You are on page 1of 15

Serikali yaipongeza The Islamic Foundation - Uk 2

huwatoa watu gizani

Museveni awahami Waislamu: Uk 3


ISSN 5618 - N0. 004 BEi: Sh800/- KSH80/- Ush1,200/-

8 Rajab 1436, Jumatatu, mei 4 - 10, 2015

www.islamicftz.org

Operesheni tokomeza
madrasa yaanza
Sheikh Mussa
Kundecha

Hofu yatanda misikitini, madrasa


Walimu, masheikh wawindwa kama paa
Wengine zaidi kukamatwa? - UK 3

IGP Ernest Mangu

Wachache
wajitokeza
hijja 2015
Na Suleiman Magali

asi ya kujisajili kwa ajili


ya Hijja 2015 ni ndogo
kutokana na mwamko
duni wa Waislamu. Kufuatia hali hiyo, taasisi za Hijja zimewahimiza waumini wenye uwezo,
hususan vijana, kujitokeza kushiriki
ibada hiyo.
Tangu 1958, Wizara ya Hijja ya
Saudi Arabia iliitengea Tanzania nafasi 25,000 kila mwaka za mahujaji,
lakini uchache wa mahujaji wanaoenda ulipelekea wizara hiyo kupunguza mgao huo hadi nafasi
3,000. Hata hivyo, kwa mujibu wa
Katibu Mkuu wa
UK 5

Head office, Lumumba Street, Opp: Viwanja vya Mnazi Mmoja, P. O Box 779 Dar es Salaam, Tanzania
Tell: 255 22 2182482/ 255 222184419, Fax: 255 22 2181424, E-mail: info@Binslum.com

15 Rajab 1436, jumatatu May 4 - 10, 2015

habari

Niqab marufuku
Congo Brazaville
Na Mashirika ya
Habari

amlaka nchini
Congo Brazaville
zimepiga marufuku watu kuvaa
mavazi yanayofunika sura zao
yakiwemo ya Kiislamu kama
niqab na burka katika maeneo yenye mikusanyiko ya
watu.

Pia mamlaka hiyo imepiga


marufuku Waislamu kutoka
nje ya nchi hiyo kuacha kutumia misikiti nyakati za usiku.
Maelfu ya watu, wengi wao
wakiwa ni Waislamu wamekumbwa na machafuko katika
nchi jirani ya Jamhuri ya Afrika
ya Kati na wamekuwa wakitumia misikiti kama sehemu ya
malazi yao.
Msemaji wa Serikali alisema

Congo ni nchi isiyofungamana


na dini yoyote na inaheshimu
dini zote, na kuongeza baadhi
ya Waislamu wanawake wamekuwa wakitumia mavazi hayo
kwa ajili ya kufanya matendo ya
kihalifu. Alisema, Serikali imekataza kutumia misikiti wakati
wa usiku kwa sababu ipo kwa
ajili ya ibada na sio malazi. Congo Brazaville ina Waislamu wasiozidi asilimia tano.

www.islamicftz.org

nyakati za swala
Na. MJI
1 DAR ES SALAAM
2 ZANZIBAR
3 TANGA
4 MOROGORO
5 MTWARA
6 ARUSHA
7 DODOMA
8 MBEYA
9 KIGOMA
10 MWANZA
11 KAGERA

FAJR
5:13
5:12
5:12
5:23
5:18
5:22
5:27
5:40
5:48
5:34
5:39

DHUHUR ASR
12:21
3:42
12:20
3:42
12:21
3:43
12:29
3:51
12:21
3:42
12:33
3:55
12:35
3:56
12:45
4:07
12:57
4:19
12:46
4:07
12:51
4:13

MAGHARIB
6:17
6:17
6:19
6:24
6:12
6:33
6:31
6:39
6:55
6:47
6:52

ISHAA
7:24
7:24
7:26
7:31
7:21
7:41
7:39
7:47
8:02
7:54
8:00

Serikali yaipongeza
The Islamic Foundation
Na Mwandishi wetu

erikali ya Mapinduzi ya Zanzibar


(SMZ) kupitia ofisi ya Makamu wa
pili wa Rais imeipongeza taasisi ya
The Islamic Foundation yenye
makao yake makuu mkoani Morogoro kwa
juhudi inazozifanya za kuisaidia Serikali kutoa
huduma mbalimbali kwa jamii.
Pongezi hizo zimetolewa na Afisa Mdhamini Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mkoani, Issa Juma Issa, kufuatia msaada wa taasisi
hiyo kwa wakazi wa kijiji cha Kisiwa Panza kilichopo Kusini Mashariki mwa mkoa wa Mkoani, katika kisiwa cha Pemba ambao walikumbwa na kimbunga kikali kilichosababisha
maafa makubwa, ikiwemo nyumba
kubomoka.
Misada hiyo yenye thamani ya zaidi ya Tsh.
Milioni 12, ilikabidhiwa kwa waathirika na

ujumbe wa The Islamic Foundation ulioongozwa na katibu wa taasisi hiyo, Sheikh Ally
Ajirani, huku viongozi wa kiserikali, akiwemo
Sheha, Diwani na kamati nzima ya uongozi wa
kijiji wakishirikiana bega kwa bega na taasisi
hiyo katika ugawaji wa misaada hiyo.
Sheikh Ajirani alisema, The Islamic Foundation ilikusanya fedha hizo kupitia michango
iliyokusanywa kupitia Radio Imaan na Televisheni Imaan na kisha kununua chakula ambacho kiligawiwa moja kwa moja kwa waathirika.
Vyakula vilivyogawiwa ni mchele, sukari,
unga wa ngano, mafuta ya kula, pamoja na
vinywaji baridi na biskuti kwa ajili ya watoto.
Tuliona wengi waliotoa misaada walichangia vifaa vya ujenzi, lakini sisi tuliona watu
waliharibikiwa makazi na mazao yao, na hivyo
tukaamua tusaidie upande huu uliosahauliwa,
alisema Sheikh Ajirani.

Afyais natural
source of sweet
drinking water
from underground stream
which is blended
with essential
minerals to support and aid perfect metabolism.

WATERCOM LIMITED
P.o. Box 20409, Plot N.4005, Kisarawe11 area
Temeke,Daresalaam, Tanzania
www.watercomtz.com, E-mail:info@watercomtz.com

Mwakilishi wa The Islamic Foundation Pemba, Sheikh Ahmed Masoud (kulia) akiwa na
msaada wa vyakula tayari kuvushwa kwenda kisiwa Panza kwa ajili ya waliopatwa na
maafa visiwani humo. (na mpiga picha wetu)

15 Rajab 1436, jumatatu May 4 - 10, 2015

habari habari

www.islamicftz.org

Wanafunzi wa
Madrasa
Rahmatul
Islamiyya,
Vingunguti jijini
Dar es Salaam.

(na Khalid Omary)

Operesheni tokomeza madrasa


A
Na mwandishi wetu

liyekuwa Makamu wa Rais


wa Marekani Dick Cheney
alipata kunukuliwa mwaka
2009 akisema, the more
ruthless the better to the world- kadiri
ukatili zaidi unavyotumika ndiyo bora
kwa dunia.
Dick Cheney alitoa maneno hayo alipokuwa akizungumzia mkakati wa
Marekani kuzifunga madrasa nchini
Pakistan na Afghanistan kwa madai
kuwa ni mazalia ya ugaidi.
Inaelekea iko kampeni ya kuziua
madrasa duniani na Tanzania inaelekea inaiga. Hali ya wasiwasi na taharuki
imewakumba waumini wa dini ya Kiislamu hapa nchini kufuatia Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama
kuendesha kampeni dhidi ya madrasa
ambapo walimu wanakamatwa kwa
wazi wazi na kinyemela.
Vyombo hivyo vya usalama vimekuwa vikiwakamata walimu wa madrasa na wanafunzi wao katika maeneo
mbali mbali ya nchi. Mikoa ambayo
walimu walikamatwa na madrasa kufungwa na kuathirika zaidi ni pamoja
Kilimanjaro, Dodoma, Kagera na Mtwara.
Habari hizi zinaotuogopesha. Ha-

Na Abdulhakim Abdalla
Nsobya.

ais wa Uganda, Yoweri


Kaguta Museveni amekosoa tabia ya kulaumu na
kuhukumu Waislamu wote
kwa vitendo viovu vinavyofanywa na
makundi maovu ya watu wachache
yanayojinasibisha na dini hiyo.
Katika makala yake alioiandika hivi
karibuni katika gazeti la Serikali la
Uganda, New Vision yenye kichwa cha
habari Wanamgambo wa Al-Shabaab
wameshashindwa vita, Rais Museveni

tuna amani kabisa. Baadhi yetu wenye


imani dhaifu wamefikiria hata kuacha
kazi ya ualimu. Tunajiuliza kwa nini
sasa? Na kwa nini sisi Waislamu?, Ustadh Mohammed wa Magomeni alisema.
Kauli kama ya Ustadh Mohammed
ilitolewa pia na walimu wengine 12 wa
madrasa waliohojiwa na gazeti hili
kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Walimu wamesema katika kampeni hii watakaoathirika ni watoto ambao
wanahitaji elimu ya dini iwasaidie katika kuishi maisha ya kumcha Mungu.
Jeshi la Polisi na Wizara ya Mambo
ya Ndani limetaja sababu ya kamata
kamata ya walimu kuwa ni kuwalinda
watoto, lakini viongozi wa Kiislamu
waliohojiwa wamesema wanaamini
kampeni hiyo inahusiana na vita dhidi
ya ugaidi, ambao wamesema haupo ila
unatengenezwa na kutafutwa watu wa
kulaumiwa.
Viongozi waliohojiwa wamesema
huu ni muendelezo wa mikakati ya kimataifa ya kudhuru Waislamu kwa kisingizio cha vita ya ugaidi. Ustaadh Malaika Ulembo wa madrsatul Rahmatil
Islamiya iliyopo Vingunguti Mtambani, Dar es salaam, alisema, kufungia
madrasa na kukamata walimu ni njama za kuupiga vita Uislamu.

Hicho ni kisingizio cha kuudhofisha Uislamu. Wote tunajua hakuna


ugaidi nchi hii, ila unatengenezwa. Pia
iweje kila jambo la ugaidi wahusishwe
Waislamu? Kama wanazifungia madrasa maana yake hakutakuwa na Uislamu na waalimu watakimbia kufundisha kwa hiyo Uislamu hautakuwepo
tena, ameeleza Ustaadh Ulembo.
Naye, Ustaadha wa Marasatul
Bayyinah ya Vingunguti Bakwata, Muniru Juma, alisema jambo hilo lililofanywa na Serikali ni baya na kuitaka Serikali iache kufungia madrasa.
Muniru alisema: Hili ni jambo
baya na halifai kwa sababu Serikali
inapochukua hatua za kuvifungia vituo
vya kufundishia dini, hakuna Muislamu yeyote atakayeweza kujua dini na
kufanya ibada yake, tunavyosikia wenzetu huko mikoani wanakamatwa tunaogopa, lakini mimi sitoacha kufundisha dini ya Mwenyezi Mungu.

Kwa upande wake mwalimu wa


Madrasatul-Ittiswaam iliyopo Kimara,
Dar es salaam, Ustaadh Abubakar
Nyamguma, ameiita kamata kamata
hiyo kama mwendelezo wa uonevu wa
Serikali dhidi ya Waislamu na inalenga
kuangamiza elimu ya dini ili isifahamike kwa vijana na watu wengine.
Ustadh Nyamguma amesema,
anashangazwa na hatua ya Serikali
kuona madrasa ni tatizo wakati historia
ya nchi kwa miaka yote inaonesha masomo ya dini ya Uislamu yalikuwa yakisomeshwa bila kibali chochote.
Ustaadh Nyamguna ameitaka Serikali isitishe vitendo hivyo kuepusha alichokiita Waislamu kulazimika kuchukua hatua za kujihami, kwani
Waislamu hawatokubali kuona wanafanyiwa dhulma ya wazi kiasi hiki.
Kwa upande wake ustaadh Shaaban Katwila, anahisi ipo hatari kubwa
inayoweza kujitokeza nchini siku za

Kama wanazifungia madrasa


maana yake hakutakuwa na
Uislamu na waalimu watakimbia
kufundisha kwa hiyo Uislamu
hautakuwepo tena

Museveni awahami Waislamu


amesema, wale wanaovichukulia vitendo vya kundi la Al-Shabaab la nchini Somalia kama ni vya Waislamu wote
ni uchambuzi dhaifu na si sahihi.
Rais Museveni ameandika kuwa
dhana hiyo dhidi ya Waislamu ni sawa
na kulaumu Wakristo wote kwa vitendo vya kiongozi muasi wa nchi yake,
Joseph Kony, ambaye alikuwa akifanya uovu wake kwa kisingizio cha dini

ya Ukristo.
Katika makala yake hiyo pia, Rais
Museveni, ameandika kuwa hata nchini Somalia kwenyewe yalipo makao
makuu ya wanamgambo wa AlShabaab sio Waislamu wote wanaowaunga mkono Al-Shabaab.
Napenda pia kuwashauri wale
ambao uchambuzi wao si wakina na
uko kinyume na ukweli, wahalifu nchi-

ni Kenya wamekuwa wakiwauwa wale


wasiokuwa Waislamu na kuwasamehe
Waislamu. Je, Jambo hili ni ishara
kuwa Waislamu wanawaunga mkono
hawa wahalifu? Lahasha.
Nimejuaje kuhusu hili? Nchini Somalia katika mji wa Mogadishu kuna
Waislam milioni mbili na nusu ambao
waliamua kuwa pamoja na majeshi ya
Umoja wa Afrika (AU) badala ya kuwa

3
usoni kwa kuwa vitendo vya kukamatwa kwa walimu hao hutokea katika
misikiti na madrasa, jambo ambalo ni
kuingilia uhuru wa dini na kuabudu.
Amesema, anachokiona ni hofu ya
serikali kudhani mafundisho wanayoyapata vijana katika dini yana lengo la
kuwaandaa kupambana nao, jambo
ambalo si sahihi. Alisema madrasa hufunza elimu ya dini kwa lengo la kumjua
Allah na jinsi ya kumuabudu.
Ustadhi wa madrasa ya TarbiyatulIslamiyya, amelaani hatua za kamata
kamata za masheikh wakati mwalimu
mkuu wa madrasa hiyo, Sheikh Awadhi Adam, alisema ingawa hajawahi
kupata mtihani kama huo, amekuwa
akisikia vitendo hivyo vikifanyika huko
mikoani.
Sheikh Adamu alisema, vitendo
hivyo vinapaswa kukemewa na
kuongeza kuwa vikiachwa hivihivi vitazalisha matatizo na migogoro kati ya
Serikali na Waislamu.
Kauli ya mwanasheria:
Gazeti la Imaan lilimtafuta Wakili,
Yahya njama, kutaka kujua msimamo
wa sheria juu ya kadhia ya kukamatwa
kwa walimu wa madrasa, ambapo alieleza kuwa kufungiwa kwa madrasa
hizo kunatokana na kutozingatia sheria
za nchi.
Wakili Njama alisema, Tanzania
haina sheria yoyote inayozungumzia
masuala ya madrasa na kwamba mambo hayo ni masuala yanayohusiana na
dini na si vinginevyo.
Hakuna sheria yoyote hapa nchini
inayotoa maelekezo ya jinsi ya kuziendesha madrasa, na kama katiba inavyosema mambo ya dini yatasimamiwa
na wahusika, kwani Serikali haina dini,
alisema wakili Njama.
Wakili Njama pia amesema, kitendo cha jeshi la Polisi kuwakamata watoto wadogo na kuwapeleka mahabusu
ni kosa kisheria, kwani watoto wale hawana makosa yoyote.
Kuwakamata watoto wadogo na
kuwapeleka mahabusu kunakiuka sheria mbali mbali za mtoto zilizopo hapa
nchini, na hata hivyo mtoto yule hana
kosa. Kama kuna kosa basi ni la mzazi
aliyempeleka kwenda kusoma katika
madrasa hizo, aliongeza Wakili Njama.
Njama amesema kuwa, vitendo vya
jeshi la Polisi kuwavizia walimu wa madrasa nyakati za usiku ni kinyume cha
sheria, kwani shughuli za madrasa hizo
zinajulikana na si sawa na kundi la
wauza bangi na wauza pombe.
Kwa mujibu wa Ustaadh Abubakar
wa Kondoa, uvamizi wa polisi haufanyiki tu kwa madrasa na vituo vya kuhifadhisha Quran, bali pia kwenye shule
za Kiislamu za awali na hata sekodnari.
Mwaka jana mimi na viongozi
wenzangu tulikwenda Shinyanga
kutembelea shule moja ya Kiislamu
mkoani hapo ili kujifunza wenzetu wanavyoendesha shule ya
UK 5
sehemu ya magaidi wa Al-Shabaab,
Museveni aliadika.
Uchambuzi huo wa Rais Museveni
unakuja katika kipindi ambacho
kumekuwa na kampeni katika nchi
kadhaa za Afrika Mashariki za kukandamiza Waislamu kwa kisingizio cha
kupambana na ugaidi. Katika harakati
hizo za danganya toto za kupambana
na ugaidi muonekano wa nje ikiwemo
mavazi ya kanzu na kilemba, pamoja
na madrasa zinazotoa elimu ya Kiislamu (Madrasa) vimekuwa kigezo cha
kuwalenga Waislamu na hivyo kukandamiza haki zao za kikatiba.

15 Rajab 1436, jumatatu May 4 - 10, 2015

www.islamicftz.org

kutoka misikitini
Fanyeni uadilifu kuitafuta nusra ya Allah
Na Nassoro Abei,
Morogoro
Waislam nchini wametakiwa kufanya
mambo mema, ikiwemo kuwasaidia viumbe
vya Allah visivyojiweza ili wapate nusra
kutoka kwa Muumba wao.
Hayo yamesemwa na Sheikh Hassan
Ahmad wakati akitoa khutba ya swala
ya Ijumaa katika msikiti wa Haqi uliopo
mtaa wa Karume, mkoani Morogoro.
Moja ya mambo yanayopelekea
Muislamu kupata nusra ya Allah ni kuwasaidia watu dhaifu na wasiojiweza, kwani watu hao wapo karibu na
Allah wakimuomba tahfiifu juu ya
matatizo yanayowasibu, alisema
Sheikh Hassan.
Katika khutba hiyo, Shekhe Hassan
aliongeza kwamba, sababu nyingine
ya Waislamu kupata nusra ya Allah ni
kufanya uadilifu baina yao na wenzi wao
katika maisha yao ya kila siku.
Sheikh Hassan alisema, Waislamu
wamejisahau kufanya uadilifu na kuwaachia wasio Waislamu, na hivyo
kuikosa nusra ya Allah Subhaanahu
Wataallah.

tujikumbushe

Rajab, Mwezi wa Kumbukizi


Vita vya kukomboa Jerusalem vilianza ndani ya Rajab
Wauaji wasamehewa na Salahud-Din Al-Ayyubiy

Maasi yatajwa chanzo


ajali za barabarani
Na Selemani Magali
Imeelezwa kuwa ajali za barabarani zinazojitokeza
nchini ni matokeo ya kukithiri kwa maasi na kwamba ili
kupata salama mbele ya Allah, jamii inapaswa kurejea
kwake kwa kufuata yale aliyoamrisha na kuacha aliyoyakataza.
Nasaha hizo zimetolewa hivi karibuni na Sheikh
Shaaban Ibrahim wakati wa swala ya Ijumaa iliyoswaliwa
msikiti wa Tungi, Temeke, Dar es salaam, ambapo
amesema, kuna haja ya kutafakari na kutubu madhambi
ili Allah atupunguzie maafa haya.
Sheikh Ibrahim amewataka madereva kufanya shughuli zao kwa ikhlaswi na kwamba wanapohusika katika kusababisha ajali watubie kwa Allah, kwani kufanya
hivyo kutapunguza ajali nyingi za barabarani.
Sheikh Ibrahim amewataka madereva wa Kiislamu
wakiua katika ajali bila kukusudia wafunge miezi miwili
mfululizo au kutoa fidia ya ngamia 100 kwa zile nchi
zenye ngamia au kutoa dhahabu gramu 425 ikiwa kama
kafara.
Sambamba na hilo amewaonya wale wanaohusisha
ajali hizo na ushirikina unaofanywa na viongozi wa kisiasa kwa malengo ya kusaka madaraka, kwani kufanya
hivyo ni sawa na kumshirikisha Allah.

Sheikh Kishki ahimiza


Qiyamu Llayl
Na Khalid Omary
Waislamu wameaswa kukithirisha swala za sunna za
usiku (Qiyamu Llayl) ili kuwa miongoni mwa kundi la
watu watatu wanaopendwa na Mwaenyezi Mungu na
kuwa sababu ya kuingia peponi siku ya kiyama.
Wito huo ulitolewa na Sheikh Nurdin Kishki wakati
akitoa khutba ya swala ya Ijumaa katika msikiti wa Ihsan
uliopo Temeka Vetenary jijini Dar es salaam.
Sheikh Kishki alisema, swala za usiku zinamuongezea
daraja mswaliji kwa Mwenyenzi Mungu, hivyo Waislamu
wanatakiwa wadumu kwenye Sunna hiyo.
Sheikh Kishki alitaja makundi matatu yanayopendwa
na Mwenyezi Mungu kuwa ni pamoja na watu wanaokesha usiku kwa kumnyenyekea Allah huku wakiswali na
kusoma Quran.
Sheikh Kishki alitaja makundi mengine mawili kuwa
ni watu wanaotoa sadaka kwa siri tena katika wakati
mgumu, na watu waliopigana vita vya jihad bila kuwapa
mgongo maadui, aidha washinde au wafe wakiwa ni
mashahidi.

Na Mwandishi Wetu

wezi wa Rajab
umesheheni matukio muhimu ya
kiimani na kihistoria ya Kiislamu. Miongoni mwa
matukio muhimu zaidi ya Kiislamu yaliyotokea katika mwezi
wa Rajab ni tukio la Israa na
Miraaj.
Hili inaaminika lilitokea
mwezi wa Rajab mwaka wa 10
tangu Mtume apewe utume,
sawa na 620 Miladia. Ingawa
kuna ikhtilafu baina ya wanawazuoni kuhusu tukio hili kutokea mwezi wa Rajab, ni katika
tukio hili zilifaradhishwa swala
tano kwa Waislamu.
Tukio jingine muhimu kwa
Waislamu ni lile lililosimuliwa
katika Surat Tawba la msafara
wa kivita wa Mtume kwenda
Tabuk katika mwaka wa tisa
tangu Mtume ahamie Madina.
Mtume (Rehma na amani ziwe
juu yake) alitoka na jeshi la watu
30,000 kulikabili jeshi la Warumi ambao hatimaye waliogopa
na kukimbia. Huu ulikuwa
mwanzo wa Uislamu kuenea
duniani kote.
Tukio jingine katika historia
ya mapambano kati ya haki na
batili ni kutekwa mji wa Jerusalem na ardhi iliyokuwa chini ya
watu wa vita vya msalaba (crusaders) mwaka 583 Hijriyyah
sawa na 1187 Miladia.
Ukombozi huu wa ardhi
takatifu ya Baitul Muqaddas ulifanyika chini ya kiongozi na
jemedari wa mfano katika Uislamu, Jemedari Salah ad-Din
Yusuf bin Ayyub maarufu katika vitabu vya historia vya kimagharibi kama Saladin. Wengi
watakumbuka kitabu cha visa
vya Alfu Lela Ulela (Alfu Layla
wa layla yaani mausiku elfu

Tukio jingine lililotokea


ndani ya mwezi wa Rajab
lakini la kusikitisha kwa
Waislamu ni tukio la
kuanguka kwa dola ya
mwisho ya Kiislamu - The
Ottoman Empire mwaka
1382 Hijriyyah sawa na
1924 Miladia.
moja na usiku mmoja).
Tukio jingine lililotokea ndani ya mwezi wa Rajab lakini la
kusikitisha kwa Waislamu ni
tukio kuanguka kwa dola ya
mwisho ya Kiislamu - The Ottoman Empire mwaka 1382
Hijriyyah sawa na 1924 Miladia.
Mustafa Kamal Ataturk,
Myahudi (ambaye kwa jina lake
ikaitwa nchi ya Uturuki au Turkey) akishirikiana na Mayahudi
wenzake waliuangusha utawala
wa Sultan Mehmed Vahdattin
VI na kuifanya Uturuki nchi ya
kisekula badala ya nchi ya Kiislamu.
Ukombozi wa Baitul Muqaddas na Salahud-Din AlAyyubiy:
Katika kumbukumbu ya
matukio ya kihistoria ndani ya
mwezi huu mtakatifu wa Rajab,
tutaelezea juu ya kukombolewa
kwa ardhi takatifu ya Baitul
Muqaddas na Salahud-Din AlAyyubiy toka mikononi mwa
wapiganaji wakristo wa msalaba (Crusaders).
Mtawala wa kwanza Muislamu kusimama kidete kuzikomboa ardhi za Waislamu zilizotekwa na makafiri ni Imadu
d-Din Zink. Huyu alikuwa
mmoja wa maamiri wa Kituruki katika mji wa Aleppo (Syria)

na Mosul (Iraq).
Ingawa angeweza kuishi katika majumba ya kifahari kama
walivyokuwa wakiishi maamiri
wengine wa utawala wa waturuki, yeye alichagua kuishi maisha rahisi akijichanganya na
wanajeshi wake.
Alikuwa mchaMungu kiasi
kwamba mwanahistoria
maarufu Ibn Athir alimsifu akisema: Alikuwa zawadi waliyopewa Waislamu na Allah.
Haikuwa ajabu basi yeye kuwa
kinara wa mapambano dhidi ya
makafiri waliokalia ardhi takatifu ya Baitul Muqaddas.
Akiambatana na wapiganaji
wake waliokuwa na ari na nidhamu ya hali ya juu, huku
wakimtegemea Allah pekee,
Imadu d-Din (nguzo ya dini)
Zink alianza kuzikomboa ardhi
za Waislamu akianzia na Edessa mwaka 1144.
Edessa ulikuwa mji ambao
wapiganaji wa msalaba wakiutumia kama ngome (base) yao
nchini Syria katika uvamizi wao
wa kwanza wa Baitul Muqaddas. Baada ya kutekwa na Zink,
sasa ukawa ngome ya kupanga
mashambulizi ya kuikomboa
ardhi takatifu.
Wakati Zink akijiandaa kuukomboa mji wa Jerusalem
(Baitul Muqaddas), mwaka

1145 maadui wa Uislamu wana


Msalaba wa Ujerumani
(Franks) walimuua, na hivyo
kukatisha azma yake hiyo. Lilikuwa pigo kubwa kwa Waislamu.
Lakini kwa kuwa Imad adDin Zink hakuwa peke yake, na
kwa kuwa alikuwa ameweka
mkakati wa kuwaunganisha
Waislamu dhidi ya maadui,
mamlaka ndogo aliyoianzisha
haikusambaratika baada ya kuuawa kwake.
Madaraka yakachukuliwa
na mwanae, Nuuru d-Din Zink
na mara moja akaushambulia
mji wa Antiokia na huku akiungana na Amiri wa Dimashqi
(Damascus) ili kuunganisha
nguvu za miji miwili mikubwa
ya Syria-Aleppo na Dimashqi .
Kwa miongo kadhaa, kijana
mdogo Nuuru d-Din Zink alipambana na wapiganani wa
crusade lakini hakufaulu kuwashinda. Hatimaye, Allah
akamuinua kiongozi mpya kuja
kuzikomboa ardhi za Waislamu, naye ni Salahud-Din AlAyyubiy au kifupi Saladin.
Katika kipindi hiki, Misri ilikuwa chini ya dola ya mashia
Fatmiyyin (The Fatimid Dynasty). Watawala wa kishia walikuwa wakishirikiana na wapiganaji wa crusade waliozikalia
ardhi za Waislamu.
Pamoja na kushirikiana nao,
mwaka 1160 ma-crusaders
wakaivamia Misri kujaribu
kuiteka. Nuuru d-Din Zink
akatuma jeshi kwenda kuwahami ndugu zake Waislamu.
Kiongozi wa jeshi hili alikuwa
Jemadari Mkurdi, Shirkuh
huku Salahud-Din Al-Ayyubiy,
mpwa wa Shirkuh, akiwa miongoni mwa wapiganaji.
Itaendelea toleo lijalo.

15 Rajab 1436, jumatatu May 4 - 10, 2015

www.islamicftz.org

Wachache wajitokeza hijja 2015


Shirikisho la Taasisi za
Hijja Tanzania (TAHAFE), Dokta Ahmedi Twaha, pamoja na mgao kupungua
hadi 3,000, bado Watanzania
wameshindwa kujaza hata nafasi hizo
chache.
Akitoa mfano, Dk. Twaha ameliambia
gazeti la Imaan kuwa mwaka jana Tanzania bara pamoja na visiwani, ilipeleka
jumla ya mahujaji 2,500 tu; huku nafasi
500 zikikosa watu.
Kwa mujibu wa Dk. Twaha, safari za
Hijja mwaka huu zinatarajiwa kuanza
rasmi Agosti 16, 2015 lakini dalili zinaonesha mwitikio wa mahujaji katika
kujisajili hauridhishi, hususan miongoni
mwa vijana.
Dr. Twaha aliwataka vijana kuamka
na kujipanga kwenda kutekeleza ibada
hiyo ili kupata radhi za Allah. Alisema vijana wengi wamekuwa wakiweka kipaumbele zaidi katika masuala ya kidunia
ikiwamo kuwaza kununua magari, kujenga nyumba za kifahari, huku wakisahau kabisa kuhusu ibada hiyo.
Akitolea mfano katika mataifa mengine Dr. Twaha alisema, kumekuwa na
mwamko mkubwa barani Asia hususan
katika nchi za Malaysia, Indonesia na Pakistani ambako mahujaji wake wengi ni
vijana.
Vijana lazima wahamasishwe kuhusu ibada ya hijja, maana ibada hii ina faida

inatoka uk 1

Akitoa
mfano,
Dk. Twaha
ameliambia
gazeti la
Imaan kuwa
mwaka jana
Tanzania
bara
pamoja na
visiwani,
ilipeleka
jumla ya
mahujaji
2,500 tu;
huku nafasi
500 zikikosa
watu.

kubwa kwa kundi hilo, ikiwemo kuongeza imani, uadilifu na kuimarika kwa
maadili mema katika maisha yao yote,
alisema Dokta Twaha.

Faida za Hijja:

Hijja ni nguzo ya tano ya Uislamu.


Mtume (Rehma na mani ziwe juu yake)
amesema: Uislamu umejengwa juu ya
nguzo tano, nazo ni kushuhudia kuwa
hakuna Mungu ila Allah na Muhammad
ni mtume wake, kusimamisha swala, kutoa zaka, kufunga Mwezi mtukufu wa
Ramadhani na kuhiji Kaaba tukufu iliyoko Makka (Bukhari 1/ 7).
Ni wajibu kwa kila Muislamu,
mwenye akili timamu aliyefikia umri wa
baleghe, akijaaliwa uwezo wa kifedha na
afya, aitekeleze nguzo ya Hijja walau
mara moja katika umri wake, Allah
amesema katika Kitabu chake kitukufu:
Ndani yake zipo Ishara zilizo wazi masimamio ya Ibrahim, na mwenye kuingia humo anakuwa katika amani. Na
kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo,
kwa yule awezae njia ya kwendea. Na
atakaye kanusha basi Mwenyezi Mungu
si mhitaji kwa walimwengu (3:97).
Kwa mujibu wa mafundisho ya
Mtume, Hijja ina faida kubwa ikiwemo
mja kusamehewa madhambi yake yote
na kulipwa pepo ya Allah. Mahujaji wa-

Operesheni tokomeza
kiislamu.
Tukiwa hotelini tulikofikia tukapewa habari kwamba Mkuu
wa shule hiyo na walimu kadhaa
walivamiwa usiku wa manane na
polisi wenye bunduki na kukamatwa kisha kupelekwa kituo
cha polisi.
Polisi walidai wana shaka
kuwa shuleni pale panatolewa
mafunzo ya ugaidi. Walimu wale
hawakuachiwa mpaka siku tatu
zilipopita, wakatakiwa kuendelea
kuripoti kila siku kwa muda wa
wiki mbili na hakuna mashitaka
yaliyofunguliwa dhidi yao.
Taarifa tulizozipata kutoka
Kondoa ni kwamba, polisi walifika madrasa moja ya kuhifadhisha
Quran na kuwahoji walimu na
wanafunzi kisha wakaenda shule
ya Kiislamu mjini hapo na kufanya hivyo hivyo.
Alipoulizwa anadhani lengo la
kamatakamata na polisi kuvamia
vituo vya Kiislamu ni nini? Ustadh Abubakar alijibu nadhani
lengo ni kuwatisha wazazi wanaopeleka wanafunzi katika shule
za Kiislamu ili shule hizo zikose
wanafunzi na hatimaye zife.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba hivi sasa Waislamu
katika maeneo tofauti tofauti
nchini wakionekana wamevaa
kanzu na wamefuga ndevu au
wamevaa hijab, wamekuwa wakifwatiliwa na kubughudhiwa na
polisi.
Ziko habari za Ustadh mmoja
aliyekuwa njiani kupeleka posa
inatoka uk 3

kwa ajili ya harusi ya Muislamu


mwenzake kusimamishwa na
kuhojiwa huko Kilosa. Polisi
h aw a k u mw a c h i a m p a k a
mwenyeji wake ambaye kwa bahati ni Afisa Mtendaji eneo hilo
alipofika polisi na kuwaomba
wamwachie.
Hali si shwari kwa Waislamu,
hawa jamaa wanatusukuma
tusikokutaka. kwani wanadhani
tutaendelea kuvumilia dhulma
hizi mpaka lini? Kwani sisi tuna
mioyo ya jiwe au chuma?
masheikh zetu wako ndani zaidi
ya mwaka, wengine mitatu sasa.
Halafu wanawafuata wengine na
kufunga madrasa zetu, alilalama
mmoja wa vijana baada ya sala ya
ijumaa, wiki Iliyopita, Masjid
Taqwa, Buguruni, Dar es salaam.
Tamko la Masheikh:
Wakati habari za kamata
kamata ya walimu na kufungwa
kwa madrasa zikienea kwa kasi
nchini, kulitolewa tamko na viongozi wa taasisi za Kiislamu wiki iliyopita, tamko lililosomwa mbele
ya vyombo vya habari jijini Dar es
salaam.
A k i s o m a t a m ko h i l o ,
Mwenyekiti wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam, Sheikh Musa Kundecha, alisema vyombo vya usalama vimekuwa vikiwafuata na
kuwakamata walimu hao wa madrasa nyakati za usiku wa manane, huku wengine wakiachiwa
na wengine kutokujulikana walipopelekwa.
Kuna baadhi ya waalimu wa

madrasa wamenifuata wakielezea


kufuatiliwa na kushikiliwa na vyombo vya usalama nyakati za
usiku, alisema Sheikh Kundecha.
Sheikh Kundecha ameongeza
kuwa baadhi ya walimu wa madrasa kutokana na kuogopa
kuandamwa na kukamatwa kiholela na vyombo vya usalama,
wameamua kuacha kazi hiyo ya
ufundishaji na kuangalia mustakabali mwingine wa maisha
yao.
Kufuatia uwepo wa kadhia
hiyo, tamko hilo limesema kuwa
operesheni hizo za kisiri na za wazi
zinakiuka haki za msingi za binadamu, haki za kikatiba, kisheria
na za kiutu na kwamba ni
uchochezi dhidi ya Waislamu kwa
kuwafanya wachukiwe na
waonekane wabaya mbele ya
jamii.
Mkakati na operesheni ya
polisi inakiuka haki nyingi za binadamu, haki za kikatiba, haki za
kisheria, utu, ni uchochezi dhidi
ya Waislamu kwa kuwafanya wachukiwe na jamii na waonekane
Waislamu si waaminifu, hawapendi amani, tamko hilo lilisema.
Sheikh Kundecha amesema
kuwa, suala la kustaajabisha ni
kuwa, vyombo vya usalama haviwaiti viongozi wa Kiislamu kukaa
pamoja na kuangalia kuna tatizo
gani katika madrasa hizo, badala
yake polisi wameendeleza vitendo
vyao hivyo visivyokubalika dhidi
ya walimu wa madrasa na shule
za Kiislamu nchini.

meitwa kuwa ni wageni wa Allah na kwa


sababu hiyo Mungu anakubali maombi
yao kwa haraka. Pia, Hijja kwa wanawake
imefananishwa na Jihad.
Hijja pia imetajwa kuongeza imani ya
mumini na pia inafundisha subira, tabia
njema na ukomavu wa mwili. Kutekeleza
ibada ya Hijja kunampa muumini nafasi
ya kujifunza kuhusu Uislamu kwa
kutembelea maeneo matukufu ambako
Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake)
na maswahaba zake waliishi.

Hijja ya 2015:

Katika hatua nyingine muhimu,


Shirikisho la Taasisi za Hijja Tanzania
(TAHAFE) limetoa wito kwa waumini
wanaotegemea kutekeleza ibada ya Hijja
mwaka huu kujisajili mapema ili kurahisisha zoezi hilo katika mfumo mpya wa
kieletroniki kama ilivyoelekezwa na wizara ya Hijja nchini Saudia.
Katibu Mkuu, Dk. Twaha alisisitiza
usajili wa mapema ili kukabiliana na mabadiliko yaliyotangazwa na Saudia. Alisema mahujaji wote wanapaswa kukamilisha usajili ifikapo June 10, 2015 sawa na
Shaaban 20, 1436 Hijriya.
Nataka niwaambie mahujaji wasisubiri hadi tarehe ya mwisho, wajitokeze
sasa kujisajili katika taasisi yeyote watakayoipenda kusafiri nayo ili kutoa fursa
kwa taarifa zao kuingizwa katika

mtandao kama wizara ilivyotutaka, alisema Dk. Twaha.


Dr. Twaha alisema, iwapo mtu
atashindwa kujiandikisha, hatoweza kushiriki katika ibada hiyo takatifu, kwani
taarifa zake zitakuwa hazijapokelewa katika Wizara ya Hijja ya Suudia.
Naye Mjumbe wa Shirikisho hilo la
TAHAFE, Alhaji Haidar Kambwili
ametaja kikwazo kikubwa ambacho taasisi nyingi zinazosafirisha mahujaji hukabiliana nacho ni kuwa mahujaji wengi ni
wakulima, ambapo mwezi huu bado hawajavuna, hivyo kuwawia vigumu kuwapata.
Aidha Alhaji Kambwili amefafanua
kuwa, licha ya changamoto hizo, hakuna
budi kufuata matakwa ya Wizara Ya Hijja, vinginevyo kwa mwaka huu hakuna
mtu atakaetekeleza ibada hiyo muhimu.
Taasisi ambazo zilizo chini ya
mwamvuli wa TAHAFE ni pamoja na
Tanzania Muslim Hajj Trust, Zamzam
Centre, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na Tanzania Charitable
and Development Organization(TCDO).
Nyingine ni Darul Hadithiis Salafiya,
Hidmati Islamiya Charitable Society,
Amani Travel and Tours, Peace Travel and
Tours, Al-bir Social Development Fund,
Al-madinnah Social Service Trust, Taibah
Hajj and Umra Social Services Trust na
Manaasik Makkah Trust.
Nyingine ni Jamaarat Hajj and Umra
Travelers, Al-Markaz Shamsiya Al-islamiyya, Masjid Adil, Al-Bushra Tours
Ltd, Tabazat (Babusalama), Al-Maha
Travel and Tours Company Ltd na AlJazira International Hajj Trust.

Huu ni unyama, si jihad


Jihadi si ukatili Kinachotokea ni fikra
potofu Lengo ni kuupaka matope Uislamu
Na mwandishi
wetu

akati tukienda mitamboni, zimetufikia habari


kwamba watu wasiojulikana wamelipua bomu la kutipwa kwa mkono huko
Msolwa Morogoro kujaribu
kusambaza umati wa watu
uliokuwa unawazingira
wakiwahisi kuwa ni wahalifu.
Matukio kama haya
mara moja yananasibishwa
na Waislamu na moja kwa
moja ugaidi. Wakati tukilaani uhalifu kama huu, tunajiuliza wahusika ni akina
nani? Kwa nini wanafanya
hivi? Wanataka kuua au kujeruhi watu wasio na hatia?
Kila uchao tumekuwa
tukishuhudia au kusikia katika vyombo vya habari vijana wa kiislamu wakijitolea
kupigana katika kile kiitwacho Jihad. Si jambo la ajabu tena kuona au kusikia
wapiganaji wa Jihad au
Jihadists wamelipua na
kuua watu kadhaa.
Hali imekuwa mbaya kiasi kwamba tumekuwa tunasikia vijana wetu wasomao shule au hata vyuo

vikuu kuacha masomo yao


na kukimbilia kufa Shahidi katika vita ambavyo ni
mkakati wa maadui wa Uislamu kuusambaratisha Uislamu.
Inakuwaje kwa kijana
aliyelelewa malezi mazuri
ya kiislamu kuingiwa na
fikra hizi? Ni wapi wanakopatia fikra hizi za ukatili kwa
jina la Jihad?
Wako wanaodhani
kwamba madrasa zetu
misikitini ndiyo chimbuko
la fikra hizi na huku wengine wakidhani ni shule za
kiislamu ndizo zinazowafunza vijana mitazamo hii
ambayo katika msamiati wa
kiislamu wenye fikra hizi
huitwa Takfiriyyuun.
Uislamu ni dini ya amani
ambayo moja ya malengo
yake ni kutengeneza jamii
kwa kuilinda dhidi ya mambo matano yaitwayo Al
Maqaaswidu as-Shariyyah
yaani makusudio matano
ya Shariah.
Uislamu unahimiza
kulinda nafsi, nafsi yoyote
ile siyo tu ya mwanadamu
bali hata ya mdudu, mnyama, ndege. Nafsi ya mwanadamu haiuawi ila ikiwa
nafsi hiyo itaua nafsi nyingine kwa makusudi au

ikiwa imetenda kosa la jinai


ambalo hukumu yake ni
kifo.
Uislamu inahimiza
kulinda dini (imani) ya mtu.
Quran imeweka msingi wa
dini zote kuishi kwa amani
iliposema Hakuna kutezana nguvu katika dini, uongofu na upotofu umeshabainika (2: 256).
Si ajabu basi historia ya
Uislamu tangu zama za
Mtume na Makhalifa waongofu Waislamu waliishi na
watu wa dini zote kwa amani na kila mtu akipewa fursa
ya kuamini atakavyo kwa
sharti asiupige vita Uislamu.
Uislamu unahimiza pia
kulinda heshima za watu,
hakuna ruksa kumdhalilisha au kumuaibisha mtu.
Ndiyo maana Uislamu
umeweka hadi adhabu kwa
mtu au watu wanaovunja
heshima za wengine.
Uislamu umehimiza
kulinda kizazi. Jambo lolote
linalofanyika kuangamiza
kizazi iwe cha wanadamu
au viumbe wengine hai ni
dhambi kubwa. Iweje basi
leo watu wavae milipuko na
kujilipua wakiua watu wasio na hatia iwe Jihad?. Huu
si Uislamu hata kidogo.

15 Rajab 1436, jumatatu May 4 - 10, 2015

hutolewa na kuchapishwa
The Islamic Foundation,P.O.Box 6011 Morogoro, Tanzania,E-mail: imaanmedia3@gmail.com
mhariri mtendaji: 0715 559 944, Mhariri: 0786 779 669, afisa masoko: 0785 500 502
TOVUTI: www.islamicftz.org

tahariri / uchambuzi

Kamata kamata walimu wa madrasa ikome


H
ivi karibuni kumearifiwa matukio ya
kamata kamata ya
Masheikh na walimu
wa madrasa inayoendelea kimya
kimya sehemu mbalimbali za
nchi yetu, na kufuatia taarifa
hizo viongozi wa dini ya Kiislamu mara kadhaa wamesimama
na kutoa matamko ya kuitahadharisha na kuitaka Serikali kusimamisha kampeni hii.
Ukiangalia jinsi kampeni hii
inavyoendeshwa, utaona wazi
kuwa inapingana na kanuni za
utawala bora, inaingilia uhuru
wa Ibada, ina harufu ya ukiukwaji wa haki za msingi na za
kikatiba za watu, na pia inaonyesha undumilakuwili wa Serikali.

Madrasa ambazo zimekuwapo kwa miaka mingi, leo zinaonekana kuwa zimeanzishwa
kinyume na sheria! Pia kuna
madai kuwa mitaala ya hizi madrasa haieleweki na kwamba
watoto wenye umri wa kwenda
shule waliopo madrasa hawaendi shule. Hizi ndio baadhi ya hoja
zinazotumika kuhalalisha kampeni hii.
Kwanza, tunauliza, je kuna
sheria inayoongoza uanzishwaji
wa madrasa hapa Tanzania?
Kama sheria hiyo ipo, ni wazi
kuwa watu wengi hawaijui na
ndio maana madrasa zimekuwapo miaka nenda rudi bila
taratibu za usajili.
Lakini, hata kama sheria hiyo

ingekuwapo, ilikuwa ni wajibu


wa Serikali kuelimisha umma
kuhusu sheria na taratibu hizo
na sio kuanza kampeni ya kukamata na kutisha viongozi wa
dini.
Kuhusu suala la kinachofundishwa, ni wazi kuwa mtaala
wa dini hauihusu Serikali. Serikali ingeweza kuingilia kama
imepokea malalamiko au ina
sababu za msingi kabisa za kuamini kuwa katika madrasa husika kuna mafundisho yasiyostahili.
Serikali inapotaka kuanza
kujihusisha na mitaala ya mafundisho ya dini ni hatari, na
itakuwa inaingilia uhuru wa
kuabudu. Zipo nchi ambazo zil-

ianza hivi hivi na sasa Masheikh


hawatoi khutba za Ijumaa mpaka ikaguliwe na Serikali.
Nayo, hoja ya watoto wasioenda shule inaweza kuwa ina
mantiki, lakini je ni sahihi
kuwakamata Masheikh saa nane
usiku, kimya kimya kwa kosa
hilo? Na maafisa wa ustawi wa
jamii ambao wanapaswa kuangalia ustawi wa watoto wanafanya kazi gani?
Tunajua kuwa yapo makanisa
ya majumbani ambayo shughuli
za kiibada zinaendeshwa. Je
Serikali inawakamata na hao ili
kujua wanafundishana nini?
Huu ndio undumilakuwili tunaouzungumzia.
Sisi katika gazeti la Imaan tu-

naishauri Serikali isimamishe


kampeni hii mara moja na kuwaachia walimu na Masheikh
(kama bado wapo inaowashikilia).
Serikali ijue njia bora ya
kuondoa upungufu wowote inaouona katika madrasa au
mambo yoyote yale yanayohusisha dini, si kutumia maguvu, bali
kuzungumza na kushauriana na
viongozi wa dini.
Wote tunaitakia mema nchi
yetu kwa nini tuhasimiane
wakati tungeweza kuongea na
kuelewana? Tena inakera zaidi
pale ambapo Serikali inazungumza na makundi mengine
yenye mgogoro nao lakini sio
Waislamu.

nasaha za wiki

ei Mosi, kila mwaka ni


siku ambayo duniani
kote wafanyakazi
kutoka sekta mbali
mbali hujumuika pamoja ili kuadhimisha, kufurahia na kutafakari
mambo mbali mbali yanayozihusu
shughuli zao.
Pamoja na kwamba siku hiyo ni
sawa na sherehe zingine ambazo
hufanyika ili wahusika wafurahie
kwa pamoja, wapongezane kwa
utumishi wao kwa jamii, siku hiyo
kwa hapa Tanzania mambo huwa
ni tofauti kabisa.
Ni siku ambayo kwa wafanyakazi wengi wa sekta ya umma na zile
za binafsi huitumia kutoa malalamiko yao kwa njia ya mabango
yenye ujumbe mbali mbali na kusoma risala mbele ya mgeni rasmi.
Kiukweli ukisikia risala na kusoma mabango yao, lazima utaguswa na mambo ambayo wanayalalamikia.
Yapo mambo mengi wanayoyalalamikia wafanyakazi kama masuala ya tume ya usuluhishi, malimbikizo ya madeni yao, utozaji kodi
katika mishahara yao na
kuongezwa kwa mishahara.
Leo hii, napenda nijikite katika
suala la mshahara, hususan kima
cha chini kinachotolewa na Serikali
kwa sasa na kile kinachopendekezwa na shirikisho la wafanyakazi hapa nchini (Tucta).
Inasikitisha sana kuona katika
nchi iliojaaliwa utajiri mkubwa wa
rasilimali na iliotimiza umri wa
nusu karne tangu ipate uhuru bado
wafanyakazi wake wanazungumzia
kima cha chini cha mshahara kiwe
sh 315,000 huku ukali wa maisha
ukiwa haumithiliki.
Na pendekezo hilo la kutaka
mshahara uwe kima cha chini cha
Shs 315,000 lilitolewa na shirikisho
hilo wakati ndio kwanza Rais Ja-

Yusufu Ahmadi

Kwa hii laki 3, wafanyakazi


wataendelea kusota tu
kaya Kikwete yuko mwanzoni mwa
safari yake ya Urais mwaka 2006,
na mpaka sasa Rais Kikwete

anaondoka madarakani hajatimiza


suala hilo, inasikitisha!
Leo hii unapozungumzia kima
Rais Jakaya Kikwete

cha chini cha mshahara kiwe shs


315,000, hivi kweli huwa tunamuangalia mtu tunae tarajia kumlipa kiasi hicho au tunatumia hisia
tu.
Chukulia mfano wa gharama za
maisha ya jiji la Dar es salaam na
ukilinganisha na kiwango hicho
unapokuja katika kodi ya nyumba,
umeme, maji, mahitaji ya mtumishi, bado unaona ni kidogo mno,
jambo ambalo ni kutomtendea
haki kabisa.
Ni ukweli kwamba binadamu
huwa hatosheki, hata apewe mshahara wa mabilioni ya shilingi lazima
atahitaji zaidi ya huo, lakini ukweli
uliopo kiwango hicho cha sasa na
kinachopendekezwa ni kidogo
mno, hakikidhi mahitaji kabisa, Ni
maumivu tu!
Mwisho wa siku ufanisi unapopungua sehemu za kazi, tunakimbilia kumtafuta mchawi huku tukisahau mchawi ni sisi wenyewe, ni
mfanyakazi gani wa sasa atakaeweza kujitolea kwa nguvu zake zote
huku mshahara anaolipwa hawezi

Na pendekezo hilo la kutaka mshahara uwe


kima cha chini cha Shs 315,000 lilitolewa
na shirikisho hilo wakati ndio kwanza
Rais Jakaya Kikwete yuko mwanzoni mwa
safari yake ya Urais mwaka 2006, na mpaka
sasa Rais Kikwete anaondoka madarakani
hajatimiza suala hilo, inasikitisha!

hata kutatua changamoto za sehemu anayoishi.


Hapa nieleweke vema kuwa
sitetei rushwa, lakini kwa vimishahara hivi kiduchu lazima rushwa
izidi kutamalaki hapa nchini, ni
vigumu mtu ambae maisha yake ni
magumu kuikwepa rushwa.
Ikiwa vigogo ambao wako
kwenye sekta nyeti hulipwa mishahara minono na posho mbali mbali
wanachukua rushwa, sembuse
huyu mfanyakazi anaelipwa kiduchu asichukue rushwa? Tutazidi
kuimba sana tu kuhusu rushwa.
Ifike wakati Serikali iwe inakaa
chini na kufikiria maisha ya hawa
wafanyakazi wanaolipwa mishahara ya chini ya laki tano, isiwe inasubiri mpaka watu walalamike, hiyo
sio Serikali makini hata kidogo.
Kama alivyosema Rais Kikwete
katika hotuba yake ya Sherehe za
Mei Mosi mwaka huu kwamba
hata watangulizi wake hawakuweza kuyatatua matatizo yote ya wafanyakazi na kusema anamuachia
mtangulizi wake kama suala la kupunguza kwa kodi ya mishahara
kutoka asilimia 12 hadi 9, lakini
kwa hili la mshahara wa kima cha
chini, mi naamini uwezo huo Rais
Kikwete bado anao yeye
mwenyewe.
Kama nilivyoonesha hapo juu,
nchi yetu ni tajiri sana na ina rasilimali za kutosha, hivyo basi ni vema
Rais Kikwete na wasaidizi wake
wakakaa chini kuangalia jinsi ya
kutumia rasilimali hizo ili ziwanufaishe na walalahoi wengine.
Si busara mpaka wafanyakazi
waandamane, walalamike na wajidhalilishe ndio Serikali ijue kumbe
kuna watu wengine wanahitaji,
ianze kukaa na kujitafakari
yenyewe. Nilikuwepo!
0658 010 594

15 Rajab 1436, jumatatu May 4 - 10, 2015

www.islamicftz.org

Kutoka katika Quran na Sunnah


sheikh Tawakkal Juma
Wiki iliyopita katika
mwendelezo wa makala
zetu za Kutoka katika
Quran na Sunnah tuliishia katika maneno ya
msomi G. Margoliouth
juu ya Quran ambayo
kwa kifupi yana maana
kuwa Quran imekubalika kuwa inachukua
nafasi muhimu miongoni
mwa vitabu vya kidini
duniani japo ni kitabu
cha karibuni zaidi ukilinganisha na vitabu
vingine vya kidini.
Ms o m i G . Ma r g o l i o u t h
anaelezea kuwa Quran iliwabadilisha makabila ya Ghuba ya Bara
Arabu kutoka hali duni na kuwa
taifa la mashujaa, na kisha ikaanzisha taasisi kubwa ya kisiasa na kidini ya Muhammad. Msomi huyu alitahadharisha kuwa taasisi hizo ni
moja kati ya nguvu kubwa sana ambazo Ulaya na nchi za Magharibi
sharti zizitafakari kwa kina.
Naye Dr. Steingass anasema: A
work, then, which calls forth so
powerful and seemingly incompatible emotions even in the distant
reader - distant as to time, and still
more so as a mental development a work which not only conquers the
repugnance which he may begin its
perusal, but changes this adverse

Mshangao wa wasomi juu ya Quran


feeling into astonishment and admiration, such a work must be a
wonderful production of the human mind indeed and a problem of
the highest interest to every
thoughtful observer of the destinies
of mankind.
Maana ya maneno hayo ni:
(Quran) ni kazi inayoibua hisia
kali sana, zinaonekana kama hazipatani kwa muonekano wa nje, hata
kwa msomaji wa mbali, kiwakati na
kiakili, ni kazi ambayo haivamii tu
chuki ya msomaji ambayo anaweza
kuanza nayo anapoanza kuisoma,
lakini ghafla hubadilisha hisia hizi
za chuki zikawa mshangao, mapenzi na kuiheshimu, kazi kama hii lazima itakuwa ni zao la ajabu kabisa
lililoletwa na akili ya mwanadamu
na ni tatizo la kuangaliwa kwa kina
kabisa kwa kila mwenye kufikiri
mambo ya baadaye ya mwanadamu.
Naye Arthur J. Arberry anasema: In making the present attempt
to improve on the performance of
my predecessors, and to produce
something which might be accepted as echoing however faintly the
sublime rhetoric of the Arabic
Quran, I have been at pains to study
the intricate and richly varied
rhythms which - apart from the
message itself - constitute the Ko-

TAASISI YA KHIDMAT ISLAMIYA YENYE UZOEFU


WA MIAKA 14 KATIKA SHUGHULI ZA HIJA NA
UMRA, INAWATANGAZIA WAISLAM WOTE KUWA
GHARAMA YA HIJA KWA MWAKA 2014/ 1435H NI
DOLA 4750 TU AMBAZO ZINAWEZA KULIPWA KWA
AWAMU (KIDOGO KIDOGO).
AIDHA, GHARAMA YA KUFANYIWA IBADA YA HIJA
(KUHIJIWA) NI DOLA 1450 TU.
MALIPO YA HIJA YANAJUMUISHA GHARAMA
ZIFUATAZO:

NAULI YA NDEGE KWENDA NA KURUDI

MALAZI MAKKA, HOTELI YA NYOTA 3*,


MWENDO WA KUTEMBEA DAKIKA 7 TU
MPAKA MASJID HARAM.

MALAZI MADINA, HOTELI YA NYOTA 3*


MWENDO WA KUTEMBEA DAKIKA 3 TU
MPAKA MASJID NABAWY
(NI UKWELI USIOFICHIKA KUWA KHIDMAT
ISLAMIYA IMEKUWA IKIANDAA NYUMBA ZA
MAHUJAJI KARIBU KABISA NA MASJID HARAM NA
MASJID NABAWY).

USAFIRI WA BASI JEDDAH MAKKA,


MAKKA MADINA
HUDUMA MAALUM (SPECIAL SERVICE)
SIKU 5 ZA HIJJA
MAHEMA YENYE VIYOYOZI (AIR CONDI
TION), MAGODORO, MITO NA BLANKETI
CHAKULA MILO MITATU, KUJIHUDUMIA
MWENYEWE (BUFFET) CHAI, KAHAWA,
JUISI, SODA, MAJI NA VITAFUNWA
(SNACKS) VITAPATIKANA MASAA 24, SIKU 5
ZA HIJJA
USAFIRI WA BASI KATI YA MAKKA MINA,
MINA ARAFAT, ARAFAT MUZDALIFA,
MINA MAKKA
NGUO (IHRAM) KWA WANAUME NA
HIJAB KWA WANAWAKE, GALONI
MOJA YA MAJI YA ZAM ZAM (LITA 10)
BEGI LA KUSAFIRIA, PAMOJA NA KILO 3 ZA
TENDE KWA KILA HUJAJI
ZIARA YA MAKKA KUTEMBELEA NYUMBA
ALIKOZALIWA MTUME WETU
MUHAMMAD (S.A.W), JABAL HIRA,
JABAL THAWR, JABAL RAHMA,
MASJID JINNI, MASJID KHEIF,
MASJID NIMRAH, VIWANJA VYA ARAFAT,
MINA, MUZDALIFA NA JAMARAT

Dr. Maurice
Bucaille:
Ulinganishi
kamilifu wa
Quran na
elimu ya sasa
unatupelekea
kutambua
uwiano kati ya
viwili hivi
kama
ilivyowahi
kuonyeshwa
mara kwa
mara.

rans undeniable claim to rank


amongst the greatest literary masterpieces of mankind... This very
characteristic feature - that inimitable symphony, as the believing Pickthall described his Holy Book, the
very sounds of which move men to
tears and ecstasy - has been almost
totally ignored by previous translators; it is therefore not surprising
that what they have wrought sounds
dull and flat indeed in comparison
with the splendidly decorated original.
Tafsiri: Katika kujitahidi kujaribu kwangu kukuza kazi waliyofanya watu walionitangulia, na kutaka
kutoa kitu ambacho kinaweza
kukubalika kuwa kimetoa japo kwa

mbali uzuri na ufasaha wa Quran,


nimekuwa katika machungu kujifunza mashairi yake; lugha yake tu
ukiachilia ujumbe wake inaifanya
Quran kuwa miongoni mwa kazi
za kifasihi za juu kuliko zote za
mwanadamu. Tabia hii ya Qur-aan
na sanaa isiyoweza kulinganishwa
kama Picktall alivyoelezea Kitabu
chake, sauti zake huwafanya watu
watokwe na machozi na wawe na
hisia kali, jambo ambalo halikuzingatiwa na wafasiri waliopita; hivyo
ni jambo lisiloshangaza kuwa walichofanya kinachosha ukilinganisha
na uzuri wa asili yake iliyopambwa.
Naye Daktari Bingwa wa Kifaransa, Dr. Maurice Bucaille
anasema: A totally objective exam-

ZIARA YA MADINA KUTEMBELEA MSIKITI


WA MTUME (SAW), MAKABURI YA BAQII
(WALIPOZIKWA MASWAHABA, BAADHI YA
WAKEZE NA WATOTO WA MTUME (S.A.W.)
NA MAKABURI YA WALIOKUFA SHAHIDI
KATIKA VITA VYA UHUD
VILE VILE GHARAMA YA HIJJA INAJUMUI
SHA ZIARA YA MADINA KUTEMBELEA
MASJID QUBA, MASJID QIBLATAIN, MASJID
JUMAA, SABA MASAAJID (MAHALI KULIPO
FANYIKA VITA VYA KHANDAQ), NA
JABAL UHUD.
GHARAMA YA UCHINJAJI WA MNYAMA
WA UDHHIYA
CHAKULA MILO MITATU KUJIHUDUMIA
MWENYEWE (BUFFET) SIKU ZOTE ZA
SAFARI.

SHEIKH HASHIM AHMED RUSAGANYA, SHEIKH


JUMA RAJAB IKUSI NA SHEIKH HARUNA JUMANNE
KAPAMA WATAKUWEPO NA KUTOA MWONGOZO
KWA MAHUJAJI WAKATI WOTE.
AL-HAJJ AHMED SALEH NAHDY (HAMAD) AL-HAJJ
ZULFIKAR OSMAN (ZULLY) AL HAJJ ALTAF ABDU-LATIF NA AL HAJJ SIDIK VIONGOZI WENYE UZOEFU
WA MUDA MREFU PIA WATAKUWEPO KUWAHU-DUMIA MAHUJAJI
LENGO NI KUHAKIKISHA KILA HUJAJI ANATEKELEZA
IBADA YAKE INAVYOTAKIWA. MADAKTARI DR. HAJI
HAMDU NA DR. HAMISA THEREYA ( DAKTARI WA
AKINA MAMA) WATAKUWEPO KATIKA MSAFARA
NA MADAWA YOTE MUHIMU YATAPATIKANA
WAKATI WOTE WA SAFARI.
WAWEZA KUWAULIZA MAHUJAJI WALIOWAHI
KUHUDUMIWA NA TAASIS HII, NA WATAKUHAKIK-ISHIA UWEPO WA HUDUMA ZA KURIDHISHA.
ALHAMDULILAH DAIMA KHIDMAT ISLAMIYA
TUMEWEZA KUTEKELEZA KILA TUNACHOKIAHIDI.
TAHADHARI: NDUGU HUJAJI MTARAJIWA FANYA
UCHUNGUZI WA KINA KABLA YA KUJISAJILI KWANI
IBADA HII NI MOJAWAPO YA NGUZO TANO ZA
UISLAM KWA HIYO HAKIKISHA UNAITEKELEZA INAVYOTAKIKANA KWA NAFASI ULIYOJAALIWA,
KWANI HUJUI KAMA UTAIPATA TENA NAFASI HIYO
MAISHANI MWAKO. NDUGU MUISLAM KAMA
UNAO UWEZO USISUBIRIE MWAKANI HUJUI KAMA
UWEZO ULIONAO LEO WA AFYA NA MASURUFU
UTAENDELEA KUWEPO NA PIA UJUE GHARAMA
NAZO ZINAONGEZEKA KILA MWAKA.

ination of it [the Quran] in the


light of modern knowledge, leads us
to recognize the agreement between
the two, as has been already noted
on repeated occasions. It makes us
deem it quite unthinkable for a man
of Muhammads time to have been
the author of such statements on
account of the state of knowledge in
his day. Such considerations are
part of what gives the Quranic Revelation its unique place, and forces
the impartial scientist to admit his
inability to provide an explanation
which calls solely upon materialistic
reasoning.
Maana yake ni: Ulinganishi kamilifu wa Quran na elimu ya sasa
unatupelekea kutambua uwiano
kati ya viwili hivi kama ilivyowahi
kuonyeshwa mara kwa mara. Hii
inatufanya na kutupelekea tuamini
kuwa ni jambo lisilofikirika kabisa
kwa mtu wa wakati wa Muhammad awe ndiyo mtunzi wa maneno
haya kulingana na hali duni kabisa
ya elimu kwa wakati wake. Fikra
hizi ndizo zinazoupa ufunuo wa
Quran nafasi ya kipekee na kumlazimisha mwanasayansi mwenye akili
huru akubali kushindwa kutoa
maelezo juu ya fikra ya ulazima wa
kutegemea akili tu.
Hizi ni baadhi tu ya kauli za wasomi wakubwa kuelezea mshangao
wao juu ya Quran. Je mimi na wewe
Quran inatushangaza?
Itaendelea

KWA MAELEZO ZAIDI NA UANDIKISHAJI


WASILIANA NA:

SHEIKH HASHIM AHMAD RUSAGANYA


NAMBA YA SIMU 0715 915 008,
0784 915 008

SHEIKH ABDALLAH MOHAMED JUMA


IMAM MSIKITI WA MTORO 0713 445 545

AL-HAJJ ZULFIKAR OSMAN 0777 411 020,


0713 530 036, 0786 411 020

AL-HAJJ HAFIDH SALIM 0655 616 623,


0682 535 319

SHEIKH HARUNA JUMANNE KAPAMA


0715 985 413

AL-HAJJ ALTAF ABDULLATIF AHMED


0789 373 222

AL-HAJJ OMAR AWADH KHAMIS - MSIKITI


WA QIBLATAIN - 0715 210 666

ARUSHA: SHEIKH JUMA RAJAB IKUSI


TAYSEER STORE DUKA NO.12 MKABALA
NA NMB TAWI LA
SOKO KUU NAMBA
YA SIMU 0786 125 512, 0767 125 513,
0655 125 513

MOROGORO: AL-HAJJ AHMED SALEH


NAHDY(AHMADO)- 0715 372 776,
0773 372 776

DODOMA & SINGIDA: AL-HAJJ YUNUSU


RUGEIYAMU 0754 334 400,
0786 293 901

DODOMA & KONDOA: SHEIKH ESMAIL H.


ALLIY 0713 677 683

MULEBA, BUKOBA & DAR AL-HAJJ


MAULID ATHUMAN KYEJU 0655 883 573
KATIBU MTENDAJI
MUHSIN MOHAMED HUSSEIN
0784 /0715 /0773 - 786 680,
TAARIFA
MUHIMU
KUFUATANA
NA SHERIA
MPYA NCHINI SAUDIA,

KUFUATANA
NA SHERIA
NCHINI
SAUDIA,
TAREHE YA MWISHO
YA MPYA
KUJISAJILI
NA KUTUMA
TAREHEYA
YAMAHUJAJI
MWISHO KWA
YA KUJISAJILI
NA KUTUMA
MAJINA
NJIA YA MTANDAO
KWA
MAJINA
YA MAHUJAJI
KWA NJIA
YA MTANDAO
KWA
MWAKA
HUU NI TAREHE
8 JUNI2015
SAWA NA
MWAKA HUU
NI
TAREHE
8
JUNI2015
SAWA
NA
TAREHE 20 SHAABAN 1437
TAREHE 20 SHAABAN 1437
MAHUJAJI
WOTE
MNAOMBWAKUJISAJILI
KUJISAJILIMAPEMA
MAPEMA
MAHUJAJI WOTE MNAOMBWA
ILIKUWA
KUWANA
NAUHAKIKA
UHAKIKAWA
WASAFARI
SAFARIYA
YAHIJJA
HIJJA
ILI

15 Rajab 1436, jumatatu May 4 - 10, 2015

makala maalum

www.islamicftz.org

Historia ya Msumbiji
NA ABUU MAYSARA

aidi ya viongozi mia


saba (700) Waislamu
walishiriki katika kujibu dodoso hilo nchi
nzima ya Msumbiji kuanzia
1965 na kuhitimishwa 1967.
Mambo mawili makubwa ni
kuwa ilionekana ni muhimu
kufanya mchanganuo wa kina
kuhusu mtandao wa uongozi
wa Kiislamu na maeneo yenye
matawi ya Twariqa. Pia, kulifanyika mchanganuo wa kina
kuhusu hatari ya kisiasa kutoka
kwa Waislamu dhidi ya utawala
wa Wareno.
Lengo la Wareno ilikuwa ni
kuwaundia Waislamu uongozi
ambao ungekuwa kibaraka
kwao ili kuwazuia Waislamu
wasijiunge na Frelimo katika
mapambano yake dhidi ya Serikali. Ilisubiriwa tu fursa nzuri
ijitokeze ili kufanikisha mkakati
huo wa kuwadhibiti Waislamu.
Fursa ilijitokeza pale Sheikh
Magema mwaka 1963 alipokamatwa na polisi kwa
tuhuma za kuwa na uhusiano
na harakati za maadui wa
Wareno. Hatimaye, mwaka
1965 akafungwa ndani ya jela
yenye mateso ya kutisha ya Ibo
na akauawa akiwa gerezani
mwaka 1966.
Sheikh Magema hakuwa
kiongozi maarufu pekee kuuawa na Wareno ndani ya jela
ya Ibo. Kwa mujibu wa Muarabu Shauri, akitoa ushahidi

Mwaka 1971
tofauti za
kifiqh kati
ya Sheikh
Abubacar
Ismael
aliyehitimu
Chuo Kikuu
Madina na
masheikh
wa twariqa
kuhusu
jinsi ya
kusindikiza
jeneza kimya
au kwa sauti
ilitoa fursa
iliyosubiriwa
kwa hamu
na Wareno
kuwadhibiti
Waislamu.

Waislamu walivyotumika - 3
Kutokuelewana Waislamu mwanya kwa watawala

Muumini
wa dini
ya
Kiislamu
akiwa
msikitini
mjini
Maputo,
Msumbiji

mbele ya Kikosi Kazi Maalum cha


Umoja wa Mataifa mwezi Agosti
mwaka 1970, Sheikh Fazeira Yusuf
alipigwa risasi na kufa papo hapo
Januari 1965.
Oktoba 1965, viongozi wengi wa
Kiislamu walikamatwa huko MuiteMecuburi akiwemo Sheikh Buanamire au Panamiore Gicone, Pilale
Selege, Selemane Gicone, Mussa
Male na Navara Mulima kwa tuhuma za kuchanganya dini na siasa.
Hatimaye viongozi thelathini (30)
wa Kiislamu wakakamatwa na kuwekwa kizuizini, miongoni mwao,
Sheikh Pedro Limua Mustafa na Assoliane Avuleque. Huko Lalaua, madhila na mateso hayakuwalenga viongozi Waislamu pekee bali jamii
nzima ya Waislamu.
Mshauri wa Wareno aliandika All
the mosques were burned or destroyed, religious books seized, although it was suspected that many
had been buried, and the Islamized
population were compelled, to come
to the post headquarters, to submit to
a trial by eating pork.
Maana: Misikiti yote ilichomwa
moto au kubomolewa, vitabu vya
dini vikachukuliwa, ingawa ilihisiwa
kuwa vingi vilizikwa ardhini. Na wanajamii Waislamu walilazimishwa
kwenda makao makuu ya polisi kujisalimisha ili wafanyiwe majaribio
kwa kulishwa nguruwe.
Bwana Melo alishauri itafutwe
njia mbadala ya matumizi ya nguvu
dhidi ya Waislamu. Alieleza katika
uchambuzi wake kwamba ilioneka-

na wakati huo hakukuwa na uongozi


mmoja wa kitaifa wa Waislamu nchini Msumbiji na kwamba kila twariqa ilikuwa huru ikijiamulia mambo
yake.
Katika taarifa yake, Bwana Melo,
alihitimisha kwa maneno haya: Udhaifu wa Uislamu nchini Msumbiji
uko katika kukosekana kwa usare,
katika faraka za ndani na katika uongozi wake ulio rahisi kuvunjika. Kwa
hiyo Uislamu ni mkondo tu na siyo
nguvu.
Bwana Melo akashauri Waislamu
wanaweza kuvutwa kwa kuitafsiri
Quran yao kwa lugha ya Kireno.
Hapo ikawa mwanzo wa sera mpya
ya kuwakumbatia Waislamu ili
kupata maslahi ya kisiasa.
Desemba 17, 1968 (Ramadhan 26,
1388 Hijriyyah), Gavana wa Msumbiji Baltazar de Souza akatoa salamu
kwa Waislamu na kuwatakia heri ya
swaumu ya Ramadhan.
Dalili za kwanza za staratejia ya
Wareno kuwavuta Waislamu ilionekana katika picha aliyopigwa Gavana akiwa na Waislamu mashuhuri
wanne mara tu waliporejea kutoka
hija mwaka 1972. Kisha ikafuatia kitendo cha Serikali ya Wareno kuchapa tafsiri ya hadith kadhaa kutoka
Sahihi Bukhari kwa lugha ya Kireno.
Siku ya uzinduzi wa kazi hiyo Gavana
akawaalika masheikh maarufu wa
twariqa kisiwani Msumbiji akiwemo
Sheikh Momade Said Mujabo na
wengine 12 kutoka sehemu mbalimbali za Msumbiji.
Mwaka 1971 tofauti za kifiqh kati

ya Sheikh Abubacar Ismael aliyehitimu Chuo Kikuu Madina na


masheikh wa twariqa kuhusu jinsi ya
kusindikiza jeneza kimya au kwa
sauti ilitoa fursa iliyosubiriwa kwa
hamu na Wareno kuwadhibiti Waislamu.
Tofauti nyingine zilikuwa ni ziara
za makaburini na maulid. Wareno
wakapata nafasi kuwavuta zaidi
masheikh wenye msimamo wa
kwenda kwa sauti (wakiitwa Twaliki)
na wasoma maulid ambao walikuwa
wengi dhidi ya wenye kusindikiza
jeneza kimya kimya (wakiitwa Sukuti) na pia wakipinga maulid.
Said Mohammed Habib Bakar
ambaye alikuwa kiongozi wa matawi
zaidi ya 12 ya twariqa - l-Qaadiriyya
akatishia kuchukua hatua mkononi
dhidi ya kilichoitwa dini mpya kama
Serikali haikuchukua hatua.
Serikali ya Wareno ikamuomba
Mufti wa Comoro, Sayyid Omar bin
Ahmed kuja kumaliza mzozo huu
kuhusu bida. Mufti wa Comoro alipoamua dhidi ya wana sunnah wa
mwanzo wa Msumbiji, Wareno
wakawa wamekwishajenga heshima
yao miongoni mwa Waislamu wa
kaskazini ya Msumbiji na huo ukawa
mwanzo wa Waislamu kutumiwa na
watawala nchini humo. Ingawa
Sheikh Abubacar Ismael aliendelea
kuwasumbua Wareno, hatimae aliuawa kama walivyouawa masheikh
wenzake walioonekana kuwa tishio
kwa Serikali ya Wareno.
Kwa upande wake Serikali ya
Wareno ikazidisha ukaribu wake na
masheikh watiifu kwao, na Januari
1973 picha ya Gavana wa Kireno akishiriki katika sherehe za maulid ikapamba kurasa za mbele za magazeti
nchini humo.
Mwezi uliofuatia magazeti yakatoa picha na habari ya Gavana akiwakaribisha nyumbani mahujaji waliotoka hijja mwaka huo kwa gharama za usafiri za Serikali. Takrima ikanunua utiifu wao kwa Wareno.
Ni kwa jinsi hii Waislamu nchini
Msumbiji wakajikuta wakitumika
na kuunga mkono upande usio sahihi kwa kule kujiona wako salama
dhidi ya Wareno pasina kujua
kwamba upepo wa mabadiliko
ulikuwa unakuja.
Juni 25, 1975 Msumbiji ikapata
uhuru wake na si ajabu kwamba katika sherehe za uhuru Frelimo haikuwashirikisha viongozi wa Waislamu
kwa sababu haikuwahesabu kama
washirika wa harakati za uhuru bali
vibaraka wa Wareno.

15 Rajab 1436, jumatatu May 4 - 10, 2015

www.islamicftz.org

Msafara
wa Israa
na Miiraji
Na Sheikh Shabani Mussa

sraa na Miiraji: Haya ni maneno mawili


ya lugha ya kiarabu yenye maana mbili
tofauti. Al-israu ni neno lililochukuliwa
kutoka katika kitenzi Saraa Yasrii - Asraa ambalo kwa lugha ya watu wa Hijaz
linamaanisha mwendo au safari inayofanyika katika nyakati za usiku. Al-miirajuni
neno linatokana na kitenzi Araja -YaarujuUruujan likimaanisha lifti au ngazi inayotumiwa na malaika kuendea mbinguni.
Maana ya kiujumla

Al-Israu na Miiraju ni mjumuiko wa


misafara miwili iliyofanyika ndani ya usiku
mmoja: ule wa kutoka Makka mpaka Baitul
Maqdis (Palestina) wakati wa usiku unaoitwa Al-israu na ule wa kutoka Qudsi kwenda
mbinguni unaitwa Miiraji.
Aya zilizoizungumzia safari ya Israa
Allah anasema: Utukufu ni wake Yeye
aliyempeleka mja wake usiku (mmoja tu)
kutoka Msikiti Mtukufu (wa Makka) mpaka
msikiti wa mbali (Beytul Maqdis) ambao
(tumeubariki na) tumevibariki vilivyo pembezoni mwake, tulimpeleka hivyo ili tumuoneshe baadhi ya alama zetu. Hakika
Yeye (Allah) ni Mwenye Kusikia (na)
Mwenye Kuona(Al-israa aya ya: 1).
Aya zilizoizungumzia safari Miiraj:

Aya zinazozungumzia safari ya Miiraj katika Quran zinapatikana katika Suurat Annajm (53:1-18). Allah anasema: Naapa kwa
nyota zinapoanguka. Kwamba mtu wenu
(huyu Nabii Muhammad) hakupotea (kwa
ujinga) wala hakukosa, (hali ya kuwa anajua), Wala hasemi kwa matamanio (ya nafsi
yake), hayakuwa haya (anayosema)
isipokuwa ni wahyi uliyofunuliwa (kwake),
Amemfundisha (Malaika) Mwenye nguvu
(sana) Mwenye uweza (53:1 - 4).
Allah anaendelea: Na yeye (huyu) Jibril
akalingana sawa sawa. Na yeye yu katika
upeo wa kuona (katika mbingu kwa juu kabisa). Kisha akakaribia (kwa Mtume) na
akateremka. Ukawa (ukaribu wao) baina ya
upinde au karibu zaidi. Na akamfunulia
huyo Mtumwa wake (Allah) hayo aliyoyafunua, Moyo haukusema uwongo uliyoyaona. (Moyo wake ulisadikisha haya
yaliyotokea)(53:5 - 11).
Allah anaendelea: Je ! mnabishana naye
juu ya yale anayoyaona (daima)?Na
(Mtume) akamuona(jibril) mara nyingine
(kwa sura ile yake ya Kimalaika katika usiku
wa Miiraji). Kwenye Mkunazi wa kumalizikia mambo yote). karibu yake ndiyo kuna
hiyo Bustani, (pepo) itakayokaliwa (maisha
na watu wema), Kilipoufunika Mkunazi
huo kilichoufunika (katika mambo ya kiajabu ya mbinguni), Jicho halikupepesa wala
halikuruka mpaka (uliowekewa), Kwa yakini aliona (Mtume Muhammad) mambo
makubwa katika alama, (Qudra) za Mola
wake)(53:5 - 19).

Safari hii ilifanyika lini ?

Quran na vitabu vyote vilivyokusanya hadith za Mtume (Rehema na amani ziwe juu
yake) na vile vya Sira kwa pamoja vinathibitisha kufanyika kwa safari hii ya Israa na Miiraji, lakini tofauti kubwa iliyopo mbele ya
wanazuoni wa kale na sasa ni katika siku,
mwezi na mwaka iliyotokea safari hii
adhimu.
Imamu Ibnu Kathir(Allah amrehemu)
katika kitabu chake Al-bidayatu Wannihayatu 3/135 ananukuu kutoka kwa: Ibnu
Asakir kwa kuzitaja hadith nyingi zinazoihusu safari hii ya Israa na Miiraji kuwa,
Ilitokea awali ya kuteuliwa kwa Mtume
Muhammad (Rehema na amani juu yake).
Amma Ibnu Is-haq yeye alieleza kufanyika
kwa safari hii ilikuwa ..Kiasi cha Miaka
kumi baada ya kuteuliwa kwa Mtume Muhammad (Rehema na amani juu yake).
Na mapokezi ya Imamu Bayhaqiy kutoka
kwa Mussa bin Uqbah kutoka kwa Zuhriyakisema: Mtume alifanya safari ya Israa
Mwaka mmoja kabla ya kuelekea Madina.
Na kauli kama hiyo imetolewa pia na: Ibnu
Lahiyahkutoka kwa Abi As-wad naye kutoka kwaUr-wah.
Kisha Imam Hakimakapokea kutoka
kwa Al-As swammi naye kutoka kwa Ahmad bin Abdil-Jabbar naye kutoka kwa Yunus bin Bukayr naye kutoka kwa Asbaat bin
Nasri naye kutoka kwa Ismail Suddiy.
kuwa:Mtume alifaradhishiwa swala tano
Beytul Maqdis kwenye usiku aliopelekwa Israa miezi kumi na sita kabla ya kuhama.
Na kwa kauli ya Assuddiy safari ya Israa
ilifanyika katika mwezi wa Dhul-qaadah
wakati kwa kauli ya Zuhriy na Urwah safari
ya Israa ilifanyika Mwezi wa Rabiul-awwal.
Na amesema Abubakarbin Abi Shaybah:
Alitusimulia Athumani naye kutoka kwa
Saidbin Miynaa naye kutoka kwa Jabir na
Ibnu Abbas kwa pamoja walisema: Mtume
alizaliwa katika siku ya Jumatatu ya tarehe
kumi na mbili Mwezi wa Rabiul-awwal katika mwaka wa Ndovu,ndicho kipindi alichopewa Utume, alichopelekwa Miiraji
mbinguni, na ndani ya mwezi kama huo alihama na kufa. Lakini katika riwaya hii kuna
mkatiko. Na kauli hii ndio iliyochaguliwa na
kutumiwa na Al-hafidhu Abdul-ghaniybin

Sururi Al-maqdisiy katika kitabu chake cha


Sira, lakini ameitaja hadith ambayo Sanad
yake siyo sahihi.(Imam Ibnu Kathir anasema) tumeitaja riwaya hiyo (inayoeleza) Safari ya Israa ilifanyika tarehe Ishirini na saba
ya mwezi wa Rajabukatika fadhila za mwezi
wa Rajab. Na Allah ndiye Mjuzi zaidi.
Na kuna wanaodai kuwa, safari ya Israa
ilifanyika Ijumaa ya kwanza ya Mwezi wa
Rajabu, usiku ambao imezushwa ndani
yake swala mashuhuri na wala haina asili
inayofahamika kama swala ya (Araghaaib).
Na Allah ndiye Mjuzi zaidi.
Mtume katika safari hii alifuatana na malaika Jibril (Amani ya Allah iwe juu yake)
wakitokea nyumbani kwa Umu Hanii bint
Abi TwalibAllah amridhie.Kijiografia nyumba hii ilikuwa upande wa Shiibu ya Abi
Twalib, upande wa Mashariki ya mji wa
Makka kwenye eneo la Al-hujun, eneo ambalondipo alipokuwa anaishi Mtume kwa
kipindi hicho.
Malaika Jibril (Amani ya Allah iwe juu
yake)alimchukuwa Mtume kutoka nyumba
hiyo akiwa na athari ya usingizi na kwenda
naye mpaka kwenye Msikiti Mtukufu wa
Makka kwa safari ya Baytul maqdis. Na
ikumbukwe; safari zote mbili zilifanyika
ndani ya usiku mmoja.
Imethibiti kutoka katika hadithi sahihi
kwamba safari ya Israa na Miiraji ilianza
kwa Mtume kufanyiwa upasuaji ambapo alitolewa moyo, kusafishwa na kujazwa hekima na imani. Swahaba Abi DharriAllah amridhie, anasimulia kutoka kwa Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) akisema:
Likaezuliwa paa la nyumba yangu nami
nikiwa Makka, ghafla akateremka Jibril,
akakipasua kifua changu, kisha akakikosha
kwa maji ya Zamzam, kisha akaja na beseni
la dhahabu lililosheheni hekima na imani
na kuzijaza kifuani kwangu na kukifunga,
kisha akaukamata mkono wangu, na
kupanda nami mpaka mbinguni. (Rejea
Fat-hul baari: 1/460). Upasuaji huu ulifanyikia kwenye eneo la Hatwiym au
Hijri(kwenye eneo la Alkaabah). Na ulilenga kuusafisha na kuujaza moyo wa Mtume
hekima, imani na utayari wa kuzishuhudia
alama kubwa kubwa za Mola wake.
Na hii haikuwa mara ya kwanza kwa

Mtume(Rehma na amani ya Allah iwe juu


yake), kufanyiwa upasuaji kama huo, historia inaonesha Mtume (Rehma na amani ya
Allah iwe juu yake) alishafanyiwa upasuaji
kama huo alipokuwa na umri wa miaka mitano au sita, wakati anacheza na watoto
wenzake kwenye kijiji cha Baniy Saaidah
alikokuwa analelewa na Bi Halima
Saadiyah.
Hata hivyo, kila upasuaji ulikuwa na lengo lake.Upasuaji wa kwanza ulilenga
kukiondosha kilinge cha Shetani kwenye
moyo wa Mtume rehema na amani ya Allah
iwe juu yake na upasuaji wa pili ulilenga
kukijaza kifua cha Mtume hekima na imani.
Imepokewa kutoka kwa Anas bin Malik
anaeleza kwamba; Mtume alifuatwa na Jibril wakati anacheza na watoto, (Jibril) alimkamata na kumpiga mweleka, alikipasua
kifua chake na kuutoa nje moyo, na akalitoa
pande la damu moyoni mwake, kisha
akamwambia: Hiki ndio kilinge cha shetani
kwako, kisha akaukosha ndani ya beseni la
dhahabu kwa maji ya zamzam, alipomaliza
aliushona na kuurejesha kwenye sehemu
yake.
Watoto walikwenda mbio kwa mama
yake (yaya)na kumwambiaMuhammad
ameuawa. Walimchukuwa mama yake akiwa amebadilika rangi (kutokana na fazaa).
Swahaba Anas anasema: Nilikuwa ninaiona athari (ya mshono wa) shazia kifuani
kwake.Bi Halima alipouona msukosuko uliyompata mwanawe wa kulea aliingiwa na
wasiwasi na kuamua kumrejesha haraka
kwa mama yake.(Rejea Muslim 2/18 Babul
Israa).
Usafiri uliyotumika

Katika safari hiyo Mtume alisafiri kwa


mnyama mweupe wa peponi, mwenye kasi
ya ajabu, aliye na umbo la kati ya punda na
nyumbu, anayefahamika kama Buraaq.
Buraaq huweka kanyagio lake pale unapoishia upeo wa jicho lake.
Mtume (Rehma na amani ya Allah iwe
juu yake) alimtumia mnyama huyu katika
safari yake ya ardhini yaani- kutoka Makkah
mpaka Masjidul aqswa na kurudi Makkah.
Itaendelea toleo lijalo

15 Rajab 1436, jumatatu May 4 - 10, 2015

10

www.islamicftz.org

Je hutenguka udhu wa
mwanamke aliyemkosha najisi mwanawe?

VITu Vinavyotengua udhu

Swali: Aliulizwa Sheikh Muhamad bin Ibrahim Alu Sheikh (Allah


amrehemu): Mwanamke aliyetawadha kwa ajili ya swala halafu
mwanawe akachafuka na kuhitaji
kusafishwa najisi na kuogeshwa,
je tendo hilo hutengua udhu
wake?
Jawabu: Kama atagusa
moja ya tupu ya mtoto udhu
utatenguka, asipogusa utupu
udhu hautatenguka kwa sababu
ya kumkogesha mtoto. Hata
kama kuogesha kutapelekea kuigusa najisi kwa mkono wake,
anachotakiwa baada ya hapo ni
kusafisha mkono na kuchukua
tahadhari isitapakae najisi
kwenye kiwiliwili au kwenye
nguo zake. (Fataawa na Rasailu
za Sheikh Muhamad bin Ibrahim 2/75).

udhu unachanguka au la?


Jawabu: Hauchanguki udhu wa
mtu aliyetawadha kwa kuisafisha
najisi iliyo kwenye kiwiliwili
chake au cha mtu mwingine,
isipokuwa kama aligusa utupu
wa mtoto. Kwa kugusa utupu
ndio udhu utatenguka. Hakuna
tofauti na mtu kugusa utupu
wake mwenyewe. (Majallatul
buhuthil Islamiyah 22/62)

Je huchanguka udhu
wa mtu aliyeosha
najisi ya watoto
wake?
Swali: Iliulizwa kamati
ya kudumu ya fat-waa:
Mimi nina wana wadogo,
na nilishatawadha, na nikaosha najisi za wanangu, je

Je kugusa utupu
wa
mtoto
mdogo ku-

natengua udhu?

Swali: Iliulizwa kamati ya kudumu ya fat-waa: Je kugusa utupu wa


mwanangu mdogo wakati wa kumbadilisha nguo zake kunatengua
udhu wangu?
Jawabu: Kugusa utupu bila ya
kiziwizi kunatengua udhu, sawa utupu uliyoguswa ni wa mtoto au wa mtu
mzima. Haya yanathibitishwa na
kauli ya Mtume (Rehema na amani
ya Allah juu yake), pale aliposema:
Mtu atakayegusa utupu wake na atawadhe. Na utupu wake hauna tofauti
na utupu wa mtu mwingine. (Fataawa lajnatud Daimah 5/265).

Je kutoka upepo kwenye utupu wa mwanamke kunatengua udhu?

Swali: Aliulizwa Sheikh Muhamad bin Swaleh Uthaimin (Allah


amrehemu): Je kutoka upepo
kwenye utupu wa mwanamke ku-

natengua udhu?
Jawabu: Hili halitengui udhu,
kwani upepo huo haukutoka mahali
pa najisi, kama utokavyo ushuzi
kwenye njia ya haja kubwa. (Fataawa
na Rasailu za Sheikh Uthaimin
4/197).

Je kutoka upepo kwenye utupu wa mwanamke kuna batilisha


swala ?

Swali: Iliulizwa kamati ya kudumu ya fat-waa: Mwanamke anaposwali, na kwenda rukuu na sujudu,
na mara nyingi (hali hii hutokea) anaposujudu na anapoketi baina ya sijida mbili, na anapoketi kwa ajili ya kutoa shahada, hutokwa na upepo
kwenye utupu wake, kiasi cha kusikiwa na walio pembezoni mwake, je kitendo hicho kinabatilisha swala ya
mwanamke? Na wakati mwingine
hutokwa upepo kidogo mno kiasi cha

fat-wa kwa mwanamke wa kiislam


sheikh Shabani Mussa

kutosikiwa na yeyote, je nayo inabatilisha udhu na swala?


Jawabu: Kutoka upepo kwenye
tupu ya mbele hakutengui udhu. (Fataawa lajnatud Daimah 5/259).

Je kumgusa mwanamke
kunatengua udhu?

Swali: Aliulizwa Sheikh Muhammad bin Swaleh Uthaimin: Je


kumgusa mwanamke kunatengua
udhu?
Jawabu: Kauli iliyo sahihi, kiujumla kumgusa mwanamke
hakutengui udhu, isipokuwa kama
atatoka kitu. Ushahidi wa hili ni yale
yaliyothibiti kuwa Mtume (Rehma
na amani ziwe ju yake) alikuwa anawabusu baadhi ya wake zake na kuingia kwenye swala bila ya kutawadha
(tena) kwani asili ni kutochanguka
udhu, mpaka ipatikane dalili sahihi
tena ya wazi inayothibitisha
kuchanguka udhu. Mtu alishatimiza
twahara yake kwa muktadha wa dalili
ya kisharia, na kilichothibiti kwa
muktadha wa kisharia hakiondoshwi
isipokuwa kwa dalili ya kisharia, na
kama utatolewa ushahidi wa neno la
Allah Au mmewagusa wanawake
(An Nisaa aya ya: 43), Au mmeingiliana na wanawake (Al-Maidah aya
ya: 6). Jawabu: Muradi wa (Al-mulaamasah) katika aya ni kuundama
kama ilivyothibiti kutoka kwa Ibn
Abbas. (Fataawa na Rasailu za Sheikh
Uthaimin 4/201).

afya yako

Pazi Mwinyimvua

tafiti mbalimbali unaonyesha


kuwa karibu asilimia 90 ya
magonjwa sugu yanayomkabili binadamu huanzia tumboni, hasa kutokana ulaji usiofaa.
Kiharusi, mshtuko wa moyo, matatizo
ya figo, kisukari, kuhara, unene na uzito
kupita kiasi, saratani, kukosa choo kikubwa
na upungufu wa nguvu za kiume na kike ni
baadhi ya magonjwa yanayoweza
kuchangiwa na ulaji usiofaa. Licha ya hali
hiyo inayotishia afya, baadhi ya matangazo
ya biashara ya vyakula yanawateka watu
wengi na kuwaingiza katika ulaji mbaya.
Ufahamu sahihi juu ya namna chakula kinavyonufaisha au kudhuru afya ya mlaji ni
njia madhubuti itakayoiokoa jamii.
Dini ya Kiislamu inamafundisho mengi kuhusu chakula, ikiwemo tahadhari
kadhaa kwa wanadamu kuhusu kile wanachokitia katika matumbo yao. Kwa leo tujifunze hadith moja tu ya Mtume Muhammad (Rehema na amani zimshukie).
Mtume anasema: Hajapatapo mwanadamu kujaza chombo kilicho na shari kuliko tumbo lake, vyamtosha mwanadamu
vijitonge vitakavyousimamisha uti wake
wa mgongo. Kama hakufanya hivyo (ikiwa
hapana budi kula) basi theluthi moja iwe
ni ya chakula na theluthi (ya pili) iwe ni ya
maji na theluthi (ya mwisho) iwe ni ya
pumzi (Ahmad, Ibn Majah na Hakim).
Namna kuu tatu ambazo ulaji usiofaa
unavyoweza kusababisha maradhi ama
hata kifo ni kula chakula kingi kupita mahitaji ya mwili, kula chakula kisichoweza
kuupa mwili virutubisho vyote vinavyohitajika na kula chakula chenye sumu au vijidudu vinavyosababisha maradhi.
Kula sana vyakula vyenye mafuta na lehemu mbaya (bad cholesterol) kunaweza
kuharibu mishipa ya damu na kusababisha
ugonjwa wa kiharusi. Kula sana vyakula

Chakula kinavyoweza kudhuru afya

Mtu akikosa vyakula vya


protini mwili utanyongea
na atapata matatizo ya
moyo na viungo vingine
kushindwa kufanya kazi
vyenye chumvi nyingi huongeza kupita kiasi madini ya sodium ambayo yanaongeza
shinikizo kubwa la damu.
Kula sana vyakula vya wanga na mafuta kunaongeza uzito na unene kupita kiasi
na hivyo mtu kuwa katika hatari ya kupata
ugonjwa wa kisukari, kiharusi, presha ya
kupanda, baadhi ya viungo kufanya kazi
kwa tabu, maumivu ya mifupa, magonjwa
ya moyo na aina mbalimbali za saratani.

Kunywa maji kiasi kidogo kwa siku na


kula vyakula visivyokuwa na nyuzi lishe
(dietary fibers) huchangia mtu kukosa
choo kikubwa. Mtu apate choo kikubwa
angalau mara moja kwa siku. Kukosa choo
kikubwa kwa wakati kunaweza kusababisha sumu na bakteria wabaya waliomo katika kinyesi kuingia katika mfumo wa
damu. Kukosa choo kikubwa pia kunapelekea magonjwa ya utumbo mpana na hata

kupoteza maisha pale iwapo kinyesi kitaganda sana katika utumbo na operesheni
ikachelewa kufanywa kwa mgonjwa.
Mtu akikosa vyakula vya protini mwili
utanyongea na atapata matatizo ya moyo
na viungo vingine kushindwa kufanya kazi.
Vyakula vinavyotokana na wanyama ni
chanzo kizuri cha protini kutokana na
kuwa na virutubisho vyote muhimu vya
amino acids.
Karanga, maharage na soya pia vina vitamini kwa wingi. Samaki ni chanzo kizuri
cha protini na mafuta mazuri kiafya, na
yana Omega 3 inayosaidia kumwepusha
mtu kupata magonjwa ya moyo. Hata
hivyo, ulaji wa nyama nyekundu kama vile
ngombe, mbuzi, kondoo na ngamia ziliwe
isizidi nusu kilo kwa wiki.

Miaka milioni mbili iliyopita binadamu alikuwa anakula vyakula vya asili kama
nyama, samaki, matunda, mbogamboga,
jamii ya karanga, mbegu na baadhi ya
vyakula vya mizizi. Zaidi ya hayo, watu walikuwa wanatembea sana kwa miguu, wanafanya kazi za kutoka jasho, hawakai chini muda mrefu na walikuwa wanaishi kijamii na kusaidiana.
Siku hizi katika miji, watu wengi wanatumia vyakula vilivyosindikwa viwandani
ambavyo mara nyingi vina sukari, mafuta
na chumvi nyingi. Vitu hivyo ni hatari sana
kwa afya. Pia, vyakula vilivyosindikwa viwandani vina kemikali zinazovifanya
vyakula hivyo visiharibike haraka. Kemikali hizo zinaweza kudhoofisha afya ya
mlaji.
Zaidi ya hayo, watu wengi siku hizi katika miji wanakaa sana ofisini, wanakaa
sana kutazama televisheni na kutumia
simu, kuingia katika intaneti, au kucheza
michezo kwa kutumia kompyuta au simu.
Vilevile, watu wengi hawalali vya kutosha, licha ya kuwepo ushahidi wa kisayansi
unaomtaka kila mtu mzima kulala kwa saa
7-10 kwa siku ili mwili ufanye kazi vizuri.
Matokeo ya kutolala vya kutosha watu
wengi wana msongo wa mawazo wa kudumu.
Salama ya mwanadamu wa sasa ni kurudi katika asili, kama mwili wake ulivyoumbwa. Mwanadamu anatakiwa ale vyakula vya asili vilivyo sawa na mpango wa vinasaba na baolojia. Pia, kula kwa kiasi, kupunguza chumvi, mafuta, sukari na kemikali katika vyakula. Kurudi katika asili pia
ni pamoja na kutembea kwa miguu baadhi
ya nyakati, kuishi pamoja na kusaidiana,
na kuushughulisha mwili kwa kufanya
mazoezi au kazi za kutoka jasho.
0754 654 900

15 Rajab 1436, jumatatu May 4 - 10, 2015

11

www.islamicftz.org

uchumi na biashara
JAMAL ISSA

Hayo ni kwa
kuwa wamesema: Biashara
ni kama riba
(Quran 2:275)
Sifa njema na shukran
anastahiki yule ambaye
ametukamilishia dini
yetu na akairidhia kuwa
utaratibu kamili wa maisha yetu. Rehma na amani zimfikie kipenzi chetu
mtume Muhammad (Rehma na amani ziwe juu
yake) pamoja na wanaofuata muongozo mpaka
siku ya mwisho.
Ndugu mpezi msomaji
karibu tena katika mfululizo wa makala zetu juu
ya biashara na uchumi
katika Uislamu.
Katika makala ya leo
tutadurusu juu ya riba.
Somo hili kwa kweli ni
pana na halijulikani na
wengi, kwani riba ipo katika namna nyingi sana.
Uchumi wa Kiislamu
umejengwa juu ya msingi
madhubuti usiojikita katika riba. Allah ameharamisha riba na akahalalisha biashara kama anavyotufahamisha katika
Qurani tukufu: Lakini
Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na
ameiharimisha riba
(2:275).
Kwa uzito wa uharamu wa riba, Mtume (Rehma na amani ziwe juu
yake) akaichagua kuwemo katika mambo ya
msingi ya kutuonya katika khutba yake ya
mwisho.
Baada ya kumshukuru
Allah alianza khutba kwa
kusema: Enyi watu!
Nisikilizeni maneno yangu vizuri, kwani sidhani
kama baada ya mwaka
huu nitakuwa pamoja
nanyi. Hivyo sikilizeni
kwa makini nitakayoyasema na (maneno haya)
mfikishieni kila asiekuwepo hapa leo.
Baada ya kusema

Ukweli kuhusu riba


maneno mengine, akasema, Allah amekukatazeni kula riba. Hivyo riba
zote zimeondoshwa na
mna haki ya kubaki na rasilimali (mitaji) yenu.
Hamna haki ya kudhulumu wala kudhulumiwa.
Allah ameharamisha riba
na riba zote za Abbaas ibn
Abdul Muttallib zimeondoshwa.
Riba twaweza kuifasiri
kwa maana ya jumla
kama ziada anayoipata
mtu bila kuitolea jasho
kwa kufanyakazi.
Kwa mfano; mtu au
taasisi ya kifedha inayotoa mkopo kwa riba,
mkopaji anarudisha
mkopo na ziada (riba)
ambapo mkopeshaji
ananufaika na ziada hiyo
bila kuitolea jasho.
Riba sio sawa na biashara kwa sababu haikidhi vigezo vya biashara,
kwani kwenye biashara
kuna uwezekano wa
kupata hasara au faida,
lakini kwenye riba kuna
uwezekano wa kupata faida tu.
Kwenye utaratibu wa
ukopeshaji wenye riba
mkopeshaji anakuwa ana
kinga ya kutopata hasara,
kwani mkopeshwaji
hulazimika kulipa mkopo
wake pamoja na kiasi
kingine cha ziada kama
riba kwa hali yoyote ile
hata bila kuzingatia amepata hasara au faida katika biashara aliyowekeza
mkopo huo.
Hivyo utaratibu huo
husababisha dhuluma,
unyonyaji na kuwafanya
wakopaji watumwa wa
kuwatumikia wakopeshaji na hatimae wanaishia kunasa katika
dimbwi la madeni na
umaskini.
Uchumi uliojengwa

Moja ya taasisi
ya fedha ya
Kiiskamu
ambayo hutoa
mikopo bila
riba.

katika misingi ya riba huwafanya


matajiri wadumu katika utajiri na
maskini wadumu katika umaskini, na hudumisha tofauti kubwa
ya kipato - income inequality
baina ya matajiri na maskini,
kwani mlango wa ugawaji wa kipato - income distribution hufungwa kwa kuwapa kinga matajiri ya kupata hasara na kuwa na
uwekezaji usiokuwa na hatari ya
kupata hasara - risk free investment, ambapo kundi kubwa la
maskini na watu wa kipato cha
chini na kati hubeba hasara hiyo.
Mwenyezi Mungu huiondolea
baraka riba, na huzibariki sadaka.
Na Mwenyezi Mungu hampendi
kila mwenye kukana na afanyae
dhambi (2:276).
Aya hii inatuwekea bayana
yakua uchumi au biashara ambayo imejengwa katika msingi wa
riba, Allah huiondolea baraka, bilashaka baraka ya Allah Subhanaahu Wataallah ikiondoka
matatizo ya kiuchumi na biashara
hayawezi kuisha na hatuwezi
kuwa na uchumi madhubuti
usioyumba.
Jambo lingine muhimu kulidurusu hapa ni upi uhusiano wa
riba na sadaka? Kama tulivyoona

Mwenyezi
Mungu
huiondolea
baraka
riba, na
huzibariki
sadaka. Na
Mwenyezi
Mungu
hampendi
kila mwenye
kukana na
afanyae
dhambi
(2:276)
Allah alivyohusianisha riba na biashara. Kwanini hapa tena anahusianisha riba na sadaka?
Kwa kweli mtoaji sadaka hutoa
bila ya kutaraji kunufaika na chochote kama ziada, isipokuwa
kumridhisha Allah kwa kuwasaidia viumbe wake na kuwatizama kwa jicho la rahma, lakini riba

ni kinyume cha sadaka, kwani


anayekopesha kwa riba hukopesha ili kujinufaisha kwa kupokea
ziada.
Hivyo, riba hujenga jamii ya
watu wanyonyaji, wasiojali na kuguswa na hali za binaadamu wenzao na riba hujenga jamii ya
wenye kujali na kuguswa na hali
za wenzao na hutengeneza jamii
yenye kusaidiana na kunyanyuana kiuchumi.
Aidha Uislamu una mtizamo
tofauti kabisa katika dhana nzima
ya kuongeza na kukuza mali.
Wapo wanaofikiria kwa kutumia
riba wanaweza kuongeza na
kukuza mali zao, Uislamu umeruhusu biashara na kuamrisha
zaka na kuhamasisha sadaka ili
kuongeza mali na mgawanyo wa
kipato katika jamii.
Allah anasema: Na mnachokitoa kwa riba ili kiongezeke katika mali ya watu, basi hakiongezeki mbele ya Mwenyezi
Mungu. Lakini mnachokitoa kwa
zaka kwa kutaka radhi ya
Mwenyezi Mungu, basi hao ndio
wataozidishiwa(30:39). Leo imekuwa jambo la kawaida si tu katika mfumo wa kifedha na uchumi kujikita katika riba, bali hata
kwa baadhi ya Waislamu kuchukua mikopo yenye riba katika
taasisi za kifedha kama benki na
vyama vya kuweka na kukopa
(SACCOS) kwa ajili ya biashara
zao wakidhani eti watafanikiwa.
Allah anatufahamisha kwa
kusema, Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni
riba zilizobakia, ikiwa nyinyi ni
Waumini.Basi msipofanya jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu
na Mtume wake. Na mkitubu,
basi haki yenu ni rasilimali zenu.
Msidhulumu wala msidhulumiwe (2:278-279).
Enyi mlioamini! Msile riba
mkizidisha juu kwa juu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kufanikiwa (3:130).
Vipi tutafanikiwa kuwa na
uchumi bora, imara, endelevu na
biashara zenye mafanikio ilihali
tumejikita katika riba wakati Allah na Mtume wake wametangaza vita dhidi ya wanaojihusisha na
riba na Allah amewalaani?!!!
Kujua aina za riba, usikose toleo lijalo In sha Allah.
jakham@rocketmail.com,
0713 996 031

Watu maarufu wasiokuwa Waislamu wasemavyo kuhusu Uislamu


James A. Michener (1907-1997):
Mmarekani, mwandishi maarufu wa vitabu
aliyepewa digrii ya pili ya heshima (Honorary Masters) katika nyanja tano kutoka
vyuo vikuu vikubwa 30 duniani na ambaye
pia alipewa medali ya Rais wa Marekani
ijulikanayo kama Presidential Medal of
Freedom, ambayo ni medali ya juu zadi ya
kiraia nchini Marekani alisema:

No other religion in history spread so rapidly as Islam.


The West has widely believed that this surge of religion
was made possible by the sword. But no modern scholar
accepts this idea, and the Quran is explicit in the support of
the freedom of conscience. (Islam: The Misunderstood Religion,
Readers Digest, May 1955, uk. 68-70)
Tafsiri: Hakuna dini nyingine katika historia iliyoenea kwa kasi kama Uislamu. Ulimwengu wa kimagharibi umeamini sana kwamba kuibuka huku kwa dini (ya Uislamu) kuliwezeshwa na jambia. Lakini hakuna
msomi wa kisasa anayekubali fikra hii, na Quran iko wazi katika kuunga mkono uhuru wa mawazo.

15 Rajab 1436, jumatatu May 4 - 10, 2015

12

www.islamicftz.org

ncha ya kalamu
Sheikh Muhammad Issa

Wanasiasa wasiwaogope viongozi wa dini


N

i mara nyingi
tumesikia
Msichanganye
dini na siasa
huku sababu kubwa inayotolewa ni kwamba dini haina nafasi katika maisha ya
kijamii ya nchi ya kisekula,
bali ni jambo linalomhusu
mtu binafsi.
Katika nchi za kidemokrasia ya kweli siyo tu dini na
wana dini hujihusisha na siasa, bali kuna vyama vya kisiasa vya kidini vinavyoshiriki
katika uchaguzi na hata kutawala na hakuna jambo linaloharibika. Nchi hizo zina
maendeleo makubwa tu kiuchumi, kijamii na kiteknolojia.
Baadhi ya nchi hizo barani
Ulaya na majina katika vyama
husika katika mabano ni Albania (Christian Democratic
Party), Ubelgiji (Christian Social Party), Ujerumani (Christian Democratic Union (CDU)
ambacho kinasemwa kuwa ni
mshirika wa karibu wa Chadema.
Barani Asia, nchi zenye vyama vya kisiasa vya kidini ni Indonesia, nchi yenye idadi kubwa
ya Waislamu duniani (Christian
Democratic Party) na Samoa (Samoan Democratic United Party).
Kwa Afrika, nchi zenye vyama
vya kidini ni Rwanda Christian
Democratic Party, Afrika ya Kusini
vyama saba vya kidini- African
Christian Democratic Party, United Christian Democratic Party,
Christian Democratic Alliance, Al

Jama-ah Muslim Political Party,


Christian Democratic Party, African Muslim Party, Christen Party/
Christian Party.
Edmund Burke katika kitabu
chake: Thoughts on the Cause of
Present Discontents aliandika:
The only thing necessary for the
triumph of evil is for good men to
do nothing yaani, Kitu pekee
muhimu kuwezesha uovu kushinda ni pale watu wema wanapokaa
pasina kufanya chochote.
Lakini katika nchi zetu hizi zinazojifunza demokrasia, wanasiasa wanataka viongozi wa dini ambao kimsingi ndiyo watu wema zaidi katika jamii, wasipaze sauti
kukemea maovu yatendwayo na
watawala kwa kisingizio cha dini
isichanganywe na siasa.
Nionavyo, madai haya si kweli,
bali ni woga wa wanasiasa kuogopa
viongozi wa dini. Ni namna ya
watawala hasa wa nchi za kiafrika
kunyamazisha sauti za viongozi wa
dini ambao mamilioni ya watu huwasikiliza na kuwatii.
Tunapoelekea katika uchaguzi
mkuu 2015 tutasikia sana kauli za
watawala kuwakemea viongozi wa
dini wasijiingize katika siasa. Huu
ni woga unaotokana na uchu wa
kungangania madaraka au wanaogopa kivuli chao wenyewe kwa
sababu hawakuwajibika ipasavyo.
Ni kutokujiamini.
Kuelekea uchaguzi mkuu wa
Uingereza wa 2015, Kanisa Anglikana limetoa waraka likiwashauri waumini wake jinsi ya kushiriki
katika uchaguzi mkuu. Waraka
huo unakichwa cha habari New
Kind of Politics yaani Aina mpya

Tunapo elekea katika


uchaguzi mkuu 2015
tutasikia sana kauli
za watawala kuwa
kemea viongozi wa dini
wasijiingize katika
siasa. Huu ni woga
unaotokana na uchu
wa kunga ngania
madaraka

ya siasa uliwataka wakristo kutumia kura zao prayerfully yaani kiibada.


Kimsingi kudai kuwa dini na
siasa havichanganyiki ni kuvunja
Katiba ya Jamhuri ya Muungano
ya 1977 ibara ya 18 (1) (a) (c) isemayo: kila mtu-(a) anao uhuru wa
kuwa na maoni na kueleza fikra
zake; (b) anayo haki ya kutafuta,
kupokea na kutoa habari bila ya
kujali mipaka ya nchi; (c) anao
uhuru wa kufanya mawasiliano na
haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake.
Kuna kosa gani kwa kiongozi
wa dini kutoa nje mawazo yake
kuhusu jambo lolote la nchi yake?
Au viongozi wa dini hawana mawazo juu ya haya yote wayaonayo
au wayasikiayo yakitendwa au
kusemwa na wanasiasa? Dhana ya
kutengeanisha dini na dola iliyoibuka huko Ulaya karne ya 18 ambayo ndiyo msingi wa usekula
haikulenga kuwanyamazisha vi-

ongozi wa dini wasijihusishe na


siasa, bali ililenga kuwazuia watawala wasiingilie dini.
Na dhana hii ndiyo inayokubaliana na mantiki kwa sababu watawala hawana mashiko ya kuingilia
mambo ya dini, kwani usekula
hauna mafundisho kuhusu dini.
Usekula ni fikra za watu, wakati
dini ni mafundisho ya Mungu.
Kinyume chake viongozi wa
dini wanaweza kujihusisha na
mambo ya siasa na utawala kwa
sababu maandiko ya dini zao
yamesheheni maelekezo kwa waumini wa dini hizo kuhusu siasa na
utawala. Ndiyo maana hata wanaposhika madaraka watawala huapa kwa mujibu wa dini zao.
Uhuru wa mawazo hauwezi
kwenda pasina uhuru wa kutoa na
kupata au kupewa habari, uhuru
wa vyombo vya habari, uhuru wa
kukusanyika watu pasina kuvunja
sheria na haki ya wananchi kuwakosoa watawala. Vinginevyo tu-

natengeneza udikteta kwa jina la


demokrasia. Kuwanyamazisha viongozi wa dini wasitoe mawazo
yao nje kuhusu mambo mbali
mbali yahusuyo nchi yao iwe ni
katiba mpya, uchaguzi au jinsi nchi
inavyoendeshwa ni kuinyima nchi
fursa ya kunufaika na mawazo ya
watu wema katika jamii ili maovu
na waovu wapate kushinda.
Kama si hivyo ni nini maana ya
siasa? Jibu fupi na zuri kabisa la
swali hili lilitolewa na mwanafalsafa Mgiriki, Aristotle aliposema:
Politics is how ought we to order
our life together yaani Siasa ni
kuhusu jinsi gani tutakavyoyapangilia maisha yetu kwa pamoja.
Sasa huku kuwazuia viongozi
wa dini wasiseme kuhusu siasa kunatoka wapi? Kwa msingi wake
siasa ni utashi wa kimaadili ndiyo
maana kuna maadili ya viongozi
ambayo yalitegemewa kuhakikisha kuwa viongozi wa kisiasa wanatenda haki. Neno haki lenyewe
ni neno la kiroho linalofundishwa
katika vitabu vya dini.
Ni jinsi gani tutapanga maisha
yetu kwa pamoja ambayo ndiyo
siasa inatuhitaji sote tushiriki.
Kuzizuia fikra za wananchi kwa
kuwa tu mawazo yao ni ya kidini ni
mtazamo kinyume kabisa na
demokrasia shirikishi ambayo
ndiyo msingi wa nchi za dhana ya
demokrasia ambayo Tanzania tunaifuata. Kwa msingi huu, misikiti,
makanisa na mahekalu yako katika hadhi sawa kikatiba na vyama
vya siasa, vyama vya wafanyakazi/
wanataaluma, wakulima na asasi
nyingine zilizoanzishwa kwa
malengo maalum.
Hata kama chama cha kisiasa
kingeasisiwa katika misingi ya dini
kama vile tulivyovitaja awali,
inapokuja kwenye masuala ya kisiasa hoja ni kama alivyosema Aristotle: jinsi gani tutapanga maisha yetu kwa pomoja na si dini
moja kwa moja. Kufanya hivyo
ndiyo salama kwa taifa.
Unapozuia mawazo ya viongozi
wa dini yasitolewe hadharani, unachochea mawazo hayo kutolewa
sirini jambo ambalo ni hatari kwa
taifa. Nchi nyingi ziliingia katika
machafuko kwa sababu ya kuzuia
wananchi kutoa mawazo yao hadharani.
Kuwanyamazisha viongozi wa
dini wasitoe mawazo yao nje hakuna maslahi kwa taifa, na ni hatari
kwa mustakabali wa taifa. Ni wito
wa kutaka uovu ushinde kama alivyosema Edmund Burke: Kitu
pekee muhimu kuwezesha uovu
kushinda ni pale watu wema wanapokaa kimya pasina kufanya chochote. Je, ndivyo tunavyotaka iwe
kwa Tanzania yetu?
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiwa na viongozi wa dini jijini
Dar es Salaam.

15 Rajab 1436, jumatatu May 4 - 10, 2015

13

www.islamicftz.org

Mahusiano ya kibinadamu
USTAADH HABIB HAMIM

Maana ya ulemavu

Hii ni safu mpya katika


gazeti la Imaan inayohusiana na habari za walemavu ambao ni sehemu
muhimu katika jamii yetu.
Lengo la makala hizi ni
kuelimishana kuhusu
ulemavu, maana yake, aina
za ulemavu, haki zao, na
muhimu zaidi ni kuhusu
njia nzuri ya walemavu
kuishi vizuri katika jamii na namna bora jamii
inapaswa kuishi na walemavu.
Katika makala haya ya kwanza nitazungumzia maana ya ulemavu na
maana ya mtu mwenye ulemavu. Katika kuangalia tafsiri ya ulemavu niliangalia vitabu kadhaa hapa Tanzania

na nje ya nchi hususan Sudan ambako niliishi na kusoma kwa muda mrefu.
Ulemavu kwa ujumla unatafsiriwa
kuwa ni kukosa au kushindwa kuwa
na fursa ya kushiriki katika maisha ya
kawaida ya kijamii kwa kiwango sawa
na wengine kwa sababu za kimaumbile, kiakili au sababu za kijamii. Ulemavu unaweza kuwa katika maeneo
yafuatayo: kuona, kusikia, akili, viungo kama mkono au mguu, kuongea,
tabia au ulemavu mchanganyiko.
Kwa hiyo basi, ulemavu unaweza kupelekea ugumu wa kutembea, uzito
wa kujifunza, utamkaji wa shida, na
kujitenga katika eneo fulani la tabia.
Ulemavu mwingine huhitaji uangalizi maalum.
Kwa upande mwingine, mtu

mwenye ulemavu ni mtu mwenye udhaifu au upungufu wa viungo, fahamu au akili kwa muundo wa kudumu,
na ambaye uwezo wake wa utendaji
kazi umepungua kutokana na vikwazo vya kimtazamo na kimazingira.
Mtu mwenye ulemavu anaweza kuwa
ameathirika kimwili, katika kuona,
kiakili, kisaikolojia, kielimu au kimawasiliano na atakuwa amepungukiwa
na uwezo wa kujisimamia mambo
yake ya kawaida katika mazingira ya
kijamii. Mfano wa ulemavu ni kukosa
uwezo wa kuona. Hii ndio maana ya
ulemavu, wiki ijayo Mola Muumba
akipenda, tutazungumzia aina
mbalimbali za ulemavu.
habibmitwe@yahoo.co.uk
0718 561 149

mapitio ya vitabu
Kitabu: Al Fusuul Fii Mustwalahi
Hadiithi r-Rasuuli
Mwandishi: Haafidh Thanaau-llwaahi Zaahidy
Mfasiri: Sheikh Muhammad Issa

Mlango wa Tatu - Waitwavyo wapokezi wa


hadith
Swahaabiyyu: Ni kila Muislamu
aliyekutana na Mtume (Rehma na
amani ziwe juu yake) akiwa mwenye
kumwamini na akafa katika imani.
Na maswahaba wote ni wenye
kutegemewa na waadilifu. Kutokujulikana kwao hakuathiri usahihi (wa
hadith husika).
Taabi: Ni yeyote yule aliyekutana na swahaba katika hali ya imani
na akafa katika hali hiyo. Inatakikana ili kukubalika upokezi wake awe
mwenye kutegemewa.
Tabu Taabi: Ni yeyote yule aliyekutana na Taabi miongoni mwa
waumini, na inatakikana ili kukubalika upokezi wake awe mwenye
kutegemewa
At-Thiqah: Ni yeyote yule aliyekusanya baina ya uadilifu na ukamilifu wa kuthibiti mambo na kufanya vizuri na uadilifu. Inampasa
mpokezi wa hadith awe mwenye
kushikamana na ukweli na uaminifu
na uchaMungu na kusalimika kwake
na shirki na bida na ufaasiq na uovu
na kukosa maadili mema.
Na muradi wa udhibiti wa mpokezi na kufanya kwake uzuri: Ni kule
kusikia kwake simulizi kama inavyotakikana, kuifahamu kwake ufahamu wa ndani na kuhifadhi kamili
pasi na kusitasita na kumakinika
kwake katika yote haya kutoka waka-

ti wa kusikia hadi wakati wa kuisimulia (yeye).


Al-Adlu: Ni Muislamu aliyebaleghe, mwenye akili timamu ambaye hutekeleza faradhi na anayejiepusha na madhambi makubwa na
asiyedumu katika madhambi madogo madogo. Na anajiheshimu kwa
tabia njema na ada nzuri nzuri.
Ad-dhwabtu: Ni yule ambaye
hufanya uzuri katika aliyoyahifadhi
kifuani mwake katika hadith kwa
namna ambayo huzikumbuka kwa
usahihi wakati wowote ule atakao ili
kuzisimulia, au amehifadhi katika
kitabu chake ambacho ameandika
ndani yake mapokezi yake na akakilinda dhidi ya kufutika na kubadilika na kuharibika na mfano wa hayo.
Na hufahamika kuwa kwake mwenye
kudhibiti kwa kuafikiana upokezi
wake na upokezi wa wengine wenye
udhibiti na uhifadhi katika matamshi na aghlabu katika maana.
Al-Mutqinu: Ni Mwenye
udhibiti pamoja na kuwa na ziada ya
nguvu kubwa ya udhibiti
At-thabtu: Ni Muadilifu
mwenye udhibiti kwa daraja la juu
kabisa la nguvu za udhibiti.
Al-Haafidhu: Ni yule aliyehifadhi hadith laki moja, matini na Isnadi (mtiririko wa upokezi wake hadi
kwa Mtume) kwa mujibu wa rai mojawapo. (Mfano Al-Haafidh Ibn
Hajar Al Asqalaaniy, Al Haafidh Ibn
Rajab n.k)
Al Hujjat: Ni yule ambaye elimu
yake imesheheni hadith laki tatu
(kutokana na rai mojawapo). Na upokezi wa kila mmoja miongoni mwa
hao ni sahihi na wenye kukubalika
na iwapo utungo wa upokezi wake
utaepukana na kukatika au kup-

wekeka na kuwa na ila


Ad-dhwaifu: Ni mpokezi ambaye udhibiti wake umepungua au
uadilifu wake umeporomoka. Na upokezi wake ni dhaifu na wenye kukataliwa iwapo atapwekeka nao. Iwapo
utapatilizwa (na upokezi mwingine)
huondoka udhaifu wake kwa kule
kupatilizwa
Majhuulul-ayn: Na huitwa (vile
vile) Majhuul-adaalat Dhwaahiran
Wabaatwinan, naye ni yule ambaye
hajawa mashuhuri kwa kutafuta
elimu yeye mwenyewe, wala
Maulamaa hawamjui na wala upokezi wake haujulikani ila kwa upande wa mpokezi mmoja tu. Na upokezi wake haukubaliwi kwa mujibu
wa wanawazuoni wa hadith.
Majhuulul Haali: Naye ni

mwenye kujulikana uwepo wake kwa


upokezi wa watu wawili kutoka
kwake na hivyo akaongezeka kuwa
miongoni mwa walio mashuhuri
kwa elimu, na wala yeyote hakumuona kuwa ni mwenye kutegemewa.
Al Mastuuru: Ni huyo huyo Majhuulul Haali, na huitwa Majhuulul
Adaalah Baatwinan Laa Dhwaahiran yaani asiyejulikana uadilifu
wake kwa siri lakini siyo dhahiri. Na
hukumu ya mapokezi yake ni kukataliwa
Mutahhamun Bil Kadhbi: Ni
yule ambaye urongo wake umethibiti
katika kusimulia watu na jambo lake
hilo likatangaa. Na upokezi wake si
wenye kukubaliwa kwa ujumla
wake.
Al Kadhhaabu: Ni yule ambaye
urongo wake juu ya Mtume (Rehma
na amani ziwe juu yake) umethibiti,
iwe kwa nia mbaya kama kuzua kwa
wazandiki na wazushi hadithi kwa
lengo la kubadili na kupotosha(dini)
au kwa nia njema kama ilivyopokelewa kutoka kwa baadhi ya
Masufi na wenye kudai kuweka hadithi katika mambo ya fadhila. Na
upokezi wake ni wenye kukataliwa
kwa ujumla wake.
Al Matruuku: Ni yule ambaye
uadilifu wake umedondoka kwa
kuthibiti urongo wake katika
kusimulia watu. Na upokezi wake ni
wenye kukataliwa na wala udhaifu
wake hauondoki kwa kupatilizwa na
kwa ushahidi.
Al-Mubtadau: Ni mtu wa Bida
katika itikadi au matendo. Na Bida
ni kumuabudia Allah kwa yale ambayo Allah hakuyaamrisha. Au ni
itikadi katika kitendo maalum kama
vile ni jambo la kisharia katika kuli-

fanya au muonekano, na sababu ni


(kutaka) kujikurubisha kwa Allah na
kupelekea kupata ujira na thawabu
pamoja na kwamba Sharia haikuliweka kimuonekano au kulithibitisha
kwa kujikurubisha na kupata thawabu.

Nayo (Bida) ni ya namna


mbili:

1- Yenye kukufururisha: Nayo ni


ile ambayo inalazimisha kufuru, na
upokezi wa mwenye Bida hii ni
wenye kukataliwa kwa ujumla wake.
2-Yenye kumfanya mtu faasiq:
Nayo ni ile inayomsababishia mtu
ufasiki na upokezi wa mwenye Bida
hii hukubalika kwa masharti mawili;
Asiwe mwenye kuitia watu kunako Bida yake.
Na kwamba upokezi wake usiwe
wenye kutia nguvu Bida yake.
19- Al Mukhtalitu: Ni yule ambaye nidhamu ya akili yake imeharibika kwa sababu ya maradhi au
madhara au umri mkubwa na mfano
wa hayo au vitabu vyake vimepotea
akawa hawezi kutimiza aliyokusudia
kuyasimulia kwa namna iliyo sahihi.
Kwa aliyoyasimulia kabla ya
kuchanganyikiwa hukubalika iwapo
ni miongoni mwa wenye kutegemewa na yale ya baada ya kuchanganyikiwa na vile vile yale ambayo haijulikani je ni ya kabla au baada ya
kuchanganyikiwa hayo hayakubaliki.
20- Al Wadhwau: ni yule ambaye
hubuni hadith kumsingizia Mtume
(Rehma na amani ziwe juu yake) kwa
kuzua. Na upokezi wake ni wenye
kukataliwa kwa ujumla wake.
Itaendelea toleo lijalo

15 Rajab 1436, jumatatu May 4 - 10, 2015

hazina yetu

14

www.islamicftz.org

Na Yusuph Amin

Nairobi nchini Kenya na baadae


kurejea nyumbani ambako alipandishwa cheo na kuwa dereva wa
gari moshi, na kisha msimamizi injini ya treni na kustaafu akiwa kama
mkaguzi wa mitambo ya injini ya
gari moshi.
Akiwa shirika la reli, Abas alifanya kazi katika vituo vya Tabora,
Moshi, Dar-es-Salam, Voi pamoja
na Nakuru vya nchini Kenya na
wakati huo huo akifanya jitihada katika kujifundisha elimu ya dini katika maeneo hayo.
Abas aliishi maisha ya kawaida
na pia moja kati ya mambo aliyokuwa akiyazingatia ni majukumu
aliyopewa na Waislamu, jambo ambalo lililompa ari ya kazi na kupelekea baraza kupiga hatua kubwa ya
maendeleo.
Abas alikuwa akiheshimika sana
kwa rafiki zake na alikuwa na
mapenzi makubwa na ndugu wa karibu na nje ya nyumbani kwake. Pia
alikuwa ni mtu wa kupenda kufanya
mazoezi ili kulinda afya ya mwili.

kiona vyaelea ujue vimeundwa ni msemo


maarufu wa Waswahili.
Mtume, maswahaba na
vizazi vya Waislamu waliotangulia
walifanya kazi kubwa ya kuupigania
Uislamu hadi kwa uwezo wa Allah
ukatufikia sisi.
Katika zama hizi pia tunao watu
waliojitolea kwa hali na mali kuuhami Uislamu. Kwa hapa Tanzania,
mmoja kati ya watu watakaokumbukwa katika kuendeleza Uislamu
ni marehemu Abas Kilima aliyekuwa mwasisi na Katibu Mkuu
wa kwanza wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania.
Kama ambavyo ukisoma historia
utagundua kipindi kigumu zaidi
kwa Waislamu ni wakati Mtume alipoanza kuitangaza dini, ndivyo hali
ilivyokuwa wakati Baraza Kuu
linaanzishwa ambapo wachache
waliunga mkono.
Kukosekana uungwaji mkono
wa wengi haukurudisha nyuma jitihada za kutekeleza azma ya Abas na
wenzake. Badala yake walijitolea kufanya kazi za baraza hilo kwa moyo
mkunjufu wakitawakkal kwa Allah.
Nia thabiti, msimamo imara na
msaada wa Allah vilishinda nguvu
ya vikwazo na changamoto na hatimae juhudi za waasisi zilizaa matunda, huku Kilima akibeba jukumu
kubwa.
Ni nafasi yake maalum katika
harakati za uundwaji wa Baraza Kuu
ndio imepelekea baadhi ya wachambuzi wa masuala ya dini ya Kiislamu
kusema muonekano wa sasa wa
Baraza Kuu unafungamana kwa kiasi kikubwa na mchango wa marehemu Abas Kilima.
Katika mahojiano maalum na
ndugu wa Abas , aitwaye Ally Kilima
gazeti la Imaan liliambiwa kuwa
Abas alihamasika na kupata ujasiri
wa kushiriki harakati za kidini
ikiwemo kuunda Baraza Kuu kupitia ushiriki wake katika jumuiya ya
Warsha ya Waandishi wa Kiislamu.
Hiyo ilikuwa ni kipindi kifupi baada
ya kustaafu kazi Shirika la Reli alilolitumikia kwa muda mrefu.
Wazo la kuunda Baraza Kuu pia
lilichangiwa na uzoefu ambao Abas
alioupata wakati akiwa Shirika la
Reli katika miji ya Voi, Nakuru na
Nairobi nchini Kenya. Akiwa huko
alishuhudia mshikamano mkubwa
wa Waislamu ingawa walikuwa
wachache ukilinganisha na Tanzania ambako Waislamu walikuwa
wameparaganyika.
Abas na wenzake walifanya jitihada kubwa hadi Baraza Kuu
likaundwa na kusajiliwa.
Licha ya kukosa rasilimali
muhimu kwa wakati huo na
uchanga wa taasisi yenyewe, Abas
na wenzake walifanikisha mambo
mengi, ikiwemo kuendesha semina
na warsha zinazoihusu dini ya Kiislamu na Waislamu ambazo baadhi
yake zilisimika misingi ya mafanikio
ya sasa. Warsha zilizoandaliwa
ziliendeshwa na wasomi wa Kiislamu kama vile Profesa, Dokta Tigiti
Sengo, Profesa Omar Kasule na Profesa Kigoma Ali Malima.
Katika uongozi wa Abas , semina
nyingi zililenga kutafakari namna
bora ya kuandaa mifumo bora ya
kuendesha taasisi za Kiislamu, semina ambazo zilichochea wengi kujitambua na kutoa dira katika kuunganisha umma wa Waislamu Tanza-

Je wanazuoni wanamzungumziaje?

Abas Kilima (kulia) akiwa na Sheikh Abubakar Mwilima katika moja ya hafla za Kiislamu.

Abas Kilima

Muasisi wa Baraza Kuu la Taasisi za


Kiislamu Alikuwa mfano wa kuigwa
katika kuutumikia Uislamu
nia. Abas akiwa Katibu Mkuu alishirikiana na Mwenyekiti wake,
Salum Khamis katika kulitangaza
baraza mikoa yote ya Tanzania.
Abas atakumbukwa pia kwa
kushughulikia utafiti wa Julai 18,
1991 uliofanywa na wanataaluma
wa Kiislamu kuchunguza dhulma
dhidi ya Waislamu wa Tanzania katika elimu ya juu, utafiti ambao umeleta matokeo chanya kwa umma wa
Waislamu.

Historia yake:

Abas Shaaban Kilima alizaliwa


Septemba 29, 1938 mtaa wa Usagara mjini Tabora akiwa mtoto wa

kwanza kati ya watoto saba wa mzee


Shaaban Kilima na bi Amina
Salmini.
Abas alipata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Tabora mjini baadae akaendelea na elimu ya
kati (middle school) katika shule ya
Mwanhala wilayani Nzega. Baadae
alijiunga na shule ya sekondari ya
Tabora boys na baadae shule ya
ufundi ya Ifunda.
Kuhusiana na elimu ya dini, alipata elimu ya msingi ya Kiislamu
kwa babu yake, Juma Salmin,
mjomba wake, Khamis Idi na mwalimu Khamis bin Daudi. Pia alikuwa
akihudhuria semina mbalimbali ku-

jifunza elimu ya dini kwa nyakati tofauti. Baada ya kuhitimu masomo


yake katika shule ya ufundi Ifunda,
Abas aliajiriwa katika Shirika la Reli
la Afrika Mashariki na wakati huo
huo akihudhuria kozi mbalimbali
hadi kupata stashahada ya Uhandisi
wa Mashine (Mechanical Engineering).
Hapo awali Abas aliajiriwa kama
mchochea kuni, wakati huo treni
zikiwa zinatumia kuni au mkaa katika kuziendesha. Baadae akapandishwa daraja na kufanya kazi
katika kitengo cha kuunga mabehewa.
Abas aliendelea na elimu huko

Kwa upande wake Yassin Kachechele amesema, Abas alikuwa


kiongozi mwenye kutekeleza ahadi
na alileta mabadiliko katika kuwatumikia Waislamu. Yasin anakumbuka kuwa ni Abas aliyeshirikiana na
marehemu Profesa Kigoma Malima
kufanikisha ununuzi wa vyombo vya
matangazo vya Radio Kheir.
Baada ya kufariki Profesa Malima, Abas na wenzake walibeba jukumu la kwenda kitengo cha forodha uwanja wa ndege kwa ajili ya kukomboa vyombo hivyo.
Amir wa Baraza Kuu la Jumuiya
na Taasisi za Kiislamu Tanzania,
Mussa Kundecha anamzungumzia
Abas kuwa ni zaidi ya kiongozi,
kwani alijitolea kutumikia baraza
kwa nafsi na hata mali yake ili
kutafuta radhi za Allah.
Amir Kundecha anasema, umati
wa watu waliojiotokeza katika mazishi yake ambapo walifunga barabara
kadhaa za jiji la Dar es Salaam ni
ushahidi kuwa Abas alikuwa kiongozi bora wa umma wa Waislamu
wa Tanzania na hilo limethibitika.
Ingawa watu wengi hawafahamu, moja ya siri kubwa ya mafanikio
yetu ni Abas Kilima, tukiwa ni sehemu ya Jumuiya zinzounda Baraza
Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, alikuwa mara kwa mara akitupitia ofisini kutupa hamasa na
miongozo ya kazi, anaeleza Muhammed Sheikh, mmoja wa viongozi waandamizi wa Jumuiya ya Vijana wa Kiislamu Mwenge
(MYMCO) akimuelezea Abas . Jumuiya hiyo kipindi hicho ilikuwa na
ofisi zake Msikiti wa Ijumaa
Mwenge, Dar es Salaam.
Abas pamoja na mkewe Rukia
binti Fundi walifariki mwaka 1998
kwa ajali ya gari iliyotokea katika mji
mdogo wa Chalinze mkoani Pwani
wakitokea kijiji cha Mwailange
kwenye mazishi ya binti yake.
Hadi anaitikia wito wa kurejea
kwa Allah Subhanahu Wataala,
Abas aliacha wake wawili, watoto
kumi na wajukuu kadhaa.
Tunamuomba Allah Subhanahu
Wataala amrehemu Abas Kilima,
amsamehe madhambi yake na amuingize katika peponi, Aaamin.
Maelezo ya Makala haya ni kwa
mujibu wa ndugu wa marehemu
Abas , Injinia Ally Kilima.

15 Rajab 1436, jumatatu May 4 - 10, 2015

watoto / matangazo

www.islamicftz.org

Kona ya watoto

KIDATO CHA TANO NA KURUDIA MITIHANI

ZAHRA EBRAHIM

Wajue wanawake watukufu


Wajue wanawake watukufu: Asiya, Maryam, Khadija na Fatima

Asiya, Maryam, Khadija na Fatima ni wanawake wanne walio bora zaidi katika Uislamu.
Ubora wao unatokana na matendo yao makuu
katika kupigania dini ya Mwenyezi Mungu
Subhaanahu wa Taala na kutafuta radhi zake.
Hebu tuone nini kinawafanya wanawake
hawa wawe maalum kiasi cha kubashiriwa kuingia katika pepo ya Allah yenye kila aina ya
starehe, makazi ya kifakhari, bustani tulivu,
mavazi, vyakula, mito ya vinywaji na neema nyingi ambazo dunia haijapata kuzishuhudia.

Asiya alimuamini Allah

Asiya alikuwa ni mke wa Firauni, mtawala


wa Misri katika zama za Nabii Musa (Amani iwe
juu yake). Firauni alikuwa katili, tajiri na mbabe
aliyekufuru kwa kujiita mungu. Ukafiri wa
Firauni haukumzuia Asiya kumuamini Allah
Subhaanahu Wataala. Asiya angeweza kulewa
katika anasa za Firauni, lakini alichagua kutafuta radhi za Allah. Ni yeye huyu Asiya ambaye alimlea Nabii Musa (Amani iwe juu yake).

Maryam alimtumikia Allah

Kama ambavyo mama yake, mke wa Imran,


alivyoahidi kwa Allah (3:35), Maryam alikuwa
akihudumia msikiti siku nzima usiku na mchana huku akivumilia tabia za watu. Kadhalika akiwa bikira, Mungu alimchagua Maryam kuwa
mama wa Nabii Issa (Amani iwe juu yake). Maryam hakukutana na mwanaume bali Allah alisema kuwa, na Nabii Issa akawa (3:45-47).

15

Mtume Muhammad (Rehma na amani ziwe


juu yake) alikuwa wa kwanza kusilimu na alimuunga mkono Mtume kwa hali na mali katika
kazi yake ya Unabii. Mtume hakuongeza mke
mpaka Khadija alipofariki. Khadija anatajwa
kuwa alikuwa mke aliyemuunga mkono
mumewe katika kazi zake, mama aliyependa
watoto wake na mfanyabiashara mahiri.

Fatima, msafi aliyeishi maisha


rahisi

Fatima mara zote alikuwa muangalifu sana


kuhusu hijaab yake. Fatima alikuwa ni Muislamu aliyejilinda na maasi, mtoto mzuri kwa wazazi wake, mke aliyemjali mumewe, mama aliyependa wanawe. Tangu akiwa mdogo, Fatima
alisimama kidete katika harakati za kumhami
baba yake na kazi yake ya Utume. Fatima alisaidia kutibu watu waliojeruhiwa vitani na aliishi maisha rahisi. Katika hadith iliyopokewa na
Bukhari na Muslim Mtume alipenda kusema:
Fatima anatokana na mimi, yule amkasirishaye
amenikasirisha mimi.
Maswali
Sura ipi katika Quran inajulikana kwa jina
la mama wa Nabii Issa (Amani iwe juu yake)?
Mke wa kwanza wa Mtume Muhammad
anaitwaje?
Nani katika wanawake watukufu alikuwa
akitibu watu waliojeruhiwa vitani?
Mke wa Firauni zama za Mtume Mussa
alikuwa ni nani?
Taja mambo matatu ambayo ukiyafanya
yanaweza kukupeleka peponi

Khadija: wa kwanza kusilimu

Khadija ambaye alikuwa mke wa kwanza wa

ILALA ISLAMIC SECONDARY

USAJILI
S.2401

KWA WASICHANA TU

IPO: ILALA-AMANA-MTAA WA ARUSHA: MASJID SHAFII


SHULE YA BWENI NA KUTWA

MASOMO

Math, Phy, Chem, Bios, Geo, Civ, Eng, Kisw, Commerce,


COMBINATION
PCM,PCB,CBG,HGL,HGK,HGE,HKA,HEA
UFAULU 2014
KIWILAYA 3/76, KIMKOA 10/191, KITAIFA 118/2322
Kwa shule za kiislam KIWILAYA (1) KIMKOA (2) KITAIFA (5)
Zipo nafasi za kuhamia kidato cha II, III na IV, V
MAWASILIANO
Simu: 0713 007586, 0715 187515, 0714 393822,
0714 381964

DAR ES SALAAM ISLAMIC SEC.


KWA WAVULANA TU

USAJILI
S.4384

Ipo Ilala-Bungoni: Masjid Taqwa


MASOMO
Math, Phy, Chem, Bios, Geo, Civ, Eng, Kisw, Commerce, B/
COMBINATION
PCM,PCB,CBG,HGL,HGK,HGE,HKA,HEA
UFAULU 2014
Kama Ilala Islamic, imetenganishwa toka Ilala Islamic
Zipo nafasi za kuhamia kidato cha II, III na IV, V
MAWASILIANO
Simu: 0713 007586, 0715 187515, 0714 393822, 0714 381964
Sifa

1. Kwa daraja la I, II, III Apate angalau D tatu za kombi yake


2. Kwa daraja la iv Apate C tatu za kombi yake
3. Aliekosa sifa ya 1 na 2 ataruhusiwa kuanza kidato
cha v huku anarudia mitihani

Ada ni nafuu na inalipwa kwa awamu nne


MLETE MWANAO APATE ELIMU NA MALEZI BORA

Mwanza
Arusha

Kigoma
Tabora

Moro
Dsm

Masafa ya Imaan FM
1
2
3
4
5
6

Daresalaam
Morogoro
Arusha
Mwanza
Kigoma
Tabora

104.5 Mhz
96.3 Mhz
90.8 Mhz
105.6 Mhz
92.5 Mhz
101.6 Mhz

7
8
9
10
11
12

Mbeya
Dodoma
Ruvuma
Mtwara
Zanzibar
Pemba

90.3 Mhz
102 Mhz
94.2 Mhz
90.9 Mhz
104.5 Mhz
104.5 Mhz

Mbeya
Ruvuma
Mtwara

Ukweli
kuhusu
riba

Uk 11
15 Rajab 1436, jumatatu May 4 - 10, 2015
ardhi, lengo likiwa kushughulikia
mahitaji ya kijamii kwa wanawake.
Baada ya kupata ardhi baraza huwataka akina mama hao kuorodhesha mahitaji yao ili kupata urahisi
wa kuyashughulikia.
Mayasa alisema ardhi inaweza
k u t u m i k a k u a n z i s h a m i ra d i
mbalimbali kwa manufaa ya wanawake na Uislamu, ikiwemo zahanati, vituo vya wanawake, shule,
miradi ya kilimo na kumbi za mikutano.
Katika kuhakikisha kazi za baraza zinasonga mbele, Mayasa amesema baraza limeweka mikakati
mbalimbali kwa siku za baadae kwa
kuhakikisha wanawake wa Kiislamu wanainuka kiuchumi, ikiwemo
kuanzisha Benki ya Kiislamu ya
Wanawake.

Lakwamua
maelfu ya wanawake kiuchumi
Lajipanga
kuanzisha benki
ya Kiislamu

Baraza la Wanawake
wa Kiislamu Tanzania

Na Yufuph amin

likana kama Islamic Credit Society


(ICS) ulioanzishwa na Baraza hilo.
Kwa mujibu wa Naibu Katibu
wa Baraza hilo kitaifa, Mayasa
Sadallah, malengo ya baraza ni
kukuza na kuendeleza mradi wa
ICS kuwa benki ya wanawake wa
Kiislamu.
Akichanganua mradi wa kuweka na kukopa, Mayasa amesema
wakinamama hujumuishwa katika
vikundi vya watu 30, ambapo kila
kimoja huwekeza na kukopeshana
kwa kuzingatia madaraja mbalimbali yanayotokana na kiasi walichoweka katika mfumo ambao
hauna riba, ambapo wanachama
wanaweza kukopa hadi Tsh. Milioni
2. Mayasa aliliambia gazeti la Imaan kuwa ICS yenye wanachama
zaidi 25,000 inaendeshwa kwa
umakini mkubwa, ambapo ili kuhakikisha mambo yanakwenda,
baraza hufanya vikao vya ICS kila
katikati na mwisho wa mwezi ili kujua idadi ya waliowekeza na kukopa.
Hata hivyo, uchumi sio eneo pekee ambalo baraza limefanikiwa.
Mafanikio mengine muhimu ya
baraza ni katika harakati za
daawah. Wakinamama wamefaidika sana na darasa za kinamama za
mitaa na majumbani zinazoendeshwa siku za ijumaa na jumapili, mihadhara ya kila wiki, makongamano ya kila mwezi na pia
warsha mbalimbali kwa wanawake
wa Kiislamu walioko mtaani na
wale wa serikalini.
Kama ilivyo katika miradi ya
fedha, mradi huu wa kuendelezana
kiroho pia unaratibiwa kwa uangalifu, ambapo kila baada ya miezi
mitatu viongozi wa mkoa, wilaya na

ama mfuatiliaji wa historia utakuwa unajua jinsi


mwanamke alivyokuwa
akidhalilishwa na kukandamizwa hususan enzi za ujahiliya
(Kabla ya ujio wa Mtume Muhammad, Rehma na amani ziwe juu
yake).
Kuja kwa Mtume Muhammad
(Rehma na amani ziwe juu yake)
kulileta mapinduzi makubwa katika Uislamu na dunia kwa ujumla,
ikiwa ni pamoja na kupandisha hadhi na thamani ya mwanamke. Katika aya mbalimbali za Quran
tukufu, Allah anaelezea alivyomtukuza mwanamke.
Harakati za kuhakikisha hadhi
na heshima ya wanawake inabaki
juu ilipelekea wanawake wa Kiislamu wa Tanzania kuunda Baraza
Kuu la Wanawake wa Kiislamu
mwaka 2000, likiwa chini ya Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu.
Baadae mwaka 2008, baraza
hilo lilijisajili Wizara ya Mambo ya
Ndani na kuwa taasisi inayojitegemea.
Baraza hili limewaunganisha
wanawake katika mapambano ya
kujikomboa kiuchumi, kuwaendeleza katika taaluma ya dini ya Kiislamu, kuwastawisha kijamii na
pia limekuwa chombo cha kupaza
sauti za wanawake wa Kiislamu wanapokabiliwa na tishio lolote.
Athari chanya ya shughuli za
baraza hili iko wazi, hususan kiuchumi. Wanawake wengi wamejikwamua kimaisha kutokana na mradi wa kuwekeza na kukopesha kwa
wanawake wa Kiislamu unaoju-

kata hukutana kutathmini ripoti ya


kazi iliyofanywa, mahudhurio na
taarifa ya matatizo yaliyojitokeza.
Kwa kuwa baraza halina wafadhili viongozi hujichangisha kupata
pesa za kusaidia kazi ya ulinganiaji
kupitia ziara mbalimbali mijini na
vijijini, ambapo imepelekea akina
mama wengi kufahamu dini yao.
Wanawake wengi sasa wanajua
jinsi mwanamke wa Kiislamu anavyotakiwa kutekeleza majukumu
yake kijamii kwa kufuata taratibu
za kisheria, pia wamefahamu sitara
ya mwanamke ilivyo na kuondoa
misimamo hasi juu ya hijab, Mayasa alisema.
Kwa mujibu wa Mayasa, wanawake wengi wamejenga imani
kwa baraza, ambapo baadhi yao
huwatembelea ofisini na kutaka
ushauri au msaada wa kutatuliwa
matatizo yao. Kadhalika, baadhi ya
wadau huleta misaada kama vile
nguo na vyakula ambavyo baraza
hupeleka kwa wahitaji.
Kuhusiana na vyanzo vya mapato ya kuendeshea baraza, Mayasa
amesema chanzo kikubwa ni
michango ya wakinamama
wenyewe, ingawa baraza pia lina
maduka machache yaliyopo nje ya
misikiti wanayoimiliki ambayo
wameyapangisha. Amesema mapato hayo husaidia kuendesha shughuli za baraza.
Kadhalika, kila mkoa unapaswa
kuchangia makao makuu kiasi kidogo cha fedha kila mwezi. Mikoa
nayo huwa na utaratibu wao wa
kuchangisha wanachama ili
kuendesha shughuli zao.
Uanachama wa Baraza la Wanawake unaombwa kwa kujaza
fomu za kuomba uanachama kuto-

ka katika wilaya husika. Sifa


muhimu kubwa ya kuwa mwanachama ni kuwa Muislamu, baleghe.
Muundo wa Uongozi:
Bodi ya wadhamini yenye watu
tisa ndio chombo cha juu kabisa katika muundo wa uongozi wa Baraza
la wanawake. Chini ya bodi ya wadhamini kuna viongozi wa kitaifa
ambao ni Mwenyekiti au Amira;
Fatuma Juma, Naibu Mwenyekiti;
Khadija Ahmad, Katibu Mkuu,
Hawra Shamte, Naibu Katibu, Mayasa Sadallah na Mweka Hazina,
Mwajuma Kimia.
Kadhalika, kuna wajumbe saba
wa kamati ya utendaji. Kwa upande
wa kamati, kuna kamati ya taaluma
ambayo ndani yake kuna idara ya
daawah na pia kuna kamati ya ya
mipango, uchumi na fedha.
Katika uongozi wa mkoa, kuna
viongozi wakuu watano na wajumbe saba wa kamati tendaji,
kama ilivyo katika ngazi ya taifa.
Utaratibu wa uendeshaji baraza
kwa mikoa na wilaya ni kama ule
wa kitaifa. Hata hivyo ngazi za
misikiti na madrasa huwakilishwa
na wanawake watatu kwa kila
msikiti.
Kwa upande wa matawi, Mayasa
amesema baraza limefungua matawi mikoa yote ya Tanzania bara na
lina wawakilishi kwa upande wa
Zanzibar. Baraza hufanya mkutano
mkuu kwa mwaka mara moja ambapo huhudhuriwa na viongozi wa
ngazi zote za wilaya, mikoa na taifa.
Malengo ya baadae:
Katika kuinua wigo wa huduma
zake, baraza lina mpango mkakati
kuhakikisha kila mkoa unamiliki

Changamoto:
Akizungumzia changamoto zinazolikabili baraza, Mayasa amesema, kutokana na wingi wa taasisi
wapo wanaodhani kuanzishwa
baraza kuu la wanawake kumevunja shughuli zao. Lakini alitaka taasisi nyingine zisiwe na wasiwasi
kwani baraza halimzuii mtu kutoka
taasisi moja kujiunga na nyingine
kwa wakati mmoja.
Aidha amezitaja changamoto
nyingine kuwa ni baadhi ya mitazamo ya watu wa dini kuhusu mwanamke imekuwa kikwazo katika kufikia malengo. Wajumbe hukosa
ruhusa kwa waume zao kwa kuona
ni watu wa kukaa nyumbani na hawaruhusiwi kufanya shughuli za
dini.
Changamoto nyingine ni nguvu
ndogo ya uchumi, hivyo baraza
linakaribisha sadaka na zaka kutoka kwa waumini mbalimbali.
Pia amewataka wanawake kuondosha dhana kuwa hakuna
umuhimu wa kutafuta elimu, na
kuongeza kuwa, matokeo ya
kukiukwa kanuni za kitabibu kwa
magonjwa ya wanawake kutibiwa
na madaktari wanaume yametokana na dhana hii potofu.
Mayasa amesema, wao kama
baraza wamekuwa wakifanya semina katika vyuo vya kitabibu vya
IMTU na Kairuki ili kuwashawishi
wanafunzi wa kike wasome kwa
juhudi na watumie elimu yao kuisaidia jamii.
Licha ya kuwepo changamoto
hizo, baraza limepata mafanikio
katika uungwaji mkono kwa kiasi
kikubwa, si tu kwa wanawake, bali
hata kwa taasisi za wanaume.
Akifafanua hilo Mayasa amesema, wanapata ushirikiano kutoka
kwa Chama cha Wanataaluma wa
Kiislamu (TAMPRO) katika masuala ya kitaaluma. Pia taasisi ya The
Islamic Foundation, hususan kupitia vyombo vyake vya habari, ambapo vimekuwa vikisaidia kutoa
matangazo ya makongamano
pasipo gharama yeyote.
Katika suala la ujenzi wa misikiti, taasisi ya Islamic Relief Organization ya nchini Kuwait imekuwa
ikisaidia ujenzi wa misikiti pindi
wanapohitajia.
Mayasa amewataka wanawake
wa Kiislamu watambue kuwa Baraza Kuu la Wanawake ni chombo
chao na si cha mtu fulani, hivyo
wakiunge mkono kikamilifu, kwa
mali na nafsi zao katika kuipigania
dini ya Allah.

hutolewa na kuchapishwa na The Islamic Foundation, P.O.Box 6011 Morogoro, Tanzania E-mail: imaanmedia3@gmail.com

You might also like