You are on page 1of 12

www.annuurpapers.co.

tz

Sauti ya Waislamu

(16) USHIRIKA WA HIJJA!


Wajibu wa kwenda Hijja unawahusu mwenye uwezo na WENYE UWEZO (Qurani, 3:97). Inawezekana tukaenda sote Hijja kwa kuchanga tukapelekana mmoja mmoja kila mwaka katika familia, mtaa, msikiti, na kadhalika. Bila shaka Allah Atalifurahia hili na Atamimina neema kubwa juu yetu. Waislamu, tusisubiri, tuchukuwe hatua! Karibuni Ahlu Sunna wal Jamaa. Gharama zote ni Dola 4,300. Tafadhaliwasiliana nasi ifuatavyo: Tanzania Bara: 0717224437; 0777462022;Unguja: 0777458075;Pemba: 0776357117

Mamlaka kamili ndiyo malengo ya mapinduzi


Asema Maalim Seif na kushauri Wanaotaka kupumua wasipuuzwe Moyo ataka Zbar iwe na Uraia wake

Ni Diamond Jumapili
ISSN 0856 - 3861 Na. 1073 RAJAB 1434, IJUMAA MEI 31-JUNI 5, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Ya NECTA, propaganda kujadiliwa Bakwata, Jumuiya waikabili Serikali Wahoji USIRI, kuita Wakristo pekee Hali ya Sheikh Ilunga, India kuelezwa

Mtanzania mahakamani kusingizia Waislam ugaidi


Na Bakari Mwakangwale

MWENYEKITI wa kamati ya maridhiano Mzee Hassan Nassor Moyo

Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.

CHUO Cha Kiislamu Cha Al-jazeera, cha Jini Mwanza, kimelikisha Mahakamani Gazeti la Mtanzania, kikidai dia ya Shilingi Bilioni Mbili, kufuatia kuripoti habari kuwa Chuo hicho kinaendesha mafunzo ya Ugaidi. Gazeti hilo litokalo kila siku, limefunguliwa mashitaka na Chuo hicho na kwa mara ya kwanza limefikishwa

Mahakamani April, 30, 2013, katika Mahakama Kuu ya Jijini Mwanza, kujibu mashitaka yanayolikabili, na kuahirishwa hadi Julai 16, 2013. Hata hivyo kesi hiyo imedaiwa kushindwa kusikilizwa na kulazimika Jaji anayesikiliza kesi hiyo Mh. Mwangesi, kuiarisha kufuatia mwakilishi wa gazeti hilo Jini Mwanza, kudai kuwa hakuwa na
Inaendelea Uk. 2

SHEIKH Ilunga Hassan Kapungu akiwa hospitalini nchini India. Picha ndogo juu kushoto ni mke wake akiimuuguza nchini humo.

2
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Tahariri/Habari
AN-NUUR

RAJAB 1434, IJUMAA MEI 31- JUNI 5, 2013

AN-NUUR

MAONI YETU

Mtanzania mahakamani kusingizia Waislam ugaidi


Inatoka Uk. 1

INATARAJIWA kuwa Waislamu watafanya kongamano kubwa katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam Jumapili ijayo. Katika kongamano hilo inatarajiwa kuwa pamoja na mambo mengine, kutazungumziwa uamuzi wa Serikali kujitoa kutahini somo la dini katika mitihani ya kitaifa. Habari za awali zinafahamisha kuwa, katika kufikia uamuzi huo, Serikali ilikutana na wadau wa elimu kutoka taasisi za Kikriso pekee bila kuwashirikisha Wa i s l a m u . H a t a B A K W A T A inayojulikana kama kipenzi cha Serikali na inayotambuliwa na Serikali kama msemaji na mwakilishi wa Waislamu, haikualikwa katika kikao hicho cha majadiliano. BAKWATA walipewa tu taarifa baada ya Serikali kukubaliana n a Wa k r i s t o , t e n a ikaambiwa kuwa taarifa hiyo iwe siri (wasiambiwe Waislamu?). Kama ilivyoelezwa katika habari yetu i n a y o o n g o z a , B A K W A T A wameshaiandikia Serikali kupinga uamuzi huo na kusajili malalamiko yao kwamba inakuwaje Serikali kukaa na upande mmoja tu wa jamii kupitisha maamuzi makubwa yenye athari kwa watu wote bila ya kuwashirikisha Waislamu. Kwa upande mwingine, taarifa za uhakika ni kuwa japo suala la mitihani ya kidato cha nne na sita ni la muungano, hata Serikali ya Zanzibar haikuarifiwa wala

Huu ndio Mfumokristo

kushirikishwa katika kupitisha uamuzi huu. Na mpaka BAKWATA na Islamic Education Panel wanawasilisha malalamiko yao Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, bado Serikali ya Zanzibar ilikuwa haapewa taarifa rasmi. Sisi tunajaribu kukiri: Kama Zanzibar ingekuwa kama ilivyo Rombo au Kibosho, kwa maana ya kuwa na idadi kubwa ya Wakristo kiasi cha asilimia 90 ya Wazanzibari wote, je, bado Serikali ingekaa bila ya kuishirikisha Zanzibar katika kujadili na kupitisha maamuzi makubwa kama hayo yanayohitaji ridhaa ya pande zote mbili za muungano? Hali kama hizi na utendaji kama huu, ndio aliowahi kusema Dkt. John Sivalon kwamba inakuwa tabu mtu kujua kwamba je, hili ni la Serikali au ni la Kanisa. Kwa upande mwingine, utendaji kama huu ndani ya Serikali, ndio unapelekea Waislamu k u s e m a k u wa k u n a mfumokristo usio rasmi kikatiba na kisheria unaoendesha mambo. Na ndio wanaoupiga vita kwa sababu unawabagua na kuwadhulumu Waislamu. Sisi tunasema kuwa kuwashutumu, kuwakemea na kutishia kuwachukulia hatua wanaodai kuwa kuna mfumokristo, sio ufumbuzi na wala hakuwezi kuondoa malalamiko na madai y a Wa i s l a m u . N a kama inadaiwa kuwa madai haya yatavuruga amani, basi kuwakemea hakutaleta amani. Amani ya kweli na ya kudumu italetwa kwa kuyatambua na kuyashughulikia madai ya wanaolalamika.

hati ya mashitaka. Wa k i o n g e a n a Mwandishi wa habari hizi, kwa njia ya simu kutoka Jijini Mwanza, viongozi wa Chuo hicho wamesema tayari wameshalifungulia mashitaka gazeti hilo, baada ya kukaidi kukanusha tuhuma dhidi ya Chuo chao. Mjumbe wa Bodi ya Chuo cha Al-Jazeera, Sheikh Jabir Katura alisema kwamba wameshalikisha gazeti hilo katika Mahakama Kuu ya Jini Mwanza, na kukutana na mwakalishi wao, aliyedai hakuwa amejiandaa. Sheikh Jabir Katura, alisema kuwa mwakilishi huyo aliye h a p o J i j i n i M wa n z a aliieleza Mahakama kuwa walikuwa hawana taarifa rasmi, hivyo shauri hilo lililazimika kuahirishwa. Mwenyekiti wa Chuo hicho, Alhaj Ramadhani Mazige, akizungumzia kilichojiri katika kesi h i yo , a l i s e m a a wa l i waliliandikia gazeti hilo, wakiwataka wathibitishe yale waliyoandika kuhusu Chuo chao kupitia Gazeti lao la Mtanzania katika matoleo matatu, lakini hawakufanya hivyo. Tu l i w a p a m u d a wa wiki mbili ili wathibitishe habari zile, wakashindwa kufanya hivyo, na kuwaeleza nia yetu ya kuwakisha M a h a k a m a n i wa s i p o f a n ya h i v yo , lakini hawakuonyesha ushirikiano wowote. Mpaka muda huo ukaisha. Alisema Alhaji Mazige. Alhaj Mazige, alisema kesi hiyo iliyo chini ya Jaji Mwangesi, imekaa katika sura mbili kwanza, Al-Jazeera inadai fidia ya kuchafuliwa na kudhalilishwa hivyo ilipwe kiasi cha Shilingi Bilioni Moja. Ama alisema, madai

ya pili ni ya Ramadhani Maziga, ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Al-Jazeera, na ni Diwani wa Kata ya Nasio, aliyetajwa k wa k u d h a l i l i s h w a kwa kutajwa kwa jina akidaiwa anawapiga majini viongozi wakubwa hivyo kushindwa kwenda kushughulikia kadhia ya chuo chake ikiwa ndiye anawakaribisha Al Shabab na magaidi wengine. Kwa kuwa alitajwa kwa jina katika gazeti hilo, na yeye naye ametaka kuthibitishiwa hayo madai yaliyoandikwa na gazeti hilo la Mtanzania, naye alipwe fidia ya Bilioni moja, hivyo jumla gazeti hilo linatakiwa litoe fidia ya Shilingi Bilioni mbili kwa misingi hiyo. Alisema Alhaj Mazige. Awali Alhaj Mazige, alilieleza gazeti hili kuwa , April 30, 2013, walika Mahakamani, ambapo alijitokeza mwakilishi wao, aliyemkumbuka kwa jina moja la Fred, ambaye mbele ya Mahakama, alidai kuwa ni mwakilishi wa Mkoa wa Mwanza wa gazeti hilo. Alisema, mwakilishi huyo, alidai Mahakamani hapo kuwa alipigiwa simu na Makao Makuu ya Gazeti hilo Dar es Salaam, kwamba leo (April 30, 2013) ni kesi yao hivyo ahudhurie Mahakamani. Akiwa Mahakamani hapo, Alhaji Mazige, alidai mwakilishi huyo aliieleza Mahakama kuwa hajapata maelezo ya mashitaka yanayowakabili, zaidi ya kutakiwa na wakuu wake ake hapo tu. Alhaj Mazige, alisema wakili wao aliyemtaja kwa jina la Shekh Waziri, alithibitisha kuituma hati hiyo ya mashitaka Dar es Salaam, hata hivyo alidai Jaji anayesikiliza kesi hiyo, aliamuru waondoke wakakamilishe zoezi hilo, na mwakilishi wao

apatiwe pia. Hakimu alitupa siku 21, turekebishe utata huo kisha tumpelekee majibu ya pande zote mbili, huku akitupangia tarehe ya kusikilizwa tena kesi hiyo ambayo itakuwa Julai 16, 2013. Alisema Alhaji Mazige. Alhaji Mazige, alisema siku hiyo hiyo ya April 30, walishughuliki suala hilo, na kumkabidhi mwakilishi wa gazeti hilo (Fred) akasaini na kupeleka kopi Mahakamani kama alivyo amuru Jaji, na sasa alidai wanasubiri majibu kutoka kwa gazeti la Mtanzania. Mpaka hivi naongea na wewe, ( Jumatano wiki hii) hatujayapata majibu yao toka April 30, 2013, na tulipewa siku 21, sisi tuandike na wao wajibu, hatujui watatoa lini majibu yao, sisi tuna subiri tarehe ya kwenda Mahakamani, ifike. Alisema Alhaji Mazige. Alhaji Mazige, alisema kwa mara ya kwanza zilipotoka habari hizo walivuta subira, lakini katika toleo lingine lilofuata waliendelea na habari hizo, ambazo aliziita ni za uzushi zenye lengo la kuupaka matope Uislamu na Waislamu nchini, jambo ambalo liliwapa mshtuko mkubwa. Alisema, iliwalazimu wawaandikie barua ya k u wa t a k a wa s i t i s h e habari zao kwa kuwa hazina ukweli na ni za uchochezi, huku wakiwatahadharisha kuwa endapo w a t a e n d e l e a watawachukulia hatua za kisheria. H a t a h i v yo a l i d a i walipuuza, nakutoa tena kwa mara ya tatu habari hizo zikiwa na uzushi uleule. Alhaji Mazige, alisema gazeti hilo liliandika habari hizo katika matoleo yake tofauti tofauti kwa kupamba vichwa vya habari vikisema, Hofu ya Alqaida nchini, Njia fupi ya Mwanza hadi AlJazeera.

Ni Diamond Jumapili Mamlaka kamili ndiyo


Na Bakari Mwakangwale

Habari

RAJAB 1434, IJUMAA MEI 31- JUNI 5, 2013

AN-NUUR

WAISLAMU Jijini Dar es Salaama wanatarajia kufanya Kongamano ambalo pamoja na mambo mengine, watajadili dhamira ya Serikali ya kufuta Masomo ya Dini mashuleni. M e n g i n e yatakayozungumziwa ni juu ya propaganda inayoendelea nchini a m b a p o Wa i s l a m u w a m e k u w a wakibambikiziwa shutuma mbalimbali kwa lengo tu la kuwapaka matope. Kwa mujibu wa waandaaji wa Kongamano hilo, Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Kongamano hilo litafanyika siku ya Jumapili ya Juni 2, 2013, katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Upanga, Jijini Dar es Salaam. Taarifa hiyo ilisema kuwa Kongamano hilo linatarajia kuanza majira ya saa tatu asubuhi na kuhitimishwa saa nane mchana, na kuwataka Waislamu kuka kwa wingi. Kongamano hilo linafuatia kikao cha pamoja cha Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini wakiwepo Baraza Kuu la Waislamu nchini, BAKWATA ambapo walihoji hatua ya Serikali kukutana kisiri na taasisi za Kikristo na kukia hatua ya kufuta mitihani ya Somo la dini katika mitihani ya taifa. Katika kikao hicho kilichofanyika katika o f i s i z a TA M P R O

mapema Jumatatu wiki hii, mjumbe kutoka Bakwata alisema kuwa wao washaiandikia Serikali kupinga uamuzi huo na kuhoji ni kwa nini jambo hilo limefanywa SIRI bila ya kuwashirikisha Waislamu. Kwa upande mwingine, Islamic Education Panel walitoa taarifa wakisema kuwa nao washaiandikia Serikali kupinga jambo hilo na kusema kuwa limefunikwa na utata mwingi na hasa ilivyokuwa Serikali ilikaa na Wakristo pekee na kuchukua maamuzi ambayo yatakuja kuathiri Waislamu hasa ikizingatiwa kuwa kila mwaka Vyuo Vikuu vya MUM, Chukwani, Tunguu na Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar, vinachukua wanafunzi waliofaulu somo la Islamic Knowledge kwa ajili ya kozi za Sheria na Shariah, I slamic Banking/Marketing pamoja na kozi za

Ualimu na Islamic Studies. Taarifa za kiuchunguzi zinaonyesha kuwa pamoja na kuwa suala la mitihani ya kidato cha nne na sita ni la Muungano, l a k i n i Wi z a r a y a Elimu na Mafunzo ya Amali, Zanzibar, haikushirikishwa katika suala hili na hadi Waislamu Bara wanakutana kujadili suala hili, bado Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilikuwa haijaariwa. Kwa mujibu wa taarifa za waandaaji wa kongamano hilo, lengo kubwa ni kuwapa taarifa Waislamu na kuwaunganisha katika kukabiliana na changamoto kama hizi. Pia yatazungumziwa matukio yanayoibuka mara kwa mara hapa nchini na kuhusishwa Waislamu moja kwa moja hata kabla ya kufanyiwa uchunguzi, jambo ambalo ni

malengo ya mapinduzi
Na Mwandishi Wetu

Inaendelea Uk. 7

WAZANZIBARI wanapodai kuwa na mamlaka kamili ya nchi na dola ya Zanzibar, wanatetea haki na maslahi ya nchi yao, na kwamba hakuna sababu ya kubezwa wala kupuuzwa. Hayo yamesemwa na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, katika ukumbi wa Salama hoteli ya Bwawani, wakati akifungua kongamano la pili la kitaifa linalohusu Maridhiano ya Wazanzibari. Maalim Seif amesema, dhamira ya msingi ya ukombozi wa Zanzibar kupitia Mapinduzi ya Januari 12, 1964, ni Zanzibar kuweza kujitawala yenyewe na kuwa na mamlaka kamili. Hata hivyo akasema kuwa dhamira ya Mapinduzi ilianza kukiukwa baada ya kutiwa saini kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao uliipunguzia Zanzibar mamlaka yake. Kwa hiyo akawataka wanakongamano hao kuwaongoza wajumbe wa mabaraza ya katiba katika kutetea maoni na maslahi ya Zanzibar. Maalim Seif amefahamisha kuwa akiwa ni kiongozi wa Zanzibar, atasimamia na kutetea mawazo ya Wazanzibari walio wengi katika kupata haki zao za msingi ndani na nje ya Zanzibar.

SHEIKH Ilunga Hassan Kapungu akiwa hospitalini nchini India hivi karibuni.

Akifafanua zaidi kuhusu msimamo wake amesema hiyo haina maana kuwa Wa z a n z i b a r i h a w a t a k i Muungano, bali wanataka kuwepo kwa Tanzanyika na Zanzibar zenye mamlaka kamili, halafu kuwepo na muungano wa mkataba, ili kila nchi iweze kuendesha mambo yake kwa uhuru. Kuwa na mamlaka kamili sio kwa maslahi ya watu wachache bali kwa watu wote, ni kama mvua, yaani inaponyesha mimea yote inanawirika, alifafanua Maalim Seif na kuongeza, Tu n a t a k a k u r e j e s h a heshima ya nchi yetu, tuwe na sera na Wizara yetu ya Mambo ya Nje, bendera yetu ipepee nchi za kigeni, Umoja wa Mataifa na Jumuiya nyengine za Kimataifa zikiwemo Jumuiya ya Madola, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Afrika Mashariki. Akizungumzia kuhusu mafanikio ya maridhiano amesema yamerejesha umoja wa Wazanzibari na kuondosha uhasama na chuki miongoni kwa wananchi. Ameipongeza kamati ya maridhiano chini ya Mwenyekiti wake Mzee Hassan Nassor Moyo kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuyaendeleza maridhiano hayo na umoja wa Wazanzibari. Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano ambaye ni mwanasiasa mkongwe wa Zanzibar Mzee Hassan Nassor Moyo amesema maridhiano hayo yaliyoasisiwa na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, yameondoa fitna na chuki zilizodumu kwa muda mrefu miongoni mwa wananchi. Amesema kamati yake inaisubiri kwa hamu kubwa rasimu ya Katiba mpya itakayotolewa, ili waweze kuichambua kuona kama imezingatia maoni ya wananchi na maslahi ya Zanzibar. Akiwasilisha mapendekezo ya kamati hiyo Mzee Moyo amesema kila nchi katika Muungano inapaswa kuwa na uraia wake, sera yake ya mambo ya nje na Muungano uwe na JINA la Muungano wa Jamhuri za Tanzania au United Republics of Tanzania.

MATUKIO/MAKALA

RAJAB 1434, IJUMAA MEI 31- JUNI 5, 2013

AN-NUUR

KITUO CHA MAFUNZO NA AJIRA CHA TAMPRO

SEMINA YA UFUGAJI BORA WA KUKU WA KIENYEJI


Jumuiya ya Wataalamu wa Kiislam Tanzania (TAMPRO) kupitia Kituo chake cha mafunzo na Ajira inawatangazia Semina ya Mafunzo ya Ufugaji Kuku wa Kienyeji na Ujasirimali kwa kutumia wataalamu wenye uzoefu wanaoshughulikia masuala hayo kwa muda mrefu. Semina itakuwa kama ifuatavyo:Walengwa: Wafugaji, wanaotaka kuanza kufuga, wajasiriamali wadogo wadogo na watakaopenda . Siku: Kuanzia Jumamosi, Jumapili na Ijumatatu terehe 8 -10 June 2013 Muda: Saa 3:00 asubuhi - 10:00 jioni Mahala: Osi Kuu ya TAMPRO Magomeni Usalama, Dar es Salaam Mada: Njia za ufugaji wa kuku, Uchaguzi wa kuku kwa ajili ya kufuga, Kuandaa chakula bora, magojwa ya kuku na tiba yake, Utunzaji wa vifaranga na mayai nk. Vile vile mafunzo ya kutafuta soko la bidhaa zinazotokana na kuku, kutunza mahesabu na kumbukumbu za fedha pamoja jinsi ya kukuza mtaji yatatolewa.
BAADHI ya Waislamu wakiwa katika sherehe za Maulid ya Mtume Muhammad (s.a.w.) yaliyofanyika Msikiti Allah Karim - Kazimzumbwi Kisarawe mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kujisajili: Shilingi 50,000/= kwa mtu mmoja. (Kwa ajili ya cheti cha ushiriki, Kitabu cha muongozo, na chakula kwa siku zote tatu) Muhimu: Washiriki watapatiwa vyeti na kitabu cha muongozo wa ufugaji kuku kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili ili kukidhi haja. Pia watapata fursa ya kutembelea na kusoma kwa vitendo (eld) Kujisajili: Ili kujisajili tuma SMS kwenye namba 0714 151532, 0767151532, 0716574266 au ka TAMPRO Makao Makuu, Magomeni Usalama, jirani na Halmshauri ya Manispaa ya Kinondoni. Wahi kuijiandikisha kwani nafasi ni chache. Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia 0714 151532, 0767151532, 0716574266 au info@tampro.org

Masjid Aswabirina

Kitunda kibeberu Dar es salaam. Uongozi wa Masjid Aswabirina Tunapenda kutoa shukran zetu za Dhati kwa Waislamu wote waliofanikisha Msikiti huu kukia hapa ulipo. Hivyo basi tunatarajia kufanya ufunguzi wa msikiti huo tarehe 28 Shaaban ili uanze kutumika Rasmi katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Ili kufanya ufunguzi huo tunaomba msaada wenu wa kujengewa choo, Kisima cha maji pamoja na ununuzi wa Uwanja uliopo mbele ya Msikiti gharama ya uwanja huo ni Milioni Tisa ( 9) kwa ajili ya upanuzi wa ujenzi wa shule ya awali na chuo. Pia Tunaendelea kuwaomba wahisani waendele kutusaidia ili kufanikisha kukamilika kwa ujenzi huu. Tuma Mchango wako Account Na: K.C.B 3300386233 jina la A/c Aswabirina au kwa Tigo Pesa 0714 565619 au Mpesa 0753 673820 Amir Khatibu Yunus

MRATIBU MAFUNZO TAMPRO MAKAO MAKUU

Ahlul Daawa Hajj And Travel Agency


Inawatangazia Waislamu wote Kuwa Imeandaa Safari ya Hijja Mwaka 2013 Sawa na Mwaka 1434 Hijria kwa Dola US$ 3550 tu. Umra kwa Mwezi wa Ramadhani itakuwa ni Dola US$ 1995 Fomu zinapatikana katika osi zifuatazo:1. Osi ya Ahlul Daawa Dar es salaam Mtaa wa Dosi na Mkadini Nyumba Namba 26 Mkabala na Showroom ya Magari Tel 0713 730 444, au 0773 804101 au 0785 930444 na 0773 930444. 2. Osi ya Ahlul Daawa Zanzibar Rahaleo Tel 0777 484982 au 0777 413 987. 3. Abubakar Maulana wa Markaz Kiwalani Dar es salaam 0784 453838 4. Abdallah Salehe Mazrui ( HOKO) Dar es salaam 0715 724 444 5. Salim Is-haq Dar es salaam 0754 286010 au 0774 786101 6. Dukani kwa Abdala Hadh Mazrui wete pemba 0777 482 665 7. Dukani kwa Mohamed Hadh Mazrui Mkoani Pemba 0777 456911 8. Sheikh Daudi khamis sheha 0777 679692 9. Maalim Seif Humoud Hamed Kijichi Zanzibar 0777 417736 Wahi kulipia. Osi ya Ahlul Daawa Dar es salaam 0713 730 444 au 0773 804101 au 0785 930444. Osi ya Ahlul Daawa Zanzibar Rahaleo 0777 484982 au 0777 413 987. Maalim Seif Humoud Hamed Kijichi Zanzibar 0777 417736 Sheikh Salim Mohamed Salim 0774 412974 au Kupitia A CCOUNT NAMBA 048101000030 NBC Tanbih: Atakae maliza Taratibu zote kuanzia sasa Mpaka 15 July 2013 atapata Punguzo la asilimia 16% atalipia $ Dola 2982 tu. Atakae maliza Taratibu zote kuanzia Tarehe 16-july Hadi Tarehe 15 Augost 2013 atapata Punguzo la Asilimia sita 6% atalipia Dola $3337 tu. Kutakuwa na umra ya utangulizi kabla ya Umra ya Hijja kwa atakae maliza kufanya hivyo. Atakae maliza taratibu zote mwanzo ndie atakae shughulikiwa mwanzo. Ukilipia kwa njia ya Account kwanza piga simu 0774 412975. Kumbuka Kikundi cha Ahlul Daawa Kwa Bei nafuu kuliko wote na Huduma bora Kuliko wengi. Nyote mnakaribishwa

Masjid Mtambani inawatangazia Waislamu wote kuwa itafanya mhadhara mkubwa Inshaalah siku ya Ijumaa (Leo) Tarehe 31/05/2013. Muda: Baada ya Swala ya Ijumaa. Mahala: Masjid Mtambani Wahadhiri: Ust. Filambi na Ust. Siraj Kutoka Morogoro Wabillah Tauq

Muhadhara Mtambani

5
Na Mwandishi Maalum KAULI ya Umoja wa Afrika kukosa imani na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), inaonekana kuwiana na mtizamo wa wasomi mbalimbali mashuhuri ambao wanaituhumu ICC kupoteza dira na uhalali wake. Mmoja wa wasomi hao mashuhuri ni Profesa Noam C h o m s k y, r a i a m s o m i bingwa wa Marekani ambaye anamwona Rais Obama kama muhalifu ambaye inabidi akishwe ICC. Katika kikao chao kilichofanyika jijini Addis Ababa hivi karibuni, viongozi hao wameishutumu ICC kama chombo kisicho na uadilifu, chenye ubalakala (double standard) kinachoandama zaidi viongozi wa Afrika. Akitoa shutuma hizo, Waziri Mkuu wa Ethiopia ambaye ni Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika, Hailemariam Desalegn, anasema kuwa, Mahakama ya Uhalifu ya KimataifaInternational Criminal Court (ICC) ilianzishwa ili kuzuiya watu kutesa na kuuwa wengine bila ya kuchukuliwa hatua. Hata hivyo akasema kuwa hivi sasa mahakama hiyo imepoteza wasifu wake na kuwa kama chombo cha kuwasaka Waafrika. The intention was to avoid any kind of impunity but now the process has degenerated into some kind of race hunting. Alisema Hailemariam Desalegn huku akihimiza kuwa watakisha

Habari za Kimataifa/Tangazo

RAJAB 1434, IJUMAA MEI 31- JUNI 5, 2013


malalamiko yao Umoja wa Mataifa. Amesema, toka ICC ianzishwe, asilimia 99% ya watu waliokishwa ICC ni watu Weusi utadhani ni wao tu wanaofanya uhalifu. Mtizamo huo na hayo yanayosemwa na Desalegn ndiyo aliyosema Profesa Noam Chomsky hivi karibuni katika mahojiano yaliyopewa anuwani Obama Must be Taken Before ICC for the War on Terror - Noam Chomsky. Akihojiwa na Shirika la Habari la PT hivi karibuni, Prof. Chomsky anasema kuwa katika watu ambao wanatakiwa kuwa ICC hivi sasa, ni George W Bush, Tony Blair na Rais Barack Obama. Bush, Blair na Obama ni budi wakishwe ICC lakini hilo haliingii akilini. Alisema Chomsky huku akionyesha kuwa kutokana na kutokuwa na uadilifu katika ICC, inaonekana kama jambo la ajabu mtu japo kukiria tu kuwa kuna uwezekano wa Rais wa Marekani kuka mbele ya ICC. Ni kama haiwezekani. Angalia Mahakama ya Jinai ya Kimataifa (ICC)- ni Waafrika Weusi au wengine ambao nchi za Magharibi haziwapendi. Bush na Blair wanastahili kuwepo huko. Hakuna uhalifu mkubwa zaidi (duniani) hivi karibuni kama uvamizi wa Irak. Obama inabidi afikishwe hapo kwa vita dhidi ya ugaidi. Lakini hiyo haiingii akilini Inaendelea Uk. 6

AN-NUUR

AU wamesema kweli
ICC imepoteza dira na uhalali wake Raia tu wa USA hawezi kusimama ICC ICC Ikithubutu Uholanzi inavamiwa Chomsky aeleza ugaidi wa Bush, Blair

UHURU Kenyatta, Rais wa Kenya

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE


NAFASI ZA UALIMU NGAZI YA CHETI 2013/2014
WAISLAMU MNATANGAZIWA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI CHUO CHA UALIMU KIRINJIKO ISLAMIC A. SIFA: Muombaji awe na sifa zifuatazo: (a) Ufaulu wa kidato cha 4 usiopungua alama 27 katika kikao kimoja cha mtihani, asiwe amekaa zaidi ya miaka mitano (5) tangu amalize kidato cha nne. (b) Awe na credits 4 kiwango cha C endapo amekaa mtihani kwa vikao zaidi ya kimoja. (c) Kuhitimu kidato cha 6 ni sifa ya nyongeza. B. MAELEKEZO MUHIMU KWA WAOMBAJI WOTE 1. Fomu ya maombi iambatanishwe na vyeti (leaving and Academic certicates) vya kidato cha 4 pamoja na picha ya hivi karibuni. 2. Tarehe ya usaili na mwisho wa kurudisha fomu imesogezwa mbele hadi tarehe 22/6/2013 saa 2:00 asubuhi kutokana na kufutwa kwa matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa awali. 3. Vituo vya usaili ni hivi vifuatavyo: (a) Kirinjiko Islamic T.C SAME (b) Ubungo Islamic T.C DSM (c) Nyasaka Islamic S.S. Mwanza 4. Kwa wale ambao walisharudisha fomu wanatakiwa wawasilishe result slips za matokeo mapya mapema kwenye osi waliporejesha fomu hizo ili yaunganishwe na fomu zao. 4. Fomu zinapatikana kwa gharama ya shilingi elfu kumi. Soma vituo vinavyopatikana fomu katika ukurasa wa 9 wa Tangazo la Shule za IPC.:

6
Na Omar Msangi
WASWAHILi wana msemao, mgeni njoo mwenyeji apone. Hivi sasa zimepamba harakati za ujio wa Rais wa Marekani Barack Obama anayetarajiwa kuingia nchini Julai 1, 2013 akiandamana na jumla ya watu wasiopungua 1,000. Kwa mujibu wa taarifa za baadhi ya vyombo vya habari wiki hii, kuna wasiwasi mkubwa kwamba huenda hoteli zenye hadhi ya kimataifa zilizopo jijini Dar es Salaam, hazitatosheleza malazi ya wageni. Iwapo taarifa hizo kama zilivyoripotiwa katika baadhi ya magazeti ni kweli, hatujui Serikali yetu itafanya utaratibu gani kuhakikisha kuwa nchi haingii aibu kwa kushindwa kuwapatia wageni wetu mahali pa kulala. Kwa upande mwingine, Serikali kupitia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernad Membe, imesema kuwa inaandaa taratibu za mapokezi ikiwa ni pamoja na kuchapisha sare maalum zitakazovaliwa na vikundi vya burudani. Vitu vingine ni fulana na kofia maalum kwa mapokezi hayo. Lakini pia Serikali imetoa taarifa ya awali ikionyesha jinsi Watanzania watakavyonufaika na ujio huo. Kubwa linalosemwa hivi sasa ni kuwa tumeaminika k w a Wa m a r e k a n i m p a k a tumeongezewa donge la fedha za fuko la Millennium Challenge Corporation ( MCC), na kwa hiyo mengi yanatarajiwa kuletwa zikiwemo fursa za kibaishara. Pamoja na ukweli na uzuri wa yote hayo, nadhani yapo mengine mawili ambayo kama tukijipanga vizuri, tunaweza kuyapata kutokana na ujio wa Rais Obama. Na kwa hakika

MAKALA

RAJAB 1434, IJUMAA MEI 31- JUNI 5, 2013


kuu ya pili na katika zama zile za vita baridi, nchi za NATO ziliunda jeshi na harakati za siri maarufu Operation Gladio. Kwa mujibu wa kitabu cha mwanahistoria wa u-Swiss, Daniele Ganser, kupitia Operation Gladio, kulifanyika ugaidi wa kutisha dhidi ya watu wasio na hatia wakiwemo wanawake na watoto na kwamba ugaidi huo ulifanywa na magaidi walioandaliwa na kupewa mafunzo na NATO na halikadhalika kulipwa na NATO. Na zaidi magaidi hao wakiwajibika kwa NATO kupitia mashirika ya kijasusi ya nchi hizo, hasa yale ya Marekani na Uingereza. Yaliyoandikwa katika kitabu cha Ganser, NATOs Secret Armies: Operation Gladio and Terrorism in Western Europe, yamethibitishwa na vyombo vya sheria vya Italia, Switzerland pamoja na Ubeligiji na pia kuzua mjadala katika bunge la Ulaya. You had to attack civilians, the people, women, children, innocent people, unknown people far removed from any political gameThe reason was quite simple. They were supposed to force these people to turn to the State to ask for greater security. Tafsiri isiyo rasmi: Ilibidi kushambulia raia, watu wa kawaida, wanawake, watoto, watu wasio na hatia, wasiojulikana, walio mbali kabisa na mchezo wowote wa kisiasa, Sababu ilikuwa rahisi sana. Walikuwa wanatakiwa wawalazimishe watu hawa...... kuielekea Dola na kuomba usalama zaidi. Hayo ni maelezo ya mmoja wa washiriki wa harakati za kigaidi za Gladio (Gladio operative), Vincenzo Vinciguerra, wakati alipopandishwa kizimbani nchini Italia mwaka 1984. Vi n c e n z o Vi n c i g u e r r a

AN-NUUR

Mgeni njoo mwenyeji apone


Tutumie vyema ujio wa Rais Obama
KUJIHAKIKISHIA, USALAMA WA NCHI YETU. Nitafafanua. Kwa kitambo sasa tumekuwa na ushirikiano wa karibu sana na Marekani katika masuala ya usalama na ulinzi. Kupitia ushirikiano huo, tumekuwa tukipatiwa mafunzo, vifaa na hata kufanya mazoezi ya pamoja. Na ni kupitia ushirikiano huo pia na pengine kwa kuamini kuwa wenzetu wana utaalamu mkubwa zaidi kuliko sisi, na kubwa zaidi, kudhani kwamba wana nia jema na sisi, tumekuwa tukiwaita watusaidie hata katika matukio ya uhalifu ambayo vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi yoyote, vinaweza kufanya bila kuhitajia msaada wa nje. Hivi sasa makachero wa FBI, ambao ni kama sehemu ya polisi wa ndani wa Marekani, wapo nchini wakitusaidia kuchunguza tukio la kupigwa risasi na kuuliwa Padiri Evarist Mushi pamoja na lile la kulipuliwa bomu katika Kanisa jijini Arusha lililosababisha vifo vya watu watatu. Hadi sasa hakuna taarifa ya awali ambayo ishatolewa kuhusiana na uchunguzi unaoendelea, muhimu ikiwa ni nani kahusika, katumwa au anashirikiana na akina nani (wa nje au wa ndani) na kwa lengo gani. Muhimu ninalotaka kusema kutokana na ushirikiano huu ni kuwa kuna kila sababu ya kujihakikishia sisi wenyewe kuwa kupitia ushirikiano huu ndio tutakuwa salama zaidi na sio kinyume chake. Historia ni mwalimu. Tunafahamu kuwa baada ya vita

Rais wa Marekani Barack Obama


mimi naamini haya ndio muhimu zaidi kwa Taifa letu. Moja ni KUHAKIKISHIWA /NA SISI WENYEWE

Inatoka Uk. 5 (kwamba Rais wa Marekani naye asakwe kupelekwa ICC kama anavyosakwa Omar Hassan El Bashir na Uhuru Kenyatta!). Alisema Chomsky akijibu s w a l i k u t o k a RT k u w a iwapo anadhani kuwa kuna uwezekano wa kuona wahalifu wa vita Weupe kutoka mataifa yenye himaya kusimama kizimbani jinsi Rios Montt alivyosimama? Efrain Rios Montt alikuwa Rais wa Guatemala ambaye anashutumiwa kwa kufanya mauwaji ya kutisha kwa watu wake ambapo inakisiwa kuwa alikaribia kuhilikisha kabisa kabila la watu wa ki-Maya. Chomsky anasema kuwa haki haiwezi kutendeka kama Marekani nayo haitasimama kizimbani kwani ilihusika sana katika mauwaji hayo wakati ikiendesha siasa za kibeberu Guatemala na Latin Amerika kwa ujumla. Marekani ilihusika na

AU wamesema kweli
jambo hilo katika hatua zake zote, Mwishowe kulikuwa na makala asubuhi hii ikisema kuna kitu kinakosekana katika mashitaka hayo, nafasi ya Marekani. Nilifurahi kuona makala hiyo. Akijenga hoja yake kuhusu uhalifu wa Bush na Blair, Prof. Chomsky anasema kuwa hakuna uhalifu mbaya unaozidi ule wa kuvamia nchi ya watu, kufanya mauwaji ya raia wasio na hatia na kuharibu miji na vijiji. Akasema kuwa kuna kanuni zinazorudi nyuma miaka 800 wakati wa Magna Carta inayosema kuwa watu hawawezi kuuawa na dola bila kuhukumiwa na raia wenzao. Akasema, visingizio vyovyote vitakavyotolewa juu ya uvamizi wa Marekani, haviwezi kutengua kanuni hii ambayo ina umri wa miaka 800. Nilizungumzia Magna Carta, ambayo ina umri wa miaka 800, lakini kuna kitu kingine ambacho kina umri wa miaka 70 takriban. Kinaitwa jopo la Nuremberg, ambayo ni sehemu ya msingi wa sheria ya sasa ya kimataifa. Inaelezea uvamizi kama jinai kubwa zaidi, inayotofautiana na makosa mengine ya kivita, na inajumuisha uovu mwingine unaofuata. Uvamizi wa Marekani na Uingereza ilikuwa ni mfano bora zaidi wa uvamizi (wa nchi huru), hilo halina maswali. Ambayo ina maana kuwa walikuwa wawajibika kwa maovu yote yaliyofuata kama mabomu (ya kujitoa mhanga, kutegwa,

Inaendelea Uk.10

n.k.) Mizozo mikali ilianza, ikaenea kote katika ukanda huo. Ni kweli kuwa ukanda huo unachanwachanwa na mzozo huu. Hii ni sehemu ya uovu uliofuata. Alisema Prof. Chomsky akionyesha jinsi uvamizi wa Marekani katika nchi ya Iraq ulivyoleta balaa kubwa. Akasema kuwa sio tu kwamba inakuwa vigumu kumkisha Mahakamani Rais wa Marekani au Waziri Mkuu wa Uingereza, lakini ICC haiwezi kumgusa raia tu wa kawaida wa Marekani. Akifafanua akasema kuwa kuna sheria ya Marekani ambayo barani Ulaya inaitwa Sheria ya kuvamia Uholanzi. Hiyo ni Sheria ya Bunge la Marekani iliyosainiwa na Rais, ambayo inamruhusu Rais kutumia nguvu

kumwokoa raia wa Marekani aliyepelekwa The Hague (ICC) kujibu mashitaka. Akizungumzia kwa upande wa Rais Obama anasema kuwa, huyu ni Rais ambaye anatumia mbinu ya kuuwa kama namna ya kuboresha sera za Rais aliyemtangulia George W Bush ya kukamata na kutesa. Mbinu za Bush zilikuwa kuwakamata watu na kuwatesa, Obama ameboresha - anawaua tu na yeyote mwingine atakayekuwa karibu. Alisema Chomsky akinukuu makala katika gazeti la Wall Street Journal akisisitiza kuwa anachofanya Rais Obama katika mauwaji ya droni ni ugaidi wa kutisha kwa sababu anauwa watuhumiwa na walio jirani na mtuhumiwa. Shambulio la droni ni silaha ya kigaidi; Inaendelea Uk. 10

Makala

RAJAB 1434, IJUMAA MEI 31- JUNI 5, 2013

AN-NUUR

Ni Diamond Jumapili
Inatoka Uk. 3

SHEIKH Ilunga Hassan Kapungu akiwa hospitalini nchini India. Kushoto ni mkewe.

hatari. Ilisema taarifa hiyo. Aidha, imefafanua taarifa hiyo kwamba, Waislamu watatanabahishawa hatari ya mwenendo huo na baada ya mkutano huo utakao hutubiwa na Masheikh mbalimbali kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar, yatatolewa maazimio ya pamoja. Kongamano hilo litahudhuriwa na wajumbe kutoka

mikoani, na baada ya hapo yatatolewa maazimio ya pamoja k a m a Wa i s l a m u Kitaifa, kwa lengo la kuchukua tahadhari baada ya kutahadharishwa na Masheikh wao. Ilisema taarifa hiyo. Mmoja wa viongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T), alipohojiwa uwepo wa Kongamano hilo na maudhui yake alithibisha hilo na kudai maandalizi yanaendelea huku

akisistiza Waislamu kuhudhuria kwa wingi. Alisema, miongoni mwa mambo ambayo yatapewa nafasi kubwa kujadiliwa katika Kongamano hilo la Waislamu ni kuhusu Serikali kuamua kufuta mitihani ya somo la dini jambo ambalo limestua Waislamu wengi nchini. Aidha alisema kwamba Waislamu watajadili upepo wa matukio makubwa yaliyotokea nchini

na kuhusishwa kwa namna moja ama nyinge na Waislamu nchini. Kiongozi huyo alisema, wamekuwa wakipokea simu nyingi kutoka kwa Waislamu ndani na nje ya Jiji, wakitaka kujua kwa kina hatua za Serikali kufuta mitihani ya kitaifa ya somo hilo. Tokea taarifa za kufutwa mtihani wa kitaifa wa somo la Maarifa ya Uislamu unaosimamiwa na Serikali kuwafikia W a i s l a m u ,

wamekuwa wakipiga simu kutaka kujua mustabali wa somo hilo, hivyo tumeona ni vyema tufanye Kongamano kujadali suala hili kwa pamoja. Alisema Kiongozi huyo. Habari zilizotukia wakati tukienda m i t a m b o n i zilifahamisha pia kuwa fursa hiyo itatumika kutoa taarifa fupi juu ya hali ya Sheikh Ilunga Hassan Kapungu na maendeleo ya matibabu yake.

Makala

RAJAB 1434, IJUMAA MEI 31- JUNI 5, 2013

AN-NUUR

Na Khalid S Mtwangi

THERE is little doubt that tension between Christians and Muslims has lately taken a turn for the worse as never before in the history of this country. It is amazing and a credit to the people that streets and households in cosmopolitan melting pots such as Dar es Salaam look serene. Before now it would NOT have been correct to suggest that this unfortunate situation as well applied to relation between religions. Dr Magoti Evarist has alluded to such a state of affairs in his missive in the CITIZEN ON SUNDAY of May 5, 20. But as was manifestly demonstrated during the MwembeChai fracas here Muslims vented their anger at the Government leaving the string of churches and other Christian establishments in the vicinity, and there are quite a number, untouched. During this catastrophic manifestation of naked power in their possession some Government ofcials simply decided to stamp their power and authority on Muslims to teach them a lesson they would never forget. The sad fact about this matter is that Christian brethren, including those one would have given credit with having a broader outlook on the affairs of the world, have decided to live in a cocoon in so far Muslim affairs are concerned. There is every reason to arrest this obviously perilous situation that could be pregnant with a manifestation that could be predictably detrimental to peace and harmony of the people of this country. However there must be a

variation of suggestions that have been put forward by Dr Magoti Evarist. My suggestion, or indeed, recommendation would be to appeal to the Church hierarchy to preach to their ock fair play in everyday life. It amazes many Muslims that Christians, especially among the intelligentsia and the academia, are wholly oblivious, indeed immune, to the many complaints that are aired by Muslims about what has been termed as dhulma that happens to be the Muslims lot. It would appear that to them that is simply a lot of hot air? Take a load of this. A team of ofcials from the Ministry of Education proceeds to Morogoro to hide themselves to complete an urgent peace of assignment. Eid el Udh-ha happens to fall when these ofcials are ensconced out there building the nation. The man in charge simply does not recognise Eid el Udh-ha so he insists the ofcers keep on working and need not attend prayers on that very important Holy Day to remember Nabii Ibrahim SA who is accepted by all as the Father of all Monotheism that ostensibly would include what is known today as Christianity. But come Sunday the whole team was given the day off to attend prayers. Needles to point out that the man in charge professed Christianity!!! Again at Morogoro. The Municipal Education Officer writes officially to all primary school head teachers to submit to him a list each of all Roman Catholic pupils in their schools. What for? Complaints were directed at the Ministry by Muslim organizations, but as a rule and Muslims are used to it , the bureaucracy in the Government would not respond; they never do. A teacher in one Tanga goes into a tirade against Rasu-ul-Llah Muhammad SAW and Islam generally. To their credit Muslims do not breath fire regarding what is really kashfa with

RELIGIOUS TENSION: THE CHURCH IS IN A TRAP


a capital K but simply complain bitterly to officials who matter. No disciplinary action was initiated against this antiMuslim blasphemer. Dr Magoti is aware of the trenchant condemnation that is aired by everyone, clergy politician et al when, say, a Muslim declares that according to the teachings of his religion Jesus was simply a Rasul of Allah and he is recognised as such by Muslims. That surely cannot be kashfa. But since MFUMOKRISTO says so then it is. In my opinion, Dr Magoti, everyone will win if two aspects of the matter are recognized, accepted and worked on. First the bureaucracy is to wean themselves of the teachings by the church that Islam is an enemy. Considering what is heard the Christian clergy preach there is inherent animosity within some of the sermons. In this context it must also be accepted that Churches have for a long time churned out literature that is blasphemous to Muslims. Dr Evarist may wish to look for the book with title WANA WA IBRAHIM that is purveyed around by the Catholic Church. In leaets distributed by the Lutheran Church Rasul-ul-Llah Muhammad SAW is called a false prophet and they go out to misquote the Quran and Hadith to justify the blasphemy. There is a lot more than this. Muslims never did seek help nor hide behind Government apron strings. Second it behoves upon the Church hierarchy to be truthful as far as Islam is concerned. There is a great amount of anathema and pet aversion towards anything Islam and Muslim among the clergy. Remember when the killing at MwembeChai was virtually given the thumbs up by among the highest in the Catholic Church; similarly they blamed the victims in the Pemba killings in 2001.

FAIR LAND DISTRIBUTION

Here you have a good example of representatives of Christianity who simply have no time for Islam and Muslims. What about the attitude of Muslims in this country towards their Christian cousins? First, being a tiny minority in the establishment Muslims have no opportunity to ex their weak muscles. Those that are waungwana would not want to be lumped with the uneducated kanzu clad lot, and they know which side of their thick slice of boo is smeared with all the goodies. Muslims do not seek any privileged position; but they seek only haki. Finally, Dr Magoti Evarist needs to be congratulated for the courage he has shown in his missive. It is rare for some one of his stature to accept though grudgingly that there are faults elsewhere as well and not just among Muslims. Archbishop Eliezar Sendoro is one Christian clergy who has taken pains

NAFASI ZA KAZI Inawatangazia nafasi ya kazi upande wa wauzaji (Salesman) Sifa za muombaji Awe kijana wa kitanzania Awe na umri kati ya miaka 25-45 Awe tayari kuweka dhamana ya mali isiyohamishika Awe na wadhamini watatu ( 3) wenye ajira zinazotambulika kiserikali Awe na elimu siyochini ya kidato cha nne Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitatu katika fani hiyo. MAWASILIANO Zaidi: Piga Simu: 0789 272 737 Maombi yote yatumwe katika mtandano. Email: fairlandcom@yahoo.com Au kwa Barua S.L.P 4804- DSM MAOMBI YAAMBATANISHWE NA PASSPORT SIZE.

Makala

RAJAB 1434, IJUMAA MEI 31- JUNI 5, 2013

AN-NUUR

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE


NAFASI ZA KIDATO CHA TANO 2013/2014
1. 2. 3. 4. 5. 6.

Shule hizi ni za Kiislamu zenye lengo la kuwapa wanafunzi taaluma ya hali ya juu na malezi bora ya Kiislamu kwa gharama nafuu. Shule hizi ni za mchanganyiko wa wavulana na wasichana na zinapokea wanafunzi wa bweni tu. Masomo yanayofundishwa ni Islamic knowledge, Combinations za SAYANSI, ARTS, BIASHARA pamoja na COMPYUTA. Muombaji awe na Crediti 3 au zaidi na angalau D ya Elimu ya Dini ya Kiislamu katika matokeo ya kidato cha nne. Ikiwa ana F au hakufanya Elimu ya Dini ya Kiislamu, basi awe tayari kusoma programu maalum ya Maarifa ya Uislamu atakapokuwa kidato cha tano. Kwa wale ambao walisharudisha fomu wanatakiwa wawasilishe result slips za matokeo mapya mapema kwenye osi waliporejesha fomu hizo ili yaunganishwe na fomu zao. Waombaji wapya wenye sifa wanashauriwa kuendelea kuchukua fomu.Tarehe ya mwisho ya kurejesha fomu itatangazwa baadaye. Fomu za Maombi zinapatikana kwa gharama ya shilingi 10,000/= katika vituo vilivyoorodheshwa hapa chini.
Arusha Kilimanjaro Osi ya Islamic Education Panel Jambo Plastic Ghorofa ya 2 mkabala na msikiti Mkuu Bondeni - 0763 282 371/ 0784 406 610 Moshi: Msikiti wa Riadha 0654 723 418 Same: Kirinjiko Islamic Secondry School: 0784 296424/0655 697 075 Uongofu Bookshop: - 0784 982525/ Mandia Shop - Lushoto: 0782257533 Nyasaka Islamic Secondary School 0717 417685/0786 417685 Osi ya Islamic Education Panel - Mwanza - Mtaa wa Ruji mkabala na Msikiti Al-Amin 0785 086 770 Duka la Kansolele -Stendi ya zamani sokoni - 0714587193 Bukoba: Alhuda Caf Kwa mzee Kinobe karibu na osi za TRA. - 0688 479 667 Msiikiti wa Majengo-0718866869 Kahama osi ya AN NUUR Karibu na msikiti wa Ibadhi: 0753 993930 Ubungo Islamic High School 0754 260 241/0712033556 Osi ya Islamic Ed. Panel Temeke -Msikiti wa Nurul Yakin 0655144474 Wasiliana na Ramadhani Chale :0715704380 Hijra Islamic Primary School : 0716 544757/0712 325086 Osis ya Islamic Ed. Panel karibu Nuru snack Hotel 0714285465 Babati: Shule ya Msingi Hangoni: 0784 667575 Msikiti wa mwanga Kigoma: 0753 355224 Kibondo Islamic Nursery School: 0784 442860 Kasulu: Murubona Isl.SS. 0714710802 Wapemba Store: 0784 974041/0786 959663 Amana Islamic S.S 0786 729 973 Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa NURU 0715 681701/0716791113 Mkuzo Islamic High School. 0716 791113 Duka la vifaa vya Kiislamu nje ya Msikiti wa Uyole 0713 200209 Rexona Video mkabala na Mbeya RETICO: 0713 200209 Sumbawanga: Masjid TAQWA 0717082 073 Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784 944566 Madrastun Najah: 0714 522 122 Wete: Wete Islamic Education Center: 0777 432331 Madrasatul Fallah: 0777125074Osi ya ust. Yusufu Ally jirani na msikiti mkuu 0653705627

Tanga Mwanza Musoma Kagera Shinyanga Dar es SalaamMorogoro Dodoma Singida Manyara Kigoma Lindi Mtwara Songea Mbeya Rukwa Tabora Iringa Pemba Unguja Maa -

6. Pia Fomu zinapatikana kwenye Tovuti: www.ipctz.org. Ikumbukwe kuwa watakaopata fomu kupitia tovuti (download) watatakiwa kuzilipia wakati wa kuzirejesha.

USIKOSE NAFASI HII ADHIMU WAHI KUCHUKUA FOMU SASA!

Wabillah Tawiq MKURUGENZI

10
alishitakiwa kwa mauwaji ya polisi watatu waliolipuliwa kwa bomu lililokuwa limetegwa katika gari mwaka 1972. Ni katika kesi hiyo ambapo siri ya kuwepo harakati za kigaidi za Gladio zilifichuka. (Tanzama CIA Organized Secret Army in Western Europe-Washington Post, Novemba 14, 1990). Ufupi wa maneno Vincenzo Vinciguerra anasema kuwa watu wasio na hatia, raia, wanawake na watoto, walishambuliwa na kuuliwa (kufanyiwa ugaidi), ili kusimika kitisho na kuwafanya raia kutaka ulinzi zaidi kutoka kwa Serikali. Hapana shaka wakati huo wa siasa za vita baridi, waliosingiziwa kufanya ugaidi huo ni Wakomunisti, vyama vya siasa na makundi katika jamii yenye mrengo wa kikomunisti. Kwa mujibu wa taarifa zilizofichuliwa na aliyewahi kuwa kachero wa FBI Sibel Edmonds, kinachoitwa vita dhidi ya ugaidi hivi sasa na wanaoitwa magaidi hivi leo, ni watu walioandaliwa, wakapewa mafunzo, fedha na kuwezeshwa na mataifa hayo hayo ya NATO katika operesheni mpya inayojulikana kama Gladio B. Chini ya operesheni hiyo inaelezwa kuwa, mwaka 1997 NATO walimwomba Rais Hosni Mubarak awaachie huru Waislamu waliotuhumiwa kumuuwa Anwar Sadat na ambao wana uhusiano na Ayman al-Zawahiri (Al Qaida) na wafungwa hawa wakasarishwa kwa ndege hadi Uturuki chini ya uangalizi wa Marekani ambapo waliunganishwa na wanaodaiwa kuwa ni magaidi hivi sasa. Zaidi Edmonds anasema kuwa akiwa mkalimani wa FBI (Kiarabu na Kifursi) alishuhudia al-Zawahiri na Mujahideena wengine wanaoitwa hivi leo magaidi, wakikutana na maosa waandamizi wa Serikali ya Marekani katika Ubalozi wa Marekani, Baku katika nchi ya Azerbaijan. Wakati uhalisia wa uwepo wa Gladio barani Ulaya ni suala la nyaraka za historia. Edmonds amesema kuwa mkakati huo huo

Inatoka Uk. 6

Mgeni njoo mwenyeji apone

Makala

RAJAB 1434, IJUMAA MEI 31- JUNI 5, 2013


Alipomaliza tu, mikono kadhaa ilikuwa juu na alipopata fursa mjumbe kutoka Kenya/ Uganda alimshambulia muAngola huyo kwa kutetea kampuni ya kibeberu kwa zawadi kiduchu inayotoa kwa Angola wakati inavuna mabilioni ya dola kila mwaka. Akakumbushwa jinsi makampuni hayo ya mabeberu yalivyosababisha maafa makubwa katika vita ya Angola kupigania kupora madini na mafuta. Huku wanampa Savimbi silaha kuuwa wananchi, huku makampuni yao yanapora mali. Akaambiwa kuwa kilichokuwa kimetarajiwa ni yeye kusema kuna mkakati gani kwa Chevron kulipa dia kwa wananchi wa Angola na namna gani watakomesha unyonyaji unaoendelea, sio kuzungumzia zawadi kiduchu ya dola milioni moja kwa mwaka wakati kwa muda huo huo wanakomba mafuta ya mabilioni ya dola. Imepigwa sana ngoma mpaka Bungeni kwamba, tumekuwa watu wa kuaminika kwa Marekani mpaka tumeongezewa fungu nono katika mfuko wa Millennium Challenge Corporation (MCC). Sasa maadhali anakuja mfadhili na muhisani wetu, pengine tungetumia kipindi hiki cha maandalizi kupiga hesabu, ni kiasi gani makampuni ya Marekani yanavuna kupitia makampuni yao ya madini (mafuta/gesi/uranium kama yapo au kama yanakuja) na hawa Symbion, halafu tulinganishe na zawadi wanayotupa. Tukiweza kufanya hivyo, tutakuwa na nafasi nzuri katika mazungumzo yetu na mgeni wetu ili tu kuhakikisha kuwa tunanufaika na rasilimali zetu badala ya kuwanufaisha wengine. Hoja hapa ni kuwa tusijemkabidhi mtu mwingine kukama ngombe wetu tuliyemlea na kumnenepesha; anakama maziwa lita 25 kwa siku, anatugawia robo lita kwa mwezi, halafu tunampigia magoti kwa shukrani.

AN-NUUR

KACHERO wa zamani wa FBI Sibel Edmonds.


ulichukuliwa na makao makuu ya jeshi la Marekani (Pentagon) katika miaka ya 1990 katika medani mpya ya mapambano, yaani barani Asia; na kwamba badala ya kutumia mashabiki hatari wa utawala wa kifashisti wa Ujerumani (wakati wa Vita Vikuu vya Pili) waliwatumia mujahideen wakifanya kazi chini ya bin Laden kadhaa, na Al-Zawahiri. Inaelezwa kuwa mkutano wa mwisho wa Gladio unaofahamika katika vyombo vya habari ulifanyika katika Kamati ya Pamoja ya Siri (Allied Clandestine Committee) jijini Brussels (makao makuu ya NAT0) mwaka 1990. Wakati Italia ilikuwa ndiyo imelengwa zaidi katika operesheni zake barani Ulaya kongwe, Edmonds anasema kuwa Uturuki na Azerbaijan zilikuwa njia za kuwezesha operesheni mpya na tofauti katika Asia, wakitumia watu walioshiriki katika kampeni dhidi ya Urusi nchini Afghanistan, wanaoitwa Waafghani wa Kiarabu ambao walikuwa wamefundishwa na Al Qaeda. Kinachosisitizwa hapa ni kuwa kama ilivyofanyika katika ile Operation Gladio, katika inayoitwa vita ya ugaidi hivi leo, ipo pia Operation Gladio B ambapo lengo ni kuzivuruga nchi lengwa zijione hazina amani wala kuwa salama bila ya kupata msaada wa kikachero na kijeshi kutoka nchi za kibeberu. Kupitia Operation Gladio B, nchi za kibeberu hupata fursa ya kutawanya makucha yake ya kijeshi na kuzikamata nchi inazozitaka na hivyo kupata fursa nzuri ya kutamalaki

Inatoka Uk. 6 hatulizungumzii hivyo. Ni kwamba, kiria, unatembea mtaani na hujui kuwa dakika tano zijazo kutakuwa na mlipuko mtaa wa pili kutoka angani, ambako huwezi kuona. Kuna mtu fulani atauawa, na yeyote atakayekuwa karibu atauawa, na huenda ukajeruhiwa kama uko hapo. Hii ni silaha ya kuwatisha watu. Inavitisha vijiji, mikoa, maeneo makubwa. Kusema kweli ndiyo kampeni kubwa zaidi ya vitisho vya kigaidi iliyowahi kuwepo, tena kwa mbali. Pamoja na uhalifu wote huo anasema Prof. Noam Chomsky kuwa si jambo la kukirika kuwa itaka siku

Rais wa Marekani asimame katika ICC. Wa k a t i h u o h u o mwandishi mashuhuri John Pilger naye amezungumzia suala hilo akisema maafa yanayotokea Iraq hivi sasa ni msiba unaowakumbusha walimwengu kuwa wahalifu ambao hawajafikishwa mahakamani. Katika makala yake From Iraq, a tragic reminder to prosecute the war criminals, John Pilger ametaja mambo mawili ukiacha mauwaji yaliyofanyika wakati wa uvamizi.

AU wamesema kweli
Anasema, kutokana na tati mbalimbali, hivi sasa kuna ongezeko kubwa sana la ugonjwa wa saratani na watoto wanaozaliwa wakiwa na ulemavu na maumbile yasiyo ya kawaida (congenital malformations). Na kwamba ongezeko la matatizo hayo ya kutisha ni kutokana na uraniua iliyokuwepo katika mabomu (depleted uranium shells UD) yaliyolipuliwa Iraq. Anasema, taarifa zinaonyesha kuwa kabla ya uvamizi wa Marekani, kulikuwa na wastani wa watu wawili mpaka watatu wa ugonjwa, lakini sasa kunatokea wagonjwa 35 kila mwezi. Tafiti zaidi zinasema kuwa kiasi miaka mitano ijayo, wagonjwa wa saratani watakuwa kati ya asilimia 40 mnpaka 48 ya wagonjwa wote na kwamba hata mimea imeathirika na matumizi ya mabumu hayo yenye uranium kiasi cha kutokulika. John Pilger anasema msiba unaowakumba wananchi wa Iraq hauna tofauti na ule wa Hiroshima na Nagasaki. Kwa upande mwingine Pilger anasema kuwa uvamizi wa Bush na Blair huko Iraq

kuchuma na kuzuiya washindani wengine miongoni mwa mataifa makubwa kuingia katika nchi hizo. Lakini jingine ni kuwa nchi ikiwa na fujo, haiwezi kuwa imara na kupata muda wa kutafakari kuweka sera nzuri na msimamo imara wa kulinda rasilimali zake. Kongo, DRC, ni mfano tosha. Sasa pengine kwa ujio huu adhimu kwetu, ingekuwa vyema kama katika mazungumzo yetu na mgeni wetu Rais Barack Obama, tutaingiza na agenda hii. Kwamba katika ushirikiano wetu huu, ukiwemo huu wa kuwepo kwa FBI kutusaidia kuchunguza bomu la Arusha, je, haitatuingiza katika harakati za Operation Gladio B? Vi n c e n z o Vi n c i g u e r r a anasema kuwa kitendawili cha Peteano bombing na Bologna massacre ambapo waliuliwa watu 85, kinateguliwa kwa kufichuka harakati za Operation Gladio. Sasa itakuwa ni vyema na sisi kujihakikishia kuwa hatuwi na akina Valerio Fioravanti na Francesca Mambro miongoni mwetu wa kutuletea maafa kama lile la Kanisani Arusha. Katika kikao cha mashirika ya mafuta katika nchi za Afrika Mashariki (East Africa Petrolium Conferenece) mwaka 2008 kilichofanyika katika Hoteli ya Ngurudoto, Arusha, na kufunguliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete, alikuwepo mjumbe mualikwa kutoka Angola akiwakilisha Shirika la Petroli la Chevron. Katika hotuba yake mjumbe huyo akitumia vielelezo vya picha, alieleza jinsi kampuni ya Chevron kutoka Marekani inavyotoa misaada, huduma na asante kwa wananchi wa Angola, hasa wanaozunguka migodi. Alisema, msaada wao kwa wananchi ni Dola milioni moja kwa mwaka ikijumuisha ujenzi wa visima vya maji na madarasa ya shule za msingi.

umeacha msiba wa mauwaji ya wenyewe kwa wenyewe ambapo kila uchao kuna mtu/ watu wanauliwa au kutiwa vilema. Akimnukuu Von Sponeck, anasema kuwa taarifa ya Serikali ya Iraq inaonyesha kuwa kiasi watoto milioni 4. 5 wamekuwa yatima kwa baba na mama kutokana na vita. Hiyo ni sawa na kusema kuwa asilimia 14 ya watoto wa Iraq ni yatima huku mamilioni wakiwa hawana makazi. Anamalizia Pilger akisema kuwa uhalifu na uovu huo waliofanyiwa watu wa Iraq, unaita ukisema kuwa kuna mhalifu kajificha mahali anatakiwa kukamatwa na kukishwa mahakamani.

11

Bora ujirani mwema kuliko udugu wa ukhasama


Na Ibrahim Noor lilikuwa ni sura ya muungano wenyewe. Waswahili wana msemo usemao mwenye macho haambiwi tazama. Gwaride lilikuwa ni sauti kubwa na ya uwazi kabisa kuwa haya majeshi ndiyo yatakayoulinda muungano. Ukoloni uliokuwa na nguvu kubwa za kijeshi siku zote uliwadharau watawaliwa walipodai haki zao kwa kuwaona watawaliwa ni watu duni na watawala kujiona kuwa wanalo jeshi kubwa na kwa kuamini kuwa nguvu za kijeshi ndizo zitakazowashinda wananchi katika kudai haki yao. Wakoloni waliamini sana kuwa bunduki na risasi zitaweza kuuwa upiganiaji wa uhuru na haki za wananchi waliotawaliwa. Watanzania wenye fikra kama hizi hawajasoma vizuri katika taarikh za ukoloni, na la kusikitisha zaidi ni kuwa hawajasoma vya kutosha kutokana na taarikh yao wenyewe tokea walipoonekana kama ni watu duni na Watawala wao mpaka mtawala mwenyewe kusalimu amri na kuwapa uhuru wao watawaliwa wananchi wa Tanganyika. Uundaji wa muungano wenyewe, tokea aw ali, ulikuwa hauna uhalali wowote kutokana na wananchi wala haukuwa na lengo la umoja wa haki bali ulikuwa na lengo la kukandamiza. Haiwi ukitaka kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa bila ya kupata ridhaa za wananchi, lakini kuunda kubwa zaidi la muungano na nchi nyingine iwe Marais wawili -- Nyerere na Karume -- ndio inatosha waamue kufanya hivyo, na baada ya kuungana ndiyo wafanye mazingaobwe yao ya kuuhalalisha muungano batil; hili halikubaliki. Ubaya mkubwa sana ni kuwa Marais hao wawili walizifanya nchi wanazoziwakilisha mamlaka zao binafsi na wakachukua khatua bila ya kuwashauri wananchi kwa njia ya kura ya maoni. Hata mashirika ya biashara hayawezi kuungana bila ya wenye mali zao katika mashirika hayo kuulizwa na kushirikishwa katika kuamua huo muungano. Mashrika mengine inabidi kuwauliza wote waliokhusiana na mashirika hayo wamiliki, wafanyakazi, wanunuzi na kadhalika. Na ukizingatia usanii alioufanya Nyerere ya kumwondosha Wakili Mkuu wa Serikali ya Zanzibar asishiriki wala asiwe na nafasi ya kumshauri Karume kukhusu katiba iliyoandikwa na mawakili wake Nyerere, huku akijua ka kuwa Karume hakusoma na haelewi vizuri yaliyoandikwa kiqanuni, hili pekee linatosha kubatilisha Katiba ya Muungano. Pamepita mazingaombwe makubwa, na hii mizozano ni moja tu katika matunda ya sumu ya usanii. Wala matatizo hayatasita milele baina ya Zanzibar na Tanganyika. Wala kuziba viraka katika tambara bovu hakutaondosha matatizo bali yatazidi tu kila kukicha. Linalohitajiwa kwanza si kuziba viraka katika tambara raru bali kuwauliza wananchi iwapo wanautaka huo muungano ama la. Pili, iwapo wanautaka pande zote mbili, uwe muungano wa aina gani? Tatu, mambo yepi yawemo kwenye muungano na yepi yasiwemo. Hivi ifanywavyo sasa ya kuchukua maoni ya wananchi wachache au wa kuteuwa ni kuendelea na usanii wa kisiasa wakati matokeo yake yameshajulikana. Hiki ni kiinimacho ambacho hakihusiani na kuziondosha shida ziliopo na ni mazingaombwe ambayo yanazidi kuzielekeza kubaya hizi nchi mbili. Hata wananchi wa nchi zote mbili wakisema wanautaka muungano uendelee, mungano wa serikali mbili ni kudanganyana mchana kweupe. Hainiingii akailini pawe na serikali mbili, zilizofanya mkataba wa kuunda serikali ya muungano yenye kushughulikia mambo ya muungano na pia iwepo serikali ya Zanzibar, lakini ya Tanganyika isiwepo lakini badala yake ya Mungano iwe pia ni serikali ya Tanganyika! Ni wazi kabisa kuwa usanii huu ni moja katika mbinu za kuimeza Zanzibar, kama si leo, kesho. Kama lazima uwepo muungano, basi uwe wa serikali tatu. Mambo ya Tanganyika yawe wazi kabisa kama ni ya Tanganyika na ya Zanzibar yawe ya Zanzibar na ya muungano yawe ya muungano. Wala Zanzibar isipoteze utaifa wake na kiti chake katika Umoja wa Mataifa. Ukija muungano wa Afrika Mashariki, Zanzibar isiwakilishwe na yoyote ila na Wazanzibari wenyewe. Na ikitaka kuingia katika mikataba ya kimataifa isiwe ya kwenda kujidhalilisha Dar es Salaam kwa kuomba rukhsa kama ambavyo rukhsa mtumwa kwa bwana wake. Kwa mambo yalivyo hivi sasa, kila lililokuwa muhimu, Wazanzibari shuruti wakaombe rukhsa Dodoma; na wasipopewa rukhsa hawawezi kulifanya hata jambo hilo liwe linatakiwa na Wazanzibari tisini katika mia kama kwa mfano kujiunga na OIC. Kwa Wazanzibari na wengi wenye akili zao timamu, muungano huu haujaweza kudhihirisha faida zake bali ni mabaya yaliyozidi, kwani khasara zake ni kubwa zaidi kuliko faida zake. Wakati mwingi umepotezwa kwenye muungano huu usiokuwa na uadilifu na usawa na wenye kuibana Zanzibar kwa kila njia, huku propaganda zikitangaza kuwa ni muungano wa aina ya pekee katika Afrika ulioishi miaka 49 bila ya kututajia sifa hata moja ya uzuri wa muungano wenyewe kwa Zanzibar. Haya ni sawa na kusema kuwa Msumbiji ilitawaliwa na Waportugizi kwa miaka zaidi ya mia nne, kwa hivyo uhusiano wa kikoloni na Upochugizi bora uachiliwe uendelee! Najuwa ka kuwa Watawala wa Tanzania watastaajabu na kukereka kulinganishwa na Waportugizi, na kustaajabu kwao na hadi kuudhika kwao ni alama kubwa ya kuwa bado hawaelewi kuwa utawala wao ni wa kikoloni na utawala wa kikoloni siku zote ni muovu kwa watawaliwa. Asiyekuwa na uwezo wa kuliona hili si mwingine zaidi ya mtawala muovu. Ni wazi kabisa kuwa ingelikuwa Zanzibar iko huru kujitendea mambo yake ya ndani na ya nje ingelikuwa iko mbali kwa maendeleo ya kila aina. Ikiwa hukubaliani na mawazo haya, unahitaji kujichunguza ukweli wako ili uhakikishe haya yasemwayo majukwaani Zanzibar. Kuwa mkweli na vuta kalamu na karatasi; upande mmoja andika faida za muungano uliopo kwa Zanzibar na upande wa pili andika khasara zake uangalie mwenyewe jinsi khasaza zilivyokuwa ni nyingi kuliko faida inayopata Zanzibar kwa Muungano ambao kwa hakika si muungano. Kwa upande wa Tanganyika hata huna haja ya kuandika chochote, ikutoshe tu kuwa imepata faida ya kuwa ndio Tanzania, serikali yake ndiyo serikali ya muungano iliyo juu ya serikali ya Zanzibar. Kama muungano huu una manufaa, basi muungano na nchi nyingine za Afrika Mashariki na hata zaidi ya hizi lazima uwe na manufaa makubwa zaidi. Kinachozizuia nchi hizi kuungana ni nini? Hakuna hata nchi moja itakayokubali kuingia katika muundo wa muungano kama ulioko baina ya Tanganyika na Zanzibar. Muungano ambao hauko sawa kwa chochote. Nguvu zote na amri zote zinatoka Dodoma! Tumeelezwa na Wa t a n g a n y i k a w e n g i walioandika makala kuwa Watanzania wengi wanautaka muungano uendelee. Ni kweli kabisa kuwa Watanzania wengi wanautaka muungano uendelee. Lakini tujiulize: Ni Watanzania kutoka upande gani wa muungano wanaolilia muungano usivunjwe? Jawabu ni kuwa ni Watanganyika wengi ndiwo wenye kuutaka muungano usivunjike. Lakini pia ni ukweli kabisa kuwa si muhimu hata kidogo iwapo Watanzania wengi wanautaka muungano. Ni muhimu Wazanzibari wengi wawe wanautaka au hawautaki huo muungano. Hata iwapo Watanganyika wote wenye idadi zaidi ya milioni arubaini wanautaka muungano, muungano unakuwa hauna uhalali iwapo wengi ya Wazanzibari hawautaki, kwani huu ni muungano wa nchi mbili na wengi wa upande wowote ukiwa haupendelei muungano uendelee basi muungano unakuwa hauna uhalali. Kwa Watanganyika kushikilia lazima uwepo muungano ijapokuwa Wazanzibari wengi hawautaki inakuwa ni ya mkoloni kulishikilia koloni lake lisimtoke. Narejelea tena kusema kuwa iwapo Watanganyika wotewote wenye idadi ya zaidi ya milioni arubaini wakisema wanautaka muungano, na kwa upande wa pili zaidi ya nusu ya Wazanzibari ambao idadi yao hata haitafika milioni moja wakiamua kuwa hawautaki muungano, basi muungano ni batil; na hili ndilo linaloogopwa hata ukaona watu wanakataa kata kata kuwepo kwa kura ya maoni ya kuchagua kama wanautaka au hawautaki muungano. Inavyoonesha ni kuwa Wa z a n z i b a r i w e n g i hawautaki muungano, maana wamechoshwa nao kwa dhiki zake zilizoletwa na usanii na kubanwa Wazanzibari katika kila sehemu ya maisha yao. Juu ya hayo, muungano wenyewe si jambo lililokuwa na umuhimu ukikiria kwa makini. Na kukusanya maoni ya watu hapa na pale kama ifanywavyo hivi sasa ni mbinu ya kukwepa kura ya maoni. Huu ni usanii wa hali ya juu kabisa ya kuudanganya umma ili kukwepa hiyo kura ya maoni. Wala muungano hauna umuhimu wa maana ukizingatia kero na mashakil yake. Lenye umuhimu ni ujirani mwema. Hivi mambo yendavyo inaonesha wazi kuwa muungano huu hauwaridhishi Wazanzibari wengi. Na iwapo baada ya kuvunjika muungano Watanganyika watawafanyia Wa z a n z i b a r i n g u m u na vitimbi, basi itazidi kuthibitisha kuwa watawala hawakuwa na niya ya kuwa ndugu na jirani wema tokea awali. Nawatakia kila la kheri

Makala

RAJAB 1434, IJUMAA MEI 31- JUNI 5, 2013

AN-NUUR

HIVI karibuni tumesoma makala mengi yaliyoandikwa na Watanzania Bara na machache yaliyoandikwa na Wazanzibari kukhusu muungano. Makala zilizoandikwa na Watanzania Bara takriban zote zilikuwa zikiusifu na kuutukuza muungano, lakini makala na barua nyingi zilizoandikwa na Wa z a n z i b a r i , k h a s a katika mitandao, zilikuwa zinaonesha wazi kutokuridhika kwao na muungano na wengine kutaka muungano uvunjike leo kabla ya kesho. Katika maelezo ya Wazanzibari wengi unaona wazi kuwa muungano umewabana vibaya sana kiuchumi na katika mambo mengi mengineyo yanayoendesha nchi, na tumesoma vile wanavyoona uchungu kuiona nchi yao ilivyotawaliwa kwa m a b a v u n a Ta n z a n i a Bara. Lakini Tanzania Bara wengi hawahisi hivyo; wanaona utawala wao ni bora kuliko tawala zote zilizotangulia. Lakini ukitizama utaona kuwa aina ya muugano uliopo unaweza kulinganishwa na muundo wa ukoloni wa Kifaransa ambao ni tafauti na wa Kiingereza. Waingereza walitawala makoloni yao na waliotawaliwa walijua moja kwamoja kuwa wametawaliwa. Lakini, Mfaransa alizifanya koloni zake kuwa ni sehemu ya Ufaransa na mtawaliwa alikuwa na haki ya kuwa Mfaransa na hata kuhamia Ufaransa bila ya matatizo na kuweza kushiriki katika maisha na siasa za huko Ufaransa. Huu ndio muundo wa ukoloni wa Tanganyika juu ya Zanzibar. Wafaransa wengi sio kuwa walistaajabu tu kwanini katika hali kama hiyo ya watawaliwa kuwa wana haki Ufaransa kudai uhuru wao, bali Wafaransa wengi waliudhika sana kuona nchi zilizotawaliwa kudai uhuru wao. Sasa nenda ukawaulize waliotawaliwa na Wafaransa, kama vile Algeria, Ngazija na kwingi kwingineko, kwanini basi wakadai uhuru wao usikilize jawabu zao. Tanzania Bara pia, kama Wafaransa, wanastaajabu sana wanapowasikia Wazanzibari wengi wakidai uhuru wao watokane na utawala wa mabavu wa Bara, lakini Wazanzibari wengi wanaoathirika na muungano hawana taabu ya kukuelezea yanayowaathiri wao na nchi yao. Hivi karibuni tumeshuhudia pia gwaride la majeshi ambalo

12

AN-NUUR
MAKALA

Taasisi ya Khidmat Islamiya inawatanganzia Waislamu wote Safari ya Hijja kwa Gharama ya Dola 4450 tu. unaweza kulipa kwa awamu (Kuhijiwa) ni Dola 1450 tu. Kuondoka ni 5/10/2013 kurudi 27/10/ 2013 Piga Simu 0784 786680, 0713 986 671, 0774 786 680 E-Mail) hajjkhidmat@gmail.com , Tovuti (Website) www.khidmatislamiya.com

Safari ya Hijja Dola 4450 tu. 1434/2013

12

RAJAB 1434, IJUMAA MEI 31, JUNI 5, 2013

Hatari ya kuchafuka amani nchini:


Na Bakari Mwakangwale SERIKALIimetakiwa kuwa macho na propaganda za udini zinazoelekezwa dhidi ya jamii ya Waislamu nchini kwani inaashiri mwisho mbaya. Tahadhari hiyo imetolewa na Shura ya Maimam wa Ahlu Sunna Waljamaa ya Jijini Arusha, katika Kongamano lililofanyika, Mei 26, 2013, katika Msikiti wa Ijumaa, Bondeni, jijini humo. Akisoma tamko la Waislamu katika Kongamano hilo, kufuatia mlipuko wa bomu uliotokea hivi karibuni katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Josefu Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, Ustadhi Mustafa Kiago, alisema Waislamu wanaitaka Serikali kujifunza kwa yaliyojiri nchini Rwanda, kisha itekeleza wajibu wake inavyostahili ili kuondoa mmomonyoko wa amani nchini. Kwa upande wetu tunaona huu ni wakati muafaka kwa Serikali na jamii mbali mbali kutafuta suluhisho la kudumu la matatizo yaliyojitokeza ili kudumisha amani na utulivu, badala ya kuacha propaganda hii ya chuki dhidi ya jamii ya Waislamu itawale, Alisema Ustadh Kiago. Alisema, hivi sasa imekuwa ni jambo jepesi kuwanyooshea vidole Waislamu pasi na kuwa na ushahidi, hata pale matukio ya mashambulizi au ya mauaji ambayo yana hitaji uchunguzi wa vyombo vya usalama na Jeshi la Polisi. Ustadh Kiago alisema mfano hai ni matamshi ya Askofu Laizer wa Kanisa Kuu la Kilutheri (KKKT)Arusha, aliyoyatoa katika vyombo mbalimbali vya habari mwaka jana May 2012. Alisema, Askofu huyo alizusha kuwa anazo habari za kutosha na za uhakika kuwa kuna vijana zaidi ya 300 wa Kiislamu katika eneo la Unga Limited katika Msikiti mmoja wakifanya mazoezi ya Kareti tayari kujiandaa kufanya uhalifu katika Makanisa. Ustadh Kiago alisema siyo tu kwamba Askofu huyo aliwasingizia Waislamu jambo la uongo, bali tayari alipandikiza chuki kwa Wa k r i s t o w a w a c h u k i e Waislamu na kuwaona ni maadui zao. Shura hii ya Maimamu ililaani vikali shutuma hizo, lakini Serikali iliukalia kimya uzushi huo, wala haikumtaka Askofu huyo athibitishe au kukanusha, hili ni moja kati ya mambo ambayo ni viashiria vya wazi

Serikali yatwishwa lawama


vya kuandaa mazingira ya kuhatarisha amani katika nchi yetu baina ya makundi mawili ya kidini. Alisema Kiago. Kiago alisema ifike mahali sasa kwa baadhi ya viongozi wa siasa na wale wa Madhehebu mengine ya dini wawe na uadilifu, pindi tukio la jinai linapotokea iachwe sheria ichukue mkondo wake. Tunavishauri vyombo vya dola kufanya shughuli zake kwa umakini katika kuyafuatilia kwa ukaribu matukio hayo na kutoipa

Na Bakari Mwakangwale

Mchawi ghasia Mtwara ni Serikali yenyewe, CCM


zinazopelekea vurugu hizo ni kutokana na Serikali kuicha nyuma kimaendeleo Mikoa ya Kusini kwa muda mrefu na yanayoibuka sasa ni kikomo cha uvumilivu wao. Machano alikumbushia kauli ya Rais Kikwete, alipoongea na Wabunge mwanzoni mwa utawala wake, aliyethitishia Bunge kwamba kuna mikoa ambayo ipo nyuma kimaendeleo. Kwa mujibu wa Ust. Machano, alidai miongoni mwa Mikoa aliyoitaja Rais Kikwete, ni Kigoma, Tabora, Tanga, Lindi na Mtwara, na ambaye aliahidi kufanya juhudi kuhakikisha inakwamuka kiuchumi. Alisema, wananchi wa Mtwara, wanaona hakuna dalili yoyote ya kuinuliwa kiuchumi, na zaidi chini ya Serikali ya CCM, wanaumizwa katika masuala ya malipo ya mazao yao ya Korosho, kupitia stakabadhi ghalani. Mbaya zaidi, Ust. Machano, alisema ni kuona Rais huyo huyo anataka gesi isarishwe kwenda, Dar es Salaam, na kupingana na wananchi wa Kusini. Ust. Machano, alisema wananchi wa Mikoa ya Kusini wamekuwa wavumilivu kwa muda mrefu, pamoja na kubaki nyuma kimaendeleo tokea nchi hii ipate uhuru. Alisema, ukifatilia rekodi katika chaguzi kuu wa (Rais, na Wabunge) utabaini kwamba Mikoa ya Kusini inaongoza kwa kuichagua CCM, huku chama hicho kikiifanya mikoa hiyo kuwa ni shamba la bibi la kuvunia kura za Chama hicho, kisha kuwatekeleza. Ust. Machano, alisema ustaarabu huo wa uvumilivu wao na kufanywa daraja kila uchaguzi unapoka bila kujali hali zao za kiuchumi wanapoingia madarakani, ndiyo inayowapa jeuri viongozi hao kupuuza maoni yao kuhusu suala la gesi. Ust. Machano, aliwatanabahisha viongozi wa Serikali kwamba, binaadamu ana kikomo cha uvumilivu, na kwamba sasa wananchi wa Mtwara wanaamka na wamechoka na ahadi zisizotekelezeka. Alisema, msimamo wa wananchi wa Mtwara, ni kutokana na kuelewa mwenendo wa Serikali yao, kwamba gesi hiyo ikisafirishwa, wao hawatonufaika nayo kama ilivyo katika zao la Korosho. Alisema, Serikali inatakiwa kutoa majibu sahihi yatakayo kinaisha akili na kra zao kutonana na hoja zao, lakini alidai, majibu mepesi na rahisi ya Serikali

nafasi propaganda iwe ndio mwongozo wao ili isiwe ni chanzo cha Taifa letu kutumbukia katika vurugu za kidini. Alisema Ustadh Kiago. Kiago alitaadharisha kwamba mauaji makubwa yaliyotokea nchini Rwanda, yalianza katika sura kama hiyo ambapo jamii moja ilikuwa ikisingiziwa maovu. Alisema, wakati jamii hiyo ikilalamika kuhusiana na propaganda hizo, vyombo vya dola na wanasiasa wake walipuuza na kuegemea upande mmoja wa jamii ya Wanyarwanda bila ya kufanya juhudi za kufuatilia uhakika wa Propaganda

na dhuluma zilizokuwa zikilalamikiwa. Aliitanabahisha Serikali, viongozi wa Madhebu yote pamoja na wanasiasa na jamii kwa ujumla kwamba, Kimsingi katika nchi hii hakuna mgogoro kati ya Waislamu na Wakristo. Alisema makundi hayo mawili huko mitaani yanaishi pamoja kwa kushirikiana katika mambo mbalimbali ya kijamii. Hivyo alisema, Serikali itambue kuwa kuna watu wachache ambao wanataka kulitumbukiza Taifa katika machafuko, na kwamba ikiwa makini (Serikali) ina uwezo wa kuzima vuguvugu hili linaloashiria hali mbaya nchini.

SERIKALI na Chama tawala Cha CCM, vimetajwa kuwa ndiyo chanzo cha vurugu Mkoani Mtwara, kwa kuicha nyuma kimaendeleo mikoa ya Kusini. Madai hayo yametolewa na Ustadhi Salum Machano, akiwahutubia Waislamu Ijumaa ya wiki iliyopita Masjidi Haqa, Buguruni Jijini Dar es salaam. Ust. Machano, alikuwa akizungumzia vurugu zilizoibuka mapema wiki iliyopita Mkoani Mtwara, wananchi wakigomea mpango wa Serikali kuisafirisha Gesi kwenda Jijini Dar es Salaam, kutoka Mkoani humo. Akitoa taarifa Bungeni, kufuatia ghasia zilizoibuka Mkoani Mtwara, wiki iliyopita Waziri wa Mambo ya ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, alisema, Serikali itahakikisha inawasaka vinara wa vurugu hizo ndani na nje ya nchi na kuhakikisha inawatia mbaroni. Ust. Machano, alisema Serikali isitafute mchawi kufuatia kuibuka kwa vurugu zinatokana na sakata la gesi bali wachawi ni wao wenyewe. Akifafanua, Ust. Machano, alisema sababu

hayawezi kufuta msimamo walionao zaidi ya kulipoza na kuibuka mara kwa mara. Ust. Machano, alisema katika nchi hii kuna wananchi wapo katika shida kwa muda mrefu, wakiwemo watu wa Mikoa ya Kusini. Matumizi sahihi ya akili ni kuhoji unapoletewa maelezo au taarifa, lazima mwenywe akili timamu ahoji ili apate ufafanuzi, na ndio maana Mitume wote walipata changamoto kutoka kwa watu wao na wao (Mitume) walikuwa wakijibu hoja, na si vitisho. Alisema Ust. Machano. Alisema, katika Quran suratul Bakara, Allah (sw), amemzungumzia Nabii Ibrahim, baba wa Imani kwamba ametumia akili yake vizuri katika kuhoji. Nabii huyu alihoji kwa Allah akitaka kujua ni vipi atamfufua mwanaadamu siku ya kiama, ili moyo wake upate yakini zaidi. Alisema Ust. Machano. Ust. Machano, alidai kwamba ni kawaida ya viongozi ambao wameishiwa majibu kwa watu wanaowaongoza, kutokana na kutokuwa na ahadi za kweli, na kinyume chake badala ya kujibu hoja huwashambulia.

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

You might also like