You are on page 1of 12

www.annuurpapers.co.

tz

Sauti ya Waislamu

Agizo la Maaskofu lazua balaa Mbeya


Msikiti wachomwa moto Tunduma Mwingine wanusurika kimaajabu Ilikuwa kama Kaba na Jeshi la Tembo

ISSN 0856 - 3861 Na. 1065 JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA -APRILI 5 -11, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Mwenyezi Mungu amesema katika Qur ani, wenye kukufuru kwa kutokwenda Hijja (baada ya kupata uwezo), Allah hana haja na viumbe wote! (3:97) Hii ni hatari! Wenye uwezo wasipoisimamisha Hijja ipasavyo, Allah Anatughadhibikia sote! Si balaa hili? Tutubu kwa kuhimizana, kushirikiana, na kuhamasishana. Karibuni Ahlu Sunna wal Jamaa. Gharama zote ni Dola 4,300. Tafadhaliwasiliana nasi ifuatavyo: Tanzania Bara: 0717224437; 0777462022;Unguja: 0777458075;Pemba: 0776357117.

(10) HASARA ZA KUTOHIJI ZINATUENEA SOTE!

Hakuna upepo mbaya wala shetani Tanzania

Rais Kikwete hajasomewa Itiqaafu Ushahidi wa upendeleo huu hapa Masheikh wetu wanashangaza sana

BAADHI ya kinamama wa Kiislamu wakishiriki katika zoezi la kuchangia damu salama lililofanyika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam wiki iliyopita. Habari kamili Uk. 12.

Kukamatwa mtuhumiwa Uamsho wafutiwa kesi Mauwaji ya Padiri Mushi Lakini kitanzi bado kipo shingoni
RAIS Jakaya Kikwete

Soma Uk. 6

SHEIKH Khamis Mataka

Polisi, DPP : Ni Sarakasi na utata mtupu Je, alikamatwa kumridhisha Kardinali Pengo?

Na Mwandishi Wetu

MAHAKAMA ya Mwanakwerekwe, Zanzibar, imefuta kesi iliyokuwa

ikiwakabili viongozi kumi wa Jumuiya ya Uamsho, visiwani Zanzibar. Mahakama hiyo, imekia Inaendelea Uk. 3

2
AN-NUUR

Tahariri/Habari/Tangazo

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA APRILI 5-11, 2013

AN-NUUR

S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Itiqaaf zitawachua viongozi madhalimu


Na Bakari Mwakangwale I M E D A I WA k u w a utaratibu unaoendelea wa Waislamu kumshitakia Mwenyezi Mungu shida zao, utawafichua viongozi madhalimu. Ikaelezwa kuwa hiyo ni kwa sababu kila aliyedhulumu huwa na wasiwasi kuwa dua itampata kwa udhalimu wake aliofanya hivyo hatakosa kuweweseka. Kwa muda sasa Waislamu wamekuwa wakifanya Ibada ya Itiqaf kila Jumamosi katika Misikiti mbalimbali ya Jijini Dar es Salaam. Wakiongea kwa nyakati tofauti, baadhi ya viongozi wa Itiqaf, wamesema kimsingi dua hizo zimeanza kufanya kazi. Imam wa Msikiti wa Tungi, Temeke Jijini Dar es Salaam, ambao ni moja ya Misikiti uliyofanya Ibada hiyo, Sheikh Shaaban Ibrahim, amesema Rais Kiwete amekuwa kimya muda wote Waislamu wanapolalamika na kuibuka sasa baada ya Waislamu kuamua kumueleke Mwenyezi Mungu. Imam Ibrahim, akasema Rais Kikwete, hapaswi kuwa na hofu na ibada hiyo, kwani hakuna siku ambayo ametajwa kiongozi yoyote wa nchi, katika Itiqaf hizo bali Waislamu wamekuwa wakimlilia Mungu wao, baada ya kutumia njia zote kuomba haki zao kukwama. Sisi tumeamua kumshitakia Mwenyezi Mungu, kwa ujumla tunaomba katika Itiqaf zetu kuwa kama kuna mtu anaufanyia hila Uislamu na Waislamu wa nchi hii, basi Allah (s.w), apindue hila zao na amkuhukumu mtu huyo kwa ubaya wake. Alifafanua Imam Ibrahim. Imam Ibrahim alisema, kwa kawaida ya Dua haimgumsi mtu ambaye hana tatizo husika, na kama yeye (Rais) anajiona hana mkono katika madhila yanayowakuta hivi sasa Waislamu, hana sababu ya kuwa na wasiwasi kwani Mwenyezi Mungu hadhulumu mtu. Tu n a s e m a k w a s a s a mwendo ni wa dua katika usiku wa Itiqaf kila jumamosi, na hatutoacha kwani hakuna mwingine wa kumlilia zaidi ya Allah (sw), na Jumamosi ijayo (Kesho) tunaendelea na Itiqaf, katika Msikiti wa Makukura, Buguruni. Alisema Imam Ibrahim. Alisema, hoja ya Waziri Mkuu kukutana na viongozi wa dini, ni hoja walishaitoa siku nyingi, lakini katika hatua hiyo, aliasa kuwa pawe na mazingatio kwamba hao viongozi wa dini wawe ambao wanakubalika na Umma wa Kiislamu. Naye Ustadhi Abubakar Shaaban, aliye Mratibu wa Elimu ya Dini ya Kiislamu Temeke, alisema Waislamu hawamlengi mtu katika dua zao zinazoendelea hivi sasa, bali ni kwa yoyote yule anayekusudia kuwafanyia shari Waislamu. Sisi tunasema kwamba Itiqaf zitaendelea sana na bado zipo sana lakini si kwa ajili ya mtu fulani, hatumkusudii Mwema (IGP), wala Kova, wala Mh. Rais Kikwete, tunamkusudia yoyote hata kama ni Sheikh wa Msikiti,

MAONI YETU

Kamishna wetu Mussa haya ndiyo mliyojifunza kwa FBI?


K AT I K A g a z e t i l a Mwananchi la Jumamosi iliyopita ukurasa wa pili ipo picha iliyoelezwa kuwa ndiyo picha ya siku. Picha hiyo inamwonyesha mtoto mdogo akibusu Kinyago kilichochongwa kuwakilisha mwili wa Yesu kikiwa kimepigiliwa misumari katika Msalaba. Maelezo ya picha yakasema kuwa huyo ni muumini wa Kanisa Katoliki akibusu msalaba alipohudhuria ibada ya Ijumaa Kuu katika Kanisa la Msimbazi jijini Dar es Salaam. Tuseme kuwa hakuna Muislamu mwenye tatizo na Wakristo kwa vile eti w a n a a m i n i k u w a Ye s u aliyezaliwa na kutahiriwa siku ya Saba na baadae kutundikwa msalabani kuwa ndiye Mungu Mkuu wao mwokozi wao. Wa i s l a m u w a n a w e z a wasikubaliane na imani hiyo kama ambavyo Wakristo hawakubali kuwa Mungu ni Mmoja asiye katika Utatu kama wanavyoamini Waislamu, lakini haiwezi kuwa sababu ya kugombana. Wakiparurana, basi kuna mmoja kamdhulumu na kumuonea mwenzake. Na dawa hapo ni kumwambia anayedhulumu aache dhulma. Baada ya kusema hayo, labda tukumbushe mambo mawili. Katika mauwaji ya Mwembechai baadhi ya vyombo vya habari viliwahi kuchapisha picha ya polisi aliyeshika rungu akiwa kamkwida mtoto mdogo chini ya miaka 10 ambaye (mtoto huyo) anaonekana kushangaa tu. Maelezo katika picha hiyo yakasema kuwa hivi ndivyo Polisi walivyozidiwa nguvu na Waislamu (hadi kutumia risasi za moto na kuuwa.)! Kipo pia kile kisa cha wanawake wawili wa Zanzibar (Pemba?) waliotolewa katika vyombo vya habari wakiwa wameshika mapanga wakiwa

Yasije tu kuwa yale ya mtoto wa Mwembechai Au wale wanawake magaidi walioshika panga
na nyuso za kushangaa na za huzuni. Jeshi la Polisi likasema kuwa hao ni baadhi ya magaidi waliotaka kuvamia vituo vya Polisi na kupora silaha. Kwa leo tuachane na hayo maana Waswahili wanasema yaliyopita si ndwele. Habari zilizopo ni kuwa Jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa mauwaji ya Padiri Evarist Mushi. Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari, Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa alisema kuwa walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo baada ya kuchora michoro ya sura ya mtu kwa kutumia watu walioshuhudia tukio kisha kuandaa utaratibu ambapo watu mbalimbali walifanya utambuzi wa muhalifu huyo. Swali ambalo pengine Watanzania wangependa kujua ni hili: Je, huu ndio utaalamu Polisi wetu waliojifunza kutoka kwa FBI? Je, wasingewaalika FBI, wasingeweza kufanya mchoro huo na kufanya gwaride la utambuzi? Tunavyojua ni kuwa ili Polisi wamkamate mtu na kumtuhumu kwa uhalifu fulani, ni lazima pawe na mazingira na sababu za kutosha za kujenga tuhuma hizo. Matumaini yetu ni kuwa hayo yote yamezingatiwa katika ukamataji ambao tunaambiwa kuwa ushafanyika. Lakini la pili ni matarajio yetu pia kuwa, taratibu zote za kisheria na haki zitazingatiwa katika kulitizama shauri hili na kwamba Polisi na waendesha mashitaka watafanya kazi yao kitaalamu na kwa uadilifu. Hatutarajii kwamba jambo hili litaongozwa na kuathiriwa na kauli kali kali za Maaskofu ambao tunaambiwa kuwa wameijia juu Serikali. Wala hatudhanii kuja kuona kuwa kuna watuhumiwa wamekamatwa huku wenyewe na wananchi wanaowafahamu wakibaki wakishangaa kama alivyokuwa akishangaa yule mtoto aliyedaiwa kuwazidi nguvu Polisi Mwembechai!

anayeufanyia hila Uislamu pamoja na Waislamu. Alisema. Akizungumzia madai kuwa Serikali inawapendelea Wakristo, Ust. Salim Machano, alisema Waislamu hawaongei bila kuwa na ushahidi. Alisema,, Waislamu wanavyo vigezo na ushahidi ni jinsi gani Serikali inavyo libeba Kanisa na kuwapuuza Waislamu na kwamba kukanusha hoja Machano.

anakokanusha Rais Kikwete ina maana anakana pia kauli zake mwenyewe. Ust. Machano, alianisha na kunukuu misaada ambayo Rais, mwenyewe alitamka kama msaada kwa Kanisa, kuwa Machi 19, 2011, katika shere za kusimikwa Askofu Gervance Nyaisonga, Rais Kikwete alisema kuwa katika bajeti ya mwaka 2 0 1 0 - 2 0 11 , M a k a n i s a yalipewa Tsh. Bil 61.9. Na kwamba katika bajeti 2009-2010, Makanisa yalipewa Tsh bil. 50, ambapo katika gazeti moja litokalo kila siku la Machi 20, 2011, lilinukuliwa likidai kuwa katika kila bajeti ya Serikali kuna asilimia fulani kwa Makanisa kwenda katika sekta ya elimu na afya, kutokana na MoU ya mwaka 1992. JK, anaposema Serikali yake haipendelei dini yoyote ina maana anayakataa maneno yake? Au mbona lile gazeti lililonukuu taarifa ile hajawahi kukanusha. Waislamu sio wajinga, anachotakiwa ni kurekebisha hali hii ili usawa na haki vipatikane. alis ema na kuhoji Ust.

Itkaf Masjid Makukura

Uongozi wa Masjid Makukura - Buguruni jijini Dar es Salaam unawaarifu Waislamu wote kuwa, kutakuwa na Ibada maalum ya Itkaf msikitini hapo. Siku: Jumamosi (kesho) tarehe 06/04/2013 baada ya swala ya Ishaa. WOTE MNAKARIBISHWA WABILLAH TAWFIQ

Habari

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA APRILI 5-11, 2013

AN-NUUR

Agizo la Maaskofu lazua balaa Mbeya


Na Bakari Mwakangwale Alisema, kabla ya vurugu hizo palifanyika kikao kikubwa Mjini hapo kilichoshirikisha Mkuu wa Mkoa, Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC), na maofisa wengine wa Mkoa kwa ujumla. Alisema Ust. Twahir, kwamba katika kikao hicho, kilichofanyika katika Hoteli ya Ukinga Hill, Mkuu wa Mkoa, Bw. Kandoro, alisisitiza kuheshimu maamuzi ya Serikali, kwamba suala la kuchinja libaki kama lilivyokuwa awali wakati likitafutiwa ufumbuzi wake. Maaskofu walimjibu Mkuu wa Mkoa kuwa wao wamepata maagizo kutoka kwa viongozi wao wa Baraza l a M a a s k o f u Ta n z a n i a (TEC), na waliisoma barua ya maagizo hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa, Bw. Abbas Kandoro, na RPC. Alisema Ust. Twahir. Imedaiwa kuwa baada y a h a p o Wa k r i s t o h a o walifanya nguvu kuchinja siku ya Jumatatu na Jumanne, bila kuruhusiwa baada ya kuhamasishwa na Maaskofu wao wa Taifa. Ustadh Twahir alisema wale waliogoma kuchinjiwa na Waislamu, walinukuu maagizo ya Maaskofu wao kuwa ni marufuku kula kilichochinjwa na Muislamu, hivyo walidai hawawezi kwenda kinyume na viongozi wao. Twahir alisema baada ya kugomewa kuchinja, walianza kufanya fujo mitaani na chaajabu alidai fujo hizo zilielekezwa katika Misikiti hapo mjini. Alisema, kundi kubwa la Wakristo walivamia Msikiti Mkuu wa Ijumaa, Masjid Jamaa, wakiwa na matairi ya magari na petroli, lakini zoezi la kuwasha moto lilishindikana kwa Kudra za Mwenyezi Mungu. Matairi yalikuwa yanatoa moshi tu bila kuwaka, mpaka walipoka askari na kuanza kuwakamata na kuwatawanya, na wengine wakakimbia. Alisema Ustadh Twahir. Nassoro Msham, aliye msimamizi wa Msikiti uliovunjwa na kuchomwa moto, alise m a M s i k i t i umebomolewa kuta, milango na madirisha sambamba na kuchomwa moto, majira ya saa saba mchana siku ya Jumatano. Ust. Mussa, alisema Msikiti huo umejengwa kwa nguvu za Waislamu, katika harakati za kuongeza nyumba za Ibada kwa Waislamu, pamoja na mafundi wanaojenga barabara iendayo Sumbawanga. Kwa upande wake alisema, sababu kubwa za vurugu hizo ni mvutano wa suala la kuchinja, ambapo alika Mkuu wa Mkoa na kukutana na viongozi wote wa Dini, na katika kikao hicho, alishauri suala hilo wasubiri maamuzi ya ngazi za juu baada ya Waziri Mkuu kukutana na viongozi wa Dini. Lakini alisema, Wakristo hawakukubaliana na maelezo hayo ya Mkuu wa Mkoa Bw. Abasi Kandoro, ambapo siku ya Jumatano wiki hii, walikusanya ngombe wao na kwenda machinjioni, lakini ilishindikana wao kuchinja kutokna na ulinzi kuwa mkali. Waliposhindwa huko sasa walirudi huku mjini kwa jaziba na hasira, walianza kufanya maandamano na fujo za kila aina, kwakweli hali ilikuwa ni mbaya kwa siku nzima hapa Tunduma. Alisema Ustadh Mussa. Ustadh Mussa alisema vurugu hizo zilizidi na Wa k r i s t o h a o w a l i a n z a kuelekea katika Misikiti ya Mjini na kuvamia Msikiti Mkubwa wa Ijumaa. Alisema, baada ya kushindwa kuudhuru Msikiti huo, ambapo moto waliowasha ulikuwa ukigoma kuwaka kuchoma Msikiti, ndipo walielekea katika Msikiti uliopo mbali kidogo na eneo hilo la mjini, katika Msikiti mpya uliokuwa ukiendelea kujengwa, wakiwa na mashoka, mapanga na mawe pamoja na vyuma. Huu Msikiti ulikuwa katika

AGIZO la Baraza la Maaskofu kuwataka waumini wao kuchinja na kuacha mara moja kula nyama inayochinjwa na Waislamu, limezua balaa mjini Tunduma. Msikiti mmoja umechomwa moto huku mwingine ukinusurika kimaajabu kama ilivyonusuriwa Al-Kaaba ilipovamiwa na Jeshi la Tembo. Hayo yametokea kufuatia vurugu zilizotokea juzi kutokana na hatua ya baadhi ya maaskofu kulazimisha Wakristo kuchinja katika machinjio ya mji. Taarifa kutoka katika mji huo mdogo wa Tunduma, zimeeleza kuwa, vurugu hizo zimeibuka baada ya Maaskofu kudaiwa kulazimisha kutekeleza maagizo ya Baraza la Maaskofu Taifa (TEC), likiwataka Wakristo kuchinja. Taarifa hizo zimeeleza kuwa kabla ya kuibuka kwa vurugu hizo siku ya Jumatano wiki hii, palifanyika kikao baina ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Abbas Kandoro, Kamanda wa Polisi mkoa (RPC) pamoja na viongozi wa Dini, Maaskofu na Masheikh. Hata hivyo, Maaskofu hao imedaiwa kugomea rai ya Mkuu wa Mkoa, pale alipowataka kuwa na subira wakisubiri, wakati Serikali ikilitafutia ufumbuzi suala hilo kitaifa. Katika vurugu hizo, baadhi ya mashuhuda wamelieza gazeti hili kwa njia ya simu kuwa, Msikiti wa Ijumaa, Masjidi Jamaa, mjini hapo ulinusurika kuchomwa moto na watu wanaodhaniwa kuwa ni Wakristo, waliokasirika kuzuiwa kuchinja huku Msikiti mpya ukiharibiwa vibaya na kuchomwa moto na watu hao. Sijafanya tathmini kamili, kutokana na uharibifu huo, lakini kwa haraka haraka ninavyoona hapa inaweza kufika kiasi cha Tsh. 12 milioni. Alisema Ustadhi Nassoro Msham, akithibitisha uharibifu uliofanywa katika Msikiti huo. Akisimulia tukio hilo, kiongozi wa Masjid Jamaa, Ustadhi Twahir Mussa, alisema vurugu hizo zimetokana na Maaskofu kulazimisha kuchinja, na kukaidi maelezo ya Mkuu wa Mkoa Bw. Abbas Kandoro.

Kukamatwa mtuhumiwa Mauwaji ya Padiri Mushi


Na Mwandishi Wetu
WAKATI Mahakama Kuu Zanzibar ikiamuru kuletwa mahakamani kwa mtuhumiwa wa mauaji ya Padri Evaristus Mushi, utata mkubwa umegubika suala la kukamtwa mtu huyo baada ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) Zanzibar kuinyima Polisi kibali cha kumfikisha mahakamani. Mtuhumiwa huyo Omar Mussa Makame (37) aliyekuwa mgombea uwakilishi wa Jimbo la Rahaleo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 kupitia tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) bado anashikiliwa na polisi Zanzibar na anatetewa na Kampuni ya Uwakili ya AJM Solicitors and Advocate. Mtu huyo, Omar Mussa Makame wa Zanzibar alitarajiwa kupandishwa kizimbani juzi, lakini ofisi ya DPP ilikataa kutoa kibali kwa Polisi kufanya hivyo. Awali Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisema kuwa wameshindwa kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo kwa vile DPP hakuwapa kibali. Alipoulizwa sababu ambazo zimemfanya DPP asitoe kibali hicho, alisema ni vyema akaulizwa yeye mwenyewe kwani ndiye aliyetoa sababu hizo. Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar, Ibrahim Mzee Ibrahim alipofuatwa osini kwake juzi ilielezwa kuwa yuko kwenye mkutano na mwandishi wa habari hizi akalazimika kumuandikia juu ya suala hilo kupitia kwa Katibu Muhtasi wake. Alijibu kwa njia ya maandishi majibu yake yakiwa na maneno matatu tu: Kamuone Kamishna Mussa. Alipoandikiwa tena kuwa Kamishna Mussa ndiye aliyesema aulizwe yeye kwani ndiye uliyetoa sababu alijibu kupitia kwa Katibu Muhtasi wake: Yeye (Kamishna) anazijua sababu kwa nini hataki kuzisema? Nendeni kwake mukamuulize. Alipoulizwa mara ya pili juu ya majibu hayo ya DPP Ibrahim, Kamishna Mussa alisema kwamba yeye hawezi kujibu mambo ya mtu mwingine. Ndio majibu yake ninayo, lakini yeye (DPP) ndiye aliyetoa sababu kwa hiyo ndiyo yeye anayetakiwa kuzisema sio mimi,

hatua za mwisho za ujenzi, ulikuwa ushapigwa bati, plasta, na kuwekwa milango na madirisha, tulikuwa katika hatua ya kuweka sakafu tumalizie, sasa wamechoma moto bati zimeungua na chini kumebomolewa. Alisema Ustadh Masham. Alisema, wakati tukio hilo likitokea, la kuchoma na kuvunja Msikiti huo, Waislamu walikuwa eneo la mjini wakilinda Misikiti hiyo, na hawakudhania kuwa Wakristo hao wataka huko kutokana na umbali wake. Alipoulizwa kama kuna Waislamu waliokamatwa katika vurugu hizo, alisema katika tukio hilo Waislamu, hawakujibu mashambulizi, bali muda mwingi walikuwa Msikitini pasi na kutoka.

Uamsho wafutiwa kesi


Inatoka Uk. 3

nadhani hii ndiyo haki, aseme mwenyewe, alisema Kamishana Mussa. Mtuhumiwa huyo yuko mikononi mwa Polisi tangu Machi 17 mwaka huu alipokamatwa kuhusiana na mauaji hayo ya Padre Mushi aliyeuawa Februari 17 mwaka huu wakati akienda kuongoza ibada katika Kanisa la Mtakatifu Teresia liliopo Beit el Raas nje kidogo ya mji wa Zanzibar. Kwa upande mwingine, juzi mchana wakili wa Kampuni inayomtetea mtuhumiwa, Abdalah Juma Mohamed aliwasilisha Mahakama Kuu ya Zanzibar maombi ya Habeas Corpus Application chini ya kifungu cha 390 cha Sheria Inaendelea Uk. 5

uwamuzi huo wakati viongozi hao walipokishwa Mahakamani hapo mapema wiki hii. Katika kesi hiyo, watuhumiwa walidaiwa kuwa walitoa matamko ya uchochezi yanayohatarisha uvunjifu wa amani na kusababisha fujo. Hakimu Ame Msaraka Pinja amesema kuwa ameamua kufuta kesi hiyo kutokana na upande wa mashitaka kushindwa kukamilisha ushahidi wa kuwatia hatiani

watuhumiwa. Hata hivyo, Masheikh hao bado wanaendelea kuwepo rumande kutokana na kesi nyingine inayowakabili iliyo katika Mahakama Kuu Vuga. Hiyo ndiyo kesi ambayo Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali, DPP, amezuiya dhamana. Pamoja na kesi hiyo katika Mahakama Kuu, zipo pia kesi nyingine mbili zinazohusiana na maandamano na mihadhara zilizopo katika Mahakama za Mwanakwerekwe na Mfenesini.

4
Na Ally Selemeni MAKALA hii imeitwa safari toka Nuruni kwa sababu Waislamu tumeiacha nuru ya Uislamu na kutumbukia katika giza la kuiga tamaduni za kimagharibi. Hakuna kipindi ambacho wanadamu wamekuwa wakiyumba kiujuzi na k iu tamad u n i k ama iliv y o katika zama hizi za utandawazi (Globalization). Jamii inapita katika mabadiliko makubwa huku kasi ya mabadiliko hayo ikitofautiana, lakini kila mahali tunaiona nguvu ile ile ya mabadiliko ambayo haitoi mwanya wa kusimama wala kujiuliza. Katika hili ulimwengu wa Kiislamu haujanusurika. Tunaona desturi na fikra za zamani zinatoweka na mpya zinachukua nafasi. Je, hali hii inatupeleka wapi na ni kwa kiasi gani inaoana na dira na mfumo na utamaduni wa Kiislamu? Makala hii haitoi majibu kamili ya maswali hayo yote. Bali inaangalia kwa kina tatizo moja kati ya matatizo mengi yanayowakabili Waislamu hivi leo, yaani ni upi msimamo wetu Waislamu kuhusu utamaduni wa kikari. Mbali na watu kutotangamana kiimani, lakini ipo sababu nyingine ambayo kimsingi inawalazimisha Waislamu kuepuka kuiga ustaarabu na utamaduni wa kikafiri (Umagharibi), ambao una mambo mengi yaliyosheheni chuki ya ajabu dhidi ya Uislamu. Kwa kiasi fulani chuki hizo zimerithiwa toka Ulaya ya

Makala

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA APRILI 5-11, 2013


mrefu bila kupatiwa suluhu. Nayo sio nyingine bali ni dhana ya udini na hata baada ya kujidhihirisha, bado haionekani juhudi ya kistaarabu ya kuondoa dhana hii. J e , n i w a p i Wa i s l a m u tulipokosea? Uislamu una tatizo gani? Je, ni kweli Uislamu ni nguvu iliyokwisha kama wasemavyo maadui na waliokata tamaa miongoni mwetu? Je, Uislamu umeishiwa hoja na hakuna tena manufaa kwa walimwengu? Je, ni kweli Uislamu umedhoofu? Historia inatufundisha kuwa ustaarabu na tamaduni zote za binadamu zina uhai sawa na ule wa viumbe vingine vyenye uhai. Hupitia katika awamu mbalimbali sawa na viumbe vyenye uhai, huzaliwa hupitia ujana, utu uzima, uzee na hatimaye hutoweka kabisa. Tamaduni nazo hufa zikifikia mwisho wake na kutoa mwanya kwa tamaduni mpya. Lakini sidhani kama Uislamu ambao ni dini na utamaduni wa Mwenyezi Mungu, unaweza kupitia hatua hizo. Wenyewe upo na Allah (s.w) alishaahidi kuilinda dini yake. Basi tusibweteke kwa kuwa Mwenyezi Mungu aliahidi kuilinda dini yake. Bila shaka aliahidi kuilinda kwa kupitia Waislamu wenyewe. Basi tusisubiri machungu zaidi katika kuulinda Uislamu na Waislamu. Uislamu wa kweli hatunao tena mioyoni mwetu, umebaki Uislamu wa maneno, yaani wa tamko tupu. Tuamke na kila mmoja atimize wajibu wake katika Uislamu. (Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa namba 0719 760 437)

AN-NUUR

Safari kutoka katika Nuru

zamani kwa Wagiriki na Warumi, kwani wao walijihesabu kuwa ndio watu pekee waliostaaribika na wengine hasa Waislamu, wao ni washenzi. Tangu wakati huo, makari hawa waliamini juu ya ubora wao dhidi ya Waislamu. Hata hivyo, hilo pekee halitoshi kuwa sababu ya chuki yao dhidi ya Uislamu. Hata jambo linalohusu Uislamu, msimamo wao hauwi tu wa kupuuza jambo hilo tofauti na wanavyofanya kwa dini na

Na Sheikh Ahmad Ragab


SHUKRANI zote anastahiki Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe wote, na rehema na amani zimkie kiumbe aliye mkamilifu na Imamu wa Mitume, Mtume wetu Muhamad (S.A.W). Kwa hakika dini ya Kiislamu inatofautiana na nyingine kwa uwepesi wake, misamaha, uwepesi katika ibada na sheria zingine. Na hii ni alama muhimu ya dini. Alikuja Mwarabu mmoja kwa Mtume (S.A.W), Mtume akamwamrisha yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu kwake miongoni mwa ibada mbalimbali na twaa nyingine, na akaziona ni dini nyepesi. Ibadan a twaa alizoamrishwa zinatekelezeka hazina taabu wala mashaka na anaweza kila mtu kuzitekeleza. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, Na hakufanya Mwenyezi Mungu kwenu katika dini uzito. Na amesema tena, Anataka Mwenyezi Mungu kwenu wepesi

na wala hataki kwenu uzito, Surat Alhajay (78). Na katika hadithi ya Mtume (S.A.W) amesema, hakika dini ni nyepesi. Na haitii yeyote ugumu isipokuwa itamshinda. Na amesema, Wameangamia wale wenye kuuliza sana Mitume yao. Alisema hivyo mara tatu na kwamba hao ni wale wenye kutia ugumu dini. Na miongoni mwa tofauti ya dini hii ya Kiislamu ni kwamba ni dini ya kusamehe. Basi kusamehe ni alama miongoni mwa alama za ukarimu na miongoni mwa njia ambazo alizokuwa akipita Mtume (S.A.W), na katika kuwazoesha anaowalingania ni kuwafanyia wema kwa kusamehe, na hiyo ndiyo ukamilifu wa hekima za Mtume (S.A.W). Amemsemesha Mwenyezi Mungu kwa neno lake, Samehe na amrisha mema na wapuuze wajinga, (Aaraf-199). Na neno lake Allah, Na wala haiwi sawa kwa wema na ubaya, fanya lililojema zaidi (Fuswilah-34). Na ilikuwa kusamehe kwake (S.A.W) ni athari kwa watu wengi sana kushawishika kusilimu katika idadi kubwa ya watu na wakaingia katika Dini makundi kwa makundi kwani alisamehe Mtume (S.A.W). Mtume (S.A.W) alimsamehe Mwarabu mmoja ambaye alilinoa panga akiwa na nia ya kukata shingo yake. Naye akiwa amejicha kivulini chini ya mti, lilianguka panga toka mkononi na akalichukua Mtume (S.A.W), akasema yule mtu,

Uislamu ni dini nyepesi na ya msamaha


ewe Muhamad kuwa mtu bora. Basi akamsamehe Mtume (S.A.W) yule mtu. Akarudi yule mtu akiwa ni Muislamu, naye akiwa na idadi ya watu wengi katika kabila lake wakaingia katika dini ya Kiislamu, naye akawa anasema kuwaambia watu wake, mimi nimekujieni nikitoka kwa mtu bora kuliko watu wote na msamaha anaurithisha kwa watu. Basi baadhi ya watu huchukua zawadi katika kusamehe kwa kudhani kuwa kunaridhiwa kusamehe. Imekuja dalili ya wazi inayojulisha kuwa kusamehe huinua daraja la mja na inakuwa ni sababu ya utukufu wake. Na katika hadithi amesema Mtume (S.A.W) kwamba, Hamzidishii Mola mja msamaha isipokuwa atakuwa Mtukufu na kusamehe ni tabia inayomjulisha mtu kuwa ana nguvu na kusalimika nafsi yake. Kusamehe hujulisha juu ya usa wa moyo kutokana na roho ya uadui, na kujipamba na tabia ya kusamehe hupelekea kuipumzisha nafsi na hutuliza moyo. Amesema mwenyezi Mungu, Na yeyote atakaye samehe na kusuluhisha, basi malipo yake yapo kwa Mungu kwani yeye hawapendi wanaodhulumu. Uislamu unahimiza waumini wake kujipamba na tabia hii ya kusamehe kwa maraki hadi kwa maadui na wale uliotofautiana nao dini. Amesema Mwenyezi Mungu, Wanatamani wengi katika waliopewa kitabu, laiti wangewarudisha baada ya Imani yenu mkawa makari tena, mahasidi kutokana na nafsi zao baada ya kubainika haki, basi wasameheni, ishi nao vizuri hadi alete Mwenyezi Mungu amri yake, kwa hakika Mwenyezi Mungu juu ya kila kitu ni muweza. Msamaha una athari kubwa na nzuri kwa mja hapa Duniani na akhera kwa mtu moja kwa jamii. Hapa Duniani ni utulivu wa nafsi na kutulia moyo na utulivu wa kra na usalama wa viungo na kutulia afya na maisha bora. Ama huko akhera ni kufaulu kwa kupata msamaha wa Mwenyezi Mungu. Amesema Mwenyezi Mungu, Nawasamehe, hivi hampendi awasameheni Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu ni msamehevu na ni Mwenye Rehema. Na akasema tena, Na yeyote atakayesamehe na akasema kwa moyo, Basi malipo yake ni kwa Mwenyezi Mungu. Kwani yeye hawapendi wanaodhulumu. Ama athari za msamaha kwa jamii ni kuziunganisha nyoyo na kushikamana watu, kusafika kwa jamii kutokana na magonjwa ya moyo miongoni mwa choyo

tamaduni nyingine. Linapokuwa ni suala linalohusu Uislamu, chuki zinachukua nafasi na sambamba na propaganda za kishabiki na upotoshaji wa hali ya juu. Lakini linapokuwa ni jambo ambalo halihusiani na Waislamu au Uislamu, mara zote wahusika wataonesha utulivu na kutafakari hali iliyopo ili kupata jawabu sahihi. Kwa ujumla Waislamu na Uislamu wao wanatazamwa

kama watu wasiostahili haki, maadui na wakosaji wanaosubiri hukumu. La kwao linaonekana kama sio suala linalofaa kufanyiwa utafiti ili kupata suluhu kistaarabu. Chuki imeshapandikizwa na hamasa ya Vita ya Msalaba inazidi kushika hatamu. Chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu imekuwa kama donda ndugu katika nyonyo zao. Hivi sasa imejitokeza dhana iliyokuwa imejicha kwa muda

na uhasidi na kupungua kwa matukio kama kuua, kuiba (wizi) na mengineyo, miongoni mwa matukio yanayopelekea kujaa kwa mahakama katika mambo ya kipuuzi yanayotokana na kutosamehe. Na katika ukubwa wa sheria za Kiislamu kwamba, umehimiza kusamehe yote yanayotokea kati ya mume na mke ili lisitokee jambo la kuukata mji na mapenzi na huruma kati ya watu. Ameseme Mwenyezi Mungu mtukufu, Na kama mtawaacha kabla ya tendo la ndoa mkiwa mmeshalipa mahari zao, mna haki ya kuchukua nusu ya mahari. Isipokuwa mkiwasamehe, au wasamehe wazazi wenu ambao wana majukumu kwenu. Na kama mtasamehe ni bora na msisahau mema kati yenu. Kama ulivyohimiza uislamu juu ya kusamehe pale linapotokea kosa la kuua. Na kuwataka ndugu wa aliyeuliwa kusamehe akasema: Na yule atakayesamehe kwa kuuliwa ndugu yake na akafuatilia kwa wema na akatekeleza ihsani, huo ni msamaha toka kwa Mwenyezi Mungu na upole. Na hili ndilo himizo la sheria ya Kiislamu katika kuhakikisha kuwa, hii ni tabia tukufu na ni dalili juu ya uwepesi na ulaini wa dini ya Kiislamu katika sheria zake kwa watu.

Habari za Kimataifa

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA APRILI 5-11, 2013

AN-NUUR

CAIRO Msemaji wa Rais Muhammad Mursi wa Misri amepinga vikali uvumi wa kurejeshwa balozi wa Misri huko Tel Aviv, inayoikalia kwa mabavu Palestina. Ihab Fahmy, amesema kuwa hadi sasa hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyika juu ya kuanzishwa tena shughuli za kidiplomasia kati ya pande hizo mbili. Mwezi mmoja uliopita, viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel

Misri yakataa kumrejesha balozi wake Tel Aviv

KHALID Mashal.

KHALID Mashal, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati za Mapambano ya Kiislamu Palestina Hamas, jana usiku alipitishwa na wajumbe wa ngazi za juu wa wanaharakati hao kuendelea kushikilia wadhifa wake huo kwa kipindi kingine cha miaka minne ijayo. Taarifa kutoka Cairo zinasema kuwa, Ismail

Mashal achaguliwa tena kuiongoza Hamas


Haniya, Waziri Mkuu wa serikali halali iliyochaguliwa na wananchi wa Palestina, ambaye hivi sasa yuko nchini Misri pamoja na Mussa Abu Marzouq, watakuwa wasaidizi wa Khalid Mashal. Aidha viongozi waandamizi wa Hamas waliwachagua wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa chama hicho. Awali, Khalid Mashal alitangaza kuwa atangatuka kwenye wadhifa huo utakapomalizika muda wa uongozi wake, lakini viongozi waandamizi wa Hamas wamepinga mpango huo na kumtaka aendelee kushikilia wadhifa huo. Kwa muda mrefu Khalid Mashal amekuwa akiishi Syria, kufuatia kuwindwa na majasusi wa kizayuni ambao wamedhamiria kumuua. (IRIB)

TAMKO KWA VYOMBO VYA HABARI

UBALOZI WA DOLA YA PALESTINA DAR ES SALAAM

waliwataka viongozi wa Misri wamrejeshe Atif Salim, balozi wa nchi hiyo mjini Tel Aviv. Misri iliamua kumuita nyumbani Atif Salim, ikilalamikia hatua ya kichokozi na isiyo ya kibinadamu ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kushambulia eneo la Ukanda wa Gaza mwezi Novemba mwaka jana. Huko Israel pia imeelezwa kuwa inasikitishwa kutokana na kukosekana kiunganishi cha mawasiliano kati ya Rais Mursi na viongozi wa utawala wa Israel.

Wito wa Uchunguzi Kuhusu Wafungwa wa Kipalestina Hili si tukio la kipekee. Wanaougua Ugonjwa wa Saratani Kwani tarehe 22 Februari

Kukamatwa mtuhumiwa mauwaji ya Padiri Mushi


Inatoka Uk. 3 ya Makosa Jinai sura ya 7 ya mwaka 2007 inayomtaka mtu anayemshikilia mtu mwingine au chombo chochote bila kumfikisha mahakamani kwa saa 24 aeleze mahamaka sababu za kushikilia mtu bila kumfikisha mahakamani au amwachie huru. Mawakili hao walimtaka Mkurugenzi wa Mkosa ya Jinai Zanzibar (DCI) na juzi Naibu wake Kamishina Msaidizi wa Polisi Yusuf Ilembo alika mbele ya Jaji Isack Mkusa, kusikiliza shauri hilo. Mawakili wa Kujitegemea upande wa mlalamikiwa waliowakilishwa na Shabani Juma Shabani pamoja na Shaibu Ibrahim waliiomba mahakani hiyo iamuru kuachiwa kwa mteteja wao. Hata hivyo, Jaji Mkusa alisema, kutokana na maombi hayo kuletwa chini ya kiapo ni vema pia Upande wa serikali nao ukapewa muda wa kujiandaa kuweza kujibu hoja hizo chini ya kiapo. Baada ya kusikilza pande zote mbili, Jaji Mkusa chini ya kifungu cha sheria section 8 ya mwaka 2006 inatoa nafasi kwa mtu kupewa dhamana lakini kwa

Wapalestina wakilaani kifo cha Maisara Abu Hamdiyeh aliyekuwa mfungwa wa Israel

jinsi mahakama itakanyoona inafaa. Lakini wakati huo huo muhusika naye aletwe mahakamani wakati wa kusikiliza shauri lake kulingana na section 8. Kutokana na utata unaoligubika suala hili, zipo tuhuma na wasiwasi kuwa huenda mtuhumiwa alikamatwa tu kisiasa na hakukuwa na sababu za msingi za kumtuhumu. Wa n a o j e n g a d h a n a h i i wanasema kuwa ile kukamatwa Bwana Makame mara baada ya tamko kali la Kadinali Pengo akiichagiza na kuikemea Serikali, huenda ndio sababu Polisi waliibuka na kutafuta mtu wa kumtoa muhanga kuitikia shinikizo la Kadinali huyo kama walivyofanya katika kadhia ya Mauwaji ya Mwembechai. Padre Mushi aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Kanisa la Minara Miwili Zanzibar aliuawa asubuhi ya February 17 mwaka huu kwa kupigwa risasi wakati akijiandaa kuendesha ibada katika kanisa la Mtakatifu Theresia nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

W A Z I R I w a Mamlaka ya Palestina anayeshughulikia wafungwa, ametangaza kuwa kuna ongezeko kubwa la ugonjwa wa saratani miongoni mwa wafungwa wa Kipalestina waliofungwa katika magereza ya Israel. Kwa mfano, katika muda wa miezi mitatu mwaka huu wafungwa wapatao 25 wamegundulika kuwa wana saratani. Inasadikiwa kuwa hii ni kwa sababu watawala wa Israel wanawadunga wafungwa sindano zenye sumu ya carcinogens ambayo inasababisha saratani. Hivi majuzi, muathirika aliyefariki kutokana na kitendo hiki cha kishenzi ni Mpalestina wa miaka 64 aitwae Bwana Maysara

Abu Hamdya, ambaye alikufa kutokana na saratani tarehe 2 Aprili 2013. Alikufa baada ya kukataliwa matibabu na wakuu wa magereza ya Israel. Abu Hamdya alikuwa gerezani tangu mwaka 2002 akitumikia kifungo cha maisha. Afya yake ilianza kudhoofika mno lakini hakupewa matibabu yoyote akiwa gerezani. Matokeo yake alizidiwa na satarati iliyoenea mwilini mwake na hivyo kusababisha kifo chake. Wa k a t i akiwa mahututi ndipo watawala walipompeleka hospitali ambako alilazwa akiwa na maumivu makali na uvimbe mwilini, akiwa amekonda, hawezi kuzungumza, kula wala kulala.

mwaka huu mfungwa mwengine wa Kipalestina, Bwana Arafat Jaradat, alifariki baada ya kuteswa akiwa katika gereza la Israel. Ubalozi wa Dola ya Palestina nchini Tanzania unatoa tamko hili likiishutumu Israel kwa kifo cha Abu Hamdiah pamoja na kwa ongezeko la saratani miongoni mwa wafungwa wa Kipalestina katika magereza ya Israel. Ubalozi kwa hiyo unatoa wito wa kuundwa kwa Tume ya Kimataifa ili kuchunguza vifo hivi vya wafungwa wa Kipalestina. Ni wajibu wa Jumuia ya Kimataifa kuendesha uchunguzi huu kwa haraka ili kuhakikisha kuwa wahalifu wanaosababisha vifo hivi wanachukuliwa hatua za kisheria bila ya kuchelewa. Kwa mujibu wa Makubaliano ya Geneva, ni wajibu wetu kuchukua hatua siyo tu kuhusu vifo vya Abu Hamdya na Arafat Jaradat, bali pia kuhusu wafungwa wa kisiasa wa Kipalestina takriban 5000 ambao leo hii wanadhalilishwa katika magereza ya Israel na wanakabiliwa na hatari kwa maisha yao.

6
Na Omar Msangi
NDANI ya Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) kuna mchungaji ambaye husimamia masilahi ya wanafunzi na watahiniwa wa Kikristo. Mchungaji huyu ni mwajiriwa wa Serikali na hulipwa mshahara na Serikai. Habari kutoka ndani ya Baraza hilo zinafahamisha kuwa huyu mtu wa Kanisa wa sasa, wala hana sifa za ualimu au utaalamu wa mitihani. Ni Mchungaji tu na msomi wa Biblia. Hata hivyo, kwa upande wa Waislamu hakuna mtaalamu wa somo la Maarifa ya Uislamu wala Lugha ya Kiarabu, pamoja na kuwa Waislamu wamelalamika sana na kuhoji juu ya suala hilo. Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Dr. Joyce Ndalichako aliwahi kunukuliwa mwaka jana akisema kuwa hajaajiri mtaalamu wa Somo la Maarifa ya Kiislamu na Lugha ya Kiarabu kwa sababu hajapewa kibali na Serikali. Sasa sikiliza kauli ya Rais Kikwete: Napenda kuwahakikishia Watanzania wenzangu kuwa mimi na Serikali ninayoiongoza, hatupendelei upande wo wote. Vyombo vya usalama vinatambua wajibu wake na kama haifanyiki ni ulegevu wa mtu tu katika kutimiza wajibu wao na siyo kwamba ni sera na maelekezo yangu au ya Serikali. Naandika maoni haya na nitayaandika kwa urefu kidogo na hii ni kuitikia wito wa Mheshimiwa Rais Kikwete kwamba vyombo vya habari visaidie kuliepusha taifa letu kuingia katika vita ya kidini. Rais Kikwete ametoa wito huu katika kukamilisha hotuba yake kwa wananchi, tarehe 31 Machi, 2013 ambapo alisisitiza kuwa iwapo waandishi wa habari hawatatimiza wajibu wao katika kuondoa migogoro ya kidini nchini watakuwa wamefanya usaliti mkubwa. Rais Kikwete akionyesha kuwa taifa letu linapita katika kipindi kibaya alisema kuwa kuna upepo mbaya wa shetani unapita ambao viongozi wa dini wana wajibu wa kuhakikisha kuwa hali ya hewa inasashwa na kurejesha nchi yetu na watu wake katika maisha tuliyozoea. Na akasema kuwa Serikali itaitisha mkutano wa viongozi wa dini mapema mwezi ujao (ili wajadili na kuchukua hatua za kuondoa upepo huo mbaya.) Akiunga mkono umuhimu wa kuwepo mkutano wa viongozi wa Kiislamu na Kikristo, Sheikh Khamisi Mataka amesema kuwa wao kama Masheikh waliliona hilo na mapema kwamba kuna ulazima kwa Masheikh na Mapadiri kukutana kuzungumzia tofauti zilizopo na kutafuta namna ya kurekebisha mambo. Sheikh Mataka aliyasema hao akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya BBC Jumatatu jioni wiki hii. Pengine katika kutoa mchango wangu na kuitikia wito wa Mheshimiwa Rais Kikwete, nianze na kusema kuwa kama ni kutokea mgogoro wa kidini, machafuko na hata

MAKALA

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA APRILI 5-11, 2013


na mkakati wa kuwadhulumu Waislamu katika elimu. Na hii ikafanyika kwa namna tofauti tofauti. Moja ni ile iliyotumika kuchukua watoto wa Kikristo kutoka maeneo yenye Wakristo wengi kwenda kuchukua nafasi za watoto wa Kiislamu wa mikoa ya Pwani na Morogoro, kuchukua majina ya watoto wa Kiislamu na kuwapa nafasi hizo watoto wa Kikristo, kuacha kuwachagua watoto wa Kiislamu waliofaulu vizuri na kutoa nafasi kwa watoto wa Kikristo walio na alama za chini kama alivyowahi kueleza Mzee Bori Lilla. Na yote haya yaliwezekana kwa sababu zile Bodi, Kamati na majopo ya kuchagua wanafuzi wa kupata elimu ya juu, zilikuwa za Wakristo watupu na wakati mwingine wenyeviti wakiwa mapadiri. Lakini tusisahau pia wakati serikali hivi leo ikiwapongeza Wakristo (eti) kwa kuisaidia serikali kutoa huduma za elimu, lakini ni serikali hiyo hiyo toka wakati wa ukoloni imekuwa ikitoa pesa kuyapa makanisa yajenge na kuendesha shule. Na hatuyasemi haya kwa elimu ya kichwa au kwa kuzua tu, hii imethibitishwa na kiongozi wa Kanisa Katoliki pale aliposema kuwa iwapo serikali ingeamua kusitisha ruzuku yake kwa shule za Wakristo, basi wangelazimika kuzifunga shule hizo kwa sababu walikuwa wakitegemea pesa hizo za walipa kodi kwa asilima 100! Hili ndilo tatizo. Tunaposema kuwa tunataka kuwakutanisha Masheikh na Wachungaji, je, wao ndio waliokuwa wamekaa hapo awali na kupitisha azimio la kuitaka serikali iwapendelee Wa k r i s t o n a k u w a b a g u a Waislamu? Wanakutana ili kufanya nini, kuitaka serikali sasa iache ubaguzi huu? Kinachotokea hivi sasa ni kuwa uhuru umekuwa mkubwa. Hapo awali Waislamu walikuwa hawana pa kusemea. Waislamu wamepata mdomo na mahali pa kusemea na siasa za leo zinaruhusu. Wanasema juu ya dhulma na ubaguzi waliofanyiwa na wanaoendelea kufanyiwa. Lakini kwa upande mwingine, waliopewa a better chance nao wamekuwa kama muonja asali. Wamenogewa wanataka hali hii idumu hivi hivi waendelee kufaidi. Ndio maana utaona kuwa ikitokea Idara fulani ya serikali ina watumishi labda 11, ikitokea tu Waislamu wakafika 5 inakuwa nongwa, na hasa inapokuwa Rais ni Muislamu. Haitaangaliwa kuwa walioteuliwa wana sifa au la, utaangaliwa U-Alhaj wao. Ila ikitokea ni Wakristo watupu, wala hutasikia mtu akihoji na kutuhumu udini! Hali hii ndiyo inayoonekana kuleta msuguano baina ya Waislamu na Wakristo hivi sasa kama tutakavyozidi kufafanua. Swali ni je, huu tuuite kuwa ni upepo mbaya wa shetani? Kama ni upeo mbaya basi ni upepo mbaya wa Masheikh, viongozi wa dini na serikali kwa upande mwingine. Kwa upande Inaendelea Uk. 7

AN-NUUR

Hakuna upepo mbaya wala shetani Tanzania

Rais Kikwete hajasomewa Itiqaafu Ushahidi wa upendeleo huu hapa Mchelea mwiba guu huota tende
kidini inayodaiwa kuwepo. Kama ni upepo mbaya na shetani, basi ushetani huo ni huu wa kuwa na taasisi za Kiserikali na Umma lakini zikiwa kama Parokia ambazo hujali zaidi masilahi ya Wakristo badala ya Watanzania kwa ujumla kama Waislamu wanavyolituhumu Baraza la Mitihani. Na Shetani huyu hahitaji mtaalamu wa kupunga wala Masheikh wa kusoma Ruqya na Wachungaji walokole wa kutoa mapepo. Hata hivyo, kwa Rais Kikwete kuja na hoja za shetani mbaya hatumshangai, yeye ni mwanasiasa. Na wanasiasa wana namna zao za kuhakikisha kuwa wanadumu madarakani. Wanaoshangaza ni Masheikh na kauli zao za kisiasa. Nabii Mussa alipotumwa kwa Firauni aliambiwa: Nenda kwa Firauni. Hakika yeye amezidi jeuri. Umwambie: Je! Unapenda kujitakasa? Nami nitakuongoa ufike kwa Mola wako Mlezi, upate kumcha. (79: 17-19) Ila tu alichotahadharishwa Nabii Mussa na ndio ubinadamu wenyewe ni kwamba asimvunjie heshma Firauni katika kumkishia ujumbe wa Allah. Amwambie kwa lugha laini. Vitabu vimerekodi na hata leo mtu akitaka kuvisoma vipo madukani na maktaba kwamba, toka ukoloni kulikuwa

RAIS Jakaya Kikwete


vita, haitaletwa na upepo mbaya wa shetani. Tanzania hakuna upepo mbaya wala shetani anayechangia misuguano ya

Uhusiano wa Wakristo na Waislamu


Ndugu Wananchi; Jambo la tatu ninalopenda

kuzungumza nanyi leo ni uhusiano wa Waislamu na Wakristo nchini. Jambo hili nimeshalizungumzia mara kadhaa siku za nyuma, lakini nalazimika kulisemea tena kutokana na hali ilivyo sasa. Tumefikia mahali ambapo kama viongozi na waumini wa dini hizi kubwa mbili hawatakubali kubadili muelekeo wa sasa, tunakoelekea ni kubaya. Nchi yetu nzuri tutaivuruga na sifa yake ya miaka mingi ya Waislamu na Wakristo kuishi pamoja kidugu, kwa upendo, ushirikiano na kuvumiliana itatoweka. Tanzania itaacha kuwa kisiwa cha amani na kuingia katika orodha ya nchi zenye migogoro na hata vita vya

wenyewe kwa wenyewe. Ndugu Wananchi; Nyaraka na kauli kali kali zinazotolewa na viongozi wa dini za Kikristo na Kiislamu zinanishawishi kuamini haya niyasemayo. Nyaraka na kauli hizo zina mambo mawili makuu. Kwanza, kwamba kila upande unatuhumu, kushutumu na kulaumu upande mwingine kwa kufanya vitendo viovu dhidi ya dini yake. Kauli na mihadhara ya kudhalilisha dini za wengine, kunajisi vitabu vitakatifu, kuchoma moto nyumba za ibada, mzozo kuhusu nani achinje na kuuawa kwa viongozi wa dini ni baadhi ya mambo yanayotolewa mifano. Na, pili kwamba kila upande unailamu Serikali kwa kupendelea upande mwingine.

Wakristo wanalaumu kwamba mihadhara ya kudhalilisha Ukristo inaendeshwa na Serikali haichukui hatua. Aidha, Wakristo wanateswa na viongozi wao kuuawa na Waislamu, lakini Serikali haichukui hatua. Kwa ajili hiyo wanadai kuwa Serikali imeshindwa kulinda uhai wa raia wake. Wanasema pia kwamba Serikali inapendelea upande wa Waislamu. Ndugu Wananchi; Waislamu nao wanadai kuwa kitabu chao kitakatifu, y a a n i Q u r a n Tu k u f u , kinadhalilishwa kwa kuchanwa, kuchomwa moto na kukojolewa na Wakristo na Serikali haichukui hatua yo yote ya maana. Waislamu wananyanyaswa katika nchi yao, wanakamatwa
Inaendelea Uk. 7

7
wa Masheikh ni kuwa badala ya kuiambia serikali ukweli kwamba inafanya ubaguzi, wanapiga siasa na propaganda. Wanatoa kauli zilezile za wanasaisa za kuwashutumu wadhulumiwa. Badala ya kusema Firauni amezidi jeuri hadi kujiita Mungu Mkuu, wanaungana na Firauni kuwalaumu wachawi waliomkataa Firauni wakasilimu baada ya kuiona haki! Vi o n g o z i w a K i k r i s t o (na Waumini wao) nao kwa vile walishaahidiwa kupewa a better chance, wanataka upendeleo huo udumu. Kwa upande wa serikali imekuwa kana kwamba imetiwa kitanzi shingoni. Inaonyeshwa jinsi ilivyowadhulumu Waislamu inajifanya haioni. Inaonyeshwa inavyowapuuza Waislamu, inasema wanaoleta madai hayo ndio wachochezi. Ni wadini! Labda tuseme mambo mawili hapa. Katika mauwaji ya Mwembechai, msingi wa mauwaji yale ni serikali kutaka k u w a k o m e s h a Wa i s l a m u waliokuwa wakihubiri kuwa Yesu si Mungu. Al-Marhum Mzee Katambo wa Msikiti wa Kibo, wakati huo akiwa na umri zaidi ya miaka 80 aliwekwa ndani kwa zaidi ya miezi sita. Huyu hakuwa mhadhiri wa Biblia kama walivyo akina Mazinge. Yeye alikamatwa kwa vile ni Mzee wa Msikiti na msikitini kwake kulifanyika muhadhara kukanusha kuwa Yesu si Mungu. Sasa labda tuulize, lini sheria za nchi hii ziliharamisha mtu kusoma aya ya Quran inayosema kuwa Yesu Si Mungu? Mzee gani wa Kanisa aliwahi kukamatwa na kuwekwa ndani kwa sababu Padiri kahubiri kuwa Yesu ni Mungu kanisani jambo ambalo kwa imani ya Kiislamu mbingu zinakaribia kupasuka kwa ghadhabu kutokana kufru hiyo? Haya ndiyo mambo wanayolalamikia Waislamu. Ubaguzi na upendeleo huu ndio wanaolalamikia Waislamu ambapo kwa upande mwingine Wakristo wanataka serikali iendelee kuwakamata Masheikh wanaohubiri kuwa Yesu si Mungu, ila wachungaji wao wawe huru kupita nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa, shule kwa shule na vituo vya mabasi kuhubiri uungu wa Yesu na kuikashifu Quran kuwa ni kitabu cha mashetani na wachawi. Kuna mambo mawili yalitokea wakati wa Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi. Moja ni pale alipomteuwa Alhaji Profesa Kighoma Ali Malima kuwa Waziri wa Elimu. Katika mambo makubwa aliyofanya Malima kuisiadia serikali na nchi yake, ni kuonyesha mwanya uliokuwa ukitumika kufanya ubaguzi wa kidini katika elimu. Prof. Malima alitoa maelekezo kuwa darasa la saba wakishafanya mtihani kwa namba na mitihani kusahihishwa na kuwekwa alama walizopata, namba zisivishwe majina mpaka uchaguzi wa wanaokwenda sekondari utakapofanyika. Kwa

Makala

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA APRILI 5-11, 2013


kuliko hata alivyofanya Mwalimu Nyerere. Katika kipindi hiki Masheikh wetu wakafanya dhambi na kosa kubwa ambalo wanaendelea kulifanya mpaka leo. Badala ya kumuona Mwinyi kama Rais wa Tanzania wakamtizama kama Muislamu. Kwa hiyo badala ya kukemea dhulma inayofanywa na serikali kuwafanyia Waislamu, wakasimama naye kumhami dhidi ya makombora ya Maaskofu. Huo ulikuwa mkakati wa Wakristo kwa Rais Muislamu ili waendelee kufaidi ile ahadi waliyopewa na Mwalimu Nyerere ya kulipa kanisa upendeleo! Na huu ndio mkakati wanaotumia hata leo kwa Rais Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete. Kumshutumu kwa mambo yasiyopo ili aogope kufanya uadilifu, awe mtu wa kujihami asiambiwe mdini. Utakuta ndio hao hao wanaobeza hata shule za Kata kwa sababu zikiimarika, hakuna mtu wa kumbagua asisome. Jambo la pili lililotokea wakati wa Mzee Mwinyi ambalo litatusaidia kuona kuwa kama ni ushetani ni wetu wenyewe ni ile kadhia ya mabucha ya nguruwe. Sheria za miji juu ya mifugo zinafahamika. Lakini wakati ule ilifikia mahali nguruwe kufugwa ovyo mpaka katika baadhi ya maeneo (Ubungo, Dar es Salaam), nguruwe wakawa wanaingia misikitini na kufia humo. Haikuwahi kusikika hata mara moja mfugaji wa nguruwe kukamatwa kwa kuachia nguruwe wake kuranda hadi kuingia na kufia msikitini. Kivumbi kilitokea Waislamu walipochoka baada ya kuona wanadharauliwa na kupuuzwa kila wanapopeleka malalamiko serikalini na vituo vya polisi. Hapo ndio serikali ikachachamaa baada ya bucha la nguruwe kuvunjwa. Rais Mwinyi akaagiza guvu za dola ziwaangukie Waislamu. Aliyekuwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa John Samwel Malecela akalipindua suala lile likawa la Waislamu siasa kali wasiotaka kuona Mkristo akila shwaini wake. Ila habari ya nguruwe kuingia msikitini ikaachwa, ile kuwa Masheikh wa Wilaya nzima waliandika barua serikalini kulalamika nyama ya nguruwe kuuzwa katika mabucha ya kawaida hali iliyopelekea mama mmoja kulishwa nyama hiyo haramu, likawekwa pembeni. Likawa suala la serikali kupambana na Waislamu siasa kali. Masheikh wakateswa sana. La kusikitisha ni kuwa wale Masheikh ambao hawakuguswa, wakasimama upande wa serikali na wafunga nguruwe kuwashutumu wenzao kuwa ni siasa kali. Hapo serikali ikapata nguvu ya kusema apendaye kula ngiri, chura ale, utadhani tatizo lilikuwa Waislamu kuwakataza Wakristo kula nguruwe. Na tafsiri za aya za Quran zikabadilishwa. Badala ya sema enyi makari ikasemwa sema enyi watu wa dini nyingine. Maana Rais (na baadhi ya Masheikh)

AN-NUUR

Inatoka Uk. 6

maelezo ya Malima mwenyewe, kwa mwaka ule idadi ya watoto wa Kiislamu waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza iliongezeka kwa asilimia 40. Hii tafsiri yake ni kuwa watoto wa

Hakuna upepo mbaya wala shetani Tanzania


Kiislamu walikuwa wakikatwa majina yao wakati wa uteuzi. Kilichotokea ni Malima kupigwa vita akidaiwa kuleta udini mpaka akangolewa katika Wizara hiyo.

Inatoka Uk. 6 ovyo, hawapewi fursa sawa na kwamba Serikali inawapendelea Wakristo. Wanasema nchi inaendeshwa kwa mfumo wa Kikristo. Mimi binafsi wananishutumu kuwa napendelea kushiriki zaidi kwenye shughuli za Wakristo kuliko za Waislamu kama vile harambee za kujenga Makanisa na shule za Makanisa. Naambiwa kuwa mwepesi kushiriki maziko ya Maaskofu kuliko Masheikh wanapofariki. Ipo Misikiti mitatu hapa Dar es Salaam wamenisomea itikafu nife. Katika itikafu hiyo wamewajumuisha Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Ndugu Suleiman Kova. Ndugu Wananchi; Napenda kuwahakikishia Wa t a n z a n i a w e n z a n g u kuwa mimi na Serikali ninayoiongoza, hatupendelei upande wo wote. Hatufurahishwi na kitendo cha mtu kudhalilisha dini ya mwenzake ndiyo maana wapo wahadhiri wa dini ya Kiislamu na wahubiri wa dini ya Kikristo wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa nyakati mbalimbali. Vy o m b o v y a u s a l a m a vinatambua wajibu wake huo na kama haifanyiki ni ulegevu wa mtu tu katika kutimiza wajibu wao na siyo kwamba ni sera na maelekezo yangu au ya Serikali. Mtakumbuka kuwa mara kadhaa nimewakumbusha Wakuu wa Mikoa na Wilaya na wakuu wa vyombo vya usalama kuacha ajizi katika kutimiza wajibu wao kwenye suala hili. Ndugu Wananchi; Mimi binafsi sibagui, hushiriki shughuli za Wa i s l a m u n a Wa k r i s t o kila ninapoalikwa labda nikose nafasi kwa sababu nyinginezo. Nimeshafanya shughuli nyingi za Waislamu kama vile Maulid ya Mtume Muhamad S.A.W., safari za Hija, ujenzi wa misikiti

Uhusiano wa Wakristo na Waislamu


na madrasa na mengineyo mengi. Nimeshashiriki mazishi ya Masheikh kama nifanyavyo kwa Maaskofu na watu mbalimbali Waislamu na Wakristo. Pale ambapo sikushiriki mazishi ya Sheikh au Askofu itakuwa ni kwa sababu ya kubanwa na shughuli nyingine ambazo lazima nifanye mimi, au taarifa ilikuwa ya muda mfupi. Kwa upande wa Waislamu desturi yetu ya kuzika mara mtu anapofariki huwa kikwazo kwangu kushiriki hasa ikiwa ni nje ya Dar es Salaam kwa sababu ya taratibu za kumsarisha Rais kutoka mahali pamoja kwenda pengine siyo nyepesi. Wakristo hawana utaratibu huo, huwa wanaweza kusubiri hivyo huniwia rahisi kushiriki. Ndugu Wananchi; Napenda kuwahakikishia kuwa Serikali yetu haijashindwa kulinda usalama wa raia wake au viongozi wa dini na nyumba za ibada. Kama ingekuwa hivyo, tungeshuhudia mauaji ya raia, viongozi wa dini na matukio ya kuchomwa nyumba za ibada yakiwa mengi hapa nchini. Lakini hivyo sivyo. Nawasihi sana ndugu zangu Wa k r i s t o n a Wa i s l a m u kuwa tusiyachakulie matukio ya kuuawa kwa Mchungaji Mathayo Kachila kule Buseresere, Geita, na Padri Evaristus Mushi kule Zanzibar, au kumwagiwa tindikali Sheikh Fadhili Soroga, Naibu Mufti wa Zanizbar, kupigwa risasi Padri Ambrose Mkenda na kuchomwa moto kwa Makanisa Zanzibar na Mbagala, Dar es Salaam kuwa ni kielelezo na ushahidi wa Serikali kushindwa kutimiza wajibu wake. Kila tukio lina mazingira yake, hakuna ushahidi wa vyombo vya Serikali kuzembea. Hakuna ushahidi wa matukio hayo kuunganika. Mpaka sasa hatujapata ushahidi wa kuwepo kikundi cha Waislamu wanaopanga kuua viongozi wa Kikristo na kuchoma moto Makanisa

Mwinyi naye akaandamwa kwa tuhuma za udini mpaka akawa kila wakati anakuwa mtu wa kijihami ili asiambiwe kuwa mdini. Matokeo yake akawa anawabamiza zaidi Waislamu

hapa nchini. Ndugu Wananchi; Kifo cha Mchungaji Mathayo Kachila wa Buseresere ni matokeo ya vurugu zilizosababishwa na mzozo kati ya Wakristo na Waislamu kuhusu kama nyama iliyochinjwa na Wakristo Kanisani nayo iuzwe kwenye bucha iliyopo pale kijijini ambayo kwa mazoea huuzwa nyama iliyochinjwa na Waislamu. Katika ugomvi na vurumai hizo ndipo watu kadhaa wa pande zote walijeruhiwa na Mchungaji kupoteza maisha. Si tukio unaloweza kulihusisha na mengineyo nchini. Ni la pale pale Buseresere na limeanzishwa na kuhusisha Wakristo na Waislamu wa Buseresere kwa sababu zao. Hivi kama kusingekuwepo na mzozo wa nyama ile kuuzwa katika bucha ile kuumizana kule na mauaji yale yangetokea? Kabla ya mzozo ule Wakristo na Waislamu wa Buseresere hawakuwa na ugomvi baina yao. Walikuwa wanaishi kidugu na kushirikiana katika shughuli zao za kujitafutia riziki huku kila mmoja akimuabudu Mungu kwa misingi ya dini yake. Hivyo kutumia tukio hilo kutoa wito kwa Wakristo wote kuwa kuuawa kwa Mchungaji Kachila ni sawa na kuuawa kwa Wakristo wote nchini kulikofanywa na Waislamu ni kulikuza tatizo isivyostahili. Busara ituongoze kutafuta njia ya kuwapatanisha Wakristo na Waislamu wa Buseresere wazungumze, waelewane na waendelee kuishi pamoja kama ilivyokuwa awali. Hata mzozo wa kuchinja wanaweza kuumaliza. Mbona bucha za kitimoto zipo na watu hawajapigana. Kutumia mzozo wa Buseresere kueneza chuki kati ya Wakristo na Waislamu nchi nzima si sawa. Hatuwatendei haki Watanzania. Ndugu Wananchi; Kuuawa kwa Padri Evaristus Mushi wa Zanzibar ni tukio linalojitegemea
Inaendelea Uk. 9

anaogopa akisema Enyi

Inaendelea Uk. 9

Makala

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA APRILI 5-11, 2013

AN-NUUR

Masheikh na Maaskofu, waache wakutane


katahiriwa. Hivyo wako tayari kula nyama iliyochinjwa na Muislamu kwa sababu wana uhakika kuwa imechinjwa kihalali na mtu mwenye tohara. Inatambulika kuwa waliozua balaa la kuchinja ni baadhi ya wafuasi wa madh-hebi hizi za Pentecoste wanaofadhiliwa sana na Born Again wa Marekani. Watu hawa ndio mwanzo wa mauwaji makubwa yaliyokuwa yakitekelezwa na viongozi kama vile Bw George H Bush aliyekuwa Rais wa United States of America, aliyeapa kueneza Vi t a Vy a M s a l a b a . P i a itambulike kuwa hawa Born Again (hakika wanaitwa F U N D A M E TA L I S T S ) hawataki kabisa kusikia kuwa kuna Uislamu na Ukatoliki duniani kiasi kwamba Papa wanamtuhumu anaeneza ushirikina (wanamwita purveyor of superstition) . Tazama website za kina Pat Robertson ama marehemu Jerry Falwell. Haya waliozuwa hawa wanaotaka wawe wakichinja wao wamezua sokomoko huko Geita mpaka yakatokea maafa na mchungaji kauwawa. Kwa hawa jamaa sio hilo tu la kuchinja, chuki yao ya Uislamu na Waislamu imeendelea kupita hapo. Hapa Tanzania kuna kampuni moja inayomilikiwa na Muislamu ambayo inatengeneza aina nyingi ya vyakula na vinywaji. Hivi karibuni kampuni hiyo imeamua kuweka nembo inayoonyesha kuwa chakula hicho mteja alochonunua ni HALAL. Hii maana yake ni kuwa Muislamu anaweza kukila chakula hicho bila wasi wasi kuwa kimekiuka amri za dini ya Kiislamu kuhusu vyakula. Mtindo huu umeenezwa duniani kote hivi sasa. Imetambulika kuwa baadhi ya waumini wa Ukristo humu Tanzania wanakataa kununua na kutumia bidhaa yeyote yenye nembo hiyo ambayo ni alama ya msikiti au neno HALAL ama kwa Kiarabu) . Ikiwa chakula hiki ni halali kwa Muislamu ndio kusema pia ni halali kwa Muyahudi. Na ikiwa ni halali kwa Muyahudi BASI NI HALALI KWA WANAYEMWITA YESU (Rasu-ul-Llahi Issa AS). Sasa inakuwaje wakatae chakula ambacho wanayemwita MUOKOZI anaweza kukila bila kuwa haram?? Halafu yametokea mauwaji ya Fr Evarist Mushi huko Zanzibar. Inasikitisha sana kuwa bila kuwepo ushahidi wowote lawama za mauwaji hayo wametwikwa Waislamu kama waumini wa Uislamu. Maana yake sio kama aliyetenda kitendo hicho ni muhalifu ambaye ana jina la Kiislamu. Inaelekea kuwa aliyeuwa ni Muislamu na aliyefanya uhalifu huo ameutekeleza kwa sababu ya Uislamu wake. Shutuma hizo hazikutoka kwa Wakristo tu bali Masheikh nao wamejitosa kwa hoja na aya za Kurani kumlaani huyo Muislamu ambaye mpaka sasa hajajulikana. MaAskofu na Wakristo wote kwa ujumla wamefarijika sana! Masheikh wamewafariji Wakristo na kuwahuzunisha wafuasi wao Waislamu. Kuhusu hili kama ulitakikana ushahidi wa kuwa nchi hii ina Mfumokristo tazama uwezo mkubwa alionao Muhashamu Polycarp Cardinal Pengo kuhuu mkasa huu. Amedirikli kuikemea Serekali kuwa hawajampelekea repoti ya upelelezi wao juu ya kuuawa kwa Rev Fr Evarist Mushi. Hakika kufuatana na ukali wake bila shaka alikuwa akitegemea kuwa patakuwa na kiongozi Serekalini ambaye atakuwa anampa brieng upelelezi unavyoendelea. Kufuatana na matokeo haya machache yaliyoorodheshwa ni rahisi kufikia maamuzi kuwa kweli kumetokea msuguwano kati ya Wakristo na Waislamu. Hali kama hiyo hakika inaweza kuwa hatari sana kwa nchi hii. Isipokuwa ikumbukwe kuwa WaTanzania, na hasa Wa Ta n z a n i a Wa i s l a m u ni wastahmilivu sana na kwa kawaida huheshimu sana sheria na viongozi. Mafunzo yao ya MADRASA yanawafanya wawe na heshima kwa walio viongozi wenye madaraka. Hii ni kweli kabisa ingawa kunaweza kutokea wasomaji wasikubaliane na hoja hiyo. Waislamu wamekuwa wakiitwa kuwa ni docile (wanyonge sana). Kweli hali hiyo imeanza kubadilika lakini hayo ni kwa sababu kila kitu kina mwisho wake. Wanaelewa kuwa huko nyuma wametumiwa sana kwa maslahi binafsi na kusimika Ukristo. Wanamkumbuka kwa dhati Al Marhum Sheikh Mzee Takdir, mpiganaji shupavu wa uhuru. Mabadiliko hayo kwanza yamedhihirika katika mihadhara waliyokuwa wakiihubiria katika miaka ya tisini. Hii iliwaudhi sana Wakristo na ajabu ni kwamba wale wasomi ndio waliokuwa wakichomwa zaidi ya Wakristo wa kawaida ambao walipendelea sana kuendesha mijadala kwa hoja wakishindana na hawa wahadhiri wa Kiislamu. Lakini kukasirika kule ilidhihirisha kiasi Waislamu walivyokuwa wakionewa kila siku kuwa wao ni docile. Lakini ikumbukwe huko nyuma kulikuwa na mihadhara mingi ya wahubiri Wakristo wengi walikuja nchini humu na waliyokuwa wakiita kwa mfano September Crusade na kadhalika. Mihadhara hii ya Wakristo nayo wahadhiri wake walikuwa wakijaribu kuuchambua Uislamu wakipotosha mafundisho ya dini hiyo ya kweli ya Allah. Waislamu hawakulalamika kusema kuwa Uislamu ulikuwa ukikashwa. Bado hata hivyo wale waliosoma maandishi kama vile kitabu WANA WA IBRAHIM walifahamu kiasi gani si tu Uislamu ulikuwa ukikashiwa bali hata Rasul-ul-Llah Muhammad SAWalikuwa akidharauliwa. Imeandikwa kuwa Uislamu hauwezi kuwa ni dini ya kweli kwa sababu Warabu, akiwemo Mtume Mhammad SAW walitokana na kizazi cha Ismail AS na huyu Ismail alizaliwa na mtumwa na wala huyo Ismael AS hakubarikiwa. Kwa hiyo wanasema Uislamu hauwezi kuwa ni dini ya kweli. Soma kitabu hicho WANA WA IBRAHIM ama DINI MBALI MBALI NA UTUME WETU. Vyote hivi vimeandikwa na Kanisa Katoliki. Yo t e h a y a y a k i t o k a Waislamu hawakulalamika KASHFA hata siku moja. Wakristo walipolalamika tu ati dini yao inakashiwa Serekali nzima ilikuja juu. Sasa hivi kweli Ukristo umesimama kwenye msingi dhaifu ambao hauwezi labisa kustahmili upekuzi wenye mantik? Cardinal Manning wa Westminster aliwahi kunukuliwa akisema kuwa Dogma supersedes history (yaani amri inaweza kuwa bora na juu ya matukio ya historia). Huyu Cardinal Manning sio kiongozi wa kawaida tu, yeye aliyekuwa msaidizi wa karibu sana wa Papa Paul VI aliyetoa mafundisho kuwa Papa hakosei (Infallibility of the Pope) anapokuwa katika kiti cha enzi. Kweli kutokana na haya yote uko ule mkwaruzano kati ya Wakristo na Waislamu nchini humu. Hata wale maadui wa kivita ya kuuwana hasa kuna siku lazima wakae chini kuzungumzia uhasama wao. Wamarekani wanazungumza na Taliban. Kuna shida moja lakini ambayo ni lazima ikubalike na upande wa Wakristo. Waislamu wana

Na Khalid S Mtwangi

MUHESHIMIWA Rais Jakaya Mrisho Kikwete amependekeza Masheikh na Maaskofu wakutane wazungumze kuhusu kule kusuguwana kulikojitokeza hivi karbuni. Hakika ndugu Wakristo wamezua makubwa hivi karibuni na lawama zimelengwa kwa Waislamu. Mkristo alikojolea Kurani, Waislamu walitoa taarifa Polisi kwani kitendo hicho ni kosa la jinai kwa sheria za nchi. Lakini huko Polisi, kwa sababu wanazozifahamu wenyewe, ambazo si kazi kubwa kutanabahi ni zipi, wao walijichelewesha kuchukua hatua za kisheria zinazotakikana. Waislamu wakapoteza subra na kuchukua sheria mikononi mwao na matokeo yake yakawa vurugu tupu. Waislamu wakilaumiwa kwa mkasa huo. Kiongozi wa Polisi angetegemewa kusema ukweli wa mambo yalivyokuwa, lakini yeye alitangaza tu kuwa amechoka na wafanya fujo. Hakuwataja hao wafanya fujo ni kina nani lakini mtu yeyote yule mwenye akili ya kufikiri haingekuwa kazi kubwa kutambua kuwa hao ni Waislamu. Imekuwa ni ajabu kubwa sana nchini humu kumezuka rabsha kati ya Waislamu na Wakristo kwa sababu ya kuchinja wanyama ambao nyama zao zinauzwa katika mabucha. Mimi sasa ni mzee na maisha yangu yote nimeyamalizia nchini humu; haikutokea hata siku moja Wakristo wazue ugomvi kwa sababu ya kuchinja. Raki yangu Mchagga kanieleza kuwa huko kwao kila siku wamependelea Muislamu awachinjie ngombe ama mbuzi wa chakula. Kwa mila zao wao hawawezi kula nyama iliyochinjwa na mwanamume ambaye hakutahiriwa. Kwa hiyo hata kwa Mchagga mwenzao mwanamume hawawezi kuwa na uhakika kabisa kuwa huyo bwana katahiriwa. Kwa zaidi ya asilimia tisini na tisa mwanamume mtu mzima Muislamu atakuwa

historia ya kuvumiliana sana na wenzao Wakristo; historia ya nchi hii ni wazi kabisa kwa hilo. Ubaya ni kuwa hawa ndugu Wakristo hasa wale walio na madaraka, makubwa na madogo, hawakubali kabisa kuwa Waislamu wanadhulumiwa baadhi ya haki zao. Huko nyuma ghadhabu za Waislamu kutokana na dharau na dhuluma kama hizo zilikuwa zikielekezwa kwa Serekali na sio kwa Wakristo ama Makanisa. Wakati wa kadhia ya MwembeChai hakuna hata kanisa moja kati ya yale yaliokaribu na msikiti huo yaliguswa na Waislamu. Ghadhabu zote zilielekezewa kwa watendaji wakiwemo Polisi waliowapiga risasi na kuwauwa wasiokuwa na silaha yeyote. Baadae imeonekana kuwa ni hawa watendaji Serekalini walio Wakristo ndio wanafanya dharau kwa Waislamu na ndio kwa mfano wanaochagua wanaoendelea Form I ama FormV na ambao wanahakikisha kuwa Wa i s l a m u w a n a o p e w a nafasi hizo ni wachache. Baada ya MwembeChai askari Muislamu aliyetoa maoni kuwa kitendo kile hakikuwa sahihi alimwaga unga wakivunde na ikabidi akaufuate nyumbani kwao Katonyanga (Ujiji). Sasa iwe kweli MaAskofu na Masheikh wakutane wanawezaje kubomoa ukuta huu uliojengwa na watumishi Serekali walio Wakristo hasa ikikumbukwa kuwa kwa muda mrefu hawa viongozi wa dini ya Kikristo wamekuwa wakiwafundisha wafuasi wao kuwa Uislamu si dini. Mtume Muhammad SAW ni Mtume bandia (false Prophet). Waislamu ni watu wajinga hawakusoma na wako dhalili. Ikiwa kama MaAskofu hawatakubali kuwafundisha waumini wao heshima na adabu kwa Waislamu hata pakiwa na mikutano mingapi huwo msuguwano hautakwisha na pengine makubwa zaidi yatazuka. Amani iko mikononi mwa hawa watendaji wa Serekali walio Wakristo; ni wao waache dhulma na watende haki kwa wote. Waislamu hawataki upendeleo wowote wanataka haki yao tu. Mwisho ikubalike kuwa Waislamu hawaukashifu Ukristo. Hili lilipelekwa mpaka Mahakama ya Rufaa na Mahakimu wakahukumu kuwa Waislamu wanapohubiri kufuatana na mafundisho ya dini yao hiyo sio kashfa kwa Ukristo wala Wakristo. Kwa nini ukweli huu haukubaliwi?

9
makafiri kama ilivyokuja katika Surat Al Kafiruun, atashutumiwa na Wakristo kuwa naye siasa kali! Kumbe masikini aya yenyewe kwa upande mwingine inachofanya ni kuwatetea Wa k r i s t o n a M a k a f i r i , kwamba wasibughudhiwe katika Imani yao, ila na wao wasiwalazimishe Waislamu mambo yao. Wao (makari) wana dini yao na Waislamu wana Dini yao. Sasa kama ni upepo mbaya na ushetani ni huu. Serikali kutosimama katika haki na Masheikh kupiga siasa na propaganda za kuifurahisha Serikali badala ya kusema kweli. Bila shaka tunakumbuka kile kisa cha alioyekuwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Frederick Sumaye kudai kuwa kuna watu wamehitimu ugaidi na wameingia nchini tayari kulipua hospitali ya Muhimbili. Mara baada kauli hiyo Profesa Jahazi na wenzake wawili wakakamtwa. Hili liunganishe na ile kauli ya polisi kuwa kuna Waislamu wanapanga kulipua makanisa hali iliyopelekea jeshi hilo kuranda kutwa mitaani na jirani na makanisa likidai kuwa linawalida Wakristo. Labda tuulize, katika matukio haya, serikali ilikuwa inaimarisha uelewano, amani, umoja na mshikamano baina ya Waislamu na Wakristo au ilikuwa ikipandikiza chuki na uhasama? Kama ni upepo mbaya wa shetani, basi ndio huu. Na huu hauondolewi kwa kuwakutanisha Masheikh na wachungaji. Kama ni kukutana wakutane wakiwa na dhamira ya kujadili mapungufu haya ya serikali, kuiambia ukweli na kuitaka iache mchezo huu mbaya. Tuje katika suala maarufu la OIC japo Tanzania kujiunga na Jumuiya hiyo inaweza isiwasaidie sana Waislamu katika mfumo huu uliopo. Serikali kupitia Waziri wake wa Mambo ya Nje ilitoa kauli Bungeni kwamba baada ya kufanya uchunguzi na utati wa kina, imeridhika kwamba Tanzania kujiunga na OIC hakuna madhara na ilikuwa tayari kufanya hivyo. Lakini msimamo huo ulikuwa tofauti na wa Maaskofu. Na tuliona Waziri Membe akiitwa kwa Kadinali Pengo na kwenda mbio mbio ambapo baada ya hapo, iulize serikali vipi OIC usikie majibu yake! Lakini tukumbuke pia kuwa baada ya Mheshimiwa Membe kuitwa kwa Askofu Pengo, Masheikh nao waliona ni vyema wakamuone Waziri wamuulize, vipi msimamo wa serikali umebadilika na kuwa ule wa Maaskofu? Membe
Inatoka Uk. 7

Makala

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA APRILI 5-11, 2013


Tuliariwa kuwa kuna mtu aliingilia msafara wa Rais Kikwete akamgonga Askari (Traki) na kumuuwa. Taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari ni kuwa mtuhumiwa yule baada ya kukamatwa alifikishwa mahakamani na kupewa dhamana hapo hapo. Ukiuliza utaambiwa kuwa hii ni haki yake ya ki-Katiba (au ni kwa vile alikuwa akiendesha gari la kanisa na kwa hiyo ni mtu wa kanisa?). Hivi akina Ponda wao hawana haki ya Kikatiba? Hili akina Sheikh Mataka hamuwezi kulijadili na kuhoji mpaka mkutane na maaskofu? Wapo Waislamu waliandamana kwenda kwa DPP kuhoji ni kwa nini akina Ponda wananyimwa haki yao ya dhamana. Baadhi yao walikamatwa na kufikishwa mahakamani. Hivi ninapoandika maoni haya wanatumikia kifungo cha mwaka mmoja. Hapa hatuhoji sheria iliyowatia hatiani au kuingilia uhuru wa mahakama. Lakini si vibaya tukijiuliza, ni mara ngapi watu wa vyama vya siasa wamefanya maandamano yaliyopigwa marufuku na serikali? Ni mara ngapi wanaoitwa wanaharakati hufanya maandamano na kubeba mabango ya kuitukana na kuidhalilisha serikali? Je, tulishawahi kusikia wamekamatwa, kufikishwa mahakamani na kufungwa jela? Katika jitihada za kutaka aonekane na Wakristo kuwa ni mtu mzuri sana, Mzee Ally Hassan Mwinyi aliwahi kusema kuwa serikali yake ilimfunga Mheshimiwa Mbunge Muislamu aliyekamatwa na pembe za ndovu na kumwachia huru (kumsamehe) Padiri aliyekamatwa kwa kosa hilo hilo. Huu ndio upepo mbaya na hautaondoka kwa vikao vya Masheikh na Maaskofu. Serikali itende haki. Haya ya kuuliwa Padiri na madai ya kuchomwa makanisa, tuachie vyombo vya dola vifanye kazi kama aliyosema Rais. Lakini tusisahau ule urongo uliopigiwa kelele na wachungaji kuwa kuna makanisa yamechomwa Yombo wakati si kweli. Tusisahau pia yale mazingira ya kutatanisha ya madai ya kuchomwa kanisa Unguja ambapo taarifa ya polisi na mlinzi iliashiria kuwepo kwa mchezo wa kuigiza (inside job). Tumalizie kwa kusema kuwa hakuna kitu kinaitwa kumsomea mtu Itiqaaf kama Rais Kikwete alivyodai kuwa kasomewa Itiqaaf ili afe. Mtu hufa kwa siku zake. Ipo Misikiti mitatu hapa Dar es Salaam wamenisomea itikafu nife. Katika itikafu hiyo wamewajumuisha Inspekta Jenerali wa Polisi, Saidi Mwema na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Ndugu Suleiman Kova. Amesema Mheshimiwa Rais Kikwete katika kuonyesha kuwa Inaendelea Uk. 10

AN-NUUR

hakutaka kuwaona mpaka leo japo walimpa heshma ya kumfuata osini kwake sio kumwita kama alivyoitwa na Kadinali Pengo na kwenda mbio! Sasa huu ndio upepo mbaya na kama ni ushetani ndio huu ambao unatiliwa nguvu na

Hakuna upepo mbaya wala shetani Tanzania


ushirikina wa baadhi ya masheikh ambao hawaiambii
kweli serikali. Labda tumuulize Sheikh wetu Khamisi Mataka, watakapokutana na wachungaji, ndio watapata ujasiri wa kuiambia serikali ukweli kuhusu MoU, Mauwaji ya

Uhusiano wa Wakristo na Waislamu


Inatoka Uk. 7 na ubishi wa kitoto na kijana mwenzake, lakini kitendo hicho kiliwakasirisha Waislamu. Kijana huyo alikishwa kituo cha Polisi. Baadhi ya Waislamu wenye msimamo mkali walika kituoni hapo wakidai wapewe huyo kijana wamuadhibu wao. Jeshi la Polisi lilikataa. Kukatokea mzozo kati ya waumini hao na Polisi na baada ya kushindwa walichokitaka baadhi yao walipotoka pale, wakaenda kufanya uhalifu wa kuvunja, kuiba na kuchoma moto Makanisa. Ndugu Wananchi; Baada ya tukio la Mbagala hapajakuwepo na tukio la kuchomwa Kanisa mahali popote kwa upande wa Bara. Aidha, hapajawahi kuwepo tishio lililothibitika la watu kutaka kuchoma Kanisa popote. Lakini maneno ya vitisho vya kuchoma Makanisa yako mengi hasa kupitia mitandao ya simu za mkononi. Kila ujumbe wa namna hiyo ulipokishwa kwenye vyombo vya usalama uchunguzi umefanywa na hata hatua za tahadhari kuchukuliwa lakini hakuna hata taarifa moja iliyothibitika kuwa na chembe ya ukweli. Hata dalili hazijakuwepo. Tulichojifunza ni kuwa ujumbe na vitisho vya aina mbalimbali hupelekwa kote, kwa Wakristo na Waislamu. Upo unaowalenga Wakristo ukiwaambia wenzao Waislamu wanapanga kuwadhuru. Na upo wanaopelekewa Waislamu wakiambiwa Wakristo wanao mipango mibaya dhidi yao. Watanzania wenzangu nawaomba mtanabahi na mjue kuwa wapo watu wanacheza mchezo mchafu wa kuwagonganisha na kutaka kuwagombanisha Wakristo na Waislamu kwa sababu wanazozijua wao na kwa faida yao. Wanapandikiza chuki kwa lengo la kutaka Wakristo na Waislamu wagombane. Wanapandikiza chuki baina ya Serikali na waumini wa dini zetu kuu mbili ili ionekane Serikali imewatelekeza raia wake. Ni mchezo mbaya, tusikubali kucheza ngoma tusiyoijua. Hivi ndugu zangu mmekaa chini na kujiuliza kumetokea nini kipya hata leo kuwa na mhemko kama huu kati ya Wakristo na

Mwembechai, NECTA, Idadi ya Wakuu wa Wilaya/Mikoa, M a w a z i r i , Wa k u r u g e n z i , Makatibu Wakuu n.k walio Waislamu ikilinganishwa na Wakristo? Ndio watapata mdomo wa kumtetea Sheikh Ponda na Masheikh wa Uamsho kwamba wanashikiliwa bila ya kupewa dhamana kwa dhulma?

halina uhusiano kabisa na lile la Buseresere, Geita. Hapakuwa na mzozo kuhusu nani achinje. Bado uchunguzi wake unaendelea na tumehusisha vyombo vya upelelezi vya nje vishirikiane na vyetu kufanya uchunguzi. Tumefanya hivyo kwa sababu ya ugumu uliopatikana katika uchunguzi wa matukio ya kabla yake. Yaani ile la kupigwa risasi na kujeruhiwa kwa Padri Ambrose Mkenda na kumwagiwa tindikali kwa Naibu Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhili Soroga. Bado hakuna mafanikio ya kutia moyo. Na bado tunajiuliza kama matukio hayo matatu yanahusiana. Je, Makanisa kuchomwa moto kule Zanzibar nako kuna uhusiano wowote na matukio yale matatu? Uchunguzi unaoendelea unaweza kufumbua fumbo hilo. Kuna watu wanadhani yanahusiana na kwa sababu nzuri. Lakini inabaki kuwa ni dhana ya kibinadamu mpaka ukweli halisi utakapobainika. Bado kazi ya uchunguzi inaendelea kufanywa na vyombo vya usalama vya nchi yetu wakishirikiana na wenzao wa nje. Katika mazingira hayo, ni mapema mno kumnyooshea kidole mtu ye yote na kuilaumu Serikali ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Serikali siyo mshirika katika mauaji hayo, na haina sababu ya kufanya hivyo. Ndiyo maana tunahangaika usiku na mchana kupata jawabu. Ndugu Wananchi; Hali kadhalika tukio la Makanisa ya Mbagala, Dar Es Salaam kuvamiwa, kubomolewa, mali kuibiwa na kuchomwa moto tarehe 12 Oktoba, 2012 nalo lina mazingira yake maalum. Chanzo chake ni mzozo uliotokana na tukio la kusikitisha la kijana mmoja Mkristo kukojolea Kitabu Kitakatifu cha Waislamu, yaani Quran Tukufu. Pamoja na maelezo kuwa walikuwa

Waislamu na kutishia kuleta vita baina nchini kote? Ndugu Wananchi; Serikali haijapuuzia kila palipotokea matukio ya uhalifu. Wa t u 7 6 w a n a o t u h u m i w a kuharibu na kuchoma moto Makanisa kule Mbagala na kufanya fujo kituo cha Polisi wamekamatwa na kesi zao zinaendelea Mahakamani. Kwa upande wa tukio la Buseresere lililosababisha kifo cha Mchungaji Mathayo Kachila, watu 17, wakiwemo waumini wa dini ya Kikristo na Kiislamu walikamatwa na kesi zao zinaendelea. Wapo walioshitakiwa kwa mauaji na wapo walioshitakiwa kwa kufanya vurugu. Jeshi la Polisi bado linawatafuta watu wengine waliohusika na uhalifu huo ili na wao wakamatwe. Kwa upande wa Zanzibar, watu 10 wanaotuhumiwa kuchoma Makanisa wamekamatwa na kesi zao zinaendelea. Bado hajakamatwa mtu kwa tukio la mwisho la kuchoma Kanisa baada ya kuuawa Padri Evaristus Mushi. Uchunguzi unaendelea. Ndugu Wananchi; Kwa upande wa kujeruhiwa kwa Padre Mkenda, bado uchunguzi haujakamilika pamoja na kuwapo taarifa kadhaa zinazoendelea kufanyiwa kazi. Kuhusu uchunguzi wa mauaji ya Padre Mushi, baada ya jitihada kubwa kufanyika ikiwa ni pamoja na kushirikisha nchi zilizobobea katika uchunguzi wa makosa ya aina hii, hatua ya kutia moyo imekiwa. Mtu mmoja amekamatwa na wengine wanaendelea kutafutwa. Ndugu Wananchi; Kwa upande wa kanda na vituo vya redio nako pia Serikali imechukua hatua. Watu kadhaa wamekamatwa na kufikishwa Mahakamani katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwa kurekodi na kusambaza kanda zinazochochea chuki na vurugu za kidini. Wapo Waislamu na Wakristo. Wapo watu wengine ambao wanaendelea kutafutwa. Zipo taarifa kuwa baadhi yao wamekimbilia nchi za nje. Jeshi la Polisi limeomba msaada wa Polisi wa Kimataifa, yaani Interpol, kusaidia kuwatafuta na kuwarejesha nchini. Vituo Inaendelea Uk. 11

10
Na anza kutakadamu, kwayo isimu adhimu Ni kitendo cha nidhamu, cha kumtaja Rahimu Yatueleza ilimu, alotufunza Imamu Mkaja watoka wapi, na wauliza wajuzi Ni hivi tu juzijuzi, moyo ulipo khiyari Kubaidi uchafuzi, na tamaa za suduri Kurukaruka ka Mbuzi, maisha yana khururi Mkaja watoka wapi, na wauliza wajuzi Mwili wahitaji stara, mavazi yalo sambamba Kuswali isitikhara, kuepuka ya mtumba Isichafuke tijara, alodhamiri muumba Mkaja watoka wapi, nawauliza wajuzi Nilipanda majahazi, kulisaka pumziko Nazo treni jozijozi, sikuambulia kito Bara ndio muokozi, mtima wangu suuziko Mkaja watoka wapi, nawauliza wajuzi Posa nikaipeleka, kwa mafundisho murua Ilinipate fanaka, wazaziwe kunijua Zimiminike Baraka, wanijaze nazo dua Mkaja watoka wapi, nawauliza wajuzi Yakarudi mashariti, nazo kanuni pomoni Malaki nayo manoti, mkaja nao undani Kaniki nayo mashati, usinga navyo vidani Mkaja watoka wapi, nawauliza wajuzi Najiuliza maswali, asiliye nijuzeni Mafundisho ya Rasuli, au toka kwa Rahmani Nithibitishe kauli, kiti cha babu cha nini Mkaja watoka wapi, nawauliza wajuzi Ndee nawaulizeni, muhadithi na fakihu Jawabu nipatieni, zenye ladha na rihu Moshi ndio masikani, raufu tumsabihu Mkaja watoka wapi, nawauliza wajuzi Hapa ninatua nanga, fatawa kuzikaribu Kichwa nacho chanigonga, namsubiri tabibu Anijibu kimalenga, au darsa mujarabu Mkaja watoka wapi, nawauliza wajuzi

Mashairi/Makala
MKAJA ASILIYE WAPI?

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA APRILI 5-11, 2013

AN-NUUR

Hakuna upepo mbaya wala shetani Tanzania


Inatoka Uk. 9 wapo Waislamu wanaomtuhumu kuwa anawapendelea Wakristo. Pengine tuseme kuwa alichosema Rais Kikwete ni ushahidi mwingine wa madai ya Waislamu. Ameongeza ushahidi mwingine kutoka Ikulu. Kule Baraza la Mitihani (NECTA) tumesema kuwa wameajiri Mchungaji wa kusimamia maslahi ya vijana wa Kikristo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa mtihani

NDEE SWALEHE (swahiba wa mnyonge) CHUO KIKUU CHA WAISLAMU MOROGORO

Kalamu i mkononi, ukweli kukujuzeni, Kuhusu yetu amani, kuzidi kuwa shakani, Dhulma ndicho kiini, cha toweko la amani, Udhalimu na amani, katu havitangamani. Viwili hivi jamani, si leo tangu zamani, Muhali na asilani, kutangamana chunguni, Vinginevyo tafrani, amini usiamini, Udhalimu na amani, katu havitangamani. Pengi paso na amani, dhulma hikosi ndani, Lichungue si utani, jambo hili kwa makini, Kweli utajabaini, hata kama ni mwakani, Udhalimu na amani, katu havitangamani.

DHULMA NA AMANI !

Amani ya mumiani, kamwe si ya kuamini, Nchi tenge tahanani, nyingi chanzo mumiani, Twaweka nchi kwa nini, rehani kwa mumiani, Udhalimu na amani, katu havitangamani. Kukichungua kiini, kwa kina na tamakuni, Ni jukumu letu ndani, katu si la mumiani, Mvunjifu namba wani, wa amani duniani, Udhalimu na amani, katu havitangamani. Nachombeza msidhani, mithali nitakupeni, Aloivunja amani, kwa utuvu nijuzeni, Iraq na Afghani, kama si yeye ni nani, Udhalimu na amani, katu havitangamani. Saddamu kitanzini, alomtia ni nani, Kulikoni na kwanini, twazidi kumuamini, Katu sinaye imani, kwa amani ya nchini, Udhalimu na amani, katu havitangamani. Suluhisho si auni, kutoka ughaibuni, Bali haki kuthamini, kwa insafu za insani, Hapo ya kweli amani, itatangaa nchini, Udhalimu na amani, muhali kutangamana. ABUU NYAMKOMOGI MWANZA.

unaotungwa haukosewi kimaudhui, lugha na kiimani. Lakini kwa upande wa Waislamu, somo la Maarifa ya Uislamu linaonekana ni jambo la bora liende. NECTA imekataa kuajiri mtaalamu wa somo hilo. Yupo mtaalamu wa Lugha ya Kiingereza, Kiswahili na Kifaransa. Lakini kwa sababu Kiarabu kinaonekana ni Uislamu, mtaalamu wa Kifaransa asiyejua hata Alifu, ndiye huambiwa asimamie Lugha ya Kiarabu! Lau Ikulu pangekuwa na mtaalamu wa Kiislamu wa kuangalia hotuba za viongozi wa kitaifa wanapoalikwa katika hafla za Kiislamu, au kuzungumzia mambo ya kiimani ya Kiislamu, hatudhani kuwa hotuba ya Mheshimiwa Rais Kikwete ingekuwa na sentesi kama hii ya kusomewa Itiqaf. Lakini inavyoonekana ni mtindo ule ule wa Mirathi ya Kiislamu kupewa hakimu Mkatoliki au Mlokole asiyejua Aya wala Hadithi. Ukiuliza utaambiwa kuwa, kuwa na Mahakama ya Kadhi ni U-Dini! Mbona hatusemi kupumzika Jumapili na MoU ni Ukristo! Watu wanakaa Itiqaaf Msikitini kusoma Quran, kuswali, kumdhukuru Mweyezi Mungu, kufanya Istighfari na ibada mbalimbali. Wanatumia pia fursa hiyo kumlilia Mola wao kutokana na shida mbalimbali zinazowakabili. Rais Kikwete hana sababu ya kuwa na hofu kwa sababu hata kama katajwa na kuombewa dua mbaya katika Itiqaaf hizo, kama hakuwakosea Waislamu; laana hiyo haitamgusa. Itawarudia waliomlani. Hiyo ndio kanuni ya Mwenyezi Mungu. Kwamba ukimwombea mtu dua mbaya na kumlani kwa madai ya uwongo wakati hajakukosea wala kukudhulumu, basi laana hiyo haianguki chini.

H I V I s a s a Wa k r i s t o wanaotaka wachinje na nyama wanayochinja iuzwe mabuchani kama wanavyofanya Waislamu, wanaonekana kama watu wakoro. Ni kweli wanaweza kuwa ni wakoro, lakini swali ni je, ukoro huu wameupata wapi? Mbona madai wanayoyaleta hivi sasa hawakuyaleta mwaka 1911, 1961 wala 2005? Kwa maana mbona tatizo hili halijawahi kuwepo toka Ukristo umeingia nchini? Au kuna Biblia Mpya imekuja? Kule kwetu Usangi kuna wazee wa Kiislamu waliporwa mashamba yao ili kupisha ujenzi wa shule ya Kanisa. Pamoja na kulalamika sana, hawakulipwa hata senti moja kama dia. Padiri Dr. John Sivalon katika utafiti wake ameeleza kuwa Maaskofu waliwahi kutoa kauli kwamba wasingependa kuona umoja wa Waislamu chini ya East Africa Muslim Welfare Society (EAMWS) Ukiwepo. Haikuchukua muda Serikali ikapiga marufuku Jumuiya hiyo na taasisi zote za Kiislamu zilizokuwa zikishughulika na kuwaletea maendeleo katika elimu na huduma za kijamii. Katika utafiti huo kama alivyouchapisha katika kitabu chake Kanisa Katoliki na Siasa Tanzania anasema kuwa wakati ule kukiwa na hali ngumu ya kiuchumi (wakati wa Mwalimu Nyerere), Maaskofu walitaka waruhusiwe kuingiza vitu kutoka Kenya japo mpaka wa Kenya na Tanzania ulikuwa umefungwa. Wakapewa kibali hicho ambapo waliingiza bidhaa (kutoka nchi nyingine za nje) bila ya kulipa kodi. Walitaka Serikali ichote pesa katika Hazina ya Taifa kuwapa waendeshe taasisi zao za elimu na afya. Wakapewa kinyemela na baadae kuhalalishwa kwa MoU. Kuna kisa kimoja ambapo wanafunzi wa Chuo cha Ushirika Moshi walitaka kujenga Msikiti na kibali wakapata. Lakini ghafla Kiongozi wa Watawa wa Kikatoliki akasema hataki Msikiti katika eneo hilo. Ikawa tabu kujenga Msikiti. Kauli ya

Mgogoro wa Kuchinja

Humrudia aliyeitoa. Sasa labda badala ya Mheshimiwa Rais Kikwete kushughulishwa na Itiqaaf za Waislamu angejiuliza, hivi katika nchi hii, hakuna Waislamu wenye sifa ya kuwa Wakuu wa Mikoa, Wilaya na nafasi mbalimbali

serikalini mpaka ikie mahali baadhi ya vikao vya taasisi za kiserikali na mashirika ya umma vikifanyika waliohudhuria wanajikuta wapo kama walivyokutana kwenye Misa?
Inaendelea Uk. 11

Sister ikawa na nguvu sana. Katika ile kadhia ya mabucha ya nguruwe, walalamikaji walikuwa Waislamu. Kwamba nguruwe walikuwa wakifugwa na kuuzwa ovyo bila kufuata sheria za miji. Hakuna Mkristo aliyeguswa kwa kuachia nguruwe wake hadi kuingia Misikitini. Ukali wa Serikali ulionekana pale Waislamu walipojaribu kuchoma banda la nguruwe mtaani kwao, nguruwe ambao huachiwa wakaranda ovyo mitaani. Mifano ni mingi sana lakini tugusie hili la inayodaiwa kuwa Mihadhara ya Kashfa. Yupo kijana Korogwe aliwahi kukamatwa na kuwekwa ndani kwa sababu aliandika katika baisikeli yake kuwa Yesu Si Mungu. Ni kweli kwa imani yake ya Kiislamu Yesu Si Mungu, lakini aliwekwa ndani. Hili likafuatiwa na lile shinikizo la Paroko Camillius Lwambano ambaye aliitaka Serikali iwakamate na kuwatia adabu watu wanaohubiri k u w a Ye s u s i M u n g u . Masheikh na wahubiri wa Kiislamu wakakamatwa hali iliyoishia na kufanya mauwaji Mwembechai. H i v i n d i v y o Wa k r i s t o walivyolelewa na Serikali. Wa k i s e m a w a n a s i k i l i z w a Serikali inatekeleza. Ndio maana Serikali inashindwa kujiunga na OIC au kuanzisha Mahakama ya Kadhi. Malezi haya yamewakisha Wakristo mahali pa kujiamini sana na kwa hakika kuwa na kiburi kwamba walitakalo lazima liwe. Ndio maana hivi sasa wanaishangaa Serikali vipi inawazuiya kuchinja na Waislamu wakala. Maaskofu wamesema, marufuku Tanzania kujiunga na OIC au kuwa na Mahakama ya Kadhi, mwelekeo ni Serikali kutii. Sasa wanasema, lazima Wakristo wachinje na nyama iuzwe sokoni na mabuchani. Wamejisemea Waswahili, mchelea mwiba guu huota tende. Na mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.

11
Inatoka Uk. 10 Je, ile kauli aliyotoa Dodoma kuhusu MoU, ndio majibu sahihi ya madai ya Waislamu kuhusu ubaguzi nchini? Wapo watu wapo ndani na haki yao ya dhamana kama Katiba ya nchi inavyoagiza imezuiliwa. Mambo kama haya yalishawahi kutokea wakati wa Sheikh Kassim Juma Bin Khamisi, Sheikh Pazi, Sheikh Abdallah Chata na masheikh wengine ambao waliwekwa ndani kwa zaidi ya miezi sita kwa sababu dhamana yao ilizuiwa. Kama lipo la kumshughulisha Rais Kikwete, basi ni mambo kama haya maana hatujawahi kusikia katika historia ya nchi hii kwamba kuna Padiri au Mzee wa Kanisa aliyewahi kufanyiwa mambo kama haya. Muhimu zaidi kwa Mheshimiwa Kikwete kuzingatia ni kuwa Kila mchunga ataulizwa. Na siku hiyo hakutakuwa na Saidi Mwema wala Kamanda Kova wa kutuma FFU mitaani. IGP atatoka wapi wakati tunaambiwa kuwa siku hiyo utakapo kuja ukulele. Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye. Na mamaye na babaye. Na mkewe na wanawe. Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha. Rais Kikwete anasema kuwa Waislamu wanamtuhumu kuwa anapendelea Wakristo na kwa upande mwingine Wakristo nao wanamtupia lawama kuwa anawapendelea Waislamu. Wakati wa Rais Ally Hassan Mwinyi lilifanyika jambo moja zuri sana japo halikukamilishwa. Ilikuwa ni katika kipindi cha Mzee Mwinyi, Maaskofu walikuja juu sana na kauli zao kali kali kuwa Waislamu wanakashifu Ukristo. Alichofanya Mwinyi ni kuita mkutano wa pamoja baina ya Masheikh na Maaskofu pale Ikulu. Masheikh wakaja na vielelezo vyao kuonyesha na kukanusha kuwa hawatukani wala kukashifu Wakristo. Maaskofu nao wakatakiwa walete ufafanuzi na ushahidi wa kuonyesha ni mambo gani au ni kauli zipi wakisema Waislamu wanaukashifu Ukiristo. Maaskofu hawakurudi tena Ikulu mpaka leo kuleta ufafanuzi na ushahidi wao. Lakini hawakuacha kuichagiza serikali juu ya madai yao kuwa Waislamu wanakashifu Ukristo. Sasa maadhali Mheshimiwa Rais amesema kuwa Waziri

Makala

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA APRILI 5-11, 2013


Mkuu amepanga kufanya mkutano wa pamoja baina ya viongozi wa Kikristo na wa Kiislamu, sisi tunadhani kuwa mkutano huo utakuwa na maana iwapo Waislamu wataambiwa waje na ushahidi wao kuonyesha jinsi wanavyobaguliwa, kudhulumiwa na kukandamizwa na serikali. Na kwa upande wao Wakristo nao waje na ushahidi kuonyesha jinsi serikali inavyowapendelea Waislamu na kuwatesa Wakristo. Vinginevyo itakuwa ni kupiga tu siasa ambazo hazitasaidia kuepusha Taifa hili na migogoro ya kidini. Tatizo hapa ni kuwa kuna watu wamekuwa wakidhulumiwa na wengine wakifaidi katika mfumo wa dhulma. Wanaodhulumiwa wanataka dhulma ikome, w an ao f aid ik a k u to k an a na mfumo wa dhulma na ubaguzi wanataka dhulma iendelee. Na moja ya mbinu zao ni kujifanya wao ndio wadhulumiwa na wanaoonewa kama inavyofanya Israel kwa Wapalestina.

AN-NUUR

Hakuna upepo mbaya wala shetani Tanzania

RAIS Jakaya Kikwete (kulia) na Muft Sheikh Issa Shaaban Simba

Uhusiano wa Wakristo na Waislamu


Inatoka Uk. 9
viwili vya radio yaani Kwa Neema FM cha Sengereme na Radio Imani cha Morogoro vimefungiwa kwa muda wa miezi sita. Baada ya muda huo kupita, Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano itaamua ipasavyo. Ndugu Wananchi; Nimeyaeleza haya kwa kirefu kuwahakikishia kuwa Serikali inajali usalama wa raia wake wa mali zao na amani na utulivu wa nchi yetu. Kamwe hatujashindwa kulinda raia wa nchi wa yetu na yapo mambo mengi yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika kuhakikisha kuwa Watanzania wa dini zote, makabila yote, rangi zote na mahali po pote walipo wako salama. Tunataka kuona watu wanaendelea kuishi kwa amani, upendo, ushirikiano na mshikamano kama tulivyokuwa tunaishi siku zote. Tunapenda kuona Watanzania wanaepuka mambo yanayowabagua na kusisitiza yale yanayowaunganisha. Tujiepushe kuyapa kipaumbele yale yanayotugawa. Ndugu Wananchi; Athari za mzozo kuhusu kuchinja kule Geita iwe fundisho kwetu sote. Tuazimie sote kuwa yaliyopita si ndwele, tugange yajayo. Hebu tukirie maisha yetu Watanzania yatakuwaje kwenye shughuli za kijamii kama vile sherehe, harusi, ngoma na misiba iwapo tutaanza kuwa na chakula tofauti kwa Waislamu na Wakristo. Fikiria itakuwaje kwenye hospitali, shule na vyuo pawe na majiko mawili au labda hata mabwalo mawili ya chakula kwa Waislamu na Wakristo. Jeshini nako kuwe na majiko na mabwalo ya Waislamu na Wakristo. Hali iwe hivyo hivyo kwenye migahawa na maeneo mengine yenye huduma ya chakula. Ndugu zangu, tunataka kuipeleka wapi nchi yetu? Tunataka kujenga nchi ya namna gani? Mimi naamini tukifanya hivyo huo utakuwa ndiyo mwanzo wa kubaguana kwa kila kitu na kila jambo na kuligawa taifa kwa namna ambayo hatutakuwa wamoja tena. Huko tunakoelekea siko, ni kubaya. Tubadilike, na wakati

ni huu. Viongozi wa dini waongoze njia wawaepushe waumini wao na taifa letu na janga hili. Ndugu Wananchi; Bado narudia kusisitiza umuhimu wa viongozi wa dini zetu kubwa mbili kukutana na kuizungumzia hali hii na kuipatia ufumbuzi. Ni wao kuliko mtu mwingine ye yote wenye majawabu ya matatizo haya. Ni masuala yanayohusu imani za dini na yanafanywa na viongozi wa dini na wafuasi wao kwa jina la dini zao. Serikali ina wajibu wa kulinda amani. Kazi yetu itakuwa rahisi kama waumini hawatafanya

vitendo vitakavyosababisha uvunjifu wa amani. Wa kuongoza waumini lipi jema na lipi baya ni viongozi wa dini. Ndugu Wananchi; Nimeshakutana na viongozi kadhaa wa madhehebu na taasisi za dini za Kikristo na Kiislamu kuzungumza nao kuhusu jambo hilo. Nimepata faraja kuona kuwa wote wanasikitishwa na mambo yanayotokea hivi sasa na wameona busara ya viongozi wa dini kuzungumza ili kuondoa tofauti zilizojitokeza. Wanakiri kuwa hali ilivyo sasa siyo ya kawaida kwa Tanzania na Watanzania. Kuna upepo mbaya wa shetani unapita ambao viongozi wa dini wana wajibu wa kuhakikisha kuwa hali ya hewa inasafishwa na kurejesha nchi yetu na watu wake katika maisha tuliyoyazoea. Maisha ambayo waumini wa dini tofauti wanaishi pamoja kwa udugu, upendo, ushirikiano na mshikamano kwa misingi ya ubinadamu wao na Utanzania wao. Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda, ameshaeleza dhamira ya Serikali ya kuitisha mkutano wa viongozi wa dini mapema mwezi ujao. Ni matumaini yangu kuwa wote watashiriki wenyewe bila ya

kutuma wawakilishi. Lazima tupate jawabu kwa maslahi ya taifa letu na watu wake. Ndugu Wananchi; Kabla ya kumaliza hotuba yangu napenda kutumia nafasi hii kuwaomba na kuwasihi waandishi wa habari wasaidie kuliepusha taifa letu kuingia katika vita vya kidini. Waache kushabikia taarifa zinazochochea na kujenga uhasama baina ya waumini wa dini zetu. Nawaomba wapime athari za taarifa zao kabla ya kuziandika au kuzitangaza. Wawe makini na maneno wanayotumia. Katika hali tuliyonayo sasa lazima sote tuazimie kuondoa tofauti za kidini na kujenga umoja miongoni mwa Watanzania wa dini zote. Wasipofanya hivyo, wataliingiza taifa katika mgogoro mkubwa ambao hauna msingi kama ilivyotokea katika nchi jirani. Nawaomba wamiliki wa vyombo vya habari kutambua kuwa wanao wajibu wa kuhakikisha vyombo vyao havitumiki kuleta mifarakano kwa kuchochea uhasama baina ya Wakristo na Waislamu. (Hii ni sehemu ya JAKAYA MRISHO KIKWETE, R A I S WA J A M H U R I YA M U U N G A N O WA TA N Z A N I A , K WA WANANCHI, TAREHE 31 MACHI, 2013)

AN-NUUR
12

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA APRILI 5-11, 2013

Usikose nakala yako ya AN-NUUR kila Ijumaa

Vijana wa Kiislam wapigwa msasa


Na Bakari Mwakangwale
IMEELEZWAkuwa kupigania haki ni kazi ngumu na yenye changamoto nyingi. Sheikh Ahmed Ayoub Kidege, ameeleza hayo akiongea katika Semina ya Vijana wa Kiislamu iliyofanyika katika Shule ya Kiislamu Ununio, Tegeta Jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita na kushirikisha vijana wa Kiislamu kutoka Mikoa mbalimbali nchini. Akiwasilisha mada yake yenye anuani, Nafasi ya Kijana Katika Kuhuisha Uislamu, Sheikh Kidege, toka Mkoani Tanga alisema, kijana wa Kiislamu au Muislamu yeyote atakapoamua kuzungumza haki lazima ataandamwa na kukumbwa na misukosuko. Kidege alisema ili uwe salama kama Muislamu dhidi ya Serikali yenye utawala kama huo, lazima uwe Muislamu wa kuvaa Kanzu, kujenga Misikiti, kuendesha na kuwashughulisha Waislamu katika Maulidi na si nje ya hapo. Uislamu wa kuvaa Kanzu, kujenga Misikiti, kusimamia Maulid, haumstui Kafiri au Serikali yenye misingi ya kuegemea upande mmoja wa kundi katika jamii. Lakini Uislamu wa kutaka haki isimame, kuondoa dhulma, Serikali watapanga mikakati ya kukushughulikia. Alisema Kidege. Hata hivyo, alitanabaisha kwamba asieleweke vibaya au hana maana kuwa Maulidi, ujenzi wa Misikiti na kuvaa Kanzu ni vitu ambavyo havitakiwi au havina maana katika Uislamu, bali ni katika kufafanua juu ya changamoto na uzito wa kupigania haki na kusema kweli. Sheikh Kidege, alisema Kuhuisha Uislamu katika jamii maana yake ni kuweka mikakati itakayowezesha Waislamu kutekeleza wajibu wao wa kusimamisha haki, kuamrisha mema, kukataza maovu na kuhakikisha haki inatendeka. Kwa upande wake Katibu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T), Sheikh Ramadhani Sanze, aliwataka vijana wa Kiislamu kuratibu na kupanga mambo yao sawasawa kabla ya kuyaendea. Sanze alisema kijana anapofanya mambo yake

hatakiwi kukurupuka au kubahatisha bali awe katika mipango madhubuti ambayo mwisho wake ulete tija na ufanisi katika j Sanze aliwataka vijana wa Kiislamu kuwasoma na kujifunza kutoka kwa Maswahaba kama Omar, Hamza, Khalid bin Walid, Ally, Othman, Bilali bin Rabah na wengineo ili kujifunza ni kwa namna gani waliweza kukabiliana na maadui wa Uislamu. Sanze alisema ujana ni amana, na ndio maana Mwenyezi Mungu ameweka mipaka kwa kuulizwa siku ya siku kuwa katika mapito ya ujana wako uliutumiaje.

Na Bakari Mwakangwale

Waislamu jijini Dar wachangia Damu


hospitali tano kubwa Jijini Dar es Salaam. Alizitaja Hospitali hizo ambazo zimenufaika na huduma za Akhlaaqul-Islaam (JAI) kuwa ni Hospitali za Mikoa ya Kinondoni, Ilala, Temeke, Ocean Road pamoja na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ambapo kwa kiasi kikubwa Taasisi hiyo imeweza kutoa huduma za dawa, Usari na mazishi. Jumuiya imefanikiwa kutoa huduma kwa wagonjwa elfu kumi, katika vituo vitano vya hospitali hapa Jijini, pia tumefanikiwa kukusanya damu kwa kushawishi jamii na kupata jumla ya uniti 924. Lakini pia tumeweza kupunguza mrundikano wa wagonjwa na maiati kwa kusubiri huduma kama vile Madawa, Usari na Mazishi. Alisema Ust. Salim, mbele ya mgeni rasmi. Alisema, katika harakati hizo za kutoa huduma kwa wagonjwa kumekuwa na mwitikio mzuri kwa wanajamii katika kutoa huduma kwa kujitolea, jambo ambalo limewawezesha kupanua huduma zao katika Hospitali za Mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Morogoro na Pwani. Ust. Salim, alisema pamoja na kupata mwitikio huo, lakini bado kunahitajika nguvu za ziada kulingana na upana wa mahitajio kwa kuielimisha jamii umuhimu wa kila mmoja kuwa tayari kusaidia kwa hali na mali harakati za kuinusuru jamii iliyokata tamaa na mtihani wa maradhi. Ust. Salim, alimweleza Naibu Waziri wa Afya, kwamba katika harakati zao hizo za kutoa huduma kwa hiyari wamekuwa wakikutana na vikwazo vya kiutendaji baina ya Taasisi yao na baadhi ya watumishi katika sekta hiyo ya afya. Mheshimiwa Waziri, mashirikiano ya kiutendaji baina yetu na baadhi ya watumishi si mazuri katika harakati zetu hizi, pia kupanda mara kwa mara kwa bei za Madawa na vifaa vya tiba nalo ni tatizo kubwa, kwa ujumla hizo ni changamoto kwetu. Alisema Ust. Salim, bila kufafanua zaidi. Awali Ust. Salim, alisema, Jumiya hiyo inatambua hali halisi ya maisha ya kila Mtanzania pamoja na

MGENI Rasmi Naibu Waziri wa Afya Mh. Seif Rashid (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Jumuiya ya Kiislamu ya Akhlaaqul-Islaam, ya Jijini Dar es Salaam, katika zoezi la kuchangia damu salama katika viwanja vya Msikiti wa Muhimbili, mwishoni mwa wiki iliyopita.

JUMUIYA ya Kiislamu ya Akhlaaqul-Islaam, ya Jijini Dar es Salaam, imefanikiwa kukusanya damu kiasi cha uniti 924, kutoka kwa wanajamii sambamba na kupunguza mrundikano wa wagonjwa na maiti kwa kusubiri huduma mbalimbali. Hayo yamebainishwa na Ustadhi Saad Ahmed Salim, akisoma risala ya Jumuiya hiyo mbele ya mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Afya Mh. Seif Rashid, katika viwanja vya Msikiti wa Muhimbili, mwishoni mwa wiki iliyopita. Waislamu mbalimbali chini ya Jumuiya hiyo, walifika katika Hospitali hiyo ya Taifa ya Muhimbili, ikiwa ni siku ya kuchangia Damu kwa hiyari, ambapo waliitikia wito wa kutoa damu kwa hiyari. Ust. Salim, alisema mbali na kuchangia damu kwa kiasi hicho Jumuiya hiyo, pia imefanikiwa kutoa huduma kwa wagonjwa wapatao elfu kumi (10,000) katika

kuzingatia kupanda kwa gharama za matibabu, dawa za binadamu na vifaa mbalimbali vya tiba. Kwa maana hiyo alisema Ust. Salim, kwamba Jumuiya hiyo chini ya kaulimbiu yake ya Huruma na Upendo imekusudia kutoa huduma zote stahiki kwa wagonjwa wa jinsia zote, waliopo majumbani na hospitalini, bila kujali imani zao za kidini. Ust. Salim, alianisha h ud uma zitolew azo na Jumuiya hiyo kila siku kuwa ni kuwaombea dua na kuwafariji wagonjwa, kuwanunulia dawa za matibabu zilizokosekana hospitalini, kuwachangia damu. Alizitaja huduma zingine zitolewazo kwa wagonjwa na Jumuiya hiyo ya Kiislamu kuwa ni pamoja na kuwafanyia usa katika hali zote stahiki, kuwapatia chakula kwa kufuata maelekezo ya daktari, pamoja na kufanya usa wa mazingira mahospitali. Jumuiya ya Waislamu kitengo cha Afya na Ustawi wa Jamii (JAI), ni Taasisi isiyo ya Kiserikali, ambayo ilianzishwa miaka mitatu iliyopita.

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

You might also like