You are on page 1of 16

www.annuurpapers.co.

tz

Sauti ya Waislamu

Watuhumiwa Kesi ya Sheikh Ponda wawakaanga Polisi mahakamani


Wadai walivamiwa msikitini wakiwa katika ibada Waikana BAKWATA na kudai hawazijui kazi zake Wasema kiongozi wao ni Quran na Sunna za Mtume

ISSN 0856 - 3861 Na. 1061 RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 8 - 14, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Hakuna kitu kinachowaliza wenye akili zaidi kuliko wasiwasi wa kuokoka na Moto na kupata Pepo! Hijja peke yake ndiyo inayoweza kumsasha muislamu na madhambi yote, akarudi kama siku aliyozaliwa na mama yake, na akapata Pepo katika muda wa siku tano. Hivyo hakuna matumizi bora ya fedha kuliko kwenda Hijja. Wewe ndugu yetu ushakwenda mara ngapi?KaribuAhlu Sunna wal Jamaa. Gharama zote ni Dola 4,300 tu. Tafadhaliwasiliana nasi ifuatavyo: Tanzania Bara: 0717224437; 0777462022;Unguja: 0777458075;Pemba: 0776357117.

4)KUPATA PEPO KWA SIKU TANO!

Ni usiku wa Itiqaf T.I.C Kichangani kesho

Hamad, amesema Zanzibar imepoteza fursa nyingi kwa kutokuwa mwanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kiislamu Duniani (OIC). Na Mwandishi Maalum, Maalim Seif Sharif Zbar KIKOSI Maalum cha kutuliza ghasia (FFU) kikiwa katika eneo la Markaz Chang'ombe Hamad, ambaye ni Makamo Jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2012. KATIBU Mkuu wa Chama wa Kwanza wa Rais wa c h a Wa n a n c h i , C U F Inaendelea Uk. 3 Maalim Seif Sharif

Maalim Seif awakumbusha Zanzibar OIC


Ujio wa FBI: Ni Msiba
Sasa ndio giza limetanda kweli Sio alipokufa Mwalimu Nyerere

Mwenyekiti wa Jumuiya wa Jumuiya ya Al-Yousuf Sheikh Al-Youseif (kushoto) akiwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Osini kwake Migombani.

Waislamu kukutana kutawakal kwa Allah (s.w) Masheikh kujadili kulegalega mahusiano ya kidini

2
www.annuurpapers.co.tz

Tahariri/Tangazo
Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 8 - 14, 2013

AN-NUUR

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786


MAONI YETU

Ujio wa FBI: Ni Msiba


IMETOKA taarifa ya Jeshi la Polisi kuwa tayari maafande wetu wanashirikiana na makachero wa FBI kuwanasa watuhumiwa wa m a u a j i y a P a d re Evarist Mushi. Pengine swali ambalo Watanzania wangependa kujua ni hili. Katika ushirikianao huu, nani anamtuma kazi mwenzake? Au tuulize vingine, huu ni ushirikiano au askari wetu wanatumwa kazi na wageni wao FBI? Tunauliza hivi kwa sababu tuliwaona watu hawa alipokuja Bill Clinton hapa. Hawakuwaamini kabisa wanausalama wetu kiasi cha kumdhalilisha aliyekuwa Rais wetu Benjamin William Mkapa kwa kulinusisha gari lake kwa mbwa. Au Tumesahau? Alipokuja Mzee Mzima George W Bush wakaweka vijana wao mpaka kwenye dari ya Ikulu yetu! Hivi sisi ndio tuliowaomba wapande au walipanda wenyewe bila hata ya kungoja ruhusa yetu? Mtu anakuja nyumbani kwako halafu anakupekuwa mpaka chumbani kwako. Je, hivi tuliridhia udhalilishwaji ule? Je, hapa kuna kushirikiana

Sasa ndio giza limetanda kweli Sio alipokufa Mwalimu Nyerere

au wao kufanya watakavyo? Tusisahau kuwa hawa ndio wale waliosema kwa kujiamini na jeuri kuwa Iraq kuna silaha za maangamizi. Lakini baada ya walilokusudia kufanikiwa kwa maana kuwa baada ya kuvamia nchi ya watu na kuuwa mamilioni ya watu na kufanya uharibifu na ufusadi wa kutisha, wenyewe hao hao bila ya aibu wakasema kuwa waliongopa, Saddam hakuwa na silaha za maangamizi. Kama alivyosema Rais wetu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na kama alivyosema Waziri wa Mambo ya Ndani Mheshimiwa Emmanuel Nchimbi na pia baadhi ya makamanda wetu wa Polisi, inavyoonekana tunawaamini sana washirika wetu hawa. Lakini swali ni je, kama watatuambia Uamsho wana kiwanda cha silaha za maangamizi kama walivyodai kuwa zipo kule Iraq tutaamini maadhali wamesema wao? Tuna ubavu wa kupinga watakayosema kama tutakuwa na wasiwasi kuwa wanaongopa au sio sahihi? Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Kimataifa kwa ujumla ilisema Iraq hakuna silaha za maangamizi na ikapinga nchi hiyo

kuvamiwa, lakini Marekani ikavamia ikafanya ufisadi iliokusudia kufanya. Je, na sisi tupo tayari kubeba gharama ya matokeo ya ukachero wao kama itakuja katika sura ileile ya madai ya silaha za maangamizi Iraq? Akizungumza katika mahojiano maalumu na baadhi ya vyombo vya habari wiki iliyopita, Kamishna wa Polisi Zanzibar, Musa Ali Musa alithibitisha kwamba jeshi lake limekuwa likishirikiana na FBI katika upelelezi huo na kwamba idadi ya waliokamatwa imeongezeka. Ni kweli tumekuwa tukishirikiana na FBI katika upelelezi ili kuhakikisha kuwa, wahusika wa tukio la kuuawa kwa Padri Mushi wanakamatwa. Hii itasaidia kupunguza vitendo vinavyohusishwa na matukio ya kigaidi yakiwamo mauaji,alisema Kamishna Musa. Labda tuulize, ujuzi gani na ufahamu gani wa kuwajua Wazanzibari na Watanzania waliokuja nao FBI kiasi cha kuwezesha kufika tu wanakamatwa watu? Au wamekuja na orodha yao na polisi wetu wanafanya kutumwa tukamatie yule na yule na yule? Yamewahi kufanyika mauwaji mengi sana nchini hapa, yakiwemo ya Kamanda wa Polisi Mwanza, lakini yote yalichukuliwa kama matukio ya kihalifu na vyombo vyetu vya usalama na sheria vikayashughulikia kwa umakini mkubwa. Kitu

gani kinawafanya polisi wetu wakimbilie kuleta msamiati wa ugaidi katika tukio hili? Je, huu ni wao wenyewe au wameletewa na washirika wao FBI? Sisi tunadhani kuwa kabla ya polisi wetu kukimbilia kuwa na imani na ujuzi na ufanyaji kazi wa FBI, wangefanya kwanza semina nao wawaombe wawafahamishe uzuri na kwa kituo kile kizungumkuti cha Anthrax Terror Attack kimeishia wapi? T u n a s e m a kizungumkuti kwa sababu awali wataalamu hao tuliowaagiza kutoka Washington na wenzao katika ukachero nchini mwao walisema kuwa kimeta kile kilitoka kwa Al Qaida waliotumwa na Saddam Hussein. Walimwengu wakaonyeshwa na bahasha zilizoandikwa Allahu Akbar ili kukazia kuwa waliohusika ni Waislamu, Al Qaida. Hata hivyo baadae wakawa wanaparurana

wenyewe kwa wenyewe baada ya taarifa kuvuja kuwa kimeta kile kilitokea katika maabara zao wenyewe, tena za kijeshi. Katika kitisho kile cha kimeta ilielezwa kuwa watu saba walikufa. Je, sisi tumejiandaa kulipa gharama kiasi gani (katika sura ya kuuliwa au kuteswa Watanzania wasio na hatia) kama mambo tutakayofanyiwa ni sawa na haya ya Anthrax Terror Attacks na yale ya silaha za maangamizi Iraq? Kwa hakika kwa mtu yeyote mwenye akili yake timamu na hasa akiwa na japo chembe ya uzalendo na mwenye kujali ubinadamu na utu wake, akitafakari juu ya ujio huu wa FBI, hatakosa kuona kuwa tumekwa na msiba. Kama tuliambiwa kuwa giza limetanda alipokufa Mwalimu Nyerere, zile zilikuwa nyimbo na ngonjera tu za kuomboleza msiba, sasa ndio giza limetanda kweli.

P.O. Box 55105, Tel: 2450069, 0712 974428 Fax: 2450822 D Salaam E-mail: ipcubungoislamic@gmail.com

UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL

Maandalizi kwa wanaorudia Kidato cha IV, 2013


UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL inatangaza kozi maalum ya maandalizi kwa wanaorudia kufanya mtihani wa Kidato cha IV, 2013. Programu hii itaanza tarehe 28/02/2013 hadi tarehe 28/08/2013 Jumatatu hadi Jumamosi saa 2:00 kamili Asubuhi hadi saa 9:10 Alasir. Masomo yatakayofundishwa ni:Elimu ya Dini ya Kiislamu, English Language. Lugha ya Kiarabu. Basic Mathematics, History, Geography, Civics, Physics, Chemistry, Biology, Book Keeping, Commerce. Kiswahili Fomu za kujiunga zinapatikana shuleni kwa Tshs 10,000/=

Mlete mwanao apate Elimu bora itakayomwezesha kujiunga na Kidato cha Tano.
Kwa mawasiliano zaidi piga namba: 0714 888557/0659 204013 Wabillah Tawiq MKUU WA SHULE

Watuhumiwa Kesi ya Sheikh Ponda wawakaanga Polisi mahakamani


Na Bakari Mwakangwale MASHAHIDI wa upande wa utetezi katika kesi inayomkabili Sheikh Ponda Issa Ponda, wamedai askari Polisi waliwavamia na kuwapiga wakiwa katika ibada ya Itiqafu, ndani ya Msikiti wa Markaz Changombe, jijini Dar es Salaam, usiku wa Oktoba 16, 2012. Mashahidi hao ambao ni washtakiwa katika kesi hiyo namba 145/2012, walitoa madai hayo mbele ya Hakim Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Bi. Victoria Nongwa, walipokuwa wakitoa ushahidi wao mahakamani hapo Jumatano wiki hii, na kueleza kuwa wanakana mashtaka yote yanayowakabili. Mbali na madai hayo, washtakiwa hao ambao kila mmoja alipanda kizimbani kutoa utetezi wake, kwa ujumla walilikana BAKWATA, wakidai wanaisikia tu lakini hawaitambui pamoja na Mufti Sheikh Shaaban Simba. Wakiongozwa na Wakili wao Bw. Juma Nassoro, mashahidi hao walisema kwamba walika katika Msikiti wa Markaz Changombe kwa lengo la kufanya ibada ya Itiqafu, yenye fadhila nyingi miongoni mwa ibada za Kiislamu. Walidai pamoja na kujiandaa na ibada hiyo, hawakuweza kuitekeleza kwani ilipofika majira ya saa tisa usiku, muda ambao ndio muafaka kwa ibada hiyo, walisikia vishindo, geti kuvunjwa na kisha mlango na madirisha ya Msikiti kuvunjwa na askari kuingia ndani na viatu vyao na kuanza kuwashambulia. Shahidi namba moja Bi. Kulthumu Mfaume, ambaye pia ni mshtakiwa namba mbili, akiwa kizimbani aliiambia Mahakama kuwa alisikia kuna ibada ya Itiqafu katika Chuo Cha Kiislamu Markazi, ndipo alipolazimika kwenda kwa ajili ya Ibada hiyo. Usiku tulishtuka baada ya kusikia geti likivunjwa na mara mlango wa Msikiti nao ulibamizwa na kuvunjika, kisha niliona askari wakiingia ndani na mabuti yao, walitupiga sana na walikuwa wanaume tupu, kisha walituingiza katika magari yao Alisema Bi. Kulthumu. Bi. Kulthumu alisema pamoja na kujitetea kwamba wapo katika ibada ya Itiqafu na kuhoji kosa lao ni nini, alidai askari hao hawakuwaelewa na walizidisha kipigo. Akijibu maswali ya Wakili wa Serikali, Bw. Tumaini Kweka, kwamba alipataje taarifa za ibada hiyo ya Itiqafu, Bi. Kulthumu alisema akiwa njiani alisikia wakitangaza Msikitini, na kwa kufahamu umuhimu wa ibada hiyo alilazimika kwenda. Alipoulizwa ni nani kiongozi wake, Bi. Kulthumu alijibu hana kiongozi bali yeye huongozwa na Quran na Sunna za Mtume Muhammad (s .a .w). Kwa upande wake, shahidi namba mbili Bi. Zainab Mohammed (50), ambaye katika kesi hiyo ni mstakiwa namba tatu, akitoa ushahidi wake alisema alikamatwa na askari Polisi akiwa katika Ibada ya Itiqaf ndani ya Msikiti wa Chuo Cha Kiislamu Markazi Changombe, na alipata kipigo kutoka kwa askari hao. Kuhusu ni wapi alipata taarifa za ibada hiyo, alisema alipata kupitia kwa muumini mwenzake, ambapo baada ya kufika hapo Markaz, hakufanya shughuli yoyote zaidi ya kufanya ibada ndani ya Msikiti huo. Alipoulizwa ni nani mmiliki wa eneo alilokamatiwa, alisema kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu, anafahamu kuwa Misikiti yote ni mali ya Waislamu na kila Muislamu ana haki ya kufanya ibada yoyote. Shahidi namba tatu Bi. Zaidani Yusuph (66), aliileza Mahakama kuwa wakati alipokiwa ndani ya Msikitini Markaz Changombe kwa ajili ya ibada ya Itiqaf Oktoba 16 mwaka jana, aliona askari wanaume wakiingia upande wa wanawake usiku baada ya kuvunja geti na mlango wa Msikiti na kuanza kuwapiga. Shahidi huyo ambaye ni mshatakiwa namba nne, alisema kipigo alichopata kutoka kwa Polisi, alijeruhiwa kidole cha mguuni huku askari hao wakimtoa maneno ya kejeli. Kwa umri wangu huu sikufanya ubishi wowote, lakini walinipiga licha ya kuwauliza kosa langu ni nini, walizidisha kipigo na walifanya unyama mkubwa. Alisema Bibi huyo. Wakili wa Serikali Bw. Tumaini Kweka, alipomuuliza ni nani kiongozi wake akiwa kama Muislamu, Bi. Zaidan alijibu kwa kujiamini kuwa kiongozi wake ni Qur an na Sunna na hata alipoulizwa nani msimamizi wake alisema hana zaidi ya Qur an. Wakili Kweka alipomuuliza kama anaifahamu BAKWATA, Bi. Zaidani, alisema, Siijui, sitaki kuijua wala sitaki kuisikia, hata huyo Mufti, simjui. Akitoa ushahidi wake mbele ya Hakim Bi. Victoria Nongwa, shahidi namba tano, Juma (22), alisema ilimlazimu kuacha ibada zake majira ya saa tisa usiku mara baada ya kusikia vishindo nje, kwani geti lilivunjwa ukafuatia mlango wa msikiti na kisha aliona askari Polisi wakiingia ndani ya msikiti . Alisema mara baada ya kuingia msikitini walianza kuwapiga na kuamuru wafanye wanavyotaka wao. Aliongeza kuwa Walivamia bila kutoa tangazo lolote na kwamba, vurugu zao ndizo zilizokuwa ishara kuwa eneo hilo kwa muda huo halikuwa shwari. Alisema Juma. Naye alipoulizwa kama anaifahamu BAKWATA, alisema anaifahamu kuwa ni Taasisi ya Kiislamu kama zilivyo taasisi zingine za dini. Baada ya kuliizwa kama ana mahusiano na chombo hicho alijibu kuwa haimuhusu. Tukiwa ndani ya msikiti majira ya saa nane usiku kwenda tisa, tulisikia kishindo nje, kabla hatujakaa sawa tulisikia mlango wa msikiti ukibamizwa na mara waliingia askari kama wale(akionyesha baadhi ya askari FFU waliokuwa mahakamani hapo) na waliingia viatu vyao Msikitini. Alisema shahidi huyo namba tano, Bi. Farida Lukoko (53). Bi. Farida ambaye ni mshitakiwa namba 7, alionyesha Mahakamani hapo alama za majeraha mikononi mwake, alisema kuwa alipigwa marugu mikononi na mgongoni, jambo ambalo alidai kuwa hadi sasabado anasikia maumivu makali katika sehemu hizo. Alisema kipigo hicho kilimfanya asijitambue baada ya kuanguka chini. Baadaye alielezwa na wenzake kuwa alinyanyuliwa na askari hao kwa kushikwa miguu na mikono kisha kurushwa ndani ya gari. Shahidi mwingine ambaye ni mshitakiwa namba tisa Athumani Salim, alipoulizwa kama anaifaham Bakwata, alisema anaisikia tu, lakini inajishughulisha na nini, hajui. Alipoulizwa ni wapi anapta taarifa za kuandama kwa mwezi, alisema Waislamu wanafunga na kufungua kwa mujibu wa Quran na Sunna, popote unapoandama au kwa kukamilika kwa idadi ya siku katika mwezi huo. Naye shahidi namba nane Adama Ramadhani (40), aliulizwa na mwendesha mashtaka wa Serikali Bw. Kweka, kama anafahamu kazi za Bakwata, alisema anachojua kazi yake kubwa ni kuwatangazia Wa i s l a m u m w e z i w a Ramadhani unapoandama na pindi unapomalizika na si vinginevyo. Kwa ujumla Mashahidi wote walidai Mahakamani hapo kuwa, hakuna shahidi yeyote upande wa mashtaka aliyewataja kuwa ni wavamizi wa kiwanja wanachoshutumiwa kuvamia. Washatakiwa hao wameanza kutoa utetezi wao Jumatano wiki hii kufuatia Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Bi. Victoria Nongwa, Jumatatu wiki hii kusema Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49, wanakesi ya kujibu. Wa s h i t a k i w a w o t e wanakabiliwa na makosa

Habari

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 8 - 14, 2013

AN-NUUR

Maalim Seif awakumbusha Zanzibar OIC


Inatoka Uk. 1

manne, isipokuwa mshtakiwa namba moja (Sheikh Ponda) na mshtakiwa namba tano (Ust. Mukadam), ambao wanakabiliwa na mashtaka matano. Hakim Nongwa alisema pamoja na Mawakili wa upande wa utetezi kutoa maelezeo ya kina katika utetezi wao juu ya shauri hilo, Mahakama imeona ni vyema iwape nafasi washitakiwa waweze kupanda kizimbani kutoa utetezi wao. Mahakama inaona washtakiwa wote waliokamatwa katika kiwanja kile, ni vyema wapande kizimbani ili watoe utetezi wao, waseme sababu zilizofanya waingie pale. Alisema Hakimu Nongwa. Kwa mujibu wa Wakili wa upande wa utetezi Bw. Juma Nassoro, ameileza mahakama hiyo kuwa jumla ya mashahidi sitini wataka mahakani hapo kutoa ushahidi wao upande kwa upande wa utetezi.

Serika l i y a Z a n z i b a r, aliongeza kuwa iwapo Zanzibar ingepata fursa ya kuwa mwanachama wa OIC, ingekuwa mbali kiuchumi kwa vile Jumuiya hiyo imekuwa ikichangia sana maendeleo ya kiuchumi kwa nchi wanachama. Maalim Seif alieleza hayo katika viwanja vya Jamhuri Jimbo la Makunduchi, wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliotishwa na Chama hicho hivi karibuni. Kielezea kusikitishwa kwake na kitendo cha Zanzibar kukoseshwa Uanachama wa Jumuiya hiyo, alisema kitendo cha Zanzibar kuzuiwa kujiunga na jumuia hiyo huenda ni mpango maalum ulioandaliwa wa kuipotezea Zanzibar umaarufu duniani. Zanzibar ndio dola kongwe zaidi katika ukanda huu wa Kusini mwa Afrika, lakini tumepoteza umaarufu wetu, alieleza kwa masikitiko. Alielezea kusikitishwa kwake na vitendo vya baadhi ya viongozi wa upande wa pili wa Muungano, kwa kutoithamini Zanzibar

na kuipotezea haki zake ambazo ingepaswa kuzipata. Maalim Seif alitoa mfano wa ujio wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, ambaye alizuru nchini siku za hivi karibuni na alipowasili nchini Rais Mwai Kibaki wa Kenya. Alisema wageni wote hao hakuna aliyepelekwa Zanzibar na kuelezea kasoro hiyo kuwa ni miongoni kwa vitendo vinavyoinyima Zanzibar fursa. Pamoja na yote hayo, lakini Wawakilishi wa Zanzibar walitakiwa waende wakatoe maoni y a o m b e l e y a Wa z i r i huyo wa Oman, lakini kwa masikitiko makubwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania aliyapuuza maoni na mapendekezo ya Wazanzibari. Sijui inakuwaje Waziri wa upande mmoja anaweza kuiamulia nchi yenye Rais, alieleza na kuhoji. Maalim Seif alifahamisha kuwa mambo yote hayo yanatokana na Zanzibar kutokuwa na mamlaka kamili na kwamba, wakati umeka sasa kwa Wazanzibari kuungana

Inaendelea Uk. 4

Habari

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 8 - 14, 2013

AN-NUUR

Ni usiku wa Itiqaf T.I.C Kichangani kesho


Na Bakari Mwakangwale

WAISLAMU kutoka sehemu mbalimbali nchini, wanatarajiwa kufanya ibada maalum ya Itiqafu kesho, katika Msikiti wa Kichangani T.I.C Magomeni, Jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kutawakali kwa Mwenyezi Mungu na kuomba dua maalum kutokana na matatizo ya kiimani yanayoendelea nchini. Kwa mujibu wa taarifa

Kuhifadhisha watoto Quran ni kujenga maadili mema


Na Bakari Mwakangwale

kutoka kwa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T), imeeleza kwamba Itiqafu hiyo itaanza msikitini hapo majira ya saa tatu, usiku wa Jumamosi (Kesho) kuamkia siku ya Jumapili. Itiqafu hii imeandaliwa na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu itaanza majira ya saa tatu usiku wa Machi 9, mpaka Machi 10, Alfajiri. Viongozi na wajumbe kutoka mikoani watahudhuria Itiqafu hiyo. Imesema taarifa hiyo. Mmoja wa viongozi

wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T), aliyejitambulisha kwa jina moja la Abdallah, alisema itiqafu hiyo itatanguliwa na Semina na mkutano wa viongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini utakaofanyika katika Hoteli ya Lamada Ilala Boma jijini. Semina hiyo itafanyika siku ya Jumamosi kesho Machi 9, 2013, kuanzia majira ya saa tatu asubuhi mpaka saa nane mchana. Taarifa hiyo ya Jumuia na

Taasisi za Kiislam nchini, ilieleza kuwa hivi sasa inafahamika kwamba nchi yetu inapita katika kipindi kigumu cha mahusiano ya kidini. Ta a r i f a i m e e l e z a kuwa kutokana na hali ilivyo, viongozi wa Dini ya Kiislam, wameona kuwa wana wajibu wa kukutana ili kuelimishana na kujadili hali hiyo, na hatimae kuishauri serikali na Watanzania namna bora ya kuimarisha mahusiano ya kidini.

Tayari Jukwaa la Waislam Tanzania (Tanzania Muslim Forum), limekamilisha maandilizi kwa ajili ya Semina na Mkutano wa Viongozi hao, lengo likiwa ni kuelimishana na kujadili hali ya kulegalega kwa mahusiano ya kidini nchini, na kutizama ni namna gani hali hiyo itaepukwa. Mkutano huo utahudhuriwa na Masheikh n a Vi o n g o z i k u t o k a Jumuiya mbalimbali za Kiislam kutoka jijini Dar es Salaam na mikoani.

WAZAZI wa Kiislamu wametakiwa kutoa kipaumbele kwa watoto wao kuihifadhi Quran, ili iweze kuwajenga katika maadili mema na kuwaepusha vitendo vibaya. Wito huo umetolewa na Ustadhi Mbwana Urari, wa Taasisi ya Afrika Muslim Agency, wakati akiongea mara baada ya mashindano ya kuhifadhi Quran kwa vijana wa Kiislamu, yaliyofanyika katika Msikiti wa Makukula Buguruni, Jijini Dar es salaam. Ustadhi Mbwana, alisema katika Ulimwengi wa sasa wazazi wanawahimiza kuwapeleka watoto wao katika Madrasa ambazo zinahifadhisha Quran, ili wasije kujiingiza katika mambo yasiyoendana na maadili mema. Alisema hivi sasa maadili na nidhamu katika jamii yamemomonyoka kwa kiasi kubwa, lakini njia pekee ya kujenga na kurudisha maadili hayo ni kuwafundisha watoto dini yao kupitia katika Madrasa zinazo hifadhisha Quran. Alieleza kuwa madhumuni makubwa ya kuandaa mashindano hayo, ni kuwafanya vijana wa Kiislamu kukijua kitabu chao kitukufu cha Quran kupitia njia ya kuzihifadhi aya za Quran katika vifua vyao. Alisema kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi

Mungu kifuani katika umri mdogo, ndiyo njia ambayo ikitumiwa na wanazuoni wakubwa. Hii ni njia ambayo imefundishwa na Mtume (s a w), ikafuatwa na Maswahaba wa Mtume. Na sisi vilevile tunaiendeleza njia hiyo ili kuienzi na kuilinda Qur an, mbali na kuifanya jamii kuishi katika misingi ya maadili mema yenye nidhamu ya kumjiua Mwenyezi Mungu Alisema Ust. Mbwana. Aidha aliwasihi vijana wa Kiislamu wanapaswa kutambu kwamba, kuhifadhi na kuisoma Quran ni kwa manufaa yao hapa duniani na kesho akhera. Kutokana na sababu hiyo, aliwataka wanafunzi hao waelewa kwamba, wanapohimizwa kusoma, basi waichukue rai hiyo kwa kwa uzito kwani elimu pekee ndiyo itakayo wajengea maisha mazuri hapa duniani na kesho akhera. Akizungumzia hatua ya Taasisi ya Afrika Muslimu Agency kugawa vitabu bure kwa Waislamu, Ust. Mbwana alisema lengo ni kurahisisha kutoa mafundisho ya Kiislamu, ili jamii iweze kuujua Uislamu wao kwa urahisi. Tu n a g a w a v i t a b u vyenye mafunzo ya Uislamu bure, ikiwa ni katika muendelezo ule ule wa kutaka Waislamu wayajue mafunzo

mbalimbali ya dini yao bure bila ya gharama yoyote ile. Alisisitiza Ust. Mbwana. Katika kilele hicho cha mashindano ya Quran, Waislamu waliweza kupata vitabu mbalimbali vyenye mafundisho ya Uislamu kama vile Mwanamke katika Twahara, stara ya mwanamke (Hijabu), ambavyo viligaiwa na Taasisi hiyo. Mashindano hayo ni mfululizo wa kazi za kila siku za Kiislamu ambazo hufanywa na Taasisi ya Afrika Muslim Agency. Naye Ustadhi Shaaban Hijja wa Masjid Makukula, Buguruni Jijini Dar es salaam, katika hotuba yake ya swala ya Ijumaa Msikitini hapo, alisisitiza suala la Waislamu kuipigania dini yao kwa hali na mali. Alisema Mwenyezi Mungu alishafahamisha kuwa biashara ambayo itawaokoa watu na adhabu yenye kuumiza ni kumuamini Allah (s.w) na Mtume wake, kisha kupigania jihadi dini ya Mungu. Akifafanua zaidi, Ustadhi Hijja alisema jihadi ina mapana yake na kwamba, haina maana tu ya kuitetea dini kwa silaha, bali hata kuhifadhisha watoto Quran na kuwapa elimu kwa ujumla nayo ni jihadi.

Alisema, suala la kuhifadhisha watoto Qur an, huchukuliwa kama ni

Maalim Seif awakumbusha Zanzibar OIC


Inatoka Uk. 3 wakulima kwa kuongeza tija na kupata maendeleo kwa kipindi kifupi. Amewataka viongozi wa mkoa wa Kusini Unguja kuwaunga mkono wataalamu wa kilimo hicho, ili waweze kuwaelimisha wakulima wengi zaidi k atika eneo

jambo dogo, lakini katika Uislamu ni jambo kubwa na lina uzito wake.

ili kuweka mustakbali mwema wa nchi yao. Akielezea kuhusu demokrasia ya vyama vingi, Maalim Seif aliwataka wananchi kuwa huru kuitumia fursa hiyo kwani ni haki yao ya kikatiba.

Amesema kila mtu yuko huru kujiunga na chama chochote cha siasa na kuwa na imani ya dini anayoitaka bila ya kuingiliwa katika maamuzi hayo. Hatua hiyo imekuja baada ya aliyekua kaimu Katibu wa Vijana wa CCM Wilaya ya Kusini Bw. Muaze Haji, kujiengua katika chama hicho na kujiunga na CUF. Akizungumza katika mkutano huo Bw. Muaze alisema hakushawishiwa na mtu kujiunga na CUF bali ameamua baada ya kuona kuwa anachokipigania Maalim Seif kina maslahi kwa Wazanzibari wote. Kabla ya mkutano huo Maalim Seif alitembelea shamba la kisasa la kilimo cha migomba la Bw. Haji Kinazi, ambapo alieleza kuwa kilimo hicho kinaweza kuwakomboa wakulima kwa kuongeza uzalishaji na kukuza kipato chao. Alisema iwapo kilimo hicho kitaendelezwa, kitaweza kuwakomboa

hilo na mikoa mengine ya Zanzibar. Kwa upande wake mkulima wa kilimo hicho bw. Haji Kinazi, amesema tayari ameshaona mafanikio ya kilimo hicho na kwamba anakusudia kukiendeleza zaidi ili aweze kujikomboa kiuchumi. Alisema tatizo kubwa lililokuwa likimkabili ni uhaba wa maji, lakini hivi sasa wanaimarisha miundombinu ya maji na kuendeleza kilimo hicho kwa uhakika. Naye mtaalamu wa kilimo hicho Bw. Omar Mohd alisema, mazao yatokanayo na kilimo hicho cha kisasa ni mazuri na yanaweza kuleta tija kubwa
kwa wakulima. Amesema kupitia utaalamu huo, migomba inaweza kustahamil i maradhi na

ukame na kuwawezesha wakulima kupata mazao mengi yaliyo bora ambayo wanaweza kusarishwa nje ya nchi.

Mholanzi aliyekuwa anauchukia Uislamu asilimu


Ukurusa wa twitter wa Mholanzi aliyesilimu Arnoud van Doorn, ambaye ni mwanasiasa maarufu wa Uholanzi aliyekuwa mstari wa mbele kwa chuki dhidi ya Uislamu, sasa amesilimu. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la IQNA, Arnoud van Doorn, ambaye alikuwa katika chama kimoja na Geert Wilders, Mholanzi anayeendesha harakati za chuki dhidi ya Uislamu, sasa amesilimu baada ya kuutambua Uislamu kama njia ya haki maishani. Tovuti ya islamic-events. be imechapisha taswira ya akaunti ya ukurusa wa kijamii wa twitter wa van Door, chini ya anuani ya mwanzo mpya ambapo pia shahada mbili zimeandikwa kwa lugha ya Kiarabu. Awali ilikuwa vigumu kwa Waislamu wengi Ulaya kukubali kuwa mwanasiasa huyo aliyekuwa na chuki kali dhidi ya Uislamu amesilimu. Lakini von Doorn mwenyewe amethibitisha ukweli wa habari za kusilimu kwake. Amesema kukubali kwake

Habari za Kimataifa

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 8 - 14, 2013

AN-NUUR

OIC kuanzisha mfuko kulinda matukufu ya Kiislamu


Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu (OIC), imetangaza kuwa imeamua kuanzisha mfuko wa fedha kwa ajili ya kutetea na kulinda dini ya Kiislamu na matukufu yake. Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano cha OIC yenye makao yake huko Jeddah Saudi Arabia, Essam al Shant, amesema kuwa Jumuiya hiyo inafanya juhudi za kuanzisha mfuko wa fedha kwa ajili ya kulinda na kuitetea dini ya Kiislamu, shaksiya na matukufu ya dini hiyo kwa kuungwa mkono na wanachama wake, pia na sekta

Sudan yaituhumu Uganda kuwa ni tishio kwa amani


KHARTOUM Serikali ya Sudan imesema kuwa, Uganda ni tishio kwa amani na uthabiti wa nchi hiyo. Abubakar Al-Siddiq Muhammad Al-Amin, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Kigeni wa Sudan ameituhumu serikali ya Kampala kwamba, imekuwa tishio kwa amani na uthabiti wa nchi hiyo. Abubakar Al-Siddiq Muhammad Al-Amin, amesisitiza kwamba siasa ambazo Uganda inazifuata pamoja na uchochezi wa Kampala ni tishio kwa amani na uthabiti wa Sudan na eneo lote la Ukanda wa Maziwa Makuu. Msemaji huyo wa Wizara ya Mambo ya Kigeni ameongeza kuwa, hatua ya serikali ya Uganda ya kuwapatia hifadhi viongozi na wapiganaji wa makundi yenye silaha, inahatarisha usalama na amani wa eneo hilo. Ameongeza kuwa serikali ya Khartoum ikishirikiana na asasi za eneo hilo la Afrika na za kimataifa, itaendelea na juhudi zake za kuchua hatari za siasa za Uganda. Aidha Bw. Abubakar Al-Siddiq amesema mwezi Julai mwaka huu, Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu watakutana katika kikao chao nchini Angola, kwa lengo la kujadili mashtaka ya Sudan dhidi ya Uganda, kuhusiana na suala la Kampala kuwapatia hifadhi wapiganaji wa makundi ya waasi.

Uislamu ni suala binafsi na hivyo kwa sasa hataki kulijadili zaidi.

Somalia yadai iko tayari kuzungumza na al Shabab


MOGADISHU Rais Hassan Sheikh Mahmoud wa Somalia ametangaza kuwa yuko tayari kufanya mazungumzo na kundi la wanamgambo wa al Shabab la nchini humo. Hata hivyo akizungumza na vyombo vya habari mjini Doha Qatar, Rais Hassan Sheikh alisema mazungumzo hayo hayatawashirikisha w a n a m g a m b o ambao wanasakwa na taasisi za kimataifa au wanaokabiliwa na tuhuma

binafsi. OIC imesema kuwa kufuatia pendekezo lililotolewa na Kuwait la kuasisi mfuko huo wa fedha, Jumuiya hiyo sasa inajiandaa kuunda timu ya ufuatiliaji, kwa ajili ya kuainisha fedha zinazohitajika kuanzisha mfuko huo. Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano cha Jumuiya hiyo, amesema kuwa mfuko huo ambao makao yake makuu yatakuwa nchini Kuwait, ni mfuko wa wakfu na kwamba utakuwa ukitetea na kuilinda dini ya Kiislamu na matukufu yake pamoja na shakhsia wa Kiislamu. (IRIB)

RAIS Omary El-Bashir wa Sudan

za kutenda jinai za kivita. Aidha Rais huyo amesema kuwa, amefanya mazungumzo na Amir wa Qatar juu ya masuala yanayohusu mahusiano ya pande mbili, na kimataifa. K u n d i l a wanamgambo wa al Shabab linalotuhumiwa kufungamana na mtandao wa al Qaeda, linadhibiti baadhi ya maeneo katikati na kusini mwa Somalia, na mara kadhaa limekuwa likipambana na vikosi vya serikali na vile vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika AMISOM.

Makala

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 8 - 14, 2013

AN-NUUR

Na Mwandishi Maalum

Zanzibar imtafute James Bond


tumepata habari ya kuuwawa kwa risasi kwa Padiri Paroko ya Mkunazini Bwana Evaristo Mushi, aliyeuwawa na watu wasiojulikana huko Mtoni Betrasi majira ya asubuhi ya Jumapili tarehe 17 Februari, 2013. Kitendo cha mauwaji haya ni cha kinyama na hatuna budi kukilaani kwa Nguvu zote, bila kujali imani, rangi, kabila wala dini. Ni kitendo cha kukilaani kwa sababu si kitendo cha kiungwana kwa upande mmoja na kwa upande wa Pili, ni matokeo ya tendo hili, hasa hapa Zanzibar, tena kipindi hiki cha machafuko ya fitina za kiudini mseto sanjari na siasa, basi yatatufika makubwa, kwa kutokea jambo hili lilofanywa na maharamia wasiojulikana kwa sasa. Yatatufika makubwa kwa sababu yaelekea kuna mpango maalum ulioandaliwa, na hatujui ni akina nani, wanaolenga kutugombanisha na kututia nakama kutoka kwa mataifa yenye nguvu, na tena yaliyokuwa hayana Imani na mataifa ya Kiislamu yote duniani. Zanzibar ni moja kati ya mataifa ambayo baada ya Somalia, na bara Arabu kubomolewa na Mayahudi na manasara, ndio iliyobaki na kuna kila

K WA w a l e w e n g i waliokuwa washabiki wa sinema miaka ya 1960, sina shaka wanamkumbuka sana muigizaji mmoja wa Kiingereza anaejulikana kwa jina la kisanii kama James Bond, 007. James Bond ni kachero wa kufikirika katika hadithi na maandiko ya awali ya mwandishi Ian Flemming. Kachero huyu amechorwa kuwa ni ngao na nguzo ya ufumbuzi wa siri zenye utata mkubwa na kuhatarisha usalama wa nchi ikiwemo Uingereza. Kwa jinsi alivyo na uwezo mkubwa wa kuitambua kazi yake na kuifanya vilivyo, James Bond, hupambana na makundi ya watu wabaya wenye nia ya kuvuruga amani na usalama wa watu duniani. Kabla sijaporoja sana na kuacha njia niliyokususdia, naomba niwatambulishe kuwa makala hii inakuja kwa kumnasibisha muhusika James Bond, na hali ya hujuma na fitina iliyoelekezwa katika visiwa vya Zanzibar na wananchi wake, hasa mara tu baada ya muamko mkubwa wa wananchi kudai haki zao za kimsingi katika Muungano. Muda mfupi uliopita,

WANANACHI wa Zanzibar wakiwa katika moja ya mikutano yao ya hadhara iliyowahi kufanyika visiwani humo. [Picha kutoka Maktaba yetu] dalili kuwa zamu yetu ya kuhujumiwa imeka. Labda sasa, niwarudishe tena nyuma kidogo kwenye kichwa cha habari. Nilisema tunahitaji James Bond, na hili nisieleweke kwamba nimemsahau Mola, hapana, namtumia James Bond kisanii zaidi ili kutoa ujumbe wangu niliokusudia. Nje ya hapo nabaki na imani kamili kuwa ni Mungu pekee atakaetuokoa na hujuma hizi. Nafikiri kwa hili nimefahamika, kwa wale waumini . Muundo wa fitina na hujuma tuliyopangiwa Zanzibar unafanana na ile hujuma iliyopangwa na kikundi kimoja cha maharamia waliojificha katika Pango la Volcano (Crater) kule Japan, katika filamu ya James Bond ya mwaka 1967, inayoitwa You only live twice, ambapo muhusika mkuu James Bond (Sean Connery) anatumwa kufuatilia kadhia hio. Filamu inaanza kwa satalaiti moja ya Marekani iliyokwenda katika sayari ya Venus, kumezwa na satalaiti nyengine iliyokuwa na nembo ya Urusi (USSR). Tukio hili lilizua mtafaruku mkubwa ambapo Marekani walimshutumu Mrusi kwa hujuma hii. Mrusi alikataa kata kata kuhusika na hujuma hii lakini Marekani ilionya kuwa iwapo tukio kama lile litatokea tena, basi kutazuka vita kuu ya tatu ya dunia. Kadhia hii kwa vile ilikuwa ikipangwa na kikundi cha waasi waliojificha milimani kwenye pango la mlima wa volcano, watu waasi wasioitakia mema dunia, na watu wasio na hatia, lilikuwa jaribio la hujuma gumu kubainika. Kwa hali hii uwezekano wa kutokea vita ulikuwa mkubwa kwani chanzo cha tatizo kilikuwa hakijajulikana hasa. Kwa bahati nzuri, Serikali ya Uingereza ikamnasihi Mmarekani kuwa haioneshei kwamba Urusi walihusika na ikaahidi kufatilia. Kama kawaida, Uingereza ilimtuma James Bond (Sean Connery) kwenda Japan kufuatilia ukweli. Hali ilikwa ngumu lakini kwa ujasiri mkubwa Bond, aliweza kuibaini njama na tina iliyokuwa imepangwa kuwagombanisha Marekani na Urusi na kuipatia ufumbuzi sekunde chache kabla ya satalaiti ya pili kuliwa tena na satalaiti ya adui. James Bond akaoka dunia na maafa makubwa. Sasa kwanini tunamhitaji aje na huku? Naam, kwa muda mrefu sana kuna dalili nyingi na majaribio mengi ya kuiharibia jina Zanzibar kwa kupitia visingizo vya Uislamu wenye msimamo mkali. Kisa na sababu, Wazanzibar wamedai nchi yao. Hichi ndicho kilichowachongea. Tumeona kuanzia kutekwa kwa Ustadh Farid, Mungu akatuokoa na maafa. Akamwagiwa tindikali Soraga, Mungu akasimama nasi. Kapigwa Risasi Padre Mkenda, tukaponea chupu chupu. Haya ni moja ya majaribio machache tu yanayaonasibishwa na Uisilamu ili kuichafua Zanzibar na kuondoa amani iliyopo, inayofanywa na kikundi maalum chenye nia mbaya ya kuhujumu Uislamu na ustawi wa Z a n z i b a r. Tu m e o n a matukio ya maandamano na fujo za kutiwa moto makanisa, maskani, kuuliwa polisi Bububu, zote hizo ni tna na hujuma chini ya mwavuli mmoja ambao ni James Bond tu angeweza kuuchuwa kwa sasa, ukitoa Muumba. Kwa upande mwengine, likuepukalo lina heri nawe na likufikalo lina heri pia, wakati anauwawa padre Mushi, viongozi kadhaa wa Uamsho wako Rumande kwa miezi, na hata harakati zao zimekufa. Sasa kisingizio kitatolewa

TANGAZO! TANGAZO! TANGAZO! SHAMBA LINAUZWA


SHAMBA LA EKARI 14 LINAUZWA KWA HARAKA LIPO CHAMAZI-DOVYA DAR ES SALAAM BEI NI MAELEWANO KWA MAWASILIANO: PIGA SIMU: 0759 450425 0784 463207 0754 479783 WAHI MAPEMA BAHATI NI YAKO

Usipokunywa vodka utaishia kushabikia mpira!


Na Dr. Noordin Jella
M WA N A FA L S A FA (Philosopher) wa Urusi Mr. Lev Tostov aliwahi kusema hivi Serikali yoyote ile duniani inafanana sana na raia inayowatawala, haiwezekani raia wawe wa aina moja, na serikali iwe ya aina nyingine. Hayo ni maneno yaliyowahi kutolewa na mwandishi maarufu wa vitabu na mwanafalsafa wa Kirusi ambaye kazi zake zinaheshimika duniani kote. Urusi ni nchi ambayo muda mwingi ni wakati wa baridi, kipindi cha baridi ni miezi tisa na miezi ya joto ni miezi mitatu tu katika mwaka mzima. Kulingana na hali ya hewa ya nchi hiyo na pia ukizingatia siasa za kikomunist ambazo kama nilivyowahi kusema hapo awali kwamba ni siasa za matabaka kati ya watawala na watawaliwa; siasa za kudhibitiana kwamba usikiri wala usifanye kama utakavyo, bali ukiri na kufanya kama ambavyo serikali inavyotaka; ili kutimiza lengo lake la kuwadhibiti raia wa Urusi na kufanya yale waliokuwa wamekusudia serikali ikitumia kitengo chake cha usalama wa taifa wa nchi hiyo (KGB) iliweza kuweka mikakati ya kuwadhibiti wananchi kwa kuwafanya wawe walevi muda wote, na washindwe kufuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yanaendelea katika nchi yao. Serikali ilijenga viwanda vingi vya kutengeneza pombe kali ya vodka na kujenga vibanda kila mita mia moja vya kununulia vodka hizo kwa kutumbukiza senti tano na kupata glasi moja ya vodka! Kulingana hulka hii kila mtu akawa mlevi na mwisho Urusi ikabakia kuwa taifa la walevi na huku wakomunist wakiendelea kulisadi taifa hilo. Wanafunzi wa kigeni waliokuwa wanasoma Urusi enzi hizo walikuwa walevi na baadaye kuanzisha timu za kunywa pombe; hivyo kukawa na ligi ya kuchuana ni nchi gani inakunywa vodka kuliko nchi nyingine! Kwenye mashindano ya ligi hii waliokuwa wanachukuwa kikombe mara kwa mara walikuwa ni Zambia, Uganda na Zimbabwe. Nilipofika Urusi kwa mara ya kwanza nilifuatwa na wenyeji niliowakuta huko na swali

Makala

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 8 - 14, 2013

AN-NUUR

la kwanza kuulizwa ni kama ninakunywa pombe au sinywi; wakiwa na maana kama nakunywa nijiunge na timu yao ya kunywa vodka! Na niliposema sinywi nikawa nimewavunja moyo kwa vile wamekosa mchezaji mpya. Na ndiyo maana wanafunzi wengi toka Urusi miaka ya nyuma walikuwa wakirudi nyumbani ni walevi wa kupindukia. Watanzania siyo walevi wa vodka kama vile wenzetu wa kule Urusi hii pia inachangiwa na hali ya hewa. Tanzania ni nchi ya joto kali, na vodka ni pombe ambayo ukiinywa lazima mwili unawaka moto, lakini pamoja na kwamba sisi siyo walevi wa vodka ila sisi tumeingia katika ulevi mwingine wa kushabikia mpira! Ushabiki wa mpira umekuwa kama ugonjwa wa kuambukiza ambao umesambaa kwa kila Mtanzania haijalishi anaishi mjini au kijijini; ushabiki wa mpira umekuwa ugonjwa ambao umesambaa mpaka kwenye damu zetu (football maniac). Kila kona ukipita ni matangazo ya kuonyesha mechi za mpira wa ligi za Ulaya, na serikali imetutengenezea kitu kinachoitwa digitali hivyo watu wote wamesahau kila kitu isipokuwa mpira wa ligi

ya Ulaya ndiyo taswira ya taifa sasa hivi. Watu wa rika tofauti wote kwa pamoja kra zao zote zipo kwenye ligi ya Ulaya. Afadhali hata basi tungelikuwa tunashabikia ligi ya kwetu hapa nyumbani ili tuweze kukuza kiwango cha mpira cha nchi yetu kwa kuchangia na kununua bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na vilabu vyetu hapa nyumbani! Lakini cha kushangaza sisi tunashabikia vipaji vya nchi zingine na watu wengine wamediriki hata kutoa michango yao kwa vilabu vya huko Ulaya wakati timu zetu hapa zinadoda! Kama ambavyo nimesema kwamba tatizo hili la ushabiki wa mpira kwa vilabu vya Ulaya si kwa watu wazima tu basi, hapana, hata watoto wadogo wamepumbazwa sana na ligi ya Ulaya; na kwa kuthibitisha maneno yangu haya nadhani mnakumbuka hata kwenye matokeo ya mtihani ya kidato cha nne wanafunzi wengi wamechora picha za wachezaji wa mpira wa ligi ya Ulaya kama vile Messi na mengineyo! Warusi wao walikuwa wajanja pamoja na kwamba waliwaruhusu watu wote wanywe vodka ili waweze kufanya walivyotaka, lakini walikuwa makini

sana kutokuwaruhusu watu wote wenye akili na vipaji mbali mbali kunywa vodka, walikuwa hawaruhusiwi kabisa labda kama ni kwenye sherehe tu basi na pia siyo kwa kiwango cha kulewa. Walioruhusiwa kunywa

mpaka kujikojolea ni wale watu wa kawaida wasiokuwa na umuhimu sana katika kukiri juu ya hali ya uchumi na maendeleo ya nchi kwa ujumla. Sasa sijui sisi serikali yetu inakiria nini kuhusu ushabiki huu wa mpira wa ligi ya Ulaya ambao sasa umegeuka kuwa siyo starehe tu, bali pia umekuwa ni sehemu ya maisha ya Watanzania na sehemu ya elimu muhimu kwa vijana wetu wanaosoma shule za msingi na sekondari! Watoto wengi wanashinda kwenye vibanda vinavyoonyesha ligi za mpira wa Ulaya hata wakati mwingine wa masomo, na jioni badala ya kujisomea pia wapo mbele ya runinga wanaangalia mpira! Najua serikali inakusudia nini kuhusu hili, lakini imekusudia vibaya kwa vile hata kama imeamua kutudhibiti sisi wazazi ambao ni watetezi wa taifa la leo, lakini ni kwanini isione kwamba si haki kukidhibiti pia kizazi cha kesho! Warusi nao pia walikuwa wakomunist lakini siyo kila mtu aliruhusiwa kunywa vodka, hapana. Sasa sisi mbona wote tumefunguliwa TV tuangalie ligi ya mpira ya Ulaya wakati twiga na dhahabu vinayoyomaa!!!??? Ndiyo maana nasema usipokunywa vodka utaishia kushabikia mpira.

TANGAZO
VITABU VIPYA VYA MIHADHARA, MASWALI NA MAJIBU BAINA YA WAHADHIRI WA KIISLAMU NA WACHUNGAJI, PAMOJA NA MAWAIDHA YA SHEIKH NURDIN KISHKI. VINAPATIKANA MSIKITI WA MTORO (DUKANI KWA SAIMU) KARIAKOO. PIA VINAPATIKA KATIKA MADUKA YOTE YA VITABU VYA DINI JIJINI DAR ES SALAAM, KWA JUMLA NA REJAREJA. PATA NAKALA YAKO SASA. 0713 47 10 90, 0685 47 10 90, 0773 19 46 6.

TANGAZO

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 8 - 14, 2013

AN-NUUR

Makala

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 8 - 14, 2013

AN-NUUR

MUHESHIMIWA Rais Mstaafu, Al Haj Mzee Ali Hassan Mwinyi, amependekeza Masheikh na Maaskofu wakutane wazungumze kuhusu kule kusuguwana kulikojitokeza hivi karbuni. Hakika ndugu Wakristo wamezua makubwa hivi karibuni na lawama zimelengwa kwa Waislam. Mkristo alikojolea Qurani, Waislam walitoa taarifa Polisi kwa kuwa kitendo hicho ni jinai kwa sheria za nchi. Lakini huko Polisi, kwa sababu wanazozifahamu wenyewe, ambazo si kazi kubwa kutanabahi ni zipi, wao walijichelewesha kuchukua hatua za kisheria zinazotakikana. Kwa ujinga wao Waislam wakapoteza subra na kuchukua sheria mikononi mwao na matokeo yake yakawa vurugu tupu, Waislam wakilaumiwa kwa mkasa huo. Kiongozi wa Polisi angetegemewa kusema ukweli wa mambo yalivyokuwa, lakini yeye alitangaza tu, kuwa amechoka na wafanya fujo. Hakuwataja hao wafanya fujo ni kina nani lakini mtu yeyote yule mwenye akili ya kukiri, haingekuwa kazi kubwa kutambua kuwa hao ni Waislam. Imekuwa ni ajabu kubwa sana humu nchini kuzuka rabsha kati ya Waislam na Wakristo kwa sababu ya kuchinja wanyama, ambao nyama zao zinauzwa katika mabucha. Mimi sasa ni mzee na maisha yangu yote nimeyamalizia nchini humu; haikutokea hata siku moja Wakristo wazue ugomvi kwa sababu ya kuchinja. Rafiki yangu Mchaga kanieleza kuwa huko kwao kila siku wamependelea Muislam awachinjie ngombe ama mbuzi wa chakula. Kwa mila zao, wao hawawezi kula

Na Khalid S Mtwangi

nyama iliyochinjwa na mwanamume ambaye hakutahiriwa. Kwa hiyo hata kwa Mchaga mwenzao mwanamume, hawawezi kuwa na uhakika kabisa kuwa huyo bwana katahiriwa. Kwa zaidi ya asilimia tisini na tisa mwanamume mtu mzima Muislam atakuwa katahiriwa. Hivyo wako tayari kula nyama iliyochinjwa na Muislam kwa sababu wana uhakika kuwa imechinjwa kihalali na mtu mwenye tohara. Inatambulika kuwa waliozua balaa la kuchinja ni baadhi ya wafuasi wa madh-hebi hizi za Pentecost wanaofadhiliwa sana na Born Again wa Marekani. Watu hawa ndio mwanzo wa mauwaji makubwa yaliyokuwa yakitekelezwa na viongozi kama vile Bw. George H Bush, aliyekuwa Rais wa Marekani, aliyeapa kueneza Vita Vya Msalaba. Pia itambulike kuwa hawa Born Again (hakika wanaitwa FUNDAMETALISTS) hawataki kabisa kusikia kuwa kuna Uislam n a U k ato li k i d u n i an i kiasi kwamba, Papa wanamtuhumu kuwa anaeneza ushirikina (wanamwita purveyor of superstition). Tazama website za kina Pat Robertson ama marehemu Jerry Falwell. Haya waliyozuwa hawa wanaotaka wawe wanachinja, wamezua sokomoko huko Geita mpaka yakatokea maafa kwa Mchungaji kauawa. Halafu yametokea mauaji ya Fr. Evarist Mushi, huko Zanzibar. Inasikitisha sana kuwa bila kuwepo ushahidi wowote, lawama za mauwaji hayo wametwikwa Waislam kama waumini wa Uislam. Maana yake sio kama aliyetenda kitendo hicho ni muhalifu ambaye ana jina la Kiislam, la. Inaelekea kuwa aliyeuwa ni Muislam na aliyefanya uhalifu huo ameutekeleza kwa sababu ya Uislam wake. Shutuma hizo hazikutoka kwa Wakristo tu bali baadhi ya Masheikh nao walijitosa kwa hoja na aya za Qurani kumlaani huyo Muislam ambaye mpaka sasa hajajulikana. Maaskofu na Wakristo wote kwa ujumla wamefarijika sana! Masheikh wamewafariji

Masheikh na Maaskofu kukutana

MZEE Ali Hassan Mwinyi

MAALIM Ally Bassaleh

ASKOFU Alex Malasusa

Wakristo na kuwahuzunisha wafuasi wao Waislam. Kufuatana na matokeo haya machache yaliyoorodheshwa, ni rahisi kufikia maamuzi kuwa kweli kumetokea msuguwano kati ya Wakristo na Waislam. Hali kama hiyo hakika inaweza kuwa hatari sana kwa nchi hii. Isipokuwa ikumbukwe kuwa WaTanzania, na hasa WaTanzania Waislam ni wastahmilivu sana na kwa kawaida huheshimu sana sheria na viongozi. Mafunzo yao ya MADRASA yanawafanya wawe na heshima kwa walio viongozi wenye madaraka. Hii ni kweli kabisa ingawa kunaweza kutokea wasomaji wasikubaliane na hoja hiyo. Waislam wamekuwa wakiitwa kuwa ni docile (wanyonge sana). Kweli hali hiyo imeanza kubadilika lakini hayo ni kwa sababu kila kitu kina mwisho wake. Wanaelewa kuwa huko nyuma wametumiwa sana kwa maslahi binafsi na kusimika Ukristo. Wanamkumbuka kwa dhati Al Marhum Sheikh Mzee Takdir, mpiganaji shupavu wa uhuru. Mabadiliko hayo kwanza yamedhihirika katika mihadhara waliyokuwa wakiihubiria katika miaka ya tisini. Hii iliwaudhi sana Wakristo na ajabu ni kwamba, wale wasomi ndio waliokuwa wakiudhika zaidi, kuliko Wakristo wa kawaida ambao walipendelea sana kuendesha mijadala kwa hoja, wakishindana na hawa wahadhiri wa Kiislam. Lakini kukasirika kule

ilidhihirisha kiasi Waislam walivyokuwa wakionewa kila siku kuwa wao ni docile. Lakini ikumbukwe huko nyuma kulikuwa na mihadhara mingi ya wahubiri Wakristo wengi walikuja nchini humu na waliyokuwa wakiita kwa mfano September crusade na kadhalika. Mihadhara hii ya Wakristo nayo wahadhiri wake walikuwa wakijaribu kuuchambua Uislam wakipotosha mafundisho ya dini hiyo ya kweli ya Allah. Waislam hawakulalamika kusema kuwa Uislam ulikuwa ukikashfiwa. Bado hata hivyo wale waliosoma maandishi kama vile kitabu WANA WA IBRAHIM walifahamu kiasi gani si tu, Uislam ulikuwa ukikashwa bali hata Rasulul-Llah Muhammad (SAW) alikuwa akidharauliwa. Na kwa hakika Wakristo wengi hawamkubali wala kumuamini Muhammad (sw). Imeandikwa kuwa Uislam hauwezi kuwa ni dini ya kweli kwa sababu Warabu, akiwemo Mtume Mhammad (SAW) walitokana na kizazi cha Ismail (AS), na huyu Ismail alizaliwa na mtumwa na wala huyo Ismail (AS) hakubarikiwa. Kwa hiyo wanasema Uislam hauwezi kuwa ni dini ya kweli. Soma kitabu hicho WANA WA IBRAHIM ama DINI MBALI MBALI NA UTUME WETU. Vyote hivi vimeandikwa na Kanisa Katoliki. Yote haya yakitoka, Waislam hawakulalamika KASHFA hata siku moja.

Wakristo walipolalamika tu, eti dini yao inakashiwa Serikali nzima ilikuja juu. Sasa hivi kweli Ukristo umesimama kwenye msingi dhaifu ambao hauwezi kabisa kustahimili upekuzi wenye mantiki? Cardinal Manning wa Westminster aliwahi kunukuliwa akisema kuwa Dogma supersedes history (yaani amri inaweza kuwa bora na juu ya matukio ya historia). Huyu Cardinal Manning sio kiongozi wa kawaida tu, yeye alikuwa msaidizi wa karibu sana wa Papa Paul VI, aliyetoa mafundisho kuwa Papa hakosei (Infallibility of the Pope) anapokuwa katika kiti cha enzi. Kweli kutokana na haya yote, uko ule mkwaruzano k a t i y a Wa k r i s t o n a Waislam nchini humu. Hata wale maadui wa kivita vya kuuana, hasa kuna siku lazima wakae chini kuzungumzia uhasama wao. Wamarekani wanazungumza na Taliban. Kuna shida moja lakini ambayo ni lazima ikubalike na upande wa Wakristo. Waislam wana historia ya kuvumiliana sana na wenzao Wakristo; historia ya nchi hii ni wazi kabisa kwa hilo. Ubaya ni kuwa hawa ndugu Wakristo, hasa wale walio na madaraka, makubwa na madogo, hawakubali kabisa kuwa Waislam wanadhulumiwa baadhi ya haki zao. Ushahidi umetolewa kwa mfano, maandiko ya Dr. Sivalon katika kitabu chake KANISA KATOLIKLI NA SIASA YA TANZANIA Inandelea Uk. 12

Je, tunahitaji Intifada ya tatu Palestina?


Wiki chache zilizopita kumekuweko na ongezeko la ardhi ya Palestina kuvamiwa katika maeneo ya Ukingo wa Magharibi na hasa katika Jerusalem Mashariki (al Quds). Kumekuweko pia na migomo ya njaa inayoendeshwa na wafungwa wa Kipalestina katika jela za Israel. Wafungwa hawa wa kisiasa ni pamoja na Samer Issawi, aliyegoma kula kwa muda unaozidi siku 220. Wa k a t i h u o h u o mfungwa wa miaka 30, Arafat Jaradat, ameuawa kwa kuteswa na maosa wa Israel. Jambo hili limepelekea Wapalestina wengi kupandwa na hasira na kuandamana kote. Kutokana na vitendo vya namna hii, swali limekuwa likiulizwa i w a p o Wa p a l e s t i n a wanahitaji kuanzisha Intifada (mapambano) ya tatu dhidi ya wavamizi wa Kiisraeli. We n g i w a m e k u w a wakizungumzia uwezekano wa Intifada mpya dhidi ya Israel inayoikalia kimabavu ardhi ya Palestina. Wa a n d a m a n a j i wanaopinga utesaji wa raia wa Palestina wamejenga mahema na kukaa katika maeneo yanayotishiwa kuvamiwa na Israel. Haya ni maeneo ya Babeshams, Kanaan katika Hebron, Beit Safafa na Al Karmah iliyo kaskazini mwa Jenin. Wa k a t i h u o h u o , wafungwa Wakipalestina waliogoma kula katika jela za Israel wamewahamasisha wananchi wengi kujitokeza na kuonyesha mshikamano wao katika sehemu zote za Ukingo wa Magharibi na Gaza. Lengo ni kudhihirisha azma ya Wapalestina kuufanya ulimwengu uelewe hali ya Wapalestina na jinsi wanavyodhalilishwa na Israel. Lakini yote haya hayatatosha kuifanya Israel ijitoe katika maeneo ya Palestina iliyoyavamia. Inawezekana ulimwengu mzima ukaunga mkono harakati ya Wapalestina dhidi ya Israel yenye majeshi na silaha nzito. Lakini hii itachukua muda mrefu na ni mchakato mrefu utakaochukua miaka mingi. Kwa upande mwengine harakati za Wapalestina bila ya kutumia nguvu zinaweza zikawaaibisha maraki wa Israel katika nchi za magharibi, hasa Marekani ambayo inaisaidia Israel bila ya kutumia mantiki wala kufikiri. Mwishowe watatanabahi umuhimu wa kuilazimisha Israel iachane na uvamizi wa Palestina na badala yake itafute njia itakayoleta amani na utulivu wa kudumu katika mashariki ya kati . Kwa vyovyote, Wapalestina hawahitaji Intifada mpya bali wanahitaji uelewa mzuri kuhusu madai yao ya ukombozi, kisha waieleweshe Marekani. Njia hii ni muhimu hasa kwa vile hivi karibuni tutakuwa na ziara ya Rais Obama nchini Israel na katika maeneo ya Palestina yaliyovamiwa na Israel. Makala na Kituo cha Habari cha Palestina (Tanzania) Palestine Information Centre (Tanzania) Contact us: P.O Box 20307, 612 UN Road Upanga West, Dar es Salaam Tel: 2152813, 2150643 Fax: 2153257 Email: pict@pal-tz.org We b s i t e : w w w. p a l tz.org

10

Makala

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 8 - 14, 2013

AN-NUUR

MMOJA wa kijana wa Kipalestina aliyejeruhiwa na majeshi ya Israel.

kupigania ukombozi na uhuru wa nchi yao. Pamoja na upinzani huu mkali unaoonyeshwa n a Wa p a l e s t i n a dhidi ya Israel, wao hawazungumzii kuanzishwa kwa Intifada ya tatu. Hata hivyo upinzani wa Wapalestina ni dhidi ya uvamizi wa ardhi yao na Israel pamoja na udhalilishwaji na ukandamizwaji unaofanywa na Israel. Kila Israel inavyozidisha ukandamizaji huo, ndivyo na Wapalestina nao wanavyoongeza upinzani wao dhidi ya wavamizi. Ni kweli upinzani huu wa Wapalestina wanaodai haki yao ya kitaifa, unaweza ukachukua taswira tofauti. Lakini kilicho dhahiri ni k u w a Wa p a l e s t i n a hawatatumia nguvu. Rais Mahmoud Abbas, anasisitiza upinzani bila ya kutumia nguvu, akisema yeye hayuko tayari kuburuzwa katika umwagaji wa damu, jambo ambacho Israel wanataka lifanyike. Kwa upande wa pili, watawala wa Israeli

na vyombo vyao vya habari wanawachochea Wapalestina waelekee kwenye Intifada mpya. Wanaelewa kuwa wao ndio wenye nguvu na silaha za kisasa zinazoweza kuwaua Wapalestina kwa urahisi. Kwa kuwachochea Wapalestina waingie uwanjani, Israel watakuwa na kisingizio cha kutumia silaha zao za maangamizi, pamoja na kufanya majaribio ya silaha zao mpya, kama walivyofanya huko Lebanon na Gaza. Wapalestina wanaotumia nguvu watasingiziwa kuwa ni magaidi na Waisraeli watapata kisingizio cha kuwashambulia kwa madai ya kile wanachopenda kukiita ulinzi wa Israel. Wakati huohuo, Israel inaendesha propaganda zao kwa kudai kuwa hawawezi kufanya mazungumzo ya amani na Wapalestina. Kwa maneno mengine, harakati za ukombozi wa Palestina zitatoa mwanya kwa Israel kuzidisha ukandamizaji wake dhidi ya wananchi wa Palestina,

huku wakidai kuwa Israel imezungukwa na maadui wanaotishia usalama wake. Watazungumzia kile wanachokiita mihimili ya uovu inayoundwa na Iran, Syria, Hezbollah na Hamas. Wa n a c h o h i t a j i Wapalestina kwa kweli si Intifada nyingine dhidi ya udhalimu wa Israel, bali ni ukombozi na Uhuru wa ardhi yao iliyovamiwa na Israel. Kwa bahati mbaya lengo hili haliwezi likakiwa kwa kutupa mawe mbele ya majeshi ya Israel yenye silaha nzito na za mauaji. Intifada mpya ya Wapalestina ni pamoja na maandamano yanayofanyika kila siku na kila wiki, dhidi ya Israel katika maeneo kama Bilin, Nilin na Maasara,Hebron, Kafr Qaddoum na Jenin. Migomo ya njaa inayoendeshwa na mashujaa wa Kipalestina walio katika magereza ya Israel. Jitihada hizi hazitazaa matunda ya haraka ya kuikomboa Palestina. Kitakachofanyika ni

Uke wenza katika malezi ya watoto


Na Pendo Masasa MTOTO anayo haki k u p a t a m alezi b ora kutoka kwa wazazi wake wawili, yaani baba na mama yatakayo muwezesha kuwa mtu mwema katika jamii baadae. Wazazi wanahusika na malezi ya mtoto tangu akiwa tumboni kwa mama hadi kukia umri wa mtu mzima wa kujitegemea. Malezi ya mtoto yamegawanyika katika sehemu kuu mbili, malezi ya kimwili na malezi ya kiroho. Malezi ya kimwili ni yale yote yanayohusika katika makuzi ya mtoto, yaani awe na afya, ale vizuri, alale vizuri, avae vizuri na akue vizuri akiwa na afya njema. Malezi haya huanza mara tu mimba inapotunga. Baba anawajibu wa kumtunza mkewe barabara kwa kumpatia vyakula maalum, ili mama na mtoto wake tumboni wawe na afya nzuri. Pamoja na huduma nyingine, baba ana wajibu wa kumpa mkewe upendo na faraja, hasa katika kipindi cha ujauzito hadi kujifungua. Ni jukumu la mama na baba kufuata masharti ya kulea mimba wanayopewa na daktari na hata baada ya kuzaliwa mtoto. Ni jukumu la baba na mama kutoa malezi ya kiroho (kimaadili na kumjua Mwenyezi Mungu) kwa watoto wao au familia. Pamoja na kuhakikisha kuwa mtoto analelewa vizuri kimwili, lakini ili mtoto amudu maisha yake bila taabu hapo baadae na kuwa mtu mwema, ni lazima alelewe kimaadili na kiimani na wazazi wake. Yeyote mwenye kujua lengo la kuumbwa mwanadamu, hawezi kuacha kuzingatia maadili kwa mwanaye. Mtoto aliyelelewa vyema kimaadili, ataweza kuwatendea wema wazazi wake, jirani zake na jamii inayomzunguka kwa ujumla. Uislamu huwa unamtazama mwanadamu kama Khalifa wa Allah (s.w), yaani ni msimamizi wa sheria za Allah ili ziweze kufuatwa kikamilifu na kurahisisha maisha. Haya yote anayapata mwanadamu iwapo alipokuwa mtoto, alipata wazazi wazuri waliyohakikisha mtoto wao anapata malezi yote ya kimwili na kiroho kwa usahihi. Mtoto anapoanza kuongea na kuelewa kile anachokieleza na anachoelezwa, basi mkazo wa mafunzo ya kimaadili na dini huanzia hapo. Hilo lifanyike wakati huo kwa kuwa mtoto kwa kipindi hiki, ana uwezo mkubwa sana wa kuelewa anachofundishwa na kunasa. Akiwa mtu mzima bila kufanyika jitihada hizi muhimu za kimalezi, ni wazi kuwa mzazi hawezi tena kumwambia au kumfunza jambo akatii. Hali hii inapotokea, kundi la watu ubishi, wenye kibri na watovu wa nidhamu hujengeka. Hata hivyo kumekuwa na tatizo la ufahamu mdogo sana katika malezi ya watoto wanaopatikana katika ndoa ya mke zaidi ya mmoja. Kukosekana kwa ufahamu wa kimalezi katika ndoa hizi pamoja na kutozingatiwa mafunzo ya Quran na sunna za Mtume (saw), imeshuhudiwa mizozo na uhasama mkubwa ya kifamilia katika familia za aina hii. Katika eneo hili, wazazi wengi wamekuwa wakipotoka ambapo hutupilia mbali malezi ya watoto na kuangalia maslahi yao binafsi. Mke mmoja anaingia tamaa ya kutaka wanawe kuwa zaidi ya watoto wa mke mwenzie. Wakati mwingine mke mmoja anatamani familia yake kuwa na hali nzuri zaidi kuliko ya mke mwenzie. Hali hii imesababisha akina baba kukabwa na kuletewa kila aina ya maneno ya uzandiki, ili tu akubaliane na matakwa ya mke mwenye nia ya namna hii ndani ya familia ya uke wenza. Hapa ndipo baba asiye makini, anajikuta akianza kuzoea kidogo kidogo kujali zaidi familia ya mke mmoja ili kumridhisha, huku akisahau somo la uadilifu kwa wake wengine tofauti na somo la Quran na hadithi za Mtume zinavyoelekeza. Atahangaika kukidhi matakwa ya kichoyo na kutizama tu malezi ya kimwili kwa mke huyu na wanawe, kuliko yale ya kimaadili. Hali kama hii inapotokea, mara nyingi athari inakuwa zaidi kwa watoto. Kwanza huachwa wakikosa msingi mzuri wa malezi stahiki, na nafasi hiyo huchukuliwa na nafsi ya uadui katika familia. Mke humchukia mke mwenzie, motto humchukia ndugu yake kwa mama mwingine. Tena wake wengine wanathubutu kuwaambia watoto wao bila woga kwamba wasimpende mama mkubwa au mdogo na wanawe kwa sababu si mama yao, wala watoto wao sio ndugu zao kwasababu hawajazaliwa pamoja. Inafika mahali mtoto anashirikishwa katika mvutano wa uhasama kati mke mmoja dhidi ya mwingine. Kwa vitendo kama hivyo mtoto anajengeka katika hali hiyo mpaka ukubwa wake. Kuwafanyia chuki ndugu zake na mama yao mkubwa au mdogo. Chuki, uadui na tabia chafu zinaingia ndani ya familia ya ndugu wa baba mmoja. Wakati mwingine mke mmoja anaambukiza wanawe chuki kwa mke mwenzie na wanawe. Wa k a t i m w i n g i n e atazua visa vya kutaka mume kumwacha mke mwenzie au kuondokewa neema ya ndoa. Watoto watafundishwa uongo

11

Makala

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 8 - 14, 2013

AN-NUUR

Huruma na mapenzi ni alama za Uislamu


Mwenyezi Mungu kwenu pale mlipokuwa maadui, na akaziunganisha nyoyo zenu na mkawa ndugu, Hadi mwisho wa aya hii amebainisha Mtume (S.A.W) mapenzi ya Muislamu kwa nduguye. Muislamu ni ukamilifu wa imani. Amesema Mtume (S.A.W), haamini mmoja wenu hadi apendelee kwa nduguye lile analolipenda yeye. Na amesema tena Mtume (S.A.W), ogopa yaliyokatazwa utakuwa mcha Mungu, na ridhia kwa alivyokupa Mwenyezi Mungu utakuwa tajiri katika watu. Na Mfanyie mema jirani yako utakuwa mwenye imani na pendelea kwa nduguyo lile unalolipenda wewe utakuwa muislamu. Hebu tusikie neno la mshairi akifafanua sifa za ndugu wa kweli pale aliposema. Hakika ya ndugu yako wa kweli ni yule anayekuwa nawe, na yule aliye kwa muda atakukimbia na hatakusanyika na yanayojulisha juu ya umuhimu wa mapenzi kati ya Waislamu na nduguye. Kwamba Mtume (S.A.W) amekataza ugomvi na chuki na kununiana Waislamu na kutokuzungumza zaidi ya siku tatu, akasema Mtume (S.A.W) Haifai kwa Muislam kumnunia Muislamu mwenzie zaidi ya siku tatu, na mbora wao ni yule anayemuanza mwenzie kwa salamu. Unahimiza sana Uislamu juu ya kueneza

wowote kumwambia baba, ilimradi mke mwenza aonekane mbaya na hata kuachika. Tabia hiyo inajengeka kwa mtoto kidogo kidogo. Kuwa muongo na kuharibu mahusiano ya familia linakuwa jambo la kawaida kwake hadi ukubwani. Madhara mengine anayoweza kuyapata mtoto ni kule kuhisi kuwa baba anampendelae mama mwingine. Japokuwa kweli baba anaweza kuwa na udhaifu wa kibinadamu, basi mke asiwe tena kichocheo. Badala ya kukaa na mzazi mwenzake kuzungumzia upungufu huo na kujadili namna ya kuuondoa kwa siri na kuyamaliza, ndio kwanza anauchochea maafa katika Inaendelea Uk. 12

mapenzi na huruma kati ya Waislamu, kwamba Muislamu anapompenda Muislamu mwenzie basi amwambie kuwa ninakupenda kwa ajili ya Mungu. Alikuja mtu mmoja kwa Mtume

Dk. Emad Rabie Ahmad Mohamed Shukurani zote ni za Mwenyezi Mungu na Rehema na Amani zimkie yule aliyeletwa kuwa ni Rehema kwa viumbe wote, Bwana wetu Muhamad na Jamaa zake na sahaba zake wote. Ama baada ya utangulizi huu, kwa hakika huruma na mapenzi ni alama za Uislamu. Kwa hakika umekuja Uislamu ili kupandikiza kanuni za udugu na kusaidiana watu na ili waeneze huruma na mapenzi kwa viumbe vyote. Ametuonyesha Allah (sw) katika Surat Al Imrami, juu ya neema hii inayojulisha utukufu wa jambo hili la kueneza udugu na huruma, mapenzi na kusogeleana na kuwa karibu badala ya kukimbiana na kunyanya paana na kuchukiana. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, Na shikamaneni katika kamba ya Mwenyezi Mungu nyote na wala msifarikiane, na zikumbukeni neema za

Awe anawapenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake k u lik o v itu v in g in e n a ampende mtu isipokuwa kwa ajili ya mwenyezi Mungu hadi mwisho wa hadithi hii tukufu. Kama isipokuwa muumini na awachukue waharibifu na mafisadi na waovu na yote hayo ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Na katika hadithi yenye maana hii, yeyote Mwenye kupenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na akachukia kwa

(S.A.W), anasema ewe Mtume (Mimi ninampenda Fulani, Mtume akasemsa nenda ukamwambaie juu ya mapenzi na huruma hiyo iwe ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa sahihi ya maneno ya Mtume (S.A.W), amesema mambo matatu atakayekuwa nayo, basi amepata utamu wa imani.

ajili ya Mwenyezi Mungu na akatoa mali kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na akazuia mali kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwa hakika amekamilika imani.

12
Kifungo si suluhisho!
Mtimani nina ghamu, kwa kifungo cha Imani, Kunena yanilazimu, kwa uchungu ikhiwani, Kwa idhaatu adhimu, leo kuwa kifungoni, Kuifungia Imani, katu sio suluhisho. Suluhisho muadhamu, la mazonge ya nchini, Ni haki kustakimu, sawa kwa kila insani, Si kwa Imani kudumu, miezi sita kifungoni, Kuifungia Imani, katu sio suluhisho. Haki ni jambo adimu, kwa baadhi ya insani, Si leo tangu kadimu, kwa hapa petu nchini, Tangu enzi za Mwalimu, si za juzi za Imani, Kuifungia imani, katu sio suluhisho. Haki chungu kwa dhalimu, si leo tangu zamani, I tamu kwa madhulumu, bila kujali Imani, Dhuluma ndiyo jarimu, na si Redio Imani, Kuifungia Imani, katu sio suluhisho. Haki daima dawamu, huwa ni yenye kuwini, Tangu enzi za Adamu, baba wa wote insani, Haki ni yenye kukumu, hata pasipo Imani, Kuifungia Imani, katu sio suluhisho. Kalamu ya madhulumu, i karibu ukingoni, Vyovyote itavyokumu, dhuluma haitawini, Tatizo ni udhalimu, na si Redio Imani, Kuifungia Imani, katu sio suluhisho. Allah alimu-hakimu, kwa Kifungo cha Imani, Wamjua muhujumu, wa Redio yetu Imani, Twakwomba umuhukumu, akhera na duniani, Haki ndiyo suluhisho, si kuifunga Imani. ABUU NYAMKOMOGI MWANZA.

Mashairi/Barua

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 8 - 14, 2013

AN-NUUR

Inatoka Uk. 10

Masheikh na Maaskofu kukutana


zilielekezewa kwa watendaji wakiwemo Polisi waliowapiga risasi na kuwaua wasiokuwa na silaha yeyote. Baadae imeonekana kuwa ni hawa watendaji serikalini walio Wakristo ndio wanafanya dharau kwa Waislam na ndio kwa mfano, wanaochagua wanaoendelea Form I ama Form V, na ambao wanahakikisha kuwa Waislam wanaopewa nafasi hizo ni wachache. Baada ya MwembeChai, askari Muislam aliyetoa maoni kuwa kitendo kile hakikuwa sahihi alimwaga unga wakivunde na ikabidi akaufuate nyumbani kwao Katonyanga (Ujiji). Sasa iwe kweli Maaskofu na Masheikh wakutane wanawezaje kubomoa ukuta huu uliojengwa na watumishi serikali walio Wakristo, hasa ikikumbukwa kuwa kwa muda mrefu hawa viongozi wa dini ya Kikristo wamekuwa wakiwafundisha wafuasi wao kuwa Uislam si dini. Mtume Muhammad (SAW) ni Mtume bandia (false Prophet). Waislam ni watu wajinga hawakusoma na wako dhalili. Ikiwa kama Maaskofu hawatakubali kuwafundisha waumini wao heshima na adabu kwa Waislam, hata pakiwa na mikutano mingapi, huo msuguwano hautakwisha na pengine makubwa zaidi yatazuka.

BARA 1953 HADI 1985. Haielekei kama kuna viongozi wa Serikali, wanasiasa na watendaji (civil servants) kama

msikiti huo, yaliguswa na Waislam. Ghadhabu zote

kwa serikali na sio kwa Wakristo ama Makanisa. Wakati wa kadhia ya MwembeChai hakuna hata kanisa moja kati ya yale yaliyo karibu na

wamesoma klijitabu hiki. Halafu aliyeandika kitabu DEVELOPMENT AND FRELIGION IN TANZANIA, kilichoandikwa na Jan P van Bergen, ambaye katoa siri zinazohusu mawazo ya Hayati Mwalimu Nyerere kuhusu Uislam na Waislam, kuwa yeye ni Mkatoliki na ni Rais wa nchi hii mwenye madaraka makubwa sana. Afisa wa Elimu wa Munispaa ya Morogoro anapowaandikia walimu wa shule za msingi kuwa anataka majina ya wanafunzi wa Kikatoliki waliomo darasa la saba, maana yake nini. Hata pale wadau wengine walipolalamikia kitendo hicho kwa maandishi, si Wizara ya Elimu wala Osi ya Waziri Mkuu walioona kwamba hawa waliolalamika wanastahili kupewa heshima ya kupelekewa majibu. Iko mifano mingi ya dharau ya namna hiyo dhidi ya Waislam kutoka Serikalini. Huko nyuma ghadhabu za Waislam kutokana na dharau na dhuluma kama hizo zilikuwa zikielekezwa

ndiyo chanzo cha matatizo yote.

Inatoka Uk. 11 familia kwa kuwaeleza wanawe udhaifu huo. Kitendo cha mama kumwambia mwanawe udhaifu huo, fahamu ka kuwa mtoto atapunguza mpenzi kwa baba yake na kwa mama yake mkubwa au mdogo na kwa ndugu zake wanaotokana na mama mwingine na hatimaye kwa familia nzima kwa ujumla. Hata atakapokuwa mtu mzima, hatamjali baba yake wala mama mdogo au mkubwa na wanawe pia, jambo ambalo ni kosa kubwa kwa mtoto kutowatendea wema wazazi wake. Jamii itabakia kumlaumu kuwa hajali mzazi au wazazi wake, kumbe wazazi w enyewe

Uke wenza katika malezi ya watoto


Wake wenza wakiishi katika udugu, watoto nao watajifunza mengi mazuri kimaadili. Kwanza wataona jinsi familia ya baba na wake zake wanavyopendana, watajiona kama wamezaliwa tumbo moja. Watasaidiana kwa hali mali kidugu, watajenga upendo wa kweli wao kwa wao na kwa wazazi wao hadi wanakuwa watu wazima. Kwa familia ya uke wenza wanaopendana namna hii, ni vigumu mtu baki kujua utofauti wa mama na watoto hao bila kuambiwa. Hata pale wazazi watapokwenda katika maisha ya barazak, watakuwa wameacha familia katika mstari ulionyooka. Pia katika familia ya uke wenza iliyolelewa kimaadili hadi ukubwani, itakuwa vigumu kutokea mizozo ya familia inayoegemea katika misingi

katika CIVIL SERVICE ni waumini wa Kanisa Katoliki. Hivi Kanisa hilo halifundishi kutoa haki kwa wote bila upendeleo? Hivi wale waliomo katika CATHOLIC OLD BOYS ASSOCIATION (COBA) hawaipendi nchi ya Tanzania kuweza kulegeza kamba angalau kidogo kwa usalama wa Tanzania? Mwisho ikubalike kuwa Waislam hawaukashifu Ukristo. Hili lilipelekwa mpaka Mahakama ya Rufaa na Mahakimu wakahukumu kuwa Waislam wanapohubiri kufuatana na mafundisho ya dini yao, hiyo sio kashfa kwa Ukristo wala Wakristo. Kwanini ukweli huu haukubaliwi?

Amani iko mikononi mwa hawa watendaji wa serekali walio Wakristo; ni wao waache dhulma, dharau na kibri, na watende haki kwa wote. Waislam hawataki upendeleo wowote wanataka haki yao tu. Kumbuka Askofu Mkuu mstaafu Elinaza Sandoro, mara nyingi alikuwa akisema kuwa panapokuwa hakuna haki, hapawezi kuwa na amani. Ni yeye tu aliye kiongozi wa Kikristo anayeyaona hayo? Hakuna wengine wa madh-hebi zingine kama vile Katoliki wanatambua hayo? Kutokana na maelezo ya Muhasham Polycarp Cardinal Pengo, idadi kubwa zaidi ya waliomo

ya tofauti za uzao wa wazazi wa kike. Mtoto akifunzwa tabia njema bila kujenga hisia za utofauti ndani ya familia ya uke wenza, akawa na heshima na kuwatii wazazi wake hata kama sio wa kumzaa, akawaheshimu na kuwatii wake za baba yake, nao wake wenza wakaona kuwa watoto wao wote ni wa familia moja, ya baba mmoja, watafaulu na kuwa familia ya mfano bora wa kuigwa katika jamii. Amesema Mtume (s.a.w), wakirimuni watoto wenu na muwafunze tabia njema. Ni vyema tukaishi na familia zetu kwa furaha, upendo, kuaminiana na masikilizano ili kuleta picha halisi ya maisha mazuri ya Kiislamu. Tuishi na familia zetu huku tukifahamu kuwa kila mmoja wetu ni mchunga na kila

VIWANJA VILIVYOPIMWA KONGOWE KIBAHA TOWNSHIP REGISTERED PLAN No. 70995 BLOCK H
PLOT HATUA ENEO MRABA GHARAMA TSH

H1 H2 H3 H4 H5 H6 H7 H8 H9 H10 H11

50 x 29 32 x 32 50 x 30 37 x 30 50 X 45 33 x 37 60 x 45 50 x 40 67 x 50 70 x 45 90 x 50

1341 Sqm 1136 Sqm 1470 Sqm 1115 Sqm 2259 Sqm 1566 Sqm 2423 Sqm 1984 Sqm 3564 Sqm 2842 Sqm 3780 Sqm

4,023,000/= 3408000/= 4410000/= 3345000/= 6750000/= 4695000/= 7269000/= 5952000/= 10692000/= 8526000/= 11340000/=

Vipo Barabara ya Kongowe-Soga Kilomita moja toka barabara ya Morogoro. Simu No.0755 090 754/0715 090 754.

13

MAKALA

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 8 - 14, 2013

AN-NUUR

Yanapotokea leo tusisahau Mwembechai


Aliyekuwa askari polisi achua makubwa
jazba yaliyorushwa hewani na Radio Tumaini inayomilikiwa na kuendeshwa na Kanisa Katoliki. Kuwa amesikia Yesu akitukanwa katika mhadhara wa Mwembechai na akaitaka serikali iseme kama imeshindwa kutekeleza ahadi yake ya kuishughulikia mihadhara. Bila uchunguzi haraka haraka serikali kupitia mkuu wa mkoa wa Dar es salaam wa wakati huo, Bwana Yusuph Makamba, akaahidi kuchukua hatua za haraka juu ya mhadhara huo na akawaomba samahani Wakristo wote nchini walioathiriwa na mihadhara hiyo. Jumanne,10 Februari,1998, Mkuu wa Polisi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kamanda Alfred Gewe, naye akasisitiza kuwa serikali itachukua hatua kali dhidi ya wahadhiri wa Kiislamu wanaohubiri kwa kutumia Biblia. Usiku uliofuata walianza kukamatwa Maimamu wa Msikiti wa Mtambani, Kibo na Mwenge kwa kuviziwa majumbani mwao usiku usiku karibu na alfajiri. Tarehe 11, Februari, 1998 kikosi cha askari polisi wenye silaha waliizingira shule ya Kiislamu ya Ubungo, wakidai kumtafuta Bw. Shabani Magezi, aliyekuwa miongoni mwa wa hadhiri wa ulinganisho wa dini kwa kutumia Biblia na Quran. Walijibiwa kuwa Magezi hakuwa muajiriwa wala mwanafunzi wa Ubungo Islamic High School. Alhamisi saa 9 alasiri 12 Februari,1998 askari kumi na mbili wenye silaha wakavamia Msikiti wa Mwembechai na kumkamata Magezi, baada ya saa moja toka kukamatwa kwa Magezi, wakaja askari wa kutuliza ghasia FFU na kuzingira msikiti ili mtu asitoke. Ilipoka saa 2 usiku askari wengi zaidi wenye silaha waliongezwa na kuzunguka eneo lote la Mwembechai na wapita njia walianza kukamatwa. Ilipotimu saa 7:00 usiku TANESCO wakakata umeme na askari wakaanza kutupa mabomu ya machozi ndani ya msikiti, kisha wakaingia na kuanza kuwapiga waumini, kuwajeruhi, kuwaburuta na kuwatupia ndani ya makarandinga watu kiasi cha mia tatu hivi. Swali la msingi hapa la kujiuliza, Kwanini serikali iliwaamuru polisi kuvamia msikiti na kwapiga kisha kuwakamata Waislamu waliokuwa katika nyumba ya ibada, tena kwa kuwakatia umeme? Nini hasa kosa lao? Ili kujisafisha, Waziri wa mambo ya Ndani wakati huo Ali Ameir na Kamanda Alferd Gewe walitoa kauli kuwa ilibidi polisi wavamie msikiti ule kwa kuwa ulituhumiwa kucha wahalifu. Siku iliyofuata Ijumaa, 13 Februari, 1998 eneo lote la Mwembechai lilizungukwa na askari polisi. Pamoja na hivyo Waislamu walimiminika kwenda kuswali na kupata taarifa ya yaliyotokea usiku uliopita kwa ndugu zao waliokamatwa. Baada ya swala ya Ijumaa, walielezwa waelekee kituo cha Magomeni kuwawekea wenzao dhamana. Walipotoka kuanza safari kwenda kituo cha polisi Magomeni, wakavamiwa na askari polisi, Waislamu wake kwa waume, watoto kwa vikongwe, walipigwa virungu, mateke, wakaburuzw a na kutupwa kwenye malori na kupelekwa mahabusu. Ilikuwa ni kama jeshi la kivita limevamia wapiganaji katika uwanja wa mapambano, kumbe masikini ni Waislamu wakitoka katika swala ya Ijumaa. Mapambano yakapamba moto baina ya Waislamu, wasio Waislamu wakitumia mawe kupambana na askari hao, huku vikosi vya askari vikiongezeka kadri muda unavyokwenda. Amri zilitolewa kuwalenga shabaha walokusudiwa kwa kauli zilizosikikika Piga Yule, Piga shaba, yule piga shaba (rejea mkanda wa mauaji ya mwembechai wa ITV). Silaha za moto zikarindima, Waislamu wanne (4) wakauawa pale pale na maiti zao zikaburuzwa na kutupiwa ndani ya gari la Polisi kama mizoga. Mamia ya Waislamu wakiwemo wanawake zaidi ya mia mbili walijeruhiwa na kuwekwa mahabusu. Baada tu ya mauaji ya Mwembechai, mkutano mkuu wa chama tawala, CCM, mwenyekiti wake akiwa Benjamini Mkapa, ambaye pia alikuwa Rais wa nchi, uliipongeza serikali kwa hatua iliyochukua Mwembechai. Pia kiongozi Mkuu wa kanisa Katoliki, Polycarp Kadinali Pengo, aliunga mkono mauaji yale ya Waislamu akidai kuwa, askari wale walikuwa na haki ya kuwapiga risasi za moto kwa kuwa nao walikuwa wakiwatupia mawe. Akajaribu kuhalalisha kwa kurejea kisa cha Nabii Daud kuwa jiwe nalo linaua kama Daud (a.s) alivyomuua mfalme Jalut kwa jiwe. An-nuur ya wiki ile ilimuuliza swali Kadinali Pengo, katika tukio la Mwembechai nani alikuwa Daud na nani Jalut? Mtoto Chuki Athumani, aliyekuwa akipita njia kutokea shuleni akapigwa risasi na kuachwa siku kadhaa bila matibabu hospitali ya taifa Muhimbili. Hadi leo Chuki ni kilema wa maisha, hawezi kutembea ila kwa msaada wa baiskeli ya miguu mitatu na hakuna kiongozi wa serikali anayejali au hata kukumbuka. Miongoni mwa watu walioteswa na kufa muda mfupi baada ya kutoka Gerezani ni Imamu wa msikiti wa Mtambani Sheikh Abdallah Chata. Akitoa maelezo Bungeni wakati huo, Waziri wa mambo ya ndani Ali Ameir, akaliambia Bunge kuwa Mwanafunzi Chuki alikuwa na karatasi za uchochezi. Serikali haikueleza kama alipigwa risasi kabla au baada ya kukutwa na karatasi hizo za uchochezi, pia kama kakutwa na karatasi zinazodaiwa za uchochezi adhabu yake ni kupigwa risasi. Na hata hizo karatasi zenyewe hazijaoneshwa hadi leo hii 2013. Tu k i o l a M w e m b e c h a i liliwakasirisha sana Waislamu. Waislamu waliiomba serikali iunde Tume huru kuchunguza m a u a j i y a Wa i s l a m u Mwembechai, Serikali ilikataa. Mwanasheria mmoja kwa jina maarufu, Abuu Azizi alimwandikia Mwanasheria Mkuu wa serikali kumuomba aishauri serikali juu ya kuundwa kwa Tume huru ya uchunguzi juu ya mauaji ya Mwembechai. Ombi lake pia lilipuuzwa. Baadhi ya wabunge akaliomba Bunge liunde Tume ya uchunguzi. Ombi hilo lilikataliwa kwa hoja kuwa hakukuwa na pesa. Hatimaye Halmashauri Kuu ya Waislamu walimwandikia Rais kumwomba, pamoja na mambo mengine, serikali iunde Tume huru ya uchunguzi. Katika majibu yake alisema: Kuhusu suala la Mwembechai mimi nilifikiri tulishaelewana haitasaidia sana kuunda tume ya uchunguzi, maana tunajua kilichotokea. Na tunajua kuwa zile fujo, ambazo hatimaye zilihitaji nguvu kubwa za dola kuzizima, hazikuwa na uhusiano na mambo ya dini kabisa. Ndio maana miongoni mwa watu waliokamatwa walikuwapo watu ambao wala si Waislamu. Bado haja na hoja ya kuunda Tume sijaiona. Ikumbukwe kati ya Februari na Aprili,1998 hapa nchini kulikuwa na kesi iliyosisimua kidogo, juu ya Mbwa aliyeitwa kwa jina la immigration. Bwana Anatory Kachele Chizu, mwenye mbwa huyo alishitakiwa yeye na mbwa wake katika mahakama ya mwanzo na Bwana Stanley Anyitike, mfanyakazi wa uhamiaji huko Sumbawanga kwa kosa la kumuita mbwa wake jina la immigration . Akitoa hukumu Hakimu wa mahakama hiyo Bwana Onesmo Zunda, alimhukumu Bwana Chizu kwenda jela miezi sita na mbwa wake kuuliwa. Papo hapo maaasa wa uhamiaji wakamuua mbwa yule kwa rungu. Kesi na hukumu ile vilizua mjadala ndani na nje ya nchi kukia Jaji Mkuu wakati huo, Francis Nyalali, alisema hukumu ile ni kiroja, kinyume cha sheria

Na Suleiman Ramadhani

Naam haki hupewi ila huchukuliwa rights are never given are taken, ni maneno yasiyosahaulika ya mpigania haki za waamerika weusi na Uislamu kwa ujumla Malcom X. Huo ndio ukweli ulio wazi kwa wapigania haki wote duniani. Imepita sasa miaka kumi na tano toka yalipotokea mauaji ya Mwembechai, hakuna anayejali dhulma iliyofanyika ya kukatisha maisha ya Waislamu w ann e kw a maku s ud i na kuwaachia vilema wengine. Hili litabaki historia ya maandishi na huzuni kwa kizazi cha leo na kesho. Kila unapoibana haki na yenyewe hujidhihirisha na hatimaye huonekana pia mwisho wa siku hushinda. Serikali ya awamu ya tatu iliwadhibiti na kuwakandamiza Waislamu. Viongozi wa Kanisa Katoliki waliichochea na kuishinikiza serikali ya Mkapa idhibiti m i h a d h a r a y a Wa i s l a m u iliyokuwa kero yao kwa kipindi chote cha Rais Mwinyi. Kama wafanyavyo sasa hivi. Mwaka mmoja kabla ya mauaji ya Mwembechai, Askofu Elinaza Sendoro, alikaririwa na gazeti la Mtanzania, 21 Februari, 1997 akisema Mihadhara ya dini itazua vita. Pia gazeti la Majira, 10 Aprili, 1997 lilimkariri Askofu Basil Sambano, akilalamikia mihadhara ya kidini na katika tahariri yake ya tarehe 2 April, 1997 Majira liliandika Ushauri wa Askofu Pengo kuhusu mihadhara uzingatiwe. Kauli hiyo aliyoizungumzia mhariri ilitolewa na kufanyiwa kazi mwaka mmoja baadaye katika mauaji ya Mwembechai, kauli hiyo ilisema: Hakuna sababu ya kuhoa kuudhi mtu au kikundi fulani cha watu. Tunasema katika hilo ni vizuri kutumia mbinu za kumwua nyani. Kauli hiyo imebeba msemo wa Kiswahili usemao Ukitaka kumuua nyani usimtazame usoni. Kauli hii ilikuwa ikiiagiza serikali kuwashughulikia Waislamu bila kuwaangalia wao wana hadhi gani katika jamii, au wana haki gani katika jamii. Wa i s l a m u w a l i k u w a wakiendesha mhadhara wa dini kwenye uwanja uliopo msikitini Mwembechai, Dar es Salaam kwa siku kadhaa bila tatizo lolote mwanzoni mwa mwezi Februari, 1998. Mhadhara huo ulihudhuriwa na watu wa dini mbalimbali. Hapakuwa na tukio lolote lile la uvunjifu wa amani, badala yake yalisikika malalamiko ya Padri wa Parokia ya Mburahati, Padri Camillius Lwambano, tena kwa

Inaendelea Uk. 14

Yanapotokea leo tusisahau Mwembechai


na kinyume na haki. Pasina kuombwa, Idara ya mahakama iliona umuhimu wa kuchunguzwa kuuliwa kwa mbwa. Uchunguzi ukaanza kufanyika mara moja. Kwa Waislamu pamoja na kuombwa, serikali haikuona umuhimu wa uchunguzi wa mauaji ya Mwembechai. Na pia ikakataa kufanya uchunguzi wa Muislamu Mohamed Omari (50), aliyefia mikononi mwa polisi 18 Mei,1998. Mbwa akawa anathamani kwa serikali kuliko Muislamu!! Mauaji ya Waislamu ni miongoni mwa vielelezo vya kuonesha dhulma, ubaguzi na kunyimwa haki kwa Waislamu hapa nchini. Hadi leo walioua Mwembechai na waliompiga risasi mwanafunzi Chuki, hakuna aliyewagusa kiserikali ingawa wengine waliofanya matukio hayo, inasemekana walishatangulia akhera kusubiri hukumu isiyo na upendeleo kesho kiyama mbele ya Allah (swt). Mwenyezi Mungu awalipe walokufa kwa ajili ya dini yao, na awape faraja wale wote waliopata madhara kwa kuonewa na awalipe malipo mema duniani na kesho Akhera. Amin Pamoja na mauaji na mjeraha waliyoyapata Waislamu wakati wa zoezi hilo maalum la Mwembechai, wapo waliopata madhara ya kufukuzwa kazi kwasababu tu ya Uislamu wao na masikitiko yao juu ya mauaji yale ya Mwembechai. Hapa tumuangalie mmojawapo ambaye alifukuzwa kazi ndani ya jeshi la polisi kama alivyojieleza mwenyewe Septemba, 2000 katika mahojiano na mwanahistoria maarufu, Mohamed Said wakiwa Dar es Salaam. Zahaki Rashid, anaelezea kilichomkuta akiwa Sajenti wa Polisi katika sakata la mauaji ya Msikiti wa Mwembechai tarehe 13 Februari 1998. Anasema siku ile alikuwa kitengo cha Mawasiliano pale polisi (Communication Control unit) kituo cha polisi cha kati. Japokuwa, kilichomtokea yeye akafukuzwa kazi mwaka ule, kinaweza kueleweka vizuri kama utapata taarifa ya kilichomtokea miaka kumi iliyopita akiwa mwanafunzi Tabora Boys kidato cha sita. Alisoma shule ya sekondari ya wavulana Tabora kwa miaka sita mfululizo. Alifanya mtihani wake wa kidato cha sita mwaka 1990, lakini kwa kipindi chote alichokuwa hapo, alikuwa ni kiongozi wa wanafunzi wa Kiislamu. Baadaye akawa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya wanafunzi wa Kiislamu mkoa wa Tabora. Moja ya kazi alizozifanya ni kuhamasisha wanafunzi wa Kiislamu kusoma na kufanya mitihani ya maarifa ya Uislamu. Wanafunzi wote waliojisajili somo hilo walifaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza kidato cha

14

Makala

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 8 - 14, 2013

AN-NUUR

Inatoka Uk. 13

nne. Walifanya vizuri katika maarifa ya Uislamu na masomo mengine pia. Matokeo hayo ya Zahaki na wenzake yaliwapa moyo wanafunzi wengine wa Kiislamu kujisajili kwa ajili ya somo hilo. Matokeo yao ya mtihani wa mwaka 1990 kidato cha sita, kiasi fulani yalimshitua kila mmoja. Walifaulu vizuri masomo yote lakini somo la Islamic Knowledge walifeli. Mfano Zahaki alifaulu vizuri masomo ya Fizikia, Kemia na Baiyolojia. Wote waliofanya maarifa ya Uislamu katika shule yao mwaka huo walifeli somo hilo. Wanafunzi wa Kiislamu wengi walichukia somo la maarifa ya Kiislamu na kujiondoa katika usajili wa kulifanyia mtihani. Zahaki alikatishwa tamaa na kushangazwa juu ya kufeli kwake somo hilo. Walipofuatilia Baraza la Mitihani Dar es Salaam akiwa na wenzake Ayubu Masenza, Ali Kalisi kujua tatizo, wakaambiwa walifanya mtihani mmoja tu kati ya mitatu ya somo hilo waliyotakiwa kufanya. Zahaki anasema walifanya yote mitatu na si mmoja kama walivyoelezwa lakini vitabu vya kujibia vya mitihani miwili havikuonekana. Haya pia yalithibitishwa na msimamizi wa usahihishaji wa somo hilo kwa mwaka ule Bwana Burhani Mtengwa, kuwa walipewa na kusahihisha vitabu vya majibu ya mtihani mmoja tu (we received and marked only one paper) kutoka shule ya wavulana Tabora. Uchunguzi wa wanafunzi ulionesha kuwa hujuma hii ilifanywa na Mkuu wa shule yao wa wakati huo Bwana Alexander Ndeki, ambaye alikuja kuwa Kamishina wa Elimu, na lengo ilikuwa kuwakatisha tamaa wanafunzi wasisome somo hilo. Anakumbuka Mkuu yule wa shule alitumia kipindi kimoja cha Baraza la Shule la Wanafunzi, kutilia msisitizo umuhimu wa kutotumia majina ambayo hayaelezei wewe ni dini gani. Alisema majina kama Kitanga Wanja au Maziku Masanja yalikuwa yakiwachanganya. Hakikisha una jina linalokutambulisha wazi wewe ni dini gani ili tuweze kukusaidia haraka unapokuwa na shida. Anasema Zahaki wakati ule hakulipa umuhimu jambo lile hadi 1998, alipojua jina lake lilivyomgharimu kwa utambulisho wake wa kidini. Na ilikuwa 1998, bila kutarajia, kufeli kwake kwa Islamic Knowledge kukamrudi katika osi ya Kamanda wa Polisi wa mkoa Alfred Gewe. Akizidi kusimulia mkasa huo anasema; Nilipojiunga na jeshi la Polisi 1992 haikunichukua muda mrefu kugundua kuwa katika mtazamo wa askari wenzangu Wakristo, waliunganisha moja kwa moja kati ya uhalifu na dini linapokuja suala linalomhusu Muislamu. Mkristo akifanya uhalifu, hata liwe kosa kubwa vipi, hatahusishwa na yeyote isipokuwa yeye mwenyewe. Wakati Muislamu akifanya uhalifu hata kama ni dogo kiasi gani itahusishwa na jamii

nzima ya Kiislamu. Askari Wakristo watakuja kwangu na kulalamika,Ustaadh, unaona watu wako wanavyofanya waliniita Ustaadh kwa kuwa nilikuwa nachunga sala na nilijitahidi kuishi Kiislamu. Ni mauaji yaliyofanywa na Polisi Msikiti wa Mwembechai, ndiyo yaliyogeuza maisha yangu. Siku ile nilikuwa zamu ya mchana na kujikuta katika wakati mgumu, nilikuwa nikipokea mawasiliano yote osini juu ya kinachoendelea Mwembechai. Kamanda wa operesheni alikuwa Bwana Kombe. Nilichokisikia kwa maosa wa Polisi Wakristo Mwembe chai kilinitisha, walisema kwa uwazi Hawa Waislamu wamezidi sana, lazima leo tukawakomeshe. Ndiyo bwana! wanatukera sana sisi Wakristo, leo watatukoma. Kila taarifa ya kifo cha Muislamu kilipokelewa kwa shangwe na furaha. Iliniuma sana kuona kuwa hata sheria hazifuatwi ila ni chuki za kidini zilizowekwa mbele. Anaeleza Sajenti Zahaki kuwa; baada ya tukio la Mwembechai nilipokuwa nikikutana na waumini wiki mbili baadaye zilikuwa ni ngumu kwangu, kwani walikuwa wakiniuliza Ndugu zetu mbona mnatuuwa? Tumekukoseeni nini, mbona mnatuua? Tukio lililobadili historia ya maisha yangu, na ambalo lilipelekea kufukuzwa katika jeshi la polisi, lilitokea saa 2.00 asubuhi ya Jumapili tarehe 1, Machi 1998. Nilikuwa na utamaduni wa muda mrefu kuwaruhusu askari Wakristo walio chini yangu, ambao wote walikuwa Wakristo, kwenda Kanisani Jumapili. Walipoondoka siku ile, nilianza kusoma nakala ya gazeti la AnNuur ambalo liliendelea kuripoti habari za Mwembechai. Nilipomaliza kulisoma, niliinua kichwa juu na kutazama kalenda iliyokuwa ukutani ambayo bado ilisomeka mwezi Februari, na siku hyo ilikuwa siku ya kwanza ya mwezi Machi. Niliishusha ile kalenda mezani na kuizungushia duara tarehe 13 ya Februari kwa peni nyekundu. Nikachora mishale mingi kuelekea tarehe ile na kuanza kuandika maoni yangu, niliandika, hii ni siku Waislamu walipouawa Mwembechai; ni siku Waislamu walipoteswa Mwembechai; ni siku Waislamu wanawake walipoharasiwa Mwembechai; ni siku msikiti wa Mwembechai uliponajisiwa, nakadhalika. Nikaandika polisi walivyotakiwa kufanya kwa mujibu wa sheria za polisi, katiba ya nchi na nikamnukuu Abraham Lincon. Polisi walitakiwa wawakamate watuhumiwa na kuwakabidhi mahakamani na si kuwaadhibu. Niliandika kwa hisia za ndani. Niliiacha ile karatasi mezani mwangu, nilirudi nyumbani huku maneno Ndugu zetu mbona mnatuua? likijirudia kichwani mwangu huku nikijiuliza siku ya hukumu nitajibu nini mimi? Msabato, Staff Sergent Richard Ogutu, aliichukua ile kalenda na kuipeleka kwa uongozi. Tarehe 3 Machi, 1998

nikaitwa kwa RPC Alfred Gewe, pamoja naye, alikuwepo Mkuu wa Operesheni ya Mwembechai Mr. Kombe na Asa Usalama wa Mkoa (RSO), Saidi Mwema (IGP kwa sasa), Staff officer, Buka Kibona na SSP Sammari. Nilihojiwa na Alfred Gewe. Mahojiano yetu yalikuwa kama ifuatavyo; A G : We w e n i Z a h a k i Rashid? ZR: Ndiyo AG: Ni mtu wa Kigoma? ZR: Ndiyo AG: Nimeona katika taarifa zako kuwa umesoma Uislamu. Je, unaujua Uislamu vizuri? ZR: Ndiyo, Mie sio mjinga wa dini yangu. Naufahamu Uislamu vizuri. AG: Unaujua Uislamu vizuri wakati ulipata F ya Islamic Knowledge? ZR: Nilibaki kimya. (nikimkumbuka headmaster aliyenisababishia kupata F na inajirudia tena kukumbushwa iliniuma sana) AG: Uko upande gani katika sakata la Mwembechai? ZR: Nijibu kama Ofisa wa Polisi au kama Muislamu? AG: Kwanini unaniuliza swali hilo? ZR: Kwasababu ulianza kunihoji juu ya ufahamu wangu dhidi ya Uislamu. Najua wewe ni RPC na mimi ni Osa wa Polisi. Swali lako linanichanganya. Ndio maana nakuuliza nikujibu kama Osa wa Polisi au kama Muislamu? AG: Je, umeandika chochote kile juu ya tatizo la Mwembechai katika gazeti, karatasi au sehemu yeyote ile? ZR: (Sikutaka kupoteza muda nikajibu wazi). Ndiyo, Tarehe 1 March,1998 niliandika tukio hilo katika karatasi ya kalenda. AG: Kalenda yenyewe ndiyo hii? ZR: Ndiyo yenyewe. AG: Tutachunguza, tukigundua hauko pamoja nasi, tutakuruhusu ukapige magoti kwenye makapeti msikiti wa Mwembechai. Nikafukuzwa kazi rasmi katika jeshi la polisi tarehe 1 Agosti, 1998. Uamuzi ule uliwasilishwa kwangu tarehe 1 Juni 1999 na kamanda wa Polisi wa wilaya kituo cha Oysterbay (OCD), Bwana Magosi, alinisomea kwa niaba ya RPC, Alfred Gewe kama ifuatavyo: 1. Mtuhumiwa ni mfuasi mtiifu wa imani ya Kiislamu. 2. Kwahiyo tunaamini, akiendelea kubaki katika jeshi la polisi, hawezi kutimiza imani yake vizuri. Ni vizuri akawa nje ya jeshi, hivyo aweze kufuata dini yake bila kikwazo. 3. Hatujui ni kwa kiwango gani jeshi la polisi limeathirika na kuwepo kwake katika kitengo cha uzuiaji wa makosa ya jinai kipindi cha utumishi wake. 4. Alichokifanya ni uhaini. 5. Kwa hivyo nimependekeza kwa IGP, kuwa afukuzwe. Anaweza kukata

rufaa kama hatoridhishwa na maamuzi. Hayo ndio maamuzi yaliyochukuliwa na Alfred Gewe kama RPC kumfukuza Asa wa Polisi kwa kuwa tu, anafuata dini yake ya Kiislamu vizuri. Zahaki anaeleza kuwa wakati wa kupambana na uhalifu, askari wa jeshi letu la polisi ambao ni Wakristo wazuri huchukuliwa kama rasilimali na wale Waislamu wanaofuata dini yao vizuri huonekana ni watu hatari. Kuwa Muislamu mzuri ni kigezo kikubwa cha kutokuwa na sifa ndani ya jeshi la polisi. Waislamu kwa kadri watakavyoifuata dini yao vizuri hawatakiwi kuajiriwa na jeshi la Polisi. Ndio maana hadi leo hii askari Waislamu ni waoga na hawataki kujulikana kama wanaufuata Uislamu wao, wengine hata kufanya ibada ni ngumu kwao ili kuwaridhisha wenzao kuwa wako pamoja. Haya ni mambo ya kusikitisha s a n a , w a k a t i Wa k r i s t o wakionekana wa thamani kwa uumini wao mzuri wa Kikristo, Waislamu wamekuwa wakibaguliwa na kuonekana ni watu hatari kwa kufuata Uislamu wao, na hawafai kulitumikia jeshi la polisi. Huyo huenda ni mmoja tu kati ya wengi wanaofukuzwa kazi au kuhamishwa vituo ambao taarifa zao hazijawekwa hadharani. Leo ni miaka kumi na tano (15) sasa toka mauaji ya Mwembe chai yatokee na madhara yake yapo hadi leo. Uimara na ujasiri wa imani kwa Waislamu umeongezeka maradufu. Waislamu hawajaacha kudai haki pale wanapodhulumiwa. Hakuna kiongozi wa serikali anaye wasikiliza wanapodai kuonewa na kudhulumiwa. Wanapoamua kuandamana kuonesha hisia zao huandamwa kwa virungu, mateke na mabomu ya machozi na hatimaye kukamatwa na kujazwa mahabusu bila matatizo au dhulma wanayoilalamikia kuondolewa. Mpaka sasa kuna kesi zaidi ya ishirini dhidi ya Waislamu humu nchini zikihusisha serikali na Waislamu, ikiwemo ile ya Sheikh Ponda Issa Ponda na waumini wengine arobaini na tisa. Ndugu zangu wananchi na viongozi wapenda haki na kupenda kuiona haki inatendeka, sio wakati wakukata tamaa kuipigania haki. Kwani haki inaendana na Mwenyezi mungu na dhulma inaendana na sheitwan. Haki itasimama tu siku moja na wale wote walioipigania haki watakumbukwa daima duniani na kesho akhera watapata malipo mema pamoja na wema waliotangulia. Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize Nuru yake ijapo kuwa makari watachukia Quran 9:32.

15

TANGAZO

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 8 - 14, 2013

AN-NUUR

NAFASI ZA KIDATO CHA TANO 2013/2014


Waislamu kote nchini mnatangaziwa nafasi za kidato cha Tano kwa shule zifuatazo:

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE


1.

KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL NYASAKA ISLAMIC SECONDARY SCHOOL UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOO L

SAME KILIMANJARO MWANZA DAR ES SALAAM

Shule hizi ni za Kiislamu zenye lengo la kuwapa wanafunzi taaluma ya hali ya juu na malezi bora ya Kiislamu kwa gharama nafuu. Shule hizi ni za mchanganyiko wa wavulana na wasichana na zinapokea wanafunzi wa bweni tu. 2. Masomo yanayofundishwa ni Islamic knowledge, Combinations za SAYANSI, ARTS, BIASHARA pamoja na COMPYUTA. 3. Muombaji awe na Crediti 3 au zaidi na angalau D ya Elimu ya Dini ya Kiislamu katika matokeo ya kidato cha nne. Ikiwa ana F au hakufanya Elimu ya Dini ya Kiislamu, basi awe tayari kusoma programu maalum ya Maarifa ya Uislamu atakapokuwa kidato cha tano. 4. Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni tarehe 18 /05 /2013 5. Fomu za Maombi zinapatikana kwa gharama ya shilingi 10,000/= katika vituo vilivyoorodheshwa hapa chini. 6. Arusha Kilimanjaro Tanga Mwanza Musoma Kagera Shinyanga Osi ya Islamic Education Panel Jambo Plastic Ghorofa ya 2 mkabala na msikiti Mkuu Bondeni - 0763 282 371/ 0784 406 610 Moshi: Msikiti wa Riadha 0654 723 418 Same: Kirinjiko Islamic Secondry School: 0784 296424/0655 697 075 Uongofu Bookshop: - 0784 982525/ Mandia Shop - Lushoto: 0782257533 Nyasaka Islamic Secondary School 0717 417685/0786 417685 Osi ya Islamic Education Panel - Mwanza - Mtaa wa Ruji mkabala na Msikiti Al-Amin 0785 086 770 Duka la Kansolele -Stendi ya zamani sokoni - 0714587193 Bukoba: Alhuda Caf Kwa mzee Kinobe karibu na osi za TRA. - 0688 479 667 Msiikiti wa Majengo-0718866869 Kahama osi ya AN NUUR Karibu na msikiti wa Ibadhi: 0753 993930 Ubungo Islamic High School 0754 260 241/0712033556 Osi ya Islamic Ed. Panel Temeke -Msikiti wa Nurul Yakin 0655144474 Wasiliana na Ramadhani Chale :0715704380 Hijra Islamic Primary School : 0716 544757/0712 325086 Osis ya Islamic Ed. Panel karibu Nuru snack Hotel 0714285465 Babati: Shule ya Msingi Hangoni: 0784 667575 Msikiti wa mwanga Kigoma: 0753 355224 Kibondo Islamic Nursery School: 0784 442860 Kasulu: Murubona Isl.SS. 0714710802 Wapemba Store: 0784 974041/0786 959663 Amana Islamic S.S 0786 729 973 Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa NURU 0715 681701/0716791113 Mkuzo Islamic High School. 0716 791113 Duka la vifaa vya Kiislamu nje ya Msikiti wa Uyole 0713 200209 Rexona Video mkabala na Mbeya RETICO: 0713 200209 Sumbawanga: Masjid TAQWA 0717082 073 Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784 944566 Madrastun Najah: 0714 522 122 Wete: Wete Islamic Education Center: 0777 432331 Madrasatul Fallah: 0777125074Osi ya ust. Yusufu Ally jirani na msikiti mkuu 0653705627

Dar es Salaam Morogoro Dodoma Singida Manyara Kigoma Lindi Mtwara Songea Mbeya Rukwa Tabora Iringa Pemba Unguja Maa -

Pia Fomu zinapatikana kwenye Tovuti: www.ipctz.org. Ikumbukwe kuwa watakaopata fomu kupitia tovuti (download) watatakiwa kuzilipia wakati wa kuzirejesha. USIKOSE NAFASI HII ADHIMU WAHI KUCHUKUA FOMU SASA! Wabillah Tawiq MKURUGENZI

16

AN-NUUR
16
Na Mwandishi Maalum, Zanzibar

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 8 - 14, 2013

Usikose nakala yako ya AN-NUUR kila Ijumaa

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 8 - 14, 2013

AN-NUUR

Al-Yousuf kujenga nyumba 400 za wananchi Pemba


JUMUIYA ya Al-Yousuf imeahidi kujenga nyumba mia nne (400) za mkopo nafuu katika kijiji cha Kiuyu, Wilaya ya Micheweni Pemba. Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Sheikh Al-Youseif , a m e t o a ahadi hiyo alipokuwa na mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Ofisini kwake Migombani. Sheikh Al-Youseif, amesema kuwa mradi wa ujenzi wa nyumba hizo pamoja na ule wa kilimo inalenga kukibadilisha kijiji hicho kuwa cha kisasa na chenye maendeleo. Aidha amefahamisha kuwa Jumuiya yake imeshawishika kuanzisha miradi hiyo ya maendeleo, baada ya kuona kuwa wananchi wa kijiji hicho wanaishi katika mazingira magumu. Sheikh Al-Youseif, ameeleza kuwa tayari juhudi za ukusanyaji wa fedha kwa ajili ya ujenzi huo zimeshaanza kuchukuliwa, sambamba na kuimarisha kilimo cha umwagiliaji ambacho kimebainika kustawi vyema katika eneo hilo. Tu m e f a n y a uchunguzi na kubaini kuwa ardhi ya Kiuyu ni ya jiwe sehemu ya juu, lakini chini ni nzuri na yenye rutba na kwamba, inakubali kustawisha kilimo cha mazao aina mbalimbali hasa cha mbogamboga, alifafanua Sheikh AlYouseif. Katika hatua nyengine, S h e i k h A l - Yo u s e i f amekabidhi shehena ya nguo kwa ajili ya wakaazi wa kijiji hicho cha Kiuyu Micheweni. Nguo hizo ni pamoja na vitambaa kwa ajili ya wanawake, surauli, na mashati ikiwa na lengo la kuwasaidia wananchi hao. Aidha Sheikh huyo ameiomba serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, kumpatia orodha ya wanafunzi wote wa Kiuyu ili aweze kuwapatia sare za skuli. Naye Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, ameishukuru Jumuiya ya Al-Youseif kwa misaada yake kwa Zanzibar na kwamba inasaidia kupunguza tatizo la umaskini nchini. Amesema uamuzi wa kukipa kipaumbele kijiji cha Kiuyu ni sahihi, kwani ni miongoni mwa vijiji vilivyoachwa nyuma kimaendeleo kwa kipindi kirefu. Ameongeza kuwa mradi wa kilimo ulioanzishwa katika kijiji hicho utakuwa chachu ya maendeleo, hivyo amewaomba wakaazi wa eneo hilo kuuenzi na kuuendeleza kwa juhudi zao zote mradi huo ili uweze kuleta mafanikio yanayokusudiwa. Ameahidi kusimamia ugawaji wa nguo hizo, ili kuhakikisha kuwa zinawafikia walengwa na kufikia lengo lililokusudiwa.

Sheikh Mkuu BAKWATA mkoani Kagera afariki dunia


Na Shaaban Nassibu, Muleba
SHEIKH Musa Athumani Kagimbo (85), ambaye alikuwa Sheikh wa Bakwata mkoa wa Kagera, amefariki dunia Jumapili iliyopita ya Machi 03. Sheikh Kagimbo alifikwa na mauti alipokuwa nyumbani kwake katika kijiji cha Nshamba wilayani Muleba, baada ya kuuugua kwa muda mrefu ambapo baadae alilazwa katika Hospitali ya mkoa wa Kagera. Akizungumza na gazeti hili, msemaji wa familia ya Kagimbo, ambaye ni mtoto wa Sheikh Kagimbo na kiongozi wa Waislamu wilaya ya Muleba, Sheikh Zacharia Musa Kagimbo, alisema kuwa kifo cha baba yake kilitokea machi 03 majira ya saa 3:15 asubuhi. Alisema mauti yalimkuta Sheikh Kagimbo siku mbili baada ya kuonekana kupata nafuu ya maradhi na kuruhusiwa kutoka hospitali ya mkoa na kwenda kupumzika nyumbani kwake Nshamba. Lakini siku ya Jumapili alizidiwa na wakati wanafamilia wanafanya harakati za kumrejesha Hospitali, aliaga dunia. Alisema kuwa marehemu kabla ya kukutwa na umauti, alikuwa akisumbuliwa na maradhi mbalimbali na alikaa kwa muda katika manispaa ya Bukoba akipatiwa matibabu ya aina mbalimbali, lakini juhudi za madaktari hazikufanikiwa kumponya hadi akafariki. Tu m e m u u g u z a m z e e wetu muda mrefu. Madaktari walijitahidi kumpatia matibabu lakini Allah (sw) alishapanga siku yake ya kuondoka duniani. Inna Lillahi Wa inna ilaihi rajiuunna. Alisema Sheikh Zacharia Kagimbo. Marehemu Sheikh Musa Athuman Kagimbo, alizaliwa mwaka 1928. Alisoma elimu ya msingi hadi darasa la nne na kupata elimu ya dini ya Kiislamu nchini Uganda. Marehemu ameacha wajane wawili, watoto 25, wa kike 10 na wa kiume 15, wajukuu 125 na vitukuu 44. Naye Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) mkoa wa Kagera Abdul Marick Mwijage, alisema kuwa Sheikh Musa Kagimbo, katika uhai

SHEIKH Musa Athumani Kagimbo (kushoto), ambaye alikuwa Sheikh wa Bakwata mkoa wa Kagera, amefariki dunia Jumapili iliyopita ya Machi 03.

wake alikuwa kiongozi wa kusimamia Uislamu akianzia kijiji cha Nshamba na mwaka 1,975 alipata nafasi ya kuwa Shekhe wa wilaya ya Muleba hadi 1,993. Mwijage alisema kuwa mwaka huo wa 1993 alifariki Shekhe wa mkoa, Sheikh Mikidadi Yusufu Katula wa kijiji cha Muhutwe. Alisema kufuatia kutangulia mbele ya haki Sheikh Katula, Baraza la Maulamaa mkoa lilimpendekeza Sheikh Musa Kagimbo kushikilia kiti hicho baada ya kukubalika na waumini. Marehemu wakati wa uhai wake alipenda kusisitiza mshikamano, akipinga mtafaruku wa kutengana na amesimamia miradi mingi ya Kiislamu Muleba na mkoa kwa ujumla. Kilichopo sasa ni kumuombea apumzike na kupata radhi zake Allah (S.W). Alisema Mwijage. Aidha Katibu huyo aliwataka waumini kumuenzi Sheikh Kagimbo kwa yale mema aliyoanzisha na kuyasisitiza wakati wa uhai wake, ikiwa ni pamoja na kuimarisha mahusiano kwa madhehebu yote ya kidini bila kujali tofauti za kiitikadi, za kimadhehebu au mitazamo.

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

You might also like