You are on page 1of 16

www.annuurpapers.co.

tz

Sauti ya Waislamu

(5) TAJIRIKA KWA KUHIJJI!


Mtume(saw) amesema, Mahujaji wanarudishiwa kila walichokitumia katika Hijja, shilingi moja kwa milioni moja. Hivyo twende wengi, na mara nyingi kuhiji. Kadhalika tutumie mali zetu KUISIMAMISHA NGUZO YA HIJJA. Jiunge na Ahlu Sunna wal Jamaa. Gharama zote ni Dola 4,300. Tafadhaliwasiliana nasi ifuatavyo: Tanzania Bara: 0717224437; 0777462022;Unguja: 0777458075;Pemba: 0776357117.

Njama za kulitumbukiza Taifa katika machafuko zachuliwa


Vyombo vya habari, Serikali yahusishwa Waislamu watoa tamko zito, watoa onyo Waeleza Serikali inavyokoleza tna, chuki

ISSN 0856 - 3861 Na. 1062 JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 15-21, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda.

Ukweli wadhihiri juu ya muungano


Maoni ya Baraza yafunga mjadala Si suala la Mzee Moyo wala Uamsho Ni la wananchi na Wawakilishi wao

WAZIRI mstaafu, Frederick Sumaye.

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini , Said Mwema

Nchimbi ajiuzulu - Maalim Seif


Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi

kujiuzulu katika wadhifa wake kutokana na kushindwa kusimamia Wizara yake katika wa majukumu KATIBU mkuu wa Chama cha utekelezaji Wananchi CUF Mh. Maalim yake. Akizungumza katika mkutano Seif Sharif Hamad amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Inaendelea Uk. 6 Nchi Dkt. Emmanuel Nchimbi

Mahakama kupitia pingamizi dhamana ya Imam Hamza Uk. 6

2
AN-NUUR

Tahariri/Habari/Tangazo

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 15 - 21, 2013

AN-NUUR

S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Ukweli wadhihiri juu ya muungano


Na Mwandishi Wetu UKWELI sasa upo wazi. Hoja ya Zanzibar kama nchi na Dola kamili, si suala la watu wachache, bali la wananchi na Wawakilishi wao katika Bunge. Hilo linadaiwa kufahamika baada ya kufichuka kuwa maoni ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar juu ya Katiba Mpya yanafanana na yale yaliyowahi kutolewa na Mzee Hassan Nassor Moyo, Mansour, Masheikh wa Uamsho na Wazanzibari walio wengi. Inaelezwa kuwa pamoja na mambo mengine, katika maoni yao Wawakilishi wamesisitiza hoja ya kuwepo kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotokana na Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Ikafafanuliwa katika nukta hiyo kuwa ni lazima Katiba Mpya ijayo ihakikishe kuwepo na maeneo maalum ya mamlaka ambayo Zanzibar ina uwezo nayo kama nchi (Mamlaka ya Dola ya Zanzibar). Habari za uhakika zinafahamisha kuwa maoni yaliyowahi kutolewa na baadhi ya Wawakilishi kama Mheshimiwa Jussa juu ya muundo wa muungano na hadhi ya Zanzibar katika muungano huo, yanajitokeza katika maoni ya pamoja ya Wawakilishi katika Baraza yaliyowasilishwa na Spika Pandu Ameir Kicho kwa idhini ya Kamati ya Uongozi na Shughuli za Baraza ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar. H a b a r i h i z o z i n a f a h a m i s h a k u w a Wa w a k i l i s h i wanapendekeza kuwepo na Mamlaka ya Zanzibar huru na Mamlaka ya Tanganyika huru ndani ya Jamhuri ya Muungano. Katika hali hiyo, kinachosisitizwa ni kuwa Mamlaka ya Muungano yawekwe wazi na kwamba kuwe na usawa wa Ushirikishwaji katika Mamlaka ya Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar. Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari katika Baraza na katika Tume ya Jaji Warioba, inapendekezwa kuwa ile hali ya sasa ambapo jambo linaweza kuingizwa katika muungano bila kupata ridhaa ya Zanzibar ipigwe marufuku. Na zaidi ni kuwa maadhali zilizoungana ni nchi mbili huru, kila moja ikibaki na dola yake kamili, basi hata katika utoaji wa Rais wa muungano na makamo wake liwe ni jambo la kupokezana. Sambamba na hilo, kinachosisitizwa ni kuwa utungaji wa sera na sheria za muungano, lisiwe ni jambo la kufanyika Dodoma katika mamlaka za muungano, bali Dola mbili zihusike na kuridhia. Pamoja na maoni hayo kama yanavyodaiwa kuwasilishwa kwa Tume, inashauriwa pia kuwa kila nchi iwe na rasilimali zake na kwamba zile za muungano zitambuliwe na hizo ndio zitumike katika uendeshaji wa mamlaka za muungano. Na kama kutakuwa na kugawana mapato kutokana na rasilimali hizo, basi ugawaji ufanyike kwa uwiano maalum utakaokubaliwa kwa pamoja na pande mbili za Muungano. Duru za kisiasa nchini zinafahamisha kuwa kama Tume ya Jaji Warioba itafanya kazi yake kwa uadilifu na kujali maoni ya wananchi na vyombo vyao vya uwakilishi, hakuna namna ya kukwepa kufanya mabadiliko makubwa katika mfumo wa muungano. Na kwamba hakuna namna nyingine ya kufanya mabadiliko hayo yawakilishe matakwa ya wananchi (Wazanzibari) na hivyo kukubalika na kupata uhalali wa kisiasa, ila kwa kukia hatma ya kurejesha nchi na Dola mbili kama zilivyokuwa kabla ya 1964 na ndio watu wajadili mfumo wa muungano. Kwa kweli kama mwisho wa yote muundo huu wa muungano hautabadilika na kuleta mpya ambapo kila nchi (Tanganyika na Zanzibar) zitakuwa Dola mbili zenye haki sawa katika muungano huo mpya, kile kinachoitwa kero za muungano kitaendelea kuwepo na mwishowe itakuwa zogo lisilo na sababu. Bora kufanya marekebisho kwa njia za kiungwana na demokrasia kuliko kusubiri kusambaratika kama ilivyotokea katika baadhi ya nchi la Ulaya Mashariki. Alisema mchambuzi mmoja wa siasa za Zanzibar akitoa maoni yake.

MAONI YETU

Wanaopandikiza ugaidi Tanzania ndio magaidi


KAULI aliyotoa Makamu wa Kwanza wa Rais w a Z a n z i b a r, M a a l i m Seif Sharif Hamad hivi karibuni akitahadharisha kuwa huenda kuna watu wenye nia mbaya ambao wameamua kuyatumia matukio ya kuuawa na kujeruhiwa viongozi wa kidini, kujenga chuki si ya kupita bila kutiliwa mkazo. Katika kauli hiyo alipokuwa akihutubia katika haa ya Maulid ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), huko Mjini Kiuyu, Wilaya ya Wete, Kaskazini Pemba, Maalim Seif alisema kuwa inasikitisha kuona wapo baadhi ya viongozi wenye nia chafu dhidi ya Zanzibar wenye tabia ya kutoa kauli za kujenga chuki na fitna miongoni mwa Wazanzibari. Ni jambo la kusikitisha kuna watu wenye nia chafu dhidi ya Zanzibar, ambao wameamua kuyatumia matukio haya kujenga chuki miongoni mwa Wazanzibari wenyewe kwa wenyewe, alionya Maalim Seif. Makamu wa Kwanza wa Rais alisema kinachoonekana kuna ajenda imetayarishwa ya kutaka kulazimisha chuki za kidini Zanzibar, licha ya kuwa Zanzibar ina historia ya dahari ya watu kuvumiliana na kuishi kwa pamoja, pamoja na kuwepo watu wa imani tafauti. Akawataka wananchi wote wa Zanzibar hivi sasa wawe macho na ajenda zinazolengwa kuwavuruga na waendelee kuishi kwa mshikamano na umoja kama ambavyo wamekuwa wakiishi. Maalim Seif katika nasaha zake alisema kuwa wapo watu wanaolazimisha kuwepo ugaidi Zanzibar ili wapate sababu ya kuwadhuru Wazanzibari (Waislamu). Alisema inasikitisha kuona baadhi ya viongozi na magazeti ya Tanzania Bara yanachochea chuki za kidini na kusema kuwa Zanzibar kuna Ugaidi. Na kwamba hali hiyo inaonesha kuwa kuna

Kauli ya Maalim Seif izingatiwe

ajenda imetayarishwa kutaka kulazimisha chuki za kidini Zanzibar, kwa sababu huko Tanzania Bara kumetokea matukio mabaya zaidi, lakini hayajahusishwa na ugaidi. Alitoa mfano matukio ya kuuawa kwa Kamanda wa Polisi Mkoa, na kuchinjwa kwa Padri huko Geita, kuwa ni mabaya kabisa, lakini hakuna hata chombo cha habari kimoja kilichohusisha matukio hayo na Ugaidi. Nasema Zanzibar hakuna Ugaidi, hakuna ugomvi wa kidini. Yanayotokea yametusikitisha sana, ni matokeo ya uhalifu wa kupindukia, linaloweza kufanywa lifanywe kuwanasa wahalifu hawa, na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sharia, alisema Makamu wa Kwanza wa Rais. Aliwataka wananchi wote wa Zanzibar kwa wakati huu kuwa watulivu na wasitawaliwe na jazba na wala wasichokozane, pia wasikubali kuchokozeka. Sisi tungependa kutilia mkazo kwa kusema kuwa kwa hakika wanaopalilia agenda ya ugaidi ndio magaidi kwa sababu wanachofanya ni kujenga mazingira ya kuteswa na kuuliwa watu wasio na hatia. Uzoefu unaonyesha kuwa mahali popote duniani ambapo wachafuzi, mafatani na wasaliti walifanikiwa kupandikiza kitisho cha ugaidi, basi kilichofuatia ni mateso na mauwaji kwa wananchi wasio na hatia. Ni kutokana na uzoefu huo kama unavyodhihiri katika nchi za Afghanistan, Pakistan, Yemen, Kenya, Somali na huko Amerika ya Kusini katika miaka ya nyuma, tunadhani kuwa itakuwa jambo la busara kusisitiza nasaha hizi za Maalim Seif na kuwataka Watanzania wote kuwazomea na kuwakomesha wale wote wanaotaka kupandikiza chuki za kidini na kitisho cha ugaidi miongoni mwetu. Tukifanya hivyo itakuwa salama kwetu sote, lakini tukiwafumbia macho na kuwachekea, tujue itakuwa msiba kwetu sote pia.

Uongozi wa Masjid Tungi, Temeke jijini Dar es Salaam unawaarifu Waislamu wote kuwa, kutakuwa na Ibada maalum ya Itqaf msikitini hapo. Siku: Jumamosi ijayo tarehe 23/03/2013 msikitini hapo baada ya swala ya Isha.
WOTE MNAKARIBISHWA WABILLAH TAWFIIQ

Itqaf Masjid Tungi

Njama za kulitumbukiza Taifa katika machafuko zachuliwa


Na Mwandishi Wetu

Habari
kama hiyo kutolewa na Waziri Mkuu hadharani, lau angetokea jasusi yeyote akailipua hospitali hiyo na kuuwa raia wengi wasio na hatia, hivi nani ambaye asingeamini kuwa uovu huo umefanywa na Waislamu? Linasema na kuhoji tamko la Waislamu kwamba kwa nini serikali ipandikize chuki ya aina hiyo kwa raia wake? Na inafanya hivyo kwa masilahi ya nani? Mfano wa pili unaotolewa kuonyesha jinsi serikali inavyopandikiza chuki na kupalilia fitna na uhasama kati ya Waislamu n a Wa k r i s t o , n i p a l e ilipodai kuwa Waislamu

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 15 - 21, 2013

AN-NUUR

JUMUIYA na Taasisi za Kiislamu nchini, zimetoa tamko kuelezea na kutoa tahadhari juu ya kampeni zinazoendelea za kulitumbukiza Taifa katika machafuko ya kidini. Katika tamko hilo ambalo limewasilishwa rasmi kwa Waziri Mkuu, Serikali ya Jamhuri ya Tanzania imetuhumiwa kuhusika kuchochea chuki na kupandikiza farka na fitna miongoni mwa Waislamu na Wakristo jambo lililoelezwa kuwa ni la hatari. Jambo la hatari sana ambalo sasa linatudhuru, ni kampeni za serikali za kuwasingizia Waislamu mambo mazito ya kuhatarisha amani na utulivu nchini ili kuhalalisha dhana kuwa Waislamu ni watu hatari. Imesema sehemu ya tamko hilo na kutoa mfano wa uzushi uliowahi kutangazwa na aliyekuwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Frederick Sumaye. Ikaelezwa kuwa katika uzushi huo Sumaye alidai kuwa kuna magaidi wa Kiislamu waliokuwa wamefuzu mafunzo nje ya nchi na walikuwa wamerejea nchini na kwamba shabaha yao ya kwanza ilikuwa kulipua hospitali ya Muhimbili. Na kweli baada ya kauli hiyo ya Sumaye, Waislamu watatu wafanyakazi wa Muhimbili akiwemo Profesa Jahazi, bingwa wa Bio-Chemistry, wakatiwa mbaroni kwa tuhumza za kupanga kuilipua hospitali. Ta m k o h i l o l a Waislamu linasema kuwa japo watuhumiwa wote waliachiwa baada ya siku chache, lakini tayari sumu ya propaganda chafu ilikuwa imekwishapenyezwa. Kwa Waziri Mkuu kutangaza uzushi kama huo, ni dhahiri kuwa lengo lilikuwa ni kuwafanya wananchi wengine wawachukie Waislamu kwa kukusudia kufanya uovu wa kulipua hospitali. (Na) la kuzingatia hapa ni kwamba baada ya kauli

wakitumiwa na watu wa nje walikuwa wamepanga kulipua makanisa siku ya Jumapili tarehe 2 Septemba 2001. Hiyo ilikuwa ni baada ya maandamano ya Waislamu ya tarehe 24 Agosti 2001 Wa i s l a m u w a k i p i n g a kufungwa Hamisi Dibagula kwa kusema kuwa Yesu si Mungu. Ta m k o l i n a s e m a kuwa baada ya kauli hiyo ya serikali kuwa Waislamu wana mpango wa kulipua makanisa, askari walitawanywa makanisani kuwalinda Wakristo dhidi ya Waislamu wanaotaka kuwadhuru kwa mabomu.

Je, baada ya kauli hizo, akitokea jasusi yeyote akatega bomu na kuuwa watu kanisani, ni nani atakayeshutumiwa kwa mauwaji hayo kama si Waislamu? Tamko linahoji. Pamoja na shutuma hizo kwa serikali, vinashutumiwa pia baadhi ya vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikizua urongo dhidi ya Waislamu na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa. Umetajwa mfano wa yale madai kuwa Waislamu walikuwa wameandaa jeshi na silaha za kuulia Wakristo na kwamba alipokuwa Rais, Alhaj Ally Hassan Mwinyi alikuwa amewagawia

WA K O L O N I w a Kijerumani na wa Kiingereza waliamini kuwa Waislamu ni watu hatari sana, kidini na kisiasa. Hivyo waliweka mikakati kadhaa ya kuwadhibiti. Imani hiyo ya wakoloni ilitokana na msimamo madhubuti wa Waislamu wa kuwa tayari kwa udi na ambari kupambana na wakoloni hao ili nchi yetu iwe huru. Vema, mmetuhukumu tunyongwe nasi tumekubali. Tumekubali kwa sababu ni sisi wenyewe tulioendea maji ya dawa Ngarambe kwa hiari yetu; kwa sababu hatukuona haki ya kutawaliwa na nyinyi wahuni. Na kwa sasa kwa kuwa mmenipata, basi ninyongeni haraka kusudi jina langu libaki likikumbukwa kwamba nilikuwa mmoja niliyepigania nchi yangu (Selemani Mamba, Maji Maji hero). Kauli ya shujaa Suleiman Mamba aliyowaambia wakoloni wa kijerumani wakati wa kunyongwa kwake tuliyoinukuu hapo juu inaonesha msimamo huo ambao ni wa hatari kwa maslahi ya wakoloni. Ili kulinda maslahi yao, wakoloni wakaona njia rahisi ni kutugawa ili watutawale. Kwa kuwa waliosimama kidete

Kiini cha Tatizo


kupambana nao kisiasa walikuwa ni Waislamu, wakatumia dini kutugawa. Kwa bahati mbaya, dhana hii kuwa Waislamu ni watu hatari sana kidini na kisiasa imekumbatiwa na awamu zote za serikali ya Tanzania, bila kuzingatia kilichowafanya wakoloni wawachukie Waislamu. Na serikali za awamu zote zimekuwa zikihakikisha kuwa zinaweka mikakati ya kuwadhibiti raia hawa ambao ni hatari kwa usalama wa nchi. Itoshe tu kwa sasa kusema kuwa katika nchi yetu Wakristo wa madhehebu mbalimbali, Walutheri, Waanglikana, Wakatoliki, Wasabato, na wengineo wanayo haki na uhuru wa kuratibu mambo yao na kuchagua viongozi wao bila ya kuingiliwa na dola. Lakini kwa Waislamu s i v y o . Vy o m b o v y a Usalama lazima vihusike katika kuamua nani awe kiongozi mkuu wa watu hawa hatari! Kwa hiyo serikali imetugawa na inaendelea kutugawa baina ya raia wapenda heri na raia wapenda shari. Tunajua kuwa wapo viongozi kadhaa ambao ni Wakristo waliowahi kuishauri serikali (wakati wa uongozi wa Mheshimiwa Mkapa) kuwa sasa Waislamu nao waachwe huru kuchagua viongozi wao kama raia wengine. Tunawashukuru kwa moyo wao huo wa kizalendo, japo serikali bado inaamini njia nzuri ya kuimarisha umoja wetu ni kuwadhibiti na kuwadhoosha Waislamu. Na kwa bahati mbaya, dhana hiyo pia imekuwa ikiungwa mkono na baadhi ya viongozi wa makanisa. Jambo la hatari sana ambalo sasa linatudhuru, ni kampeni za serikali za kuwasingizia Waislamu mambo mazito ya kuhatarisha amani na utulivu nchini ili kuhalalisha dhana kuwa Waislamu ni watu hatari. Tunataja hapa mifano michache tu kwani orodha ya uzushi ni ndefu. Januari 2001, Waziri Mkuu wa wakati huo, Mheshimiwa Frederick Sumaye aliita waandishi wa habari kuwataarifu kuwa serikali inazo taarifa kuwa magaidi waliopata mafunzo nje ya nchi wamerejea nchini na kwamba wamepanga kuilipua Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, na kwamba vyombo vya dola vitawatia nguvuni. Na kweli mara baada ya kauli hiyo Waislamu watatu wafanyakazi wa Muhimbili akiwemo Profesa Jahazi, bingwa wa Bio-Chemistry, wakatiwa mbaroni kwa tuhuma za kupanga kuilipua hospitali. Wote waliachiwa baada ya siku chache, lakini tayari sumu ya propaganda hiyo chafu ilikuwa imekwishapenyezwa. Kwa

Waislamu majambia ya kuwachinjia Wakristo wote nchini. Ukiacha matukio hayo ya miaka ya nyuma, tamko linagusia pia jinsi matukio ya hivi karibuni ya sakata la kuchinja Wakristo na lile la kuuliwa Padri Zanzibar, yanavyovishwa gamba la ugaidi na watuhumiwa wakiwa ni Waislamu. Na katika jitihada hizo za kuwachafua Waislamu, inatajwa kuwa ndio sababu serikali imekimbilia kuwaita FBI bila kujali kuwa kufanya hivyo ni kujidhalilisha. Tamko linasema kuwa mabeberu wenye kiu na rasilimali zetu, wanatumia mwanya huo kujipenyeza kikachero na kijeshi huku sisi tukidhani na kufurahia kuwa tunashirikiana na taifa kubwa kumbe tumejitia wenyewe kitanzi cha ukibaraka. Hakuwezi kuwa na ushirikiano wa kweli baina ya nchi yenye nguvu na nchi dhaifu. Katika ushirikiano wa nchi kama hizo ukweli ni kwamba nchi dhaifu inakuwa ni kibaraka tu wa nchi yenye nguvu. Tamko la Waislamu lilisema hayo likinukuu sehemu ya hotuba mashuhuri sana ya kuwaaga wananchi wa Marekani iliyotolewa na Rais George Washington 19 Septemba, 1796. Ta m k o l i k a s i s i t i z a kuwa kwa waliosoma na kulielewa Azimio la Arusha, yote aliyosema G e o r g e Wa s h i n g t o n , aliyasema Mwalimu Nyerere katika jitihada zake za kulinusuru taifa letu. (Lakini) leo kwa papara yetu ya kujipendekeza kwa Wamarekani imekia hadi kuwakaribisha ndani ya kambi zetu za jeshi kana kwamba na wao ni Watanzani wenzetu! Ni kutokana na ukweli huo alioeleza aliyekuwa Rais wa Marekani G e o r g e Wa s h i n g t o n , tamko limeonyesha jinsi hao washirika wetu wanavyotumia udhaifu wetu mpaka kukamata vijana wetu na kuwapachika ugaidi huku serikali yetu ikishindwa kuwatetea. Baada ya serikali yetu Inaendelea Uk. 4

Njama za kulitumbukiza Taifa katika machafuko zachuliwa


Inatoka Uk. 3
k u f u n g u a mlango wa kuwasingizia Waislamu mambo yanayohatarisha amani na usalama wa nchi, Wamarekani wameutumia udhaifu wetu huo kutuparaganya zaidi na kwa kasi kubwa. Hapa ukatajwa mfano wa kukamatwa Ghailani akidaiwa kuwa ndiye aliyelipua ubalozi wa Marekani mwaka 1998 na serikali yetu ikashindwa kumtetea. Prof. Haroub Othman, (Mwenyezi Mungu amrehemu) alifanya kila aliloweza kumtetea mtoto huyu lakini hakufanikiwa. Allah atamlipa kwa jitihada zake na amjaaliye kijana huyu aliyetolewa kafara subra na hatma njema. Lakini kuthibitisha kauli ya Washington kuwa sisi tunakuwa vibaraka tu katika ushirika wetu na mataifa makubwa, tamko la Waislamu linasema kuwa wakati viongozi wetu walishindwa kutoa kauli ya kumtetea Ahmed Khalifan Ghailani, viongozi wa Uingereza waliwaombea askari wao wawili, Brett Richard na Nigel David ambao Novemba 10, 2004 walimbaka kwa zamu msichana wa Kitanzania Konjesta Mwikaye katika fukwe za Hoteli ya Silversand na kisha kumwua. Hatukuweza kuwakisha mahakamani wabakaji hao waliombaka Mtanzania na kumuuwa! Katika kumalizia tamko lao, Jumuiya na Taasisi za Kiislamu zimetoa ujumbe unaosema kuwa kama walivyopigania uhuru kuondoa ubaguzi na ukandamizaji wa kikoloni, watasimama kidete kupinga mpango huu wa makusudi wa kuwagawa Watanzania na kuleta machafuko ya kidini kwa manufaa ya mabeberu. Hatukupigania uhuru ili kukitokea tatizo lolote miongoni mwetu tuwaombe watu wa nchi nyingine kuja kulitatua! Waislamu tunajua kuwa kila anayepingana na mabeberu anakuwa gaidina kwa uzoefu wetu wa miaka hamsini wa namna serikali yetu inavyowatizama Waislamu, tunataraji kuwa mwaka huu utakuwa wa mateso makubwa kwa Waislamu na hasa kwa viongozi wetu kwa kubambikiziwa kesi zisizokuwa na kichwa wala miguu, kudhalilishwa na kunyimwa dhamana kama mbo ya kuwaadhibu. Hata hivyo tamko likawataka Waislamu wasivunjike moyo wala kukata tamaa na kurejea nyuma bali washikamane na msimamo wa Mzee wao Inatoka Uk. 3 Waziri Mkuu kutangaza uzushi huo, ni dhahiri kuwa lengo lilikuwa ni kuwafanya wananchi wengine wawachukie Waislamu kwa kukusudia kufanya uovu wa kulipua hospitali. Lakini la kuzingatia hapa ni kwamba baada ya kauli kama hiyo kutolewa na Waziri Mkuu hadharani, lau angetokea jasusi yeyote akailipua hospitali hiyo na kuuwa raia wengi wasio na hatia, hivi nani ambaye asingeamini kuwa uovu huo umefanywa na Waislamu? Na kwanini serikali ipandikize chuki ya aina hiyo kwa raia wake? Ni kwa masilahi ya nani? Tarehe 24 Agosti 2001, Waislamu waliandamana Dar es Salaam kupinga kufungwa kwa Dibagula kwa sababu ya kusema Yesu si Mungu. Serikali ilitoa kauli mbili kuhusiana na maandamano hayo. Ya kwanza ni kwamba watu wote walioandamana ni mamluki waliopewa pesa (kiasi cha shilingi elfu moja hadi elfu mbili na mia tano) kutoka nje ya nchi ili waandamane. Kauli hii ililenga kuwafanya Waislamu waonekane kuwa ni vibaraka wa mabwana wa nje. Na kauli ya pili ilisema kuwa Waislamu walikuwa wamepanga kuyalipua makanisa siku ya Jumapili ya tarehe 2 Septemba 2001. Na kwamba serikali imeweka utaratibu wa kuyalinda. Na kweli maaskari wakatawanywa makanisani kuwalinda Wakristo dhidi ya Waislamu wanaotaka kuwadhuru kwa mabomu! Je, baada ya kauli hizo akitokea jasusi yeyote akatega bomu na kuuwa watu kanisani, ni nani atakayeshutumiwa kwa mauaji hayo kama si Waislamu? Kazi hiyo ya kuchochea chuki dhidi ya Waislamu imekuwa pia ikifanywa Shujaa Selemani Mamba. Selemani Mamba ambaye alikataa kutawaliwa na wakoloni wahuni akapambana nao na alipokamatwa na kufikishwa katika kitanzi cha kunyongewa hakuomba msamaha bali kwa uzalendo na ushujaa mkubwa alisema maneno yafuatayo: Vema mmetuhukumu tunyongwe nasi tumekubali. Tumekubali kwa sababu ni sisi wenyewe tulioendea maji ya dawa Ngarambe kwa hiari yetu; kwa sababu hatukuona haki ya kutawaliwa na nyinyi wahuni. Na kwa sasa kwa kuwa mmenipata, basi ninyongeni haraka kusudi jina langu libaki likikumbukwa kwamba nilikuwa mmoja niliyepigania nchi yangu. Ni kwa kufuata

Habari

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 15 - 21, 2013

AN-NUUR

msimamo huo wa Sheikh Selemani Mamba, tamko la Waislamu likasema kuwa Waislamu wataendelea kupinga mpango huu wa makusudi wa kuwagawa Watanzania kwa msingi ya kidini. Na kwamba kwa kufanya hivyo watakuwa wametoa mchango wao katika kudumisha amani, utulivu na mshikamano katika nchi hii. watu wa nchi nyingine kuja kulitatua! Tumesikitishwa sana na mfano mbaya unaooneshwa na serikali yetu ya kuwakimbilia watu wasio na uchungu wowote na nchi yetu kuja kutusaidia kutatua mambo yetu. Na tunashangazwa na tabia ya wananchi wenzetu wanaodhani kuwa matatizo yetu makubwa au madogo ya kiutawala yanaweza kumalizwa kwa kuyapeleka kwenye Baraza la Wawakilishi wa Marekani. Haya ni matatizo yetu na ni lazima tufanye kila njia kuyatatua sisi wenyewe. Waislamu tunajua kuwa kila anayepingana na mabeberu anakuwa gaidi na sasa nchi zetu zimeanza kupewa drone za kuulia raia wao. Sisi tunaapa hatutakwenda kuwalalamikia Marekani au watu wengine matatizo na misukosuko inayotukumba kama raia. Tutafanya kila tunaloweza upatikane ufumbuzi unaotokana na sisi wenyewe kama raia wa nchi hii. Kwa uzoefu wetu wa miaka hamsini wa namna serikali yetu inavyowatazama Waislamu, tunatarajia kuwa mwaka huu utakuwa wa mateso makubwa kwa Waislamu na hasa kwa viongozi wetu kwa kubambikiziwa kesi zisizokuwa na kichwa wala miguu, kudhalilishwa na kunyimwa dhamana kama mbo ya kuwaadhibu watu hatari kidini na kisiasa. Hilo likitokea tutalazimika kutafakari hatima yetu baada ya miaka hamsini ya kuvumilia. (Sehemu ya Tamko la Waislamu lililowasilishwa kwa Waziri Mkuu kuhusu Kampeni Zinazoendelea za Kulitumbukiza Taifa Katika Machafuko ya Kidini.)

na baadhi ya vyombo vya habari bila ya kuchukuliwa hatua yoyote. Kwa mfano jarida maarufu la Family Mirror toleo la pili la Mei 1993, lilitangaza kwa maandishi ya kukoza kuwa vijana 500 wa Kiislamu wamejiandikisha katika Jeshi la Kiislamu ili kuwauwa Wakristo, na kwamba serikali imekamata bandarini makontena ya silaha za Jeshi la Waislamu. Waziri wa Mambo ya Ndani wa wakati huo alikiri kuwa alikuwa nazo taarifa hizo. Katika toleo lililotangulia ilidaiwa kuwa Waislamu walikuwa wamepanga kuuchoma moto ubalozi wa Vatican nchini na kumwua Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki la Dar es Salaam, Muadhama Kadinali Polycarp Pengo. Jarida jingine la Tanzania Analysis la 22 Julai, 1995 lilidai kuwa Rais Mwinyi amewagawia Waislamu majambia ya kuwachinjia Wakristo wote nchini, kwa sababu Waislamu hawataki Mkristo awe Rais. Baada ya serikali yetu kufungua mlango wa kuwasingizia Waislamu mambo yanayohatarisha amani na usalama wa nchi, Wamarekani wameutumia udhaifu wetu huo kutuparaganya zaidi na kwa kiasi kikubwa kwa kushirikiana na serikali yetu wenyewe. Serikali ya Marekani nayo ikautumia mwanya huo kudau kuwa mtoto Ghailani kuwa ndiye aliyeulipua Ubalozi wa Marekani mwaka 1998 na ikamkamata na kumpeleka Guantanamo kwa ridhaa ya serikali yetu. Prof. Haroub Othman, (Mwenyezi Mungu amrehemu) alifanya kila aliloweza kumtetea mtoto huyu lakini hakufanikiwa. Allah atamlipa kwa jitihada zake na amjaalie kijana huyu

Kiini cha Tatizo

aliyetolewa kafara subira na hatima njema. Hatujui kama viongozi wetu wamewahi kuwaomba viongozi wa Marekani kumwachia kijana huyo, kama walivyoomba Waingereza na kufanikiwa kuwanusuru raia wao. Lakini tunajua kuwa viongozi wa Uingereza waliwaombea askari wao wawili, Brett Richard na Nigel David ambao 10 Novemba 2004 walimbaka kwa zamu binti wa Kitanzania Konjesta Mwikaye katika fukwe za Hoteli ya Silversands na kisha kumwua. Waislamu tulipigania uhuru wa nchi yetu ili sisi wananchi wa nchi hii tuwe na haki na uhuru wa kujiamulia mambo yetu sisi wenyewe. Hatukupigania uhuru ili tuwe vibaraka wa watu wengine. Tulipigania uhuru kwa kushirikiana na Watanzania wenzetu wa makabila na dini mbalimbali ili tuishi kwa amani na udugu kama raia huru na sawa katika nchi yetu. Hatukupigania uhuru ili baada ya uhuru utaratibu ule ule wa kuwagawa raia kwa misingi ya dini au ukabila uendelee. Kama tulivyosimama kidete kuupinga ubaguzi miongoni mwetu wakati wa kupigania uhuru na tukafanikiwa, tutaendelea kuupinga mpango huu wa makusudi wa kutugawa ili kuwe na machafuko nchini kwa manufaa ya wakoloni mamboleo, na Insha-Allah tutafaulu. Waislamu tulipigania uhuru kwa kujua kuwa maana ya kujitawala ni pamoja na kuwa na uwezo wa kuyakabili na kuyatatua matatizo yetu sisi wenyewe. Hatukupigania uhuru ili kukitokea tatizo lolote miongoni mwetu tuwaombe

5
TEHRAN RAIS Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na mwenzake wa Pakistan Asif Ali Zardari, Jumatatu ya wiki hii wamezindua rasmi awamu ya kwanza ya ujenzi wa bomba la kusarisha gesi utakaogharimu mabilioni ya dola. Marais hao wawili wamehudhuria hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika mpakani mwa nchi hizo mbili na kuhudhuriwa pia na Waziri wa Mafuta wa Iran Rostam Qasemi na Waziri wa Mambo ya Nje Ali Akbar Salehi. Bomba hilo litasafirisha gesi asilia kutoka Iran kuelekea nchini Pakistan na viongozi wa nchi hizi mbili, wamesema kuwa mradi huo utaimarisha amani, usalama na maendeleo ya Iran, Pakistan pamoja na mataifa mengine ya eneo hilo. Bomba hilo la gesi litakalokuwa na urefu wa kilometa 1,600, litapunguza uhaba wa nishati nchini Pakistan kwa kusafirisha kila siku cubic meters za gesi asilia milioni 21.5 (8.7 billion cubic meters kwa mwaka) kutoka Iran hadi Pakistan. Hata hivyo baada ya kuzinduliwa rasmi awamu ya kwanza ya ujenzi wa bomba hilo la kusarisha gesi kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hadi Pakistan, serikali ya Marekani imeingilia kati mradi huo na kutoa vitisho vya kuiwekea vikwazo Pakistan kwa vile imeshirikiana na Iran kwenye mradi huo. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani Victoria Nuland, amesema kuwa Washington imeingiwa na wasiwasi juu ya ujenzi wa bomba hilo la kusarisha gesi kutoka Iran hadi Pakistan. Licha kuwepo vikwazo kadhaa, mradi wa bomba la gesi kutoka Iran hadi Pakistan utatekelezwa ipasavyo, amebainisha Waziri wa Habari na Utangazaji wa Pakistan, Firdous Ashiq Awan, katika mkutano wa hadhara ulioitishwa katika wilaya ya Marla mjini Lahore mwishoni mwa wiki. Wa s h i n g t o n b a a d a ya kusikia mpango huo imekuwa ikifanya jitihada za kuishinikiza Pakistani kufuta mradi huo licha ya kwamba Pakistan imekuwa ikihangaika kukidhi mahitaji yake ya nishati, ambayo yameongezeka kwa kasi siku

Habari za Kimataifa

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 15 - 21, 2013

AN-NUUR

Iran na Pakistan zazindua mradi wa bomba la gesi


za hivi karibuni. Mwezi uliopita, jarida la International Herald Tribune, liliripoti kuwa Marekani imekuwa ikijaribu kuishawishi Islamabad kujitoa katika mradi huo wa gesi kutoka Iran na kuahidi kuwa ingetoa kwa Pakistan mkataba wa kuipatia nchi hiyo gesi ya bei rahisi zaidi. Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran alisema licha ya mashinikizo makubwa yanayotolewa na Marekani juu ya uzinduzi wa mradi huo, nchi za Magharibi hazina haki ya kuzuia mradi huo utakaogharimu kiasi cha dola bilioni 7.5. Imekadiriwa kuwa ujenzi wa bomba hilo lenye urefu wa kilomita 1,600 utachukua muda wa miaka miwili.

Bunge Ethiopia kujadili mgao wa maji mto Nile


ADDIS ABABA Serikali ya Ethiopia imekusudia kujadili makubaliano ya Entebbe kwenye bunge la nchi hiyo juu ya kugawanywa kwa uadilifu maji ya mto Nile. Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Ethiopia imeeleza kuwa, makubaliano ya Entebbe ya kugawana maji ya mto Nile yanapingwa vikali na nchi za Sudan na Misri, ambazo zimekuwa zikitumia kikamilifu maji yam to huo katika kilimo cha umwagiliaji. Makubaliano ya Entebbe yanataka kupunguza hisa ya nchi za Misri na Sudan na kuziongezea hisa nchi nyingine zinazochangia maji ya Mto Nile kwa njia ya usawa. Tanzania, Kenya, Uganda, Ethiopia, Rwanda, na Eritrea zilitangaza kwamba makubaliano ya mwaka 1929, hayakuwa ya kiadilifu hivyo ziliamua kutia saini makubaliano ya Entebbe ya mwezi Mei 2010 kwa lengo la kugawana kwa usawa matumizi ya maji ya Mto Nile. Ukiacha matumizi mengine, hivi karibuni Tanzania ilishakamilisha mradi mkubwa wa maji ya bomba kutoka ziwa Victoria, maji ambayo yamesambazwa katika mabomba mkoani Shinyanga. Taarifa ya wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia imeeleza kuwa, mpango wa kujadili mgawo wa maji ya Nile ulisimamishwa kwa sababu ya zoezi la uchaguzi

RAIS Mahmoud Ahmednejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (kulia) na Rais wa Pakistan Asif Ali Zardari, wakisaini mkataba wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Iran kwenda Pakistan mwanzoni mwa wiki hii.

Karzai abaini Marekani inazungumza kwa siri na Taliban


KABUL Rais Hamid Karzai wa Afghanistan, ameendelea kuishambulia Marekani na kuikosoa vikali akisema kuwa, Washington imekuwa ikifanya mazungumzo na Taliban kila siku huko nchini Qatar. Rais Karzai ametoa matamshi hayo makali dhidi ya Marekani sambamba na safari ya Chuck Hagel, Waziri wa Ulinzi wa Marekani nchini Afghanistan, hali inayoonesha kuwepo hitilafu baina ya Washington na Kabul. Karzai amesisitiza kuwa, mashambulizi yanayofanywa na kundi la wanamgambo wa Taliban nchini Afghanistan,

wa Rais na Bunge nchini Misri. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, nayo tayari imeshatia saini makubaliano hayo na nchi ya Sudan Kusini pia imetangaza kuwa itayasaini hivi karibuni. Nchi 11 zinazochangia maji ya Mto Nile ni Uganda, Kenya, Tanzania, Rwanda, Misri, Sudan, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Eritrea na Burundi.

yanatoa huduma kwa Marekani hasa kwa kutilia maanani kwamba, Taliban na Washington wamekuwa wakifanya mazungumzo bila ya serikali ya Kabul kuwa na taarifa ya mazungumzo hayo. Ta y a r i s e r i k a l i y a Marekani imetoa taarifa na kukanusha vikali tuhuma za kuweko uhusiano kati yao na kundi la Taliban. Wakati huo huo Rais Karzai amevipiga marufuku vikosi vya kigeni vinavyoongozwa na Marekani kuingia katika maeneo ya Vyuo Vikuu vya nchi hiyo na kuwatia mbaroni wanachuo. Amesisitiza kuwa, hatua hizo zinakinzana na mamlaka ya kujitawala Afghanistan.

Habari/Matangazo

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 15 - 21, 2013

AN-NUUR

Mahakama kupitia pingamizi dhamana ya Imam Hamza


Na Shaban Rajab
na upande wa Jamhuri dhidi ya mshtakiwa Imam Hamza Omari. Ust. Hamza, alikamatwa hivi karibuni na kuwekwa mahabusu ambapo baadae alifikishwa Mahakamani na kufunguliwa kesi ya uchochezi na kuvunja amani.

MAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Nyamagana, imesema itapitia hoja zilizowasilishwa Mahakamani hapo na Wakili wa upande wa utetezi, kupinga zuio la dhamana lililowekwa

Nchimbi ajiuzulu - Maalim Seif


Inatoka Uk. 1

wa hadhara wa Chama hicho uliofanyika katika viwanja vya Mbagala Zakhiem Maalim Seif ambae pia ni Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema Dkt. Nchimbi analazimika kujiuzulu kutokana na wizara yake kushindwa kusimamia ulinzi wa Wananchi na mali zao. Amesema, jukumu la ulinzi wa raia na mali zao ni jukumu la serikali hivyo kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi ambayo ndio yenye jukumu la kusimamia ulinzi imeshindwa kutekeleza wajibu huo. Amesema matukio ya kihalifu yanayo endelea kujitokeza nchini iwemo kushambuliwa pamoja na kuuwawa kwa viongozi na raia wasio na hatia kunatokana na serikali kushindwa kuimarisha ulinzi kwa raia wake. Kumekuwa na matukio mbalimbali ya kihalifu yanayotokea hapa nchini ambayo Waziri Nchimbi na wizara yake wameshindwa kuyatafutia ufumbuzi hadi leo, hivyo hana budi kujiuzulu kwani ameshindwa kutekeleza wajibu wake kama waziri anaehusika usalama wa raia na mali zao, alisema Maalim Seif. Akizungumzia matukio ya kushambuliwa kwa viongozi wa dini yaliotokea Zanzibar hivi karibuni kuwa hayapaswi kuhusishwa na itikadi za kidini kutokana na utamaduni wa muda mrefu wa kuvumiliana kidini uliojengeka kwa Wananchi wa Zanzibar. Aidha Maalim seif amechukizwa na kauli ya Dkt. Nchimbi kulihusisha tukio la kuuwawa kwa Padre Evarist Mushi na matukio ya kigaidi na kusema tukio hilo si la kigaidi kwani Zanzibar hakuna ugaidi. Huyu ana lengo gani na Zanzibar hata kutangaza ugaidi kwa Zanzibar kwani Zanzibar hakuna ugaidi na wala hautatokea kamwe. Alisema

Maalim Seif. Akizungumzia mwenendo wa Serikali ya Umoja wa kitaifa ya Zanzibar amesema Serikali kwa kiasi kikubwa imefanikiwa kuleta maendeleo kwa Wananchi wake ikiwa ni pamoja na kuinua juhudi za wakulima katika ukuzaji wa kilimo chenye tija kwa wakulima na taifa kwa ujumla. Amesema kuwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefanikiwa kuinua zao la karafuu kwa kupandisha bei ya karafuu kutoka shilingi elfu tatu kwa kilo hadi elfu kumi bei ambayo inampa mkulima asilimia thamanini ya bei ya soko la dunia. Pia imefanikiwa kukuza kilimo cha mpunga kwa kuwapatia wakulima wa kilimo hicho kwa kuwapatia wataalamu wa kutosha pamoja na kushusha gharama za pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea na dawa za kuulia wadudu ili kuwawezesha wakulima kulima kilimo chenye tija na kuondokana na utegemezi wa chakula kutoka nje. Aidha amesema kuwa serikali imefanikiwa kuongeza kiwango cha mishahara ya wafanyakazi hadi asilimia ishirini na tano kwa wafanyakazi wa kima cha chini ili kuweza kujikimu kimaisha. Nae Naibu katibu mkuu wa CUF Tanzania Bara Mh. Julius Mtatiro amewataka wanachama hicho kujitokeza katika kuwania nafasi za ujumbe wa mabaraza ya katiba ili kuweza kupata katiba bora itakayo endana na mahitaji ya Wananchi. Amesema kuwa kutokushiriki katika mabaraza ya katiba ya wilaya kutawapa nafasi watu wasiotaka maslahi mazuri kwa wananchi kuingia katika mabaraza hayo jambo litakalo sababisha kukosekana kwa katiba bora.

Sheikh Jabir Katura (kulia) akisisitiza jambo katika moja ya mikutano yake hivi karibuni.
Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Bw. Mwambapa, alisema Mahakani hapo Jumatano wiki hii kwamba, ufafanuzi juu ya madai ya Wakili wa upande wa utetezi yaliyowasilishwa Mahakani hapo ya kutaka kuondolewa zuio la dhamana kwa mshtakiwa, utatolewa Machi 27, 2013, kesi hiyo itakapotajwa tena. Sheikh Jabir Katura, mmoja wa viongozi wa Kiislamu wanaofuatilia kesi hiyo, alisema Waislamu wengi wa Kanda ya Ziwa wanaona kama kesi aliyofunguliwa Imam Hamza, imelenga kumshikisha adabu kutokana na na kutoa msimamo ambao ulimkera Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuhusu sakata la kuchinja Mkoani Geita. Alisema kuwa wakati wa sakata la kuchinja kule Geita, Imam Hamza alikuwa kiongozi wa upande wa Waislamu katika hatua za kutafuta suluhu juu ya mzozo huo. Alisema katika mazungumzo ya kupata suluhu yaliyohusisha pande mbili kati ya Waislamu na Wakristo chini ya Waziri Mkuu Pinda, upande wa Waislamu wakiongozwa na Imam Hamza, ulitaka kwanza watuhumiwa Waislamu ambao wameswekwa ndani kufuatia kadhia iliyotokea, nao kuachiwa kama ambavyo wenzao Wakristo walivyoachiwa, ili mazungumzo hayo yawe ya suluhu ya haki na ya kweli. Sheikh Katura, alisema pengine msimamo huo wa Imam Hamza na Waislamu ulimkera Waziri Mkuu na sasa inaonekana kuwa kuna haja ya kumshikisha adabu. Alisema pamoja na kwamba moja ya sababu za kumkamata na kumfungulia kesi Imam Hamza, ni madai ya kusikika akifanya uchochezi kupitia mahubiri yake katika CD, lakini alisema katika CD hizo, hakuna ambapo Imam Hamza, kachochea zaidi ya kueleza hali ya yale yaliyojiri kule Geita na kufafanua jinsi Waislamu wanavyopuuzwa kila wanapojitetea. Ndege wote watalia lakini akilia Bundi ni uchuro, ni mojo ya CD inayotajwa kusikika Imam Hamza akihubiri, ambayo inadaiwa kuwa kuna uchochezi ndani yake.

Ahlul Daawa Hajj And Travel Agency

SHAMBA LINAUZWA
SHAMBA LA EKARI 14 LINAUZWA KWA HARAKA LIPO CHAMAZI-DOVYA DAR ES SALAAM BEI NI MAELEWANO KWA MAWASILIANO: PIGA SIMU: 0759 450425 0784 463207 0754 479783 WAHI MAPEMA BAHATI NI YAKO

Inawatangazia Waislamu wote Kuwa Imeandaa Safari ya Hijja Mwaka 2013 Sawa na Mwaka 1434 Hijria kwa Dola US$ 3550 tu. Umra kwa Mwezi wa Ramadhani itakuwa ni Dola US$ 1995 Fomu zinapatikana katika osi zifuatazo:1. Osi ya Ahlul Daawa Dar es salaam Mtaa wa Dosi na Mkadini Nyumba Namba 26 Mkabala na Showroom ya Magari Tel 0713 730 444, au 0773 804101 au 0785 930444 na 0773 930444. 2. Osi ya Ahlul Daawa Zanzibar Rahaleo Tel 0777 484982 au 0777 413 987. 3. Abubakar Maulana wa Markaz Kiwalani Dar es salaam 0784 453838 4. Abdallah Salehe Mazrui ( HOKO) Dar es salaam 0715 724 444 5. Salim Is-haq Dar es salaam 0754 286010 au 0774 786101 6. Dukani kwa Abdala Hadh Mazrui wete pemba 0777 482 665 7. Dukani kwa Mohamed Hadh Mazrui Mkoani Pemba 0777 456911 8. Sheikh Daudi khamis sheha 0777 679692 9. Maalim Seif Humoud Hamed Kijichi Zanzibar 0777 417736 Wahi kulipia. Osi ya Ahlul Daawa Dar es salaam 0713 730 444 au 0773 804101 au 0785 930444. Osi ya Ahlul Daawa Zanzibar Rahaleo 0777 484982 au 0777 413 987. Maalim Seif Humoud Hamed Kijichi Zanzibar 0777 417736 Sheikh Salim Mohamed Salim 0774 412974 au Kupitia ACCOUNT NAMBA 048101000030 NBC Tanbih: Atakae maliza Taratibu zote kuanzia sasa Mpaka 15 July 2013 atapata Punguzo la asilimia 16% atalipia $ Dola 2982 tu. Atakae maliza Taratibu zote kuanzia Tarehe 16-july Hadi Tarehe 15 Augost 2013 atapata Punguzo la Asilimia sita 6% atalipia Dola $3337 tu. Kutakuwa na umra ya utangulizi kabla ya Umra ya Hijja kwa atakae maliza kufanya hivyo. Atakae maliza taratibu zote mwanzo ndie atakae shughulikiwa mwanzo. Ukilipia kwa njia ya Account kwanza piga simu 0774 412975. Kumbuka Kikundi cha Ahlul Daawa Kwa Bei nafuu kuliko wote na Huduma bora Kuliko wengi. Nyote mnakaribishwa

7
Na Bakari Mwakangwale WAISLAMU wametakiwa kukataa propaganda zinazopandikizwa na watu wasioitakia mema nchi hii, kuwa kuna uhasama baina ya Waislamu na Wakristo. Wi t o h u o u m e t o l e w a na Amir wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T), Sheikh Mussa Yusuph Kundecha akiongea na viongozi wa Jumuiya na Taasisi mbalimbali za Kiislamu katika semina maalum iliyofanyika katika Hoteli ya Lamada, Ilala Jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita. Amir Kundecha amesema Waislamu siku zote kilio chao kipo kwa Serikali na si Wakristo na msingi mkubwa wa malalamiko yao ni kutotendewa haki kama watu wengine katika jamii. Amir Kundecha aliwataka viongozi hao kufikisha ujumbe huo kwa Waislamu ili kuepuka na kukataa propaganda zinazolazimishwa kuwa kuna uhasama baina ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu katika jamii. Ningelikuombeni mkaondoe dhana hiyo katika jamii kwa maana maalumu na maana mahususi, kataeni kuonyesha kuna mvutano na wasiokuwa Waislamu, sisi tuna tatizo na Serikali yetu kupuuza madai yetu. Alisema Amir Kundecha. Alisema, kimsingi katika nchi hii hakuna mgogoro kati ya Waislamu na Wakristo kwani wanaishi pamoja kwa kushirikiana katika mambo mbalimbali ya kijamii. Amir Kundecha alionyesha wasiwasi wake kwa Serikali kwamba inaweza kuwa chanzo cha kuvunjika kwa amani kutokana na kupuuza na kutoshughulikia madai ya msingi ya Waislamu. Alianisha madai hayo kuwa ni pamoja na tatizo la Baraza la Mitihani, kuwepo kwa Mahakama ya Kadhi, suala la Tanzania kujiunga na OIC na kuwepo kwa MoU kati ya Serikali na Makanisa. Akifafanua hayo alisema, umma wa Kiislamu nchini una tatizo dhidi ya Serikali yao kwa kuzuiwa kuwa na mahusiano ya kitaasisi na Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya OIC. Ukitazama hoja zinazotolewa kuzuiwa Waislamu kuwa na mahusiano na Taasisi hiyo pamoja na Serikali kujiridhisha kuwa hakuna Tatizo Tanzania kujiunga utakuta ni hoja zisizo na msingi kabisa.

Habari/Matangazo

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 15 - 21, 2013


haki Waislamu, jambo ambalo alidai wanatamkama kwa mapana kuwa Waislamu, mgomvi wao ni Serikali yao na si watu wa imani nyingine. Alisema, wakati fulani kipindi cha uchaguzi, Wakatoliki walitoa ilani ya uchaguzi wakatoa na waraka, Mh. Kingunge (Ngombalemwiru), alisema haiwezekani chombo cha dini kikatoa ilani, na kwamba ilani hutolewa na Chama Cha siasa. Alisema, baada ya muda, Shura ya Maimam nayo ilitoa Muongozo wa Waislamu Katika Uchaguzi, lakini alidai kilichofuata baada ya muongozo huo ni kauli ya Rais Kikwete akisema kwamba yanayofanywa na viongozi wa dini sio sahihi, wakati hakuweza kusema lolote juu ya Ilani ya Maaskofu.. Alisema, kauli hiyo ya Rais Kikwete, iliambatana na ahadi ya kuwaita viongozi wa Dini ili kukaa pamoja kuzungumzia masuala hayo kwa ujumla kutokana na mwenendo uliopo kutokuwa mzuri. Amir Kundecha, alisema ilifika siku viongozi wa dini waliitwa, kwa Wakristo yaliitwa madhehebu yao yote ya Kikristo lakini kwa Waislamu Serikali iliwaita Bakwata tu, na kuziacha Jumuiya zingine za Kiislamu. Sisi tunasema, Serikali kwa maana nyingi sana imekuwa si sikivu kwa wasiokuwa Waislamu, kwa muda mrefu, hivi kweli Waislamu nchini wamekuwa wabaya kiasi hicho.? Alisema na kuhoji, Amir Kundecha.

AN-NUUR

Kundecha atoa mwongozo kwa viongozi wa Waislamu

Asema tatizo ni serikali sio Wakristo

Amir wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T), Sheikh Mussa Yusuph Kundecha akiongea na viongozi wa Jumuiya na Taasisi mbalimbali za Kiislamu katika semina maalum iliyofanyika katika Hoteli ya Lamada, Ilala Jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita.

Alisema, akiwa katika moja ya mkutano wa viongiozi wa dini, alipata kusimama kiongozi mmoja akidai kuwa OIC, ni taasisi ya kidini na ni hatari kabisa kwa umoja wa kitaifa na amani ya nchi. Alisema, baada ya kutolewa kwa hoja hiyo, alimtaka mtoa hoja aonyeshe kipengele cha Katiba ya OIC, ambacho ana wasiwasi nacho huku akihoji uhalali wa kuwepo nchini Ubalozi wa Makao Makuu ya Kanisa Katoliki Vatcan, ili hali hiyo si nchi. Akifafanua hali ya mvutano kama huo, Amir Kundecha, alisema kinachotaka kujengwa miongoni mwa wanajamii ni kuonesha kuwa upo mvutano na tatizo baina ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu nchini. Alisema, mfano wa hivi sasa ni kuwa Waislamu wameilalamikia Serikali kuhusu Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), lakini wanapuuzwa. Nyinyi kwa umri wenu, mmepata hata siku moja kusikia Waislamu wakilalamika juu ya jambo hilo? Nasema tunapuuzwa kwa sababu Serikali imekataa kwa makusudi kuona uzito wa tunacho kilalamikia na siku zote imepuuza jambo hilo. Alisema Amir Kundecha.

Alisema, kadhia hiyo n a N E C TA , Wa i s l a m u waliipeleka kama tatizo mahala husika, lakini alidai kwa kuwa kuna dhana ya kupuuza jambo likisemwa na Waislamu, hata kama lina ukweli, badala yake walipewa majibu yasiyofaa. Amir Kundecha, alisema CHADEMA, walipeleka hoja yao binafsi katika kikao cha Bunge lililopita kuhusu N E C TA , n a u k i a n g a l i a yale yaliyolalamikiwa ni sawa na yale malalamiko ya Waislamu yaliyopuuzwa, kilichobadilika ni mahali palipoandikwa Waislamu pameandikwa CHADEMA. Amir Kundecha, alidai kwamba tatizo lingine la Waislamu na Serikali yao ni kugawanywa (na Serikali) kwa nguvu miongoni mwa Waislamu. Akitolea mfano juu ya madai hayo, Amir Kundecha alisema, wakati Waislamu wanahangaika na masuala ya Mahakama ya Kadhi, Waislamu walikubaliana kuunda timu ya pamoja, kutoka Jumuiya na Taasisi mbalimbali za Kiislamu. Alisema, timu hiyo iliundwa ikiwa na washiriki 25, kwa bahati mbaya alidai katika kikao kilichoitishwa na Serikali na kufanyika Mkoani

Dodoma, mgeni rasmi akiwa ni Makamu wa Rais, Dk. Ghalib Bilali, Serikali iliamua kuwagawa Waislamu. Serikali kwa makusudi ikaamua kutugawa Waislamu, ikijua kabisa wanachokifanya kitaleta mtafaruku mkubwa huku nje. Timu ina uwakilishi wa Taasisi 25, lakini Serikali ikaiita Taasisi ya Bakwata tu, na kuwapa fulsa ya kuchagua Makadhi nchi nzima. Aliainisha Amir Kundecha. Alisema, ipo mifano mingi juu ya Serikali kuwapindishia

MASJID MUZDALIFA - MBEZI KWA YUSUFU


KUPATA AKAUNTI NA. 011206008550 NBC BENKI Tunapenda kuwafahamisha kuwa kwa muda mrefu tumekuwa tukiomba michango ya ujenzi wa msikiti kupitia namba za simu. Kwa sasa tunaomba michango yote itumwe kupitia Account Namba 011206008550 NBC. Jina la Account MASJID MUZDALIFA - MBEZI KWA YUSUFU Hata hivyo kama kutakuwa na mahitajio ya kupata maelezo/ufafanuzi kuhusiana na Ujenzi wa Masjid Muzdalifa tumia nambari za simu za Mwenyekiti nazo ni 0713 673 216 na 0754 952 008. pia tunawafahamisha kuwa namba za simu zifuatazo zisitumike tena kwa jambo lolote lile linalo husu MASJID MUZDALIFA - MBEZI KWA YUSUFU (0717 649413 na 0657 531367)

TANGAZO

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 15 - 21, 2013

AN-NUUR

9
Na Ahmed Omar Khamis

Makala

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 15 - 21, 2013


Uchunguzi unaendelea lakini zipo dalili nyingi za kuyahusisha matukio haya na njama za kuijengea Zanzibar picha ya UGAIDI mbele ya jamii ya kimataifa. Wauwaji wanaonekana ni watu waliotumwa na mtandao maalum ili kutimiza agenda yao hii. Hapa hatuwezi kusema ni akina nani na nani lakini kwa mujibu wa kile kinachoendelea Zanzibar itoshe kuamini kuwa ni mipango maalum ya kuiteka nyara sauti ya umoja wa Wazanzibari ambayo bila ya woga kutoka kwa Wazanzibari wenyewe, viongozi wao wakuu na taasisi kadhaa za serikali yao kwamba wanataka mabadiliko kutoka katika mfumo wa sasa wa Muungano kwenda katika mfumo mpya wa muungano utakaoipatia Zanzibar mamlaka yake kamili kitaifa na kimataifa. Kwa kuwa kuna taasisi za dini ya Kiislamu zilibeba agenda hii kwa ari na hamasa ya hali ya juu, isije wakatafutiwa sababu. Wazanzibari wameishi na ndugu zao wa kikristo kwa karne nyingi sana huku utamaduni wa dini ya Kiislamu ukiwa ni wenye kutawala Zanzibar. Katika kipindi chote hicho Wakristo wamekuwa wakiwaheshimu Waislamu kwa kila hali na hivyo Waislamu hawakuiona haja wala sababu ya kuwabugudhi Wakristo. Hata Askofu Shayo akizungumzia kadhia hii alipata kutamka mimi nimeishi Zanzibar kwa miaka 20 sasa, sikupata kuona haya. Haya ni mapya sana, haya ni mambo maalum katika agenda maalum. Haya si mambo ya kidini wala ugaidi bali ni vitimbi vinavyopangwa kiufundi vya kuhakikisha Wazanzibari hawakii lengo lao. Hebu tujiulize ni kwa nini mauwaji ya mtu mmoja ambayo si mauwaji ya kawaida kwa Zanzibar kwa ghaa sana yanaitwa mauwaji ya ugaidi? Kuyaita mauwaji haya ugaidi ni kwa sababu aliyeuwawa ni Padri na hivyo iaminike kauliwa na Waislamu? Kule Bara watu kadhaa wamekua wakiuliwa katika kadhia kadha wa kadhaa hatujaona viongozi wa Bara kuyaita matukio hayo kuwa ni ugaidi. Ni kwa nini Zanzibar?

AN-NUUR

SIKU ya tarehe 3 Machi 1996, enzi zile Wazanzibari walipogawanywa na kutiwa chuki baina yao, ilidaiwa na serikali kuwa masa watatu wa usalama waliokuwa kwenye doria huko katika kijiji cha Shengejuu, kisiwani Pemba, walipigwa na kuporwa silaha na wanakijiji. Kwa sura ya kawaida ya uaskari, ni vigumu kuaminika kwamba askari watatu wakiwa na silaha mikononi waporwe silaha zao wote watatu na wapigwe bila ya wao hata kujeruhi mtu yeyote au kujeruhiwa wao wenyewe. Muda sio mrefu, siku ya pili yake tu, kijiji hicho kilivamiwa na kiasi cha askari wapatao 300 wa kikosi cha FFU na jeshi la wananchi (JWTZ) waliokuwa wako kamili kivita. Unyama, mateso na vitendo vya kihuni walifanyiwa wananchi wa kijiji cha Shengejuu waliokuwa hawana hatia yoyote. Baadhi ya wanakijiji walipigwa hadi kuzirai, wengine waliibiwa mali zao kama vile kuku na mbuzi, maduka yaliporwa, wanawake walibakwa na watu wapatao 80 waliwekwa ndani. Kati ya watu hao 80, watu 30 waliachiliwa huru na waliobaki waliendelea kusota ndani kwa kipindi kirefu sana. Kiongozi mmoja mkuu wa SMZ wakati ule, aliwahi kufanya mkutano na waandishi wa habari kuelezea hali ya mtafaruku inayoendelea katika kijiji hicho cha Shengejuu, na hapa namnukuu moja ya kauli zake aliyoitoa kupitia kikao hichoSasa tunataka kuwafanya watu wajue kama serikali ipo. Katika enzi hizo wafuasi wa CUF walikuwa wakisingiziwa kuhusika na hujuma mbalimbali kama vile kuchomwa moto madarasa ya skuli, kupaka vinyesi kwenye kuta za skuli, kutia vinyesi kwenye visima n.k. Hizi bila shaka zilikuwa ni mwendelezo wa propaganda chafu za kisiasa zilizokuwa na lengo la kujenga picha ya uongo na kuhalalisha hujuma dhidi ya watu wasio na hatia. Waliokuwa wakifanya haya ni watu waliofundishwa vyema propaganda na siasa chafu za uchochezi. Wa k i t e k e l e z a v i t e n d o hivyo huku wakilindwa na

Wanaoleta agenda ya ugaidi hawaitakii mema Zanzibar


Wazanzibari ili wasifikie lengo lao kwa kupitia mbinu hizo zilizotumika huko nyuma za kuandaa uongo na kuupandikiza katika jamii. Bila shaka wakitarajia uongo huo utaweza kuzaa chuki na tna miongoni mwa makundi mbali mbali yaliyoshika kamba ya pamoja kutafuta maslahi ya nchi yao na hivyo kuiwachia kamba hiyo na kusambaratika. Chuki ambazo zinajengwa hapa ni baina ya CUF na CCM kwa vitendo kama vile vya kuzichoma moto maskani za CCM na kuwasingizia CUF. Kuwatesa wafuasi wa CUF kwa visingizio mbali mbali kama vile kupambana na UAMSHO ili wafuasi wa CUF wakasirike na serikali na chao kwa kuwa CUF ni sehemu ya serikali hiyo. Wafuasi wa CUF wakikasirika dhidi ya chama chao itakuwa tayari umefanikisha kulisambaratisha kundi kubwa linashikilia engine ya kudai mabadiliko na hivyo kuliwacha kundi hilo likiwa dhaifu. Inabidi hapa ichukuliwe tahadhari kubwa sana isije ikawa kuna watu wameunda makundi maalum ya uharamia, kuratibu na kutekeleza vurugu, kuchoma moto maskani za CCM, kuchoma moto makanisa na kushambulia kama ilivyokuwa Shengejuu. Hivi karibuni kumeibuka vitendo vya kuwashambulia kwa risasi na kuwauwa viongozi wa dini ya Kikristo kwa kutumia bunduki. Usiku wa tarehe 25/12/2012 Padri wa kanisa Katoliki mjini Zanzibar Ambrose Mkenda amepigwa risasi na watu wasiofahamika akiwa anawasili nyumbani kwake ambapo watu hao waliokuwa wamepanda chombo aina ya vespa wamepiga risasi akiwa getini ndani ya gari kuingia nyumbani kwake maeneo ya Tomondo visiwani humo. Siku ya tarehe 16/02/2013 Padri Everist Mushi wa kanisa katoliki huko visiwani Zanzibar, alipigwa risasi kichwani na watu wasiojulikana na kufariki papo hapo wakati akielekea kwenye ibada katika kanisa katoliki Mtoni Zanzibar.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Dr. Emmanuel Nchimbi


askari polisi. Madhumuni ni kuendelea kupata fursa ya kuwatesa raia wasio na hatia kwa kuwapiga, kuwaweka gerezani na k u w a u a . Wa l i o k u w a wakifanya vitendo hivyo hawakujua kwamba walikuwa wanaonekana na wanafuatiliwa nyendo zao na hivyo kufahamika wao na waliowatuma. Katika hatua nyengine Siku moja wanakijiji hao hao wa Shengejuu katika nyakati za usiku wakiwa katika doria yao ya kuangalia ni nani hasa wanaofanya vitendo hivi, walifanikiwa kuwafumania watu hao. Wakiwa wanaendelea na doria, wanakijiji hao waliiona gari yenye namba za usajili ZNZ-12633 ikisimama kiasi cha umbali wa mita 100 hivi kutoka ilipokuwepo skuli ya Shengejuu (Soma kitabu cha Dr. Bakari, 2001 kiitwacho The democratization process in Zanzibar). Ghaa watu watatu waliokuwa na galoni la mafuta ya petroli walishuka kutoka katika gari hiyo. Haraka haraka wakamwaga mafuta na kuchoma baadhi ya majengo ya shule hiyo na kukimbia. Wanakijiji wakajitokeza ghafla na kuwazingira wahalifu hao. Lakini mara milio ya risasi hewani ikasikika na watu hao kuingia ndani ya gari yao na kukimbia. Wanakijiji waliwahi kuuzima moto huo. Ilithibitika kuwa watu waliofanya vitendo hivyo ni wanamaskani waliokuwa wakilindwa na wanausalama ndio waliokuwa wakitekeleza vitendo na hujuma zile kwa nia ya kukizulia chama cha CUF na kuwatesa raia bila ya hatia yoyote kwa maslahi binafsi ya kisiasa. Maadui wa Zanzibar baada kuliona wimbi la kudai mabadiliko katika mfumo na muundo wa Muungano wa Tanzania linaongezeka, wameamua kujipanga upya na kujaribu kuwasambaratisha

10

Makala/Tangazo

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 15 - 21, 2013

AN-NUUR

Wanawake wa Kipalestina chini ya utawala wa Israel


MACHI 8 mwaka huu ulimwengu uliadhimisha siku ya wanawake. Katika maeneo ya Palestina yaliyovamiwa na Israel, wananchi husheherekea siku hiyo ya wanawake kwa kukumbuka madhila wanayopata. Wa k a t i ulimwengu ukiwa unaadhimisha siku ya wanawake, hali ni tofauti kwa wanawake wa Kipalestina wanaokandamizwa na Israel. We n g i w a o w a n a t e s e k a kutokana na mashambulizi ya Gaza ya Novemba 2012. Kutokana na mashambulizi hayo ya kijeshi Wapalestina 171 waliuawa, 102 kati yao wakiwa raia wa kawaida pamoja na wanawake 14. Aidha raia wa Kipalestina 625 walijeruhiwa vibaya , kati yao wakiwa wanawake 93. Haya ni matokeo ya mashambulizi ya Israel kwa kutumia silaha nzito za maangamizi. Huu ni uhalifu wa sheria ya kimataifa ambayo imepiga marufuku mauaji ya raia wakati wa vita. Licha ya sheria hiyo, majeshi ya Israel yanashambulia bila ya kuangalia nani raia na nani mpiganaji. Pia hayaangalii majengo yanayoshambulia ni ya kijeshi au ya kiraia. Matokeo yake ni kuwa wanawake na watoto wanashambuliwa na kuuawa na majeshi hayo. Huu ni uharamia wa kivita na uhalifu wa sheria ya kimataifa Kwa mfano, Novemba 18, 2012, majeshi ya Israel yalishambulia kwa makombora na kuteketeza nyumba ya familia ya al-Dalu, katika maeneo ya Gaza. Matokeo yake watu 10 wa familia hiyo walikufa, wakiwemo wanawake wanne na watoto watano. Katika mashambulizi kama hayo ya Novemba 19, 2012, mtoto mmoja na wanawake wawili kutoka familia ya Abu Zour, waliuliwa kwa makombora ya majeshi ya Israel. Aidha wanawake wa Palestina pia wanateseka kisaikolojia kutokana na kupoteza wanafamilia katika mashambulizi ya Israel. Maelfu ya wanawake wanaathirika kwa vile wamegeuzwa wakimbizi katika nchi yao. Miaka ya hivi karibuni wanawake wengi wameathirika kutokana na sera ya Israel huko Gaza. Kwa mfano, wanawake wengi wanazuiliwa kuwatembelea watoto wao au waume zao walio katika magereza ya Israel. Wakati huo huo wanazuiliwa kuwatembelea ndugu zao kwa vile Gaza imezingirwa na majeshi ya Israel. Gaza ni sawa na jela kubwa duniani. Utawala wa Israel umekuwa pia unawakandamiza raia wa Palestina kwa kuwanyima mahitaji yao ya lazima kama dawa na matibabu. Wakati huohuo wazayuni hao wamewawekea vikwazo Wapalestina ili wasiweze kutembeleana baina ya wale wanaoishi maeneo ya Gaza na Ukingo wa Magharibi. Kituo cha Palestina cha Haki za Binadamu kimeitaka jumuia ya kimataifa kutekeleza wajibu wake kwa kuchukua hatua za kuzuia mateso haya yanayowasibu raia wa Palestina, hususan wanawake ambao ndio wanateseka zaidi. Kituo hicho pia kimeitaka mamlaka inayosimamia utekelezaji wa Makubaliano ya Nne ya Geneva, kuilazimisha Israel iheshimu makubaliano hayo kwa kuhakikisha kuwa wanawake na raia wote wa Palestina wanalindwa ipasavyo. Aidha, asasi ya kutetea haki za wafungwa (Addameer) imetangaza kufunguliwa kwa Bibi Abla Saadat, ambaye alikamatwa akiwa anasafiri kuelekea mkutano wa kimataifa tarehe 21 Januari 2003. Baada ya kukamatwa alipewa kifungo cha miezi minne bila ya kufunguliwa mashtaka. Akafunguliwa tarehe 7 Machi 2003. Alipokamatwa hakupewa sababu ya kufungwa na alipoachiliwa kabla ya muda pia hakupewa sababu. Addameer ilitoa risala siku ya wanawake iliyosema wananchi wanakumbuka wanawake 65 wa Kipalestina walio katika jela ya Ramleh nchini Israel. Kati yao 10 ni wasichana wenye umri chini ya miaka 18. Wawili walifungwa wakiwa chini ya miaka 15. Wasichana hawa wamefungwa katika hali isiyokubalika kimataifa na kinyume cha mkataba wa kimataifa wa haki za watoto. Mkataba huu unasema watoto chini ya miaka 18 hairuhusiwi kuwekwa katika hali inayowadhalilisha na kuwatesa. Pia hairuhusiwi kuwafunga bila ya sababu maalum inayoeleweka kisheria. Wanawake sita wamefungwa bila ya kukishwa mahakamani, yaani bila ya mashtaka au kesi. Mwanamke mmoja, Bi. Tahani Al Titi, amefungwa katika hali hii tangu Juni 13, 2002. Mtindo huu wa kuwafunga wanawake bila ya mashtaka umekuwa ukiongezeka sana hivi karibuni. Kati ya wafungwa hawa wanawake, kuna kina mama wakiwa na watoto wadogo. Mmoja ni Bibi Mervat Taha, aliyekamatwa tarehe Juni 13, 2002 wakati akiwa na mimba. Akajifungua akiwa jela anatumikia adhabu ya miezi 20. Pia kuna mtindo wa kuwafunga wanawake wa Kipalestina ili kuwashinikiza wanafamilia wao wanaotafutwa na Israel au walio kifungoni. Mfano mmoja ni Bibi Abla Saadaat, mke wa katibu mkuu wa chama cha PFLP Bw. Ahmad Saaadat, pamoja na Bibi Asma

Wanawake wa Kipalestina wakidhalilishwa na majeshi ya Israel


Abu Al Hayjah, mke wa Jamal Abu Al Hayjah, aliyefungwa katika jela ya Israel. Huyu Bibi Al Hayjah ana magonjwa kadha. Ameonekana anaugua saratani ya ubongo na amefanyiwa upasuaji mara mbili. Alikuwa akingojea kupasuliwa mara ya tatu ndipo alipokamatwa na akatupwa jela. Na hali ya maisha katika jela ni ya kinyama. Wafungwa wa kike huwekwa katika sehemu mbili. Walio katika sehemu moja hawaruhusiwi kuonana na wenzio walio katika sehemu ya pili. Pia wafunga hao hupewa adhabu za kijumla, yaani wanaohusika na wasiohusika. Adhabu moja ni marufuku ya kutembelewa na ndugu na jamaa. Adhabu nyingine ni kuwekwa katika chumba cha giza kisicho na dirisha kwa muda mrefu. Wengine huzuiwa kupata chakula au vitu kutoka nje. Wakati huo huo vyumba vya wafungwa wa kike husachiwa mara kwa mara na vitu vyao hupokonywa au kuharibiwa. Nguo zao huchafuliwa na vyakula hutupwa. Wafungwa hao pia hunyimwa matumizi ya umeme au maji ya moto kama njia ya kuwaadhibu. Chakula wanachopewa huwa hakitoshi, hakiliki na hakikidhi mahitaji ya mwili, matokeo yake ni kuwa wafungwa hao hupata matatizo ya kiafya. Ndio maana afya ya wafungwa wa kike ni dhaifu sana. Wanapougua magonjwa hawapatiwi matibabu. Mara nyingi wafungwa wa Kipalestina hubaguliwa kwa vile hawapatiwi huduma wanazopatiwa wafungwa wa Kiisrael. Wanapohitaji matibabu huwa wanacheleweshwa. Badala ya kukimbizwa hospitali hupewa vidonge vya kutuliza maumivu bila ya kujali magonjwa yanayowasumbua. Wafungwa wa kike wa Kipalestina wanaolalamika huadhibiwa. Kwa mfano, mnamo Julai 2002 waliamua kugoma kula. Matokeo yake askari wa jela waliwatupia mabomu ya machozi katika vyumba vyao vidogo. Wengi wao walijeruhiwa. Baada ya hapo wafungwa wa kike wanne wakahamishiwa jela nyingine na wakafungiwa katika vyumba vya giza. Kwa vile wafungwa wa kike wananyimwa haki ya kutembelewa na familia zao kwa muda unaozidi mwaka mmoja, matokeo yake wanakosa nguo au vitu vya matumizi ya kawaida vinavyoletwa na ndugu zao. Zaidi ya mwaka mmoja sasa familia zao kutoka Ukingo wa Magharibi wamekuwa wakikataliwa vibali vya kuwatembelea wafungwa katika gereza ya Ramleh. Hii ni kinyume na Makubaliano ya Nne ya Geneva. Mawakili wanaojaribu kuwatembelea wafungwa wa kike, nao mara nyingi

husumbuliwa na kudhalilishwa na maofisa wa magereza. Wanalazimishwa kusubiri kwa muda mrefu, hadi saa nne, kabla ya wafungwa kuletwa kwao. Matokeo yake ni kuwa mawakili hao hushindwa kukutana na wafungwa wote waliokusudia kuwaona kwa sababu muda wao humalizika kwa haraka. Kwa mfano, Februari 4, 2003, wakili wa Addameer, Bw. Mahmoud Hassan, alilazimika kusubiri kwa saa tatu katika jela ya Neveh Terzah kabla ya mfungwa kuletwa. Hakuna sababu yoyote iliyotolewa kwa wakili huyo kuwekwa ndani ya gereza akisubiri kwa muda wote huo. H i v i n d i v y o wanavyodhalilishwa wafungwa wa kike katika magereza ya Israel. Katika muda wa miaka 43 iliyopita inakisiwa kuwa wanawake wa Kipalestina takriban 10,000 wamekamatwa na kufungwa chini ya amri ya wavamizi wa Kiisraeli. Wafungwa wa kike kwa kawaida huwa wanafungwa katika jela za Hasharon na Damon. Jela hizi ziko nje ya maeneo ya Palestina yaliyovamiwa mwaka 1967. Huu ni uhalifu wa kifungu cha 76 cha Makubaliano ya Geneva, ambacho kinasema dola inayovamia nchi nyingine hairuhusiwi kuwafunga raia wa nchi hiyo nje ya nchi yao. Imeandaliwa na Kituo c ha Habari cha Palestina (Tanzania) P.O Box 20307, 612 UN Road Upanga West, Dar es Salaam Tel: 2152813, 2150643 Fax: 2153257 Email: pict@pal-tz.org Website: www. pal-tz.org

VIWANJA VILIVYOPIMWA KONGOWE KIBAHA TOWNSHIP REGISTERED PLAN No. 70995 BLOCK H
PLOT HATUA ENEO MRABA GHARAMA TSH

H1 H2 H3 H4 H5 H6 H7 H8 H9 H10 H11

50 x 29 32 x 32 50 x 30 37 x 30 50 X 45 33 x 37 60 x 45 50 x 40 67 x 50 70 x 45 90 x 50

1341 Sqm 1136 Sqm 1470 Sqm 1115 Sqm 2259 Sqm 1566 Sqm 2423 Sqm 1984 Sqm 3564 Sqm 2842 Sqm 3780 Sqm

4,023,000/= 3408000/= 4410000/= 3345000/= 6750000/= 4695000/= 7269000/= 5952000/= 10692000/= 8526000/= 11340000/=

Vipo Barabara ya Kongowe-Soga Kilomita moja toka barabara ya Morogoro. Simu No.0755 090 754/0715 090 754.

11
Na Dr. Noordin Jella
ZANZIBAR kwa miaka mingi kimekuwa ni kisiwa cha amani ya kweli hata ukaangusha kiroba cha mamilioni ya pesa atakayeziokota atazipeleka Zanzibar TV kwa mtangazaji au msikitini kwa Imamu ili akatangazie umma mwenye mzigo wake aje achukue. Lakini baada ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi hapa nchini mwaka 1992 kisiwa hiki cha amani kimejikuta mara kwa mara kikitwishwa lawama za kigaidi zinazotolewa na wanasiasa uchwara waliochoka kukiri kwa kigezo maalumu cha kuibaka demokrasia na ustaarabu visiwani humo. Ta t i z o l a k u b a k w a k w a demokrasia visiwani Zanzibar ni tatizo sugu na la muda mrefu lakini kabla sijathibitisha hilo hapo baadae, ningeomba tuangalie kwa makini na upana maana ya ugaidi. Kwanza kabisa kabla hatujaanza kuliangalia suala lenyewe kwa kirefu, ni vizuri tuyajibu maswali machache muhimu yafuatayo: Ugaidi maana yake nini? Nani anaweza kuwa gaidi? Je, kuna aina ngapi za ugaidi? Je, Nchimbi ana uzoefu au uhusiano gani na ugaidi au magaidi? Je, gaidi anaweza kuwa mtu binafsi au hata serikali inaweza kuwa ya kigaidi? Haya ni maswala muhimu sana ambayo kila mmoja wetu anatakiwa atafute majibu yake ili tuweze kuhalalisha msemo wa Nchimbi au kuukanusha: Gaidi ni neno la kigeni ambalo limefanywa kutafasiriwa kwenye lugha ya Kiswahili lakini neno lenyewe linatokana na neno la Kiingereza la Terrorist. Sasa kulingana na tafasiri ya neno hili kutoka kwenye kamusi ya Kiingereza ya Oxford ni kwamba gaidi ni mtu ambaye anatumia vitendo vya vurugu na huku vikiambatana na vitisho vyenye madhumuni ya kushinda au kudhibiti aidha serikali au jamii. Kulingana na tafasiri hii, mtu au serikali inaweza kuwa gaidi. Aina za ugadi zinaweza kuwa nyingi inategemea na mtu au serikali imeamua kutumia mbinu zipi? Kulingana na tafasiri ya ugaidi nilivyoielezea hapo juu, Waziri Nchimbi kama mwanasisa (Mbunge) inawezekana kabisa tena mara nyingi tu katika harakati zake za kuwa mbunge aidha alishawahi kuwa gaidi au alishawahi kuwasadia magaidi hasa ukizingatia kwamba uchaguzi wa viongozi wa umma hapa nchini si huru na wala si wa haki! Tumeshaona kwamba mtu au kikundi cha watu kinaweza kuwa cha kigaidi, pia serikali inaweza kuwa ya kigaidi au taasisi za serikali na vyombo vya umma kama vile kitengo cha usalama wa taifa, jeshi la polisi, tume ya uchaguzi, takukuru nakadhalika. Pamoja na tafasiri ya neno ugaidi kama lilivyoelezewa kwenye kamusi ya Oxford, lakini uelewa wa neno hili kwa

Makala

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 15 - 21, 2013

AN-NUUR

Mr. Nchimbi: Ikiwa Bara Uhalifu, Zanzibar ugaidi!


Amefanya kweli Maalim Seif kuhoji Wanasiasa uchwara watawaponza

MAALIM Seif Sharif Hamad


nchi za magharibi ni tofauti na uelewa tunaouelewa sisi hapa nyumbani; na ndiyo maana Maalim Seif Shariff Hamad amekuwa akipinga kauli za Nchimbi kwa vile anajua ni jinsi gani ambavyo neno ugaidi limetumika kuibaka demokrasia ya Zanzibar kwa zaidi ya miaka 20 sasa. Je, padre hawezi kupigwa risasi na jambazi aliyekuwa na nia ya kumuibia sadaka zilizotolewa na waumini? Ni kwa nini Nchimbi asitumie kwanza neno jambazi badala ya gaidi? Angelikuwa IGP Said Mwema ndiye aliyekuwa ameulizwa kuhusu tukio hilo la kuuwawa kwa padre, naamini asingelisema ni ugaidi bali angelisema ni jambazi, kwa vile IGP ni polisi na ni mtaalamu wa vitendo vya uhalifu, lakini kwa vile Nchimbi ni mwanasiasa, amerukia neno ugaidi kwa vile lina maslahi makubwa ya kisiasa hasa ukilinganisha na jinsi ambavyo nchi za Magharibi zinavyolitafasiri neno hilo, na jinsi ambavyo wafuasi wa CUF walivyoweza kudhulumiwa kwa miaka 20 mfulululizo. Tukio hili lingelikuwa limetokea kule Amerika wasingelisema ugaidi, bali wangelidai aidha kwamba ni mwizi, mdunguaji au mtu amefyatua risasi kwa makusudi au bahati mbaya na kumuua padri. Tangu tuanze mfumo wa vyama vingi vya siasa hapa nchini mwaka 1992 uchaguzi wa Zanzibar haujawahi kuwa wa huru na haki hata siku moja (hayo ni maoni yangu) na kulingana na dhuluma waliofanyiwa raia wa Zanzibar, wamekuwa wakijitahidi kutafuta haki yao ya kimsingi na ya kikatiba, lakini

DR. Emmanuel Nchimbi


serikali ya muungano imekuwa ikikihusisha chama cha CUF na ugaidi na kuweza kuzishawishi nchi za Magharibi ziidhinishe na kuhalalisha dhuluma hiyo kwa kigezo cha kigaidi! Yule anayeanzisha dhuluma siyo gaidi bali yule anayedai haki yake ndiye gaidi! Ajabu gani hii! Na serikali ya Marekani imekuwa mustari wa mbele sana katika kuhakikisha kwamba Zanzibar inatawaliwa kimabavu kwa kigezo cha kigaidi! Mwaka 2000 uchaguzi wa Zanzibar ulimwaga damu ya Watanzania baada ya wafuasi wa CUF kukataa matokeo na kufanya maandamano matokeo yake walikufa watu 75 wakiwemo raia na polisi, na wakati mauwaji hayo yanatokea Rais Mkapa alikuwa Uswizi kwenye mkutano, na alipojulishwa kuhusu mauaji hayo alirudi nyumbani na alipofika akaanza kushangaa kwamba kwa nini wamuambie ni watu 75 wakati ni watu 17 tu waliokufa? Yeye kwake watu 17 ni wachache sana, lakini mkirie mtu mwenye watoto wawili tu, (sijui Mkapa ana wangapi). Sasa kama wangelikuwamo kwenye hilo kundi la watu 17 si anabaki na watoto sifuri? Sisi tumejibu maswali mengi kuhusiana na ugaidi hivyo ni wakati muafaka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani Dr. Emanuel Nchimbi kujibu maswali yafuatayo ili tuweze kutatua matatizo yanayoikabili jamii ya visiwani Zanzibar. Je, kitendo cha Dr. Stephen Ulimboka kutekwa nyara na kuteswa kisha kutupwa porini kama mbwa, ni ugaidi au ni utawala bora? Je, kitendo cha Dr.

IGP Said Mwema


Harris Mwakiyembe kuwekewa sumu na kuumuka mwili mzima siyo ugaidi? Je, kitendo cha polisi wakiwa katika sare za kazi kuwakamata wafanyibiashara wa madini wa Ifakara kuwanyanganya madini na pesa zao na kisha kuwauwa ni ugaidi au ni utawala bora? Je, kitendo cha kuchakachua matokeo ya chaguzi mbalimbali hapa nchini siyo vitendo vya kigaidi? Je, chama cha siasa kinachojenga mazingira ya vitisho kwa raia wake ili kishinde uchaguzi siyo ugaidi? Je, Jeshi la wananchi wa Tanzania linalojenga mazingira ya vitisho kwa wananchi wake hasa wakati wa uchaguzi mkuu kwa makusudi ya kukisaidia chama cha CCM kishinde uchaguzi huo siyo ugaidi? Je, vitendo vya uporwaji wa ardhi hapa nchini na watu wanaoitwa wawekezaji wakishirikiana na viongozi mbalimbali wa serikali siyo ugaidi? Je, vitendo vya kuugandamiza umma kwa kutumia mtutu wa bunduki na kungangania mikataba ya dhahabu ya kinyanganyi siyo ugaidi? Je, kujenga mazingira ya vitisho ili wananchi wakubaliane na vile serikali inavyotaka siyo ugaidi? Nadhani kwa leo maswali haya yanamtosha Nchimbi, na akiyajibu viruzi kwa heru kubwa ataweza kubadilisha msemo wake juu ya kuwawa padri. Wanasiasa wamekuwa watu wepesi sana kukurupuka na kutumia maneno mazito ambayo wakati mwingine yaweza kuliingiza taifa katika wingu zito la woga kwa maslahi ya kisiasa tu! Vitendo vinavyotokea Zanzibar pia hutokea hata huku Tanganyika lakini cha ajabu

matukio kama hayo yakitokea huku Bara wanasiasa wanatumia maneno mengine kuyatafasiri, isipokuwa yakitokea kule kisiwani Zanzibar basi tayari lazima matukio hayo yahusishwe na ugaidi kwa vile neno Ugaidi lina mashiko mazuri na matamu sana kwa serikali ya CCM. Serikali ya CCM wameweza kufaidi matunda ya Zanzibar kwa kutumia neno rahisi sana kulitamka la Ugaidi kwa zaidi ya miaka 20 sasa! Hivyo kwa mtu mchambuzi mzuri wa mambo ya siasa hapa nchini hasa siasa za kule Zanzibar hatashangaa hata kibaka akihusishwa na vitendo vya ugaidi kwa vile neno hilo linaleta kula! Wazanzibar na Watanganyika wote kwa ujumla wapo katika kipindi muhimu sana cha kutafuta katiba mpya itakayoweza kuyaongoza mataifa haya mawili kwa miaka mingine mingi ijayo. Wananchi wa Zanzibar wamekuwa wawazi kwa kueleza bayana kwamba hawaridhiki na mfumo wa muungano uliopo hivi sasa na kwa maana hiyo walikuwa wanataka mfumo huo ubadilishwe; pia kwa upande wa Tanganyika nao wanataka serikali yao iliyouwawa tangu mwaka 1964 ifufuliwe na kuwe na muungano wa kweli unaozijumuisha nchi hizi mbili kiukweki na kikamilifu. Kwa vile tunajua kwamba siasa ni mchezo mchafu; nina wasiwasi neno ugaidi lisije kutumiwa kama kigezo cha kubaka democrasia ya kupitisha katiba inayoandaliwa hivi sasa, hasa ukizingatia kwamba wananchi wa Zanzibar walio wengi hawautaki muungano kama ulivyo hivi sasa! Kuuwawa kwa padri kumeifanya serikali ihusishe vyombo vya nje vya ulinzi vya Marekani kama vile FBI. Kwa Wamarekani neno Ugaidi wao ni biashara kubwa sana ambayo inawaingizia mabilioni ya dola kila mwaka (terrorism is a big business), hivyo nchi yoyote duniani bila ya kujali kwamba ipo kona gani ya dunia, madhali imesema kuna ugaidi basi Wamarekani wapo tayari wakati wowote wapeleke askari wao wakafe huko potelea mbali, lakini wahakikishe kwamba wanafanya biashara kubwa kutokana na neno hilo la ugaidi! Sisi tunapolitumia neno ugaidi, hatufikirii suala la biashara, hapana, bali sisi tunasema hivyo ili kuibaka demokrasia tuendelee kuwepo madarakani na huku tukiwa tumeshawawezesha wale wakosoaji wakubwa duniani wa ubakwaji wa demokrasia kufanya biashara inayotokana na neno ugaidi ambalo tayari tumewatonya nalo! Mwisho kabisa napenda nimshauri Dr. Nchimbi kama mwanasiasa mchanga anayetaka kujivunia ujana wake wa siasa hapo baadae atakapokuwa mzee, kwamba aachane na siasa za kizazi cha wazee wa CCM ambazo zimepitwa na wakati; siasa za wazee hao hazina mvuto tena Tanzania.

12
Sheikh huyu Sheikh gani
Simtaki Sheikh huyu, sifa zake siyo njema, Yafaa kumuepuka, Sheikh huyu sio mwema, Yazidi yake jeuri, wala hana sifa njema, Sheikh huyu Sheikh gani, aso faida na umma. Yu pamoja na kar, hajui cheo neema, Hugawa Waislamu, kwa zao dhamira njema, Ghururi za ulimwengu, Sheikh zimemwandama, Sheikh huyu Sheikh gani, aso faida na umma. Kitabu chakojolewa, mbio mbio kulalama, Kakojolea mtoto, asitupiwe lawama, Hivi unakithamini, kitabu chake Rabana, Sheikh huyu Sheikh gani, aso faida na umma. Majumba hata magari, sio vitu vya maana, Ipo siku siku moja, vyote vitakusakama, Muogope Mola wako, adhabu zake ni pana, Sheikh huyu Sheikh gani, aso faida na umma. Bora wangu ufukara, kesho nipate salama, Kuliko maisha bora, dhulma kukutawala, Huwezi pata salama, tubu utaangamia, Sheikh huyu Sheikh gani, aso faida na umma. Mwisho ninakuusia, ewe Sheikh ulo Dar, Wengi waloangamia, fedha ziliwahadaa, Waliuza utu wao, dini wakaikataa, Sheikh huyu Sheikh gani, aso faida na umma. Abaa Abdul-azizi (Ngamia wa Jangwani) Dar.

Mashairi/Barua/Makala

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 15 - 21, 2013

AN-NUUR

Tunataka kuwaona watuhumiwa mahakamani


Ndugu Mhariri, Assalaam alaikum. Huwa wakati mwengine sitaki kuandika chochote au kusema kitu. Lakini kila siku mambo yanazidi; na chumvi inazidi kutiwa Zanzibar, na hatimaye mantiki inatoweka katika kra za binadamu. Sasa hivi tumesikia kuwa kuna watuhumiwa wamekamatwa kwa kuhusishwa na mauwaji ya Padri Evarist Mushi, lakini, kama watuhimiwa wamekamatwa tokea tarehe 17 Februari 2013 (baadhi yao), kwa nini hatusikii kuwa wamefikishwa mahakamani? Nakiri bado ile sheria ya masaa 48 tokea kukamatwa kwako ukishwe mahakamani bado ipo. Tuseme na hawa waliokamatwa juzi juzi tu, na hao waliokuja kutusaidia (kwa mujibu wa Kamishna wa Polisi Mussa Ali Mussa) kuna watu wapya wamekamatwa hatuoni kukishwa mahakamani. Au hawa sheria zao nyengine kwa vile imemhusu Padri? Bado imekuwa kitendawili kwangu: kwa nini pia upelelezi usianzie pale kanisani, au katika mfumo mzima wa kanisa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla? Upelelezi huu umekuwa upande mmoja tu. Ni kweli khulka ya binadamu siku zote inakuwa ina upendeleo fulani wa upande mmoja, lakini katika kazi kama hizi kinachotakiwa ni ukweli na uadilifu, sio kuegemea upande mmoja tu.

Kama ningeliwezaga, nami pia kuandika, Kalamu ningeshikaga, maswali ningewatwika, Wote wanaovuruga, amani yetu hakika, Kama ningeliwezaga, hofu kando kuiweka. Kama ningeliwezaga, kusema na kutamka, Kipaza ningeshikaga, yote ningeyatapika, Yanayo tuumizaga, kote yangeli sikika, Kama ningeliwezaga, hofu kando kuiweka. Kama ningeliwezaga, kutunga zikatungika, Habari za kuwazuga, wananchi potosheka, Mapema tungekaga, nchi yetu kuchafuka, Kama ningeliwezaga, hofu kando kuiweka. Kama ningeliwezaga, ukweli kuutamka, Ningelivalia njuga, bahari nikaivuka, Visiwani tiananga, wauaji kuwasaka, Kama ningeliwezaga, hofu kando kuiweka. Kama ningeliwezaga, kuongopa pasi shaka, Ningeliwachafuaga, nyote mkawa mwanuka, Kwangu ningesashaga, uchafu ukaondoka, Kama ningeliwezaga, hofu kando kuiweka. Kama ningeliwezaga, kuamuru Amrika, Wote ningeliwaswaga, barazani vibaraka, Ummatumewachokaga,nanyingizenu dhihaka, Kama ningeliwezaga, hofu kando kuiweka. Kama ningeliwezaga, kufuta likafutika, Baraza ngelifutaga, kabisa likafutika, Moyo wa niumizaga, kushoto wakijiweka, Kama ningeliwezaga, hofu kando kuiweka. Kama ningeliwezaga, kutangaza Tanganyika. Visiwani hawanaga, sheria imeshindika, Raia kumilikaga, silaha mekatazika, Kama ningeliwezaga, hofu kando kuiweka. Kama ningeliwezaga, uliza likajibika, Nani aliyempaga, silaha ikatumika? Mauaji kafanyaga, au nje ametoka? Kama ningeliwezaga, hofu kando kuiweka. Kama ningeliwezaga, kaditama nimeka, Hili ningelisemaga, uongo siyo kichaka, Timamu kujichaga, majinuni sina shaka, Kama ningeliwezaga, hofu kando kuiweka. Isihaka Hemed Mzuzuri Morogoro

Kama!

Msamaha katika Uislamu


wa Kiislamu:- Msamaha wa Kiislamu katika sheria zake inakusudiwa kwamba, Uislamu ni dini nyepesi na msamaha na sheira zake zote zinasimamia juu ya huu msingi mkuu. Amesema mwenyezi Mungu (anataka Mwenyezi Mungu kwenu wepesi na wala hataki kwenu uzito). Na pia amesema tena (Na wala hataki kuwafanyieni katika dini uzito) Surat Haji, na amesema, Na mcheni mwenyezi Mungu kiasi muwezacho. Taghabun 16. Pia amesema,Hamlazimishi Mola mtu yeyote isipokuwa lile unalioweza kulifanya. Na miongoni mwa hadithi za Mtume (SAW) ile aliyoipokea Imamu Bukhari katika Sahihi zake, kwamba dini ni nyepesi na atakayeitia ugumu dini isipokua itamshinda. Basi anayetazama kwa makini juu ya dalili hizi za aya na hadithi zinabainika kwake, na kumfafanulia kuwa sheria zote za Kiislamu zimejengewa katika wepesi na msamaha na ulaini. Msamaha wa Uislamu katika kuhudumiana (Kuishi vizuri). Kwa hakika umelingania Uislamu kwa Waislamu juu ya msamaha katika kuhudumiana, katika kuuza na kununua na kukopa na kulipa na kuyafanya mambo hayo kunapelekea katika Rehema za Mwenyezi Mungu na mapenzi yake. Maana ya msamaha katika kuuza ni kuwa, asiwe muuzaja bahili juu ya bidhaa zake na mwenye kupandisha bei bidhaa na kutaka faida zaidi, bali awe mpole na mwenye kuridhia kwa kidogo akipatacho miongoni mwa faida. Msamaha katika kununua. Awe mwenye kununua mwepesi katika kununua kwake asiwe mlaliaji wala muombaji punguzo ili asizuie bidhaa hiyo kuuzika. Msamaha katika kudai.

Hapa ndipo inapozuka shaka kubwa miongoni mwetu kuamini au kutoamini mfumo mzima wa utoaji haki, utendaji haki. Sisi siku zote tunaingia ndani ya tukio, kama alivyofanya Waziri wa Mambo ya Ndani Mheshimiwa Dr. Emmanuel Nchimbi. Lakini tujue kuwa polisi kama taasisi, sidhani kama wananchi wengi wanaiamini vya kutosha. Mnakumbuka lile tukio la kuibiwa mfanya biashara Dar es Salaam juzi juzi tu; na pesa zilizopatikana waligawana jamaa! Hiyo ripoti ya Afande Suleiman Kova iko wapi? Kama polisi imefikia kufanya haya na mengine mengi itakuaje? Tumuamini nani? Mwananchi Zanzibar

Na Sheikh Mohamed Obaida


Shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu na rehema na amani zimfikie Bin Abdillahi huyu ni neema yenye kutegemewa na jamaa zake na sahaba zake na wale wote waliomfuata yeye ama baada ya utangulizi huu. Mpenzi msomaji, makala hii anuani yake utakuta imekusanya maneno matatu yenye herufi chache, lakini mwenye kutafakari maneno haya, atayakuta yamebeba maana kubwa miongoni mwa mambo muhimu ambayo hapaswi kuyakosa kwa watu wote. Na kabla hatujaingia katika somo la msamaha katika Uislamu, tunapenda kwanza tuitambulishe kwenu maana ya msamaha kwa lugha ya kiarabu na mpatano wa wanazuoni. Ama msamaha kwa lugha ni salama na uwepesi. Kwa makubalianoya wasomi, ni kusamehe watu katika huduma mbalimbali kwa kufanya wepesi wa mambo na kulainisha, ambako kunaonyesha uwepesi na bila ya kutumia nguvu. Miongoni mwa vitu vilivyo wazi kabisa katika msamaha

Aombe deni lake au haki yake kwa upendo na sio kwa ubabe na iwe kwa ulaini bila kutumia nguvu na achunge hali ya mdeni wake, na akiwa hana kitu amsubirie au amsamehe hilo deni lake. Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu, Na anapokuwa mdaiwa hana kitu, na asubiriwe hadi atakapopata na mtakapotoa sadaka ni kheri kwenu ikiwa mnajua . Barakat 28. Msamaha katika ulipaji deni:Arudishe haki kwa mwenyewe kwa wakati waliokubaliana na wala asimlazimishe kwa nguvu, kisha akafuatia kutekeleza haki kwa mwenyewe na wingi wa asante na dua au kumkimbia ikiwa anaweza. Na mfano hai na bora kabisa ni ule ambao mtu mmoja alikuwa anamdai Mtume, akaja kuliomba deni hilo kabla ya muda, akakusudia Sayidina Omar kutaka kumuua, Mtume akasema; Nilitarajia kuwa utaniamrisha kuwa nimlipe, tena kwa vizuri zaidi, akaamrisha alipwe deni lake na ziada, akasema hii ziada ni malipo ya kule kumtisha kwako ewe Omar. Vile vile miongoni mwa msamaha wa Kiislamu ni kuongea maneno mazuri na kauli nzuri. Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu, Nasema waambie waja wangu waseme yaliyo mazuri zaidi. Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu, Neno zuri ni sadaka. Hii ni baadhi ya mifano hai ya kuonyesha msamaha wa Uislamu, ambao laiti tunge yazungumzia kwa upana, basi pasingalitosha. Lakini tunatosheka na maneno haya mafupi ambayo yatampa msomaji picha ya uhakika juu ya msamaha wa Kiislam na utukufu wa sheria zake. Basi Mwenyezi Mungu ndiyo mumwezeshaji.

13

MAKALA

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 15 - 21, 2013

AN-NUUR

Pamoja na ugaidi, tuangalie na yale aliyosema Kikwete


Na Ibrahim Mohammed Hussein HIVI karibuni Waziri wa Mambo ya ndani aliitangazia Dunia kwamba sehemu moja ya Tanzania kuna ugaidi, sehemu hiyo ni Zanzibar. Kisa cha kuitangazia Dunia ni kuuwawa kwa kiongozi wa Kanisa. Rais Jakaya Kikwete ameahidi kuagiza wapelelezi na makachero kutoka nchi za nje kusaidia upelelezi. Huu ni uamuzi wa busara ikiwa tutautumia vyema kuchunguza mauaji yaliyotokea huko nyuma na haya yanayoendelea kutokea hivi sasa. Suala la usalama wa raia na mali zao ni suala la Muungano. Wa z a n z i b a r i b a d o wanataka kujuwa ukweli wa mambo juu ya kuuwawa Viongozi na raia wengi wa nchi hii. Waziri kuiambia Dunia kwamba Zanzibar kuna magaidi ni jambo zito sana. Uzito wa jambo hilo unategemea Dunia itakavyolipokea neno la Waziri wa Mambo ya Ndani wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano la kuipata tafsiri ya Ugaidi. Wengi wetu tunaposikia neno ugaidi linatajwa kwenye vyombo vya habari, basi haraka hutujia kumbukumbu ya zile hujuma za kigaidi zilizofanywa katika vituo vya Biashara vya jijini New York, Marekani, maarufu September 11. Wengi pia miongoni mwetu tunaposikia habari za mashambulizi ya kigaidi, basi hutujia zile kumbukumbu za hujuma za kigaidi zilizofanywa dhidi ya majengo ya Balozi za Marekani huko Dar es Salaam na Nairobi mwaka 1998. Tafsiri ya neno ugaidi kwa wengi wetu ni mashambulizi yanayofanywa na kundi la watu wanaodai haki zao kwa kutumia nguvu na ukatili dhidi ya mahasimu wao. Kitendo cha ugaidi siku zote au kwa kawaida, hunasibishwa na harakati za kisiasa za mapambao ya kitabaka, kati ya tabaka la wanaokandamizwa dhidi ya dola. Hii ndio dhana iliyojengeka siku hizi miongozi mwa watu wengi Ulimwenguni kote. Maana ya neno Ugaidi au kwa Kiingereza Terrorism ni kitendo chenye kutia hofu na kusababisha maafa na machungu makubwa. Ugaidi si dhana mpya ulimwenguni kama wengi wetu tunavyodhani. Ugaidi ni neno jipya katika msamiati wa Kiswahili ambalo limeanza kutumika baada ya kuzuka wimbi la mashambulizi ya kigaidi Duniani. Huko nyuma, kiasi cha miongo mitatu iliyopita neno hili halikuwepo ingawa vitendo hivi vilishamiri sana huko ulaya na mashariki ya kati. Hivi leo, jamii duniani kote imejenga dhana ya mtazamo wa upande mmoja, kwamba ugaidi ni kitendo cha kikatili kinachofanywa na kundi fulani dhidi ya dola au tabaka la mwenye nguvu za kisiasa na kiuchumi nao pia huweza kufanya vitendo vya kigaidi. Mfano wa nukta hii, ni kwamba dola yeyote isiyo heshimu haki za binaadamu na haki nyengine za raia basi dola hiyo itakua inafanya vitendo vya kigaidi na hivyo hugeuka na kua dola ya kigaidi. Kama maana halisi ya ugaidi ni kutia hofu inayowaletea wanaadamu maafa na mchungu, kwa hivyo hata dola kama inafanya hivyo dhidi ya raia zake basi nayo huitwa dola ya kigaidi. Kama itasemwa kuwa Zanzibar kuna ugaidi, basi ugaidi huo utakuwa wa dola ambao ulianza mara baada ya Mapinduzi matukufu ya 1964. Wale vijana wa zamani watakumbuka kwamba awamu ya kishindo kilichotia hofu na machungu makubwa miongoni mwa Wazanzibari. Vi j a n a w a l e o n a o p i a watakumbuka jinsi gani raia walivyoteseka mara baada ya kuanzishwa mfumo wa siasa za vyama vingi. Ugaidi wa dola uliofanyika katika awamu ya kwanza ya serikali ya Mapinduzi ulifanywa dhidi ya Wazanzibari kwa visingizio mbali mbali vikiwemo kuwadhibiti wapinga Mapinduzi, wezi wa mali ya umma, tuhuma za kupindua serikali na kadhalika. Mpinga Mapinduzi kwa wakati huo, alikua hata Yule aliepitikiwa na usingizi wa jioni wakati Bwana Mkubwa alipokua akihutubia mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Maisara. Wengine waliitwa wapinga Mapinduzi kwa kua watoto wao waliikimbia nchi kwa sababu za kitoto tu. Hivi ndivyo ilivyokuwa dola ya Tanzania ikiwatendea raia zale. Nasema Tanzania kwa sababu Wazanzibari wote ni raia wa Tanzania na suala la uraia ni suala la Muungano. Katika kipindi hicho hakukua na sheria wala mahakama za kiraia bali mahkama za kimapinduzi zilizo hukumu kwa chuki na utashi wa Bwana Mkubwa na kamati yake ya watu 14. Mahakama za miji ya Unguja na Pemba zilikua na wazee waliokua wakiwafunga raia bila ya hatia yoyote. Wananchi wengi wasio na hatia waliathirika chini ya mahakama hizi. Wakati huo wa ugaidi wa dola, hata askari wa chama cha ASP-Valantia, nao walikua na sauti na amri ya kumpiga mtu mijeledi na kumlaza mtu ndani. Katika hali hiyo ya kutokuwepo kwa sheria na haki watoto wengi walipoteza baba zao, wanawake wengi walipoteza waume zao na watu wakapoteza ndugu, maraki na hata wachumba wao. Haya yalifanywa na dola dhidi ya raia zake. Ilikua haipiti wiki moja bila kusikia, mume wa fulani kachukuliwa, baba yake fulani kachukuliwa, ndugu

Inaendelea Uk. 14

Pamoja na ugaidi, tuangalie na yale aliyosema Kikwete


yake Fulani kachukuliwa au mjomba yake Fulani kachukuliwa usiku wa manane. Hali hiyo iliwatia hofu na machungu makubwa raia. Vibuhuti na simanzi viliingia majumbani. Huo ndio uliokua ugaidi wa dola dhidi ya raia zake. Ugaidi wa dola katika siku za awamu ya kwanza ya Mapinduzi ulivuka mipaka hata ya kidini kwa kulazimisha ndoa zisizo kua na idhini ya wazee. Kama idhini ilitolewa na mzazi basi ilikua chini ya khofu kubwa. Wake na watoto waliopotelewa na waume na baba zao hawakuelezwa, angalau wakatimiza masharti ya kidini ya eda na urithi. Ndoa hizo zilikua si lolote bali ni zinaa na makadhi na masheikh wakijua hivyo, lakini waliwaogopa watawala kuliko Mola wao. Baadhi ya watoto wa kike walioolewa chini ya mpango huo wa mpata mpatae walifanya majaribio kadhaa ya kujiua au kuzihatibu mimba zilizoingizwa chini ya zinaa hiyo ya jumla jamala. Hivyo ndivyo Dola inapokua ya

14

Makala

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 15 - 21, 2013

AN-NUUR

Inatoka Uk. 13

kigaidi-State Terrorism. Dola linapokua gaidi hua hatari kuliko chui mla watu, mwenye njaa kali. Wakati Fulani Mfalme mmoja huko katika China ya kale, alikitembelea kijiji kimoja katika mahmia yake. Alipoka kwenye kijiji hicho alimkuta mama mmoja analia kwa uchungu mkubwa na huku anaomboleza. Mfalme akaingiwa na huzuni na akasimamisha msafara wake, kisha akamuuliza yule mama, nini kilichomsibu. Mama yule akamueleza Mfalme kwamba mwanawe ameliwa na chui asubuhi ya siku ile. Mfalme akambembeleza sana na akamtia moyo kwa kumwambia kua asikate tamaa Mwenyezi Mungu atampa mtoto mwengine. Yule mama akapiga mayowe na kuangua kilio kuliko cha mwanzo. Mama yule akamwambia mfalme, chui huyu kaua mume wangu kwanza na kisha kaua watoto wangu watano na huyu wa leo ni wa sita, sina tena mtu mimi. Mfalme akahuzunishwa sana na masahibu yaliomkuta mama yule. Baadae mfalme

yule akamshauri yule mama aondoke kwenye kijiji kile. Mama yule akamwambia mfalme kwamba siwezi kuhama hapa, kwani katika kijiji chetu kuna utawala mzuri unaoheshimu haki za watu. Mfalme akasema, kumbe watawala wabaya ni hatari kuliko chui mla watu. Vivyo hivyo, kumbe dola linapokua gaidi ni hatari kuliko chui mla watu. Dola linapokua gaidi maisha ya raia hua kitu kisicho na thamani na utu wa mtu hua hauna maana. Lakini baya zaidi ni kua dola inapokua gaidi hua si rahisi kujibadili na hata ikicha kucha zake basi meno yake yataonekana pale inapocheka. Zanzibar hivi sasa ni tulivu na shwari kutokana na damu nyingi iliyomwagika huko nyuma ambayo hatimae ilipelekea kupatikana hiki kifaa kinachoitwa Mwafaka. Lakini madhara na simanzi za enzi ya dola ya kigaidi bado zipo na ni vigumu kusahaulika kwa sababu bado serikai zilizopo madarakani hazitaki kukubali kwamba mambo yaliofanyika huko nyuma yalikua ni makosa makubwa

ya kisiasa na kijamii. Sasa hivi katika ulimwengu wetu huu kumezuka utamaduni wa kisiasa ambao unaleta mwelekeo mwema wa kuleta umoja wa kitaifa, utengemano na uzalendo. Utamaduni huu ni ule wa kutafuta maridhiano kwa nia ya kusahau yaliopita na kuanza ukurasa mpya katika Taifa. Ili kuondoa sura mbaya ya ugaidi wa dola uliofanyika huko nyuma dhidi ya raia basi haitakua jambo la aibu serikali kukiri kua waliotangulia walitenda kosa. Kinyume cha hivyo, serikali zetu zinapoendelea kukaa kimya na kujifanya viziwi basi huenda jambo hili huko mbele likachukua sura nyengine. Viongozi wetu wasijifanye vipofu na viziwi, wasikilize na watazame nini kinatokea ulimwenguni hii leo kuhusu masuala kama haya. Kumnyima mwananchi haki yake ya kiraia kuihoji Serikali na pia kuwakataza watu wasiyaseme maovu yaliofanywa na Serikali dhidi ya raia zake ni bado kuendeleza ugaidi wa dola. Hivi sasa Kadinali Pengo ametoa matamko mazito anasema:

Hili si tukio la dharura, kiasi kwamba watu wetu wa usalama wa Taifa washindwe kuzuia, hili lilijulikana na lingeweza kuzuilika. Kwa maneno hayo ya Kardinali panahitajika uchunguzi wa hali ya juu. Vile vile tusikimbilie ugaidi tu, hata kauli ya Rais Kikwete alioitoa miezi ya nyuma ya kuwaonya baadhi ya Viongozi wa dini ambao wanajishirikisha na uuzaji wa madawa ya kulevya ni vizuri kutupiwa macho. Siku zote tunasikia kwamba Zanzibar ni njia kuu za madawa ya kulevya. Jambo hilo lisidharauliwe hata kidogo, lifanyiwe kazi. Pia tusisahau kuwa Wajerumani walichoma moto jengo la Bunge la Wajerumani ili wapate kuwasingizia wapinzani wa serikali na kuwakamata na mwishowe kuwauwa. Ni jambo zuri kushirikiana na maraki zetu ili kuwatafuta wauwaji hawa. Lakini wananchi wote wa Tanzania wanangojea ripoti ya uchunguzi itolewe kwa vile pesa nyingi za walipa kodi zitatumika kwa shughuli hiyo.

NAFASI ZA MASOMO YA UALIMU NGAZI YA CHETI 2013/2014


WAISLAMU MNATANGAZIWA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI CHUO CHA UALIMU KIRINJIKO ISLAMIC A. SIFA: Muombaji awe na sifa zifuatazo: (a) Ufaulu wa kidato cha 4 usiopungua alama 27 katika kikao kimoja cha mtihani, asiwe amekaa zaidi ya miaka mitano (5) tangu amalize kidato cha nne. (b) Awe na credits 4 kiwango cha C endapo amekaa mtihani kwa vikao zaidi ya kimoja. (c) Kuhitimu kidato cha 6 ni sifa ya nyongeza. B. MAELEKEZO MUHIMU KWA WAOMBAJI WOTE 1. Fomu ya maombi iambatanishwe na vyeti (leaving and Academic certicates) vya kidato cha 4 pamoja na picha ya hivi karibuni. 2. Fomu irudishwe siku ya kufanyiwa usaili tarehe 8/6/2013 saa 2:00 asubuhi. 3. Vituo vya usaili ni hivi vifuatavyo: (a) Kirinjiko Islamic T.C SAME (b) Ubungo Islamic T.C DSM (c) Nyasaka Islamic S.S. Mwanza 4. Majibu yatatolewa kwa watakaochaguliwa tu. 5. Fomu zinapatikana kwa gharama ya shilingi elfu kumi katika vituo vinavyoonekana ukurasa wa 15 katika tangazo la Shule.

15

TANGAZO

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 15 - 21, 2013

AN-NUUR

NAFASI ZA KIDATO CHA TANO 2013/2014


Waislamu kote nchini mnatangaziwa nafasi za kidato cha Tano kwa shule zifuatazo:

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE


1.

KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL NYASAKA ISLAMIC SECONDARY SCHOOL UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOO L

SAME KILIMANJARO MWANZA DAR ES SALAAM

Shule hizi ni za Kiislamu zenye lengo la kuwapa wanafunzi taaluma ya hali ya juu na malezi bora ya Kiislamu kwa gharama nafuu. Shule hizi ni za mchanganyiko wa wavulana na wasichana na zinapokea wanafunzi wa bweni tu. 2. Masomo yanayofundishwa ni Islamic knowledge, Combinations za SAYANSI, ARTS, BIASHARA pamoja na COMPYUTA. 3. Muombaji awe na Crediti 3 au zaidi na angalau D ya Elimu ya Dini ya Kiislamu katika matokeo ya kidato cha nne. Ikiwa ana F au hakufanya Elimu ya Dini ya Kiislamu, basi awe tayari kusoma programu maalum ya Maarifa ya Uislamu atakapokuwa kidato cha tano. 4. Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni tarehe 18 /05 /2013 5. Fomu za Maombi zinapatikana kwa gharama ya shilingi 10,000/= katika vituo vilivyoorodheshwa hapa chini. 6. Arusha Kilimanjaro Tanga Mwanza Musoma Kagera Shinyanga Osi ya Islamic Education Panel Jambo Plastic Ghorofa ya 2 mkabala na msikiti Mkuu Bondeni - 0763 282 371/ 0784 406 610 Moshi: Msikiti wa Riadha 0654 723 418 Same: Kirinjiko Islamic Secondry School: 0784 296424/0655 697 075 Uongofu Bookshop: - 0784 982525/ Mandia Shop - Lushoto: 0782257533 Nyasaka Islamic Secondary School 0717 417685/0786 417685 Osi ya Islamic Education Panel - Mwanza - Mtaa wa Ruji mkabala na Msikiti Al-Amin 0785 086 770 Duka la Kansolele -Stendi ya zamani sokoni - 0714587193 Bukoba: Alhuda Caf Kwa mzee Kinobe karibu na osi za TRA. - 0688 479 667 Msiikiti wa Majengo-0718866869 Kahama osi ya AN NUUR Karibu na msikiti wa Ibadhi: 0753 993930 Ubungo Islamic High School 0754 260 241/0712033556 Osi ya Islamic Ed. Panel Temeke -Msikiti wa Nurul Yakin 0655144474 Wasiliana na Ramadhani Chale :0715704380 Hijra Islamic Primary School : 0716 544757/0712 325086 Osis ya Islamic Ed. Panel karibu Nuru snack Hotel 0714285465 Babati: Shule ya Msingi Hangoni: 0784 667575 Msikiti wa mwanga Kigoma: 0753 355224 Kibondo Islamic Nursery School: 0784 442860 Kasulu: Murubona Isl.SS. 0714710802 Wapemba Store: 0784 974041/0786 959663 Amana Islamic S.S 0786 729 973 Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa NURU 0715 681701/0716791113 Mkuzo Islamic High School. 0716 791113 Duka la vifaa vya Kiislamu nje ya Msikiti wa Uyole 0713 200209 Rexona Video mkabala na Mbeya RETICO: 0713 200209 Sumbawanga: Masjid TAQWA 0717082 073 Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784 944566 Madrastun Najah: 0714 522 122 Wete: Wete Islamic Education Center: 0777 432331 Madrasatul Fallah: 0777125074Osi ya ust. Yusufu Ally jirani na msikiti mkuu 0653705627

Dar es Salaam Morogoro Dodoma Singida Manyara Kigoma Lindi Mtwara Songea Mbeya Rukwa Tabora Iringa Pemba Unguja Maa -

Pia Fomu zinapatikana kwenye Tovuti: www.ipctz.org. Ikumbukwe kuwa watakaopata fomu kupitia tovuti (download) watatakiwa kuzilipia wakati wa kuzirejesha. USIKOSE NAFASI HII ADHIMU WAHI KUCHUKUA FOMU SASA! Wabillah Tawiq MKURUGENZI

16

AN-NUUR
16

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 15 - 21, 2013

Usikose nakala yako ya AN-NUUR kila Ijumaa

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 15 - 21, 2013

AN-NUUR

Na Bakari Mwakangwale SERIKALI imetakiwa kuacha kupiga propaganda chafu dhidi ya Waislamu. Wito huo umetolewa na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, katika ukumbi wa Hoteli ya Lamada, Jijini Dar es Salaam, Jumamosi ya wiki iliyopita. Akisoma tamko la Waislamu kupitia Jumuiya na Taasisi mbele ya waandishi wa habari, Maalim Yassin Kachechele, alisema Serikali inapaswa kuwa makini katika kushughulikia kadhia za kidini zinazojitokeza hivi sasa nchini kabla ya kuelekeza shutuma na madai kwa Waislamu kwani ni hatari. Serikali iwe makini isiyachukulie mambo haya upande mmoja tu kuwa hayo ni mambo ya ugaidi na ugaidi huo ukaelekezwa k w a Wa i s l a m u , n i hatari. Alisema Maalim Kachechele. Maalim Kachechele, alisema hivi sasa kumekuwa na kamatakamata kwa vijana wa Kiislamu na kutiwa ndani na hata kufunguliwa mashata kwa tuhuma za uchochezi wa kidini. Hivyo, kupitia tamko hilo Maalim Kachechele, alisema vyombo vya dola vinapaswa kufanya shughuli zake kwa umakini katika kuyafuatilia kwa ukaribu

Serikali iache propaganda chafu dhidi ya Waislamu

BAADHI ya viongozi wa taasisi za Kiislamu wakiwa katika semina iliyoandaliwa na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini na kufanyika katika Hoteli ya Lamada, Ilala Jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Maalim amkabili Warioba juu ya mamlaka ya Zbar


Na Mwandishi Wetu

matukio hayo ili isiwe chanzo cha kulitumbukiza Taifa katika vurugu za kidini. Tamko hilo lilisema, kuuwawa na kujeruhiwa kwa

viongozi au waumini wa dini zote nchini hakukuanza sasa, kwani ishatokea pia Masheikh na Waislamu kuuwawa na hata kujeruhiwa lakini Serikali

haikusema kuwa matukio hayo ni mipango ya kigaidi, dhidi ya dini yoyote. Maalim Kachechele, alisema imekuwa ni desturi

hivi sasa kila inapotekea kwa Waislamu kuelekeza madai yao kwa Serikali yao, huibuliwa uvumi na tuhuma kwao kuwa wana mipango ya kuvamia na kuchoma Makanisa, vituo vya Polisi au osi za Chama fulani cha siasa. Hivi Waislamu wajihisi vipi kwa tuhuma kama hizo zisizo na ushahidi? Ni wazi mwenendo huu unawatia wasiwasi Waislamu kuwa kuna agenda ya siri dhidi yao na pia hujenga chuki na wenzao Wakristo. Alisema Maalim Kachechele. Tamko hilo lilifafanua k u w a , Wa i s l a m u k a m a wanaadamu wengine wanapenda kuishi kwa amani na utulivu, na kwamba hakuna binaadamu anayependa kusemwa vibaya, kuishi kwa hofu na ukosefu wa amani. Alisema, mwenendo wa kuwalaumu Waislamu kuwa wanavunja amani si jambo la kuvumilia kwani linajenga mfarakano miongoni mwa Waislamu na Wakristo. Kulikuwa na sababu gani kwa Serikali kukimbilia kusema ni tukio la kigaidi wakati haijafanya uchunguzi? Huku si kutoa muelekeo wa majibu ya uchunguzi? Kwani kila mauaji yanayofanyika nchini ni ugaidi? Inaonekana lengo ni kuwapaka tope Waislamu pamoja na dini yao. Limesema na kuhoji tamko hilo.

CHAMA cha wananchi CUF kupitia Katibu Mkuu wake ambae pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, kimemuhakikishia Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania, Jaji Joseph Wa r i o b a , k w a m b a Wazanzibari kwa umoja wao hawatokubali chochote kile ambacho kitasababisha kukosekana kwa Zanzibar yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa itakayofuatiwa na mfumo mpya wa ushirikiano na Tanganyika kupitia

Muungano. Maalim Seif aliyasema hayo huko Makunduchi mkoa wa kusini Unguja hivi karibuni alipokuwa akizungumza na wananchi mbali mbali kwenye mkutano wa hadhara. Katika mazungumzo yake Maalim Seif amesema kuwa maoni ya Wazanzibar walio wengi wanataka mamlaka kamili ya nchi yao, kwa hiyo ni lazima jambo hilo litimie. Kufuatia mkutano huo Maalim Seif amesema kuwa kwa sasa Zanzibar haiwezi tena kukubali kukosa mamlaka yake ya kuwa na udhibiti wa mambo ya nje na mahusiano ya kimataifa kwani imechoka na

udhalilishaji inaofanyiwa kupitia Serikali ya Muungano. Maalim ametolea mifano mbali mbali ukiwemo ule wa Serikali ya Muungano kuilazimisha Zanzibar kujitoa katika Umoja wa Nchi za Kiislamu (OIC) mwaka 1993. Alifahamisha wazi kuwa kwa sasa Zanzibar inataka kuwa na Wizara na Waziri wake wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na haitokubali chochote chini ya hapo. Amesema kuwa udhibiti wa mambo ya nje ndiyo kigezo cha nchi kukubalika na kutambulika kimataifa na Zanzibar inataka kurejesha mamlaka hayo na kurejesha kiti chake kwenye Umoja wa Mataifa.

KATIBU Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

You might also like