You are on page 1of 2

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail:
ikulucommpress@googlemail.co
m
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425

PRESIDENTS OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA
ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete ametuma salamu za rambirambi na maombolezo kumlilia Mwenyekiti wa
Chama cha Siasa cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, ambaye
alipoteza maisha katika ajali ya gari iliyotokea alfajiri ya leo, Jumapili, Oktoba 4, 2015,
katika Kijiji cha Msolwa, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Katika salamu zake za rambirambi kwa Chama cha DP, Rais Kikwete amesema:
Nimepokea kwa huzuni kubwa taarifa za kifo cha Mwenyekiti wenu na Mtanzania
mwenzetu, Mchungaji Christoher Mtikila ambaye nimeambiwa amepoteza maisha
katika ajali ya gari Mkoani Pwani akiwa njiani kurejea mjini Dar es Salaam akitokea
kwao Njombe.
Kwa hakika, kifo cha Mchungaji Mtikila ni pigo kubwa kwa Chama cha
Democratic Party ambacho kimempoteza kiongozi wake mkuu. Aidha, kifo hicho ni
pigo kwa medani za siasa katika Tanzania na kimetunyanganya mmoja wa viongozi
hodari na wazalendo, aliyekuwa na msimamo thabiti na usioyumba katika kutetea
mambo ambayo aliyaamini katika maisha yake yote, amesema Rais Kikwete na
kuongeza:
Ni jambo la kusikitisha pia kuwa tunampoteza Mchungaji Mtikila katika
kipindi cha mchakato muhimu wa kisiasa nchini ambako mchango wake ulikuwa
unahitajika sana. Hakika, tutamkosa mwenzetu katika uwanja wa siasa za nchi
yetu.

Ameendelea Rais Kikwete, Nawatumieni nyie wana-democratic Party salamu


za dhati ya moyo wangu na pole nyingi kwa kuondokewa na kiongozi wetu mkuu, wa
miaka mingi na wenye uzoefu wa uongozi wa chama cha siasa.
Aidha kupitia kwenu, napenda kuitumia pole zangu nyingi familia ya
Mchungaji Mtikila. Nawapa pole sana wanafamilia, ndugu na marafiki na napenda
wajue kuwa niko nao katika kipindi hiki cha majonzi ya kuondokewa na mhimili wa
familia. Naungana nao katika majonzi. Aidha, naungana nao katika kumwomba
Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke pema roho ya Mchungaji Christopher
Mtikila. Amen.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
04 Oktoba, 2015

You might also like