You are on page 1of 12

www.annuurpapers.co.

tz

Sauti ya Waislamu

(22) AHLU SUNNA WAL JAMAA


Inawatangazia Waislamu wote kuwa imeanza maandalizi yake kwa ajili ya HIJJA 2013 kwa lengo la KUONGEZA UFANISI KATIKA IBADA ZA MAHUJAJI WETU kwa gharama za Dola 4300. Lengo letu ni kukamilisha mipango yetu kabla ya kumaliza mwezi mtukufu wa Ramadhani.Tafadhali wasiliana nasi ifuatavyo: Tanzania Bara: 0717224437; 0777462022;Unguja: 0777458075;Pemba: 0776357117.

Mwanafunzi aliza waumini Mtambani


Adai kupigwa teke na mwalimu akienda kuswali Wanafunzi Wakristo wasimama kidete kumtetea

ISSN 0856 - 3861 Na. 1079 SHAABAN 1434, IJUMAA , IJUMAA JULAI 12 - 18, 2013 BEI TShs 500/=,

Wakumbukeni kwa Dua Tanzania tusimame Masheikh walioko ndani imara kuinusuru nchi
Tuzingatie aliyosema DCI Manumba
Uk. 7

KATIBU Mkuu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ramadhan Sanze akiongea na vyombo vya habari katika kongamano la kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani lililofanyika katika Hoteli ya Golden Jubilee Tower jini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Kesi ya Victor imeishia wapi?


Mwenzako akinyolewa, tia kichwa chako maji Tutizame Pakistan ilikokishwa sasa inatukanwa Ilianza na kudai Masheikh, Uamsho ni magaidi Sasa Taifa la nyuklia, limegeuzwa mwanasesere
Uk. 3

MWANAFUNZI Abubakar Ally.

Allah awape Subra, malipo mema Wanaodhulumu wajitathmini upya Wakumbuke, ipo siku ya Hukumu

Uk. 3

2
www.annuurpapers.co.tz

Tahariri/Makala
Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

SHAABAN 1434, IJUMAA JULAI 12 - 18, 2013


sasa ni taifa na serikali iliyofeli na iliyodhalilika, hao hao waliowafikisha hapo sasa wanawakejeli na kuwatukana. Anasema, wanada kuwa serikali yote ya Pakistan na vyombo vyake vya usalama imenunuliwa na CIA na wanatamba wakisema kuwa kila mmoja wao ana bei yake, tena rahisi sana. He also claimed that the US CIA had been able to deeply penetrate Pakistani society, quoting a US intelligence ocer as having allegedly told him: You are so cheap we can buy you with a visa, with a visit to the US, even with a dinner we can buy anyone. Amenukuliwa Pasha akitoa ushahidi katika Tume hiyo iliyoundwa na serikali ya Pakistan. We are a failing state, even if we are not yet a failed state. Luteni Generali Ahmed S h u j a Pa s h a a l i s e m a akihitimisha maelezo yake. Swali la msingi ni je, Pakistan imefikaje hapo? Mchezo wote huu umeanzia k a t i k a i n a yo i t wa v i t a dhidi ya ugaidi. Serikali ya Pakistan wakati huo chini ya Generali Perves Musharaff, iliaminishwa kuwa ndani ya Pakistan kuna magaidi na ikatakiwa kufungua milango yake kwa makachero na askari wa Marekani kusaidia kupambana na magaidi hao. Pakistan ikasifiwa sana na Marekani kuwa ni mshirika muhimu katika vita dhidi ya ugaidi. Na ikawa inapewa misaada mbalimbali mingi ikiwa ya kikachero na kijeshi. Ikakia mahali askari na makachero wa Marekani kufanya Pakistan kama uwanja wao wa nyumbani. Wanaweza kufanya lolote bila kuulizwa. Kupitia ushirika huu, wananchi wengi wa Pa k i s t a n wa m e u l i wa wakiwemo watoto wa Madrasa, wanafunzi shuleni, akina mama mitaani, sokoni na mahali pengi ambapo yalifanywa mashambulizi ikidaiwa k u wa wa n a o p i g wa n i magaidi. Ni kupitia ushirikiano huu, makachero na askari wa Marekani walifunguliwa milango na kufanya wanavyotaka huku matukio yaliyodaiwa kuwa ni mashambulizi ya kigaidi nayo yakizidi. Kwa maana nyingine, ushirikiano huo, ndio uliozua balaa zaidi kwani wameuliwa watu wengi wasio na hatia, hasa katika kipindi hiki cha kutumia ndege zisizo na rubani (drone). Kabla ya hapo hapakuwa na mauwaji ya kiwango hicho. Na hii ni moja ya vielelezo kuwa kila ushirika huu ulipoanzishwa, ndio ulileta balaa zaidi kama ambavyo hivi sasa Iraq kuna mauwaji zaidi ya kikabila na kidini, mambo ambayo hayakuwepo kabisa wakati wa Saddam Hussein. Tumelieleza tukio hili kwa urefu kwa sababu kwa muda mrefu sasa kumekuwa na jitihada za kuisajili nchi yetu kuwa ni nchi yenye makundi ya kigaidi. Juhudi hizi zilianza kwa vitisho na tahadhari zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya balozi za nje hapa nchini au serikali zao. Wakati huo, serikali zetu, kwa maana ya muungano na Zanzibar, zilikuwa zikifanya juhudi kukanusha habari hizo za kuwepo kitisho cha ugaidi wakisema Dar es Salaam na Zanzibar ni salama kwa hiyo watalii waje. Hali hiyo imekwenda mpaka sasa imekia mahali viongozi wetu na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinaimba wimbo huo huokuwa kuna kitisho cha ugaidi! Nchi si salama! Jambo la kukumbukwa na kuzingatia hapa ni kuwa vitisho hivi vilianza, hata al Shabab wenyewe hawakuwepo. Lakini ukiacha vitisho na tahadhari iliyokuwa ikitolewa kupitia balozi na nchi za nje juu ya hatari ya ugaidi Tanzania na Afrika Mashariki, kulikuwa na zile taarifa ambazo zilikuwa zikipandikiza chuki kati ya Waislamu na Wakristo. Hicho ni kipindi ambapo tulikuwa tukisikia habari za Waislamu kuingiza majambia, mara Waislamu wanataka kulipua hospitali ya Muhimbili na mambo kama hayo. Na karibuni hivi ndio yakaibuliwa haya ya al Shabab na tuhuma za kulipua makanisa na kuangamiza watu wa dini nyingine. Tunachotaka kusema hapa ni kuwa ukitizama taarifa kama zile za madai ya mtoto wa Kiislamu kuingia ubalozi wa Marekani na kigaloni cha mafuta ya taa, madai ya kuingia nchini waliodaiwa magaidi akina Fazul na haya ya sasa hivi ambapo jitihada zimekuwa zikifanyika kuunganisha baadhi ya Masheikh na taasisi za Kiislamu na kinachoitwa ugaidi wa al Shabab au Boko haram; Inaendelea Uk. 4

AN-NUUR

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786


MAONI YETU

MAPEMA wiki hii tume iliyokuwa imeundwa kuchunguza tukio la kikosi maalum cha Marekani kuvamia makazi yaliyodaiwa kuwa ya Usamah Bin Laden na kumuuwa (The Abboabad Commission) imetoa taarifa yake. Katika uvamizi huo uliofanyika usiku wa tarehe 1 Mei, 2011, inadaiwa kuwa serikali ya Pakistan ilikuwa haina habari kabisa kwamba tukio kama hilo litafanyika, wala kuwa na taarifa kuwa Usama Bin Laden alikuwa akiishi eneo hilo. Pamoja na taarifa ya Tume kuonyesha kuwa v i o n g o z i wa S e r i k a l i kuanzia Rais na hata Waziri wa Ulinzi hawakuwa na habari wala kuarifiwa rasmi baada ya uvamizi kufanyika, taarifa hiyo ya kurasa 336 inasema kuwa hata polisi walioka eneo la tukio baada ya kufanyika mauwaji walizuiwa kufanya chochote kwa hiyo hapakuwa na taarifa yoyote ya kipolisi kuhusu uvamizi na mauwaji hayo. K a t i k a t a a r i f a h i yo imeelezwa kuwa kitendo cha askari wa Marekani kufanya uvamizi katika ardhi ya Pakistan bila ya kuomba ruhusa wala k u a r i f u v y o m b o v ya kiusalama na kijeshi, ni kitendo cha uhalifu wa kivita na kukiuka sheria za kimataifa. Lakini pia ni kitendo kinachodhihirisha k u wa Pa k i s t a n k u n a serikali kama hakuna, kuna jeshi na Idara ya Usalama kama hakuna. Wote, wanasiasa, viongozi wa serikali na taasisi za keshi na usalama wa nchi, zimefanywa kuwa hazina maana yoyote. Kaputi! Serikali imelaumiwa, Idara ya Usalama imelaumiwa, Polisi wamelaumiwa na kila waliokuwa wangeweza kuhusika kwa namna moja

Tanzania tusimame imara kuinusuru nchi


au nyingine. Ufupi wa maneno, taarifa imesema k u wa Pa k i s t a n , t a i f a lililokia kuwa na silaha za nyukili, limegeuzwa kuwa mwanasesere na kiroja cha karne. Limekosa heshma na kudharaulika kabisa kiasi cha watu kutoka nchi nyingine, kuingia na kufanya harakati za keshi bila kujali kuwa hiyo ni nchi huru yenye serikali na Rais wake. R i p o t i h i y o inayopatikana katika mtandao wa Aljazeera na iliyochambuliwa kwa marefu na mapana katika kituo cha televisheni cha Aljazeera kuanzia Jumanne hadi hii leo, inamnukuu Waziri wa Ulinzi wakati huo Chaudhry Ahmed Mukhtar, akisema kuwa hakujua chochote juu ya uvamizi wa Marekani na wala hakuambiwa kilichotokea baada ya uvamizi. Akihojiwa na Tume hiyo alisema kuwa yeye alijua kuwa kikosi cha makomandoo wa M a r e k a n i wa m e i n g i a na kufanya uvamizi na kumuuwa Usama Bin Laden kupitia magazeti. A n a s e m a b a a d a ya kusikia kilichotokea k u p i t i a v yo m b o v ya habari, akapata pia simu kutoka kwa binti yake anayeishi New York, Marekani akimuuliza juu ya tukio hilo. Ripoti inafichua zaidi kuwa hata baada ya uvamizi, Serikali ya Marekani haikushughulika kutoa taarifa kwa Serikali ya Pakistan. Kilichofanyika ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Marekani (US Chairman of the Joint Chiefs of Sta Commiee) Admiral Mike Mullen, kunyanyua simu na kumwarifu Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Pakistan, (Pakistani Chief of Army Staff ) General Ashfaq Pevez Kayani. Sasa

ilikuwa ni kazi ya Kayani kumwarifu Rais wake au kuacha. Kwa mujibu wa taarifa ya Tume, Generali Kayani alitoa taarifa kwa serikali masaa kadhaa baada ya tukio na kuongeza k u wa u c h u n g u z i wa o umebaini kuwa serikali yote na vyombo vyake vya dola vilikuwa kizani na waliofanya uvamizi, walifanya kana kwamba hakuna serikali au Idara za Usalama na Ulinzi za Pakistan. Kama kuna aliyetumika, anasema Chaudhry Ahmed Mukhtar, alitumika kama kachero; mtumishi wa CIA na unaweza kusema kuwa msaliti wa Pakistan. Kama alivyonukuliwa Mkuu wa Idara ya Usalama (ISI), Lt-Gen Ahmed Shuja Pasha akisema, yote hayo ikijumuishwa na madai kuwa Usama Bin Laden aliweza kuishi Pakistan kwa miaka 9 bila serikali kujua mpaka alipouliwa na Wamarekani, ni ushahidi tosha kuwa serikali na vyombo vyake vimelemaa na kufeli kabisa. Akionyesha wasiwasi wake kuwa huenda hiyo inatokana na wengi katika watendaji muhimu kununuliwa na kutumikia masilahi ya nchi nyingine b a d a l a ya k u i t u m i k i a Pakistan, anatoa mfano wa Saeed Iqbal, Kanali wa jeshi mstaafu ambaye alionekana akivinjari eneo lililodaiwa kuwa makazi ya Usama akipiga picha huku akitembea na gari lisilopenya risasi. Anasema Iqbal alitoweka mara baada ya tukio na uchunguzi unaonyesha kuwa alikuwa mtumishi wa CIA. Akielezea ilichovuna Pa k i s t a n k a t i k a h i k i kinachodaiwa kuwa uraki na ushirikiano na Marekani ambao ndio kilichopelekea haya ya Abboabad, Pasha anasema: We are a very weak state, also a very scared state. Taifa ambalo limefikia hatua ya kuweza kutengeneza bomu la nyukilia, limefanywa kuwa very weak and very scared state. Na kwamba kufeli huku: not so much of specic individual or institutional failure, but with a problem of collective and systemic failure. Lakini la kutisha zaidi mkuu huo wa Idara ya Usa l a ma ya Pa k i st a n , Lt-Gen Ahmed Shuja Pasha, anasema kuwa baada ya kufanywa nchi yao ifikie mahali kuwa

Na Bakari Mwakangwale

Mwanafunzi aliza waumini Mtambani


swala ya Ijumaa. Alisema Abubakar. Alisema, wakati wao wakikatazwa kuvaa Kanzu na koa (Baraghashia) iwe nje au darasani, wenzao Wakristo huvaa rozali wakiwa nje na darasani, bila bughudha yoyote. Akielezea mkasa uliomkumba, Abubakar alisema, alipokuwa anatoka bwenini akiwa ndani ya kanzu yake, kabla hajamaliza mazingira ya shule alikutana na mwalimu aliye mtaja kwa jina moja la Jailo. Alisema, aliulizwa na mwalimu huyo kwamba anakwenda wapi, naye alimjibu kwamba leo (siku hiyo) ni Ijumaa hivyo anaelekea kuswali. Abubakar, aliendelea kusimulia mahojiano na mwalimu huyo kwamba alimuuliza kuwa hilo alilovaa ni vazi gani, naye alimjibu kuwa hiyo ni kanzu. Akaniuliza, kwani hilo vazi limeruhusiwa kuja nalo hapa shuleni? Nikamwambia, katika fomu ya kujiunga hapa shule imeeleza tuje na nguo za nyumbani za heshima, hivyo na hii kanzu ni miongoni mwa vazi la heshima. Alisema akirejea mahojiano yake na mwalim Jailo. A k a s e m a , b a a d a ya kumjibu hivyo mwalimu huyo alihamaki, na kuhoji kwa kusema, hilo ni vazi la heshima? ambapo alimjibu ndiyo ni vazi la heshima na ndio maana naenda nalo katika ibada, Alisema, mwalimu huyo akaendelea kumhoji kama hajawahi kupewa maelezo kuhusu vazi hilo shuleni hapo, huku akimjibu kuwa hajaona sehemu ambayo wamezuiliwa kuvaa vazi kanz Mwalimu yule, akaona sasa amwite mwalimu wa nidhamu, alipofika pale nae kwa ukali aliuliza hilo ni vazi gani, nami nikamjibu hii ni kanzu, hapo hapo alirusha teke na kunishambulia katika sehemu za korodani, nikaanguka chini, yeye akaondoka. Alisema huku alikilia na kufanya Waislamu waliokuwa wakimsikiliza kugugumia kwa vilio. A b u b a k a r, a l i s e m a alisikia maumivu makali, jambo ambalo lilifanya
kufika katika eneo la tukio na kumuinua na kwenda kumuombea ruhusa ili wampeleke hospitali. Alisema, walimu walionyesha kutokuwa tayari kutoa ruhusa. Waligoma kutoa ruhusa, jambo ambalo liliamsha hasira za wanafunzi. K wa t u k i o l i l e h a t a Wakristo hawakufurahishwa nalo na ndio walikuwa mstari wa mbele kwa kuwa Waislamu wengi walitoka kwenda kuswali, walisimama kidete wakisema lazima niende hospitali, kwani nilikuwa nalalamika maumivu makali. Alisema Abubakar. Alisema, baada ya muda,

Habari

SHAABAN 1434, IJUMAA JULAI 12 - 18, 2013

AN-NUUR

wanafunzi wenzake wengi wa kiwa Wakrtisto,

M WA N A F U N Z I Abubakar Ally, amewaliza Wa i s l a m u b a a d a y a kuelezea mkasa wa udini unaowakumba wanafunzi wa Kiislamu katika shule ya Sekondari Kahororo, Mkoani Kagera. Abubakar alisimama mbele ya Waislamu katika Msikiti wa Mtambani, Ijumaa wiki iliyopita, baada ya kutakiwa na Imam Hamza Omari, kutoa ushahidi jinsi kadhia ya Udini, ilivyokithiri shuleni hapo dhidi ya wanafunzi wa Kiislamu. Katika maelezo yake Abubakar, aliye muhitimu wa kidato cha sita, a m e s e m a k u wa k u n a baadhi ya walimu ambao kinyume kabisa na maadili ya kazi yao, wamekuwa wakidhihirisha chuki dhidi ya wanafunzi Waislamu. Akitoa mfano alisema kuwa yeye binafsi alipigwa teke bila ya kosa hali iliyosababisha hata wanafunzi Wakristo kuingilia kati kumtetea. Alisema, siku ya tukio alikuwa akienda msikitini kuswali Ijumaa lakini akazuiwa na mwalimu kwa madai kuwa hakutakiwa kuvaa kanzu. Alisema, mwalimu wa nidhamu ( Jailo) ndiyo kero kwa wanafunzi wa Kiislamu shuleni hapo, kwani hataki hata kuona Waislamu wakiswali. Pa l e S h u l e n i k u n a Kanisa kubwa sana kwa sababu shule hiyo zamani ilikuwa ni ya Kanisa, lakini sisi kuna chumba tu na hata hiyo adhana yenyewe huadhiniwa taratibu bila kutumia spika lakini bado iinaonekana kuwa ni kero. Alisema. Alisema, siku ya Ijumaa huambiwa wasitoke kwenda Msikini mpaka wapate kibali maalum na mwalimu ana uwezo wa kuwaruhusu au kuwakatalia. Lakini alidai, wenzao Wakristo siku za jumamosi na jumapili ni ruksa kutoka tu kwenda kwenye ibada bila kibali chochote. I l a s i s i Wa i s l a m u huambiwa siku ya Ijumaa mpaka tuombe ruhusa k wa n z a n a k u p a t i wa k i b a l i m a a l u m u k wa ajili ya kwenda kuswali

Wakumbukeni kwa Dua


Ustadh huyo akiongea n a m wa n d i s h i a n a s e m a WAISLAMU wametakiwa ameona atoe wito na nasaha k u l e t a d u a k w a w i n g i hizo kwa sababu hata kama kuwaombea Masheikh wa w a n a o w a s h i k i l i a w a n a Uamsho waliowekwa ndani, mamlaka kwa mujibu wa Allah awape subra na malipo sheria kuamuru mtu awekwe mema kutokana na mtihani ndani bila ya dhamana, lakini wenye mamlaka hayo uliowakuta. Wakitoa wito huo kwa wangetakiwa kutizama pia nyakati tofauti, baadhi ya ubinadamu. Masheikh wetu wanafunga Waislamu jini Dar es Salaam R a madhani wakiwa wamesema kuwa kwa mujibu wa mafundisho ya Quran, korokoroni, hatujui hali ya Sheria na katiba ya nchi, futari, daku na ibada zao za Masheikh hao hawajapatwa tarawehe na witri, zitakuwaje; na hatia yoyote na hivyo n a h a y a w a n a f a n y i w a hawastahiki kuadhibiwa, na wakiwa ni watuhumiwa tu, kinachowakuta ni moja ya pengine kwa Ramadhani mitihani ambayo Allah ndiye hii wangetakiwa hao wenye atakayewalipa. madaraka, kama ni Waislamu, Kwa mujibu wa Sheria za wakati wakifuturu na wake Kiislamu, kama wanadamu zao, wakumbuke kuwa kuna wangesikilizwa kwa madai watoto ambao wamekosa yao, wangedai damu na mali huduma ya futari kutoka kwa za watu wengine. Kwa hiyo ni wajibu wa mdai kuleta baba zao na kuna wake ambao ushahidi kuthibitisha madai wamekosa furaha ya kufuturu na waume zao. yake. Amesema muumini Amesema Ustadh Shakir akisisitiza kuwa mpaka sasa mwingine aliyejitambulisha hakuna ushahidi wowote kwa jina moja la Mustafa uliotolewa kuwatia hatiani na kuongeza kuwa kama Masheikh hao na kwamba mtu amepatwa na hatia na kuwashikilia bila ya dhamana kufungwa, hilo ni jambo ni kama kuwaadhibu bila ya jingine, lakini sio katika hali kosa kuthibiti. Katika hali hiyo akasema hii ambayo mtu ananyimwa kuwa, ingekuwa ni vyema kwa dhamana huku kukiwa na walioshikilia mpini na wenye malumbano ya kisheria iwapo madaraka ya kuwazuiya ni haki na ni katika sheria Masheikh hao, wakatizama kuwafanyia hivyo. upya Sheria zilizopo, iwapo Mi nadhani katika hali wanachowafanyia Masheikh kama hii ya malumbano, kama wa Uamsho ni sawa, haki na ilivyojitokeza katika kesi hii ubinadamu. juu ya suala la dhamana, Akasema, anayasema hayo nadhani wenye mamlaka akihofia kuwa kama kuna namna yoyote ya dhulma, wangeshika ile busara kuwa wenye madaraka wasidhani ni bora ukafanya kosa la kuwa dhulma hiyo itapita bure kumuacha huru mkosaji bure, lakini wajue kuwa yupo (kama ushahidi una utata), Mfalme wa Siku ya Malipo kuliko ukamuadhibu mtu na huyo ndiye Hakimu wa asiye na hatia. Wanajisikiaje mahakimu. wakisimama katika tarawehe

alipewa ruhusa na kupewa kiasi cha shilingi elfu kumi kwa ajili ya matibabu huku baadhi ya walimu wakimtaka kutosema kuwa amepigwa na mwalimu bali alieleze kuwa amepigwa na mpira. Alisema walipofika wa l i e l e z a u k we l i k u wa amepigwa teke na mwalimu, akatakiwa kwenda Polisi kwa ajili ya kupata fomu ya matibabu (PF3), na alipoka Polisi alipewa kisha akarudi hospitali. Kufika hospitali, PF3, ilizuiliwa kumbe yule mwalimu aliyenipiga alikuwa ameshaka hapo hospitalini cha ajabu wahudumu (manesi) walianza kunishawishi kuwa yaishe tu, kwa kuwa mimi ni mwanafunzi tena nipo kidato

cha sita. Alisema Abubakar. Alisema, katika mazingira hayo, hakupewa fomu hiyo ya Polisi na alipoingia kwa daktari baada ya kumueleza tatizo lake alipinga kunipa matibabu bila PF3, na kumtaka aende kuidai. Aliniambia niifuate, kwa kuwa wanafunzi wenzagu wa l i k u we p o p a l e , wo t e tulirudi kwa mhudumu yule (nesi) na kumzonga atoe PF3, akaitoa ndipo nilipoendelea kupata matibabu. Alisema. Pamoja na madai hayo, hadi tunakwenda mitamboni, mwandishi wa habari hizi hakuweza kufanikiwa kupata maelezo ya upande wa pili kwa maana ya uongozi wa shule na mwalimu Jailo mwenyewe.

Na Mwandishi Wetu

wanaswali huku katika kra zao ikiwajia picha ya watu walio ndani kutokana na kauli na amri zao? Alisema na kuhoji. Kwa upande mwingine Ustadh Shakir ambaye amesema kuwa yeye hazungumzi kama mtu mwenye wadhifa katika taasisi yoyote ya Kiislamu, bali kama Muislamu wa kawaida, amesema kuwa anadhani itakuwa vyema kwa taasisi za Kiislamu kutafuta namna ya kusaidia katika jambo hili. Amesema, lengo sio kuingilia uhuru na mamlaka ya mahakama wala kuvunja sheria, bali kujaribu kufanya k a z i ya k i wa k i l i k u o n a kama kuna uwezekano wa kurahisisha Masheikh hao kupata haki yao ya dhamana. Moja ya mafunzo ya Ramadhani ni kujenga moyo wa huruma, hebu tuwahurumie wenzetu walio ndani kwa kutizama ni kwa vipi tunaweza kuwasaidia kupata haki yao ya dhamana, itakuwa haionyeshi udugu na mshikamano wa Kiislamu kama tutakaa kimyaa bila kufanya juhudi yoyote. Amesema. Waislamu ni kama mwili mmoja ambapo kiungo kimoja tu kikipata tatizo, mwili mzima hupata maumivu, basi tukifutari tuhakikishe kuwa na familia za Masheikh walio ndani nao wamefuturu. Aidha, kama sheria na taratibu zinaruhusu, basi tuhakikishe kuwa Masheikh na Maimamu wetu walio ndani, nao wanafutari vizuri kama tunavyofutari sisi.

HABARI

SHAABAN 1434, IJUMAA JULAI 12 - 18, 2013

AN-NUUR

Misikiti iimarishe umma Tanzania tusimame sio kuleta faraka-Imam


Inatoka Uk. 2
Na Bakari Mwakangwale
Mtume (s a w) aliingia Msikiti kukuta vikundi viwili, kimoja kikimtaja Mwenyezi mungu, ikiwa si jambo dogo hata kidogo na kikingine kikisomea. Mtume (s a w) baada ya kuwaona alichagua kundi la wanaosoma na akasema hao wanamuomba Mwenyezi Mungu, huenda wakakubaliwa au wasikubaliwe katika wanayo yaomba, lakini hawa wanaosoma nafasi ya kukubaliwa ni kubwa zaidi, kwa sababu wanachofanya ni kitu bora. Alisema Shkh. Mohammed. Aidha alisema, nafasi nyingine ya Msikiti ni kujenga amani kwani Uislamu unahimiza sana amani kutona na Mwenyezi Mungu kushusha aya kadhaa zikitaja amani. Sheikh Mohammed, alisisitiza kwamba Misikiti isiwe sehemu ya mizozano, magomvi na mifarakano, kuvurugana baiana ya Waislamu kwa Waislamu au na wanajamii. Alisema, Mtume katika kuonyesha heshima ya Misikiti alika akasema kwamba ndani ya Msikiti anayesoma Qur an na aisome pasi ya kunyanyua sauti yake kiasi kwamba akamkera mwingine. Sasa ikiwa tu kuisoma Qur an, kwa kunyanyua sauti Mtume hapendi vipi sasa ikiwa utanyanyua sauti kwa mizozano na faraka ndani ya Msikiti, kosa kubwa sana hatuna budi Waislamu kuepukana nalo. Aliasa. Akielezea nafasi ya Msikiti katika Uislamu, Shkh. Mohammed, alisema mara tu baada ya Mtume kuka Madina, akitoka katika mji wa Makka, cha kwanza alichokifanya ni kujenga Msikiti. Hii ni kuonyesha kwamba Msikiti ni kituo kikuu cha watu, kwani maswahaba kama Ally, Othama na Abubakar walengwa kiimani Msikitini. Alisema Shkh. Mohammed. Alisema, ukiona Msikiti umeimarishwa ujue watu hao ni wale waliojengeka kiimani, kwani katika surat Tawba Allah anasema kuwa wale wanaoimarisha Miskiti ya Allah ni wale ambao wameamini siku ya mwisho na kusimamisha swala na hao ndio wanaoimarisha Misikiti.

Tufanye mema katika Ramadhani


Na Bakari Mwakangwale WAISLAMU wametakiwa kuupokea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, kwa kuzingatia mafundisho ya Uislamu na miiko ya ibada hiyo ili waweze kuwa wachamungu. Wi t o h u o u m e t o l e wa na Imam wa Masjidi Mtambani, Ustadhi Suleiman, akiwahutubia Waislamu katika hotuba yake ya swala ya Ijumaa wiki iliyopita. Imam Suleima, alisema Waislamu tayari wameukabili Mwezi Mtukufu wa Ramadhani hivyo ni wajibu wao kuzingatia na kufuata misingi ya ibada hiyo ili waweze kufikia lengo la funga. Waislamu mwezi wa Ramadhani umetukabili, mwezi ambao umekusanya

WA I S L A M U w a m e a s w a kujenga Misikiti kwa ajili ya kuimarisha umma wa Kiislamu na si kubomoa, kwani Misikiti kama hiyo isipewe nafasi katika jamii. Hayo yamesemwa na Sheikh Abdulkadir Mohammed, akitoa nasaha zake mbele ya Waislamu katika uzinduzi wa Masjidi Taqwa, Ilala Jini Dar es Salaa, mwishoni mwa wiki iliyopita. Alisema, Misikti ambayo ipo kwa ajili ya kuweka mikakati ya kubomoa jamii, Misikiti hiyo haina nafasi katika jamii, bali msikiti ijengwe kwa ajili ya manufaa kwa umma na jamii kwa ujumla. Misikiti ijengwe kwa ajili ya kuimarisha umma na si kubomoa, kwani hata Mtume alisema, Misikiti hiyo haina nafasi katika jamii. Alisema Sheikh Mohammed. Shkh. Mohammed, alisema Msikiti ni sehemu ya kujenga watu kielimu, kwamba iwe ni kituo cha elimu isiwe ni sehemu ya kiibada tu. Alisema, katika tukio moja

Kongamano Masjid Tungi - Temeke


Baraza Kuu la Wanawake wa Kiislamu Tanzania linawaalika wanawake wote wa Kiislamu katika Kongamano litakalo fanyika Inshaallah Msikiti wa Tungi Temeke Jumamosi Tarehe 13/07/2013 Saa 2:30 hadi saa 7:00 Mchana ,Mada swaumu. Tuzingatie Muda. Ukipata Taarifa hii Mwaambie na mwenzio. Naibu katibu Taifa Bi. Mayasa Sadallah.

kila aina ya kheri ambazo unazozijua na usizo zijua, tuupokee Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa bashasha ili mwisho tuwe ni wenyewe kufutiwa madhambi na kufikia lengo la funga. Alisema Imam Suleiman. Alisema, ukifuatilia katika Qur an, kheri za Mwezi wa Ramadhani, zilizomo kwa siku moja, mbili hata mwezi mzima hutoweza kuzielezea zikaisha, hivyo ni wajibu kwa Waislamu kuhimizana, kukumbushana na kuhamasishana ili kuweza kuzipata kheri hizo. Akisherehesha hadithi ya Mtume (s a w), Imam Suleiman, amesema miongoni mwa anayepata khasara katika Mwezi huu ni yule ambaye inamdiriki Ramadhani, mpaka inamalizika hakufutiwa madhambi yake. Mimi na wewe, je tutakuwa katika kundi hili au tutakuwa ni wenye kushindana katika kheri ili tuweze kuepukana kuwa katika kundi la wenye kupta hasara. Alisema Imam Suleiman. Alisema, Mwezi huu kila ulipokuwa ukimkia Mtume (s a w), alikuwa akiacha shughuli zake zote akifunga kibwebwe kufanya ibada kuliko alivyokuwa akifanya siku za kawaida.

utaona kuwa kile kilichofanyika Pakistan ndio kinatakikana kufanyika Tanzania. Zinasambazwa habari kuwa kuna mtandao wa magaidi wa al Shabab, lakini hakuna maelezo kuwa wapo wapi, ni akina nani na hawakamatwi na kufikishwa m a h a k a m a n i . Tafsiri yake ni kuwa ukishajenga hoja hiyo, siku yoyote panaweza kufanyika shambulio na kumkamata yoyote na kudai kuwa ndio yale makundi ya kigaidi yaliyodaiwa kuwepo nchini. Na hili, hakuna litakapotupeleka ila k we n ye m a c h a f u k o na mauwaji ambayo pengine itakuwa rahisi kuona mwanzo wa k e , l a k i n i h a t m a yake itakuwa ngumu kukiwa. Mwandishi Murtaza Hussain akiandika kutoka Toronto, Canada anatukumbusha akisema kuwa ni wakoloni wa Kibeligiji waliokuwa wakitawala Rwanda waliopandikiza chuki za kikabila kati ya Watutsi na Wahutu, ambapo baadae walipatikana w a p u m b a f u waliozichochea zikazaa mauwaji ya Kimbari mwaka 1994 na kuangamiza takribani roho milioni moja za Wanyarwanda. Katika nchi ambazo ukabila hauna nguvu kama nchi za Kiislamu (Kama Pakistan na Iraq) anasema wanatumia u-Shia na u-Usunni. Ambapo kwa nchi kama Tanzania, watatumia Ukristo na Uislamu. Sasa ni wajibu kwetu sote, tunaposikia b a a d h i ya we n z e t u waka na madai kuwa wamekamata komputa mpakato zenye maneno yenye kuchochea k u a n g a m i z wa wa t u wa dini nyingine, t u w a a m b i e , watuonyeshe na sisi tuyasome maneno hayo na watuthibitishie kuwa hawakuandika wao. Yote hii ni katika

Tu n a a m i n i k u w a Watanzania ni watu na heshma zao, wazalendo wenye kujali utu wa o n a u b i n a d a m u wa o . H a wa t a k u b a l i kukishwa huko. Tumefikisha. Isije kusemwa kuwa hatukusema. Wabillahi Tawq

watu watakaopita mitaani na Misikitini wakitangaza sera za ki-al Shabab. Kuyasema haya ndiyo Jihad na zawadi yetu An nuur kwa nchi hii, kwa Waislamu na Watanzania wote kwa ujumla. Na kama kutakuwa na baya lolote litakalotuka, basi ni kwa ajili ya kuiepusha nchi hii na balaa tunaloliona mbeleni. Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi. Allah anashuhudia kuwa tumefikisha. Na hatukufanya haya kwa nia ya kuleta uchochezi, bali kwa lengo la kuinusuru nchi hii na maafa. Tu m e f a n y a h a y a kuwanusuru waja wa Allah wasitumbukizwe katika m c h e z o wa k u u wa n a au kuuliwa ili kutimiza malengo ya mabeberu kama inavyotokea Syria, Iraq, Afghanistan, Pakistan, Yemen na Somalia. Tu m e y a s e m a h a y a t u k i h o f u , i s i j e k u wa n a s i s i t u k a c h e z e wa kama ilivyochezewa Pakistan, mwisho wa yote wanatukanwa wakiambiwa: You are so cheap we can buy you with a visa, with a visit to the US, even with a dinner we can buy anyone.

kuchukua tahadhari za kuinusuru nchi yetu maana tunajua kuwa kama kuna mtu anataka kuleta balaa la vita ya wenyewe kwa wenyewe, m l a n g o wa k u p i t i a Tanzania utakuwa wa kidini. Ni kwa sababu hii, sisi kama chombo cha habari, tunaona tuna dhima kubwa na deni kubwa kwa nchi hii, kuhakikisha kuwa kama kuna chochote tunachoweza kufanya kuiepusha nchi hii na balaa hili, tunalifanya. Ndio maana tunatoa wito kwa Waislamu na Watanzania wote, kuwa macho na wapiga limbi hawa wa ugaidi pamoja na

AU yasitisha uanachama wa Misri


Tarehe ya Uchaguzi yatangazwa ElBaradei apingwa, ajitoa
Waziri Mkuu wa serikali ya mpito ya nchi hiyo. Mbali na kukataa pendekezo hilo, Al-Baradei amependekeza wadhifa huo uchukuliwe na Ziyad BahaudDin. Aidha kiongozi huyo wa upinzani, ametaka kuchukua wadhifa wa Naibu wa Waziri Mkuu katika masuala ya kisiasa. Wakati hali ikiwa hivyo, Rais wa serikali ya mpito ya Misri Adly Mansour, ametangaza kwamba uchaguzi wa Bunge nchini humo utafanyika mwaka 2014. Rais Mansour ameongeza kuwa, mara baada ya kufanyika uchaguzi wa Bunge, itatangazwa tarehe ya kufanyika uchaguzi wa Rais. Rais wa serikali ya mpito ya Misri ana kipindi cha miezi sita cha kuifanyia m a r e k e b i s h o k a t i b a ya nchi hiyo ambayo hivi sasa imesitishwa. REUTERS Msemaji wa kiongozi wa mpito nchini Misri, Adly Mansour, amearifu kuwa mchakato wa kumpata Waziri Mkuu wa taifa hilo bado unafanyika. Wakati kiongozi huyo akitoa kauli hiyo kumekuwa na tetesi za kutaka kuteuliwa Dk. Mohamed Elbaradei, ambaye amekosolewa vikali kwa kudaiwa kutofaa kushika wadhifa huo. Taarifa za ndani zilimtaja D k . E l B a r a d e i , a m b a ye alikuwa kiongozi wa zamani wa masuala ya usimamizi wa nyuklia katika Umoja wa Mataifa-UN kushika wadhifa huo. Ta a r i f a z a k u t a k i w a kuteuliwa kwake zimekuwa zikikosolewa kwa madai kuwa kiongozi huyo asingefaa kwa chochote. Hata hivyo Dk. Mohamed al Baradei ambaye ni kiongozi wa upinzani nchini humo, amekataa pendekezo la kuwa Wakati huohuo, Msemaji wa Rais wa serikali ya mpito wa Misri amesema kuwa, matukio yaliyojiri jana mjini C a i r o h a ya we z i k u z u i a uundwaji wa serikali mpya. Ahmad al Musalmani, amesema kuwa mapigano yaliyotokea kati ya wafuasi wa Harakati ya Ikhwanul Muslimin na vikosi vya usalama mbele ya makao ya Gadi ya Rais Mashariki mwa Cairo, hayawezi kuzuia juhudi za kuundwa serikali m p ya a u k u t e k e l e z wa mpango uliobuniwa na jeshi la nchi hiyo. Ta k r i b a n w a t u 5 3 wa m e u l i wa we n g i wa o wakiwa ni wafuasi wa chama cha Muslim Brotherhood na kiongozi aliyeondolewa madarakani Mohamed Morsi, nje ya kambi ya Jeshi jijini Cairo mwanzoni mwa wiki. Chama cha Morsi, Muslim Brotherhood, kilichoongoza maandamano dhidi ya Jeshi na Mapinduzi dhidi ya Kiongozi wao, wamelitupia lawama Jeshi na Polisi kwa kupoteza maisha ya watu hasa wafuasi wa Chama chao. Ikhwanul Muslimin imesema kuwa, wafuasi wake wameuawa wakati jeshi la Misri lilipoushambulia umati wa watu waliokuwa wameketi chini nje ya kambi z a o wa k i p i n g a k i t e n d o cha kupinduliwa Rais Muhammad Morsi. Wa t u wa l i o s h u h u d i a wa m e e l e z a k u wa , j e s h i lilitumia silaha za moto kuwatawanya wafuasi wa Muhammad Morsi katika mji wa Nasr, Mashariki mwa Cairo. Jeshi nalo limetupa lawama kwa makundi waliyoyaita ya kigaidi. Nacho chama cha upinzani Freedom and Justice (FJP), kimetoa wito wa k u p i n g a wa l e wo t e wanaojaribu kuiba mapinduzi yao kwa nguvu. Wa f u a s i w a M u s l i m Brotherhood wameapa kuzidi kuendesha maandamano ya amani mpaka kiongozi wao atakaporejeshwa katika nafasi yake. Waandamanaji pia wametaka aachiliwe huru yeye na baadhi ya viongozi wa Ikhwanul Muslimin wanaoshikiliwa na jeshi la nchi hiyo. FJP kimeiomba Jumuia ya K i m a t a i f a k u i n g i l i a kati kuhakikisha mauaji yanakoma nchini humo na kuzuia hali ya mambo kwani inaonekana itakuwa mbaya zaidi kama ilivyo nchini Syria. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amekemea mauaji yaliyotokea nchini Misri na kutoa wito kufanyika uchunguzi ulio huru ili kuwakisha mbele ya v yo m b o v ya S h e r i a waliohusika. Morsi anayedaiwa kushikiliwa na jeshi,

Habari za Kimataifa/Tangazo

SHAABAN 1434, IJUMAA JULAI 12 - 18, 2013

AN-NUUR

Matumaini ya Snowden kupata hifadhi yaongezeka

MILANGO yafunguka kwa Edward Snowden ya kupata hifadhi katika mataifa kadhaa ya Amerika Kusini. Bolivia imekuwa nchi ya tatu kujitolea kumuhifadhi Edward Snowden, huku R a i s wa n c h i h i yo E vo Morales, akisema yupo tayari kumuhifadhi mkimbizi huyo kama akihitaji. Bila sjaka hatua hiyo ya Rais Morales, ambaye ni mpingaji mkubwa wa siasa za mataifa ya kibeberu, inakuja kufuatia ndege yake kukamatwa na kukaguliwa nchini Ufaransda hivi karibuni, ikidaiwa kuwa ilikuwa inasadikiwa kumbeba Bw. Snowden. Hatua hiyo iliwakasirisha sana wananchi wa Bolivia, wakidai Rais wao kadhalilishwa. Hali hiyo iliilazimisha Ufaransa kuomba radhi kwa Bolivia kufuatia tukio hilo. Hatua hiyo ya Bolivia inaongeza matumaini kwa Snowden kwamba huenda akaweza kuondoka Moscow, ambapo amekwama kwa zaidi ya siku 14, kufuatia kutafutwa na Marekani kwa kosa la kuvujisha siri za kasusi za Taifa hilo. Nafasi hiyo inakuja ikiwa ni muda mfupi tu, tangu Rais wa venezuela Nicolas Maduro, kuthibitisha uamuzi wa serikali yake kumpatia hifadhi ya kisiasa mfanyakazi huyo wa zamani wa shirika la kijajusi la CIA, Edward Snowden, anayesakwa baada ya kuvujisha siri za ndani za

Marekani. Maduro ameweka wazi uamuzi huo wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa Venezuela, yaliyofanyika Ijumaa iliyopita. Rais wa Nicaragua Daniel Ortega, naye amesema kuwa nchi yake inaweza kumpa hifadhi salama Bw. Edward snowden akihitaji. Mlolongo wa nafasi za kupata hifadhi kwa jasusi huyo wa zamani, unakuja baada ya kukataliwa na mataifa mengi kati ya 21 ambayo Bw. Snowden aliomba hifadhi juma lililopita. Snowden amekuwa katika Jini Moscow toka alipowasili akitokea Hong Kong kwa takribani majuma mawili yaliyopita. Snowden anayejitahidi kuepuka mkono wa Marekani, alituma maombi ya hifadhi kwa takribani nchi 27, lakini nchi nyingi za Ulaya zimekataa ombi lake huku zile za Amerika Kusini zilizoonyesha nia ya kumpokea. Sakata la Snowden limeendelea kuzua utata katika siku za hivi karibuni, ambapo Marekani imeendelea kuhaha kuhakikisha inamtia nguvuni ili akajibu mashtaka yanayomkabili kufuatia kuvujisha siri za ndani za shirika la kasusi la CIA, kwamba limekuwa l i k i r e k o d i m a wa s i l i a n o mbalimbali yanayofanywa ya ki-electronic.

hajatokea hadharani tangu a l i p o p i n d u l i wa , l a k i n i imeariwa kuwa amewataka wafuasi wake kupigania h a k i ya o k wa k i o n g o z i waliyemchagua katika uchaguzi wa kidemokrasia. Tayari Umoja wa Afrika AU umesitisha uanachama wa Misri katika Umoja huo na kusema, hautambui mapinduzi hayo kwa sababu Morsi alichaguliwa k i d e m o k r a s i a b a a d a ya kuondolewa kwa Rais wa zamani Hosni Mubarak. Wakati Katibu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon, akiwataka viongozi kuhakikisha waandamanaji wanalindwa na kuwa salama, serikali ya Marekani na mataifa makubwa nayo imeingilia kati kwa kuwataka viongozi wa Misri kukomesha ghasia. Naye Rais Vladimir Putin wa Urusi, ameonya juu ya hatari ya machafuko yanayoendelea nchini Misri kuwa yanaweza kuitumbukiza nchi hiyo kwenye mapigano ya wenyewe kwa wenyewe. Rais Putin amesema tayari Syria imetumbukia vya kutosha katika vita vya ndani na kuwa, jambo la kusikitisha ni kuona hatari ya kutumbukia Misri katika mgogoro kama huo. Hata hivyo wachunguzi wa mambo ya siasa wanabainisha kuwa, kuangushwa kwa serikali ya Morsi imekuwa ni faraja kwa mataifa ya Magharibi kwani hawakuwa wakimuunga mkono Morsi na wala hakuwa chaguo lao.

Ahlul Daawa Hajj And Travel Agency


INAPENDA KUWA TAARlFU MAHUJAJI WAKE WOTE NA WAISLAMU KWA JUMLA KUA:IDADI YA MAHUJAJI WAO WA MWAKA HUU 2013 IMEPUNGUZWA KUTOKA MIA TATU MPAKA MIA MOJA NA SABINI TU. KWA HIVYO;(a) WALE WOTE W ALIOJIANDIKISHA W A WAHl KUMALIZA KULIPIA GHARAMA ZAO. (b) W ALIOJIANDIKISHA TU NA HAW AJALIPIA W AJE KULIPIA AU TUT A WAONDOSHA KWENYE ORODHA NA KUW APA NAFASI W ALIOKUW A TAYARI. (c) KUWASILISHA PASSPORT AU KOPI ZA PASSPORT KWA MUDA HUU. (d) PICHA MBILI PASSPORT SIZE KW A AJILI Y A VISA. 2. (a) BEl YETU NI US DOLA 3550 TU. (b) UKIWAHI KULIPIA SA SA NA KUMALIZA TARATlBU ZOTE PUNGUZO NI ASILIMIA SITA KWA HIVYO UT ALIPIA US DOLA 3337 TU NA KABLA Y A TAREHE 25 JULAY 2013. 3. KWA MAWASILIANO ZAIDI FIKA OFISINI KWAO;(a) DAR ES SALAAM MTAA W A DOSI NA MKADINI NYUMBA NAMBA 26 MKABALA NA SHOW ROOM Y A MAGARI TEL 0713 730444 AU 0785 930444 AU 0773 930444. (b) ZANZIBAR MTAA WA RAHA LEO TEL 0777484982 AU 0777413987 AU WASILIANA NA. ( c) MAALIM SElF HUMOUD KIJICHI ZANZIBAR TEL 0777417736. (d) ABDALLA SALEH MAZRUI (HOKO) TEL 0715724444 AU 0773 724444 AU 0784 724444 (e) SHEIKH DAUDI KHAMIS SHEHA PEMBA 0777 679 692 (f) SHEIKH ABUBAKARI MAULANA MARKAZ KIWALANI 0784 453 838 NA BEl NAFUU KULIKO WOTE NA HUDUMA BORA KULIKO WENGI USISAHAU AHLUL DAAWA HAJJ AND TRAVEL AGENCY

TANGAZO

SHAABAN 1434, IJUMAA JULAI 12 - 18, 2013

AN-NUUR

Ramadhan Kareem
Tunawatakia mwezi wa Kheri na Baraka
Katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan matawi yetu yatafanya kazi kuanzia Saa 3 asubuhi hadi Saa 9 alasiri kila siku
Dar es Salaam
Main Branch Golden Jubilee Tower Tel: +255 22 2129014 Fax:+255 22 2129013 Tawi la Tandamti Kariakoo (Mkabala na soko) Tel: +255 22 2185474 Fax: +255 22 2185475 Tawi la Nyerere Jengo la DRTC Tel: +255 22 2863724 Fax: +255 22 2863725

NE W

NE W

Arusha

NE W

Mwanza

Tawi la Lumumba Kariakoo Tel +255 22 2180101 fax +255 22 218410

Tawi la Arusha Jengo la Hugo Plaza Tel: +255 27 254 7496 Fax: +255 27 254 7497

Tawi la Mwanza Barabara ya Kenyatta Tel. +255 282 541 921 Fax: +255 282541922

www.amanabank.co.tz

Makala/Tangazo

SHAABAN 1434, IJUMAA JULAI 12 - 18, 2013

AN-NUUR

Bomu Kanisani Arusha:

Kesi ya Victor imeishia wapi?


Uchunguzi tulioahidiwa umebaini nini? Tuzingatie aliyosema DCI Manumba
AB 651926, mtuhumiwa ametajwa kwa jina la Adili Ally Patel wakati katika ile ya Uingereza jina ni Iqbal Hassan Ally. Habari zaidi za DCI Manumba zinasema kuwa waliwasiliana na Serikali ya Uingereza ikathibitisha kuwa Iqbal Hassan Ally ni raia wa Uingereza na kwamba mtu huyo anatafutwa kwa tuhuma za ugaidi. DCI Manumba aliendelea kudai kuwa mtuhumiwa Iqbal Hassan Ally alikutwa na komputa mpakato (lap top) ambayo ilipochunguzwa ilikutwa na maneno ya kukashifu dini nyingine. Na Omar Msangi Baada ya kushukiwa na kupekuliwa, alikutwa nakomputa mpakato yenye maandishi mengi ya kichochezi dhidi ya dini asizoziabudu. Maneno katika komputa yake yanasisitiza kuteketezwa kwa watu wa dini nyingine (hakuzitaja). Amenukuliwa Kamishna Robert Manumba akidai. DCI Manumba akaongeza kudai kuwa maneno kama hayo ya uchochezi na kutaka kuteketezwa watu wa dini nyingine, yalikutwa pia kwa mwanafunzi a n a y e d a i wa k u s o m a Inaendelea Uk. 8

K AT I K A jumla ya habari kubwa zilizopewa umuhimu mkubwa mwishoni mwa wiki iliyopita ni ile ya kukamatwa mtu mmoja katika mpaka wa Tanzania na Malawi akituhumiwa kwa kosa la ki-Uhamiaji. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa na hati mbili za kusaria, moja ya Tanzania na nyingine ya Uingereza. Katika hati ya Tanzania,

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba.

Kesi ya Victor imeishia wapi?


Inatoka Uk. 7

Makala

SHAABAN 1434, IJUMAA JULAI 12 - 18, 2013

AN-NUUR

Sudan ambaye anadaiwa pia kuwa mshirika wa Iqbal. Katika kutoa tahadhari juu ya kitisho cha ugaidi, t u k i o l a k u k a m a t wa Muingereza huyo, liliunganishwa na mabomu yaliyolipuliwa Arusha na DCI Manumba akaenda mbali kwa kuunganisha na kitisho cha Al Shabab na Boko Haram. Alisema, habari za kiintelijensia zinaonyesha k u w a Ta n z a n i a s i o salama kutokana na k u we p o v i k u n d i v ya kigaidi vinavyojificha chini ya mwavuli wa dini na kwamba hivi sasa kuna taarifa za kuwepo kikundi cha kigaidi cha al Shabab, ambacho kimekuwa kikizunguka Afrika Mashariki, kutafuta mwanya wa udhaifu na kushambulia. (HABARILEO) Kutokana na taarifa hizi za DCI Robert Manumba, Shirika la Utangazaji BBC nalo liliremba habari hizo kwa mtindo wake na kuziung anisha na mabomu ya Arusha. Authorities in Tanzania are concerned at the growth of an Islamist movement accused of links to Somalias al-Shabab. Zilisema taarifa kama zilivyopatikana katika mtandao zikisherehesha habari za kukamatwa Ally na kuzihusisha na mabomu ya Arusha na kuhitimisha kwa madai kuwa mwisho wa siku ni kitisho cha Islamists (Waislamu) walio na uhusiano na al Shabab. Kwa upande mwingine baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini, Jumamosi viliibuka na habari vikidai kuwa gaidi limekamatwa Tanzania. Gaidi mbaroni, ndivyo lilivyoripoti gazeti la NIPASHE huku l i k i k o l e z a n a k i c h wa kidogo kinachosema, Mtanzania adakwa akidaiwa kumsaidia. Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa ya gazeti la HabariLeo la Jumamosi Julai 6, 2013 ukurasa wa 31 ambao kwa kawaida ni ukurasa wa michezo, imeelezwa kuwa Muingereza huyo amepandishwa kizimbani k a t i k a M a h a k a m a ya Hakimu Mkazi, Kisutu,

akiunganishwa katika kesi ya wizi wa hati 26 za kusaria. Iqbal anaunganishwa katika kesi hiyo kwa sababu hati aliyokuwa

JULAI 7, 2005 yalifanyika mashambulizi yaliyodaiwa ya kigadi katika jiji la London. Mashambulizi hayo yaliyotokea katika vituo vya gari moshi, tena katika muda uliokuwa na watu wengi, yalidaiwa kufanywa na Waislamu watatu raia wa Uingereza wenye asili ya Pakistan na mmoja mwenye asili ya Jamaica aliyefanya kusilimu. Tu k i o h i l o l i l i p i g i wa zumari sana na likafanya ule mshikamano wa Marekani na Uingereza katika vita dhidi ya ugaidi kuimarika zaidi. Viongozi wa Uingereza wa k a t a m b a n a k u p a t a kupumua wakijenga hoja kuwa wana kila sababu ya kupigana huko Iraq na Afghanistan ili kuzuiya magaidi kuingia London na Ulaya kwa ujumla. Unapozungumzia ugaidi

Mabomu London 7/7


Uingereza, katika ulimwengu huu wa leo wa crusade iliyotangazwa na Geoge W Bush baada ya Septemba 11, 2001; London Bombing ndio tukio pekee kubwa linalopigiwa ngoma sana. Hata hivyo, hata kabla ya sherehe ya vyombo vya habari vyenye mrengo wa kuchangamkia habari za kuwabambika Waislamu ugaidi haijamalizika, watu wenye akili zao huru, walianza kuhoji na kuonyesha mashimo yanayozua wasiwasi wa kuwepo usanii katika tukio hilo. Wachambuzi mbalimbali wanajenga hoja kuwa shambulio hilo lilikuwa la kupangwa ili kuwaunganisha Waingereza katika kuunga mkono Serikali yao katika vita Iraq. Katika kujenga hoja zao wanasema kuwa shambulio hilo lilitanguliwa

n a yo i n a d a i wa k u wa miongoni mwa hati zilizoibwa kutoka Idara ya Uhamiaji jini Dar es Salaam. Wakati hayo yakijiri,

bado Watanzania wapo kizani juu ya lile bomu lililolipuliwa katika Kanisa Arusha na kuuwa watu watatu. Katika tukio hilo lililotokea Mei 5, 2013

na kuvuja habari kutoka O f i s i ya Wa z i r i M k u u , Uingereza, kwamba George Bush, aliliongopea Bunge la Congress katika madai yake kuwa Saddam Hussein ana silaha za maangamizi ili kupata kibali cha kuvamia Iraq. N i b a a d a ya k u v u j a habari hizo, wananchi wa Uingereza walizidi kupaza sauti wakitaka wanajeshi wao warejeshwe nyumbani. Blair alikuwa katika hali ngumu na Bush naye alikuwa katika wasiwasi mkubwa wa kumkosa mshirika wake mkuu kule Iraq na Afghanistan. Ni katika mazingira hayo, likatokea shambulio la 7/7 London na kwa muda likabadili hali ya hewa. Waingereza wakawa na hasira dhidi ya Waislamu na

K U M E K U WA n a k a u l i nyingi sana kuhusu al Shabab, lakini nyingi zikitoa taswira kuwa hiki ni kikundi cha kigaidi ambacho kimeanzishwa rasmi kwa lengo la kufanya ugaidi Pembe ya Afrika na Afrika Mashariki, na hata kimataifa. Al Shabab pamoja na al Qaida, imekuwa misamiati inayotumiwa kuwakilisha unaodaiwa kuwa Ugaidi. Ukisikia maneno Islamists au Waislamu wenye siasa/ msimamo mkali, basi hao mara nyingi utasikia ikidaiwa kuwa wanahusiana na ama al Shabab au al Qaidah. Taarifa ya Mkurugeni wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini, Robert Manumba kwamba Tanzania kuna kitisho cha magaidi wa al Shabab wanaovinjari kutafuta shabaha za kupiga, ni ushahidi kuwa hapa nchini, rasmi inachukuliwa kuwa al Shabab ni kundi la kigaidi lililosambaa Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika kufanya ugaidi na kwa namna nyingine kwamba wana washirika wao nchini ambao ndio hao wanaodaiwa kubeba komputa mpakato zinazohimiza kuangamizwa

Nani al Shabab
watu wa dini nyingine. Katika hali kama hii kuna kila sababu kwa Waislamu kwanza kujua hali hii, pili kujua kwa uhakika nani al Shabab na tatu kuchukua tahadhari, wase wakajikuta wakitumiwa bila kujua na kujiangamiza kwa mikono yao wenyewe. Nani al Shabab, tujiulize kama anavyojiuliza Christopher Anzalone anapouliza: Who are Somalias al-Shabab? (Wednesday, August 3, 2011). Christopher Anzalone ambaye ni mtafiti katika kitengo cha Islamic Studies, Chuo Kikuu cha McGill, amejiuliza swali hili kufuatia kauli nyingi zinazotolewa kuwahusisha al Shabab na ugaidi pamoja na madai kuwa wao ni ndugu moja na al Qaida. Baada ya utafiti wake Christopher anasema kuwa kuna uwongo mwingi unasambazwa kuhusu al Shabab ikilinganishwa na ukweli juu ya kundi hilo. Ukweli unaoepukwa na wengi wanaopiga propaganda ya al Shabab ni wa namna mbili: Moja ni kuwa al Shabab ni taasisi ndani ya Somalia ambayo inapigania Somalia kutawaliwa na Wasomali

Inaendelea Uk. 9

wenyewe na muhimu zaidi i t a wa l i we n a S h e r i a z a Kiislamu (Shariah). Al Shabab hawataki kuona serikali kama iliyopo hivi sasa wanayodai kuwa ni serikali kibaraka inayowakilisha masilahi ya mabeberu. Na kwa hiyo hawataki kuona majeshi ya nje yakiingia Somalia kusaidia kuiweka na kuilinda serikali hiyo wanayodai kuwa ni kibaraka wa madui wa Somalia. Ukweli wa pili usiozungumzwa ni kuwa waliopandikiza machafuko yaliyopo hivi sasa Somalia pamoja na kuibuka al Shabab, ni mabeberu wakiitumia Ethiopia. Ni maarufu kwa walimwengu wote kuwa baada ya vurugu, ujambazi, m a p i g a n o , m a u wa j i n a kukosekana serikali kwa zaidi ya miaka 15, ambapo juhudi za kikanda na kimataifa zilifeli kabisa kuleta amani; Wasomali wenyewe walikia mahali wakapata ufumbuzi. Kabla ya kurejea amani kwa muda, Somalia ilikuwa imeshikiliwa na wababe wa kivita (warlords) jumuiya ya kimataifa ikiwa imeshindwa kabisa kuleta amani. I l i k u wa n i b a a d a ya Jumiya ya Kimataifa na jeshi

Victor Ambrose Calist alikamatwa akituhumiwa kurusha bomu kwenye Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti, Jimbo Kuu la Arusha, na alifikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na kusomewa mashitaka 21 ya kuua na kujaribu kuua. Mbele ya Hakimu Mkazi, Devotha Kamuzora, mtuhumiwa huyo, Victor Ambrose (20), dereva wa Bodaboda na mkazi wa eneo la Kwa Mromboo, Arusha alisomewa mashitaka hayo yakiwamo matatu ya mauaji ya watu watatu waliofariki katika tukio hilo lililotokea Mei 5, mwaka huu. Mawakili wa Serikali, Zachariah Elisaria na Haruna Matagane walidai kuwa Calist pia anatuhumiwa kwa makosa 18 ya kujaribu kuua. Kuacha taarifa hizo za awali za kufikishwa mtuhumiwa mahakamani, bila kuathiri mwenendo wa kesi mahakamani, bado hakujasikika taarifa zozote za uchunguzi kama Serikali ilivyokuwa imeahidi kuwa itafanya uchunguzi na kutoa taarifa kamili juu ya tukio hilo la kigaidi. Mtuhumiwa ni nani, a m e f a n ya p e k e ya k e au kuna mtandao wa ndani pekee au ndani na nje ya nchi. Mtandao u n a u k u b wa g a n i n a unawahusisha watu gani. Je, nini malengo, siasa za ndani au za kimataifa au kutaka tu kuleta vurugu. Je, bomu hilo linahusiana kwa namna yoyote na t a a r i f a z i n a z o t o l e wa kila uchao kuwa kuna chuki za kidini na hizi za sasa za DCI Manumba kuwa kuna komputa mpakato zenye maneno yenye kuhamasisha kuangamizwa watu wa dini za watu wengine. H a yo n i b a a d h i ya m a m b o ya l i yo t a k i wa kufanyiwa uchunguzi na kufahamika. Lakini mpaka leo kimyaa!! Na hata huko mahakamani, haulikani nini kinaendelea maana inaonekana jambo lenyewe limekuwa siri kubwa toka siku ya mwanzo mtuhumiwa alipokishwa mahakamani. Baadhi ya taarifa zinadai kuwa Inaendelea Uk. 9

Inaendelea Uk. 9

9
Inatoka Uk. 8 mtuhumiwa alishapewa dhamana. Pe n g i n e b a d a l a ya kutegemea taarifa za kupewa na Uingereza na washirika wao na kisha kuibuka na taarifa za kuwatisha Watanzania juu ya al Shabab na komputa mpakato zenye habari za kutaka watu wa dini nyingine kushambuliwa na kuangamizwa, tungezingatia kwanza taarifa zilizotokana na uchunguzi wetu wenyewe katika kukamatwa mtuhumiwa Victor Calist Ambrose na uchunguzi wa lile bomu lililolipuka katika mkuano wa CHADEMA Arusha na kuuwa watu watatu. N a n i Vi c t o r, b o m u analotuhumiwa kurusha kalipata wapi, kapewa na nani, nani wapo nyuma yake na mambo kama hayo. Au kama si yeye aliyelirusha kutokana na ushahidi utakaowasilishwa mahakamani, lakini ukweli unabaki kuwa kuna bomu lilirushwa Kanisani likauwa watu. Nani alihusika? Kwanini? Kwa malengo gani? Kama tuna nia ya kujua ukweli juu ya kitisho cha ugaidi Tanzania, na hakuna agenda ya siri, uchunguza juu ya bomu la Arusha, na tukiufanya sisi wenyewe bila kutegemea akili na maelekezo ya watu wengine, ingetusaidia sana kuliko hizi habari za kuambiwa na Uingereza/ FBI. Na sababu yake ni moja tu lakini ya msingi na yenye kujitosheleza: Hawa tunaodhani kuwa wana utaalamu hata tukawaita kutusaidia, wa s h a p o t e z a s i f a ya kuaminika, hasa katika matukio kama haya yanayodaiwa kuwa ya kigaidi. Mpaka hivi sasa lile tukio la London bombing limekuwa mwiba kwa serikali ya Uingereza kutokana na maswali na ushahidi unaoibuka kujenga wasiwasi kuwa huenda tukio lile lilikuwa la kupangwa na serikali yenyewe. Terror Expert: London Bomber Was Working For MI5 Khan used as informant for security services. Whats Behind the London Aacks?. Report: Israel Was Warned Ahead of First Blast. 7/7 links with British intelligence agencies dont end with Khan. Terror expert John Loftus told Fox News. Dayside show that alleged London bombing mastermind Haroon Rashid Aswat was an MI6 intelligence asset that British security helped protect and hide before the bombings.

Makala
The bombing of the London Underground was a false-ag operation designed to keep the West mired in war. Dont believe otherwise. H i v i n i b a a d h i ya vichwa vya habari na baadhi ya sehemu za makala na uchambuzi wa wataalamu mbalimbali

SHAABAN 1434, IJUMAA JULAI 12 - 18, 2013


wamuunge mkono Waziri Mkuu Tony Blair katika kuendelea kuweka wanajeshi wa Uingereza kule Iraq na Afghanistan. Wakati huo wananchi wa Uingereza walikuwa wameanza kuchachamaa kupinga vita Iraq. Kwa mujibu wa wachambuzi hao, kipigo cha kweli cha kigaidi, na ukawahusisha watuhumiwa wa Kiarabu/ Wahindi, (Waislamu), kingeweza kuwafanya Waingereza kuona mantiki na umuhimu wa wanajeshi wao kupigana Iraq. Wiki iliyopita niliandika makala nikisema kuwa kutokana na hali inavyokwenda hivi sasa juu ya kinachoitwa vita dhidi ya ugaidi, Waislamu wanatakiwa kuchukua tahadhari kubwa juu ya watu wanaojitokeza na kuweka darsa za siri na kuanza kujadili harakati za al Shabab au vikundi vyovyote ambavyo hivi sasa vinatumiwa na Marekani kama kisingizio cha kuwabamiza Waislamu. Na hii ni kwa sababu kumekuwa kukifanyika mchezo wa kupandikiza makachero misikitini na katika taasisi za Kiislamu wakijifanya mujahidina, kisha kupandikiza silaha na mashambulizi (false terror attacks) ambapo vijana wa Kiislamu hukamatwa na kupachikwa kesi za ugaidi. Baada ya makala ile mtu mmoja alinipigia simu akiongea huku kakasirika sana. Yeye yote yaliyosemwa katika makala ile hakuyaona wala kuzingatia nini yalikuwa maudhui ya makala ile. Yeye aliloona ni pale tu niliposema Waislamu waepuke darsa za siri. Alitumia muda mrefu sana akidhani ananipa darsa juu ya Darul Arqam. Kilichonisikitisha ni ule unyu wa uelewa wa mambo na kutokufahamu watu wanaishi katika mazingira gani, kuelewa MUKTADHA wa sasa na wapite wapi ili wasalimike na wafanye Dawah yenye manufaa kama inavyodhihiri katika Sira ya Mtume (s.a.w). B o m u l i m e l i p u l i wa Kanisani, Arusha. Limeuwa na kujeruhi watu wasio na hatia. Taarifa ya S e r i k a l i i m e s e m a kuwa ni shambulio la kigaidi. Vyombo vya Dola vimetoa kauli kali lakini za matumaini kwa wananchi, vikiahidi kuwa uchunguzi Inaendelea Uk. 10

AN-NUUR

Kesi ya Victor imeishia wapi?

Mabomu London 7/7


Inatoka Uk. 8
ya Fox News, ikisema kuwa wakati vyombo vya dola vya Uingereza vikisema kuwa vinahangaika kumtafuta mtuhumiwa namba moja wa ulipuaji bomu London, Haroon Rashid Aswat, kwa upande mwingine vyombo hivyo vilikuwa vikimlinda na kumhifadhi mtuhumiwa huyo anayedaiwa kuwa ni mtumishi wa Shirika la kasusi la Uingereza MI-6. Katika makala na u c h a m b u z i wa k e , K u r t Nimmo, ananukuu pia gazeti la The Times likisema kuwa Aswat alitumiwa kufanya kazi na Osama bin Laden katika kambi ya mafunzo iliyokuwa imeanzishwa na CIA-ISI, kama kituo cha mafunzo cha al Qaida (al-Qaida training camp, Afghanistan). Gazeti hilo likasema kuwa limepata nyaraka za FBI zikionyesha kuwa Haroon Rashid Aswat, alipelekwa M a r e k a n i m wa k a 1 9 9 9 ambapo alipewa mafunzo ya matumizi ya silaha na kuuwa kwa kutumia sumu. Uchambuzi wa mwandishi Kurt Nimmo akitumia

wakihoji na kutoa hoja zao madhubuti kuonyesha kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba tukio linalodaiwa la kigaidi lililotokea London Julai 7, 2005 ni la kupangwa na kwamba lengo kubwa ilikuwa ni kuwaunganisha wananchi wa Uingereza na Ulaya kwa ujumla

Waarabu. Blair akapumua kidogo. They are trying to use the slaughter of innocent people to cow us, to frighten us out of doing the things that we want to do. They should not and they must not succeed, Tony Blair. The war on terror goes on.Bush Walinukuliwa viongozi hao na vyombo vya habari wakionyesha walivyofaidika na tukio hilo la 7/7. Baadhi ya taarifa zinafahamisha kuwa Israel ilikuwa inajua juu ya kutokea kwa shambulio hilo siku moja kabla na kwamba Waziri wake wa Fedha Binyamin Netanyahu, ambaye alikuwa London, alibaki hotelini kwake na hakutoka kabisa kuendelea na program zake za siku hiyo. Katika makala yake Bombing Mastermind A s w a t Wo r k s f o r M I 6 (August 2 2005), Kurt Nimmo, ananukuu habari

nyaraka mbalimbali anasema al Qaida ni taasisi bandia ya kigaidi (a fake terrorist front organization) iliyobuniwa na mashirika ya kasusi ya CIA, ISI na MI-6. Na kwamba lengo ni kutumia taasisi hiyo kupandikiza ugaidi, mauwaji, vurugu na ghasia ili kuupiga vita Uislamu na kuzuiya kabisa kupatikana kwa umoja miongoni mwa mataifa ya Kiislamu. Kama ambavyo imeandikwa na Paul Joseph Watson akinukuu taarifa ya gazeti la Guardian, Usamah bin Laden mwenyewe alikuwa akipewa fedha kutoka MI6 n a k wa m b a p a m o j a n a kuwa Abu Qatada anatajwa kuwa mmoja wa viongozi wakubwa wa al Qaida, lakini aliwahi kuhifadhiwa na MI-6 kama ilivyoripotiwa na BBC mwaka 2002. Ni kutokana na taarifa kama hizo, mwandishi Grin Tarpley, anasema kuwa: There is every reason to believe that London is one of the main recruiting grounds

Nani al Shabab
Inatoka Uk. 8
itakayogeuza Somalia mahali pa kuzalisha magaidi, Serikali ya Marekani ilianza kuwapa silaha wababe wa kivita waliokuwa wameshindwa na Umoja wa Mahkama za Kiislamu (ICU). Mwaka 2006 aliyekuwa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wakati huo Sean McCormack, alidai kuwa kamwe Marekani haitakubali kuona Somalia ikigeuzwa kuwa kiwanda cha kuzalisha magaidi ikiwa ni kama namna ya kujibu lawama zilizokuwa zikitolewa ni kwa nini Marekani inaunga mkono wababe wa kivita dhidi ya Serikali ya UIC iliyofanikiwa kuleta amani Somalia. I l i k u wa k a m a k i i n i macho na usanii wa kisiasa kwa propaganda za kimataifa, wababe wa kivita wanaosaidiwa na Marekani wakatakiwa kuanzisha kitu kinachitwa: Alliance for the Restoration of Peace and Counter-Terrorism (ARPCT) ili ionekane kuwa ni watoto wazuri wanaopambana na

Inaendelea Uk. 10

la kulinda amani kutoka Marekani kuondoka Somalia katika miaka ya mwanzo ya 1990s, na kuiacha nchi m i k o n o n i m wa wa b a b e wa kivita, hali ilizidi kuwa mbaya. Kila koo ikiwa na wa n a m g a m b o wa k e n a mahakama yake. Harakati za kupata ufumbuzi wa ndani zilianza zikiwaunganisha vijana na wafanyabiashara waliokuwa wamechoshwa na vitendo vya kiharamia. Harakati hizo zikashika kasi miaka ya 2003 na 2004 ambapo vijana waliunganisha koo wakipigania kusimamisha Sheria za Kiislam. Kwa muda mfupi kabisa wakafanikiwa kuvunja mitandao ya kambazi na kiharamia nchi ikawa na amani. Kutokea hapo ndio wakapata kuungwa sana mkono na wananchi mpaka wakafanikiwa kuunda serikali. Hata hivyo, hali hiyo haikuifurahisha Marekani. Ikitumia kisingizio kuwa ICU itakuwa serikali ya kigaidi

ugaidi. Hata hivyo katika harakati zao wakawa wanashambulia nyumba za Maimamu wa misikiti na wale wanaowakamata wakawa wanawakabidhi kwa Wamarekani. Ilikuwa ni katika kipindi hicho, Februari 2006, Umoja wa Mahakama za Kiislamu (ICU) nao wakatangaza Jihad dhidi ya ARPCT. Ilichukua muda mfupi sana ARPCT kushindwa. Kutokana na matokeo ya kazi iliyofanywa na ICU, i l i k u wa s i o r a h i s i t e n a k u wa t u m i a Wa s o m a l i a kupambana na ICU, ndio wakatumiwa Ethiopia kuvamia nchi hiyo. Serikali ya Umoja wa Mahakama ya Kiislamu ikaondolewa madarakani na baadae Marekani ikatangaza kuwa al Shabab ni kundi la kigaidi. Kilichotokea nini? Vana waliokuwa ndani ya serikali ya Islamic Courts Union (ICU), wakashika silaha kupambana na serikali iliyowekwa madarakani pamoja na majeshi ya nje yaliyoko Somalia kulinda s e r i k a l i h i y o . N a k wa

Inaendelea Uk. 10

10
Inatoka Uk. 9 wa kina utafanyika i l i u k we l i u j u l i k a n e . Amekamatwa Victor Calist Ambrose kwa kudaiwa kuonekana akirusha bomu hilo. Hakuna hata taarifa moja, iwe ya Polisi au ya vyombo vya habari iliyosema: Gaidi lililorusha bomu Kanisani lakamatwa. Kama ni kutajwa Victor, alitajwa kama mtuhumiwa na hata alipofikishwa m a h a k a m a n i , ameshitakiwa kwa mauwaji. Ila kwa kukamatwa mtuhumiwa wa kughushi pasi ya kusafiria, Iqbal Hassan Ally, tunaambiwa Gaidi mbaroni. Halafu anaunganishwa na mabomu Arusha huku tukiambiwa kuwa habari za ki-intelensia zinaonyesha kuwa magaidi wa al Shabab wapo mitaani wakitafiti sehemu za kushambulia! Nilichosema katika makala ile na ambacho nazidi kusisitiza hapa ni kuwa kwa muda sasa kumekuwa na jitihada za kupandikiza kitisho cha ugaidi wa al Qaida na al Shabab. Na yote hii, japo inaonekana katika sura yake ya nje ni kuwatafutia s a b a b u Wa i s l a m u n a kuwabamiza. Lakini itatuathiri Watanzania wote kama ambavyo mabomu ya ndege zisizo na rubani (drone) yasivyochagua mtu wa kuuwa kule Pakistan, Yemen na Somalia. Tu j u e n j a m a z a kupandikiza kitisho cha u g a i d i k i k i f a n i k i wa , t u t a k u wa n a k i b a r u a kingine cha kukidumisha ili wenye agenda yao wazidi kupata sababu ya kuendeleza malengo yao. Kila uchao maguruneti na mabomu yatakuwa yakichukua ushuru wa roho za Watanzania wasio na hatia. Je, haya ndiyo wanayoyalilia wale wanaoshabikia kuwepo u g a i d i Ta n z a n i a k wa vichwa vyao vya habari, Gaidi lakamatwa Tanzania? Mahmoud, kijana wa Kisomali anatumikia kifungo Marekani baada ya kushitakiwa kwa kesi ya ugaidi. Lakini kama nilivyoeleza katika makala iliyopita, ugaidi ule ulikuwa mchezo wa kuigiza uliofanywa na watu wanaotumiwa na FBI wakaja misikitini na kuanzisha darsa za jihad kisha kuwaahidi vijana kuwapeleka katika kambi

Makala

SHAABAN 1434, IJUMAA JULAI 12 - 18, 2013


kikundi cha kigaidi cha al Shabab, ambacho kimekuwa kikizunguka Afrika Mashariki kutafuta mwanya wa udhaifu na kushambulia.

AN-NUUR

Kesi ya Victor imeishia wapi?


za siri na kuwapa silaha. Darsa za namna hii n a m f a n o wa k e n d i o nilizosema tujihadhari nazo ise ikawa ndio yale yale ya kutaka mambo

Mabomu London 7/7


for patsies, dupes, fanatics, double agents, and other roustabouts of the terrorist scene. (9/11: Synthetic Terror, p. 156). Akimaanisha kuwa kuna kila sababu ya kuamini kuwa Uingereza imekuwa moja ya kambi kubwa ya kutoa mafunzo kwa magaidi bandia, ambao baadae hutumika kupandikiza kitisho cha ugaidi (false terror aacks) sehemu mbalimbali duniani. Na tukumbuke kuwa kwa hapa Tanzania wanatuambia kuwa: Authorities in Tanzania are concerned at the growth of an Islamist movement accused of links to Somalias al-Shabab. Kwa sababu hii, nilisema katika makala yangu iliyopita kuwa Waislamu tuwe makini sana na watu wanaopita Misikitini au mitaani na agenda za kuanzisha darsa za siri za kuhamasisha Jihad, kwani wanaweza kuwa ni akina Haroon Rashid Aswat na Abu Qarada. Na ieleweke wazi hapa kuwa hoja sio kujadili dhana ya Jihad kama ilivyokuja katika Uislamu, bali namna maadui wa Uislamu wanavyowatumia baadhi ya watu wenye majina ya

ya k u t h i b i t i s h a ya l e ya l i yo s e m wa n a D C I Robert Manumba kwamba zipo taarifa za kuwapo

Inatoka Uk. 9

Nani al Shabab
Inatoka Uk.9
na vibaraka wao. Kuhusu madai kuwa AlShabab ina uhusiano na AlQaeda, watati mbalimbali wanasema kuwa, al Shabab sio al Qaida, bali kama ni kuhusiana ni kutokana na ukweli kuwa baadhi ya viongozi wake walikuwa wapenzi wa kauli na wito wa Usama, ila ukweli unabaki kuwa al Shabab ni taasisi ya Somalia yenye malengo ya kuiokomboa Somalia kwa mtizamo wao. Wanasema pia kuwa hata kama kuna wapiganaji wa nje, basi ni wapiganaji walioingia kwa kuona wanataka kusaidiana na al Shabab katika kusimamisha Shariah. Maelezo zaidi yanasema kuwa hata pale ilipodaiwa kuwa al Shabab walishambulia nje ya Somalia kama ilivyodaiwa kuwa walifanya Kampala (kama ni kweli walipiga wao) 2010, basi itakuwa walifanya vile kwa kupata mafanikio ya ndani, kwa maana ya kuishinikiza Uganda itoe jeshi lake Somalia. Mtafiti Christopher Anzalone akihitimisha uchambuzi wake anasema kuwa pamoja na kuwa hivi sasa al Shabab wanakabiliwa na changamoto nyingi, lakini bado wanashikilia sehemu

Kiislamu au hata baadhi ya wanaharakati wa Kiislamu, kuuangamiza Uislamu na Waislamu. Jana gazeti la RAI, katika ukurasa wake wa mbele lilichapisha habari iliyokuwa na kichwa cha habari: Siri nzito Arusha. Kisha kufuatiwa na vichwa vidogo vinavyosema: Mamia ya vana wapelekwa Somalia, Darfur, Watajwa kupewa mafunzo ya kigaidi. Wakati Ji la Arusha likiwa bado na kumbukumbu ya milipuko miwili ya mabomu, imebainika kuwa zaidi ya vijana 200 wapo nchini Somalia na jimboni Darfur, Sudan, kwa ajili ya kupewa mafunzo ya kigaidi. Limesema gazeti hilo katika ufunguzi wa habari hiyo na kuongeza likisema kuwa: Chanzo cha habari kutoka katika duru za usalama mkoani Arusha kimesema kuwa, vijana wanaodaiwa kwenda Somalia kwenye kambi za kundi (la) AlShabab na Darfur ni wenye umri kuanzia miaka 15 na kuendelea. Lililo la uhakika ni kuwa, hakuna uwezekano wakatoka vijana 200 hapa

na kwenda kusomea ugaidi Somalia na Darfur, bila ya vyombo vya dola kujua. Kwa hiyo kama kungekuwepo na vijana wanaokwenda Somalia na Darfur kwa ajili ya kujifunza ugaidi, vyombo vya usalama vingekwisha wakamata wahusika k u a n z i a wa l i o p e k e k wa m p a k a wa n a o wa r u b u n i na kuwapeleka. Na kama vinajua, halafu havija wakamata mpaka RAI inaripoti, ni kwamba hao ni watu wao wanaowaandaa kwa kazi maalum. Maana kama habari hizi ni kwa mujibu wa duru za usalama, kama gazeti lilivyodai, ni kuwa Idara ya Usalama inajua. Sasa swali ni je, kwa nini haachukua hatua na badala yake ikaona ivujishe taarifa kwa gazeti? Ta a r i f a k a m a h i z i zinachoeleza bila kusema ni kuwa kuna uwezekano wa vijana kuchukuliwa na kupelekwa katika kambi zinazodaiwa kuwa ni za al Shabab, kisha baada ya kukusanya ushahidi na vielelezo, ndio wahusika wakamatwe na kutoa vielelezo hivyo kuwa kweli k u n a wa t u wa n a s o m e a ugaidi. Lakini ukweli ukiwa

kuamini kuwa wanapigana kwa niaba na kwa masilahi ya Wasomali, al Shabab wamekuwa wakifanya juhudi kuwahusisha viongozi wa koo mbalimbali na kila kada katika jamii. Kwa mujibu wa tafiti za waandishi mbalimbali na wasomi ambao wametati na kuandika juu ya al Shabab, kila ambapo al Shabab wa m e f a n i k i wa k u we k a uongozi wao, huweka gavana (wali) kama mkuu wa wilaya, mahakama (Sharia court), ofisi ya Zakat na idara ya ulinzi na polisi. Kunakuwa pia na idara za huduma kwa jamii na uchumi zikihusika na ujenzi na ukarabati wa barabara na madaraja, shule, hospitali na kilimo. Katika kipindi cha njaa miaka ya 2009 na 2010 al Shabab walifanya kazi kubwa kukusanya chakula, sadaka na Zaka kutoka kwa matajiri na kuwasaidia wananchi w e n y e n j a a . Wa l i p i g a marufuku misaada ya Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) kuingia Somalia wakisema kuwa WFD walikuwa wakisambaza chakula kilichopita wakati wa kutumiwa (expired) na pia kutumia misaada hiyo kwa masilahi ya mabeberu

kubwa ya nchi ya Somalia na hakuna dalili kwamba watatoweka kwa siku za karibuni. Anasema, moja ya changamoto ni kutengwa na jumuiya ya kimataifa, kukosa msaada wa maana kutoka kwa jumuiya hiyo na kuingia kijeshi kwa nchi za Afrika Mashariki. Hata hivyo anasema kuwa udhaifu ndani ya serikali (TFG), unaotokana na rushwa, usadi, ugomvi wa wenyewe kwa wenyewe na kukosa uoni unaotoa uongozi na matumaini kwa Wasomalia, bado al Shabab wataendelea kupata uhalali wa kuwepo na kutegemewa na Wasomali wengi. Propaganda kuwa ni magaidi na kwamba wanatawala kwa sheria kali za Kiislamu, inashindwa kufanya kazi katika maeneo wanayotawala na ndani ya Somalia kwa ujumla, kwa sababu haionekani nafuu yoyote kutoka kwa TFG. Bali kudumu kwa TFG ni kutokana na msuli wa keshi wa majeshi ya Kenya, Uganda, Ethiopia na Burundi. (Makala hii imeandikwa kwa kutumia utafiti wa mtati Christopher Anzalone (Institute of Islamic Studies at McGill University), makala za wasomi mbalimbali na taarifa za Aljazeera)

kuwa vana hao wamefanya kupandikizwa na pengine kwa kuzugwa wakiaminishwa kuwa wanapekewa kupigana Jihad. Kwa chambo hiki wakatokea watu watakaojiona kuwa wameiva tayari kwa Jihad wakanaswa. Na hawa ndio baadhi ya waandishi wa kimataifa wanawaita kuwa ni Wapumbavu wenye kudanganyika kwa wepesi (gullible idiots). Kama wapo watu walioiva barabara, tunataka kuwaona wakija na miradi ya kuwa na hospitali kila mkoa na kila wilaya, vyuo vikuu, televisheni na magazeti ya kila siku, miradi ya kilimo na uchumi ili kuwatoa Waislamu na Watanzania kwa ujumla katika njaa na umasikini. Tu n a t a k a k u w a o n a wa k i e l e k e z a J i h a d ya o kukabiliana na ujinga wa baadhi ya watu wanaokataza m a b i n t i n a v i j a n a wa o kusomea udakitari na utaalamu mwingine, lakini wenyewe wanapeleka wake zao kwa John wakatibiwe magonjwa ya wanawake huku wenyewe wakikaa nje kwenye benchi! La kusisitiza hapa kwa Watanzania wote ni k u wa k a m a t u t a k u b a l i k u p a n d i k i z i wa k i t i s h o cha ugaidi, tutaumia sote. Kwanza ili kitisho hicho kikubalike, itabidi kiwe cha kweli. Watu wauliwe na mali kuharibiwa. Lakini baada ya hapo, itabidi pia kiendelezwe. Kila baada ya muda tutakuwa tukikumbana na mashambulizi ya maguruneti na mabomu kudumisha kitisho kwa manufaa ya wenye malengo yao. Kwa wale wanaoshabikia taarifa za gaidi adakwa, inapokuwa mtuhumiwa ni Ally, lakini wakigwaya anapokuwa ni Victor, wajue k u wa h i l i l i n a l o t a k i wa likitimia, hata wao hawatasalimika. K ul e Pak ist an , ja p o inadaiwa kuwa walengwa ni magaidi, lakini makombora kutoka Drone, yameuwa maelfu ya wanawake, wazee, wanafunzi wa shule na watoto wasio na hatia wakati waliodaiwa kuwa wanalengwa idadi yao hata 20 haiki. Kombora la drone halichagui nyumba wala roho ya kuangamiza. Na maadhali ugaidi unaoliliwa kupandikizwa ni wa kidini, hapana shaka tutaumia sote Waislamu na Wakristo.

Mafunzo kutoka mapinduzi ya Misri


Na Said Rajab MPAKA alipopinduliwa Rais Morsi wa Misri wiki iliyopita, watu wengi waliounga mkono njia iliyotumiwa na Ikhwan Muslimin kuingia madarakani, ambayo walidhani ni mafanikio makubwa kwa kundi hilo la harakati za Kiislamu, sasa wameshatia akili kwamba njia hiyo haikuwa muafaka, na ilikuwa ni kupoteza tu malengo sahihi ya waasisi wa kundi hilo. Mwaka jana niliandika makala ya kutahadharisha kuhusu methodolojia hii na changamoto zake na jinsi ilivyowaangusha Waislamu wa Algeria, Uturuki na Palestina (Hamas). Watu wengi, ama hawakuelewa au walijifanya hawaelewi. Shangwe ya ushindi na matumaini hewa, iliwaondolea maarifa hata ya kuona ukweli ulio wazi. Methodolojia iliyotumiwa na Ikhwan Muslimin ya kuingia kwenye uongozi wa dola kupitia mlango wowote, na kisha kuanza kutekeleza Uislamu baada ya kuingia madarakani inafahamika vyema. Njia hii inamaanisha kuwaandaa watu hatua kwa hatua kiitikadi, kisaikolojia, kimaadili na kijamii, ili wakubali na kisha kutekeleza sheria za Mwenyezi Mungu katika nyanja zote za maisha yao. Wanaoshabikia njia hii wana hoja zao ingawa hazina mashiko ya kisheria. Msingi mkuu wa hoja yao ni kwamba Uislamu haukufunuliwa kwa Mtume Muhammad (saw) wote kwa mara moja. Kwa hiyo, kila hatua ya Uislamu i l i v y o k u j a wa k a t i u l e , inatumika kama ushahidi wa matumizi ya methodolojia hii. Mifano inayotumika zaidi ni jinsi Swala ilivyoshuka, Funga na amri ya kukataza ulevi. Kwa hiyo, wanasema, Mwenyezi Mungu Mtukufu ameteremsha sheria yake kwa binadamu kidogo kidogo. Basi na sisi tukitaka kuirejesha, inabidi tufanye hivyo. Hapo maana yake binadamu ndiyo wanaoamua jinsi gani na lini sheria ya Mwenyezi Mungu itekelezwe! Hilo ni kosa. Taasisi za utawala wa umma hazikuanguka wakati Hosni Mubarak alipoanguka nchini Misri. Na Morsi alikabiliana na upinzani mkali kutoka Mahakama ya nchi hiyo, vyombo vya habari vya umma, jeshi na polisi. Taasisi ambazo kimsingi hazipaswi kupingana na mkuu wa dola, isipokuwa zinatakiwa kumtii. Hakuwa na uwezo wa kuzifanyia marekebisho taasisi hizi kama kiongozi mkuu wa nchi. Nchi ilikabiliwa na m i g o g o r o m i k u b wa ya kiuchumi wakati Morsi alipoingia madarakani, lakini masikini ya mungu, hakuwa na nyenzo wala mamlaka anayopaswa kuwa nayo Rais, katika kurekebisha uchumi wa nchi. Wapinzani wake wa kisiasa wa kisekula, walitilia shaka sifa zake za kidemokrasia, na wapinzani wake wengine wa kisiasa Waislamu walitilia shaka sifa zake za Kiislamu. Ikawa ugali moto, mboga moto kwa Mohammed Morsi! Hali ya kisiasa na kiuchumi nchini Misri, ingeweza kumpa wakati mgumu kiongozi yeyote mahiri wa kisiasa, ambaye taasisi zote za dola ziko chini yake, wachilia mbali Mohammed Morsi, ambaye hakuwa na uwezo hata wa kuamrisha jeshi, wakati yeye ni Amiri jeshi mkuu! Kwa hiyo kushindwa kwake kusimamia baadhi ya mambo, lilikuwa ni jambo la wazi kabisa. Lengo la siasa katika Uislamu ni kushughulikia na kusimamia masuala ya umma. Uislamu umeweka misingi ya kisiasa na kiuchumi na taratibu madhubuti za kushughulikia matatizo ya kamii. Misri inakabiliwa na mgogoro mzito wa kiuchumi p a m o j a n a m a t a t i z o ya kiusalama na ufisadi wa kisiasa. Kwa kugeukia ufumbuzi wa kibeberu wa matatizo hayo (kama vile mikopo ya IMF), ili kutatua mgogoro wa kiuchumi nchini Misri, Serikali ya bwana Morsi imejenga mtazamo mbele ya umma, kwamba ubeberu ndiyo wenye fikra sahihi za kuimarisha uchumi wa Misri. Sasa kama Uislamu hautekelezwi wakati wa kutatua migogoro kama hiyo, utatekelezwa wakati gani? Dhana kwamba matatizo yanaweza kutatuliwa kwa kutumia ufumbuzi usiokuwa wa Kiislamu, ili baadaye Uislamu uweze kutekelezwa kikamilifu siyo sahihi. Kujiamini kunaweza kujengwa kwenye ufumbuzi wa Kiislamu, kwa kuona ufumbuzi huo ukifanya kazi na siyo ufumbuzi huo kutupwa wakati wa matatizo. Tatizo lolote linalopatiwa ufumbuzi kwa kurejea mfumo usio wa Kiislamu, maana yake ni kujenga mtazamo kwamba Uislamu hauhitajiki. Serikali ya Misri chini ya bwana Morsi, ilionekana kutoa umeme wa bei nafuu Gaza, wakati Cairo ikikabiliwa na changamoto ya kukatika umeme mara kwa mara. Mwaka mmoja umepita, Misri imekumbwa na upungufu wa chakula, petroli, umeme, maji na ukosefu wa ajira, wakati hali ya usalama ikidorora. Serikali ya Misri chini ya Mohammed Morsi, haikutekeleza hata ufumbuzi m m o j a wa m a t a t i z o ya kiuchumi kwa kuzingatia kra ya Kiislamu, lakini bado taswira inayojengwa duniani ni kwamba Uislamu wa Morsi ndiyo ulioporomosha uchumi wa Misri. Matatizo na changamoto zote za Misri sasa anabebeshwa Morsi na Uislamu wake, wakati inajulikana wazi alipokuwa Rais, hakuweza kutekeleza Uislamu hata kidogo katika ngazi ya dola, kutokana na mfumo ulioshindwa wa kisekula unaotawala Misri. Kiuhalisia, kushindwa kwa bwana Morsi kuitawala Misri Kiislamu, ingawa aliingizwa madarakani na umma unaotaka kutawaliwa Kiislamu, kulimfanya Rais huyo kuwa kibogoyo. Ndiyo maana ameondolewa madarakani kirahisi mno na kujenga picha duniani kwamba Uislamu haufai kutawala. Lakini tathmini sahihi ya kufaa au kutofaa

11

Makala

SHAABAN 1434, IJUMAA JULAI 12 - 18, 2013

AN-NUUR

MWEZI mtukufu wa Ramadhani umeanza. Ramadhani ni fahari kwa mja na anapaswa kuipokea hidaya hii vyema ili apate malipo mema kutoka kwa Allah (sw). Ramadhani ni siku 29 au 30 tu, katika mwaka. Na kumi la awali la mwezi ni la Rehma panapo majaliwa Mwenyezi Mungu atuvushe salama. K a t i k a m a n t i k i ya k e , mwezi huu ni wa kujifunza, kujisafisha na kujizoesha kuendelea kufanya mema kutokana na matokeo mema yanayopatikana ndani yake. Ramadhani humfanya mja kuongoka na kuwa na mwanzo mzuri wa kubadilisha maisha yake, kuanzia mtazamo, tabia na matendo yake. Mwezi huu unazowesha mfungaji kurejea yale mema na yaliyoridhiwa na Mola wake na kuachana na yale yote mabaya na

`Kumi la kwanza Ramadhani


yalikatazwa. Hii ni Ramadhani mwezi wa swaumu unahitaji mazingatio ndani yake na hata baada ya kwisha kwake. Ni wakati wa Muislamu kutulia, kufikiri na kisha kupima matokeo ya matendo yake. Mola wetu tutakabalie swaumu zetu na utukunjulie rizki ya halali, Amin. Kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani ni nguzo ya nne kati ya tano zinazosimamia dini ya Kiislamu, ambapo mtu mwenye kubalehe au kuvunja ungo hutakiwa kuitimiza. Mwezi huu una historia ya kipekee katika dini ya Kiislamu, kwa sababu ndiyo mwezi ambao kitabu kitukufu cha Qur-an kilishushwa katika usiku unaoitwa Lailatul Kadir. Swaumu au kufunga ni amri ya Mwenyezi Mungu kwa waumini wa dini ya Kiislamu kupitia kwa Mtume Muhammad (S.A.W). Amri hiyo ya Mwenyezi Mungu imetajwa katika aya ya 182 ya sura ya pili Baqarah 183, ndani ya kitabu kitukufu cha Qur-an. Katika aya hii, Allah (SW) a n a wa a m b i a Wa i s l a m u kupitia Mtume Muhammad (S.A.W) kuwa, Enyi mlioamini, mmelazimishwa kufunga (swaumu) kama walivyolazimishwa wa l i o k u wa k a b l a ye n u i l i m p a t e k u wa wa c h a Mungu. Kwa mujibu wa aya hii, u t a g u n d u a k u wa l e n g o k u b w a k w a Wa i s l a m u kulazimishwa kutekeleza ibada hii ya funga ni kwa wao kuweza kufikia ngazi au daraja la ucha Mungu wa kikwelikweli. K wa m a a n a k wa m b a endapo mja ataitekeleza ibada hii kwa kufuata sharti zote kikamilifu, dhahiri kiwango chake cha imani kitapanda. Mwezi mtukufu wa

Ramadhani umegawanyika katika makundi matatu ambayo yana siku kumi kila moja. Kila kundi moja la kumi, lina faida zake kwa mwenye kutimiza kile kilichoagizwa na Mwenyezi Mungu. Kumi la kwanza linajulikana kwa jina la Rehma (rehema), la pili Magh-fira (kusamehewa madhambi) na lile la mwisho linaitwa kumi la kuachwa huru na moto. Tumeianza Ramadhani kwa kuanzia na kumi la Rehma. Katika kipindi mja hurehemewa sana na Allah (sw) kwa kila jema analolifanya. Kwa kifupi ni kwamba kumi la kwanza ni kumi la mja kurehemewa na Mola wake. Itoshe kufahamika kwamba kila jema analofanya mja, hulipwa zaidi kuliko ambavyo analipwa katika siku za kawaida. Ndiyo maana wakati huu unaweza kushuhudia watu wakifurika katika nyumba za ibada.

kwa Uislamu kwenye utawala na uongozi wa dola, haiwezi kutolewa na wale wanaopinga Uislamu nchini Misri! Inafahamika vyema kwamba wafuasi wengi wa Ikhwan Muslimin nchini Misri walikuwa wakitumai kuanzishwa kwa utawala wa Kiislamu nchini humo, ingawa walua wazi kwamba utawala wa Morsi usingeweza kuwakisha kwenye malengo hayo. Kujua kwamba malengo yako makuu ya kisiasa yanatofautiana kabisa na sera za kisiasa unazotekeleza, inakufanya wakati wote uendeshe mambo kwa mashaka. Hali hii imejitokeza zaidi kwenye kipindi cha mwisho cha utawala wa Ikhwan Muslimin nchini Misri, ambao ulikuwa ukituhumiwa vikali kwa Uislamu wa Siasa Kali, hata pale sera walizotekeleza zilipokuwa Usekula wa Siasa Kali. Kwa hiyo kusimamisha Uislamu kidogo kidogo katika ngazi ya dola, kama walivyofanya Ikhwan Muslimin, kunaashiria udanganyifu, ingawa nia inaweza kuwa njema. Qur an imetuonya kuhusu utekelezaji nusu nusu wa sheria za Mwenyezi Mungu: Na (baadhi ya) ambao tuliwapa Kitabu wanafurahia uliyoteremshiwa. Na katika m a k u n d i ya o m e n g i n e wako wanayoyakataa b a a d h i ya h a ya . S e m a : Nimeamrishwa kumuabudu Mwenyezi Mungu tu wala nisimshirikishe. N i n a i t a K wa k e v i u m b e wenzangu waongoke (kama nilivyoongoka). Na ni kwake marejeo yangu Qur(13:36). Na namna hivi tumeiteremsha (hii Quran), hali ya kuwa ni hukumu (ya Mungu iliyoteremka) kwa (lugha ya) Kiarabu. Na kama ukifuata matamanio yao baada ya kukukia Ilimu hii, hutakuwa na raki wala mlinzi mbele ya Mwenyezi Mungu Qur(13:37). Mara nyingi Mwenyezi Mungu anatupigia mifano ya Waislamu wa mataifa yaliyopita, ili tuweze kujifunza kutokana na makosa yao. Wanaharakati wa Kiislamu duniani, lazima walinganie Utekelezaji wa Uislamu Wote kama mfumo, na watafute ufumbuzi wa matatizo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii yanayowahusu binadamu kutoka ndani ya mfumo huo. Kusiwe na matarajio hewa kwamba tukishika madaraka, basi Katiba itakuwa ya Kiislamu na mambo yote yataendeshwa Kiislamu. Hilo halijawahi kuwa na wala halitakuwa!

12

AN-NUUR
MAKALA

2nd oor, Red Cross Bldg, Bibi Titi / Morogoro Rd, PO Box 7079 DSM Phone: 255 658 225998/ 255 683 225998 Email: info@taqwaorphanstrust.org Website: www.taqwaorphanstrust.org

12

SHAABAN 1434, IJUMAA JULAI 12 - 18, 2013

Imam Hamza ahimiza Waislamu kutetea haki


Na Bakari Mwakangwale

TAQWA ORPHANS TRUST TANZANIA inawakaribisha waislamu wote kushiriki na kuchangia katika program maalum ya futar kwa yatima-Pemba na Pwani kwa mwaka 1434A.H /2013. Kwa maelezo zaidi: Piga simu namba;0658 225 998/0683 225 998/0713 300 417 au tembelea osi zetu zilizopo kwenye jengo la Red Cross lililopo kwenye makutano ya barabara ya Morogoro na Bibi Titi, mkabala na jengo la NSSF.

IMAM Hamza Omar, amewahimiza Waislamu kusimama imara katika kutetea haki. A m e s e m a , wanalotakiwa kufahamu Waislamu ni kuwa katika kupigania haki kuna gharama zake na kwamba hilo lisiwatishe. Imam Hamza, amebainisha hayo, Ijumaa ya wiki iliyopita akiwahutubia Waislamu mara baada ya swala ya Ijumaa, katika Msikiti wa Mtambani, Kinondoni Jini Dar es Salaam. Katika mawaidha yake

Maimamu Tanga waichambua rasimu ya katiba


Na Abu Ayub

Imam Hamza amesema kuwa anaamini kuwa kisa cha yeye kukamatwa, kufunguliwa kesi huku dhamana yake ikizuiliwa, ni kutokana na msimamo wake na juhudi aliyokuwa akifanya kupigania haki. Akitoa mfano juu ya yale yaliyojiri wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipofika Geita kufuatilia mgogoro wa uchinjaji, alisema kuwa Waislamu akiwemo yeye mwenyewe, walisimama kusema kweli na kueleza wazi kuwa hawapo tayari kuona wakibaguliwa na kudharauliwa. Akasema kuwa ilikuwa pale Mheshimiwa Waziri

Mkuu alipoonyesha kuwa hayupo tayari kusikiliza madai ya Waislamu, ndipo walipoamua kutoka katika kikao na hiyo ikiwa ni kuonyesha hisia zao kuwa hawaridhiki na mambo yanavyoendeshwa. Imam Hmzana alisema, baada ya kikaoa na Waziri Mkuu, haikupita muda alikamatwa, na kuwekwa ndani huku dhamana yake ikizuiliwa. Akasema, yeye binafsi anahisi kuwa kuzuiliwa huko kwa dhamana kunatokana na msimamo wake wa kusema kweli na kupigania haki.

IMAM Hamza Omar.

MAIMAMU wa misikiti mbali mbali ya jijini Ta n g a w a m e k u t a n a kwenye ukumbi wa Simba Mtoto katikati ya ji hilo kwa madhumuni ya kuangalia makosa yaliyomo kwenye rasimu ya katiba mpya na kutoa mapendekezo yao yatakayopelekwa kwenye Baraza la Katiba la Kiislamu litakalokaa tena huko jijini Dar es Salaam siku za mbele. Wa k i o n g o z w a n a mwakilishi wa Baraza hilo kwa mkoa wa Tanga, S h e i k h A l i N a s s o r, Maimamu hao baada ya mada ya ufunguzi iliyotolewa na mtaalamu wa masuala ya katiba, Sheikh Salim Barhiyaan walikaa vikundi vikundi kuvijadili vipengele 21 vilivyotajwa kuwa ni kandamizi zaidi kwa imani ya Kiislamu nchini. Baada ya kamati hizo kuangalia vipengele h i v yo wa s e m a j i wa o walisimama mbele na kueleza kwa hamasa kile kila kikundi kilichokiona

kwenye rasimu hiyo. Kikundi kilichoitwa A b u b a k a r S i d i q r. a kilisema kinataka katiba mpya kuruhusu maeneo yenye Waislamu wengi kama Zanzibar kuwa huru kujitawala kwa Sheria za Kiislamu na kusema kuwa kwa uzoefu wa nchi nyengine kama Nigeria jambo hilo wala halitozikwaza haki za raia mwengine yoyote. Zaidi ni kuwa utaratibu huo utapunguza manunguniko kwa raia wa eneo husika wanaopenda kujitawala kwa imani za dini zao. Kikundi cha Omar ibn Khattab r.a kilisema kifungu cha 5 cha ibara ya 31 ya rasimu kuhusu kilichoitwa uchochezi kwa kutetea imani ya dini kinapingana na kifungu cha 2 chenye kutoa uhuru wa kuchagua na kutangaza imani ya mtu. Yale yote yanayoruhusiwa na kifungu cha 2 ndiyo hayo hayo yanayopingwa na kifungu cha 5 cha ibara hiyo. Awali katika mada ya ufunguzi, Sheikh Salim alisema kuwa ibara hiyo

Pichani ni kiongozi wa kikundi kimojawapo akiwa na maimamu wenzake . ya rasimu inaonekana kama imewekwa kutetea imani ya Kikristo akigusia huko nyuma katika kesi iliyomuhusu Rajabu Dibagula. Dibagula alipewa h u k u m u ya k u t u m i a kifungo jela kwa kusema kuwa Yesu si Mungu jambo linaloitwa ni kashfa kwa Wakristo. Baadae hukumu hiyo ilitenguliwa pale Waislamu walipokata rufaa wakitumia kipengele cha katiba inayomalizika. Ilibainishwa kuwa kabla hata rasimu hiyo haapita, t a ya r i k u m e k u wa n a kamatakamata ya kuhusisha mawaidha ya Waislamu yanayopatikana kwenye mikanda ya aina mbali mbali zikiitwa ni kanda za kichochezi na kashfa. Katika maelezo yake, Sheikh Salim Barhiyaan a l i s e m a Wa i s l a m u hawatakiwi kukata tamaa hata kidogo kwani Mwenyezi Mungu s u b h a a n a h u wa t a a l a anaona kila walifanyalo hivyo mafanikio yanaweza kuja hata dakika za mwisho. Lakini hata hivyo ikiwa kutakuwa na matokeo kinyume chake basi kila mwenye kufanya juhudi ajue atalipwa na hataulizwa kwa kukosekana mafanikio. Alikumbusha kwamba M t u m e s wa l a L l a a h u alayhi salaam aliendelea kumlingania Ami yake, bwana Abu Talib hadi wakati wa sakaraatul mauti. Pamoja na hivyo ami yake huyo alikufa katika imani ya kishirikina na kwa hilo hatoulizwa juu ya ami yake huyo kufa katika ukari. Baada ya kumalizika kwa mijadala hiyo na majumuisha wawakilishi wa Baraza la Katiba la Waislamu walichukua mapendekezo hayo na kuahidi kuyaweka sawa kwa ajili ya kuyapeleka mbele kunakohusika.

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

You might also like