You are on page 1of 19

Sheikh Alhad akosoa malumbano ajali ya Makka- uk 5

huwatoa watu gizani

TIF yatumia Mil. 700 kuchimba visima Bagamoyo


ISSN 5618 - N0. 033 BEi: Sh800/- KSH80/- Ush1,200/-

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

Viongozi TIF wawaasa watanzania:

-Uk 5

www.islamicftz.org

Sheikh Ibrahim
Sheikh Chembea

Aref Nahdi

Busara itumike
kulinda amani
Ayatollah Ali
Khamenei

Marekani na Boko Haram


Uk 6

Head office, Lumumba Street, Opp: Viwanja vya Mnazi Mmoja, P. O Box 779 Dar es Salaam, Tanzania
Tell: 255 22 2182482/ 255 222184419, Fax: 255 22 2181424, E-mail: info@Binslum.com

Sheikh
Ponda
asubiriwa
kwa hamu
Uk 7

Na. MJI ALFAJR


1
DAR ES SALAAM
10:49
2
ZANZIBAR
10:49
3
TANGA
10:55
4
MOROGORO
10:57
5
MTWARA
10:46
6
ARUSHA
11:05
7
DODOMA
11:03
8
MBEYA
11:13

Na Kassim Lyimo
Morogoro

AASISI ya The Islamic


Foundation (TIF) imeziunganisha Shule ya
Sekondari ya Imaan na
Shule ya Sekondari ya Forest Hill
ili kukuza viwango vya taaluma
katika shule hizo.
Taarifa hiyo imetolewa na
Mwenyekiti wa TIF, Aref Nahdi
wakati akizungumza na wazazi
wa wanafunzi wa Shule ya Imaan
katika ukumbi wa Shule ya Forest
Hill.
Nahdi alisema kuwa uamuzi
huo umefikiwa baada ya Bodi ya
Shule ya Forest Hill kuomba uongozi wa taasisi ya TIF kuinganisha shule hiyo na Shule ya Imaan,
ambazo zote zinamilikiwa na taasisi hiyo.
Ni muda mrefu tumepokea
maombi kutoka kwa Bodi ya
Shule ya Forest Hill ya kuunganisha shule hiyo na Shule ya Imaan,
sasa leo tumewaita wazazi ili tuwaambie jambo hili ili nanyi
mtoe maoni yenu, alisema Nahdi.
Nahdi alisema kuwa watawapunguzia wazazi wa Shule ya Imaan gharama za vitu mbalimbali,
ikiwemo ada pamoja na kutoa
usafiri bure kwa wanafunzi wa
bweni.
Pia, tunampango wa kutengeneza mabweni katika shule hii
ya Forest kwani tuna eneo kubwa

habari / tangazo
DHUHUR ASR MAGHARIB
6:08
09:18 12:17
6:08
09:19 12:16
6:12
09:24 12:19
6:17
09:25 12:27
6:09
09:13 12:21
6:21
09:35 12:27
6:21
09:32 12:29
6:33
09:40 12:43

ISHA
1:23
1:23
1:26
1:34
1:28
1:33
1:36
1:50

Na. MJI ALFAJR


9
KIGOMA
11:28
10
MWANZA
11:18
11
KAGERA
11:25
12
TABORA
11:16
13
SHINYANGA
11:17
14
SINGIDA
11:09
15
IRINGA
11:04

DHUHUR ASR MAGHARIB


6:45
09:57 12:52
6:34
09:48 12:39
6:43
09:55 12:49
6:34
09:45 12:41
6:33
09:46 12:39
6:27
09:38 12:35
6:25
09:32 12:35

Oktoba 19 -25, 2015

Shule za sekondari Forest


Hill, Imaan kuungana
Shule za
sekondari za
Forest
(pichani juu)
na Imaan
zilizopo mjini
Morogoro.

ambalo litasaidia kujengwa kwa


m a b w e n i h ay o , A l i s e m a
Mwenyekiti huyo. Nae, Gavana
wa Shule ya Imaan, Khamis AlJabr, amewataka wazazi kushiri-

kiana na walimu katika kusima


mia maadili, kutokana na muungano wa shule hizo, ili kuimarisha maadili ya Kiislamu katika
shule hizo Hali kadhalika, wazazi

ISHA
1:59
1:45
1:56
1:48
1:46
1:41
1:43

wa Shule ya Imaan wamepongeza hatua hiyo na kuongeza kuwa


itasaidia kuboresha viwango vya
ufaulu kwa wanafunzi wa shule
hizo.

TIF yafadhili
yatima masomo
Afrika ya Kusini
Selemani Magali

aasisi ya The Islamic Foundation (TIF) imempeleka mwanafunzi Juma Kapilimbi katika chuo cha kuhifadhisha
Quran kiitwacho Tarteel Quran kilichopo katika mji wa Azadvil mjini Johansburg ikiwa ni jitihada za kumuwezesha kijana huyo kuhifadhi kitabu
kitukufu cha Allah. Akizungumza na
gazeti Imaan, Katibu Mkuu wa taasisi
hiyo, Sheikh Ally Ajirani alisema kijana
huyo ni mwanafunzi ambaye alikuwa
akilelewa katika kituo cha yatima kinachofahamika kwa jina la Darul Imaan
kilichopo Kola hili Mjini Morogoro .
Sheikh Ajirani ameongeza kuwa kijana huyo atakuwa masomoni katika
kipindi cha miaka miwili ambapo baada
ya hapo anatarajiwa kurudi nchini ili
kuendelea na masomo yake ya elimu ya
mazingira katika shule ya Forest Hill
ambayo pia inamilikiwa na TIF.
Katika hatua nyingine, Sheikh Ajirani amebainisha kuwa licha ya kituo cha
Darul Imaan, pia taasisi ya The Islamic
Foundation inamiliki vituo vingine viwili ambavyo vimejikita katika kuwalea
watoto yatima hapa nchini.

Uboreshaji wa matangazo ya TV Imaan

Kuanzia tarehe 10, Agost, 2015 kwa watumiaji wa receiver, TV Imaan itahama kutoka MPEG2 na kuwa MPEG4 (HD)
Masafa ya Satellite
Satellite: IntelSat 906 Frequency: 4066.25 Symbol rate: 1613.475 FEC: 2/3 DVBS2
Vile vile unaweza kuangalia TV Imaan kwa njia ya mtandao (online) kupitia
http:// www.ustream.tv/channel/radio-imaan-fm-2

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

www.islamicftz.org

makala

Kwa nini jamii imewasahau maustaadh?


Mussa imani sheha ,
Zanzibar

ila binadamu ana


mchango katika jamii
na hakuna awezae
kuishi bila ya msaada
wa wengine. Tajiri humuhitaji
maskini, mkulima humuhitaji
mchuuzi, mfanya biashara nae
huhitaji mazao ya mkulima.
Abiria anahitaji chombo cha dereva, na dereva hana kazi bila
abiria. Mgonjwa na daktari,
mwanafunzi na mwalimu; wote
hawa hutegemeana.
Yaani mshonano huu wa ajabu unaonesha kila mtu ni mtumishi wa mwingine na watu
hutegemeana ndio maisha
yakawa. Quran inasema: Ni
wake yeye (Allah) ufalme wa
mbingu na ardhi na wala hakujifanyia mtoto na wala hana
mshirika katika ufalme wake na
ameumba kila kitu na kukiwekea
vipimo vizuri (25:2)
Kwa hivyo, ni vyema kwa kila
mtu kumheshimu, kumjali na
kumtumia mwingine kwa nafasi
yake. Uislamu unasisitiza kumtunza na kumtumia kila mtu katika jamii kwa vile alivyo na kwa
nafasi yake ili atoe mchango
wake (nguvu, elimu, ufundi,
fikra, ushauri, mali n.k.) alimradi
maishayarahisikenayawezekane
ili kutimiza lengo la kuumbwa
mwanadamu.

Maustaadh katika jamii

Mingoni mwa watu muhimu


katika jamii ni wale tunaowaita
ma ustaadh. Ingawa maana
halisi ya neno ustaadh kwa lugha
ya kiarabu ni mhadhiri wa Chuo
Kikuu chochote kile kiwe cha Kiislamu au cha maarifa ya dunia,
hapa Tanzania neno ustaadh lina
maana nyingi, pana na zinazotofautiana. Katika jamii ya kitanzania, ustaadh ni yule afundishae
dini, Quran, kiarabu na masomo
mengine katika madrasa,
msikitini au shule za Kiislamu,
Mwalimu wa shule za kawaida ni
nadra kuitwa ustaadh. Pia, mhadhiri wa dini ya Kiislamu iwe
kwa sura ya mijadala au nyinginezo nae huitwa ustaadh.
Wakati mwingine Watanzania wametanua zaidi maana ya
neno hilo kwa kumuita ustaadh
hata mvaa kofia au kilemba,
anayefuga ndevu au anayevaa
kanzu fupi. Pia neno ustaadh
limenasibishwa na mtu mstaarabu, mkarimu, maridadi, mpole,
apendae kusamehe anapokosewa, mwenye kuijali dini yake
kwa kujitahidi kuyatekeleza kivitendo maagizo ya Mola wake na
ambaye hujiepusha na makatazo
yake.

Mchango wao

Maustaadh wakiwa ni sehemu ya jamii, wana umuhimu na


mchango mkubwa katika maisha ya kila siku hasa katika jamii
ambazo zina idadi kubwa ya
Waislamu. Maustaadh ni tegemeo kubwa la jamii katika kusima-

mia dini na imani. Hufundisha


watu, wakubwa na wadogo,
wake kwa waume, katika muda
wote usiku na mchana katika
misikiti, vyuo na viwanja vya mihadhara ili jamii ijue, ijali na
ishikamane na mafunzo ya dini
yao. Kwa maana nyingine, hufundisha jinsi ya kujenga uhusiano na Muumba wao ili wajue
na kufikia lengo la kuumbwa
kwao.
Watu wengi katika jamii zetu,
ikiwemo wakubwa, hawajui chochote juu ya dini. Baadhi hawajui
sio tu namna ya utekelezaji wa
majukumu yao bali hata majukumu yenyewe. Mama mmoja
alipolinganiwa kuhusu swala alisema: Kwani mwanamke nae
anapaswa kuswali? Mimi nilidhani swala ni kwa ajili ya wanaume tu!
Wengine wamefanya mengi
kumkasirisha Allah Taala katika
maisha yao kiasi hata hawawezi
kuyataja mbele za watu. Wanatafuta njia ya kutubu wao lakini
hawajui waanzie wapi. Na hapo
huwatafuta maustaadh ambao
huwapokea, huwaongoza jinsi ya
kutubia na kuwafundisha ibada
mpaka wanakuwa sawa sawa.
Maustaadh wamekuwa wakiwasaidia vijana wanaotaka kufanya mitihani ya taifa ya kidato
pili, nne na cha sita katika somo
la dini na kiarabu na vijana hao
wamekuwa wakifaulu vizuri na
kupata daraja zilizowawezesha
kujiunga na masomo ya juu!
Maustaadh wamekuwa wakiwasaidia watahiniwa hao bila kuchoka na kwa moyo mkunjufu
kwa njia zote za mawasiliano
ikiwemo simu ili wafikie lengo.
Kiuzoefu na kiutamaduni,
wazee wengi Waislamu huwapeleka watoto wao madrasa waki-

Katika
jamii ya
kitanzania,
ustaadh
ni yule
afundishae
dini, Quran,
kiarabu
na masomo
mengine
katika
madrasa,
msikitini au
shule za
Kiislamu

wa bado wadogo kupata mafunzo ya


awali muhimu kwa ajili ya kuyakabili
maisha yao hapa duniani na maustaadh
hupokea watoto na vijana hao wa Kiislamu katika madrasa zao. Baadhi ya watoto hao huwa hawajaweza hata kutunza usafi wa miili na nguo zao. Maustaadh katika asasi zao hizo huwafundisha vijana Quran ambayo ni muongozo
wa maisha kwa kuanza kuwatamkisha
herufi kwa herufi, neno kwa neno mpaka wanaweza kusoma Quran.
Maustaadh pia hufundisha vijana
misingi ya uhusiano na mola wao kama
vile swala, swaumu, dua na nyiradi,
pamoja na jinsi ya kuamiliana na viumbe wenzao kwa huruma,upendo,
ukweli, uaminifu, moyo wa kujitolea,
kuwaheshimu wakubwa, kuwafanyia
wema wazazi, ushujaa kupitia maisha
(sira) ya Mtume wao. Athari ya mafunzo
hayo huendelea hadi ukubwani.
Kwa ujumla, madrasa ni vituo
muhimu vya kuwafinyanga vijana, wakiwa wadogo ili wawe wanajamii bora.
Katika madrasa, utawaona watoto wa
familia masikini na hata za waheshimiwa viongozi na matajiri wakiamini
kwamba watoto wao wasipopitia madrasa wakanyooshwa na maustaadh,
watawasumbua sana hapo baadae. Watotowenginewanakuwawameshindikana huko majumbani.
Hebu niambie msomaji, kwa majukumu kama haya unamzingatia ustaadh kama nani katika jamii?
Vile vile maustaadh hutatua migogoro na ugomvi baina ya wanajamii,
hasa wanandoa, baada ya kuombwa na
wahusika au wazazi na mara nyingi Allah husaidia lengo kufikiwa. Jamii huwabebesha maustaadh jukumu hili zito
kwa kuamini wana busara na wenye
heshima kubwa mbele ya macho na
nyoyo za wanajamii.
Katika mkasa uliomkumba ustaadh
wangu Abuu Hussein, akiwa amelala
nyumbani kwake majira ya saa saba na
nusu, alishtuliwa na hodi mlangoni

kwake. Alipofungua, watu wawili, mke


na mume aliowajua kama jirani zake
walimkabili na kumuomba awapatanishe. Sheikh kwa busara na hekima, alituliza joto lao na kuwaomba warudi nyumbani usiku ule wakapumzike na kesho yake atakwenda nyumbani kwao
wakayazungumze.
Maustaadh hawapatanishi migogoro ya wanandoa tu, bali hata ya wanaushirika, majirani wenye ugomvi wa
viwanja, wazazi dhidi ya watoto,
masokoni na kwingineko. Utakuta watu
jasho linawatoka, matusi na ngumi
mkononi! Kisha ustaadh huitwa kusuluhisha naye huitikia mwito wa Allah
ulio katika kauli yake: Hakuna kheri
katika mengi ya mazungumzo yao ya
siri ila kwa yule aamrishae kutoa sadaka
au wema au kuwapatanisha watu
(4:114)
Maustaadh pia ni hitajio muhimu
wakati wa kufungisha ndoa (akdi) harusini. Licha ya maasi yanayofanywa
katika harusi nyingi za Waislamu, bado
jamii itamuita sheikh au ustaadh atoe
khutba, aisimamie ndoa na kutoa miongozo ya kisharia. Ndio utaona ustaadh
hupewa nafasi yake katika ufanikishaji
wa mipango ya harusi. Utasikia wanaulizana: Lakini sheikh hatujampata
jamani, Ustaadh Rama tunaye mbona? Akichelewa kidogo, wanaume huwasha prado zao kumfuata.
Umuhimu wa maustaadhi pia
huonekana wakati wa kuwasindikiza
wagonjwa saa ya kufa na katika taratibu
(hududi) za mazishi. Kifo kinatisha.
Jamaa wa mgonjwa huanza kumuogopa jamaa yao wakati wa kuaga
dunia. Utasikia wakisema: Nendeni
kamuiteni ustaadhi hapo jirani. Na
baada kufa ndio kabisa.
Maustaadhi hukunja kanzu zao kukabiliana na hali hiyo ngumu itakayomkumba kila mtu na kuosha, kukafini,
kusalia na hadi kuzika. Jamaa wa marehemu huwashukuru maustaadh kisha
huwasahau mpaka litokezee tena. Shughuli hizi ni nadra sana kuziona zikifanywa na wasomi wa fani za kisekula, vigogo au waheshimiwa. Wote hao huwategea masheikh na maustaadh ambao
hufanya bila khiana wakielewa kuwa
huo ni wajibu wa kidini na kijamii.

Mazingatio muhimu

Basi ona ndugu msomaji mchango


wa maustaadhi katika jamii kisha fikiria
wasingekuwapo maisha yangalikuwaje!
Hapa ndio tunapata ukweli wa maneno
ya Taabii (mwanafunzi wa Maswahaba)
Bwana Hassan Albaswry aliposema:
Lau si kuwepo wanazuoni (maustaadh) watu wangaliishi kama wanyama
Kwa kumalizia, ikiwa huu ndio
mchango, nafasi na kazi za maustaadh,
masheikh na walimu wa madrasa katika
jamii zetu, hatuoni mantiki ya serikali
wao kutolipwa mishahara. Ni kawaida
kukuta maustaadh wakizifanya kazi hizi
ngumu kwa mtindo wa kujitolea bila ya
kutaraji kuunyoosha mkono mwisho
wa mwezi. Maisha yao ni ya kupapatua
tu. Lakini baya zaidi ni mamlaka na
jamii kuwachukulia maustaadh kuwa
wakorofi wanaohatarisha amani katika
jamii na kuwatia misukosuko na kuwadhulumu. Inafaa tujiulize kulikoni
jamii inadharau maustaadh Maustaadh
kiasi hiki! Kweli shukrani ya punda ni
mateke.

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

www.islamicftz.org

kutoka misikitini
Uongozi ni majuto siku ya
kiyama - Sheikh Kishki
Na Mwandishi Wetu
Mlinganiaji maarufu nchini ambaye pia ni imamu wa msikiti
wa Vetenary uliopo Temeke
jijini Dar es salaam Sheikh
Nurdin Kishki amewaasa wagombea wa nafasi mbalimbali
za uongozi katika uchaguzi
mkuu wa mwaka huu kutambua dhima waliyonao endapo
watachaguliwa kuwaongoza
watu.
Sheikh Kishki ameyasema hayo wakati wa khutba
ya ibada ya swala ya
ijumaa iliyoswaliwa katika
msikiti huo wiki iliyopita
na kuongeza kuwa watu
wengi hupenda uongozi huku wakijifaharisha kwa vyeo na
kusahau kuwa uongozi
ni dhima inayoweza kupelekea majuto ya hali ya
juu mbele ya Allah Taala
siku ya kiyama.
Kama tungelijua dhima
ya mtu kiongozi ni ngumu
kiasi gani siku ya kiyama
sote tungekimbia uongozi
na madaraka kama vile
Punda anavyomkimbia
Simbaalidokeza Sheikh Kishki
huku akiwataka waislamu wazidi
kumuomba Allah kuipitisha salama siku ya uchaguzi na kuepusha
shari zinazoweza kujitokeza.
Kuhusiana na zoezi la uchaguzi
mkuu unaotarajiwa kufanyika
mwishoni mwa juma hili Sheikh
Kishki amesema hivi sasa watanzania wapo katika kipindi kigumu
kutokana na mawazo,fikra na
hamasa zao kuzielekeza katika
uchaguzi jambo linalopelekea
watu kusahau hata kutekeleza
ibada muhimu za dini.

Waislamu wahimizwa
kuamrisha familia zao
kufanya ibada
NA HASSAN NINGA
Waislamu nchini wametakiwa kuadhimisha mwaka mpya wa kiislamu kwa
kuamrisha familia zao kutekeleza mambo
ya kheri ikiwemo swala tano kama sehemu ya jitihada ya dini wakati wanapoingia
katika mwaka mpya wa 1437 Hijriya.
Nasaha hizo zimetolewa na Sheikh Issa
Othman Issa wakati wa ibada ya swala
ya ijumaa iliyoswaliwa katika msikiti wa
Maamuur uliopo Upanga jijini Dar es
salaam na kuwataka waislamu kujenga
mahusiano mema na familia na kwamba
kufanya hivyo ndio kutekeleza mafunzo
ya mtume rehema na amani ya Allah ziwe
juu yake.
Sheikh Othman alinukuliwa
akisema:Tunapoingia kwenye mwaka
mpya wa kiislamu,lazima tufahamu mahusiano yetu na watoto wetu yakoje na je,
mwaka uliopita tulipata nafasi ya kukaa
nao na kuwahimiza kufanya ibada au
tulikaa nao na kuwahimiza kufanya bidii
kwenye masomo tu.
Aidha Sheikh Othman aliwataka wazazi
kutambua kuwa,ni jukumu lao kuwahimiza watoto na familia kwa ujumla kutekeleza ibada mbalimbali na kwamba kama
waliteleza katika kuyaamrisha hayo basi
mwaka mpya wa kiislamu uwe ni fursa ya
kubadilisha mwenendo wa familia zao.

tujikumbushe

Tariq bin Ziyad


Sheikh Mohammad Issa

Choma moto majahazi. Ilikuwa ni amri kwa Waislamu kutoka kwa kamanda wa majeshi yaliyovuka bahari ya Mediterania kwa lengo la kuiteka Hispania au Andalusia kama inavyojulikana katika historia ya Uislamu.
Hatua hii ilifuatia mapambano ya miaka mingi kati ya majeshi
ya watawala wa Andalusia enzi
hizo na yale ya Waislamu kutoka
Magharibi na Kaskazini mwa Afrika. Waislamu walivuka bahari
kuiteka Andalusia ili kuzuia mashambulizi mapya dhidi yao.
Tariq bin Ziyad alikuwa amefaulu kutia nanga mahali penye
milima paitwapo Jabal Tariq
(Mlima wa Twaariq) hivi leo kwa
kumbukumbu ya jina lake. Kuficha historia hii iliyotukuka ya
Waislamu, wazungu wakapaita
Gilbrater. Huo ulikuwa mwaka
711 Miladia sawa na mwaka wa
92 Hijriya, enzi za utawala wa
bani Umayya uliotawala dola
kubwa ya Kiislamu kutokea Damascus (Dameshqi) nchini Syria.
Kilikuwa ni kipindi cha dola ya
Kiislamu kupanuka hadi China
na India.
Mara tu baada ya majahazi
yaliyowabeba Waislamu kutia
nanga, walijikuta wakikabiliwa
na jeshi kubwa la maadui zao.
Tariq bin Ziyad akaona dalili za
hofu toka kwa wapiganaji wake.
Hapo ndipo Tariq bin Ziyad alipofikia maamuzi yake ya kuchoma moto majahazi waliyotumia
kuvuka bahari na kila kilichomo
ndani yake.
Baada ya hapo, Tariq bin Ziyad
akatoa hutba kali yenye mguso
wa aina yake kwa kusema: Ndugu zangu katika imani, tuko hapa
kulieneza neno la Allah. Maadui
wako mbele yenu na bahari nyuma yenu. Na hamna chakula wala
maji ila kile mtakachokiteka
kutoka kwa maadui zenu kwa
panga zenu. Kwa hiyo hapa ni
aidha ushindi au kufa shahidi.
Allahu akbar! Hiki kilikuwa
kilele cha kumtegemea Allah na
azma ya kupigana kwa ajili yake
kilichooneshwa na Tariq bin Ziyad. Kwa wapiganaji katika jeshi
lake, kuitii amri ya kamanda wao
kuyachoma moto majahazi yenye
kila kitu chao kilikuwa kilele cha
utii.
Tariq bin Ziyad alikuwa mtu
wa kabila la Ulhasa katika waberiberi (Berbers) aliyeingia katika
Uislamu kutoka nchini Algeria.
Awali alikuwa mtumwa na aliposilimu akaachwa huru na bwana
wake. Huyu ndiye mtu aliyeiteka
Andalusia (Hispania) na kuupeleka Uislamu Ulaya.
Watu kama Tariq bin Ziyad,
waliokuwa watu duni kabla ya
Uislamu lakini wakapata hadhi

kubwa baada ya kusilimu ni wengi. Miongoni mwao ni Salman Al


-Farsi, Bilal bin Rabbah na Zayd
bin Al-Haaritha (Allah awe radhi
nao wote).
Jemadari wa majeshi ya Waislamu, Kaskazini mwa Afrika
alikuwa Musa bin Nusair, mmoja
wa majemadari mahiri wa Kiislamu. Tariq bin Ziyad alivuka bahari akiwa na wanajeshi 300
waarabu na waberiberi 10,000
waliosilimu.
Mfalme Roderic wa Andalusia aliwakabili akiwa na askari
100,000 dhidi ya Waislamu
10,300. Ni wazi lazima waliokuwa katika jeshi la Waislamu
wawe na hofu ya kuteketezwa na
jeshi kubwa lakini imani yao kwa
Allah iliwapa utulivu.
Tariq bin Ziyad akamuomba
Jemadari Musa bin Nusair
nyongeza ya wapiganaji na akamtumia wapiganaji 7,000 chini ya
kamanda Taarif bin Maalik Naqiy ambaye mji wa Tarifa nchini
Hispania leo unabeba jina lake.
Kabla Taarif na jeshi lake
hajafikia Waislamu, vita vikaanza
na Waislamu wakawakabili maadui kishujaa. Majeshi mawili, lile
la Waislamu na lile la makafiri
yakakabiliana katika vita vya
Guadalete ambapo Mfalme Roderic alishindwa na kuuawa
mwezi 28 Ramadhan mwaka 92
Hijriya.
Jeshi la Wahispania lililoshindwa likarejea nyuma
kuelekea makao makuu ya dola
mjini Toledo. Tariq bin Ziyad akaligawa jeshi lake vikosi vinne.
Kikosi kimoja kikalekea mji wa
Cordoba (Qurtuubah) na kuuteka.
Kikosi cha pili kikaelekea mji
wa Murcia na kuuteka na cha tatu
kilielekea mji wa Zaragoza. Kamanda Tariq bin Ziyad
mwenyewe alielekea Toledo,
wakazi wake wakajisalimisha
pasina kupigana ikawa mwisho
wa Mfalme Roderic.
Baada ya kupata habari za
ushindi wa Waislamu, Jemadari
Musa bin Nusair akafanya haraka kwenda kuongeza nguvu ili

maadui wasije kujikusanya akiwa


na wapiganaji 18,000. Majeshi
ya Waislamu kwa muda mfupi
yakateka theluthi mbili ya ghuba
ya Iberia.
Miji ya Zaragoza, Barcelona
na sehemu ya Ureno ikaangukia
mikononi mwa Waislamu. Mwaka uliofuata Waislamu wakavuka
mto Pyrenees na kuingia mji wa
Lyons nchini Ufaransa.
Huo ukawa mwanzo wa dola
ya Bani Umayya ya Magharibi
chini ya Khalifa Walid bin , dola
iliyotawala Hispania (Andalusia)
kwa miaka 750 tangu mwaka 711
hadi 1492 Waislamu walipotimuliwa Hispania katika vita ya
msalaba iliyoitwa, November
Crusade.
Kasi ya majeshi ya Waislamu
chini ya Tariq bin Ziyad kuteka
ardhi ya Andalusia na Waislamu
kufanikiwa kuikalia kwa miaka
750 inaingia katika historia ya
vita duniani zama za kati.

Athari ya utawala wa
Kiislamu Hispania

Kabla ya Waislamu kuingia


Hispania, watawala wake walikuwa watu kutoka nchi za
Skandnavia waitwao Visigoths.
Mnamo karne ya tano Miladiya,
hawa Visigoths waliiteka Hispania na kuweka utawala wao
mji mkuu ukiwa Toledo.
Kw a k u w a h aw a k u w a
wastaarabu wajuzi wa kutawala,
walikaribisha Kanisa la Roma
mwaka 565 kuendesha mambo
ya utawala. Kanisa likapata kibali
cha kueneza Ukristo na kukusanya kodi.
Watu wakawa katika tabu
kubwa, wakilipa kodi mara mbili
moja kwa watawala na nyingine
kwa kanisa. Kulikuwa na Wayahudi wengi Hispania, kipindi cha
watawala Waislamu Wayahudi
waklipata mateso makubwa
sana. Kwanza walinyimwa haki
ya kumiliki ardhi na pili walikatazwa kuabudu kwa dini yao ya
kiyahudi. Walipojaribu kupinga
hali hiyo, kanisa likawapa mateso
zaidi.
Mwaka 707 Mfalme Vietza al-

Chini ya Waislamu, Hispania ikawa


alama ya sayansi, utamaduni
na ustaarabu katikati ya
Ulaya iliyokuwa katika zama
zijulikanazo kama zama za giza.

ipoonesha kuwahurumia Wayahudi, viongozi wa kanisa walimpindua na kumweka madarakani Mfalme Rodriguez. Wayahudi wanaume wakatiwa
utumwani na wanawake wao kufanywa masuaria majumbani.

Utawala wa haki wa
Waislamu

Mara baada ya Waislamu


kuiteka Andalusia (Hispania),
haki ikatawala. Hakuna mali ya
wenyeji iliyotaifishwa. Waislamu
waliwatendea watu wote kwa
haki, wakiwemo Wayahudi,
isipokuwa waliweka mfumo wa
kodi wenye uadilifu ambapo waliolipa ni wenye uwezo tu.
Wakiongozwa na Quran na
Sunna ya Mtume (Rehma na
amani iwe juu yake), Waislamu
waliingiza ustaarabu wa Kiislamu Ulaya na popote majeshi ya
Waislamu yalipokwenda yalipokelewa kwa mikono miwili na
wakazi wa maeneo hayo.
Utawala wa Waislamu ukafanya Hispania kuwa nchi ya
kistaarabu iliyojaa haki, uadilifu
na elimu. Mtumwa yeyote aliyeingia katika Uislamu aliachwa
huru mara moja. Idadi kubwa ya
wahispani awakaingia katika dini
ya Uislamu. Watu wa dini mbali
mbali wakiwemo Waislamu na
Wayahudi waliruhusiwa uhuru
wa kuabudu kwa mujibu wa dini
zao. Siyo hivyo tu kila mwenye
elimu, ujuzi na maarifa aliruhusiwa kupata ajira katika kuhudumia jamii.
Vituo na vyuo vya elimu
vikafunguliwa huko Toledo na
Cordoba na yeyote aliruhusiwa
kuchukua elimu bure. Magwiji
wa elimu za hisabati, jiografia,
kemia, baiolojia na unajimu
wakazalishwa kutoka vyuo vikuu
huko Toledo na Cordoba.
Chini ya Waislamu, Hispania
ikawa alama ya sayansi, utamaduni na ustaarabu katikati ya
Ulaya iliyokuwa katika zama zijulikanazo kama zama za giza.
Mirefeji ya maji ilichimbwa, mazao mapya yakaingizwa na kuinua uchumi wa Hispania.
Miji ikakuwa na idadi ya
wakazi kuongezeka. Mji wa Cordoba ukawa kitovu cha elimu
Ulaya nzima na hadi kufikia
karne ya 10 Miladiya, mji huo
ulikuwa na wakazi wapatao Milioni moja yaani Manispaa.
Mwanahistoria mmoja
Mkristo anaandika: Waislamu
walianzisha ufalme ule wa Cordoba uliokuwa fahari ya enzi za
zama za kati, zama ambazo
wakati Ulaya nzima ilikuwa imezama katika ujinga na vurugu,
mji huo ulikuwa nuru ya elimu na
ustaarabu ikiuangazia ulimwengu wa magharibi.
Khalifa Walid bin bin Marwaan aliwaalika Jemadari Musa
bin Nusair na Tariq bin Ziyad
mjini Damascus. Lakini walipofika walimkuta akiwa mahututi.
Aliwashukuru na kuwapa sehemu ya mali waliyoileta kutoka katika mapato waliyokusanya.
Khalifa Walid alipofariki,
Suleiman bin Abdulmalik akamfuatia katika utawala. Tariq bin
Ziyad alifariki mwaka 720 Miladia. Historia ya Uislamu na ulimwengu haiwezi kamwe kumsahau Tariq bin Ziyad.

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

www.islamicftz.org

makala / tangazo

TIF yatumia Mil. 700 kuchimba visima Bagamoyo


Mkuu wa wilaya
aipongeza
Na Athumani Shomari, Bagamoyo

aasisi ya The Islamic Foundation


(TIF) ya mjini Morogoro ambayo pia
ni wamiliki wa redio, TV na
gazeti Imaan, imetumia zaidi ya milioni 700 kuchimba
visima wilayani Bagamoyo.
Hayo yalibainishwa hivi
karibuni mjini Bagamoyo
na Mkurugenzi Mtendaji wa
taasisi hiyo, Sheikh Ibrahim
Twaha wakati alipokuwa
kwenye ziara ya kutembelea
miradi inayoendeshwa na
taasisi hiyo wilayani humo.
Sheikh Ibrahim alisema
kuwa katika kipindi cha miaka minane taasisi hiyo imefanikiwa kuchimba visima
zaidi ya 170 wilayani Bagamoyo vyenye thamani ya zaidi ya milioni 700.
Aidha, alisema kuwa,
uchimbaji wa visima hivyo
katika maeneo mbalimbali
ya wilaya ya Bagamoyo umesaidia kwa kiasi kikubwa
kuondoa tatizo la maji wilayani humo.
Alizitaja baadhi ya sehemu zilizochimbwa visima
katika wilaya hiyo kuwa ni
pamoja na Dunda, Magomeni, Kingani, Kiromo,
Zinga Mlingotini na Kerege.
Aliongeza kuwa huduma
hiyo ya maji imelenga katika
maeneo yenye mchanganyiko wa watu ambayo yana
shida ya maji ambapo kwa
kuzingatia hilo visima hivyo

uchimbaji
wa visima
hivyo
katika
maeneo
mbalimbali
ya wilaya ya
Bagamoyo
umesaidia
kwa kiasi
kikubwa
kuondoa
tatizo
la maji
wilayani
humo
vimechimbwa katika maeneo ya soko, shuleni, kwenye
zahanati, misikitini na maeneo ya wazi ili kila mwananchi aweze kufaidika na
huduma hiyo.
Hata hivyo, Mkurugenzi
huyo wa TIF alisema kuwa
bado kuna maombi mengi
kutoka kwa jamii ya kuchimbiwa visima yaliyowasilishwa na wananchi wa Bagamoyo, na kwamba uchimbaji huo wa visima unaendelea wilayani humo ili kuwafikia wananchi wote wenye
shida ya maji katika maeneo
yao.
Akizungumzia umuhimu
wa maji katika jamii, Sheikh
Twaha alisema Mwenyezi

Mkurugenzi
mtendaji wa TIF
sheikh Ibrahim
Twaha akionja
maji kutoka
katika kisima
kilichochimbwa
Kwenye makazi
ya polisi
Bagamoyo.

Mungu ndani ya Qur ani iongeza kuwa serikali inathtukufu amesema amejaalia amini mchango huo na wakatika kila kitu uhai kutoka- nanchi pia wanapaswa
na na maji. Hivyo basi, TIF
kama taasisi ya kiislamu inazingatia kauli hiyo ya Allah
na kutoa umuhimu wa pekee katika huduma hiyo ya
maji. Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wa wilaya
Bagamoyo waliofaidika na
msaada wa TIF wamesema
kuwa wanaishukuru taasisi
ya TIF kwa kuwachimbia visima katika mitaa mbali
mbali ya Bagamoyo na kuwaondolea adha ya ukosefu
au uhaba wa maji.
Nae Mkuu wa Wilaya ya
Bagamoyo, Majid Hemed
Mwanga, ameipongeza Islamic Foundation kwa uchimbaji wa visima wilayani
humo na kuongeza kuwa
serikaliinathaminimchango
wa taasisi hiyo katika kutoa
huduma za kijamii kama
hiyo ya visima. Hemed al-

Sheikh Alhad akosoa


malumbano ajali ya Makka
Selemani Magali

meelezwa kuwa hakuna


muda wa kuendeleza
malumbano juu ya vifo
vya mahujaji, badala
yake Waislamu wanapaswa
kujikita katika maombi ili
Mwenyezi Mungu awalipe
pepo mahujaji wote waliofariki katika tukio la mkanyagano huko Jamaarat.
Wito huo umetolewa na
Sheikh wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Alhad Musa Salum
ambapo alisema waliofariki
katika ardhi ya Makka wakiwa katika Ibada, Allah huwahesabu ni waja wa peponi
kutokana na ardhi hiyo kubarikiwa kwa kuzikwa man-

abii na mitume.
Bila shaka wito wa Alhad
unawalenga Mashia ambao
tangu ajali ilipotokea wamekuwa wakiuandama Utawala wa Kisunni wa Ufalme wa
Saudia kwa tuhuma mbalimbali ambazo hazina msigi na
zimejaa uongo. Kufa Makka
na Madina si sawa na kufa
Manzese na Tandale, watu
wanapaswa kuomba kufa
katika ardhi ile kwa sababu
ni ardhi tukufu iliyobeba
watu maarufu hususan manabii na maswahaba, Alhad
alisema.
Aidha, akizungumzia mahujaji ambao hawajulikani
walipo, Sheikh Alhad alisema ana wasiwasi kuwa huen-

da baadhi yao ni katika waliozikwa mapema kabla hawajatambuliwa.


Ni wakati mgumu kwa
wanandugu, lakini niwaombe Waislamu kuwaombea ndugu zetu wawe
ni watu waliokufa mashahidi
na Allah awawezeshe kuwa
watu wa peponi Alisema
Sheikh Alhad.
Aidha kuhusu suala la viongozi wa dini moja kutoa
lugha za kejeli na matusi dhidi ya viongozi wa dini nyingine kutokana na tofauti ya
mitazamo ya kisiasa amesema suala hilo linapaswa
kukemewa kwa dhati kwani
litasababisha uvunjifu wa
amani.

kuthamini mchango huo


mkubwa uliotolewa na TIF na
kuongeza kuwa jukumu la ku-

vitunza visima hivyo ni la wananchi ili huduma hiyo iwe


endelevu.

Afyais natural
source of sweet
drinking water
from underground stream
which is blended
with essential
minerals to support and aid perfect metabolism.

WATERCOM LIMITED
P.o. Box 20409, Plot N.4005, Kisarawe11 area
Temeke,Daresalaam, Tanzania
www.watercomtz.com, E-mail:info@watercomtz.com

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

hutolewa na kuchapishwa

tahariri / nasaha

The Islamic Foundation,P.O.Box 6011 Morogoro, Tanzania,E-mail: imaanmedia3@gmail.com


mhariri mtendaji: 0715 559 944, Mhariri: 0786 779 669, afisa masoko: 0785 500 502
TOVUTI: www.islamicftz.org

Hijra ya Mtume itufunze uvumilivu na subra katika dini

umeingia mwaka wa 1437


tangu tukio la Mtume
(Rehma na amani ya Allah ziwe juu yake) pamoja
na maswahaba (Allah awe radhi
nae) kuhama kutoka mji wa Makka
na kuhamia Madina kwa sababu za
madhila waliokuwa wakifanyiwa
na watu wa kabila la Maqureysh.
Msingi mkuu wa tukio la Hijra
ni Waislamu kunyimwa fursa ya
uhuru wa kuabudu hali ambayo
kwa uhakika wake bado haijafutika
kabisa katika uso wa dunia. Hata
hivyo, yapo mambo ya msingi ya
kujifunza kupitia tukio la Hijra.
Miongoni mwa hayo ni Waislamu
kujipamba na sifa ya subra na uvumilivu.
Tunasema hayo kwa sababu
kabla ya Hijra (Maisha ya Mtume
alipokuwa Makka), Mtume (Reh-

ma na amani ya Allah ziwe juu


yake) aliweza kuwa na subira ndani
ya nafsi yake licha ya madhila aliyokuwa akifanyiwa kabla ya kupewa
amri ya kuhama na Mola wake
hivyo. Katika hili, kuna mazingatio
makubwa ndani yake.
Ili kujenga mustakbali mwema
wa maendeleo ya Uislamu na Waislamu, dhana ya umoja ambayo ndio
msingi mkuu wa mafanikio ya kila
jambo haiwezi kuepukika kwani
hata ukiona jamii fulani imesambaratika, sababu kubwa huwa ni
watu wake kukosa subira na uvumilivu.
Ukosefu wa subira na uvumilivu
hudhoofisha juhudi za maendeleo
ya dini na pia huchochea chuki na
uadui hivyo tutumie mafundisho ya
Hijra kujenga tabia ya kuvumiliana
na kusubiri kwani hiyo ndio sababu

umatano iliyopita ilikuwa ni siku


muhimu kwa Watanzania kwa
kuwa ni siku ambayo taifa lilikumbuka kifo cha muasisi wa taifa hili,
hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambaye pia baadhi ya watu hupenda
kumuita baba wa taifa.
Wengi wameazimisha siku hiyo kwa kukumbuka harakati ambazo Nyerere alizifanya, akishirikiana na wenzake na ambazo zilileta ukombozi kutoka katika
makucha ya wakoloni. Na pia anakumbukwa kwa misingi aliyoijenga ambayo imelihakikishia taifa la Tanzania amani ya
muda mrefu.
Ni kupitia jitihada zake, Tanzania imetambulika duniani kote kama ni kisiwa cha
amani, utulivu na upendo. Na watu wake
wanasifika mpaka leo kwa kuwa wakarimu
jambo ambalo hakika tunajivunia kwa sifa
hizo mbele ya nchi za kimataifa.
Hata hivyo, kumbukumbu ya Nyerere
pia inakumbusha jamii ya Waislamu kuhusu changamoto ilizopitia tangu kupatikana
kwa uhuru mwaka 1961. Sehemu kubwa ya
changamoto, ambazo zimeleta udhalili kwa
jamii yetu, zinahusu mahusiano yetu na
Serikali ambapo Serikali imekuwa ikidhibiti maendeleo ya Waislamu kwa kuwaundia
taasisi na kuwateulia viongozi wa kuwaongoza.
Jumatano hiyo hiyo, ilikuwa ni siku
muhimu kwa Waislamu ambao nao walisherehekea mwaka mpya wa Kiislamu wa
1437, Hijria yaani tangu Mtume Muhammad (Rehma na amani ziwe juu yake) alipohama kutoka Makka kwenda Madina.
Lilikuwa ni wazo la Swahaba Umar,
Khalifa wa Pili wa Uislamu (Mungu amuwie radhi) kuanza kuhesabu miaka hii ya
Kiislamu hususan baada ya kuona kuwa
kwa mara ya kwanza wanahamia katika mji
wa Madina ambao wataanza kutumia sharia ya Kiislamu. Kwa maana nyingine, ni
wakati ambao dola ya Kiislamu ilianza
kusimama na waumini wake walipata uhuru wa kujitegemea na hivyo kuanza kufanya
ibada zao kwa mujibu wa kitabu kitukufu
cha Uislamu.
Kuingia kwa mwaka huo mpya wa Kiislamu, kuna mambo mengi sana ya mazingatio ambayo waumini wanapaswa kuyapima na kuchukua hatua ili kuendelea kufanya vema katika kuimarisha dini ya Kiislamu
na pia kujiwekea mazingira mazuri ya kuwa
na mwisho mwema mara tutakapoiacha

ya kupata radhi na baraka za Allah


Taala.
Hii ni kwa sababu nafasi ya subira katika kufikia utukufu ni kubwa
na kwamba, pasina mtu kujipamba
kwa sifa hii muhimu na yenye thamani ni vigumu mtu huyo kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu
kama inavyobainisha Quran Tukufu: Lakini hawapewi wema huu ila
wanao subiri, wala hawapewi ila
wenye bahati kubwa (ya imani na
uchamungu) (41:35).
Tukio la Hijra ya Mtume ni nafasi muhimu katika kutayarisha
mazingira ya uvumilivu na kusubiri
hatimae kuziunganisha nyoyo za
Waislamu katika wakati mmoja na
kuelekea kwenye lengo moja kama
Allah Taala anavyobainisha ndani
ya Quran: Na shikamaneni kwa
kamba ya Mwenyezi Mungu nyote

pamoja, wala msifarikiane. Na


kumbukeni neema ya Mwenyezi
Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo
kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui
naye akaziunganisha nyoyo zenu;
kwa neema yake mkawa ndugu..
(3:103).
Moja ya masharti manne ya
kusimamisha Uislamu ni kuhusiana kufanya subira. Allah anasema
katika Quran: Naapa kwa Zama!
Hakika binaadamu bila ya shaka
yumo katika hasara, Ila wale walioamini, na wakatenda mema, na
wakausiana kwa haki, na wakahusiana kusubiri (103:1-3).
Tofauti za kimtazamo ni jambo
la asili, lakini suluhu yake ni watu
kujipamba na sifa ya subra na uvumilivu na hili litapelekea hata pindi
zitakapojitokeza tofauti basi watakaa chini na kunasihiana kama

inavyobainishwa hadithi iliyopokewa na Swahaba Tamim bin


Aus Addaariy (Allah awe radhi
nae).
Mtume (Rehma na amani ya Allah ziwe juu yake) amesema: Dini
ni nasiha. Tukauliza: Kwa nani?
Akasema kwa Allah, Kitabu chake,
na Mtume wake, na kwa viongozi
wa Waislamu na watu wa kawaida
(Muslim).
Wakati tukiadhimisha mwaka
mpya wa Kiislamu wa 1437, ni
wakati pia wa Waislamu kuamka
kutoka usingizini na kutumia fursa
hii kama mwanzo mpya wa kujiepusha na chuki na uadui na kujipamaba na sifa ya subira na uvumilivu na hayo ndio maadhimisho
yaliyo bora ya Hijra ya Mtume (Rehma na amani ya Allah ziwe juu
yake).

nasaha za wiki
Selemani Magali

Tofauti ya madhehebu zisiwe


kikwazo cha ulinganiaji
dunia. Nilipata bahati ya kuzungumza na goni mwa Waislamu bila ya sababu za
Maalim Kassim Abdalah wa Al-Madrasat msingi.
Nuur ya Kigogo Luhanga kuhusu mafunKatika hatua nyingine, Maalim Abdalzo, mazingatio na nini kifanyike ili Waisla- lah amezielezea mbinu ambazo Mtume
mu kuendelea kufanya mema katika kipin- Muhammad (Rehma na amani ziwe juu
di hiki ambacho
yake) amekuwa akizwamepewa fursa nyitumia katika kulinNi kupitia
ingine na mola wao
gania watu kuwa si za
jitihada zake,
muumba
kawaida na zimejaa
Maalim Abdallah alhekima na uvumilivu
Tanzania
isema kuna changamojambo lilomfanya kuimetambulika
to nyingi ambazo Waisfanikiwa kwa kiwanlamu tunapaswa kuzigo cha hali ya juu kuduniani kote
fanyia kazi, moja ikiwa
usambaza Uislamu
kama ni kisiwa
ni tatizo la maradhi ya
duniani kote.
roho. Kutokana na tatiAidha, Maalim
cha amani,
zo hili, Waislamu kwa
Abdallah alishauri
utulivu na
Waislamu wamefikia
jamii ya Kiislamu
hatua ya kutoleana
kuanza kuingiza
upendo. Na
maneno yasiyofaa kisa
mtaala wa ulinganiaji
watu wake
ni kupishana kwa mitakatika madrasa,
zamo.
markazi na vyuo
wanasifika
Maalim Abdallah
i n av y o f u n d i s h a
mpaka leo kwa velimu
anatoa mfano wa walya dini ili walinganiaji wa dini ambao
kuwa wakarimu inganiaji wa leo
mara nyingi wamekuwa
waweze kufanya kazi
jambo ambalo
wakiacha kazi yao na
zao kwa weledi.
badala yake kuzama kaKulingania kuna
hakika
tika kutangaza misihatua zake, ni somo
tunajivunia
mamo yao ya kimadhmaalum kabisa huhabi, jambo ambalo ni
wezi leo hii ukamlinkwa sifa hizo
lina taathira mbaya kwa
mtu ambaye
mbele ya nchi za gania
mustakabali wa Uislahajui kabisa hata
mu. Maalim Abdallah
Tawhid akawa sawa
kimataifa
alisema kwa miaka
na yule anayejua japo
mingi masheikh, wanazuoni na viongozi kidogo hiyo Tawhid, alisema Abdallah.
wengine wa dini ambao wamekuwa na
Naye kwa upande wake, Msemaji wa Jumsimamo tofauti wa kimadhahabi wame- muiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Rajakuwa vitovu vya kuzalisha uhasama mion- bu Katimba aliwataka Waislamu kutumia

siku hizi za mwanzo za mwanzo wa mwaka


kwa kujitafakari katika miezi 12 iliyopita
walifanya nini, wamekosea wapi na wafanye nini sasa wakati wakiuanza mwaka huo
mpya.
Ni wakati muafaka kwa Waislamu kujiuliza kwa nini wameweza kupata fursa ya
kuanza mwaka mpya wa Kiislamu huku
wengine wakishindwa, wamefanya yapi yanayompendeza Mungu na kujipanga kwa
kufanya mema zaidi kwa faida yao, alisema
Katimba
Aidha Katimba alitumia fusa hiyo kuwaonya vijana ambao wanapandikizwa
itikadi ambayo sio sahihi watumie muda
wao kusoma vizuri Quran na sunna ili kuweza kubaini ukweli. Pia, alikariri mwito
wa Maalim Abdallah wa kuzingatia na kujiuliza mbinu sahihi ambazo zimetumika
kusambaza dini kwani hivi sasa kumezuka
njia potofu za kufikisha ujumbe kwa watu.
Aliongeza kusema walinganiaji wengi
wa leo wana mapungufu mengi ikiwemo
kutokuwa na uvumilivu pamoja na kukosa
maneno ya hekima katika kufikisha mawaidha kwa watu wanaowalingania.
Katimba alisema alisema lazima kuwe
na mabadiliko kuanzia ngazi ya walinganiaji, masheikh na wanazuoni ili utaratibu wa
awali wa kulingania ambao ulikuwa ukitumiwa na Mtume uweze kutamalaki.
Niungane na masheikh kuwatakia Waislamu wote tafakuli iliyo njema juu ya mambo ambayo tumeyafanya mwaka uliopita
na tujikite sasa kuendeleza mema kwa kufanya ibada na kusaidia jamii kwa ujumla
ikiwemo wajane, yatima, na wagonjwa ili
Allah awe mwenye kutuhurumia wakati tutakaporejea kwake.

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

habari

www.islamicftz.org

Viongozi TIF wawaasa watanzania


Na Kassim Lyimo

akati wiki moja tu ikiwa imebakia kabla


Watanzania hawajachagua rais,
wabunge na madiwani, wawakilishi na masheka, viongozi wa taasisi
ya The Islamic Foundation (TIF)
wamewanasihi wadau wote katika
uchaguzi huu kutumia busara kwa
ajili ya kudumisha amani iliyopo
hapa nchini.
Wito huo umetolewa na
Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Aref
Nahdi wakati akizungumza katika
kipindi maalumu kuhusu amani
kilichorushwa hewani na Radio na
Tv Imaan, siku ya Alhamisi.
Nahdi alisema kuwa baadhi ya
viongozi na watendaji wa serikali,
viongozi wa vyama vya siasa na hata
wa dini wamekuwa wakitoa kauli
zinazoweza kusababisha au
kuchangia uvunjifu wa amani.
Watanzania tunalilia amani,
bila amani watoto hawawezi kwenda shule, kuna baadhi ya nchi watoto wanahangaika hawasomi, kinamama wananyanyasika, kutokana na nchi zao kutokuwa na amani,
alisema Nahdi.
Hivi sasa katika nchi yetu kuna
viashiria vimeanza kuibuka vya
uvunjifu wa amani, visipozungumzwa basi baada ya muda mfupi
hali ya amani itakuwa ni mbaya na
hatutampata mtu hata mmoja wa
kumlaumu, alisema Mwenyekiti
huyo wa TIF.
Katika hatua nyingine, Nahdi
amewataka wanasiasa kuangalia
maeneo wanayoyazungumza katika majukwaa yao ya kisiasa, na
kuacha maneno ya kuchafua na
kudharauliana miongoni mwao,
kwani hali ikichwa itachangia amani kupotea.
Kadhalika, alisema kuwa Waislamu wanajukumu kubwa la kulinda amani, kwa sababu mafundisho
ya dini ya Kiislamu yamehimiza
amani kwa wafuasi wake na watu
wote duniani.
Waislamu na wasiokuwa Wais-

Selemani Magali

amia ya wakazi wa mji


wa Morogoro wanategemewa kufurika
katika mahakama ya
Hakimu Mkazi mkoani humo
kusikiliza hukumu ya kesi inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi
za Kiislamu nchini, Sheikh Issa
Ponda inayotarajiwa kutolewa leo.
Kwa mujibu wa Wakili wa
Sheikh Ponda Juma Nassor, hukumu ya kesi hiyo inatolewa kufuatia
mashahidi wa pande zote mbili kumaliza kutoa ushahidi wao na pia
upande wa mashitaka kuwasilisha
hoja zao za majumuisho ya kesi
hiyo kwa maandishi.
Wakili Nassor alisema umefika
wakati mahakama kutimiza wajibu
wake katika kutenda haki na
kwamba ana matumaini makubwa
kuwa mteja wake ataachiwa kwani
hata muda wa miaka miwili am-

Mwenyekiti
wa The
Islamic
Foundation,
Aref Nahdi.

lamu tuishi kwa amani, viashiria


vya uvunjifu wa amani vimeanza
kuonekana, sisi wote ni Watanzania
haina haja ya kufikia wakati tukaanza kugombana kutokana na
sababu ndogo ndogo ambazo
zinaweza kutatuliwa, alisema Nahdi.
Akizungumzia uchaguzi, Arif
Nahdi aliwataka Waislam wote kushiriki uchaguzi mkuu na kwa am-

ani kwa kwenda kupiga kura kisha


kurudi majumbani kwani hawawajibiki kulinda kura bali hiyo ni kazi
ya mawakala wa vyama vya siasa.
Nahdi alisema kukaa vituoni
kunaweza kusababisha uvunjifu wa
amani hali ya kuwa Uislam unawataka Waislam kuwa walinzi wa amani badala ya kuleta visababishi vya
uvunjifu wa amani.
Kwa upande wake, Mkurugenzi

Mtendaji wa Taasisi ya The Islamic


Foundation, Sheikh Ibrahim Twaha ambaye aliambatana na
Mwenyekiti Nahdi katika kipindi
hicho maalum, aliwataka Viongozi
wa Serikali kutekeleza ahadi zao
kwa wananchi, kwani kutoa ahadi
ambazo huwezi kuzitekeleza husababisha maneno miongoni mwa
jamii.
Aidha, Sheikh Twaha alisema

Sheikh Ponda asubiriwa kwa hamu


bayo mteja wake ameutumikia akiwa mahabusu inatosha kuwa hukumu.
Katika kesi hiyo, Sheikh Ponda
anakabiliwa na mashtaka mawili,
kutoa matamko ya kuumiza hisia
za kidini na lile la kukusanyika
kinyume cha sheria katika eneo la
msikiti wa Dini Moja, Mungu
Mmoja ulioko eneo la Uwanja wa
Ndege, Morogoro.
Awali, Mahakama ya Hakimu
Mkazi mkoani Morogoro ilipanga
Septemba 4 mwaka huu kuwa siku
ya hukumu ya kesi hiyo, lakini ilipofika tarehe hiyo hakimu alilazimika kuiahirisha kufuatia mawakili wa serikali kushindwa kuwasilisha hoja za majumuisho, kama mahakama ilivyoagiza, jambo ambalo

Wakili Nassoro alililalamikia.


Wakili Nassoro alisema: Agosti
7 mwaka huu mimi na mwenzangu
Iddi Mselem tulimaliza kutoa ushahidi kisha mahakama iliagiza pande
zote mbili kuwasilisha majumuisho
ya kesi na mwisho ifikapo Agosti
28. Sisi tuliwasilisha ila upande wa
mashitaka haukufanya hivyo na
badala yake walileta majumuisho
yao nje ya muda Septemba 17, mwaka huu kinyume na amri ya mahakama.
Tulitarajia kesi hii ingefika
tamati yake Septemba 4 mwaka
huu lakini zoezi hilo halikuwezekana baada ya mawakili wa upande
wa mashtaka kudai hawakujua
kama walipaswa kuwasilisha hoja
hizo pamoja na ukweli kuwa walisi-

kia maagizo ya mahakama, alisema


Wakili Nassoro.
Siku hiyo ya Septemba 4, mabishano ya kisheria yaliibuka mahakamani huku mawakili wa mshtakiwa
wakijaribu kupinga ombi la upande
wa mawakili wa upande wa Serikali
la kutaka kuongezewa muda. Hata
hivyo, mahakama iliahirisha kesi
hiyo kufuatia ombi hilo la mawakili
mpaka Septemba 18, 2015 ili kuangalia uwezekano wa kuwaongezea
muda mawakili hao kujiandaa kuwasilisha hoja zao au la!
Wakili Nassoro, amesema wao
(upande wa utetezi) walipinga kitendo cha upande wa mashtaka
kuchelewa kuleta majumuisho hata
hivyo hakimu aliahidi kutolea uamuzi suala hilo siku hiyo ya huku-

Katika hatua
nyingine, Nahdi
amewataka
wanasiasa
kuangalia
maeneo wanayo
yazungumza
katika majukwaa
yao ya kisiasa, na
kuacha maneno
ya kuchafua na
kudharauliana
miongoni
mwao, kwani
hali ikichwa
itachangia amani
kupotea.
kuwa ahadi hizo, ambazo hazitekelezeki huchangia uvunjifu wa
amani, na pia aliwataka Waislamu
kuwa mbele katika kusimamia amani
Uislamu ni amani ili watu
waabudu Allahni vizuri suala la
amani lizingatiwe katika jamii,
Sheikh Twaha alisema. Alisema ni
kwa kutambua umuhimu wa amani ndio maana taasisi ya TIF ina
malengo ya kuwajenga watu kiroho.
Kwa hivyo, kuzungumza amani
ni jambo la lazima kwetu kwa sababu Watanzania wengi wanaiamni
Taasisi kwa kuwapa mazuri ya
Waislamu, alisema Sheikh Twaha.
Ni kheri tufe katika kufanya
mambo ya heri wala tusipoteze
maisha yetu katika vurugu za kisiasa kwani lengo la kuletwa duniani
ni kumuabudu Allah Taala, alisema Mkurugenzi huyo wa Taasisi ya
TIF.
Hali kadhalika, Sheikh Twaha
alisema kuwa ni aibu kubwa kwa
Muislamu kuhusika katika uvunjifu wa amani kwani dini ya Kiislamu
ni dini ya amani na wala sio dini ya
vuruga na kusababisha machafuko
katika jamii.
mu. Safari ya Sheikh Ponda ya kukaa gerezani ilianza Agosti 10, 2013
alipokamatwa baada ya kupigwa
risasi na polisi mjini Morogoro
dakika chache tu baada ya kumaliza
kuhutubia Waislamu siku ya Idi katika msikiti wa Dini Moja, Mungu
Mmoja ulioko eneo la Uwanja wa
Ndege.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi mkoani Morogoro lilikanusha kumpiga
risasi Sheikh Ponda Issa Ponda. Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro
ACP Faustine Shilogile alisema
polisi walikwenda kumkamata lakini kwa kusaidiwa na wafuasi
wake, Sheikh Ponda aliwatoroka.
Baada ya kujeruhiwa, Sheikh
Ponda alikwenda Hospitali ya Taifa
Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa
matibabu yatokanayo na kupigwa
risasi lakini polisi wakamtia nguvuni na kumfungulia mashitaka katika Mahakama ya Hakimu mkazi
mjini Morogoro.

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

www.islamicftz.org

Kutoka katika Quran na Sunnah


sheikh Tawakkal Juma

Adhabu ya kifo
huliwaza wafiwa,
hulinda uhai na
kuleta amani
Mpenzi
msomaji, katika
makala kadhaa
zilizotangulia
tulizungumzia
ubaya wa kuua kwa
mujibu wa Uislamu.
Tuligusia pia kuwa
katika Uislamu
mtu huuwawa kwa
kufanya makosa
maalumu na
adhabu hiyo ya
kifo hufanyika kwa
utaratibu maalumu
wa kisheria.

Miongoni mwa makosa yanayopelekea mtu kuhukumiwa adhabu ya kifo katika Uislamu ni kuua kwa makusudi.
Tena, ili adhabu hii itekelezwe
ni lazima ithibitike pasina shaka yoyote kuwa kweli mtuhumiwa kaua kwa makusudi.
Anasema Allah aliyetukuka
katika Quran Tukufu: Na Tumewaandikia (Sharia) humo
kwamba uhai kwa uhai, na jicho kwa jicho, na pua kwa pua,
na sikio kwa sikio, jino kwa
jino; na majeraha (kulipizana)
kisasi. Lakini atakayetolea
sadaka (haki yake akasemehe)
kwayo, basi itakuwa ni kafara
kwake. Na yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha
Allah, basi hao ndio mad-

halimu. (5 : 45).
Hii ni simulizi ya Quran juu
ya Sharia ya Taurati kuwa
miongoni mwa hukumu zilizokuwamo katika kitabu hicho
kilichoshushwa kwa Nabii
Musa ni adhabu ya kifo. Kama
adhabu hiyo haiko hivi leo
ndani ya kinachodaiwa kuwa
Kumbukumbu la Taurati, basi
watu wameiondoa, na kwa

CD za Anaashid zinazorushwa kupitia redio


Imaan zinapatikana katika sehemu zifuatazo
Morogoro -TIF Media makao makuu ya
The Islamic Foundation, Msamvu
Dar es salaam - katika ofisi ya The Islamic Foundation
iliyopo Kariakoo mtaa wa Mafia na Sikukuu jijini
Dar es Salaam.
Kwa mawasiliano piga simu
namba 0713 596 223.

hakika mengi yameondolewa.


Allah anasema ndani ya
Quran: Na tumekuteremshia (ee Muhammad) Kitabu
kwa haki kinachosadikisha
yale (yaliyokuja katika) vitabu vilivyokuwa kabla yake na
chenye kudhibiti, kushuhudia na kuhukumu (muhayminan) juu yake (hivyo Vitabu). Basi, hukumu baina yao
kwa yale aliyoyateremsha Allah; na wala usifuate hawaa
zao kwa kuacha haki iliyokujia. Kwa kila (umma) katika
nyinyi tumeujaalia sharia na
njia (Shariyah na manhaj).
Na kama angetaka, Allah angelikufanyeni umma mmoja;
lakini (Allah amekufanyeni
hivyo) ili akujaribuni katika
yale aliyokupeni. Basi shindaneni katika mambo ya
kheri. Kwa Allah pekee ndio
marejeo yenu nyote; kisha
atakujulisheni yale (yote)
mliyokuwa mkikhitilafiana
(5: 48).
Adhabu hii ya kifo imethibitishwa na Quran, Allah
aliyetukuka anasema katika
Quran: Enyi mlioamini!
mmeandikiwa (Shariyah ya
kulipiza) kisasi waliouawa.
Muungwana kwa muungwana, na mtumwa kwa
mtumwa, na mwanamke
kwa mwanamke, na anayesamehewa na nduguye kwa
lolote basi kufuatilizwa
kwake kuwe kwa wema na
kumlipa kwake iwe kwa ihsaan. Hiyo ni tahafifu kutoka
kwa Mola wenu na rahma.
Na atakayeruka mipaka baada ya hapo basi atapata adhabu iumizayo. Na mtapata
katika (kulipiza) kisasi
(kuokoa) uhai enyi wenye
akili mpate kuwa na taqwa
(2:178-179).
Wakati Wakristo wengi,
kama si wote hivi leo wanaona kuwa kwa mujibu wa mafundisho ya Biblia (ambayo
ndani yake kuna Kumbukumbu la Torati) haifai kumhu-

kumu mtu adhabu ya kifo na


pia haifai kulipa kisasi; mafunzo ni akupigaye shavu la
kushoto, mgeuzie na la kulia.
Mmoja wa wanathiolojia
wakubwa wa Kikristo aliwahi kusema: If anyone attempted to rule the world by
the Gospel and to abolish all
temporal law and sword on
the plea that all are baptized
and Christian, and that, according to the Gospel, there
shall be among them no law
or sword, tell me friend, what
would he be doing?
Mwanathiolojia huyo
anaendelea: He would be
loosing the ropes and chains
of the savage wild beasts and
letting them bite and mangle
everyone, meanwhile insisting that they were harmless,
tame, and gentle creatures;
but I would have the proof in
my wounds. Just so would
the wicked under the name
of Christian abuse evangelical freedom, carry on their
rascality, and insist that they
were Christians subject neither to law nor sword, as
some are already raving and
ranting.
Maana ya maneno hayo
ya mwanathiolojia huyo ni:
Kama mtu yoyote yule angelijaribu kutawala ulimwengu kwa kutumia Injili na
akaondoa sheria na adhabu
zote kwa madai kuwa watu
wote ni Wakristo na wamebatizwa, na kuwa kwa mujibu wa Biblia pasiwe na sheria
au adhabu; niambie rafiki
yangu angekuwa anafanya
nini kwa kitendo chake hicho?
Mwanathioljia anajibu
swali lake hilo: Bila shaka
atakachokuwa akifanya ni
kuwafungulia kamba na
minyororo wanyama wakali
na hivyo kuwaachia
wamngate na kumtafuna
kila mtu huku yeye akiendelea kusisitiza kuwa hawana
madhara, wanafugwa au ni

wapole; lakini mimi


niliyengatwa ningekuwa na
ushahidi dhidi yao katika
majeraha yangu. Ni kwa
namna hiyo waovu kwa jina
la Ukristo watautumia uhuru
huo vibaya, na hivyo kutenda
maovu huku wakisistiza
kuwa wao ni Wakristo kwa
hiyo hawako chini ya sheria
au adhabu kama baadhi walivyoanza kufanya
Wanaopinga kuendelea
kwa adhabu ya kifo sio kuwa
hawaoni umuhimu na udharura wa kuwepo na kuendelea kwa adhabu hiyo, bali
ni kuwa wakati mwingine
wanaostahili kuhukumu au
kutekeleza hukumu hizo wao
wenyewe ni wauaji. Sasa ukweli huu unawasuta. Wanakosa uhalali wa kiroho au
(moral authority). Vipi jaji
atamhukumu adhabu ya kifo
muuajiwakatijajimwenyewe
anajijua wazi kuwa amewahi
kuua tena pengine si mtu
mmoja, wawili au watatu bali
watu kadhaa?
Katika badhi ya nchi, majaji wanaweza kuhukumu
adhabu za kifo lakini maraisi
wa nchi hizo wakasuasua au
wakakataa kusaini adhabu
hizo zisitekelezwe. Ndiyo yale
ya: All cats love fish, but fear
to wet their paws. Yaani,
Paka wote wanapenda samaki lakini huchelea kulowanisha viganja vyao.
Katika makala hii na ijayo
sikusudii kuzungumza na
kutoa hoja za kwa nini adhabu ya kifo iendelee kwani
nimeshawahi kufanya hivyo
katika moja ya vipindi vya
Mada Nyeti vya TV na redio
Imaan, wala sitozungumza
udhaifu wa hoja za wanaopinga adhabu ya kifo isiendelee. Hata hivyo nashangaa
sana wapingaji wa adhabu
hiyo wanaocheza wimbo huu
huku mishipa ya uso ikiwa
imewatoka wanatunzwa na
kuchaguliwa wimbo na nani
safari hii, maana Wamerikani wanayo adhabu hii na hawataki kabisa kuitokomeza.
Pamoja na wanaojiita wanaharakati wa haki za binadamu kukomalia adhabu ya
kifo iondolewe ni dhahiri
kuwa wanachoimba na kukataa ni watu kunyongwa
kwa utaratibu wa kisheria ila
pale wanapovamiwa na majambazi bila shaka hujitoa na
kukabiliana nao kwa marungu na mapanga, na ama zangu ama zako huku wakiwahukumu kifo majambazi
waliowavamia. Huwezi kuvamiwa na jambazi kisha
ukamuelekeza kwa lugha ya
haki za binadamu eti ukiniua
utapelekwa mahakamani na
huko hutohukumiwa kifo
kwa sababu ni kinyume na
haki za binadamu! Haya yatakuwa yale ya Waswahili
ukistaajabu ya Musa

Itaendelea (tawaqaljuma@yahoo.com)

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

www.islamicftz.org

ncha ya kalamu

Sheikh Muhammad Issa

Marekani na karata ya Boko Haram


Yainyima silaha Nigeria
Yapeleka wanajeshi
Cameroon
Lengo ni mafuta, ugaidi ni daraja tu

ita dhidi ya kundi la


Boko Haram nchini Nigeria, Cameroon, Niger
na Chad imeingia katika
hatua nyingine kufuatia taarifa
kwamba Marekani inapelekea wanajeshi 300 na ndegevita sizizo na
rubani nchini Cameroon.
Rais Muhamadu Bukhari wa
Nigeria aliyeingia madarakani
miezi saba iliyopita, amekuwa akifanya kila awezalo kutimiza ahadi
ya kuwafyekea mbali Boko Haram
aliyoitoa katika kampeni za uchaguzi.
Badala ya mashambulizi ya
Boko Haram kupungua, ndiyo
kwanza yameongezeka hususan
matukio ya ugaidi wa kujilipua katika maeneo yenye watu wengi na
kusababisha vifo vya maelfu ya
watu wasio na hatia.

Marekani yakataa kuiuzia


silaha Nigeria
Mwezi Julai mwaka huu, rais
Muhamadu Bukhari aliomba
mataifa ya kimagharibi, hususan
Marekani, yaiuzie Nigeria silaha za
kisasa ili kuliwezesha jeshi la Nigeria kupambana vilivyo na Boko
Haram lakini alikataliwa.
Kwa mujibu wa rais Bukhari,
Marekani ilikataa kuiuzia silaha
nchi yake kwa madai kuwa kufanya
hivyo ni kwenda kinyume cha sheria iitwayo, Leahy law ambayo inaizuia serikali ya Marekani kuiuzia
silaha nchi yenye rekodi mbaya ya
haki za binadamu.
Ripoti ya Shirika la Kimataifa la
Kupigania Haki za Binadamu
(Amnesty International), jeshi la
Nigeria linatuhumiwa kuvunja
haki za binadamu katika mapambano yake dhidi ya Boko Haram.
Njama za Marekani
Ripoti mbali mbali za wachunguzi wa mambo zinadai kuwa
Marekani inahusika katika kuanzishwa Boko Haram kwa lengo la
kuivuruga Nigeria ili kufaidika na
hazina ya mafuta yaliyogunduliwa
nchini Chad na Cameroon.
Marekani imekuwa ikiahidi kuisaidia Nigeria kukabiliana na kitisho cha Boko Haram lakini wachunguzi wa mambo wanashangaa
kama kweli Marekani ina nia njema, kwa nini basi ikatae kuiuzia silaha Nigeria?
Kana kwamba hilo halitoshi,
pamoja na uwepo wa maafisa wa
kijasusi wa Marekani na wale wa
Israeli nchini Nigeria, mashambulizi ya Boko Haram ndio kwanza
yanaongezeka kila uchao. Hapo
kuna nini?
Ni vita ya mafuta
Katika kitabu, Petroleum and
its Impact on Three Wars in Africa:
Angola, Nigeria and Sudan,

mwandishi Adrian Gonzalez


anaandika: Oil and gas supplies
are becoming scarcer and more expensive. The hunt for the worlds
remaining resources is creating
new alliances and the danger of
fresh conflicts.
Tafsiri: Upatikanaji wa mafuta
na gesi unazidi kuadimika na kuwa
ghali zaidi. Utafutaji rasilimali
chache za ulimwengu zilizobaki
unasababisha ushirika mpya na
hatari ya migogoro mipya.
Mgogoro wa Nigeria unaosababishwa na Boko Haram na ule wa
Sudan Kusini kati ya majeshi ya
serikali ya rais Salva Kiir na waasi
wanaoongozwa na Riek Machar ni
miongoni mwa migogoro mipya
inayotokana na mataifa tajiri,
Marekani kwa upande mmoja na
China kwa upande mwingine
kugombania mafuta.
China is moving aggressively to
satiate its growing appetite for energy, potentially setting up conflict
with the United States over the
dwindling resources of the Middle
East and Africa
Tafsiri: China inavamia kwa
kasi kukidhi kiu yake ya nishati
inayoongezeka, kwa kufanya hivyo
inasababisha mgongano na
Marekani kuhusu rasilimali zinazopungua za Mashariki ya Kati na
Afrika.

Boko Haram na Ajenda ya


Mafuta
Ripoti za wachunguzi wa masuala ya migogoro ya kimataifa wanafichua kwamba kundi la Boko
Haram lilianzisha mashambulizi ili
kuinyima Nigeria fursa ya kuchimba hazina yake mpya ya mafuta katika majimbo ya bonde la Chad.
Hazina ya mafuta katika bonde

la Chad inapanuka hadi katika nchi


za Niger, Cameroon na Nigeria.
Miaka ya karibuni, Chad imekuwa
mchimbaji na msafirishaji wa mafuta kupitia bomba la kusafirisha
mafuta lenye urefu wa kilometa
1070 kupitia Cameroon.
Inasadikiwa kwamba hazina
kubwa ya mafuta hayo iko katika
eneo la Kaskazini Mashariki mwa
Nigeria kwenye majimbo ya Yobe,
Borno na Adamawa, majimbo ambayo mashambulizi ya Boko Haram yameshamiri.
Lengo ni kuizuia Nigeria
kuendesha shughuli za uchimbaji
wa mafuta katika eneo hilo kutokana na mashambulizi ya Boko Haram huku Chad, Cameroon na Niger zikiendelea na uchimbaji huo.
Wataalamu wa uchunguzi na
uchimbaji mafuta walilazimika
kusimamisha shughuli zao kwa
hofu ya kutekwa au kuuawa na wapiganaji wa Boko Haram huku

Marekani
imekuwa ikiahidi
kuisaidia
Nigeria
kukabiliana na
kitisho cha Boko
Haram lakini
wachunguzi
wa mambo
wanashangaa
kama kweli
Marekani ina
nia njema, kwa
nini basi ikatae
kuiuzia silaha
Nigeria?

wataalamu wa miamba (geologists)


wa Shirika la Mafuta la Nigeria
(NNPC) wakishindwa kufanya
kazi.
Kwa mujibu wa E&P Mag, matumaini ya kuongeza uzalishaji wa
mafuta Nigeria ili kuinua pato la
taifa katika upande wa bonde la
Chad Kaskazini mwa Nigeria
yametoweka kutokana na vitendo
vya kikatili vya Boko Haram.
Uchunguzi wa mafuta ulikuwa
unakwenda vizuri na uchimbaji
kibiashara ulikuwa unatazamiwa
kuanza mwishoni mwa 2013 au
mwanzoni mwa 2014, alisema Namadi Sambo, aliyekuwa Makamu
wa Rais wa Nigeria katika serikali
ya rais Goodluck Jonathan.

Marekani na wizi wa mafuta


Mashambulizi ya Boko Haram
yamewezesha Chad chini ya serikali
ya rais Idris Derby kuiba mafuta ya
Nigeria kwa kutumia kiitwacho,
3D oil drilling.
Mafuta hupatikana katikati ya
miamba na yanaweza kusambaa
chini ya ardhi kutoka nchi moja
kwenda nchi nyingine. Kisima cha
mafuta kinapochimbwa, mafuta
kutoka chini ya ardhi hutiririka
kwenda pale palipochimbwa.
Matokeo yake ni kwamba, kama
mwamba ulioenea nchi mbili
haukuchimbwa upande wa nchi
moja, mafuta yaliyo chini ya ardhi
ya nchi ambayo haichimbi yanavutwa kwenda kule yanakochimbwa kitendo kitwacho, capturing.
Kutokana na mashambulizi ya
Boko Haram, nchi za Chad, Cameroon na Niger hivi sasa zinachimba mafuta kwa ushirikiano na mashirika ya mafuta ya Ufaransa,
Uingereza na Marekani na hivyo
kusababisha mafuta ya Nigeria

kutiririka kwenda katika nchi hizo.


Kwa mujibu wa kile kiitwacho,
Rule of Capture, uchimbaji huo wa
mafuta ya nchi unaruhusiwa alimradi uchimbaji ufanyike ndani ya
mipaka ya nchi inayochimba. Mafuta, gesi asilia na maji yanaweza
kuchimbwa kwa jinsi hii hata kama
yatatiririka kutoka nchi nyingine.
Kulikuwa na mzozo wa eneo
lenye hazina ya mafuta kati ya Nigeria na Cameroon liitwalo Bakassi
Peninsula. Kesi iliyofunguliwa katika mahakama huko The Hegue
Uholanzi iliipa ushindi Cameroon .
Cameroon hivi sasa inafaidika
na uchimbaji wa mafuta yanayotiririka kutoka ghuba ya Guinea nchini Nigeria. Uchimbaji huu unainufaisha Cameroon na mashirika ya
wawekezaji kutoka Ufaransa.

Njama dhidi ya Nigeria


Kutokana na mashambulizi ya
Boko Haram, wawekezaji wa uchimbaji wa mafuta wa kimataifa wameikimbia Nigeria kwa sababu za
kiusalama na mabilioni ya dola
yamewekezwa Chad, Cameroon na
Niger.
Hivi sasa Chad imeongeza uzalishaji wa mafuta katika ziwa Chad
na kuhifadhiwa katika meli maalum ziitwazo Floating, Production,
Storage and Offloading vessels
zenye uwezo wa kutunza kiasi cha
mapipa milioni mbili.
Mafuta haya husafirishwa kutoka Chad kwenda bandari ya Le Havre nchini Ufaransa. Kwa hiyo,
maana yake ni kuwa Ufaransa inafaidika sana na mashambulizi ya
Boko Haram kaskazini mwa Nigeria, mashambulizi ambayo yanaizuia Nigeria kuchimba mafuta
yake. Mtandao wa kufichua siri wa
Wikileaks uliwahi kuweka hadharani kwamba mtu ajulikanaye
kama Abu Mahjin kutoka Chad aliyepewa mafunzo katika kambi ya
Marekani nchini humo, ndie hasa
muasisi wa mashambulizi ya Boko
Haram.
Lengo la uwepo wa Boko Haram ni kuinyima utulivu Nigeria ili
isichimbe mafuta eneo la Kaskazini
Mashariki na hivyo kutoa fursa kwa
mataifa ya magharibi kuiibia rasilimali yake kupitia Chad, Cameroon
na Nigeria.
Hivyo haishangazi hata kidogo
kwamba mashambulizi ya Boko
Haram yanazidi kila uchao,
Marekani inakataa kuiuzia Nigeria
silaha za kupambana na Boko Haram na Marekani hiyo hiyo inapeleka majeshi yake nchini Cameroon.
Kuongezeka kwa mashambulizi
na kuikatalia Nigeria kununua silaha yana lengo la kuendelea kuizuia
Nigeria isichimbe mafuta upande
wake hivyo kuruhusu mafuta yake
kuibiwa kupitia nchi jirani yake.
Majeshi ya Marekani kuwekwa
nchini Cameroon kama yalivyo
nchini Chad ni kwa ajili ya kulinda
wizi huo wa mafuta ya Nigeria,
kuikomoa nchi hiyo kiuchumi na
kuidhoofisha ili isiwe tishio kwa
Marekani ukanda huo.

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

makala

10

www.islamicftz.org

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

11

www.islamicftz.org

Misingi ya ufanisi wa

Siku ya Ashura:

uongozi wa Mtume

Yatakiwayo na
yasiyotakiwa
Sheikh Mohammad Issa

akika idadi ya miezi mbele ya


Allah ni kumi na miwili, tangu siku aliyoziumba mbingu
na ardhi. Hiyo ndiyo dini ya
haki kwa hiyo msizidhulumu nafsi zenu
katika miezi hiyo (Quran 9:36).
Katika hadithi iliyopokewa na Abu
Bakira (siyo Khalifa Abubakr) Allah awe
radhi nao wawili hao, Mtume (Rehma
na amani ziwe juu yake) amesema:
Mwaka una miezi kumi na miwili na
minne kati ya hiyo ni mitakatifu; mitatu
imefuatana Dhul Qadah, Dhul Hijja na
Muharram na Rajab Mudhar unaokuja
kati ya Jumaadal Akhir na Shaaban
(Bukhari)
Naam, tungali katika miezi mitakatifu
mitatu iliyofuatana na huu mwezi wa
Muharram ukiwa ndio wa mwisho katika mfululizo huo, ikiwa leo ni tarehe 6
Muharram. Allah Taala atujaalie uwe
kwetu mwezi wa kheri na baraka kwa
ajili ya dunia na akhera yetu.
Mambo ya kufanya katika Muharram
Miongoni mwa mambo ya kufanywa
na Muislamu katika mwezi huu wa Muharram ni pamoja na kukithirisha mambo ya heri sadaka, dhikr na swaumu na
kujizuia na kutenda maasi.
Swahaba Abu Huraira (Allah awe radhi nae) amesema, Mtume wa Allah
amesema: Funga bora baada ya (mwezi
wa) Ramadhan ni funga ya mwezi wa Allah wa Muharram (Muslim).
Kule kusemwa, mwezi wa Allah wa
Muharram ni ushahidi wa msisitizo wa
umuhimu wa mwezi huu. Pamoja na
hayo haikuthibitika Mtume wa Allah
(Rehma na amani ziwe juu yake) kufunga mwezi wa Muharram wote.
Historia ya siku ya Ashura
Jina Ashura linatokana na siku ya
kumi (Asharah) ya mwezi wa Muharram. Swahaba Abdallah bin Abbas (Allah awe radhi nae) anasimulia: Mtume
wa Allah alipofika Madina aliwakuta
Mayahudi wakisherehekea siku ya Ashura.
Mtume (Rehma na amani ziwe juu
yake) akawauliza: Ni siku gani hii? Wakasema: Hii ni sikukuu, siku Allah alipowaokoa wana wa Israili dhidi ya maadui
zao, kwa hiyo (Nabii) Musa alifunga
swaumu siku hii.
Mtume (Rehma na amani ziwe juu
yake) akasema: Sisi (Waislamu) tunayo
haki zaidi juu ya Musa kuliko ninyi kwa
hiyo akafunga siku hiyo na akaifanya

Said Rajab

sunna (Bukhari).
Katika upokezi wa Imam Ahmad (Allah amrahamu): Hii ni siku ambayo
Safina (ya Nuh) ilisimama juu ya mlima
Juudiy, kwa hiyo Nuuh akafunga
kumshukuru Allah (Ahmad).
Mayahudi walikuwa wameifanya siku
hii kuwa sikukuu ya kusherehekewa na
wanawake wao wakivaa mapambo mbali
mbali. Mtume (Rehma na amani ziwe
juu yake) akawaamrisha maswahaba wajitofautishe na Mayahudi kwa kufunga
swaumu siku hii ya Ashura.
Siku ya Ashura, Mayahudi walikuwa
waliisherehekea kama sikukuu. Mtume
wa Allah (Rehma na amani ziwe juu
yake) akatufundisha kufunga swaumu ili
tujitofautishe na Mayahudi kuhusu siku
hii ya kihistoria ya ukombozi kwa watu
wa Nabii Musa na Nuh (Amani ya Allah
iwe juu yao).
Swaumu ya Ashura ilitangulia
swaumu ya Ramadhan
Kufunga siku ya Ashura kulikuja kabla ya kufaradhishwa swaumu ya Ramadhani mwaka wa pili baada ya Mtume
(Rehma na amani ziwe juu yake) kuhamia Madina. Hii ni hIkma ya Allah kuwazoesha watu kitu kabla ya kukiamrisha. Mtume wa Allah alipofika Madina,
aliwaagiza Waislamu kufunga siku tatu
kila mwezi (masiku meupe) na siku ya
Ashura. Kisha Allah akaifanya swaumu
faradh (lazima) kwa Waislamu aliposema Enyi mlioamini imefaradhishwa
swaumu kwenu (2:183).
Fadhila ya funga ya Ashura
Imepokewa kutoka kwa Bin Abbas
(Allah awe radhi naye): Sikupata kumuona Mtume wa Allah akiwa na
shauku ya kufunga siku yoyote kwa
umuhimu mkubwa kuliko siku hii, siku
ya Ashura, na mwezi huu (Bukhari).
Shauku na umuhimu huu ni kutokana
na fadhila au faida za kufunga swaumu
ya Ashura kwani Mtume wa Allah (Rehma na amani ziwe juu yake) amesema:
Kwa kufunga siku ya Ashura, nataraji
Allah ataikubali iwe kafara ya madhambi
ya mwaka uliokwisha (Muslim).
Tazama fadhila kubwa ya Allah Taala
juu yetu kwamba kwa kufunga swaumu
ya siku moja tu, unafutiwa madhambi ya
mwaka mzima uliopita. Kweli Allah ni
mwenye fadhila kubwa kabisa. Ni heri iliyoje kwa wenye kukimbilia msamaha wa
Allah?
Ashura ni siku gani?
Imam Nawawi (Allah amrehemu)
anasema siku ya kumi ya Muharram

Miongoni mwa mambo ya kufanywa na Muislamu katika mwezi


huu wa Muharram ni pamoja na kukithirisha mambo ya heri
sadaka, dhikr na swaumu na kujizuia na kutenda maasi.
(Ashuurah) na ya tisa (Taasuah), ni majina mawili yanayotamkwa kwa kuvutwa
(madd) katika lugha ya kiarabu. Mwanawazuoni Bin Qudamah Al-Maqdasiy (Allah amrehemu) anasema: Ashura ni siku
ya kumi ya Muharram na vivyo hivyo bin
Abbas anasema: Mtume wa Allah alituamrisha tufunge siku ya kumi ya Muharram: (Tirmidhi).
Kilicho Sunnah
Kilicho sunna ni Muislamu kufunga
siku zote mbili yaani yaani tarehe tisa
Muharram (Taasuah) na kumi (Ashuurah). Bin Abbas (Allah awe radhi nae)
anasema: Mtume alipofunga swaumu
siku ya Ashura na akawaamrisha Waislamu, wakasema, ee Mtume wa Allah, hii
ni siku inayotukuzwa na Mayahudi na
Wakristo. Mtume wa Allah akasema:
Kama nitajaaliwa kufika mwaka ujao,
nitafunga na siku ya tisa vile vile. Lakini
ikatokea Mtume akafariki kabla ya mwaka uliofuata (Muslim).
Kwa hiyo sababu ya kufunga na siku ya
tisa (Taasuah) ni kuwatofautisha Waisla-

mu kutokamana na Mayahudi ambao


kwao siku ya kumi (Ashuurah) ni sikukuu.
Faid anyingine ni kwamba kwa kufunga
siku ya tisa, mtu ataepuka kuikosa siku ya
Ashura iwapo atakuwa hakujaaliwa kuuona mwezi wa Muharram.
Funga hata kama ni Ijumaa, Jumamosi au Jumapili.
Imam At-Wahawiy (Allah amrehemu)
anasema: Mtume wa Allah (Rehma na
amani ziwe juu yake) alitufundisha kufunga siku ya Ashura. Hakutuambia kama
ikiangukia Jumamosi tusifunge (Tazama
Mushkil al-Athar, Mjalada wa 2,Bab
Sawm Yawm as-Sabt).
Kwa hiyo hukumu ni hiyo hiyo kama
siku ya Ashura itaangukia Ijumaa au Jumapili kwani iwapo swaumu aliyozoea
mtu kuifunga itaangukia katika siku hizi
Ijumaa, Jumamosi na Jumapili, ataifunga pasina ubaya wowote.
Siku ya Ashura kwa Mashia
Waislamu Ahlu Sunnah tujihadhari
sana kwa sababu siku hizi sikukuu za

mashia zimeanza kuenezwa katika miji na


vijiji vyetu. Wengi katika Waislamu kwa
kukosa elimu hawajui asili wala maana za
sikukuu hizi za kishia.
Mashia huomboleza siku aliyouawa
mjukuu wa Mtume Hussein bin Ali (Allah
awe radhi nae na baba yake pia) siku ya
Ashura, wanazo pia sikukuu za kusherehekea kuuawa kwa Umar ibn Khattwaab
na kufa kwa Aisha (Allah awe radhi nao)
na kadhalika.
Sheikh bin Taymiyyah (Allah amrehemu) anasema kuelezea mashia kuifanya
siku ya Ashura siku ya maombolezo:
Kundi la wajinga na waovu na wapotofu
walijifanya kumtii Hussein na watu wa nyumba ya Mtume (Ahlul Bayt).
Alipouawa Hussein bin Ali, mashia
wakaifanya siku ya Ashura kuwa siku ya
kuomboleza na kulia ambapo hudhihirisha desturi za enzi za kijahiliya kama vile
kujipiga mashavu, kuchana nguo zao na
kuomboleza kijahili
Shetani amewapambia na wameifanya
siku ya Ashura kuwa siku ya kujiadhibu,
kulia, kuomboleza, kusoma tenzi na

mashairi yaliyojaa uongo mwingi. Hadithi


na simulizi zao hazina lengo zaidi ya kuamsha upya hisia zao na kuchochea chuki
baina ya Waislamu.
Chuki hizo huzifanya kwa kuwalaani
wale waliowatangulia (katika maswahaba
wa Mtume). Baadhi ya wajinga, kama vile
Naasibiyyuuna, wanaowapinga mashia
na wenye chuki dhidi ya Hussein bin Ali,
wameifanya siku hii kuwa sherehe.
Makundi yote hayo mawili (wanaoomboleza yaani mashia na wanaosherehekea
yaani Naasibiyuuna) ni wapotofu. Yote yafanywayo si katika sunna ya Mtume wala
makhalifa waongofu. Hayo hayakukukubaliwa na imam yeyote si Maalik, Sufyaan
At-thawriy, Al-laythiy, Abu Hanifah, AlAwzaiy, As-shaafiy, Ahmad bin Hambal
au Ishaaq Ar-rahwayh wala mwanachuoni yeyote wa Waislamu (Al-Fataawa alKubra). Kwa hiyo Waislamu wa madhhebu za Ahlu Sunnah wal JamaaShaafiiyyah, Hanaabilah, Haanafiyyah na
Maalikiyyah tujiepushe na kuifanya siku
ya Ashura sherehe kama Mayahudi au
maombolezo kama mashia.

i ukweli unaofahamika vyema kwamba


Mtume wa
Mwenyezi Mungu, Muhammad (Rehma na amani ya Allah iiwe juu yake)
ndie kiongozi aliyefanikiwa zaidi katika kipindi
chote cha historia ya mwanadamu. Lakini Mtume
huyu hakuwa tu ni shujaa,
kama mwandishi wa kimagharibi, Thomas Carlyle
alivyomwita. Kwa mujibu
wa Quran Tukufu, yeye ni
mfano bora wa wanadamu
wote na ametuonyesha
njia ya kufikia mafanikio
makubwa hapa duniani.
Kwa kusoma maisha ya
Mtume Muhammad (Rehma na amani ya Allah
iiwe juu yake) tunaweza
kuchota ile misingi mikuu
ambayo Mtume aliifuata
katika kufanya mambo.
Kwa hakika Muhammad
(Rehma na amani ya Allah
iiwe juu yake ) alikuwa ni
positive thinker kwa
maana halisi ya neno hilo.
Shughuli zake zote zililenga kuleta matokeo mazuri.
Alikwepa kabisa kuchukua
hatua ambazo zingeweza
kuleta madhara au kukwamisha mambo.
Ni vyema tukawaletea
wasomaji, japo kwa ufupi,
baadhi ya misingi ambayo
Mtume wa Mwenyezi
Mungu aliitumia katika
kufanikisha shughuli
zake.
Msingi wa kwanza Kuanza kufanya jambo
pale linapowezekana.
Msingi huu unafafanuliwa
vyema na msemo wa
mama Aishah, mke wa
Mtume, pale aliposema:
Kila Mtume alipolazimika kuchagua kati ya mambo mawili, mara kwa mara
alichagua chaguo rahisi
zaidi (Bukhari). Kuchagua chaguo rahisi, maana
yake ni kuanza jambo pale
panapowezekana, na mtu
anayefanya hivyo bila shaka atafikia lengo lake.
Msingi wa pili - Kuona
fursa katika changamoto.
Waislamu wa awali pale
Makka, walikabiliwa na
matatizo na changamoto
nyingi sana. Katika kipindi kile kigumu, Aya ya kuwaongoza Waislamu ndani ya Quran ilishuka:
Basi kwa hakika pamoja
na uzito kuna wepesi.
Hakika pamoja na uzito
kuna wepesi (94:5-6).
Hii ina maana kwamba
kama kuna changamoto,

basi na fursa pia zipo hapo


hapo. Kwa hiyo, njia ya
kupata mafanikio ni kupuuza changamoto na kufanyia kazi zaidi fursa.
Mfano, tunapolalamika
kwamba Waislamu wanabaguliwa kielimu hapa
nchini, ingawa kweli hiyo
ni changamoto nzito
kwetu, lakini pia Waislamu wanayo fursa ya kujenga na kuendesha shule
zao. Sasa ni vyema, kwa
mafundisho ya Mtume,
tukashikilia zaidi fursa zilizopo kuliko kuendelea
kuishi kwenye changamoto tu.
Msingi wa tatu - Kubadili eneo la harakati.
Msingi huu unatokana na
Hijra. Hijra haikuwa tu ni
tukio la kuhama kutoka
Makka kwenda Madina.
Ilikuwa ni hatua ya
kutafuta eneo bora zaidi la
kufanya harakati za Kiislamu, kama baadaye historia ilivyokuja kuthibitisha.
Hapa Mtume wa
Mwenyezi Mungu ametufundisha kubadili mbinu
na maeneo ya kufanyia
harakati, ili mradi hatua
hizo hazipingani na Aqida
y a
K i i s l a m u .
Tusinganganie kufanya
harakati katika eneo moja
tu. Makka ilipokuwa ngumu zaidi kwa Waislamu
wa awali, basi walihamia
Madina na harakati
zikaendelea kama kawaida na hatimaye wakarudi
kuikomboa Makka.
Msingi wa nne - Kumgeuza adui kuwa rafiki.
Mtume wa Mwenyezi
Mungu mara kwa mara
alikabiliwa na vitendo vya
uchokozi kutoka kwa
m a k a fi r i . Wa k at i u l e

Msingi wa nne
- Kumgeuza
adui kuwa
rafiki. Mtume
wa Mwenyezi
Mungu mara
kwa mara
alikabiliwa
na vitendo
vya uchokozi
kutoka kwa
makafiri.
Wakati
ule Quran
ilimuelekeza
Mtume
kulipa wema
kwa ubaya
aliotendewa

Q u r a n i l i m u e l e k e z a
Mtume kulipa wema kwa
ubaya aliotendewa:
Mambo mazuri na mabaya hayawi sawa. Ondosha (ubaya unaofanyiwa
kwa wema; tahamaki yule
ambaye baina yako na baina yake kuna uadui
atakuwa kama jamaa
(yako) mwenye kukufia
uchungu(41:34).
Hii ina maana kwamba
jambo jema linalotendwa
kama malipo ya ubaya uliofanywa, lina athari ya
mapigo kwa wale waliofanya ubaya. Na maisha ya
Mtume wa Mwenyezi
Mungu ni ushahidi wa kihistoria kuhusu msingi
huu.
Msingi wa tano - Kubadilisha hasi kuwa chanya. Baada ya vita vya Badr,
zaidi ya makafiri 70 walikamatwa kama mateka
wa vita. Walikuwa ni watu
walioelimika. Mtume wa
Mwenyezi Mungu alitangaza, iwapo kila mmoja
wao atawafundisha Waislamu kumi kusoma na
kuandika ataachiwa huru.
Hii ilikuwa ni shule ya
kwanza katika historia ya
Uislamu, ambapo wanafunzi wote walikuwa
Waislamu, na walimu
wote wakiwa maadui wa
Waislamu. Hapa napenda
kumnukuu mwandishi
mmoja wa Uingereza, ambaye amemueleza Mtume
wa Mwenyezi Mungu,
kama mtu aliyeweza kuona mafanikio kutokana na
hali ya kushindwa - He
was determined to write
success out of failure
Msingi wa sita - Nguvu
ya amani ni imara zaidi
kuliko nguvu ya vurugu.
Wakati Makka ilipokombolewa, wapinzani na
maadui wote wa Mtume
wa Mwenyezi Mungu waliletwa mbele yake. Walikuwa ni wahalifu wa
kivita, kwa maana zote za
neno hilo. Lakini Mtume
hakuagiza wauawe. Badala yake alisema: Nendeni,
mko huru. Matokeo ya kitendo kile cha wema yalikuwa makubwa sana.
Wengi wao walisilimu siku
ile.
Msingi wa saba - Kutokuwa na fikra mgando.
Tusifikiri kwa kutumia
vipimo viwili tu, kwamba
kama jambo haliko hivi,
basi lazima liwe vile. Kuna
jicho la tatu pia. Katika
vita maarufu vya Mutah,
Khalid bin Waliyd (Allah
awe radhi naye), kamanda
w
a inaendelea Uk 12

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

12

www.islamicftz.org

Misingi ya
uongozi
wa Mtume

afya yako
Pazi Mwinyimvua

Umuhimu wa kula
pamoja kama familia

atika mambo yanayoweza kuonekana ni


ya kizamani na mwiko
kwa wakati wa sasa ni
kula pamoja kama familia. Ukiwa kama mkuu wa familia,
jiulize mara ya mwisho ilikuwa
lini familia yako yote ilikutana
na kula pamoja mlo wa asubuhi,
mchana au usiku.
Kutokana na kubanwa na
kazi, mazowea mabaya au kwenda na wakati, kula pamoja kama
familia inayoishi nyumba moja
ni jambo gumu sana kwa watu
wengi wa zama hizi.
Hata hivyo, katika dini ya Kiislamu, kula pamoja ni jambo lililoruhusiwa na kuhimizwa
kama tunavyoliona katika
Quran na Sunna. Katika Quran
Mwenyezi Mungu anasema: Si
vibaya kwa kipofu, wala si vibaya
kwa kiguru, wala si vibaya kwa
mgonjwa, wala kwenu nyinyi,
mkila katika nyumba zenu, au
nyumba za baba zenu, au nyumba za mama zenu, au nyumba za
kaka zenu, au nyumba za dada
zenu, au nyumba za ami zenu, au
nyumba za shangazi zenu, au nyumba za wajomba zenu, au nyumba za dada wa mama zenu, au
za mlio washikia funguo zao, au
rafiki yenu.
Aya inaendelea: Si vibaya
kwenu mkila pamoja au mbali
mbali. Na mkiingia katika nyumba, toleaneni salamu, kuwa
ni maamkio yanayotoka kwa
Mwenyezi Mungu, yenye baraka
na mema. Hivyo ndivyo
Mwenyezi Mungu anavyo kubainishieni aya zake mpate
kuelewa (24: 61).

Katika Sunna, Mtume Muhammad, (Rehema na amani za


Allah zimshukie), amehimiza
kula pamoja kwa ksema: Kusanyikeni kwenye chakula chenu
ili kibarikiwe (Imepokewa na
Abu Dawud na Tirmidh).
Tafiti za sasa za kisayansi zinaonyesha kuwa kuna umuhimu
mkubwa sana wa kula pamoja
kama familia. Tafiti hizo zinapendekeza kuwa familia iwe inakula pamoja angalau mara tano
mpaka sita kwa wiki kwa mlo wa
asubuhi, mchana au usiku.
Familia inayokula pamoja
mara nyingi huwa na umoja kwa
sababu kula pamoja kunaipa familia fursa ya kukutana ana kwa
ana na kuzungumzia kero ndani
ya familia, kuwaunganisha wanafamilia, kupanga na kujifunza
kutoka kwa kila mwanafamilia.
Katika kula pamoja, ndipo tunapopata wasaa wa kuhakikisha
watoto wetu wanakula kwa mila
za dini na zile zitazowafanya waheshimike katika jamii yetu.
Humo pia, ndipo tunapopata
nafasi ya kudumisha utamaduni
wetu kwani bila ya utamaduni
tutakuwa hatuna utambulisho
(identity).
Kula ni sehemu ya furaha ya
kimaisha. Watu wanaposhirikiana katika furaha basi mara ny-

ingi matokeo yake huwa ni


kushikamana kwa mapenzi baina yao. Hapo hupatikana
mshikamano kutoka moyoni
(emotional attachment) ambayo
ni uti wa mgongo wa maisha ya
familia.
Kula pamoja pia, kunasaidia
kubadilishana taarifa za siku ile.
Kadhalika, wazazi au walezi
kupata muda wa kuwaangalia
kwa karibu watoto na vijana
wao. Mlo wa pamoja wa familia
unaongeza mapenzi, huruma,
usalama na kila mtu kujisikia
kuwa ni mwana familia hata
kama baba au mama ni rais wa
nchi au waziri au profesa wa
chuo kikuu.

Vilevile, kula pamoja kama


familia ni shamba darasa. Ndio
kusema, wakati wa kula kama
familia ni fursa ya pekee kwa wazazi au walezi kuwapa elimu,
ujuzi, miiko na kurekebisha tabia
mbaya za watoto na vijana wao
juu ya ulaji.
Wazazi au walezi wawe rafiki
kwa watoto na vijana wao, na
wawe walimu kwa matendo yao
badala ya maneno makali na ya
vitisho. La sivyo, watoto watakimbia kula na wazazi hao.
Zaidi ya hayo, kula pamoja
kunasaidia kupanua wigo wa

Familia inayokula pamoja mara


nyingi huwa na umoja kwa
sababu kula pamoja kunaipa
familia fursa ya kukutana ana
kwa ana na kuzungumzia kero
ndani ya familia

ufahamu kuhusu aina bora ya


vyakula. Baadhi ya watoto hawapendi kabisa baadhi ya vyakula kama vile ugali wa dona,
mboga za majani, maziwa ya
mtindi, kande, n.k. Kula pamoja
kama familia ni fursa nyingine
ya kujenga tabia za watoto na vijana ili wapende vyakula bora
zaidi kiafya kuliko kupenda
chipsi mayai, kuku kila siku.

Watoto na vijana wajaribishwe na kuonyeshwa vyakula hata


kutoka makabila mengine ilimradi, vyakula hivyo viwe bora
kwa afya zao kama vile mlo wa
ndizi na samaki. Mlo huu unaimarisha ubongo na akili ya
mtoto.
Wazazi wakumbuke kuwa
mtoto anachukumua muda mrefu kukikubali chakula asichokijua au asichokipenda, kwahiyo
uvumilifu unahitajika sana.
Mlo wa familia mara nyingi
huandaliwa nyumbani kwa hiyo
huwa na matunda na mboga za
majani za kutosha, maziwa au
mtindi. Vyakula hivyo ni chanzo
kikubwa cha nyuzi lishe, madini
kama ya calcium na vitamini
kama A, C, na folate (vitamini
B9), virutubisho ambavyo kwa
watoto huwa wanavikosa kutokana na wazazi kupenda fast
food.
Kwa wanaojali afya za watoto
wao, mlo wa nyumbani huwa sio
wenye vyakula vya kukaanga kila
siku, havina chumvi na sukari
nyingi, na matumizi ya vinywaji
vyenye sukari nyingi kama vile
soda na juisi za viwandani huwa
ni kiwango kidogo.

inatoka Uk 1
majeshi ya Waislamu aliamua kuondoa vikosi
vyake kwenye uwanja wa mapambano, baada ya kugundua
kwamba idadi ya wapiganaji
wake ilikuwa ndogo mno, ikilinganishwa na makafiri.
Walipofika Madina, baadhi ya
Waislamu waliwapokea kwa kejeli wakiwazomea Waoga hao!
(Furrar!). Mtume wa Mwenyezi
Mungu akasema: Hapana, siyo
waoga! (Hao ni Kurrar) wenye
kuona mbali.Watu wale wa Madina walikuwa na akili mgando ama kupigana au kusalimu amri,
lakini siyo kukataa kabisa kupigana, kama alivyofanya Khalid
bin Waliyd.
Mtume ameonyesha kwamba
mara zote kuna option ya tatu,
ambayo ni kuepuka vita na
kutafuta muda wa kujipanga vizuri zaidi. Historia inatuonyesha
kwamba baada ya miaka mitatu
y a m at ay a r i s h o , Wa i s l a m u
walielekea kwenye mpaka wa
Warumi, wakapambana vikali na
kupata ushindi mkubwa.
Msingi wa nane - Kupeleka
vita kwenye uwanja tunaouweza.
Msingi huu unatokana na vita vya
Hudaybiyyah. Katika kipindi kile,
makafiri walidhamiria kuwaingiza vitani Waislamu, kwa sababu
walikuwa katika mazingira mazuri ya kushinda.
Lakini Mtume wa Mwenyezi
Mungu, kwa uangalifu mkubwa,
alikubali masharti ya makafiri na
kuingia nao mkataba. Ulikuwa ni
mkataba wa amani wa miaka
kumi. Kabla ya mkataba huo, mahali pa kukutana kati ya Waislamu na makafiri, ilikuwa ni
kwenye uwanja wa vita tu.
Baada ya mkataba maarufu wa
Hudaybiyyah kusainiwa, eneo la
mapigano likabadilika, na sasa
uwanja mpya wa mapambano
ukawa mdahalo wa kiitikadi.
Ndani ya kipindi cha miaka miwili tu, Uislamu ukashinda kwa
kishindo, kutokana na ubora wa
Itikadi yake.
Msingi wa Tisa - Kuwa yakinifu kwenye masuala yenye utata.
Wakati wa kuandika mkataba wa
Hudaybiyyah, Mtume wa
M w e n y e z i Mu n g u a l i s e m a
yaandikwe maneno haya: Hii ni
kutoka kwa Muhammad, Mtume
wa Mwenyezi Mungu. Mjumbe
wa Maqurayshi akapinga vikali
maneno hayo kuandikwa kwenye
hati ya mkataba.
Haraka sana Mtume alipoona
jambo lile lingeleta mzozo usio
wa lazima, na kukwamisha ajenda ya msingi ya Waislamu kwenye
m k at a b a u l e , a k a b a d i l i s h a
maneno yale na kuagiza iandikwe
tu: Muhammad, mtoto wa Abdullah, na mambo yakaenda
kama yalivyopangwa.
Hii ni baadhi tu ya misingi ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu, aliitumia na kupata mafaniko
makubwa katika harakati zake za
kusimamisha Uislamu, mafanikio ambayo wanahistoria wote
maarufu duniani wameyatambua.

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

13

www.islamicftz.org

uchumi na biashara
JAMAL ISSA

Bima kwa mtizamo wa Kiislamu - (2)

hukrani njema ni zake


Muumba wa mbingu
na ardhi. Rehma na
amani zimfikie Muhammad aliye mkweli muaminifu na mwisho wa mitume.
Kisha salamu kwa wenye kufuata muongozo.
Bima inakubalika katika Uislamu pale tu inapofanywa katika utaratibu wa kudhaminiana
(takaful) au kushirikiana
(taawun) kwa pamoja katika
kubeba hasara kwa pamoja
hasara atakayoipata mmoja
wapom katika kundi.
Hivyo, bima katika Uislamu
sio mkataba wa kuuza na kununua ambapo upande mmoja
unatoa na unauza ulinzi (protection) na mwingine unakubali
na kununua huduma kwa gharama au bei fulani.
Bali katika Uislamu, bima ni
utaratibu wa kundi la watu
wenye maslahi ya pamoja kudhaminiana au kujilinda kwa
pamoja kutokana na majanga
fulani kwa kuunda mfuko maalumu unaochangiwa kutoka katika rasilimali zao, mfuko huu
utatumika kulipa fidia na
kugharamia shughuli zote za
kibima.
Katika makala haya, tutadurusu juu ya tofauti kati ya bima
ya Kiislamu (takaful) na bima
ya kawaida.
Moja, msukumo mkubwa
katika bima ya kawaida ni kupata faida na kukuza faida kwa
wanahisa. Biashara ya bima inamilikiwa na wanahisa wa kampuni ya bima.
Kwa upande mwingine bima
ya Kiislamu imejikita katika ustawi wa jamii na uhifadhi wa
jamii dhidi ya majanga. Huduma ya bima yenyewe si biashara
ya kupatia faida. Huduma ya
takaful inaendeshwa na kampuni ambayo huitwa mwendes h a j i w a t a k a f u l a m b ay o
hupokea malipo kama ada au
gawio kutoka katika uwekezaji.
Hivyo basi, biashara ya bima
humilikiwa na washiriki wa

bima huku kampuni ya bima inakuwa kama wakala wa kusimamia shughuli hiyo.
Pili, katika bima ya kawaida
faida hujumuisha ziada (under
writing surplus) ambayo ni tofauti kati ya jumla ya mishango
(premium) iliyokusanywa kutoka kwa wateja na jumla ya
madai, fidia iliyolipwa.
Hivyo, faida hujumuisha ziada katika bima na faida kutoka
katika uwekezaji. Pia ugawaji
wa faida au ziada unategemea
uamuzi wa uongozi wa kampuni
ya bima. Kwa upande mwingine
katika takaful faida haijumuishi
ziada inayopatikana baada ya
kutoa malipo ya fidia katika
mishango (premium). Pia
mkataba wa takaful ndio unaobainisha wakati na namna ya

ugawaji wa faida na sio uongozi


wa kampuni ya bima.
Tatu, katika bima ya kawaida
chanzo cha sheria na taratibu za
kuongoza mfumo wa bima ni
watu. Katika takaful chanzo cha
sharia na taratibu ni ufunuo
kutoka kwa Allah.
Nne, katika bima ya kawaida
uwekezaji wa michango (premium) unategemea maamuzi ya
kampuni ya bima pekee bila kuwahusisha wateja (policy holder). Na mara nyingi uwekezaji
huo unahusisha mambo yaliyokatazwa kama uwekezaji katika riba, maisir na maeneo mengine ya haramu. Katika bima ya
Kiislamu mkataba wa Takaful
unabainisha wapi na namna
ambayo michango itawekezwa.
Na kwa ujumla uwekezaji huo

hautahusisha maeneo yaliyokatazwa kisharia.


Tano, iwapo kampuni ya
bima ya kawaida itavunjwa, akiba (reserves) na ziada (surplus)
zinamilikiwa na wanahisa wa
kampuni hiyo. Lakini katika
bima ya kiislamu akiba na ziada
endapo kampuni ya bima itavunjwa hurudishwa kwa washiriki wa Takaful (policy holders) au hutolewa kama sadaka.
Wanazuoni wengi wanapendlea
zaidi kutoa kama sadaka.
Sita, kampuni ya bima ya Kiislamu ina jukumu la ziada la
kulipa zakat kila mwaka, tofauti
za kampuni za kawaida ambazo
hazilazimiki kulipa zaka.
jakham@rocketmail.com
+255713 996 031

bima ni
utaratibu wa
kundi la watu
wenye maslahi
ya pamoja
kudhaminiana
au kujilinda
kwa pamoja
kutokana
na majanga
fulani kwa
kuunda mfuko
maalumu
unaochangiwa
kutoka katika
rasilimali zao

Watu maarufu wasiokuwa Waislamu wasemavyo kuhusu Uislamu


Dr.
Maurice
Bucaille

How could a man, from being illiterate, become the most important
author, in terms of literary merits, in the whole of Arabic literature?
How could he then pronounce truths of a scientific nature that no other
human being could possibly have developed at that time?
Tafsiri: Inawezekanaje mwanadamu kutoka hali ya kutokujua kusoma na kuandika awe mwandishi muhimu kuliko wote kwa mujibu wa sifa za kitaaluma katika fasihi yote ya kiarabu? Inawezekanaje wakati huo kutamka hakika za kisayansi ambazo hakuna mwanadamu mwingine angeweza
kuzivumbua zama hizo?. (The Bible, the Quran and Science, 1978, p 125)

14
Sheikh Mohammad Issa

Choma moto
majahazi. Ilikuwa
ni amri kwa
Waislamu kutoka
kwa kamanda
wa majeshi
yaliyovuka
bahari ya
Mediterania kwa
lengo la kuiteka
Hispania au
Andalusia kama
inavyojulikana
katika historia ya
Uislamu.
Hatua hii ilifuatia mapambano
ya miaka mingi kati ya majeshi ya
watawala wa Andalusia enzi hizo
na yale ya Waislamu kutoka Magharibi na Kaskazini mwa Afrika.
Waislamu walivuka bahari kuiteka Andalusia ili kuzuia mashambulizi mapya dhidi yao.
Tariq bin Ziyad alikuwa amefaulu kutia nanga mahali penye
milima paitwapo Jabal Tariq
(Mlima wa Twaariq) hivi leo kwa
kumbukumbu ya jina lake. Kuficha historia hii iliyotukuka ya
Waislamu, wazungu wakapaita
Gilbrater.
Huo ulikuwa mwaka 711 Miladia sawa na mwaka wa 92 Hijriya, enzi za utawala wa bani
Umayya uliotawala dola kubwa ya
Kiislamu kutokea Damascus
(Dameshqi) nchini Syria. Kilikuwa ni kipindi cha dola ya Kiislamu kupanuka hadi China na India.
Mara tu baada ya majahazi yaliyowabeba Waislamu kutia nanga,
walijikuta wakikabiliwa na jeshi
kubwa la maadui zao. Tariq bin
Ziyad akaona dalili za hofu toka
kwa wapiganaji wake. Hapo ndipo
Tariq bin Ziyad alipofikia maamuzi yake ya kuchoma moto majahazi waliyotumia kuvuka bahari
na kila kilichomo ndani yake.
Baada ya hapo, Tariq bin Ziyad
akatoa hutba kali yenye mguso wa
aina yake kwa kusema: Ndugu
zangu katika imani, tuko hapa
kulieneza neno la Allah. Maadui
wako mbele yenu na bahari nyuma yenu. Na hamna chakula wala
maji ila kile mtakachokiteka kutoka kwa maadui zenu kwa panga
zenu. Kwa hiyo hapa ni aidha ushindi au kufa shahidi.
Allahu akbar! Hiki kilikuwa
kilele cha kumtegemea Allah na
azma ya kupigana kwa ajili yake
kilichooneshwa na Tariq bin Ziyad. Kwa wapiganaji katika jeshi
lake, kuitii amri ya kamanda wao
kuyachoma moto majahazi yenye
kila kitu chao kilikuwa kilele cha
utii.
Tariq bin Ziyad alikuwa mtu
wa kabila la Ulhasa katika waberiberi (Berbers) aliyeingia katika
Uislamu kutoka nchini Algeria.

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

makala

www.islamicftz.org

Tariq bin Ziyad:

Shujaa wa Kiislamu aliyeiteka

Mlima aliotia nanga chini yake Tariq bin Ziyad.

Awali alikuwa mtumwa na aliposilimu akaachwa huru na bwana


wake. Huyu ndiye mtu aliyeiteka
Andalusia (Hispania) na kuupeleka Uislamu Ulaya.
Watu kama Tariq bin Ziyad,
waliokuwa watu duni kabla ya
Uislamu lakini wakapata hadhi
kubwa baada ya kusilimu ni wengi. Miongoni mwao ni Salman Al
-Farsi, Bilal bin Rabbah na Zayd
bin Al-Haaritha (Allah awe radhi
nao wote).
Jemadari wa majeshi ya Waislamu, Kaskazini mwa Afrika
alikuwa Musa bin Nusair, mmoja
wa majemadari mahiri wa Kiislamu. Tariq bin Ziyad alivuka bahari
akiwa na wanajeshi 300 waarabu
na waberiberi 10,000 waliosilimu.
Mfalme Roderic wa Andalusia
aliwakabili akiwa na askari
100,000 dhidi ya Waislamu
10,300. Ni wazi lazima waliokuwa
katika jeshi la Waislamu wawe na
hofu ya kuteketezwa na jeshi
kubwa lakini imani yao kwa Allah

iliwapa utulivu.
Tariq bin Ziyad akamuomba
Jemadari Musa bin Nusair
nyongeza ya wapiganaji na akamtumia wapiganaji 7,000 chini ya
kamanda Taarif bin Maalik Naqiy
ambaye mji wa Tarifa nchini Hispania leo unabeba jina lake.
Kabla Taarif na jeshi lake
hajafikia Waislamu, vita vikaanza
na Waislamu wakawakabili maadui kishujaa. Majeshi mawili, lile
la Waislamu na lile la makafiri
yakakabiliana katika vita vya
Guadalete ambapo Mfalme Roderic alishindwa na kuuawa mwe-

zi 28 Ramadhan mwaka 92 Hijriya.


Je s h i l a Wa h i s p a n i a l i liloshindwa likarejea nyuma
kuelekea makao makuu ya dola
mjini Toledo. Tariq bin Ziyad akaligawa jeshi lake vikosi vinne.
Kikosi kimoja kikalekea mji wa
Cordoba (Qurtuubah) na kuuteka.
Kikosi cha pili kikaelekea mji
wa Murcia na kuuteka na cha tatu
kilielekea mji wa Zaragoza. Kamanda Tariq bin Ziyad mwenyewe
alielekea Toledo, wakazi wake
wakajisalimisha pasina kupigana

Vituo na vyuo vya elimu


vikafunguliwa huko Toledo na
Cordoba na yeyote aliruhusiwa
kuchukua elimu bure. Magwiji
wa elimu za hisabati, jiografia,
kemia, baiolojia na unajimu
wakazalishwa kutoka vyuo
vikuu huko Toledo na Cordoba

ikawa mwisho wa Mfalme Roderic.


Baada ya kupata habari za ushindi wa Waislamu, Jemadari
Musa bin Nusair akafanya haraka
kwenda kuongeza nguvu ili maadui wasije kujikusanya akiwa na
wapiganaji 18,000. Majeshi ya
Waislamu kwa muda mfupi
yakateka theluthi mbili ya ghuba
ya Iberia.
Miji ya Zaragoza, Barcelona na
sehemu ya Ureno ikaangukia
mikononi mwa Waislamu. Mwaka uliofuata Waislamu wakavuka
mto Pyrenees na kuingia mji wa
Lyons nchini Ufaransa.
Huo ukawa mwanzo wa dola ya
Bani Umayya ya Magharibi chini
ya Khalifa Walid bin , dola iliyotawala Hispania (Andalusia) kwa
miaka 750 tangu mwaka 711 hadi
1492 Waislamu walipotimuliwa
Hispania katika vita ya msalaba
iliyoitwa, November Crusade.
Kasi ya majeshi ya Waislamu
chini ya Tariq bin Ziyad kuteka ardhi ya Andalusia na Waislamu ku-

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

15

www.islamicftz.org

Hispania
fanikiwa kuikalia kwa miaka 750 inaingia katika historia ya vita duniani zama za kati.
Athari ya utawala wa Kiislamu Hispania
Kabla ya Waislamu kuingia Hispania, watawala
wake walikuwa watu kutoka nchi za Skandnavia waitwao Visigoths. Mnamo karne ya tano Miladiya, hawa
Visigoths waliiteka Hispania na kuweka utawala wao
mji mkuu ukiwa Toledo.
Kwa kuwa hawakuwa wastaarabu wajuzi wa kutawala, walikaribisha Kanisa la Roma mwaka 565
kuendesha mambo ya utawala. Kanisa likapata kibali
cha kueneza Ukristo na kukusanya kodi.
Watu wakawa katika tabu kubwa, wakilipa kodi
mara mbili moja kwa watawala na nyingine kwa kanisa.
Kulikuwa na Wayahudi wengi Hispania, kipindi cha
watawala Waislamu Wayahudi waklipata mateso
makubwa sana.
Kwanza walinyimwa haki ya kumiliki ardhi na pili
walikatazwa kuabudu kwa dini yao ya kiyahudi. Walipojaribu kupinga hali hiyo, kanisa likawapa mateso zaidi.
Mwaka 707 Mfalme Vietza alipoonesha kuwahurumia Wayahudi, viongozi wa kanisa walimpindua na
kumweka madarakani Mfalme Rodriguez. Wayahudi
wanaume wakatiwa utumwani na wanawake wao kufanywa masuaria majumbani.
Utawala wa haki wa Waislamu
Mara baada ya Waislamu kuiteka Andalusia (Hispania), haki ikatawala. Hakuna mali ya wenyeji iliyotaifishwa. Waislamu waliwatendea watu wote kwa haki,
wakiwemo Wayahudi, isipokuwa waliweka mfumo wa
kodi wenye uadilifu ambapo waliolipa ni wenye uwezo
tu.
Wakiongozwa na Quran na Sunna ya Mtume (Rehma na amani iwe juu yake), Waislamu waliingiza ustaarabu wa Kiislamu Ulaya na popote majeshi ya Waislamu yalipokwenda yalipokelewa kwa mikono miwili
na wakazi wa maeneo hayo.
Utawala wa Waislamu ukafanya Hispania kuwa nchi
ya kistaarabu iliyojaa haki, uadilifu na elimu. Mtumwa
yeyote aliyeingia katika Uislamu aliachwa huru mara
moja. Idadi kubwa ya wahispani awakaingia katika dini
ya Uislamu. Watu wa dini mbali mbali wakiwemo Waislamu na Wayahudi waliruhusiwa uhuru wa kuabudu
kwa mujibu wa dini zao. Siyo hivyo tu kila mwenye
elimu, ujuzi na maarifa aliruhusiwa kupata ajira katika
kuhudumia jamii.
Vituo na vyuo vya elimu vikafunguliwa huko Toledo
na Cordoba na yeyote aliruhusiwa kuchukua elimu
bure. Magwiji wa elimu za hisabati, jiografia, kemia,
baiolojia na unajimu wakazalishwa kutoka vyuo vikuu
huko Toledo na Cordoba.
Chini ya Waislamu, Hispania ikawa alama ya sayansi, utamaduni na ustaarabu katikati ya Ulaya iliyokuwa
katika zama zijulikanazo kama zama za giza. Mirefeji ya
maji ilichimbwa, mazao mapya yakaingizwa na kuinua
uchumi wa Hispania.
Miji ikakuwa na idadi ya wakazi kuongezeka. Mji wa
Cordoba ukawa kitovu cha elimu Ulaya nzima na hadi
kufikia karne ya 10 Miladiya, mji huo ulikuwa na wakazi
wapatao Milioni moja yaani Manispaa.
Mwanahistoria mmoja Mkristo anaandika: Waislamu walianzisha ufalme ule wa Cordoba uliokuwa fahari
ya enzi za zama za kati, zama ambazo wakati Ulaya nzima ilikuwa imezama katika ujinga na vurugu, mji huo
ulikuwa nuru ya elimu na ustaarabu ikiuangazia ulimwengu wa magharibi.
Khalifa Walid bin bin Marwaan aliwaalika Jemadari
Musa bin Nusair na Tariq bin Ziyad mjini Damascus.
Lakini walipofika walimkuta akiwa mahututi. Aliwashukuru na kuwapa sehemu ya mali waliyoileta
kutoka katika mapato waliyokusanya.
Khalifa Walid alipofariki, Suleiman bin Abdulmalik
akamfuatia katika utawala. Tariq bin Ziyad alifariki
mwaka 720 Miladia. Historia ya Uislamu na ulimwengu haiwezi kamwe kumsahau Tariq bin Ziyad.

Kuelekea uchaguzi mkuu na tatizo la maradhi ya nafsi - (5)


kuelekea
uchaguzi

Kuaminiana na 2015
kuepuka khiana
Na Iddi Jengo

Oktoba 25, itakuwa ni


siku muhimu kwetu kama
Watanzania. Ukihesabu
kuanzia siku ya kutoka toleo
hili Oktoba 19, zimebaki siku
6, kabla ya siku ya uchaguzi.
Moja ya mambo ynayojadiliwa sana ni namna wananachi tunavyotakiwa kushiriki
siku hiyo.
Katika mambo yanayohusu ushiriki wetu ni lile la je
watu wabaki vituoni mara
baada ya kupiga kura au la.
Mpaka naandika makala
haya, msimamo wa Tume ya
Uchaguzi (NEC) ni kuwa kila
mwanachi arejee nyumbani
kwake mara tu baada ya kupiga kura, akisubiri taarifa za
matokeo.
Hata hivyo, sheria kwa
upande mwingine inasema
mtu atatakiwa kuwa umbali
wa takriban mita mia mbili
(kiufupi ni kwamba asiwepo
jirani na eneo/kituo cha kupigia kura).
Ukitazama kwa makini,
jambo moja utakaloligundua
ni kuwa sisi wanajamii, kutokana na matukio yanayojitokeza na namna tunavyoishi, kuaminiana hakuko
miongoni mwetu. Pia, jambo
la pili utakaloligundua ni
kuwa kumekuwa na kutawala kwa khiyana miongoni
mwetu.
Jamii yoyote ikifika hapo,
ikakosa kuaminiana, jua

kuwa inaelekea kuangamia


kuliko kubaya sana. Bahati
mbaya inayotukabili ni kuwa
si jambo rahisi kujenga kuaminiana ndani ya kipindi
hiki kifupi kabla ya uchaguzi
kwa sababu tabia hizi mbili
zinafunzwa, zinajengwa na
zinalindwa zisiharibike
miongoni mwa wanajamii.
Kwa bahati mbaya, katika
jamii zetu hatuna mlezi wa
kudumu wa kuzifunza na
kuzisimamia tabia hizi.
Kutokana na kukosekana
kwa mlezi katika jamii yetu,
haya yanayotokea hayashangazi.
Mazao yoyote tunayoyaona ikiwemo hii hali ya kukosa
mlezi wa kujenga na kufundisha uaminifu, ni sisi
wanajamii na viongozi wetu
ndio tulioyapanda. Kama tunavyokariri mara kwa mara,
maradhi haya ya nafsi huwa
hayaishii kummaliza mtu
mmoja bali huwa yanaua kizazi na kizazi.
Kimsingi, hisia ya kua-

miniana ni msingi wa jamii


iliyo nzima na iliyo imara
jamii. Jamii inaweza kuwa na
furaha pindi tu mizizi ya uaminifu inapoimarishwa
barabara miongoni mwa wanajamii. Lakini watu wanapokiuka misingi hiyo na
wakaipa khiyana kipaumbele
basi jamii hiyo huingia katika
migogoro isiyo na msingi.
Kuna kanuni zinazo ratibu vipengele vyote vya maisha ya wanadamu. Na kila
umuonaye anao mchango
katika kanuni hizo kwa kuwajibika kwake kiakili, kimaumbile, kiimani, kidini,
kikabila na kinamna yeyote
ile. Kimaumbile, binadamu
hana budi ila kuishi na wanajamii wenzake na kwa kuwa
huwa pana wajibu na haki ya
kutekelezeana baina ya wanajamii, binadamu hulazimika kufuata utaratibu wa
sheria ili kuhifadhi mfumo
wa jamii kutokana na machafuko na matatizo.
Kuishi huko kwa ushiriki-

Hata hivyo, sheria kwa


upande mwingine inasema
mtu atatakiwa kuwa umbali
wa takriban mita mia mbili
(kiufupi ni kwamba asiwepo
jirani na eneo/kituo cha
kupigia kura)

ano baina ya wanajamii kunarahisisha kupatikana kwa


njia ya ufumbuzi wa matatizo
yao. Mwanadamu anapenda
kupata ufanisi na mafanikio
bila ya kutaabika kwa kuwa
ni sifa yake ya kiasili, lakini ni
lazima tufahamu kwamba
raha haipatikani ila kwa
kutekeleza wajibu kama walivyosema wahenga: Raha ni
malipo ya kutekeleza wajibu.
Katika kuyaendea maisha
kwa namna iliyo nzuri, hatuwezi kuishi bila kuwa na viongozi wanaosimamia
mambo yetu. Viongozi hao
watakuwa daraja baina yetu
na tusioweza kuwafikia pasi
na kusahau kuwa wao ndio
tutawateua kusimamia rasilimali zetu kwa uadilifu.
Kwa bahati mbaya, baadhi ya wasimamizi wetu
huwa wanatuthamini sisi tunaowapa dhamana kipindi
cha uchaguzi. Mara tu baada
ya kuwachagua, wao hawawi
daraja tena la kutuunganisha
bali wao ndio huwa wapitaji
na sisi raia tunabaki kuwashangaa tukisubiri kipindi
kingine cha kubembelezwa.

16

makala

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

www.islamicftz.org

Na Yusuph Amin

ugha ya vitendo ina nguvu zaidi kuliko maneno. Maana yake ni kwamba
vitendo vina nguvu zaidi ya maneno.
Na hii ni njia bora zaidi ya ulinganiaji
dini kwani Mtume Muhammad (Rehma na
amani ya Allah ziwe juu yake alikuwa mbora
wa tabia (Husnul Khuluuq).
Tabia njema ni kati ya sifa muhimu zaidi
ambazo hupelekea kuibuka mahaba katika
mahusiano ya kijamii.Tabia njema pia ndio
silaha aliyoitumia Mtume (Rehma na amani
ya Allah ziwe juu yake) katika kulingania
jambo lililopekea hata wasiokuwa Waislamu
kuvutiwa na mwenendo wake na hatimae
kusilimu.
Kulithibisha hilo ni pale Allah Taala anaposema: Basi ni kwa sababu ya rehema
itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndio umekuwa laini kwao. Na lau ungelikuwa mkali,
mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangelikukimbia (3:159).
Hata hivyo jambo linalosikikitisha katika
zama tulizonazo ni kushuhudia baadhi ya
Waislamu kutosheka kwa kuwa na majina
mazuri ya Kiislamu na kudhani majina yao
yatawapa mafanikio pasipo kutendea kazi
mambo yaliyoamrishwa na dini na mbaya
zaidi ni kujenga matumaini ya kupata malipo
mema akhera bila kufanya kheri yeyote hapa
duniani.
Kimsingi, mafanikio na ubora wa mwanadamu hutokana na maadili na tabia njema
na kinyume chake ni kwamba, jamii ambayo
huwa haina maadili na kuwa mbali na mafundisho ya dini huwa katika mkondo wa
kuangamia kimaadili.
Tafiti mbalimbali zinaonesha kuporomoka na kuangamia kwa mataifa mengi
duniani hakutokani tu na migogoro ya
kijeshi, kisiasa au kiuchumi bali hutokana na
kutoweka kwa maadili bora. Kwa maana nyingine naweza kusema misukosuko katika
misingi ya kimaadili ni mambo ambayo
huangamiza jamii kuliko uharibifu unaosababishwa na majanga ya asili kama vile matetemeko ya ardhi.
Samuel Smiles, mwandishi maarufu wa
Uingereza aliwahi kuandika: Ustawi na upungufu wowote katika maisha unatokana na
nguvu za dhati na uwezo wa kifikra au kimaumbile wa mwanaadamu. Ukweli ni
kuwa mafanikio na ufanisi wa mtu kwa kiasi
kikubwa hutegemea maadili bora na ukarimu wao kwa wengine.
Kutokana na Uislamu kutofautiana na
dini nyingine katika kipengele cha maadili na
tabia njema, taarifa za miaka ya hivi karibuni
zinaonesha idadi isiyowahi kutokea ya
Waingereza, takribani wote wakiwa ni wanawake, wanaingia kwa wingi katika Uislamu katika kipindi ambacho kuna migawanyiko mikubwa kabisa ndani ya makanisa ya
Anglikana na Katoliki.
Tathmini ya mabadiliko haya imesababisha kutabiriwa kuwa Uislamu utakuwa kwa
haraka sana na kuja kuwa dini kubwa yenye
nguvu katika nchi hii ya Uingereza.
Katika kipindi cha miaka 20 ijayo, idadi
ya Waingereza watakaosilimu italingana au
itashinda idadi ya jamii ya wahamiaji wa Kiislamu walioleta dini hii hapa nchini, alisemaRose Kendrick, ambaye ni mwalimu wa
mafunzo ya dini katika shule maalum ya Hull
na mtunzi wa kitabu cha kiada cha muongozo wa Quran.
Anasema: Uislamu ni dini kubwa duniani kama ilivyo kwa kanisa la Katoliki. Hakuna mtu anayeweza kudai kuwa dini husika ni
mali yake. Uislam pia unaenea kwa kasi
kubwa katika bara hili na Amerika kwa
ujumla.
Katika makala hii nitaangazia jinsi Uislamu unavyomtaka Muislamu kujikita na tabia
njema ambayo ni nguzo muhimu katika
kuendeleza Uislamu kwani Quran inatueleza
jinsi tabia ya mtume rehema na amani ya Al-

Ulinganiaji bora ni

matendo yetu mema


lah ziwe juu yake ilivyosaidia kueneza na kuz- alikuwa mtumishi wa Mtume wa Mwenyezi
ivuta nyoyo za watu katika kuukubali Uisla- Mungu na mara zote alikuwa akizungumza
mu.
kuhusu tabia njema ya Mtume.
Kabla ya kusonga mbele zaidi tunapaswa
Katika kipindi cha miaka 10 ya utumishi
kufahamu kuwa tabia njema na upole ni za- nyumbani kwa Mtume Muhammad (Rehma
wadi toka kwa Allah Taala kwani hizo ni kati- na amani ya Allah ziwe juu yake) alipata faka sifa zake hivyo tunapaswa kushikamana hari kubwa ya kumhudumia Mtume na katinazo hivyo wale wenye mioyo migumu ni ka kipindi hicho kamwe hakuona uso wake
vema wakadhibiti nafsi zao kwa kuwa wak- ukiwa umekunjika na hata wakati alipoiendelea kufanya hivyo
tendewa vitendo vya kidhawawezi kuwavuta
halimu hakuwahi kuvuta
Kutokana
watu katika jambo lolote
nyusi zake wala kutumia
na Uislamu
la mashauriano juu ya
nguvu.
kutofautiana
mambo muhimu.
Dini ya Kiislamu, daina dini nyingine ma imekuwa ikiwataka
Ukipitia historia ya
maisha ya Mtume (Reh- katika kipengele wafuasi wake waishi kwa
ma na amani ya Allah
upole, ukarimu na kujencha maadili na
ziwe juu yake), tunaweza
ga mahusiano mema na
tabia njema,
kupata mifano bora ya
watu wa jamii au dini nykuigwa katika maana nz- taarifa za miaka ingine. Tabia ya Mtume
ima ya tabia njema na
ya hivi karibuni (Rehma na amani ya Almaadili kwa mujibu wa
lah ziwe juu yake) ni
zinaonesha
Uislamu.
muhimu katika kuendeidadi isiyowahi
Mtume Muhammad
lea kwa Uislamu kutokakutokea ya
(Rehma na amani ya Alna na kukubaliana na
lah ziwe juu yake) pamoja
maumbile ya mwanadaWaingereza,
na kuwa alikuwa akimu na ndio maana
takribani
himiza tabia njema pia
Mtumekwakiasikikubwa
wote wakiwa
binafsi alikuwa mstari wa
alijipamba na mazunni wanawake,
mbele kutekeleza kwa vigumzo ya bashasha na
tendo mambo yote aliywanaingia kwa hakuwaponda maadui
okuwa akiwafahamisha
zake na aliwaheshimu.
wingi katika
watu na kutaka wayaige
Katika historia ya UisUislamu
kutoka kwake.
lamu tumeweza kushHakika Mtume (Rehma na amani ya Al- uhudia visa mbali mbali vya tabia njema ya
lah ziwe juu yake) katika kila nyanja ya mai- Mtume (Rehma na amani ya Allah ziwe juu
sha yake amejawa na tabia njema kama ana- yake). Mfano, ukiaangalia mitume na manavyosifiwa katika Quran pale Allah Taala ana- bii wote wa Allah walitumwa duniani kwa
posema: Na kwa hakika wewe (Muham- ajili ya kuwaita watu na kuwafundisha nammad) una tabia njema (68:4).
na ya kutimiza jukumu waliloumbwa kwalo
Pia swahaba Anas Bin Malik ambaye nalo ni kumuabudu Allah wakifanya kazi

hiyo kwa upole na lugha ya laini. Shughuli nyingi za kilinganiaji hazina budi kufungamana
na tabia njema kwa walinganiaji wake na
ndio maana nasema vitendo vina nguvu zaidi
kuliko maneno. Bahati mbaya wengi tumekosa hili. Kusema usichokitenda ni katika
hatari iliyo kubwa mbele ya Allah Taala anaposema: Enyi mlio amini! Kwa nini mnasema msiyo yatenda? (61:2).
Licha ya kuwa ni dini iliyosheheni desturi
zinazokubaliana na akili na kumpa mtu uongofu unaoupa nuru moyo, Uislamu pia ni dini
inayobeba maendeleo yanayofaa kwa hali,
mahala na zama zote na kwamba sheria yake
(sharia) inakidhi hali na mahitaji yote ya jamii
katika nyanja zote za maisha lakini haya yote
yamekosa mashiko kuokana na wengi wetu
kuwa wazungumzaji bila kuonesha matendo
ya kile tunachokizungumza.
Ukweli ni kwamba, maadili yetu na sheria
vimepoteza chanzo pekee cha nguvu yake,
yaani dini. Hii imetokana na jamii ya Kiislamu kuthamini na kutukuza tamaduni za nchi
za kimagharibi jambo linalopelekea watu wa
baadhi ya jamii ya Kiislamu hususan vijana
wa kike na kiume kuathirika zaidi na wimbi
hili la umagharibi.
Nimalizie kwa kusema Waislamu makini
wanafahamu kuwa propaganda dhidi ya
sharia za Kiislamu kama mauaji yanayotekelezwa na makundi ya kigaidi kama IS na
Boko Haraam si chochote bali ni udanganyifu wa nchi za Magharibi. Hivyo, katika kuuthibitisha ulimwengu kuwa Uislamu ni dini
ya maadili na tabia njema hatuna budi kuiga
mazuri yaliyofundishwa na Uislamu na si
vinginevyo.
Kwa mtazamo wa watu wenye busara kuzidisha vitendo vinavyoashiria tabia njema za
Uislamu ni bora zaidi kuliko hata mazungumzo ya muda mrefu yahusuyo dini kwani
ukiangalia riwaya mbalimbali utagundua
kuwa Mtume (Rehma na amani ya Allah
ziwe juu yake) alitenda wema kwa ubaya hata
kwa wasio Waislamu walipomkosea jambo
lililopekea wengi wao kuukubali Uislamu.
Jambo la muhimu ni kushikamana na
matendo mema yaliyoamrishwa na dini
kwani tukifanya hivyo hata wale wanaopandikiza mbegu za chuki juu ya Uislamu
watakosa hila na mbinu chafu katika kuupiga
vita Uislamu na Waislamu hivyo kudidimiza
azma yao.

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

makala

www.islamicftz.org

IDDI jengo

atika muendelezo
wa makala zetu, leo
tunaanza kuutafiti
Uislamu katika sura
yake halisi na namna wenyewe
unavyojieleza. Kwanza, ninukuu maneno ya msomi wa kimagharibi ambaye sasa ni Muislamu safi, bwana Hofman
Murad aliyejaribu kuuelezea
Uislamu.
Murad alisema: Nilianza
kuuona Uislamu kupitia macho yake yenyewe (Uislamu)
imani iliyokuwa haijapotoshwa, imani nzuri ya kuamini mungu mmoja na
atakaye baki kuwa mmoja,
ambaye Yeye ni wa pekee, ambaye ndiye Mkusudiwa, ambaye hakuzaa wala hakuzaliwa, wala hana anayefanana
naye hata mmoja ukilinganisha na miungu ya kikabila,
kimila na utatu.
Murad anaendelea: Quran
imenionesha mwono ambao
uliokuwa rahisi kuonekana na
kueleweka. Taarifa za kiasili za
Quran, mafundisho yake
yenye maadili zilinivutia sana
na kuwa ndio kitu kizuri na
bora kama dhahabu. Hivyo
hakukuwa na nafasi ya kunishawishi nisiamini ukweli wa
utume wa Muhammad. Wale
wanaouelewa uasili wa mwanaadamu hawawezi
kushindwa kuamini hekima
isiyo na mwisho aliyopatiwa
b i n a d a m u k u t o k a kw a
Mwenyezi Mungu katika njia
ya Quran.
Huo ni ushuhuda wa Murad, msomi mkubwa na mwanadiplomasia aliyeshika nafasi
nyingi. Kimsingi Uislamu ni
dini sahihi pekee inayostahiki
kuwa chaguo la kila mwanadamu mwenye akili timamu
kwa sababu zilizo wazi.
Kwanza, Uislamu ni dini ya
Mwenyezi Mungu, aliyemuumba mwanadamu kwa lengo
maalumu. Ni muumba pekee
anayejua mahitajio halisi ya
mwanadamu na ni yeye pekee
anayejua njia sahihi ya kumfikisha mwanadamu kwenye
lengo lake la maisha kwa ushahidi wa Quran.
Allah Taala anasema: Bila
ya shaka dini mbele ya
Mwenyezi Mungu ni Uislamu.
Na w a l i o p e w a k i t a b u
hawakukhitalifiana ila baada
ya kuwajia ujuzi, kwa sababu
ya uhasidi ulio kuwa baina
yao. Na anayezikataa Ishara za
Mwenyezi Mungu basi hakika
Mwenyezi Mungu ni Mwepesi
wa kuhisabu. Na pindi
wakikuhoji, basi sema: Mimi
nimeusalimisha uso wangu
kumwelekea Mwenyezi Mungu, na kadhaalika walio nifuata. Na waambie walio pewa
Kitabu na wasio na kisomo:
Je! Mmesilimu? Wakisilimu
basi wameongoka. Na
wakikengeuka basi juu yako ni
kufikisha ujumbe tu. Na
Mwenyezi Mungu ni Mwenye
kuwaona waja wake (3:19-

17

Asili yetu ni dini ya asili (7)

Kwa nini Uislamu ni dini ya asili?

20).Allah Taala anaendelea


kutia msisitizo katika kitabu
chake kitukufu: Hakika ni
juu yetu kuonyesha uwongofu
(njia sahihi). Na hakika ni yetu
Sisi Akhera na dunia. Basi nakuonyeni na Moto unao
waka! (92:12-14)
Pili, Uislamu ndio dini pekee inayotosheleza kwa ukamilifu vipengele vyote vya sifa
za dini sahihi. Hii ni kwa sababu Uislamu unaeleza ukweli
juu ya Muumba na nafasi ya
mwanadamu hapa ulimwenguni.
Uislamu unatufahamisha
kuwa ulimwengu huu na vote
vilivyomo umeumbwa na Allah taala kwa lengo maalum,
na kwa lengo hilo ndo hukumu itapitishwa juu yake, juu
ya kulipwa kheri ama shari juu
ya yale yote aliyoyafanya.
Katika Quran tuanaelezwa
kwamba mwanadamu
ameumbwa kwa lengo la kumtumikia Allah Taala : Nami
sikuwaumba majini na watu
ila waniabudu Mimi. Na sitaki
kwao riziki, wala sitaki wanilishe. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku,
Mwenye nguvu, Madhubuti
(51:56-58).
Na msistizo mwingine juu
ya lengo la kuumbwa adamu
kama ndio amri kuu linaelezwa katika Quran 98:5
isemayo: Nao hawakuam-

Uislamu
ni dini ya
kusimamia
haki, usawa
na uadilifu
katika jamii.
Miongoni
mwa mambo
yanayo
vuruga
amani
ulimwenguni
ni kuwepo
kwa dhulma
katika jamii
na dhulma
haiondoki
mpaka haki
iwepo katika
jamii

rishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia dini,


wawe waongofu, na washike Sala, na
watoe Zaka. Na hiyo ndiyo dini madhubuti.
Si lengo la kuumbwa mwanadamu pekee ndio limeelezwa ndani ya
Quran bali lengo la kuumbwa ulimwengu na vote vilivyomo pia
limeelezwa kwa ukamilifu wake katika Sura 2:29: Yeye ndiye aliyekuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi. Tena akazielekea mbingu, na
akazifanya mbingu saba. Naye ndiye
Mjuzi wa kila kitu.
Uislamu ni dini ya kusimamia
haki, usawa na uadilifu katika jamii.
Miongoni mwa mambo yanayovuruga amani ulimwenguni ni kuwepo
kwa dhulma katika jamii na dhulma
haiondoki mpaka haki iwepo katika
jamii.
Dini zote zilizoundwa na watu
ziko pale kustawisha dhulma katika
jamii matajiri na wenye hadhi
huwakandamiza raia masikini na
wanyonge. Uislamu ndio dini pekee
inayoweza kumkomboa mwanadamu kutokana na dhulma zote. Moja
ya masharti manne ya kusimamisha
Uislamu ni kusimamia haki.
Allah anasema katika Quran:
Naapa kwa Zama! Hakika binaadamu bila ya shaka yumo katika
khasara, Ila wale walio amini, na
wakatenda mema, na wakausiana
kwa haki, na wakausiana kusubiri
(103:1-3).
Aya hizo kwa ufupi zinatufahamisha kuwa Uislamu utasimama kwa

mtu binafsi na kwa jamii kwa ujumla


iwapo mambo manne yatatekelezwa
kwa pamoja na kwa ukamilifu
ikiwemo , kuamini, kutenda mema,
kuusiana kusimamisha haki na kuusiana kufanya subira.
Uislamu ni dini ya walimwengu
wote wa nyakati zote, ndio dini pekee inayofuatwa na walimwengu
wote wa sehemu zote na wa nyakati
zote na ndio dini inayokua kwa kasi
ulimwenguni.
Msomi mmoja, Jeremy Rifkin alisema: .Uislamu ndio dini ikuayo
kwa kasi zaidi duniani. Wanatakwimu wanatabiri kwamba katika
kila watu wanne, mmoja atakuwa
Muislamu miaka 24 ijayo. Kama
takwimu ni nguvu basi tujue dunia
inaegemea kwenye karne ya Waislam.
Kuhusu hilo, Allah anatukumbusha: Amekuamrisheni dini ile ile aliyomuusia Nuhu na tulio kufunulia
wewe, na tuliyowausia Ibrahim na
Musa na Isa, kwamba shikeni nini
wala msifarikiane kwayo. Ni magumu kwa washirikina hayo unayowaitia. Mwenyezi Mungu humteua
kwake amtakaye, na humwongoa
kwake aelekeaye.
Katika aya inayofuatia hiyo: Na
hawakufarikiana ila baada ya kuwajia ilimu kwa sababu ya husuda iliyo
kuwa baina yao. Na lau kuwa haikwisha tangulia kauli kutoka kwa
Mola wako Mlezi ya kuakhirisha
mpaka muda maalumu, basi bila ya
shaka palingeli hukumiwa baina yao.
Na hakika walio rithishwa Kitabu
baada yao wanakitilia shaka inayo
wahangaisha (42:13-14).
Uislamu ni utaratibu wa maisha
uliokamilika. Ni mfumo unamuelekeza binadamu namna ya kuendesha
kila kipengele cha maisha yake ya kibinafsi na ya kijamii. Ni mfumo ulio
na utaratibu unaozingatia watu
kama walivyo. Kwa kutambua kuwa
mtu anakamilika kwa kuwa na mwili
na roho, Uislamu umeweka utaratibu wa kuustawisha mwili na roho.
Uislamu ni mfumo uliotuwekea
kanuni na sheria zinazotuwezesha
kujenga afya zetu na kukuza utu
(uchamungu) wetu. Pia, kwa kutambua kuwa watu ni viumbe wanaotakiwa waishi kijamii (social beings) na
kutegemeana, Uislamu unatoa
muongozo na kuweka kanuni na
sheria ambazo humuwezesha kila
mtu binafsi na jamii kwa ujumla kuishi maisha ya furaha na amani. Uislamu pia ni mfumo ambao umeweka
mifumo ya kijamii kama vile siasa,
uchumi, utamaduni, na kadhalika
juu ya misingi ya haki na uadilifu.
Katika toleo lijalo tutaanza kuudadisi Uislamu kuujua asili yake
namna ulivyopangwa katika kuratibu maisha ya mwanadamu na kama
alivowahi kuandika bwana Hofman
Murad kwamba, Uislamu ndio
mbadala (Islam the alternative).
Jengokeya5@gmail.com
0714135201

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

18

www.islamicftz.org

darasani wiki hii

Kagimu Mk. (Science teacher) 0752 224 550

GET READY FOR MATHEMATICS

Quran, Sunna rejea yetu; siyo vyombo vya habari


inatoka Uk 20 sababu unaweza
kumuona Muislamu akaamini
lisemwalo na chombo cha mawasiliano hata likiwa na uharamu
ndani yake. Wakati mwingine tunachupa mipaka ya dini ambapo
mtu hufikia kuamini na kufuata
falsafa za kilimwengu ambazo zinapingana na mafundisho ya dini.
Imefikia hatua hata sifa za wake au
waume tunaopaswa kuishi nao katika ndoa tunatengenezewa na kutangaziwa kupitia televisheni, nasi
bila wasiwasi tumekuwa tukikubaliana nazo pasipo kujitambua.
Kuhusiana na hilo, katika hadithi iliyopokelewa na Swahaba
Abu Huraira (Allah amridhie),
Mtume (Rehma na amani ya Allah
ziwe juu yake) amesema: Mwanamke huolewa kwa mambo manne
(4), kwa mali yake, kwa ukoo wake,
kwa uzuri wake na kwa mapenzi
yake ya dini, jishindie kwa kumpata aliyeshika dini, mikono yako itabarikiwa (Bukhari na Muslim).
Pamoja na mafundisho mazuri
ya hadithi hiyo, jamii ya Kiislamu
bado imejikuta ikianguakia pua
kutokana na baadhi yetu kuacha

kufuata mafundisho ya hadithi


pindi wanapotaka kuchagua
mchumba na hatimae kujikuta
wanashindwa kudumu katika
maisha ya ndoa.
Hii ina maana kwamba watu
hubainishiwa sifa za mwanamke
anayefaa kwa ajili ya maisha ya
ndoa kupitia vipindi vya televisheni na mitandao ya inaneti na si kwa
mujibu ya maelekezo ya dini. Hivyo
basi, kwa kuwa televisheni imesema, wengi huamini kilichosemwa
kwa asilimia mia moja.
Sheikh Bin Taymiya (Allah amrehemu) anasema: Ni kitabu tu
kutoka mbinguni kinachoweza kutatua matatizo ya watu. Lau kama
watu wangeachwa kufuata rai zao
basi kila mmoja kati yao bila shaka
angekuwa na rai (yake). Sheikh
Taymiya anaendelea kusema: Kufuata matamanio katika masuala
ya dini ni kubaya zaidi kuliko kufuata mambo mengine ya starehe.
Hiyo ilikuwa ndio hali ya wasioamini miongoni mwa washirikina.
Ni kweli vyombo vya mawasiliano vina athari kubwa katika

muktadha wa kuiongoza au kuipotosha jamii kutokana na nguvu


yake yake ya kufikia kundi kubwa
la watu kwa wakati mmoja. Lakini
hiyo haina maana jamii ipumbazike kwa sababu za ajenda bunifu zitokanazo na fikra huru za kibinadamu.
Pamoja na vipindi bunifu za vyombo vya mawasiliano kulenga
maslahi ya kiuchumi kwa wanaoziandaa lakini pia vipindi hivyo
ni mojawapo ya mikakati ya dini ya
umasonia ambayo inawataka watu
wa dunia kuishi mfumo mmoja
katika kumtumikia shetani.
Katika hili niwakumbushe
Waislamu wanaojihusisha na
vipindi vya televisheni zinazojikita
katika kubuni mitindo ya maisha
ambayo ni kinyume na Uislamu
kujihadhari na adhabu iumizayo
siku ya kiyama kama anavyobainisha Allah Taala: Na atakayechagua
dini isiyokuwa ya Uislamu haitakubaliwa kwake. naye akhera
atakuwa katika wenye kupata
hasara (3:85).
Na kama alivyobainisha
Mtume, (Rehma na amani ya Al-

lah ziwe juu yake): Atakayefanya


kitendo chema katika uislam atapata ujira wake na ujira wa yule
atakayekitenda baada yake bila ya
kupungukiwa thawabu zao.Na
atakayetenda kitendo kibaya katika Uislamu atabeba dhambi zake
na dhambi za yule atakayetenda
wala hapungukiwi kitu katika
dhambi hizo(Muslim).
Hakuna haja kwa jamii ya Kiislamu kuanzisha mijadala kuhusiana na mitindo ya maisha ya kisasa
(modernazitaion) kwani jambo hili
limeleta athari kubwa tangu vyombo vya mawasiliano vikiwemo
televisheni, na mitandao ya intaneti kuwa chanzo cha kuporomoka
kwa maadili ya jamii.
Mtume (Rehma na amani ya
Allah ziwe juu yake) amesema:
Watu watazuka kutoka katika
umma wangu ambao watakuwa
wamejaa matamanio kama
ugonjwa wa kuambukizwa na mnyama unavyozagaa mwili mzima
na kuathiri mishipa na viungo vyote(Abu Dawud).
Kwa bahati, sisi Waislamu tumependelewa na Allah Taala kwa

kuletewa dini ya sawa sawa, isiyo


na shaka ndani yake na kwa sababu hiyo hakuna nafasi kwa akili au
maamuzi yamtu binafsi mbele ya
ushahidi wa maandiko yaliyotokana na Allah Taala na Mtume wake.
Katika kuhitimisha napenda
kutahadharisha jambo ambalo pia
Mtume (Rehma na amani ya Allah
ziwe juu yake0 ametutahadharisha
kupitia hadithi iliyopokelewa na
Swahaba, Jaabir bin Abdullah (Allah awe radhi nae) aliposema:
Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema: Kila mja
atafufuliwa katika hali aliyofia
nayo(Muslim).
Hadithi hii inatoa ishara ya mtu
kufufuliwa kutokana na kile alichokipenda zaidi katika maisha ya
dunia. Swali ni je,ndugu yangu
Muislamu umejiandaaje kwa siku
hiyo hali ya kuwa mtindo wa maisha uliochagua haukubalini na
matakwa ya dini ?
Tunamuomba Allah Taala atujaalie, atuoneshe haki tuweze kuifuata na pia atuoneshe batili tuweze kuiepuka ili kubaki katika radhi zake. Allah ni mjuzi zaidi.

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

matukio katika picha

www.islamicftz.org

19

Mwenyekiti wa taasisi ya The Islamic Foundation (TIF) Aref Nahdi (kushoto) akiwa katika kipindi maalum cha kuhamasisha Amani katika Tv Imaan katikati ya wiki,kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Sheikh Ibrahim Twaha na katikati ni mwendesha kipindi hicho ambaye pia ni Msimamizi Mkuu wa Tv hiyo Sheikh Chembea.

Katibu mkuu wa TIF ustadh Ally Ajirani (kulia) akibadilishana mawazo na


mkurugenzi wa Radio Fadhila iliyopo katika mji wa Conakry nchini Guinea Sheikh
Muhammad Alhaafedh Sow wakati alipotembelea ofisi za TIF mjini Morogoro.

Wanafunzi wa shule ya msingi Jitegemee iliyopo wilayani


Bagamoyo wakipata huduma ya maji katika kisima
kilichochimbwa na TIF.

Mkurugenzi mtendaji wa TIF akijaribu kisima kilichopo makazi ya polisi


Bagamoyo

Mwanafunzi Juma Yasim Kapilimbi


akiwa katika uwanja wa ndege wa
J.K Nyerere akiwa safarini kuelekea
Afrika Kusini kwenda kujiunga na
chuo cha kuhifadhisha Quran,
kilichoko Johannesburg Afrika ya
Kusini.

Mkazi wa kijiji cha Maji Mapana, wilayani Bagamoyo


akichota maji katika moja ya visima vilivyochimbwa na TIF
wilayani humo.

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

20

Tariqwww.islamicftz.org
bin
Ziyad: Shujaa
wa Kiislamu
aliyeiteka

Uk 14
6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

Yusuph Amin

iongoni mwa maafa


yanayoikabili jamii
katika karne tuliyonayo ni watu
kuathiriwa na maudhui yatokanayo na vipindi vya televisheni,
matangazo ya biashara na sinema huku maudhui yatokanayo
na vipindi hivyo yakitumika
kama rejea ya suluhu ya changamoto na matarajio yanayojitokeza katika maisha ya mwanadamu.
Mfumo wa kutegemea vyombo vya mawasiliano kama rejea
umepata umaarufu mkubwa katika nchi za Marekani na Ulaya
ambako vituo fulani vimetenga
vipindi maalum vya muongozo
wa mambo ya kijamii na mengineyo.
Mfumo huo pia umeenea kwa
kasi katika nchi zinazoendelea,
ikiwemo Tanzania, kutokana na
kasi ya maendeleo ya utandawazi
hatua inayopelekea kuwepo kwa
wimbi la vituo maalum vyenye
maudhui pacha na zile za wamagharibi zikiwa na malengo ya
kuelekeza jamii mitindo ya maisha (life styles).
Ingawa katika dini ya Kiislamu ni wajibu kwa mja kufuata
amri za Allah mlezi na Mtume
wake sambamba na kujiepusha
kufuata matamanio ya nafsi,
wapo baadhi wamekiuka hilo
kama ilivyokuwa kwa watu wa
kitabu (Mayahudi na Manaswara) ambao ni wenye kulaaniwa
na Allah Taala.
Amesema Allah Taala: Hawatokuwa radhi Mayahudi na
Manaswara mpaka mfuate mila
yao. Sema: Hakika uongofu wa
Mwenyezi Mungu ndio uongofu.
Na kama ukifuata matamanio
yao baada ya ujuzi ulio kwisha
kujia, hutapata mlinzi wala
msaidizi kwa Mwenyezi Mungu
(2:120).
Wakati tukitafakari mafundisho ya aya hiyo tutambue ya
kuwa mafundisho yanayopatikana kupitia vipindi vya vyombo
vya mawasiliano ambavyo ndio
msingi wa malezi ya jamii ya
wamagharibi yametawaliwa zai-

Quran, Sunna rejea yetu;


siyo vyombo vya habari

di na matamanio ya nafsi na
uharibifu kwani lengo lake ni kutangaza na kueneza vitu vya
anasa kwa sura ya usasa.
Kwa mfano, vipo vipindi maalum vya televisheni na maudhui
katika mitandao ya intaneti vinavyotangaza mitindo ya mavazi ya
kike na kiume isiyokubalika si tu
kwa mujibu wa dini ya Uislamu
bali hata katika tamaduni zetu za
kiafrika. Bahati mbaya ilioje
kuwa jamii imekuwa inaiga
mitindo hiyo ya mavazi kwa

malengo ya kutaka kufanana na


watu fulani maarufu.
Hata hivyo, suala la vyombo
hivyo kugeuka mwalimu wa mifumo ya maisha ya watu halionekani kuwa tishio kwa jamii
kutokana na kuzoeleka. Kwa
sababu hiyo basi, viongozi wa
makundi ya jamii wakiwemo wa
dini wanawajibika kufanya kazi
ya ziada katika kuwaelimisha
wafusi wao kuchuja mambo yasiyofaa tunayoletewa kutokana na
maendeleo ya utandawazi.

Hali ya jamii kutegemea vyombo vya mawasiliano kama rejea


ya maisha badala ya miongozo ya
dini ni ishara ya shetani na
wafuasi wake kushika hatamu ya
kuwaongoza wanadamu katika
njia ya upotovu badala ya ile ya
uongofu iliyoamriwa na mola
wao mlezi.
Maendeleo ya utandawazi pia
yameathiri kwa kiasi kikubwa
jamii ya Kiislamu hasa rika la vijana wa kike na kiume na hakika
tumeshuhudia baadhi yao wakii-

ga mifumo isiyokubaliana kidini


kama ile ya kuchanganyika wanaume na wanawake wakati wa
utekelezaji wa shughuli za kijamii kama vile harusi na misiba
ambayo ni katika mienendo ya
Wamagharibi.
Licha ya Quran na Sunna
kuwa miongozo sahihi katika
maisha ya Waislamu, jambo la
kusikitisha ni kwamba baadhi
yetu tumekuwa na mashaka na
viwili hivyo kwa kukosa yakini.
Na hii ndio inaendelea Uk 18

MOROBEST BUS SERVICE

KWA MAHITAJI YA USAFIRI WA UHAKIKA, SAFIRI NA KAMPUNI YA MABASI YA MORO BEST


KILOMBERO DAR, NA DAR - KILOMBERO
KILOSA DAR, NA DAR - KILOSA
SAFIRI NA MORO BEST KWA SAFARI ZA AMANI, UTULIVU NA UHAKIKA
MORO BEST BUS SERVICE NI KWA AJILI YAKO NA FAMILIA YAKO

hutolewa na kuchapishwa na The Islamic Foundation, P.O.Box 6011 Morogoro, Tanzania E-mail: imaanmedia3@gmail.com

You might also like