You are on page 1of 16

www.annuurpapers.co.

tz

Sauti ya Waislamu

(22) AHLU SUNNA WAL JAMAA


Inawatangazia Waislamu wote kuwa imeanza maandalizi yake kwa ajili ya HIJJA 2013 kwa lengo la KUONGEZA UFANISI KATIKA IBADA ZA MAHUJAJI WETU kwa gharama za Dola 4300. Lengo letu ni kukamilisha mipango yetu kabla ya kumaliza mwezi mtukufu wa Ramadhani.Tafadhali wasiliana nasi ifuatavyo: Tanzania Bara: 0717224437; 0777462022;Unguja: 0777458075;Pemba: 0776357117.

Profesa ailaumu Serikali malalamiko ya Waislamu


ISSN 0856 - 3861 Na. 1082 RAMADHAN 1434, IJUMAA , AGOSTI 2-8, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Agusia uwiano mbaya katika ajira Aibua mauwaji ya Mwembechai Ahoji ripoti ya mabomu Arusha

Na Bakari Mwakangwale

BAKWATA kusambaza Mashushushu misikitini


BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania, B A K W A T A , limetangaza mpango wake wa kusambaza mashushushu Misikitini. Akitangaza mpango

huo, Mufti wa Baraza hilo Sheikh Issa Shaaban Simba amesema kuwa mashushushu hao wa t a k u wa wa k i t o a taarifa zao Polisi. Mui Simba amesema kuwa hatua hiyo inakuja kufuatia hali

BAADHI ya wafanyakazi wa Benki ya Amana wakikabidhi misaada kwa kituo cha watoto yatima cha Tahdhil Quran Al-hidaaya cha Buguruni kwa Mnyamani, Ilala Jini Dar es Salaam hivi karibuni.

Magaidi wa gazeti la Rai na kisa cha Jessica Lynch


Binadamu sio mtu wa Ndio tu Tutumie vyema neema ya akili Tusiwe vipaza sauti visivyojijua

Zanzibar Daima ulingoni karibuni


Na Mwandishi Wetu
I M E FA H A M I K A k u w a Jarida litakalo fahamika kwa jina la Zanzibar Daima litazinduliwa hivi

Inaendelea Uk. 3

karibuni. Jarida hilo la kila mwezi litakuwa likichambua kwa kina matukio yanayojiri Zanzibar. Litasheheni makala za

Inaendelea Uk.5

2
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Tahariri/Makala
AN-NUUR
BAKWATA? Inahitaji shilingi ngapi kuvuta maji ya uhakika hapa badala ya mtindo huu wa kujaza maji katika mapipa na kuchota kwa makopo, hali ambayo kiusa ni utata mtupu? Huu ni Msikiti wanaposwali viongozi wa Serikali ama Ijumaa au siku za Eid, hivi wakishikwa na haja watawapeleka katika vyoo gani? Alisimulia mtu huyo jambo ambalo limethibitishwa na wengi. Sasa labda kama ni kubadilika, hali iwe imebadilika katika mwezi huu wa sita na saba ambapo gazeti hili halapata taarifa mpya. Sasa sisi tungependa kushauri kuwa pengine Sheikh Mkuu wa Bakwata na viongozi wenzake, watakuwa wamefanya jambo kubwa sana, na lipo katika uwezo wao, kama watahakikisha kuwa Misikiti yao ni misafi

RAMADHAN 1434, IJUMAA AGOSTI 2-8, 2013


n a i n a wa k i l i s h a ya l e mafundisho ya Uislamu Al Islam nadhiifu. Haya ya kufanya ukachero Misikitini hawayawezi na wakaribu yatazidi tu kutia nguvu madai ya Waislamu wengi kuwa Bakwata ni chombo cha Serikali zaidi kuliko kuwa cha Waislamu. Wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, Maaskofu wa l i t o a I l a n i ya o ya uchaguzi. Na ilisemekana kuwa baadhi ya watu wazito (Wakristo) walio serikalini, walishiriki kuandaa Ilani hiyo. Kana kwamba hiyo haitoshi, Maaskofu mbalimbali wa l i s h i r i k i k u m p i g i a kampeni mtu waliyedhani kuwa ndio anafaa baada ya kuona kuwa lile waliodhani kuwa ni chaguo la Mungu, halifai tena kwa mtizamo wao. Ilifika mahali katika baadhi ya sehemu, waumini walitengwa na makanisa yao baada ya kuonekana kuwa wanaunga mkono mtu asiyetakiwa na kanisa. Vurugu zilizotokea Arusha bara baada ya uchaguzi mpaka kuleta maafa, ilikuwa wazi jinsi maaskofu walivyokuwa wakishabikia wakiwa upande fulani wa wanasiasa na wa chama fulani. Hilo mpaka hivi sasa halijasemwa kwa uzito na vyombo vya dola au viongozi wa makanisa na kuoneshwa kuwa ni tatizo la kuharibu amani na usalama wa nchi. Lakini leo kauli kama hizi za Masheikh wetu, itajengwa picha kuwa tatizo la nchi hii ni Waislamu kwa hiyo nguvu zote za dola kama alivyowahi kujisemea Alhaji Ally Hassan Mwinyi, kwamba nguvu zote za Dola ziwaangukie. Hii ni katika mlolongo ule ule wa kuwapachika uovu Waislamu sawa na ule wa kuwapachika ugaidi. Hebu Masheikh wetu wasaidie kujenga Uislamu na nchi.

AN-NUUR

MAONI YETU

Mufti Simba ukachero mwachie Said Mwema


Unda vikundi vya usa Misikitini Anza Msikiti Bakwata Makao Makuu
KWA mujibu wa habari iliyotolewa na gazeti la NIPASHE Jumapili tarehe 28 Julai, 2013, Sheikh Mkuu na Mufti wa Bakwata ametangaza kuunda vikundi vya ulinzi na usalama kwa kila msikiti nchini. Akasema kuwa lengo la kuanzisha vikundi hivyo ni ili vifanye kazi ya ukachero. Na kwamba kazi yake kubwa itakuwa kubaini viashiria vya uvunjifu wa amani na vitakuwa vikitoa taarifa Polisi. Kwa maana kuwa vitakuwa ni mashushushu wa Bakwata wanaoitumikia Serikali/Polisi ndani ya Misikiti. Kisa na mkasa, anadai kuwa Misikiti inatumika kama majukwaa ya kisiasa. Kwa upande mwingine Sheikh Khalifa Hamis akanukuliwa akiwahimiza Polisi wachunguze Misikiti kwa sababu hata ndani ya Misikiti kuna wahalifu. Kwamba wasidhani kuwa ndani ya Misikiti h a k u n a v i t e n d o v ya JINAI. Akaunga mkono rai ya Mufti wa Bakwata ya kuunda vikundi vya kikacherondani ya Misikiti ila akatahadharisha kuwa viundwe na watu halali. Kwa upande mwingine akasema kuwa karibuni zitaanza harakati za uchaguzi Serikali za Mitaa na kisha Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, kuwa tahadhari ichukuliwe misikiti isije ikatumika kama vijiwe vya wanasiasa. Wo t e k w a p a m o j a waliyasema hayo katika futari iliyoandaliwa na taasisi ya Imam Bukhari inayoongozwa na Sheikh Khalifa Hamisi na kuhudhuriwa na Rais Ms t a a f u Al l y H a s s a n Mwinyi. Akifafanua juu ya vikundi hivyo vya kikachero Misikitini, Mufti wa Bakwata anasema kuwa uamuzi wa kuunda vikundi hivyo v ya k i k a c h e r o k a t i k a Misikiti umebuniwa kwa p a m o j a n a M k u u wa Jeshi la Polisi nchini Saidi Mwema katika kikao chao cha pamoja kilichohusisha makamanda wa ngazi mbalimbali wa Polisi. Sisi tungependa kusema kuwa pengine Mufti wa Bakwata angeshughulishwa kwanza na usafi wa Misikiti ya Bakwata. Haya ya ukachero awaachie wenye kazi zao. Tunafahamu kuwa kila nchi ina vyombo vyake vya usalama mitaani, maosini, makanisani, misikitini na hata katika kada na jamii ya vichaa. Hakuna Serikali yoyote duniani inayongoja kupewa taarifa na Masheikh au vikundi vilivyoundwa na maMui. Na ikiwa hivyo, basi Masheikh na ma-Ustadh hao watakuwa wamepewa mafunzo na kuajiriwa na Serikali. Hawateuliwi wala kupewa kazi na Mui wa Bakwata. Mpaka mwezi wa tano mwaka huu, Msikiti uliopo Makao Makuu ya Bakwata, Kinondoni jijini Dar es Salaam, ulikuwa hauna maji ya kuaminika. Ukika kuswali inabidi ukienda msalani ubebe maji na kopo kutoka mapima yaliyowekwa nje ya choo na sehemu ya kutawadhia. Hali ya usafi wa vyoo hivyo utata mtupu. Si vyoo vyenye hadhi ya Msikiti wa Mak ao M a k u u ya Bakwata. Mtu mmoja aliyesali hapo kwa mara ya mwisho mwezi wa tano, alibaki akiuliza: Hivi inahitaji shilingi ngapi kujenga vyoo visa katika Msikiti huu wa

KUMI LA MWISHO RAMADHANI


WA P E N Z I Wa i s l a m u , siku za mwezi mtukufu wa Ramadhani zinaelekea tamati. Hivi sasa tupo katika kumi la mwisho la kuwekwa mbali na moto, kati ya makumi matatu ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Wakati tukiwa katika kumi hili la mwisho, ni vyema tukajiuliza, tumefaulu kwa kiasi gani na makumi mawili yaliyopita ya Ramadhani. Yaani kumi la Rehma la lile la pili la Maghra. Ni vizuri tukajitathmini kwa vitendo vyetu kabla ya kufika siku ya kufanyiwa hisabu. Hata hivyo bado wakati upo na fursa ya kuendelea kufanya mambo ya kheri bado inaendelea. Katika kumi la mwisho, Waislamu wameruzukiwa neema nyingi na za kheri katika maisha yao hapa duniani na kesho akhera. Hazina kubwa katika kumi hili la mwisho la Ramadhani, ni Waislamu kuruzukiwa usiku mtukufu wa Lailatul Kadr. Wengi wanaufahamu kama usiku wa cheo, usiku wa kuachwa huru na maasi na mja kuzaliwa upya. Ndugu Waislamu, Allah (SW) anaupenda sana umma huu wa Waislamu. Kwa mapenzi yake juu ya umma huu, kaujalia malipo na thawabu nyingi kwa kutekeleza ibada ndogo ya usiku wa cheo, usiku mtukufu, usiku moja lakini thawabu zake ni nyingi kushinda thawabu za ibada katika miezi elfu moja. Ama kwa hakika ni usiku muhimu sana katika umri wa mwanadamu , ndani yake kuna Mwenye kuafikiwa usiku huo, basi amepata kheri ya dunia na akhera. Na mwenye kukosa usiku huo, basi amekosa kheri ya dunia na akhera. Ni khasara ilioje mtu kuishi duniani miaka mingi kisha aondoke duniani patupu bila ya kupata kheri ya dunia wala kheri ya akhera. Ndugu Muislamu tafakari na uzingatie, hujui kama utafika mwakani ili uweze kufunga Mwezi wa Ramadhani. Baadhi ya sunna za kumi la mwisho ni kufanya bidii kuswali swala ya usiku. Ni vyema kila Muislamu akawahimiza watu wake nyumbani kwake kuamka kuswali pamoja. Amesema Mtume (Saw), Mwenye kusimama u s i k u k a t i k a m we z i wa Ramadhani kwa Ikhlasi na kutarajia malipo kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyo tangulia. Moja ya mafundisho katika Sunna za Mtume (s.a.w) ni kuwa, ilipokifika kumi la mwisho, alikuwa akiamsha wake zake na familia yake kujitahidi kusimama usiku katika swala. Kutia nia ya kukaa msikitini kwa lengo la Kufanya ibada ya Ibada ya Itikaaf, kusoma zaidi Quran katika kumi hili la mwisho, ni jambo zuri kwa Waislamu katika siku hizi. Kuzidisha juhudi kutafuta usiku wa cheo, usiku bora

Mwenyezi Mungu awajaalie Waislamu kupata Lailatul Qadri


kuliko miezi elfu moja, ni bora kuliko vitu vyote vilivyomo duniani. Mwenye kuakiwa kupata usiku huu, basi ni hakika amefaulu na kupata kheri ya dunia na akhera. Katika mafundisho ya Mtume (s.a.w) alishasema kuwa ni sunna kuzidisha kusoma Quran kwa wingi, kumsifu Allah, kumtukuza, kumsalia Mtume na kutoa sadaka na ni sunna kuomba dua kwa wingi. Ndugu Waislamu, siku kumi katika kumi la mwisho ni chaguo lake Allah (SW) kwa Umma wetu na ukombozi kwenu. Umri wetu ni mfupi sana, mwanadamu hajui kama ataweza kupata nafasi tena kukia mwezi wa Ramadhani mwakani. Jambo la msingi ni kufanya bidii na juhudi kubwa kutafuta usiku wa cheo katika kumi hili la mwisho, ili tupate kheri ya usiku huu. Yule atakaye bahatika kupata usiku huu, kwa hakika huyo amefaulu hapa duniani na kesho akhera. Ni jukumu lenu kufanya bidii kumuiga Mtume katika ibada zake zote, na kushindana katika kutafuta siku wa cheo (Laylatul Qadri) katika kumi hili. Tunamuomba Allah (SW) atuajalie kuwa miongoni mwa waliochaguliwa kupata Lailatul Qadri na hatimaye kutuingiza pamoja na Mtume (s.a.w) katika Jannatul Firdaws.

BAKWATA kusambaza Mashushushu misikitini


Inatoka Uk. 1

Habari

RAMADHAN 1434, IJUMAA AGOSTI 2-8, 2013

AN-NUUR

akisema.

Bawazir azungumzia miaka 1447 ya Quran


Na Mwandishi Wetu
WAKATI Qur an tukufu ikitimiza miaka 1447, tangu kushuka kwake, Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania (Hay-at), umeutaka Ulimwengu kuishi kwa kutambua kuwepo kwa Mwenyezi Mungu. Wito huo umetolewa na Sheikh Abdallah Bawazir, akiongea kwa niaba ya Umoja huo katika osi zao zilizopo Kariakoo Jini Dar es Salaam, Jumatano wiki hii. Sheikh Bawazir ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo, alikuwa akitoa pongezi kwa Waislamu ndani na nje ya nchi kwa kushuhudia Qur an, ikikisha miaka 1447, tangu ishushwe ardhini. Pongezi kwa wingi kwa Waislamu wote Ulimwenguni kwa ujumla, kwa kufikia miaka 1447, (Jumatano hii) tokea ishuke Qur an katika ardhini. Tunasheherekea katika kumi hili la mwisho lenye Lailatulqadir, siku ambayo imeshuka Qur an. Amesema SheikhBawazir. Alisema, wakati Qur an, imekuja ikiwa ni mwongozo k wa wa n a a d a m u b a l a a lilipo duniani hivi sasa ni watu kujaribu kumkataa Mungu, ilihali vitabu vyote vimekuja vikielezea uwepo wa Mwenyezi Mungu. Qur an ni kitabu cha nne, katika vitabu vyenye uongofu, ambavyo Mwenyezi Mungu kaviteremsha kwa Mitume wake. Imeshuka Taurat, Zaburi, Injiri na Qur an ni kitabu cha mwisho ambacho kimekusanya vitabu vyote hivyo, ikitoa muongozo wa maisha ili wanaadam tuufuate na tuweze kuishi kwa amani. Amesema Bawazir. Sheikh Bawazir, alisema Ulimwengu wa leo unakwenda mahala pabaya, badala ya Mataifa makubwa kuwa mstari wa mbele kufundisha ustaarabu duniani, lakini yamekuwa yakihamasisha watu kwenda kinyume na m a a r i s h o ya M we n ye z i Mungu. Alisema, Mataifa hayo yamekuja na sera ya kuhamasisha ndoa za jinsia moja kitu ambacho ni kinyume kabisa na mwongozo na Mwenyezi Mungu alipinga na kutolea adhabu siku nyingi. Bawazir alisema suala hili halijaruhusiwa hata katika vitabu vilivyotangulia, tangu Taurat, Zaburi, Injiri mpaka Qur an, akasema ndani ya vitabu hivyo hakuna sehemu ilipohalalishwa mahusiano ya jinsia moja. Leo Ulimwengu unataka kuleta baa kubwa zaidi ya hata ya lile la kipindi cha Nabii Luti, tunapoangalia katika vitabu tunavyosoma hayo yalikuwa yakifanyika, lakini hawakufikia hatua ya kuhalalisha ndoa kama ambavyo hayo Mataifa makubwa wanavyo shinikiza Ulimwengu ukubali suala hilo. Alisema Bawazir. Sheikh Bawazir alisema wa k a t i wa N a b i i L u t i , ilikuwa katika kijji kidogo na baadhi ya vi vya jirani

inayoendelea ambapo amedai kuwa Misikiti imegeuzwa kuwa majukwaa ya kisiasa na hivyo kuhatarisha amani ya nchi. Akasema, baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakiwahamasisha Waislamu kuasi Bakwata kiasi cha kukia kudai kuwa Baraza hilo lifutwe. W a i s l a m u wanachuuzwa na wanasiasa na kusema Baraza la Waislamu Tanzania lifutwe, misikiti si kwa ajili ya siasa bali ni sehemu ya kuwaelekeza watu kutenda mema, alinukuliwa Mui Simba

Kwa mujibu wa taarifa za baadhi ya magazeti, Sheikh Mkuu, Mufti S i m b a wa B a k wa t a amesema kuwa mpango huo umependekezwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema. Akasisitiza kuwa makachero hao wa Bakwata wakishabaini viashiria vya uvunjifu wa amani, watatoa taarifa Polisi.

Akaongeza kuwa kutokana na hali hiyo BAKWATA inakusudia kuanzisha Kamati za Ulinzi na Usalama Misikitini ili kubaini viashiria vya uvunjifu wa amani.

Na Bakari Mwakangwale wamefungwa. Katika ziara hiyo, Kamati imetoa misaada kadhaa KAMATI ya Maafa ya kutoka kwa Waislamu Shura ya Maimamu imetembelea Magereza ya katika Mwezi huu wa Kimbiti Mngaru pamoja Ramadhani. Miongoni mwa misaada na Dondwe Mvuti, Mkoani waliopatiwa Waislamu hao, Pwani, ambayo baadhi ya Waislamu wa maandamano waliohukumiwa baada ya kudaiwa kuandamana kupinga Sheikh Ponda, kunyimwa dhamana ni Mchele kilo 135, Tende kilo 20, mafuta ya kula lita 20, pamoja na Maharagwe kilo 35. anayestahili kuabudiwa kwa vilihitaji kwenda kinyume Mbali na mahitaji hayo na mwongozo wa Mwenyezi kufuata sheria zake na kuacha kumbuka awali Waislamu makatazo yake. M u n g u a n a v yo t a k a , n a h a o wa l i omba vitabu Bawazir, alisema hata vikaangamizwa maangamizi mbalimbali vya dini, hivyo washirikina wa Mji wa Makka, tofauti. Alisema, wanaadamu leo waliokuwa wakimpinga kwa tulipeleka vitabu vya tafsiri nguvu zote Bwana Mtume wanajiona wameendelea Muhammad (s a w), walikuwa za hutuba za Ijumaa pamoja sana, na kutaka kufanya wanakubali kuwa Mungu na vitabu vya swala na watakavyo wakisahau kuwa yupo, ingawa walikuwa maamrisho yake. Alisema upo muongozo wa Mwenyezi w a k i a b u d u m a s a n a m u P o n d a a l i y e o n h g o z a msafara huo. Mungu. wakiamini kuwa yapo karibu Kwa mujibu wa Sheikh Nadhali hii ya makosa au na Mungu wa kweli, lakini Ponda, hali za Waislamu kufuru hii ya kupingana na zaidi wakihoa maslahi yao. hao ni nzuri na katika Qur an ikiendelea sambamba Alisema, hivi sasa Mataifa maongezi yao wameeleza na mashinikizo wanayoyatoa makubwa yanapambana kuwa hawana cha kujutia ya kuzuia misaada mpaka kuhakikisha kwamba watu katika hatua hiyo na kuwa suala hilo la kuwadhurumu wenye itikadi sahihi ya watakuwa mstari wa mbele wa n a wa k e h a k i z a o n a k u we p o M u n g u h a we z i kupigania Uislamu, hata kuwadhalilisha wanaume kuongoza, hivyo wanawapiga baada ya kifungo hicho. likubalike tufahamu kwamba vita ili waweze kuweka sheria Alisema, Waislamu hao yaliyotokea wakati wa Nabii zao ambazo zinapingana na wamekuwa wakiendeleza Luti, yatatutokea na sisi. muongozo wa Mwenyezi i b a d a n a k u wa f a n y i a Kumbuka kama vile Daawa wafungwa wengine vilikuwa ni vijiji na leo Mungu. jambo ambalo wamedai Awali Sheikh Bawazir, wamefaulu kuwabadilisha tunaambiwa kuwa Dunia ni kama Ki kimoja unadhani alisema kwamba Qur an, kitabia miongoni mwa hali itakuwaje. Alitanabaisha ilishuka kwa muda wa miaka wafungwa waliowakuta Bawazir. 23, kidogo kidogo, kwa huko. B a w a z i r a l i s e m a hekima, ili kumpa nguvu Sheikh Ponda alisema wa n a o k a t a a u w e p o wa Mtume Muhammda (s w a), kwa ujumla wameshukuru kwa kupata misaada hiyo, Mwenyezi Mungu wana katika kazi yake ya Daawa. huku wakiomba zaidi malengo ya kuweka sheria Alisema, kadhia ya kwanza hata siku ya na taratibu zao nje ya zile za iliyoshuka katika Qur an, kukumbukwa sikuku ya Idd, ili na wao Mwenyezi Mungu. ni elimu, na kubwa zaidi ni waweze kufurahi na kula Alisema, kutokana na hali ile elimu inayoambatana na vizuri katika siku hiyo ya hiyo ndiyo Mitume wengi kumjua Mwenyezi Mungu sikuku. walipata upinzania kutoka na asili ya mwanaadam Ombi lao hili kwa watawala na hata kukia ni kukubali kuwa Mungu tunalifanyika kazi lakini miongoni mwao kuuwawa, yupo. pia hii ni taarifa kwa kama ilivyokuwa kwa Nabii Hii ndiyo itikadi sahihi Waislamu wengine ambao Zakaria, Nabii Yahaya. iliyokuja na Qur an Kariim, wangependa kuwasaidia Alisema, kabla ya kushuka lakini zile zilizo zuka za ndugu zao walipo huko. Qur an, kadhia ya kumjua kumkataa Mungu hizo ni Alisema Ponda. Mwenyezi Mungu ilikuwa itikadi za makosa, kwa maana Katibu huyo wa Jumuiya inajulika amb apo Qur kwamba mtu wa kwanza na Taasisi za Kiislamu, an, imekuja kutilia nguvu ni baba yetu Adam, ambao alisema mwishoni mwa wiki suala alilokuja nalo Nabii sisi wote asili yake inarejea hii (Jumapili) wataendelea Adam (a.s) kuwa Mungu k wa k e . A l i s e m a S h k h . na ziara katika magereza yupo na yeye ndiye pekee Bawazir. mengine matatu ambayo

Katika kufanikisha mpango huo wa u s h u s h u s h u Misikitini, Maimamu na Masheikh wa Bakwata wa t a s h i r i k i a n a k wa karibu na makamanda wa Polisi na kwamba B A K WAT A M a k a o Makuu itasambaza taarifa kwa Maimamu wa misikiti nchini namna ya kutekeleza na kufanya mawasiliano na maosa wa Polisi. Msikiti wowote utakao kuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani, taarifa itatolewa Polisi (mara moja) ili kulinda amani ya nchi, Mufti Simba amesema na kunukuliwa na gazeti

moja wiki iliyopita. Sheikh huyo Mkuu wa Bakwata ameyasema hayo a l i p o h u d h u r i a futari iliyoandaliwa na Taasisi ya Imam Bukhar,

Kamati ya Maafa Shura yatembelea wafungwa

inayoongozwa na Sheikh Khalifa Hamis. Katika futari hiyo a l i k u we p o p i a R a i s Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi.

Profesa ailaumu Serikali malalamiko ya Waislamu


Na Shaban Rajab
alikuwa peke yake au lah, lakini baada ya taarifa zile mpaka leo kimya, alisema Prof. Kilian. Katika hali hiyo ikasemwa k u wa k u k o s e k a n a h a k i miongoni mwa jamii ya Watanzania, kukithiri migogoro ya udini isiyotatuliwa, ndio viashirika vikubwa vya kutoweka amani nchini. Aidha imeelezwa kuwa Serikali ndiyo itakayoingia lawamani kwa kushindwa kuchukua hatua sahihi katika kutatua mizozo ya kidini na kusimamia haki miongoni mwa wananchi wake, kiasi cha kusababisha kukithiri migogoro ya kidini na dhulma, hali inayotishia usalama wa nchi siku za usoni. Akiwasilisha mswada wake mbele ya wajumbe waliohudhuria katika mjadala huo, Profesa Benadetha Kiliani, alisema hadi sasa serikali imeshindwa kuchukua hatua sahihi kushughulikia kiini cha kuwepo hatari ya kutoweka amani nchini. Badala ya serikali kuchukua hatua za kuchunguza viini vya matatizo yanayohatarisha amani nchini na kupata suluhu ya kudumu, yenyewe imekuwa ikitumia vyombo v ya u s a l a m a k u d h i b i t i migogoro na malalamiko yanayotolewa. Kutokana na hali hiyo, Prof. Kiliani alisema pamoja na kwamba serikali inaona kuwa njia hiyo ni salama na sahihi, lakini tusitegemee kamwe kwamba vyombo hivyo vya usalama vitatatua migogoro inayohatarisha amani kwa kuthibiti zaidi. Alitoa mfano kwamba mara nyingi njia inayotumika kudhibi badala ya kutatua tatizo ni kuwepo kamata kamata inayofanyika, mtuhumiwa kubambikiwa kesi, milipuko ya mabomu ya machozi, wakati mwingine kukamata na kupiga hadi k u u a n . k . , k wa m a a n a kwamba serikali imekuwa ikishughulishwa na matokeo tu ya tatizo kuliko kuchunguza na kutatua chanzo cha migogoro. Alisema kwa staili hiyo, serikali inadhibi tu sio kuchunguza na kubaini chanzo cha tatizo na kukiondoa. Aidha alivikosoa vyama vya siasa na wanasiasa kwa ujuma, ambao wanatumia m u d a m w i n g i k u wa z a kuingia madarakani huku amani ya nchi ikiwa katika hali tete bila kuchukuliwa hatua za kuinusuru na mapema. Alisema viongozi wa kisiasa wamejikita kwenye masuala ya uchaguzi kuliko kushughulikia mogogoro ya amani na sababu kubwa ni uchu na uroho wa madaraka na kwamba hivi sasa vikao vya kuwania madaraka nani awe rais ndio mjadala mkuu. CCM hivi sasa wanatumia muda mwingi kuzungumzia uchaguzi mkuu ujao, nani atakuwa mgombea, CHADEMA nao wanatumia muda mwingi kujihami na polisi na kufuatilia kesi mahakamani. Tu n a we z a k u j i f u n z a kwa CUF, nao walikuwa na misimamo ya jino kwa jino, ngangari, lakini walibadili mbinu, wakaja na falsafa ya kujadili mambo kwa amani na imewasaidia kwa kiasi kikubwa, leo tumeona walivyofanikiwa. Kuna haja ya kubadilika, wana siasa tuanze kujadili zaidi juu ya amani iliyo hatarini, alisema Mhadhiri huyo. Zilitajwa sababu nyingine zinazoleta hofu ya kuondoka amani kuwa ni pamoja na hali ya upinzani kuja juu na kulazimu chama tawala kinajihami kutokana na mabadiliko hayo. Aidha kuongezeka kwa k i wa n g o c h a u m a s k i n i na kushitadi mfumo wa kiliberali, kumechangia matabaka katika jamii na uhuru wa kutoa maoni tofauti na enzi za siasa za ujamaa za chama kimoja. Mhadhiri wa Sheria wa Chuo hicho, Dk. Onesmo Kyauke aligusia mfumo wa utendaji wa Jeshi la Polisi katika kusimamia amani ya nchi, ambapo alisema jeshi hilo limekuwa likikiuka sheria na maadili katika kutekeleza majukumu yake, hivyo kuwa chanzo kikubwa cha uvunjifu wa amani nchini. Kuzuia maandamano ya amani na kifo cha mwandishi wa habari Daudi Mwangosi, ilikuwa mifano ya udhaifu katika jeshi hili. Dk. Kyauke alisema tatizo jingine katika jeshi hili kiasi cha kuhatarisha amani ni kukubali kuingiliwa na wanasiasa na kuelekezwa jambo la kufanya kwa maslahi ya wanasiasa hao badala ya umma wa Tanzania. Kwa upande wake Mhadhiri katika Shule Kuu ya Habari Dk. Ayoub Rioba, alisema nchi ambazo hazikurekebisha makosa ya kihistoria ya ukoloni, ndizo zinazotishiwa zaidi na ukosefu wa amani. Aidha alitaja tatizo jingine kuwa ni upendeleo katika ugawaji wa keki ya Taifa, rushwa kugombea madaraka, u b a g u z i k wa l u g h a ya wenzetu na ukandamizaji. Alivitaka vyombo vya habari kwenda mbali na kuchimbua historia zaidi ili kutambua kwamba historia ya Taifa hili sio baada ya

HABARI/Tangazo

RAMADHAN 1434, IJUMAA AGOSTI 2-8, 2013

AN-NUUR

PROFESA Benadetha Kiliani amesema hadi sasa serikali imeshindwa kuchukua hatua sahihi kushughulikia kiini cha kuwepo hatari ya kutoweka amani nchini. Profesa Kiliani ambaye ni mtaalam wa Sayansi ya Siasa na Utawala kwa Umma na Mhadhiri wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari, ameyasema hayo katika mdahalo wa kujadili mstakabali wa amani ya taifa letu miaka hamsini ayo. Mdahalo huo umefanyika katika ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita na kuwashirikisha wa n a s i a s a , wa h a d h i r i , wanachuo, taasisi za serikali na zisizo za kiserikali, viongozi wa vyombo vya usalama na wa serikali. Katika mada yake Pro. Kilian alitolea mfano wa migogoro ambayo imekosa ufumbuzi wa kudumu kuwa ni tatizo la udini kati ya Waislamu na Wakristo. Alisema kuna tatizo kati ya Waislamu na Wakristo, a m b a p o Wa i s l a m u wanalalamikia uwiano wa ajira kati yao na Wakristo serikalini. A k a s e m a , Wa i s l a m u wanaona kwamba wanakosa haki katika mamlaka za serikali na utawala kwa ujumla huku wenzao Wakristo wakiwa ndio wengi katika medani hizo. Aidha alikumbusha matatizo mengine ambayo hayakupatiwa suluhu na kusababisha jamii kuendelea kuishi kwa chuki kuwa ni sakata la Mwembe Chai, ambalo alilitaja kuwa lilikuwa maarufu zaidi kama Mwembechai saga. Alisema kuwa matatizo kati ya Waislamu na Wakristo hayajapatiwa ufumbuzi wa kudumu, zaidi ya dola kutumika kudhibiti tu tatizo, jambo ambalo amesema ni la hatari zaidi kwa amani ya Taifa siku zazo. Hata hivyo alisema migogoro ya kidini haipo kati ya Waislamu na Wakristo tu, bali hata ndani ya dini moja. Sote tunakumbuka mgogoro wa KKKT Dayosisi ya M e r u k u l e A r u s h a , mgogoro mwingine ni ule katika Dayosisi ya Pare n.k. Alitoa mfano Prof. Kilian Akibainisha zaidi namna serikali inavyoshindwa kutatua mizozo inayohatarisha amani nchini, alisema mpaka sasa Watanzania hawajui aliyelipua bomu katika mkutano wa CHADEMA kule Arusha ni nani. Kulipuliwa Kanisa kule Olasiti Arusha tumeambiwa alikamatwa kijana wa pikipiki, hatujui yule kana

uhuru bali tangu ukoloni. Aidha amevishauri vyombo vya habari kuacha kutumiwa kwa maslahi ya wanasiasa na kusababisha mogogoro na kuvunja amani, kwani mara nyingi wanasiasa huwa wanavitumia kama bunduki na kujikuta vinaingia katika kuleta machafuko na kuvunja amani ya nchi. Akihitimisha mjadala huo, Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel Nchimbi, alikiri kuwepo upungufu upande wa serikiali na wa asasi nyingine za kisiasa. Hivyo alishauri UDASA kutoishia hapo walipokia, bali waandae zaidi madala ya amani ili kuikosoa serikali na kuelekezana njia nzuri za kulinda amani ya nchi. D k . N c h i m b i aliwahakikishia waandaaji na waliohudhuria mjadala huo kwamba, atafanya juhudi kuhakikisha madala ya aina hiyo inakwenda mikoani hadi wilayani na hatimaye Taifa kwani kati ya mambo ambayo yanampa changamoto ni amani ya nchi hii. Alisema ingawa kuna vikao bado vinaendelea kati ya serikali na viongozi wa dini, lakini tatizo la udini bado halawekewa mikakati. Alisema kuwa wao walirithi nchi ikiwa na amani, hivyo wa deni la kurithisha nchi hii kwa kizazi kacho ikiwa na amani.

Habari za Kimataifa/Tangazo

RAMADHAN 1434, IJUMAA AGOSTI 2-8, 2013

AN-NUUR

BEIRUT Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah, amesema k u wa s u a l a m u h i m u kwa wanaharakati hao ni kwamba wanaungwa m k o n o n a wa n a n c h i wa Lebanon, mataifa ya Kiarabu na ulimwengu wa Kiislamu. Hassan Nasrullah, ambaye alikuwa akijibu hatua ya Umoja wa Ulaya ya kuiweka Hizbullah katika orodha yake ya m a k u n d i ya k i g a i d i , alisema Jumatano jioni wiki hii, katika karamu ya futari iliyotayarishwa na Hibzullah mjini Beirut kwamba, wana mapambano wa Hizbullah wamebadili kanuni za mapigano, wakabatilisha m i p a n g o ya a d u i n a kukomboa mateka na ardhi za Lebanon zilizokuwa katika makucha ya Wazayuni na wataendelea kuwa mwiba katika jicho za Israel. Sayyid Nasrullah amesema Hizbullah haikushangazwa na hatua ya Umoja wa Ulaya ya kuiweka katika orodha ya k e ya m a k u n d i ya kigaidi, kwani uamuzi huo ulikuwa ukisubiriwa k wa m u d a m r e f u n a kwamba,wameshangaza ni wahusika kuchelewa na uamuzi wao huo. K a t i b u M k u u h u yo wa Hizbullah amesema, Umoja wa Ulaya (EU) unatumikia maslahi ya Israel na kwamba, umoja huo umetwishwa maamuzi hayo kwa sababu yanapingana na thamani za nchi za Ulaya. Nasralla amesisitiza kuwa, harakati hiyo ya mapambano itaendelea kuwepo na itashinda kwa uwezo wake Allah. Awali Umoja wa Ulaya kuliwawekea vikwazo wanaharakati ya Hizbullah Lebanon, ambapo Bw. Nasrallah alisema, nchi hizo 28 za Ulaya zinafuata kibubusa maagizo kutoka Marekani. Julai 22, chini ya shinikizo la Marekani na utawala dhalimu wa Israel, Umoja wa Ulaya uliamua

Hizbullah inaungwa mkono na wananchi


kuliwekea vikwazo tawi la kijeshi la Hizbullah, ambapo sawa mataifa hayo yameamua kuiingiza Hizbullah katika oodha ya makundi ya kigaidi. Kwa muda mrefu Hizbullah imethibitisha kuwa, imekuwa ngome imara mbele ya chokochoko zote za utawala ghasibu wa I s r a e l n a v i t i m b i vya nchi za Magharibi ambazo zimetambua kuwa, wapambanaji wa Hizbullah ni kisiki kikubwa kinachokwamisha malengo yao machafu katika eneo hilo. Nchi kadhaa duniani ikiwemo Iran, zimeonyesha upinzani dhidi ya uamuzi huo wa Umoja wa Ulaya (EU) wa kuiweka harakati ya Hizbullah katika orodha yake ya makundi ya kigaidi, na kulaani hatua hiyo ya kuchukiza ya Umoja wa Ulaya na kuitaja kuwa ni ya kisiasa. Spika wa Majlisi ya Iran, Ali Larani, amelaani vikali hatua amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu itaendelea kuunga mkono kikamilifu harakati ya Hizbullah ya Lebanon. Bw. Larani ameongeza kuwa uamuzi wa Umoja wa Ulaya umetokana na sababu kuwa, Hizbullah i m e k u wa i k i w a l i n d a watu wa Lebanon ambao wanakabiliwa na uhasama m k u b wa wa u t a wa l a wa Kizayuni wa Israel. Larani aliashiria ushindi wa Hizbullah dhidi ya Israel katika vita vya siku 33 mwaka 2006 na kusema, ushindi kama huo umezitia wasi wasi nchi za Magharibi. Nchi za Kiarabu na ulimwengu wa Kiislamu zimetilia wasiwasi uamuzi huo wa Umoja wa Ulaya na Israel na washirika wake. Imeelezwa kuwa hatua hiyo ya Umoja wa Ulaya itazidisha chuki na hasira za walio wengi katika Mashariki ya Kati na kwenye Umma wa Kiislamu dhidi ya umoja huo. Imeelezwa kuwa kushindwa mara kwa mara kwa utawala wa Kizayuni katika mapambano na Hizbullah huko Lebanon, kumezua wasiwasi mkubwa utawala ghasibu wa Israel na washirika wake wa Kimagharibi. Kutokana na hali hiyo Israel na nchi hizo za Ulaya zimeamua kuchukua hatua kama hizo za kuiweka Hizbullah katika makundi ya kigaidi, lengo likielezwa kuwa ni kutoa nafasi ya kundi hilo kujengewa chuki na jumuia za kimataifa, lakini zaidi ikiwa ni kusaka sababu ya kulipiza kisasi dhidi ya wapambanaji hao wa Hizbullah katika upande wa pili.

Aidha kwa hatua hiyo, Umoja wa Ulaya unaelezwa kuwa unataka kuzipotosha fikra za walimwengu kuhusu sura ya kigaidi ya Israel na kuhusu misaada yake kwa makundi mbalimbali ya kigaidi ya Mashariki ya Kati hususan huko Syria.

Zanzibar Daima ulingoni karibuni


Inatoka Uk. 1
kisiasa, uchumi, burudani na utamaduni wa Kizanzibari. Hata hivyo taarifa kutoka vyanzo vyetu vya habari ndani ya Zanzibar na katika mtandao vinafahamisha kuwa kwa kuanzia jarida hilo litakuwa likipatikana katika mtandao wa Mzalendo.net na blog ya Zanzibar Daima. Upatikanaji wa jarida hilo katika mfumo wa gazeti na majarida ya kawaida kwa uchapaji na kuuzwa mitaani, unatarajiwa kuwepo baada ya m u d a k u l i n g a n a n a litakavyopokewa na jamii na pia kukamilika taratibu za kisheria. Habari za ujio wa jarida hilo zimekuja katika kipindi ambapo kumekuwa na malalamiko mengi ya wananchi juu ya hali tete ya kisiasa, kamii na kiuchumi Zanzibar. K wa u p a n d e m m o j a , wananchi wanalalamika kuwa hali ya maisha inazidi kuwa ngumu kila uchao huku huduma za kijamii zikizidi kudorora. Inadaiwa kuwa wananchi wanakosa mlo bora na wa kutosha huku wakikosa pia huduma za afya, maji na elimu bora. Hali si shwari pia kamii na kiutamaduni ambapo maadili na akhlaq za Wazanzibari zimekuwa zikipotea siku baada ya siku. Ulevi na hasa wa madawa ya kulevya, limekuwa balaa kubwa kwa vana ambapo hivi sasa makundi ya vana wa n a o n e k a n a wa k i p i t a mitaani huku wanasinzia na kutiririka mate bila breki.. Kwa upande mwingine, kuna kila dalili kuwa hali si shwari mbeleni kisiasa kutokana na visa mbalimbali ambavyo vinaonekana kuviza hali ya maelewano iliyopo baada ya kupatikana kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. K u we k wa n d a n i k wa muda mrefu Masheikh wa J u m u i ya ya M i h a d h a r a ya Kiislamu bila ya kesi yao kuzungumzwa huku wakizuiliwa dhamana, ni moja ya matukio yanayodaiwa kurejesha zile kesi za zama za siasa za fitna, chuki na uhasama. Katika zama zile inadaiwa kuwa kesi nyingi zilibuniwa kisiasa kwa kuonekana tu mtu kutofautiana na msimamo wa kiongozi au chama tawala, na hilo likatosha kumuweka ndani miezi kama si miaka na baadae kesi kufutwa. Miongoni mwa waliokumbwa na mikasa hiyo ni baadhi ya viongozi wa Chama cha Wananchi, CUF, ambao baadhi yao wamo ndani ya Serikali hivi sasa. Hali hii imetajwa kama ni ukandamizwaji wa haki za kibinadamu, kubana uhuru wa watu kutoa maoni, dhulma na uvunjaji wa sheria na katiba ya nchi. Maoni ya wengi ni kuwa Masheikh wanaoshikiliwa bila kesi zao kuzungumzwa, kama kungekuwa na kosa linalozungumzika kisheria mahakamani, kusingekuwa na sababu ya kuchelewesha kesi hiyo kwa takribani mwaka mzima sasa bila ya kuzungumzwa. Jarida hilo linakuja pia katika kipindi muhimu kwa siasa za Zanzibar ambapo kumekuwa na mgongano wa mawazo juu ya hatma ya muungano na hadhi ya Zanzibar katika muungano. Wakati baadhi ya wananchi wakitaka muungano wa S e r i k a l i Ta t u , we n g i n e wanataka muungano wa mkataba huku makada wa CCM wakijitahidi kuwashibisha wafuasi wao msimamo wa kudai kuendelea na muungano wa Serikali mbili. Kwa upande mwingine, hiki ni kipindi ambapo hata Serikali ya Umoja wa K i t a i f a i m e o n e k a n a kutokuwa madhubuti na iliyo pamoja hii ikionyeshwa na kauli zinazotofautiana na kukinzana za viongozi wake. Lakini kwa upande

mwingine, hata taasisi za Serikali vikiwemo baadhi ya vyombo vya habari, vimekuwa vikitolewa mfano wa kutoa taarifa zenye kubeza baadhi ya viongozi ndani ya serikali hiyo. Kinachojitokeza ni kuwa kila anayekuwa na msimamo tofauti na ule wa makada wa CCM juu ya muungano na hadhi ya Zanzibar katika muungano huo, huonekana kama msaliti. Haya ndiyo yanayowakuta walio katika ile Kamati ya Maridhiano, wenye maoni ya kuwa na muungano wa m k a t a b a n a wa n a o t a k a Serikali tatu. Hata kama mtu alikuwa kada mzuri wa CCM na kiongozi katika SMZ, lakini mara anapoonekana

kutokuunga mkono muundo wa Serikali mbili, basi anakuwa hapendezi tena. Wa l a h a i c h u k u l i w i kuwa hayo ni maoni yake na ana uhuru huo, tena wa kikatiba na kisheria na hata kisiasa kwa sababu huu ni wakati wa kutoa maoni. Kinachotarajiwa ni kuwa ujio wa Jarida hili, Zanzibar Daima, labda itasaidia kuchambua masuala haya, lakini kubwa zaidi kutoa elimu watu wawe na moyo wa kuwavumilia wenye maoni tofauti na yao. N a k w a m b a mwisho wa yote, kama kinachozungumzwa ni demokrasia, haki na utawala bora, basi kauli ya wengi ndio isikilizwe.

Maslahi ya kudumu ya Zanzibar hayawezi kupatikana kwa kukandamiza mawazo ya wengi, japo ukandamizaji huo unaweza kuwa na manufaa ya muda mfupi ya baadhi ya wanasiasa. Hao ni wale ambao wanaposimama katika majukwaa hutema cheche wakidai kupigania masilahi ya nchi kumbe nchi yenyewe ni nafsi zao.

Magaidi wa gazeti la Rai na kisa cha Jessica Lynch


Na Omar Msangi NI kutoka katika unabii wa Isaya ambako tunapata hadithi ya anayebakia - anayebaki kati ya roho ambaye atapeleka habari ambayo ilikuwa inapita juu ya vichwa vya umati wa watu. Kizazi cha Isaya kilikuwa kinaishi katika nyakati ngumu, na taabu kubwa zaidi zilikuwa hazijafika bado. Umati wa watu ungeendelea na njia zao mbaya na kafara zao za damu, bila kujali ghadhabu inayokuja, Lakini tumaini la siku zijazo lilikuwa kwa aliyebaki ambaye, licha ya kuzongwa mara nyingi na kupuuzwa, angekuwa amebaki na ufahamu na hata uwezo wa kuweza kuwaongoza ndugu zake wapotofu, wakati hatimaye wakiwa tayari kusikiliza. Tu n a c h o k i o n a n i mwelekeo katika shughuli za watu ambazo, kama hautasitishwa, unaweza kuvuruga mpangilio wetu wa maisha na uhuru wetu wa kijamii na kiuchumi. Hilo ni suala muhimu kwa umma mzima wa binadamu, hadi kuifikia roho iliyo duni zaidi katika uso wa sayari hii. Sasa kwanini umati haugutuki? Kwa sababu hawajastushwa, au wameshtushwa na viashiria batili. Wanaenda mara moja, halafu nyingine katika misukumo ambayo inawazamisha zaidi katika kuchanganyikiwa! (Imenukuliwa na kutafsiriwa kwa Kiswahili kutoka: Hidden Menace to World Peace- by James Gibb Stuart (1993)) Yapo mambo katika jamii yakiachwa yakakubalika, madhara yake yanakuwa n i m a k u b wa m n o n a japo wakati mwingine ya n a f a n y wa n a wa t u wachache, lakini inakuwa kama ule msemo kuwa mchuma janga hula na wa kwao. Katika hali kama hiyo inakuwa ni wajibu kwa kila mmoja wetu kufaya kila awezalo kuhakikisha kuwa anainusuru nchi na watu wake. Kiasi wiki tatu zilizopita gazeti la Rai liliandika katika ukurasa wake wa mbele habari iliyodai kuwa mamia ya vijana kutoka Arusha walikuwa wamechukuliwa kupelekwa Somalia na Darfur kwa ajili ya kupewa mafunzo ya kigaidi. Wa k a t i J i j i l a Arusha likiwa bado na kumbukumbu ya milipuko miwili ya mabomu, imebainika kuwa zaidi ya vana 200 wapo nchini Somalia na jimboni Darfur, Sudan, kwa ajili ya kupewa mafunzo ya kigaidi. I l i s e m a s e h e m u ya habari hiyo katika Rai ya Alhamisi Julai 11, 2013. Ukitaja Al Shabab, Somalia na Sudan, anachosema mwandishi bila kutamka ni kuwa vijana 200 wa Kiislamu wapo Somalia na Sudan kujifunza ugaidi. Kwa lengo gani? Habari hii ya Rai ilitanguliwa na taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba ambaye alidai kuwa amekamatwa mtu akiwa na komputa mpakato yenye maneno ya k i c h o c h e z i , ye n ye kuhamasisha watu wa dini moja kuwaangamiza watu wa dini nyingine. Japo DCI Manumba hakutaja dini wala watu wa dini gani wanataka

Makala

RAMADHAN 1434, IJUMAA AGOSTI 2-8, 2013

AN-NUUR

Binadamu sio mtu wa Ndio tu Tutumie vyema neema ya akili Tusiwe vipaza sauti visivyojijua
kuangamizwa, lakini kwa muktadha wa kipindi hiki na kwa mazingira ya Tanzania, maneno haya ni ya kuchochea chuki baina ya Waislamu na Wakristo na maneno ya kuchochea Wakristo kuuwa Waislamu a u Wa i s l a m u k u u wa Wakristo. Lakini kwa sababu aliyekamatwa ana jina la Kiislamu, basi itakuwa sahihi kusema kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akichochea Waislamu kuwaangamiza Wakristo. Lakini Manumba hakuishia hapo. Akagusia kitisho cha al Shabab ambapo alisema kuwa Tanzania si salama tena kwa sababu magaidi wa al Shabab wanavinjari Ta n z a n i a n a A f r i k a Mashariki kwa ujumla wakitafuta sehemu za kushambulia. Ukichanganya taarifa hii ya DCI Manumba na ile habari ya gazeti la RAI kuwa vana 200 (wa Kiislamu) wapo Somalia na Sudan kujifunza ugaidi, haya ni madai mazito. Mkristo akisoma habari kama hizi, moja kwa moja anajenga mawazo/maoni (opinion) kuwa akina Ali, akina Iqbal ni maadui w a Wa k r i s t o w e n y e uchu wa kuangamiza Wakristo. Kibinadamu naye, kwanza atawaona hawa ni maadui. Ataishi na kukaa nao kimtego kimtego akiwa na wasiwasi k u wa m u d a w o w o t e anaweza kushambuliwa. Kwa hiyo naye anakaa kimaarifa tayari tayari kwa kujihami. Kwa upande mwingine, kama itatokea shambulio la aina yoyote na ikatokea akauliwa Mkristo, hata kama aliyefanya hivyo ni kichaa au lilikuwa tukio la bahati mbaya (ajali),

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba. lakini akitokea mtu kusambaza habari kuwa wahusika ni Waislamu, ye ye wa l a h a t a s u b i r i kupata ukweli na usahihi wa madai hayo. Moja kwa moja ataamini kuwa ndio yale yale waliyokuwa wameambiwa kwamba kuna watu (Waislamu) wanahamasishana kuangamiza Wakristo. Kwa hiyo taarifa kama zile zilizotolewa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba na zile habari za gazeti la RAI, kwa kweli zinaweza kuacha athari mbaya na kuleta madhara makubwa k a t i k a j a m i i a m b a yo hayakutarajiwa. Sina sababu na naamini hakuna yeyote katika sisi Watanzania anaweza kusimama na kuleta madai kuwa haviamini vyombo vyetu vya dola. Lakini hoja ya msingi hapa ni kuwa kuna haja ya kuchukua tahadhari kubwa katika kutoa taarifa: Kwanza kuhakikisha kuwa tarifa zeyewe ni za kweli. Ilivyosemwa ndivyo kweli ilivyokuwa? Tunaposema Ally alikamatwa na komputa mpakato yenye maneno yanayochochea Waislamu kuwaangamzia Wa k r i s t o , n i k w e l i komputa hiyo ilikuwa na maneno hayo? Ni kweli kumputa hiyo ilikuwa ya Alli na ni yeye Ali kaandika maneno hayo? Na katika mazingira ya nchi yetu lazima tujiulize, ni kweli huko maosini tulipo na mitaani tunapoishi, hali inaonyesha kuwa kuna chuki baina ya Wakristo na Waislamu kiasi cha kukia kila upande kuhamasisha watu wa upande wake kuangamiza watu wa upande mwingine? Profesa Mahmood Mamdan ameandika kitabu chake alichokipa jina: GOOD MUSLIM, BAD MUSLIM-America, the Cold War, and the Roots of Terror. Katika kitabu hicho ukurasa wa 196 mpaka 198 ametoa visa viwili. Kimoja ni simulizi ya muuguziNesi (nurse) wa Kuwait ambaye alitoa ushahidi kwamba aliwaona askari wa Iraq wakivamia wodi ya wazazi katika hospitali anapofanya kazi na kuuwa vitoto vichanga kwa mamia. Ushahidi huo uliotolewa katika Bunge la Congress, ndio uliopelekea Bunge hilo kupiga kura kwa wingi kuidhinisha jeshi la Marekani kuingia vitani kumpiga Saddam Hussein katika vita ya mwaka 1991 iliyopewa jina la Operation Dersert Storm. Inaendelea Uk. 7

7
ilikuja kufahamika kuwa kumbe yule hakuwa muuguzi. Alikuwa binti wa Balozi wa Kuwait, Washington, na kwamba hiyo ni propaganda i l i yo t e n g e n e z wa n a kampuni ya Rendon Group (Media Consultancy) ambayo i l i k u wa i m e a j i r i wa rasmi kwa ajili ya vita ya propaganda. Gazeti la New York Times la tarehe 20 Februari, 2002 lilifichua zaidi habari hiyo pale lilipoandika kuwa kuelekea vita ilikuwa imeundwa Ofisi iliyoitwa Office of Strategic Influence (OSI) na kwamba chini ya generali Simon Worden, OSI, ilitakiwa kuzua habari za uwongo ilimuradi ziwe za kusaidia masilahi ya Marekani. Na katika jumla ya mikakati yake ilikuwa kuipa kandarasi kampuni ya Random Group ya dola 100,000 kwa mwezi kusaidia kazi hiyo. Anasema Profesa Mamdan kuwa baada ya kuchuliwa habari hizo, OSI ilivunjwa rasmi. Hata hivyo anasema k u wa k u i b u k a t e n a kisa cha Jessica Lynch rescue, inaleta utata kama kweli kitengo hicho kilivunjwa. Ufupi wa maneno anasema kuwa: Mwezi April 2003, karibu televisheni zote, redio na magaeti nchini M a r e k a n i , z i l i k u wa zimepambwa na kisa cha ujushaa wa kikosi maalum cha Marekani kilichofanikiwa kumuokoa askari wake akiitwa Jessica Lynch. Ikadaiwa kuwa tarehe 23 Machi, 2003 Jessica alivamiwa ghaa na askari wa Iraq akapambana nao mpaka risasi zikamuishia. Hapo ndipo akapigwa risasi na kujeruhiwa kwa visu akafungwa kamba na kupelekwa hospitali katika mji wa Nasariyah. Akiwa hospitali akapigwa na kuteswa sana na askari wa Iraq. Wiki moja baadae kikosi maalum cha askari wa Marekani walivamia hospitali
Inatoka Uk. 6 Hata hivyo, baadae

Magaidi wa gazeti la Rai na kisa cha Jessica Lynch

Habari/Tangazo

RAMADHAN 1434, IJUMAA AGOSTI 2-8, 2013 unafanyika mpiga picha wa lamu mmoja aliyeshiriki kutengeneza filamu inayojulikana kwa jina la Black Hawk Down alikuwa akipiga picha za video za tukio zima. Profesa Mamdan anasema kuwa hili ni tukio ambalo lilipigiwa zumari sana na kuwa kama nembo ya ushujaa wa askari wa Marekani katika vita 2003. Hata hivyo anasema kuwa t u k i o h i l o l i l i k u wa uwongo mtupu kama ulivyokuwa uwongo uliopelekea Marekani kuivamia Iraq: Madai kuwa Saddam Hussein ana silaha za maangamzi na madai kuwa yeye na al Qaidah ni kitu kimoja. Ni kwa sababu hii nadhani kuwa tuna kila sababu ya kuwa makini na taarifa ambazo zina kila dalili ya kuleta mtafaruku katika nchi. Hoja ni kuwa i n a we z e k a n a k we l i tukawakamata akina Tom na Ally wakiwa na komputa mpakato zenye maneno ya kuhimiza Waislamu kuwakata makoo Wakristo na kinyume chake, lakini tuna uhakika gani kwamba hao kina Ally na Tom sio kama yule bint wa Balozi wa Kuwait aliyedaiwa kuwa ni nesi? Mtu ni ndiyo... Ndiyo kwa maisha. Ndiyo kwa upendo. Ndiyo kwa ukarimu. Lakini mtu pia ni hapana. Hapana kwa kudharauliwa kwa binadamu. Hapana kwa unyonyaji wa watu, Hapana kwa kuchinjwa kwa kile ambacho ni cha kibinadamu zaidi katika utu: uhuru. (-Frantz Fanon: Black Skin, White Masks) Unapokubali kufanywa kipaza sauti kisichopima kama kinachosemwa ni kweli au uwongo, kina madhara au faida, kwa kweli ni kujidharaulisha kulikopita mipaka. M t u ye yo t e anayejitambua na anayejali heshma na utu wake, hawezi kukubali. Atasema hapana. Atasema hapana kwa sababu hakuna kiwango cha pesa kinachoweza kuwa ndio thamani ya ubinadamu, heshma,

AN-NUUR

Rais wa zamani wa Marekani George W Bush

hiyo wakawashinda nguvu askari wa Iraq waliokuwa wakimlinda wakamuokoa na kumpeleka hadi Kuwait. Profesa Mamdan anasema kuwa ilipigwa p r o p a g a n d a k u b wa na habari kupambwa ikilenga kuonyesha ukatili wa askari wa Iraq kuwa wanatesa hata wagonjwa hospitalini lakini pia ikionyesha ushujaa wa kikosi maalum cha askari wa Marekani. Jioni ya siku hiyo hiyo Rais George W Bush akahutubia taifa kutoka White House na kuita tukio hilo kuwa Uokozi kwa taifa. Kiasi siku nane baada ya tukio Wizara ya Ulinzi ya Marekani ikasambaza picha za video za tukio hilo kwa vyombo vya habari. Mara baada ya vita

kumalizika waandishi wa habari kutoka New York Times, the Toronto Star, El Pais na BBC, walikwenda Nasariyah kupata ukweli wa tukio lile. Askari katika hospitali aliyokuwa anatibiwa Jessica wakawafahamisha kuwa askari huyo alikishwa hapo akiwa na mejeraha, amevunjika mkono na mguu na kwamba majeraha hayo yalikuwa yamesababishwa na ajali ya gari alilokuwa akisafiria. H a k u wa a m e p i g wa risasi kabisa. Habari hizo zilithibitishwa pia na madaktari wa Kimarekani waliokuwa Iraq. Kuhusu kuteswa je? Madaktari walisema kuwa Jessica Lynch alipokishwa hospitali a l i k u wa a m e i s h i wa damu kutokana na

kuvuja damu nyingi katika majeraha na kwamba jambo la kwanza walifanya juhudi kupata damu na kumuwekea. Akiongea na waandishi hao Dr. Saad Abdul Razak anasema kuwa yeye mwenyewe na familia yake walitoa damu kumpa Jessica kwa sababu damu yao ni O Postive kama ilivyokuwa ya Jessica. I think that we save her life. Alinukuliwa Dr. Abdul Razak akisema. Vipi kuhusu uokoaji: Uchunguzi wa waandishi hao unaonyesha kuwa baada ya Jessica kupata nafuu, madaktari walitafuta namna ya kufikisha habari kwa vikosi vya Marekani kupitia Shirika la Msalaba Mwekundu (Red Cross) kwamba kuna askari wao hospitalini wanaweza kuja kumchukua. Red Cross walimchukua Jesicca na kumpeleka katika kambi ya jeshi la Marekani iliyokuwa karibu, lakini wakashambuliwa na askari wa Marekani ikabidi wakimbie na kumrejesha Jessica hospitalini. Usiku wa siku hiyo hiyo (alfajiri hakujapambazuka), ndio kikosi maalum kilika na kuanza kufyatua risasi ovyo huku makamanda wakitoa amri mbalimbali. It was like in Hollywood film. There was no Iraq soldiers, but the American Special Forces were using their weapons. They red at random and we heard explosions. They were shouting Go! Go! Go! The aack on the hospital was a kind of show, or action lm with Sylvester Stallone. A n a s i m u l i a D r. Amnar Uday akiongea na mwandishi wa BBC John Kampfner. Ta a r i f a z a i d i zinafahamisha kuwa wakati uvamizi huo

8
Na Mwandishi Maalum HIVI karibuni kwa takriban miezi miwili kumekua na midahalo mbali mbali ambayo imekuwa ikiendelea katika nchi nyingi za maswala ya Ulinzi mtandao katika nchi za Afrika. Katika Vikao tofauti vilivyo fanyika mjadila ulikuwa ni hali ya usalama wa kimtandao kwa ngazi ya kidunia na kudhihirika ya kua kumekua na ongezeko kubwa katika mwaka huu wa 2013 la makosa mtandao na wakati huo huo nchi baadhi tayari zimeweza kupiga hatua katika kukabiliana na hali hiyo. Bwana Yusuph Kileo mmoja wa Watanzania alipata fursa kuhudhuria katika mikutano hiyo akiwa ni mwanachama wa kudumu wa kikundi kinacho jihusisha na Ulinzi mtandao katika nchi za Afrika Katika kikoa kilichofanyika Afrika Kusini hivi karibuni, taarifa iliyowasilishwa na Profesa Hamadoun Toure kutoka ITU (International Te l e c o m m u n i c a t i o n Union) iliyo chini ya United Nations (Umoja wa Kimataifa) ilisema kuna mategemeo mwishoni mwa mwaka huu wa 2013 pakawa na watumiaji bilioni 2.7 wa mtandao na kwa takwimu hizo zimeonyesha kupanda kwa kasi kulinganisha na takwimu za awali zilizotolewa mwishoni mwa mwaka. Aidha ripoti iliyowasilishwa na ITU huko Geneva ilisema, kumekua na ongezeko kubwa la madhara ya m t a n d a o a m b a p o ilielezwa mitandao imekua ikiathiriwa zaidi kwa Asilimia 30, Phishing Sites spoong social networks imeongezeka kwa asilimia 125 na kuelezwa nusu ya vijana wenye umri kati ya miaka 13 hadi 17 uliimwenguni kote wamekua wakiathirrika na kilichotambulishwa kama Cyberbulling. Vile vile Tafiti zilizo wasilishwa katika ripoti ya the World Federation of Exchanges and the International Organization of Securities

Usalama wa kimtandao

Makala

RAMADHAN 1434, IJUMAA AGOSTI 2-8, 2013


na Tanzania kuiga mfano ya jitihada za nchi nyingine ili kuweza kuweka hali ya usalama mtandao nchini katika kiwango kizuri. Pia Alizisifu nchi kubwa kama China, Urusi na Marekani kwa kuwekea mkazo maswala ya ulizi mtandao kwa kuazisha majadiliiano mbali mbali ikiwemo pia kufadhili majadiliano mbali mbali yanayo husiha maswala ya ulinzi mtandao. Amewataka wananchi kuacha kutuma au kusambaza ujumbe wa kichochezi katika simu zao, kwani amenasihi waupatao ujumbe kama huo kutoka sehemu nyingine wasiusambaze badala yake waufute ili kuepuka nao kuingia katika matatizo ya kiusalama. Amewahadharisha wananchi kuacha kutuma ujumbe wa uchochezi, matusi au kashfa kwani kufanya hivyo ni kuvunja sheria za nchi. Vile vile alitoa sifa katika nchi za Afrika ikiwemo Afrika Kusini huku akieleza viongozi wengi wa Umoja wa Wataalam wa Ulinzi Mtandao ambapo yeye ni mwanachama wa kudumu na huku akitolea mfano Kenya kwa jitihada kubwa za kuwa na umoja wa wanachama katika maswala ya teknologia kwa ujumla ambapo hadi sasa wamekua wakiongoza vikao kadhaa ambavyo wataalam mbali mbali wa Afrika hususan Afrika Mashariki wamekua wakikutana na kujadili changamoto zinazo husu teknologia kupitia kivuli cha umoja huo kutokea nchini Kenya. Ama kwa upande mwingine bwana Kileo ameeleza, yuko katika hatua za awali kufanyia kazi yale yaliyo patikana katika vikao mbali mbali akiwa kama mtaalam wa Ulinzi Mtandao na Upelelezi wa Makosa ya Digitali kwa kuanzia na kile alicho kieleza Tanzania Crime Awareness Campaign na hasa anategemea kuangalia zaidi wenzetu katika nchi mbali mbali walipotilia mkazo ambapo ni katika makosa mtandao. Ingawa hakuweka wazi njia hasa ambazo amejipanga kuzitumia kwa sasa akidai bado ni mapema sana kueleza kwa kina dhamira yake hiyo.

AN-NUUR

Bwana Yusuph Kileo Akibadilishana Mawazo Na Bwana Craig Rosewarne Ambaye Ni Mwenye Kiti Wa Jumuia Ya Maswala Ya Security Mara Baada Ya Kikao Katika Mkutano Ulio Fanyika Nchini Afrika Kusini Mwishon Mwa Mwaka Jana Ili Kupitia Hali Ya Makosa Ya Kimtandao Uliohusisha Wataalam Wa Uchunguzi Wa Makosa Ya Digitali Na Mtandao Duniani Commissions zimeeleza nusu ya taasisi za fedha duniani zimeweza kuathirika na Cyberattacks pamoja na wizi mtandao hadi kufikia mwaka jana mwishoni huku ikielezwa kushindikana kutatua hali hiyo kwa takriban robo nzima ya taasisi hizo za fedha dhidi ya tatizo hilo. Hayo na mengine mengi ambayo yamepata k u j a d i l i wa k wa k i n a ya l i o n e k a n a k u wa n i changamoto kubwa katika dunia ya sasa ambapo kutakua na ugumu sana kukimbia utumiaji wa teknolojia katika maisha yetu ya kila siku huku B wa n a Yu s u p h K i l e o akitolea mifano hali ya utumiaji wa mitandao kuongezeka nchini katika sekta mbali mbali kuanzia kufanya miamala ya biashara hadi katika sekta za elimu na maeneo mengine mengi. Bwana Kileo alioongeza kwa kusema wimbi kubwa nchini limeongezeka la watu kuwa na matumizi m a b a ya ya m i t a n d a o ambapo imekua ikileta athari kubwa kwa jamii katika maeneo mengi hasa ya kibiashara lakini pia hata kutishia hali ya usalama wa nchi kwa kusambazwa maneno mbali mbali ya kutishia Amani ya nchi kwa kipindi kifupi tofauti na awali wakati matumizi ya mtandao hayakua na ongezeko lililoko sasa. Bwana Kileo alisema Ni kweli kila mtu hivi leo anahitaji teknologia ili kuweza kuwasiliana na mwingine, kufanya miamala ya kibiashara na hata kupata huduma mbali mbali ambazo zimesogezwa karibu na wananchi kwa msaada wa mtandao, lakini pia kuna watu baadhi wanatumia fursa hiyo kufanya mambo yasiyo faa kupitia mitandao hiyo hiyo ambapo baadae inaweza kupelekea usalama wa taifa letu kuingia dosari Akimnukuu Profesa H a m a d o u n To u r e , Bwana Kileo alisema, ITU imeweza kueleza mafanikio ya jitihada kuubwa zilizofanywa na nchi mbali mbali ambapo imepelekea Umoja wa Ulaya (EU) kuanzisha kilicho tambulishwa kama Framework katika ulinzi mtandao ambapo kila nchi mwanachama ameweza kunufaika katika hilo. Bwana Kileo alieleza kwa sasa ITU imeanzisha alicho kitambulisha k a m a Wo r l d s F i r s t Comprehensive Alliance Against Cyber Threats ambapo nchi 145 zinapokea huduma hiyo kwa kuwaleta p a m o j a wa d a u m b a l i mbali wenye uwezo wa kupambana na matishio ya kimtandao. Uhamasisho mkubwa umetolewa kwa serikali mbali mbali, sekta binafsi pamoja na jumuia mbali mbali kuweza kulichukulia suala hili la makosa mtandao kwa sura ya kipekee ili k u we z a k u u n g a n i s h a nguvu ya pamoja kwa nchi zote duniani kuweza kukabiliana na tishio mtandao Cyber threats ambapo baadae inaweza kugharimu dunia yetu ya leo. Pia Bwana Kileo alieleza kwa sasa nchi ya Australia wametoa muongozo wa kutekeleza mbinu kuu nne (4) za kiusalama kwa mitandao ili kukabiliana na athari zinazoweza sababishwa na matatizo ya matumizi mabaya ya mitandao huku ikielezwa hatua hiyo itaweza kupunguza kwa asilimia 85 ya kuingiliwa kwa mitandao ya nchi hiyo. Bwana Yusuph Kileo alieleza imeka wakati sasa

Makala

RAMADHAN 1434, IJUMAA AGOSTI 2-8, 2013

AN-NUUR

Palestine Information Centre (Tanzania) Israeli-Palestinian Negotiations Resume


Kituo cha Habari cha Palestina (Tanzania) Negotiations 1 August 2013

US Secretary of State John Kerry told reporters in Amman that Israeli and Palestinian negotiators have set the groundwork to resume peace talks frozen for the past three years. PLO negotiator Saeb Erakat and his Israeli counterpart have met in Washington to begin initial talks within the next week or so. Kerry has visited the Middle East six times in an eort to resume talks, which have been stalled since September 2010 due to the illegal expansion of Israeli settlements in the occupied Palestinian territories. One of three main Pa l e s t i n i a n d e m a n d s for resuming talks has been the release of about a hundred Palestinians who have been jailed since before the signing of the Oslo peace accords in 1993. The other demands are using the 1967 pre-war borders as the basis for negotiations, and freezing Israeli selement activity in the West Bank and East Jerusalem. Although the PA has called for a halt to the construction of illegal settlements, Israeli ministers have voiced opposition to a freeze on selement expansion. The presence and continued expansion of Israeli settlements in occupied Palestine has created a major obstacle for the eorts to establish peace in the Middle East. More than half a million Israelis live in over 120 illegal settlements built since Israels occupation of the Palestinian territories of the West Bank and East al-Quds more than four decades ago. The Palestinians are seeking to create an independent state on the territories of the

West Bank, East al-Quds (Jerusalem), and the Gaza Strip and are demanding that Israel withdraw from the Palestinian territories occupied in the Six-Day War of 1967. Te l Av i v, h o we ve r, has refused to return to the 1967 borders and is unwilling to discuss the issue of al-Quds. The United Nations and most countries regard the Israeli selements as illegal because the territories were captured by Israel in a war and are hence subject to the Geneva Conventions, which forbids construction on occupied lands. Since January 2013, US President Obama and Secretary of State Kerry have led a new eort in order to resume negotiations between Israel and Palestine. Israeli PM Benjamin Netanyahu has declared that he is willing to negotiate without preconditions. Such an Israeli approach, illustrated by Israeli facts on the ground, is an Israeli attempt at normalizing daily aggression, oppression, discrimination and attacks against the occupied people of Palestine. It shows once again that Israel is not interested about reaching a just and lasting peace but rather in maintaining the status quo while resisting international pressure. An Israeli commitment to the two-state solution in line with the vision of Palestine and the rest of the international community would be a positive step. U n f o r t u n a t e l y, statements and actions made by prominent members of the Israeli government prove that there is a clear ri within the Israeli government on the issue of the peace process,

while Palestine and the international community is exerting eort to resume meaningful negotiations. Many prominent gures of the ruling Israeli coalition are publicly opposing the two-state solution. At the same time, continued actions on the ground, many of which fall under the banner of Israels illegal selement enterprise, demonstrate a clear intention to destroy the possibility of two states living side by side. Official Israeli government statistics revealed that during the rst quarter of 2013, construction in the West Bank increased by 335% in comparison to the last quarter of 2012 - reaching the highest level in seven years. Settlement activity embodies the core of the policy of colonial military occupation of the land of the Palestinian people and all of the brutality of aggression and racial discrimination against our peop le t hat t his policy entails (President Mahmoud Abbas). In the short period during which Israel has talked about peace, as a response to US eorts to resume negotiations, the Palestinian people have been subjected to numerous and appalling violations at the hands of their supposed partner in those talks. These are not merely violations which prejudice the outcome of the twostate solution, not merely violations which make the prospect of meaningful negotiations incredibly difficult, not merely violations which breach

international law and almost every basic human right, but violations which are physically and continuously harming the lives and livelihoods of normal people. Palestinians face daily terror aacks and violence from the Israeli military and settlers who are granted full support from the Israeli government and its ocials. What is most shocking is that these policies and violations are carried out with a complete lack of accountability. This impunity that Israel currently enjoys is not the right environment for meaningful negotiations. The only way to open a door for credible negotiations is for Israel to implement previous agreements and respect international law. The only party able to ensure this environment is the international community. In a high-profile dismissal of the embryonic process, Israels former foreign minister Avigdor Lieberman, wrote on Facebook that there was no solution to the IsraeliPalestinian conflict, at least not in the coming years, and whats possible and important to do is conict-management. Naftali Bennett, e c o n o m i c s m i n i s t e r, insisted construction on Jewish settlements in the West Bank and East Jerusalem would continue, regardless of talks. The comments by two crucial partners in the Israeli coalition are a sign of deep hostility within the government over the agreement for preliminary talks forged by Kerry on Friday. The main sticking

point continues to be the Palestinian demand that the pre-1967 borders form the baseline for territorial negotiations, a guarantee which Israel refuses to give. If Kerry fails to persuade the Palestinians they have rm US backing on the issue, talks may fail to get o the ground. There is also disagreement over the timeframe. Israel is pushing for negotiations to last up to a year, fuelling concern among critics who believe Netanyahu is seeking to give the appearance of diplomatic co-operation while stalling for as long as possible on any outcome. Although the PA has called for a halt to the construction of illegal settlements, Israeli ministers have voiced opposition to a freeze on selement expansion. Its inappropriate for the Jewish people, for the land of Israel and for a sovereign state, Housing Minister Uri Ariel said. We are in favour of building as much as possible. The United Nations and most countries regard the Israeli selements as illegal because the territories were captured by Israel in a war and are hence subject to the Geneva Conventions, which forbids construction on occupied lands. International Relations Commission- Fateh Ramallah - Palestine Contact us: P.O Box 20307, 612 UN Road Upanga West, Dar es S a l a a m Te l : 2 1 5 2 8 1 3 , 2150643 Fax: 2153257 Email: pict@pal-tz.org Website: www.pal-tz.org

10
SIKU NIKIFANIKIWA
Siku nikifanikiwa, swali hili nitatiza Kweli nitashukuriwa, na watu wasojiweza Yatima waloliwa, nitawapa mwangaza Au taharibikiwa, kwa kuanza kujikweza Watu nitawaibia, nifanikiwe kwa shari Dhulma tawafanyia, kwa jeuri na kiburi Uchawi nitatumia, urozi tangu dahari Freemason taingia, nikawe hata kari Au nitashughulika, fanikiwe kwa halali Maharage taridhika, mchunga huku ugali Ninazoa takataka, kazi yangu ni dhalili Koradhi kusulubika, kipato kiwe halali Nitawapa sikitiko, ndugu pia Maraki Tulogombea makoko, kipindi nanuka dhiki Kutokumbuka miiko, kuwaona watubaki Mbekenyera Kirinjiko, tulisoma kwa hilaki Nitaheshimu wazazi, au nitawadharau Nitakumbuka malezi, au nitayasahau Nitamfata Mwenyezi, diniye chake kirau Nitakuwa siwezi, kwa anasa na vidau Nitafanya ihsani, au tatenda machafu Nitakuwa kama nani, lingana wake wasifu Nami hapa duniani, nitakuwa maarufu Maswali mengi kichwani, kira zangu kipo Tamati nimekia, ila jibu satoa Kazi ninawapatia, Islam lobakia Mdabiri na kujua, kisha mtaniambia Tahadhari ninatoa, nafsi kujitambua NASRI KIONE MIBAVU 0759202192 (nasrikione@yahoo.com)

Mashairi/Barua

RAMADHAN 1434, IJUMAA AGOSTI 2-8, 2013

AN-NUUR

Mhe. Maghembe chunguza utendaji DAWASCO Kibamba


Ndugu Mhariri Tafadhali, kwa ruhusa yako naomba nitoe kadhia shida ya maji inayotupata sisi wakazi wa maeneo ya Kibamba na Mbezi kupitia gazeti lako makini, ikiwa ni jitihada za kujaribu tu kukisha kwa wahusika ujumbe juu ya adha tunayoipata wakazi wa maeneo haya hivi sasa. Nikiri kwamba kwa muda mrefu kidogo, wakazi wa maeneo ya Kibamba, Makondeko na baadhi ya maeneo ya Mbezi, walikuwa wakipata huduma ya maji ya bomba ya DAWASCO mara mbili kwa wiki. Hali hiyo imebadilika ghaa kiasi cha miezi miwili sasa imepita, wakazi hao wamekuwa wakiteseka bila kupata huduma hiyo kufuatia mabomba kukata kutoa maji kama ilivyozoeleka. Wakati bomba za wakazi wa maeneo hayo zikicheua u p e p o k wa k o s a m a j i , vituo vya kuuzia maji vya DAWASCO katika maeneo hayo vimekuwa vikiendelea na biashara ya ya maji wakiwauza kwa wenye maboza, ambao nao huwalangua watu maji hayo. Jumatano alipigiwa ofisa mmoja wa DAWASCO na mkazi mmoja wa eneo hilo na kutakiwa kueleza tatizo la kutopatikana maji katika bomba za wananchi. Yeye alijibu kuwa tatizo lililopo linashughulikiwa na maji yatatoka hivyo wakazi hao wavute tu subra hadi hali itakapotengemaa. Lakini ajabu ni kwamba, wakati D AWA S C O

Mabomba ya wakazi hawana maji, viosk vyao vinalangua maji


wakishindwa kutoa sababu za kueleweka za kukosekana maji katika bomba za watu, kwenye vioski vyao vya kuuzia maji, hususan katika kituo cha Kimbamba kwa Mangi na Kile cha Mbezi Mwisho, maji hayakauki na biashara ya maji imechanganya kikamilifu. Tunashangaa, iweje bomba za wananchi zikose maji katika kipindi chote hicho, na wakati huo huo vituo vyao vya kuuzia maji kwa wenye magari vinatoa maji na kuyauza kila siku? Dawasco imekuwa ikiwauzia wanye maboza ndoo shilingi 20. Na wenye magari huwauzia wananchi maji hayo ndoo shilingi 200. Katika mazingira haya ni wazi kwamba kuna kila dalili za hujuma katika upatikanaji wa maji katika bomba za raia ili wawe wateja wazuri wa wenye maboza, ambao nao ndio wateja wakubwa wa maji ya vioski vya DAWASCO!. Ni vyema tukaelezwa s a s a k a m a D AWA S C O katika maeneo yaliyotajwa, wameamua kuwahujumu wananchi ili wafanye biashara na wenye maboza, ambao nao ndio msimu wao mzuri wa kuwalangua wananchi kwa kuwa bomba zao hazina maji. Ni vigumu kuamini kwamba kwenye vioski vyao vya kuuzia maji, yanatoka kila siku, lakini maji hayo hayo hayapatikani kwenye bomba za wakazi kwa siku zote!. Nichukue fursa hii kumueleza Waziri wa Maji

MAMA
Kifo ni haki ya mtu, na siri yake manani Nami silaumu katu, qadari za subhani Viumbe twapenda vitu, vilo bora na thamani Pia twakumbuka watu, kwa matendo ya thamani Saona kama mama, nakiri toka moyoni Ukweli ninausema, sifae nampa shani Daima likuwa hima, kuniweka furahani Ulipo lale salama, kiama wekwe peponi Linilea kwa mapenzi, ukanikanya mabaya Liniasa siwe shenzi, kuwa na tabia mbaya Stare ziso enzi, anasa na Umalaya Leo metunga utenzi, iwe ndo yangu hidaya Ukabaji hata wizi, hukutaka nihusike Ulisema majambazi, maishao sekeseke Heshima busara vazi, nivae nistirike Nisome nipate kazi, nitafanya uridhike Zabibu hata senene, ulonipa enzi zile Wakubwa pia wanene, nikaenda nao shule Kanambia niwabane, madrasa nikawale Lipeka kenda nane, sisahau siku ile Siku uliyofariki, wakaenda kukuzika Moyo ulitaharuki, umati ulioka Miaka kumi siki, mama mola kakutaka Kifocho hakikwepeki, kaburi kakufunika Mama ninakuahidi, wasia nitafatisha Dini nitajitahidi, kusoma na kufundisha Ninamuomba wadudi,Adhabuye kukwepesha Peponi ukafaidi, siku utayoamshwa NA NASRI KIONE 0759202192 (tungo zenye ulimbo) nasriibrahimu@yahoo.com

Mhe. Jumanne Maghembe, kwamba watendaji wake katika mamlaka hii wanamuangusha. Sasa hawatoi huduma ya maji bali wamekusudia kufanya biashara na wenye maboza kwa kuwakosesha watu huduma ya maji kwenye bomba zao. Ni vyema Mhe. MAghembe ukafanya uchunguzi wa kina ili kubaini ukweli dhidi yta watendaji wa eneo hili la Kibamba na Mbezi,ili kuwaondolea wananchi wa maeneo haya mateso katika kupata huduma hii ya msingi. Tu n a t a m b u a k wa m b a M a a n a D AWA S C O walichukua vioski vyao vilivyokuwa vikisimamiwa na najamii, baada ya kubaini kwamba waliopewa kusimamia vioski hivyo walikuwa wakichuma fedha nyingi kwa kuwalangua raia maji, huku wao wakishindwa kuwasilisha katika shirika kiasi cha fedha stahiki. Lakini kwa jinsi hali ilivyo sasa, kihuduma hatuoni tofauti ya wao kuchukua vioski hivyo, kwani bei wanayuzia maji yao sio bei wanayouziwa wananchi. Kwa bahati mbaya, vioski hivyo siku hizi huuza maji kwa wanaonunua maji kwa kiwango kikubwa tu, wale wanaonunua kwa ndoo au madumu hawana nafasi katika vioski hivi. Niseme tu kwamba, sasa mwezi wa pili tunaishi bila kupata maji ya bomba, bila kutolewa taarifa za msingi za kukosekana maji hayo kutoka DAWASCO. Mazinde Makeka Mbezi Luguruni -Dar

RAMADHAN KARIM

Jipatie vitabu vyenye mafunzo ya Funga ya Ramadhani, vilivyoandaliwa na Sheikh Nurdin Kishki kama vile:- Hadithi 30 kuhusu Funga ya Ramadhan. Hukumu za Funga ya Ramadhan. Ipi Idadi sahihi ya Swala ya Tarawehe. Vingine ni Ndoa Talaka na Eda. Pamoja na Uislamu si Dini ya Ugaidi. Kwa mahitaji ya jumla na reja reja, ka dukani kwa Saimu Gwao, Msikiti wa Mtoro au Ibn Hazim MediaCentre. Simu:-0713 471 090, 0715 825 672, 0773 194 646.

11

Habari/Tangazo

RAMADHAN 1434, IJUMAA AGOSTI 2-8, 2013

AN-NUUR

Mshindi apata milioni kumi mashindano ya Quran Dar


Na Azza Ally Ahmed
kuitekeleza katika matendo yao ya kila siku. Alisema kuwa mwanafunzi aliyehifadhi walau Juzuu moja, hata akipewa shilingi milioni moja haiwezi kulingana na thamani ya kuhifadhi Quran hiyo. Zawadi hizi pamoja na pesa tunazowapa wanafunzi hawa, ni kuwapa motisha tu na sio malipo sahihi kulingana na jambo nzito wanalofanya. Alieleza Sheikh Kishki. Katika mashindano hayo, washindi walipewa zawadi zikiwemo fedha taslimu ambapo mshindi wa kwanza katika kuhifadhi Juzuu moja alikuwa ni Salumu Aarif, kutoka Alhikma. Yeye alipata shilingi laki nne pamoja na jiko la gesi na cheti cha ushindi. Mshindi wa pili alikuwa ni Sharifu Twaha, ambaye alipata shilingi laki tatu na cheti cha ushindi, akifuatiwa na mshindi wa tatu ambaye ni Sakina Ashrafu kutoka Madrasa Muuminat Temeke, a l i ye p a t a sh i l i n g i l a k i mbili huku nafasi ya nne ikienda kwa Abdulrahman Abdulhakim kutoka Madrasa ya Uthmaan, aliyepata shilingi laki moja na cheti na wa tano alikuwa ni Haadad Masud kutoka Alhikma aliyepata elfu hamsini na cheti. Kwa upande wa Juzuu tatu, mshindi wa kwanza alikuwa Yusuph Said kutoka Madrasa Anour aliyeshika nafasi ya kwanza na kupata shilingi laki tano na jiko la gesi pamoja na cheti cha ushindi. Alifuatiwa na Khairat Salum kutoka Madrasa Tauhidy ya Kichi, aliyepata shilingi laki tatu, Rice Cooker pamoja na cheti cha ushindi. Mshindi wa tatu wa Juzuu tatu ni Raya Mohammed wa Madrasa Qaadiriya aliyepata shilingi laki moja pamoja na cherehani na cheti. Kwa upande wa Juzuu tano, mshindi wa kwanza ni Jafar Ahmad kutoka Alhikma Temeke aliyepata laki sita, redio pamoja na cheti, huku mshindi wa pili wa Juzuu tano Abdu-karim Bakar wa Madrasa Muuminaat kutoka Temeke ambaye alijipatia laki nne pamoja na cheti cha ushindi, huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Swalehe Suleiman wa Madrasa Anour aliyepata pesa taslim laki mbili pamoja na cheti. Katika ngazi ya Juzuu saba, nafasi ya kwanza ilienda kwa Mohammed Faiz aliyepata shilingi laki nane, baiskeli na cheti. Nafasi ya pili ilikwenda kwa Hashim Abdul- Kadir wa

SULEIMANI Omary Ally wa Al Hikma ameibuka mshindi wa Juzuu thelathini na kujinyakulia pesa taslim shilingi milioni kumi, Laptop pamoja digital Quran na cheti. Nafasi ya pili imeichukuliwa na Abdallah Abdul-Qadri Muhamad kutoka Alhikma aliyejichukulia pesa taslim milioni tatu na laki mbili na themanini, pikipiki, digital Qur-an na cheti. Nafasi ya tatu ya juzuu thelathini ilichukuliwa na Haytham Sagar Ahmad kutoka Kenya aliyejipatia milioni moja laki sita na arobaini elfu, pikipiki, Digital Quran na cheti. Katika kilele cha mashindano hayo, Mlezi wa Taasisi ya Alhikma, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, amewashukuru Waislamu kwa kuonyesha kuunga m k o n o m a s h i n d a n o ya kuhifadhi Qur`an. Alhaji Mwinyi alitoa shukrani hizo katika mashindano ya 14 ya k u h i f a d h i Q u r a n yaliyoandaliwa na Taasisi ya Alhikma Education Centre, na kufanyika katika viwanja vya saba saba jijini Dar maarufu kama viwanja vya Mwalimu Nyerere mwishoni mwa wiki iliyopita. Waislam tunatakiwa kukihifadhi na kukifuata kitabu kitukufu cha Qur`an, kwani ndio muongozo wa wanadamu. Alisema Alhaj Mwinyi. Alisema kuwa kutofuata kitabu hicho ni upotevu ulio mkubwa na kwamba, ndio maana watu wanafanya mambo ya ajabu na kupatwa n a m e n g i m a b a ya k wa kutokuwa na muongozo sahihi ambao ni Qur`an. Alhaji Mwinyi alibainisha kuwa ili kuepukana na huu utandawazi unao haribu vizazi vyetu katika jamii, dawa ni moja tu, nayo ni kufuata barabara mafundisho ya Qur`an. N a ye S h e i k h N u r d i n Kishki alisema kuwa ni vyema Waislamu wakawa na yakini kwamba, lengo la kufanya mashindano ya kuhifadhi Quran sio kutafuta pesa, bali ni kuwapa vana hamasa waweze kuendeleza Qur`an. Aidha amewataka Waislamu kuacha kupupia mambo yasiyofaa na badala yake waisome Qur`an na

aliyepata shilingi laki sita fri ya mezani pamoja na cheti na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Khamis Abdallah, ambaye naye alipata shilingi laki nne birika la kuchemshia maji pamoja na cheti cha ushindi. Washindi wote wametokea Madrasa Alhikma, Temeke. Kwa upande wa washindi wa Juzuu kumi, nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Anwar Yahya wa Madrasa Al Hikma aliyejinyakulia shilingi laki tisa na Flat Screen na DVD pamoja na cheti. Nafasi ya pili ilichukuliwa na Hamad Khamis kutoka D a r u l - U l u m a l i ye p a t a shillingi laki tano na cheti. Katika ngazi ya Juzuu ishirini, nafasi ya kwanza ilikwenda kwa Abdallah Juma wa Madrasa ya Al Hikma na kupata shilingi milioni moja, pikipiki na cheti. Nafasi ya pili ikikwenda kwa Yahya Ally wa Madrasa ya Darul- Uluum aliyepata shilingi laki nane baiskeli na cheti. Anas Abdul-Hadh wa Al Hikma alishika nafasi ya tatu na kupata shilingi laki sita, Sub-woofer na cheti.

Bilali kutoa zawadi washindi Quran Masjid Istiqama leo


Na Azza Ally Ahmed

SULEIMANI Omary Ally wa Madrasa Alhikma, aliibuka mshindi wa Juzuu thelathini na kujinyakulia pesa taslim shilingi milioni kumi, Laptop pamoja digital Quran na cheti.

Msikiti wa Istiqama, Ilala Jijini Dar es Salaam, leo (Ijumaa). Mashindano hayo yalianza Julai 21, yanatarajiwa kukia kilele leo Ijumaa Agosti 2 Msikitini hapo.
Akiongea na gazeti hili, msimamizi wa mashindano hayo Ustadhi Saleh Omari Salehe, amesema haa hiyo itafanyika msikitini hapo kuanzia saa mbili usiku baada ya swala ya Ishah. Ust. Omar alisema mbali na Makamu wa Rais, pia mashindano hayo yatashuhudiwa na Masheikh na wageni mbalimbali. Alisema mashindano ambayo yanafanyika kwa mwaka wa tatu sasa tokea yaanzishwe, ambapo mwaka huu yameshirikisha washiriki 39.

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Ghalib Bilali, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika haa ya kutoa zawadi kwa washindi wa usomaji Qur an, katika

Innalillah wainaillahi Rajiun


Mzee Athuman Songoro wa Masjid Mtambani, Kinondoni amefariki dunia. Marehemu Songoro alifariki siku ya Alhamisi (jana) na kuzikwa Adhuhur ya siku hiyo hiyo katika makaburi ya Ilala, Jijini Dar es Salaam. IMAMU Masjid Mtambani

12

AN-NUUR
MAKALA

12

RAMADHAN 1434, IJUMAA AGOSTI 2-8, 2013

Amana watoa futari kwa yatima, wajane


Na Abdulkarim S. Msengakamba.

Tanzania Muslim Hajj Trust Safari ya Hijja 2013 Uandikishaji unaendelea gharama za Hijja ni dola za Kimarekani $ 4200. Safari ni tarehe 5 na 7 Octoba, na Kurudi Tarehe 27 na 28 Octoba, 2013. Wahi kujiandikisha Sasa. Uandikishaji wa Hijja Zijazo 2014, 2015 kwa Kulipia kidogo kidogo, unaendelea. Simu: 0717 000 065, 0784 222 911, 0754 304 518, 0754 498 888 Au kupitia Tovuti yetu. www.hajjtrusttz.org.

Darasa la Saba kufanya mtihani wa Islamic


Na Bakari Mwakangwale WA N A F U N Z I w a Kiislamu wa Shule za

WASHINDI wa shindano la kuhifadhi Qur'an lililofanyika PTA Sabasaba jin Dar es Salaam wakiwa na baadhi ya Masheikh mara baada ya shindano hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki.

Msingi wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya Msingi katika somo la Dini ya Kiislamu. Mitihani hiyo inatarajiwa kuanza Agosti 14, 2013, katika Shule mbalimbali kote nchini, chini ya usimamizi wa Islamic E d u c a t i o n Pa n n e l , ambapo hatua za awali za maandalizi ya kukamilisha zoezi hilo imesha kamilika. Akizungumza na
gazeti hili, Jumanne wiki hii kiongozi muandamizi wa Islamic Education Pannel, Ust. Ibrahim

Kunema, alisema tayari semina zimeshafanyika k wa wa s i m a m i z i wa mtihani hiyo. Kunema alisema usajili wa wanafunzi wanaotarajiwa kufanya mtihani huo wa somo la dini umeshafanyika mapema tofauti na miaka ya nyuma, ambapo ilichukuliwa kama changamoto na kufanyiwa kazi mwaka huu. Hata hivyo Kunema alisema, mwaka huu kuna ongezeko la Shule na watahiniwa ukilinganisha na mwaka jana, kwani alidai Ji Dar es Salaam, Shule 276 zitashiriki na kufanya idadi ya wanafunzi watakaofanya mtihani huo kuwa zaidi ya 2500, ambazo wamethibitisha kushiriki. A l i s e m a , wa n d a a j i

wa mitihani hiyo wanatarajiwa kuanza zoezi la usambazaji wa mitihani siku ya Ijumaa (leo) au Jumamosi (kesho) katika Shule shiriki hususani Jini Dar es Salaam. Ama kwa upande wa mikoani Ust. Kunema alisema, yeye si msemaji kwa ujumla ila alidai hana shaka kuwa mitihani hiyo itakuwa imeshasarishwa na kufika katika vituo husika tayari kwa kuwafikia watahiniwa, katika siku iliyopangwa. Tunatazamia safari hii (mwaka huu) mtihani huu kufanyika takribani Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani, nako huko suala la wasimamizi limeshafanyiwa kazi kama ilivyokuwa hapa Jijiji. Alisema Ust. Kunema.

BENKI ya Kiislamu ya Amana inayoendesha shughuli zake kwa mujibu wa taratibu zinazofuata sheria za Kiislamu nchini, imet o a f u t a r i k w a watoto yatima na wajane jijini Dar es Salaam. Akizungumza na An-nuur katika zoezi la utoaji wa futari hiyo, Meneja Masoko wa Benki hiyo Bi. Fatuma Mruma, alisema katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani, Benki hiyo imeamua kutoa futari na sadaka kwa watoto yatima na wajane waishio katika mazingira magumu. Leo tumejaaliwa kutembelea katika Kituo hiki cha Tahdhil Q u r a n A l - h i d a a ya c h a B u g u r u n i k wa Mnyamani, Ilala Jini Dar es Salaam, lakini tumekusudia kuzikia familia zipatazo ishirini ndani ya Ramadhani ya mwaka huu, akiwemo mama mjane anayeishi na watoto saba Sinza. Alifafanua Meneja Masoko huyo. Alisema kuwa tayari Jopo la wafanyakazi wa Benki hiyo wametembelea na kuwafariji watoto yatima wanaoishi k w e n y e v i t u o v ya kulelea watoto hao waishio maeneo ya Te m e k e , Ta n d i k a , Kigamboni na Mtoni

jini Dar es salaam. Naye Meneja Miradi B w. D a s s a M u s s a , alisema msaada uliokabidhiwa katika vituo viwili vya kulea watoto yatima na familia za wajane, una thamani ya shilingi milioni tatu. Zoezi la kukabidhi futari hiyo lilifanyika b a a d a ya s wa l a ya Ijumaa wiki iliyopita. Kwa upande wake mkuu wa kituo Tahfidhil Qur an Alhidaaya Ust. Rashidi Hamisi Hakungwa, alielezea historia fupi ya kituo hicho alisema kilianzishwa mwaka 2 0 0 8 k i k i wa k a t i k a madrasa iliyoanzishwa mwaka 2007. Alisema kituo kilianza na watoto watano na hivi sasa kina vijana sitini, wavulana 40 na wasichana 20, wote wakiwa ni wa umri kuanzia miaka 5 hadi 15. Ustadhi Hakungwa alitoa shukrani zake za dhati kwa Benki hiyo kwa kuwakumbuka yatima, hususani katika mfungo huu wa mwenzi mtukufu wa Ramadhani na kuwapatia futari. Hata hivyo Ust. huyo amesema kuwa bado wanakabiliwa na changamoto nyingi, hasa gharama za uendeshaji wa kituo. Naye Bi. Zena Omari, mkazi wa Sinza ambaye ni mjane mwenye watoto saba, hakuwa nyuma kwa kuishukuru kwa dhati Benki ya Amana kwa msaada waliompatia.

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

Taasisi ya Khidmat Islamiya inawatanganzia Waislamu wote Safari ya Hijja kwa Gharama ya Dola 4450 tu. unaweza kulipa kwa awamu (Kuhijiwa) ni Dola 1450 tu. Kuondoka ni 5/10/2013 kurudi 27/10/ 2013 Piga Simu 0784 786680, 0713 986 671, 0774 786 680 E-Mail) hajjkhidmat@gmail.com , Tovuti (Website) www.khidmatislamiya.com

Safari ya Hijja Dola 4450 tu. 1434/2013

Markazi Ummu Suhail ni kituo cha kuhifadhisha Qur aan kwa Mabinti wa Kiislamu. Kituo ni cha bweni kipo mkoani Kilimanjaro wilaya ya hai. Umri: kuanzia miaka 13 na kuendelea. Kituo kitafunguliwa 9/08/2013 Inshaalah. Fomu za kujiunga zinapatikana msikiti wa Riadha, wahi nafasi ni chache Kwa mawasiliano zaidi tupigie simu namba 0754 029 518 Mlete mwanao apate elimu yenye manufaa.

14

RAMADHAN 1434, IJUMAA AGOSTI 2-8, 2013

AN-NUUR

15

RAMADHAN 1434, IJUMAA AGOSTI 2-8, 2013

AN-NUUR

16

RAMADHAN 1434, IJUMAA AGOSTI 2-8, 2013

AN-NUUR

You might also like