You are on page 1of 7

www.annuurpapers.co.

tz

Sauti ya Waislamu

Waislamu Kigoma wataka Tume huru Uk.4

Nyakati ladaiwa kuandika uzushi


Latakiwa kuomba radhi la sivyo.
Na Mwandishi Wetu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar amesema kuwa kuwepo kwa ruhani nchi

ISSN 0856 - 3861 Na. 1087 SHAWWAL1434, IJUMAA , AGOSTI 23-29, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Ruhani Tanganyika ndio mzizi wa fitna muungano


Asema Mwanasheria Mkuu SMZ Serikali 2 ni kuifanya ZNZ robo koloni Asisitiza zilizoungana ni nchi mbili
ya Tanganyika na ruhani Serikali ya Tanganyika, ndio mzizi mkubwa wa fitna katika muungano.

Radio Imaan FM yatoka kifungoni


Na Shaban Rajab

Inaendelea uk. 6

Mashitaka mapya Ponda

WAISLAMU katika kongamano la Mwembeyanga Jumapili iliyopita.

Uk. 6

Redio imaan inatoka kifungoni Jumapili na hivyo kutarajiwa kuwa hewani kuanzia Jumatatu. Redio hiyo yenye makao yake mkoani Morogoro, i n a m a l i z a a d h a b u ya kufungiwa kwa kipindi cha miezi sita kurusha matangazo yake nchini. Ilifungiwa na serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA,

kurusha matangazo yake kwa kipindi hicho ambapo ilianza kutumikia adhabu hiyo na kusitisha kurusha matangazo yake Jumanne ya Februari 26 mwaka huu. Kulingana na muda wa adhabu uliotolewa na serikali kwa kituo hicho, ina maana kwamba adhabu hiyo itakoma Jumapili ya Agosti 25 mwaka huu. Hivyo kuanzia Jumatatu

Inaendelea uk. 4

2
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Tahariri/Habari
AN-NUUR
wakitumia zaidi neno vita dhidi ya dawa za kulevya, lakini vita yenyewe haionyeshi matunda zaidi ya kushuhudiwa vijana, nguvu kazi ya Taifa letu ikiendelea kuteketea kila uchao, kwa maslahi ya wabinafsi wachache. Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa watanzania wamechoshwa na nyimbo hizi za mapambao ya mdomoni dhidi ya m u h a d a r a t i , h u k u wakishindwa kuona matokeo yenye nafuu. Hii yote ni kwasababu

SHAWWAL 1434, IJUMAA AGOSTI 23-29, 2013


yawezekana kabisa wanaopiga propaganda hii, kwa upande mwingine wanaweza kuwa ndio v i n a r a wa m i a n ya ya biashara yenyewe. Katika mazingira haya, ni vyema serikali ikatafuta utaratibu mwingine wa kupambana na magwiji h a wa wa m i h a d a r a t i . Na utaratibu wenyewe uanze kwa kuwachunguza na kuwashughulikia kwanza watu wa serikali wanaojihusisha na biashara hii na baadae wa s h u g h u l i k i w e r a i a wengine. Hili likifanyika kwa dhati na bila hofu, tutafanikiwa. Basi ni vyema tukaanza kwa kumuunga mkono Dkt. Mwakyembe katika hili. Vinginevyo tutaendelea kupiga propaganda za debe tupu, huku vijana wetu wakiteketea. Mwisho wa yote, Taifa litasheheni nguvu kazi ya wa b w i a u n g a , n a hatimaye tuje kuongozwa na wabwia unga na wavuta bangi, na hapo ndipo tutakapotanabahi.

AN-NUUR

Habari

SHAWWAL 1434, IJUMAA AGOSTI 23-29, 2013 Kwa upande wake Ust. Othman Mzinge, pia ameliandikia barua gazeti hilo, akilitaka kumlipa fidia ya Shilingi Milioni Kumi (10,000,000/-), sambamba na kumuomba radhi ndani ya wiki moja. Uliadika habari zenye kichwa cha habari Sheikhe Ponda sasa atengwa, katika kikao hicho ulinitaja kwa jina kuwa nilikuwa kiongozi upande Wahadhiri wa Kiislamu ilisema sehemu ya barua yake kwa gazeti hilo. Ust. Mazinge, ameliambia gazeti hilo kuwa taarifa hiyo si sahihi, na kwamba hakushiriki katika kikao hicho, zaidi gazeti hilo limelenga kuwafitinisha Waislamu na kwamba toka habari hiyo itoke kwa upande wake imemsababishai u s u m b u f u m k u b wa kutoka jamii ya Kiislamu. Awali, Ust. Salim, alisema kwamba walilazimika kumona Wa z i r i E m m a n u e l N c h i m b i , b a a d a ya kutakiwa kufanya hivyo na viongozi wakuu wa Jeshi la Polisi, kufuatia kunyimwa vibali na Jeshi la Polisi kwa ajili ya kufanya Mihadhara ya Kidini. Alisema, walikuwa wa k i n y i m wa v i b a l i hivyo katika maeneo mbalimbali Mikoani, ambapo Polisi hugoma kutoa vibali wakisema, kuwa hawezi kuruhusu kwa kuwa Mihadhara imesitishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani. Baada ya kukutana na vikwazo hivyo alisema, walilazimika kuunda kamati ya kuonana na Kamanda Suleiman Kova, na kuongea naye juu ya suala hilo, ambaye aliwataka kwenda kuonana na IGP, Said Mwema, kulingana na suala lenyewe lilivyo. Kamati ilienda kwa IGP Mwema, na kuongea naye, hata hivyo naye alitutaka tukamuone Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Nchimbi, kwa kuwa yeye ndiye alitolea kauli suala hilo. Alisema Ust. Salim, akirejea maagizo ya IGP, Mwema. Alisema, kamati hiyo ilifanya mchakato na h a t i m a y e wa l i w e z a k u o n a n a n a Wa z i r i Nchimbi, na kumueleza vikwazo wanavyokutana navyo kufuatia kauli yake ya kuzuia Mihadhara ya Kidini. Waziri (Nchimbi) alitupa maelezo kupitia hotuba yake kwa viongozi wa Dini ya Kiislamu na Kikristo katika kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, yeye akiwa mgeni rasmi. Alisema Ust. Salim. A l i s e m a , Wa z i r i Nchimbi, aliwapa hotuba yake aliyoitoa siku hiyo kwa viongozi hao na kusherehesha kwamba yale yalikuwa ni maazimio ya Jijini Dar es Salaam, na hayakuwa mikoani. Alitupa hotuba yake kama muongozo kwa Maafande, watakaokuwa wakizuia kutoa vibali mikoani, alitueleza yale maazimio yalikuwa ni ya Mkoa huu (DSM) na siyo ya nchi nzima. Alisema, akifafanua maelezo ya Waziri Nchimbi. Alisema, katika maongezi hayo, walimuomba awe mgeni rasmi katika Kongamano watakalo liandaa litakalo zungumzia amani, ombi ambalo alilikubali. Ust. Salim, alisema walilazimika kurejea kwa Waziri Nchimbi, mapema hivi karibuni, kwa lengo la kumkumbushia ahadi hiyo ambapo, Kongamano hilo, linatarajiwa kufanyika Agosti 24, 2013. Ni katika kikao hiki, ndiyo gazeti hilo la Nyakati, likatengeneza habari kwa mtazamo na malengo yake kisha kuibuka na huo uzushi wake, wakati katika kikao hicho h a p a k u z u n g u m z i wa kabisa kuhusu Sheikh Ponda na wengine na hata Ust. Mazinge pia hakuwepo kama walivyo ripoti. Alisema Ust. Salim.

AN-NUUR

MANENO kama dawa za kulevya, yamekuwa wimbo uvumao kwa nguvu hivi sasa hapa nchini, lakini ukakosa wachezaji. Ni vigumu ikapita siku bila kusikia maneno haya katika vyombo vyetu mbalimbali vya habari. Wenye mamlaka na waliopewa dhamana, ambao kwa sehemu kubwa wamekuwa ndio vyanzo vya habari hizi za dawa za kulevya, tunawasikia wakitumia kila aina ya lugha, wakijitahidi kuwadhihirishia watanzania kwamba wanapambana vikali na biashara ya dawa za kulevya hapa nchini. Wa k a t i m w i n g i n e wanaonekana wakija na lugha za matumaini zaidi, pale wanaposema wa m e wa k a m a t a wa t u kadhaa wakisafirisha au wakitumia dawa hizo. Pamoja na jitihada zao za kujaribu kuonyesha kama wanawajibika kisawasawa kwenye vita hii, lakini pia utakuta miongoni mwao, pamoja na kupewa dhamana na serikali n a v y o m b o v ya d o l a , wamekuwa wakikumbwa na kashfa za hapa na pale za kuhusika kwa namna moja au nyingine katika biashara hii ya mihadarati. Tumeshuhudia vithibiti v ya m i h a d a r a t i k a m a cocaine vikipotea au kupungua ujazo vikiwa mikononi mwa polisi, tumeshuhudia maofisa wa polisi wakijihusisha na biashara za bangi, tumesikia madai ya kwamba baadhi ya maofisa wa vyombo vya dola wakihusishwa na rushwa katika biashara hii ya mihadarati n.k. Lakini zaidi, hata Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe, naye ameonyesha mashaka yake kwa baadhi ya watendaji wa vyombo vya dola kuhusika katika biashara hii. Nasi tunapata mashaka pia, iweje watumiaji wa dawa za kulevya Mateja wamejaa mitani chwaka, n a v y o m b o v ya d o l a vinawaona na vinafahamu fika kwamba ni watumiaji wa dawa za kulevya, lakini h a wa c h u k u l i w i h a t u a zozote. Si hivyo tu, tunajua fika kwamba watumiaji

Tuache propaganda dawa za kulevya

hawa kuna mahali wanaponunulia dawa hizo, jambo ambalo ni rahisi tu kwa maofisa wa vyombo vya usalama kuamua kufuatilia hadi kumfikia mhusika wa mwisho wa dawa hizo, iweje hatua hazichukuliwi na inafanyika hivyo kwa makusudia? Inakuaje dawa hizo zipenye mahala penye usamala wa hali ya juu kama viwanja vya ndege bila wahusika kukamatwa? Katika mazingira haya, ni wazi kwamba biashara ya dawa za kulevya hapa n c h i n i , k wa k i wa n g o kikubwa hufanywa na baadhi ya watu wenye mamlaka serikalini na wafanyabiashara wakubwa. Miongoni mwao ni watumishi wasio waaminifu katika vyombo vyetu vya dola, ambao hutumia nafasi zao kama mwavuli wa kufanya uhalifu wao bila kujulikana. Lakini pia tunaona kwamba kuna uwezekano mkubwa kwamba watumishi hawa wa serikali, kwa nafasi zao serikalini hutumiwa na wafanyabiashara wakubwa wa mihadarati, kwa kuwakingia vifua wasibughudhiwe katika maeneo yanayohusika na kuingiza au kutoa mihadarati, na wakubwa hao huambulia posho nene kwa kazi hiyo. Ndio maana utaona hata jeshi letu la polisi, linakuwa ngangari kweli kweli kuwadhiti waharakati kama akina Ponda au wanasiasa kama akina Dkt. Slaa. Hawa h u s h u g h u l i k i wa k wa gharamna yeyote na mara moja hufunguliwa kesi mahakamani. Lakini uhodari huo hauonekani kuwaangukia magwiji wa biashara za dawa za kulevya! Matokeo yake, watanzania wanaambulia propaganda tu kwamba dola ipo katika mapambano ya dawa z a k u l e v ya , we n g i n e

Waislamu Sumbawanga waonyesha njia


Na Mwandishi Wetu

Kufuatia msimamo uliowekwa na Shura ya Maimamu Manispaa ya Sumbawanga, kuwa kuanzia sasa Waislamu katika Manispaa hiyo watekeleze hadithi ya Mtume Muhammad ( S AW ) y a k u o n d o a munkari kwa mikono na kwa maneno, msimamo huu umeanza kutekelezwa tangu Ramadhani 28. A wa l i Wa i s l a m u walishuhudia matangazo yakiwa yanabandikwa sehemu mbalimbali yakisomeka kuwa kutakuwa na Disko toto na usiku la wakubwa kuanzia Eid Mosi. Jambo hilo lilisababisha viongozi wa Waislamu kuwatangazia waumini wajihadhari nalo na kutakiwa kubandua matangazo yote yanayotangua sikukuu ya Eid katika Manispaa hiyo. A i d h a v i o n g o z i wa K i i s l a m u wa l i k we n d a kuonana na Mkuu wa kituo cha Polisi Sumbawanga mjini kumweleza hasara zinazopatikana kwa madisko yatakayopigwa katika kumbi za starehe siku hiyo ya Eid huku wahusika wakitangaza kuwa ni kusherekea Eid. Mbali na hasara za kiimani, Waislamu hao walimtolea Mkuu huyo wa Kituo mifano kadhaa ya madhara ikiwa ni pamoja na Taifa kupoteza Maisha ya watoto katika disko toto la Eid kule mkopani Tabora na Dar es Salaam siku za nyuma, pamoja na kukithiri vitendo vya zinaa katika sikukuu na mikesha kama hiyo. Mkuu huyo alikubaliana na Ushauri wa Masheikh na kusema kuwa sababu zao ni za msingi, hivyo akaahidi

kushirikiana na Waislamu kukomesha uovu huo wa kupiga disko kwa ajili ya sherehe ya eid. Imeelezwa kuwa hatua hiyo iliwafanya Waislamu k u a n d i k a b a r u a k wa OCD tarehe 8/8/2013 na kuthibitisha msimamo wao na kufafanu taarifa waliyoifikisha awali. A i d h a wa l i b a n d i k a v i p e p e r u s h i vilivyoandaliwa na Shura ya Maimamu kutahadharisha kuwa Eid el Fitri ni ibada ya Waislamu, hivyo hairuhusiwi kufanya sherehe za kumuasi Allah (sw). Hata hivyo taarifa zilieleza kuwa ilipofika jioni walionekana askari wa FFU wakiranda na pikipiki na kuyabandua matangazo yaliyowekwa na Waislamu. Katika Baraza la Eid lilofanyika katika viwanja vya Msikiti wa Qiblatain siku ya Ijumaa ya Eid kuanzia saa nane mchana na kuhudhuriwa na halaiki ya Waislamu, mada kadhaa zilitolewa, lakini suala maalumu lilikuwa n i k u wa t a h a d h a r i s h a Waislamu kuwa kuna hila mpya inataka kuingizwa katika Misikiti na kuwavuruga Waislamu. Ilielezwa kuwa kuna mpango wa kufanya ushushushu Misikitini na kutoa taarifa Polisi. Kufuatia kuwepo mpango wa kuanzishwa kamati za usalama misikitini, ililezwa katika baraza hilo kuwa Mtume (SAW) ameamriwa na Allah (SW) kuwapiga vita makafiri na wanafiki kwa sababu makazi yao ni Jahannam, nako ni mahala pabaya sana. (TAWBA 9:73). Hata hivyo wakati mada hiyo ikiendelea, ghafla ilisikika milio ya mabomu.

Tukio hilo lilikuja kufuatia polisi kufika katika disko na kuwaona walimu wa M a d r a s a wa k i wa n j e , wakiangalia na kukagua kwa umakini kama kuna wanafunzi wao wanaotaka kuingia disko toto ili wawazuie. Hali hiyo imedaiwa kuwa iliwalazimu baadhi ya askari waliokuwepo katika maeneo hayo kuwapigia simu wenzao k i t u o k i k u u , wa k i d a i kuwa wamezingirwa na wanahitaji nguvu za ziada ambapo waliwasili na kuwatawanya Waislamu h a o k wa m a b o m u ya machozi. Katika kuhitimisha Baraza la Eid, Amiri wa Kamati ya Kundeleza Uislamu, alitoa taarifa ya matatizo yanayoukabili umma wa Kiislamu Sumbawanga, ambapo alisema, hivi sasa tarehe ya kufanyika mtihani wa taifa wa Maarifa ya Kiislamu imegonganishwa na zoezi la unyweshwaji wa vidonge vya chanjo kwa wanafunzi. Baada ya kufuatilia suala hilo, Amiri alitoa taarifa k u wa wa m e k u b a l i a n a na Mkurugenzi na Afisa Elimu kuwa, wanafunzi wa Kiislamu hawatapewa chanjo mpaka pale watakapomaliza mitihani yao kwa utulivu. Aidha Amir huyo alitoa taarifa ya unyanyasaji wa wanafunzi wa Kiislamu katika shule za sekondari za Mafulala na Kilimani, ambapo walimu Wakuu wa shule hizo waliwataka wanafunzi wa kidato cha pili kufika Ijumaa shuleni huku wakijua siku hiyo ni ni sikukuu ya Eid . Baada ya wanafunzi hao kukataa kwenda, wenzao waliendelea kufundishwa.

KATIBU wa BARAZA KUU la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ramadhani Sanze akiteta na Imam wa Masjid Mtambani, Sheikh Suleiman Abdallah katika kongamano la Waislamu Mwembeyanga Jijini Dar es Salaam.

Na Bakari Mwakangwale

Nyakati ladaiwa kuandika uzushi


Wahadhiri wa Kiislamu Tanzania hawakumtenga Sheikh Ponda. Imesema sehemu ya barua. Katika barua yao kwa Nyakati, kulitaarifu juu ya kile walicho kiita kukithiri kwa uzushi d h i d i ya Wa i s l a m u na Uislamu nchini, imesema, katika habari hiyo kuna mengi ambayo yamejitokeza ambayo hayana ukweli dhidi ya Umoja huo. Miongoni mwa hayo yaliyoripotiwa na gazeti hilo ambayo Umoja huo unadai ni uzushi ni kuwa limedai kwamba (Umoja huo) walimweleza Waziri Nchimbi, kuwa Serikali haipaswi kuwahusisha wa o n a wa t u k a m a Sheikh Ponda, ambao hufanya Makongamano yenye kuchochea chuki b a i n a ya Wa i s l a m u Wakristo. Walimweleza namna wanavyofanya shughuli zao, kisha walimueleza kile ambacho hufanywa kwenye Makongamano kama yale yanayofanywa na akina Ponda, Hamza na akina Sheikh Ilunga, ambayo huchochea chuki. Limeripoti gazeti

UMOJA wa Hadhiri wa Kiislamu Tanzania, umesema utalichukulia hatua za kisheria, Gazeti la Kikristo la Nyakati, kwa kupotosha taarifa ya kikao chao na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Emmanuel Nchimbi. Akiongea na Gazeti la An nuur, Ustadhi Rajab Salim, alisema kuwa wamelipa gazeti la Nyakati, siku saba kukanusha taarifa hizo na endapo watakaidi watalichukulia hatua za kisheria. Katika masharti waliyotoa, Umoja huo umelitaka Gazeti hilo la Kikristo, kuomba radhi kwa uzito ule ule kulingana na walivyoripoti katika upotoshaji wao na kulitaka kukanusha kuwa hawajamtenga Sheikh Ponda. Pa m o j a n a h a y o , tunaomba gazeti lako lituombe radhi ndani ya wiki moja, katika ukurasa wa mbele kwa maandishi makubwa k a m a m l i v y o f a n ya .

hilo la Nyakati, likidai ni maelezo ya Wahadhiri hao. Ust. Salim, alidai kuwa katika kikao hicho hawakumzungumzia Sheikh Ponda, wala y o y o t e k a t i ya h a o waliotajwa na gazeti hilo, zaidi ya kuonana na Waziri Nchimbi, kwa lengo la kukumbushia ushiriki wake katika Kongamano lao walilo andaa litakalo zungumzia juu ya amani. Hata hivyo, Ust. Salim, alisema uzushi mwingi katika gazeti hilo, ni kudai kuwa katika kikao hicho kwa upande wa Wahadhiri wa Kiislamu waliongozwa na Sheikh Othman Habib Mazinge, ili hali (Mazinge) hakuhudhuria kabisa katika kikao hicho. Tunataka likanushe habari hizo, kisha lituombe radhi kwani limetuzulia uongo kwa Watanzania hususan kwa Umma wa Kiislamu, kwa kudai kuwa Umoja huo umemtenga Sheikh Ponda, sisi tupo pamoja nae na hatupingani na harakati zake. Amesema Ust. Salim.

Waislamu Kigoma wataka Tume huru


Wakumbusha ya Mwembechai
wanazofanyiwa Waislamu nchini. Likasema, tamko hilo kuwa, badala ya kuwasakama Waislamu na Masheikh wao, kwa kuwaita wachochezi, ni vyema Serikali ikaunda tume huru ya kuchunguza madai na kero zao na si kuwaziba mdomo kwa kutumia nguvu ya dola. U k w e l i h u u unadhihirishwa na mlolongo wa matukio yaliyokwisha fanywa na Jeshi la Polisi nchini, dhidi ya Waislamu kama vile mauji ya kinyama ya Mwembechai Dar es Salaam, mauaji ya Imamu akitoka Msikini Zanzibar, na mengine mengi. Lilisema tamko hilo. Shura hiyo ya Maimamu Kigoma imeitaka Serikali na vyombo vyake vya usalama kufahamu kwamba kazi inayofanywa na Sheikhe Ponda na baadhi ya viongozi wa dini ya Kiislamu ni kuitahadharisha Serikali kuacha kufanya dhulma dhidi ya Waislamu. Ikafafanua taarifa hiyo kuwa hatua hiyo ya Masheikh kuyasema madhila dhidi ya Waislamu ni kutokana n a S e r i k a l i k u s h i n d wa kuchukua hatua madhubuti juu ya madai dhidi yake. Kuudhihirishia na kuufahamisha ummah juu ya dhuluma zinazofanywa na Serikali si uchochezi kama inavyodaiwa, bali ndio njia pekee itakayodumisha amani ya nchi endapo viongozi wa nchii hii watazingatia na kuyafanyia kazi. Lilisema tamko hilo. Tamko hilo lilibainisha

HABARI

SHAWWAL 1434, IJUMAA AGOSTI 23-29, 2013

AN-NUUR

Na Bakari Mwakangwale
SERIKALI imetakiwa k u u n d a Tu m e h u r u ya kusikiliza madai ya Waislamu nchini badala ya kuyafumbia macho na kutaka kujaribu kuwaziba m d o m o k wa m t u t u wa bunduki. Wito huo kwa Serikali umetolewa na Waislamu Mkoani Kigoma, katika tamko lao lililotolewa na Shura ya Maimam Mkoani humo, mwishoni mwa wiki iliyopita, wakilaani kupigwa risasi Sheikh Ponda Issa Ponda. Waislamu hao wamesema, wapo tayari kufanya maamuzi magumu endapo Serikali haitowachukulia hatua za kisheria wale wote waliohusika na shambulio hilo chini ya Kamanda wa Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile. Tunaitaka Serikali iache mpango wake wa kupuuza na kufumbia macho madai ya Waislamu na badala yake iunde tume huru ya uchunguzi itakayosikiliza kero za Waislamu na iwe t a ya r i k u ya f a n y i a k a z i majibu ya uchunguzi huo. Limesema tamko hilo. Tamko hilo limesema, Waislamu Mkoani Kigoma wa n a a m i n i k u wa t u k i o lililofanywa na Jeshi la Polisi kushambulia kwa kumpiga risasi hadharani Sheikh Ponda, ni mpango mkakati na muendelezo wa kuwahujumu viongozi wa Kiislamu wanaotetea haki na kupinga dhuluma

kwamba, malalamiko ya Waislamu na madai yote ya n a y o z u n g u m z wa n a Sheikh Ponda, na wale wote wanaomuunga mkono yana ushahidi wa wazi na wa kisayansi. Tamko hilo lilitaja baadhi ya kero hizo ambazo Waislamu wanaitaka Serikali kutenda haki katika makundi yote kuwa ni mkataba wa kifisadi kati ya Serikali na Makanisa (Memorundum of Understanding MoU), kwamba Serikali inatoa fungu kuyasaidia Makanisa peke yake. Kadhia nyingine imetajwa kuwa ni Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) linalodaiwa kutokufanya kazi na kutekeleza wajibu wake kwa uadilifu. Umetajwa pia mfano unaojitokeza mara kwa mara ambapo viongozi wa Kiislamu huwekwa rumande na kunyimwa haki yao ya dhamana. Shura hiyo ikafafanua

k wa m b a , Wa i s l a m u wanapenda amani ya nchi yao iendelee kudumu lakini ikaitaka Serikali kufahamu kuwa msingi wa amani ya kweli ni kusimamia haki kwa makundi yote yaliyo chini ya utawala wake sambamba na kuwatendea haki raia wake wote bila kujali rangi, Kabila, Dini na ukanda. Katika hatua nyingine Shura hiyo ya Maimam Mkoani humo, imesema haitakubaliana na taarifa yeyote itakayotolewa na tume iliyoundwa na Jeshi la Polisi. Hatua hiyo ni kutokana n a Wa i s l a m u k u p o t e z a imani na Jeshi la Polisi kwa kukanusha kuhusika na tukio la kupigwa risasi Sheikh Ponda, mbele ya mamia ya Waislamu wakishuhudia shambulio hilo. Katika tukio hili Jeshi la Polisi ni mtuhumiwa namba moja hivyo taarifa yeyote itakayotolewa na tume iliyoundwa na Jeshi hilo haitakuwa ya kuaminiwa hata kidogo. Imesema Shura ya Maimam Kigoma. Shura hiyo ikasema kwamba, Waislamu Mkoani

Rais Al-Assad aapa kuungoa mzizi wa ugaidi Syria


DAMASCUS Duru mbalimbali za habari zimeripoti kupatikana mafanikio makubwa ya jeshi la Syria, katika kukabiliana na makundi ya waasi yanayoungwa mkono kutoka na madola ya Magharibi, utawala wa Kizayuni na baadhi ya nchi za Kiarabu. Aidha majeshi hayo yamezidi kuungwa mkono na wananchi katika kila kona ya nchi hiyo katika mapambano yake dhidi ya waasi wa nchi hiyo, kufuatia mafanikio ya operesheni kali za kijeshi dhidi ya waasi hao katika maeneo tofauti nchini humo. Habari zinasema kuwa, hali ya amani na utulivu imeanza kurejea taratibu. Rais Bashar al-Assad wa Syra amekutana mjini Damascus na wawakilishi wa v y a m a m b a l i m b a l i vya wananchi kutoka Mauritania, ambapo mbali na kuwashukuru kwa juhudi zao kubwa zenye lengo la kusaidia kumaliza mgogoro wa nchi yake, alisema kuwa taifa na wananchi wa Syria wameazimia kukata kabisa mzizi wa ugaidi. Alisisitiza kuwa kwa kuzingatia ushirikiano mkubwa kati ya wananchi na jeshi la nchi hiyo, Syria itafanikiwa kuwatokomeza kabisa waasi hao na kile alichokiita kuwa ni ugaidi wanaoufanya nchini humo. Kwa upande wao, wawakilishi wa vyama na makundi mbalimbali kutoka Mauritania, walitangaza kuungana kikamilifu na taifa, jeshi na viongozi wa Syria na kusisitiza kuwa, taifa hilo la Kiarabu litazidi kuwa taifa lenye nguvu, baada ya kuondokana na jinamizi la mgogoro wa sasa. Mapambano makali yameendelea kushuhudiwa nchini Syria katika mkoa wa pwani wa Attaquie, uliopo Magharibi mwa nchi hiyo ambapo jeshi limeshambulia kwa makombora na kumuuwa kiongozi mmoja wa kundi la waasi, shirika la haki za binadamu limethibitisha. Wa n a j e s h i z a i d i wametumwa katika eneo hilo linaloaminika kuwa ndio kitovu cha Rais Bashar Al Assad katika kupambana na wapiganaji walioweka kambi katika milima inayozunguka huo, ambako jeshi lilianzisha mapambano takriban majuma mawili yaliopita. Wakiwa hawana silaha za kutosha, wapiganaji hao waliamua kujiunga na makundi ya wapiganaji wa jihad wa makundi ya Kiislam kutoka nchini Iraq, licha ya uhusiano mbaya uliopo baina ya waasi na wapiganaji wa makundi ya Jihad nchini

Habari za Kimataifa/Tangazo

SHAWWAL 1434, IJUMAA AGOSTI 23-29, 2013

AN-NUUR

Kigoma wanaamini kuwa shambulio hilo lililenga kumuua kiongozi huyo, wakizingati kauli ya kibabe ya Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoitoa Bungeni. Shura ya Maimam Kigoma, ikaitaka Serikali kuunda tume huru ya uchunguzi nje ya Jeshi la Polisi, itakayo husisha viongozi wa Dini, wanaoaminiwa na ummah wa Kiislamu sambamba na kumuwajibisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile pamoja na viongozi waandamizi wa Jeshi hilo mkoani humo. Tukio la kupigwa risasi Sheikh Ponda Issa Ponda, lilitokea siku ya Jumamosi Agosti 10, 2013, Majira ya jioni, Mkoani Morogoro, baada askari Polisi kuvamia m s a f a r a w a Wa i s l a m u wa l i o k u wa wa k i e l e k e a msikitini kwa swala ya Magharibi. Shambulio hilo lilifanywa mbele ya mamia ya Waislamu waliokuwa wakitoka katika Baraza la Idd, wakielekea katika Msikiti wa Mungu Moja Dini Moja, Mkoani Morogoro.

Mahabusu 38 Ikhwan Jeshi lashambulia ngome za waasi nchini humo wauawa gerezani Misri
REUTERS Polisi 24 wa Misri wa m e u a wa h u k o S i n a i katika shambulio lililotokea Jumatatu asubuhi. Wakati huo huo, Wizara ya Mambo ya Ndani nchini Misri imetowa taarifa za kuuawa kwa wafuasi 36 wa chama cha Muslim Bradherhood, ambao walikuwa wametiwa nguvuni wameuawa jana kwa mabomu ya machozi walipojaribu kutoroka wakati polisi walipokuwa wakiwahamisha katika jela nyingine karibu na jiji la Cairo. Wizara hiyo ya mambo ya ndani nchini Misri imesema watu 36, ni wafuasi wa chama cha Rais wa zamani aliyepinduliwa na jeshi na kukamatwa Julai 3, ambapo vyombo vya usalama vimesababisha umwagaji wa damu mkubwa wakati wa kuwasambaratisha waandamanaji wanaoendelea kudai kurejeshwa madarakani mwa Rais Mohamed Morsi. Watu mia nane wamepoteza maisha nchini Misri kwa kipindi cha siku tano, huku kiongozi wa kijeshi nchini humo akiapa kuendeleza mapambano dhidi ya waandamanaji. H a y o ya n a j i r i wa k a t i wawakilishi wa nchi 28 za Umoja wa Ulaya wakitaraji kukutana Jumatatu hii jijini Brussels kujadili kuhusu hali inayoendelea nchini Misri. Kiongozi wa kijeshi jenerali Abdel Fattah al-Sissi, ambaye amezungumza mwishoni mwa wiki kwa mara ya kwanza tangu kutokea mauaji ya watu mia sita Jumatano wiki iliyopita, amesema kuwa jeshi halitovumilia hali yoyote ile ya vurugu na lipo tayari kupambana kwa kutumia nguvu kubwa ili kukomesha maandamano, bila hata kujali kauli za viongozi wa nchi za Magharibi wanaosema kuwa kunafanyika umwagaji wa damu. Jijini Bruxels mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya unafanyika, ikiwa ni kikao cha kwanza cha kidiplomasia cha hali ya juu kufanyika juu ya kuzungumzia hali ya nchini Misri.

Bismillah Rahman Rahiim

KIGAMBONI - CU.124/ KIGOGO- CU.130 Teachers` College

CHUO CHA UALIM

Nafasi za Masomo 2013/2014


UALIMU: STASHAHADA- E moja na S moja GRADE 3 A Division IV 27 CHEKECHEA Division Iv 28 na kuendelea Note: Nafasi za udhamini kwa waliopata Viwango Ngazi ya Diploma na Cheti Wahi nafasi ni chache! Asiyekuwa na viwango anaruhusiwa kusoma Ualimu huku anarudia mitihani KOZI ZA BIASHARA Secrerial Studies, Records mgt. Project Planning na mgt Ict, Simplified accountancy. Computer Applications Kwa mawasiliano zaidi tupigie 0715 860120 au 0654- 580924

Rais Bashar al-Assad wa Syra akimjulia hali mmoja wa afisa wa jeshi aliyejeruhiwa na kundi la waasi nchini humo.
Syria. M k u u wa s h i r i k a l a haki za binadamu nchini Syria, Rami Abdel Rahman, amesema majeshi ya serikali yalimiminika kwa wingi katika eneo hilo la Attaquie, kupambana na waasi na k u f a n ya m a s h a m b u l i z i makali katika maeneo yaliokuwa yanashikiliwa na waasi hao. Kituo cha televisheni ya taifa nchini Syria kimesema jeshi limefanikiwa kurejesha katika himaya yake miji iliyokuwa inashikiliwa na makundi ya waasi katika jimbo hilo, ikiwa ni pamoja na Kharata, Janzuriyeh, Baluta, Baruda na Hambushiyeh. Hata hivyo Abdel Rahman, ameeleza kuwa mapigano hayo yalikuwa makali mno na kuendelea kudhibiti baadhi ya vijiji. Kwa mujibu wa kiongozi huyo wapiganaji wengi wa makundi ya kigeni ya Jihad wameuliwa katika mapigano hayo, akiwemo kiongozi wa kundi la EIIL. Kiongozi huyo wa kundi la EIIL aliuawa wakati wa mapigano katika kijiji cha Jamusiyeh. wakati huo huo taarifa zinasema kuwa jeshi la anga nchini Syria limeshambulia eneo la Jabal al Arbaine, katika mkoa wa Edleb (Kaskazini magharibi) mwa miji ya Daraya na Zabadani karibu na Damascus, pamoja na mji wa Deir Ezzor mashariki mwa nchi hiyo. Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa watu laki moja wamepoteza maisha katika mapigano hayo, ambayo sasa yamedumu kwa miezi 29 sasa. Jumamosi mwishoni mwa juma lililopita, watu 124 wamepoteza maisha katika mapigano yaliojiri kwenye maeneo mbalimbali nchini humo.

Radio Imaan FM
Inatoka Uk.1

ijayo, kituo hicho kinatarajiwa kurejesha matangazo yake kama kawaida. Redio Imaan FM ilifungiwa kurusha matangazo yake tangu Februari 26 mwaka huu, kutokana na kile kilichoelezwa na serikali kuwa ni kwasababu ya kosa la uchochezi, sababu kubwa ikielezwa kuwa ni kuwashawishi Waislamu kutoshiriki katika zoezi la sensa ya watu na makazi lililofanyika Agosti mwaka jana, ambapo Waislamu walidai iwapo kipengele

Wakati Radio Imaan ikimaliza kifungo chake, bado hatma ya kurusha rasmi matangazo kituo cha televisheni cha TV IMAAN imekuwa ni kitendawili licha ya kituo hicho kudaiwa kukamilisha taratibu zainazohitajika. H a t a h i v y o Mkurugenzi Mkuu wa wa TCRA Prof. John Nkoma, amekuwa akieleza kuwa taratibu bado zinaendelea na zitakapokamilika leseni h i y o i t a t o l e wa k wa muombaji.

cha dini hakitajumuishwa katika zoezi hilo, basi wao hawatashiriki.

LONDON Mkuu wa taasisi ya misaada ya kibinaadamu ya Tell Mama, amesema kuna ongezeko la vitendo vya kibaguzi na mashambulizi dhidi ya Waislamu nchini Uingereza na Wales. Fiyaz Mughal, ambaye pia anafuatilia kesi za

Waislamu Uingereza wazidi kushambuliwa


vitendo hivyo nchini humo, a m e s e m a k u wa k a t i k a kipindi cha miezi 18 iliyopita, watu wasiopungua 1,200 walitekeleza mashambulizi ya kudhuru Waislamu nchini Uingereza na Wales. Mkuu huyo ameeleza k u s i k i t i s h wa k wa k e n a mashambulizi na vitendo vya ubaguzi dhidi ya jamii hiyo ndogo ya Waislamu, kwa jinsi vinavyozidi kuongezeka siku baada ya siku. Fiyaz Mughal amesema kuwa vitendo hivyo haviishii tu katika mitaa na barabara za nchi hiyo, bali pia vinashuhudiwa hata katika mitandao ya intaneti.

Kabla ya hapo, mshauri mmoja wa serikali ya London ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisisitiza kuwa viongozi wa nchi hiyo ya Ulaya wamekosa mbinu za kisiasa kwa ajili ya kukabiliana na ongezeko la mashambulizi na vitendo vya ubaguzi dhidi ya jamii ya walio wachache ya Waislamu.

Inatoka uk. 1 Amesema, ruhani huyo ambaye haonekani kwa uwazi japo yupo, ndi ye hu zaa Serik ali mbili katika muungano, muungano ambao huifanya Zanzibar kuwa kama kasoro koloni. Mwanasheria Mkuu huyo ameyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akifungua kongamano la Baraza la Katiba la Vyuo Vikuu liliondaliwa na Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Zanzibar, ZAHILFE, liliofanyika katika Ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani. Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mwanasheria Mkuu wa SMZ amesema kuwa mfumo huu wa muungano wa Serikali mbili, unainyima Zanzibar fursa ya kuamua nani awe Rais wa Nchi, kuweka sera na sheria katika mambo ya muungano. Aliwataka wanafunzi

Ruhani Tanganyika ndio mzizi wa fitna muungano


hao kuzungumzia mambo ya Muungano na kutaka kuwe na usawa kwani bila ya kuwa na usawa katika Mungano, huo si Muungano bali ni ukoloni. Alitaka kuwe na mfumo wa usawa katika Baraza la Mawaziri na Bunge na kuwe na makubaliano ya thuluthi mbili kila upande katika kupitisha sheria na kuongezwa au kupunguzwa mambo ya Muungano. Akifafanua amesema, h i y o n i k wa s a b a b u hivi sasa mambo hayo hupitishwa katika vyombo vya muungano kwa kanuni ya simple majority, kwa maana ya wengi wape na sio Wazanzibari kuulizwa kama nchi. Kwa hiyo akasema, maadhali Wazanzibari watakuwa wachache katika vyombo hivyo, likiwemo Bunge, ni dhahiri kuwa matakwa ya o n a m a s i l a h i ya o hayatazingatiwa katika masuala ya muungano. A k a s e m a p i a k u wa mfumo uliopo hautoi usawa katika rasilimali za muungano akitolea mfano wa makao makuu ya taasisi za muungano kwamba zipo Bara na hivyo ndio wanaofaidi ajira, fursa za kiuchumi, kusomesha wataalamu na mambo kama hayo. Akizungumzia ujanja, ghilba na dhulma iliyopo katika Kodi ya Mapato, amesema kodi yote huishia Bara kiasi kwamba hata yale makampuni ambayo hufanya kazi zaidi Zanzibar hutakiwa kulipa kodi Bara (mungano uliobeba ruhani Tanganyika). Ametoa mfano wa m a k a m p u n i ya s i m u a m b a y o wa k a t i y o t e yanalipa kodi huko, hivi sasa kuna kesi ambapo inashitakiwa Zantel kwa nini hailipi kodi Bara. M wa n a s h e r i a h u y o alisema kuwa hii ni dhulma na kwamba dhuma ikizidi sana hata akili hupotea. Aliitaja Sheria ya Kuanzishwa na Bank Kuu ya Tanzania kuwa aliisaini Karume mwenyewe lakini Karume alipoona mapungufu ya Seria hiyo, akaanzisha PBZ. Amesema kuwa kwa mwenye akili sio vigumu kuona dhulma hizi, ila inavyoonekana kuna mgawanyiko wa kupandikizwa. Akasema, suala la nchi sio la kufanyia mchezo na sio la kumuamini mtu yeyote kama ambavyo hakuna mtu anayeamini mtu kwa mkewe hata akiwa rafiki vipi. Amesema, hii migawanyiko ya maoni yanayoongozwa na ushabiki wa kivyama (CCM, CUF), isifikie mahali pa kuiweka nchi rehani kwa thamani ya bidhaa ya dukani kama mchele. Kwa maoni yake

Makala

SHAWWAL 1434, IJUMAA AGOSTI 23-29, 2013

AN-NUUR

Tangazo

SHAWWAL 1434, IJUMAA AGOSTI 23-29, 2013

AN-NUUR

Na Bakari Mwakangwale

Mashitaka mapya Ponda


kisha kufutiwa mashitaka, aliyofunguliwa akiwa kitandani katika Hospitali ya Muhimbili. Akiwa Mahakamani h a p o , S h e i k h Ponda, alilazimika kusomewa mashitaka anayotuhumiwa kufanya akiwa amekaa kutokana na kuwa na maumivu makali katika jeraha lake la risasi katika bega la mkono wa kulia. Sheikh Ponda alisomewa mashitaka matatu mbele ya Hakim Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Morogoro, Bw. Richard Kabate, ambayo anadaiwa kuyafanya akiwa Mkoani humo Agosti 10, 2013. Wa k i l i wa S e r i k a l i K a n d a ya M o r o g o r o , Benard Kongolo, aliiambia Mahakama hiyo kuwa Shkh. Ponda, alitenda makosa hayo akiwa katika Viwanja vya Kiwanja cha Ndege, Manispaa ya Morogoro, majira ya jioni. Imeelezwa kuwa Sheikh Ponda, anadaiwa kukiuka adhabu kwa kutoa kauli za uchochezi kwa jamii, pia anadaiwa kutoa maneno yenye nia ya kuhatarisha imani za watu wengine kwa kutoa maneno kuwa Serikali iliamua kupeleka Jeshi Mtwara, kushughulikia suala la vurugu zilizotokana na gesi kwa kuwauwa na kuwatesa wananchi kwa kuwa asilimia tisini ya wakazi wa Mtwara ni Waislamu. Katika shitaka lingine linalomkabili shkh. Ponda, ni kushawishi na kutenda k o s a , k wa k u wa t a k a Wa is la mu wa s ik u b a li uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama, kwani zinaundwa na BAKWATA, ambao ni vibaraka wa CCM na Serikali, na kama kamati hizo zitajitokeza inadaiwa aliamuru ifungwe milango na madirisha na kuwapiga. Hata hivyo, Shkh. Ponda, alikana mashitaka hayo, ambapo upande wa mashitaka ulipinga dhamana yake kwa madai kuwa. Ponda, anatumikia kifungo cha nje, na kwamba hakutakiwa kufanya kosa lakini pia anakabiliwa na makosa mengine. Upande wa mashitaka uliileza mahakama kuwa upelelezi umekamilika na kesi hiyo itasomwa tena Agosti 28, 2013. Baada ya kusomewa mashitaka hayo, Sheikh Ponda, alirudishwa mahabusu kwa helkopta,

anasema, kuendelea kwa serikali mbili ndio kutavunja muungano tena kwa fujo wakati zikiwepo serikali tatu, hata kama itafikia watu kusema hawataki tena muungano, utaondoka kwa mazungumzo na kwa amani. Alimalizia nasaha zake k wa k u s i s i t i z a k u wa msingi wa Muungano wa Tanzania ni kuungana kwa Nchi mbili huru, Tanganyika na Zanzibar, n a k wa m b a l e n g o l a kuungana kwa nchi mbili hizi ni kufanya mambo yao pamoja na kupata faida zaidi, sio Nchi moja kuitawala Nchi nyengine. Alisisitiza kuwa Katiba Mpya ni lazima itambue kuwa Zanzibar si Wilaya, si Mkoa, wala Jimbo la Tanganyika. Na kwamba ni lazima Uruhani wa Serikali ya Ta n g a n y i k a u o n d o k e maana ndio kero kubwa ya Muungano.

MAHAKAMA ya Hakim Mkazi Mkoani Mrogoro, Agosti 19, 2013, ilifurika maelfu ya Waislamu waliomiminika kushuhudia Sheikh Ponda Issa Ponda, akisomea mashitaka. Licha ya kubainika kwa muda mfupi kuwa Katibu wa Jumiya na Taasisi za Kiislamu Sheikh. Ponda, yupo Mahakamani hapo, m a e l f u ya Wa i s l a m u walimiminika ili kujua nini kinachoendelea. Sheikh Ponda, alifikishwa Mahakamnai hapo majira ya saa tano asubuhi, chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi n a wa l e wa F F U , n a kusababisha shughuli kadhaa kusimama, katika maeneo ya jirani na Mahakama hiyo, na kuelezwa kuwa hali hiyo haijawahi kutokea katika historia ya Mahakama hiyo. Sheikh Ponda, alifikishwa Mahakamani h a p o k wa H e l k o p t a , akitokea Jijini Dar es Salaam, siku hiyo hiyo b a a d a ya k u f i k i s h wa k a t i k a M a h a k a m a ya Hakim Mkazi Kisutu,

SHEIKH Ponda Issa Ponda Segerea Jijini Dar es Salaam. Awali, Hakim Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Bi. Hellen Riwa, alimfutia Sheikh Ponda, mashita ya kuhamasisha vurugu yaliyokuwa yakimkabili, kwa kile kilichoelezwa na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kuwa hana haja ya kuendelea kumshitaki.

8
Na Shaaban Rajab

HABARI/SHAIRI

SHAWWAL 1434, IJUMAA AGOSTI 23-29, 2013

AN-NUUR

UONGOZI wa Chama cha Wananchi CUF-Wilaya ya Ilala kimeliomba jeshi la polisi liache mara moja kuchukua hatua bila kufuata sheria za nchi, na kulitaka jeshi hilo kutambua wajibu wake kuwa ni kulinda na kutunza usalama wa raia na mali zao na sio kuua. K wa m u j i b u wa taarifa ya chama hicho iliyotolewa katikati ya wiki hii na kusainiwa na Mkurugenzi wake wa Haki za Binadamu Wilaya ya Ilala, Bw. Bw. Mohammed

KARIBU TENA 'REDIO IMANI'


1.Ewe redio IMANI, Mwenye aali thamani, Akhera na duniani, Karibu twakungojea. 2.Kwayo aali thamani, Uloitwaa nchini, Kufu yako simuoni, Karibu twakungojea. 3.Maadili namba 'wani', Kwalo huna mshindani, Bara hata Visiwani, Karibu twakungojea. 4.Waushika usukani, Bara nako Visiwani, Mijini na vijijini, Karibu twakungojea. 5.Kipenzi cha waumini, Hata waso waumini, Wapenda haki insani, Karibu twakungojea. 6.Watueleza bayani, Ya dunia na ya dini, Kwa ya insafu mizani, Karibu twakungojea. 7.Lengo tuweze 'baini', Stahiki ya insani, Kwa pande zote thinani, Karibu twakungojea. 8.Waibaini amani, Ya kweli na ya yakini, Changamoto duniani, Karibu twakungojea. 9.Changamoto kwa insani, Tena iso na kifani, Kwa sasa ulimwenguni, Karibu twakungojea. 10.Adayo puya huneni, Ila haki na yakini, Kumridhisha Manani, Karibu twakungojea.

Juma Mluya, ilieleza kuwa CUF wanalaani kitendo cha polisi kutumia risasi za moto kuwapiga raia wasio na hatia na kuwahalalishia makosa ya jinai. Polisi wamekuwa wakichukua sheria mkononi huku Mahakama na Taasisi nyingine za kisheria zikiangalia b i l a ya k u c h u k u a hatua, jambo ambalo

CUF Ilala walaani nao kupigwa risasi Ponda

mambo sawa, itajikuta inatumia fedha za walipa kodi vibaya kama inavyofanyika hivi sasa katika kesi ya Sheikh Ponda, ambapo helkopta inatumika kumsafirisha

Maoni yangu juu ya tukio la Ruangwa


Kila sifa njema anastahiki ALLAH (SW), mwingi wa rehema mwenye kurehemu. Muumba wa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo. Hawat a k uwa radhi juu yako Mayahudi wala Manasara mpaka ufuate mila zao. Sema: Hakika uongozi wa Mwenyezi Mungu ndio uongozi (khasa). Na kama ukifuata matamanio yao baada ya yale yaliyokufikia ya ujuzi (wa kweli) hutapata msaidizi yoyote wala mlinzi kwa Mwenyezi Mungu Ndugu mhariri, leo nimefikia kuchukua uamuzi huu wa kutoa maoni yangu juu ya tukio la shule ya sekondari MBEKENYERA kama mzazi, mlezi na mwanajamii wa RUANGWA. Nina uhakika kabisa mpaka hivi sasa ni muda mrefu sana umepita, hali vijana wa Kiislamu wakiishi kama kondoo wasio na mchunga katika vituo m b a l i m b a l i v ya E l i m u , hususani asasi za kiserikali na baadhi ya vituo na taasisi binafsi, ambavyo bado havijaelimika juu ya haki na uhuru wa maadili ya kuabudu. Tu n a a m i n i k w a m b a kila Mtanzania ana haki ya kuabudu na kila asasi inayotoa huduma za kijamii nchini kwetu, imewekewa utaratibu wa kuheshimu na kutekeleza muongozo wa namna bora ya watu wake washiriki ibada kwa mujibu wa sheria na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na miongozo mbalimbali inayotolewa na makamishna kupitia WIZARA YA ELIMU NCHINI, kama ni sehemu ya miongozo kwa wasimamizi wa vituo/asasi hizo wakiwemo walimu wakuu, bodi za shule, walimu na wafanyakazi wa shule au vyuo kwa ujumla. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutambua kwake umuhimu wa kutunza na kuhifadhi hisia za Watanzania, ambazo zimebebwa na kuongozwa k wa k i a s i k i k u b wa n a mafundisho ya imani zao, imechukua jukumu la kujali na kuheshimu uwepo wa raia wake wenye kuabudu katika kila asasi ya kijamii, zikiwemo asasi za elimu pasi na kujali madai yake kwamba serikali haina dini. Lakini licha ya kutolewa miongozo hiyo, bado kumejitokeza makundi ya watumishi wenye kudharau na kuvunja kanuni na taratibu zilizorasimishwa na serikali. Wanakuwa kikwazo kwa haki ya kuabudu kwa wengine. K a m a wa n a j a m i i wa Ruangwa tusiokubaliana na mienendo ya viongozi wa shule yetu, Leo tumeamua kutuma ujumbe huu ikilengwa kwamba, umfikie yeyote yule mwenye uwezo wa kusoma au kusikiliza na kutambua kile kilichosomwa. Kumekuwako na malalamiko mengi ya vijana wa Kiislamu juu ya manyanyaso yanayokithiri wanayokumbana nayo katika michakato yao yote ya kimasomo. Hujuma ambazo kwa misingi ya imani na kisheria ni unyanyasaji wa kidini wanazofanyiwa na baadhi ya walimu wanaojiita wakristo mashuleni. Miongoni mwazo ni:1. Kuwazuia vijana wa Kiislamu kushiriki na kutekeleza ibada, Mfano swala za Adhuhuri na Alasiri na wakati mwingine hata swala ya Ijumaa. 2. Kuwanyima fursa ya kupata haki zao za msingi za kusoma somo la ELIMU YA DINI YA KIISLAMU/ ISLAMIC KNOWLEDGE. Mfano, kutoingizwa kipindi cha Somo la Maarifa ya Uislamu katika ratiba ya shule, kwa madai kwamba kusoma somo hili kunasababisha kufeli kwa masomo mengine. 3. K u w a n y i m a na wakati mwingine kutowatolea kabisa matokeo ya Somo la ELIMU YA DINI YA KIISLAMU, hata kama s o m o h i l o l i m e f a n y wa kisheria na wameligharamia kifedha. Mfano, mitihani ya mihula na utamilifu ya wilaya na mkoa. 4. Kuwazuia kuvaa na wakati mwingine kuwavua hijabu mabinti wa Kiislamu kinyume na taratibu kwa kigezo cha kuwakagua. 5. Kuwazuia vijana wa Kiislamu na kuwakataza kabisa kuvaa mavazi yenye kuutangaza utamaduni wa vazi la Kiislamu wawapo shuleni katika siku maalum za ibada. Mfano kuvaa kanzu na kofia katika siku za ibada ya ijumaa. hata kama mwanafunzi huyo ni wa bweni. 6. Kuwahujumu vijana wa Kiislamu kupitia viongozi wao wa DINI (Maaskofu/ Mapadri na Wachungaji) kwa kuwaita Waislamu ni wadini na kuutangaza Uislamu kuwa ni udini pale inapotokea ukatekelezwa katika vituo hivyo vya kielimu. 7. Walimu Wakristo kushirikiana na wanafunzi Wa k r i s t o k u u k a s h i f u Uislamu na Waislamu kwa ujumla. 8. Kulazimishwa kwa wanafunzi wa Kiislamu shuleni kushiriki mambo yanayo pingana na imani zao. Mfano kulazimishwa kucheza miziki/ngoma wawapo shuleni na hatimaye kuadhibiwa wanapojitetea juu ya maadili ya imani yao. 9. K u i n g i z w a mashuleni sera za kitaifa z i s i z o z i n g a t i a h a k i ya maadili ya kijana/Binti wa Kiislamu katika utekelezaji wake. Mfano uingizwaji wa JKT mashuleni pasi na kutolewa mwongozo wa vazi la heshma kwa mwanamke katika kushiriki Sera hiyo. 10. W a n a f u n z i w a Kiislamu kunyimwa maeneo ya kufanyia ibada kama ambavyo ipo kwa Wakristo. Baadhi ya shule zina makanisa katika maeneo ya shule lakini si msikiti. 11. Kupangwa muda ya swala matukio muhimu yanayohitaji mjumuiko wa shule (walimu na wanafunzi) pasi na kuzingatia uwepo wa waumini wenye kuhitajika kutekeleza ibada kwa mida hiyo. Mfano imezoeleka sana kuifanya siku ya Ijumma kuanzia saa 5:00-8:00 kuwa n d i o s i k u z a k u we k wa mahafali ya shule/vyuo. Hujuma kama hizi zinazotokea takribani shule nyingi za sekondari nchini, ndizo zilizopelekea kutokea kwa tukio la vijana 24 kusimamishwa masomo katika wilaya yetu ya Ruangwa na hatimaye walimu kuwatengenezea makosa wanafunzi ili waonekane kuwa wamekosa. Mimi kama Mwanajamii wa Ruangwa mwenye uchungu na nchi yangu, nimelifuatilia tukio la R u a n g wa k wa u m a k i n i na ukaribu mkubwa sana, na kwa kufahamu athari zinazoweza kutokea hapo mbeleni kwa kuendelea kulilea tukio hili, nimeonelea leo nitoe mapendekezo yangu juu ya hatima ya mgogoro huu. Katika mapendekezo yangu juu ya nini kifanyike ili kuleta muafaka mzuri wa mgogoro huu, nimeyabaini mambo kadhaa ambayo kwa udhibitifu wake nina uhakika kabisa kwamba m g o g o r o wa S h u l e ya sekondari Mbekenyera, ni matokeo ya mrundikano wa makorokoro chungu nzima yaliyopo shuleni hapo na katika ngazi za juu za uongozi wilayani. Miongoni mwa mambo hayo ni:1. Shule ina mgogoro wa muda mrefu kati ya walimu Wakristo na wanafunzi Waislamu juu ya masuala ya kiimani. Ni wazi kabisa mgogoro huu unaohusishwa na masuala ya kiimani kati ya baadhi ya walimu Wakristo na wanafunzi Waislamu shuleni hapo, ni wa muda mrefu na hivyo umepea kwa kiwango kikubwa hata kufikia hatua ya kujenga mahusiano mabaya ya kimalezi kati ya walimu na wanafunzi hao, ambayo kwa kiasi kikubwa yanazidi kukuza uadui wa kiimani. Wanajamii wa Ruangwa tuna imani kabisa hali hii imesababishwa na Mkuu wa Shule yetu, kutokana na kasumba yake ya kutopenda kutushirikisha kama wanajamii katika kujadili mambo mbalimbali yanayojiri shuleni petu. Tumeyafuatilia maelezo ya vijana kwa kina sana, pia hata kuwashirikisha wale waliokwisha maliza mwaka zaidi ya mmoja nyuma, juu ya tunachokisikia kuwa vijana wa Kiislamu huwa wamekuwa wakifanyiwa kwa muda mrefu na Mwalimu huyo, sasa tumethibitisha k u wa n d i v y o m wa l i m u Mkuu wa Shule yetu ya Mbekenyera na baadhi ya walimu wake Wakristo, wa n a m a m b o ya u d i n i wanayowafanyia watoto wetu pasi na kuzingatia haki yao ya msingi ya kuabudu. Tuna rekodi ya matukio kadhaa ambayo wenetu wamekuwa wakifanyiwa na walimu hao, ambayo kama wanajamii na Waislamu wa Ruangwa hatujafurahikiwa nayo. Kama wanajamii wa Ruangwa hili la Mbekenyera limetugusa sana. Kweli hakuna mtu anayeweza kukubali. Uongozi wa shule ni mbaya sana. Inaonekana pia katika shule yetu hii ya Mbekenyera, hakuna utaratibu mzuri wa uongozi wa shule katika uendeaji wa masuala mbalimbali ya kinidhamu katika malezi ya wanafunzi hapa shuleni. Hali inayosababisha kila mtu kuweza kuchukua maamuzi binafsi katika kutafuta njia za utatuzi wa matatizo pindi yanapotokea, hali hii imekuwa chachu ya kutokea

Makala

SHAWWAL 1434, IJUMAA AGOSTI 23-29, 2013

AN-NUUR

11.Si kumridhi insani, Wala rajimi shetani, Wakusifu duniani, Karibu twakungojea. 12.Ndicho hasa kiini, Cha wewe kukufitini, Na kutiwa kifungoni, Karibu twakungojea. 13.Mudawe u ukingoni, Wa kutoka gerezani, Tarehe naibaini, Karibu twakungojea. 14.Mbili nane kalendani, Agosti twatumaini, Kukusikia hewani, Karibu twakungojea. 15.Jumatano fungueni, Zenu redio nyumbani, Kuipokea IMANI, Karibu twakungojea. 16.Mahabaye dumisheni, Dawamu msiikhini, Kwa vyovyote abadani, Karibu twakungojea. 17.Nyote nakutakieni, Utuvu na tamakuni, Na usikizi makini, Karibu twakungojea. 18.Yailahi Ya Manani, Twakuomba mwenye shani, Ikinge na mafatani, Karibu twakungojea. 19.Wote wa nje na ndani, Wa Bara na Visiwani, Na kote ulimwenguni, Karibu twakungojea. 20.Kwa yako Allah auni, Idumu yetu IMANI, Idhaa iso kifano, Kwa hamu twaingojea.

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wahadhiri mkoa wa Morogoro Ustadh Idd, akionyesha kibali cha polisi kuruhusu kufanyika kongamano la Waislamu Morogoro ambapo Sheikh Ponda alishambuliwa.

ABUU NYAMKOMOGI MWANZA.

linafanya matendo hayo yachukue kasi hapa nchini. Ilieleza sehemu ya taarifa hiyo ya CUF. Aidha chama hicho wameiomba m a h a k a m a k u w a t e n d e a h a k i Wa t a n z a n i a wanaofikishwa kwenye chombo hicho, kwa kuwapa dhamana kwasababu ni haki yao, kuliko kukubali sheria kuvunjwa kwa kuridhia kuondolewa haki ya dhamana kwa baadhi ya Watanzania,

kama inavyofanyika hivi sasa kwa baadhi ya watuhumiwa. Chama hicho kimeiomba serikali kuingilia kati suala la Sheikh Ponda, kwa kuwawajibisha wote wanaohusika katika kuvunja sheria na kuchukua maamuzi ambayo yanaweza kuigharimu nchi baadae na kuharibu amani uliyopo. Katika taarifa hiyo ilieleza kuwa, bila serikali kuingilia kati suala hili na kuweka

mtuhumiwa mmoja kutoka mahabusu Segerea Dar es Salaam kwenda mahakamani Morogoro kwa ajili ya kesi. Licha ya muda kupotea, lakini pia misafara ya magari yanayotumika k u m p e l e k a m t u h u m i w a m a h a k a m a n i na kumrejesha rumande, ni gharama zinazolipwa kwa k o d i z a wa n a n c h i pia, fedha ambazo zingetumika katika shughuli nyingine za maendeleo.

na kukua kwa migogoro na malumbano baina ya pande tatu zenye kuhusika na malezi ya mwanafunzi (mwalimu, mzazi, jamii). Hivi inawezekanaje kwa tukio la kuhatarisha amani katika shule litokee na Mkurugenzi wa Halmashauri na Afisa Elimu wasishtuke hata kidogo kwa utendaji mbovu wa mwalimu wao? Kwa nini sisi tusiamini kwamba ubovu huu umeanzia toka ngazi za juu? Ingelikuwa Mkurugenzi yupo imara, Afisa Elimu yupo imara hivi wapi mwalimu Ngonyani, angelipata kibri cha kufanya anayoyafanya? KUNA UKWELI U M E F I C H WA B A I N A YA PANDE HIZI MBILI (AIDHA KWA WALIMU AU WANAFUNZI) JUU YA UHALISIA WA SABABU ZA KUTOKEA KWA TUKIO. Inaonekana kuna tatizo kubwa limejificha katikati baina ya walimu na wanafunzi wao, ambalo kulingana na uzito wake, pande moja kati ya hizi mbili inatafuta namna ya kujinasua kutoka katika tatizo hilo, hali ya kuwa kulingana na muda wa tatizo lilivyopea na kukomaa, haiwezekana kwa muhusika yeyote yule kulikwepa zaidi ya kukubali. Tu m e s h t u s h w a s a n a na kitendo cha Mwalimu Mkuu na uongozi wake kutukimbia wanajamii kila mara tunapojitahidi kutafuta mazingira ya kukutana, i l i k u ya j a d i l i m a t u k i o haya yanayoendelea. Cha ajabu zaidi, kama hoja za wanafunzi dhidi yake ni za uongo, kwanini atukimbie? Na kama za kweli je! Kufanya hivyo ndio busara? U s h a u r i wa n g u k wa serikali ya Ruangwa juu ya mgogoro huu. Kwanza Mkurugenzi wa Halmashauri n a A f i s a E l i m u Wi l a ya waingilie kati suala hili ukweli ubainike. Pili, kiitishwe kikao cha haraka iwezekanavyo baina ya pande zote zinazohusika (wazazi, walimu, wanafunzi, viongozi wa dini, walimu walezi na wasimamizi wa Somo la Dini Mashuleni, kulijadili tatizo kabla halija anza kuleta madhara makubwa. Tatu, Jamii isikilizwe malalamiko yake katika mgogoro huu.

Abuu Nurain Ismail Kimbunga MBEKENYERA RUANGWA

10
Kumbukumbu ya Sheikh Rogo
Ni simanzi Afrika, Mashariki kwa hakika, Kwa mauti kumfika, Aboud si jina geni. Sheikh wetu Mujahidi, Kauliye ni Jihadi, Kila mara 'liinadi, kwa ustawi wa dini. Hakutaka kuwaficha, Jambo hili wanolicha, Kadhalika wanolacha, Kwa kudhani si la dini. Alihoji kulikoni, 'Sinadiwe hadharani, Kwani nalo ni la dini, Kama hijja kwa kifani. Alisimama thabiti, Na kwa hoja madhubuti, Lengo zende harakati, Mbele za yetu dini. Alijusurisha umma, Utambue yake dhima, Si nyingine bali hima, Ya kuinusuru dini. Alikuwa ni fataki, Dhidi ya wapinga haki, Kadhalika wazandiki, Wanoihujumu dini. Akatupa na indhari, Tuchukue tahadhari, Dhidi yazo zao shari, Na mbinuzo wanobuni. Hakuwahofu viumbe, Wenye vyeo lembelembe, Aliwapa zao tembe, Si kwa siri hadharani. Tegemeole Manani, Hili alilibaini, Si kwa kiumbe insani, Aloumbwa na Manani. Baa aliweka wazi, Kukusibu haliwezi, Ila kwa yake Azizi, Qadari iso kifani. Lengo kurufai hofu, Kwa wenye 'mani dhaifu, Wasimame mukawafu, Kuihami yao dini. Alibaini hawafu, Adhimu tunozihofu, Kifungo pamwe na ufu, Kasetize rejeeni. Zilifanywa nyingi njama, Dhidiye arudi nyuma, kadhalika na Hujuma, Kutoka nje na ndani. Nyingi alizimaizi, Na kuzitamka wazi, Pasi na kigugumizi, Wala hofu mtimani. Akatiwa gerezani, Si kwa jingine kwa dini, Hakurudi abadani, Nyuma kutetea dini. Kasiye 'liongezeka, Gerezani 'lipotoka, Kwa shababu kuwataka, Waihami yao dini. Aliomba kila mara, Safariye ya akhera, Iwe kwake ya jahara, Si ya hofu kitandani. Ilahi mghufirie, Dhunubuze mfutie, Firdaus mtie, Kwa rehemazo na shani. Nasi Allah twakuomba, Shahada zisizoyumba, Tushike imara Kamba, Hapa hadi kaburini. Abuu Nyamkomogi Mwanza.

Mashairi/Tangazo/Makala

SHAWWAL 1434, IJUMAA AGOSTI 23-29, 2013

AN-NUUR

Ndugu Mhariri, Assalaam alaikum wtw. Aliwahi kusema Muisraeli mmoja kuwa, siku zote mkaa anayekaa kimya pindi mwenzake anafanyiwa dhulma, iko siku dhulma hiyo atafanyiwa yeye. Leo Sheikh Ponda Issa Ponda amepigwa risasi, amekamatwa na kuwekwa mahabusu, akiwa bado mgonjwa, amefunguliwa mkashitaka na majeraha yake, tukikaa kimya iko siku yaliyomkuta yatatukuta mimi na wewe! Namshukuru ALLAH (SW) nilifanikiwa kumuona Sheikh Ponda akiwa hospitalini Muhimbili chini ulinzi

Tatizo sio Ponda!


mkali wa askari polisi wakiwa na silaha na mabomu ya machozi. Allah amjalie Sheikh ithibati na ISTIQAMA F I I D U N I A WA AKHERA. M w i s h o k u p i g wa risasi Sheikh Ponda iwe ni darsa kwa Waislamu wanaochukia dhulma na wakaipenda haki. Haki iko wapi? Sheikh Ponda asubuhi yake tangu nilipomjulia hali, alipelekwa gerezani Segerea na jeraha lake huku akiwa na dawa zake mkononi. K a d h i a h i i inanikumbusha kisa cha vijana wa Palestina waliomvika farasi b e n d e r a ya I s r a e l i , kisha alipokwenda upande walipo

11

Tangaz

SHAWWAL 1434, IJUMAA AGOSTI 23-29, 2013

AN-NUUR

askari wa Kiyahudi walimpokea vyema tu bila hata kumpiga risasi, pembeni yao alikuwepo mwandishi wa habari, akamuuliza yule mwanajeshi, mbona hujampiga risasi huyo farasi? Mwanajeshi alijibu, huyu farasi anawatetezi watu wa HUMAN RIGHT WATCH, akamuuliza vipi kuhusu Waislamu m n a o wa p i g a r i s a s i kila kukicha, alijibu wao hawana mtetezi. Kupigwa na kudhulumiwa ni haki yao. Serikali ijibu hoja za Sheikh Ponda, siyo k u n ya m a z i s h a k wa risasi. Mwananchi mpenda haki

1. EMPLOYMENT OPPORTUNITIES
ADVERTISMENT 1Background TANESCO http://www.tanesco.co.tz

The Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) is focusing on increasing the outreach and service quality of its Energy products for Tanzanian people. Next to its current passion as a leading provider of electricity is to be more efficient customer focused utility for Tanzania and beyond. The Company has the largest electricity generation, transmission and distribution network in Tanzania. In order to reach its goals, the Company will, in the coming years invest heavily in its generation, transmission and distribution network, its business systems and human capital. TANESCO now invites internal and external applicants who are self-motivated, honest, hardworking and committed individuals to fill the under-mentioned posts at Backbone Transmission Investment Project (BTIP).

Project Engineers - 7 posts


POSITION OBJECTIVE The Project Engineers for the Backbone Transmission Investment Project (BTIP) are required to oversee execution of Lots 1, 2, & 3 and rural electrification works subprojects of BTIP during construction works of transmission lines at respective sites. The Project Engineers reports to the Project Managers and will be assisting respective Project Managers with skills related to Transmission Line and Electrification Construction works. RESPONSIBILITIES: 1. To assist the project managers in organizing, controlling, monitoring and recording all activities related to construction management of the respective Lot. 2. Undertake review of technical standards and specifications for design works undertaken by EPC contractor, examine and review EPC contractor detail design and drawings of respective Lot for compliance with specifications and sound engineering practice. 3. Ensuring that environmental and social impact mitigation and monitoring measures in the Projects Environmental and Social Impact Assessment (ESIA) and the environmental and Social Management Plan (ESMP) included in it are appropriately executed by TANESCO and EPC contractor as well as relevant community and district and local government authorities. 4. Verify accuracy of payment invoices of EPC contractor of respective Lot to ensure that payments accurately reflect the cost of the works completed or goods supplied. 5. Ensure that safety is adequately provided for and observed in the respective Lot according to TANESCO safety rules. 6. Prepare weekly, monthly, quarterly, biannual project progress reports for submission as appropriate to TANESCO. Also prepare Project Completion Report, which outline, inter alia, achievements in relations to objectives and targets of the substation expansion. 7. Advising Project Manager any departures from work schedules on all phases of the project during construction, commissioning, performance testing and final commercial operational acceptance including proposals for reducing any delays without compromising with cost and quality of work. 8. Assist supervision team (OISF and TANESCO) on supervising contractors construction activities at the site and keeping written record of construction progress, reviewing and processing site drawings when submitted by contractor and making/reviewing design changes and preparing change orders to meet changed conditions during construction proceeding for respective Lot. PROFESSIONAL AND INTERPERSONAL DETAILS MINIMUM REQUIREMENTS: Graduate Engineers with good pass mark in BSc. in Civil (Three (3) posts) and Electrical Engineering (Four (4) posts). Excellent communications and presentation skills. Proven computer literacy Self-management and personal traits: Courage and Conviction the ability to create a sense of excitement about taking on new challenges and a belief in your capabilities to deliver results. Relentless Preparation preparing thoroughly for all important management decisions. Drive for results a deep seated inner desire to compete against standards of excellence and achieve step changes in business results. Holding people accountable the ability to give clear and unambiguous direction to individuals and teams about what they need to do in order to meet the organisations objectives. Building capability - developing individuals and groups in order to increase the capability of the whole organisation. Compelling Communication recognising that clear communication is the key to understanding. Leading Others the ability to create a compelling vision of the future and provide inspiration, clarity and direction. Leadership and self management skills: Focuses on result for the project and responds positively to feedback. Consistently approaches work with energy and a positive, constructive attitude. Remains calm, in control and good humored even under pressure. Demonstrate openness to change and ability to manage complexities.

TUNAYOFURAHA KUKUTATANGAZIENI WAISLAMU WOTE KWA KUWA VITABU MBALIMBALI VYA MAARIFA YA UISLAMU SASA VINAPATIKANA BURE KATIKA TOVUTIYETUWWW.ISLAMICEDUCATIONTZ.COM. VITABU VINAVYOPATIKANA NI HIVI VIFUATAVYO: I. II. III. IV. VITABU VYA ELIMU YA DINI YA KIISLAMU SHULE YA MSINGI KITABU CHA KWANZA HADI CHA SABA VITABU VYA ELIMU YA DINI YA KIISLAMU KWA SHULE ZA SEKONDARI KITABU CHA KWANZA HADI CHA NNE ISLAMIC KNOWLEDGE FOR FORM FIVE AND SIX VOLUME ONE,TWO AND THREE MODULI YA MBINU ZA KUFUNDISHIA ELIMU YA DINI YAKIISLAMUUALIMU MAARIFA YA UISLAMU DARASA LA WATU WAZIMA JUZUU KWANZA HADI YA SABA V. MIHTASARI YA ELIMU YA DINI YA KIISLAMU KWA ELIMU YA AWAL, SHULE ZA MSINGI,SHULE ZA SEKONDARI NA UALIMU. MAELEKEZO MUHIMU: UNARUHUSIWAKUDURUFISHA(DOWNLOAD)KWA LENGO LA KUENEZA MAFUNZO YA UISLAMU KWA UMMAH ILA HURUHUSIWIKUBADILISHACHOCHOTE WALA KUUZA. WABILLAH TAWFIQ MWENYEKITI.

Islamic Education Pane

Si mwisho wa swala tano !


Kalamu nimeishika, kunena na ikhiwani, Hatamu mloishika, kwa swala za Ramadhani, Kwa safu mkapangika, za mbele misikitini Kutimu kwa Ramadhani, si mwisho wa swala tano. Tafakarini wa Bara, na wa Zenji kwa makini, Mliokuwa vinara, wa swala za Ramadhani, SWALA tano ndiyo dira, ya wakweli waumini, Kutimu kwa Ramadhani, si mwisho wa swala tano. "Swala ni nguzo ya dini", si kauli ya kubuni, Rasuli 'keshabaini, kwa mawanda hadithini, Nasaili kulikoni, na kwanini mwaikhini, Kutimu kwa Ramadhani, si mwisho wa swala tano. Mko wapi hivi sasa, baada ya Ramadhani, Mwatarajiani hasa, kwa swala sasa 'zikhini, Mwaridhia hili kosa, la kuvunja yenu dini, Kutimu kwa Ramadhani, si mwisho wa swala tano. Mwaridhikaje mioyoni, kwa ya msimu imani, Falau la kwanini, 'mwakacha' misikitini, Kama ndiyo kulikoni, lengo lenu hasa nini, Kutimu kwa Ramadhani, si mwisho wa swala tano. Uasi kwa Maulana, twaa ni kwa Ramadhani, Kama si ushirikina, huu tuiite nini, Nielezeni kwa kina, weledi wa yetu dini, Kutimu kwa Ramadhani, si mwisho wa swala tano. Abuu Nyamkomogi Mwanza.

REMUNERATION An attractive compensation package base on performance and consummate with the responsibility will apply to the successful candidates. All positions terms of employment are performance based fixed contract. HOW TO APPLY If you are interested in the positions, apply by sending a brief application letter, clearly stating why you should be considered for the position and how you will add value. With the letter, concise curriculum vitae should be enclosed showing briefly your achievement / accomplishments for you to deserve to be considered for the position. If you do not hear from us consider yourself Unsuccessful. Phone calls soliciting for these positions by applicants will automatically lead to disqualifications. All applications should be submitted to the address below not later than fourteen days after the initial advertisement. SENIOR MANAGER HUMAN RESOURCES, TANESCO LTD UMEME PARK, UBUNGO P. O BOX 9024 DAR ES SALAAM

12

AN-NUUR
MAKALA

12

SHAWWAL 1434, IJUMAA AGOSTI 23-29, 2013

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema anasikitishwa na matukio ya hujuma yaliyojitokeza Zanzibar, ikiwemo watu kumwagiwa tindikali, na kutaka uchungunguzi wa kina ufanywe kuwabaini wahusika, na baadaye ripoti ya uchunguzi huo iwekwe wazi kwa wananchi. Amesema hatua ya kuwekwa bayana ripoti za uchunguzi wa matukio hayo ya hujuma, ni jambo muafaka katika kufuta dhana zinazojengeka miongoni mwa wananchi na jamii ya kimataifa kuhusiana na watu wanaohusika kufanya hujuma hizo. Maalim Seif ameyasema hayo katika mahojiano maalum juu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar tangu kuasisiwa kwake mwaka 1964. Amesema ili amani na mshikamano wa Wazanzibari udumu, matukio kama hayo ya hujuma ambayo yamekuwa yakiwalenga zaidi baadhi ya viongozi wa dini na hata wageni, hayana budi kuangaliwa kwa upana wake, na k u wa t a k a wa n a n c h i wajiepushe na kufikia m a a m u z i ya h a r a k a kuwahusisha wengine bila ya uchunguzi wa kina kufanywa. A l i s e m a wa n a n c h i wa l i p a t a m a t u m a i n i ya kukomeshwa kwa vitendo hivyo mara baada ya hujuma zilizofanywa dhidi ya viongozi wa dini pamoja na mripuko uliotokea katika kanisa la Arusha ambapo waliahidiwa uchunguzi wa kina utafanyika na kuhusisha wapelelezi wa kimataifa, lakini hadi sasa hakuna ripoti yoyote

Maalim ahimiza kutolewa taarifa za uchunguzi


iliyowekwa bayana. Maalim Seif ameeleza kwamba badala yake matukio ya hujuma yameendelea na wananchi kuendelea kujenga dhana ya kuwahusisha watu au makundi maalum bila ya kuwa na uthibisho, jambo ambalo ni hatari kwa usalama na utulivu wa nchi. I n g e k u wa wa k a t i ule tungesema ni siasa, lakini sasa tuna serikali ya p a m o j a Z a n z i b a r , kwa nini mambo haya yanatokea sasa, huu ni mtihani mkubwa kwetu, alisema Maalim Seif. Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama C h a Wa n a n c h i C U F , amesema pia amekuwa mgumu kuamini kuwa dini inahusika katika matukio ya hujuma yaliyotokea Zanzibar. Amesema, Zanzibar ina historia ya kipekee ya uvumilivu wa kidini duniani, kutokana na wananchi wa visiwa hivi kuishi pamoja kwa miaka mingi bila ya kubaguana kwa misingi ya dini zao. Sisi Zanzibar kiwango chetu cha uvumilivu ni k i k u b wa n a n a m b a r i moja duniani, hata ukiangalia Ukristo Afrika Mashariki mlango wake ni Zanzibar, alifafanua Maalim Seif. Akitoa mfano wa uvumilivu huo, Maalim Seif amesema hata unafika mwezi wa Ramadhan huwezi kumuona mtu wa imani yoyote akila hadharani wakati wa mchana, na kwamba wananchi wote wanashirikiana katika shughuli za kijamii bila ya kujali imani zao. Ameeleza kuwa baada ya matukio ya kujeruhiwa Padri Ambrose Mkenda, kuuawa kwa Padri Evarist Mushi na mripuko wa bomu katika kanisa mjini

Tanzania Muslim Hajj Trust Safari ya Hijja 2013 Uandikishaji unaendelea gharama za Hijja ni dola za Kimarekani $ 4200. Safari ni tarehe 5 na 7 Octoba, na Kurudi Tarehe 27 na 28 Octoba, 2013. Wahi kujiandikisha Sasa. Uandikishaji wa Hijja Zijazo 2014, 2015 kwa Kulipia kidogo kidogo, unaendelea. Simu: 0717 000 065, 0784 222 911, 0754 304 518, 0754 498 888 Au kupitia Tovuti yetu. www.hajjtrusttz.org.

Taasisi ya Khidmat Islamiya inawatanganzia Waislamu wote Safari ya Hijja kwa Gharama ya Dola 4450 tu. unaweza kulipa kwa awamu (Kuhijiwa) ni Dola 1450 tu. Kuondoka ni 5/10/2013 kurudi 27/10/ 2013 Piga Simu 0784 786680, 0713 986 671, 0774 786 680 E-Mail) hajjkhidmat@gmail.com , Tovuti (Website) www.khidmatislamiya.com

Safari ya Hijja Dola 4450 tu. 1434/2013

Arusha, Serikali iliahidi kuleta makachero wa F.B.I, na hata baada ya wasichana wa Kiingereza kumwagiwa tindikali inaelezwa wachunguzi kutoka Sckotland Yard wa p o , l a k i n i h a k u n a taarifa hadi sasa iliyotolewa kuhusiana na uchunguzi huo. Tusijiegemeze kwenye dhana, uchunguzi ndio k i t u m u h i m u . H a wa wanaoathirika na hujuma mbali ya kuwa viongozi wa dini nao ni binadamu, tujiulize jee hawakujenga uhasama au kutokufahamiana na wengine huko katika jamii, alihoji Maalim Seif. Amefahamisha kuwa ni makosa kuendesha mambo kwa dhana, kwa vile matokeo yake ni kuwaadhibu watu kwa kuwaweka ndani bila ya kuwa na hatia. Amewataka wananchi kuwa makini na waendelee kuwa wamoja, ili amani, mashirikiano na umoja uliodumu uendelee wa k a t i h u u a m b a p o Zanzibar inaadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi. Wa k a t i h u o h u o Maalim Seif amekutana na Balozi mdogo wa China aliyepo Zanzibar Chen QiMan na kuelezea umakini na uadilifu wa makampuni ya Kichina katika kutekeleza majukumu yao. Amesema mara nyingi kazi za kiufundi wanazopewa wataalamu wa Kichina zimekuwa zikitekelezwa kwa umakini na kwa wakati uliopangwa, hali inayotoa matumaini ya kuendelea kutoa tenda kwa makampuni hayo. Aidha amesifu ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya China na Zanzibar ambao umekua ukichangia maendeleo ya kiuchumi na ustawi wa

Markazi Ummu Suhail ni kituo cha kuhifadhisha Qur aan kwa Mabinti wa Kiislamu. Kituo ni cha bweni kipo mkoani Kilimanjaro wilaya ya hai. Umri: kuanzia miaka 13 na kuendelea. Kituo kitafunguliwa 9/08/2013 Inshaalah. Fomu za kujiunga zinapatikana msikiti wa Riadha, wahi nafasi ni chache Kwa mawasiliano zaidi tupigie simu namba 0754 029 518 Mlete mwanao apate elimu yenye manufaa.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiteta na wageni wake nyumbani kwake Unguja. jamii. Amemtaka balozi huyo kuwa kiungo katika kuwashajiisha watalii na wawekezaji wa China kuja Zanzibar, ili kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali za kuwaletea wananchi maendeleo. Amesema China ni mshirika wa kweli wa maendeleo ambayo imekuwa ikishirikiana na Zanzibar katika kutatua kero zinazoikabili ikiwa ni pamoja na kusaidia wataalamu hasa katika sekta ya afya. Naye balozi QiMan amesema katika kipindi chake cha utumishi hapa nchini, ameshuhudia m a f a n i k i o m a k u b wa yakipatikana yakiwemo kuimarika kwa majengo, huduma za elimu pamoja n a m i u n d o m b i n u ya mawasiliano. Ameahidi kuwa China itaendelea kushirikiana na Zanzibar na kutoa michango zaidi katika kusaidia uimarishaji wa uchumi wa Zanzibar. Balozi Chen QiMan a m e m a l i z a m u d a wa utumishi hapa nchini, b a a da ya k ui t umi k i a nafasi hiyo ya ubalozi mdogo kwa kipindi cha miaka miwili na nusu. (Habari kwa hisani ya Ofisi ya MKR)

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

You might also like