanadamu yanachangiwa na uwepo wa sumu au uchafu mwingi mwilini (waste substances), kula kupita kiasi, uchaguzi mbaya wa vyakula na
vinywaji, kutokunywa maji ya kutosha, maisha ya kufanya kazi bila ya
kutoka jasho, kutokufanya mazoezi
na mtindo mbaya wa maisha kwa
ujumla.
Makala yetu ya leo inazungumzia
umuhimu wa kufanya uchaguzi wa
vile tunavyokula na kunywa.
Kitabu Kitukufu cha Quran kikiwa ni mwongozo kwa Waislamu na
Wanadamu wote kwa ujumla, hakikuacha kutoa maelekezo kuhusu
uchaguzi wa vyakula kama tunavyojifunza katika aya mbalimbali.
Enyi watu! kuleni vilivyomo katika ardhi, halali na vizuri, wala msifuate nyayo za shetani. Hakika yeye ni
adui yenu aliye dhaahiri (Quran:
2.168).
Enyi Mlioamini kuleni vizuri tulivyokuruzukuni, na mumshukuru
Mwenyezi Mungu, ikiwa mnamuabudu Yeye Peke Yake. (Quran:
2:172).
Na kuleni katika vile alivyokuruzukuni Mwenyezi Mungu vilivyo vizuri na halali na mcheni Mwenyezi
Mungu ambaye nyinyi mnamwamini (Quran: 5: 88).
...... na kuleni (vizuri) na kunyweni
(vizuri). Lakini msipite kiasi tu. Hakika yeye (Mwenyezi Mungu) hawapendi wapitao kiasi. (Quran; 7:31).
Kwa mujibu wa aya tulizozirejea
hapo juu, Mwenyezi Mungu kupitia
Quran Tukufu anawataka Waislamu

Umuhimu wa kuchagua vyakula

na wanadamu wote kwa ujumla kufanya uchaguzi wa vyakula kwa kuzingatia vigezo viwili. Vigezo hivyo ni
uhalali na ubora (uzuri) wa vyakula.
Vyakula vya haramu tunavyotakiwa kuwa mbali navyo ni kama vile
vyakula vya wizi, mali au vyakula
vilivyopatikana kwa njia za rushwa,
nyama iliyokufa bila ya kuchinjwa,
mnyama aliyechinjwa kwa kutimiza
masharti ya wachawi, na nyama ya
nguruwe.
Kama watu wangezingatia kula
vya halali, dunia hii ingekuwa kisiwa
cha amani. Ndio kusema, tusingeshuhudia watu wakiwaua albino na
kuuza viungo vyao.
Wala tusingewaona watu wenye
dhamana ya kufanya kazi za umma au
katika sekta isiyokuwa ya umma wak-

ijilimbikizia mali kwa njia za haramu


kama wizi na rushwa.
Waislamu wengi wanajitahidi katika kufanya uchaguzi wa vyakula kwa
kigezo cha uhalali kama vile kutokula
kibudu au nyama ya nguruwe. Msiba
upo katika kufanya uchaguzi wa
vyakula kwa kuzingatia kigezo cha
ubora.
Hata yule mwenye kiwango kizuri
cha elimu ya Quran na Sunna bado
yuko mbali na utekelezaji wa mafundisho ya Uislamu wa uchaguzi wa
vyakula kwa kigezo cha ubora.
Waislamu wengine wanakwenda
mbali zaidi kwa kushangaa kuwa wafanye uchaguzi hata kwa vyakula vya
halali? Kabla ya kujibu swali hili
kisayansi, vema kwanza turejee tena
Quran Tukufu pale ilipoeleza sababu

za kufanya uchaguzi.
Na katika ardhi muna vipande
vinavyoungana (na kuzaa kwake
namna mbalimbali) na muna mabustani ya mizabibu, na mimea mingine,
na mitende ichipuayo katika shina
moja na isiyochipua katika shina
moja. Vyote vinanoshelezwa
(vinamiminiwa) na maji yale yale; na
tunavifanya bora baadhi yake (kuliko)
vyengine katika kula. Hakika katika
haya zimo ishara kwa watu wanaotia
mambo akilini (Raad, 13.3).
Katika aya hapo juu, Mwenyezi
Mungu anatufundisha namna ya
uhodari wake wa kuumba. Ingawa
maji ni yale yale na udongo ni ulele ule,
lakini anaumba aina tofauti za mimea
zenye ubora tofauti. Wanyama nao
ubora wao unatofautiana, ingawa wa-

naweza kula aina ile ile ya majani.


Kwahiyo, lazima tufanye uchaguzi
hata kwa vyakula vilivyo halali.
Watu wengi, Waislamu na wasiokuwaWaislamuhawajishughulishi
kutafuta elimu ya kujua mambo ya
vyakula. Matokeo yake wanakula kila
kinachopatikana. Hii ni hatari sana
kiafya.
Hebu tujiulize maswali haya:
Vyakula vya kukaanga na vile vya
kuchemsha vipi ni hatari kwa afya ya
mlaji, kama mtu anakula kila siku?
Ni kwa namna gani ulaji mbaya
unasababisha upungufu wa nguvu za
kiume au upungufu wa nguvu za kike,
jambo ambalo kwa sasa ni tishio la
uhai wa ndoa nyingi.
Nyama nyekundu kama ngombe,
mbuzi na nyama nyeupe kama samaki, ipi bora zaidi kiafya? Kwanini
maziwa ya mama ni bora zaidi kuliko
yale ya kopo kwa mtoto?
Ni kwa sababu gani vyakula vya kiwandani vinachangia zaidi magonjwa
kama kisukari na shinikizo kubwa la
damu kuliko vyakula vya asilia.
Baadhi ya wafugaji wa kuku wa
kisasa wanawapa kuku vidonge vya
ARV ili wakuwe haraka; nini madhara yake kiafya kwa walaji kuku?
Tuhitimishe makala yetu kwa
kuwakumbusha wasomaji wetu kuwa
muumini mwenye afya bora anapendwa zaidi na Mwenyezi Mungu kuliko muumini mwenye afya dhaifu.
Taifa imara linajengwa na watu
wenye afya bora. Ujenzi wa afya bora
unamihimili yake. Ulaji wa vyakula
vilivyo bora ni muhimili mmoja
wapo.

21 Rajab 1436, jumatatu Mei 11 - 17, 2015

13

www.islamicftz.org

uchumi na biashara
JAMAL ISSA

Aina za riba
A

metukuka
Mu u m b a
mbingu na ardhi mwenye
kuhimidiwa na kushukuriwa. Swala na salam
zimfike mbora wa viumbe aliye mjumbe wa
mwisho wa Rahman kwa
walimwengu wote, kisha
salam kwa wenye kufuata
muongozo.
Ndugu mpenzi msomaji karibu tena kwa
mara nyingine katika
mfululizo wa makala
zetu juu ya uchumi na biashara katika Uislamu.
Katika makala yetu ya leo
In Sha Allah tutadurusu
juu ya aina za riba.
Riba kwa ujumla ni
ziada au nyongeza inayopatikana bila kufanya
kazi. Riba katika lugha
ya kiarabu maana yake ni
ziada. Ama katika lugha
ya elimu ya fiq-hi maana
ya neno Riba, ni ile ziada
anayolipwa mdai juu ya
rasilimali yake.
Mwenyezi Mungu
anasema: Enyi mlio
amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba
zilizobakia, ikiwa nyinyi
ni Waumini. Basi msipofanya jitangazieni vita na
Mwenyezi Mungu na
Mtume wake. Na mkitubu, basi haki yenu ni rasilimali zenu. Msidhulumu wala msidhulumiwe

(2:278-279).
Yaani msimdhulumu
mdaiwa kwa kumtaka
zaidi ya rasilimali; wala
msidhulumiwe kwa kupunguziwa rasilimali.
Mtume (Rehma na
amani ziwe juu yake)
amesema: Jiepusheni
na mambo saba yanayoangamiza. Masahaba
(Radhi za Allah ziwe juu
yao) wakamuuliza: Ni
yepi hayo ewe Mtume wa
Mwenyezi Mungu?
Akasema: Kumshirikisha Mwenyezi
Mungu, na uchawi, na
kuiuwa nafsi iliyoharamishwa na Mwenyezi
Mungu isipokuwa ikiwa
kwa ajili ya haki (kwa aliyefanya makosa yanayostahiki kuhukumiwa
auawe), na kula riba, na
kula mali ya yatima, na
kurudi nyuma katika vita
(ukawaacha wenzako
peke yao), na kuwasingizia uongo wanawake
wema wasio na makosa
walioamini (kuwa eti
wamezini) (Bukhari na
Muslim).
Na Mtume (Rehma
na amani ziwe juu yake)
amewalaani wote wanaoshiriki katika Riba.
Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) amesema: Mwenyezi Mungu
amemlaani anayekula
Riba na anayelisha na

mashahidi wake. (Bukhari- Muslim na


Imam Ahmad).
Kuna aina kuu mbili za riba, ambazo
ni Riba An Nasiyah na Riba Al Fadhil.
Katika zama za ujahiliya aina ya kwanza
tu ilijulikana kama riba, ingawa Mtume
(Rehma na amani ziwe juu yake) alipokuja alibainisha aina ya pili ya riba.
Kwa kuwa Riba An Nasiyah ilikuwa
ndio aina pekee ya riba inayojulika katika kipindi cha ujahiliya (kabla ya Uislamu), hivyo aina hii ya riba huitwa Riba
Al Jahiliya na kwa kuwa pia aina hii ya
riba ndio iliyokatazwa moja kwa moja
katika Quran, aina hii pia huitwa Riba
Al Quran.
Riba An Nasiyah ni ziada anayolipa
mtu aliyekopeshwa kwa kushurutishwa
na mdai. Kwa mfano, mtu akitaka kukopa shilingi elfu, anashurutishwa kulipa shilingi elfu na ziada ya mia moja.
Sasa zile shillingi mia moja za ziada ndio
riba yenyewe.
Mwenyezi Mungu anatuhimiza
kuwa, ikiwa mtu anataka kumkopesha
mwenzake mwenye shida, basi amkopeshe mkopo mwema bila ya kumuongezea mwenzake dhiki, kwamba
kwa kufanya hivyo ndio baraka itokayo
kwa Mola wake huongezeka katika mali
yake mtu.
Ama unapomkopesha mwenye shida
kisha ukachukua faida ya riba, basi
huko ni kumzidishia dhiki mwenzio na
pia ni kuiangamiza mali yako na kuiondolea baraka. Riba hii pia inahusisha
ziada juu ya deni kwa sababu ya kuahirisha kulipa pale ambapo mkopaji
ameshindwa kulipa kwa wakati. Hii pia
ni haramu, kwani hukumu za mdaiwa
zipo wazi pindi muda wake unapokwisha.
Hukumu za mdaiwa ni ama kumsamehe au kumpa muda zaidi, na si

kuongeza deni.
Allah anasema: Na akiwa (mdaiwa)
ana shida, basi (mdai) angoje mpaka
afarijike. Na mkiifanya deni kuwa ni
sadaka, basi ni bora kwenu, ikiwa mnajua (2:280).
Aidha, ili kufunga mlango wa nyuma
wa kula riba, katika hadith ya Anas ibn
Malik (Radhi za Allah ziwe juu yake)
Mtume (Rehma na amani ziwe juu
yake) amekataza mkopeshaji kupokea
zawadi kutoka kwa mkopaji.
Pia, katika hadith nyingine ya Anas
ibn Malik katika Sunan al-Bayhaqi,
Mtume (Rehma na amani ziwe juu
yake) amekataza mkopeshaji kuchukua
chakula au kupanda kipando cha mkopaji kama haikuwa ada yao kabla ya kukopeshana. Ukweli ni kwamba aina hii
ya riba imeshika hatamu katika wakati
wetu huu na kuwa moja ya sehemu ya
msingi ya uchumi na biashara.
Mfumo wote wa kifedha umejengwa
juu ya riba, kutoka kwenye vyama vya
kuweka akiba na kukopa mpaka benki
zinazoitwa benki za kibiashara (commercial banks). Taasisi zote hizi hujiendesha kwa riba kama chanzo mama
cha mapato.
Kutoka kwa Abu Hurayrah: Mtume
(Rehma na amani ziwe juu yake) amesema: Kwa hakika itakuja zama kwa
mwanadamu ambapo kila mtu atakula
riba na kama hatofanya hivyo vumbi
lake litamfikia (Abu Dawud, Ibn Majah).
Aina ya pili ya riba ni Riba Al Fadhil.
Riba ya kufadhilisha ni ile ya kubadilishana pesa kwa pesa au chakula kwa
chakula na kuchukuwa zaidi.
Kwa mfano, mtu anapokwenda kubadilisha dhahabu yenye uzito wa gram
kumi kwa ajili ya kupata dhahabu nyingine iliyomvutia zaidi, akalipwa bada-

Kuna aina kuu mbili za riba,


ambazo ni Riba An Nasiyah na
Riba Al Fadhil

ALI (r.a) ANAVYOWAZUNGUMZIA ABUBAKAR,


UMAR NA UTHMAAN (r.a):
Imesimuliwa kutoka kwa
Abi Muusa Al-Ashariy,
Ali Bin Abi Twaalib (Radhi
za Allah ziwe juu yake)
alisema

la yake dhahabu yenye uzito wa gram


saba. Hiyo inahesabiwa ni riba.
Inavyotakiwa kwanza mtu aiuze
dhahabu ile kwa thamani yake, kisha
ainunue dhahabu anayoitaka. Mtume
(Rehma na amani ziwe juu yake) amesema: Msiuze Dirham moja kwa Dirham
mbili kwani nakuogopeeni riba.
Na akasema: Dhahabu kwa dhahabu, fedha kwa fedha, ngano kwa ngano,
chumvi kwa chumvi, mkono kwa mkono, atakayechukua zaidi au kutaka zaidi, kesha kula riba (Ahmed na
Bukhari).
Mtu mmoja alikwenda kwa Mtume
(Rehma na amani ziwe juu yake) akiwa
amebeba tende. Mtume (Rehma na
amani ziwe juu yake) akamwambia;
Tende hii haipatikani kwetu hapa?
Mtu yule akasema; Ewe Mtume wa
Mwenyezi Mungu, tumebadilishana
tende yetu pishi moja kwa pishi mbili za
tende hizi. Mtume (Rehma na amani
ziwe juu yake) akamwambia; Hiyo ni
riba, zirudishe, kisha uza tende yetu, halafu nunua tende hizi (Muslim).
Kwa ujumla ni haramu kuzidisha katika kubadilishana kitu cha jinsi moja.
Mtume (Rehma na amani ziwe juu
yake) amebainisha bidhaa sita ambazo
ni ngano, dhahabu, fedha, tende, shairi
na chumvi, ambapo katika kubadilishana bidhaa ya namna moja hubadilishwa
kwa bidhaa ya namna hiyo hiyo kwa
kipimo cha ujazo au uzito ulio sawa bila
kuzingatia tofauti ya ubora iliyopo.
Mathalan, kilo moja ya tende ya daraja
ya juu kwa ubora hubadilishwa kwa kilo
moja ya tende ya daraja ya chini yenye
ubora duni na si vinginevyo. Au anayehitaji tende za daraja ya juu auze tende
zake zenye ubora duni katika soko na
atumie thamani hiyo kununua tende za
daraja ya juu katika ubora. Na bidhaa
hizi hubadilishwa hapo kwa papo, mkono kwa mkono (spot transaction).
jakham@rocketmail.com 0713 996
031

Je nisikujulisheni juu ya watu bora kuliko wote baada ya Mtume wa Allah? Ni Abuu Bakr, kisha baada
ya Abuu Bakr ni Umar. Na laiti ningependa ningekujulisheni kuhusu watatu wao
(Tuhfatu Swiddiyq Fiy Fadhwaaili Abii Bakr Swiddiyq, Mjalada 1, uk. 7)

Watu maarufu wasiokuwa Waislamu wasemavyo kuhusu Uislamu

THOMAS
CARLYLE
(1795-1881):

The lies (Western slander) which the west has heaped


round this man (Muhammad) are disgraceful to ourselves only. A silent great soul, one of that who cannot but be earnest. He was to kindle the world, the worlds
maker had ordered so
Tafsiri: Uongo (kashfa za Wamagharibi) ambazo Wamagharibi wamezirundika kumzunguka mtu huyu
(Muhammad) ni fedheha tu kwetu wenyewe! (Ni) mtu mkimya mwenye moyo mkuu, mmoja miongoni
mwa wale ambao hawawezi kuwa vinginevyo ila waungwana. Alikusudiwa kuungarisha ulimwengu,
Muumba wa ulimwengu aliamuru hivyo.

21 Rajab 1436, jumatatu Mei 11 - 17, 2015

makala

14

www.islamicftz.org

Zama za ukweli na uwazi zitafika lini?


NA IDDI JENGO

kutokuwa mkweli. Akawaambia leo


ni kwa mfalme!!!
Kweli wale watu wakaenda mpaka
kwa mfalme. Kwa bahati kwa mfalme
hakukuwa na kitu. Wakaamua wakae
wapumzike. Ikapita muda mrefu bila
kurejea Juha akaona kimya naye
akaamini itakuwa kuna sherehe kweli, akafunga safari mpaka kwa mfalme
lakini hakukuta kitu. Yapo matukio
mengi ya nchi yanayotokea katika
zama hizi za uhai wetu ambayo yamelitia Taifa letu katika janga la umasikini ambao waathirika wakubwa ni raia
masikini wasiokuwa na hatia, ambao
bado wanasiasa wetu uchwara
watatumia udhaifu wa wananchi
hawa na kuwaahidi kwa maneno ya
kijifedhuli na dhihaka katika kipindi
hiki cha uchaguzi unaokuja.
Chakusikitisha katika nchi yetu
matukio makubwa ya kifisadi yalipoibuka na mafisadi wakagundulika,
hawakuonekana kwamba ni watu wa
ajabu na wabaya sana, bali walioonekana ni mashujaa, ajabu sana!!
Kwa mwenendo huu, tusitaraji
kwamba mtu anayetaka kufanya
ufisadi ataogopa, kwani anajua Tanzania bado hakuna hatua madhubuti
dhidi ya mafisadi wa kweli. Ukipima
kwa vipimo vya sawa, utagundua
kwamba bado Tanzania haijapata viongozi wazalendo wa kweli.
Miongoni mwa mambo ambayo
yanayoweza kumjengea mtu tabia ya
ukweli na uwazi ni mtu au jamii kuwa
na dhamira madhubuti katika kuyaendea mambo. Jambo la kusikitisha
kwa baadhi ya viongozi wetu walio
wengi hawana dhamira madhubuti
kwa jamii yetu ya Tanzania.

naweza ukaongopea watu


wote kwa muda mchache,
unaweza kuongopea watu
wachache kwa muda
wote, lakini huwezi kuongopea watu
wote kwa muda wote. (Abraham Lincoln)
Awali ya yote napenda nianze kwa
kumshukuru Mwenyezi Mungu
Subhanahuu Wataala na nimtakie
rehma na amani Mtume wa mwisho
(Rehma na amani ziwe juu yake) pia
niwatakie rehma na amani wale wote
wanaoshikamana na mwenendo
mwema mpaka siku ya mwisho .
Mwanadamu ni kiumbe wa kijamii anayetegemea mahitaji yake
kutoka kwa wanajamii wenzake
wakubwa kwa watoto wenye nia nzuri
ama nia mbaya, yawe mahitaji yoyote
yawayo, ya kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni au kiimani.
Mambo haya yako hivi tangu enzi
na enzi, na imekuwa ni ada katika
maisha ya mwanadamu. Yapo mambo mawili ya msingi katika mengi ambayo mwanadamu akiyakosa huwa ni
mwenye fazaa kubwa, kutengwa na
jamii na kukosa taarifa sahihi .
Kukosa taarifa na kutengwa na
jamii ni mambo ambayo yamewahi
kuikumba jamii ya Kiislamu, katika
kile kipindi kigumu cha awali cha
ujenzi wa umma imara wa Kiislamu
pale Makka.
Mtume Muhammad (Rehma na
amani ziwe juu yake) akiwa na maswahaba zake wachache waliomuamini kikweli walitengwa katika lile
bonde la shiib bin abi twalib na jamii
ya kidhalimu ya Makka, na kupelekea
kukosa taarifa na huduma za msingi
za kijamii.
Kwa tukio hilo Waislam wengi
walipoteza uhai wao. Ni tukio ambalo
Quran imeacha kumbukumbu kwetu
kama sehemu ya mafunzo. Allah Taala anasema katika Quran:
Mnadhani kuwa mtaingia
peponi, bila ya kukujieni kama yaliyo
wajia wale walio pita kabla yenu? Iliwapata shida na madhara na wakatikiswa hata Mtume na walio amini
pamoja naye wakasema: Lini nusura
ya Mwenyezi Mungu itakuja? Jueni
kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu
ipo karibu( 2: 214).
Swali lililoulizwa (nusura ya
Mwenyezi Mungu itakuja lini?) ndo
limenishajiisha kuja na mada hii. Nasi
yatupasa tujiulize, zama za ukweli na
uwazi zitafika lini? Katika maisha yetu
tumepitia na tunaendelea kupitia
zama za uongo na uwazi kama si uongo na kificho.
Watu wanakamatwa, wanapigwa
na wanafungwa kwa uwazi na unasemwa uongo wa wazi, na watu wanakamatwa, wanapigwa, wanafungwa kwa kificho na unasemwa uongo
kwa lengo la kuthibitisha na kuhalalisha dhulma hizo.
Moja ya jambo la msingi katika
maisha ya mwanadamu ni kujifahamu yeye mwanadamu ni nani na
analengo gani katika ulimwengu huu
ulio wazi lakini uliojaa kificho?
Kufahamu lengo la maisha, kutamuwezesha mwanadamu kufanya
mambo yake kwa namna iliyo kuwa
nzuri na kuwa na matarajio ya hakika
katika kila analolifanya .
Ukweli kuhusu lengo la maisha ya
mwanadamu ni jambo la msingi sana
ambalo kwa bahati mbaya halijulika-

Tanzania yetu ipo katika mchakato wa


uchanguzi unaotarajiwa kufanyika
Oktoba, ambapo tutampata Rais wa
awamu ya tano. Awamu ya kwanza
ya Mwalim Julius Kambarage Nyerere
ilikuwa ngumu kwa wote lakini, kwa
Waislamu ilikuwa ni ngumu zaidi.
ni na wengi miongoni mwetu. Na
uongo kuhusu lengo la maisha ndio
unatangazwa na kusimamiwa waziwazi utapelekea mwanadamu kuangamia.

anzania yetu ipo katika


mchakato wa uchanguzi
unaotarajiwa kufanyika
Oktoba, Mungu akipenda
ambapo tutampata Rais wa awamu
ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania. Awamu ya kwanza ya
Mwalim Julius Kambarage Nyerere
ilikuwa ngumu kwa wote lakini, kwa
Waislamu ilikuwa ni ngumu zaidi.
Awamu ile ilikuwa ngumu zaidi
kwa Waislamu kwa sababu ndio tulikuwa tunatoka kutawaliwa na wakoloni na kuwa Taifa huru na wapambanaji (Waislamu) hawakuthaminiwa kiwango kinachostahiki. Kilikuwa
ni kipindi cha kauli mbiu nyingi
ikiwemo Ujamaa, Azimio la Arusha
n.k. ambazo utawala ulijaribu kuzifanyia kazi (1963- 1985).
Awamu ya Alhaji Ali Hassan
Mwinyi (1985-1995) ilifuata ambapo
Tanzania ilipata neema kidogo kwa
baadhi ya wanajamii lakini kwa Wais-

lamu hali ilikuwa bado ngumu zaidi.


Moja ya kauli mbiu iliyoshtadi kipindi
hicho ilikuwa ni awamu ya rukhsa.
Tukiachana na awamu hiyo, awamu iliyofuata ambayo ndio kiini cha
mada yetu ilikuwa kipindi cha Benjamini William Mkapa, awamu iliyobatizwa, zama za ukweli na uwazi.
Moja ya mambo aliyasema Rais Mkapa kipindi cha utawala wake akilihutubia bunge mjini Dodoma alisema: miongoni mwa mambo ya
msingi katika utawala bora lazima
ujipambe na sifa ya ukweli na uwazi
katika kufanya maamuzi, hii ni kwa
viongozi wa siasa na watumishi wengine wa umma, katika masuala ya
ukusanyaji mapato na matumizi.
Jambo la kuzingatia ni suala la ukweli na uwazi (Trufullness and transparency ). Mambo haya ni katika
msingi wa uhuru, uadilifu wa maisha
ya mwanadamu na viumbe wengine.
Ukweli ni jambo zuri na kila mtu anapenda aambiwe ukweli.
Kinyume cha ukweli ni uongo. Na
hakuna mtu anapenda kuambiwa
uongo. Kwa kusimamia ukweli dhumuni letu ni kuwa na uhuru kamili,
usawa na haki kwa njia yoyote itakay-

ohitajika. Zipo kauli nyingi kuhusu


ukweli baadhi ni hizi zifuatazo.
Unaweza kuepuka ukweli lakini
huwezi kuepuka matokeo ya kuukwepa ukweli ( Ayn Rand,19051982).
Ukweli upo katika upande unaoonewa (Malcom X).
Kweli haiachi kuwa kweli kwa
sababu watu wanaikataa
Ukweli huwa haudhuriki wala
haunatijiki isipokuwa mtu/jamii ndo
itafaidika kwa ukweli wake au itadhurika kwa kupuuza ukweli.
Kwa kuwa na kauli mbiu nyingi
haimaanishi ndo mmefanikiwa katika kauli mbio hizo, moja ya jambo linalotuangamiza kama taifa ni kuwa
na baadhi ya viongozi wetu waandamizi ambao si wa kweli katika
maneno na vitendo, mpaka wanajidanganya wenyewe.
Mfano, Juha yeye alikuwa anajitahidi kuwa na ratiba zote za maeneo
yenye sherehe katika mji wao. Siku
moja ikawa hana ratiba yoyote ya
sherehe. Kwa kuwa watu wake wanapata taarifa kutoka kwake wakamfuata kumuuliza leo wapi? Juha alikuwa
hataki kuonekana hajui, akaamua

hamira ni jambo ambalo


msingi wake ni uaminifu
na upendo wa kweli. Kwa
maana nyingine, raia wa
Tanzania wanahuruma na upendo na
nchi yao ndo maana huwa wanajitahidi kwa kadri ya haja kutekeleza majukumu kwa namna wanavyoweza,
lakini wanakatishwa tamaa na baadhi
ya viongozi.
Uislam umeipa dhamira kipaumbele. Mtume (Rehma na amani ziwe
juu yake) anasema: Kila jambo/tendo la mtu hukubaliwa kutokana na
nia/dhamira yake
Kwa kuwa na dhamira madhubuti, sote kwa pamoja viongozi na raia
tutaiwezesha nchi yetu kupiga hatua
kubwa na kuepusha mizozo na
migongano isiyo ya msingi. Ukweli na
uwazi utawezesha mambo yetu kuwa
mepesi, na Mwenyezi Mungu atatusamehe makosa yetu. Hayo ni mafundisho ya Quran, kitabu kilicho
muongozo kwa wanaadamu.
Hakika wale wanaoupotoa ukweli
uliomo katika Ishara zetu hawatufichikii Sisi. Je! Atakaye tupwa motoni
ni bora au atakaye kuja kwa amani
Siku ya Kiyama? Tendeni mpendavyo,
kwa hakika Yeye anayaona mnayo yatenda. (41:40).
Enyi mlioamini! Mcheni
Mwenyezi Mungu na semeni maneno
ya kweli. Mwenyezi Mungu atakusahilishieni (kukutengenezeeni) mambo yenu na atakusameheni madhambi yenu. Na anaye mtii Mwenyezi
Mungu na Mtume wake, bila ya shaka
amefanikiwa mafanikio makubwa.
(33:70-71).

Jengokeya5@gmail.com 0783
174 730

21 Rajab 1436, jumatatu Mei 11 - 17, 2015

15

www.islamicftz.org

Mahusiano ya kibinadamu
USTAADH HABIB HAMIM

Ulemavu wa akili ni nini?


Ulemavu wa akili ni hali ya matatizo aliyonayo mtu kutokana na upungufu wa akili unaomzuwia kujifunza
na kutekeleza majukumu au kazi anazozifanya mtu wa kawaida asiyekuwa
na ulemavu, anaefanana naye kwa
umri, kiutamaduni, kiuchumi, na kijamii.
Kutokana na upungufu wa akili,
muathirika wa maradhi ya akili
atashindwa kutimiza mahitaji yake
kama ilivyo kwa mtu wa kawaida.
Mahitaji hayo yanaweza kuwa ni
ya kielimu, kisaikolojia, kimaisha,
kikazi, kiuchumi na kiafya.

Ulemavu wa akili:

Jamii inatakiwa kutambuwa uwepo wa watu wenye ulemavu, kuwathamini kwa ubinadamu wao na
kuwafanyia ihsani na wema kama Allah Taala anavyotuamrisha ndani ya
Quran tukufu akisema:
Na saidianeni katika wema na
uchamungu. Wala msisaidiane katika
dhambi na uadui. Na mcheni
Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi
Mungu ni mkali wa kuadhibu (5:2).
Katika hadith, Mtume anasema:
Kwa hakika Allah ameandika thawabu za kutenda ihsani katika kila kitu.

Ikiwa suala la kutendewa wema na


ihsani linapaswa kutendewa watu
wote bila kubaguwa, ni muhimu zaidi
kutendewa watu wanaohitajia, hususan watu wenye mahitaji maalum
kama ya ulemavu. Thawabu zinazopatikana kwa kuwatendea ihsani na
kuwatendea wema watu wenye mahitaji maalum, ni nyingi ukilinganisha
na pale unapowatendea wema na ihsani watu wa kawaida.
+255 718 561 149 habibmitwe@
yahoo.co.uk

TOVUTI ZA KIISLAMU

mapitio ya vitabu
Kitabu: Al Fusuul Fii Mustwalahi Hadiithi rRasuuli
Mwandishi: Haafidh Thanaau-ll-waahi
Zaahidy
Mfasiri: Sheikh Muhammad Issa
MlangowaTatu Hadith zenye kukubaliwa

1. Swahihu:Nazo zimegawika
mafungu mawili;-

-Swahihu Lidhaatihii: Ni Hadith yenye


upokezi ambayo upokezi wake umeungana
kuanzia mwanzo wake mpaka mwisho
wake kwa kunukuliwa na mwadilifu
mwenye udhibiti kamili kutoka kwa
wapokezi wa mfano wake na wala asipwekeke wala kuwa na ila.
-Swahihu Lighayrihii: Ni hadith ambayo

upokezi wake umeungana kuanzia mwanzo


wake hadi mwisho kwa kunukuliwa na
Mwadilifu ambaye udhibiti wake umekuwa
mdogo akinukuu kutoka kwa mwenye
daraja ya juu (kuliko yeye), lakini ikapatilizwa kwa njia nyingine ya upokezi iliyo sawa
na hiyo au iliyo sahihi, na wala isiwe ya
kipekee au yenye ila. Nayo si kama Swahihu
lidhaatihii kwa nguvu.

2. Al Hasan: Nayo imegawika


mafungu mawili;

- Hasanun Lidhaatihii: Ni Hadith ambayo upokezi


wake umeungana kwa kumnukuu
mwadilifu ambaye udhibiti
wake umepungua akinukuu kutoka kwa

mwenye daraja sahihi na wala asipwekeke


wala kuwa na ila. Nayo ni ya
hadhi ya chini kuliko Swahihu lighayrihii.
-Hasanun Lighayrihii: Ni Hadith ambayo mpokezi wake amedhoofishwa,si kwa
Ufaasiq wala urongo au niile ambayo upokezi wake umekatika, lakini udhaifu wake
ukaondoka kwa kupatilizwa au kuweko
ushahidi (uliosahihi).
3.AlMahfuudhu:Ni hadith ambayo
ameisimulia aliyetegemewa zaidi, tofauti
na upokezi wa anayetegemewa kwa kuzidi
au kupungua katika matini au Sanad yake.
4. Al Maruufu: Ni hadith ambayo ameisimulia mwenye kutegemewa, tofauti na alichosimuliwa aliye dhaifu.

China yalaaniwa kwa


kulazimisha Waislamu
kuuza nguruwe, pombe
Mwandishi Wetu na Mashirika ya Habari

aislamu nchini wamelaani hatua ya


Serikali ya China ya kulazimisha
ndugu zao nchini humo kuuza vitu
vya haramu kwa kisingizio cha
kupambana na Waislamu wenye siasa kali.
Amir wa Shura ya Maima mu na Mwenyekiti
wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Mussa
Kundecha amesema kwamba suala hilo ni haramu, litaendelea kubaki haramu na halikubaliki
huku akikielezea kuwa kitendo hicho ni uchokozi
na ukandamizaji wa haki za Waislamu.
Naye, Sheikh Muhammad Issa, Naibu Katibu
wa Baraza la Sunna ameita hatua hiyo ya China
kuwa inalenga kudhoofisha Uislamu, lakini haitafanikiwa.
Kwa mujibu wa kituo cha habari cha Interna-

tional Business Times, maduka na migawaha ya


Waislamu nchini China iliamriwa kuuza pombe
na sigara ili kudhoofisha nguvu za Waislamu wengi katika mji wa Xinjiang.
Nacho kituo cha habari cha Radio Free Asia
kimesema, wauzaji watakaokiuka amri hiyo
watafungiwa maduka yao na kushtakiwa.
Kituo hicho kimeripoti kuwa, hali hiyo ni mfululizo wa kampeni za kupinga dini ya Kiislamu
inayoenedeshwa na utawala wa China kwa kisingizio cha kupambana na imani kali za kidini.
Hata hivyo, lengo halisi la Serikali ya China ni
kudhoofisha ushawishi wa Kiislamu kasikazini
magharibi mwa China.
Mamlaka za nchini humo katika mji wa
Laskuy umetoa tangazo kwa wakazi wa kijiji cha
Aktash kuwa: Migahawa na masoko katika kijiji
chetu lazima yaweke nembo mbali mbali za
pombe na sigara katika maduka yao. Wenye

maduka pia wanaamriwa kutangaza bidhaa hizo


katika maonesho.
Mamlaka za nchini humo zimeonya kuwa:
Mtu yeyote atakaepuuza tangazo hilo na
kushindwa kutii agizo, maduka yao yatafungwa,
biashara zao zitasimamishwa na hatua za kisheria
zitachukuliwa dhidi yao.
Tangazo hilo linasema kuwa, amri hiyo imetoka katika ngazi za juu za Chama cha Kikomunist
kinachotawala nchini humo.
Kwa mujibu wa gazeti la The Washington Post
la nchini Marekani linasema kuwa, maofisa wa
Serikali na watoto katika jimbo hilo la Xinjiang
lenye idadi kubwa ya Waislamu wamezuiliwa
kuhudhuria misikitini au kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani, amri ambayo ilianza June
mwaka jana, huku katika maeneo mengine nchini
humo, wanawake wakizuiliwa kuvaa nikabu na
wanaume kutokufuga ndevu ndefu.

Na Khalid Omary

ila sifa njema anastahiki Mwenyezi


Mungu Muumba wa kila kitu, na Rehma na amani zimfikie kipenzi chetu
Mtume Muhammad pamoja na wanaofuata muongozo mpaka siku ya mwisho.
Baada ya kuiangazia tovuti ya Tanzil.net
naamini msomaji wa safu hii utakuwa umeipitia,
unaitumia na kuendelea kuelimika.
Leo tunaangazia tovuti nyingine yenye mafunzo ya dini, iitwayo Alifta.com.
Tovuti ya Alifta ni tovuti iliyopo huko-Saudi
Arabia na imejikita kwenye Fat-wa za masheikh
mbalimbali wa jopo maalum la masheikh watano
linalojulikana kama Wanachama wa Kamati ya
Kudumu ya Wanazuoni ya IFTA. Katika tovuti hii
unaweza kupata fat-wa mbalimbali, lakini wao
wamekwenda mbali zaidi kwa kuweka fat-wa kwa
kila mwezi husika. Kwa mfano, katika mwezi huu
wa Rajab kuna fat-wa zote za mambo yanayohusu
dini katika mwezi husika. Kwa mfano utapata kujua, swaumu katika mwezi huu imezungumzwa
vipi kwa mujibu wa Quran na Sunna, kadhalika
masuala ya umra na mengineyo. Vilevile utapata
kujifunza vitu vingi na dini yetu kwa ujumla kupitia vipengele vya mada tofauti tofauti,kama vile
uchambuzi wa kina na kitaalamu wa kila moja katika nguzo tano za Uislamu.
Kupitia tovuti hii ya Alifta.com, utaweza kupata
khutba za Sheikh Abdul Aziz Ibn Abdullah Ibn
Muhammad al Shaykh pamoja na Fat-wa zote za
Sheikh Ibn Baz, bila kusahau historia na maisha
ya masheikh wanaochangia na kufanya kazi ya kuuelimisha umma wa Kiislamu kupitia mtandao
huu. Kupitia mtandao huu, unaweza kupekua,
kutafuta na kusoma mada zote kwa lugha zaidi ya
nane tofauti, ikiwemo Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa, Kichina, Kihispania, Kiurdu, Kituruki,
Ki-indonesia na Kifarsi.
Wasimamizi wa mtandao huu hawakuwasahau wale wenye matatizo ya macho, kwani unaweza kubadilisha rangi ya nyuma ya muonekano wa
mtandao background kwa rangi ambayo
itaendana na uwezo wa macho yako ili isiweze
kukuumiza hata kama umekaa nayo kwa muda
mrefu.
Kwa ushahidi wa hayo unaweza ukatembelea
kupitia www.alifta.com
0683 110 006

21 Rajab 1436, jumatatu Mei 11 - 17, 2015

16

www.islamicftz.org

makala ya dini

atika toleo lililopita tulizungumzia kwa ufupi, maana


ya Israa na Miiraji, aya zilizoizungumzia safari hiyo,
siku, mwezi na mwaka iliyotokea msafara huu. Tukio lililomtokea Mtume
kabla ya safari, na tukahitimisha na
aina ya usafiri uliyotumika katika safari
hiyo.
Ndugu msomaji, andamana nami
katika makala hii ili ubaini pamoja
nami kuwa, aya za Quran na hadith sahihi zinazoisimulia safari hii ya Israa na
Miiraj, zinabainisha kuwa; Safari mbili
hizi zilifanyika kwa mwili na roho, na
Mtume akiwa hadhiri, kwa ushahidi
ufuatao:
Mosi: Allah ameanza kulisimulia
tukio hili la msafara wa Israa na Miiraj
kwa tas-bih (Sub-hana): Utakasifu ni
wa Allah Na kwa kawaida
Waarabu na Waislamu wanapolistaajabu jambo au tukio lisilo la kawaida
katika maisha yao ya kila siku, husema
Subhana Llah, kama ishara ya
mshangao kwa jambo lililoduwaza
kwa kukhalifu kawaida.
Pili: Surat Al-israa ilipoanza kwa
tasbih Utakasifu ni wa Allah aliyempeleka mja wake, bila ya shaka ilikuwa
inatoa taswira fulani kwa Waislamu
kuwa: Punde kuna jambo la ajabu
litafuata na kuwashangaza wengi, na
jambo lenyewe, ni safari ya Israa na Miiraj iliyouhusisha mwili na roho ya
Mtume Muhammad (Rehma na amani ya Allah iwe juu yake).
Tatu: Kitenzi kilichotumika kwenye
aya ni Asraa. Kitenzi hiki hakitumiki
kwa mtu aliye usingizini/aliyelala na
kilugha humaanisha safari iliyofanywa
na mtu nyakati za usiku ikijumuisha
mwili na roho sambamba na kumjumuisha anayepeleka na anayepelekwa.
Nne: Aya inaonesha Mtume (Rehma na amani ya Allah iwe juu yake)
hakwenda mwenyewe katika safari hii
ya ajabu, bali alipelekwa na aliyempeleka ni Allah mwenyewe.
Allah anasema: Utakasifu ni wa
Allah aliyempeleka mja wake. Kupeleka kunafahamika. Namna alivyompeleka zaidi ya tulivyoelezwa hatujui.
Kuhoji jinsi alivyompeleka ni uzushi na

NA SHEIKH SHABANI MUSSA

Safari ya Israa na Miiraji haikuwa ndoto

kuamini kuwa alipelekwa na Allah ni


wajibu.
Tano: Neno Mja wake popote
linapotumika huwakilisha kiwiliwili
sambamba na roho, na wala halitumiki
kwa kuiwakilisha roho pasi na kiwiliwili. Na lau Mtume angekwenda kiroho, Allah angesema: Asraa biruuhi
abdihi. Lakini fasaha ya Quran haineni hivyo. Tanabbahi !
Sita: Tumeelezwa katika hadith
kadhaa zilizo sahihi kwamba (Rehma
na amani ya Allah iwe juu yake) alisafiri
kwa mnyama wa peponi (Buraq) aliye
na kimo cha kati ya punda na nyumbu.
Wala hakuna hata sehemu moja katika
hadithi panaposema kwamba Mtume
(Rehma na amani ya Allah iwe juu
yake) aliota amempanda Buraq wakati
anakwenda Masjidul-aqswa!. Hali
inayothibitisha alikwenda kwa mwili
na roho.
Saba: Lau Safari ya Israa na Miiraji
ingefanyika kindoto hakungekuwa na
sababu ya kuita safari hizo muujiza na
hata washirikina wasingekuwa na
sababu ya kumpinga Mtume (Rehma

na amani ya Allah iwe juu yake) kwani


kupitia ndoto mtu huweza kuona au
kufanya vitu vingi vya ajabu.
Lakini kilichosababisha mshangao,
ubishani na hata baadhi ya Waislamu
dhaifu wa imani kurtadi ni baada ya
kuambiwaMtume (Rehma na amani
ya Allah iwe juu yake) aliifanya safari
hiyo kwa mwili na roho na si ndoto,
tena ndani ya muda mchache wa usiku
na kuona kwa jicho yale aliyoyaona.
Allah anasema: Jicho halikupepesa
wala halikuruka mpaka (uliowekewa).
Jicho ni sehemu ya kiungo cha mwili
na si roho. Imam Ibnu Qayyim anaeleza: Jicho la Mtume halikuangalia kulia
wala kushoto wala zaidi ya lilipopangiwa. Hii ni kuthibitisha jinsi Mtume alivyoiva na kukomaa kimaadili.
Na neno lake: Tulimpeleka hivyo
ili tumuoneshe baadhi ya alama zetu.
Na neno lake: Kwa yakini aliona
mambo makubwa katika alama za
Mola wake. (Rejea: Annaj-mu: 17-18).
Nane: Kutajwa kutopepesa jicho,
kupelekwa na kuoneshwa alama za Allah ni ishara kuwa Mtume alikuwa ha-

dhiri kwa mwili na roho wakati wa


tukio na si ndoto. Tisa: Hadith kadhaa
sahihi zinaeleza kwamba Mtume (Rehma na amani ya Allah iwe juu yake)
alipofika kwenye Masjidul- aq-swaa aliwaswalisha Mitume, na alikunywa
maziwa, huu nao ni uthibitisho
mwingine wa kihadith kufanyika kwa
safari hii kwa mwili sanjari na roho.
Hatuoni hata sehemu moja inayoeleza kwamba Mtume (Rehma na amani ya Allah iwe juu yake) aliota anawaswalisha Mitume wenzake kwenye
Masjidul- aqswa na kunywa maziwa !.
Kumi: Hadith zote sahihi za Mtume
(Rehma na amani ya Allah iwe juu
yake) zinathibitisha kwamba Mtume
alisafiri kutokea Makka mpaka Masjidul aqswa kwa Buraq, hatujaona hata
sehemu moja inayosema Mtume (Rehma na amani ya Allah iwe juu yake),
aliota amepanda Buraq. Na kifasihi
kiwiliwili na roho ndicho kinachopanda mnyama na si roho pasi na kiwiliwili.
Kumi na moja: Ama dai la wanaosema, safari ya Israa na Miiraj ilifan-

yika usingizini na kutoa ushahidi wa


neno la Allah: Na hatukuyafanya
maono yale tuliokuonesha ila ni kuwajaribu watu. (Al-israa: 60). Na kudai
kwamba; kilugha Ru-uyaa hufanyika
usingizini pekee, dai hili si sahihi na
halina mashiko ya moja kwa moja.
Neno Ru-uyaa katika lugha ya Kiarabu huja baadhi ya nyakati likimaanisha maono ayaonayo mtu awapo usingizini, au ayaonayo awapo hadhiri, na
wakati mwingine humaanisha kile
akionacho mtu kwa njia ya wahyi/
ufunuo, hivyo kuingangania maana
moja peke yake na kuziacha nyingine
kunahitaji dalili na dalili hapa haipo.
Ama neno Ru-uyaa kwa maana ya
maono anayoyaona mtu awapo hadhiri ni kama tukio hili lililomtokea
Mtume katika usiku wa Israa na Miiraj.
Imepokewa na Imam Bukhari (Allah
amrehemu) kutoka kwa Swahaba Ibnu
Abbas (Allah amridhie), wakati analifasiri neno la Allah:
Na hatukuyafanya maono yale tuliyokuonesha ila kuwajaribu watu
(wataamini au hawataamini). [Al-israa: 60]. Kisha akasema: Huko ni
kuona kwa jicho alikooneshwa Mtume
(Rehma na amani ziwe juu yake), usiku
aliopelekwa mpaka Beytul-maqdis.
(Fat-hul baar: 8/218 na Zadul-masiyr
fiy Ilmit tafsiir: 5/35 na Sunanut Tirmidhiy 5/302).
Na Imam Bukhari ananukuu tena
kutoka kwa swahaba Ibnu Abbas (Allah amridhie) akisema: Huko ni kuona kwa jicho, na yawezekana hekima
ya huko kuona kuitwa Ru-uyaa ni kwa
sababu mambo ya ghaibu kimaono
hutofautiana na maono ya asili, na ndio
maana yakalinganishwa na yale yaonwayo usingizini. (Rejea Fat-hul baariy
19/448 Mlango: Awwalu maa budia
bihi rasulullah).
Endelea kuandamana nami katika
toleo lijalo ili upate faida insha Allah.

mila na desturi
HAFSWA MADIWA

Kwa nini vijana hawataki kuoa au kuolewa

azeti la Imaan limepata


fursa ya kuhojiana na baadhi ya wasichana waliomaliza vyuo mbalimbali
walioolewa na ambao hawajabahatika kupata nusra jijini Dar es Salaam
kuhusiana mtazamo wao juu ya ndoa.
Kuhusu ndoa, Quran inatuambia:
Na katika ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi
zenu ili mpate utulivu kwao. Naye
amejaalia mapenzi na huruma baina
yenu. Hakika katika haya bila ya shaka
zipo ishara kwa watu wanaofikiri.
(30:21)
Aidha, kwa mujibu wa Mtume
Muhammad (Rehma na amani ziwe
juu yake) ndoa ni katika sunna zake
na yoyote asiyetekeleza sunna zake
hana shirika naye (Sunan Ibn Majah).
Katika mjadala juu ya kwa nini vijana wengi wanachelewa kuoa, Ashura Almasi amesema, moja wapo ya
sababu zinazopelekea hali hiyo ni

mmomonyoko wa maadili.
Mmomonyoko wa maadili unaanzia katika ngazi ya familia. Watoto hawapelekwi madrasa kujifunza elimu
ya dini na badala yake mtoto anapelekwa shule za kikristo. Matokeo yake
anakua katika maadili ya kutokumjua
Allah Taala. Mtoto anayekulia mazingira ya kutokumjua Allah hatoona
umuhimu wa kuoa au kuolewa, badala yake ataendekeza uzinifu. Aidha
Ashura aliongeza kwamba, vijana
wengi hawana hofu ya Mwnyezi
Mungu na hii inapelekea wao kuwa
mbali na mafundisho ya Mtume wetu
Muhammad (Rehma na amani ziwe
juu yake). Katika Qur-an tunafahamishwa kuwa: Hakika waumini ni
wale ambao anapotajwa Mwenyezi
Mungu nyoyo zao hujaa khofu, na wanapo somewa aya zake huwazidisha
imani, na wakamtegemea Mola wao
Mlezi. (8:2)
Kama vijana tungekuwa na imani

ya kweli tungekuwa na hofu ya Allah


na tungeacha zinaa.
Katika mahojiano na mhitimu
mwingine wa chuo, Subira lymo alisema kuwa, sababu nyingine inayopelekea vijana wa Kiislamu
kuchelewa kuoa au kuolewa ni athari
za utandawazi.
Utandawazi unaenda sambamba
na kuenea kwa tabia za kimagharibi
ambazo nyingi zinakinzana na Uislamu. Vijana wa Kiislamu wanaiga
tabia na mitazamo hiyo bila kuzingatia kuwa zinaenda kinyume na mafundisho ya Allah. Vyombo vinavyochochea utandawazi ni pamoja na
mitandao ya kijamii na teknolojia nyingine za kisasa za mawasiliano.
Naye mhitimu mwingine wa chuo
Neema Husein, akizungumzia upande wa wanawake, amesema wasichana wengi wanaogopa ndoa, hususan za wake wengi, wanapoangalia
wenzao waliotangulia kuolewa wana-

vyoishi katika maisha yao hayo ya


ndoa.
Neema Husein amesema baadhi
ya wanaume wamekosa uadilifu wanapooa wake zaidi ya mmoja.
Quran imeruhusu mwanamme
mwenye uwezo aowe mke zaidi ya
mmoja kwa sababu tofauti tofauti, lakini wanawake wengi waliopo kwenye
ndoa zenye mke zaidi ya mmoja
wamepitia karaha na tabu nyingi sio
kwa sababu Allah alikosea, bali kwa
sababu wanaume wamekosa uadilfu,
alisema Neema.
Lakini kwa upande mwingine, vijana wa kiume nao wamelalamika
kuwa wasichana wengi wa siku hizi
wana tamaa ya mali na hivyo basi hupenda kuolewa na wanaume wenye
pesa, huku kigezo cha dini kikitupiliwa mbali. Ikitokea kijana hana mali
hawezi kumpata msichana aliyependa
kumuoa.
AbdulQadir Oumar, mmoja kati

ya vijana ambaye hajaoa, mkazi wa


Magomeni Makuti anasema: Wakati
fulani unataka kuoa, lakini msichana
anaweza kukupenda na akawa hata
tayari kuzini na wewe, lakini sio
kuolewa nawe kwa sababu umaskini
wako. AbdulQadir anasema, kutokana na tamaa za wasichana, vijana
wengi huamua kutafuta kwanza maisha kabla ya kuingia katika ndoa.
Kwa mujibu wa AbdulQadiri tamaa za wasichana mara nyingi zimepelekea usaliti katika ndoa. Tunaona
haya kwa wenzetu waliotangulia na
ndio maana nasi tu waoga.
AbdulQadir na wengine waliochangia mada walishauri kuwa vijana
warudi katika misingi ya dini na waoe
mapema ili kujiepusha na maasi ya zinaa na kupata radhi za Allah ambaye
anasema katika Quran Tukufu: Wala
msikaribie uzinzi. Hakika huo ni
uchafu na njia mbaya (17:32).
Aidha wameshauri vijana na wana
ndoa kwa ujumla wazingatie misingi
ya ndoa ambayo kubwa zaidi ni hofu
kwa Mungu, upendo, kuvumiliana,
ukarimu, kuheshimiana na kuyafumbia macho matatizo madogo madogo
ambayo yanatokea kwa mmoja wa
wanandoa.

21 Rajab 1436, jumatatu Mei 11 - 17, 2015

makala ya kimataifa

www.islamicftz.org

17

Mataifa ya
Magharibi
yanavyosaidia
dhulma
Palestina
Na Yusufu Ahmadi

oja ya migogoro
mikubwa inayotikisa na kuugawa
ulimwengu kwa
kipindi kirefu ni ule wa Israel na
Palestina. Ajenda ya mgogoro
huu imejitokeza mara nyingi
katika vikao vya Umoja wa
Mataifa (UN) tangu ulipoundwa mwaka 1945.
Licha ya vikao vilivyolenga
kuushughulikia mgogoro huo,
hali imebaki kama ilivyo, huku
wakazi wa Palestina wakiendelea kuteseka chini ya utawala wa
kimabavu wa Kizayuni.
Pamoja na mgogoro huo
kuangazwa zaidi mara baada ya
kuundwa kwa taifa la Israel
hapo mwaka 1948, sintofahamu ya eneo hili ilianza tangu
mwaka 1917 mara baada ya azimio la Balfour lililotangaza
msimamo wa Uingereza wa kuunga mkono uanzishawaji wa
taifa la Israel katika ardhi ya Palestina.
Azimio hilo lilitolewa kupitia
barua ya Waziri Mkuu wa
wakati huo, kwenda kwa kiongozi wa jamii ya Wayahaudi,
Baron Rothschild.
Katika miaka ya 1920s
wenyeji walishaanzisha upinzani dhidi ya ujio wa Wayahudi
nchini Palestina, huku Israeli
nayo ikiunda vikundi vya siri vya
kigaidi, vikiwemo Haganah na
Irgan ili kukabiliana na wenyeji.

Kuundwa kwa Israel


1948
Wakati Umoja wa mataifa
(United Nations) unaundwa
hapo Oktoba 24, 1945, Palestina ilikuwa miliki ya taifa la
Uingereza. Umoja wa Mataifa
wa wakati huo ukiitwa League
of Nations, ulioundwa January
10, 1920 na kudumu kwa miaka
26 ndio ulioipatia Uingereza
mamlaka ya kuitawala Palestina
mwaka 1922.
Kabla ya azimio lao la Balfour, Waingereza walipendekeza taifa hilo lianzishwe nchini
Uganda, jambo ambalo lilipingwa na Wayahudi, walioitaka
ardhi ya Palestina tu.
Moja ya sababu zilizoifanya
Uingereza kubadili uamuzi na
kuruhusu Wayahudi kujenga
makazi yao Palestina badala ya
Uganda ni woga wa baadhi ya
wanasiasa wa kukosa uungwaji

mkono toka kwa Waingereza


wenye asili ya Kiyahudi.
Pili, Uingereza ilikubali
ombi la Wayahudi kwa sababu
ya ushawishi wa Chaim Azriel
Weizmann, mkemia aliyemiliki
kampuni ya Weizmann Institute of Science ya kutengeneza
kemikali za acetoni ambazo
Uingereza ilizihitaji katika
mambo ya silaha.
Sababu ya tatu, ni uhusiano
wa dini ya Kikristo na ile ya Kiyahudi, ambapo inaaminiwa
kurejea kwa Wayahudi katika
ardhi ya Palestina walipokuwepo karne kadhaa nyuma, kunasafisha njia ya kurejea kwa
mkombozi wa Wakristo, Yesu
ambaye Waislamu wanamtambua kama Issa bin Maryam.
Hata hivyo, azimio la
Waingereza la Balfour liliitaka
Israel kuzingatia haki zote za
wenyeji bila kwabughudhi. Sehemu ya tamko inasema ...na
ifahamike kuwa pasiwepo na
unyanyasaji wowote wa haki za
kiraia na kidini kwa Waarabu
wa Palestina. Kiyume na matarajio ya Uingereza, ghasia zilizuka mara kadhaa.
Mwaka 1947, Serikali ya
Uingereza ililipeleka suala la
Palestina katika Umoja wa
Mataifa (UN) kulitafutia ufumbuzi na kupelekea kuundwa
kwa kamati maalum ya wajumbe 11 walioenda Palestina
kuchunguza tatizo.
Wakati Wayahudi walishirikiana na kamati hiyo, uongozi
wa Palestina waligoma kushiriki
baada ya kubaini kamati hiyo ilielekea kuipendelea Israel.
Kamati ilimaliza kazi yake
Agosti 1947, ambapo katika azimio namba 181(II) ilipendekeza kugawanywa kwa Palestina
na kuunda mataifa mawili, Palestina na Israeli, huku mji wa
Jerusalem ukipewa hadhi maalum na kusalia chini ya uangalizi
wa Umoja wa Mataifa.
Katika hali ya sintofahamu,
May 14, 1948, Uingereza ilijiondoa kama msimamizi wa Palestina na kuondoa majeshi yake.
Siku hiyo hiyo Wayahudi wakatangaza rasmi kuundwa kwa
taifa la Israeli.

Kuzuka kwa Vita


Waarabu hawakuridhika na
kuundwa kwa taifa la Israel na
kupelekea kuzuka kwa
mgogoro. Mwaka 1948 vita ya

Moja ya
sababu
zilizoifanya
Uingereza
kubadili
uamuzi na
kuruhusu
Wayahudi
kujenga
makazi yao
Palestina
badala ya
Uganda ni
woga wa
baadhi ya
wanasiasa
wa kukosa
uungwaji
mkono
toka kwa
Waingereza
wenye asili
ya Kiyahudi.

kwanza baina ya Waarabu wakiiunga mkono Palestina dhidi ya


Israel ikazuka na kudumu hadi
1949, ambapo Umoja wa Mataifa uliingilia kati na kufanikisha
kusainiwa kwa makubaliano ya
kusitisha vita.
Hata hivyo, kutokaa na vita
hiyo, Wapalestina 750,000 waliondolewa katika ardhi yao na
kuwa wakimbizi.
Vita nyingine vilipiganwa
1967 na 1973 huku Israeli ikiendelea kupora ardhi ya Warabu.
Katika vita ya 1967 Israeli ilinyakua maeneo ya Sinai, Ukanda
wa Gaza, Ukingo wa Magharibi
ikiwemo mashariki ya Jerusalemu na miinuko ya Golani iliopo
nchini Syria.
Ukiacha vita hivyo, Wapalestina wameendelea kupinga ukaliaji wa ardhi yao kwa mabavu.
Harakati hizo zinajulikana kama
intifada neno la kiarabu lenye
maana ya mtikisiko.
Katika Intifada ya kwanza
mwaka 1987 hadi 1993, Wapalestina wa nyanja zote, vijana, wafanya biashara, wafanyakazi,
wanawake na watoto, waliandamana, waligoma kulipa kodi na
kususia shughuli za kiuchumi
kupinga uvamizi wa kijeshi wa
Israeli.
Katika maandamano hayo ya
amani yaliyodumu kwa miaka
sita, zaidi ya Wapalestina 1,000
waliuawa huku maelfu wakijeruhiwa na baadhi kuwekwa kizuizini.
Intifada ya kwanza ilisitishwa
mwaka 1993 kwa makubaliano
ya Oslo baina ya kiongozi wa
Chama cha Ukombozi wa Palestina (PLO) hayati Yaseer Arafat
na aliyekuwa Waziri Mkuu wa
Israeli Yitzhak Rabin, ambapo
kila mmoja alitambua uwepo wa
taifa la mwenzake.
Intifada ya pili iliyojulikana
kama Al-Aqsa iliendeshwa
mwaka 2000 kufuatia Kiongozi
wa upinzani na baadae waziri
mkuu wa Israeli, Ariel Sharon
kuzuru eneo la Haram al-Sharif
katika mji wa Jerusalem, hatua
iliyopingwa na Wapalestina kwa
maandamano.
Intifada ya pili ilidumu hadi
mwaka 2003, ambapo katika
siku tano za mwanzo Wapalestina 50 waliuawa na 1,500 walijeruhiwa.
Baraza kuu la Usalama la
Umoja wa Mataifa lililaani nguvu kubwa iliotumiwa na utawala

wa kizayuni kudhibiti maandamano katika azimio lake namba


1322 la mwaka 2000.

Kuibuka kwa Hamas


Mnamo 2005, Israeli iliondoka katika eneo la Gaza ambalo
walilikalia kwa mabavu na kisha
Januari 2006, Chama cha Hamas kilishinda viti vingi vya
bunge katika uchaguzi mkuu na
hivyo Rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas wa chama
cha Fatah alilazimika kuunda
serikali mpya ya Palestina akishirikiana na aliyekuwa kiongozi
wa Hamas Ismail Haniyeh.
Ushindi wa Hamas ulizikasirisha nchi za magharibi zilizohofia msimamo wa chama hicho
ambacho tangu miaka ya 1980
kimepinga kuitambua Israeli na
makubaliano yote yalifanywa
huko nyuma na kupendelea
mapambano ya silaha zaidi kuliko mazungumzo.
Hamas imeendelea kupambana na Israel katika eneo la
Gaza. Mwaka 2006 kulikuwa na
mapambano makali kati ya June
na Novemba baada ya Israel kuvamia Ukanda wa Gaza kufuatia
kutekwa kwa mmoja wa askari
wake.
Mapambano ya Israel na Wapalestina yamekuwa yakiendelea
huku karibu kila mwaka maelfu
ya Wapalestina wakiuawa, kujeruhiwa na makazi na mali zao
kuharibiwa.
Katika mapambano ya mwaka jana pekee takribani Wapalestina 1,777 waliuawa na wengine wengi zaidi kujeruhiwa,
ambapo Israeli ilipoteza watu
wapatao 68 tu.
Usugu wa mgogoro
Licha ya jitihada mbali mbali
za kutafuta amani, mgogoro huo
uliodumu zaidi ya nusu karne
haujapatiwa uvumbuzi. Israeli
inayoungwa mkono na mataifa
mengi ya magharibi ikiendelea
kuyakalia kimabavu maeneo
kadhaa ya ardhi ya Wapalestina
yakiwemo yale ya ukanda wa
Gaza na ukingo wa Magharibi.
Suluhisho pekee linalotajwa
ili kumaliza uhasama baina ya
mataifa hayo ni kuhakikisha kila
upande unautambua mwenzake
kama kama dola huru (Sovereign), jambo ambalo Israeli hailitaki kulisikia, na hivyo Wapalestina nao kukataa kuitambua Israeli. Mfano wa jitihada hizo za

kuwepo kwa mataifa mawili


huru, ni makubalianao ya mwaka 1995 yaliosainiwa kati ya
Waziri mkuu wa Israeli wa wakati ule, Yitzhak Rabin na kiongozi
wa Palestina, Yasser Arafat, ambapo Israeli ilikubali kuondoa
utawala wa kijeshi katika ardhi
ya Palestina na kukabidhi madaraka kwa serikali ya mpito ya
Palestina ili ianze kujitawala
yenyewe.
Jitihada hizo hazikuwafurahisha baadhi ya Wazayuni, kwani
hapo Novemba 4, mwaka 1995,
Waisraeli wenye msimamo mkali walimuua Waziri Mkuu,
Yitzhak Rabin, jijini Tel Aviv,
tukio ambalo lililaaniwa dunia
nzima.
Sio hivyo tu, hata pale baadhi
ya mabunge ya nchi za Ulaya
yanapojaribu kupiga kura ya
kuitambua Palestina kama yalivyofanya mabunge ya Ufaransa
na Bunge la Umoja wa Ulaya
mwaka jana, Israeli na mshirika
wake wa karibu Marekani zimekuwa zikipinga juhudi hizo na
hivyo kuzorotesha amani eneo
hilo.

Wajibu wa Waislam kuiunga mkono Palestina


Suala la mgogoro wa Palestina lina harufu ya ukiukwaji
mkubwa wa haki za binadamu
na ndio maana hata baadhi ya
viongozi wa nchi zisizo za Kiislamu kama hayati Rais Julius Nyerere, Nelson Mandela, ukiachia
mbali Muamar Ghadaff na Idd
Amin walipaza sauti kuupinga
utawala wa kimabavu wa Israeli.
Kwa Waislamu, popote walipo duniani, ni wajibu kwao
kuiunga mkono Palestina kwa
hali na mali, dhidi ya uonevu wa
Israeli.
Ukiachia suala la kiutu, kwa
mujibu wa mafunzo ya Uislamu,
Waislamu ni ndugu, bila kujali
mipaka ya nchi. Katika moja ya
mafundisho yake Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) anaufananisha Uislamu na mwili
ambao sehemu moja ikiugua,
mwili wote hudhoofu. Ukiacha
udugu wa Kiislamu, kuna suala
la maeneo matukufu yaliyopo
mji wa Jerusalem iliyokuwa qibla ya kwanza ya Waislamu (sehemu Waislamu waelekeayo wakati wanaswali), kabla ya Makka.
Jerusalem ni miongoni mwa miji
mitakatifu duniani ambayo
Waislamu wanaenda kuzuru.

18

21 Rajab 1436, jumatatu Mei 11 - 17, 2015

www.islamicftz.org

21 Rajab 1436, jumatatu Mei 11 - 17, 2015

watoto / tangazo

www.islamicftz.org

19

kona ya watoto
nahida esmail

MBWA

Umewahi kusikia kuhusu mbwa aliyetajwa katika Quran?

Uislam unatufundisha kuwa na huruma kwa


wanyama na kuwatendea vizuri. Kuna wanyama
wengi wametajwa katika Quran .
Swali: Unajua sura gani katika Quran inamtaja mbwa?
Jawabu: Surat Kahf (Sura ya 18) kisa cha
watu wa pangoni.
Nawe utawadhania wamacho, na hali
wamelala. Nasi tunawageuza kulia na kushoto.
Na mbwa wao amenyoosha miguu yake ya mbele
kizingitini. Kama ungeli watokea hapana shaka
ungeli geuka kuwakimbia, nawe umejaa khofu
(18:18).

Unakijua kisa cha watu wa


pangoni?

Ni kisa ambacho ndani yake Allah (Subhaanahu Wataallah) anataja waumini wazuri
ambao walijificha pangoni wakiwa na mbwa
wao.
Hapo zamani za kale, katika mji mdogo, kulikuwa na kundi la vijana, ambao walimuamini
Mwenyenzi Mungu. Hata hivyo, waliishi na watu
ambao walipotoka na waliosahau maana halisi
ya kumuabudu Mungu mmoja.
Watu hao waliopotoka, walitengeneza sanamu ya mbao na mawe na kuanza kuyaabudu.
Mfalme aliwalazimisha wale vijana wachaMungu kuabudu masanamu. Walipokataa, Mfalme
aliwaagiza walinzi wake wawaadhibu vijana
wale.
Hata hivyo Allah, kwa rehema zake aliwasaidia wale vijana waumini wakakimbia na kujificha
pangoni. Allah akawafanya walale kwa miaka
300! Mbwa pia alilala mlangoni mwa pango
pamoja nao.
Walipoamka, hawakujua walikuwa wamelala
kwa muda gani. Walidhani walilala kwa labda
siku moja au masaa kadhaa.
Walikuwa na njaa, kwa hivyo mmoja wao alienda mjini na sarafu ya fedha kununua chakula.
Hata hivyo, huyo aliyeenda mjini alikuta kila kitu
kilikuwa kimebadilika kabisa.
Akakutana na mtu ambaye alikuwa akiuza

chakula na kumpa hiyo sarafu ya fedha. Muuza


chakula hakuweza kuijua hiyo sarafu na akamchukua mtu yule mpaka kwa mfalme wake.
Mjumbe yule aliyetumwa kununua chakula
akamhadithia mfalme kuhusu kisa chake na
wenzake waliokuwa wamelala pangoni. Kisha
aliongozana na mfalme na watu wa ule mji mpaka kule pangoni wakajionee.

Tunachojifunza:

Lazima tumuabudu Mungu mmoja siku zote.


Tumtegemee Allah.
Tukimuabudu Yeye, Allah atatulipa na kutusaidia.

Ukimtii Yeye, Allah atakulinda.

Unajua kuwa kusoma Surat


Al-Kahf kila ijumaa kuna faida
kubwa?

Yeyote atakayesoma Surat Al-Kahf siku ya


Ijumaa, atakuwa na nuru itakayongara kutoka
Ijumaa hadi Ijumaa inayofuata.
Unajua kuwa Allah atatulipa kwa kuwatendea wanyama wema?
Mtume wa Allah amesema: Kuna mtu wakati anatembea alisikia kiu na akaingia kwenye kisima na kunywa maji.

Wakati akitoka, aliona mbwa akihema kwa


kupaparika huku akila tope kwa sababu ya kiu
kali. Yule mtu akasema: Huyu (mbwa) anapata
shida kama niliyoipata mimi.
Hivyo basi (akaingia kisimani) akajaza maji
kwenye kiatu, akakibeba kwa kukingata kwa
meno yake, akapanda na kumpatia mbwa yule
maji.
Allah alifurahishwa kwa matendo yake mema
na kumsamehe dhambi zake.
Watu wakauliza: Ewe Mtume wa Mungu!
Tutalipwa kwa kuwatendea wema wanyama?
Akajibu: Ndio, kuna malipo kwa kumtendea
wema kila kiumbe chenye uhai (Bukhari).

Mwanza
Arusha

Kigoma
Tabora

Moro
Dsm

Masafa ya Imaan FM
1
2
3
4
5
6

Daresalaam
Morogoro
Arusha
Mwanza
Kigoma
Tabora

104.5 Mhz
96.3 Mhz
90.8 Mhz
105.6 Mhz
92.5 Mhz
101.6 Mhz

7
8
9
10
11
12

Mbeya
Dodoma
Ruvuma
Mtwara
Zanzibar
Pemba

90.3 Mhz
102 Mhz
94.2 Mhz
90.9 Mhz
104.5 Mhz
104.5 Mhz

Mbeya
Ruvuma
Mtwara

21 Rajab 1436, jumatatu Mei 11 - 17, 2015

20

www.islamicftz.org
MGOGORO
SAUDIA NA
IRAN: SIASA
AU DINI?

Uk 10
21 Rajab 1436, jumatatu Mei 11 - 17, 2015

Katika
kuhakikisha
inafikia
lengo la
kuupeleka
mbele
Uislamu na
Waislamu,
mwaka 1993
jumuiya ya
MSAUD chini
ya kamati
ya wazee
wa Kiislamu
ilianzisha
mpango wa
masomo ya
ziada katika
Shule ya
Kiislamu ya
Ridhwaa,
Kinondoni,
Dar es
salaam.

NA YUSUPH AMIN

uala la elimu hupewa kipaumbele katika maisha ya


binadamu kwani ni ibada
na hutamalaki na kila
kipengele cha uendeshaji wa majukumu ya kilimwengu na hata yale ya
akhera.
Kumekuwa na tafsiri mbalimbali
kutoka kwa wasomi wa dini ya Kiislamu na makundi tofauti kuhusiana
na dhana nzima ya elimu.
Wapo wanaodhani kuwa elimu
ya kidunia ambayo kwa kiasi
kikubwa imetokana na fikra, utashi
na falsafa za binadamu kuwa haifai
kujifunza.
Lakini dini ya Uislamu ina mtazamo upi kuhusu elimu?
Allah subhanahu wataala anasema: Soma kwa jina la Mola wako
mlezi (96:1) na hili ndilo agizo la
kwanza kutoka kwa Allah kwa
Mtume Muhammad (Rehma na
amani ziwe juu yake).
Pia Mtume Muhammad (Rehma
na amani ziwe juu yake) ameamrisha
Waislamu, waume kwa wake kutafuta elimu.
Hii inathibitisha kuwa, kwa upande wa dini ya Kiislamu suala la
kuitafuta elimu yenye manufaa (ya
dunia na akhera) limepewa uzito
mkubwa.
Kwa kuzingatia hilo, uongozi wa
Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu
ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(MSAUD) unaendesha mpango
maalum wa kuwaandaa kitaaluma
vijana wa Kiislamu wanaofikia 800
ngazi ya sekondari kwa lengo la kutanua wigo wa ufaulu. Mpango huo
unajulikana kama Msaud Tuition
Program (MTP).
Katika kuliangazia hili, gazeti la
Imaan limefanya mahojiano na
mwenyekiti wa jumuiya ya wanafunzi hao, Ustadh Said Athuman ili kujua zaidi kuhusu harakati za jumuiya
hiyo, hususan mpango wao wa masomo ya ziada kwa wanafunzi wa
shule za sekondari.
Kwa mujibu wa Ustadh Said,
MTP ni matokeo ya ajenda muhimu
zilizopelekea kuundwa kwa jumuiya
hiyo, na hiyo ilitokana na ukweli
kwamba miongo kadhaa iliyopita
kulikuwa na idadi ndogo ya Waislamu wanaojiunga na elimu ya juu.
Ustadh Said alitaja sababu za
uchache wa vijana wa Kiislamu katika vyuo vikuu kuwa ni pamoja na vijana hao kushindwa kumudu gharama za masomo na mazingira magumu ya utafutaji elimu.
Katika kuhakikisha inafikia lengo
la kuupeleka mbele Uislamu na
Waislamu wenyewe, mwaka 1993
jumuiya ya MSAUD chini ya kamati
ya wazee wa Kiislamu ilianzisha
mpango wa masomo ya ziada katika
Shule ya Kiislamu ya Ridhwaa, Kinondoni, Dar es salaam.
Ustaadh Said alisema, jumuiya iliazimia kuwanyanyua vijana kitaaluma ndio maana masomo yote yanayotolewa na kituo hicho ni sawa na
bure, isipokuwa kiasi cha shilingi
30,000 ambacho mwanafunzi atatakiwa kulipa kwa mwaka kwa ajili

MSAUD inavyoadhimisha wajibu


wa elimu katika Uislamu nchini
ya mambo madogo madogo.
Ustadh Said amesema, katika
kuendesha masomo MSAUD imekuwa ikishirikiana na walimu wa
fani mbalimbali kutoka vyuo vya
DIT, MUHAS, SUA, IMTU na Ardhi, hatua ambayo imesaidia kupambana na changamoto ya ukosefu wa
walimu wa sayansi na silabasi
kushindwa kumalizika kwa wakati.
Ustadh Said alisema, pamoja na
kufungua vituo vya MTP vilivyopo
katika shule za Ridhwaa na Al-furqan, Tabata, Jumuiya pia huhamasisha walimu wa Kiislamu kufanya
mazoezi ya kufundisha (TP) mikoa
yenye changamoto ya walimu,
ikiwemo Pemba na Zanzibar pamoja
na mikoa ya kusini ya Lindi na Mtwara.
Akizungumzia mafanikio ya
mpango huo, Ustadh Said amesema,
kutokana na jitihada za walimu,
athari imeonekana, kwani namba ya
vijana wa Kiislamu kujiunga na
elimu ya juu inaongezeka mwaka
hadi mwaka.
Mwenyekiti huyo, pia amesema,
MSAUD inalea vijana kiimani kwa
kuwapatia elimu ya dini ili wawe
watu wema na wacha Mungu, kwani

wengi wao wanapopata elimu ya


dunia hudhani dini haina nafasi katika maisha yao.
Ustadh Said alisema, katika somo
la Quran wanafunzi hugawanywa
madaraja manne (4), ambapo daraja
la kwanza na pili huwa wanafundishwa namna ya kusoma Quran, wakati
daraja la tatu na nne hufundishwa
hukumu za Quran, yaani Ahkaami
ttaj-wiid.
Mbali na tuisheni za MTP kuwa
na mafanikio makubwa kwa umma
wa vijana wa Kiislamu, pia jumuiya
imefanikiwa kutoa viongozi mbalimbali wa kidini na kijamii katika nchi,
wakiwemo viongozi wa sasa wa Chama cha Wana Taaluma wa Kiislamu
(TAMPRO) na wale wa TAMSYA.
Pia MSAUD imeweza kutunga
mtaala wa elimu ya dini kwa walemavu wa macho na wenye matatizo
ya kutosikia. Mitaala hiyo hutumiwa
na vituo mbalimbali vya walemavu
hao vilivyopo Temeke, Yombo jijini
Dar-es-salaam.
Mwenyekiti huyo wa MSAUD
amewataka vijana wa Kiislamu kuwa
mfano wa kuigwa ili kuacha athari
kwa jamii kwa kutenda yaliyo mema
yatakayoifanya jamii kuiga mwenen-

do wao. Amesema, ikiwa watatekeleza hilo wataweza kupandikiza fikra


chanya kwa walio wengi ambao hawafikirii uwezekano wa mtu kuwa
msomi na wakati huo huo kubaki
kuwa mcha Mungu kwa kuwatumikia Waislamu na Uislamu.
Gazeti la Imaan liliwatafuta baadhi ya viongozi wa zamani wa
MSAUD kupata maoni yao kuhusu
Umoja huo na jinsi ulivyowasaidia
kukua kitaaluma na kiuongozi.
Hussein Kapuya aliyekuwa Amir
kati ya 2011-2012 ameizungumzia
MSAUD kama taasisi iliyomjenga
kiimani, lakini pia kumtimizia
malengo yake kitaaluma.
Akikumbuka enzi za uongozi
wake, Kapuya alisema, walifanikiwa
kulipia ada baadhi ya wanafunzi
wenye shida na pia kuunganisha wanafunzi wa Kiislamu na Waislamu
wa maeneo mengine ya dunia kwa
kujenga mahusiano na mataifa ya
Sudan, Kenya na India katika kufanya utafiti na kubadilishana uzoefu
katika masuala ya dini na taaluma.
Kuhusiana na program ya MTP
alisema, tofauti na awali, sasa zinaendeshwa kwa ustadi mkubwa zaidi.

Naye, Jumbe Ali ambaye naye aliwahi kuongoza Jumuiya hiyo alisema, enzi zao walitoa fursa kwa vijana
kufahamu elimu ya dini kwa uwazi
na urahisi kupitia misikiti, hususan
kwa wale waliokosa fursa ya kujifunza elimu hiyo utotoni.
Kiongozi mwingine aliyepita ambaye hakutaka kutajwa jina lake,
amesema, akilinganisha na sasa,
kipindi cha uongozi wake Waislamu
hawakuwa wenye kujiamini katika
kutetea haki zao kutokana na sababu
za kisiasa na ukosefu wa vyombo vya
kuwasilishia matatizo yao.
Aidha amefafanua kuwa MSAUD
ya wakati huo haikuwa jumuiya ya
wanafunzi tu, bali Waislamu wa nchi
nzima kutokana na kukosekana kwa
watetezi wa dini, kinyume na sasa
ambapo kuna taasisi nyingi kama
vile TAMPRO, TAMSYA na Baraza
Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu. Rai hii pia iliungwa mkono na
mwalimu Sadick Gogo, mmoja wa
viongozi waliopita wa MSAUD.
Jumuiya ya wanafunzi wa kiislamu wa chuo kikuu cha Dar-es-salaam (MSAUD) ilianzishwa miaka
ya 1960s na umaarufu wake ulidhihiri mwaka 1970.

hutolewa na kuchapishwa na The Islamic Foundation, P.O.Box 6011 Morogoro, Tanzania E-mail: imaanmedia3@gmail.com

You might also like