You are on page 1of 15

Hotuba ya Rais wa Uganda Idi Amin Dada mwaka 1972 - Uk 4

huwatoa watu gizani


Msomi, mwanaharakati aliyebobea

Sheikh Said Musa: kwenye utungaji vitabu - Uk 5


ISSN 5618 - N0. 002 BEi: Sh800/- KSH80/- Ush1,200/-

1 Rajab 1436, Jumatatu, april 20 - 26, 2015

www.islamicftz.org

Ugaidi Tanzania
Waandishi wageuka mahakimu

Mufti Kayongo
alikuwa kisima
cha maarifa

Waislamu wawa washukiwa

Ugaidi oklahoma

Na Abdalhakim
Nsobya.

lhamisi, wiki iliyopita


ilikuwa ni siku ya majonzi makubwa kwa
wananchi wengi wa
Uganda, hususan Waislamu,
baada ya Mufti, Sheikh Zubayiri
Sowedi Kayongo (83) kuitikia
wito wa kurejea kwa Muumba
wake, Allah (Subhanahu
wataalah).
Mufti Kayongo alifariki akiwa jijini Dar es Salaam, katika
Hospitali ya Agha Khan kutokana na shinikizo la damu na
kuswaliwa katika Msikiti wa
Shadhily, Kariakoo, kabla ya
kusafirishwa nchini Uganda
kwa maziko.
Mufti Kayongo alikuwa nchini katika ziara ya kidaawah.
Katika kuonesha kuguswa na
kifo chake, Waziri wa habari wa
Uganda, Meja Jenerali Gim
Muhwezi alimuelezea UK 2

Ugaidi hispania

wahanga - ugaidi wa israel

Head office, Lumumba Street


Opp: Viwanja vya Mnazi Mmoja, P. O Box 779 Dar es Salaam,
Tanzania, Tell: 255 22 2182482/ 255 222184419
Fax: 255 22 2181424, E-mail: info@Binslum.com

Habari
Uk 3

1 Rajab 1436, jumatatu Aprili 20 - 27 , 2015

habari

www.islamicftz.org

Mufti Kayongo alikuwa kisima cha maarifa


inatoka uk 1

Mufti Kayongo
kama Nguzo ya maarifa ya Uislamu na mtu muhimu katika masuala
ya ushauri. Sheikh Zubayiri Kayongo ni nani?
Sheikh Kayonga alizaliwa mwaka 1932 katika wilaya ya Kiboga
kusini mwa Uganda, huku elimu
yake ya dini ya Uislamu akiipata
Lamu nchini Kenya na visiwani
Zanzibar.
Kupitia elimu yake hiyo ya dini,
Mufti Kayonga aliweza kufungua
madrasa nyumbani kwake ambayo
ilitumika kufundishia viongozi wengi wa dini wa sasa nchini Uganda na
kwengineko.
Wakati Marehem Idd Amini akizindua rasmi Baraza kuu la Waislamu nchini Uganda mwaka 1972,
kama chombo cha kuwaunganisha

Waislamu, Mufti Kayonga alikuwa


ni miongoni mwa Masheikh walioteuliwa katika Baraza hilo.
Mwaka 1993 alichaguliwa kuwa
Naibu Mufti wa Uganda mpaka
mwaka 2000 alipostaafu ili kupisha
uteuzi wa viongozi wengine wa dini.
Lakini mwaka 2009, Mufti
Kayongo alichaguliwa kuwa Mufti
wa Uganda na baadhi ya wafuasi
wake waliopinga uteuzi wa Mufti wa
sasa, Sheikh Shabani Mubaje ambae
ndie anatambuliwa rasmi na Serikali kama Mufti.
Na ili kuondoa mgogoro na kuwaridhisha wafuasi wa Sheikh
Kayonga na kuleta amani ya jumla
ya nchini humo, Serikali ya Yoweri
Museveni iliamua kumtambua
Sheikh Kayongo kama Mufti na
kumpa gari na walinzi, hivyo Ugan-

da ikawa na Mamufti wawili kwa


wakati mmoja. Sheikh Kayonga alianza safari yake ya kuutumikia Uislamu miaka ya 1950 nyumbani
kwake Kitezi karibu na jiji la Kampala ambapo alifungua Madrasa iliyozalisha Masheikh wengi waliopo
Uganda kwa sasa.
Sheikh Kayongo katika maisha
yake yote alikuwa akihubiri dini
huku madrasa yake hiyo ikidumu
hadi alipofariki. Sheikh Kayongo
alikuwa ni mtu wa vitendo, hakutumia cheo chake ili kujinufaisha, bali
kwa ajili ya kuuhuisha na kuusimamisha Uislamu.
Kwa upande wangu, nilibahatika
kukutana na Sheikh Kayongo mwaka 2013 katika Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Dar es Salaam tukisubiri kuelekea Entebe, Uganda.

Afyais natural
source of sweet drinking water from underground stream which
is blended with essential minerals to
support and aid perfect metabolism.

WATERCOM LIMITED
P.o.box 20409, Plot N.4005, Kisarawe11 area Temeke,Daresalaam, Tanzania
www.watercomtz.com
E-mail:info@watercomtz.com

Nilimsogelea ili kumsalimia. Nilishangaa Mufti Kayongo alipoinuka


kwenye kiti chake na kunipa mkono,
jambo ambalo si la kawaida kwa viongozi kumpa heshima ya kiasi hicho mtu wa kawaida kama mimi.
Katika masaa yote mawili tukiwa
hewani kuelekea Entebe, Mufti
Kayongo alitumia muda wake wote
kuniusia mafundisho ya dini na jinsi
ya kuishi duniani.
Katika kumsimulia Mufti
Kayongo, mmoja wa watu waliokuwa karibu na Sheikh Kayongo,
Sheikh Abdulnoor amemtaja marehemu Kayongo kama mtu mtulivu,
ambae alionesha uadilifu katika dini
yake:
Tutamkumbuka kwa kuwa kisima cha maarifa, na miongoni mwa
waanzilishi wa Baraza Kuu la Wais-

lamu nchini Uganda, kiukweli kifo


chake ni pigo kwetu.
Nae Mufti wa sasa, Sheikh Mubajje katika salamu zake za rambirambi amemsifu Sheikh Kayongo
kuwa alikuwa mchapakazi katika
kuitumikia dini ya Uislamu.
Sheikh Kayongo alikuwa Muislamu wa kweli ambaye alifundisha
viongozi wengi wa dini tangu mwaka 1950 alipoanza kufundisha,
anasema Mufti Mubajje.
Kiukweli Mufti Kayongo
ameacha pengo kubwa katika dini
ya Uislamu na kwa wananchi wa
Uganda na ulimwengu kwa ujumla.
Atakumbukwa kwa jitihada zake
kubwa za kueneza dini kwa miongo
sita.
Allah aiweke roho yake mahala
pema peponi. Amiin.

Vyuo vyajadili mtaala


wa Kiislamu vyuo vikuu
Na Abdulla Ali, Maelezo
Zanzibar

aziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi


na Utumishi wa Umma Zanzibar, Haroun Suleiman amewataka wasomi wa Kiislamu kuunga mkono uanzishwaji wa mtaala wa taaluma
ya maarifa (epistemolojia) ya Kiislamu ili kuwawezesha vijana kwenda sambamba na mabadiliko yanayotokea kila siku duniani.
Haroun aliyasema hayo wakati akifungua
warsha ya siku tatu kujadili utungaji wa mtaala
wa epistemolojia ya Kiislamu wa masomo
ya vyuo vikuu uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Abdurahman AlSumait kilichopo Chukwani, Zanzibar.
Haroun alisema, dini ya Kiislamu ni neema
kutoka kwa Allah ambayo hutofautisha kati ya
binadamu na viumbe vingine, hivyo ni wajibu
wa kila Muislamu kuthibitisha hilo kwa
kuelewa nyanja zote za Uislamu zilizofungamana na Quran na Sunnah ambavyo ndio
misingi mikuu ya epistemolojia ya Kiislamu.
Waziri Haroun amesisitiza kuwa katika kufikia lengo hilo, ipo haja kwa Waislamu kujifunza na kuelewa mafunzo ya Quran na Sunnah za Mtume (Rehma na amani ziwe juu
yake), kwani kuna tofauti kubwa kati ya epistemolojia ya Kiislamu na epistemolojia nyingine
ambazo huchanganya mawazo ya watu.
Ametanabahisha kuwa kwa sasa vyuo vingi
ulimwenguni hata katika nchi za Kiislamu
vimetawaliwa na mtaala usio wa Kiislamu
jambo ambalo hupelekea kuzalisha wataalamu
ambao wanakuwa kidunia zaidi na wasio na
hofu ya Allah, huku wakifanya mambo kwa
kuangalia utashi na maslahi binafsi.
Naye, Makamo Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Abdurahman Al-Sumait, Prof.
Hamed Rashid Hikmany amesema warsha
hiyo ina lengo la kujadili hatua za mchakato wa
kuoanisha na kutunga mtaala unaozingatia
maeneo makuu ya kujifunza yakiwemo ufahamu, stadi za mazoezi, namna ya kutatua matatizo na stadi za sayansi, mawasiliano, uongozi,
stadi za pamoja, menejimenti ya taarifa stadi
na majukumu ya kijamii pamoja na taaluma

Waziri Haroun
amesisitiza
kuwa katika
kufikia lengo
hilo, ipo haja
kwa Waislamu
kujifunza
na kuelewa
mafunzo ya
Quran na
Sunnah za
Mtume (Rehma
na amani ziwe
juu yake)
na kanuni na stratejia za uhakiki.
Zaidi ya wataalamu 40 wakiwemo wa vyuo
vikuu, maprofesa na watafiti kutokea vyuo
vikuu tisa vya nchi za Afrika Mashariki na Chuo
Kikuu kimoja cha Malaysia walikutana kwa
ajili ya warsha hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya
Kimataifa ya Fikra za Kiislamu inayoitwa (International Institute of Islamic Thought - IIIT)
yenye makao makuu yake nchini Malaysia kwa
kushirikiana na Chuo chake.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi na


Utumishi wa Umma Zanzibar, Haroun
Suleiman.

1 Rajab 1436, jumatatu Aprili 20 - 27 , 2015

habari habari

www.islamicftz.org

Waislam
wakiwa katika
Mahakama ya
Kisutu, jijini Dar
es Salaam, hivi
karibuni katika
moja ya kesi
zinazowakabili..
(na mpiga picha
wetu)

Na Waandishi Wetu

yombo vya habari vya Tanzania na mitandao ya kijamii vimegeuka mahakimu baada ya kuwatangaza
washukiwa wa uhalifu kumi waliokamatwa Morogoro katika msikiti
wa Sunni uliopo Kidatu wilaya ya Kilombero kuwa ni magaidi wa AlShabaab kutoka Somalia.
Katika tukio hilo, watu kumi walikuwa wanashikiliwa na polisi kwa
madai ya kukutwa na milipuko 30,
sare za kijeshi, risasi, bendera nyeusi
yenye maandishi ya Mungu Mmoja,
majambia, bisibisi na vinginevyo.
Kadhalika, kufuatia tukio la kukamatwa kwa watuhumiwa hao, tayari
baadhi ya Waislamu wamejikuta wakishikiliwa na polisi kwa muda na
kuachiwa kwa kuhisiwa kuwa wahalifu.
Uchunguzi wa gazeti hili umeonesha kuwa, kinyume na maadili ya uandishi wa habari, baadhi ya vyombo viliarifu kuwa watu kumi waliokamatwa
Morogoro ni magaidi.
Maadili ya uandishi wa habari yanasema mtu hawezi kutangazwa
mhalifu mpaka mahakama imkute na
hatia. Lakini katika mkasa wa Kilombero mkoani Morogoro vyombo vya
habari havikusubiri hata uchunguzi
wa polisi kabla ya kupitisha hukumu
yao.
Vituo kadhaa vya redio viliibuka na
breaking news vikidai kuwa gaidi
mmoja ameuawa na wengine kumi
kukamatwa na polisi wakiwa msikitini, habari ambayo ilidakwa juu kwa
juu na mitandao ya kijamii iliyochapisha kila aina ya uzushi.
Baada ya tukio hilo, matukio mawili ya Waislamu kushukiwa kuwa ni
magaidi yameripotiwa mkoani Morogoro.
Katika tukio la kwanza, Waislamu
raia wa kigeni wanaofanya kazi ya kutangaza dini (Tabligh) walikamatwa
katika msikiti wa Masjid Nnur uliopo
Kihonda, Mazimbu road, Morogoro

Ugaidi Tanzania
mjini asubuhi ya siku ya Alhamisi ya
April 16 na kufikishwa kituo cha polisi
cha Morogoro. Baada ya mahojiano
mafupi, wenyeji wao waliwasilisha hati
zao za kusafiria na vibali vingine na
polisi waliawaachia huru.
Katika tukio la pili, wafanyakazi wa
vyombo vya habari vya Imaan, ambao
walikuwa wakisafiri kutoka Kilombero walikokuwa katika kazi maalum ya
kukusanya habari kuelekea Morogoro
walikamatwa eneo la Mikumi na
kuhojiwa na polisi.
Kwa mujibu wa Sheikh Ally Ajrani,
Katibu Mkuu wa taasisi ya The Islamic Foundation aliyekuwa katika msafara huo; chanzo cha kukamatwa ni
pale waliposimama katika daraja moja
huko Kilombero kwa ajili ya kupiga
picha eneo ambalo walikuta ajali ya
pikipiki na baiskeli. Askari wa kikosi
cha usalama barabarani aliyekuwapo
eneo hilo alipiga picha gari yao na kuchukua namba za usajili na kisha kuwasiliana na wakubwa zake.
Wafanyakazi hao wa vyombo vya
habari vya Imaan walikuwa na
muonekano wa Kiislamu, kama ilivyokuwa kwa Waislamu wale raia wa kigeni waliokamatwa kule Kihonda.
Matukio haya mawili yanatia wasiwasi kuwa huenda mavazi au
muonekano wa Kiislamu, ikiwemo
kufuga ndevu, kuvaa kanzu, hijabu
vinaweza kumuweka mtu matatani
kwa kushukiwa kuhusika na vitendo
vya uhalifu, jambo ambalo linawaweka Waislamu kitanzini.
Hata hivyo haya yanayotokea Tanzania ni sehemu ya mkakati mpana wa
kimataifa wa kuupaka matope Uislamu kama ambavyo Ken Livingstone,
Meya wa jiji la London mwaka 2007
alikiri, akinukuliwa katika gazeti la

The Guardian la huko huko Uingereza.


Katika habari iliyochapwa chini ya
kichwa cha habari: Study shows demonization of Muslims (uchunguzi
unadhihirisha ushetanishaji Waislamu) Meya Livingstone alisema: Mtazamo wa jumla unaoneshwa na vyombo vya habari ni kwamba Uislamu ni
kitisho kwa nchi za magharibi. Kuna
kiwango kikubwa cha Ushetanishaji
Uislamu katika vyombo vya habari
ambacho hakuna mtu mwenye akili
huru ataona ni sawa. Ni asilimia nne tu
(4%) kati ya habari 352 zilizofanyiwa
uchunguzi ziliandika vizuri kuhusu
Uislamu.
Meya Livingstone aliongeza:
Madai ni kwamba, kwa ujumla hakuna taswira chanya au ya haki kuhusu

Uislamu inayooneshwa. Nafikiri kuna


ushetanishaji (demonization) wa Uislamu unaoendelea ambao unadhuru
mahusiano ya jamii na kuibua hisia za
tahadhari miongoni mwa Waislamu.
Ukweli ni kwamba Demonization
ya Uislamu na Waislamu haiishii tu
Uingereza, bali ipo Ulaya nzima,
Marekani na kwingineko duniani.
Kwa hapa Tanzania, matukio ya Kilombero, Amboni Tanga na kwingineko yanathibitisha kuwa mwendo ni
huo huo.
Vingi katika vyombo vya habari
nchini kuanzia tangu kuanza kwa hiyo
inayojulikana kama vita dhidi ya ugaidi na kutungwa Sheria ya Ugaidi na
Bunge la Tanzania mwaka 2002,
vimekuwa vikiandika habari za kuwahusisha Waislamu na Uislamu na vitendo vya kigaidi. Hata matukio ya
ujambazi ya kawaida, yamekuwa yakihusishwa na ugaidi na Waislamu kutajwa.
Huko nyuma vyombo vya habari
vilirindima na habari juu ya kituo cha
kiislamu kisiwani Ukerewe kiitwacho
Aljazira vikaita kuwa ni kambi ya ma-

Kwa namna vyombo vya


habari vya nchi yetu
vinavyozidi kuripoti juu
ya hofu hizi za kufikirika,
lakini si za uhalisia,
basi, vyombo vyetu vya
habari kimsingi vinashiriki
kikamilifu kuitangaza Al
Shabaab na hata kuisaidia
kupata wafuasi miongoni
mwa baadhi ya vijana wa
Kitanzania wasiojitambua
na walio kwenye umasikini
mkubwa unaochangiwa pia
na kukosa ajira

3
funzo ya ugaidi, habari ambazo hazikuwa na kweli wowote na zikaisha
hivi hivi.
Baadaye ikavuma habari ya magaidi huko mapango ya Amboni Tanga
lakini ikagundulika kuwa wale ni majambazi tu ingawa awali vyombo vya
habari viliripoti kuwa ni magaidi wa
Al-Shabab.
Video ya uongo ikasambazwe
kwenye mitandao ya kijamii ili kukoleza kitisho cha Al-Shabab Tanzania.
Katika vita hiyo dhidi ya ugaidi, misikiti haikusalimika huku, baadhi ikivunjwa na masheikh kubambikiziwa kesi
za ugaidi na kunyimwa dhamana.
Kwa ujumla, taswira inayojengwa
katika jamii yetu ni kwamba ukimuona Muislamu kwa asilimia fulani
anaweza kuwa ugaidi. Ni katika muktadha huu, jamaa wa Tabligh kutoka
India walijikuta wakisombwa kutoka
msikitini Kihonda hadi kituo cha polisi
Morogoro wakishukiwa kwa ugaidi.
Mfano mzuri ni tukio la Aprili 14
kukamatwa watu 10 msikitini huko
Kidatu wilayani Kilombero ambalo
vyombo vya habari haraka vililihusisha
na ugaidi wakati mtu mmoja alipokamatwa kanisani akiwa na bastola
siku ya pasaka huko Bagamoyo
hakuhusishwa na ugaidi wala dini
yake haikutajwa.
Hata jinsi tukio hili la Kilombero
lilivyoripotiwa na vyombo vya habari
ni ushahidi wa kuthibitisha aliyoyasema Meya Livingstone kwamba kuna
njama (conspiracy) ya kuitisha jamii
wauone Uislamu na Waislamu kama
mashetani (demonization of Islam).
Swali la msingi la kujiuliza, ni kwa
nini vyombo vya habari vinaandika
habari hasi za Uislamu na Waislamu
na kuwahusisha na ugaidi? Na ni nini
athari ya propaganda hizi dhidi ya Uislamu?
Swali hili linajibiwa na Makia Freeman, Mhariri wa The Freedom Articles. Kwa maoni yake, Freeman anazigawa njama (conspiracy) za vyombo
vya habari dhidi ya Uislamu na Waislamu sehemu mbili, vyombo vya
habari vya ndani ya nchi husika na vyombo vya habari vya kimataifa.
Kuhusu vyombo vya habari vya
ndani ya nchi, Freeman anasema:
Sababu kubwa ya kuushetanisha Uislamu ndani ya nchi ni hii ni kuiwezesha Serikali inayotawala kuchukua
haki na uhuru (wa Waislamu) kwa kisingizio cha uongo, kitu ambacho wasingeweza kukifanya (pasina kisingizo
hicho).
Ni kweli kabisa. Waislamu wangapi
wasio na hatia wamenyangnywa haki
na uhuru wao kwa kisingizio cha ugaidi? Kwa maana nyingine tuhuma za
ugaidi ni mbinu mpya ya watawala
madhalimu duniani kuwadhibiti
Waislamu.
Mhariri Freeman anasema: Ni kanuni ya msingi ya watawala waovu
kwamba kadiri wananchi wanavyozidi
kujawa na khofu kwa tuhuma za ugaidi, ndivyo inavyokuwa rahisi kuwadhibiti na kuwafanya watumwa ndani
ya nchi yao.
Kuhusu lengo la njama hizi za ugaidi dhidi ya Uislamu na Waislamu kimataifa, Freeman anasema: Lengo la
kushetanisha Uislamu kimataifa katika uwanja wa siasa, ni jingine kabisa.
Katika uwanja huu, lengo ni kuchochea migogoro na vita.
Kama vita vya Ghuba vilivyomuondoa Saddam sababu ni ugaidi wa
Saddam na kumiliki silaha za maangamizi - uwongo, vita vya Afghanistan,
Libya, Syria, Yemen na kwingineko
kulikofanyika mashambulizi UK 12

1 Rajab 1436, jumatatu Aprili 20 - 27 , 2015

www.islamicftz.org

kutoka misikitini
Waislamu wapewa
fimbo ya propaganda
Yusuph Amin na Selemani Magali
Kufuatia kukithiri kwa propaganda za
ugaidi zenya lengo la kuupaka matope
Uislamu na Waislamu ili kuweza kuwahujumu Waislamu, wito umetolewa kuwataka
Waislamu kuzidisha umakini katika
shughuli zao, huku wakiimarisha umoja
na ushirikiano miongoni mwao.
Wito huo umetolewa, Ijumaa iliyopita, katika misikiti ya Mtambani na
Kichangani iliyopo Kinondoni na Magomeni, jijini Dar es Salaam.
Wakitoa wito huo, katika khutba
za swala ya Ijumaa, Imam wa
msikiti wa Mtambani, Sheikh
Suleiman Abdallah na Imam wa
Kichangani, Sheikh Omary Alhady,
walisema kuwa, zama zilizopo zinahitaji
sana kutumia akili vizuri, kwani mbinu
zinazotumika kuuhujumu Uislamu na
Waislamu zimeratibiwa kwa umakini wa
hali ya juu. Allah Subhaanahu Wataala
anasema: Hakika katika kuumbwa
mbingu na ardhi na kukhitalifiana usiku
na mchana ziko ishara kwa wenye
akili (3:190), alinukuu aya hiyo, Sheikh
Alhady akiwasisitiza Waislamu kutumia
akili zao ipasavyo kubaini na kukabiliana na
propaganda ya ugaidi. Kwa upande wake, huku
akirejea matukio kadhaa yanayodaiwa kuwa
ya kigaidi yanavyotumiwa kuuchafua Uislamu
na Waislamu, Sheikh Suleiman, ambaye pia
ni Naibu Amir wa Shura ya Maimam Tanzania,
alisema: Tusikubali kugawanywa, pamoja na
umakini, lazima tuwe na umoja wa nyuki kukabiliana na hali hii.

Mwanazuoni wa Yemen akemea


wanaotukana maswahaba
Na Khalidy Omary
Waislamu wametakiwa kuwa makini na kulikemea
genge la watu wanaowapinga na kuwatukana maswahaba wa Mtume Muhammad (Rehma na amani ziwe juu
yake).
Rai hiyo ilitolewa na Rais wa Wanawazuoni wa nchi
ya Yemen, Sheikh Ahmad bin Hassan Al Muallim wakati
akitoa khutba ya ijumaa, wiki iliyopita, katika msikiti
wa Vetenari, Temeke jijini Dar es salaam. Khutba hiyo
ilifasiriwa na Sheikh Nurdin Kishki.
Sheikh alisema, hivi sasa kuna mtandao mkubwa wa
watu, unaohusisha vyombo vya habari, wanaowapinga
na kuwatukana waziwazi maswahaba wa Mtume, hivyo
Waislamu wanatakiwa kukemea hali hiyo.
Chukueni tahadhari kwa kila yule ambaye anawatukana maswahaba wa Mtume (Rehma na amani ziwe
juu yake) muwachukie na wala msiwapende kwani
kuwapenda ni dalili ya unafiki na kuwachukia ni dalili ya
imani, alisema Sheikh Al Muallim.

Mahakama ya kadhi kwa


Waislamu suala la kiibada
Sheikh Mustapha Na Jasmine Shamwepu,
Dodoma
Sheikhwa mkoa wa Dodoma, Mustapha Rajab amewataka viongozi wa dini ya Kikrito nchini kuacha kutumia nafasi zao kuishawishi Serikali kupinga uwepo wa
mahakama ya kadhi kwa kuwa suala hilo ni la kiibada.
Sheikh Rajab aliyasema hayo hivi karibuni wakati akizungumza na Waislamu mkoani hapa kwenye msikiti wa
Gadaff. Alisema, suala la mahakama ya kadhi ni muhimu
sana kwa Waislamu nchini, kwani litawasaidia katika
masuala yao ya kiibada kama vile mambo ya mirathi,
talaka na mengineyo.
Wakati huohuo, Sheikh Rajab ametoa wito kwa Waislamu ikifika wakati wa uchaguzi mkuu wa rais, wabunge
na madiwani kuwa makini kwa kuhakikisha hawawachagui viongozi ambao baadae wanashindwa kusimamia
maslahi yao, ikiwemo mahakama ya kadhi.

tujikumbushe

Hotuba ya Rais wa Uganda


Jenerali Idi Amin Dada wakati akizindua Baraza Kuu la
Waislamu la Uganda (UMSC) katika kituo cha mikutano
ya kimataifa nchini humo, June 1, 1972, saa kumi jioni:
Mheshimiwa Kadhi
Mkuu wa Uganda
Waheshimiwa viongozi wa dini
Waheshimiwa ndugu
wanachama wa Baraza Kuu la Wislamu
nchini Uganda
Mabibi na mabwana,
Awali ya yote napenda kutumia fursa hii kuwakaribisha kwa
dhati wageni wetu adhimu
kutoka Misri, Makka, Libya, Pakistani na Sudan ambao uwepo
wao hapa umepamba vema
tukio hili. Uwepo wao hapa kuungana na ndugu zao katika
kushuhudia uzinduzi wa Baraza
Kuu la Waislamu la Uganda na
kusimikwa kwa mara ya kwanza
kwa Kadhi Mkuu wa Uganda ni
ishara ya ushirikiano mpya
wenye matumaini makubwa
kati ya nchi yetu na nchi na mashirika mnayoyawakilisha. Ni
matumaini yangu ushirikiano
huu mpya utaendelea kukua na
kuimarika.
Leo nina furaha ya kipekee
ambayo siwezi hata kuielezea
kwa maneno labda kwa hisia tu.
Kwani leo tunashuhudia kuwashwa kwa taa ya mara ya pili
ya Uislamu hapa nchini, taa ambayo kwa mara ya kwanza iliwashwa takribani miaka 100 iliyopita huku kipindi cha katikati
jitahida mbali mbali zimekuwa
zikizuia taa hiyo isiwake nchini
humu.
Wakati Uislamu ilikuwa
ndio dini ya kwanza miongoni
mwa dini za kisasa kuingia katika ardhi hii, ukuaji wake umekuwa ni kwa kasi ndogo ukilinganisha na dini nyingi. Sababu
za kurudi nyuma kwa dini hii
zipo wazi. Zinapatikana kutokana na makundi yaliyomo
ndani ya dini hii ya Uislamu,
makundi ambayo kitu pekee kinachowaunganisha ni kitabu
kimoja kitakatifu cha Quran.
Makundi ambayo kila moja lina
viongozi wake, misikiti yake na
mipango yake tofauti.
Hali hiyo imepelekea kuwepo kwa Masheikh tofauti tofauti,
na hii ni kwa sababu ya kukosekana kwa mamlaka moja iliyoazishwa kwa mujibu wa
mafundisho ya Uislamu
ili kudhibiti Masheikh
wengi wa makundi.
Kibaya zaidi, baadhi ya
Waislamu
wamezuili w a
kuswali

katika baadhi ya misikiti,


makundi hayo yamekuwa yakibishana kuhusu siku sahihi ya
kuswali Idd-el-Fitri, huku kudhoofika kwa dini kunashuhudiwa kwa mapigano ya Waislamu
wenyewe ndani ya misikiti.
Mapambano hayo mara moja
au mbili yamepelekea baadhi ya
waumini kupoteza maisha.
Cha kushangaza zaidi, malumbano hayo hayatokani na
tofauti za kufasiri Quran au mafundisho ya Mtume Muhammad (Rehma na amani ziwe juu
yake). Ukweli unaouma ni
kwamba, hao wanaoitwa viongozi wametumia dini kwa manufaa yao binafsi ya kisiasa, kikabila, na kimakundi na kupuuza
ustawi wa Waislamu wote nchini. Hali hili imepelekea ukosefu
wa chombo kimoja chenye
mamlaka ya kuwahudumia
Waislamu wote hapa Uganda,
kudhibiti na kugawa fedha kwa
faida ya Waislamu wote.
Leo kwa mara ya kwanza katika historia ya Uislamu hapa
nchini, makundi tofauti ya
Waislamu yanaungana katika
chombo kimoja ambacho kitaupeleka mbele Uislamu hapa
Uganda. Asije akatokeza mtu
atakayebeza umuhimu wa kazi
zitakazokuwa zikifanywa na
Baraza hili Kuu la Waislamu
(UMSC).
Leo kwa mara ya kwanza,
nina matumaini kuanzia sasa
kutakuwa na chombo ambacho
mambo muhimu ya Waislamu
yatakuwa yakiendeshwa kwa
manufaa ya wapenzi wa Mtume
wetu Muhammad (Rehma na
amani ziwe juu yake).
Utatuzi wa migogoro na kutokuelewana baina ya Waislamu kutafanyika kupitia
chombo hiki.
Pia mipango
mbali mbali
ya kitaifa
yenye lengo la
kuwanufais h a

Idi Amin Dada

Waislamu itashughulikiwa na
Baraza hili.
Hijja itashughulikiwa na
Baraza hili. Huko nyuma uandaaji wa hijja haukuwa wa kuridhisha hata kidogo, kwani kila
kundi lilishughulika na mashirika ya ndege au mawakala, lakini
mahujaji waliokuwa wakifanya
safari walikuwa wakitozwa viwango tofauti vya nauli. Baadhi
ya mahujaji walitapeliwa.
Kutokana na kutokuwepo
kwa chombo kimoja cha kuandaa hijja, tukio la kusikitisha lililomuhusisha mwanamke wa
Uganda lilitokea mapema mwa-

ya shida za zaidi ya miezi miwili.


Ni miujiza kwamba mama
huyu yu hai akiwa nasi hapa
nchini. Angeweza kufariki kama
raia wengine wa Uganda walivyofariki katika miaka iliyopita
wakati wakitekeleza nguzo hii
muhimu katika imani yetu.
Kwa hali hii, naamini
kwamba maisha ya walau wachache kati ya Waganda waliopoteza maisha katika hijja
yangeweza kunusuriwa endapo
tungekuwa na chombo maalumu kama Baraza hili kuratibu
safari zao za hijja.
Kwa sasa Baraza Kuu la

Wakati Uislamu ilikuwa


ndio dini ya kwanza
miongoni mwa dini za
kisasa kuingia katika
ardhi hii, ukuaji wake
umekuwa ni kwa kasi
ndogo ukilinganisha na
dini nyingi.
ka huu nchini Saudi Arabia.
Mwanamke huyo aliwasili Jeddah na kukuta kiongozi aliyeratibu safari yake hiyo ameachwa
na ndege.
Mama huyo alikuwa na fedha. Kiongozi wa kundi lingine
toka Uganda aliyewasili Jeddah
akiwa na binti huyo katika
ndege moja, alimfukuza na kumuacha binti huyo akihangaika.
Akaishiwa na hela. Akiwa hajasoma, hakuweza kuzungumza
lugha yoyote inayofahamika na
yoyote. Baada ya majuma
kadhaa, binti huyo alidhaniwa kuwa kafariki.
Ndugu na marafiki zake wa
hapa nchini walipewa taarifa ya
kifo chake. Ni kwa
mapenzi ya
Mwenyezi Mungu
Muweza mama
yule alinusurika
katika mazingira
hayo magumu
nakusaidiwa
kurudi
nchini
baada

Waislamu limeanzishwa, wale


Waislamu wenye dhamira ya
kwenda hijja wanaweza kuweka
matarajio yao katika chombo
hiki kwa matumaini makubwa.
Wakati wa safari yangu nje
ya nchi, nimekuwa nikiwasiliana na mashirika mbali mbali
ya kidini. Mengi ya mashirika
yameonesha nia ya kuwasaidia
ndugu zao wa Uganda kwa kuwapa msaada wa fursa za masomo (scholarship) na mengineyo.
Kama tusingekuwa na Baraza
hili, tusingeweza kupata neema
hii kubwa. Kwa uwepo wa Baraza hili, tutaweza faidika kutoka
kwao. Bila shaka, Baraza hili
litaimarisha ushirikiano wetu
na Waislamu wengine duniani
kote. Lakini pia lazima tukiri
kuwa, Uislamu nchini Uganda
unachechemea ukilinganisha
na jumuia zingine za kidini katika masuala ya elimu ya dunia.
Sababu za hali hii inanasibishwa
na kutokuwepo huko nyuma
kwa mamlaka kuu yenye wajibu
wa kupanga na kutekeleza mipango ya kuinua kiwango cha
elimu kwa Waislamu.
Natarajia Baraza hili kuwekeza jitihada zake nyingi, si
katika kuratibu tu shughuli za
mashirika ya kidini hapa nchini,
lakini pia kuandaa mikakati
ambayo itakuza shughuli zilizopo ili kusukuma mbele kiwango
cha elimu kwa Waislamu wa
Uganda.
Itaendelea toleo lijalo.

1 Rajab 1436, jumatatu Aprili 20 - 27 , 2015

hazina zetu

www.islamicftz.org

Ni vigumu kutambua
mchango wake katika
uandishi wa vitabu
kutokana na kutofahamika na wengi ukilinganisha na wanatasnia
wengine wa fani yake.
Alianzia katika fani ya
useremala na baadae
akawa msomi mkubwa
na hatimaye kuibuka
kuwa mwandishi wa
vitabu mbalimbali. Huyu
ndiye Sheikh Said Musa
ambaye hivi karibuni
mwandishi wetu
Yusuph Amin amefanya mahojiano naye na
kufahamu mengi kutoka kwake.
Gazeti la Imaan: Tueleze historia yako kwa ufupi.
Sheikh Said: Jina langu kamili
ni Said Musa Kisaka Kilomboche
Torogha Mkasirwa Mkule (Sammuki Tomm). Nimezaliwa mwaka
1943 katika kijiji cha Simbom Center, kata ya Msangeni, tarafa ya Ugweno wilaya ya Mwanga, mkoani
Kilimanjaro.
Gazeti la Imaan: Elimu yako
uliipata wapi?
Sheikh Said: Nilianza elimu
yangu ya msingi mwaka 1951 hadi
1956 katika shule ya Muslim School
Kilindini wilaya ya Moshi vijijini.
Baadae nikajiunga na sekondari ya
Muslim Academy ya mjini Zanzibar
kuanzia mwaka 1960 hadi 1963 na
wakati huo huo nikawa napata
elimu ya dini wakati wa jioni (magharibi) kwa Sheikh Abdallah Saleh
Alfarsy ambako nilijifunza fani
mbalimbali za dini zikiwemo tafsiri
ya Quran, nahwu, lugha ya kiarabu,
fiqhi, hadith na tawhid. Nilihitimu
mafunzo yangu ya dini mwaka
1966.
Nikiwa Zanzibar, mbali na
Sheikh Alfarsy nimejifunza elimu ya
dini pia kwa Masheikh mbalimbali,
akiwemo Sheikh Seyyid Omar Abdallah, Seyyid Ahmed Hamid
Mansab, Seyyid Ali Ahmad Badawi,
Seyyid Abdu-rahman Ahmed Assiriy, Sheikh Suleiman Alawiy,
Sheikh Sultan Muhammad Al-marashiy na Sheikh Said Muhammad
Alkindy, Sheikh Abbas (kutoka
Tumbatu), Sheikh Mahmud wa
Makadara na Sheikh Ramadhan
(wa Kwakhan).
Gazeti la Imaan: Kwa nini uliamua kwenda kutafuta elimu Zanzibar?
Sheikh Said: Hapo awali nilikuwa katika chuo cha Mbale
wilaya ya Mwanga mkoa wa Kilimanjaro nikajifunza Quran tukufu
pamoja na ufundi seremala kuanzia
1957 hadi 1959. Hapo ndipo Sheikh
Shaaban Rashid ambaye kwa sasa
ni Sheikh wa mkoa wa Kilimanjaro
aliponipa fursa ya kwenda Zanzibar

Sheikh Said MuSsa:


Msomi, mwanaharakati aliyebobea
kwenye utungaji vitabu
kusoma elimu zaidi.
Gazeti la Imaan: Unamzungumziaje mwalimu wako Sheikh
Alfarsy?
Sheikh Said: Sheikh Alfarsy
alikuwa ni mtu wa watu kwa maana
mwenye mahusiano mema na kila
mtu na pia alikuwa mtu mcheshi na
mwepesi katika kufanya maamuzi.
Sheikh Alfarsy ameacha athari
kubwa ambayo jamii inanufaika
nayo mpaka hii leo.
Kwa mfano amefanya kazi
kubwa katika kuandika tafsiri sahihi
ya Quran, alieneza sunnah na kupinga bidaa, amefanya mapinduzi
makubwa kwa kuifanya fani ya uandishi wa vitabu kuwa na tija na
amepelekea kundi kubwa la wahadhiri wa Kiislamu kuondoa woga
katika kufikisha ujumbe wa Allah
(yaani daawah) na pia ameleta
mchango muhimu katika uandishi
wa vitabu.
Gazeti la Imaan: Ulianza lini
uandishi wa vitabu?
Sheikh Said: Uandishi wa vitabu nilianza rasmi mnamo mwaka
1958. Kitabu cha kwanza kilichosahihishwa kilitoka mwaka 1961 na
kuchapishwa mwaka 1963. Hadi
kufikia sasa nimeshaandika vitabu
takriban 200 vikiwemo vya dini na
visivyo vya dini.
Miongoni vya vitabu vya dini
nilivyoandika ni twahara, udhu na
swala, dua za kuswalia, tafsiri ya alaqidatul islaamiyah (mambo
ya tawhiid), tafsiri ya Alalarbainan Nawawiyyah na tafsiri ya Alarabiynul qudsiyyah.
Kwa upande wa vitabu
visivyo vya dini ni kama
vile wito kwa walimwengu wote kuhusu

Mwandishi wa makala
hii akifanya mahojiano
na Sheikh Said Musa.

amani, namna ya kutunga mashairi


na mashairi ya kimaendeleo.
Gazeti la Imaan: Vitabu unavyoandika vinabeba maudhui gani?
S h e i k h S a i d : Maudhui
makubwa katika vitabu vyangu vingi yamebeba ujumbe wa kuelimisha
jamii ya kiislamu juu ya kuzingatia
maadili, vilevile fiqhi, tawhiid, hadith, tenzi na mashairi.
Gazeti la Imaan: Fani ya uandishi wa vitabu ina ugumu gani?
Sheikh Said: Ugumu ambao
waandishi wengi wanakumbana
nao katika fani hii ni kuvunja sheria
za uandishi, kukosekana ujuzi wa
kile kinachoandikwa, kukosekana
kwa utaalam na lengo la kitabu unachokiandika, uwepo wa sentesi ndefu zisizo na umuhimu wowote katika matumizi, kutozingatia matumizi ya lugha sanifu na kutumia lugha
zinazoleta utata mpaka kuleta mfarakano.
Gazeti la Imaan: Je uandishi
wa vitabu vya dini umechochea mabadiliko yeyote katika jamii za Waislamu na Uislamu?

Sheikh Said: Mabadiliko ni


mengi, kwa mfano jamii za Kiislamu zimeelewa maana ya bidaa katika Uislamu ni kitu gani, halikadhalika watu wamerahisishiwa kupata
usahihi wa ibada mbalimbali katika
Uislamu kama vile swala, zaka n.k.
Gazeti la Imaan: Ni ipi tofauti
kati ya uandishi na utunzi?
Sheikh Said: Tofauti ni
kwamba, mwandishi ni mtu anayeandika vitu au mambo mbalimbali
na mtunzi ni mtungaji wa vitu
mbalimbali kama vile sanaa, michezo ya kuigiza au kitu chochote anachodhani kitaleta manufaa kwa
jamii. Nakumbuka Sheikh Alfarsy
mara nyingi alipokuwa akinisahihisha ninapoandika nenoutunzikwa
kuniambia neno sahihi linalofaa kutumia ni utungaji kwa sababu ukisema utunzi maana yake ni utunzaji wa vitu.
Gazeti la Imaan: Katika maktaba zetu kumekuwa na uhaba
mkubwa wa vitabu vyenye taarifa
muhimu za dini ya Kiislamu, labda
tatizo liko wapi?

Ugumu ambao
waandishi wengi
wanakumbana nao katika
fani hii ni kuvunja
sheria za uandishi,
kukosekana
ujuzi wa kile
kinachoandikwa,
kukosekana
kwa utaalam na
lengo la kitabu
unachokiandika

5
Sheikh Said: Tatizo si kwamba
hakuna watungaji, isipokuwa wengi
wa watungaji hawaafiki suala zima
la usahihishwaji wa vitabu vyao. Hii
inatokana na vitabu vingi vya dini
kutokuwa na rejea za kutosha. Ili vitabu vya dini viwe bora lazima viambatane na dalili za Quran na Sunnah na wapokezi sahihi na vile vile
kutumia hadith nyingine zisizokuwa za Bukhari na Muslim.
Ni bora zaidi kutumia hadith zilizofanyiwa uchambuzi maalum wa
hadith kuthibitisha usahihi wake
japo zimetolewa na Nasai, Tirmidh,
Ibni Majah n.k vinginevyo mtu
anaweza kuandika hadith isiyopokelewa na Bukhari na Muslim
na kumbe siyo sahihi. Baadhi ya
waandishi wengi hawazingatii hayo,
bali wengine husema tu Mtume
(Rehma na amani ziwe juu yake)
amesema bila kubainisha hadith
hiyo ni sahihi au imepokelewa na
nani.
Gazeti Imaan: Je unadhani ni
kipi kilichokosekana katika taaluma
ya uandishi wa vitabu Tanzania?
Sheikh Said: Kwa kweli kasoro
ni nyingi. Kwa mfano, vitabu vingi
vinakosa ukurasa wa yaliyomo na
utangulizi. Pia baadhi ya vitabu
havina vichwa vya habari katika
kurasa zake, haviandikwi hatimiliki
na vilevile vimekuwa na tatizo la
matumizi ya lugha sanifu.
Gazeti Imaan: Mwamko wa
jamii za watanzania katika usomaji
wa vitabu ukoje?
Sheikh Said: Mwamko kusema
kweli ni mdogo kwa kuwa watu
wengi hawana muda wa kujituliza
kusoma vitabu ingawa wapo wachache ambao hujitahidi kusoma vitabu vidogo. Nakumbuka Sheikh
wangu aliwahi kuniusia niwe
naandika vitabu vidogo vidogo kwani wasomaji tulionao
sio wa kusoma vitabu
vikubwa
na kama
nitaamua
kuandika
vitabu basi
vidogo viwe
vingi zaidi
k u l i k o
vikubwa.

1 Rajab 1436, jumatatu Aprili 20 - 27 , 2015

hutolewa na kuchapishwa
The Islamic Foundation,P.O.Box 6011 Morogoro, Tanzania,E-mail: imaanmedia3@gmail.com
mhariri mtendaji: 0715 559 944, Mhariri: 0786 779 669, afisa masoko: 0785 500 502
TOVUTI: www.islamicftz.org

tahariri / uchambuzi

Ugaidi usitumike kuwakandamiza Waislamu


N
chi yetu inapitia
kipindi kigumu
ambapo kumekuwa na tetesi za
tishio la ugaidi, hususan baada
ya mashambulizi ya chuo kikuu cha Garissa kule Kenya.
Tukio la hivi karibuni lililotokea huko Kilombero, Morogoro la kukamatwa watu 10
ikidaiwa kuwa walikuwa na
milipuko, risasi, nguo za jeshi
na bendera ya Al-Shabaab
limezidi kuongeza hofu miongoni mwa wananchi.
Kutokana na ukweli
kwamba mashambulizi ya kule
Garissa yalifanywa na kundi la
Al Shabaab (kama walivyodaiwa kukiri kuhusika) na
kwamba watuhumiwa wa Morogoro walikamatwa wakiwa
msikitini, vyombo vya habari
ikiwemo mitandao ya kijamii
nchini vimeongeza kasi ya kuishambulia dini ya Allah na
Waislamu wakiipaka matope

na kuihusisha na ugaidi.
Sisi katika Gazeti la Imaan
tunapenda kuweka kumbukumbu sawa kwa kusema Uislamu hauhusiani na haufundishi
ugaidi na kwamba matukio
haya yasitumike kama kisingizio cha kunyanyasa Waislamu
na kuwanyima haki zao.
Ijulikane kwamba hata
kama waliokamatwa Morogoro wangethibitika kuwa
ni magaidi, kamwe hawawezi
kuwa wanawakilisha Waislamu. Lakini ni wazi pia kuwa
vyombo vingi vya habari na
mitandao ya kijamii vimeshawahukumu watu wale kuwa ni
magaidi, tena wa Al-Shabaab,
hata kabla ya uchunguzi wa
polisi kukamilika.
Hata hivyo, uzoefu wa matukio kadhaa yaliyowahi kutokea huko nyuma nchini unaonesha tabia ya kupenda kutia chumvi matukio ya kawaida ya kiuhalifu yaonekane

kuwa ni ugaidi na kuhusisha


Uislamu, mfano mzuri ni ule
wa Tanga katika mapango ya
Amboni. Haya yanayotokea
yanatupa wasiwasi Waislamu
hasa tukikumbuka mijadala
ya mahakama ya kadhi ambayo ilitumika hoja ya ugaidi
kupinga uwepo wa mahakama
hiyo. Tukijua umbali ambao
maadui wa Uislamu wanaweza kwenda ili tu kuuchafua
Uislamu, ni wajibu wetu kuwa
waangalifu.
Kumbukumbu zetu za tukio
lililotokea kule Marekani la
mtu mmoja Michael Conrade
Sibley, aliyefunguliwa mashtaka huko Atlanta mwezi uliopita kwa kutega bomu katika
sehemu ya bustani ya kupumzikia kwa lengo la kuwachongea Waislamu ingali
mbichi akilini mwetu.
Katika tukio hilo, Sibley
akiongozwa na chuki dhidi ya
Uislamu, hakujali kuwa anah-

atarisha maisha ya Wamarekani wenzake akaweka mabomu


ndani ya begi na kitabu cha
Quran, huku akijiita mzalendo. Sibley alifanya tuko hilo
Nov 4, mwaka jana ingawa
alikiri kufanya hivyo Machi
20, mwaka 2015.
Matukio mangapi ya aina
hii yanatokea duniani kote ili
tu kutengeneza sababu ya kuwaandama, kuwakandamiza
na kuwanyima Waislamu haki
zao. Waingereza wanasema
Ukitaka kumuua paka, mpe
jina baya.
Athari ya haya yanayotokea
kuhusishwa na Uislamu ni
kuwa mtu anayeonekana
kama Muislamu aidha kimavazi, kimuonekano na
vinginevyo atakuwa ni
mshukiwa moja kwa moja
akionekana katika maeneo fulani kama ilivyotokea kwa
waandishi wetu wa vyombo
vya Imaan waliokamatwa baa-

da ya kuonekana karibu na
daraja moja ambapo walisimama kuangalia ajali iliyotokea eneo hilo.
Kulikuwa na watu wengi
waliosimama kuangalia, lakini
ni wao waliokuwa katika
muonekano wa kigaidi kwa
mavazi yao na athari zao za
Uislamu. Mwisho tunasisitiza
tena kuwa Uislamu haufundishi ugaidi na haufungamani
na ugaidi ingawa wapo Waislamu wanaofanya vitendo vya
kigaidi kama ambavyo wapo
watu wa dini nyingine wanaofanya vitendo hivyo, ila tu
ugaidi unapofanywa na watu
wa dini nyingine dunia husita
kuuita ugaidi.
Na hii ndio maana rubani
msaidizi Andreas Gunter Lubitz wa shirika la Germanwings aliyeua watu 150 kule
Ufaransa hakuitwa gaidi bali
mgonjwa wa akili. Dunia ilimsikitia badala ya kumlaani!

nasaha za wiki

ati ya Machi 13 hadi


April 12 mwaka 2015
watu 103 walifariki
dunia kutokana na
ajali kubwa nane za barabarani.
Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya
karibuni ya mkuu wa kikosi cha
usalama barabarani DCP Mohamed Mpinga.
Kasi ya vifo vinavyotokana na
ajali imeendelea kuongezeka. Kila
uchao, vyombo vya habari vinaarifu kuhusu ajali za kutisha zinazoua mamia ya watu. Watanzania
sasa, tumeanza kuzoea habari
hizo.
Lakini takwimu ni namba tu.
Habari halisi zinazoweza kuelezea
athari za ajali hizi zipo nyuma ya
takwimu hizi. Habari halisi ni visa
vya maisha ya watu waliokuwa na
ndoto nyingi zilizozimika kama
kibatari.
Wapo vijana ambao walifariki
katika ajali hizi punde tu baada ya
kuhitimu elimu ya chuo kikuu.
Unaweza kuhisi uchungu wa
mzazi aliyejitahidi kulea kijana
wake, kumuongoza kwa miaka
yote hiyo! Inauma sana.
Wapo wakina mama na watoto
waliobaki wajane na yatima baada ya baba, mhimili wa familia
kufariki dunia. Huenda mwanaume alikuwa tegemeo katika
utafutaji riziki. Huenda mwanaume huyu alikuwa ni mfanyabiashara ambaye hana hata pensheni. Unaweza kuhisi uchungu
wa mama na watoto hawa na jinsi
maisha yao yatakavyoenda kubadilika ghafla?

Oumar Moukhtar

Utafiti wa kisayansi usaidie


kujua chanzo ongezeko la ajali
Zipo hadithi za familia nzima,
baba, mama na watoto, walioteketea katika ajali hizi. Uchungu kiasi gani unawakumba ndugu, jamaa na marafiki zao?
Wapo watu waliopata ulemavu
wa kudumu kutokana na ajali
hizi. Ulemavu wa namna hii unabadili kabisa maisha ya baadhi ya
watu, ambao huanza kujichukia
na kupitia kupata matatizo mengine ya kisaikolojia. Miongoni
mwa hawa, wapo waliotamani
kufa kuliko kuishi na ulemavu.
Kuna visa vya walemavu waliopoteza ajira kutokana na kukosa
uwezo wa kufanya kazi tena. Inauma sana hasa ukizingatia mtu
anaupata ghafla ulemavu huu
kama kufumba na kufumbua.
Tukienda katika mtazamo wa
Kiislamu, tunaamini Allah alishakadiria haya na ndio maana
yametokea. Lakini, sisi binadamu
ni viumbe tuliopewa akili ya kuzingatia mambo, na hivyo basi tu-

nao wajibu wa kuchunguza sababu za kuongezeka ajali hizi na kuchukua hatua muafaka.
Kinyume na hali hiyo, kinachoendelea hapa Tanzania ni kutupiana lawama kati ya wadau wanaohusika katika kadhia hii.
Madereva wanalaumu wamiliki kuwa hawawalipi vizuri na
kwa sababu hiyo wanaendesha
magari wakiwa na msongo wa
mawazo kutokana na matatizo ya
kimaisha. Madereva pia wanailaumu Serikali kwa kushindwa
kusimamia maslahi yao na
kushindwa kuboresha miundo
mbinu hususan barabara ambazo
zinatajwa kuwa nyembamba na
zenye mashimo.
Serikali pia inalaumiwa sana
kwa kukosa udhibiti mzuri katika
utoaji leseni za kuendesha magari
kiasi kwamba watu wengi wanapata leseni kwa njia za panya bila
kujaribiwa.
Jeshi la polisi, kupitia kikosi

chake cha usalama barabarani pia


kimenyoshewa vidole na wadau
wengi kwa sababu ya tabia ya
ufisadi na ulaji rushwa. Inadaiwa
kuwa askari wa kikosi hicho
wamekuwa wakifumbia macho
makosa ya dhahiri ya wahudumu
wa mabasi, ikiwemo kujaza abiria
na mizigo kupita uwezo wa gari,
mwendo wa kasi na kutozingatia
alama za barabarani.
Serikali kwa upande wake inaamini uzembe wa madereva na
ujuzi mdogo wa kutenda kazi yao
ndio chanzo cha ajali nyingi na
matokeo yake ikaja na wazo la
madereva kwenda kusoma.
Wamiliki wa mabasi pia wanatupiwa lawama kwa kutorekebisha hitilafu za kiufundi za
magari yao kwa tamaa ya pesa.
Inatajwa kuwa wamiliki hawataki
kutumia fedha kurekebisha
magari na pia wanaona muda
utapotea na hivyo kukosa pesa.
Abiria nao hawajanusurika na

Zipo hadithi za familia nzima, baba, mama


na watoto, walioteketea katika ajali hizi.
Uchungu kiasi gani unawakumba ndugu,
jamaa na marafiki zao?

lawama. Wakati abiria wengi


wamekuwa wakishabikia mwendo wa kasi, ni wao ndio huwa wa
kwanza kulaumu mwendo kasi
wa dereva pindi ajali inapotokea.
Kwa nini hawakumshinikiza dereva apunguze mwendo au kutaarifu vyombo husika, mara nyingi
polisi huhoji.
Kunyosheana vidole huku na
kuchukua hatua bila utafiti wa
kisayansi hakuwezi kuleta tija,
kama uzoefu unavyoonesha.
Huko nyuma tulikuwa na majaribio kadhaa ya kudhibiti ajali
ikiwemo kwa kufunga vidhibiti
mwendo. Vilidumu? Vilipunguza
ajali?
Nasaha zangu ni kuwa sasa tufanye utafiti wa kisayansi na tutumie majibu ya utafiti kutuongoza katika kutafuta jawabu la
namna ya kupunguza ajali za
barabarani.
Mambo ya guess work hayana
nafasi katika karne hii ya sayansi
na teknolojia. Kuhisi na kubuni ni
sababu mojawapo ya malumbano
na ubishi unaoendelea juu ya
chanzo cha kuongezeka ajali.
Uamuzi wa Serikali, ambao
baadae uliufuta, wa kuwataka
madereva wakasome haukutokana na utafiti bali kazi ya kubuni
na ndio maana madereva walibisha na kuigeuzia Serikali kibano
kuwa ndio chanzo cha ajali.
Kukata mzizi wa fitina, jawabu
pekee ni kufanya utafiti ili kujua
sababu za ongezeko la ajali na
mchango wa kila mdau katika
tatizo hili na je nini kifanyike?

1 Rajab 1436, jumatatu Aprili 20 - 27 , 2015

www.islamicftz.org

Kutoka katika Quran na Sunnah

penzi msomaji bado


tunaendelelea na
makala yetu tuliyoyaanza wiki iliyopita.
Pamoja na kuwa Quran ni maneno
ya Allah hebu tuangalie walau kwa
mukhtasari watu waliojadili, kwa
fikra zao, juu ya mtunzi wake wanasemaje.
Katika KamusiEncyclopedia
ya Kikatoliki juzuu ya sita, chini ya
mada ya Quran, wamesema: Over
the centuries, many theories have
been offered as to the origin of the
Quran.Today no sensible man
accepts any of these theories. Maana ya maneno haya ni:kwa karne
nyingi nadharia nyingi zimeibuliwa
juu ya asili ya Quran... Leo hakuna
mtu mwenye akili timamu
anayekubali yoyote miongoni mwa
nadharia hizi.
Kwa kifupi kuna nadharia kadhaa za wasiokuwa Waislamu zinazozungumzia utunzi wa Quran
tukufu. Wasio Waislamu wametofautiana sana kuhusiana na nani
kaitunga hii Quran isipokuwa wote
wanakubaliana kuwa Quran ilitamkwa kwa mara ya kwanza na mtu
ambaye alizaliwa katika mji wa
Makkah, mji ulioko katika Bara
Arab mnamo karne ya sita akiitwa
Muhammad (Rehma na amani
ziwe juu yake).
Ama kuhusiana na chanzo au
asili ya Quran, wasiokuwa Waislamu wamegawanyika katika

Na sheikh Tawakkal Juma

Nadharia mbalimbali juu ya asili ya Quran


makundi matatu.
Kuna wale wanaoamini kuwa
Muhammad (Rehma na amani
ziwe juu yake) mwenyewe ndiye
alikuwa mwandishi wa hii Quran.
Kundi la pili wanaamini kuwa Muhammad (Rehma na amani ziwe
juu yake) siye aliyeiandika hii
Quran lakini alijifunza kutoka kwa
mtu mwingine au watu wengine.
Kundi la tatu linaamini kuwa
Quran haijatungwa na mwanadamu bali ni maneno ya Allah.
Miongoni mwa nadharia zinazomuelezea Muhammad (Rehma
na amani ziwe juu yake) kuwa ndiyo chanzo au mtunzi wa Quran zinadadisi sababu mbalimbali za
yeye kutunga Quran. Moja ya nadharia inazungumziaMaterial gain
as the motiveyaani kutafuta mali
kuwa ndio sababu ya Muhammad
(Rehma na amani ziwe juu yake)
kutunga Quran, baadhi ya wengine
wakatajadesire for Power and Glory, yaani uchu wa madaraka na
umaarufu.
Wananadharia wengine wa-

kasema Muhammad (Rehma na


amani ziwe juu yake) alikuwa
anatakaUnity and Liberation of
Arabs yaani kuleta umoja na kuwakomboa waarabu. Na wapo waliosema Muhammad alitaka kuleta
mageuzi ya roho (moral reformation).
Pia wapo waliodai kuwa Muhammad (Rehma na amani ziwe
juu yake) aliitunga Quran pasina
kujijua yaani unconscious fabrication na wengine waliokuja na nadharia ya kifafa (epileptic theory) na
nyinginezo.
Uchunguzi huru na yakinifu unaonyesha kuwa nadharia hizi zote si
chochote bali uongo mtupu na haziingii katika akili ya mtu mwenye
akili timamu anayeisoma Quran
kwa kuzingatia.

MAUDHUI YA QURAN:

Kama ilivyo kawaida, kila kitabu


kina maudhui. Maudhui makuu ya
kitabu hiki ni lile lengo la kuumbwa
mwanadamu, ambalo ni kumtumikia Allah. Pamoja na kuwa haya

ndio maudhui makuu, ndani ya


kitabu hiki pia kuna maudhui mengine mbalimbali ambayo yanalenga
kumkinaisha mwanadamu ili aliendee lengo lake la kuumbwa.
Maudhui haya yote yameashiriwa
katika sura ya kwanza, yaani Suratul-Faatiha.

MAJINA YA QURAN:

Jina maarufu la kitabu hiki ni


Quran, lakini kutokana na utukufu wake na sifa zake adhimu
kimepewa majina mengine kama
Kipambanuzi (Alfurqaanu, Al
Bayaanu, Attibiyaanu, Albayyinnatu), Tukufu (AlAdhwiimu,
AlAzizi), Yenye Hekima (Alhakiimu), Nuru (Anuur), Muongozo
(Alhudaa), Ukumbusho (Attadhkratu), Rahma (Arrahmatu), Ponyo (Asshifaa), Kitabu Chenye Kubainisha (Alkitaabul Mubiinu),
Utajo Mtukufu (Adhikrul Hakiimu), Njia Iliyonyooka (Asswiratul
Mustaaqiimu) n.k.
Hiki ni kitabu pekee ambacho
kimebaki katika uasili wake tangu

Kwa kifupi kuna nadharia kadhaa za


wasiokuwa Waislamu zinazozungumzia
utunzi wa Quran tukufu

kiteremshwe tofauti na vitabu


vingine ambavyo kalamu ya
waandishi na mafarisayo imevifanya kuwa uongo, kama Yeremia 8:8
isemavyo. Kulingana na tabia ya
Mayahudi ya kubadilisha maneno
ya Allah ni vigumu sana kwa sasa
hata kujua katika vitabu vingine ni
lipi neno la Allah na ni lipi neno la
mwanadamu.
Sehemu kubwa sana ya vitabu
vingine sasa imekuwa ni maneno
ya wanadamu yenye kuendana na
matashi yao, ndio maana utaona
kuwa wakitaka kumla nguruwe
ambaye kaharamishwa na Allah
watapachika andiko lao pale kuwa
si kila kiingiacho ni najsi bali kitokacho! Atakayeitikadi katika
Waislamu au akawa na shaka ya
aina yoyote kuwa Quran imepungua, kwa mujibu wa Shariah ya Kiislamu anakuwa amepotoka na
kutoka katika Uislamu.
Jambo jingine la ajabu kuhusu
kitabu cha Quran ni kuwa tofauti
na vitabu vingine ndiyo kitabu pekee kilichohifadhiwa hata na watoto wadogo na wale wasiojua hata
maana ya neno moja la kiarabu.
Hii ni tofauti na vitabu vingine
ambavyo hakuna mtu hata mmoja
dunia nzima aliyehifadhi vitabu
hivyo neno kwa neno, mwanzo hadi
mwisho. Tena kimehifadhiwa si katika uandishi tu bali hata namna ya
usomaji wake!
Itaendelea

mlinganiaji
Na Sheikh Muhammad Duwaysh
UMUHIMU WA KHUTBA YA
IJUMAA:

Sita, khutba ya ijumaa na swala


yake hurejelewa kila wiki na hivyo
katika mwaka mmoja mwenye
kuswali ijumaa husikiliza khutba
hamsini na mbili (52). Kwa hiyo
khatwibu akizipa khutba zake uzito
unaostahiki na akazipangilia maudhui zake mada kamili kila khutba,
khutba hizo huwa ni semina iliyosheheni hazina kubwa ya ilmu na
mawaidha yenye kuendelea.
Hii ndiyo nafasi ya khutba kimaana mbele za watu na ndiyo
khutba zenye athari. Uchunguzi
kuhusu athari ya khutba ya ijumaa
uliofanyika nchini Misri unaonesha
kwamba 78% ya wasikilizaji khutba
huathirika moja kwa moja na yale
yasemwayo na khatwibu. Na kati ya
hao 71% wakasema kwamba wao
hutekeleza yale yasemwayo na khatwibu.
Makhatwibu wa ijumaa katika
msikiti mmoja nchini Misri walikubaliana mmoja wao atoe khutba
kuhusu riba. Wakagawa maswali
dodoso kabla ya khutba kwa waliohudhuria yenye swali je unafahamu
nini kuhusu riba?
Matokeo yakaonesha 85% walikuwa wanaufahamu sahihi juu ya
riba. Lakini baada ya khutba matokeo yakaonesha kuwa 97% wa-

Mpaka tutakapofaidika na Khutba za Ijumaa - 2


likuwa wanafahamu ufahamu sahihi ikiwa ni ongezeko la 12%.
Katika maswali dodoso kulikuwa
na swali juu ya adhabu ya mla riba.
Kabla ya khutba 33% tu walikuwa
wakijua adhabu ya mla riba, lakini
baada ya khutba idadi ikapanda
hadi 59%. Asilimia 71 walikuwa
wakijua kuwa benki za Misri zinajishughulisha na miamala ya riba,
baada ya khutba ikawa 94%.
Uchunguzi huo ukaonesha
kwamba 50% walikuwa wakipendelea kuweka fedha katika benki za
Kiislamu lakini baada ya khutba
ikapanda hadi 64%. Mwisho pakaoneshwa kwamba 34% watatoa nasaha kuhusu riba kwa watu wengine
na 31% wataacha miamala ya riba.
Uchunguzi kama huu ni ushahidi kwamba khutba ya ijumaa ina
athari kubwa kwa wenye kuswali
swala ya ijumaa na hapo ni pindi
wanapomkuta khatwibu mwenye
kuathiri kwa khutba na vitendo
vyake.
Saba, wahudhuriaji katika khutba ya ijumaa daima huzidi
kuongezeka kadiri muda unavyokwenda kinyume na muhadhara au
darsa ambapo wasikilizaji wanawe-

za kuwa wanaondoka wakati mtoa


mada anaendelea. Kwa khutba ya
ijumaa ni mpaka mada ya khatwibu
ikamilike ndio watu huondoka na
kwa hiyo ujumbe mzima hupatikana.
Baada ya kujua yote haya, je haipaswi kwetu makhatwibu kupewa
uzito mkubwa na muda wa kutosha
kwa maadalizi ya khutba ya ijumaa na kujihimu kutumia
mbinu mbali mbali kuhakikisha kuwa zinakuwa na
athari?
Na ni kwa nini taasisi na
jumuiya za Kiislamu haziandai semina kwa ajili ya
kuwawezesha makhatwibu wetu kutoa khutba zenye kutimiza
malengo ya swala ya
ijumaa na hivyo
kuinua viwango
vyao?
Haya ni maswali ya kujiuliza
kwa pamoja ili
kuziba pengo
linaloonekana
a m b a p o
misikiti mingi

inayoswaliwa ijumaa hakuna


mpango wa kuhakikisha kuwa
khutba zinakuwa chachu ya mabadiliko ya
Waislamu
na jamii kiimani, kielimu, kimaadili,
kiu-

chumi na kijamii. Khutba zinapaswa kuandikwa na kuhifadhiwa


kama rejea za siku za baadae.
Hatuwezi kubadilika mpaka tutakaponufaika kutokamana na
khutba zetu za ijumaa.
Itaendelea toleo lijalo
Waislamu wakisikiliza
mawaidha ya ibada ya
Ijumaaa.

1 Rajab 1436, jumatatu Aprili 20 - 27 , 2015

makala maalum

www.islamicftz.org

Historia ya Msumbiji;

Msikiti Mkuu jijini Maputo

Waislamu walitahadharishwa
dhidi ya Frelimo
Mpango
mkakati uliandaliwa kwa siri na
Wareno
Masheikh
walipingana wao
kwa wao

Waislamu walivyotumika - 1
Na ABUU MAYSARA

atika ulimwengu wa ushindani takriban katika kila


nyanja ya maisha; uchumi,
siasa, dini, n.k, ni rahisi kwa
mtu au kikundi cha watu kujikuta akitumika kwa maslahi ya wengine na pengine hata kwa madhara yake
mwenyewe.
Katika kipindi hiki tunapoelekea katika kura ya maoni kuhusu katiba inayopendekezwa na uchaguzi mkuu nchini,
Waislamu kama wanajamii wengine
wanapaswa kuwa makini dhidi ya kutumika kwa namna yoyote ile kwa maslahi
ya mtu au kikundi chochote kile.
Hili ni katazo kama alivyotufunza Allah katika Suurat Al Qasas (28:86) alipomwambia Mtume Muhammad (Rehma na amani ziwe juu yake):Na wala
ulikuwa hutaraji kuteremshwa kwako
kitabu isipokuwa ni rehma kutoka kwa
Mola wako, basi usiwe egemeo/msaada
kwa makafiri.
Pia Allah Subhaanahu Wataala
akasimulia kutokana na Nabii Musa
(Rehma na amani ziwe juu yake):Ee
Mola wangu, kwa vile ulivyoneemesha
juu yangu, basi kamwe sintokuwa egemeo/msaada kwa watu waovu(28:17).
Lakini ni mara ngapi Waislamu kwa
kujua au kutojua tumetumika kwa
maslahi ya watu wengine huku tukiidhuru dini yetu au sisi wenyewe? Katika
makala hii, tutadondoa sehemu katika
historia ya Msumbiji wakati wa mapambano ya chama cha FRELIMO ya kudai
uhuru kutoka kwa Wareno ili kuona jinsi baadhi ya Waislamu wenzetu huko
walivyokubali kutumiwa na Wareno na
madhara yake.
Hii ni tafsiri ya makala iitwayo Islam
in the Service of Colonialism? Portu-

guese Strategy during the Armed Liberation Struggle in Mozambique iliyoandikwa na Edward A. Alpers.
Kwa mujibu wa Askofu Mkuu wa
Lourenco Marques, Kadinali Teodosio
de Gouveia, Waislamu walimkaribisha
Vasco da Gama katika kisiwa cha
Msumbiji mwaka 1497. Wakiongozwa
na ari yao ya vita vya msalaba na uchu
wa kuhodhi rasilimali, Wareno waliuona Uislamu na Waislamu kama maadui
wakubwa kabla hata ya kutweka nanga
kuja Afrika.
Wakati Wareno waliporejea Msumbiji kwa mara ya pili mwishoni mwa
karne ya kumi na tisa safari hii kama wakoloni katika kinyanganyiro cha mataifa ya Ulaya kugawana Afrika, wakakuta
wimbi la kuenea kwa Uislamu eneo la
Kaskazini mwa Msumbiji kutokea
pwani.
Hali hii iliamsha ari na moyo miongoni mwa maafisa watawala, askari
Wakireno na wawakilishi wa Kanisa
Katoliki ya kupambana na Uislamu katika vita vya msalaba eneo la Kaskazini
mwa Msumbiji. Inakuwaje basi Wareno
waamue kuwaweka viongozi wa Waislamu nchini Msumbiji katika safu yao
dhidi ya Frelimo wakati wa vita vya
ukombozi wa Msumbijimiaka ya 1960
hadi 1970?
Ili kupata jibu la kitendawili hiki, tunahitaji kujua kitu kuhusu historia ya
Msumbiji ya karne ya ishirini iliyopelekea Wareno kufikia uamuzi huu wa kihistoria wa kuwatumia Waislamu kuwasaidia kupambana na Frelimo.
Kukua kwa Uislamu na Sera ya
Wareno nchini Msumbiji:
Kama mahali popote Afrika ya
Mashariki, nyenzo kubwa ya kuenea
kwa Uislamu mwanzoni mwa karne ya
20 ilikuwa niTwariqa- jumuiya za Kis-

ufi. Twariqa ya Shaadhiliyya iliingia kisiwa cha Msumbiji mwaka 1896 kutokea
Comoro na Zanzibar na kufuatiwa na
Qadiriyya.
Awali Twariqa ya Shaadhiliyya iliingia kupitia walinganiaji kutoka visiwa vya
Comoro na hadi leo kuna uhusiano imara na Comoro. Tawi la kwanza la Twariqa ya Qadiriyya nchini Msumbiji liliundwa na Sheikh kutoka Zanzibar.
Taratibu twariqa zote hizi mbili ya
Shaadhiliyya na ile ya Qadiriyya zikaanza kueneza matawi yao kuelekea bara ya
Msumbiji kupitia barabara na reli,
wakati huo huo ukoloni wa Kireno ukijikita nchini Msumbiji. Tawi jingine la

twariqa ya Qadiriyya likafunguliwa jimboni Niassa kupitia Tanganyika (sasa


Tanzania) na Nyasaland (sasa Malawi).
Hadi kufikia mwaka 1930, wakazi
wengi waafrika kaskazini mwa Msumbiji walikuwa Waislamu huku wakatoloki
wakiwa wachache na waanglikana wakiwa wachache zaidi. Dalili ya kwanza ya
Wareno kuwaona Waislamu kuwa ni
tatizo ilijitokeza mwaka 1937 kulipokutikana vipeperushi (bila shaka kutokea
Zanzibar) vikielezea furaha ya Waislamu
kwa Dola la Kihabshi (Abyssinia, wakati
huo mtawala wake akiwa Muislamu)
kuwashinda Waitalia.
Wareno waligundua kuwa chanzo

Wakati Wareno
waliporejea Msumbiji
kwa mara ya pili mwishoni
mwa karne ya kumi na tisa
safari hii kama wakoloni,
wakakuta wimbi la kuenea
kwa Uislamu eneo la
Kaskazini mwa Msumbiji
kutokea pwani

cha vipeperushi hivyo ni raia wa


Msumbiji mwenye asili ya kiarabu.
Wareno wakaona kutokuwepo kwa
wakatoliki kaskazini mwa Msumbiji ni
tatizo kwani kunawaacha wakazi wa
eneo hilo chini ya ushawishi wa Waislamu kwa kuwepo madrasa na misikiti
ambamo ndani yake itikadi dhidi ya wazungu na wakristo hufundishwa.
Hali hii ilipelekea utawala wa Wareno
kuanzisha mjadala juu ya mbinu za kudhibiti Uislamu. Moja ya fikra ilikuwa ni
kufunga misikiti na madrasa zote. Kulikuwa na sheria ya Wareno iliyotaka
kila shule iwe imesajiliwa na taasisi nyingi za kielimu za Waislamu hazikuwa
na usajili. Mbinu hii ya kutaka madrasa
zisajiliwe iliwahi kuibuka hapa Tanzania.
Mwisho, Wareno waliona hatua ya
kufunga madrasa na misikiti ya Waislamu ni kujitafutia balaa kwani ingeongeza chuki ya Waislamu dhidi ya Wareno.
Wareno waligundua kuwa madrasa
na misikiti ni kama chakula kwa Waislamu, wangeweza kuingiza ushawishi
wao katika uendeshaji wake, lakini si
kuzikandamiza. Kutokana na kukosekana mfumo imara wa elimu wa kikatoliki eneo la kaskazini ya Msumbiji,
mamlaka ya Wareno katika wilaya hiyo
iliamua kuacha hali jinsi ilivyo.
Ingawa iliamuliwa kuziacha madrasa na misikiti iendelee katika eneo la
kaskazini mwa Msumbiji, hali haikuwa
hivyo katika jimbo la Cabo Delgado na
Porto Amelia. Huko Wareno walizifunga madrasa na misikiti kwa masiku kadhaa na kunyanganya vitabu vya dini ya
Kiislamu Machi 1937, uamuzi ambao
baadae ulifutwa na gavana mpya wa
jimbo la Niassa mwezi Oktoba 1938.
Jambo lililowachanganya zaidi
Wareno ni nafasi ya Zanzibar katika

1 Rajab 1436, jumatatu Aprili 20 - 27 , 2015

www.islamicftz.org

mambo ya Uislamu na Waislamu nchini


Msumbiji, kwani Zanzibar ilikuwa kitovu cha harakati zote za Uislamu Afrika
Mashariki na Kati nyakati hizo.
Mwanzoni mwa mwaka 1930, mzozo wa kidini katika jimbo la Cabo Delgado ulipelekwa kwa Kadhi Mkuu wa
Zanzibar kwa ajili ya kutolewa fatwa.
Miaka michache baadaye, Mkaguzi wa
Utawala (Administrative Inspector) aitwaye Pinto Correa aliielezea hatari hii.
Pinto alisema:Waislamu wengi wanaendelea kutii ushawishi wa Masheikh
kutoka Zanzibar na ushahidi thabiti tunao. Madrasa na misikiti inashamiri kila
sehemu ikiashiria mshikamano wa kidini ambao kwa Waislamu ni sawa na muundo wa kisiasa unaoelekezwa na
kuendeshwa na wageni kutoka Tanganyika, Nyasaland na hata Kenya.
Hatimaye, Pinto alibuni mkakati wa
kudhibiti alichokiona kuwa kitisho
kikubwa kwa utawala wa Wareno
kaskazini mwa Msumbiji kutokana na
ushawishi mkubwa wa kiongozi wa
Twariqa ya Qadiriyya, Sheikh Abdul
Majid kutoka Macufi kote wilayani Lurio.
Katika mkakati wake aliandika
hivi:Kwa kuwa haiwezekani kuiangamiza imani ya Waislamu, kwa hiyo
kwa sasa, ili kudhibiti kuenea kwake, tunapaswa kuidhibiti na kuielekeza kwa
maslahi ya taifa la Wareno.
Mkakati wake ukajumuisha serikali
kufadhili ukarabati wa misikiti jimboni
Macufi. Katika andiko aliloandaa liitwalo Kuutaifisha Uislamu wa wenyeji,
alibuni mkakati wa kutekeleza mbinu
hii kwa kuanzisha mfuko maalum
utakaochangiwa fedha na serikali ya
mkoloni uitwaoMfuko wa Ureno kwa
ajili ya Waislamu ambapo fedha zingetokana na kodi za serikali za mitaa.
Pinto aliona mkakati huu kuwa ni sehemu ya mapambano ya kudumu kati
ya Ukristo dhidi ya Uislamu kwani
Ukristo ulikuwa unazorota na Uislamu
kupata nguvu, hususan baada ya kiongozi mmoja wa Kanisa katika kisiwa cha
Ibo kusilimu.
Hapa Pinto aliiga tu mbinu ya Afisa
wa Serikali Mfaransa, aitwaye Lyautey
huko Morocco, aliyejifanya rafiki na kutoa misaada kwa Waislamu huku akiwa
si tu Mkatoliki na mwanajeshi bali pia
mfuasi wa Jesuit! (Kitengo Maalum cha
Ujasusi cha Kanisa Katoliki Duniani).
Pamoja na ukweli huo, Lyautey aliacha wosia karibu na kufa kwake akiandika kwa mkono wake maneno
yafuatayo ili yaandikwe juu ya kaburi
lake:Hapa amelala Padri Lyautey, raia
wa Ufaransa nchini Morocco, na ambaye kamwe katika maisha yake hakusahaau kuuheshimu Uislamu!!!
Mrithi wa Pinto kama Mkaguzi wa
Utawala wilayani Cabo Delgado aliandika katika ripoti yake ya ukaguzi
kwamba wilaya imejaa Masheikh ambao wamefundishwa Tanganyika kiasi
kwamba inahofiwa Uislamu kupanuka.
Wakati huo huo akaishauri serikali
kwamba hatua ya mamlaka ya utawala
kuifunga misikiti na madrasa na kuisimamia haikuwa na mantiki yoyote.
Hadi kufikia miaka ya 1950, Wareno
nchini Msumbiji walikuwa bado hawajawa na mkakati wa kudhibiti kilichoshuhudiwa na watawala kuwa ni
kukua na kuimarika kwa Uislamu hasa
kaskazini mwa Msumbiji. Wakati huo
huo harakati za mapambano ya kuikomboa Msumbiji kutoka katika makucha
ya Wareno ilikuwa imeshaanza kuvuka
mpaka kutokea Tanganyika.
Inaaminika kwamba wanamgambo

Stratejia ya
wamagharibi
kuwagawa
Waislamu
Ilipoishia wiki iliyopita .. Waislamu
washika mwendo wa zama za jadi ya kiislamu
(traditional orthodox Islam) wana chembechembe ya demokrasia zinazoweza kutumika kupambana na msimamo wa kikandamizaji
na kiimla wa siasa kali, ingawaje hawafai kuwa
chombo cha kutegemewa cha demokrasia ya
Kiislamu.
Nafasi hii inaliangukia kundi la wanamageuzi wa kiislamu (Islamic modernists) ambao utendaji wao una kikwazo kwa sababu
kadhaa ambazo ripoti hii itazizungumzia.
Ili kuchochea mabadiliko chanya kwa ulimwengu wa kiislamu kuelekea demokrasia
kubwa zaidi, usasa na kuendana na mfumo wa
kimataifa wa zama hizi, taarifa ya RAND inashauri ifuatavyo:
The United States and the West need to
consider very carefully which elements, trends,
and forces within Islam they intend to strengthen; what the goals and values of their various
potential allies really are; and what the broader
consequences of advancing their respective
agendas are likely to be.
Marekani na nchi za magharibi zinahitaji
kutafakari makundi gani, mtiririko wa matukio
na nguvu ndani ya Uislam za kuzipa nguvu;
(pia) kungamua malengo na maadili ya wawezao kuwa washirika wao na matokeo ya kuzisaidia ajenda zao.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mbinu
mchanganyiko kwa ajili ya makundi mbali
mbali inaonekana kuwa na matunda mazuri
zaidi. RAND wanashauri:
Kwanza, ungeni mkono wanamageuzi wa
kiislam, chapisheni na kusambaza maandiko
yao kwa gharama nafuu ili watu waweze kuyapata kwa urahisi, wahimizeni waandike fikra zao
kwa ajili ya umma na hasa vijana, ingizeni fikra
zao katika mitaala ya elimu ya Kiislam (Kumbuka mradi wa Conrad na mtaala wa elimu ya
kiislam na kuchapisha vitabu Tanzania bara na
Zanzibar), wapeni jukwaa waufikie umma
kueleza fikra zao (vipindi vya radio, runinga,
magazeti, mitandao ya kijamii n.k).
Fanyeni tafsiri, maoni na fatwa zao kwenye
masuala ya msingi ya dini ya kiislamu yaufikie
umma wa Waislamu ili kushindana na siasa
kali na wahafidhina ambao wana tovuti, mitambo ya uchapaji, mashule, vyuo na nyenzo nyingine za kusambazia fikra zao.
Wawekeni wasekula na wanamageuzi kama
mila mbadala Counterculture kwa vijana ambao hawajaharibiwa na fikra za siasa kali.
Wezesheni na himizeni ufahamu wao kuhusu
historia ya Uislam kabla na historia ya ulimwengu usio wa kiislamu na mila nyingine katika vyombo vya habari na mitaala ya nchi husika. (Rejea propaganda ya upotoshaji wa historia ya utumwa Afrika Mashariki kupitia mitaala
na vitabu vya historia mashuleni). Propaganda
zinasema Uislamu na Waislamu ndio wa kulaumiwa kuhusu utumwa na wazungu ndio
wapiga vita utumwa.
Wasaidieni (wasekula na wanamageuzi ya
kisasa wa kiislam) kuendeleza taasisi huru za
kijamii kutia nguvu utamaduni wa kiraia na
kutoa nafasi kwa wananchi wa kawaida kujifunza kuhusu mfumo wa kisiasa wa kimagaharibi na kuelewa misimamo yao. Msomaji kumbuka kuundwa kwa taasisi mbali mbali za kiis-

Mbinu nyingine
waliyowashauri
wamarekani
waitumie
katika kuupiga
vita Uislam ni
kuongeza idadi ya
wanafunzi wenye
fikra za usasa
(modernists)
katika vyuo vya
kiislamu vya
kihafidhina kama
vile Chuo Kikuu
cha Madina, Al
Azhar n.k.
lamu ambazo kazi yao kubwa ni kupinga juhudi
za Uislam na Waislam kuusimamsiha Uislamu
huku zikipewa majukwaa mbali mbali kuelezea
fikra zao.
Ama kuhusu makundi mawili yaliyobakia
kati ya yale manne walishauri: Waungeni
mkono wahafidhina dhidi ya siasa kali, tangazeni ukosoaji wa wahafidhina kukosoa ukatili
na fikra za siasa kali, chocheeni kutokuelewana
kati ya wahafidhina na siasa kali, Pingeni ushirikiano kati ya wahafidhina na siasa kali na
chocheenii ushirikiano kati ya wanamageuzi
wa kisasa na wahafidhina ambao wako karibu
yao kimtazamo katika baadhi ya mambo.
Pale inapowezekana, wapeni elimu wahafidhina kuwawezesha kuwa weledi kwa mijadala
na siasa kali. Siasa kali mara nyingi ni wazungumzaji na watoa hoja wazuri wakati wahafidhina wanajua zaidi kuhubiri Uislamu ulivyo
tu.
Katika nchi kama za Asia ya Kati, wahafidhina watahitaji kufundishwa na kufundwa
kuhusu Uislamu sahihi (orthodox Islam) ili
waweze kujitetea dhidi ya hoja za siasa kali.
Msomaji ona mbinu hii, wamarekani wanaambiwa wawafundishe Waislamu Uislamu sahihi
si kwa kuwa wanaukubali Uislamu bali wautumie kuwagonganisha Waislamu. Kwa hiyo
tuwe macho na ufadhili wa watu kama hawa.
Mbinu nyingine waliyowashauri wamarekani
waitumie katika kuupiga vita Uislam ni
kuongeza idadi ya wanafunzi wenye fikra za usasa (modernists) katika vyuo vya kiislamu vya
kihafidhina kama vile Chuo Kikuu cha Madina,
Al Azhar n.k. Lengo ni kuwafanya wausome
Uislamu sahihi kwa nia ya kuja kuupinga huku
wakiwachanganya Waislamu kwa kuwa watakuwa wamehitimu katika vyuo vikuu vinavyokubalika na Waislamu.
Wanastratejia wa RAND wanaendelea
kushauri; Tofautisheni makundi mbali mbali

ya wahafidhina na wapeni nguvu wale walio


karibu na usasa (modernism) kama vile madhehebu ya Hanafi dhidi ya madhebebu nyingine za kiislamu. Wahimizeni sana watoe fatwa na kuzieneza ili kudhoofisha fatwaa za mawahabi.
Pia walishauri kuenezwa na kukubalika kwa
fikra za Usufi (mtazamo wa kuachana na dunia
na kujishughulisha na akhera tu). Lengo ni
kwamba Waislamu wengi wakiwa na mtazamo
huu wa kisufi, basi maadui wa Uislamu hawatopata upinzani wowote katika masuala ya dunia yao. Hili ndilo lengo la kundi la Al Hauthi
huko Yemen.
Kabilini na pambaneni na siasa kali, pingeni tafsiri yao juu ya Uislamu na onesheni makosa ya tafsiri yao hiyo. Fichueni uhusiano wao
na makundi na vitendo haramu. Tangazeni
sana athari za matendo yao ya kikatili.
RAND wanashauri, Onesheni kutokuweza
kwao kutawala na kuleta maendeleo chanya ya
nchi na jamii zao. Msomaji kumbuka Rais Mohamed Mursi na utawala wa Ikhwanil Muslimiyna huko Misri jinsi ulivyonyimwa misaada na
Marekani na washirika wake ili Ikhwan
waonekane hawawezi kutawala na kuleta
maendeleo na hatimaye ukapinduliwa.
Uelekezeni ujumbe huu haswa haswa kwa
vijana, washika ibada wa kihafidhina na Waislamu walio wachache katika nchi za magharibi
na makundi ya wanawake. Epukeni kuonesha
mnatambua au kuheshimu vitendo viovu vya
siasa kali na magaidi. Watangazeni kama ni
watu waliochanganyikiwa na waoga na katu
msiwatangaze kwa namna itakayofanya
waonekane kama mashujaa wakatili.
Wahimizeni wanahabari kuchunguza
mienendo na tuhuma za ufisadi, ubadhirifu wa
fedha, undumilakuwili na ufuska katika medani za makundi ya siasa kali na magaidi na kuzitangaza sana katika vyombo vya habari.
Himizeni migogoro baina ya makundi ya
siasa kali. Waungeni mkono wasekula kwa kuwachambua wafaao kuungwa mkono na wasiofaa. Himizeni kutambulika kwa siasa kali
kama adui wa watu wote na pigeni vita wasekula kuungana na makundi yanayoipinga
Marekani kama vile wapigania utaifa na watu
wa itikadi za mrengo wa kushoto.
Ungeni mkono fikra ya kutenganisha dini
na dola kuwa inakubalika hata katika Uislamu
na kwamba fikra hiyo haihatarishi imani ya
mtu bali ndiyo haswa huiimarisha.
Kisha RAND wakasema, mbinu yoyote
mtakayoitumia tunashauri ifanyike baada ya
kutafakari kwa kina na kufahamu fika uzito wa
baadhi ya masuala, maana inayoweza kupatikana kwa kuzingatia watunga sera wa
Marekani na misimamo katika baadhi ya masuala, athari za misimamo hiyo kwa makundi
mengine ya kiislam ikiwa ni pamoja na hatari
ya kuyahatarisha makundi yale ambayo tunalenga kuyasaidia na athari zisizotarajiwa za kusaidia makundi hayo katika muda mfupi mbeleni.
Hatimaye RAND wakamalizia taarifa yao
kwa kushauri mbinu kuu zifuatazo ziada ya
hizo zilizotangulia.

Makala hii kutokana na makosa ya kiufundi haikumalizika mpaka mwisho wiki iliyopita, kutokana na umuhimu wake tumelazimika kuiendeleza katika toleo hili MHARIRI.

1 Rajab 1436, jumatatu Aprili 20 - 27 , 2015

10

www.islamicftz.org

ncha ya kalamu
Sheikh Muhammad Issa

go go r o u n aoendelea nchini Yemen, ambao umevuka


mipaka na kuhusisha mataifa ya nje unaweza kuonekana
kama mgogoro wa kisiasa tu.
Hata hivyo, ukweli ni
kwamba mgogoro huu ni zaidi ya siasa. Ni mgogoro wa
kidini kati ya mashia na Ahlu
Sunnah wal Jamaa. Wanaoitwa ma-Houthi si wengine
bali ni mashia wa dhehebu la
Zaydiyyah lililopata kuitawala
nchi hiyo miaka mingi nyuma.
Mwaka 1962 utawala wa
ma - Houthi ulimalizika kwa
mapinduzi ya kijeshi ambayo
yaliibadili Yemen kuwa nchi ya
kisekula.
Chimbuko la ma-Houthi,
ambao jina lao rasmi ni Ansarullah yaani wenye kumnusuru Mungu, ni vuguvugu la vijana wa kishia liitwalo AlShabab Al-Mumin, yaani vijana
waumini lililoibuka baada tu ya
Yemen mbili kuungana mwaka
1990.
Jamii ya mashia ya Zaydiyyah ya Yemen walikuwa wakiilalamikia serikali ya Yemen
kwamba inawabagua, imejaa
rushwa, ina uhusiano na Saudi
Arabia na kwamba kituo cha
elimu cha Masalafi huko Saadah
kinaeneza imani ya masuni eneo
ambalo kihistoria ni eneo la
mashia.
Mwaka 2004, ma-Houthi walianzisha mapambano ya silaha kati
yao na majeshi ya serikali. Baada ya
vipindi kadhaa vya mapigano na
kusitisha mapigano hatimaye maHouthi wakaibuka kwa nguvu mwaka 2011 baada ya vuguvugu la maandamano ya raia yaliyozikumba nchi
za kiarabu maarufu kama Arab
Spring.
Kiongozi wa ma-Houthi wa
wakati huo aitwaye Hussein Badrudiyn al-Houthi (kwa hiyo jina maHouthi latokana na jina la kiongozi
wao) aliuwawa katika mapigano
hayo.
Hatimaye, mwaka 2014 maHouthi wakauteka mji mkuu wa
Yemen, Sanaa na kusababisha Rais

Vita ya Yemen ni
mkakati wa Iran
kueneza ushia
Abdurasuul Mansour Hadi kukimbilia Aden. Ma-Houthi wakajizatiti
kuiteka Yemen na hapo Saudi Arabia
na nchi nyingine kumi za kiarabu za
kisunni zikaanzisha mashambulizi
ya anga dhidi ya ma-Houthi kwa
lengo la kuurejesha utawala wa rais
Hadi aliyechaguliwa na wananchi.
Lakini nguvu kubwa kama hii ya
ma-Houthi wanaitoa wapi? Iran,
naam ma-Houthi wanasaidiwa na
Iran. Tarehe 18 Oktoba mwaka 2014,
Iran iliitisha mkutano wa washirika
wake uitwao, The International Islamic Awakening Association (Chama cha kimataifa cha uamsho wa
Kiislamu). Ni katika mkutano huo
ndipo mpango wa mashia wa kutawala nchi za mashariki ya kati kwa
itikadi ya ushia ulidhihiri.
Katibu Mkuu wa umoja huo Dr.
Ali Akbar Velayati alinukuliwa akisema kuwaambia wajumbe kutoka
ma-Houthi: Tuko hadhiri juu ya
ushindi wenu na tumefurahi sana
kuhusu ushindi huu. Uhusiano wetu
na ma-Houthi unarudi nyuma kitambo kirefu sana na tunajua fikra za
Sadrudiyn Houthi ambaye ni kiongozi wa kiroho wa Ansarullah na
baba wa shahidi Hussein Houthi na
Abdulmalik Houthi ambaye ni kiongozi wa ma-Houthi nchini Yemen
(hivi sasa).
Akaendelea kusema: Nina furaha kwamba ma-Houthi na kiongozi
wa mapinduzi nchini Yemen wanaongoza harakati za busara na za
kijasiri nchini Yemen.
Mara nyingi, Iran hukanusha kuwasaidia ma-Houthi lakini kwa kauli
za viongozi wake kama hizi inaonesha kuna mkakati maalum wa
mashia wa Iran kutawala nchi za kiarabu kwa kusimika utawala wa
mashia wenzao.
Dr. Velayati alinukuliwa
akisema: Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran inaona fahari kubwa

Wapiganaji wa Shiha
nchini Yemen.

kwa Ansarullah (ma-Houthi) na


kwamba inataraji jukumu kama la
Hizbullah ya Lebanon litafanywa na
Ansarullah nchini Yemen.
Kwa hiyo kwa mujibu wa Velayati,
kinachotokea nchini Yemen ni
mwamko wa Kiislamu (Islamic
Awakening), lakini kimsingi ni ushindi wa mashia kuwashinda masuni.
Dr Velayati anakiri: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inawaunga mkono
Ansarullahi (ma-Houthi wa Yemen)
na inaona harakati yao iko sambamba na utekelezaji wa sehemu ya
mwamko wa Kiislamu.
Kwa upande wao, wajumbe wa
ma-Houthi walioshiriki katika mkutano huo walitamka wazi kwamba
Ayatollah Khamenei siyo tu kiongozi
wa Iran bali ni kiongozi wa Waislamu wote duniani.
Huu ndio ukweli wa kinachotokea Yemen. Saudi Arabia haikuunda muungano wa kuwapiga maHouthi kwa lengo jingine bali kuzuia
mashia kutimiza malengo yao ya
kuzitawala kwa itikadi ya kishia nchi
za kiarabu hata ikibidi kimabavu.
Kwa mujibu wa chanzo hicho cha
habari cha mashia wenyewe, Dr Velayati alipoulizwa kuhusu manufaa
ya mapinduzi ya ma-mashia Houthi
nchini Yemen alijibu: Suala
muhimu ni kwamba njia ya kuikomboa Palestina iko Yemen kwa sababu
Yemen iko mahali muhimu kistratejia na karibu na bahari ya Hindi,
ghuba ya Oman na (mlango bahari)
bab el-mandeb.
Kukomboa Palestina hutumika
na Iran kama ngao ya kufichia lengo
lao kuu ambalo ni kutawala kwa
itikadi ya kishia eneo lote la mashariki ya kati. Tangu lini mashia
wakawa
na uchungu na

masunni wa Palestina wanaowatambua Abubakar, Umar na Uthman


(Radhi za Allah ziwe juu yao) kuwa
ni makhalifa wa Mtume (Rehma na
amani ziwe juu lake) mpaka wawe
tayari kuikomboa Palestina?
Naye mwakilishi wa kiongozi wa
kidini wa mashia Ayatollah Ali
Khamenei aitwaye Ali Shirazi, akiongea na Vikosi vya Walinzi wa Mapinduzi vya Quds alinukuliwa na Defa
Press akisema: Jamhuri ya Kiislamu
inawaunga mkono moja kwa moja
ma-houthi nchini Yemen, Hizbullah
Lebanon na wanamgambo nchini
Syria na Iraq. Kwa hiyo kinachoendelea nchini Yemen ni sehemu ya
picha kubwa inayoihusu Iran na
mkakati wake wa kutawala nchi za
kiarabu kwa itikadi ya ushia.
Hivi karibuni, Iran hususan kupitia kiongozi wake wa kidini, Ayatollah Ali Khamenei, imenukuliwa ikilaani kwa nguvu mashambulizi ya
anga ya nchi za kisunni za kiarabu
yanayoongozwa na Saudi Arabia kuwalenga ma-Houthi nchini Yemen.
Ali Khamenei amenukuliwa akisema: Uvamizi wa Saudia dhidi ya
Yemen na watu wake wasio na hatia
ni kosa...umeweka mfano mbaya katika eneo (la ghuba).
Iran haikuwahi kusema lolote
huko nyuma wakati ma-Houthi
wakiwaua masunni nchini Yemen
kwa silaha, fedha na mafunzo waliyoyapata kutoka Iran. Sasa inaona
mkakati wake wa kuitawala Yemen
unakwenda kombo ndiyo inapaza
sauti kutaka mazungumzo ya amani.
Katika vita hiyo ya maneno, Ayatollah Khamenei alisema: Riyadh
haitoibuka mshindi katika uvamizi
wake, akiwa na maana
Saudi Arabia na washirika wake hawatowashinda maHouthi.
0785 955 859

Huu ndio
ukweli wa
kinacho
tokea
Yemen.
Saudi
Arabia
haikuunda
muungano
wa
kuwapiga
ma-Houthi
kwa lengo
jingine
bali kuzuia
mashia
kutimiza
malengo
yao ya
kuzitawala
kwa itikadi
ya kishia
nchi za
kiarabu
hata ikibidi
kimabavu

1 Rajab 1436, jumatatu Aprili 20 - 27 , 2015

11

www.islamicftz.org

uchumi na biashara
Na Selemani Magali

Ijue Saccos ya kiislamu ya TAMPRO


N
eno saccos ni maarufu
hapa Tanzania hususan
katika zama hizi ambapo kila kundi la kijamii linajiunga ili kukabiliana na
changamoto za kiuchumi.
Saccos ni ufupisho wa maneno
ya kiingerezaSavings and Credit
Cooperative Society yaani Vyama
vya Ushirika vya Kuweka Akiba na
Kukopa. Vyama hivi mara nyingi
huundwa na watu wenye malengo
yanayofanana kama Waislamu,
walimu, wakulima, wafanyabiashara au wafanyakazi wa eneo au
kampuni husika.
Historia ya saccos inatokana na
watu wa hali ya uchumi ya chini na
kati kushindwa kupata sifa za kupata mikopo katika mabenki. Hivyo,
wataalamu wakaja na utaratibu
huu wa kuwakusanya pamoja na
kuunda mfuko wa kuhifadhi pesa
zao huku wakikopeshana kwa utaratibu maalum.
Miaka ya karibuni, Serikali imekuwa ikifanya kampeni kubwa kuhamasisha uundwaji wa saccos na
matokeo yake kumekuwa na
mwamko wa makundi mbalimbali
kuunda saccos au kujiunga na saccos.
Waislamu hawakubaki nyuma
katika uundaji saccos. TAMPRO
Saccos iliyopo Magomeni iliundwa
ili kuwakusanya Waislamu walioko
kwenye miamala yenye riba (haramu) na wale walioweza kujizuia ili
wasaidiane, wanasihiane na kuelimishana ili wapate mafanikio
duniani na kesho akhera.
TAMPRO Saccos ilisajiliwa
April 2010 kwa namba ya usajili
DSR.1257 na kuzinduliwa May
2010, ikiwa na makao yake makuu
Magomeni Usalama, jijini Dar es
Salaam, karibu kabisa na ofisi za
manispaa ya Kinondoni. Kwa sasa
ina matawi pia Morogoro, Mwanza
na Arusha.
Ni muhimu kwa Waislamu kuzijua saccos za Kiislamu ili waliozama
katika miamala ya riba wajue njia
mbadala ya kujikwamua kiuchumi
na wale ambao wamejizuia wajue
kuwa kuna mbadala wa mifumo
mibaya ya riba ambayo mtu anaweza kuitumia na kujikomboa kiu-

chumi. Matatizo yaliyopo katika


taasisi za kifedha za kisekula si riba
tu, bali pia mifumo hii ya fedha imewalazimisha Waislamu kutoka nje
zaidi ya mipaka ya Allah kwa kutoa
rushwa. Pia, baadhi ya Waislamu
wamefilisiwa na kuingia katika majanga mengine katika biashara zao
na maisha kwa ujumla.
Meneja wa TAMPRO saccos,
Abuu Firdaus Abdullah anasema,
kwa Muislamu yeyote anayemuogopa Allah anawajibu wa kujiunga na taasisi za fedha za Kiislamu ili
kunufaika na mikopo isiyo na riba
na kujiepusha na majanga mengine.
Saccos za Kiislamu kama zilivyo
saccos zingine zinakumbwa na
changamoto nyingi ikiwemo ile ya
kushindwa kukidhi mahitaji ya wanachama wake. Mfano, saccos ya
Tampro inauwezo wa kukopesha
mpaka milioni sabini kwa mwezi
huku kiwango cha juu cha kukopesha kwa mwanachama kikiwa
5,000,000. Kutokana na maombi
mengi, baadhi ya wanachama wanachelewa kupata mikopo.

Katibu Mkuu
wa Jumuiya ya
Wataalam wa
Kiislamu
Tanzania
(TAMPRO), Pazi
Mwinyimvua
akifafanua
jambo katika
moja ya
mikutano ya
wanachama wa
jumuiya hiyo.

Ni muhimu kwa
Waislamu kuzijua
saccos za Kiislamu
ili waliozama katika
miamala ya riba
wajue njia mbadala
ya kujikwamua
kiuchumi
Changamoto nyingine
inayoikabili saccos ya TAMPRO ni baadhi ya watu kuwa
wazito kurejesha fedha. Katika saccos nyingine, wanachama wakishindwa kurejesha
fedha, hatua za kufilisiana
hufuata. Lakini katika saccos
za kiislamu kama ilivyo TAMPRO saccos hali ni tofauti.
Njia ya kiimani hutumika zaidi.
Hata hivyo, ingawa katika
saccos za Kiislamu suala la
kudai marejesho ni la kiimani, Firdaus anasema wanach-

ama wanatakiwa kujenga


utamaduni wa kulipa ili wengine waweze kukopeshwa.
Kubaki na amana bila ya
kurejesha ni sawa na kurudisha nyuma taasisi.
Ili kufaidika na huduma
za saccos Muislamu anatakiwa ajiunge na asasi yeyote
anayoipenda yenye misingi ya
dini na kuwa mwanachama
wao, kisha aanze kujiwekea
akiba na hisa zake.
Kwa mfano kwa sasa
TAMPRO saccos wanatoa
mkopo wa aina moja tu un-

aoitwa kisheria Qard Hassan


ambapo mwanachama atakopeshwa fedha taslimu na
kutakiwa kuzirejesha bila riba
kwa muda uliopangwa.
Katika saccos ya TAMPRO, masharti ya kukopa ni
pamoja na kuwa mwanachama kwa kipindi cha miezi mitatu, na kukamilisha na kulipia hisa na gharama za
uendeshaji za mwaka mzima.
Kiasi cha mkopo kinachotolewa na saccos za Kiislamu
hakina tofauti na saccos za
kawaida. Mwanachama atakopeshwa mara mbili ya akiba yake. Tofauti iliyopo ni
riba. Katika saccos za kiislamu mwanachama hatoi riba
kwa kiasi alichokopa.
Mfano, akiba yako ni Tsh.
mil 5 unaweza kukopa Tsh.
mil 10 na utarejesha fedha
hizo bila ya nyongeza ya fedha. Kwa sasa, Saccos ya TAMPRO inauwezo wa kukopesha mwanachama wake kiasi
Tsh. milioni 5 na marejesho
ya mikopo yanatakiwa yafanyike kila mwezi kwa muda
usiozidi miezi 12 (mwaka
mmoja). Akizungumzia mafanikio, meneja wa saccos ya
TAMPRO, Firdaus, anasema
mafanikio walioyapata ni
pamoja na ile Qadar ya Allah
ya kuiwezesha kuendelea kuwepo kwa miaka mitano ikiendelea kutoa huduma.
Mpaka sasa TAMPRO
saccos ina wanachama 1,000
na ina uwezo wa kutoa mikopo kwa wanachama wake
yenye thamani isiyopungua
TZS.70,000,000/= kila
mwezi.
Kidogo kidogo, imewawezesha wengi katika wanachama wake kumiliki na
kuendeleza makazi na biashara zao pamoja na malipo
ya ada za shule na vyuo
mbalimbali.
Si nia yangu kuitangaza
TAMPRO Saccos, lakini kwa
manufaa ya Waislamu walio
wengi ambao wamekuwa
wakiteseka na wengine kuchupa mipaka ya Allah
mtukufu, nawausia waumini
kujiunga na SACCOS za Kiislamu ili kukwepa miamala
yenye riba.

tovuti za kiislamu
Tanzil.net
Assalam alaykum msomaji wa
gazeti la Imaan. Hii ni safu itakayokutambulisha tovuti mbalimbali
zenye maudhui ya dini ya kiislam. Hii
ni dunia ya sayansi na teknolojia na
Waislam hatuna budi kuendana na
wakati, bila kuchupa mipaka ya Allah
Subhanaahu Wataallah.
Ipo mitandao au tovuti nyingi ambazo zina maudhui ya Kiislam katika
mada mbalimbali ikiwemo Qur an,
Sira, Hijja, Hadith za bwana Mtume
(Rehma na amani ziwe juu yake) na

mambo mengine mengi ya kidini.


Leo tutaanza kuiangalia tovuti ya
Tanzil.net. Hii ni tovuti ambayo ilianzishwa miaka nane iliyopita na Profesa wa Chuo Kikuu cha Teknolojia cha
Sharrif (Sharrif University of Technology), Hamid Zarrabi. Chuo hiki kipo
nchini Iran.
Tovuti ya Tanzil.net imejikita katika Quran tukufu. Mtembeleaji wa tovuti hiyo anaweza kuisikiliza Quran
kupitia wasomaji 26 tofauti, wakiwemo wasomaji maarufu kama Abdul Bast, Abdurahman, Sudais, Saad

Na Khalid Omary
al Ghamad na wengine.
Ukitembelea tovuti hiyo vilevile,
unaweza kupata tafsiri ya aya husika,

tena kwa kusoma au


kusikiliza. Tovuti hiyo ina
tafsiri zisizopungua lugha
thalathini za nchi tofauti
ikiwemo lugha ya Kiswahili kupitia Sheikh Ally
Muhsin al Barwan. Vile vile
kuna kurasa itakayo kuwezesha kusoma tafsiri
peke yake kuanzia mwanzo
hadi mwisho, tena kwa saizi na aina ya maandishi ya
chaguo lako.
Tovuti ya Tanzil.net pia inakupa

nafasi ya kupata takwimu mbalimbali


za Quran. Kwa mfano, unataka kujua
neno ahad limetokea mara ngapi katika Quran, Tanzil.net itakuonyesha
na aya ambazo neno husika limejitokeza. Kwa uchache huo ndio
mtandao wa Tanzil.net. Kufurahia
elimu kubwa iliyopo katika mtandao
huo unaweza ukaingia katika tovuti
yao ya www.Tanzil.net ufaidike zaidi.
Kwa maoni, ushauri piga au
tuma ujumbe kwa 0683 110 006

1 Rajab 1436, jumatatu Aprili 20 - 27 , 2015

12

www.islamicftz.org

afya yako
Pazi Mwinyimvua

Umuhimu wa
elimu ya lishe
M
akala yetu ya wiki hii
inaanza kwa kuainisha
ulazima wa kuitafuta
elimu ya chakula na
lishe bora katika jamii.
Neno lishe linaweza kuelezwa
katika maana tofauti. Kwa muktadha wa makala hizi, neno lishe
linamaanisha jumla ya hatua mbali
mbali kuanzia uchaguzi wa chakula,
maandalizi ya chakula, ulaji wa
chakula na jinsi miili yetu inavyochukua virutubisho na kuvitumia
katika kumpatia mlaji afya bora.
Maana yake ni kwamba lishe
bora hutokana na ulaji unaofaa,
yaani chakula cha kutosha,
chenye mchanganyiko wa virutubisho vyote katika uwiano
unaotakiwa.
Kwa upande mwingine,
utapiamlo au lishe duni ni hali
mbaya ya lishe inayosababishwa na mambo mbalimbali ikiwa
ni pamoja na ulaji usiofaa. Utapiamlo unaweza kusababishwa na
kula mlo ulio
na virutubisho
vichache au
vingi kulingana na
mahitaji.
Kula
mlowenye
virutu-

Inatoka uk 3 ya Marekani na wa-

shirika wake sababu ni ugaidi. Ushetanishaji (demonization) wa Uislamu


ni jaribio la propaganda la kupaka
matope mafundisho ya Uislamu kwa
rangi mbaya kiasi kwamba watu watakuwa tayari kwenda vitani-kuua- ili
kuungamiza Uislamu.
Kwa juhudi hizi za vyombo vya
habari kushetanisha Uislamu na
Waislamu, vyombo vya dola vitaua
Waislamu na hakuna kitakachotokea
maana watakaokuwa wameuawa ni
magaidi. Watanzania watakuwa
washaandaliwa kuamini kwamba
miongoni mwao kuna adui ambaye si
mwingine bali Muislamu.
Kiitwacho vita dhidi ya ugaidi ni
mkakati mkubwa wa kimataifa kutengeneza mazingira ya vita kuu ya tatu ya
dunia. Vita hii inaandaliwa iwe kati ya
majeshi ya Marekani na washirika
wake dhidi ya majeshi ya Waislamu
kwa upande mwingine na inawezekana China na Urusi wakawa kundi moja
na Waislamu si kwa sababu za kiimani
bali kwa kuwa kwao dhidi ya sera za
wamagharibi.
Kila ukisikia matukio ya kigaidi,
kaa chonjo kwani watengeneza migogoro na vita watakuwa wako kazini.
Ni vijana wangapi walipewa mafunzo
na hao hao wapika majungu dhidi ya
Uislamu na wakaenda vitani kuuwa

bisho vichache visivyokidhi mahitaji


huleta upungufu mlo, wakati mlo
wenye virutubisho vilivyozidi mahitaji huleta kiribatumbo. Vilevile aina
mbalimbali za madini na vitamini
zikizidi mwilini huleta madhara.
Watu wengi wanajitahidi kutafuta elimu ya mambo mbalimbali
kama vile kuendesha
gari,
kutumia simu
n
a
kompyuta, kutum i a
mbolea
a u k u ny unyizia
dawa mimea shambani.
La-

kini, watu hao hao wengi wao hawajishugulishi kabisa kupata elimu ya
chakula na lishe ambayo itawasaidia
kujua ni aina gani ya chakula wale,
na kuna uhusiano gani baina ya
chakula wanachokula kila siku na
kuimarika au kuharibika kwa afya
zao.
Zaidi ya hayo, ni kwa namna gani
ulaji mbaya unasababisha upungufu
wa nguvu za kiume au upungufu wa
nguvu za kike. Ni imani yetu kuwa
wasomaji wa makala hizi za chakula
na lishe wataongeza ari na kasi yao
katika kujifunza elimu ya chakula
na lishe ili iwasaidie kuzikabili
changamoto za ulimwengu wa sasa
katika maswala ya chakula na lishe.
Miaka ya nyuma, hasa katika
bara la Afrika watu walikuwa wanatumia kwa kiasi kikubwa vyakula
vya asili kutoka shambani. Zama
hizi, hasa baada ya maingiliano na
nchi zilizoendelea, watu wengi hasa
katika miji wanakula vyakula vilivyosindikwa katika viwanda.
Usindikaji wa vyakula katika
zama za sasa unajulikama kama
dhambi
isiyoepukika
(necessary evil).
H i i
ni kwa

Ugaidi Tanzania
na kuuawa kwa jina la Jihad feki?
Wakati wowote ule usikiapo magaidi Waislamu wanatajwa katika vyombo vya habari, basi zingatia sana
yafuatayo; Mosi, Huo ni ushetanishaji
wa Uislamu na Waislamu ambao haupaswi kuruhusiwa uendelee hata kidogo kwani madhara yake, kama alivyosema Meya Livingston, ni hatari
kwa mahusiano ya jamii.
Makundi mengi ya kigaidi yamekuja kudhihirika kuwa yaliandaliwa
kimafunzo, silaha na fedha na hao hao
mabwana wa vita dhidi ya ugaidi. Je,
wajua kuwa kirefu halisi cha kundi la
ISIS ni Israel Security Inteligence Services? Yaani Idara ya Huduma za Kijasusi ya Israel? Tafsiri inayotolewa ya
ISIS ni Islamic State in Iraq and Syria
ina lengo la kuchafua fikra ya kweli ya
Islamic State ili watu waogope dola
yoyote ile ya Kiislamu.
Bernard Lewis, muasisi wa
Fourth-Generation Warfare alipata
kusema: Hatuhitaji majeshi kutoka
bara moja kwenda jingine ambayo
yataamsha hisia za uzalendo na kurejea kwetu kama maiti kama ilivyotokea

Afghanistan na Vietnam, lakini tunapaswa kutafuta mawakala ndani ya


nchi shabaha watakaofanya kazi ya
wanajeshi (wetu), na tunahitaji vyombo vya habari kupotosha ukweli kwa
watu na pesa za kuwagharamia
(mawakala) Kwa hiyo kwa mujibu
wa Bernard Lewis, vyombo vya habari
ni sehemu muhimu sana ya vita dhidi
ya ugaidi ambayo kikweli ni vita dhidi
ya Uislamu na ni vita kwa ajili ya kudhibiti mafuta ya mashariki ya kati na
kusimika mfumo mpya wa ulimwengu (New World Order).
Pili, kama kuna magaidi Waislamu
wasiotokana na wamagharibi, ambao
ni sehemu ndogo kabisa ya umma wa
Waislamu. Hao hawawakilishi mamia
ya mamilioni ya Waislamu na watakuwa na sababu ya kwa nini wanapigana. Waislamu wanajua jinsi ya kuishi na wasio Waislamu kwa amani
kama Mtume Muhammad (rehma na
amani ziwe juu yake) na maswahaba
walivyofanya.
Na daima kumbuka kwamba ugadi
hauna dini wala kabila wala rangi.
Kuna magaidi wengi tu Wakristo,

sababu, dunia ina idadi kubwa ya


watu ambao kuwalisha kwa kutumia njia za asili ni jambo lisilowezekana. Ndio maana leo tuna
kuku wa kisasa, machungwa ya
kisasa, n.k. Fikiria nchi kama Tanzania ambayo kwa sasa idadi ya wananchi wake wanakaribia milioni
50. Ifikapo mwaka 2050 idadi inakisiwa kufikia milioni 88. Bila ya kuwepo vyakula vya kusindika maisha
yatakuwa magumu hasa katika miji.
Hata hivyo, vyakula vilivyosindikwa vina changamoto zake,
hasa chumvi, sukari, mafuta na
kemikali nyingi zinazowekwa ili kuvifanya vyakula hivyo visiharibike
katika muda mfupi.
Kwa hiyo, kuwa na elimu ya kutosha juu ya chakula na lishe kutatusaidia kupunguza athari mbaya
inayoletwa na ulaji wa vyakula
vilivyosindikwa.
Kwa hakika, katika zama zetu
hizi mada muhimu ya kuzungumzwa kwa njia mbalimbali na sehemu tofauti ni elimu ya chakula na
lishe. Kuongezeka kwa matumizi ya
vyakula vilivyosindikwa viwandani
kunakwenda sambamba na
kuongezeka kwa magonjwa ya kisasa yanayotokana na ulaji mbaya
kama vile unene na uzito kupita kiasi kwa watoto na watu
wazi-

Wayahudi, Wahindu na kadhalika.


Nchini Ireland ya Kaskazini, Wakristo
wa Kikatoliki na Waanglikana waliuana kwa miongo kadhaa hadi walipopatana. Jerry Adam na IRA yake walikuwa magaidi.
Aprili 19 mwaka 2001 Timothy
Mcveigh raia wa Marekani, mkrito alilipua jengo la serikali huko Oklahoma
na kuawa watu 168 wengi wao watoto
wa shule. Hakuitwa gaidi mkristo.
Walioua maelfu ya watu kwa bomu
la atomiki huko Hiroshima ni Waislamu? Walioanzisha vita vya kwanza na
pili vya dunia vilivyoua mamilioni ya
watu ni Waislamu? Walioanzisha vita
vya Vietnam na kuua mamilioni ya
watu ni Waislamu? Walioua Waislamu huko Bosnia na Kosovo ni Waislamu? Waliofanya mauaji ya kimbari
Rwanda ni Waislamu? Wote hawa ni
magaidi kwa tafsiri yao wenyewe ya
ugaidi.
Tatu, vyombo vya habari vinauza
khofu. Vinajaribu kutengeneza adui
wa kubuni (Bogeyman) na huyo si
mwingine bali Muislamu. Vinafanya
hivyo ili wewe uweze kumuogopa au
kumchukia Muislamu.
Katika nchi nyingi za kiafrika, wapigania uhuru walikuwa magaidi. Baada ya shambulizi la Septemba 11 huko
marekani hivi sasa magaidi ni Waislamu. Vyombo vya habari viko katika

ma, shinikizo la juu la damu, kisukari, ugonjwa wa moyo, saratani,


upungufu wa nguvu za kiume na
kike, n.k.
Pia, kutokana na matangazo ya
biashara katika vyombo vya habari
juu ya vyakula yanawafanya watu
wengi kuingia katika hatari ya ulaji
mbaya.
Njia moja madhubuti ya kuikabili changamoto hiyo ni kuwa na
elimu ya kutosha juu ya chakula na
lishe. Elimu hii itamsaidia mtu kufanya uchaguzi wa chakula bora na
kupika vyakula hivyo kwa njia za
salama kiafya. Katika nchi nyingi
duniani na hapa Tanzania, wataalamu wa chakula na lishe wanashauri
elimu ya chakula na lishe iwekwe
katika mitaala kuanzia elimu ya
msingi.
Utafiti mbalimbali unaonesha
kuwa mtoto akijifunza elimu ya
chakula na lishe katika umri mdogo,
ataendelea kuwa na hiyo athari katika umri mkubwa. Kwa kukosa
mwongozo wa namna bora ya ulaji,
watoto wataangukia katika ulaji
mbaya unaopelekea unene na uzito
kupita kiasi hali ya kuwa wanaumri
mdogo.
Unene na uzito kupita kiasi sio tu
unaathiri afya, bali pia unaleta
msongo wa mawazo (emotional
stress) kwa watoto. Shule zikiwa na
programu ya kuelimisha ulaji bora zinaweza
kuokoa afya ya
watoto hasa
unene na kiribatumbo.
0754
654900

utumishi wa watawala wa dunia. Kwa


hiyo usikurupuke kuamini kila kinachoandikwa kuhusu ugaidi hususan
ugaidi unapohusishwa na Waislamu.
Umefika wakati wahariri wa vyombo vya habari wabadilike na kuandika habari za ukweli kuhusu matukio.
Kuendeleza propaganda ya wamagharibi kwamba Waislamu ni hatari
kwa usalama wa nchi na ni kuielekeza
nchi katika chuki na uhasama wa kimakundi jambo ambalo litakapofikia
kuzaa matunda hakuna atakayesalimika.
Mwandishi mmoja wa gazeti la
wiki nchini anaonya juu ya mwenendo
huu wa vyombo vya habari kuandika
habari za kuchombeza ugaidi akisema: Kwa namna vyombo vya habari
vya nchi yetu vinavyozidi kuripoti juu
ya hofu hizi za kufikirika, lakini si za
uhalisia, basi, vyombo vyetu vya habari
kimsingi vinashiriki kikamilifu kuitangaza Al Shabaab na hata kuisaidia
kupata wafuasi miongoni mwa baadhi
ya vijana wa Kitanzania wasiojitambua na walio kwenye umasikini
mkubwa unaochangiwa pia na kukosa
ajira.
Ni vema vyombo vya habari vya
Tanzania vikazikumbuka nasaha hizi
kikamilifu ili visije kuwa vimeshiriki
kuitumbukiza nchi katika lindi la ugaidi wa kweli.

1 Rajab 1436, jumatatu Aprili 20 - 27 , 2015

13

www.islamicftz.org

fat-wa kwa mwanamke wa kiislam


Na sheikh Shabani Mussa

Kwa nini fatwa kwa mwanamke wa Kiislamu?


Awali ya yote, Allah anasema:
Nasi hatukuwapeleka (kuwa Mitume) kabla yako isipokuwa wanaume ambao tuliwafunulia Wahyi.
Basi waulizeni wenye kumbukumbu
(za vitabu vya Allah) ikiwa nyinyi
hamjui) [An Nahli aya ya: 43]
Kama tunavyofahamu hivi sasa
kumejitokeza mambo mengi ya kimaendeleo, na kuna mambo kadhaa
ya kisharia yanayohitaji fatwa na
ufafanuzi wa kisharia. Na hapo ndipo tunapohitaji kupata mitazamo ya
kielimu ya wanazuoni wetu (Allah
awahifadhi) kwa kudhihirisha uwepo wao katika jamii na kutoa fatwa
za kielimu zitakazoutoa umma katika matatizo na kumkwamua mwanamke wa Kiislamu na mitanziko
inayomkabili.
Imeelezwa kuwa,Mama ni chuo
ukimuandaa. Kwa kulizingatia hili,
gazeti lako la Imaan limetenga ukurasa huu wa kukupatia fatwa za wanazuoni waliobobea wa zama hizi
zitakazomhusu zaidi mwanamke
wa Kiislamu kivitendo kuliko nadharia. Kadhalika, Mtume (Rehma
na amani ya Allah iwe juu yake), alitenga muda maalum wa kuwafundisha wanawake sharia
mbalimbali za dini ya Kiislamu, kuwalingania na kuwajuza hukumu za
kisharia zinazowahusu. Wake zake
pia walishiriki katika kazi hii adhimu
ya kuwafundisha wanawake wenzao
masuala nyeti yahusuyo dini yao.
Kwa kuzingatia hilo, gazeti la Imaan linakupa fursa mwanamke kujielimisha mambo mbalimbali yahusuyo dini yako kama ilivyokuwa
katika zama za Mtume (Rehma na
amani ya Allah iwe juu yake).
Na hizi ni juhudi za kibinadamu,
na haziwezi kusalimika na makosa.
Jukumu na kazi yetu ni kufasiri na
kuyaratibu maneno ya wanazuoni.
Endapo ndugu msomaji utakuwa
na pendekezo au jambo linalohitaji
uzindushi na ufafanuzi usisite kututanabahisha na hilo ndilo tunalolihitaji. Mada ya leo katika fatwa kwa
mwanamke wa Kiislamu inahusu

vinavyozuwia udhu.
Vinavyozuwia udhu:
Hukumu ya udhu wa mwanamke aliyepaka rangi ya kucha.
Swali: Aliulizwa Sheikh Muhamad bin Swaleh Uthaimini Allah
amrehemu: Ni ipi hukumu ya udhu
wa mwanamke aliyepaka rangi ya
kucha?
Jawabu: Haifai kwa mwanamke anayeswali kupaka rangi za kucha
kwani rangi za kucha zinazuwia
maji kufika kwenye kiungo kinachooshwa na kila kinachozuwia
maji kufika kwenye kiungo hakifai
kutumiwa na mtu anayetawadha au
kujitwaharisha. Allah anasema:
Osheni nyuso zenu na mikono

yenu... (5: 6). Iwapo mwanamke


ana rangi juu ya kucha zake, bila
shaka itazuia maji kufika kwenye
kiungo na hatuwezi kusema kuwa
ameosha mkono wake bali itakuwa
ameacha faradhi kati ya faradhi za
udhu au josho.
Na kwa mwanamke asiyeswali,
kwa sababu ya hedhi mathalan,
Yeye hakatazwi kupaka rangi ya
kucha isipokuwa aweza kukatazwa
kama itakuwa ni kati ya mapambo
mahasusi kwa wanawake wa
kikafiri. Kwa hali hiyo haitofaa
kwani kuna kujifananisha na
makafiri. (Fatawa na Rasailu za
Sheikh Ibn Uthaimin 4/148)
Hukumu ya udhu kwa mtu aliyepaka hina kwenye mikono yake
Swali: Liliulizwa jopo la kudu-

mu la fatwa: Yasemwa kumepokewa riwaya kutoka kwa Mtume


kwamba, Udhu hausihi ikiwa vidoleni kuna rojo lililoganda au rangi au
udongo. Nami huwaona baadhi ya
wanawake wakiwa wamepaka rojo
la hina kwenye miguu yao, na
huswali hivyo, je yafaa? Kwani wanapokatazwa husema hii ni safi.
Jawabu: Kwa tunavyofahamu
hakuna hadith iliyopokewa kwa
tamko hilo. Ama kubaki kwa athari
ya rangi ya hina kwenye miguu na
mikono hakuathiri, kwa sababu
rangi ya hina haina tabaka tofauti na
unga unaonata, udongo na rangi ya
kucha ambavyo huwa na tabaka linalozuwia maji kufika kwenye ngozi. Kwa kuwa kuna tabaka linalozuwia maji kufika kwenye ngozi, udhu

hauwezi kusihi. Hivyo, ni lazima ukwanguliwe mithili ya unga ulionata.


(Fataawa Laj-natud Daimah 5/217)
Hukumu ya udhu bila ya kukwangua rangi ya kucha
Swali: Liliulizwa jopo la kudumu la fat-wa: Tuliwasikia baadhi ya
wanazuoni wanasema: Inajuzu kwa
mwanamke kutawadha bila ya kukwangua rangi ya kucha, ni yapi maoni yenu?
Jawabu: Rangi ya kucha ikiwa
na tabaka (layer) kwenye kucha
hapo hakutakuwa na udhu mpaka
tabaka liondoshwe kwanza kabla ya
kutawadha. Kama rangi haina tabaka, udhu utasihi na hakutakuwa na
tofauti na hina. (Fataawa Laj-natud
Daimah 5/218).

mapitio ya vitabu
Kitabu: Al Fusuul Fii Mustwalahi Hadiithi r-Rasuuli
Mwandishi: Haafidh Thanaau-llwaahi Zaahidy
Mfasiri: Sheikh Muhammad Issa
Mlango wa Pili: Majina ya Matini
za Hadith
Hadith: Ni kile kilichoegemezwa kwa Mtume (Rehma na amani
ziwe juu yake) miongoni mwa kauli,
kitendo au kuridhiya au sifa. Na ama
muradi wa kuridhiya (At-taqriyr) ni
kitendo kilichotendwa au kauli iliyonenwa mbele ya Mtume (Rehma na
amani ziwe juu yake) au akapata
habari zake na asikikataze.
Na muradi wa As-swifah: ni kila
ambacho ni sifa miongoni mwa sifa
za Mtume (Rehma na amani ziwe juu
yake) za kimaumbile kama: Alikuwa

Mtume wa Allah (Rehma na amani


ziwe juu yake) mzuri wa sura kuliko
watu wote na mzuri wa maumbile, si
mrefu sana wala si mfupi (Ameisimulia Muslim kwa nambari 2337).
Na (sifa) za kitabia, kama alivyo
katika hadith ya Anas (Radhi za Allah ziwe juu yake) Alikuwa Mtume
wa Allah (Rehma na amani ziwe juu
yake) mzuri wa tabia kuliko watu
wote (Ameisimulia Muslim kwa
nambari 2310).
Al-Khabaru: Hutamkwa na
kukusudiwa hadith kwa maana ambayo iliyokwisha tajwa (hapo juu), na
vile vile hukusudiwa kwalo maana iliyopana zaidi kuliko hadith miongoni
mwa (vyenye) kuhabarisha.
Al-Atharu: Hutamkwa na
kukusudiwa kwalo hadith za Mtume
(Rehma na amani ziwe juu yake) na

(pia) hukusudiwa chochote ambacho


kimeegemezwa kwa Maswahaba na
Taabiiyna miongoni mwa kauli na
matendo.
As-Sunnah: Kwa wanawazuoni
wa Ilmu ya Hadith na watu wa Usuuli, (Sunnah) ni kila kinachorejea kwa
Mtume (Rehma na amani ziwe juu
yake) miongoni mwa kauli, kitendo
au kukiri (kwake).
Na katika utambuzi wa wanawazuoni wa Fiq-h: As-Sunnah ni Kile
kilichothibiti kutoka kwa Mtume
(Rehma na amani ziwe juu yake) katika hukumu na kisiwe faradh au wajibu. Na katika utambuzi wa wanawazuoni wa mawaidha na uongozi,
As-sunnah ni chochote kile dhidi ya
uzushi (bidaa).
Al-Marfuu: Nayo ni mafungu

mawili: (Al-Marfuu) Swariyhu:


Nayo ni hadith ambayo imeegemezwa kwa Mtume (Rehma na amani
ziwe juu yake) kauli au kitendo au
kukiri wazi wazi.
(Al-Marfuu) Ghayru Swariyhu:
Nayo ni kauli ya swahaba au kitendo
chake ambacho si miongoni mwa
yale yawezayo kuwa ni ya kutamkwa
au kutendwa kutokana na rai au jitihada (ya mtu) kama vile kutoa habari
kuhusu mambo yaliyopita au yatakayokuja. Na vile vile lile ambalo
hupatikanwa kwa kutendwa kwake
thawabu makhsusi au adhabu makhsusi, na huitwa Marfuan Hukman pia.
Al-Mawquufu: Ni hadith iliyoegemezwa kwa swahaba, kauli au
kitendo, sawa sawa sanad (mtiririko
wa wapokezi) yake iwe imeungana au

imekatika.
Al-Maqtuu: Ni kile kilichoegemezwa kwa taabii na waliofuatia
miongoni mwa kauli au kitendo,
sawa sawa sanad yake iwe imeungana
au imekatika.
Muttafaqun Alayhi: Ni hadith
ambayo wamekubaliana kupatikana
kwake (Imam) Bukhari na Muslim
(Rehma za Allah ziwe juu yao) katika
sahihi zao mbili (Sahihi Bukhari na
Sahihu Muslim).
Al-Musnad: Ni hadith Marfuu
ambayo sanad yake imeungana.
Al Hadiythul Qudsiyyu: Ni kila
anachosimulia Mtume (Rehma na
amani ziwe juu yake) kutoka kwa
Mola wake kwa matamshi au maana
na kisichokuwa Quran.
Itaendelea toleo lijalo

1 Rajab 1436, jumatatu Aprili 20 - 27 , 2015

14

www.islamicftz.org

Nyakati za swala
M koa wa M o rogoro, Kale
nda yanyaka
tiza swala

M koa wa M w anza, Kale


nda yanyaka
tiza swala

Apri
l / 15
20

Tar
ehe

Siku

Fajr M w i
sho wa Al
faj
i
r

Apri
l / 2015

Dhuhr

Asr

M aghrib

Zanzi
barSouth Regi
on,Pra
yerTi
m es Schedul
e A
pri
l / 2015

I
sha

Date

Day

Fajr

Sunri
se

Dhuhr

Asr

M aghrib

I
sha

13

M on

5:
25

6:
34

12:
33

3:
53

6:
31

7:37

13

M on

5:
39

6:48

12:
50

4:07

6:
52

7:57

13

M on

5:14

6:
23

12:
23

3:42

6:
23

7:28

14

Tue

5:
25

6:
34

12:
33

3:
53

6:
31

7:37

14

Tue

5:
39

6:48

12:
50

4:07

6:
52

7:57

14

Tue

5:14

6:
23

12:
23

3:42

6:
23

7:28

15

W ed

5:
25

6:
34

12:
33

3:
53

6:
30

7:37

15

W ed

5:
38

6:47

12:
50

4:07

6:
51

7:57

15

W ed

5:14

6:
23

12:
23

3:42

6:
22

7:28

Thu

5:
38

6:47

12:49

4:07

6:
51

7:57

16

Thu

5:14

6:
23

12:
23

3:42

6:
21

7:27

Tar
ehe

Siku Fajr M w i
sho wa Al
faj
i
r

Dhuhr

Asr

M aghrib

I
sha

16

Thu

5:
25

6:
34

12:
32

3:
53

6:
30

7:36

16

17

Fr
i

5:
24

6:
34

12:
32

3:
52

6:
30

7:36

17

Fr
i

5:
38

6:47

12:49

4:07

6:
50

7:56

17

Fr
i

5:13

6:
23

12:
22

3:42

6:
21

7:27

18

Sat

5:
24

6:
34

12:
32

3:
52

6:
29

7:35

18

Sat

5:
38

6:47

12:49

4:07

6:
50

7:56

18

Sat

5:13

6:
22

12:
22

3:42

6:
21

7:27

19

Sun

5:
24

6:
34

12:
32

3:
52

6:
29

7:35

19

Sun

5:
37

6:47

12:49

4:07

6:
50

7:56

19

Sun

5:13

6:
22

12:
22

3:42

6:
20

7:26

M koa wa Tanga ,Kal


enda ya
nyak
atiza swala

Tar
ehe

Siku

FajrM w i
sho wa Al
faj
i
r

Apri
l / 2015

Zanzi
barNorth Regi
on,PrayerTi
m es Schedul
e A
pri
l / 2015

M koa wa M beya, Kale


nda yanyakatiza swala

Apri
l / 2015

Dhuhr

Asr

M aghrib

I
sha

Date

Day

Fajr

Sunri
se

Dhuhr

Asr

M aghrib

I
sha

Tar
ehe

Siku

Fajr M w i
sho wa Al
faj
i
r

Dhuhr

Asr

M on

5:14

6:
23

12:
24

3:43

6:
23

7:29

13

M on

5:41 6:
50

12:49

4:09 6:47

7:53

M aghrib

I
sha

13

M on

5:18

6:
27

12:
28

3:46

6:
28

7:34

13

14

Tue

5:18

6:
27

12:
28

3:46

6:
28

7:34

14

Tue

5:14

6:
23

12:
24

3:43

6:
23

7:29

14

Tue

5:41 6:
50

12:49

4:09 6:47

7:53

15

W ed

5:18

6:
27

12:
28

3:46

6:
28

7:33

15

W ed

5:14

6:
23

12:
23

3:43

6:
23

7:28

15

W ed

5:41 6:
50

12:49

4:09 6:46

7:52

16

Thu

5:18

6:
27

12:
27

3:46

6:
27

7:33

16

Thu

5:14

6:
23

12:
23

3:42

6:
22

7:28

16

Thu

5:41 6:
50

12:48

4:09 6:46

7:52

17

Fr
i

5:18

6:
26

12:
27

3:46

6:
27

7:33

17

Fr
i

5:14

6:
23

12:
23

3:42

6:
22

7:28

17

Fr
i

5:41 6:
50

12:48

4:09 6:45

7:51

18

Sat

5:17

6:
26

12:
27

3:46

6:
26

7:32

18

Sat

5:14

6:
23

12:
23

3:42

6:
21

7:27

18

Sat

5:41 6:
50

12:48

4:08 6:45

7:51

19

Sun

5:17

6:
26

12:
27

3:46

6:
26

7:32

19

Sun

5:13

6:
23

12:
22

3:42

6:
21

7:27

19

Sun

5:41 6:
50

12:48

4:08 6:44

7:51

M koa wa Ki
gom a ,Kal
enda ya
nyakatiza swala

Tar
ehe

Siku

Fajr

M wi
sho wa Al
faj
i
r

M koa wa Dar s
e Salaa
m

Apri
l / 2015

Dhuhr

Asr

M aghrib

I
sha

Tar
ehe

Siku

Fajr

,
Kal
enda ya nyak
atiza swala

M wi
sho wa Al
faj
i
r

Dhuhr

M koa wa Arusha , Kale


nda yanyakatiza swala

Apri
l / 2015

Asr

M aghrib

Apri
l / 2015

I
sha

Date

Day

Fajr

Sunri
se

Dhuhr

Asr

M aghrib

I
sha

M on

5:
26

6:
35

12:
37

3:
54

6:
39

7:44

13

M on

5:
51

7:00

1:01

4:19

7:01

8:
07

13

M on

5:15

6:
24

12:
24

3:43

6:
23

7:29

13

14

Tue

5:
51

7:00

1:01

4:19

7:01

8:
07

14

Tue

5:15

6:
24

12:
24

3:43

6:
23

7:29

14

Tue

5:
26

6:
35

12:
37

3:
54

6:
39

7:44

15

W ed

5:
51

7:00

1:01

4:19

7:00

8:
06

15

W ed

5:15

6:
24

12:
24

3:43

6:
22

7:28

15

W ed

5:
26

6:
34

12:
37

3:
54

6:
38

7:44

16

Thu

5:
51

7:00

1:00

4:19

7:00

8:
06

16

Thu

5:15

6:
24

12:
23

3:43

6:
22

7:28

16

Thu

5:
25

6:
34

12:
36

3:
54

6:
38

7:43

17

Fr
i

5:
51

6:
59

1:00

4:19

7:00

8:
06

Fr
i

5:
25

6:
34

12:
36

3:
54

6:
37

7:43

18

Sat

5:
50

6:
59

1:00

4:19

6:
59

8:
05

19

Sun

5:
50

6:
59

1:00

4:19

6:
59

8:
05

17

Fr
i

5:15

6:
24

12:
23

3:43

6:
21

7:28

17

18

Sat

5:15

6:
24

12:
23

3:43

6:
21

7:27

18

Sat

5:
25

6:
34

12:
36

3:
54

6:
37

7:43

19

Sun

5:14

6:
24

12:
23

3:43

6:
21

7:27

19

Sun

5:
25

6:
34

12:
36

3:
54

6:
37

7:43

mila na desturi
Na mwandishi wetu

Kamari ni kazi ya shetani


I
mekuwa ni kawaida kila inapofika mwisho wa wiki kukutana
na watoto, vijana na hata watu
wazima wakiwa wamejikusanya
vijiweni, mikononi wameshika peni
na karatasi ili kupiga pesa kupitia
shughuli yao ambayo kimsingi ni haramu na haimpendezi Allah
Subhaanahu Wataala.
Si daktari, si mwalimu, si mwanafunzi na hana majukumu katika
ofisi yoyote, lakini utamkuta mtu
ameninginiza peni juu ya mfuko wa
shati lake na karatasi mkononi.
Peni na karatasi hizo zinafanya
kazi moja: kubeti. Neno kubeti
limetokana na neno la kiingereza betting lenye maana ya ubashiri au
kamari. Hawa wanabashiri matokeo
ya mechi za michezo ya mpira wa
mguu, ngumi, mbio za farasi na michezo mingineyo.
Katika kituo husika, mbashiri hupewa karatasi yenye ratiba kamili za
mechi za kila timu (wengine wana-

bandika ubaoni). Mara nyingi timu


yenye uwezo zaidi ya mpinzani wake
huwa na pointi chache.
Pointi hizo ndizo zinazomjulisha
mtu huyo anaebashiri ni timu gani
akiibashiria itampa fedha nyingi zaidi. Baada ya hapo, mbashiri huchagua timu anazozihitaji kuzitabiria, kisha kumpa mhudumu wa kituo na
kutolewa tiketi iliyochapwa. Karatasi
hiyo ni maarufu kwa jina la mkeka.
Mchezo huo haramu, ulioenea na
unaozidi kusambaa kwa kasi unachagizwa na utitiri wa vituo na makampuni mbalimbali ya kamari karibu
kila kona na mitaa ya jiji la Dar es salaam na nchi nzima kwa ujumla.
Yapo mambo mengi yanayosukuma watu kuingia kwenye mchezo huu
mchafu ikwemo ushawishi wa marafiki wabaya na tamaa ya kujipatia
fedha nyingi kwa urahisi na muda
mfupi kiasi (dakika 90) tena kwa
uwekezaji mdogo wa mtaji unaoanzia
shilingi mia tano!

Kibaya zaidi hata watoto


wengi wameingia kwenye
kamari, ingawa majengo ya
kamari yameandikwa mtu
chini ya miaka 18 haruhusiwi
kuingia. Katazo hilo halizuii
watoto kucheza kamari ambapo hutumia ujanja wa kutuma wakubwa kuwanunulia mkeka.
Ndiyo maana
mwanzoni mwa
makala haya
nilieleza watoto,
vijana na watu
wazima hushirikiana katika mchezo
huu.
Mmoja wa watoto aliyeathirika na
kamari (jina tunalihifadhi) ni mwanafunzi wa darasa la saba katika moja
ya shule za hapa jijini Dar es salaam.
Mtoto huyo anasema alianza kamari
tangu mwaka jana na amekuwa akili-

Mchezo huo haramu, ulioenea na unaozidi


kusambaa kwa kasi unachagizwa na utitiri
wa vituo na makampuni mbalimbali ya
kamari karibu kila kona nchi nzima

wa
fedha
nying i . C h a ajabu zaidi hajawahi
kushinda hata shilingi elfu mbili!
Mtoto huyo anasema hatoacha
kucheza akiamini siku moja atapata
fedha nyingi.
Kiukweli hadi ushinde fedha nyingi ni kazi ngumu. Tangu nipo la sita
hadi leo bado sijaambulia chochote
ila ipo siku tu ntapiga pesa nyingi na
hapo ndio ntaacha kubeti, anasema.
Kizazi hiki kinachopotea ilhali tu-

nakiona kinahitaji ukombozi.


He b u fi k i r i a ,
kwanza ni mtoto
mdogo, pili
amecheza
kamari mwaka
mzima na tatu
anaahidi
hatoacha kamari
hadi ashinde fedha nyingi kufikia
kiasi alizowekeza. Kijana
huyu ndie
anayetegemewa kuwa taifa
la kesho.
Ukiacha watoto, vijana ni kundi
jingine lililoathirika
sana na kamari.
Miongoni mwao
wameacha kazi na hushinda kwenye
kumbi za kamari wakitegemea malipo yatokanayo na mchezo huu haramu.
Ni wakati muafaka kwa jamii kuamka na kupinga mchezo huu haramu
unaoathiri si tu watoto na vijana wa
wa kiislamu, bali hata wasiokuwa
Waislamu. Inashangaza zaidi kuona
baadhi ya Waislamu wanaswali
khamsa swalawat lakini wanacheza
kamari.
Shime Waislamu na watanzania
kwa ujumla, kuanzia wazazi majumbani, viongozi wa dini, waandishi wa
habari tuungane kuondoa janga hili.

1 Rajab 1436, jumatatu Aprili 20 - 27 , 2015

watoto / tangazo

www.islamicftz.org

15

kona ya watoto
NA NAHIDA ISMAIL
Unajua nini kuhusu nyangumi?
Nyangumi sio samaki bali
ni mnyama jamii ya mamalia
wakubwa.
Nyangumi wanapumua kupitia
mashavu yanayopitisha hewa
mpaka katika mapafu.
Nyangumi wana damu ya joto.
Nyangumi wa rangi ya bluu ni
nyangumi mkubwa zaidi akiwa na
urefu wa wastani wa futi 94 (mita
29) - karibu sawa na kimo cha
jengo la ghorofa tisa.
Wanyama hawa wakubwa wanakula kamba wadogo (krill).

Je umewahi kusikia kuhusu


kisa cha Nabii Yunus na
nyangumi?

Nabii Yunus (Amani iwe


juu yake) alitumwa na Allah
Subhaanahu Wataala kuwakumbusha watu kuhusu ujumbe wa
kweli: Kumuabudu YEYE, ALLAH
pekee na wafanye mambo mema
na kuwaonya na adhabu kali,
iwapo watafanya vinginevyo.
Hata hivyo, watu hawakutaka
kumsikiliza Nabii Yunus (Amani iwe juu yake) na walifanya
mambo mengi ambayo Allah
Subhaanahu Wataala ameyakataza.
Yunus alipoteza subira kutokana na matendo ya watu na
kuamua kuondoka kwa hasira.
Alipanda meli ili kuvuka bahari.
Lakini akiwa katikati ya bahari,
alitupwa baharini na kumezwa
na nyangumi mkubwa. Ndio!
Alimezwa mara moja, mzima
mzima, na kujikuta tumboni mwa
nyangumi!
Nabii Yunus akatua ndani ya
tumbo la nyangumi ambako
kulikuwa na giza kali. Nabii Yunus

(Amani iwe juu yake) aliogopa


sana. Akapata muda wa kufikiria
juu ya nini kilichotokea.
Alifikiria kwa nini aliondoka katika mji wake, kwa nini alitupwa
baharini na kwa nini alibaki kuwa
hai ndani ya tumbo la nyangumi.
Nabii Yunus aligundua kuwa
alikosea kuwaacha watu.
Alipaswa kuwa mvumilivu na
kuendeleza wito wake kwa watu
kumrudia Muumba wao, Allah
Subhaanahu Wataala.

Nyangumi alielewa kuwa


alimmeza Mtume wa Mwenyezi
Mungu. Nyangumi alikuwa pia
akitii amri ya Mwenyezi Mungu
Mtukufu.
Nabii Yunus alimuomba Allah
msamaha. Aliomba kwa moyo
wake wote na kusema: Oh Allah,
hakuna Mungu isipokuwa Wewe.
Ni Wewe pekee nakutukuza.
Nimekosea. Kama hutanisaidia,
nitapotea milele.
Allah alisikai dua ya Nabii

Yunus (Amani iwe juu yake) na


kumsamehe. Allah akamuamuru
nyangumi amteme Yunus (Amani
iwe juu yake) na akatoka kutoka
katika tumbo la nyangumi akiwa
hai na alimshukuru Allah. Yunus
(Amani iwe juu yake) alirudi
kwa watu na kuendelea kuwaita
katika njia ya uongofu.

Mambo tunayojifunza:

Tuwe na subira na uvumilivu.

Ukigundua kuwa umefanya


kosa rudi kwa Allah na utubu.
Nasi pia tusome dua ya
Nabii Yunus (Amani iwe juu yake)
- Laa ilaha illa anta subhaanaka,
inni kuntu min adh-dhalimeen
(Hapana mungu isipo kuwa
Wewe Subhanaka Uliye takasika.
Hakika mimi nilikuwa miongoni
mwa wenye kudhulumu).
Ni muhimu tuendelee kuwaita watu katika uongofu.
Dua zina nguvu kubwa.

Mwanza

105MHz

Arusha

90.8 MHz

Kigoma

92.5 MHz

Tabora

101.6 MHz
Morogoro

96.3 MHz

Mbeya

90.3 MHz
Ruvuma

Masafa ya Imaan FM

94.2MHz

Mtwara

90.9MHz

Vita ya Yemen
ni mkakati wa
Iran kueneza
ushia

Uk 10
1 Rajab 1436, jumatatu Aprili 20 - 27 , 2015

JAI inavyohuisha tabia za Kiislamu

Wanajumuiya ya Akhlaaqul Islamiya (JAI),


wakiwa hospitali ya Tumbi, Kibaha, hivi
karibuni, katika moja ya harakati zao.

Yajipanga kujenga hospitali ya Wanawake


Na Khalid omary

apa nchini zipo jumuiya


na taasisi nyingi ambazo
zinaihudumia jamii bila
kujali tofauti ya dini wala
kabila. Moja kati ya jumuiya hizo ni
Jumuiya ya Tabia za Kiislamu (JAI)
au kama inavyotambulika,Jamiya
tul Akhlakul Islamiy iliyoasisiwa miaka saba iliyopita.
Yafuatayo ni mahojiano kati ya
gazeti hili na Amir wa jumuiya hiyo,
Sheikh Yahya Masau kuhusiana na
maendeleo ya taasisi hiyo tangu ilipoanzishwa.
Imaan: Tueleze historia ya taasisi
yenu kwa ufupi.
Masau: Jumuiya ya tabia za Kiislamu ilianzishwa mwaka 2008 na
watu saba huko Mwananyamala katika msikiti wa Taqwa. Tulianza shughuli zetu kwa kutembelea na kufariji wagonjwa hospitali ya Mwananyamala.
Baadae tukahamasisha misikiti
mingine ya Mwananyamala kuungana na sisi katika ibada hii, kabla ya
kupanua shughuli hizi mkoa mzima
wa Dar es Salaam. Kwa sasa kazi yetu
imepokelewa na inatekelezwa

takriban nchi nzima.


Imaan: Nini malengo na shughuli kuu za taasisi kwa sasa?
Masau: Lengo letu kuu ni kuulingania Uislamu kwa kuonesha kwa
vitendo tabia nzuri za Kiislamu katika jamii yetu. Kwa kufanya hivi tunaimarisha imaan za Waislamu na
kuwavuta katika Uislamu wasio
Waislamu.
Shughuli zetu ni pamoja na kusaidia wagonjwa ambao hawana
ndugu, ikiwemo wanaofikishwa
hospitalini na polisi pasina ndugu
zao kuwa na taarifa. Pia tunawatolea
damu wagonjwa, tunapokea na
kulea watoto wachanga wanaotupwa, ambapo huko nyuma wamekuwa wakipelekwa kwenye taasisi za
dini nyingine.
Kadhalika, tunasaidia kuwarejesha majumbani kwao baada ya
kupata matibabu na kuruhusiwa
wagonjwa walioharibikiwa na wasiokuwa na nauli, tunawaombea dua
wagonjwa, tunawasafisha (kuwaogesha) na kusafisha mazingira ya
hospitali.
Pia tunanunua madawa, kuwalipia gharama za vipimo wagonjwa
wasio na uwezo na kukarabati au ku-

Wizara ya Afya yawatunuku cheti

nunua vifaa mbalimbali vinavyokosekana hospitalini.


Imaan: Je mna matawi na kama
yapo mangapi?
M a s a u : Tu n a m s h u k u r u
Mwenyezi Mungu takriban kuanzia
miaka minne hadi mitano iliyopita
maeneo mengine ya nchi yetu
wameweza kuipokea kazi hii. Kwa
sasa,tuna matawi katika mikoa 21.
Mkoa wa mwisho kuufikishia kazi
hii ni Mwanza na Shinyanga. Tuna
vituo vya kazi 32 nchi nzima. Kwa
Dar es salaam vituo vyetu vya kazi ni
hospitali za Mwananyamala,
Muhimbili, Ocean Road, Temeke na
Amana.
Imaan: Bila shaka kufanya shughuli hizi mnahitaji fedha. Nani anafadhili shughuli zenu?
Masau: Kwa kweli wafadhili
namba moja ni sisi wenyewe, tunaliendeleza jambo hili kwa hali na
mali. Ukiacha sisi, misikiti inatuunga
mkono kwa kiasi kikubwa. Wadau
wetu wengi wanapatikana misikitini. Kadhalika, baadhi ya makampuni na wafanyabiashara wanatuchangia ili kuongeza baraka
kwenye biashara zao. Hivi ndivyo tunavyojiendesha.

Imaan: Kwa siku mnahudumia


wastani wa wagonjwa wangapi?
Masau: Hatuna idadi maalum
ya wagonjwa tunaowahudumia,
idadi hubadilika kutegemeana na
siku, hata hivyo hawapungui wagonjwa watano katika kila kituo. Na
kwa Dar es salaam wahitaji ni wengi
zaidi kuliko mikoani. Kadhalika kila
siku kuna tofauti ya aina ya uhitaji
ikiwemo watu wa kusafirishwa,
madawa, kulipia vipimo na kujitolea
damu. Na kwa upande wa ratiba
yetu ya utoaji wa huduma, tunatoa
huduma kila siku kama wagonjwa
wanavyougua kila siku.
Imaan: Ni changamoto zipi
mnakutana nazo katika utendaji
wenu kwa ujumla?
Masau: Changamoto zipo.
Wakati tunaanza watu wengi
hawakutuelewa tuna malengo gani.
Kwa sasa, tunashukuru tumeeleweka. Changamoto kubwa kwa sasa ni
kipato. Mara nyingi mahitaji ya wagonjwa huwa makubwa kuliko uwezo
wetu.
Pia ipo changamoto ya usafiri
kwa baadhi ya maeneo zilipo hospitali, hususan Ocean Road ambako ni
mbali na maeneo ya makazi ya watu.

Kwa upande wa ushirikiano na wauguzi, madaktari na wadau wa kiserikali, tunapata ushirikiano mzuri,
kwani tumefuata taratibu za kisheria
na tunatambulika kwa Mkurugenzi
wa Manispaa na waganga wakuu wa
hospitali zote. Taasisi yetu imesajiliwa Serikalini.
Imaan: Kama akipatikana mfadhili mngehitaji nini kuwaongezea
nguvu ya kufanya shughuli hii?
Masau: Kwa sasa, hewa ya oxygen inayomsaidia mgonjwa kupumua ni tatizo kubwa. Madawa yamekuwa ghali. Wangejitokeza wafadhili
tungewaonesha aina ya dawa zinazohitajika.
Imaan: Kuna mambo yoyote ya
kujivunia yanayotokana na kazi
yenu?
M a s a u : Tunamshukuru
Mwenyenzi Mungu hii ni moja kati
ya jumuiya zinazoongoza kusaidia
wagonjwa. Tumekuwa tukiongoza
katika zoezi la kutoa damu mpaka
kutunukiwa cheti cha damu salama
kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii. Cheti tulitunukiwa na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Dr.
Hussein Mwinyi.
Kwa upande wa Jumuiya, tuna
msikiti mmoja uliopo maramba
mawili, shamba la hekari nne huko
Bagamoyo na lingine la hekari tatu
Chamazi. Pia viwanja viwili vilivyopo
Kigamboni na Kibaha.
Imaan: Ni yepi malengo yenu katika kutanua shughuli za taasisi siku
zijazo?
Masau: Kilio cha Waislamu kwa
sasa, pamoja na mambo mengine, ni
kukosa hospitali zetu, na hilo ndio
limekuwa lengo namba moja la taasisi yetu. Kwa kuanzia, tuna mkakati
wa kutafuta ardhi kwa ajili ya miradi
hiyo.
Tunakusudia kujenga hospitali
maalum za wanawake na watoto zitakazosaidia kuwatibu wanawake ili
wasitirike kwa kutibiwa na wanawake wenzao. Pia zitakuwepo zitakazowatibia wanaume.
Vilevile tunakusudia kujenga
kituo cha kulea watoto yatima ili
wale watoto wanaotupwa hospitalini
wasiishie katika vituo vya kanisa tu.
Imaan: Wito wako kwa Waislamu na Watanzania kwa ujumla.
Masau: Waislamu tusiwe wavivu, tujumuike katika ibada hii
muhimu ya kuhudumia wagonjwa,
ambayo si tu Mtume Muhammad
(Rehma na amani iwe juu yake) aliisisitiza, lakini pia aliifanya katika
uhai wake na kupelekea watu wengi
kuingia katika Uislamu. Hapo tutakuwa tumefuata tabia ya Kiislamu
na tabia ya Mtume Muhammad
(Rehma na amani iwe juu yake).

hutolewa na kuchapishwa na The Islamic Foundation, P.O.Box 6011 Morogoro, Tanzania E-mail: imaanmedia3@gmail.com

You might also like