Professional Documents
Culture Documents
tz
Sauti ya Waislamu
ISSN 0856 - 3861 Na. 1081 RAMADHAN 1434, IJUMAA , JULAI 26- AGOSTI 1, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=
Waislamu wanatambua msimamo wenu wa kupigania haki, pia wanaamini kukamatwa kwenu ni ukweli wa methali isemayo kiza kinapozidi kuwa kinene, ndivyo kupambazuka kunavyo karibia.
RAIS wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein (katikati) akiteta na Makamu wake, Maalim Seif Sharif Hamad. Kulia ni Sheikh Farid Hadd.
Walimu tatizo sugu hijab mashuleni Kisa cha Veer Pratap Singh Waraka wa Serikali wazidi kupuuzwa na Masheikh wa Uamsho
Wazazi watakiwa kusimama kidete
akizungumzia kadhia mbalimbali za uvaaji wa Hijjab kwa wanafunzi wa kike katika shule za msingi. Alisema walimu wengi wamekuwa wakitoa maelekezo kwa wanafunzi wa Kiislamu, wakitaka wavae Hjab wanazotaka wao ambazo zipo nje ya sheria na mafundisho ya Kiislamu. Ust. Ngalongela, alisema amekuwa akifutilia suala la uvaaji wa vazi hilo kwa wa f u n z i wa K i i s l a m u katika shule zilizopo Kata ya Kawe, na kukutana na vikwazo kutoka kwa walimu wa shule hizo. Awali Ust. huyo alika Inaendelea Uk. 2
Na Bakari Mwakangwale I M E E L E Z WA k u w a wenye ufahamu wa kutafsiri Hijjab ni Waislamu na si walimu, ambao wamekuwa wakiwabughudhi wanafunzi wanaovaa vazi hilo kwa mujibu maelekezo ya dini yao wanapokuwa shuleni. Hayo yamebainishwa na mratibu wa Islamic Education Pannel, wilaya ya Kinondoni, Jijini Dar es Salaam Ust. Rajabu Ally Ngalongela, wakati
Hii ndiyo nchi yangu: Ukweli, Haki itawale Waliodaiwa si mapapai hayataoza, wajitizame Wanafanya nini kuleta Haki Sawa kwa Wote
Zanzibar ya leo ni nchi yenye kuhuzunisha; haisikitishi tu, bali inahuzunisha. Ni nchi yenye kutatanisha, wakati mwingine hujikanganya yenyewe. Na viongozi wake? Naona hata haina haja ya kuwaeleza walivyo. Uk. 7
2
www.annuurpapers.co.tz
Tahariri/Makala
Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam
AN-NUUR
katika madhara makubwa sana. Ama kuhusu hilo, Mtume wa Allaah (Saw) amesema: Mwenye kunywa pombe duniani, kisha hakuleta toba, atanywima Akhera (al-Bukhaariy na Muslim). Hadithi hii inamaanisha kuwa mlevi anayaendelea na ulevi wake, na akakosa kuomba maghra kabla ya kufa kwake, hatokuwa ni mwenye kuipata Akhera. Hii inatuleta katika mashariti ya toba. Ni hakika kuwa ili toba kukubaliwa ni lazima Muislamu atekeleze masharti kadhaa. Ikiwa kosa lake linaingiliana na haki ya Allah aliyetukuka, b a s i m we n ye k u t u b i a anatakiwa atimize mashariti matatu ambayo ni kuacha maasi kabisa,
kwa kuwa sare walizokuwa wamezivaa ni tofauti na wenzao shuleni hapo. Alisema Wajumbe wa Waislamu walitoa maelezo kuhusu usahihi wa vazi hilo la hab na kubainisha kuwa, zile zinazovaliwa na wanafunzi wengi si h i j a b k wa m u j i b u wa Uislamu, bali wanafunzi wanalazimika kuvaa hivyo kutokana na walimu kuzikataa hab stahiki. Ust. Ngalongela, alisema waliwaeleza walimu shuleni hapo kuwa suala la hijab, Waislamu wana waraka wa serikali wa kuwaruhusu baada ya kudai vazi hilo kuvaliwa kwa wanafunzi wa kike wa Kiislamu mashuleni na vyuoni. Serikali iliruhusu vazi hilo livaliwe mashuleni na vyuoni, lakini kwa kuwa yenyewe haina dini, haikutoa maelekezo ya muundo wa hijab, bali tunaojua ni sisi Waislamu, walimu mnapaswa kujua hijab inavaliwaje kutoka kwa Waislamu. Alisema Ust. Ngalongela. Akibu hoja ya walimu kuwa wengi wanavaa hijab na hawafukuzwi, alisema hao wasiofukuzwa wapo nje ya vazi la hab na hao wanaowafukuza ndio haswa wanaovaa hab sahihi katika Uislamu. Ust. Ngalongela pia alipinga hoja ya walimu waliodai kuwa wanafunzi hao wapo nje ya sare na wanachafua utaratibu wa shule, akisema haiwezekani Inaendelea Uk. 4 wafukuzwe kwa hoja hiyo
Na Bakari Mwakangwale
Habari
AN-NUUR
akiwahutubia waumini wa Nungwi. A i d h a S h k h Po n d a , aliwataka waumini wa Nungwi kujiimarisha kwa miradi ya maendeleo kwa kutumia vizuri hazina kubwa ya ardhi waliyonayo ambayo imekuwa ikivamiwa kwa kasi kubwa na wawekezaji wa mahoteli ya kitalii, ambao kwa asilimia tisini wanaharibu utamaduni wa Mzanzibar. Sheikh Ponda, alisema Jumuiya ya UAMSHO, inatarajia kufanya muhadhara mkubwa siku ya Ijumaa (leo) katika M s i k i t i wa M b u y u n i , lengo likiwa ni kufanya majumuisho ya mihadhara iliyofanyika akiwa huko wiki iliyopita.
wakati walimu wenyewe hajui hab ni nini. Alisema baada ya mjadala wa muda mrefu na kuonekana kama somo limeelewaka, mkuu wa shule alitaka wanafunzi hao waliofukuzwa kuendelea kuvaa hivyo, lakini akitaka wasiongezeke wanafunzi wengine. Mkuu wa shule alisema, kuwaruhusu wengine sasa hivi itakuwa kuwachafua wanafunzi kwa kutofautiana katika sare, hivyo alidai tusubiri mpaka mwakani watakapoweka sheria ya hab tuliyoitaka. Alisema Ust. Ngalongela akirejea hoja za mwalimu. Hata hivyo hoja hiyo ilipingwa na Waislamu na mkuu wa shule kulazimika kukubaliana na Waislamu kuwa, ndani ya miezi miwili wanafunzi wote wa Kiislamu wawe wanavaa hab za aina moja. Kufutia matukio hayo, Ust. Ngalongela, aliwataka Waislamu kuelewa kuwa kuvaa Hjab ni Sharia ya dini yao na kwa upande wa mamlaka (Serikali) sheria ya nchi yao imeruhusu, hivyo ni jukum lao kusimamia amri hizo katika Dini na ile ya Serikali. Kwa miaka zaidi ya m i t a t u s a s a , U s t . N g a l o n g e l a a m e k u wa akitoa maelekezo sahihi ya habu kwa mujibu wa Uislamu kuwa ni nguo
ni hivyo, basi ameafiki. Alisema Ust. Ngalongela. Mkuu wa Shule hiyo ambaye alikuwa ni Mkristo, alitaka kujua nembo ya shule itakaa eneo lipi la vazi hilo, ambapo walikubalina ikae ama juu ya juba au chini kabisa mwa shati (nusu kanzu). Baada ya kuruhusiwa mwanafunzi huyo, wa l i j i t o k e z a we n g i n e waliovaa kama mwenzao, hata hivyo wanafunzi hao nao walifukuzwa na mkuu wa shule msaidizi. Ust. Ngalongela, alisema alionana na mwalimu huyo kisha kumweleza kuwa tatizo hilo walishalimaliza na Mwalimu Mkuu, lakini mwalimu huyo hakuliaki, akidai kuwa hizo sio habu zinazotakiwa shuleni. Ust. Ngalongela alieleza k u wa a l i p o s i k i M k u u wa Shule hiyo karudi kutoka safari ya msibani, alirudi na kuonana naye n a k u m u e l e z a j u u ya kufukuzwa wanafunzi wengine kwa kuvaa hab sahihi. Alisema baada ya kuongea na Mkuu wa Shule, alionyesha kushangaa na kuhoji kwa nini jambo hilo linakuwa linajirudia shuleni kwake. Ust. Ngalongela, alimweleza kuwa tatizo ni yeye mkuu wa shule, kwani baada ya kulimaliza tatizo la hab kwa mwanafunzi wa awali, hakuchukua jukumu Inaendelea Uk. 4
HABARI/Matangazo
AN-NUUR
Ujumbe wa Umoja wa Nchi za Visiwa vidogo katika Bahari ya Hindi umezuru Zanzibar kwa ajili ya kuifahamisha serikali ya Zanzibar juu ya mikakati ya kusimamia mazingira ya nchi za visiwa. Ujumbe huo ulioongozwa na Ronald Jumeau wa Sychelees, ulika osi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Migombani, kwa ajili ya kumuelezea mipango ya mkutano mkuu wa
la kuwafahamisha walimu wake juu ya usahihi wa vazi hilo kwa wanafunzi wa kike wa Kiislamu. Katika tukio lingine shuleni hapo, mwanafunzi mmoja alipigwa na mwalimu kisha kutakiwa kuvua hijabu yake. Kesi ya kupigwa mwanafunzi huyo ilikishwa Msikitini. Tukio lile liliwagusa Waislamu wa Kawe, baada ya kuona linajirudia mara kwa mara katika shule hiyo hiyo, taarifa zilisambazwa na waliamua kwenda shule hapo kuhoji kwa nini binti huyo apigwe kwa ajili ya hijab. Alisema Ust. Ngalongela. Alisema siku hiyo akiwa ameongozana na mzazi wa
alikuwa na kikao nao, ili suala hilo lisirudie katika shule zao. Hata hivyo, baada ya kufuatiliwa katika kikao baina yake na wakuu wa shule, Mratibu huyo hakulizungumzia suala hilo kama alivyowaahidi Waislamu. Kadhia ya hab haikuishi hapo, kwani katika Shule ya Msingi Ukwamani Kawe, mwanafunzi mwingine alifukuzwa. Lakini baada ya Ust. Ngalongela kuzungumza na mkuu wa shule na kupewa waraka wa serikali unaoruhusu vazi hilo la Hjab, Mkuu huyo wa shule alimwita mwanafunzi aliyefukuzwa, kisha alimruhusu kuvaa hab hiyo lakini akimtaka akimtaka kutowaeleza wenzake.
k u z i w e z e s h a k u wa endelevu. Licha ya kuwa Zanzibar inaingia katika umoja huo kupitia Ta n z a n i a , i m e k u wa ikinufaika na miradi mbalimbali ya uhifadhi wa mazingira. Ujumbe huo pia umekutana na Waziri wa Nchi Osi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Ferej, ambaye ameelezea matumaini yake juu ya Zanzibar inavyoweza kunufaika na umoja huo. Alisema Zanzibar itaendelea kutoa kila aina ya ushirikiano kuhakikisha kuwa nchi za visiwa zinafanya kazi pamoja na kujifunza mafanikio yaliyokiwa na nchi nyengine, ili kufikia malengo ya kuwa na maendeleo endelevu. Amefahamisha kuwa nchi za visiwa ikiwemo Zanzibar zimekuwa zikikumbwa na changamoto kadhaa za kimazingira, ambapo hivi sasa baadhi ya maeneo ya kilimo Zanzibar hayafanyi kazi kutokana na kuvamiwa na maji ya chumvi na kuwafanya wakulima wa maeneo hayo kutokuwa na cha kufanya. Hata hivyo serikali imekuwa ikichukua juhudi kuona kuwa changamoto hizo zinapungua.
NAFASI ZA MASOMO KIDATO CHA TANO 2013-2014 MICHEPUO YOTE YA SAYANSI ,SANAA NA BIASHARA IPO
PCB,PCM,CBG,PGM,HGL,HGK,HKL,EGM,HE,ECA,KLA
SHULE NI YA BWENI NA KIPEKEE KWA MABINTI WA KIISLAMU KIMAADILI, KIMALEZI BORA YA KIISLAM TUNENDELEA KUPOKEA WANAFUNZI KWA KIDATO CHA TANO NA WAHAMIAJI KIDATO CHA KWANZA NA TATU 0713465437, 713515054 AU 0756082772
STASHAHADA (DIPLOMA)
CHUO NI CHA BWENI KWA WASICHANA NA WAVULANA ADA NI NAFUU SANA NA INALIPWA KWA AWAMU WAHI SASA NAFASI NI CHACHE NA WANANDOA WANAKUBALIWA
MKUU WA CHUO
0713 673495
RAMADHAN KAREEM
Habari za Kimataifa/Tangazo
AN-NUUR
CAIRO Muhammad Morsi, Rais aliyengolewa madarakani na jeshi na kuendelea kushikiliwa katika mahabusu za jeshi hilo nchini Misri, ameanza mgomo wa kula. Televisheni ya Russia Today, imemnukuu kiongozi mmoja wa kundi la Ikhwanul Muslimin, Muhammad al Baltaji, akisema katika mahojiano yaliyofanywa na televisheni hiyo kuwa, Morsi ameanza mgomo wa kula mwishoni mwa wiki. Wakati huo huo Waziri Mkuu wa serikali ya mpito ya Misri Hazem al Beblawi, ametaka kukiwa mapatano ya kitaifa ili kuhitimisha migawanyiko miongoni mwa raia wa nchi hiyo. Wa m i s r i k a d h a a wameuliwa katika ghasia zilizoiubuka kati ya wapinzani na wafuasi wa Muhammad Morsi. Akizungumza na t e l e v i s h e n i ya s e r i k a l i mapema wiki hii, al Beblawi alisema kuwa wakati umeka sasa wa kufikiwa suluhu ya kitaifa kwa kuwa Misri imegawanyika. Beblawi amesema, Misri imekuwa uwanja wa mapigano na m i k wa r u z a n o k u f u a t i a k u p i n d u l i wa M o r s i n a kuongeza kuwa, kufikiwa suluhu ya kitaifa ni njia pekee inayoweza kuiondoa Misri katika hali ya sasa. Rais wa muda wa Misri, Adly Mahmoud Mansour, ameunda Kamati ya Wataalamu wa Sheria, ambao watapandekeza mabadiliko katika katiba ya sasa, ambayo inasema taifa hilo linapaswa kutawaliwa kwa misingi ya sheria za Kiislamu. Rais Mansour, Jumamosi iliyopita aliteua kamati ya wataalamu kumi, ambao watapendekeza marekebisho katika katiba ya sasa iliyoidhinishwa wakati wa utawala wa Mohammad Morsi, aliyepinduliwa na jeshi mwanzoni mwa mwezi huu. Katiba ya mpya ya Misri iliidhinishwa rasmi Desemba 2012 kufuatia wananchi kuipitisha kwa kura kwa asilimia 64. M i e z i s i t a b a a d a ya kuidhinishwa katiba hiyo, jeshi la Misri lilimuondoa madarakani Rais Morsi na kuwatia mbaroni wananchama waandamizi wa harakati ya Ikhwanul Mislimin pamoja na kumshikilia Morsi mwenyewe.
Wananchi wa Misri baada ya kuuangusha utawala wa ki Imla wa Hosni Mubarak, walikuwa wakisisitiza kuwepo katiba mpya
FAMILIA ya Rais aliyeondolewa madarakani nchini Misri Mohamed Morsi, imetangaza uamuzi wa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Mkuu wa Majeshi, Jenerali Abdel Faah Al Sisi, kwa kuendelea kumshikilia mateka kiongozi huyo wa Chama cha Muslim Brotherhood. Mtoto wa kike wa Morsi aliyefahamika kwa jina la Shaimaa Mohamed Morsi, ndiye aliyetangaza mpango huo wa kuchukua hatua za kisheria dhidi Jenerali Al Sisi, ambaye ndiye aliyetangaza kwamba Morsi anashikiliwa na Jeshi. Shaimaa ameweka wazi kwamba watachukua hatua hizo za kisheria kwa kuangalia sheria za ndani ya nchi hiyo na hata zile za kimataifa, huku akimtaja mara kadhaa Jenerali Al Sisi kuwa ndiye aliyeongoza mapinduzi ya kijeshi ya kumwaga damu na kumuondoa baba yake madarakani. Binti huyo wa alisema kile kinachofanywa na Jeshi ni utekeji nyara, hivyo wao watachukua sheria dhidi ya hatua hiyo. S h a i m a a a m e wa e l e z a waandishi wa habari Jijini Cairo kuwa, wamelitaka Jeshi kumuachia Morsi, lakini limeendelea kumshikilia kwa madai ya sababu za usalama na kiafya, jambo ambalo limeendelea kuwaacha bila majibu. Familia ya Dk. Morsi imeshasema kuwa haifahamu sehemu alipo baba yao kwa sababu jeshi halawapa taarifa zozote na kwamba, ndiyo maana wameona ni wakati muafaka sasa wa kuchukua hatua za kisheria.
ya Al Alam Ahmad al Siou, ametiwa mbaroni. Hata hivyo Maasa hao wa usalama hawakutoa sababu za kitendo chao hicho. Tangu Dkt. Morsi apinduliwe na jeshi, maasa usalama nchini humo wamezifunga stesheni kadhaa za televisheni ikidaiwa kuwa ni katika kile kinachoonekana kuwa ni kuzima juhudi na sauti za wapinzani wa mapinduzi hayo nchini humo.
huru wafungwa wote wa kisiasa, akiwemo Muhammad Morsi, Rais aliyeenguliwa madarakani nchini Misri. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ujerumani Guido Westerwelle, amesema kuwa vyama na makundi yote ya kisiasa ikiwemo Harakati ya Ikhwaanul Muslimiin, yanapaswa kuwa na nafasi kwenye serikali ijayo ya Misri.
6
Na Omar Msangi
VEER Zaara ni sinema ya Kihindi ya mwaka 2004 iliyotolewa na kampuni ya lamu Yash Raj Films. Nadhani ilipewa jina hili kwa sababu ya majina ya washiriki wake wakuu ambao ni Veer Pratap Singh na Zaara Hayat Khan. Katika sinema hii kinaelezwa kisa cha mtu mmoja Mhindi kutoka India aliyekamatwa na kufungwa jela Pakistan kwa miaka 22 akidaiwa kuwa ni jasusi. Sinema inapofunguka anaonekana mfungwa mmoja yupo katika sero ya pekee kajawa na huzuni tele upweke ukimuelemea. Inavyoonekana ilikuwa majira ya baridi kwa sababu anatetemeka kwa baridi na kanyikunyata na blanketi. Taratibu ananyanyuka na kukiendea kiriba cha maji kilichokuwa kimewekwa kwa mbali karibu na lango la chuma. Anapokichukua na kutaka kunywa maji anasita anaposikia sauti ya Athana. Allahu Akbar, Allahu Akbaru (Mungu mkubwa Mungu mkubwa). Hii inakua kama ishara k wa k e k u wa k a t i k a t i ya tabu ile, bado yupo Mungu wa kumlilia na kumtegemea. Kilichofuatia ni kuonekana wakili kana binti ambaye anajipa moyo na kujiambia kwamba lazima amsimamie Veer Pratap Singh mpaka apate haki yake. Hata hivyo, hii ikiwa kesi yake ya mwanzo toka kumaliza kosi yake ya sheria, Wakili wa Serikali, mkongwe, Zakir Ahmed ambaye h a j a wa h i k u s h i n d wa hata katika kesi moja, anambeza akimwambia hataambulia chochote watakapopambana mahakamani. Ve e r P r a t a p S i n g h ndio jina lake halisi, lakini katika kesi ushahidi uliowasilishwa mahakamani ulidai kuwa yeye ni Rajesh Rathore. Rajesh Rathore ambaye alidaiwa kuwa ni kachero wa I n d i a n a a l i i n g i a Pakistan kwa ajili ya kufanya ujasusi. Upande wa mashitaka ukawasilisha vielelezo na ushahidi, kimoja wapo kikiwa ni hati ya kiapo aliyosaini Rajesh Rathore ikidaiwa kuwa anakiri kuwa hilo ndio jina lake na kweli yeye ni jasusi kutoka India. Kwa ushahidi huo Veer Pratap Singh (Rajesh Rathore) akahukumiwa kifungo cha maisha. Baada ya kukaa jela kwa
Makala
AN-NUUR
Inaendelea Uk. 7
7
Inatoka Uk. 6
ya kimeza na kumwacha Veer kuamua anayoa au anasuka. Ni makaratasi hayo, ambapo inadaiwa kuwa Veer Pratap Singh ni Rajesh Rathore na kwamba yeye ni kachero aliyeingia Pakistan kufanya ujasusi. Sinema inamwonyesha Veer akikumbuka ahadi yake mbele ya Zaara (ash back) kwamba hata kama ataolewa na mtu mwingine, ikitokea ikalazimu yeye kutoa uhai wake kwa ajili yake, atafanya hivyo. Veer akaona kuwa ni lazima atimize ahadi yake. Akasaini kiapo kile cha mahakama na ukawa ndio ushahidi uliomtia hatiani. L a k i n i wa k a t i Ve e r akishushwa katika gari na kupelekwa polisi, gari lile alilokuwa akisafiria mbeleni linapata ajali mbaya na abiria wote kufariki. Kwa hiyo kule India, wakajua kuwa Veer kafa. Huku nyuma Zaara naye akajuwa kuwa Veer kafa. Sinema ni ndefu, lakini baada ya Saamiya kufanikiwa kumshawishi Ve e r k u z u n g u m z a , inaonekana wapo mahakamani. Mwisho wa yote anapatikana Zaara na kuja mahakamani kutoa ushahidi kuwa yule si Rajesh Rathore, bali Veer Pratap Singh na inabainika wazi kuwa hat i zilizowasilishwa mahakamani ilikuwa za kughushi. Lakini hata kabla ya Zaara kufika mahakamani, askari mmoja aliyekuwepo wakati kesi hiyo inabuniwa, alishikwa na imani na kusema kweli kuwa Baniani wa watu hakuwa na hatia na kwamba hilo jina la Rajesh Rathore, sio lake. Kwa uchungu mkubwa na uso wa huruma, jaji aliyekuwa akisikiliza kesi ile alimtaka radhi Veer kwa niaba ya Serikali na watu wa Pakistan. Lakini hiyo inakuja baada ya Veer Pratap Singh kukaa jela kwa miaka 22. Aliyekuwa wakili wa Serikali ya Pakistan katika kesi hii, Zakir Ahmed, ambaye anasifika kwa k u t o k u s h i n d wa h a t a kesi moja (hii ilikuwa ya kwanza), baada ya kumalizika kesi alikwenda na kumshika mkono Saamiya na kumpongeza. Alieleza mengi, lakini makubwa mawili: Moja ni jinsi wanasiasa na watu wenye madaraka Serikalini wanavyoweza kusababisha
Habari/Tangazo
AN-NUUR
JULAI 12 dunia ilishuhudia jinsi Malala Yusufzai, msichana kutoka Pakistan mwenye umri wa miaka 16, alivyotolewa ukumbi na kupokelewa New York na Ban Ki Moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Isitoshe, tarehe hiyo ambayo ndiyo siku yake ya kuzaliwa ilitangazwa rasmi na Ban Ki Moon kuwa sasa itakuwa ikijulikana kuwa ni Siku ya Malala. Lengo ni kuwapatia elimu watoto wote duniani. Malala Yusufzai Siku hiyo msichana huyo alipewa fursa adhimu ya kuhutubu kwenye mkutano wa kwanza wa Baraza la Vana la Umoja wa Mataifa kwenye makao makuu ya Umoja huo, New York. Alitoa hotuba ya kusisimua katika mazingira yaliyo
Inaendelea Uk. 8
k u m p a n d i s h a k we n ye jukwaa la Umoja wa Mataifa. Simlaumu Malala kwa utukufu alioupata. Lakini ninaulaumu ulimwengu kwa kimya chake pale watoto wengine wanapouliwa takriban kila siku kama si Afghanistan basi Iraq; kama si Iraq basi Syria au Pakistan au Somalia. Nchini Afghanistan na Pakistan mara kwa mara watoto huuliwa ama na wanajeshi wa Kimarekani au wa NATO au huuliwa na vile vyombo vya Kimarekani virukavyo angani bila ya rubani. Mara zote hizo huambiwa kwamba watoto hao waliuliwa kwa makosa. Huko Syria, Iraq, Somalia na Pakistan wakati mwingine
Inaendelea Uk. 8
8
Inatoka Uk. 7 watoto huuliwa na makundi ya watu wenye itikadi za kidini zilizo sawa na zile za Mataliban wa Pakistan. Kwa hakika miongoni mwa wenye kufanya unyama Syria ni Mataliban wa Pakistan wale wale waliotaka kumuua Malala. Juzi tu walitangaza kuwa mamia ya wapiganaji wao wamekwishapiga kambi Syria na wanashirikiana na kundi la Jabhat al-Nusra dhidi ya serikali ya Bashar. Makundi hayo mawili pamoja na lile la al-Qaeda katika Iraq na mingineo yenye itikadi kama zao yako chini ya mwavuli wa Syrian Islamic Front (SIF). Huko Syria Mataliban na wenzao wamekuwa wakiwaua watoto, wanawake pamoja na wazee. Lakini wakuu wa dunia hii wamekaa kimya kwa vile wauaji hao wanampinga Bashar. Kuna kimya kingine kinachonishangaza. Nacho ni cha wanaharakati wa K i z a n z i b a r i wa l i o z i b a midomo yao kuhusu madhila yanayowakuta wale waliokuwa wakiwaita Mashekhe wetu wa Uamsho. Tangu mashekhe hao 10 waanze kukamatwa Oktoba 16, 2012 mpaka leo kesi yao haijatajwa mahakamani. Hadi sasa wamesomewa tu mashitaka dhidi yao, mashitaka ambayo yanahusika na vurugu zilizotokea Zanzibar Mei mwaka jana. Wa s h i t a k i w a h a o wa l i f i k i s h wa m a r a ya mwisho mahakamani Julai 3 mwaka huu na walitarajiwa kupandishwa tena mahakamani Julai 18. Washitakiwa wenyewe ni Farid Hadi Ahmed, Msellem Ali Msellem, Mussa Juma Issa, Azan Khalid Hamdani, Suleiman Juma Suleiman, Khamis Ali Suleiman, Hassan Bakari Suleiman, Ghalib Ahmada Omar, Abdalla Said Ali na Fikirini Majaliwa Fikirini. M a s h i t a k a yanayowakabili ni kuchochea vurugu, kuharibu mali za umma na za watu binafsi zenye thamani ya shilingi milioni 5 0 0 , k u f a n ya v u r u g u katika eneo la Magogoni na kuhatarisha usalama wa taifa la Zanzibar. Wa n a s h i t a k i w a p i a kuhusu kadhia ya Farid Hadi Ahmed aliyetoweka Oktoba 16, 2012. Shekhe huyo aliibuka siku nne baadaye akidai kwamba alitekwa nyara na watu waliovaa barkoa
Makala
AN-NUUR
za kisiasa. Serikali inazidi kujifaragua ikiamini kwamba kuwatia adabu viongozi wenye muelekeo wa Kiislamu hakutowakera wakubwa wa dunia hii. Labda serikali inaamini kwamba balozi za Marekani na Uingereza zitayafumbia macho wanayotendewa mashekhe hao kwa sababu z i m e k w i sh a t i wa s u mu ya Uamsho kusingiziwa ugaidi. Ndio maana kesi hiyo ikawa inaakhirishwa na kuakhirishwa kwa lengo la kuwaweka ndani tu mashekhe hao. Mara ya mwisho Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar alisema wanasubiri waletewe daari la kesi kutoka Mahakama ya Rufaa, Dar es Salaam. S i j u i Wa z a n z i b a r i wenzangu wanapofuturu na aila zao katika mwezi huu mtukufu kama
Mazungumzo yakaisha. Watu wale wakati ule waliodaiwa sio mapapai na wakiona kuwa walikuwa wakidhulumiwa, kwamba sheria ilitumika vibaya dhidi yao, hivi sasa wapo madarakani katika nafasi m b a l i m b a l i . S wa l i n i je, kuna juhudi yoyote wanayofanya kuhakikisha kuwa haki kwa wote, ukweli na uadilifu unakuwepo? Kutokana na ushahidi uliowasilishwa mahakamani, Veer Pratap Singh alikaa jela miaka 22 ndio inakuja kujulikana kuwa ushahidi ulikuwa wa uwongo. Nani atalipa dhulma hii? Japo Jaji aliomba radhi kwa niaba ya Serikali ya Pakistan kwa sababu ilikuwa Jamhuri ndiyo iliyomshitaki Veer, samahani hii italipa mateso ya miaka 22 jela? Miaka 22 mke amekosa mapenzi ya mume, watoto wamekosa malezi na huduma ya baba, huenda wamekuwa chokoraa, mitaani, samahani itasaidia nini? Ni kwa kuzingatia yote hayo, Wakili Zakir Ahmed alimshukuru Saamiya Siddique akimwambia, ahsante sana kwa kunionyesha upande wa pili: Ubinadamu, Ukweli na Haki.
9
Na Said Rajab. T U A N G A L I E mfano mwingine wa kimapinduzi kutoka kwenye Sunna ya Mtume wa Mwenyezi Mungu. Watawala wa Qurayshi walimuomba baba yake mdogo Mtume amuombe Muhammad (saw) kwa niaba yao, aachane kabisa na harakati zake. Baba yake mdogo alimkabili Mtume kwa mapendekezo haya: Kama unataka wadhifa a u h a d h i , wa k u u wa Maqurayshi wako tayari kukupa wadhifa wowote unaotaka; Kama unataka kuwa mkuu wa Makka yote hii, wakuu wa Maqurayshi wa k o t a ya r i k u k u p a ukubwa huo; Kama umeshikwa na mapepo wabaya, basi wakuu wa Maqurayshi wa k o t a ya r i k u k u p a mganga bora kabisa aliyekuwepo. Mapendekezo mawili ya kwanza yanaonekana kuwa mazuri. Baadhi ya Waislamu wa leo, wanaokwenda na wakati, wangekimbilia mapendekezo hayo, wakidhani ni fursa ya kusimamisha Uislamu kwa kutumia njia iliyowekwa na makari. Kwanini Mtume wa Mwenyezi Mungu alikataa mapendekezo yote hayo? Katika hali na mazingira hayo, nini lilikuwa jibu la Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa Waislamu wa zama zote? Kwa haki ya Mwenyezi Mungu, Ewe baba yangu mdogo, hata kama wangeliweka jua kwenye mkono wangu wa kulia na mwezi kwenye mkono wangu wa kushoto, ili niache harakati hizi, sitoacha mpaka Mwenyezi Mungu anipe ushindi au nife nikifanya kazi hii. Kauli hii ya kitume ndiyo iliyopaswa kuwa maelezo mafupi ya kinga ya kimapinduzi ya Waislamu, dhidi ya mbinu zote chafu za makafiri, kuwaingiza Wa i s l a m u k w e n y e mfumo wao, ili kuwatoa kwenye malengo mapana ya Kiislamu. Msimamo h u o wa k i m a p i n d u z i wa Mtume, ndiyo uliowakomboa Waislamu wa awali kutoka kwenye aina zote za woga: Wala hawakuwa wenye kumdhuru yoyote kwa hayo ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Qur (2:102) Na kama Mwenyezi Mungu akipenda
kunidhuru, uombezi wako hautanifaa kitu, wa l a h a wa t a n i o k o a ! Qur(36:23) Sema: Halitatusibu ila alilotuandikia Mwenyezi Mungu Qur (9:51) Aya nyingi ndani ya Qur an zinazungumzia jinsi ya kuwakomboa Waislamu kutokana na utumwa wa kifikra na kuwategemea viumbe b a d a l a ya M we n ye z i Mungu: ..bila shaka wale m n a o w a a b u d u mkamuacha Mwenyezi M u n g u , w a o hawakumilikiini riziki, takeni riziki kwa Mwenyezi Mungu, na Muabuduni na Mshukuruni. Kwake mtarudishwa Qur(29:17) Sema: Ni nani anayekuruzukuni kutoka mbinguni na ardhini? Waambie: Mwenyezi Mungu Qur(34:24) Hakika hiyo ndiyo riziki yetu (tutakayowapa), isiyomalizika (isiyotindika) Qur(38:54) Na mwisho, msukumo wa kimapinduzi wa Quran unakabiliana pia na kifo. Muislamu haogopi kufa. Lakini hiyo haina maana kwamba Waislamu wa n a p e n d a k u u a a u kuuliwa. Muislamu anakabiliana na kifo iwapo kifo hicho kitakuwa ni kitendo cha ibada au uchamungu. Baadhi ya Waislamu wanaotumiwa na Taghut wanaogopa sana kifo. Wanaziogopa hata Aya za Quran kuhusu changamoto ya kifo: Bila shaka sisi tunahuisha na kufisha, na marejeo ni kwetu Qur(50:43) Na sisi ndiyo tunaohuisha na tunaosha; na sisi ndiyo warithi (wa yote hayo wakati ambao hapana kitakachokuwa kihai) Qur(15:23) N a ye n d i ye aliyekuhuisheni kisha atakufisheni, kisha atakufufueniQur (22:66) Na kwamba Yeye ndiye anayeleta ya kufurahisha na kuhuzunisha. Na kwamba Yeye ndiye Afishaye na kuhuisha Qur(53:43:44). Sisi tumekuwekeeni mauti, basi hatutashindwa (kukufueni wala) Qur(56:60) Ni mtazamo wa kimapinduzi tu uliyo ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mungu, ndiyo unaoweza kuondoa vipengele vyote
Uislamu na Mapinduzi - 2
v ya wo g a wa k i j i n g a kwa Waislamu. Baada ya Waislamu kujawa na hamasa hii ya kimapinduzi, n d i p o wa t a k a p o we z a kukabiliana vilivyo na Taghut. Waislamu wa awali walipokuwa tayari wameshajengwa kwenye msingi huo wa kimapinduzi, Aya zifuatazo za Quran zilishuka: Basi waandalieni nguvu mziwezazo (silaha) na mafarasi waliofungwa tayari tayari, ili kwazo muogopeshe maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu.. Qur (8:60). Kwa yakini Mwenyezi Mungu anawapenda wale wanaopigana katika njia yake safu safu, kama kwamba wao ni jengo moja lililokamatana barabara Qur(61:4). Na nyote piganeni na makari kama wao wote wanavyopigana nanyi.. Qur(9:36) Na piganeni katika njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanaokupigeni wala msipindukie mipaka (mkawapiga wa s i o k u p i g e n i ) Q u r (2:190). Na piganeni nao mpaka kusiwe na mateso (wao kuwatesa waislamu bure), na dini iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu Qur(2:193). Ewe Mtume (wa Mwenyezi Mungu)
Makala
AN-NUUR
wahimize walioamini waende vitani Qur(8:65). Enyi mlioamini! Mkutanapo vitani na wale waliokufuru msiwageuzie migongo (mkakimbia) Qur(8:15). Aya hizo na nyingine nyingi ndani ya Qur an zinatosha kuondoa taswira potofu ya Mtume Muhammad (saw), ambayo Waislamu poa (moderates) wa leo wanataka kuenga. Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa ni mwanamapinduzi hasa wa Kiislamu. Amekamilika idara zote. Mtume ambaye ndiye kiigizo cha Waislamu wote, alishiriki vita 27 ikiwemo misafara. Aliagiza kuangamizwa kwa watu 400 wa kabila la Bani Quraida, waliotaka kuwahujumu Waislamu baada ya makubaliano, akiwemo kafiri mmoja aliyeitwa Ubay bin Khalaf. Agizo la Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa makamanda wake, wakati wa ukombozi wa Makka (Fathu Makka), lilikuwa wasimuue mtu yeyote, isipokuwa kama mtu huyo alikuwa na nia ya kuwaua Waislamu. Lakini pamoja na hayo, kuna baadhi ya watu Mtume aliagiza wauawe, hata kama wangekutwa wamejisalimisha ndani ya
RAMADHAN KARIM
Funga na Hukmu zake, Watu 10 Walioruhusiwa kula Mchana wa Ramadhani, Mambo 10 yasiyoharibu funga Maswali na majibu
SWAUMU YA RAMADHAN
VINAPATIKANA MSIKITI WA MTORO KATIKA DUKA LA SAIMU GWAO NA IBN HAZM MEDIA CENTRE Mawasiliano: 0713 471090
Jipatie vitabu vyenye mafunzo ya Funga ya Ramadhani, vilivyoandaliwa na Sheikh Nurdin Kishki kama vile:- Hadithi 30 kuhusu Funga ya Ramadhan. Hukumu za Funga ya Ramadhan. Ipi Idadi sahihi ya Swala ya Tarawehe. Vingine ni Ndoa Talaka na Eda. Pamoja na Uislamu si Dini ya Ugaidi. Kwa mahitaji ya jumla na reja reja, ka dukani kwa Saimu Gwao, Msikiti wa Mtoro au Ibn Hazim MediaCentre. Simu:-0713 471 090, 0715 825 672, 0773 194 646.
10
Nabtadi kuangaza, Sunnah hii kwa kaumu, Si sawia kuibeza, kwani ni Sunnah adhimu, Si nyingine nadokeza, Tarawehe ya msimu, Sunnah hii ya msimu, kwanini twaipuuza.
Mashairi/Habari
AN-NUUR
Tarawehe, si sunnah tu !
Si sunnah twajisemeza, kupunguza umuhimu, Kathiri twaipuuza, kwa ghururi ya rajimu, Ya kwake twayatukuza, japo ya kyendawazimu, Sunnah hii ya msimu, kwanini twaipuuza. Nini tutamueleza, Hakimu wa mahakimu , Hilo ka tuuliza, siku ile ya hukumu, Yu nani wa kumjuza, amama atakadamu, Sunnah hii ya msimu, kwanini twaipuuza. Twadunisha yenye izza, twaadhimisha ya ghamu, Yatotunyima mwangaza, kwa la kaburi dhwalamu, Akhera nako ni kiza, na mzomzo nadamu, Sunnah hii ya msimu, kwanini twaipuuza. Yalo laghwu twatukuza, ya kheri hatuna hamu, Karata kutwa twacheza, pasipo kukosa hamu, Na nikahi twachombeza, bayana kwa maharimu, Sunnah hii ya msimu, kwanini twaipuuza. Kwa pool twajitokeza, lilosheheni haramu, Kamari linoikuza, kwa kulisi kaumu, Allah alotukataza, twapokezana kwa zamu, Sunnah hii ya msimu, kwanini twaipuuza. Kucheza bao twaweza, mchana kutwa twadumu Wasaa twaupoteza, kwenye dhumna kukumu, Na runinga zatumeza, kama joka la mdimu, Sunnah hii ya msimu, kwanini twaipuuza. Thamaniya metimiza, risala yangu metimu, Kwa Mola kujisogeza, si kwa faradhi kutimu, Bali kujinyenyekeza, kwa sunnah kujilazimu, Sunnah hii ya msimu, si vyema kuipuuza. ABUU NYAMKOMOGI MWANZA.
MSIKITI uliojengwa na Taasisi ya Africa Islamic Relief of Kuwait katika Shule ya Sekondari ya Kiislamu ya Aljebra Kigamboni Dar es Salaam, umekabidhiwa shuleni hapo na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Sami Mohamed hivi karibuni.
Mashindano hayo yameandaliwa na taasisi ya Khidmatul Quran Islamic Foundation ya jini Dar es Salaam.
*MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, amewahimiza W a i s l a m u kushirikiana na kusaidiana kwa dhati ili kudumisha umoja miongoni mwao. Alifafanua kwamba umoja na mshikamano ndio nguzo ya kuzidisha mapenzi miongoni mwa Waislamu, hivyo kutaka utamaduni huo uendelezwe kwa maslahi wananchi na taifa kwa ujumla. Maalim Seif alitoa kauli hiyo alipokuwa akitoa shukrani kwa Masheikh na wananchi waliojumuika naye katika futari a l i yo i a n d a a n y u m b a n i k wa k e Mbweni kwa ajili ya viongozi hao wa dini. Aliwashukuru Masheikh kwa kujitokeza kwa wingi
katika futari hiyo na k wa m b a , k i t e n d o hicho ni ishara ya mapenzi waliyonayo v i o n g o z i wa d i n i kwa viongozi wao wa kitaifa. Wa k a t i h u o huo, Maalim Seif amehitimisha ziara yake ya kutembelea wagonjwa na wawa kwa upande wa Unguja, baada ya kufanya ziara katika mkoa wa Mjini Magharibi. Aw a l i a l i f a n y a ziara katika wilaya za Kusini na Kati Unguja, yakiwemo maeneo ya Kizimkazi Mkunguni, Kijini Makunduchi, Jambiani na Ndani. Makamu huyo wa Rais pia alitembelea maeneo ya wilaya za Mjini na Magharibi na kuonana na wa g o n j wa k a t i k a maeneo ya Mbweni, Tomondo, Magogoni na Mji Mkongwe. Akiongozana na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa
Nchi, Osi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Fatma Abdulhabib Ferej na Naibu Waziri wa Elimu Zahra Ali Hamad, Maalim Seif alianza ziara yake mapema asubuhi katika mitaa wa Mbweni matrekta, Kiembe samaki na Mwanakwerekwe, kabla ya kusitisha ziara hiyo kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya wanajeshi wawili wa Zanzibar wa l i o f a r i k i h u k o Darfur nchini Sudan. Hata hivyo alihitimisha ziara hiyo kwa kutembelea Jimbo la Mji Mkongwe, ambako alikwenda kuwajuilia hali na kuwafari mzee Salim Mzee wa Darajani na mzee Ali Yussuf wa Mkunazini. Maalim Seif pia anatarajiwa kufanya ziara akma hiyo katika mikoa ya Pemba hivi karibuni, ndani ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
11
Na: Mujahid Mwinyimvua
Makala/Habari
kutumika kama futari. Kundi la pili la vyakula ni vyakula vinavyokaa tumboni kwa muda mrefu (kiasi cha saa 6 mapa 8 au zaidi). Vyakula hivyo ni kama vile nafaka na mbegu ngano, shahiri, mtama, mahindi, mchele na maharage. Inashauriwa na wataalamu wa vyakula wa kiislamu kuwa vyakula kama hivi viliwe kama daku au usiku sana kwa wale wanaoshindwa kuamka na kula daku. Vyakula hivi vitawapa nguvu ya kuhimili mikiki mikiki ya saumu mchana na pia wataweza kumudu majukumu mengine ya kazi za mchana. Kwa hiyo, vyakula hivi ndio vizuri zaidi kuliwa kama daku. Katika funga nia kubwa ya Mwenyezi Mungu ni kupima utii wetu kwake, sio kutukomoa. Ndio maana funga ya Kiislamu inahimiza kula daku karibu na alfajiri na kutufuru mara tu jua linapo zama. Maana yake hizo ni takriban saa 14 (kati ya saa 24 za siku nzima) (pale ambapo mchana so mrefu) zinatosha kupima utii wetu kwa Mola. Hii maana yake ni kuwa Uislamu unazingatia namna Allah a l i v yo u u m b a m w i l i . Swaumu ya muda fulani ni tiba katika mwili, lakini ukizidisha muda sana bila mwili kuupa chakula, utakidhuru kiwiliwili hasa ubongo. Madai ya baadhi ya watu Baadhi ya wasiokuwa waislamu wanabeza na kudai kuwa sisi tunakula a l f a j i r, h a l a f u n d i o tunafunga. Wajaribu na wao kufunga japo kwa saa 12 tu wataona ugumu wa swaumu, hasa kwa a s i e f u n g a k wa i m a n i ya kumkubali Mola Muumba. Tunakumbuka Mwalimu Julius K. Nyerere alivyofunga na waislamu enzi za kudai uhuru, kabla ya jua kuzama alisema kichwa kinamuuma na apewe asproo. Masheikh wakamhamasisha asubiri mpaka muda wa kufuturu ulipoka. Hii ndio swaumu haina mchezo kwa mtu anaependa dunia tu. Kwa hakika kula na kufanya jimai ndio furaha kubwa katika maisha ya kidunia, na wengi wanamuasi Mola kwa hayo mawili, yaani tumbo na utupu. Makundi ya vyakula Wa t u w a n a o f u n g a wanatakiwa kuchagua na kula vyakula kutoka katika makundi mbalimbali kwa
AN-NUUR
Daku ni chakula kinacholiwa usiku wa manane kwa ajili ya kujiandaa kufunga siku inayofuata. Kula daku ni jambo lililokokotezwa sana na Uislamu kama tunavyojifunza katika Quraa na Hadithi za Mtume Muhammad (rehma na aman zmfke): .....Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa Alfajir katika weusi wa usiku..... (Quran: 2:187). Mtume Muhamad (rehma na aman zmfke) amesisitiza sana kula daku. Tuone hadithi moja ifuatayo: Kuleni daku, kwani ipo baraka katika kula daku. Na tofauti ya fadhila ya funga zetu sisi na Ahlul Kitabu (Wayahudi na Wakristo) ni huko kula daku. Mlo bora wa daku Vy a k u l a v i n a w e z a kugawanywa katika makundi makuu mawili kwa kigezo cha muda wake wa kukaa tumboni. K u n d i l a k wa n z a n i vyakula vinavyo chukua muda mfupi, saa 2 mpaka 4 kusagwa. Mfano wa vyakula hivyo ni vile laini kama ndizi, viazi na matunda. Kama tuliona katika makala zilizopita, vyakula laini ni vizuri
kila mlo wa futari na daku. Makundi hayo ya vyakula ni: Nafaka, vyakula aina ya mizizi na ndizi za kupika Kundi hili la vyakula linajumuisha nafaka kama mahindi, mchele, mtama, ulezi na ngano; ndizi za kupika na vile vya aina ya mizizi kama magimbi, mihogo na viazi. Vyakula hivi huupa mwili nishati (nguvu) vile vile vitamini, madini na protini kiasi kidogo. Vy a k u l a j a m i i y a mikunde, vile vya kokwa na vyenye asili ya wanyama Vy a k u l a v i l i v y o k o katika kundi hili ni pamoja na maharage, mbaazi, karanga, korosho, nyama, samaki, mayai na maziwa ambavyo vyote ni chanzo kikubwa cha protini. Pia, vyakula hivyo ni chanzo cha vitamini na madini. Matunda Matunda ni chanzo kizuri cha vitamini C, vitamini za aina nyingine na baadhi ya madini. Kundi hili linajumuisha matunda kama matikiti, zabibu, mapapai, maembe, machungwa, limau, ndimu, machenza, nanasi, pamoja na matunda pori kama ubuyu, mabungo na ukwaju. Mboga mboga Kundi hili linajumuisha matembele, kisamvu, majani ya maboga,
AL-MADRASATIL FADHAKIL iliyopo Kata ya KIBAMBA kwa kushirikiana na uongozi wa Madrasa pamoja na USTADH WA MADRASA wameandaa mashindano ya kuhifadhi QUR'AN JUZUU Tatu (3) na HADITHI ZA MTUME (S.A.W.). Kwa wanafunzi wa Madrasa Kata ya Mbezi na Kibamba. Ynayotarajiwa kufanyika Ramadhani ya (11) mpaka Ramadhani ya (14). Kwa ajili ya kuitukuza na kupata fadhira zaidi za Qur'an na sifa zaidi za Mtume Muhammad (S.A.W.) wanaomba Waislamu wote Watanzania wenye uwezo. Na wale wote waliojaaliwa na Allah (s.w.) wawasaidie ili kufanikisha kupata zawadi za kuwapa motisha vijana wote watakaoshiriki ambao ni zaidi ya (80) na wanawaomba kuhudhuria kwa watakaojaaliwa na Allah (s.w.). Kwa mawasiliano: 0757 375993 MWENYEKITI 0171 649313 USTADH
Msaada unahitajika
Inawaomba Waislamu kuchangia kamati ili iweze kusaidia Familia za Waislamu 52 walioko Jela. Tuma Mchango wako kwa Amiri Buiya S. Buiya 0763 241270 M.pesa na 0655 241270 Tigo pesa Katibu Ally Mbaruku 0777 816040 Ezy Pesa au 0784 816040 Airtel Money Kwa mawasiliano zaidi pia unaweza ukapiga simu kwa Namba hizo hapo juu. Unapotoa katika kheri, hakika umejiwekea akiba isiyoharibika.
12
AN-NUUR
MAKALA
Bismillah Rahmanir Rahim UMOJA WA WANAFUNZI WA KIISLAM WALIOSOMA NCHINI SUDANI (INTERNATIONAL UNIVERSITY OF AFRICA)
UWAWASU
INA WAALIKA WASOMI WOTE WALIOSOMA NCHINI SUDAN KUHUDHURIA MKUTANO MUHIMU MAALUMU NA FUTARI YA PAMOJA MKUTANO UTAFANYIKA KATIKA
UKUMBI WA ITIQAMA- MSIKITI WA ILALA
12
TAREHE 2-8-2013 sawa na mwezi 24 Ramadhani baada ya swala ya ijumaa. Sote tuwasili hapo Tafadhari mjulishe na mwingine asikose
FARIDA Jumaa (8), akisoma Qur an katika mashindano ya kuhifadhi Qur an, yaliyofanyika Yombo, Jini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. wanazingatia maadili ya dini yao. Kwa upande wake, mgeni rasmi katika hafla hiyo ambaye ni Mkurugenzi msaidizi wa Chuo Cha M a r k a z i C h a n g o m b e , Doktour Swalahuden Maftaha, alisema mbora miongoni mwa watu ni yule aliyeisoma Qur an kisha akaifundisha. Aliwataka walimu wanaofundisha na kuhifadhisha Qur an, kutoa mafunzo pia kwa watoto hao kuisoma, kuihifadhi kisha kuizingatia ili waweze kukia lengo. Kila anayeifundisha Qur an atilie mkazo pia kwa kuzingatiwa ile maana yake, maana yale ni maamrisho k u t o k a k wa M we n ye z i Mungu kisha yafanyiwe kazi, ikiwa hilo litazingatiwa tunaweza kufika mbali. Alisema Doktour Maaha. Aidha, Mkurugenzi huyo wa Markazi Changmbe, aliwataka walimu wa Madrasa, kufundisha na kuhimiza ibada ya swala kwa vijana wanaowasomesha Qur an, kwani alidai haifai kwa anayeisoma Qur an, (hadhi) kisha asiwe mwenye kusimamisha swala. Jumla ya Madrasa nane zilishiriki katika mashindano hayo yaliyoandaliwa n a u m o j a wa M a d r a s a zinazohifadhisha Qur an, Yombo. Umoja huo ulianzishwa mwaka 2011, umesema m p a k a s a s a wa m e p a t a mafanikio kadhaa ikiwa ni kupata ongezeko kubwa la vana wanaohifadhi Qur an katika Madrasa hizo. Mafanikio mengine yametajwa kuwa ni umoja huo kutoa wanafunzi (Mahadhi) wanao kwenda kushiriki mashindano mbalimbali yakiwemo ya Afrika Mashariki. Umoja huo umesema, mbali ya mafanikio hayo lakini pia wamekutana na changamoto mbalimbali i k i we m o u p u n g u f u wa Misahafu, Juzuu na vitabu mbalimbali. Pia tuna uhaba wa maeneo ya kufundishia ikiwemo tatizo sugu la mishahara kwa walimu wanaohifadhisha na kufundisha Qur an. Tu n a o m b a wa d a u mbalimbali kutuunga mkono katika kuondoa changamoto hizo kwa lengo la kustawisha Uislamu na vana wetu kwa ujumla. Ulisema uongozi huo.
nchi washirika kila mmoja atumie fedha yake katika nchi yao ili kuondosha msongano wa maingiliaona ya kifedha. Walisema kuwa hatua hiyo itaziwezesha nchi washirika wa Muungano kujitegemea katika kukuza uchumi wao kwa kuwa na fedha yake badala ya kuwapo kwa fedha ya pamoja kwa nchi zote. Tunaamini wazi kuwa kila nchi mshirika wa Muungano wa Tanzania akatumia fedha yake katika nchi yake kwa kiasi fulani itasaidia sana katika kutafautisha nchi na nchi badala ya kuwapo kwa fedha ya pamoja, walisema wajumbe hao. Masoud Saleh a k i wa s i l i s h a k a z i z a vikundi alisema kuwa ni vyema kwa Tume ya mabadiliko ya katika ikaliondoa suala la Polisi kuwa la Muungano na badala yake suala hilo kuwa la nchi washirika. Alisema kuwa kazi kubwa ya Jeshi la Polisi ni kulinda raia na mali zao, hivyo ni vyema tume ikaona kuwa ili nchi washirika kuwa nguvu katika utawala wao hakuna budi suala hilo wakapewa wao badala ya kuwapo kwa Serikali ya Muungano. Kwa kuwa Jeshi l a Po l i s i l i n a k we n d a sambamba na mahitaji ya wananchi hivyo tunashauri kwa tume suala hilo wakaachiwa n c h i wa s h i r i k a h a s a ukaangali kila mmoja atakuwa na katiba ya nchi yake, alisema Masoud. Alifahamisha kuwa pindi suala hilo likaachiwa Serikali ya Muungano, i n a we z e k a n a l i k a t o a huduma kinyume na malengo yao, kutokana na kila nchi watakuwa na
Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.
Taasisi ya Khidmat Islamiya inawatanganzia Waislamu wote Safari ya Hijja kwa Gharama ya Dola 4450 tu. unaweza kulipa kwa awamu (Kuhijiwa) ni Dola 1450 tu. Kuondoka ni 5/10/2013 kurudi 27/10/ 2013 Piga Simu 0784 786680, 0713 986 671, 0774 786 680 E-Mail) hajjkhidmat@gmail.com , Tovuti (Website) www.khidmatislamiya.com
Markazi Ummu Suhail ni kituo cha kuhifadhisha Qur aan kwa Mabinti wa Kiislamu. Kituo ni cha bweni kipo mkoani Kilimanjaro wilaya ya hai. Umri: kuanzia miaka 13 na kuendelea. Kituo kitafunguliwa 9/08/2013 Inshaalah. Fomu za kujiunga zinapatikana msikiti wa Riadha, wahi nafasi ni chache Kwa mawasiliano zaidi tupigie simu namba 0754 029 518 Mlete mwanao apate elimu yenye manufaa.
14
AN-NUUR
15
AN-NUUR
16
AN-NUUR