You are on page 1of 3

Na Mwandishi Wetu

MGOMBEA jimbo la Monduli kupitia Chama Cha Mapinduzi


(CCM), Namelok Sokoine, ameahidi kuendeleza yote aliyoasisi,
kusimamia na kutekeleza aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo,
Edward Lowassa.
Namelok, amemtaja Edward Lowassa, kuwa ni miongoni mwa
viongozi walioitendea mengi jimbo hilo katika kipindi chake cha
uongozi.
Nitajidanganya nikibeza kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na
Lowassa hapa Monduli kwa kuboresha huduma za elimu, afya,
miundombinu na nyingine nyingi. Lowassa, baba yangu Edward
Moringe Sokoine na Lepilal Moloimet ni alama muhimu kwa wana
Monduli kwa mchango wao kwa jamii yetu, alisema Namelok,
mtoto wa waziri mkuu wa zamani, Edward Moringe Sokoine
Akizungumzia uamuzi wake wa kuwania ubunge, Namelok
alisema Lowassa ndiye alinitambulisha kwa wazee wa mila na
wana Monduli kuwa ninafaa kurithi kiti chake cha ubunge.
Sitaiangusha imani hiyo kwa kuwatumika wana Monduli kwa
kuendeleza yote aliyoanzisha, kusimamia na kutekeleza,
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni za ubunge jimbo la
Monduli jana, alimtaja Lowassa kuwa ndiye mwalimu wake
kisiasa na kuahidi kumheshimu, kushirikiana naye kwa faida na
maslahi ya wana Monduli huku akibainisha kuwa mahusiano yao
hayawezi kutetereshwa na harakati au tofauti za kiitikadi
kisiasa.
Uhusiano kati ya familia ya Lowassa na hayati Edward Moringe
Sokoine
umejengwa
katika
misingi
imara
isiyoweza

kutetereshwa na masuala ya kisiasa au wanaojipitisha kuomba


uongozi kwa kutumia jina la Lowassa, alisisitiza Namelok
Akitaja vipaumbele vyake iwapo atachaguliwa kuwa mbunge wa
Monduli, Namelok alisema ataboresha huduma za kijamii
ikwemo elimu, afya, mawasiliano, miundombinu akianzia pale
alipofikia Lowassa.
Nitatumia uwezo, nguvu na ushawishi wangu wote
kushughulikia na kumaliza kero ya migogoro ya ardhi kati ya
wafugaji, wakulima wakubwa, hifadhi za taifa na jeshi la
wananchi (JWTZ), ambao kwa mapenzi ya taifa baba yangu
aliwapa eneo la mafunzo ya kijeshi kwa sharti kuwa litatumiwa
pia kwa ajili ya malisho lakini hivi karibuni wafugaji wanazuiwa,
alisema Namelok.
Kwa upande wake, mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Dk Asha
Rose Migiro aliwaomba wakazi wa Monduli kuwachagua
wagombea wa CCM kuanzia ngazi ya udiwani na ubunge, lakini
akisita kutaja nafasi ya urais na jina la mgombea wa CCM, John
Magufuli kutokana na hisia za wananchi waliohudhuria mkutano
huo kuonekana kumuunga mkono mgombea wa Chadema, Edward
Lowassa.
Chagueni madiwani na mbunge wa CCM, Namelok Sokoine
pamoja na viongozi wengine wa CCM, alisema Dk Migiro bila
kutaja nafasi ya Urais wala jina la Magufuli
Akizungumzia kitendo cha wananchi waliohudhuria mkutano huo
kuonyesha kumuunga mkono Lowassa katika nafasi ya urais
kilimlazimisha mwenyekiti wa kamati ya kampeni za CCM jimbo
la Monduli, Paul Kiteleki kuwataka viongozi na makada wa

chama hicho kuepuka suala la kura za urais na kutaja jina la


Magufuli ili kuepuka kuchafua hali ya hewa inayoweza
kukinyima chama hicho hata zile za udiwani na ubunge.
Kwa wana Monduli, Lowassa ni nguzo muhimu. Wanampenda na
kumheshimu kwa kuwatendea mema mengi wakati wa uongozi
wake kama mbunge. Tunalazimika kufanya kampeni kwa
tahadhari na kupima upepo linapofikia suala la kuomba kura za
urais Monduli, alisema Kiteleki alipoulizwa alichowaeleza
wananchi kwa lugha ya Kimaasai.
Kiteleki alilazimika kuingilia kati kutuliza hali ya hewa
iliyokaribia kuchafuka baada ya makada wa CCM Amina Mollel
na Victor Njau kuomba kura za urais na kumtaja Magufuli
katika mkutano huo na kupokewa na kelele za Lowassa
Lowassa.na ishara ya vidole viwili inayotumiwa na Chadema
Kuhusu hali ya kisiasa Monduli, Katibu wa umoja wa vijana wa
ccm (UVCCM), mkoa wa Manyara, Ezekiel Mollel ambaye ni
mzaliwa wa Monduli alisema ingawa chama hicho tawala kina
wasiwasi wa kura za urais kutokana na imani ya wananchi kwa
Lowassa, lakini kina kinauhakika wa kushinda viti vya udiwani
katika kata 16 kati ya ishirini za jimbo la Monduli kutokana na
wananchi wengi kuendelea kukiamini CCM na wagombea wake wa
ubunge na udiwani.

You might also like