You are on page 1of 12

www.annuurpapers.co.

tz

Sauti ya Waislamu

(20) UMESHAWAPELEKA WATOTO HIJJA?


Sahaba mmoja alimnyanyua mtoto wake mdogo na kumuuliza Mtume(saw), Na huyu ananufaika na Hijja? Mtume(saw) akajibu, Ndiyo, na wewe unapata ujira (kutoka kwa Mola wako). Wangapi tumewapeleka watoto wetu Hijja? Milioni ngapi tunatumia kwa maharusi ya fahari na mambo mengine ya kidunia? Karibu uwaandikishe watoto na wafanyakazi wako Ahlu Sunna wal Jamaa.Gharama zote ni Dola 4,300. Tafadhaliwasiliana nasi ifuatavyo: Tanzania Bara: 0717224437; 0777462022;Unguja: 0777458075;Pemba: 0776357117.

JKT balaa kwa Wasichana Waislamu


Wavalishwa bukta, wengi wagoma kwenda Kongamano kubwa kufanyika Dar kupinga Sio kaputura itakayoleta Uzalendo na Utaifa

ISSN 0856 - 3861 Na. 1077 SHAABAN 1434, IJUMAA , IJUMAA JUNI 28 JULAI 4, 2013 BEI TShs 500/=,

Wanajeshi wakoleza kipigo kwa Waislamu


Mkuu wa Mkoa atuhumiwa kuhusika Masheikh, vijana wakimbia familia Watuhumu kuwepo hujuma za kidini

Mwakilishi wa Balozi wa Saudia nchini, Bw.Aaqil (Kulia) akigawa nyama ya Mbuzi waliochinjwa na Mahujaji katika Ibada ya Hja ya mwaka 2012, kwa Waislamu, Mei 25 Jini Dar es Salaam. Picha Na Bakari Mwakangwale.

Kama Zanzibar ilisalimika Tanganyika ilitowekaje!!!!


Amesema kweli Jaji Joseph Warioba Serikali mbili zitavunja Muungano
NI kipofu gani atabisha kwamba Tanganyika na Zanzibar hazikufa baada ya ujio wa Muungano? Wanaodai mfumo wa Serikali mbili, wanatoa wapi ujasiri potofu na wa kihafidhina kupotosha umma juu ya mfumo halali wa Muungano uliokusudiwa? Wa t u a m b i e ; k a m a Zanzibar ilisalimika, Tanganyika ilitowekaje? (Soma Uk. 7)

BAADHI ya vana wa Kidato cha sita waliomaliza mafunzo ya JKT.

Mhe. Shamsi Nahodha, Waziri wa Ulinzi

2
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Tahariri/Makala
AN-NUUR

SHAABAN 1434, IJUMAA JUNI 28 JULAI 4, 2013

AN-NUUR

MAONI YETU

BARABARA ya Morogoro imekuwa nyeupe, hakuna mchuuzi wala vichuuzwa. Ombaomba wote maeneo ya Fire, Kariakoo, Posta, Kisutu na maeneo mengine jijini wamesombwa. Wenye maduka walitawanya bidhaa katika viambaza vya maduka yao, operesheni Obama imewamudu na sasa bi dhaa zipo ndani ya maduka na si nje tena. Mama lishe wameshafungishwa vibanda vyao. Hata hivyo wasiwasi wetu ni iwapo ombaomba na walemavu hao tuliozoea kuwaona kila siku katika maeneo hayo wanahifadhiwa sehemu salama ili wasirejee tena barabarani au la. Tu n a o n a h a t a k i l e Kipande cha barabara pale makutano ya barabara ya Mandela na Morogoro, kuanzia eneo la darajani Riverside hadi eneo la taa za kuongozea magari Ubungo, eneo ambalo liliachwa kwa muda mrefu bila kurekebishwa licha ya kuwa ni kero ya muda mrefu kutokana na ubovu, sasa pamewekwa lami sa kabisa. Bila shaka kufanya hivyo, ni kufanikisha ziara ya Rais Obama katika mtambo wa kuzalisha umeme wa Symbion pale Ubungo Power Station. Bila shaka ni ujio wa Rais Obama ambao umeleta ari hii ya uwajibikaji wa muda mfupi. Hatua hizi za haraka na za muda mfupi z i n a z o c h u k u l i wa n a serikali na taasisi zake katika kipindi hiki cha m a a n d a l i z i ya z i a r a ya Rais Obama nchini, zingekuwepo hata wakati mwingine jiji la Dar es Salaam lingekuwa la kupigiwa mfano japo

Tungewajibika ki-Obama tungeka mbali

Wanahabari kataeni kuwa kipaza sauti cha tabaka kandamamizi


Biashara ya udini, chuki si yenu
Na shaban Rajab I M E E L E Z WA k u w a vyombo vya habari nchini, viko katika hatari kubwa ya kumezwa na tabaka kandamizi dhidi ya wakandamizwaji iwapo hawatakataa kuwa kipaza sauti cha agenda za tabaka kandamizi. A i d h a wametahadharishwa kuwa iwapo wataendelea kuweka pembeni maadili na maslahi ya umma na kubeba agenda za tabaka kandamizi na kushindwa kutimiza wajibu wao wa kimsingi wa kupanga agenda zao za habari (seing the agenda) watanunuliwa na kusambaratishwa. Hayo yameelezwa katika Kongamano la Mwaka la Maadili ya U a n d i s h i wa H a b a r i , ambalo liliambatana na Mkutano Mkuu wa Wadau wa Habari (NGC) ulioandaliwa na Baraza la Habari nchini (MCT), na kufanyika katika Hoteli ya Blue Pearl, jini Dar es Salaam mwanzoni mwa wiki hii. Akisherehesha muswada uliowasilishwa n a B w. M a k wa i a wa Kuhenga, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mwalimu Bashir A l l y, a l i s e m a m f u m o kandamizi wa watawala hauwezi kujisambaratisha wenyewe mpaka pale utakaposambaratishwa. Mwalimu Bashiri alivitaka vyombo vya habari kuwa makini na kutumia weledi kuibua agenda za siri zilizojicha zinazoletwa na tabaka kandamizi kwa mgongo wa udini, badala ya kuwa vipaza vya kufanikisha yale yanayohubiriwa na tabaka hilo kwa lengo la kutimiza agenda zao huku maslahi ya umma na wanyonge wakiathirika zaidi. Kauli za funga yule, kamata wale, tesa, toa jicho ni kauli za tabaka tawala kandamizi, kauli hizi zinaweza kutolewa pia na vibaraka wa tabaka hilo. Alifafanua. Kutokana na hali hiyo, msomi huyo aliwataka wanahabari kuvua vikaragosi (mask) zilizovikwa katika nyuso zao ili kuuweka mfumo huo kandamizi uchi, kwa kuripoti habari zenye maslahi kwa umma badala ya kuripoti habari zinazosababisha chuki miongoni mwa jamii. Niwahakikishieni kabisa, wanahabari mpo katika kipindi kigumu hivi sasa kuliko kipindi kingine chochote, msipo kuwa kitu kimoja hasa kwa kushikana kupitia baraza lenu hili, mtanunuliwa na mtatumika kwa maslahi ya mfumo kandamizi. Tabaka hili kandamizi linahitaji sana vyombo vya habari kutimiza malengo yake, kwa upande mwingine, tabaka kandamizwa nalo linawahitaji na kuwategemea sana katika kutetea haki zao dhidi ya takaba kandamizi, k a m a h a m t a k u wa n a msimamo kwa tabaka la wanyonge, hamtaaminiwa. Kutoandika lugha kali na za chuki inategemea msimamo uliochagua, wa tabaka kandamizi au kandamizwaji alifafanua mwalimu Bashir. Akitoa mfano wa m a u a j i ya h a l a i k i ya Rwanda mwaka 1994, Bw. Bashir alisema matokeo yanaonyesha kuwa wanahabari na vyombo vya habari kwa ujumla, waliweka pembeni maadili yao ya kazi na maslahi ya umma, wakabeba agenda za tabaka kandamizi za kueneza uhasama, chuki na ukabila na matokeo yake, taifa lilifura chuki na uhasama na kikatokea kilichotokea. Awali Bw. Kuhenga alisema udini umekuwa ni chambo wanachotumia wanasiasa kwa maslahi binafsi. Alitosa mfano kuwa baada ya kulipuliwa kanisa mkoani Arusha, amani iliendelea. Alisema licha ya mlipuko, wameona kilichokusudiwa hakijafanikiwa na Watanzania wameendelea kushikamana. Sasa wameingia kwenye s i a s a k wa m t i n d o wa matukio yanayofanana kufuatia bomu lililolipuka tena kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za udiwani za CHADEMA. Alisema propaganda za udini ni mfumo wa kuuziwa mbuzi kwenye

kwa usafi na mpangilio mzuri wa ji. Lakini zaidi uwajibikaji huu ungekuwa umelikisha taifa hili mbali kimaendeleo. Lakini wapi, imekuwa ule msemo wa nguvu ya soda au moto wa kifuu unaowaka waka viongozi kama Obama na kuzimika mara tu

wakiondoka. Lakini kwa upande mwingine, Ji haliwezi kuwa ni maeneo maalum tu ya Posta, barabara ya Morogoro, Buguruni na Ubungo pekee ambako bwana mkubwa atapita. Hata Tegeta, Mbezi, Kimara, Ilala, Mbagala, Changombe, Temeke nako ni sehemu kubwa tu ya jiji letu lakini operesheni hizi hazionekani huko! Ni ushauri wetu kwamba, iwapo uwajibikaji huu unaoonekana sasa katika maeneo atakapozuru Obama, ungekuwa ndio ada ya watendaji wetu hata maeneo mengine ya nchi, leo yangekuwa mbali kimaendeleo. Ulinzi na usalama ungekuwa wa uhakika k w a Wa t a n z a n i a , barabara zetu zinazopitika kwa taabu huko mitaani zingepitika kwa mwaka mzima. Usafi ungemaliza kipindupindu cha kila mwaka. Tatizo la maji sa na salama ingekuwa historia. Basi ni vyema tukaanza sasa kuzoea nidhamu ya uwajibikaji wa ki-Obama katika kuwatumikia Watanzania. Nidhamu ya kiutendaji inayoonyeshwa kwa Obama, sasa tuiendeleze hata katika kuwatumikia
Watanzania.

gunia. Akahoji, kuendelea kutoa habari hizo zenye sura ya kutimiza agenda za watu, wahariri kwenye postimortem wanajadili na kupanga agenda gani. Alihoji kuna umuhimu gani wa kuwatangaza hao waeneza kauli za chuki na udini kuliko kuangalia agenda zao na maslahi nchi? Bw. Makwaia aliongeza kuwa siku za nyuma, vyombo vya habari pamoja na kuwa na sera zake, lakini msingi wake ulikuwa umoja wa kitaifa, kuhimiza maendeleo na kwamba ilikuwa nadra sana kiongozi wa kisiasa kwenda kwenye haa za kidini, labda haa yenyewe iwe na sura ya kitaifa. Alisema lakini siku hizi viongozi wanazisaka na kujipeleka wenyewe kwenye hafla hizo za kidini, huku vyombo vya habari navyo vikiwa mstari wa mbele kuripoti habari hizo na kuhoji, kuna haja gani ya vyombo vya habari kuwa vipaza sauti vyao. Akihitimisha mada ya Bw. Kuhenga, Mwalimu Bashir Ally alisema lazima vyombo vya habari vitambue kwamba itikadi ya leo ni itikadi kali ya soko huru ambapo hata mapenzi yamekuwa bidhaa katika mfumo huo. Alisema udini inawezakuwa biashara kubwa kwa watu (Mfumo kandamizi) na wanahabari wakawa sehemu ya biashara hiyo. Alisema badala ya vyombo vya habari kusaidia kuzima agenda za biashara hiyo, wanaripoti agenda yenyewe ya kuvutana kuchinja na kuchinjana na kufanikisha agenda iliyokusudiwa. Alishauri kipindi hiki cha hatari, wanahabari n a B a r a z a l a o M C T, k u wa k i t u k i m o j a n a kuwa na msimamo wa pamoja bila kujali athari zinazowaandama za kiusalama kwani wajibu wao ni kutumikia umma. Alisema kinyume cha wanahabari hao kuwa na umoja na msimamo wa pamoja, wakishindwa kuwa na agenda kwa mstakabali wa umma, watanunuliwa.

Habari

SHAABAN 1434, IJUMAA JUNI 28 JULAI 4, 2013

AN-NUUR

JKT balaa kwa Wasichana Waislamu


Na Mwandishi Wetu
kuwa waliokuwa mstari wa mbele walikuwa wazee wa Kiislamu na sababu yake ni moja tu: wao ndio walikuwa wadhulumiwa wakubwa, walitaka iondoke ile dhulma ya kubaguliwa Waislamu katika elimu. Alisema na kuongeza kuwa, leo zaidi ya miaka 50 baada ya kuwa huru, haitakuwa sahihi kwa Serikali k u wa n y i m a wa t o t o wa Kiislamu haki yao ya kwenda JKT kwa kuwawekea sharti la kuvaa kaputura kinyume na maadili ya dini yao. Tunachoiomba Serikali ni kuwa itizame upya sare hii ya kaputura ili isiwe kikwazo kwa mabinti wetu, alisema mzazi huyo. Akitoa malalamiko yake mzazi mwingine alisema kuwa kinachosemwa ni kuwa lengo la kupeleka vana JKT ni kujenga uzalendo, maadili, umoja na utaifa. Sasa kama hayo ndiyo malengo, mi sidhani kuwa hayo hayawezi kupatikana bila ya kuvaa bukta, sio bukta itakayojenga utaifa, ila kama watalazimisha, bukta hiyo hiyo ndiyo itakuwa sababu ya kuvunja umoja na utaifa kwa sababu idadi kubwa ya mabinti wa Kiislamu watakataa kwenda au hata wakienda kutazuka mgogoro wa kugomea bukta na wakitendewa vibaya Waislamu na Masheikh wao wataingilia kati na hilo litazua mgogoro kwa nchi nzima. Alisema na kutahadharisha mzazi huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Kiravu na kuongeza kuwa angependa kuona jambo hili likichukuliwa na taasisi za Kiislamu za kitaifa kuzungumza na mamlaka husika. Kwa hakika hili si suala langu binafsi au la Muislamu mmoja mmoja, ni la Waislamu wote na ingekuwa vyema taasisi za kitaifa za Kiislamu zikachukua agenda hii na kutafuta namna ya kuwasiliana na Serikali ili kulitafutia ufumbuzi. Alimalizia mzazi huyo akisema kuwa hapana ubishi kuwa mpango wa JKT ni mzuri na kwamba yeye binafsi ameupokea kwa mikono miwili, ila tu lililo muhimu kwa sasa ni kushughulikiwa hii changamoto ya bukta kwa wasichana. Wakati huo huo, habari tulizozipata tukienda mitamboni zimefahamisha kuwa viongozi wa taasisi za Kiislamu wamefanya shura na kukubaliana kulifikisha jambo hili kwa Waislamu kwa maana ya kuliandalia utaratibu wa kongamano au khutba za Ijumaa ili lifahamike vizuri. Kwa upande mwingine wakasema kuwa watalikisha rasmi Serikalini wakiomba sare ya bukta iondolewe. Habari za awali zinafahamisha kuwa Jumuiya na Taasisi za K ii slamu, wanaandaa barua kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wakitaka jambo hili kutizamwa upya na kuwekewa utaratibu mzuri ili isekukia mahali JKT zikawa m a k a m b i ya wa s i c h a n a Wakirsto watupu. Taarifa zaidi zinasema kuwa kesho Jumamosi kutakuwa na mkutano wa viongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu jini Dar es

WAKATI Serikali imeanza kurejesha utaratibu wa wanafunzi wanaomaliza kidato cha sita kwenda JKT kwa muda kabla ya ama kwenda vyuo vikuu au kuanza kazi, yameibuka malalamiko k u t o k a k w a Wa i s l a m u wakisema kuwa kuna dosari zinatakiwa kushughulikiwa ili kuhakikisha kuwa mambo yanakwenda vizuri. Kubwa linalolalamikiwa ni mavazi. Wazazi wengi wamekuwa wakilalamika na kusema kuwa watalazimika kuwazuiya mabinti zao kwenda JKT kwa sababu imeonekana kuwa wanapoka huko huvishwa nguo zisizoendana na maadili ya imani zao. Wengi walioka na kutoa maoni yao katika ofisi za gazeti hili wanasema kuwa wangependa sana kuona watoto wao wakienda kulitumikia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). Hata hivyo wakasema k u wa wa n a l i o m b a j e s h i hilo kutizama upya suala la mavazi hasa kwa upande wa wasichana. Wa k a s e m a b a d a l a ya kuvaa bukta (kaputura fupi), wanaomba JKT wabadili sare hiyo na kuweka suruali. Mi sioni kama kuna sababu ya msingi ya kuwavalisha wasichana chupi (bukta), wanaweza kuvaa suruali na wakapiga kwata na kufanya kazi kama kawaida, kwa hiyo mi naomba uongozi wa JKT kubadili sare hii ili wasiwakwaze mabinti wetu, wazingatie kuwa suala la imani ni haki ya kikatiba ya mwananchi, sasa wasimkwaze kiimani katika kupata haki yake ya kujiunga na jeshi hilo. Amesema mzazi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Omar Said ambaye amesema kuwa yeye binafsi atashindwa kumruhusu binti yake kwenda JKT mwaka huu kama anavyowajibika, lakini hata kama yeye angetaka binti aende, binti mwenyewe hayupo tayari kuvalishwa bukta. Hii mimi naona si haki kwa sababu kwa kuweka sare ya bukta inakuwa kama njia ya uhakika ya kuwakwaza mabinti wa Kiislamu, inakuwa kama wakati ule wa ukoloni ambapo Waislamu wengi walikosa kusoma kwa kuepuka kubatizwa. Alisema. Katika ufafanuzi wake akasema kuwa Serikali za kikoloni ziliweka utaratibu wa kutoa elimu uliowakwaza Waislamu ambapo kulikuwa na sharti la kubatizwa ndio mtu asome jambo lililofanya wazee wengi kutowapeleka watoto wao shule. Ukitizama historia ya kupigania uhuru nchini utaona

Wanajeshi wakoleza kipigo kwa Waislamu


Na Mwandishi Wetu
m a t e s o h a yo wa l i k u wa wakiulizwa nani mfadhili wao na kwa nini wanamsumbua Mkuu wa Mkoa. Swali jingine ni kutakiwa kueleza nini chama chao. Baadhi ya Waislamu ambao wametajwa kuwa majeruhi wa kipigo hicho cha wanajeshi, ambao walikamatwa Mei mwaka huu ni Issa Ndinda, Hamis Mnunga, Ally Mtepa, Said Namata, Ismail Nyambi, Salum Sudi (Saibogi) pamoja na Ismail Fakhi Mfaume. Mwananchi mmoja mkazi wa Mtwara ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini kwa usalama wake, amesema kuwa Waislamu wa Mtwara wanashangazwa na zoezi hilo la kuwakamata na kuwakongota kuwalenga wao pekee. Tunashangaa tupo watu wa imani tofauti, kwanini kina baba wa Kiislamu wawe waleng wa wak ub wa wa zoezi hili la utesaji, mpaka sasa hakuna mtu wa imani nyingine aliyekamatwa au aliyepigwa zaidi ya Waislamu. Zoezi hili linatutia wasiwasi k wa k u wa l i n a o n e k a n a kuwa na sura ya udini na chuki zaidi na haliwagusi watu wengine. Alilalamika mwananchi huyo. Hata hivyo taarifa zinabainisha kwamba zoezi hilo la kamata piga dhidi ya Waislamu Mtwara, linatokana na kongamano la Shura ya Maimamu katika viwanja vya Mashujaa mkoani Mtwara Januari 27, 2013. Katika Kongamano hilo, pamoja na mambo mengine, lilizungumzia kadhia ya wanaMtwara kupinga ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam. Aidha inadaiwa kuwa kuna uwezekano mkubwa Mkuu wa Mkoa huo Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia, akahusika na zoezi hilo kufuatia Waislamu kumtaka aondoke baada ya kuwatusi watu wa Mtwara kuwa ni mbumbumbu na wakamtaka kwanza aombe radhi. Wa i s l a m u M t wa r a wanaamini kuwa Mkuu wa Mkoa ndiye aliyetoa amri ya kukamatwa na kupigwa kwao kinyume na sheria. Alisema kuwa wanachama wa vyama vya siasa, ambao nao ni waathirika wa kile

Salaam ambao watapanga na kuratibu kongamano kubwa la Waislamu kuzungumzia jambo hili na kulipitishia maamuzi. Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika kabla ya kuanza mwezi mtukufu wa Ramadhani.

HALI si shwari Mtwara ambapo kumekuwa na madai ya kukamatwa vana wa Kiislamu, Masheikh na kushushiwa vipigo. Kamatakamata hiyo inadaiwa kufanyika nyumba kwa nyumba na hupelekwa katika kambi ya Naliendele ambako wanatembezewa kipigo kikali hali inayosababisha baadhi ya watu kuzikimbia familia zao na kutafuta macho. Kana mmoja aliyenusurika kufikishwa kambini kwa kutoroka wakati wakipelekwa huko amesimulia jinsi watu wanavyopigwa huku hali ikielezwa kuwa ni shwari. Amesema kuwa kina baba wengi wamezikimbia nyumba zao na kuziacha familia zao zikiteseka, kufuatia zoezi linaloendelea la wanajeshi kuwasaka na kuwakongota. Mateso yanayotolewa ni pamoja na kuvuliwa nguo kucharazwa bakora na kumwagiwa upupu. Jambo ambalo limewastua Waislamu wengi ni kuwa idadi kubwa ya wanaokamatwa ni Waislamu hasa vana wa Kiislamu na wazee waliokuwa m s t a r i wa m b e l e k a t i k a harakati za Kiislamu kupitia Baraza Kuu na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu. Ta a r i f a z i l i z o p a t i k a n a juzi, zilibainisha kwamba wanajeshi hao wanamtafuta kwa udi na uvumba Alhaj Namakanya, ambaye amekimbia kwa kuogopa kukamatwa na kuangukia kipigo kutoka kwa wanajeshi hao. Ta a r i f a z i m e a r i f u kuwa Sheikh Ramadhani Mataukahizo, ambaye alikamatwa hivi karibuni, ameachiwa na kurejea n y u m b a n i l a k i n i a k i wa anaugulia kwa kipigo. Ust. Bonge Mtarika, yeye ameelezewa kuwa amerejea nyumbani kutoka kambini Jumatatu ya wiki hii akiwa hoi. Habari tulizozipata zinafahamisha kuwa Ustadh Bonge Mtalika pamoja baadhi ya watu waliokuwa wamekamatwa wamerejea na kuelezea jinsi walivyoteswa. Wamesema, walivuliwa nguo kumwagiwa upupu na kucharazwa bakora. Wamesema, wakati wa

k i n a c h o d a i wa k u wa n i kupinga gesi kwenda Dar, wao walikamatwa na kufunguliwa kesi mahakamani. Uledi Hasan, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi mkoa wa Mtwara, Hamza Masoud, Katibu wa TLP, Katan Ahmad Katan, Mwenyekiti wa Vana Taifa CUF, Said Issa Kulaga, Katibu wa CUF Mtwara mjini walikamatwa kistaarabu na kesi zao zinaendelea katika mahakama ya Wilaya Mjini. Lakini hali ni tofauti kwa Masheikh na wanaharakati wa Kiislamu ambao wamekuwa wakisakwa na wanajeshi majumbani na katika sehemu zao za kazi na wanaokamatwa kupelekwa kambi ya jeshi Naliendele ambako huambulia kipigo. Imeelezwa kuwa wanajeshi hao wana orodha ya majina ya vijana wanaharakati wa kiislamu na Masheikh ambao wanasakwa. Itakumbukwa kuwa Mei 22, 2013 ghasia zilibuka mkoani Mtwara baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Pro. Sospeter Muhongo, kueleza azma ya serikali ya kutekeleza mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam, kufuatia kugunduliwa gesi nyingi huko Msimbati mkoani humo. Hata hivyo Prof. Muhongo alisema gesi hiyo haitasarishwa ikiwa gha, kwa maana kuwa mtambo wa kusasha gesi utajengwa Mtwara. Siku za hivi karibuni, Mbunge wa Viti maalum Clara Mwatuka, alieleza Bungeni kuwa hali ya Mtwara si shwari kwani watu wanasakwa majumbani mwao na kupigwa na kwamba wengine wameshakimbia familia zao. Aliitaka Wizara ya Mambo ya Ndani kutoa maelezo juu ya kadhia hiyo. Naye Mwenyekiti wa kikao hicho Jenister Muhagama, alifafanua zaidi kwa kuitaka Wizara kuchukua hoja ya mbuge huyo na kufuatilia na kutoa majibu mapema. Lakini pamoja na jitihada hizo bungeni, kipigo kutoka kwa wanajeshi kwa wananchi wa Mtwara kimekolea zaidi na hakuna hatua zilizochukuliwa hadi sasa.

Baraza Kuu lazindua Osi ya Wanawake


Na Azza Ally Ahmed
Allah kwa kutoa mali yake na kumpa Mtume ili kuhakikisha dini ya Allah Inasimama.. Aidha alisema kuwa hivi sasa ni vigumu kuwataja wasomi wakubwa wa Kiislamu duniani, bila kuwataja wake zake Mtume ( S.a.w) Bi. Aisha (R.a) akiwemo katika kundi hilo. Amewataka wanawake hao wa Baraza Kuu kutambua kuwa tayari Allah (sw) ameshawaongoa, basi wawe ni chachu ya kuhakikisha wanawake wengine kupitia wao, wanamjua Mola wao kwa vitendo na kuifuata dini kwa ukamilifu wake. Aidha amewakumbusha kuwa wana jukumu zito la kuhakikisha wanawalingania kwa uadilifu na kwa mapenzi na upole wa hali ya juu wanawake wenzao, ambao h a wa j a t a m b u a j u k u m u kubwa walilo nalo. Amewataka wanawake hao kuwaamsha wenzao ili wajue nafasi zao katika Uislamu na katika kijamii, ili kuweza kuleta maendeo ya Waislamu na jamii nzima kwa ujumla. Kwa upande wake, Imamu wa Msikiti wa Mtambani Sheikh Suleiman Abdallah, amewataka wanawake wa Kiislamu kujua kuwa Uislamu ulipiganiwa na wanawake pamoja na wanaume. Walitoa kwa nguvu zao, nafsi zao na mali zao mpaka dini ya Allah ikasimama. Aidha aliwakumbusha kuwa ilipofanyika Hijra ya Mtume (s.a.w), hawakuwa wanaume pekee, pia wa n a wa k e wa l i k u we p o katika vita zilizopiganwa akiwataja wake wa Mtume.

HABARI

SHAABAN 1434, IJUMAA JUNI 28 JULAI 4, 2013

AN-NUUR

BARAZA Kuu la Jumuia na Taasisi za Kiislamu nchini limezindua rasmi Ofisi ya Baraza Kuu la Wanawake, itakayoshughulikia kazi za Wanawake wa Kiislamu nchini. Uzinduzi huo umefanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Mwembechai, jijini Dar es Salaam ambako ndipo zilipo Osi hizo. Katika haa ya uzinduzi wa ofisi hiyo, wanawake wa Kiislamu wametakiwa kuipigania dini yao kwa gharama yoyote hasa katika kipindi hiki kigumu, ambapo dini na wana dini wanaandamwa na aina nyingi za maadui. Amiri wa Vijana Sheikh Shaaban Mapeyo, katika uzinduzi wa osi hiyo alisema kuwa makari walichelewa kujua nafasi ya mwanamke katika jamii, wakati hayo Mtume aliyajua tangu enzi za Mitume na akajua umuhimu wa mwanamke katika kuleta maendeleo katika jamii, ndio maana kina Bi. Khada, walikuwa na nafasi kubwa katika kuisaidia dini kusonga mbele. Leo hii makafiri ndio wanagundua kuwa mwanamke anatakiwa kuwa na haki sawa na mwanaume, ndio pale wanapokuwa na msemo wao kuwa ukiona mwanamme ana maendeleo ujue kuna mwanamke nyuma ya k e . L a k i n i Wa i s l a m u wanajifunza kutoka kwa Mtume Muhammad (s.a.w) na kwa mke wake Khadah, jinsi alivyopigania dini ya

BAADHI ya wanawake wa Kiislamu wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa osi ya Baraza la Wanawake Tanzania mwishoni mwa wiki iliyopita jini Dar es Amesema ukisoma katika tarekhe, inatuonyesha kuwa m wa n a m k e a l i k u wa wa kwanza kufa shahidi, hali inayoonyesha umuhimu wao kushiriki katika maendeleo. Alisema Bi. Khada, mke wa Mtume ambaye alikuwa tajiri mkubwa, baada ya kuolewa tu na Mtume, alitoa pesa yake yote kumpa Mtume kwa ajili ya kuisimamia dini ya Allah (s.w). Aidha alisema kazi kubwa aliyoifanya Bi. Khada, ndio leo hii Uislamu unaonekana kusambaa duniani kote, ikiwa ni matokeo ya juhudi kubwa aliyoifanya mwanamke yule. Pia ukisoma katika tarekhe, mtu wa mwanzo kumfuata na kumuamini Mtume, alikuwa ni mwanamke. Sheikh Abdallah pia alionyesha jinsi wanawake walivyo na nafasi katika kuleta maendeleo, pale alipomzungumzia mke wa Nabii Ibrahim, Mama yake na Ismail yaani Bibi Hajra. Nabii Ibrahim alipomchukua na kumuacha katika jangwa bila maji wala chakula, ndipo pale aliposema B i b i H a j r a k u m wa m b i a Mtume kuwa kama hilo ni agizo kutoka kwa Allah, basi yeye yuko radhi katika hilo. Hizo ni harakati walizofanya wanawake enzi za Mitume pamoja na nafasi zao. A k i wa s h u k u r u wa l e waliotoa michango yao ya hali na mali kufanikisha kupatikana osi hiyo, Ukht. Mayasa Sadallah, ambaye ni Katibu wa Baraza, akiwashukuru Waislamu waliochangia Baraza hilo hivi karibuni katika ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni ambapo shilingi milioni 12 zilitolewa kama ahadi na milioni moja taslim zilikusanywa. Hivyo amewaoba Waislamu wote walioahidi kutoa michango yao wajitahidi kuitoa ili kufanikisha malengo yaliyopangwa. Aidha amewakaribisha kina mama wa Kiislamu katika Osi yao mpya. Ukhy Mayasa amewakumbusha pia kina mama kuhudhuria mkutano wa baraza hilo unaoanza leo mkoani iringa Darul uloom. Mkutano huo hufanyika kwa mwaka mara moja, ili kujadili changamoto pamoja na mafanikio, pia mikakati waliojiwekea kuyaingiza katika utekelezaji, mkutano huo unaohudhuriwa na viongozi wa baraza hilo pamoja na Maamirat kutoka mikoa yote ya Tanzania.

Jumuiya ya wataalamu wa Kiislamu ( TAMPRO) kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Inakukumbusha Collection Campaign kuchangia Nguo na viatu vilivyo katika hali nzuri kwa ajili ya Jamii zetu zilizo vijijini. Kukusanya piga Simu 0786 665 375/ 0712 665 375 au ka osi zote za TAMPRO Mikoani.

Collection Campaign

Walimu Ridhwaa Seminary wapewa zawadi


Na Mwandishi Wetu B a r a z a l a Wa d h a m i n i Masjid Ridhwaa, uliopo Kinondoni Mkwajuni Jini Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita lilitoa pongezi na motisha kwa walimu na wafanyakazi wa shule ya Seminari ya Ridhwaa, kufuatia kupata matokeo mazuri ya kidato cha sita katika mwaka huu. Hafla hiyo imefanyika shuleni Ridhwa Seminary mwishonbi mwa wiki ambapo Mwenyekiti wa Baraza hilo Mzee Ramadhani Swalehe Tarish, alisema kuwa wamefarijika sana ndio maana wameamua kuwapa pongezi walimu na wafanyakazi wengine wa shule hiyo kwa matokeo mazuri ya kidato cha sita huku yale ya kidato cha nne yakionekana kuwa ni ya kutia moyo. Tunawomba na kuwasihi mkazane na kuongeza juhudi ili kupata matokeo yaliyo bora zaidi ya haya katika mtokeo yajayo. Bw. Msonde Tarish ambaye kitaaluma ni mtaalamu wa mambo ya uchumi kwenye fani ya masoko (Marketing), kufuatia matokeo ya kidato cha sita yaliyotangazwa hivi karibuni na Naibu Katibu M t e n d a j i wa B a r a z a l a Mitihani ya Taifa (NECTA) kati ya wanafunzi 43 waliofanya mtihani huo, wanafunzi 42 walifaulu na mmoja tu ndiye aliyefeli. A l i o n g e z a k u wa k wa matokeo hayo, vijana 40 waliohitimu wataweza

kujiunga na vyuo vikuu mbalimbali. Kwa matokeo haya vana wetu 40 watakwenda kusoma shahada ya kwanza mbalimbali na wawili watakwenda kusoma Diploma, mmoja tu ndio amefeli, hata hivyo shule yetu imekuwa ya 10 kati ya shule 31 za mkoa wa Dar es salaam na imeshika nafasi ya 70 kati ya shule 369 za Tanzania nzima. Haya ni mafanikio mazuri sana kwa shule, vana wetu na jamii ya Tanzania kwa ujumla, alisema Tarishi. Akizungumza kwa niaba ya B a r a z a Wa d h a m i n i , Mwenyekiti huyo alisema pamoja na kwamba zawadi walizotoa ni ndogo, lakini Inaendelea Uk. 8

Habari za Kimataifa/Tangazo

SHAABAN 1434, IJUMAA JUNI 28 JULAI 4, 2013

AN-NUUR

Hollande kupambana na chuki dhidi ya Uislamu


Mwanamke Mwislamu mjamzito ahujumiwa
Kaskazini mwa Ufaransa. Viongozi wa Muungano wa Taasisi za Kiislamu nchini Ufaransa (UOIF), wamesema katika mkutano wao na waandishi wa habari kwamba, chuki na uadui dhidi ya Waislamu limekuwa jambo la kawaida nchini humo na kuwataka viongozi wa serikali ya Paris, kuvunja kimya chao na badala yake kukabiliana na vitendo hivyo viovu. Nalo Baraza la Utamaduni la Waislamu nchini Ufaransa (CFCM) limetangaza kuwa, zaidi ya Misikiti kumi imeshavunjiwa heshima tangu kuanza mwaka huu wa 2013. Katika siku za hivi karibuni nchini Ufaransa kumeshuhudiwa ongezeko kubwa la hujuma dhidi ya wanawake Waislamu wanaovaa habu, mitandio au burka. Wiki iliyopita mwanamke wa Kiislamu aliyekuwa amevaa habu, alishambuliwa na magenge ya kibaguzi ya Wanazi mamboleo katika kitongoji cha Argenteuil jini Paris. Imefahamishwa kuwa mwanamke huyo aliyekuwa na umri wa miaka 21, alikuwa na mimba ya miezi minne ambayo aliipoteza kufuatia hujuma hiyo. Wakili wake anasema alishambuliwa barabarani na watu ambao walaribu kupasua mtandio wake huku wakimpiga mateke tumboni. Kufuatia kitendo hicho cha kinyama, watu wa l i o k u wa n a h a s i r a waliandamana mbele ya osi za Meya wa Argenteuil, kulalamikia ongezeko la hujuma za magenge ya Wanazi mambo-leo dhidi ya Waislamu. Meya wa mji huo amelaani hujuma hiyo na kusema hatakubali chuki

PARIS Rais wa Ufaransa Francois Hollande, ameahidi kupambana na vitendo vya kiadui na chuki dhidi ya wafuasi wa dini ya Kiislamu nchini humo. Akizungumza mbele ya h a l a i k i k u b wa ya wawakilishi wa taasisi na asasi za kiserikali na kiraia pembezoni mwa ji la Paris, Rais Hollande amesisitiza kuwa vitendo vya chuki na ubaguzi, hasa dhidi ya Waislamu vinapaswa kukomeshwa. Miongoni mwa vitendo vya chuki na uadui dhidi ya wafuasi wa dini ya Kiislamu mwaka huu, ni mashambulizi kadhaa yaliyofanywa dhidi ya wanawake waliovaa habu katika eneo la Val- dOise,

MFANYAKAZI wa zamani wa Idara ya Ujasusi Marekani (CIA), Edward Snowden, ambaye anatafutwa na taifa hilo kwa kosa la uhaini kufuatia kutoa taarifa za siri juu ya mpango wa Marekani kuhusu uchunguzi wa matumizi ya mawasiliano ya ki elektroniki, hadi sasa haulikani alipo, licha ya duru nyingi kuendelea kutaja kuwa bado yupo nchini Urusi. Rais wa Urusi, Vladimir Putin, ambaye yupo kimya hadi sasa kuhusu suala hilo la Snowden, huenda akalizungumzia wakati wa ziara yake katika ji la Turku nchini Finland, ambako anataraji kufanya mkutano na vyombo vya habari. Rais wa Marekani Barack Obama, amesema serikali yake itatumia njia zote za kisheria kuhakikisha inamtia nguvuni mfanyakazi huyo wa zamani wa CIA. Jumanne hii kulikuwa na taarifa kwamba Snowden yupo nchini Urusi, ambapo Serikali ya Marekani iliiomba Moscow kushirikiana nayo katika kumsarisha nchini Marekani jasusi huyo wa zamani wa kituo cha Ujasusi CIA, ili kujibu tuhuma dhidi yake. Msemaji wa Usalama wa Taifa nchini Marekani, Caitlin Hayden, amefahamisha kuwa kutokana na ushirikiano wa mataifa

Marekani yazidi kuhangaika na jasusi Edward Snowden


hayo mawili ulioimarika tangu kutokea mlipuko jini Boston wakati wa mbio za Marathon, na utekelezwaji wa usarishaji wa wahalifu wakuu, kuna matumaini makubwa kwamba serikali ya Urusi itamfukuza Edward Snowden nchini Marekani ili akapambane na mahakama. Msemaji huyo alieleza kusikitishwa na hatua ya s e r i k a l i ya H o n g K o n g kumuacha Snowden kuelekea Urusi, licha ya ombi halali la Marekani la kutaka kukamatwa kwake kama unavyoruhusu mkataba wa ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili. Hayden amesema wamewasilisha lawama zao kwa Hong kong na serikali ya China kupitia njia za kidiplomasia na kufahamisha kuwa, uamuzi kama huo unaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa uhusiano uliopo kati ya Marekani na Hong Kong na Marekani na China. Bw. Edward Snowden, anatafutwa na Marekani kufuatia kuvujisha taarifa za siri dhidi ya taifa hilo kwamba limekuwa likichunguza mawasiliano ya ki elektroniki. Taarifa zinaeleza kuwa Snowden, aliwasili Jumapili nchini Moscow akitokea Hong Kong, ambako alikimbilia na sasa anadaiwa kuwa anatafuta hifadhi ya kisiasa nchini Ecuador. Marekani imekuwa ikitaka kushikiliwa hati yake ya kusaria na kuomba

mfanyakazi huyo wa zamani wa CIA na Shirika la Usalama wa Taifa (NSA) kuzuiliwa kundelea na safari yake. (www. r.fr)

BRASILIA Rais Dilma Rousse wa Brazil, ameelezea uamuzi wa serikali ya nchi hiyo wa kuitisha kura ya maoni juu ya marekebisho ya kisiasa nchini humo. Rais Rousse amesema kuwa, serikali ya Brazil imeamua kuitisha kura hiyo ya maoni kwa lengo la kukomesha maandamano d h i d i ya s e r i k a l i n a machafuko ya kijamii yaliyoikumba nchi hiyo. Mara baada ya kufanya mazungumzo na magavana, Mawaziri na Mameya wa mi yote nchini humo, Rais Rousse ameongeza kuwa suala la

Rais Rousseff wa Brazil kuitisha kura ya maoni

kutekelezwa dhidi ya Uislamu au (Islamophobia) katika mji huo. Hata hivyo Waislamu wanasema makundi ya Wanazi mamboleo, yameonekana mjini humo na kwamba hakuna hatua zozote za kisheria zinazochukuliwa dhidi yao.

kufanyika marekebisho ya kisiasa limekuwa likipewa kipaumbele na serikali na kusisitiza kuwa, hivi karibuni watachaguliwa wajumbe wa jopo litakalokuwa na jukumu la kutayarisha mchakato wa mabadiliko ya kisiasa nchini humo. Wananchi wa Brazil wamekuwa wakiandamana wakipinga gharama kubwa za kuandaa fainali za kombe la dunia mwaka 2014 nchini humo, wakitaka serikal iboreshe kwanza hali ya maisha na huduma za umma kwa wananchi.

Ahlul Daawa Hajj And Travel Agency


INAPENDA KUWA TAARlFU MAHUJAJI WAKE WOTE NA WAISLAMU KWA JUMLA KUA:IDADI YA MAHUJAJI WAO WA MWAKA HUU 2013 IMEPUNGUZWA KUTOKA MIA TATU MPAKA MIA MOJA NA SABINI TU. KWA HIVYO;(a) WALE WOTE W ALIOJIANDIKISHA W A WAHl KUMALIZA KULIPIA GHARAMA ZAO. (b) W ALIOJIANDIKISHA TU NA HAW AJALIPIA W AJE KULIPIA AU TUT A WAONDOSHA KWENYE ORODHA NA KUW APA NAFASI W ALIOKUW A TAYARI. (c) KUWASILISHA PASSPORT AU KOPI ZA PASSPORT KWA MUDA HUU. (d) PICHA MBILI PASSPORT SIZE KW A AJILI Y A VISA. 2. (a) BEl YETU NI US DOLA 3550 TU. (b) UKIWAHI KULIPIA SA SA NA KUMALIZA TARATlBU ZOTE PUNGUZO NI ASILIMIA SITA KWA HIVYO UT ALIPIA US DOLA 3337 TU NA KABLA Y A TAREHE 5 AUGUST 2013. 3. KWA MAWASILIANO ZAIDI FIKA OFISINI KWAO;(a) DAR ES SALAAM MTAA W A DOSI NA MKADINI NYUMBA NAMBA 26 MKABALA NA SHOW ROOM Y A MAGARI TEL 0713 730444 AU 0785 930444 AU 0773 930444. (b) ZANZIBAR MTAA WA RAHA LEO TEL 0777484982 AU 0777413987 AU WASILIANA NA. ( c) MAALIM SElF HUMOUD KIJICHI ZANZIBAR TEL 0777417736. (d) ABDALLA SALEH MAZRUI (HOKO) TEL 0715724444 AU 0773 724444 AU 0784 724444 (e) SALIM IS-HAQ DAR ES SALAAM TEL 0754286010 AU 0774786101 KW A BEl NAFUU KULIKO WOTE NA HUDUMA BORA KULIKO WENGI USISAHAU AHLUL DAAWA HAJJ AND TRAVEL AGENCY

TANGAZO

SHAABAN 1434, IJUMAA JUNI 28 JULAI 4, 2013

AN-NUUR

7
Na Mwandishi Wetu
INGAWA si kawaida, lakini naomba nianze makala yangu na hitimisho, badala ya utangulizi. Kwamba pendekezo la mfumo wa Muungano wenye Serikali tatu (Shirikisho), la Tume ya Marekebisho ya Katiba ya Jaji Joseph Warioba, ndiyo mfumo sahihi unaotakiwa chini ya Mkataba wa Muungano, uliotiwa sahihi na waasisi wake, Mwalimu Julius Nyerere wa Tanganyika na Sheikh Abeid Amani Karume wa Zanzibar, Aprili 22, 1964. Kwa mantiki hiyo, ilichofanya Tu m e ya J a j i Wa r i o b a , s i kupendekeza mfumo mpya, bali ni kurejesha mfumo sahihi uliovurugwa kibabe tofauti na kile kilichokusudiwa chini ya M u u n g a n o h u o , k a m a tutakavyoona katika makala haya. Kwa hili, hakuna kipya kilichoanzishwa na Tume, mbali na kutukumbusha tu kile kilichokusudiwa chini ya Muungano huo wa nchi mbili hizo. M k a t a b a wa k i m a t a i f a uliofikiwa kwa HIYARI kati ya nchi mbili zilizokuwa huru; Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, juu ya ushirikiano kwa mambo kadhaa chini ya masharti MAALUM, unajulikana kama Mkataba wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Makala/Tangazo

SHAABAN 1434, IJUMAA JUNI 28 JULAI 4, 2013


Rais wa Tanganyika ambaye alikuwa Rais wa Kwanza wa Muungano, kuwa Rais wa Tanganyika na pia Rais wa Muungano, chini ya Katiba ya Tanganyika iliyorekebishwa, hadi Muungano utakapopata Katiba yake. Ilivyotokea ni kwamba si Tume ya kupendekeza Katiba iliyoteuliwa, wala Bunge la Katiba lililoitishwa na hivyo, kwa kipindi cha miaka 13 mfululizo tangu 1964, Muungano uliendeshwa kwa Katiba ya muda hadi mwaka 1977 ilipotungwa Katiba ya sasa ambayo uhalali wake unahojika, kama nilivyoeleza hapo juu. Zipo kumbukumbu na ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa Tume ya Katiba haikuundwa kutokana na mfarakano baina ya Waasisi wa Muungano, kutokana na Mzee Karume kuamini kuwa aliingia Mkataba wa Muungano wenye Serikali tatu. Ndiyo maana, kadri Mwalimu alivyokuwa akizidi kusisitiza Muungano wenye Serikali mbili, Mzee Karume aliona kama amesalitiwa; na si mara haba alisikika akisema kuwa Muungano umembana kama koti, na hivyo uvunjwe! Kwa upande wake, Mwalimu, kwa kuchoshwa na vitisho vya Karume, alinukuliwa akisema; kama Wazanzibari kwa nia njema, na bila ya kurubuniwa

AN-NUUR

Mkataba huo ndio uliozaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa nchi mbili hizo kujivua mambo hayo tu kila upande (maarufu kama Mambo ya Muungano), na kuyaingiza kwenye kapu moja lililoundiwa Serikali ya kuyasimamia, maarufu kama Serikali ya Muungano, na kuziacha nchi hizo kubakia na mamlaka mengine, kwa yote yasiyo ya Muungano. Mambo kumi na moja (11) kwa mujibu wa Ibara ya 5 ya Mkataba huo ni pamoja na; (a) Katiba na Serikali ya Jamhuri ya Muungano; (b) Mambo ya Nje; (c) Ulinzi (si Ulinzi na Usalama kama ilivyo sasa); (d) Polisi; (e) Mamlaka juu ya Hali ya Hatari; (f) Uraia; (g) Uhamiaji; (h) Biashara ya Nje na Mikopo; (i) Utumishi wa Umma katika Jamhuri ya Muungano; (j) Kodi ya Mapato kwa watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa; (k) Bandari, usari wa anga wa kiraia, posta na simu za maandishi (Telegraphs). Kuthibitisha kwamba Ta n g a n y i k a n a Z a n z i b a r hazikufa kufuatia kuzaliwa kwa Jamhuri ya Muungano, angalia

Kupinga Serikali tatu ni kusaliti Muungano asilia


matakwa machache yafuatayo ya Mkataba wa Muungano. Sote tunafahamu namna Muungano huo ulivyofikiwa kwa njia ya dharura kwa shinikizo la mataifa makubwa katika kuokoa hali ya kisiasa Zanzibar. Kwa dharura hiyo, Muungano ulianzishwa bila maandalizi ya Katiba. Kwa hiyo, iliwekwa wazi ndani ya Mkataba huo (Ibara ya 6) kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano, kwa makubaliano na Makamu wa Rais, ambaye pia ndiye Mkuu wa Serikali ya Zanzibar; (a) Atateua Tume ya Kupendekeza Katiba ya Jamhuri ya Muungano; (b) Ataitisha Bunge la Katiba likihusisha wawakilishi kutoka Tanganyika (na si Tanzania wala Tanzania Bara, majina ambayo si ya Kikatiba) na kutoka Zanzibar kwa idadi watakayoona inafaa ndani ya mwaka mmoja kutoka siku ya Muungano, kwa ajili ya kujadili na kupitisha Katiba ya Jamhuri ya Muungano. Niharakishe kutamka mapema hapa kwamba huu ndio utaratibu unaotakiwa kufuatwa katika kupata Katiba ya Jamhuri ya Muungano, na

kwamba utaratibu uliotumika katika kutunga Katiba ya 1977 inayotumika sasa, kwa kuigeuza Tume ya Watu 20 ya vyama vya TANU na ASP iliyopendekeza kuunganishwa kwa vyama hivyo na kuzaa Chama cha Mapinduzi (CCM), na kuwa Tume ya kupendekeza Katiba iliyopo sasa, ni batili kwa mujibu wa matakwa ya Mkataba wa Muungano. Hivi kwamba uhalali wa Katiba hiyo, iliyozaliwa kwa utaratibu batili, unahojika. Tume ya sasa ya Jaji Warioba, imezingatia matakwa ya Mkataba h u o wa M u u n g a n o , k a m a yalivyobainishwa kwenye Ibara ya 7 (a) na (b) ya Mkataba. Na kwa kuwa ilikuwa dhahiri kwamba kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu siku ya Muungano, Muungano huo usingekuwa na Katiba, ilikubaliwa kwa mujibu wa Ibara ya 2, 3, 4 na 6 ya Mkataba wa Muungano, kwamba Katiba ya Tanganyika itumike kwa muda kama Katiba ya Muungano, kwa kuingiza katika Katiba hiyo, mambo yote kumi na moja (11) ya Muungano; na hivyo kumfanya (kwa muda)

Inaendelea Uk. 9

8
kutoka nje, wataona Muungano unawabana na hivyo hawauhitaji tena, asingewapiga mabomu kuwalazimisha kuendelea na Muungano huo. Na katika kipindi hicho hadi sasa, marekebisho lukuki yenye kuleta kero na mkanganyiko kwa Muungano yalifanyika kiimla kwa chukizo na mitafaruku ndani ya Muungano. Kwa mfano, kitendo cha kuongeza mambo ya Muungano kutoka kumi na moja ya kimkataba hadi 23, ni ukiukaji dhahiri wa Mkataba huo wa kimataifa pamoja na sheria mbili za Muungano (Acts of Union) za mwaka 1964, zilizohalalisha utekelezaji wa Muungano huo kwa misingi ya Mkataba wa Muungano. Ukiukaji huo wa Makubaliano ya Muungano, bila hofu ya k u h o j i wa , n a a m b a o k wa sehemu kubwa ulifanyika kwa ubabe wakati wa utawala wa Chama kimoja kushika hatamu za uongozi wa nchi, umejenga imani potofu kwamba Serikali ya Muungano inaweza kunyakua na kujiongezea mamlaka yoyote inayofikiri inafaa kufanya hivyo, ambayo vinginevyo ni mamlaka ya nchi za Tanganyika na Zanzibar. Haya yamewezekana kutokana na sababu kuu mbili. Mosi, ni kwa wananchi kuchwa Mkataba wa Muungano, na hivyo tafsiri ya Muungano kuwa haki ya wahadhina wachache wa kisiasa, tena kwa kupotosha kwa maslahi yao binafsi. Pili, ni ubabe chini ya utawala wa Chama kimoja, ambapo kuhoji Muungano lilikuwa kosa kubwa linalokaribia uhaini. R a i s wa a wa m u ya p i l i wa Zanzibar, Sheikh Aboud Jumbe, mwaka 1984, alitaka ufafanuzi juu ya ni upi mfumo sahihi wa Muungano, lakini, licha ya kwamba alitumia haki yake hiyo ya Kikatiba kuhoji, alivuliwa nyadhifa zote za uongozi wa Chama, Muungano na Visiwani. Dalili za ubabe huo uliozoeleka kutaka kujirudia, zimeanza kujionyeha tunapoambiwa kwamba Kamati Kuu ya CCM, hivi karibuni imeketi na kuazimia kukataa pendekezo la Muundo wa Serikali tatu, na kutaka Muundo wa Serikali mbili uendelee, pengine ama kwa makusudi au kwa kutoelewa kuwa wanakiuka matakwa ya Muungano; au kwa kuelewa lakini bado wakiamini kwa kujidanganya kwamba Watanzania bado wamelala juu ya jambo hili. Ubabe huo wa kichama, ukiruhusiwa kujirudia, unaweza kukaribisha machafuko ya kisiasa yanayoepukika, na hata kuvunja Muungano wenyewe. Wanasiasa wetu wanapaswa kusoma vyema alama za nyakati na hisia za wananchi, na si hisia za viongozi, na kuoanisha kwa makini kero za Muungano ambazo zimeyumbisha Muungano wetu tangu uanzishwe miaka 49 iliyopita ili kuiepushia nchi mitafaruku ya kisiasa. A i d h a , Wa t a n z a n i a wamechoka na kero za Muungano na mitafaruku yake.

Makala

SHAABAN 1434, IJUMAA JUNI 28 JULAI 4, 2013


mambo yake ya ndani yasiyo ya Muungano, kama ambavyo tu Zanzibar inavyosimamia mambo yake hivi sasa. Kwa kuwa, kwa mfano, uraia ni jambo la Muungano, hapatakuwa na Watanganyika wala Wazanzibari, bali raia wa nchi hizi watajulikana kama Watanzania. Vivyo hivyo, kwa kuwa Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Kimataifa ni jambo la Muungano, Tanzania, na si Tanganyika wala Zanzibar, zitakazofahamika kama nchi au Taifa kimataifa. Na ndivyo itakavyokuwa kuhusu Ulinzi na Usalama, kwamba kushambuliwa kwa Tanganyika au Zanzibar ni kushambuliwa kwa Tanzania. Tanzania, na si Tanganyika wala Zanzibar, ndiyo itakayokuwa dola na Rais wa Tanzania ataendelea kuwa Mkuu wa Vikosi vyote vya Ulinzi na Amiri Jeshi Mkuu. M a a d a m , Tu m e ya Marekebisho ya Katiba ya Jaji Warioba, kwa mujibu wa Ibara ya 1 (3) ya rasimu yake, imebainisha kwamba msingi mkuu wa mapendekezo ya marekebisho hayo, ni Mkataba wa Muungano ya m wa k a 1 9 6 4 , a m b a yo , kama tulivyoona, unatambua muundo wa Shirikisho lenye Serikali tatu, basi msingi huo uzingatiwe na kila mtu wakati wa kujadili rasimu hii ili tuweze kubakiza na kulinda Muungano uliokusudiwa. (Makala hii imetolewa kama ilivyopatikana katika moja ya mitandao ya kamii.)

AN-NUUR

Inatoka Uk. 7

Kupinga Serikali tatu ni kusaliti Muungano asilia


Ni bora wanasiasa wakaziacha sauti za wananchi zisikike katika mchakato huu wa Katiba Mpya. Kutokufa kwa Tanganyika na Zanzibar kama nchi huru, zenye mamlaka ya nchi kwa mambo yasiyo ya Muungano, kunathibitishwa na Ibara ya 5 ya Mkataba wa Muungano inayobainisha kwamba pamoja n a S e r i k a l i ya M u u n g a n o kubeba mambo kumi na moja ya M u u n g a n o , S h e r i a z a Tanganyika na za Zanzibar zilizopo na zitakazotungwa, zitaendelea kuwa na nguvu katika nchi husika. Sheria hizo ni nyingi, lakini itoshe tu kutoa mifano ya sheria mbili za mwaka 1971, miaka saba baada ya Muungano, zilizoendelea kutambua kuwapo na kutamka nchi ya Tanganyika kwa kuheshimu Mkataba wa Muungano. Moja ya sheria hizo ni Sheria ya Ndoa ya 1971, ambayo imetamka kote kuwa ni kwa ajili ya Tanganyika na kwa wakazi wa Tanganyika. Nyingine ni Sheria ya (muda) ukomo wa Madai (The Law of Limitation Act) ya mwaka 1971, ambayo inatamka wazi ni kwa ajili ya na katika Tanganyika pekee; na sheria nyingine nyingi. Kwa mantiki hiyo, kwanini isiwe kweli kwamba Muungano unaotakiwa na uliokusudiwa tangu mwanzo, ni wenye mfumo wa Serikali tatu, kwa maana ya Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar (ambazo hazikufa) na Serikali ya Shirikisho, kwa mambo kumi na moja tu ya Muungano? Lakini pia, Ibara ya 6 (a) ya Mkataba wa Muungano wa mwaka 1964, inatanabahi kuwa; Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano, atakuwa Mwalimu Julius Nyerere, na atatekeleza shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa mujibu na kwa kuzingatia matakwa ya Mkataba huo, kwa kusaidiwa na Makamu wa Rais wawili, Mawaziri na Ma-Osa wengine atakaowateua kutoka Tanganyika na Zanzibar. K wa m a e l e z o h a y o , n i kipofu gani atabisha kwamba Ta n g a n y i k a n a Z a n z i b a r hazikufa baada ya ujio wa Muungano? Wanaodai mfumo wa Serikali mbili, wanatoa wapi ujasiri potofu na wa kihadhina k u p o t o s h a u m m a j u u ya mfumo halali wa Muungano uliokusudiwa? Watuambie; kama Zanzibar ilisalimika, Tanganyika ilitowekaje? Katiba ya Muda ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1965, kwa kutambua uwepo wa Tanganyika hai, na kwa kuzingatia Mkataba wa Muungano, ilibainisha ifuatavyo katika ibara yake ya 13: Kutakuwa na Makamu wawili wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, ambapo mmoja atakuwa Msaidizi Mkuu wake kwa shughuli za kitendaji upande wa Zanzibar, na ambaye atajulikana pia kama Rais na Mkuu wa Serikali ya Zanzibar; na mwingine atakuwa Msaidizi Mkuu wa Rais kwa shughuli za kitendaji kuhusiana na Tanganyika. Tena Katiba hiyo hiyo, Ibara ya 20 na 24 (b) inasema: Rais atateua mkuu wa mkoa kwa kila mkoa ndani ya Tanganyika, na Bunge litakuwa na uwezo wa k u r e k e b i s h a i d a d i ya mikoa kwa Tanganyika na kwa Zanzibar Na kuhusu majimbo ya uchaguzi, Katiba hiyo ya Muda ya mwaka 1965, ikiwa ni mwaka mmoja baada ya Muungano, na iliyozingatia na kuheshimu m a t a k wa ya M k a t a b a n a Sheria za Muungano kabla ya kuchakachuliwa na wahadhina wa siasa za kibabe kwa njia ya marekebisho, katika Ibara ya 25 (1) na 25(3) inasema: Tanganyika itagawanywa katika majimbo kwa kuzingatia wakazi wa majimbo na kila jimbo litawakilishwa na mbunge mmojaTume ya Uchaguzi itapitia upya mgawo wa majimbo ya uchaguzi ya Tanganyika kila kipindi kisichopungua miaka minane, na kisichozidi miaka kumi Mara nyingi, ubabe uliotumika kufanyia marekebisho Katiba yetu kinyume na matakwa ya Muungano asilia, umefanywa

Walimu Ridhwaa Seminary wapewa zawadi


Inatoka Uk. 4 pamoja na udogo wake lakini inaamanisha jambo la shukrani hivyo kuomba wahusika waipokee kwa mikono miwili. Tungeweza kutoa zaidi ya hii, lakini wahenga walisema mtu hujikuna kadri ya mkono wake unapoka hata kama ni pipi muipokee, ndio kitu tulichokichagua kuonyesha furaha yetu kwenu ,alisisitiza Mwenyekiti huyo. Hata hivyo Bw. Tarish aliwakumbusha walimu na wafanyakazi wengine wa shule hiyo kwamba, pamoja na matokeo hayo waliyopata, kuna haja ya kuongeza bidii katika kutekeleza majukumu yao ipasavyo, ili kuleta ta na chachu zaidi ya mafanikio. Alitilia mkazo zaidi masuala ya nidhamu kwa walimu na wanafunzi wao. Aidha alisisitiza walimu kupambana vikali na tatizo la ucheleweji wanafunzi shuleni, kuongeza mkazo katika ufundishaji, kuzingatia usa wa shule na mazingira, mambo ambayo kwa pamoja yataleta ya mafanikio shuleni hapo na kwa jamii nzima ya Kiislamu. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Elimu ya Shule hiyo Alhaji Hassan Mnjeja, ambaye alikuwa mgeni rasmi wa tafra hiyo, alitoa kongole (pongezi) na shukurani za dhati kwa Uongozi wa Baraza la Masjid Ridhwaa kwa kutambua mchango wa wafanyakazi wa Taasisi hiyo, akisema kuwa kitendo cha kutoa zawadi ni motisha kubwa kwa walimu na wafanyakazi katika kuchapa kazi zaidi. Alhaji Mnjeja ambaye kitaaluma ni mwalimu, alisema motisha ni jambo la msingi sana kwa wafanyakazi kwani huwa ni kichocheo katika kutenda kazi zaidi na kutekeleza majukumu bila kusukumwa. Alisema motisha huwajenga walimu kisaikolojia kwa kufanya kazi zaidi huku wakitarajia kuungwa mkono zaidi. Alisisitiza umuhimu wa kufanyika mazoezi ya ukaguzi wa mara kwa mara kwa walimu na wafanyakazi wengine ili kuwakumbusha walimu juu ya majukumu yao. Naye Mkuu wa shule B w. A h m e d S o v u , k wa niaba ya walimu wenzake aliwashukuru Wadhamini kwa zawadi na kujali juhudi zao wanazozifanya katika kuhakikisha Seminari ya Ridhwaa inarudi katika historia yake iliyokuwa nayo siku za nyuma. Aidha aliwataka walimu

kwa maelekezo ya Chama Tawala, hata Chama hicho kukia kuwa sehemu ya Katiba ya Muungano wakati ikifahamika wazi kuwa vyama vya siasa si jambo la Muungano. Muundo wa Shirikisho lenye Serikali tatu uliokusudiwa chini ya Mkataba wa Muungano wa 1964, na ambao umependekezwa pia na Tume ya Katiba ya J a j i Wa r i o b a , n i m f u m o unaotambulika kimataifa chini ya Sheria za Kimataifa. Ni mfumo ambapo nchi zaidi ya moja huungana kwa mambo nyeti kadhaa, kama vile uraia, mambo ya nje, ulinzi na usalama, Polisi na kadhalika, na kuyaundia Serikali Kuu moja kuyasimamia, na kuziacha nchi husika kusimamia na kudhibiti mambo yake yote mengine yasiyo ya Muungano. Bila shaka, wakati Mwalimu Nyerere alipomwagiza M wa n a s h e r i a M k u u wa k e wa Serikali, Roland Brown, Aprili 19, 1964; aandae rasimu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa muundo na mfumo wa uhusiano wa Serikali ya Uingereza na Serikali ya Ireland Kaskazini, alikuwa na maana ya Muungano aina ya Shirikisho kama nilivyoeleza hapo juu. Chini ya mfumo huo, na kama ilivyopendekezwa na Tume ya Jaji Warioba, Tanganyika na Zanzibar zitasimamia

Inaendelea Uk. 9

kufundisha hasa kwani ndiyo kazi waliyoajiriwa kwayo. Wa l i m u f u n d i s h e n i , ndiyo kazi yenu na mkichapa kazi mtaona faida yake kwani mtaitangaza shule yenu na nyie wenyewe mtakuwa na soko zaidi. Huko ndiko kuupiganiaUislamu na jamii ya Kiislamu. Alisaa mkuu huyo wa shule. A l i s e m a k u wa h a t u a za kinidhamu zitaendelea kuchukuliwa kwa walimu na wafanyakazi wengine, ambao watashindwa kutekeleza majukumu yao ya kufundisha kwa vizingizio mbalimbali ambavyo havina ta kwa taasisi ya Ridhwaa Seminari. Aidha Walimu wa seminari hiyo nao waliwashukuru wadhamini kwa kutambua mchango wao na kuwapa motisha. Mwalimu Mwandamizi wa Taaluma wa shule hiyo Bw. Tanu Kamaze, alisema kwa kawaida zawadi ina pande mbili, moja ni furaha na upande wa pili ni changamoto. Hivyo upande wa c h a n g a m o t o n i wa l i m u kuchapa kazi zaidi na akasisitiza kuwa idara yake itaendelea kuwakumbusha walimu wote wajibu wao huo.

9
Na: Mujahid Mwinyimvua
WIKI iliyopita tulikumbushana takwimu zinazoonyesha ukubwa wa tatizo la lishe isiyofaa hapa Tanzania ambayo inasura mbili. Sura ya kwanza ni pale ambapo watu wanapokosa kula chakula kinachotosheleza mahitaji ya mwili, ambapo matokeo yake hasa kwa watoto ni kudumaa au hata vifo. Sababu kubwa ya ukosefu wa c h a k u l a n i u m a s i k i n i wa kipato ambapo mtu au familia inashindwa kuzalisha au kununua chakula cha kutosha. Moja ya sababu ya umasikini wa kipato ni uvivu na kutokuwajibika. Sura ya pili ya lishe isiyofaa a m b a yo i n a j i t o k e z a z a i d i kwa watu wanaoishi mijini, ni pale ambapo watu sio tu wanamwaga vyakula bali pia wanakula sana na kupekea kuugua magonjwa kama vile kisukari, kansa, kiharusi, shinikizo la damu magonjwa ya moyo, na ukusofeu wa nguvu za kiume na kike. Tatizo la shibe iliyopitiliza na kumwaga vyakula linasababishwa na uchoyo na kukosa elimu ya lishe. Leo tutatazama namna Uislamu unavyo himiza wa t u k u j i t u m a k a m a n j i a ya kupambambana na njaa inayoletwa na umasikini wa kipato, na hatimae kuondo lishe isiyofaa. Uislamu umeleweka vibaya Ni ukweli usiotaka utafiti wa kisayansi kuwa baadhi ya watanzania wakiwemo waislamu ni wavivu na hawafanyi kazi iwe ya kilimo au shughuli zingine. Msiba mkubwa hata baadhi ya waliobobea elimu ya Qur an na Sunnah hawataki kufanya kazi, wanaishi kwa kubangaiza tu. Kazi za kilimo, ufugaji au zile za ujuzi kama seremala au ushonaji wanaona ni laana, wakati mitume mbalimbali walifanya sana kazi hizo. Mwenyezi Mungu akipenda funga ya Ramadhani itaanza baada ya siku kumi zijazo. Tutakuja kuona baadhi ya waislamu hasa katika miji wanakopa ili wanunuwe futari na hana habari tena ya kulipa madeni hhayo. Au waislamu wengine watatumia uwongo ili wapate fedha za chakula cha futari na daku. Kibaya zaidi, kama ilivyolezwa katika tovuti ya Alhidaya kuwa baadhi ya waislamu (waliomasikini) wanajaribu kuonyesha kuwa, kuipa nyongo dunia ni mtu kuishi kimasikini, na umasikini ni miongoni mwa sifa za ucha Mungu, na baadhi yao wanaona kuwa umasikini ni moja miongoni mwa Sunnah za Mtume Muhammad (Rehma na Amani za Mwenyezi Mungu zimkie) kwani kiongozi huyo alikuwa masikini na ilikuwa inapita siku tatu nyumbani kwake hakukokwi moto kwa mujibu wa maelezo ya Mama wa Waumini Aaishah (Radhi za Mwenyezi Mungu zimkie). Mtizamo huo sio sahihi hata kidogo, kama tutakavyokuja kuona katika makala haya baadae kidogo, in Shaa Allah. Hali katika mkoa wa Lindi Tutazame hali ya mkoa wa Lindi kama mfano wa hali mbaya katika mikoa au maeneo yenye waislamu wengi hapa nchini, ili tuelewe vizuri hoja yetu ya Uislamu kueleweka vibaya. Gazeti la MAJIRA la Februari 16, 2013, ambalo taarifa yake ya hapa chini kwa kiasi fulani

Makala

SHAABAN 1434, IJUMAA JUNI 28 JULAI 4, 2013


zaidi hapa Tanzania na wengi wao hawajitumi. Katika mwezi unaokuja wa Ramadhani, nguvu zielekezwe katika mapambano dhidi ya umasikini wa kipato na ule wa kikra, na kila msikiti uandae mpango kazi wake. Pia kila msikiti lazima uwe na kamati na kuanza kutafuta ardhi nje ya mji na kuanza mradi wa kilimo na ufugaji. Ili ikikia Ramadhani ingine watu wapate futari kutoka shambani kwao. Na vilevile wanyama wa kuchinjwa katika msimu wa Hja ya mwakani (2014/2015) watoke katika shamba la msikiti. Bila ya hivyo, omba omba tunaowaona leo katika misikiti ya mijini wataongezeka na hatutaweza kuwanusuru ndugu zetu hao ambao wengi wao ni kina mama na watoto zao. Baadhi ya kinamama hao ni wajane au wamekimbiwa na waume zao kwa sababu mbalimbali ikiwemo maisha magumu. Tu m u o m b e M w e n y e z i Mungu atukutanishe wiki ayo ili tuone namna Qur an na Sunnah zilivyoelekeza maswala ya vyakula, lishe na ujenzi wa afya bora.

AN-NUUR

wameitoa kutoka katika Utati wa Kidemografia na Afya Tanzania, kwa kimombo unaitwa Tanzania Demographic and Health Survey, inasema kuwa Mkoa wa Lindi ni miongoni mwa mikoa 30 ya Tanzania ambapo una jumla ya watu 596,760, na inakadiriwa asilimia 51 ya watu wake wako katika kiwango cha chini cha umaskini cha Taifa. Pia, kwa hali ya lishe mkoa wa Lindi ni mkoa wa pili kwa watoto wenye udumavu kwa asilimia 54, ukiongozwa na mkoa wa Dodoma wenye watoto asilimia 56 wenye udumavu. Mkoa huo pia, una watoto wa umri wa miezi 0-59 ambao wana uzito pungufu kwa asilimia 23.7, watoto wa umri wa miezi 0-59 wana anemia (upungufu wa damu mwilini) ambao sawa na asilimia 76.8. Gazeti hilo linazidi kuandika kuwa mkoa wa Lindi ni miongoni mwa mikoa yenye fursa nzuri ya kilimo, huku wilaya ya Ruangwa wakitumia ardhi kwa kilimo kwa asilimia 34 tu, huku wakiwa na eneo la hekta 4332 la kilimo cha umwagiliaji ambapo kati ya hizo hekta 80 tu ambayo sawa na asilimia 1.8 ambazo kwa sasa ndo zinatumika kwa kilimo cha umwagiliaji. Pamoja na mkoa huo kutegemea kilimo kama shughuli kuu za kiuchumi, wanawake wanaonekana kuwa wazalishaji wakubwa lakini wanaume wanaonekana kuwa wasimamizi na wamiliki wa mazao hayo baada ya mavuno, matatizo ya kinsia (kama talaka) ni tatizo kubwa linalojitokeza kipindi cha mavuno ambapo wanaume wengi wanaoa wake wengine baada ya kuona wana mazao mengi. Hali hiyo huchangia kaya n y i n g i z i n a z o o n g o z wa n a wanawake kukosa chakula cha kutosha cha kulisha kaya zao kutokana na chakula kingi kuchuliwa na wanaume. Kwa mkoa huu kaya masikini zenye watoto wa umri wa miezi 6-24 wanapata tatizo la kula mlo wa aina moja katika kipindi cha kilimo. Uislamu na vita dhidi ya umasikini wa kipato Msomi mashuhuri katika u l i m w e n g u wa k i i s l a m u , Profesa Muhammad Qutb katika kitabu chake cha Islam the Misunderstood Religion (Uislamu ni Dini Iliyofahamika Vi b a ya ) a m e o n y e s h a v ya kutosha namna gani Dini ya Kiislamu ilivyoeleweka vibaya kwa waislamu wenyewe na wasiokuwa waislamu. Kuwa na tabia ya uvivu, kudharau kazi za halali na kuwa mbangaizaji, mkopaji asielipa, na kuona kuwa mtu kuwa masikini ndio ucha Mungu ni mambo yaliyokinyume na Uislamu. Turejee tena hapa chini ushahidi uliobainishwa na tovuti ya Alhidaya kuhusu hoja tulizozieleza hapo juu. Vilevile, tovuti hiyo ikabainisha namna Uislamu unavyofundisha ili kuukabili umasikini wa kipato. Uislamu ni Dini ya kazi ni Dini ya kuimarisha na kustawisha ardhi kama Alivyotuamrisha Allaah. Uislamu si Dini ya omba omba na mtu akawa kila mwaka anasubiri Zakaah na Swadaqah tu, hana kazi yoyote, bali tabia hiyo imekemewa vikali na Mtume (Rehma na Amani

Mlo bora kwa aliefunga saumu-2


za Mwenyezi Mungu zimkie) aliposema: Hatoacha mtu kuomba watu mpaka ataletwa siku ya Qiyaamah na uso wake ukiwa hauna kipande cha nyama. (AlBukhaariy na Muslim). Pia, Mtume (Rehma na Amani za Mwenyezi Mungu zimfikie) amehimiza watu kufanya kazi katika hadithi zifuatazo: Hajawahi mja kula chakula chenye kheri kuliko kile alichokichuma kwa mkono wake (Al-Bukhaariy). Mmoja wenu kubeba kuni mgongoni mwake, ni bora kuliko kumuomba mtu ampe au amnyime (Al-Bukhaariy na Muslim). Alhidaya pia, inatukumbusha kwa kusema kazi ndio msingi mkuu wa chumo la halali, na ndio nyenzo muhimu aliohimizwa binadamu katika kuijenga ardhi. Na Mwenyezi Mungu akaidhalilisha ardhi kwa ajili ya matumizi na faida ya mwanaadamu. Aidha, ardhi ndio msingi mkuu wa riziki kwa wanaadamu, na kama mwanaadamu ataitumia vizuri na kwa uadilifu basi utajiri wote umo ardhini, kama vile mazao, chakula, madini ya chuma na mengine, gesi asilia, mafuta, ujenzi wa miundo mbinu, n.k. Mwenyezi Mungu anasema katika Qur an: Yeye ndiye Aliyejaalia ardhi iweze kutumika (kwa kila myatakayo) kwa ajili yenu, basi nendeni katika pande zake zote na kuleni katika rizki zake (Surat Mulk; 67:15). Ni dhahiri kua, aya na hadithi za hapo juu na nyingine ambazo hatukuzitaja kutokana

n a n a f a s i m k u wa n d o g o , zinaonyesha kuwa Uislamu sio dini ya kivivu wala ubangaizaji. Na wale wote wenye tabia hizo na hali ni waislamu, hata kama wakiwemo wanaojiona ni wasomi wa Quran na Sunnah, wanaufahamu mbaya. Wajibu wa Masheikh na Maimamu Kuna njia mbalimbali za kupambana na umasikini wa kipato katika jamii. Njia moja ni kuwaelimisha wananchi ili wauchukie umasikini na kuongeza kasi yao katika kuibua fursa zinazowazunguka na kujiletea maendeleo. Kama tulivyoona hapo juu msisitizo wa Quran na Sunnah, tunawaomba Masheikh na Maimamu zetu waliomstari wa mbele katika kuupigania Uislamu, kuongeza juhudi zao hizo hasa katika ajenda ya vita dhidi ya umasikini. Licha ya rasimali nyingi kuwepo katika mikoa yenye waislamu wengi kama vile ardhi yenye rutuba, lakini waislamu katika mikoa hiyo ndio masikini

Masjid Mtambani inawatangazia Waislamu wote kuhudhuria kwa wingi katika Mhadhara Mkubwa utakao fanyika tarehe 28/06/2013 baada ya swala ya Ijumaa msikitini hapo na tarehe 29/06/2013 siku ya Jumamosi hapo hapo mtambani mhadhara utaanza saa 3:00 Asubuhi Kina mama tu. Mhadhiri: Babie Sheghele au maarufu baba Kiruwasha kutoka Morogoro. Wabillah Tawq
BISMILLAHIR RAHMANIR RAHIIM

Muhadhara

CHUO CHA UALIMU UNUNIO


DAR ES SALAAM
USAJILI NA: CU. 112

MAFUNZO YA UALIMU 2013 NAFASI ZA MASOMO


SIFA ZA MUOMBAJI

STASHAHADA (DIPLOMA)
AWE AMAMALIZA KIDATO CHA S ITA NA KUPATA KUANZIA PRINCIPLA (E) 1 NA S UBS IDIARY (S )-1

CHETI (GRADE III A)


AWE AMAMALIZA KIDATO CHA NNE NA AMEPATA ALAMA ZIS IZOZIDI DIV IV-27 ALIYERUD IA (RES ITING) AWE NA C-4

CHUO NI CHA BWENI KWA WASICHANA NA WAVULANA HUDUMA ZETU NI ZA KIWANGO CHA HALI YA JUU. ADA NI NAFUU SANA KULIKO POPOTE NA INALIPWA KWA AWAMU WAHI SASA NAFASI NI CHACHE WAHITIMU WOTE WANAAJIRIWA SERIKALINI
KUJIUNGA NA CHUO PIGA SIMU MOJA KWA MOJA CHUONI

MKUU WA CHUO

0713 673495 0713673405

CHUO KITAFUNGULIWA TAREHE 16/07/2013. CHUKUA FOMU MAPEMA

MSAJILI 0715 822332 0756 822332 0784 822332

NAFASI ZA KIDATO CHA TANO F5 KWA WASICHANA COM B ZOTE


NA WANAORUDIA MTIHANI ZINAPATIKANA KUNDUCHI GIRLS ISLAMIC HIGH SCHOOL KWA MAWASILIANO PIGA 0713 465437AU 0713 515054
FOMU ZINAPATIKANA KWA MAWAKALA WETU MIKOANI AU PIGA SIMU MOJA KWA MOJA
CHUONI AU SHULENI, HAKIKISHA UMEPEWA FOMU ZA CHUO CHA UALIMU UNUNIO SI VINGINEVYO

10
Assalaamu aleikum warahmatu-Llahi wabarakatuhu, Hja ni nguzo ya tano na ya mwisho katika nguzo za Kiislamu. Lakini hakuna nguzo iliyochambuliwa na kuwekwa bayana zaidi na Mwenyezi Mungu katika Qurani kuliko Hja. Qurani inatosha kabisa kumwezesha Mwislamu kuhi kikamilifu na kwa ufanisi mkubwa. Hoja hii inaashiria umuhimu wa Hijja katika maisha ya Mwislamu. Hja imekusanya mafunzo na hekima zilizomo katika nguzo zote nyengine, na kisha imekamilisha uzuri wa Uislamu. Hivyo kiumbe yoyote ( Jini au mwanadamu) hawezi kubuni jambo lolote, katika nyanja yoyote ya maisha, ambalo linaleta manufaa zaidi kwa wengine kuliko mafundisho ya Uislamu. Hivyo ni lazima Waislamu tufahamu Hekima au falsafa, madhumuni au malengo, na mafunzo au faida za kila moja ya nguzo na miongozo ya Uislamu. Kukosa kwetu kufahamu mambo haya ndiyo sababu kubwa inayozuiya Waislamu tusikae katika nafasi yetu ya kuiongoza dunia. MADHUMUNI NA MALENGO YA HIJJA: Hivi tunapokwenda Hja tunategemea kufanikisha lengo gani; au kwa nini t u m e a m r i s h wa k we n d a Hijja? Ni imani yangu kwamba kama jibu la swali hili lingefahamika vyema, Watanzania tungejaza ndege nyingi kwenda kuhiji kila mwaka musimu unapoingia. Ni kweli kabisa kuwa Hja haiko katika mipango ya wengi miongoni mwa vana wa ki-Islamu wenye uwezo wa kifedha, afya, na mengineyo. Baadhi yao wanaona Hijja ni jambo la kuzingatia mtu anapofikia umri mkubwa. Wasiokuwa wachambuzi wanaweza kuiona Hijja kuwa ni mzigo au tatizo, na pengine kuhisi inapingana na Hoja ya Mwenyezi Mungu Anayoikariri katika Qur-ani kuwa: (Mwenyezi Mungu) Hakuweka amri yoyote ngumu katika Dini (AlHajj, 22:78) Au kuwa: Mwenyezi Mungu Anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito. (Al-Baqara, 2:185) Bila shaka karne moja tu iliyopita haikuwa rahisi kwa mahujaji wanaotoka Kigoma, kwa mfano, kwenda Hja. Hakukua na kipando chochote wakati huo; si ndege, wala Reli, wala magari, nk. Wanahitaji muda gani kuka Dar es Salaam; na kama wakiondoka watu 100, wangapi unadhani wangekuwa na nafasi ya kufika salama. Wanaofika Dar es Salaam salama wanasubiriwa na safari ya bahari kuu yenye mawimbi makali kwa kutumia majahazi yanayotegemea upepo ya muda usiopungua mwezi baharini kuelekea Jiddah.

Makala

SHAABAN 1434, IJUMAA JUNI 28 JULAI 4, 2013


HADHI NA HESHIMA YA HAJJ KATIKA UISLAMU: Anayekwenda kuhiji kwa kuitikia wito wa Allah anakuwa mgeni wa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu Anawaenzi na Anaonesha furaha na mapenzi yake kwa mahujaji katika lugha Anayotumia kuwahutubia mahujaji katika Qur ani. Allah anasema: Na jitengenezeeni zawadi. Kwa hakika zawadi bora kuliko zote ni ucha Mungu. Na nicheni Mimi enyi wenye akili! (Al-Baqara, 2:197) Tamko la Uuli-l-albaab limetumika katika Qur-ani kama ni tamko maalum kwa watu maalum wanavyuoni, wenye kumjua Allah na kufahamu hekima na busara za amri zake na kuziamini. Lakini ni pahala pawili tu katika Qur ani tamko hili limetumika katika sura tamu, ya upenzi, na ya kubembeleza, Yaa uli-l-albaab, yaani Enyi wenye akili!. Hivyo Waislamu tunahitaji tufahamu kuwa anayeamua kuchanga fedha zake na akafunga safari ya Hijja anakuwa amefanya uamuzi unaothaminiwa mno na Allah. Heshima yake kwa Mola Mkarimu inakuwa kubwa sana. Bali Mwenyezi Mungu Ameonya katika Qurani kuwa mtu wa aina hiyo anapokuwa katika safari hiyo aheshimiwe sana na asivunjiwe heshima kabisa. Hoja hii inapatikana katika Aya ifuatayo: Enyi mlioamini, msivunje heshima ya .. wanaoiendea Nyumba Takatifu wakitafuta fadhila kutoka kwa Mola wao na radhi zake. (Al-Maida, 5:2) Hajji anadhaminiwa na Mola wake wakati wote tangu anatoka nyumbani kwake kwa kuitikia wito huo wa kwenda Hja mpaka anarudi. Ufafanuzi huu unapatikana katika Hadithi ya Mtume (SAW) iliyopokelewa na Sayyidina Jabir(RA), kama ifuatavyo: Hakika nyumba hii (Al-Kaaba) ni nguzo katika nguzo za Kiislamu. Mwenye kuikusudia kwa Hijja au Umra amedhaminiwa na A l l a h , a k i f a M we n ye z i Mungu Atamtia Peponi, na akirudi kwa watu wake salama atarudi pamoja na ujira mkubwa na zawadi nyingi. (Aabraany) Katika Hadithi nyengine ya Sayyidina Jabir (RA), Mtume (SAW) amesema, Mwenye kufa njiani kwenda Makka au kurudi, basi hatokusanywa Siku ya Qiyama wala hatohisabiwa. (Usbuhani) Tu t a k a p o k u s a n y w a Siku ya Qiyama kungoja kuhesabiwa kwa miaka isiyo na hesabu, wenzetu wanaokufa katika safari ya Hja hawatokuwemo. Wao watafufuliwa huku wanaleta Talbiya na watavushwa moja kwa moja na kupelekwa Peponi.

AN-NUUR

Malengo, faida, na falsafa ya Hijja


(Mwandishi: Muhammad AbdulRahman Dedes, Zanzibar.)

Na wafikao Jiddah salama wanasubiriwa na safari ya jangwani hadi Makka na Madina. Bila shaka safari hiyo ni ngumu na nzito. Ni kweli kabisa kuwa safari hiyo ilikuwa ngumu sana na nzito sana. Wak o wasafiri wen g i karne zilizopita walikuwa wa k i f a n ya s a f a r i n z i t o na ngumu kama hizo na kuliko hizo kwa ajili ya kutafuta dunia, yaani mali na mengineyo, bila ya kuwa na uhakika wa mafanikio. Waliongozwa na tamaa ya kibinaadamu tu. Hakukuwa na uhakika wowote wa mafanikio. Lakini walitumia mali zao, nguvu zao, kuacha familia zao, bali na kubahatisha uhai wao katika kufanya safari ndefu na nzito. Ilikuwa pata potea, wakifanikiwa walitegemea mambo yatakuwa mazuri katika maisha yao yaliyosalia, pindipo wakifa inakuwa basi ajali kazini. Wachache miongoni mwao waliridhika kuwa wakifa jina lao litabaki likitajika duniani. La muhimu katika maudhui yetu hapa leo ni kuwa watu hao hawakuwa wameamrishwa na Mwenyezi Mungu. Tofauti yao na sisi Waislamu ni kuwa sisi tumeamrishwa na Allah. Kwa bahati nzuri Mwenyezi Mungu Ametuambia kuwa Hakuacha kitu katika Kitabu Chake; yaani hakuna swali ila majibu yake yanapatikana katika Kitabu Kitakatifu, Qurani. Katika Qurani, Suratil Hajj (22), Aya za 27-30, Mwenyezi Mungu Anatoa majibu ya kwa nini akatuamrisha kwenda Hijja. Mwenyezi Mungu (SW) Anasema: Na watangazie watu Hijja.ili washuhudie manufaa yao na walitaje jina la Mwenyezi Mungu katika siku maalum na waizunguke Nyumba ya Kale.Hayo ndiyo kheri yake mbele ya Mola wakekwa kumtakasia imani Mwenyezi Mungu, bila ya kumshirikisha. (22:27-31)

1. Kuitikia wito wa Mweyezi Mungu Aliyetuumba (22:27), jambo ambalo ni haki Yake Allah (3:97) 2. Kushuhudia mambo yenye manufaa kwetu; 3. Kutaja jina la Allah katika siku tukufu na katika ardhi takatifu. 4. Kuizunguka nyumba (takatifu) ya kale kwa vile hiyo ni kheri kwetu. Na hayo yote tukayafanye katika hali ya kumtakasia Mola imani zetu (22:31). Katika kufafanua maana ya Aya ya 28, Sayyidina Abdulla ibn Abbas (RA) amesema kuwa manufaa ambayo Allah Amewaandalia wageni wake (yaani mahujaji) yanapatikana katika maisha Hajji hapa duniani na pia kesho Qiyama. Siri ya manufaa haya Anaua mwenyewe Mwenyezi Mungu. Lakini hapana shaka ni makubwa sana kuliko taabu, gharama na mitihani i n a yo m k u t a M w i s l a m u anapofanya safari ya Hja. WAKATI GANI TWENDE HIJJA? Mwenyezi Mungu Ameweka wazi katika Qurani (Suratul Hajj, Aya 27) kuwa Yeye ndiye aliyetoa WITO wa kwenda kuhi kwa anayepata uwezo. Hali kadhalika, Allah Ameitangaza Hijja kuwa ni HAKI yake kutoka kwa watu: Na ni haki ya Mwenyezi Mungu juu ya waja kuwa wahiji katika nyumba hiyo kwa mwenye kuweza kuendea njia hiyo. Na atakayekanusha, basi Mwenyezi Mungu siyo Muhitaji kwa walimwengu. (Aal Imran, 3:97). Katika Aya hii, Mwenyezi Mungu Amebainisha kuwa ambaye hakwenda kuhiji na ilhali ya kuwa mtu huyo aliwahi kuwa na uwezo fulani katika maisha yake, basi Allah hana haja naye tena. Ufafanuzi wa maneno haya ya Allah unapatikana katika Hadithi mbali mbali.

ni:

Hivyo malengo ya Hijja

Kwa mfano, katika Hadithi iliyonakiliwa na Imamu Abi Daud, Bwana Mtume(SAW) amesema: Hakuna dharura katika Uislamu, Mwislamu ambaye hakuhiji (na ilhali aliwahi kuwa na uwezo wa kuhi), basi Uislamu hautomtambua (yaani hatohisabiwa miongoni mwa Waislamu Siku ya Qiyama) . Kwa maana hiyo Bwana Mtume (SAW) ametoa wito kwa kila Mwislamu kwa kusema, Harakizeni kwenda Hja kwani hakuna anayeyajua yaliyo mbele yake. (Usbuhani) M a u t i h a ya n a m i a d i , wa l a h a ya c h a g u i u m r i , wala chochote chengine. Kadhalika uwezo unaweza ikatoweka wakati wowote, na mwanadamu unaweza ukazukiwa na mambo b a a d a ye k a t i k a m a i s h a yako ukakosa nafasi ya kwenda Hajj. Ukweli huu unabainishwa na Bwana Mtume (SAW) katika Hadithi iliyopokelewa na Sayyidina Abdullah ibn Abbas (RA) kama ifuatavyo: Mwenye kutaka kwenda Hijja, basi afanye haraka. Kwani anaweza kuja kuumwa, au anaweza kupotelewa na uwezo wa kumudu masurufu ya safari, au anaweza kutokezewa na haja, (na akashindwa kwenda). (Ahmad na Abu Daud) Hivyo Mwislamu apatapo tu uwezo anatakiwa asingoje kuoa wala kujenga wala asingoje kuka umri mkubwa, wala jengine lolote. Afuate wasia wa Mtume (SAW), mara tu apatapo uwezo, hata akiwa ndio kwanza amebaleghe, akimbilie kutekeleza fardhi na haki ya Muumba kwa vile hajui mja yaliyo mbele yake. Kubwa kuliko yote Mwislamu asiye akafa kabla ya kwenda Hja! Maimamu watatu wamewakiana kuwa wajibu wa kwenda Hijja unamthibitikia mwislamu mara tu anapopata uwezo.

11

Tangazo
Bismillaahir Rahmaanir Rahiim

SHAABAN 1434, IJUMAA JUNI 28 JULAI 4, 2013

AN-NUUR

MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI PAMOJA NA NGAZI YA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2013 / 2014
Wafuatao wamechaguliwa kujiunga na mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Stashahada pamoja na Ngazi ya Che kwa Vyuo vya Ualimu vya Kirinjiko Islamic Teachers College na Ubungo Islamic Teachers College kwa mwaka wa masomo 2013 / 2014.
NA. JINA KAMILI TANUWIR IDRISA MWITAGE BIHAWA JAMALDIN BIHUSNA MZAMILO FATIME A. BAKARI HADIJA HABIBU SHABANI HAFSA CHAREMA HAWA MOHAMEDI KULTHUM SUDI LEMA MARIAM ABDALLAH ALLY MARYAM KHAMIS ALLY MWADAWA OMARY OTHMAN MWAJABU TWAHIR OTHMAN MWAJUMA HASSAN MWAJUMA SHAFII KANGILE MWANTUMU RAHIIM MDEE NUSWAIBA HASHIM OMAR SHAKILA ISMAIL MYOVELA SHAM CHANZI SITI BAYUNI MUNISI TAUSI SAIDI MSEKWA UMMUKULTHUM OMARY WARDA YUSUF KITUTA ZAINABU ABUBAKARI MKUKI ZAKIA A. SHEMNKAI ZENA ABUBAKARI MVUNGI ME KE KE KE KE KE KE KE KE KE KE KE KE KE KE KE KE KE KE KE KE KE KE KE KE CHUO KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE

A: MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA STASHAHADA


NA. JINA KAMILI ABDALLAH H. HASSAN 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. ABEIDI SALIMU AHMADI BAKARI MNUNGAMO ALLY SINGANO EFREM F. BAKARI HAMAD H. ALI HAMIDU M. NGUHWE HEMEDI J. SHEIZA KIZAMI K. WASAGA MAULID ABASI RAMADHANI MIRAJI M. MANGA MZAMIRU B. MUSSA NASSORO J. MWERANGI RAMADHANI BARIYE RASHID Z. ATHMAN SULEIMAN S. MOHD FATMA SULEIMAN SIGE MARYAM M. ALLY MWAJUMA S. LUHULO MWANAARABU HEMEDI RUKIA KINONGO UPINDE ZUWENA SH. SALEHE JINSI ME ME ME ME ME ME ME ME ME ME ME ME ME ME ME ME KE KE KE KE KE KE CHUO ALICHOCHAGULIWA UBUNGO T.C UBUNGO T.C UBUNGO T.C KIRINJIKO T.C UBUNGO UBUNGO T.C UBUNGO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C UBUNGO T.C UBUNGO T.C KIRINJIKO T.C UBUNGO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C UBUNGO T.C UBUNGO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C UBUNGO T.C

18. 19.

23. 24. 25.

29. 30.

34. 35. 36.

Maelekezo ya kujiunga na Chuo yanapakana Kirinjiko Islamic Teachers College (Same), Ubungo Islamic Teachers College (Dar es Salaam) na Nyasaka Islamic Secondary School (Mwanza) kuanzia tarehe 02/07/2013. Kwa maelezo zaidi wasiliana na Mkuu wa Chuo cha Ubungo Islamic Teachers College kwa simu namba 0712 557099 / 0688131397 au Mkuu wa Chuo cha Kirinjiko Islamic Teachers College kwa simu namba 0787 188964 / 0657 705878.

MUHIMU:
Usaili wa mara ya pili Ngazi ya Che kwa wale waliochelewa kuchukua fomu utafanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 20/07/2013 kaka vituo vya:- Kirinjiko Islamic Teachers College (Same), Ubungo Islamic Teachers College (Dar es Salaam) , Nyasaka Islamic Secondary School (Mwanza),Mkuzo Islamic Secondary School(Songea Ruvuma) na Katoro Islamic Secondary School(Bukoba) Inshaallah. Usaili wa mara ya pili Ngazi ya Stashahada utafanyika vyuoni:Kirinjiko Islamic Teachers College (Same) na Ubungo Islamic Teachers College (Dar es Salaam) kwa maelekezo zaidi wasiliana na wakuu wa vyuo husika . (Ubungo T. C :- 0712 557099 / 0688131397, Kirinjiko T.C :- 0787 188964 au 0657 705878) Fomu zinaendelea kutolewa na zinapakana kwa mawakala wetu kote nchini. Wabillah Tawiq

B: MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI (KIRINJIKO ISLAMIC TEACHERS COLLEGE)


NA. 2. 3. JINA KAMILI ABDULRAHMAN HEMED SAID ABUBAKARI LAHE ABUBAKARI ALMAS KASSIM AMRI NASORO FARAJI DOTTO BAKARI MASALU HASSAN ABBAS MSANGI JUMANNE ATHUMAN MALILO MAULID MOHAMED LIGAGA MKUDE KOMU MOHAMEDI MOHAMED HUSSEIN MOHAMED MILANZI MUSTAFA SAADI MWALIMU MWATANDA SIRAJI ATHUMAN BONYA ME ME ME ME ME ME ME ME ME ME ME ME ME ME CHUO KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C KIRINJIKO T.C

7. 8. 9.

13. 14.

MKURUGENZI - IPC

12

AN-NUUR
MAKALA

12

SHAABAN 1434, IJUMAA JUNI 28 JULAI 4, 2013

Usikose kusoma AN-NUUR kila Ijumaa

Polisi amchapa makonde kijana akimsikiliza Ponda


Na Bakari Mwakangwale
MKANDA (CD) uliorekodi Kongamano la Sheikh Ponda Issa Ponda, siku moja baada ya hukumu yake imesababisha kipigo kwa Muislamu kutoka kwa Polisi Wilayani Gairo, Mkoani Morogoro. Akiongea na gazeti hili kwa njia ya simu mapema wiki hii akiwa katika kituo cha Polisi Wilaya ya Gairo, Bw. Ashraf Rafael, amesema alipigwa ngumi ya taya na kifuani na afande aliyemkamata, pamoja na kutii amri. Muislamu huyo, amelalamikia kipigo hicho na kudai kuwa imemsababishia maumivu makali kichwani na kifuani huku akidai kunyimwa fomu ya matibabu ya Polisi (PF3), kutoka kituoni hapo. Bw. Ashraf, alisema alikamatwa Juni 19, 2013, akiwa katika osi ya kaka yake ya kurekodi akiwa akiangalia Kongamano la Sheikh Ponda, alilofanya Msikiti wa Mtambani, siku moja baada ya hukumu yake. Tulikuwa katika osi ya ndugu yangu ya kurekodi CD, iliyopo hapo Gairo, tulikuwa tukiangalia sisi wenyewe CD ile, wakaja maafande na kutuambia kuwa tunafanya uchochezi kupitia ile CD. Sasa nipo kituo cha Polisi cha Wilaya ya Gairo, hapa nimekuja kuchukua PF3, kwa sababu nilipigwa siku ile lakini wananizungusha tangu asubuhi nimewaeleza lakini hawanipi. Alisema Bw. Ashraf. Alisema, akiwa ofisini hapo alikamatwa na askari mmoja akiwa amelewa huku akimtukana, kisha aliamuriwa kupanda katika gari lao. Bw. Ashraf, alidai kwamba wakiwa wanaelekea katika kituo cha Polisi, akiwa yeye na afande huyo aliyelewa alimshambulia kwa ngumi mbili, moja katika taya na ingine puani. Alisema, baada ya kukishwa kituo cha Polisi majira ya saa tatu usiku walimlaza selo, kesho yake asubuhi Waislamu walifuatilia suala hilo, lakini wakawa wanazungushwa kumpatia dhamana. Baada ya kutwa nzima, ya siku iliyofutia, majira ya jioni ndipo walinipatia dhamana, hata hivyo leo (Jumatatu Juni 24, 2013) nipo hapa kituo cha Polisi, nina maumivu makali sana katika sehemu nilizopo pigwa. Alisema Bw. Ashraf. Alisema, akiwa kituoni hapo, akidai PF3 ili aende hospitali kwa ajili ya kupata matibabu, maafande hao waligoma kumpatia wakidai kwamba hakupigwa. Ikiwa wataninyima kabisa itabidi niondoke, nikameze vidonge vya maumivu tu, lakini kutokana na maumivu niliyonayo nahitaji kwenda hospitali nikapate vipimo zaidi kwani toka siku hiyo nikiinama damu inatoka puani. Alisema Bw. Ashraf. Akiongea huku akikatisha mazungumzo kwa kukohoa mara kwa mara, alifafanua kuwa toka alipokamatwa hajapelekwa Mahakamani, kwani baada ya kupata dhamana alitakiwa arudi tena kituoni hapo siku ya Jumatatu (wiki hii). Bw. Ashraf, alidai kuwa akiwa kituoni hapo maafande walimueleza kuwa, CD hiyo inaleta uchochezi na yeye anafanya ushawishi wa uchochezi wa kidini. Alisema, hata katika jarada lake la mashitaka wameandika Kesi ya ushawishi wa uchochezi wa kidini, na kudai kwamba anaipinga Serikali. Bw. Ashraf, alidai kukataa madai hayo aliyoelezwa na Polisi, na kuwaeleza kwamba Sheikh Ponda ni kiongizi wake, na anafuatilia mawaidha yake na maelekezo yake. Alisema, alitoa maelezo yake kuwa alilazimika kununua CD, hiyo kwani hakufanikiwa kuwepo siku ambayo Sheikh Ponda alihutubia Waislamu Mtambani. Walinihoji mambo mengi sana, walichukua maelezo yangu, na waliniuliza nilichukua CD hiyo kwa madhumuni gani niliwaeleza kwa madhumuni ya kuona na kupata ujumbe kutoka kwa viongozi wangu kwa kuwa sikuwepo siku ya mkutano huo. Alisema Bw. Ashraf. Bw. Ashraf, alisema Polisi aliyekuwa akimuhoji alichukua maelezo yake yote lakini alikataa kuandika kuwa amepigwa na afande mwenzake, badala yake aliambiwa atakutanishwa na mkuu wa upelelezi ambaye ndiyo bosi wao kwa ajili ya malalamiko yake. Lakini mpaka natolewa kwa dhamana, sikukutanishwa na huyo afande mpelelezi, leo naka hapa (Jumatatu) na waeleza wananijibu kwa jeuri, nimewaomba hata wanipe dawa kupitia huduma yao ya kwanza (First ID) wamesema wao sio duka la dawa. Alisema Bw. Ashraf. Hata hivyo alidai kwamba, Afande mmoja aliamua kumpigia Daktari mmoja simu mbele yake akimtaka ampokee kwa ajili ya matibabu. Afande mmoja alihoji kuwa kama shida yangu ni kwenda hospitali, nikamjibu ndiyo, aliamua kumpigia simu daktari mmoja wa hospitali ya Gairo, na kusema kuna mhalifu anakuja umpatie matibabu, hata hivyo daktari huyo alikataa. Alisema akirejea maongoze yake na Afande huyo. Akizungumzia sakata hilo, Katibu wa Shura na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Mkoani Morogoro, Ustadh Jaffar Siraj, alidai kwamba Polisi Wilayani Gairo, wanafanya kazi kwa udini zaidi kuliko kufuata maadili ya kazi yao. Alitolea mfano akirejea tukio katika kipindi cha Sensa ya watu na makazi, kwamba pamoja na Serikali kutoa amri kutaka waliokamatwa waachiwe, lakini Polisi wa Gairo waliendelea na kesi hizo ndani ya miezi sita. Huyu Ashraf, ana kaka yake alikamatwa na Polisi hao hao wakidai anashawishi Waislamu wasishiriki sensa, waliendeleza kesi hiyo Mpaka miezi miwili iliyopita, baada ya kulalamikia suala hilo kwa RCO wa Mkoa, ndipo ilipomalizwa. Alisema Ust. Siraj. Alisema, kwa sasa wanakusudia kwenda Gairo, kuzungumza na Mkuu wa Polisi wa Wilaya, ili kumkabili na kumueleza waache kufanya kazi kwa mtazamo wa kidini zaidi. Alifafanua kwamba, CD ile haijapigwa marufuku na wala si kosa mtu kufuatilia mawaidha ya imani yake, ndio sababu wanahizi hatua aliyochukuliwa Muislamu mwenzao ina harufu ya chuki za kidini zaidi. Gazeti hili lilipo wasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro (RPC), kwa njia ya simu kuzungumzia kadhia hiyo, simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa. Hukumu ya Shkh. Ponda Issa

SHEIKH Ponda Issa Ponda.


Ponda na wenzake ilitolewa katika Mahakama ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam, Mei 8, 2013. Ambapo, Ijumaa ya Mei 9, Sheikh Ponda, alihutubia Waislamu kati Msikiti wa Mtambani, pamoja na mambo mengine, aliwataka Waislamu kuendelea kupigania haki zao na kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwao.

Waislamu Msikiti wa Morogoro wachangia damu


Na Mwandishi wetu.
za ibada ya Ijumaa. Alisema japokuwa baadhi wanakuja kituoni kuchangia damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya wananchi wenzao, lakini wameona ni vyema kuwatafuta walipo ambapo mchango utakuwa mkubwa zaidi. Leo inabidi tukiri kuwa tulichelewa kufanya maandalizi, wengi hawakufahamu mapema japokuwa wengine wanakuja pale kituoni kutoa damu zao kwa ajili ya kuokoa maisha ya wananchi wenzao, ambao huwa ni ndugu zao ambao ni wagonjwa wao. Alisema Bw. Kupuya. Kuhusu matumizi ya damu hiyo, Bw. Kupuya alisema huwa wanatoa taarifa kuhusu masuala mazima ya damu katika hospitali hapa nchini, kuwa damu haiuzwi. Alisema iwapo mtu yeyote atauziwa damu, basi atoe taarifa kwa kupiga simu namba 0715339 282 lakini muda wa kazi tu. Baadhi ya waumini wa Msikiti huo wa Morogoro waliojitokeza kuchangia kutoa

WAUMINI wa Kiislamu wamejitolea kuchangia kutoa damu katika zoezi lililofanyika katika Msikiti wa Morogoro, Ilala Jijini Dar es Salaam, baada ya swala ya Ijumaa Juni 21,2013. Zoezi hilo limefanyika ikiwa ni sehemu ya kutekeleza mpango wa Taifa wa Damu Salama, kwa ajili ya kuokoa maisha ya wagonjwa mahospitalini mbalimbali nchini. Kiongozi na Mtalamu wa damu Bw. Linus Kupuya, alisema Mpango wa Taifa Damu salama ni endelevu na sababu zilizosababisha kufanya zoezi hili misikitini ambako ni maeneo ya ibada, ni kuzidi kuwa karibu na wadau wakubwa ambao ni waumini. Hata hivyo alisema katika Benki yao kuna upungufu wa damu ndio maana wamelazimika kuwatafuta Waislamu mahali ambako wanapatikana kwa wingi zaidi husan katika siku

damu, walisema wanafanya hivyo kwa kuwa wanajua faida na umuhimu wa kuchangia. Hivyo walijitokeza kwa moyo mmoja wakiongozwa na Katibu wa Msikiti huo Ust. Abdulrahman. Mtaalamu Kupuya alisema siku hiyo pamoja na kwamba hawakufanya maandalizi, damu kiasi cha unit 20 kilipatikana. Alisema mtoaji damu akihitaji kutoa tena, ni baada ya kupita miezi mitatu. Hata hivyo kadi yake inamruhusu kama ana mgojnwa, atapatiwa damu kupitia kadi hiyo. Naye Ust. Abdulrahman Ally, alisema kuchangia damu ni moja ya majukumu ya Waislamu katika kuokoa maisha ya wanadamu. Alitoa wito kwa Jamii kwa ujumla kuwa, anaposikia Muislamu kuwa kuna zoezi kama hilo, anatakiwa kulichangamkia kwa kuwa anapata faida kubwa. Alisema kuwa faida hizo anazipata hapa duniani na kesho huko akhera ana fungu lake kwa kusaidia kuokoa maisha.

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

You might also like