You are on page 1of 11

HABARI

HabariZA
za
NISHATI
nishati&MADINI
&madini

NewsBulletin
MKOMBOZI
Wabunge
http://www.mem.go.tz

Toleo
No.89
51
Toleo No.

LimesambazwaLimesambazwa
kwa Taasisi nakwa
Idara
zote
Taasisi
naMEM
Idara zote MEM Tarehe
- 23-29 Januari , 2015
Oktoba 16 - 22, 2015

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA RASMI BODI YA TANESCO -Uk2

Bomba la gesi lenye


ukubwa wa kipenyo
cha inchi 36 na urefu
wa kilomita 477
kutoka Mtwara hadi
Dar es Salaam ambalo
linasafirisha gesi
inayozalisha umeme
katika kituo cha
Kinyerezi I jijini Dar es
Salaam

Waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA

Somahabari Uk.2

Mtambo wa Kufua umeme Megawati 150


kutokana na Gesi Asilia wa Kinyerezi I jijini Dar
es Salaam.

Kituo cha Kuchakata Gesi Asilia


cha Madimba

Rais Jakaya Kikwete

Waziri wa Nishati
na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo

Naibu Waziri wa Nishati na


Madini, anayeshughulikia
Madini Stephen Masele

Naibu Waziri wa Nishati na


Madini anayeshughulikia
Nishati, Charles Kitwanga

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,


Mhandisi Felchesmi
Mramba

Mkurugenzi Mkuu wa
REA, Dk. Lutengano
Mwakahesya

JK ameweka misingi sahihi kwa Rais Ajaye Mwihava

JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo wa Msimbati-Uk4

Soma
habari
Uk. 3

Ofisi ya M awasiliano Serik alini inapokea habari za matukio mbalimbali


kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizar a ya Nishati na Madini
Ofisi ya Mawasiliano Serik alini inapokea habari za matukio mbalimbali
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
kwa
ajili ya
News
Bullettin
hiiGhorofa
na Jarida
la(MEM)
Wizar
a yapepe:
Nishati
na Madini
au Fika
Ofisi
ya Mawasiliano
ya Tano
Barua
badra77@yahoo.com
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: badra77@yahoo.com

Habari za nishati/madini

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Hayawi hayawi sasa yamekuwa


Na Mohamed Saif

atimaye
mradi
mkubwa wa Kitaifa
wa miundombinu ya
kuchakata na kusafirisha
gesi asilia kutoka Mtwara
na Songo Songo hadi Dar es Salaam
umekamilika na kuzinduliwa.
Mradi huo ulizinduliwa rasmi
na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete
tarehe 10 Oktoba, 2015 katika hafla
iliyofanyika
Madimba
mkoani
Mtwara na kushuhudiwa na viongozi
mbalimbali wa Kitaifa, Mabalozi
kutoka nchi mbalimbali na wananchi.
Rais Kikwete alisema hatua hiyo
ni njia mojawapo kuelekea kwenye
uchumi imara katika nyanja mbalimbali
ikiwemo uanzishwaji wa viwanda
kwani kutakuwa na nishati ya umeme
yenye uhakika ambayo itazalishwa kwa
kutumia gesi asilia.
Aliuelezea mradi huo kuwa ni
mkubwa na wa aina yake kuwahi
kufanyika nchini na utasaidia kwa kiasi
kikubwa kuondoa tatizo la umeme na
kuchochea maendeleo endelevu ya
kiuchumi.
Rais
Kikwete
alizungumzia
umuhimu wa suala la Uwajibikaji
kwa Jamii yaani Corporate Social
Responsibility (CSR) na kuliagiza
Shirika La Maendeleo ya Petroli
Tanzania
(TPDC)
kuhakikisha
linasaidia jamii inayozunguka mradi
huo wa Madimba kwa kuchimba
visima na kusaidia huduma nyingine.
Suala la CSR halina mjadala,
wananchi huku wana shida ya maji,
lakini pia msiishie kwenye maji tu bali
pia msaidie na mambo mengine. Hii sio
hisani, ni wajibu wenu kufanya hivyo,
alisema.
Aidha, Rais Kikwete aliishukuru
Serikali ya China kwa utayari wake wa
kujenga miundombinu ya mradi husika
na kusisitiza umuhimu wa ushirikiano
baina ya Tanzania na China.

>>>

Rais Kikwete azindua mradi wa Kitaifa wa Miundombinu


ya Kuchakata na Kusafirisha Gesi Asilia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete (katikati waliokaa) akiwa katika
picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Kituo cha Kuchakata Gesi cha Madimba mara baada ya
kutembelea kituo hicho. Kushoto kwake ni Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene
na kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt
James Mataragio.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,


Dkt. Jakaya Kikwete akizindua jiwe la msingi
la mradi wa Kuchakata na Kusafirisha Gesi
Asilia kutoka Madimba (Mtwara) na Songo
Songo (Lindi) hadi Dar es Salaam.

Mtambo wa kuchakata Gesi Asilia uliopo Madimba Mkoani Mtwara

NewsBulletin

Habari za nishati/madini

http://www.mem.go.tz

JK ameweka misingi sahihi


kwa Rais Ajaye Mwihava

MEM

Tahariri
Na Badra Masoud

Makubwa yamefanyika
sekta ya Nishati

Wengi tutakumbuka wakati Rais wa awamu ya nne Mhe. Dk. Jakaya


Mrisho Kikwete alipoingia madarakani mwishoni mwa mwaka 2005
nchi yetu ilikuwa katika mgawo wa umeme na hadi ilipoingia mwaka
2006 mgawo huo wa umeme uliendelea kuwa mkali.
Mgawo huo ulitokana na kukauka kwa Mabwawa ambayo
yanatumika kuzalisha umeme ambayo kwa kipindi hicho ndiyo yalikuwa
chanzo kikubwa na pekee cha kuzalisha umeme.
Baadhi ya watafiti na wana mazingira walieleza kwamba kukauka
kwa mabwawa hayo kunatokana na sababu kubwa mbili ambazo ni
mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kilimo kinachofanywa na baadhi
ya watu katika vyanzo vya maji (upstream) ambapo huchepusha maji na
kushindwa kufuata mkondo wake.
Kutokana na mgawo huo wa umeme Serikali hiyo ya awamu ya
nne kupitia Wizara ya Nishati na Madini iliamua kuchukua hatua za
makusudi na madhubuti kuanza kukabiliana na hali hiyo ya mgawo
na kipaumbele kikiwa ni kujenga mitambo ya kuzalisha umeme kwa
kutumia nishati mbadala hususan gesi asilia.
Serikali iliruhusu Kampuni binafsi kuchimba gesi na kusafirisha
pamoja na kuwauzia Makampuni binafsi, viwanda na TANESCO ili
TANESCO nayo iweze kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia.
Ilipofika mwaka 2008 Serikali ilikamilisha ujenzi wa mtambo wa
kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia wa Ubungo I wenye uwezo
wa kuzalisha Megawati 102.
Mwaka 2009 mtambo mwingine ulikamilika wa Tegeta wenye
uwezo wa kuzalisha Megawati 45 na mwaka 2012 Serikali ilizundua
mtambo wa Ubungo II (Megawati 105). Mitambo yote hiyo inazalisha
umeme kwa kutumia gesi asilia na inamilikiwa na Serikali kwa asilimia
mia moja.
Serikali pia ilijenga mitambo mingine ya kuzalisha umeme kwa
kutumia gesi asilia ya Mtwara (Megawati 18) na Somangafungu mkoani
Lindi (Megawati 7.5).
Ili kuwa na umeme wa uhakika katika gridi ya taifa kwenye mikoa
ya Kanda ya Ziwa, Serikali ilijenga pia mtambo mwingine wa kuzalisha
umeme kwa kutumia mafuta mazito wenye uwezo wa kuzalisha
Megawati 60 uliopo Nyakato, Mwanza.
Kutokana na gesi asilia kugundulika kwa wingi katika mikoa ya
Kusini mwa Tanzania yaani Lindi na Mtwara, Serikali iliamua kujenga
bomba kubwa la gesi kutoka Mtwara na Lindi pamoja na mitambo ya
kuchakata ambapo gesi hiyo inazalisha na kusafirishwa hadi kwenye
mitambo ya kuzalisha umeme kwani gesi inayozalishwa na kuuzwa na
watu binafsi haitoshelezi katika kuzalisha umeme.
Aidha, kutokana na bomba la gesi kujengwa na mitambo yake,
Serikali iliona ni busara kujenga mtambo wa Kinyerezi I wenye uwezo
wa kuzalisha Megawati 150.
Mitambo yote ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia
iliyojengwa na Serikali tangu mwaka 2008 hadi sasa 2015 imefikia jumla
ya Megawati 484.5 ya umeme wote unaozalishwa na mitambo hiyo ya
Serikali kupitia TANESCO. Hayo ni mafanikio makubwa katika sekta
ya Nishati katika kipindi cha Serikali ya awamu ya nne.
Pamoja na kwamba Serikali ya awamu ya nne inaondoka madarakani
mwishoni mwa mwaka huu lakini imeacha misingi mizuri na jitihada
kubwa za kuendelea kuboresha sekta ya nishati hususan katika kuzalisha
umeme.
Ni ukweli ulio wazi kwamba kukamilika kwa mtambo wa Kinyerezi
I ndiyo mwanzo wa kuanza kwa ujenzi wa mitambo mingine ya
kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia ya Kinyerezi II, Kinyerezi
III na Kinyerezi IV kwani zipo kila dalili za kuandaa na kuendelea kwa
ujenzi huo kuwapo kwa eneo lenyewe ambapo mitambo hiyo itajengwa
na wahusika wameshaanza kazi.
Hivyo tuna kila sababu ya kuipongeza Serikali ya awamu ya nne
inayoongozwa na Mhe. Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kwamba
imefanya juhudi kubwa katika kuhakikisha kwamba upatikanaji wa
umeme unaongezeka ili Taifa la Tanzania litakapofika mwaka 2025 liwe
ni taifa la uchumi wa kati na mafaniko hayo yote yatatokana na kuwapo
kwa umeme wa kutosha na wa uhakika.
Hii ni dhahiri kwamba maendeleo ya nchi yoyote duniani yanatokana
na upatikanaji wa umeme wa uhakika hivyo lazima wote tutambue
kwamba bila umeme hakuna maendeleo hivyo, umeme ni maendeleo.

>>> Amtaja ndiye Kinara kuhudhuriwa na wananchi wanaozunguka


ilipo mitambo hiyo, baadhi ya Mabalozi
kuongeza uzalishaji umeme eneo
wanaoziwakilisha nchi zao nchini, Mashirika
>>> Mramba - Kinyerezi
I mitambo ya Kisasa

Na Asteria Muhozya,
Dar es Salaam

aimu Katibu Mkuu wa Wizara


ya Nishati na Madini, Mhandisi
Ngosi Mwihava, amesema kuwa,
Watanzania wanayo sababu ya
kupongeza jitihada zilizofanywa
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete katika sekta
ndogo ya nishati hususan umeme kwani katika
kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne hali ya
uzalishaji umeme imeongezeka ikilinganishwa
na ilivyokuwa awali.
Mhandisi Mwihava aliyasema hayo wakati
wa Uzinduzi wa Mitambo ya kufua Umeme
wa kiasi cha Megawati 150 Kinyerezi I jijini
Dar es Salaam ,uzinduzi huo uliofanywa na
Rais Kikwete mwanzoni mwa wiki na

ya Kimataifa, Uwakilishi wa Benki ya


Maendeleo ya Afrika (AfDB), baadhi ya
watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini,
watumishi wa Shirika la Umeme Nchini
(Tanesco),Wakandarasi waliojenga mitambo
hiyo na wanaotarajia kujenga vituo vingine vya
kuzalisha umeme vya Kinyerezi II na III.
Mwihava alisema kuwa, Rais Kikwete
ameweka misingi sahihi kwa Rais ajaye
wa Serikali ya Awamu ya Tano kutokana
na kuwezesha ongezeko la vituo vya kufua
umeme ukiwemo pia mradi mpya wa umeme
wa Kinyerezi I na miradi mingine ya umeme
inayoendelea kutekelezwa maeneo mbalimbali
nchini.
Umeweka rekodi ya kuwa Rais
aliyeongeza megawati nyingi zaidi za umeme
katika historia ya nchi yetu tangu uhuru ikiwa
ni asilimia 60 ya mitambo yote iliyowekwa
na Serikali tangu tupate uhuru mwaka 1961,
alisema Mwihava.
Katika hili tuna kila sababu ya

>>Inaendelea Uk. 5

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava


akieleza jambo wakati wa uzinduzi wa Mitambo ya Kufua umeme wa gesi wa
megawati 150 Kinyerezi I.
KWA HABARI PIGA SIMU
kitengo cha mawasiliano

TEL-2110490
FAX-2110389
MOB-0732999263
Bodi ya uhariri
Mhariri Mkuu: Badra Masoud
Msanifu: Lucas Gordon
Waandishi: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson
Mwase Teresia Mhagama, Mohamed Saif, Rhoda James ,
Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya

Five
Pillars of
Reforms

increase efficiency
Quality delivery
of goods/service
satisfAction of
the client
satisfaction of
business partners
satisfAction of
shareholders

Habari za nishati/madini

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

JK ameweka misingi sahihi kwa Rais Ajaye Mwihava

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Mhandisi Felschemi Mramba (wa
pili kulia) akiweleza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (katikati),
pamoja na wageni waliohudhuria halfa ya uzinduzi wa mitambo ya Kinyerezi I jijini Dar es Saalam
kuhusu miundombinu ya kusafirisha umeme wakati wa Uzinduzi wa hiyo. Rais aliitembelea
mitambo yote iliyopo Kinyerezi I kabla ya kuizindua rasmi.

>>Inatoka Uk. 3
kupongeza jitihada zilizofanywa na
Rais Kikwete, na hili limethibitisha
jitihada zilizofanywa na, Chama Cha
Mapinduzi (CCM). Pamoja na hayo
unaondoka ukiwa umeacha miradi
mikubwa ya umeme uliyo katika hatua
mbalimbali ikiwemo ya Kinyerezi
II hadi IV ambayo gharama za
ukwekezji huo ni wa Serikali na sekta
binafsi ambapo inafikia takriban Dola

za Marekani Bilioni 4 sawa na shilingi


trilioni 8.
Mwihava pia aliitaja mitambo
ya Kufua umeme iliyojengwa katika
kipindi cha mwaka 2005-2010 kuwa
ni pamoja na Vituo vya kufua Umeme
vya Ubungo I kinachozalisha megawati
102, Ubungo II megawati 105, Tegeta
megawati 42, Mtwara megawati
18, SomangaFungu megawati saba
na nusu, Nyakato megawati 60 na
Kinyerezi I megawati 150, ambavyo

vyote vinafanya jumla ya megawati


484.5, vyote vikiwa vimeunganishwa
katika gridi ya taifa.
JK amewezesha uwepo wa
mitambo mipya ya kufua umeme
kwa asilimia 47 ndani ya kipindi
cha miaka 10. Haya ni mafanikio
makubwa. Lakini vipo vituo vingine
vinavyozalisha umeme nje ya gridi
kama ilivyo kituo cha Kigoma,
alisema Mwihava.
Kwa upande wake Mkurugenzi

Mtendaji TANESCO, Mhandisi


Felchesmi Mramba aliielezea mitambo
ya Kinyerezi I kuwa ni mitambo mipya
na ya kisasa yenye teknolojia ya hali
ya juu ambayo ni aina ya mitambo
ambayo inatumika kuendesha ndege
aina ya boeing.
Huu ni uwekezaji mkubwa.
Tanesco tutaendelea kutekeleza
majukumu yetu kwa uadilifu hivyo
wananchi
tarajieni
mabadiliko
makubwa ya nishati ya umeme
kutokana na mitambo yetu na miradi
mingine kwani itakuwa mbadala wa
vyanzo vya maji,alisema Mramba.
Mramba aliongeza kuwa, mbali
na Mradi wa Kinyerezi I, Tanesco
inaendelea na utekelezaji wa miradi
mingine ya umeme na kuutaja mradi
wa Backbone wa Iringa hadi
Shinyanga utakaozalisha Kv 400,
Makambako- Songea Ruvuma Kv
220 na mwingine kutoka Tanzania
hadi nchini Kenya wa Kv 400.
Matatizo yaliyopo sasa ni ya
muda mfupi. Tutakuwa na umeme
wa kutosha baada ya kukamilika
kwa miradi hii, uunganishaji umeme
kwa sasa umefikia asilimia 30 kutoka
asilimia 10, wakati idadi ya watumiaji
wa umeme imefikia asilimia 40,
aliongeza Mramba.
Kinyerezi I ni kituo kimojawapo
kati ya vituo vinne vitakavyojengwa
Kinyerezi Jijini Dar es Saalm ambapo
kukamilika kwake kutawezesha
uzalishaji wa umeme wa kiasi cha
megawati 1290. Kituo cha kinyerezi I
pekee kimegharimu takribani Dola za
Marekani milioni 183 sawa na shilingi
za Kitanzania bilioni 400.

Kasi ya uzalishaji wa umeme yahitajika - Kikwete


Zuena Msuya na
Nuru Mwasampeta.

ais
Jakaya
Kikwete
amelitaka Shirika la
Umeme
Tanzania
(Tanesco) kuongeza juhudi
katika kujenga mitambo ya
kuzalisha umeme ili kupunguza mgawo
unaoikumba nchi hivi sasa.
Rais Kikwete alisema hayo hivi
karibuni wakati wa uzinduzi wa kituo
cha kufua umeme cha Kinyerezi 1
uliofanyika mwanzoni mwa wiki jijini
Dar es Salaam ambacho kina uwezo wa
kuzalisha umeme wa kiasi cha Megawati
150 kwa wakati mmoja pindi mashine
zote nne zitakapowashwa.
Aidha ilielezwa kwamba megawati
hizo 150 zitachangia kufikia kiasi cha
megawati 350 zinazotarajiwa kuzalishwa
katika mradi wa Kinyerezi 1 baada ya
kukamilika kwa ujenzi na kuwashwa kwa

mitambo mingine mitatu iliyopo katika


eneo hilo. Mitambo hiyo inatarajiwa
kukamilika na kuwashwa ifikapo
January 2016 hivyo kuchangia katika
kupunguza tatizo la umeme linaloikabili
nchi yetu hivi sasa, alibainisha.
Kikwete alisema kuwa kwa sasa
Tanzania inakabiliwa na upungufu
mkubwa wa umeme kutokana na
ukame mkubwa ulioikumba nchi kwa
mara ya kwanza na kusababisha baadhi
ya uzalishwaji wa umeme kupungua
na baadhi ya mitambo kama Kidatu
kufungwa.
Kutokana na ukame huo, Kikwete
ameitaka Tanesco kuongeza kasi ya
kujenga mitambo mingine ya kuzalisha
umeme kwa njia ya gesi, upepo, tungamotaka na nyinginezo ili kuondokana na
kutegemea umeme wa maji ambao sasa
umekuwa si wa uhakika.
Mabwawa
tuliyokuwa
tukiyategemea kuzalisha umeme yote
yamekauka, ikiwemo Mtera ambayo

sasa imezima mitambo yake. Kidatu


ambayo iko mbioni kuzimwa , Kihansi
inazalisha robo ya uwezo wake,Hale,
vile vile Nyumba ya Mungu hivyo ni
lazima tuwe na mbadala wa kuzalisha
umeme na tusirudi katika kutumia
mafuta mazito yanayoiingiza nchi katika
kutumia gharama kubwa za uzalishaji
wa umeme, alisema Rais Kikwete.
Aidha, alitaka kuharakishwa kwa
ujenzi wa vituo vingine vya kuzalisha
umeme ikiwemo Kinyerezi II,Kinyerezi
III, na Kinyerezi IV ambapo ujenzi
wa Kinyerezi II unatarajiwa kuanza
mwanzoni kwa mwaka ujao mara tu
baada ya kukamilika kwa mitambo
yote Kinyerezi I na kukamilika ifikapo
mwaka 2017.
AidhaRaisJakayaKikwetealibainisha
kuwa Kenya ni nchi inayozalisha umeme
kwa wingi ikifuatiwa na Tanzania lakini
baada ya ugunduzi wa gesi asilia na
kukamilika kwa ujenzi wa vituo vya
kuzalisha umeme Tanzania itakuwa na

uwezo wa kuzalisha umeme wa ziada


ambao utauzwa nchini humo.
Alisema nchi zilizoonesha nia ya
kununua umeme toka Tanzania kuwa
ni Kenya, Rwanda, Uganda, Burundi
pamoja na Zambia hivyo umeme
utasaidia hata kukua kwa uchumi wan
chi kutokana na kuuza nishati umeme.
Imebainika
kuwa
umeme
unaotarajiwa kuzalishwa kutokana
na gesi asilia kuwa ni megawati 1,220
kwa mchanganuo ufuatao; Kinyerezi
I itazalisha megawatt 150, Kinyerezi II
megawatt 240, Kinyerezi III megawatt
300 na mwisho ni Kinyerezi IV
itakayozalisha megawatti 330
Kabla ya uzinduzi wa mradi huu
mkubwa wa umeme mheshimiwa Rais
alizindua bomba la kusafirisha gesi asilia
kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara hadi
Dar es Salaam pamoja na kituo cha
kuchakata gesi asilia kilichopo Madimba
mkoani Mtwara.

NewsBulletin

Habari za nishati/madini

http://www.mem.go.tz

Tanzania yaingia katika orodha nchi zenye gesi asilia

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli


Tanzania (TPDC), Mhandisi James Mataragio, akiongea na
waandishi wa habari katika mitambo ya kuchakata gesi
Magimba, Mtwara

Na Asteria Muhozya

meelezwa kuwa, kutokana na


kukamilika kwa miundombinu
ya kuchakata na kusafirisha
gesi asilia kutoka Mtwara,
Lindi hadi Dar es Saalaam
kunaifanya Tanzania kuingia katika
orodha ya nchi zenye nishati ya gesi
asilia.
Aidha, ilielezwa kuwa, Tanzania
inayo nishati ya kutosha kukidhi
mahitaji muhimu kwa uwekezaji
mkubwa, wa kati, wajasiriamali
wadogo na uwepo wa nishati hiyo
ni nguzo kubwa katika kuchochea
maendeleo ya viwanda na ukuaji
uchumi ikiwemo pia maendeleo ya
jamii.
Hayo yalielezwa na Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la maendeleo
ya Petroli Tanzania (TPDC),
Mhandisi James Mataragio wakati
wa uzinduzi wa miundombinu ya
kuchakata na kusafirisha gesi asilia
iliyofanyika mwishoni mwa wiki,

Madimba, mkoani Mtwara.


Mataragio aliongeza kuwa,
kutekelezwa kwa mradi huo
kutasaidia kwa kiwango kikubwa
katika maendeleo ya nchi kutokana
na ukweli kwamba, nishati ndiyo
msingi mkuu wa maendeleo kwa
nchi yoyote Duniani.
Vilevile, Mataragio alisema
kuwa, kukamilika kwa mradi
huo kuna faida nyingi ikiwemo
wazalishaji wengine wa gesi asilia
kuweza kulitumia bomba hilo
bila masharti magumu na hivyo
kuchochea uwekezaji.
Pia alieleza kuwa, matumizi
ya gesi asilia kwenye maeneo
mbalimbali ikiwemo viwandani,
taasisi, majumbani, matumizi
ya magari na kuzalisha umeme
yataongezeka na hivyo kusaidia
kupunguza uchafuzi wa mazingira
kwa kiwango kikubwa.
Alizitaja faida nyingine za mradi
huo kuwa ni pamoja na kuongeza
pato la Serikali kutokana na kodi,
mrabaha na gawio kwa uuzaji

Mitambo ya kupokea gesi asilia iliyo katika eneo la


SomangaFungu, wilayani Kilwa, mkoani Lindi. Gesi hiyo
inapokelewa kutoka mitambo ya Kuchakata gesi iliyopo
Madimba-Mtwara na SongoSongo, ambapo husafirishwa
kuelekea katika kituo cha Kinyerezi I, Jijini Dar es Salaam kwa
ajili ya kufua umeme.

Sehemu ya Mtambo wa kuchakata gesi asilia uliopo katika eneo


la Madimba, Mtwara.

Moja ya visima vya maji safi vilivyojengwa kutokana na mradi wa gesi asilia. Visima hivi vina
uwezo wa kuzalisha maji safi na salama lita 60,000 kwa siku ambayo yanatumiwa na zaidi ya
wakazi 3000 wanaozunguka eneo la Madimba, mkoani Mtwara.

wa gesi asilia kwa wingi ikiwemo


kuongeza pato kwa Halmashauri
za Mtwara na Kilwa kupitia pato la
kodi ya huduma.
Aliongeza
kuwa,
mradi
huo utaokoa fedha za kigeni
zinazotumika sasa kuagiza mafuta
nje ya nchi kwa ajili ya kuzalisha
umeme, kupunguza uharibifu wa
mazingira unaotokana na ukataji
miti na kuleta unafuu kwa wananchi
watakaotumia gesi asilia kwenye
shughuli za kiuchumi ikiwemo
kuchochea utafutaji wa mafuta na
gesi asilia nchini.
Vilevile, alisema kuwa, mbali na
faida hizo, mradi huo umesaidia
upatikanaji maji safi kwa matumizi
ya binadamu ambapo tayari kijiji
cha Madimba kimeanza kupatiwa
huduma ya maji ya kiasi cha lita
60,000 kwa siku na kutumiwa na
zaidi ya wakazi 3000.

Habari za nishati/madini

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Kufuatia kukamilika kwa Mradi wa Kitaifa wa Gesi Asilia

>>> Upungufu wa Umeme


kuwa historia
>>> Viwanda kuongezeka,
ajira nyingi kuzalishwa

Baadhi ya Wananchi waliohudhuria hafla ya kihistoria ya uzinduzi


wa mradi wa miundombinu ya kusafisha na kusafirisha gesi kwenye
eneo la Madimba, Mkoani Mtwara hivi karibuni.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete


(katikati) akikagua Kituo cha Kuchakata Gesi Asilia cha Madimba.
Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo
ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt James Mataragio akifuatiwa na
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene.

Na Mohamed Saif

meelezwa kwamba kutokana


na uzinduzi wa mradi mkubwa
wa Kitaifa wa miundombinu ya
kuchakata na kusafisha gesi asilia,
upungufu wa umeme utakuwa

historia.
Hayo yameelezwa kwenye hafla ya
uzinduzi wa mradi huo hivi karibuni
Madimba Mkoani Mtwara na Waziri
wa Nishati na Madini, George
Simbachawene wakati akimkaribisha
Rais Jakaya Kikwete kuzindua rasmi

mradi huo.
Waziri Simbachawene alimpongeza
Rais Kikwete kwa jitihada zake za
kuhakikisha mradi huo unafanikiwa.
Wapo baadhi ya Watanzania
ambao wanahoji kuwa unapoondoka
madarakani unatuacha achaje?,
nataka
niwaambie
Watanzania
wenzangu Mheshimiwa Rais Kikwete
aliikuta Tanzania ikiwa na kiasi cha gesi
iliyogunduliwa cha futi za ujazo trilioni 8
lakini anatuacha na futi za ujazo trilioni
52, alisema.
Alisema kuwa Serikali imewekeza
kwa asilimia 100 katika mradi huo na
kuongeza kwamba uamuzi wa Serikali
kukubali kuwekeza katika mradi huo
ni uamuzi unaoonesha namna Serikali
ilivyodhamiria kutafuta suluhu ya
changamoto za kusambaza gesi kwa
watumiaji na pia kuondoa adha ya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete (katikati waliokaa) akiwa katika picha
ya pamoja na Viongozi mbalimbali pamoja na Wakandarasi wa Mradi kutoka Kampuni za CPTDC, CPE
na CC za China mara baada ya kukagua Kituo cha Kuchakata Gesi Asilia cha Madimba.

ukosefu wa umeme wa uhakika nchini.


Uamuzi huu ni utekelezaji wa Ilani
ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi
ya 2010 kuhusu upanuzi wa matumizi
ya gesi asilia, alisema Simbachawene.
Alisema kuwa dhamira ya Serikali
ni kuhakikisha kwamba gesi asilia
inapatikana kwa ajili ya kuzalisha
umeme na wananchi wengi zaidi kupata
gesi kwa matumizi ya majumbani na
viwandani.
Aliongeza kuwa ni wazi kwamba
matumizi hayo ya gesi asilia yataongeza
kasi ya ukuaji uchumi kwa mtu mmoja
mmoja na kwa Taifa kwa ujumla,
alisema Simbachawene.
Waziri Simbachawene alisema
kutokana na mradi huo, viwanda nchini
vitaongezeka na kubainisha kwamba
tayari Kampuni ya Dangote imefungua
kiwanda cha kuzalisha saruji.
Alisema kiwanda hicho kitatoa
ajira kwa Watanzania wengi na hivyo
kupunguza tatizo la ajira nchini.
Aidha, mbali na kiwanda hicho,
Simbachawene alisema viwanda vingine
vitakavyojengwa ni vya mbolea na vya
plastic.
Kampuni ya Dangote imefungua
kiwanda
cha
kuzalisha
saruji
kitakachokuwa kikubwa katika Afrika
na kitatoa ajira kwa Watanzania 1,366
ambapo 697 watakuwa vibarua na 699
watakuwa ni wa kudumu katika fani
mbalimbali, alisema.
Waziri Simbachawene aliishukuru
Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China
kwa kuunga mkono dhamira ya Serikali
kwa kutoa vibali kwa mashirika yake
hususan China Petroleum Technology
and Development Corporation (CPTDC)
pamoja na Benki ya Exim ya China
kuweza kufanya tathmini ya mradi na
kukubali kutoa mkopo wa masharti
nafuu na hivyo kufanikisha kukamilika
kwa mradi huo.
Vilevile Simbachawene aliwashukuru
Mawaziri waliomtangulia katika Wizara
ya Nishati na Madini ambao ni William
Ngeleja na Profesa Sospeter Muhongo
kwa mchango wao katika mafanikio
ya ujenzi na hatimaye kukamilika kwa
miundombinu husika.

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Habari za nishati/madini

Ufahamu undani wa Mradi wa Kitaifa wa miundombinu ya Gesi Asilia


Mohamed Saif na Teresia >>>
Mhagama
>>>
i tukio la kihistoria kuwahi >>>
kufanyika nchini ambapo
Rais wa Jamhuri ya >>>

Muungano wa Tanzania,
Dkt Jakaya Kikwete
alizindua rasmi mradi mkubwa wa
kitaifa wa Miundombinu ya Kuchakata
na Kusafirisha gesi asilia.
Hafla hiyo ya uzinduzi ilifanyika
hivi karibuni kijijini Madimba ambapo
kumejengwa
miundombinu
ya
kuchakata gesi asilia na kushuhudiwa
na viongozi mbalimbali wa Kitaifa,
mabalozi wa nchi mbalimbali na mamia
ya wananchi wa Mkoani Mtwara na
maeneo mengine ya Tanzania.
Awali, akitoa maelezo ya utangulizi,
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika
la Maendeleo ya Petroli Tanzania
(TPDC), Dkt James Mataragio alisema
miundombinu ya kuchakata na
kusafirisha gesi asilia imekamilika na
inamilikiwa na Shirika la Maendeleo ya
Petroli (TPDC) kwa asilimia 100.
Akiuelezea mradi huo, alisema
bomba la gesi lina uwezo wa kusafirisha
gesi asilia kiasi cha futi za ujazo milioni
784 kwa siku kwa kiwango cha juu
bila mkandamizo (compression) na
matumizi yakiongezeka zaidi linaweza
kusafirisha kiasi cha futi za ujazo hadi
milioni 1,002 kwa siku kwa kuongezea
mgandamizo pale Somanga-Fungu.
Alisema usafirishaji wa gesi asilia
katika bomba hilo kubwa kutoka
mkoani Mtwara hadi Dar es Salaam
lenye ukubwa wa kipenyo cha inchi
36 na urefu wa kilomita 477 umeenda
sambamba na kukamilika kwa mitambo
ya kuchakata gesi hiyo iliyojengwa katika
eneo la Madimba mkoani Mtwara na
Songosongo mkoani Lindi.
Hii ni kusema kwamba gesi hiyo
itasafishwa katika vituo vya Madimba
na Songo Songo kabla ya kusafirishwa

Rais Kikwete auzindua rasmi tarehe 10 Oktoba, 2015


Unamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100
Ni mkubwa na wa aina yake kuwahi kufanyika nchini
Umegharimu Dola za Marekani zipatazo bilioni 1.225

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania


(TPDC), Dkt James Mataragio akitoa maelezo ya utangulizi wakati
wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa miundombinu ya kuchakata na
kusafirisha gesi asilia iliyofanyikia Madimba Mkoani Mtwara

Hatua mbalimbali za ujenzi


wa bomba la kusafirishia gesi
asilia kutoka Mtwara hadi Dar es
Salaam kabla ya kukamilika kwa
mradi huo
Kituo cha Kuchakata Gesi Asilia cha Madimba

katika bomba hilo ambapo mitambo ya


Madimba inao uwezo wa kuchakata
gesi futi za ujazo zipatazo milioni 210
kwa siku na mitambo ya Songo Songo
ina uwezo wa kuchakata gesi futi za
ujazo zipatazo milioni 140 kwa siku.
Alisema jumla ya gharama za
ujenzi wa mradi huo wa kusafisha na
kusafirisha gesi mpaka kukamilika
kwake ni Dola za Marekani zipatazo
bilioni 1.225, ambapo asilimia 95 ni
mkopo kutoka Benki ya Exim ya China
na huku asilimia 5 ikitoka Serikalini.
Alieleza kwamba gharama hizo
zimegawanyika ambapo mtambo wa
kusafisha gesi asilia wa Songo Songo
umegharimu Dola za Marekani
151,735,000; Mtambo wa Kusafisha gesi
asilia wa Madimba umegharimu Dola
za Marekani 197, 877,000 na Bomba la
kusafirisha gesi asilia limegharimu kiasi
cha Dola za Marekani 875, 715,000.
Miundombinu hii inamilikiwa na
Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC)
kwa asilimia 100.
Katika kuhakikisha kuwa gesi hii
inawafikia wananchi wengi nchini,
alisema Serikali imeweka matoleo/
viunganishi katika sehemu mbali mbali
ili kuwezesha kusambaza gesi katika
maeneo mbalimbali ambapo bomba kuu
linapita na huku akitaja maeneo hayo
kuwa ni Mtwara mjini, Lindi, Somanga
Fungu, Kilwa na Mkuranga.
Ni dhahiri kuwa uwepo wa gesi
asilia utainufaisha Tanzania katika
masuala mbalimbali ikiwemo kuzalisha
umeme, kutumika kama nishati
viwandani, taasisi, majumbani, kwenye
magari kusaidia kupunguza uharibifu
wa mazingira unaotokana na ukataji
miti na kuleta unafuu kwa wananchi
watakaotumia gesi asilia kwenye
shughuli zao za kiuchumi.
Vilevile alisema gesi italinufaisha
Taifa kuongeza Pato la Serikali kutokana
na kodi, mrabaha na gawio kwa uuzaji
wa gesi asilia, kuongeza pato kwa
Halmashauri za Mtwara na Kilwa
kupitia pato la kodi ya huduma (Service
Levy) ambayo ni asilimia 0.3 ya mauzo
ya gesi asilia na hivyo kuokoa fedha za
kigeni zinazotumika kuagiza mafuta nje
ya nchi kwa ajili ya kuzalisha umeme.
Ufunguzi rasmi wa kazi ya kutandaza
bomba kutoka Madimba hadi Dar
es Salaam, ulifanywa na Rais Jakaya
Kikwete kwa kuweka jiwe la msingi
katika eneo la Kinyerezi jijini Dar es
Salaam mnamo tarehe 8 Novemba
2012.

Habari za nishati/madini

8
NewsBulletin
HAFLA YA UZINDUZI WA MIUNDOMBINU YA
KUCHAKATA NA KUSAFIRISHA GESI ASILIA
http://www.mem.go.tz

1
4
2
5
3

1.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya


Kikwete (katikati) akikagua Kituo cha Kuchakata Gesi
Asilia cha Madimba. Kushoto kwake ni Waziri wa Nishati na
Madini, George Simbachawene akifuatiwa na Mkurugenzi
Mtendaji wa TPDC, Dkt James Mataragio. Kulia kwake ni
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu akifuatiwa
na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,
Mhandisi Ngosi Mwihava.

2.

Mtambo wa Kuchakata Gesi Asilia wa Madimba, Mkoani


Mtwara

3.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt


Jakaya Kikwete (kulia) akisikiliza maelezo yaliyokuwa
yanatolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt.
James Mataragio (hayupo pichani). Kulia kwake ni Waziri
wa Nishati na Madini, George Simbachawene, Balozi wa
China nchini Tanzania, Lu Youqing na anayemfuatia ni
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete.

4.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya


Kikwete akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Kituo
cha Kuchakata Gesi Asilia cha Madimba. Kulia kwake
ni Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene
akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima
Dendegu. Kushoto kwake ni Mke wa Rais, Mama Salma
Kikwete. Wengine ni Viongozi mbalimbali wa Kitaifa.

5.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt


Jakaya Kikwete akipatiwa maelezo na Meneja Mitambo
ya Kuchakata Gesi Asilia, Mhandisi Sultan Pwaga
(aliyenyoosha mikono) kuhusu Mradi wa Kuchakata Gesi
Asilia wa Madimba. Wengine katika picha ni viongozi
mbalimbali wa Kitaifa waliohudhuria hafla ya uzinduzi
wa Mradi.

NewsBulletin

Habari za nishati/madini

http://www.mem.go.tz

UZINDUZI MTAMBO WA KUZALISHA UMEME KWA


KUTUMIA GESI ASILIA KINYEREZI I
Picha N0. 1, 2, ikionesha baadhi ya mitambo ya
kufua umeme iliyopo katika eneo la Kinyerezi I, jijini
Dar es Salaam. Picha N0. 3 ni kituo cha kupooza na
kusambaza umeme kichopo Kinyerezi I jijini Dar es
Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.


Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja
na baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Nishati na
Madini.

10

Habari za nishati/madini

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

UZINDUZI MTAMBO WA KUZALISHA UMEME KWA


KUTUMIA GESI ASILIA KINYEREZI I

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya


Maendeleo ya Afrika (AfDB), Tonia Kandiero (wa pili kulia) pamoja
na wageni wengine alipowasili eneo la Kinyerezi I, jijini Dar es
Saalam

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi (TANESCO), Dkt. Mighanda


Manyahi (wa pili kulia) kwa niaba ya TANESCO akimkabidhi Rais
Jakaya Kikwete zawadi ya picha inayoonesha baadhi ya miradi
mikubwa ya umeme iliyotekelezwa kipindi cha Serikali ya Awamu
ya Nne. Wengine wanaoshuhudia kutoka kushoto ni kaimu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava, na
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Meck Sadik

Baadhi ya Watumishi kutoka Shirika la Umeme Tanzania


(TANESCO), wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa mitambo ya Kufua
umeme ya megawati 150 ya Kinyerezi I.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Shirika
la Umeme Nchini (TANESCO).

Baadhi ya Wananchi wanaoishi eneo la Kinyerezi waliohudhuria


uzinduzi wa Mitambo ya kufua umeme ya Kinyerezi I wakifuatilia
hafla ya uzinduzi

Baadhi ya wageni mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Madini,


TANESCO, mashirika ya Maendeleo, viongozi wa Kitaifa na
wawakilishi kutoka Balozi mbalimbali nchini wakifuatilia hafla ya
uzinduzi.

NewsBulletin

Habari za nishati/madini

http://www.mem.go.tz

11

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


WIZARA YA NISHATI NA MADINI

TAARIFA KWA UMMA


UMILIKI WA MITAMBO YA UZALISHAJI UMEME
Hivi
karibuni
zimeibuka
taarifa 6
zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii
zikimnukuu Waziri wa Nishati na Madini,
George B. Simbachawene akisema kuwa 7
mitambo yote ya uzalishaji umeme nchini
inamilikiwa na Kampuni binafsi.
8
Tunapenda kuutaarifu Umma kuwa taarifa
hizi ni za uongo kwani Waziri Simbachawene
hajawahi kutoa tamko la kuwa mitambo ya 9
kuzalisha Umeme yote nchini ni ya kampuni
binafsi bali alichosema ni kuwa, baadhi ya
mitambo ni ya kampuni binafsi na mingine
10
inamilikiwa na Serikali.
Mitambo inayomilikiwa na Serikali ni:1
2
3
4
5

Kinyerezi I (Gesi) yenye uwezo wa MW


150 ambapo MW 35 zimewashwa leo 12
Oktoba 2015;

Kidatu (Maji) yenye uwezo wa MW 204


4
ambayo kwa sasa inazalisha MW 27;
Kihansi (Maji) yenye uwezo wa MW 180
ambayo kwa sasa inazalisha MW 45;
Pangani (Maji) yenye uwezo wa MW 68
ambayo kwa sasa inazalisha MW 17;
Nyumba ya Mungu (Maji) yenye uwezo
wa MW 8 ambayo kwa sasa inazalisha
MW 5;
Hale (Maji) yenye uwezi wa MW 21
ambayo kwa sasa inazalisha MW 4; na

11 Mtera (Maji) yenye uwezo wa MW 80


ambapo mitambo yake imezimwa (MW0);

Kwa hiyo, Jumla ya kiasi cha umeme


Ubungo I (Gesi) yenye uwezo wa MW kinachopatikana katika mitambo hiyo kwa
102 ambayo kwa sasa inazalisha MW 85; sasa ni Megawati 337 kati ya Megawati 870
zinazotakiwa kuzalishwa.
Ubungo II (Gesi) yenye uwezo wa MW
105 ambayo kwa sasa inazalisha MW 70; Mitambo inayomilikiwa na watu binafsi ni:Tegeta (Gesi) yenye uwezo wa MW 42 1
ambayo kwa sasa inazalisha MW 42;
2
Nyakato (Mafuta) yenye uwezo wa MW
3
60 ambayo kwa sasa inazalisha MW 42;

IPTL (Mafuta) yenye uwezo wa MW100


ambayo kwa sasa inazalisha MW 80;
Aggreko (Mafuta) yenye uwezo wa MW
70 ambayo kwa sasa inazalisha MW 70;
SONGAS(Gesi) yenye uwezo wa
MW180 ambayo kwa sasa inazalisha

MW 158; na
Symbion (Gesi) yenye uwezo wa MW
112 ambayo kwa sasa inazalisha MW 74.

Hivyo mitambo hii ya watu binafsi inazalisha


umeme wa kiasi cha Megawati 382 kati ya
Megawati 462 zinazohitajika.
Ieleweke kuwa Serikali inajitahidi kuiwasha
mitambo hiyo yote inayomilikiwa na Serikali na
Binafsi ili izibe pengo la umeme wa maji ambao
umepungua kutoka MW 561 hadi MW 88. Ili
nchi isiwe na mgawo wa umeme zinahitajika
MW 1332 ambapo kwa sasa kiasi cha umeme
kinachopatikana ni Megawati 719.
Awali tulikuwa na upungufu wa megawati
takribani 450 lakini tumefanya juhudi za kuwasha
mitambo mbali mbali tangu wiki iliyopita na sasa
upungufu uliobaki ni kati ya MW 200 na 250.
Serikali kupitia TANESCO inatoa rai kwa
Watanzania kuendelea kuvumilia kipindi hiki
cha mpito kwani inajitahidi kwa hali na mali
kuwasha mitambo iliyobaki ya gesi ya Kinyerezi
yenye uwezo wa kuzalisha umeme wa kiasi
cha megawati 150 hivyo hadi ifikapo tarehe 20
Oktoba, 2015 hali ya upatikanaji wa umeme
itaanza kutengemaa.
Asanteni na poleni kwa usumbufu
unaojitokeza.
Imetolewa na;a
WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Waziri wa Nishati na Madini,


George Simbachawene

You might also like