You are on page 1of 16

www.annuurpapers.co.

tz

Sauti ya Waislamu

Sheikh Azzan hoi Hospitalini Mnazi Mmoja Uk. 11

Waislamu wahoji mapingu yote ya nini

Matibabu Sheikh Azzan yasubiri Mahakama


Victor naye alikuwa gaidi wa LRA au Eta?
Tukihangaika na asidi Unguja Tusisahau taarifa ya bomu Arusha Pengo asaidiwe kabla hajakwama
Na Omar Msangi
THE Lord's Resistance Army (LRA), au kwa upande mwingine ikijulikana kama Lord's Resistance Movement, ni kundi la harakati za kijeshi linaloongozwa na Joseph Kony, ambalo linapigania kuona Uganda inatawaliwa kwa Amri Kumi za Mungu, kama zilivyotajwa katika Biblia. Taarifa mbalimbali za kitafiti na kisomi zinaonyesha kuwa LRA ilianzishwa ili kukabiliana na Jeshi la Uganda Uganda People's Defence Force (UPDF), wakati huo likiitwa National Resistance Army (NRA) kabla ya Rais Yoweri Kaguta Museveni, kukamata na kutawala nchi. Wakati huo, NRA/UPDF ilishutumiwa kufanya vitendo vya mauwaji, ubakaji, kutesa watu, uporaji na kuwatia watoto wadogo katika vita. U k i a c h a m i g o g o r o ya kikabila iliyokuwa imetawala Uganda na kwa muda mrefu ikawa haikupatiwa ufumbuzi, kilicholipua mapambano ya LRA ni mgogoro uliokuwa ndani ya jeshi. Kulikuwa

ISSN 0856 - 3861 Na. 1091 DHULQADAH 1434, IJUMAA , SEPT. 20-26, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Kamanda Mussa

Wakili wa Sheikh Ponda ataka shitaka lifutwe


SHEIKH Azzan Khalid Hamdan (kushoto). Sheikh Ponda Issa Ponda (kulia).

KAMANDA Mussa. n a s h u t u m a k u wa j e s h i limetawaliwa na watu wa Kaskazini mwa Uganda. Kulikuwa na kitu kikijulikana kama NRM/A, Luwero Triangle, wakipinga hali iliyokuwepo ambapo m a d a r a k a ya l i s h i k i l i wa n a wa t u wa K a s k a z i n i toka Uhuru, huku kijamii ikionekana kuwa wa-Kusini wanadhulumiwa. Na kwamba

Kesi yashindwa kuanza kusikilizwa Waislamu waitupa Tume ya Polisi

Inaendelea Uk. 4

2
www.annuurpapers.co.tz

Tahariri/Tangazo
Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

DHULQADAH 1434, IJUMAA SEPT.20-26, 2013

AN-NUUR

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Mahujaji wajiandae vyema na Hija


HIJA ni nguzo ya t a n o ya U i s l a m u iliyofaradhishwa kwa waumini kama tunavyojifunza katika katika Quran 3:97: Na Mwenyezi M u n g u amewawajibishia watu wafanye hija katika nyumba hiyo (Al-Kaaba) yule awezaye kufunga safari kwenda huko. Na atakayekanusha (asiende na hali ya k u wa a n a u we z o ) basi Mwenyezi Mungu si muhitaji anayewahitajia walimwengu. N d u g u katika Uislamu unayekusudia kufanya ibada ya Hijja mwaka huu, awali ya yote tunakupa hongera na kukutakia kila la kheri katika safari hii ya ibada. Y a k u p a s a umshukuru Mwenyezi Mungu kwa kukupa afya na uwezo katika kuiendea nyumba yake tukufu na kongwe iliyoko Makkah, ili kutimiza nguzo ya tano ya Uislamu. Hata hivyo, tunalazimika kutoa maoni japo kwa u f u p i , i l i k u we z a kuweka sawa baadhi ya mambo ambayo ni sehemu muhimu ya m a a n d a l i z i ya kuiendela ibada hii, ili yasije yakafanyika makosa iwe ni kwa kusahau au kutofahamu na kutia doa ibada hii adhimu k a t i k a m a i s h a ya Muislamu.

Siku hizi baadhi ya mahujaji wamekuwa wakifanya makosa kadhaa katika kutekeleza matendo mbalimbali ya ibada hii. Mtume (SAW) kawaamuru watu wachukue matendo na ibada ya Hijja kutoka kwake. Katika kipindi hiki, mwenye kujiandaa kuhiji safari hii anatakiwa akumbuke kufanye mambo kadha kabla kuingia safarini. Kwanza kabisa ni ni kutia nia kwa Allah (sw) aliyetukuka na k u t a k a s i k a ; k wa n i Allah hapokei ila kilichokuwa kwa ajili yake pekee. Hii ni hatua muhimu sana kwa Mahujaji wetu waratajiwa kuitimiza kabla ya kuondoka. W a l a hawakuamrishwa ila kumuabudu M we n ye z i M u n g u kwa kumtakasia dini, waache dini za upotofu, na wasimamishe sala na kutoa zaka, na hiyo ndiyo dini iliyo sawa (Albayyinah, 5) Mwenyezi Mungu ndiye wa kutakasiwa dini bila kushirikishwa (Az-zumar, 3) Mwenye kunuia kuhiji, ajipambe na tabia nzuri, ajizuilie nan a maneno na matendo machafu na maovu. Ajitahidi kuishi na watu kwa wema. Hujaji anatakiwa alete toba ya kweli kutokana na kila kosa alilofanya, ili aje kwa Mola wake akiwa msafi wa moyo. Ni sharti la muhimu sana kwa Hujaji kuwachia

wanaomtegemea matumizi ya lazima hadi atakaporudi kutoka Hija. M t u m e ( S AW ) anasema: Ni kosa la kumtosha mtu kuwatupa waliomlazimu. Ameipokea Bukhari. Ni jambo jema kwa Hujaji kuchukua mahitaji ya kutosheleza kwa ajili ya safari yake, ili abaki katika tabia ya kupendeza na kuwa huru wakati wote wa ibada ya hija. Imepokewa kutoka kwa Ibnu Abbas ( R A) a m e s e m a : Wa t u w a Ye m e n walikuwa wakihiji na hawachukui mahitaji ya safari wakisema: Sisi ndio tunaomtegemea Allah. Wakifika Makka huwaomba watu. Allah (SW) akateremsha kauli yake: Na jichukulieni mahitaji ya safari, kwani mahitaji bora ya safari ni uchaMungu. Ameipokea Bukhari na Abu Daud. Hujaji anahitajika alipe madeni yake, arudishe alivyoazima

na amana za watu, na aepukane na kila jukumu lililo juu yake. Ni vyema Hujaji kabla ya safari yake akaandika wasia wake na haki zilizomlazimu. M t u m e ( S AW ) anasema: Si halali kwa mtu Muislamu aliye na kitu cha kuusia kulala siku mbili ila na wasia wake umeandikwa, uko kichwani kwake. Ameipokea Rabiu, Bukhari na Muslim. Kabla ya kusafiri, Hujaji awatake radhi watu wa nyumbani kwake, jamaa zake, jirani zake na wenzake na awaage anapoondoka. Aidha anayekwenda Hija analazimika kujifunza namna ya kuhiji na mapema. Ifahamike kuwa ibada haiswihi kwa asiyeijua. Ni vyema a n a ye j i p a n g a k wa Hija, akachukua kitabu kilichokusanya mambo ya n a y o h u s u i b a d a ya hija kumwongoza vyema. Ibada ya Hija ni furaha na raha kubwa.

Ili kuondoa hofu au mashaka kwa Hujaji na akawa na furaha wakati wote wa kutekeleza ibada yake, ni jambo bora zaidi iwapo atafuatana na watu wema watakaomsaidia kutekeleza ibada za hija. Ajitahidi matumizi yake yawe ya halali yasiyo na shaka. Wajuzi wa ibada hii wanapendekeza s a f a r i i k a wa s i k u ya A l h a m i s i k a m a tunavyojifunza katika Sahihi mbili kutoka kwa Kaab bin Malik (RA) amesema: Mara chache Mtume (SAW) aliingia safarini siku isiyokuwa Alhamisi, ikiwa imempita basi ni siku ya Jumatatu; maana ndiyo siku aliyohama Mtume kutoka Maka. Baadhi ya wanazuoni wa m e s h a u r i k u wa Hujaji anaposafiri, basi aiage nyumba yake kwa rakaa mbili na aombe dua ya safari. Tunawatakia maandalizi mema Mahujaji wetu.

Ubungo Islamic high School


P.o. Box 55105 Tel: 2450069, 0712 974428, fax: 2450822 Dar es salaam. E-mail: ipcubungoislamic@gmail.com

MAANDALIZI YA KUJIUNGA KIDATO CHA I, 2014 (PRE- FORM ONE ORIENTATION COURSE)
UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL inatangaza program maalum ya maandalizi ya kujiunga na kidato cha kwanza 2014. Program hii itaanza tarehe 16/09/2013 hadi tarehe 16/12/2013. Jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa 2:00 kamili asubuhi hadi saa 9:00 Alasir. Masomo yatakayofundishwa ni:Elimu ya dini ya Kiislamu, English language, Lugha ya kiarabu, basic Mathematics na Computer. ADA: Ni Tshs 60,000/= (Elfu sitini) tu. Inalipwa yote kabla ya kuanza programu. Fomu za Kujiunga zinapatikana shuleni BURE baada ya kulipa ada. Mlete mwanao apate Elimu yenye tija itakayomweze kujiunga na kidato cha kwanza. Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba: 0714 888 557/0712 974428 Wabllah tawfiq Mkuu wa Shule

Wakili wa Sheikh Ponda ataka shitaka lifutwe


Na Bakari Mwakangwale kuanza kusikilizwa kesi hiyo na kuahirishwa tena kwa mara nyingine, ili hoja hiyo ifanyiwe kazi. Hakim amekubaliana na pingamizi la DPP k u wa S h e i k h P o n d a , asipewe dhamana na kesi imeahirishwa tena kufuatia ombi letu kwa Mahakama. Alisema Nassor. Hata hivyo wakili huyo a l i d a i k u wa H a k i m u Kabate, alitoa maelezo k u wa h a n a m a m l a k a ya kutengua pingamizi la DPP, na kwa mujibu wa sharia, pia hatakiwi kufafanua ni kwa vipi maslahi ya Taifa na usalama wa Taifa unahatarishwa na kwamba, DPP akisema ndiyo kasema. A m a k u h u s u Tu m e iliyoundwa na Jeshi la Polisi k u c h u n g u z a k u p i g wa risasi Sheikh Ponda Mjini Morogoro, Wakili hiyo alisema hajapata kusikia kama Tume hiyo imefanya kazi kwa usahihi tangu iteuliwe. Ninachoelewa ni kwamba Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, ndiyo inayoendelea na uchunguzi na imeshafanya mahojiano na baadhi ya wananchi mkoni humo na ndiyo ambayo Waislamu na wananchi kwa ujumla wanasubiriwa ripoti yake. Alisema wakili Nassor. Kwa upande wake Amir wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu mkoani Morogoro, Sheikh Ayoub Myinge, alisema Wa i s l a m u wa l i i k a t a a Tume ya Jeshi la Polisi na hawakutoa ushirikiano kwa Tume hiyo hivyo hawaelewi itakuja na itatoa ripoti gani. A l i s e m a Wa i s l a m u walitoa hoja kuwa wanahitaji kuhojiwa na Tume huru na si hiyo ya Polisi, kwa kuwa Waislamu ndio wanaowatuhumu polisi kumpiga risasi kiongozi wao. Wao (Tume ya polisi) wanalazimisha zaidi kutoa maelezo ya tukio hilo, Waislamu hatukuwa tayari, wametumia njia zao kuokoteza watu na kuwahoji kisha kupata m a e l e z o wa n a y o j u wa wao. Alisema Sheikh Myinge. Alisema ni jambo ajabu Waislamu wa Morogoro kuikubali Tume ya Polisi na kutoa ushirikiano kwao, kwani wao ndio waliofungua kesi dhidi Sheikh Ponda na Polisi hao hao ndio wanaoendesha kesi hiyo inayoendelea katika Mahakama ya Mjini Morogoro. Sheikh Myinge, alisema baadaye ilifika Tume za Haki za Binadamu na Utawala Bora, ambayo walikaa na Waislamu na walitoa ushirikiano kwa Tume hiyo kwa asilimia mia moja. A l i s e m a Tu m e h i y o ilikaa mjini humo kwa siku nne wakifanya mahojianao ambapo awali ilifika hospitali ya rufaa ya Morogoro na baadae kwa Waislamu na kisha kwa Jeshi la Polisi. Amir huyo alisema kuwa, yeye alisimamia kutoa mwongozo kwa Tume hiyo, ili kuruhusu mashuhuda (Waislamu) kutoa maelezo na ushirikiano bila hofu baada yeye kama kiongozi wa Waislamu kuridhika. Tulitimiza hili baada ya kuwasiliana na viongozi wa Kitaifa Jijini Dar es Salaam, pamoja na wakili we t u n a k u j i r i d h i s h a kwamba Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ndiyo inastahili kupewa ushirikiano, na mimi nilitoa muongozo kwa Waislamu. alibainisha Sheikh Myinge. Kabla ya kusikilizwa kesi hiyo, Waislamu kutoka sehemu mbalimbali nchini walikutana katika Ibada ya Itiqaf, usiku wa Jumatatu katika Msikiti wa Mungu Mmoja Dini Moja mjini humo na asubuhi yake walielekea mahakama ya mjini Morogoro. Hata hivyo Sheikh Myinge alisema Waislamu wanaishangaa Serikali kupitia Jeshi la Polisi, kutumia gharama na n g u v u k u b wa k a t i k a uendeshaji wa kesi hiyo kuliko uhalisia wa jambo lenyewe. Sheikh Ponda amerudishwa mahabusu Segerea baada ya mahakama kumnyima dhamana. K e s i imeahirishwa hadi Oktoba 1, 2013.

Habari

DHULQADAH 1434, IJUMAA SEPT.20-26, 2013

AN-NUUR

MAHAKAMA ya Hakim Mkazi Mjini Morogoro, imetakiwa kufuta mahamani hapo shitaka la kwanza linalomkabili Katibu wa Taasisi na J u m u i ya z a K i i s l a m u Nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda, la kudaiwa k u k i u k a m a s h a r t i ya hukumu ya kesi ya Kisutu. Wakili wa Sheikh Ponda, Juma Nassor, ameieleza mahakama hiyo Jumanne wiki hii kuwa, kosa hilo lilifikishwa Mahakamani hapo kimakosa. Hoja hiyo ilisababisha mvutano mkali wa kisheria baina ya Wakili wa Sheikh Ponda, na mawakili wa Serikali, hali ilimlazimu Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Richard Kabate, kuahirisha kesi hiyo kwa mara nyingine hadi Oktoba Mosi, mwaka huu. Hakimu Kabate, alilazimika kuahirisha kesi hiyo ili kutoa muda kwa Mahakama iweze kupitia vifungu vya sheria juu ya ombi la wakili wa upande wa utetezi kama shitaka hilo lifutwe au liendelee kusikilizwa mahakamani hapo. Wa k i l i N a s s o r o , alilieleza Gazeti hili nje ya Mahakama, kuwa shitaka hilo linalohusiana na kukiuka masharti ya hukumu ya kesi ya Kisutu, limepelekwa Mahakama ya Morogorogo kimakosa, k wa s a b a b u n i j a m b o linalopaswa kurudishwa k a t i k a M a h a k a m a ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam alipohukumiwa mtuhumiwa. Alisema kwa mujibu wa sheria, Mahakama iliyomhukumu ndiyo inayoweza ikapitia na kuona kama hukumu yake imekiukwa au la, badala ya kwenda kufungua kesi mahala kwingine. Awali wakili Juma Nassoro, alisema kwamba kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kusilikiza maamuzi ya kupatiwa dhamana Sheikh Ponda, ili kesi ya msingi iweze kusikilizwa. Hata hivyo alisema, baada ya Mahakama kukubaliana na pingamizi la DPP,la kuzia dhamana ya mteja wake, ndipo alitoa o m b i k wa M a h a k a m a ya kufutwa shitaka la kwanza, hatua ambayo imesababisha kushindwa

Matibabu Sheikh Azzan yasubiri Mahakama


Na Shaban Rajab KUFUATIA urasimu wa kupatikana kibali cha serikali kumruhusu Naibu Amir wa Jumuia ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMIKI),Sheikh Azzan Khalid Hamdam, kwenda kutibiwa nje ya nchi, huku hali yake ya afya ikiendelea kudhoofu hospitalini Mnazi Mmoja Zanzibar, sasa juhudi za zimeelekezwa mahakama kuu ya Zanzibar kunusuru hali. Taarifa zilizopatikana jana zimeeleza kwamba tayari wakili wa Sheikh Azzan, Bw. Salum Tawfiq, jana amewasilisha Mahakama Kuu ya Zanzibar barua ya kuitaka mahakama hiyo kumpatia ruhusa Sheikh Azzan, kwenda kutibiwa nje ya nchi kufuatia maradhi yake kukosa matibabu visiwani humo huku hali yake ikiendelea kudhoofu zaidi kadiri siku zinavyokwenda. Akizungumza na Annuur jana, mmoja wa viongozi wa Jumuia hiyo, Sheikh Saidi Amour, alisema ripoti ya madaktari inayoelezea juu ya maradhi ya Sheikh Azzan, wameipata Jumatano wiki hii baada ya kutolewa Jumatatu iliyopita. Ripoti ya madaktari tulikuwa tukiisubiri kwa muda, imetolewa Jumatatu wiki hii na wakili aliipata ripoti hiyo Jumatano. Tayari wakili ameshaandika barua ya kuomba dhamana na kuiwasilisha Mahakama Kuu, ili kumruhusu Sheikh Azzan kutibiwa nje kwa kuwa utaratibu wa serikali unazidi kuchelewesha matibabu yake na hali ya S h e i k h i k i e n d e l e a kudhoofu, alisema Sheikh Amour. Hali ya afya Sheikh Azza imeendela kudhoofu huku akiendela kukosa matibabu sahihi kufuatia madaktari kuibaibnisha kwamba maradhi yake yanastahili matibabu nje ya nchi. Tayari serikali kupitia Wizara ya Afya Zanzibar imeshabainisha kwamba Sh eik h Azzan hawezi k u t i b i wa h a p a n c h i n i na kwamba anatakiwa kupatiwa matibabu nje ya nchi. Hata hivyo serikali imeshindwa kumsafirisha Sheikh Azzan haraka nje ya nchi kwa ajili ya matibabu hayokwa kile kilichodaiwa kuwa kuwepo idadi kuibwa ya wagonjwa wanaotakiwa kusafirishwa kutibiwa nje ya nchi kwa utaratibu wa kiserikali. Iliibuka hoja ya kutakiwa matibabu ya dharura kwa Sheikh Azzan kulingana na hali yake ya maradhi, lakini hakuna hatua za dharura zilizoonekana kuchukuliwa hadi sasa. Sheikh Azzan amelazwa katika hospitali ya rufaa Mnazi Mmoja tangu Septamba mwaka huu baa da ya kupoteza nguvu akiwa mahaburu. Baadae ilibainika kuwa anasumbuliwa na maradhi ya figo, lakini madaktari wakabaini kuwa maradhi hayo hayawezi kutibiwa hospotalini hapo na kwamba anatakiwa akatibiwe nje ya nchi. Hata hivyo kumekuwepo n a u c h e l e w e s h a j i wa kibali cjha matibabu hayo serikalini, hali inayolazimu Sheikh kuendelea kuugulia hospitalini hapo. K u t o k a n a n a ucheleweshaji huo, Septemba 8 mwaka huu, J u m u i a ya U A M S H O iliiandikia serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Vikosi vya SMZ, ikiilalamikia serikali kuchelewesha matibabu ya sheikh huyo. Katika barua hiyo, UAMSHO ilidai kuwa u c h e l e we s h a j i h u o n i matayarisho ya mauaji ya makusudi kwa Sheikh Azzan Hamdani. Aidha sehemu ya barua hiyo ambayo nakala ya k e t u n a y o , i l i e l e z a katika siku arobaini za m wa n z o z a k u we k wa mahabusu Sheikh Azzan na wenzake, waliwekwa katika mahabusu maalum kila mmoja akifungiwa katika chumba chake kwa muda wa saa ishirini na nne, kwa siku arobaini bila kupata mwanga wa jua na kusababisha wengi wao kupoteza nuru za macho, baadhi yao kupata ugonjwa wa kutosikia harufu na wengine uziwi. Ilieleza barua hiyo kwamba siku ya Agosti 31,2013 Sheikh Azzan alizimia usiku na kupata nafuu siku ya Jumapili saa moja asubuhi, ambapo majira ya saa 2:00 asubuhi alipelekwa kwa machela hospotali ya rufaa Mnazi Mmoja ambako aliendelea kuzimia na kupata fahamu. Ilieleza taarifa hiyo kuwa baada ya madaktari kumfanyia vipimo walibaini kuwa maradhi yake hayawezi kutibiwa hospitalini hapo.

4
dhulma hiyo iliwezekana kwa sababu jeshi lilikuwa limeshikiliwa na watu wa Kaskanzini. Hoja na madai yakawa, lazima hali hiyo ikomeshwe. Walichofanya NRM/A, n i k u v u n j a ya l i y o k u wa makubaliano ya Nairobi (Nairobi Agreement),kitu kilichosababisha uhalifu mkubwa kufanyika dhidi ya watu wa Acholi. Hii ilikuwa ni pamoja na ubakaji, liwati, uporaji, kuharibu vyakula na mambo kama hayo. Na haya yalifanyika huku baadhi ya maafisa wa jeshi waliokuwa wa-Acholi wakishuhudia, jambo lililowafanya kujiunga na uasi, na hivyo kuishia kwa LRA. Hiyo ilikuwa mwaka 1986. Ilikuwa ni katika mazingira haya, kundi la waasi wa LRA lilizaliwa likiwa na malengo ya kukabiliana na walichodai kuwa ni uovu uliokuwa ukifanywa na NRA na hatimaye kuweka serikali itakayokuwa ikiongozwa na Amri Kumi za Mungu pamoja na mila za ki-Acholi. Itikadi inayoongoza kundi h i l i i m e t a j wa k u wa n i mchanganyiko wa Msimamo Mkali wa Kikristo (Christian fundamentalism) na imani/ tamaduni za Kiafrika (hasa Acholi). Kiongozi wake Joseph Kony, anajieleza kama mtume na msemaji wa M u n g u a l i ye t u m wa kumwangamiza Museveni na jeshi lake. Mtu huyu Joseph Kony, anayejitaja kama msemaji wa Mungu na anayetaka Uganda itawaliwe kwa Amri Kumi za Mungu, japo awali alisema kuwa kaja kuwanusuru watu wanaouliwa, kuteswa, kubakwa na kuporwa mali na jeshi la NRA, lakini mwenyewe amefanya ukatili wa kutisha ikiwa ni pamoja na kuuwa watu, ubakaji, kuwakata viungo, kupora na kuwatia watoto wadogo katika vita. Ni kutokana na haya yote, kundi la LRA, likatangazwa kuwa ni kundi la kigaidi. Jirani na Uganda kuna nchi inaitwa Somalia. Hii ni nchi ambayo kwa takriban miaka 20 sasa imekuwa haipo katika amani toka alipopinduliwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Siad Bare. Baada ya juhudi za kikanda na kimataifa kushindwa kutatua mgogoro wa nchi hiyo, kupitia juhudi za Wasomali wenyewe, mwaka 2006 nchi ilipata amani, ikawa na serikali iliyoweza kuwadhibiti wababe wa kivita na wananchi wakaanza kuishi maisha ya kawaida kabisa. Hata hivyo, amani hiyo haikukaa muda mrefu. Nchi ikavamiwa, serikali iliyokuwepo ikangolewa madarakani, hali ya machafuko, mapigano n a m a u wa j i i k a r u d i n a kuendelea mpaka leo. Ni katika mazingira hayo, waliibuka vijana wa al Shabab, kupambana na wavamizi na baada ya mvamizi wa awali kuondoka (Ethiopia), na sasa kupambana na majeshi kutoka nje, yanayodaiwa kulinda amani. Hiyo ni mifano miwili ya makundi ya upinzani ya kupigania maslahi fulani na kupinga uvamizi/serikali,

Makala

DHULQADAH 1434, IJUMAA SEPT.20-26, 2013


waumini wao kujizuiya kulipiza kisasi. Hebu fikiria katika mazingira haya ya Kamanda Musa kupigia debe propaganda za al Shabab na madai ya baadhi ya wachungaji kuwa hivi ni vita dhidi ya Wakristo, hivi mtu mbaya akitokea na kulipua kanisa ambapo anahakikisha kuwa anauwa watoto na makumi kadhaa ya watu wasio na hatia, kuna Askofu ataweza kuwazuiya waumni wake wasilipe kisasi? Jumapili iliyopita, ilikuwa siku ya huzuni kubwa kwa wakazi wa miji ya Hillah, Iskandariyah, Karbala na Kut. Watu zaidi ya 58, wasio na hatia, waliuliwa katika kile kinachodaiwa kuwa ni mwendelezo wa chuki na machafuko ya kiitikadi, baina ya Wasuni na Washia wa Iraq. Umwagaji huo mkubwa damu ulisababishwa na m f u l u l i z o wa m a b o m u yaliyolipuliwa katika miji hiyo kwa nyakati tofauti, huku yakiacha mamia ya majeruhi. Watafiti na wachambuzi wa mambo wanakubaliana kuwa kabla ya uvamizi wa M a r e k a n i m wa k a 2 0 0 3 , Iraq haikuwa na mauwaji ya namna hii. Lakini pia upo ushahidi wa kutosha u k i we m o wa wa va m i z i wenyewe kwamba u g a i d i h u o u l i f a n y wa k u p a n d i k i z wa . N a m n a yake ilikuwa kuwa msikiti wa Mashia unalipuliwa, inasingizia kuwa ni Sunni wamefanya hivyo. Kesho unalipua wa Sunni unasema ni Shia. Kwa mtindo huo una uhakika kuwa baada ya muda wataendelea kuuwana wenyewe kwa wenyewe katika mtindo wa kulipizana kisasi. Hayo ndiyo yanayotokea Iraq hivi sasa. Lakini kuna wasiwasi pia kuwa mengi ya mashambuzi hayo kwa sasa, hufanywa na wale wale walioyaanzisha mara ya kwanza ili kudumisha kitisho cha ugaidi na kufanya nchi hiyo, isitulie. Kama wapo watu wanaoshabikia propaganda z a k u o n a Wa i s l a m u wanatangazwa kuwa ni magaidi, kwanza wafahamu kuwa ili kitisho cha kweli kitimie, lazima kwanza ufanyike ugaidi wa kweli. Patalipuliwa mahali na watakaokufa ni Watanzania, wakiwemo Waislamu na Wakristo. Pili, ili kitisho kidumu, milipuko na m a t u k i o k a m a h a y o ya kigaidi hayatakoma kama ambavyo tunasikia hivi sasa yakiendelea Pakistan, Afghanistan, Yemen na s a s a K e n ya . Tu t a d u m u nayo mwishowe tutaletewa Drone. Je, kwa propaganda hizi za al Shabab, hayo ndiyo tunayotamani yatufike? Kamanda Musa, hapo ndipo tunapokusudia kuifikisha Tanzania? La kuzingatia hapa ni kuwa tunapokubali kuwa washenga wa propaganda za kusimika ugaidi Tanzania, tufahamu kuwa madhara yatakuwa juu yetu sisi sote. S a s a t u n a u h u r u wa kuchagua: kuitosa nchi yetu ilipo Yemen na Pakistan au tuinusuru.

AN-NUUR

Inatoka Uk. 1

Victor naye alikuwa gaidi wa LRA au Eta?


katika Afrika. Ukija Ulaya kuna ETA. ETA ambayo ni kirefu cha maneno ya Kihispania, Euskadi Ta Askatasuna ("Basque Homeland and Freedom"), ni kundi la waasi katika nchi ya Hispania lililoanzishwa mwaka 1959 likipigania kujitenga na kuwa nchi huru majimbo saba yaliyo Kaskazini mwa Hispania na Kusini Magharibi wa Ufaransa. Katika kuendesha haraka hizo, Euskadi Ta Azkatasuna, Eta, ilianza kama harakati za wanafunzi wa k i p i n g a u t a wa l a wa udikiteta wa kijeshi wa generali Franco. Chini ya udikiteta wa Franco, lugha ya watu wa majimbo hayo saba (Basque), ilipigwa marufuku, utamaduni wao ukapigwa vita kama kitu kisichotakiwa kuonekana, imani za asili zikazuiwa na wasomi wao ambao walionekana kuwa wataongoza mapambano ya kupigania haki za wazalendo wa Basque wakawa wanakamatwa, kuteswa na hata kuuliwa. Baada ya kufariki dikiteta Franco mwaka 1975, zilikuja siasa za demokrasia ambazo zilisaidia watu wa Basque kupata madaraka ya ndani (home rule).Ukiacha ukweli kuwa bado nchi ya Basque, i n a d h i b i t i wa n a S p a i n , lakini ina Bunge lake, Idara yake ya Polisi, inadhibiti masuala yote ya elimu na kodi. Hata hivyo, bado ETA wanapambana kuhakikisha kuwa wanapata Uhuru Kamili na Madaraka Kamili. Ila tu kwa sasa wamepunguza sana vitendo vya kutumia nguvu na silaha katika kupigania madai yao. Wanakwenda zaidi kisiasa, mazungumo na kidiplomasia. Lakini ukirejea historia ya ETA, imefanya vitendo vya mauwaji na ugaidi wa kutosha mpaka kikastahiki kuitwa kuwa ni kikundi cha kigaidi. Wakati NRA, imebakia kuwa ni tatizo la Uganda, na ETA, tatizo la Hispania, mabeberu wenye agenda z a o S o m a l i a , wa n a t a k a k u t u a m i n i s h a k u wa a l Shabab ni tatizo la Tanzania, Uganda, Kenya na dunia, kama walivyofanya kwa al Qaida yao. Kwa bahati mbaya, kumekuwa na vipasa sauti ambavyo vikitiwa tu betri, huimba wimbo wa ugaidi wa al Shabab Afrika Mashariki. Wiki iliyopita kulifanyika uhalifu mwingine tena wa kumwagiwa tindi kali. Aliyemwagiwa na kuumia vibaya usoni na kifuani, ni Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Cheju, Zanzibar, J o s e p h M w a n g a m b a . Tumefahamishwa kuwa hivi sasa polisi wanafanya msako na uchunguzi ili kuwabaini waliohusika na uhalifu huo na tunaambiwa kuwa watu wapatao 15 wamekamatwa wa k i w e m o wa l i o d a i wa kukutwa na tindikali. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Kamishna wa Polisi Zanzibar, alisema kuwa miongoni mwa watu waliokamatwa ni vijana wanaojihusisha tu tuhuma za mauwaji. Hapakuwa na shitaka la ugaidi na mpaka leo haijulikani uchunguzi wa polisi umeishia wapi. Labda Kamanda Mussa atusaidie, yule mtuhumiwa wa Arusha naye alikuwa akijishughulisha na vitendo vya kundi gani la siasa kali za kidini? LRA au ETA? Kama kuna nia njema, mimi nasema kuwa iwapo ule uchunguzi wa bomu la Arusha ungefanyika kitaalamu, ukweli ukafahamika kuwa nini hasa kilitokea, nani wahusika na nini agenda zao, wala tusingepata tabu na haya ya tindikali au madai ya kuchomwa moto makanisa Zanzibar. Ila ukisikiliza kauli ya Kamanda Musa, ukirejea yale ya Uamsho na kauli za huko nyuma za wanasiasa wetu na makamanda wetu wa polisi, jambo lililowazi ni kuwa kumekuwa na kampeni kubwa sana ya kusimika kitisho cha ugaidi katika nchi hii. Na magaidi wenyewe, lazima wawe wa ki-al Shabab. Alipopigwa risasi na kufa Padiri kule Zanzibar, ilikuwa dhahiri kuwa kulikuwa na watu waliodhani kuwa huo ungeweza kuwa mlango wa kuingilia kutimiza lengo hilo. Kwa bahati mbaya baadhi ya vyombo vya habari vilihusika sana pamoja na baadhi ya makanisa ambayo hata hivyo kwa kujua ufadhili wao unapotoka, haikushangaza sana. Baadhi ya wachungaji wakatoa wito wa kulipiza kisasi na kusambaza taarifa za uwongo juu ya kuchomwa makanisa. Hata hivyo, baadhi ya Maaskofu wa Kanisa Katoliki, walionyesha ukomavu, umakini na uzalendo wa hali ya juu sana kwa kutoa wito kwa waumini wao waachane na mawazo potofu ya kulipa kisasi. Muadhama Polycarp K a d i n a l i Pe n g o , a k i wa kiongozi wa ngazi ya juu kabisa nchini kwa Kanisa Katoliki, alitimiza wajibu wake wa kiroho, kidini na kijamii kwa kuhimiza uvumilivu na kujizuiya na mawazo ya kulipa kisasi. Kwa hakika Watanzania wanatakiwa kuona na k u t h a m i n i k a z i k u b wa iliyofanywa na kiongozi huyo. Hata hivyo la kuzingatia ni kuwa kama kuna watu wamedhamiria kusimika kitisho na kiwe cha kweli, kwa mtindo huu wa matukio kama lile la Arusha ambapo polisi na wanasiasa wanatoa kauli kali, lakini mwisho wa yote haielezwi kesi imeishia wapi, hali kama hiyo inatoa fursa kwa matukio kama hayo kufanyika tena na tena hadi lengo la wabaya litakapotia. Katika tukio la kuuliwa Padiri Zanzibar, Maaskofu wa Kikatoliki walifanikiwa kuwatuliza waumini wao. Lakini kwa mtindo huu wa propaganda za ki-al Shabab na mwisho wa kesi za akina Victor kutokujulikana, wasiwasi ni kuwa itafika mahali viongozi wa dini watashindwa kuwazuiya

Kamanda Musa na imani kali za kidini na siasa zenye mwelekeo wa kikundi cha Al Shaabab cha Somalia. Alisema baadhi ya vijana hao walikamatwa wakitaka kwenda kujiunga na Al Shaabab na walikiri kuwa wanakwenda kupigana vita vya Jihad. Kwa mujibu w ataarifa za magazeti, Kamishna Mussa alipoulizwa baada ya mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na mahali ambako vijana hao walikuwa wanaelekea kupigana vita ya Jihad, hakueleza zaidi ya kusema wanawahoji zaidi kwa kuwa wana wasiwasi kuwa wanajihusisha na kikundi cha Al-Shaabab. Maelezo kama haya ya Kamanda Musa, si mara ya kwanza kusikika kutoka Idara ya Polisi. Mara kadhaa makamanda wetu wa Polisi, wamekuwa wakileta ngonjera na porojo za al Shabab na Boko Haram, wakilenga mambo mawili. Kwanza kutaka wananchi waamini kuwa al Shabab ni kikundi hatari cha kigaidi ambacho kinafanya ugaidi bila mipaka. Kwamba kutokea Mogadishu, kimesambaa Nairobi, Kampala na Dar es Salaam kufanya mashambulizi ya kigaidi. Pili, kuwaaminisha kuwa magaidi hao wapo nchini, na wana kambi zao za kutoa mafunzo ya kigaidi kwa vijana (wa Kiislamu na Masheikh zao.) ETA, japo imefanya sana vitendo vya kigaidi, Ulaya, lakini inajulikana kuwa walifanya hivyo kupigania kile wanachokitetea. Hutasikia ikisemwa kuwa ETA inapanga mipango ya k u l i p u a N e w Yo r k , Washington au Zanzibar. LRA nayo ni hivyo hivyo. Kule Arusha lililipuliwa bomu kanisani, watu wakafa na wengine kujeruhiwa vibaya. Tukaambiwa kuwa mlipua bomu alikuwa a m e k u s u d i a k u m u u wa Mwakilishi wa Papa nchini. Katika maelezo ya awali ikadaiwa kuwa lile lilikuwa ni shambulio la kigaidi. Hata hivyo baada ya kukamatwa mtuhumiwa Victor, hatujui mpaka leo zile tuhuma za ugaidi zimeishia wapi, maana hata mashitaka ya awali mahakamani yalitaja

5
WAKATI waasi wakiendelea kushindwa na majeshi ya serikali ya Syria katika medani za kisiasa na kijeshi, kundi linalojiita Muungano wa Kitaifa wa Wapinzani wa i s h i o n j e ya S y r i a , limemchagua Bw. Ahmad Twa'amah Alkhadhar, kuwa Waziri Mkuu wa muda wa serikali iliyotajwa kuwa ni ya mpito nchini Syria. Bw. Alkhadhar alichaguliwa na wapinzani wa serikali ya Damascus wanaoungwa mkono na serikali za Saudia na Uturuki Jumamosi iliyopita, katika kikao kilichofanyika mjini Istambul, Uturuki. Twaamah ni mgombea wa kwanza kuwania nafasi hiyo, akimrithi Ghassan Hito, aliyejiuzulu wadhifa huo mwezi Julai, kufuatia kushindwa kuunda serikali kutokana na kupingwa na Saudi Arabia. Muungano wa Kitaifa wa wapinzani waishio nje ya ya Syria ulimchagua Hito, mfanyabiashara mweye uraia wa Syria aishiye nchini Marekani Machi 18 mwaka huu, kuwa Waziri Mkuu wake na kumpa jukumu la kuunda serikali ya mpito ya Syria. Hata hivyo serikali hiyo bandia, ilikabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa wajumbe wa muungano huo wa wapinzani, akiwemo Mkuu wa zamani wa muungano huo Ahmad Moaz al Khatib, hali kadhalika Saudi Arabia. Kushindwa kwa Bw. Hito kuunda serikali hiyo ya muda, kuliuweka mwelekeo wa wapinzani wa serikali ya Damascus chini ya maswali mengi mbele ya madola yanayowaongoza wapinzani hao. Hii ni kwa sababu katika kipindi cha karibu miaka mitatu ya mgogoro wa Syria, kundi hilo siku zote limekuwa likishuhudia mgawanyiko

Habari za Kimataifa

DHULQADAH 1434, IJUMAA SEPT.20-26, 2013

AN-NUUR

Waziri Mkuu serikali ya Mpito Syria achaguliwa


k a t i ya wa j u m b e wa k e sambamba na kufanyiwa mabadiliko mara kwa mara. Suala hilo linaashiria kuwepo mtafaruku baina ya wajumbe wa muungano huo, hivyo kuzidi kudidimiza malengo ya wanaowaunga mkono ambao ni baadhi ya n c h i z a K i a r a b u n a Kimagharibi. Bw. Ghassan Hito alijiuzulu wadhifa wake siku mbili baada ya kuchaguliwa Ahmad Assi Jarba, ambaye ni mtu wa karibu sana na Saudia. Kabla ya hapo na baada ya kujiuzulu Moaz al Khatib, Mkuu wa zamani wa mungano huo George Sabra, alipewa kazi ya kuwaongoza waasi hao. Hata hivyo kutokana na tofauti nyingi za ndani, George Sabra naye hakuweza kufanikisha matakwa ya wajumbe wa genge hilo. K wa m u d a m r e f u s a s a waasi wa Syria waishio nje ya nchi wameshindwa kutatua ugomvi wao muda mrefu, hivyo kushindwa kabisa kuvutia ushawishi wa wananchi. Aidha wapinzani hao wameshindwa kuteua mwakilishi atakayeongoza timu yao ya mazungumzo katika kikao cha Geneva 2. Vinara wa chuki dhidi ya serikali ya Damascus, hususan Marekani, imekwishauonya Muungano huo wa Kitaifa wa Wapinzani kuwa ikiwa hautaweza kumchagua mtu wa kuongoza timu yao katika mazungumzo ya kikao cha Geneva 2, basi utakatiwa misaada. Ripoti zinasema kuwa, baada ya Ahmad Twa'amah Alkhadhar kuchaguliwa k u wa Wa z i r i M k u u wa kundi hilo Jumamosi usiku, hakugusiakabisa mizozo

Sudan yaitaka Waasi wasalimisha silaha jeshi la Syria Marekani iache kuituhumu kwa ugaidi
KHARTOUM Serikali ya Sudan imeitaka Marekani kuiondoa nchi hiyo katika orodha ya nchi zinazotuhumiwa kuunga mkono ugaidi. Hayo yamesemwa n a N a i b u Wa z i r i wa Mambo ya Nje ya Sudan, Rahmatullah Muhammad Othman, alipokutana na Donald Booth, mwakilishi mpya wa Marekani katika masuala ya Sudan na Sudan Kusini mjini Khartoum. Rahmatullah amesisitiza kuwa, Marekani inapaswa kuliondoa jina la nchi hiyo katika orodha ya nchi zinazotuhumiwa na nchi hiyo ya Magharibi kuunga mkono ugaidi, kwani hadi sasa hakuna ushahidi wowote unaoihusisha Khartoum na vitendo vya kigaidi. Amesema kuwa, serikali ya Khartoum inatarajia kuwa mjumbe huyo mpya wa Marekani nchini humo, ataweza kufanya shughuli zake kwa mujibu wa sheria za kimataifa. Marekani ililiweka jina la Sudan katika orodha ya nchi zinazotuhumiwa kuunga mkono ugaidi mwaka 1993.

RAIS Bashar al - Assad wa Syria


iliyopo baina ya wanachama wa kundi hilo wala na mauaji ya raia yanayofanywa na makundi ya kigaidi nchini Syria, badala yake alidai kuwa wapinzani wanakusudia kuanzisha Jamhuri mpya nchini Syria, ambayo ndani yake haitakanyagwa haki ya mtu yeyote yule. Wachunguzi wa mambo ya siasa za Syria wamesema kuwa, mabadiliko ya kila siku katika uongozi wa waasi hao yanasababishwa na mivutano mikubwa iliyopo baina ya wajumbe wa muungano huo, licha ya genge hilo kuungwa mkono na nchi mbalimbali duniani zikiwemo za Kiarabu na za Magharibi. Wakati hali ikiwa hivyo, k wa u p a n d e m w i n g i n e serikali ya Syria imeendelea kutotetereka katika kampeni yake ya kuyasafisha makundi ya kigaidi na kusambaratisha njama za maadui wa taifa hilo la Kiarabu. Wakati hali ikiwa hivyo, makumi ya waasi wenye silaha katikati mwa Syria wameendelea kujisalimisha kwa jeshi la nchi hiyo pamoja na silaha zao. Wakazi wa eneo Shanshar na katika viunga vya eneo hilo katika mkoa wa katikati wa Homs, wamejisalimisha kwa vikosi vya jeshi la Syria baada ya kukabidhi silaha zao na kuahidi kutobeba tena silaha na kwamba, watarejea katika maisha ya kiraia. Katika upande mwingine, vikosi vya jeshi la Syria vimegundua na kukamata idadi kubwa ya silaha na zana za kivita katika oparesheni waliyoifanya kwa ajili ya kurejesha amani katika moja ya mashamba ya eneo la Tadmur mkoani Homs, ambayo magaidi walikuwa wakiyatumia kama maficho yao. (irib.ir)

TEHRAN Meli zote za kivita za Jeshi la Wanamaji la Iran sasa zinasheheni ndege zisizo na rubani au drone zenye uwezo wa kuruka masafa marefu baharini. Hayo yamedokezwa na kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Iran, Admeli Habibollah Sayyari, ambaye ameongeza kuwa katika miezi michache ijayo Iran itazindua nyambizi mpya ijulikanayo kama Fateh (mshindi). Hadi sasa Iran

Meli za kivita za Iran zinasheheni 'drones'


i m e z i n d u a n ya m b i z i kadhaa za kisasa kabisa zilizoundwa nchini hapo huku ikikarabati kikamilifu zile zilizonunuliwa kutoka nje ya nchi. Admeli Sayyari amenukuliwa akisema kuwa hivi sasa Jamhuri ya K i i s l a m u ya I r a n inakaribia kujitosheleza kikamilifu katika uundaji na ukarabati wa nyambizi za kisasa zaidi duniani. Katika miaka ya hivi karibuni, Iran imepiga hatua kubwa katika kujitosheleza kwenye sekta ya ulinzi na usalama kwa kujitengenezea zana za kivita kama vile ndege, vifaru, manoari, nyambizi na rada. Iran imesisitiza kuwa uwezo wake mkubwa wa kijeshi si tishio kwa nchi yoyote, kwani sera yake ya ulinzi imejengeka katika msingi wa kujihami. Katika hatua nyingine, M k u u wa S h i r i k a l a Nishati ya Atomiki la Iran, Dk. Ali Akbar Salehi, amesema kuwa serikali ya Urusi itakabidhi kituo cha nyuklia ya Bushehr, kilichopo Kusini mwa Iran ifikapo tarehe 24 ya mwezi huu. Ali Akbar Salehi ameongeza kuwa, zoezi la kujaribiwa na hatimaye kukabidhiwa kituo hicho kwa wataalamu wa Irani litachukua muda wa siku 14. Ameongeza kuwa, pamoja na kwamba wataalamu wa Irani watakabidhiwa rasmi kituo hicho, lakini wa t a a l a m u wa U r u s i wataendelea kuwepo hadi kitakapomalizika kipindi

cha dhamana. Ijumaa iliyopita Rais Hassan Rohani wa Iran, aliku tana na kufanya mazu ngumzo na Rais Vladmir Putin wa Urusi wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) huko Bishkek, Kyrgyzstan na kusisitiza kuwa m a z u n g u m z o k a t i ya Tehran na kundi la 5+1 yanapaswa kuandaliwa haraka ili utafutwe ufumbuzi wa mizozo dhidi ya miradi ya kuzalisha nishati ya nyuklia ya Iran. (irib.ir).

6
Na Said Rajab
HII inayoitwa vita "dhidi ya ugaidi" imewafanya Waislamu duniani kote wamulikwe na vyombo vya habari vya kimataifa. Kila siku inayopita kuna matukio mapya kuhusu U i s l a m u n a Wa i s l a m u duniani, na vyombo vya habari vinatafatuta maoni ya Masheikh, wanasiasa, wasomi, viongozi wa taasisi na watu wa kawaida mitaani. Ingawa hiki ni kipindi kigumu sana kwa Waislamu duniani, lakini pia ni fursa kwao kutekeleza jukumu ambalo Mwenyezi Mungu ametuumbia. Mwenyezi Mungu anasema ndani ya Qur'an: "Nyinyi ndiyo umma bora kuliko umma zote zilizodhihirishiwa wa t u ( u l i m w e n g u n i ) mnaamrisha yaliyo mema na mnakataza yaliyo mabaya na mnamwamini Mwenyezi Mungu"Qur(3:110). U m m a wa Wa i s l a m u duniani unakabiliwa na shinikizo kubwa la kutakiwa kutoa maoni yanayolingana n a s e r a z a m a t a i f a ya magharibi, ikiwa ni pamoja na kutakiwa kufunga mdomo kuhusu madhila wanayotendewa Waislamu ulimwenguni kote! Kuna hatari mashambulizi ya propaganda dhidi ya Wa i s l a m u ya n a p o z i d i , Waislamu wakaanza kujitetea kwa kulegeza misimamo ya K i i s l a m u n a s h e r i a zake, kama wanavyofanya baadhi ya ndugu zetu. Ni jambo la msingi sana kwa Waislamu kutosalimu amri kwa kupindisha ujumbe wa Uislamu kwa sababu ya shinikizo hili. Lengo siyo kuzifurahisha serikali za magharibi. Badala yake, wanatakiwa kung'ang'ania kwenye misimamo ya Kiislamu na kufikisha ujumbe wa Uislamu kwa hekima na mawaidha mazuri, bila kuvunja msingi wowote wa dini, wala kuwadhuru Waislamu. Hili ni jukumu la Waislamu wote, wanaume, wanawake, wazee na vijana. Kiigizo chao bila shaka ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Masahaba wake. Ama, kuhusu majibu ya Sheikh Mohammed Issa, kwenye kipindi cha Dira ya Dunia kinachorushwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) wiki mbili zilizopita, kuhusiana na mgogoro wa Somalia, niseme tu ilikuwa bahati mbaya. Wakati mwingine si rahisi sana kwa Masheikh kutambua mbinu chafu za vyombo vya habari, au ajenda za siri zinazobeba mahojiano wanayofanya. Miye namfahamu Sheikh Mohammed Issa. Ni mtu makini, mahiri na mwenye ufahamu wa kutosha kuhusu siasa za ulimwengu na Waislamu. Alikuwa na dhamira njema kabisa wakati akijibu swali l a m wa n d i s h i wa B B C , isipokuwa mwandishi yule ndiye aliyeficha dhamira mbaya. Katumia majibu sahihi ya Sheikh kufanikisha malengo yake maovu. Nia hasa, siyo

Makala

DHULQADAH 1434, IJUMAA SEPT.20-26, 2013


yaliyoletwa na bwana wetu Masihi (Yesu) yanatoka kwenye chanzo kile kile" Mfalme Najash alisikiliza kisomo cha Qur'an kwa makini sana mpaka akamwaga machozi kwa jinsi Qur'an ilivyomgusa. Akasema, "Kwa kweli haya na kile ambacho Mussa ameleta, vinatoka sehemu moja. Ninyi wawili mnaweza kwenda, na kamwe sitawakabidhi watu hawa kwenu" Wale wajumbe wawili wa Maqurayshi wakaondoka kwenye Kasri la Kifalme vichwa chini na wakaanza kufikiria njia nyingine ya kukamilisha kazi yao. Siku ya pili wakaenda kwa Najash na kumwambia; "Waislamu wanasema mambo mabaya kuhusu Masihi, waite uwaulize kuhusu jambo hilo." Najash alifanya hivyo na Ja'afar alimjibu; "Siye t u n a s e m a k u h u s u Ye s u kile ambacho Mtume wetu amekileta. Yeye ni Mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Siyo Mungu wala mwana wa Mungu". Najash akawafukuza wale wajumbe wa Maqurayshi mikono mitupu. Hapa ndiyo kwenye hoja yangu ya msingi sasa. Kwa bahati mbaya, historia imemjenga sana mfalme Najash, katika tukio hili la Waislamu kuhamia Abyssinia. Mchango wa sahaba Ja'afar bin Abi Talib hauonekani wazi. Najash ndiye anayeonekana shujaa wa tukio lile la kihistoria. Miye silaumu hapa, wala roho hainiumi, kwanini mfalme Mkristo ameng'ara zaidi kwenye tareikh ya Waislamu kuliko Sahaba! Lakini, kweli kabisa, ukiwa mwandishi wa habari na m wa n a f u n z i wa ' M a s s Communication' kama mimi, lazima shujaa wako atakuwa Ja'afar bin Abi Talib katika tukio lile. Ja'afar, kama msemaji wa Waislamu, ndiye aliyemvuta Najash upande wa Waislamu. Ja'afar alikuwa 'Mass Communicator' aliyewiva kweli kweli! Kupitia makala hii ndogo, ningependa tumuangalie kwa makini Sahaba Ja'afar b i n A b i Ta l i b , k a m a msemaji wa Waislamu, ili tuchote mafunzo muhimu aliyotuachia. Somo la kwanza, ambalo Ja'afar amefundisha Waislamu kupitia hotuba yake kwa mfalme Najash, ni kwamba usilegezwe msimamo wa Sheria za Kiislamu, wakati unapowasemea Waislamu au kuwasilisha hoja za Kiislamu mahali popote. Wa i s l a m u w a l i k u w a kwenye wakati mgumu sana mbele ya mfalme Mkristo Najash. Kushindwa kujenga hoja madhubuti, kulikuwa na maana ya kurejeshwa Makka, ili kukabiliana na mateso zaidi na pengine kifo. Lakini, licha ya hali ngumu waliyokuwa nayo, hawakulegeza msimamo wa dini yao kwa kumfanyia rukuu Najash, ingawa hatua ile ingeweza kuwavurugia dhamira yao ya kuomba hifadhi. Lakini pamoja na kwamba Wa i s l a m u w a l i g o m a kumfanyia rukuu Mfalme Najash, walifafanua Inaendelea Uk. 11

AN-NUUR

kuendeleza mjadala huu, isipokuwa mambo kama haya yanapotokea, huacha mafunzo muhimu kwetu, i l i t u we z e k u r e k e b i s h a mapungufu na kutumia vizuri fursa zinazojitokeza kwenye vyombo vya habari, lengo likiwa kusukuma mbele ajenda za Waislamu na siyo za maadui wetu. Nimeona nitumie kisa cha Waislamu wa awali waliohamia Abyssinia (Ethiopia ya kale), ili kujenga hoja yangu, na ningewaomba sana Masheikh, wanazuoni, wahadhiri na viongozi wa taasisi za Kiislamu hapa nchini, ambao mara kwa mara huzungumza na vyombo vya habari wazingatie sana jambo hili. Tukisoma vizuri mfano wa Masahaba wakati walipohamia Abyssinia, tunaweza kuchota mafunzo mengi ya msingi, ambayo yanaweza kutumiwa mpaka leo na Waislamu. Wa i s l a m u w a a w a l i walipata madhila mazito yasiyovumilika kutoka kwa utawala wa Maqurayshi m j i n i M a k k a . Wa k a t i Maqurayshi waliposikia kundi la Waislamu, wakihofia kukufurishwa kwa nguvu, wamehamia Abyssinia, basi nao wakatuma wajumbe wawili kuwafuatilia. Lengo lao lilikuwa kuwaharibia Waislamu hao, wakitarajia kwamba mfalme wa A b y s s i n i a , a m b a y e alikuwa Mkristo, Najash, a n g e wa f u k u z a k w e n y e ufalme wake na kuwarejesha Makka kutokana na fitna watakayopika. Wajumbe wale walifika Abyssinia, wakawapa zawadi majenerali wa Najash, ili wasaidie kumshawishi mfalme awarejeshe Makka wakimbizi wa Kiislamu. Wale wajumbe waliwaambia majenerali wa Najash, "Kuna wapumbavu kutoka kwetu wamekimbilia kwenye nchi ya Mfalme; wameacha Dini yetu na hata yenu hawaikubali, na wameleta Dini mpya ambayo sisi na ninyi wote hatuijui. Wakuu wetu wametutuma kwenu ili mtusaidie kuwarejesha nyumbani. Naomba mtupe watu hao, sisi ndiyo tunaojua makosa waliyofanya." Wa j u m b e w a l e p i a walikula njama na majenerali wa Najash, wakiweka mazingira magumu kwa Mfalme kuzungumza na Waislamu, wakihofia wasije kumwambia ukweli ulivyo. Majenerali wakakutana na Najash na wakamshauri awakabidhi Waislamu kwa watu wao. Lakini Mfalme akataka kusikia kutoka kwa Waislamu wenyewe kabla hajaamua. Ja'afar bin Abi Talib, ndiye aliyekuwa kiongozi na msemaji wa Waislamu wa l i o h a m i a A b y s s i n i a . Wakati yeye na Masahaba wengine walipoingia kwenye mahakama ya Najash, wa l i g o m a k u m u i n a m i a Mfalme huyo, ikiwa ni ishara ya heshima, kama walivyofanya wengine wote

Masheikh na vyombo vya habari

Tujifunze kwa Ja'afar!

SHEIKH Mohamed Issa


ukumbini mle, wakiwemo wale wajumbe wawili wa Maqurayshi. Walipoulizwa kuhusu hili, Ja'afar alijibu; "Sisi ni Waislamu, kitendo kile ni mwiko kwetu kumfanyia yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu tu." Kisha Ja'afar akatoa hotuba yake, akiwasilisha Uislamu kwa Najash. Alisema, "Ewe M f a l m e ! S i s i t u l i k u wa watu wajinga na tuliishi kama wanyama wa porini. Mwenye nguvu miongoni mwetu akimtafuna mnyonge. Hatukuwa na sheria ya kutii i s i p o k u wa m a m l a k a ya kibabe.Tuliabudu masanamu yaliyotengenezwa kwa mawe au mbao, na wala hatukujua chochote kuhusu heshima ya binadamu". "Kisha Mwenyezi Mungu, kwa rehema zake, akatutumia mjumbe wake ambaye alikuwa ni miongoni mwetu. Tulijua kuhusu ukweli na uadilifu wake.Tabia yake ni ya kupigiwa mfano, na alikuwa ni miongoni mwa kizazi bora kabisa cha Waarabu". "Ametulingania kumuabudu Mungu mmoja, na ametukataza kuabudu masanamu. Ametusisitiza kusema kweli, na kuwalinda wanyonge, masikini, waadilifu, wajane na mayatima. Ametuamrisha kuwaheshimu wanawake na kutowadhalilisha". " Tu l i m t i i n a k u f u a t a mafundisho yake. Watu wengi katika nchi yetu ni wapagani, na hawakupenda sisi kuingia kwenye Dini hii mpya inayoitwa Uislamu. Wa k a a n z a k u t u t e s a , n a kutokana na mateso yao, ndiyo maana tumekimbia na kutafuta hifadhi kwenye ufalme wako." Wakati Ja'afar alipomaliza hotuba yake, Najash alimuuliza, "Je? Una chochote kutoka katika kile ambacho Mtume wenu amekuja nacho kutoka kwa Allah kunisomea?" Ja'afar alijibu, "Ndiyo" na akasoma Surah Maryam kutoka mwanzo mpaka pale Mwenyezi Mungu aliposema: "(Mariamu) akawaashiria kwake (yule mtoto wamuulize yeye). Wakasema: Tuzungumzeje na aliye bado mtoto kitandani?" (Yule mtoto) Akasema: "Hakika mimi ni mja wa Mwenyezi Mungu, amenipa Kitabu na amenifanya Nabii. Na A m e n i f a n ya m b a r i k i wa popote nilipo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai. Na (ameniusia) kumfanyia mema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, muovu. Na amani iko juu yangu siku niliyozaliwa na siku nitakayokufa na siku nitakayofufuliwa kuwa hai" Qur (19:29-33) Wale vigogo walio karibu na Najash waliposikia hivi wakasema, "Haya na yale

7
Na Alhaj Abdallah Tambaza

ZIMEBAKI takriban siku chache tu, Waislamu kutoka pande mbalimbali za dunia wataanza kumiminika katika miji mitakatifu ya Makkah na Madinnah, kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hijja. Ibada hii, hasa iliasisiwa na Nabii Ibrahim (A.S.W), miaka takriban 4000 BC (kabla ya kuzaliwa Yesu Kristo), pale alipoamriwa na Mola wake ahame kutoka kwao maeneo ya Iraq kwenda nchi ya Hijaz (Saudia Arabia siku hizi) na huko ajenge Kaaba tukufu kwa ajili ya kuabudiwa Mungu mmoja. Hijja ilifaradhishwa mwaka wa 9 AH, iliposhushwa Surat AlImran Aya 97 inayosema: Na Hijja katika nyumba ya Mwenyezi Mungu ni wajibu ambao ni deni analodaiwa mwanadamu na Allah, kwa wale wenye uwezo. Na katika Aya nyingine ya 196 ya Sura ya AlBakara, Allah anatuambia: Na ikamilishe Ibada ya Hijja na Umrah kwa ajili ya Allah na muuogopeni Allah. Hijja ni haki ya Mwenyezi Mungu; na kwamba kadri unavyoahirisha kwenda Hijja na uwezo unao,huachwi hivi hivi tu, ndivyo unavyozidi kujiongezea madhambi na kama utakufa hivyo, basi ni sawasawa na aliyekufa kama Myahudi, M n a s wa r a , a u K a f i r i yeyote yule! Allah (swt), amesema ametuletea Hijja katika miezi maalumu (Mfungo mosi, Mfungo pili, Mfungo tatu) ili papatikane mkusanyiko mkubwa wa watu (kiyyam lnnas), kutoka kila mahala kwa ajili ya kuonana na kuelewana; kustawisha jamii na pia kutupumzisha na mishughuliko mbalimbali ya kidunia. Amani, upendo na utulivu ndio sifa kuu ya miji ya Makkah na Madinnah, ni maneno ya Sheikh Amran Kilemile, aliyoyasema katika Semina ya Hijja iliyoandaliwa na Taasisi ya Tawheed katika Ukumbi wa Karimjee, Agosti 31 mwaka huu, iliyobeba anuani ya Falsafa ya Hijja. Aidha, miezi hiyo imekusudiwa iwe ni ya kuwapumzisha watu na misukosuko mingine,

vikiwamo vita, ukosefu wa amani na chakula. Miji ya Makkah na Madinnah, pamoja na ardhi yake kuwa ya jangwa, imebarikiwa neema nyingi za vyakula, utajiri mkubwa wa mafuta pamoja na maji ya Zamzam yasiyokauka. Mtu akiingia katika m a e n e o ya H a r a m , huwa amesalimika na maovu yote, kwani ni marufuku kabisa mtu kutenda tendo lolote la uovu katika maeneo hayo. Hata ukiokota kitu hapo kiache hapohapo; hakuna kusema ni riziki yako kama tufanyavyo tunapookota vitu ndani ya daladala hapa kwetu. Wenye kazi yao watakihifadhi kitu hicho mpaka mwenyewe apatikane. Tu l i wa h i k u a n d i k a katika makala za Hijja zilizotangulia kwamba, kusudio la Hijja, its essence and raison detra lilikuwa ni kwa Walimwengu wote na si kwa Waislamu peke yao kama inavyoonekana leo hii. Hakika nyumba ya kwanza waliyowekewa watu kwa ibada ni ile iliyoko Makkah, iliyobarikiwa na yenye uwongofu kwa WALIMWENGU wote. Ndani yake zipo ishara zilizo wazimasimamio ya Ibrahim na mwenye kuingia humo anakuwa katika amanina kwa ajili hiyo imewawajibikia watu kuhiji ndani ya nyumba hiyo na atakayekanusha Mwenyezi Mungu si muhitaji kwa walimwengu,(AlImran 3:96 97) Habari za Hijja zimetajwa kwa wingi sana ndani ya Qurani Tukufu. Ndugu yangu msomaji ukipata wasaa, basi ziangalie Aya zifuatazo ndani ya Qurani kwa faida zaidi: Surat Ibrahim: 37; Surat Nisaa: 124; Suratil Bakara: 125-126; Suratil Qasas: 57; Bakara: 198; Suratil Hajj 26,29; Suratil Assafat na nyinginezo nyingi. Hijja ina nguzo kuu nne, ikiwamo kuwa katika vazi la Ihram (zile shuka mbili nyeupe); kisimamo cha Arafah; kuzunguka Kaaba mara saba; na mwisho ni kutembea baina ya Safa na Marwa. Mambo mengine ni ya wajib na sunna, ambayo hata yakikosa kutendwa hayawezi kubatilisha Hijja ya mtu. Va z i l a I h r a m , linamkumbusha mja tukio la kufa na kufufuliwa lililo mbele yake; kwamba

Falsafa ya Ibada ya Hijja

Makala

DHULQADAH 1434, IJUMAA SEPT.20-26, 2013

AN-NUUR

atakuwa katika hali inayofanana na hiyo siku ya hesabu, hata kama alikuwa na mali na utukufu wa aina gani hapa duniani; na kwamba umati wote ulewatu milioni mpaka sita mbele ya Allah una daraja moja. Allah (swt) hakuiweka Kaaba tukufu mahala pale ilipo hivi hivi tu. Alijua anachofanya, maana yeye ndiye aliyeumba dunia hii na vilivyomo ndani yake. Mitandao yote ya Intaneti (search engines), sasa inathibitisha kwamba mahala ilipo Kaaba tukufu ndio katikati ya Dunia (center of the universe), na kwamba mji wa Makkah ndio mji ulio katikati ya ardhi kavu ya Dunia ukitoa bahari. (Mecca is the center of the dry land). Angalia google, wikipedia, yahoo, pamoja na cnn. com uone maajabu haya yalivyoelezewa. Kaaba tukufu ndio msikiti kiongozi, kwa maana ya kwamba misikiti yote duniani inaelekea kwayo. Hata kabla hujaizunguka Kaaba ile, kile kitendo cha kuiangalia tu na ukaishangaa na kuduwazwa (mesmerized) nayo, basi husababisha mja kupata thawabu zisizo na mfano. Pia, kila hatua anayotumia mtu kuizunguka anapanda daraja na kufutiwa madhambi. Habari zinasema, katika u s a wa i l i y o p o K a a b a kuelekea mbinguni, ipo nyumba nyingine ijulikanayo kama Bait lMaamur iliyopo peponi, ambayo kila wakati malaika 70,000 huingia

humo kumwabudu Allah na wakitoka hawapati nafasi kama hiyo tena, kwani wanaingia wengine 70,000. Wanazuoni mbalimbali wamekubaliana, kwamba mambo yanayofanyika kwenye nyumba hiyo (Bait lMaamur ) ndiyo hayo hayo yanayopatikana katika Kaaba. Wanasema hata lile jiwe jeusi Hajar laswed limedondoshwa kutoka huko. Pe m b e z o n i k i d o g o na Kaaba, kuna jiwe lililohifadhiwa ndani ya chupa yenye rangi ya dhahabu. Jiwe hilo lina nyayo (footprints) za Nabii Ibrahim zilitokana na kukanyaga mahala hapo wakati akipandisha mawe ya kujenga Kaaba miaka karibu 4000 BC. Mahala hapo patakatifu panaitwa Makamu Ibrahim, ambapo hujaji humpasa kusali raka mbili za sunna kwa heshima ya mahala hapo. Hijri Ismail, wengine hukiita Kisima cha Zamzam, ni sehemu n y i n g i n e ya m i u j i z a i l i y o p o p a l e k we n ye Kaaba. Hicho ni kisima cha maji ambacho kilipatikana k i m i u j i z a k wa m t o t o Ismail, kupigapiga miguu yake na maji yakatoka baada ya mamake Hajar kumlilia Mwenyezi Mungu kwenye vilima vya Safa na Marwa. Shina la kisima hicho, ambacho hutoa lita 39,000 kila saa, lipo karibu na A l K a a b a . M a j i ya k e hayakatiki na wala hayana tope wala vijidudu kama ya Dawasco. Pia hayahitaji dawa kusafishwa, kwani yenyewe ni tiba ya maradhi

mbalimbali. Maji haya ya miujiza, hunywewa kwa nia. Ukinuia yakate kiu basi ya t a f a n ya k a z i h i y o ; ukinuia iwe ni chakula basi yatakushibisha; ukinuia iwe ni pozo la maradhi basi Mungu hujaalia ikawa ndio tiba yako. Hutolewa bure na ni marufuku kuuzwa. Kunywa tani yako na mengine peleka zawadi kwenu utokako, hutaulizwa na mtu. Vilima vya Safa na Marwa ni mahala pengine patakatifu, kwani Hujaji anatakiwa azungukuke vilima hivyo mara saba, kukumbuka tukio la Mama Hajar, kutafuta maji. Atakapokamilisha anyoe au apunguze nywele zake. Hakika Safa na Marwa ni katika ishara za kuwapo kwa dini ya Mwenyezi Mungu,(Suratil Bakara 158). Siku ya Mwezi 9 Dhulhija, kwa mwezi muandamo wa Saudia, ndiyo siku ya Arafah. Mahujaji wote watakuwa hapo kuanzia asubuhi hivi na wawe wameondoka viwanjani hapo kabla ya swala ya Magharibi, ambayo

wataiswali Muzdalifah. Habari zinasema, hapa Arafah ndipo mahala ambapo baba yetu Adam na mama Hawa walipokutanishwa baada ya kutolewa peponi. Ni katika viwanja hivyo walipoanzisha kizazi hiki chote cha binadamu. Pia, ilikuwa ni hapo Arafah, Malaika Jibril alipomtafsiria Nabii Ibrahim (asw) maana ya ile ndoto kwamba Allah, amemtaka amchinje

Inaendelea Uk. 9

8
Na Said Rajab

Makala

DHULQADAH 1434, IJUMAA SEPT.20-26, 2013 sababu yoyote ya msingi. Hassan Nadal ni askari wa jeshi la Marekani na Robert Bales pia ni askari wa Marekani aliyekuwa nchini Afghanistan. Inaonyesha wazi k wa m b a , m a a n a ya haki kwa mtazamo wa Marekani, kuua watoto, wanawake na vikongwe wasio na hatia, siyo uhalifu mkubwa ambao mhusika anaweza k u p e wa a d h a b u ya kifo. Pia inathibitisha kwamba kelele zote hizi za haki za binadamu, haki za wanawake na haki za watoto ni za bure. Hazina ukweli ndani yake. Zinatumiwa tu na wanademokrasia wa Kimagharibi kukamilisha ajenda zao chafu. Ulimwengu wa Magharibi hautambui maana halisi ya haki za binadamu, wala hauna habari na rehema na mapenzi kwa watoto, wa l a h a u j u i h a d h i , heshima na utukufu wa

AN-NUUR

SIKU chache zilizopita, matukio mawili yametokea nchini Marekani, ambayo yamedhihirisha wazi sura halisi ya demokrasia ya kimagharibi, ikiwa ni pamoja na kubainisha maana ya usawa na haki kwa mtazamo wa Kamarekani. Wamarekani wawili, Robert Bales na Hassan Nadal, wote wameua watu na wote wamekiri makosa ya mauaji mbele ya mahakama ya Kimarekani. Mahakama imemnusuru mmoja wao na adhabu ya kifo na kumpatia mwingine adhabu ya kifo. Robert Bales, ambaye aliua watu wengi zaidi, alipewa nafasi ya kuishi na Hassan Nadal, ambaye aliua watu wachache zaidi, alihukumiwa adhabu ya kifo. Mahakama ya Marekani imempa Robert Bales, nafasi ya kuishi kwa sababu aliua watoto wadogo, wanawake na wazee, usiku wa manane wakati wakiwa wamelala majumbani mwao. Hawakuwa na nia ya kumuua au kumuumiza mtu yeyote. Na wala hawakuwa na namna yoyote ya kujihami. Na Hassan Nadal,

Maana ya haki kwa Marekani


timamu inaelekeza wazi kwamba mtu aliyemwaga damu ya watoto, wanawake na vikongwe wasiojiweza, ndiye aliyepaswa kupewa adhabu ya kifo, kwa sababu hakuridhika n a k u wa u a t u , b a l i alichoma moto miili yao baada ya kuwachinja. Lak i ni m a ha ka m a ya Marekani imefanya kinyume chake kwa sababu Hassan Nadal, ameua Wamarekani na Robert Bales ameua Waafghanistan! Kwa mujibu wa kanuni na taratibu za demokrasia ya Kimarekani, maisha ya Wamarekani yana hadhi na heshima kubwa zaidi na maisha ya watu wengine hayana thamani wala heshima. Hassan Nadal, amesema kwenye maungamo yake kwamba amewaua askari

Hassan Nadal,

alihukumiwa adhabu ya kifo kwa sababu aliwaua askari wa Marekani, mchana kweupee, tena kwenye kambi ya jeshi wak ati walipokuwa w a k i p e l e k w a Afghanistan na Iraq kwenda kutesa na kuua watu wasio na hatia, na tena walikuwa na uwezo na zana zote za kujihami. Mtu ambaye amewaua

askari hakuidhalilisha miili yao na akaiacha pale pale ilipofia. Mtu huyu amehukumiwa adhabu ya kifo. Lakini, kwa upande mwingine, mtu ambaye ameidhalilisha miili ya watoto, wanawake na vikongwe, kwa kuikata kata na kisha kuichoma moto, ameonekana anastahili kuishi. Mantiki yenye akili

Robert Bales

Jihad al-Hadad wale wa Marekani, ikiwa wanawake. ni hatua ya kulipa kisasi Ni dini tukufu ya kwa ajili ya raia wasio U i s l a m u t u , n d i y o na hatia wanaoteswa na inayolinda na kuhifadhi kuangamizwa nchini haki za binadamu wote. Iraq na Afghanistan. Kwa mujibu wa dini hiyo, A s k a r i w a l i o u a w a watu wote, hata wakiwa na Nadal walikuwa wakijiandaa kwenda wa rangi na kabila gani, wana haki sawa. Kwa Iraq na Afghanistan. Robert B a l e s mujibu wa demokrasia alin u s u r i ka a d ha b u ya m a g h a r i b i , wa l e ya kifo kwa sababu wenye nguvu tu ndiyo aliwaua watoto wadogo, wenye haki zaidi ('might wanawake na vikongwe is right') . Haizingatii ili kufurahisha nafsi k a b i s a h e s h i m a ya yake tu. Hakuwa na binadamu.

Makala

DHULQADAH 1434, IJUMAA SEPT.20-26, 2013


mmoja mtu mzima, anayeitwa Sheikh Khudhaifa. Msafara wake wa kuja msikitini unaongozwa na mapikipiki n a b a r a b a r a h u f u n g wa namna wafanyavyo marais hapa kwetu. Ndugu yangu msomaji jitayarishe kulia ukiswali nyuma ya babu huyu, kwani yeye anaweza kulia ghafla katikati ya swala akitokea kukumbana na maneno mazito ya Mungu. Lakini wakati mwengine atakuliwaza kwa sauti yake nyororo na maridadi. Sijui wewe, lakini mimi nilikuwa nalia naye bila kujijua! Ndani ya msikiti huo kuna eneo la mbele linalojulikana kama Rawdha. Ndani ya Rawdha ndipo ilipokuwapo nyumba ya Mtume. Kaburi lake, lile la Sayidna Abubakar na Sayidna Omar yamo humo pia. Ipo vilevile mpaka leo membar au dais aliyokuwa anatolea khutba zake za Ijumaa, ikiwa bado na uhalisia uleule wa kizamani. Pembeni yake ipo ya Abubakar pia. Nilipoziangalia vizuri nguzo za Rawdha niligundua ni za dhahabu. Taa zake k u b wa z i n a z o n i n g i n i a

AN-NUUR

Falsafa ya Ibada ya Hijja

Tawheed alitusimulia habari zake: Kabla ya kujengwa msikiti huu, Mtume alikuwa akiacha msikiti wake na kuja hapa jangwani kuswali swala za Iddi na zile za kuomba mvuasiku moja wakati wakiomba mvua ghafla pakafanya mawingu na mvua ikanyesha hata kabla watu hawajatimka. Kwa muujiza ule, kuanzia hapo pakaitwa eneo la Ghamama na ulipokuja kujengwa msikiti ukapewa jina la Ghamama. Msikiti huu umesheheni vitu vingi sana vya kihistoria ya dini ya Kiislamu. Matembezi yako ya m j i wa M a d i n n a h yatakufikish a Masjid

Inatoka Uk. 7
mwanawe Ismail. Mara moja Ibrahim (asw) na mwanawe Ismail walielekea maeneo ya Minna kutekeleza amri hiyo. Baada ya kuonyesha utii, Allah, aliwaletea kondoo wamchinje badala yake. Sunna hii ya kuchinja imetakiwa kuadhimishwa na Waislamu wote wakati wa Sikukuu ya Eid ludhhiya, k wa k u c h i n j a m n ya m a (mbuzi, ngombe, kondoo, ngamia). Hapa kwetu huwa hatuchinji kwa kisingizio cha kukosa uwezo na badala yake tunachinja kuku na kula pilau wenyewe. Subhanna! Ibrahim kakubali kuchinja mtoto, wewe hata mbuzi unaona ni ghali kumchinja kwa kutaka radhi za Mola wako? Hiyo ni imani dhaifu kabisa! Unakubali siku hiyo, iliyopewa jina la Siku ya Kuchinja (Eid lUdhhiya), ipite na wewe ukose t h a wa b u z o t e z i l e k wa ubakhili tu. Mbuzi wamejaa tele Vingunguti na watu wanaweza kuchanga na kununua mnyama wakanuia p a m o j a . T h a wa b u h i z i tunazoziacha zipite hivi hivi miaka nenda miaka rudi si zingetufaa siku ya siku kwa kuziba mapengo? Kilima cha Jabal Rahma kiko hapo maeneo ya Arafah pia. Mahala hapo ndipo aliposimama Mtume Muhammad (asw) katika Hijjat Lwadaa (Hijja ya Kuaga) na kutoa khutba yenye maneno ya kupigiwa mfano akisisitiza uadilifu wa viongozi na utoaji wa haki hasa kwa wanawake. Ni hotuba muhimu sana kwa walimwengu mpaka leo hii.

kama leo hii viongozi wa kidunia wa sasa wangeisoma khutba ile, basi duniani leo hii watu wangeishi pasi na uonevu, dhulma na aina yoyote ya uovu usingekuwapo asilaan!,Haya ni maneno ya Sheikh Twaha Banne, katika semina kwa Mahujaji iliyofanyika Ukumbi wa Karimjee Septemba 8, mwaka huu. Amesema: ukiwa katika viwanja hivi vya Arafah, ni fursa adhim ya kulia sana kwa Mola wako kwani hakuna siku nyingine i l i y o c h o m o z e wa n a j u a ambayo Allah huwaachia huru watumwa wake na adhabu ya moto kama siku hii ya Arafah. Kwa wale ambao hawatopata bahati kwenda kutekeleza Hijja, dini inawataka wafunge siku hiyo ya kisimamo, mwezi 9 na siyo mwezi 10 Dhulhija kama Masheikh wetu wa hapa kwetu wanavyotuelekeza. Alhaju Arafah! Na Arafah iko Makkah tu. Hakuna Arafah Mpwapwa wala Tandahimba. Ni vyema basi tukawa tunafunga mwezi 8, kama mwezi umeandama tofauti na nchi ya Saudia. Ubishi na misimamo ya kiitikadi inatutia hasarani tu. Ukiwa njiani unaelekea Muzdallifah, kuna eneo linaloitwa Wadi lMukhasir. Hapa ni mahala ambapo aliteketezwa Abraha na Jeshi lake la tembo wakati akijiandaa kuingia Makkah kuibomoa Kaaba. Allah (swt) alileta ndege hewani wakiwa na vijiwe vya moto vilivyoangamiza kila kitu. Kisa hiki kinasimuliwa vizuri ndani ya Qurani Suratil Fil

(Alamtara). Tu k i o h i l o n i k u b wa ambalo hata mazazi ya Mtume Muhammad yalikuwa yanahesabiwa kutokana na tarehe ya tukio la angamizo la jeshi la tembo. Tarehe ya kuzaliwa Nabii Muhammad ni 571 Miladia. Kabla ya Mtume hajahamia Madinnah, tarehe za Kiislamu zilikuwa zikihesabiwa kutokana na tukio hilo. Ni mahala pabaya na Mtume ameagiza watu wapite haraka mahala hapo. Hujaji huna hiyari hapo bali ni utekelezaji tu! Maana Mtume amesema Hudhuani manasikakum (chukueni kutoka kwangu kuhusu Hijja yenu). Jabal Hira, ni pango ambalo liko Mlima Noor. Ni mahala ambapo Mtume alifuatwa na Jibril na kusomeshwa Aya za mwanzo za Qurani Suratil Alaq (Iqra). Ni msitu mnene kwelikweli unaoogopesha kukutana na mtu usiyemjua akakupa habari nzito kama hizo. Ni mlima mrefu unaochukua takriban saa nzima mpaka kuupanda. Ghar Thowr, ni pango jengine ambalo Mtume alijificha na Sayidna A b u b a k a r , k u wa k i m b i a watu waliotaka kumwua wakati akielekea Madinnah. Kimiujiza, Allah aliweka tandabui mlangoni wakapoteza maboya na watu wale hawakuona kitu ingawa walifika mpaka hapo. K at ik a ziara yak o ya mji wa Madinnah, hujaji utapata fursa ya kuswali na kuutembelea Msikiti wa Mtume (Masjid Nabbawi). Ni msikiti mkubwa sana unaopendeza kwelikweli. Imam wake mkuu ni Babu

(hanging chandalliers) zinangara sana usiku kama mchana vile. Fursa inapatikana kwa wewe kwenda karibu na kaburi la Mtume kumwombea dua; halafu u s o g e e k a b u r i n i k wa Sayiddna Abubakar na Omar uwaombee dua pia. Wapi tena utaipata nafasi kama hiyo kuyashuhudia makaburi ya watukufu kama hao na kuwaombea dua? Ni ushahidi tosha kwamba wewe sasa darja yako imepanda!

Ukimaliza hayo utatokea mlango mkubwa unaoitwa Babu Jibril, mlango ambao umepitwa mara kadhaa na Malaika Jibril katika safari zake kwa Mtume. Wamepita pia maswahaba wakubwa wakubwa njia hiyo. Wapi utayapata hayo kama huendi Hijja? Swala moja utakayoisali katika msikiti huu ni sawa na swala 1000 za misikiti mingine. Kwa hiyo ukiwa Madinnah, ni lazima ujipinde kufanya ibada kisawasawa na kumwomba maghfira Mwenyezi Mungu akusamehe makosa yako. Hatua chache mbele ya msikiti huu, kuna eneo linaloitwa Bakhee. Hapo ni mahala alipozikwa Sayiddna Othman Bin Afan, watoto na wakeze Mtume pamoja na Maswahaba wengine. Ni mahala muhimu

Qubba, ambao ndio msikiti wa mwanzo kujengwa na Mtume nje kidogo na mji wa M a d i n n a h a k i t o k e a Makkah; na hapo ndipo mahala iliposwaliwa swala ya mwanzo ya Ijumaa. Mtume amesema mtu akijitwaharisha kutoka kwake na kwenda mahala hapo akaswali rakaa mbili, basi ni sawa kama aliyefanya Umra. Milima ya Uhud ni sehemu nyingine ya kutembelea, maana mahala hapo ndipo ilipopiganwa vita ya Uhud, a m b a v y o Wa i s l a m u 7 0 walipoteza maisha yao kwa kupigania dini hii. Makaburi yao yako pale likiwamo la Jemadari Sayyidna Hamza. Ni mahala panapohuzunisha sana. Mwisho, naona nichukue fursa hii kuwashukuru sana wa t u wa M a d i n a h k wa ukarimu wao waliouonyesha wakati wa Mtume, ambao mpaka sasa unauona ukitembelea sehemu mbalimbali. Shukrani za kipekee ziende kwa viongozi na wananchi wote wa Saudia kwa kuuenzi na kuutukuza Uislamu kwa kudumisha mila hii ya Nabii Ibrahim mpaka leo kwa kuandaa kila mwaka Ibada hizi za Hijja (single handedly), bila msaada wa nchi nyingine k a m a wa n a v y o f a n y i wa watu wengine wanapopewa kuandaa mambo ya kidunia kama mashindano ya Kombe la Dunia au Michezo ya Olimpiki. Nchi wenyeji hudai fidia kwa gharama zao. Kupokea kwa niaba ya

kupazuru ili kuwaombea dua watukufu waliozikwa hapo. Ukitembea kidogo upande wa nyuma ya msikiti huu, utakutana na Masjid Ghamam. Tukiwa hapo mwaka jana, Sheikh Abdallah N d a u g a , a l i ye o n g o z a matembezi ya kundi la mahujaji wa Taasisi ya

Allah wageni zaidi ya milioni sita; wale, wanywe, wasafiri na wapate pa kulala kwa kipindi cha mwezi mzima sio kazi ndogo. Mungu an alipa
hapa hapa. Leo Saudia ni nchi tajiri kupindukia! Sasa ndugu yangu Mwislamu, kama bado hujawazia kufanya safari hii, wakati ndio huu ili na wewe Mungu akulipe leo na kesho kama anavyowafanyia Wasaudi! Wabillah Tawfik! Simu: 0715 808 864

Email: atambaza@ yahoo.com

10
Siri haiitwi siri, itapozidi wawili Hata iwekwe nadhiri, filihali na fidhuli Watakiwa ufikiri, ili upate fisuli Jasiri alo msiri, wakumwambia amali Fanani mfananize, kwa umbo na sifa zake Nia asikutatize, aanzapo sekeseke Hamumu haiba ndize, maizi na uzishike Ujue usibakize, undani wa mboni yake Nami ninaye rafiki, Thabiti yake fanani Asokuwa mnafiki, mwenye kuchunga hisani Tupo sote kwenye dhiki, raha na hata tabuni Hababi yustahiki, jina lake Qurani Wa pili ni kikulacho, aliye nguoni mwangu Huyu nipo naye macho, nyendo zake na mizungu Chambilecho na uficho, nakama zake ni chungu Jina shetani na ndicho, chafitini walinwengu Taswira za mboni hizi, zina hakika kamili Rafiki yangu kipenzi, hakuachi bilikuli Ibilisi simenzi, atakupa idhlali idhilali Shetani yake mapenzi, yatakufanya fedhuli Qurani ndo halili, rafiki wa maishani Hasanati huhamili, akhera na duniani Shufaa siku himili, ikakutoa tabuni Shetani rafiki fuli, kiama atakuhini Na Nasri Kione nasriibrahimu@yahoo.com No: 0759202192

Mashairi/Makala

DHULQADAH 1434, IJUMAA SEPT.20-26, 2013

AN-NUUR

Ndani ya mboni yake

Ulimi nyama laini,yasifika kwa lisani Zitokazo akilini, za uzembe na makini Zanena ya fikirani, mabaya au ya shani Kauli ni tathmini, kupima wake undani Busuri zao bayani, wanojua duniani Kuna watu na shetani, tunu za hawa fanani Kazisifu burhani, vitabu vya rahmani Bilikuli havidhani, kathibiti Subhani Ulimi wake shetani, husema kwa dalihini Kwa hii yake fanani, Mola haupi auni Hupotosha buldani, kwa chambilecho pomoni Bui walo wanandani, Burkata na jioni Ulimih una hisani, wasakama yetu dini Wasemaji buharini, kunena uongo fani Semwa twavunja amani, magaidi limwenguni Mepenya mahakamani, atapata haki nani? Ulimi hauthamini, subu tele mdomoni Banati sasa ni duni,ulimi unawahini Swali chonyota kichwani, nikifanya tathmini Mwenendo huu jamani, wazazi hamuuoni Ulimi wangu jamani, wosia huu ni deni Usimseme fulani, kumsengenya jirani Kiumeni na kikeni, asiya za kudhani Ithbati ndo thamani, ya kuniponya moyoni. Tambua ukinihini, utawekwa na dayani Siku ya mwisho motoni, kwa dhambi za duniani Kaisome furqani, ujue wake undani Ikuponye maishani, pate ingia peponi. Na Nasri. I. Kione NO: 0759202192 nasriibrahimu@yahoo.com

Ulimi

NDUGU Mhariri wa gazeti letu tukufu la An-nuur, naomba nami unipatie nafasi japo kidogo niweze kutoa langu la moyoni. Agosti 10, 2013 siku ya Jumamosi majira ya saa 12:00 jioni, lilipotokea tukio la kusikitisha la kujeruhiwa kwa risasi begani Sheikh Ponda Issa Ponda. Tukio hilo lilifanywa na mmoja wa askari waliouzingira mkusanyiko wa waumini wa Kiislamu, waliokuwa wakihudhuria kongamano la Kiislamu lililofanyika mjini Morogoro. B a a d a ya t u k i o kupita takriban saa tatu, Kamanda Polisi mkoa wa Morogoro, alisikika akiutangazia umma kuwa Sheikh kajeruhiwa. Mbali na kujeruhiwa huko, alidai kuwa alikuwa akisakwa na jeshi la polisi ili afunguliwe m a s h t a k a ya k i l e

Sheikh Ponda ana haki ya kudai fidia


wa lich o d a i p olis i kuwa alitoa matamshi ya uchochezi, ambayo yalikuwa ni hatari kwa usalama wa nchi. B a a d a y a k u t h i b i t i k a kujeruhiwa Sheikh, m e n g i ya l i s e m wa kupitia vyombo vya h a ba ri. Mion g o n i mwa hayo ni wito uliotolewa na wa n a h a r a k a t i n a viongozi kadhaa wa d i n i , wa k i i i o m b a serikali ifanye haraka kuunda Tume huru kuchunguza na kubaini haraka sababu za Sheikh Ponda kupigwa risasi, nani aliyemfyatulia risasi na kumjeruhi. Si hivyo tu, vyombo vya habari viliutangazia umma kuwa, askari aliyehusika kumfyatulia risasi Sheikh alikamatwa ili kulisaidia jeshi la polisi katika suala zima la upelelezi. Wito wa kuundwa wa Tume na kutiwa mbaroni kwa askari huyo, ni ushahidi na uthibitisho wa wazi kuwa kitendo cha askari, ambaye ni mtumishi serikalini kumpiga risasi Sheikh, kilikuwa ni hukumu aliyohukumiwa Sheikh hata kabla hajafikishwa kwenye vyombo vya sheria. Hata kama Sheikh angekamatwa na kufikishwa mahakamani na akapatikana na hatia ya kuhatarisha amani ya nchi je, hukumu yake ingelikuwa ni kupigwa risasi hadharani? Sasa tujiulize, kama Sheikh alihukumiwa kabla ya kufikishwa mahakamani, na hukumu hiyo ikawa ni kupigwa risasi je, si kweli kuwa Sheikh atakuwa hakutendewa haki? Na je, kutoa maneno ya uchochezi, h u k u m u ya k e n i kupigwa risasi? Na serikali haioni kuwa ina kila sababu ya

NDUGU Waziri wa Mambo ya Ndani John Nchimbi. Tu n a l o j e s h i l a Ulinzi la Wananchi, JWTZ, kazi yake kuu ni kulinda mipaka ya nchi yetu Tanzania na usalama wake. Tu n a l o J e s h i l a Magereza, kazi yake kubwa ni kusimamia wafungwa. Tunalo Jeshi la Polisi ambalo kazi yake ni kulinda usalama wa raia na mali zao. Tunalo jeshi ya kujenga Taifa, ambalo linajihusisha zaidi na uzalishaji na kuimarisha uzalendo wa vijana wetu. Tunacho kikosi cha F F U k wa a j i l i ya kutuliza ghasia. Tu n a c h o k i k o s i cha zimamoto, kazi yake ni kupambana na maafa na majanga pale yanapotokea. Pia tunavyo vikosi vya mgambo ambavyo mara nyingi huajiriwa na Halmashauri za Miji na Manispaa za Miji. Aidha inafahamika

Barua ya wazi kwa Mhe. Nchimbi


kwamba katika miaka ya h i v i k a r i b u n i , zimeanzishwa kampuni za binafsi za ulinzi ambazo zimeajiri watu, baadhi yao wakiwa ni mgambo, wastaafu wa majeshi n.k kwa ajili ya kulinda mali za wateja wao. Lakini kwa muda mrefu limekuwepo hili jeshi linaloitwa Jeshi la Wokovu lililo chini ya Kanisa, lenye kambi yake maeneo ya makutano ya VETA Chang`ombe na barabara ya Kilwa karibu na JKT. Hili jeshi la wokovu kazi yake nini kwa umma wa Watanzania. Lakini tufahamishwe zaidi k wa m b a we n z e t u wamepataje kibali cha kuwaruhusu kumiliki jeshi hilo, na labda nihoji zaidi kwamba, kama kuna utaratibu kwa madhehebu ya dini kumiliki jeshi la kiroho? Na kama upo utaratibu huo upo je? N d u g u Wa z i r i Nchimbi, sisi raia tunataka kupata maelezo kutoka kwako kuhusu Kanisa kuwa na jeshi la wokovu la kiroho ili kuondoa maswali ambayo baadhi yetu bado hatuna majibu yake. N d u g u Wa z i r i Nchimbi, Serikali inasema haina dini, kwanini siku ya Jumamosi na Jumapili serikali imebariki kuwa siku za mapumziko kitaifa na nafasi kwa wafuasi wa madhehebu ya Wakristo kutekeleza inada zao lakini nafasi hiyo haipatikani Ijumaa kwa wafuasi

kumfidia kutokana na ulemavu ambao ameupata Sheikh kutokana na kuathirika viungo vyake? Nionavyo mimi, madai ya fidia yalistahiki kufanywa haraka sana baada ta tukio la kujeruhiwa Sheikh Ponda. Hakuna mtu yeyote katika huu ulimwengu anayefahamu thamani ya mwili wa mwanadamu isipokuwa yule aliuumba tu. Hivyo basi, ifahamike kuwa mwili wa m w a n a d a m u haulinganishwi na kitu chochote, hata kama kitu hicho kitakuwa na thamani ya trilions za shilingi. Natoa wito kwa wanasheria wanaomtetea Sheikh Ponda, wafanye haraka kufungua kesi ya mad ai ili Sheikh alipwe haraka iwezekanavyo. Mzee Himidi Athumani D o d o m a Tanzania.

wa Kiislamu? Ta f a d h a l i N d u g u Wa z i r i N c h i m b i , tufafanulie hili pia ili kuweka mizani sawa. Mwaka mpya wa Kikristo ni siku ya mapumziko. Mwaka wa Kiislamu kitaifa hakuna mapumziko wala hautambuliki. Nasikia Waislamu nao wameomba siku ya mwaka mpya wao, nayo iwe ya mapumziko kitaifa, lakini bado hakuna majibu. Hili nalo Mhe. Waziri unaliona je hili. Mikidadi Ally Box 28001 Kisarawe.

Tuma barua, mashairi na maoni binafsi kwa E-mail ifuatayo: annuurpapers@yahoo.co.uk tutaichapisha bila upendeleo. Mhariri

11

Makala

DHULQADAH 1434, IJUMAA SEPT.13-19, 2013

AN-NUUR

Msiisaliti Zanzibar kwa maslahi binafsi


asilia. Narudia kusema na kusisitiza hakuna kundi linaloitwa Wazenjibara au Wa b a r a z e n j i i s i p o k u wa kuna Wazanzibari wanaoishi Tanganyika na Watanganyika wanaoishi Zanzibar. Kuishi upande wowote wa muungano hakumpotezei mtu utaifa wake wa asili. Hivyo jina la kujiita Wazenjibara ni ujanja tu wa kutaka kulinda maslahi binafsi chini ya kivuli cha wanyonge wenzangu na mie. Kunyimwa kitambulisho cha Uzanzibari sio kwa sababu ya kuishi Tanganyika kwani hata kule Zanzibar wapo watu wamenyimwa vitambulisho hivyo licha ya kuwa wao ni wazawa ambao hata siku moja hawajawahi kupanda meli kuja Tanganyika na wao hao tuwaite nani au tuwatie katika kundi lipi. Pia wanadai eti kuna Wa b a r a z e n j i ya a n i Watanganyika wanaoishi Zanzibar. Ni sawa wapo Watanganyika wanaoishi Zanzibar, waliokwenda kuhamia Zanzibar kuna sheria wakiifuata wanaweza kuomba kuwa Wazanzibari na wanaozaliwa Zanzibar ni sawa na Wazanzibari wengine hupata haki zote kama ni kupiga au kupigiwa kura na miongoni mwao tayari wamekuwa ni mawaziri na viongozi katika majimbo ya uchaguzi. Mifano si ipo au ni nadharia Mzee Hassan Nassor Moyo ni mmoja kati ya watu wanaojinasibu na kusema wazi wazi kuwa yeye ni Mzanzibari licha ya baba yake kuwa ni Mtanganyika kutoka Songea lakini yeye ni Mzanzibari mzalendo kindakindaki. Mzee Moyo inamuuma Zanzibar kwani ndio nchi ya k e n a wa l a h a j a j i i t a Mbarazenji kama walivyo wenzake wenye maslahi binafsi kuliko uzalendo wa nchi ya Zanzibar. Nikupongeze Mzee kwa ule msemo wa wazalendo wengi kuwa Zanzibar kwanza Shengesha baadae. Wanaojiita Wazenjibara wamewasaliti wenzao wa Zanzibar katika harakati za kudai Zanzibar huru kwa kutanguliza maslahi yao kuliko kuangalia maslahi ya walio wengi. Wanadai Wazanzibari wana fursa nyingi katika muungano hivyo ukivunjika watapata hasara kubwa. Hebu tujiulize ni Mzanzibari gani ambaye anataka muungano uvunjike na hata kama ukivunjika wale wote wanaoishi Tanganyika kutoka mataifa mengine wameungana au Wazanzibari na Watanzania kwa jumla waliopo nchi za nje kwa lengo la kuishi na kufanya kazi wapo huko kutokana na muungano? Nikimnukuu Mheshimiwa Mansour Yusuf Himid alipokuwa akihutubia kongamano ukumbi wa Salama, hoteli ya Bwawani mara baada ya kufukuzwa na CCM kuhusiana na msimamo wake wa Muungano, alisema: "Mwenziwe sitaki, basi". Sasa ya nini kujipachika majina ambayo hayapo na kutaka kuwapuruza wengine kwa masuala ya watu wachache. Ndugu zangu munaojiita Wazenjibara musitumie kichaka cha Wazanzibari kutekeleza mambo yenu hebu kuweni wawazi na sio kuwasemea kwani Wazanzibari wamesema wenyewe bila ya kuogopa kuwa tumechoka na sasa tuangalie upya. Hivi mnadhani ile dhana yenu ya dozi kamili mukimaanisha kuwa na serikali moja na nchi moja, ndio suluhisho la matatizo yaliopo? na vipi mutambuliwe nyinyi kama kundi maalumu munaojita Wazenjibara na wengine kuwaita Wabarazenji? Nasisitiza kuna Wa z a n z i b a r i wa n a o i s h i Ta n z a n i a B a r a k a m a k u n a h i t a j i k a k u u l i z wa waitwe au wafuatwe mitaani wanamoishi na kuulizwa maoni yao, na sio kusemewa na wafanyabiashara waliojibatiza jina la Wazenjibara. Hakuna anayepinga na kukataa muungano, isipokuwa uwe wa haki kama mmoja wa Wazanzibari alivyosema ukirithi nyumba mbovu unaikarabati ili iwe imara na kuendelea kuishi. Tuache maneno ya kuwadanganya wengine kuwa nyinyi ni popo hamjulikani kama ni wanyama ama ndege. Naona wamebeba kauli ya U V C C M ya k u s e m a tutayalinda, tutayatetea, t u t a p i g a n i a , t u t a ya e n z i potelea mbali. Kama ni hivyo, na wengine tayari wanasema kitaeleweka. Basi tusubiri huku tukizingatia kuwa Wazanzibari tayari wamesema wenyewe na h a wa k u w e k a m a wa k i l i wanaojiita Wazenjibara. Rasimu ya katiba iliyopo inatoa fursa ya mtu kuwa na uraia wa nchi mbili tusubiri ipite ili nyinyi munaodai kuwa ni Wazenjibara muwe Watanganyika kamili na wale Wazanzibari wabakie kuwa Wazanzibari na sio kutoa takwimu za bandia kuwa ongezeko la idadi ya watu

Na Rashid Alghafri
KWANZA kabisa sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia kuwa miongoni mwa waja wake wanaojua kusoma na kuandika licha ya kuwa sio msomi kama wanavyojiita au kuitwa wengine madaktari au vinginevyo. Baada ya hayo ningependa nizungumzie kile nilichokikusudia ambacho ni kuhusiana na kikundi cha watu wachache wenye maslahi binafsi kutaka kuwaburuza wengine ili kuwakingia kifua na kuwatoa sadaka na kafara. Ni ukweli usiopingika na ambao utabaki kuwa hivyo ya kuwa ndani ya Muungano h u u wa Ta n g a n y i k a n a Z a n z i b a r u l i o f i k i wa n a kufanyika takribani miaka hamsini sasa, ni wa nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar. Lakini la kushangaza ni pale linapotokea kundi na kujipachika jina wakijiita Wazenjibara na kudai wao si Wazanzibari halisi wala Watanganyika asilia jambo linalowapelekea kukosa haki zao za kimsingi kila upande wa muungano. H a k u n a Wa z e n j i b a r a na hao wanaojiita jina hilo ki-uhalisia na kisheria ni Wazanzibari kabisa wala hilo halihitaji mwanga kumulikwa na haki wanazodai kuzikosa sio kweli, kwani wanadai haki ya kupiga kura Zanzibar hata ya Rais wa Zanzibar na kusema hawapati kwa vile wao wanaishi huku Tanganyika, au kunyimwa kitambulisho cha Mzanzibari mkaazi. Nataka nisema hilo sio wanalolikusudia na wanaogopa kuwa wakweli k wa n i wa l e wa n a o t a k a kuwateka ili wabebe mabango na kuwakingia kifua wanaweza kukataa ukweli ukibainika dhidi yao. Suala la kupiga ama kupigiwa kura kwao ni jambo wanaloliona ni kupoteza wakati wao na kule kudai hawana kitambulisho cha Mzanzibari mkaazi si kweli wala wasilete kisingizio cha kuwa wao hawana kwa vile tayari wanaitwa Wazenjibara. Wale wote waliokuwa mstari wa mbele pale Ukumbi wa Karimjee wiki iliyopita n i Wa z a n z i b a r i a m b a o vitambulisho vilivyopo Zanzibar wanavyo na kama hawana tujiulize vipi wamepata paspoti Zanzibar wakati wanadai haki hiyo wanaikosa Zanzibar na kama wamepata hapa Tanzania Bara, vipi wapate hali ya kuwa wao si Watanganyika

Inatoka Uk. 6 msimamo wao huo katika namna ya kitaalamu, mpaka Mfalme Najash mwenyewe akawaelewa na hatimaye kukubaliana nao. K w a h i y o , unapowasilishwa ujumbe wa Uislamu, lazima zizingatiwe kanuni za Kiislamu wakati wote.Usifanyike udanganyifu, usengenyaji, wala kumpaka mtu matope, k u s i we p o k u t u k a n a a u kulegeza kanuni yoyote ya Kiislamu. Mbinu za kijinga kama 'ends justify the means' (njia yoyote inafaa mradi ufike), hazina nafasi katika kuwasilisha ujumbe wa Uislamu. Somo la pili ambalo Ja'afar bin Abi Talib ameliacha ni k wa m b a , u s i p i n d i s h we ujumbe wa Uislamu, wakati unapousemea Uislamu. Ja'afar alipoulizwa na Mfalme Najash juu ya mtazamo wa Uislamu kuhusu Nabii Issa (as), wala hakumung'unya maneno. Hakujaribu kuficha wala kupindisha mtazamo wa Uislamu. Alisema wazi Uislamu unamuona Nabii Issa, kama Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na si Mungu wala mtoto wa Mungu. Sasa yasipindishwe au kuficha baadhi ya mambo

katika Uislamu, ili kujenga mtazamo ambao utafurahiwa zaidi na serikali au vyombo v y a h a b a r i . Wa i s l a m u hawana sababu ya kuonea haya maadili yao kwa mujibu wa maandiko ya Kiislamu, na lazima wakatae madai ya mataifa ya Magharibi kwamba Uislamu ndiyo sababu ya ugaidi unaotokea duniani hivi sasa. Somo la tatu ni kuelewa hadhira unayozungumza nayo na mazingira yaliyomo. Najash alikuwa Mfalme Mkristo. Na mazingira yote pale ukumbini yalikuwa ya Kikristo. Sasa angalia jinsi Ja'afar alivyokuwa mahiri wa kutumia kwa usahihi fursa iliyopatikana kwa manufaa ya ajenda yake! A l i p o t a k i wa k u s o m a Qur'an, katika Aya zote zilizoshuka wakati ule, Ja'afar alichagua Aya kutoka Surah Maryam inayoelezea moja ya miujiza ya Nabii Issa (as). Unajua kwanini alichagua Aya za Surah Maryam? Alijua Najash angeweza kuhusisha mambo yale yeye mwenyewe. Na kweli kisomo kile kilileta athari kubwa kwa Mfalme Najash mpaka

Masheikh na vyombo vya habari

Mkoa wa Mjini Magharibi ni kubwa kuliko Mkoa wa Lindi. Hivi inaingia akilini kweli ninauliza kama alivyouliza mmoja kati ya wazalendo, makao makuu ya nchi kufananishwa na Lindi! Ni akili kweli? Mbona Dar es salaam kuna idadi kubwa iliyokithiri ya watu h a wa a m b i w i f u r s a i p o Manyara. Nyinyi walinda maslahi musiwauze Wazanzibari na nchi yao kwa thamani ya duka la madira, mabanda ya kuku, juisi za miwa na mashamba ya mananasi Bagamoyo. Kama kweli munawaonea huruma Wa z a n z i b a r i n a k u d a i wanafaidika na muungano ili hilo litimie, basi jaribuni kufanya cha kuonekana kule Zanzibar wafaidike na hapo muwambie hayo mutakayo kama watakusikilizeni na sio kutaka kuwafanya ngazi na kuwapandia ili kufikia munapo hitaji kwa maslahi yenu binafsi. Kudai wanasiasa wanaodai mfumo mwingine wa muungano wanafanya hivyo kwa kuwa wamekosa hadhi ya ushindani katika muungano ni sawa na matusi kwani kuna kigezo kipi cha ziada ambacho hawana. Wanao dai mfumo wa mpya wa muungano sio wanasiasa pekee, bali ni Wazanzibari wote ambao akili zao ni barabara na wazalendo kindakindaki. Ndugu zangu munaojipa na kujibatiza jina la bandia na kusaliti ndugu zenu, bora niwape pole na kuwambia wamechelewa na wamepitwa na wakati kwani Wazanzibari wameamka na sasa basi wamechoka na kudai waachiwe wapumue.

akalia. Je? angesoma Surat Kafiruun katika mazingira na muktadha ule, mambo yangekuwaje pale ukumbini? Kuelewa hadhira unayozungumza nayo na kuchagua mifano hai, ambayo hadhira hiyo inaweza kulinganisha katika mazingira yao ni muhimu sana. Tunapozugumza na vijana, wanataaluma, wasomi, wanasiasa au vyombo vya habari, ujumbe utabaki kuwa ule ule, lakini mitindo na mbinu za lugha hubadilika kulingana na muktadha, kama alivyosisitiza mhariri wa An-nuur kwenye toleo lililopita. Somo la nne, ambalo Ja'afar bin Abi Talib, kama m s e m a j i wa Wa i s l a m u amefundisha, ni kutoogopa kusema ukweli wa dhulma, hata akiwa katika mazingira magumu kiasi gani. Wa j u m b e wa w i l i wa Maqurayshi walijaribu kwa hila kumzuia Mfalme Najash asiwasikilize Waislamu, kwa sababu waliogopa Waislamu wale wangewaumbua kwa Mfalme. Lakini Ja'afar alipotoa hotuba yake mbele ya Mfalme, alifichua

mateso yote na unyama wa Maqurayshi, kwa namna hiyo, akijenga mtazamo wa mahakama ile dhidi ya Maqurayshi. Ja'afar bin Abi Talib, alikataa kabisa kunyamazia unyama wa Maqurayshi, hata kama yeye na wenzake, iwapo wangerejeshwa Makka, mateso yao yangekuwa makali zaidi. Mataifa ya Magharibi na mawakala wao katika nchi zetu hizi, wanatumia kila njia kunyamazisha sauti za wadhulumiwa. Mateso, propaganda, vitisho, vifungo virefu jela na mauaji, hutumiwa kuwafunga midomo wale wenye ujasiri wa kupaza sauti za wanyonge na kukosoa unyama wa watawala. Nimalizie tu kwa kusisitiza kwamba, hata ukiwa katika hali ngumu kiasi gani, muongozo wakati wote unaweza kupatikana kwenye kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna za Mtume wake. Pia inapaswa kusoma maisha ya Masahaba wa Mtume, ambao walikuwa ni binadamu wa makabila na mazingira tofauti, wenye uwezo mbalimbali na udhaifu, na ambao wameweza kufinyanga haiba zao kwa mujibu wa Uislamu.

12

AN-NUUR
MAKALA

DHULQADAH 1434, IJUMAA SEPT.20-26, 2013

AN-NUUR

12

SHAWWAL 1434, IJUMAA

SEPT. 20 - 26, 2013

Wanazuoni wa Kiislamu waitaka serikali kuunda Tume Maalim Seif arejea


Na Mwandishi Wetu SERIKALI imetakiwa kuunda Tume Maalumu kuchunguza wa kina wa matukio ya kupigwa r i s a s i n a k u m wa g i wa tindikali viongizi wa dini na wahusika wafikishwe kwenye vyombo vya sheria. Wito huo umetolewa na Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu nchini HAY-ATUL ULAMAA, jijini Dar es Salaam katikati ya wiki hii. Si mara chache, tunasikia matukio kama haya nchini bila ya kumjua muhusika wa dhuluma hizi. Sheikh Soraga, Sheha Mohammed Kidevu wa Zanzibar na mfanyabiashara maarufu Said Saad, wa Dar es Salaam, wote hao wamekuwa waathirika wa tindikali na hakuna aliyekamatwa kuhusika na matukio hayo, ilieleza taarifa ya wanazuoni hao. Wa n a t a a l u m a h a o wameeleza kuwa kwa mustakabali huo, wanalaani vikali kitendo cha kumwagiwa tindikali Padri wa Kanisa katoliki Jimbo Kuu la Zanzibar, Anselmo Mwang`amba. Katika taarifa yao kwa vyombo vya habari, iliyosaniwa na Mwenyekiti Umoja wa Wanazuoni hao Sheikh Amran Kilemile, imesema kuwa matumizi ya silaha za moto, kama alivyouliwa Padri Mushi na

Tanzania Muslim Hajj Trust Safari ya Hijja 2013 Uandikishaji unaendelea gharama za Hijja ni dola za Kimarekani $ 4200. Safari ni tarehe 5 na 7 Octoba, na Kurudi Tarehe 27 na 28 Octoba, 2013. Wahi kujiandikisha Sasa. Uandikishaji wa Hijja Zijazo 2014, 2015 kwa Kulipia kidogo kidogo, unaendelea. Simu: 0717 000 065, 0784 222 911, 0754 304 518, 0754 498 888 Au kupitia Tovuti yetu. www.hajjtrusttz.org.

Na Mwandishi Maalum Zbar MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amewasili nchini Jumatatu akitokea India alikokwenda kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya yake. Maalim Seif, aliwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdallah

SHEIKH Abdallah Bawazir, mjumbe wa HAY-ATUL ULAMAA. hivi karibuni kujeruhiwa vibaya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Sheikh Ponda Issa Ponda, ni matukio ya hatari ambayo yanaweza kubadili sura nzuri ya Tanzania. Taarifa hiyo imeeleza kuwa vitendo kama hivyo vinaashiria chuki baina ya Watanzania wenyewe kwa wenyewe, vitakapoachwa na kuendelea vitasababisha amani, utulivu, na busara kutoweka nchini. Sisi Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania (Hayatul Ulamaa) tunawasisitizia Watanzania wenzetu kurejea katika utamaduni wetu tuliokuwa nao karne nyingi zilizopita, utamaduni wa kuvumiana na kushirikiana katika kuilinda amani hapa nchini ilieleza sehemu ya taarifa hiyo. Hata hivyo wanazuoni hao wamewatahadharisha Viongozi wa dini na wengineo, kutokurupuka kuelekeza tuhuma kwa kikundi dhidi ya kikundi vingine na kwamba, si halali tukio kama hilo kuhusishwa na udini, Uzanzibar wala U t a n g a n y i k a k a b l a ya kufanyika uchunguzi na kupata dalili sahihi za kutosheleza.

Mwinyi Khamis. Mapokezi hayo ambayo pia yalihudhuriwa na viongozi pamoja na wafuasi wa Chama C h a Wa n a n c h i C U F , yaliambatana na shamra shamra mbalimbali za burudani. Maalim Seif, aliondoka nchini Agosti 24 mwaka huu kuelekea India kwa ajili ya uchunguzi wa k a wa i da wa a f ya yake, utaratibu ambao amekuwa akiufanyika tangu alipofanyiwa upasuaji wa goti miaka mitatu iliyopita.

DIKTETA wa zamani wa Tunisia, Zain al Abideen b i n A l i , a m e t e u l i wa kuwa mshauri wa mwanamfalme Bandar bin Sultan, Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Saudi Arabia. Ali ambaye alikuwa k i b a r a k a wa n c h i z a Magharibi, alikimbilia na kupewa hifadhi nchini Saudi Arabia, baada ya serikali yake kuangushwa na kungolewa madarakani na wananchi n a wa n a h a r a k a t i wa Tunisia mwaka 2011. Bandar bin Sultan, anatuhumiwa kuwa anaongoza na kuyasaidia kifedha na kwa silaha makundi ya kigaidi nchini Syria. Imeelezwa kuwa Bw. Ali baada ya

Dikteta wa zamani Tunisia awa mshauri wa mwana mfalme


kukimbilia nchini Saudi Arabia pamoja na familia yake, aliishi kwa muda wa mwaka mmoja mjini Jeddah kwenye kasri la kifalme la Fahd bin

Marekani yapinga Rais Bashir kushiriki kikao UN


NEW YORK SERIKALi ya Marekani imetangaza kuwa, inapinga Rais Omar Hassan al-Bashir wa Sudan kushiriki katika kikao kijacho cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imetangaza kuwa, tayari imeshapokea ombi la viza la Rais huyo wa Sudan kwa ajili ya kuelekea New York, kushiki katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa baadaye mwezi huu. Taarifa ya Wizara hiyo ya Marekani imebainisha kwamba, Rais al-Bashir anapaswa kwenda katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, yenye makao yake The Hague Uholanzi kujibu tuhuma za mauaji na jinai za kivita zinazomkabili. Hata hivyo Wizara hiyo haijasema kama itakataa kumpatia viza ya kuingia New York Rais huyo wa Sudan. Mwaka 2009 na 2010, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ilitoa hati ya kutiwa mbaroni Rais Omar al-Bashir akikabiliwa na tuhuma za kutenda jinai dhidi ya binadamu na mauaji katika jimbo la Darfur, Magharibi

Abdulaziz, mfalme wa zamani wa nchi hiyo na kisha akaelekea kwenye mji wa Abha, ulioko umbali wa kilomita 450 kusini mwa mji wa Jeddah.

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

mwa Sudan. Uhusiano wa Marekani na Sudan umezidi kuzorota ambapo wakati fulani ndege z a kivita za Washington ziliingia katika anga ya Sudan na kukishambulia kiwanda kimoja cha kutengeneza dawa jijini Khartoum, ikidai kuwa ni kiwanda chicho kinatengeneza silaha za sumu.

13

DHULQADAH 1434, IJUMAA SEPT.20-26, 2013

AN-NUUR

14

DHULQADAH 1434, IJUMAA SEPT.20-26, 2013

AN-NUUR

15

DHULQADAH 1434, IJUMAA SEPT.20-26, 2013

AN-NUUR

16

DHULQADAH 1434, IJUMAA SEPT.20-26, 2013

AN-NUUR

You might also like