You are on page 1of 16

www.annuurpapers.co.

tz

Mtume (SAW) amesema kuwa Mwenye kuhiji amedhaminiwa na ni mgeni wa Allah (SW).Tupende sana kuwa wageni wa Mola wetu na kupata dhamana ya Mwenyezi Mungu. Tulishaitwa sote tangu zama za Nabii Ibrahim (AS), na hakuna wito mwengine binafsi. Gharama zote ni Dola 4,300 tu. Karibu Ahlu Sunna wal Jamaa.Tafadhali wasiliana nasi ifuatavyo: Tanzania Bara: 0717224437; 0777 462 022; ISSN 0856 - 3861 Na. 1060 RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 1 - 7, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= Unguja: 0777 458 075; Pemba: 0776 357 117.

Sauti ya Waislamu

(3) HIJJI UDHAMINIWE NA ALLAH!

Mwinyi awataka Masheikh, Maaskofu kukutana


Bassaleh, Kilemile, Abubakar Zuber, Juma Poli, wateuliwa Askofu Gamanywa, aomba apewe muda Lengo kurejesha utulivu na uhusiano mwema

Hofu ya vurugu za kidini nchini

Jaji akerwa upande wa mashtaka kupoteza muda kesi ya Uamsho


Alghaithiyyah, Zanzibar

RAIS Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi

Wakili: Sheikh Ponda hawana kesi ya kujibu


Na Mwandishi Wetu

amekataa hoja za upande wa mashataka za kutaka JAJI Mkuu wa Mahakama kutokusikilizwa ombi K u u y a Z a n z i b a r, la upande wa watetezi Inaendelea Uk. 4 Abraham Mwampashi,

Al-jazeera kulipeleka Uk. 3 Mtanzania Mahakamani

Sheikh Jabir Yusuph Katura, mmoja wa viongozi wa taasisi ya Al-Jazeera Islamic Centre, Ukerewe akisisitiza jambo wakati akiongea na waandishi wa habari Jiji Mwanza.

WAKILI wa upande wa washtakiwa Bw. Juma Nassoro, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana kuwa, wateja wake hawana kesi ya kujibu. Wakili huyo ameeleza kuwa kwa mujibu wa maelezo ya mashahidi wa upande wa mashtaka, ambao mpaka sasa

wameshakamilisha kutoa ushahidi wao, washtakiwa hawana kesi ya kujibu kulingana na mashtaka wanayoshtakiwa nayo. Akitoa utetezi wake Mahakamani hapo, alisema hakuna mahali ambapo mashahidi wamedhihirisha kwamba Sheikh Ponda na wenzanzake wameiba mali, katika ardhi ya Markazi
Inaendelea Uk. 4

2
www.annuurpapers.co.tz

Tahariri/Tangazo
Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 1 - 7, 2013

AN-NUUR

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786


MAONI YETU

BAADA ya mazishi ya Padri Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Minara miwili Zanzibar, aliyeuliwa Februari 17, Askofu wa Kanisa hilo Jimbo la Zanzibar, Augustino Shayo, alitoa kauli ambazo sisi tunaona ni za msingi sana katika kukabiliana na hali ilivyo huko Zanzibar. Askofu Shayo, alisema kuwa kunahitajika umakini mkubwa kipindi hiki katika kuwasaka wauaji, na jambo la msingi ni watu wasihusishe mauaji hayo na chuki za kiimani, akimaanisha Waislamu na Wakristo. Askofu Shayo alisema ana miaka zaidi ya 25 anaishi na kufanya kazi Zanzibar, lakini hakuwahi kukutana na matatizo ya kihalifu yanayotokanana chuki za kiimani. Amesema akiwa Zanzibar, amekutana na kufahamiana na watu wengi, na anawafahamu wazee na vikongwe, ambao wamezaliwa na kukulia katika Uislamu wao, lakini hajawahi kuwasikia wakiwaletea wenzao Wakristo vurugu au kuhusika na uhalifu wowote kwa sababu ya tofauti ya imani zao. Askofu Shayo alifafanua zaidi kwamba, kama ni wahalifu, wapo wa imani zote. Wapo w a h a l i f u Wa i s l a m u na wahalifu Wakristo. Akasema wahalifu wachache ambao ni Waislamu, hawawezi kuhalalisha jamii

Zizingatiwe kauli za Askofu Shayo, Maalim Seif

nzima ya Waislamu na imani yao kuwa ya wahalifu na kuchukiwa. Na katika Ukristo, w a h a l i f u Wa k r i s t o wachache hawawezi kuwafanya Wakristo wote waonekane kuwa ni wahalifu na kuleta chuki dhidi ya jamii nzima ya Kikristo. Kwa maana hiyo, alisema si vizuri kueneza propaganda chafu dhidi ya Waislamu na imani yao kwa sababu ya wahalifu wachache, na kwamba jambo hilo ni la hatari. Alisema kama anayetuhumiwa na mauaji ya Askofu Mushi atakuwa ni Muislamu, basi ashughulikiwe kwa mujibu wa sheria kama mhalifu si kwa mtazamo wa dini yake. Katika kipindi hicho hicho, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, naye alitoa kauli yake kwa Wazanzibar. Maalim Seif alisema kinachoonekana Zanzibar, ni ajenda iliyotayarishwa ya kutaka kulazimisha chuki za kidini Zanzibar, licha ya kuwapo kwa historia ya miaka mingi ya watu kuvumiliana na kuishi kwa pamoja na kuwapo watu wa imani tafauti. Alisema inasikitisha kuona wapo baadhi ya viongozi wanakuwa na nia chafu dhidi ya Zanzibar, kwa kuwa na tabia ya kutoa

kauli za kujenga chuki na tina miongoni mwa Wazanzibari chini ya kivuli cha matukio hayo ya mauaji. Vitendo vya kuuawa na kujeruhiwa viongozi wa kidini Zanzibar, ni mambo mageni. Wengi wanafahamu historia ya Zanzibar, imekuwa ni mfano bora wa uvumilivu wa kiitikadi za kidini licha ya kwamba asilimia 98 ya wananchi wake ni Waislamu. Wazanzibari ni wamoja, lakini wenye nia mbaya wanayachukulia matukio haya ya mauaji, kutaka kuwagawa na kuletea mtafaruku kwa kujaribu kuonyesha kuwa kuna tofauti za kidini Zanzibar wakati siyo kweli. Watu hawa wameamua kuyatumia matukio ya kuuawa na kujeruhiwa kwa viongozi wa kidini ili kuvunja umoja wa Wa z a n z i b a r i , l a k i n i nasema hakuna ugaidi Zanzibar, Alinukuliwa Makamu huyo wa Rais. Maalim Seif pia alisikitishwa na wanaobeba agenda ya ugaidi. Serikali imeshatoa maelekezo ya kufanyika uchunguzi wa kina, lakini wakati uchunguzi wenyewe ukiwa unaendelea, baadhi ya viongozi na vyombo vya habari wanachochea chuki za kidini na kusema kuwa Zanzibar kuna ugaidi. Lakini ugaidi huu kwanini kipindi hiki na hakikuwa kile cha mauaji ya Januari 27, 2000. Kipindi ambacho makumi ya Wazanzibar waliuliwa na wengine kukimbilia ukimbizini Shimoni Kenya. Kwa bahati wengine wamereja hivi majuzi na kupokelewa na serikali, japo awali ilikataa kuwepo wakimbizi hao. Kwa ujumla tuseme tu kwamba, wananchi wote wa Zanzibar wanatakiwa kuwa macho na ajenda zinazopenyezwa kipindi

hiki kuwavuruga na kuwagawanya kiimani. Wanatakiwa kuendelea kuishi kwa mshikamano na umoja kama ambavyo wamekuwa wakiishi. Lakini pia tuna imani kwamba serikali ya Zanzibar itasaidia kuhakikisha agenda chafu za kugawa watu kwa misingi ya imani, agenda za kujenga chuki kuliko kupata utulivu wakati huu hazifaulu. Kutokana na kauli aliyoitoa Maalim Seif, ambayo kimsingi ni kauli ya serikali ya Zanzibar,

ni imani yetu kwamba uchunguzi dhidi ya wauaji wa Padri Mushi, hautageuzwa kuwa sababu ya Wazanzabar wasio na hatia kuteswa Guantanamo kwa hoja za ugaidi badala kuwabaini wauaji halisi. Tunaamini utafanyika uchunguzi wa haki dhidi ya wauaji, kama unavyofanyika kwa wauaji wengine kwa kutumia taratibu zetu za kisheria na wahusika kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria zetu za jinai.

Kumradhi Sheikh Hilal Shaweji Kipozeo


KATIKA toleo letu lililopita Uk.6, kwenye makala iliyokuwa na somo Sheikh Said John (shariff) neno marhum liliingia kimakosa wakati wa kunukuu jina la Sheikh Hilal Kipozeo, ambaye ametajwa katika makala hiyo kama Marhum Sheikh Hilal Kipozeo. Tunapenda kuwajulisha wasomaji wetu kwamba Sheikh Hilal Kipozeo ni hai na bukheri wa afya. Halikua kusudio letu kuingiza neno marhum wakati wa kuandika jina lake, bali limeingia kimakosa. Kwa msingi huo tunamuomba radhi Shekh Hilal Said Kipozeo na familia yake kwa usumbufu walioupata kutokana na makosa hayo. Lakini pia tunawaomba radhi ndugu jamaa na maraki zake pamoja na wasomaji kwa ukakasi walioupata kufuatia kuwepo neno hilo. Mhariri

P.O. Box 55105, Tel: 2450069, 0712 974428 Fax: 2450822 D Salaam E-mail: ipcubungoislamic@gmail.com

UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL

Maandalizi kwa wanaorudia Kidato cha IV, 2013


UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL inatangaza kozi maalum ya maandalizi kwa wanaorudia kufanya mtihani wa Kidato cha IV, 2013. Programu hii itaanza tarehe 28/02/2013 hadi tarehe 28/08/2013 Jumatatu hadi Jumamosi saa 2:00 kamili Asubuhi hadi saa 9:10 Alasir. Masomo yatakayofundishwa ni:Elimu ya Dini ya Kiislamu, English Language. Lugha ya Kiarabu. Basic Mathematics, History, Geography, Civics, Physics, Chemistry, Biology, Book Keeping, Commerce. Kiswahili Fomu za kujiunga zinapatikana shuleni kwa Tshs 10,000/=

Mlete mwanao apate Elimu bora itakayomwezesha kujiunga na Kidato cha Tano.
Kwa mawasiliano zaidi piga namba: 0714 888557/0659 204013 Wabillah Tawiq MKUU WA SHULE

Mwinyi awataka Masheikh, Maaskofu kukutana


Na Bakari Mwakangwale RAIS Mstaafu, Ally Hassan Mwinyi, amewataka viongozi wa Dini nchini kukutana na kuzungumza kuhusu kuyumba hali ya mahusiano ya kidini inaotishia kuvuruga umoja wa Kitaifa uliopo sasa. Alhaj Mwinyi, ametoa wito huo wakati akizungumza na viongozi wa dini ya Kiislamu nchi za Afrika Mashriki na viongozi wa dini ya Kikristo, katika hoteli ya Serena, Jijini Dar es Salaam, katika mkutano uliandaliwa na Taasisi ya Jopo la Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, uliozungumzia amani na uvumilivu wa kidini nchini. Ili kuondoa hali hiyo na kuleta mahusiano mema baina ya dini hizo nchini, iliamuliwa katika mkutano huo iundwe Kamati Maalum, itakayopanga mkakati wa kuwakutanisha viongozi wa dini kuu mbili za Kiislamu na Kikristo, ili waweza kuwa na mazungumzo ya pamoja baina yao. Katika mkutano huo, iliamuliwa kwamba iundwe Kamati ya watu kumi, watano kutoka upande wa Wakristo na watano kutoka kwa Waislamu. Imefahamishwa kuwa baada ya makubaliano, waliteuliwa baadhi ya wajumbe mchanganyiko kutoka katika taasisi mbalimbali kwa ajili ya kuunda timu ya kutekeleza suala hilo. Kwa upande wa Waislamu, kutoka BAKWATA, aliteuliwa Sheikh Abubakar Zuber, katika Taasisi ya HYAT, aliteuliwa Maalim Ally Said Bassaleh na kutoka Baraza Kuu, aliteuliwa Sheikh Mussa Kundecha ambapo kutoka Taasisi ya Answar Sunna, aliteuliwa Sheikh Juma Poli pamoja na mjumbe mmoja kutoka Visiwani Zanzibar. Hata hivyo, alipotakiwa Askofu Gamanywa kutoa mapendekezo ya viongozi kutoka kwa Wakristo, aliomba apewe muda akisema kwamba Wakristo wana madhehebu na Taasisi mbalimbali hivyo aliomba muda ili wakalifanyie kazi suala hilo. Awali Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, alisema viongozi wa dini wamekutana na kuzungumzia suala la amani katika jamii inayoishi katika mchanganyiko wa dini tofauti. Alisema mazungumzo hayo yamekuja wakati kuna hitilafu ambazo zimeendelea kujitokeza katika jamii wanayoishi watu wa dini mchanganyiko na kuleta hofu katika jamii hivi sasa. Alhaji Mwinyi alisema ili kurejesha amani, utulivu na mahusiano mema baina ya wafuasi wa dini tofauti nchini, kuna haja ya kuwepo mazungumzo baina ya viongozi wa dini hizo kuzungumzia yanayoendelea kutokea hivi sasa nchini. Alisema kukutana viongozi wa pande mbili za dini kubwa nchini, kutasaidia kutafuta sababu za mpasuko wa kidini unaolinyemelea Taifa. Kwamba mara nyingi uvunjifu wa amani unapotokezea katika siasa, wenyewe wanasiasa huachwa kushughilikia kutafuta ufumbuzi mgogoro huo. Lakini kunapotokea uvunjifu wa amani kutokana na Dini, huwa kuna hatari viongozi wa siasa kuingilia mambo hayo ya kidini. Kutokana na hali hiyo, alisema inatakiwa viongozi wenyewe wa kidini waachiwe watafute ufumbuzi. Kwa upande wake, mgeni rasmi katika mkutano huo Dr. Abdallah Nasif, alieleza kwamba watu kuishi pamoja ni jambo zito, hivyo inapotokea hitilafu baina yao katika jamii, ni vyema kufanya mazungumzo ambayo yanaweza kutatua migongano inayoweza kutokea katika jamii. Dk. Nasif Akizungumzia kuhusu kutokea uhalifu wa mauaji na kisha yakahusishwa na Uislamu moja kwa moja, inakuwa si sahihi kwani Uislamu hauruhusu kuuwa mtu bila ya sababu yoyote ya msingi. Pia alisema si vizuri kuhisi watu kufanya uovu kwa kigezo cha imani yao. Dk. Nasif, alisema kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu, anayeua mtu bila ya sababu akidhani kwa kufanya hivyo atakwenda peponi, ajue kwamba makazi yake yatakuwa ni motoni, kwani Uislamu siku zote unafundisha juu ya mahusiano mema baina ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu. Kwa upande wa Askofu Gamanywa, alisema malengo makuu katika kila dini ni matatu, ambayo ni kuabudu, kueneza imani ya dini husika na tatu kutoa huduma za kiijamii kwa wanaohitaji. Lakini Askofu Gamanywa, alieza kwamba mambo hayo ili yaweze kufanyika yanahitaji usawa pasi na vikwazo. Alibainisha kwamba kuta zilizopo baina ya dini hizo mbili, (Uislamu na Ukristo) ndio sababu kuu ya viashiria vinavyoshuhudiwa vya kuvunjika kwa mahusiano kunakotokea hivi sasa. Akizungumza katika mkutano huo mara baada ya mapendekezo ya kuundwa kwa kamati hiyo, Maalim Ally Bassaleh, alisema Askofu Gamanywa, amesema kwamba hakutarajia kusikia yale ambayo yamesemwa katika mkutano huo, kwamba Uislamu haukubaliani na vitendo vya kuuwa. Alisema kutokana na hali inayoendelea hivi sasa, picha inayotolewa ni kwamba Waislamu ni watu hatari na watu wasiokuwa na mahusiano mema na wasiokuwa Waislamu Jambo la Waislamu na Wakristo kukaa pamoja na kujadiliana juu ya jambo ambalo ni sawa baina yao lilishaagizwa katika Qur an tukufu. Alisema Maalim Bassaleh. Akifafanua kwa

Habari

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 1 - 7, 2013

AN-NUUR

SHEIKH Suleiman Kilemile kusherehesha aya ya Qur an inayozungumzia suala hilo, Maalim Bassaleh alisema Mwenyezi Mungu amewataka Wa i s l a m u k u s e m a k w a kuwaambia watu wa Kitabu (Mayahudi na Wakristo) kuwa (njooni) wakutane katika lile jambo (neno) lililosawa baina ya Waislamu na wao.

Al-jazeera kulipeleka Mtanzania Mahakamani


Na Bakari Mwakangwale

UONGOZI wa Chuo cha Kiislamu cha Al-jazeera (Al Jazeera Aslamic Centre) kilichopo visiwa vya Ukerewe Jijini Mwanza, umesema utalipeleka Mahakamani Gazeti la Mtanzania, endapo litakaidi kukanusha taarifa zake kuwa chuo hicho kinatoa mafunzo ya kigaidi. Uongozi wa Taasisis hiyo umekanusha habari ilizochapishwa na gazeti la Mtanzania toleo la tarehe 13 Februari 2013, na toleo la tarehe 20 februari 2013 zikikitaja kituo hicho kufadhiliwa na makundi ya Al-Qaeda na Al-Shabab yanayoaminika kuwa na mtandao mkubwa wa ugaidi duniani. Akizungumza kwa masikitiko na mwandishi wa habari hizi, Sheikh Jabir Yusuph Katura, ambaye ni mmoja wa viongozi wa Chuo hicho alisema uongozi na wadau kwa ujumla wa Chuo hicho walizipokea taarifa hizo kwa mstuko mkubwa. Alisema wao kama viongozi wa bodi ya kituo hicho, tayari wamekutana kujadili kashfa iliyoelekezwa dhidi ya chuo hicho. Kwa kupitia kwa

wakili wao, wameuandikia Mhariri wa Gazeti hilo wakimtaka akanushe taarifa hizo au athibitishe ndani ya siku saba. Sheikh Jabir, alisema katika barua hiyo kuna mambo kadhaa wameyaainisha, ikiwa ni pamoja na kutaka kulipwa fidia kwa kiasi cha pesa kilichopangwa, ambacho ni bilioni mbili, sambamba na kumsasha Mwenyekiti wao wa Bodi kwa kumuita Muuaji. Tumelitaka gazeti hilo (Mtanzania) likanushe taarifa zao za uzushi dhidi ya chuo chetu, au wathibitishe yote waliyoyaripoti. Tumewapa siku saba, wakanushe na watuombe radhi, kinyume chake wakikaidi tutawapeleka Mahakamani. Alisema Sheikh Jabir. Alisema habari zilizoripotiwa na gazeti hilo ni za uongo, uzushi na ufitini. Alisema kwa uhalisia, kituo chao hakifanyi shughuli yeyote yaliyo nje ya masuala ya elimu ya dini. Alisema hata hayo mazoezi ya kareti na judo, pamoja na kuwa si kosa kufanya michezo hiyo kisheria, lakini wao hawatoi mafunzo hayo. Pia alisema kituo hicho hakina watoto wadogo,

kama ilivyoripotiwa bali kuna vijana wenye umri kati ya miaka 15-30. Hata hivyo alisema wakazi wanaoishi jirani na kituo hicho wameshangaa kusikia taarifa hizo. Aliongeza kuwa wakazi hao wamesikika katika vyombo vya habari wakihojiwa wakisema kwamba, hawajawahi kuona watu wakiingia chuoni kwa mitumbwi wala Makontena kama ilivyoripotiwa, kwani hakuna mtumbwi unaoweza kubeba Kontena. Maelezo ya gazeti la Mtanzania yalikuwa yamejaa chuki za kidini dhidi ya Uislamu kwani yote waliyoyasema ni uzushi mtupu. Hata huo uzio waliosema si kama walivyoandika, bali ni wa kawaida sana hata mtu akitumia nguvu anaweza kuuvunja. Alisema Sheikh Jabir Naye Sheikhe Musa Kunenge, ambaye naye ni miongoni mwa waanzilishi wa Chuo hicho amesema kuwa, chuo chao kilipata idhini ya Waislamu kwenye msikiti, kisha kikafuata taratibu zote za kisheria, ikiwa ni pamoja na kupata kiwanja na baadae usajili na shughuli zote zinatendeka kwa haki na uhalali.

Inatoka Uk. 1

Jaji akerwa upande wa mashtaka kupoteza muda kesi ya Uamsho


ombi hilo, na kujibiwa na Mwanasheria wa serikali kutoka Osi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, Ramadhan Naseeb kuwa ni kweli ombi hilo limepokelewa tangu mwaka jana na sio jipya. Hivyo alimtaka mwendesha mashtaka huyo kuwasilisha maelezo yake ya kuweka pingamizi hizo wakati ombi hilo litakaposikilizwa kwa kuwa ombi hilo sio jipya dhidi ya upande wa serikali. Kusikiliza ombi ni Februari 28 mwaka huu serikali kama mtapinga ni siku hiyo hiyo na kama mtaleta ombi ni siku hiyo, Nasema nisingependa kupoteza muda kwa maelezo ya mambo ya kiufundi. Na kuahirisha kesi hadi siyo hiyo niliyoitaja. Alisema Jaji Mwampashi Aw a l i M w e n d e s h a Mashitaka wa Serikali Ramadhani Naseeb, aliiomba Mahakama Kuu ya Vuga kutosikiliza ombi la kuondoa pingamizi la dhamana katika kesi inayowakabili viongozi wa Jumuiya ya Uwamsho na mihadhara ya Kiislamu. Naseeb alitoa ombi hilo baada ya upande wa utetezi kuwasilisha barua ya kuitaka Mahakama kufanya mapitio kuhusu pingamzi iliyowekwa na upande wa Mashtaka ya kuzuia wateja wao wasipewe dhamana, ambapo Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar (DPP) kwa mamlaka aliyopewa amefuta dhamana za washitakiwa hao. Washtakiwa hao ni Sheikh Farid Hadi Ahmed (41) mkaazi wa Mbuyuni, Mselem Ali Msellem (52), mkaazi wa Kwamtipura, Mussa Juma (37), mkaazi wa Makadara, Azzan Khalid Hamdani (43), mkaazi wa Mfenesini, Suleiman Juma, mkaazi wa Makadara, Khamis Ali na Hassan Bakari (39), mkaazi wa Tomondo. Washitakiwa wote kwa pomaja wanakabiliwa na mashtaka matatu yakiwemo Uharibifu wa mali, Kushawishi, kuchochea na kuwarubuni watu kufanya fujo, huku mshitakiwa Azan akikabiliwa na makosa manne moja likiwa la uvunjifu wa amani. Mawakili wa upande wa utetezi wakiongozwa na Salim Towfiq, Abdallah Juma na Suleiman Salim, waliwasilisha mapema ombi la kuitaka mahakama kufanya mapitio kuhusu pingamizi iliyowekwa na

Habari

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 1 - 7, 2013

AN-NUUR

wa washitakiwa kuhusu pingamizi ya dhamana. Jaji Mwampasi alitoa ufafanuzi huo wakati akisikiliza kesi ya viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) na kusema, asingependa kupoteza muda kutokana na madai ya kuwepo mambo ya kiufundi (technicality) yanayokwamisha serikali kutoa maelezo ya kuzuia dhamana kwa washatakiwa. Alifafanua kwamba, iwapo kuna maelezo yeyote juu ya pingamizi lao, basi ni vizuri Serikali ikatoa maelezo yake siku ambayo kesi itasikiliwa mahakamani hapo. Jaji Mwampashi alisemza mahakamani hapo kwamba, angependa kujua sababu za upande wa mashtaka kutoka osi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar (DPP), kutoleta utetezi wao mapema huku ikizingatiwa kuwa muda wa kesi hiyo ulikuwa ukiendelea kuyoyoma ambapo kisheria ingetakiwa kesi kuanza kusikilizwa. Alisema kwa kuwa kesi ya msingi tayari ipo, ni vizuri mahakama ikaendelea kusikiliza hoja ya serikali juu ya pingamizi hilo na wala asingependa kupoteza muda kuchrelewa kupata maelezo hayo kwa kuelezwa sababu zinadaiwa kuwa ni za kiufundi, kwa kuwa ombi kuhoji sababu za kuzuia dhamana lilitolewa na upande wa utetezi tangu mwaka jana. Kesi ya msingi bado ipo mahakamani. kilichotakiwa kusikilizwa pale ni ombi la kuondoa pingamizi, nisingependa kupoteza muda kwa maelezo ya mambo ya kiufundi. Kimsingi nimepokea ombi lakini sio jipya, sasa kama mna chochote mtakisema hiyo siku,alisema Jaji huyo na kuongeza kuwa anataka kufahamu kutoka upande wa serikali kuwa ni kitu gani wanakipinga wakati hakuna kifungu cha sheria kinachozuwia. Jaji Mwampashi alihoji upande wa serikali kama wanaona mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza

Inatoka Uk. 1 Changombe. Alisema kuwa hata anayedaiwa kumiliki eneo hilo kupitia kampuni ya Agritanza, Bw. Suleiman alisema kuwa alilazimika kusimamisha ujenzi kwa kuwa eneo husika lina mgogoro wa ardhi. Hivyo ushahidi wake ulidhihirisha kwamba kesi iliyokuwa inastahili kusikilizwa ni ya mgogoro wa ardhi na sio uchochezi, kuiba mali au vinginevyo. Wakili Nassoro, alisema kesi hiyo ililetwa Mahakani hapo kwa jazba lakini haikustahili kusikilizwa katika Mahakamani hiyo. Aidha alisema kuwa hata mafundi ujenzi wa uzio uliowekwa na wamiliki wa Kampuni ya Agritanza, inayodaiwa kumiliki kiwanja hicho, waliithihitishia Mahakama kwamba Sheikh Ponda na wenzake, hawakuwahi kuiba mali. Alisema kuwa vifaa

Wakili: Sheikh Ponda hawana kesi ya kujibu


vinavyodaiwa kuibwa, vilitumika kwa ujenzi wa Msikiti wa muda katika eneo hilo. Hata mashahidi wa upande wa mashtaka kutoka Bakwata, hawakuthibisha kuwepo wizi wa mali, na hata walipohojiwa hawakuweza kutoa ushahidi wa moja kwa moja kuhusu kiwanja hicho. Alisema hata eneo linalodaiwa kuwa walipewa na Agritanza, ili kubadilishana na eneo lililopo hapo Markaz Changombe, nalo hawalijui zaidi ya kusema tu kuwa lipo Kisarawe. Aliongeza katika utetezi wake kuwa nao maosa ardhi hawakuweza kufikishwa Mahakamani kuthibitisha ukweli wa umiliki wa kiwanja hicho kwa mlalamikaji, japo kuna barua ililetwa kutoka ardhi, lakini Wakili Nassoro alisema barua hiyo haitoshelezi, bali wahusika walitakiwa kuka mbele ya Mahakama ili kuthibitisha mmiliki halali wa eneo

Mkurugenzi wa Mashitaka ya kuzuia dhamana ya washitakiwa hao. Touk alisema kuwa ni vyema mahakama ikatumia busara ya kulisikiliza ombi hilo kwa sasa kutokana na

wateja wake kuwa ndani kwa muda mrefu sasa. Wa s h i t a k i w a h a o wamerejeshwa rumande hadi Febuari 28 mwaka huu, kwa kusikilizwa pingamizi yao.

hilo. N a y e w a k i l i Ya h y a Njama, alisema kuwa hata katika tukio la kukamatwa watuhumiwa, halikufanyika katika eneo la mgogoro, bali watuhumiwa walikamatwa wakiswali usiku katika Msikitini wa Markazi, uliopo katika chuo kinachoongozwa na Wamisri ambao ndio wamiliki wa chuo hicho, tofauti na ilivyodaiwa kuwa walikamatwa wakiwa katika kiwanja kinacholalamikiwa. Hivyo mawakili hao wa upande wa utetezi wamedai kuwa, kulingana ushahidi wa upande wa mashtaka ambao tayari umeshawasilishwa Mahakamani hapo, haionekani watuhumiwa wanashtakiwa kwa makosa gani. Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Bi. Victoria Nongwa, ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 4, 2013, kwa ajili ya kuendelea kusikiliza upande wa utetezi.

BAADHI ya washitakiwa katika kesi ya Sheikh Ponda wakiwa Mahakama ya Kisutu jana kusikiliza utetezi wao.

Habari za Kimataifa

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 1 - 7, 2013

AN-NUUR

CAIRO Rais Mohammed Morsi wa Misri, ametangaza kufanyika kwa uchaguzi wa Baraza la Bunge la nchi hiyo Aprili 27 katika vipindi vinne, na kikao cha kwanza cha Baraza hilo kitafanyika Julai 6. Kwa mujibu wa amri hiyo ya Rais, katika kipindi cha kwanza, upigaji kura katika uchaguzi huo utafanyika katika mikoa mitano ikiwemo Cairo, Port Said na El-Minya, kuanzia tarehe 27 hadi 28 Aprili, katika awamu ya pili upigaji kura utafanyika katika mikoa minane ikiwemo Giza, Alexandria na Suez kuanzia Mei 15 hadi 16, na awamu ya upigaji kura huo utafanyika katika mikoa mingine minane ikiwemo Luxor, Qena na South Sinai kuanzia Juni 2 hadi 3 mwaka huu. Awamu ya mwisho upigaji kura utafanyika katika mikoa sita, ikiwemo Assiut na Fayoum kuanzia Juni 19 hadi 20. Mwezi Juni mwaka jana, Mahakama Kuu ya Misri ilitoa uamuzi wa kupinga

Uchaguzi wa Bunge la Misri kufanyika Aprili


uteuzi wa Baraza la chini la Bunge la nchi hiyo lililochaguliwa mwanzoni mwa mwaka jana na kutaka livunjwe kwa kuwa baadhi ya vifungu vya sheria ya uchaguzi vinakiuka katiba. Hata hivyo taarifa zinaeleza kwamba Rais Muhammad Mursi, ametoa wito wa kufanyika mazungumzo na makundi ya upinzani kuhakikisha kuwa kunapatikana uadilifu na uwazi katika uchaguzi ujao wa Bunge Aprili 22. Mursi ametupilia mbali madai kwamba tarehe ya uchaguzi hakupangwa katika muda mwafaka na kusema kuwa, hali ya sasa ya Misri inafaa kwa uchaguzi. Rais Musri pia amesema kuwa yeye ni Rais wa Wamisri wote na kwamba, hana ugomvi na chama chochote cha kisiasa. Baadhi ya vyama vya upinzani nchini humo vimetishia kususia uchaguzi huo wa Bunge, vikimtuhumu Mursi na chama chake cha Ikhwanul Muslimin kungangania madaraka.

Iran kutengeneza vituo vipya 16 vya nyuklia Shule za Kiislamu zangara Uingereza
Rais Mohammed Morsi wa Misri TEHRAN K i t e n g o kinachoshughulikia nishati za nyuklia cha Jamhuri ya Kiislam ya Iran, Atomic Energy Organisation (AEOI), kimetangaza azma yake ya kuendeleza teknolojia hiyo kwa kutengeneza vituo vipya kumi na sita vya nyuklia katika siku zijazo. Jitihada hizo zinaendelea wakati Marekani na raki zake wakiendelea kuishinikiza Jamhuri hiyo ya Kiislamu kuacha mpango wake wa nyuklia wenye malengo ya amani, ambao unafanya kazi zake chini ya wasimamizi wa umoja wa mataifa. AEOI imeeleza katika taarifa yake mwishoni mwa wiki kwamba, mitambo hiyo mipya ya nishati itajengwa kuzunguka nchi, yakiwemo maeneo ya upande wa jirani na bahari ya Caspian Kaskazini na upande wa Ghuba na Bahari ya Oman Kusini. Jimbo la Kusini la Khuzestan na majimbo mengine ambayo hayakutajwa Kaskazini Magharibi pia ni sehemu ya maneo mapya yalipangwa kujengwa vinu hivyo. Wakati Iran ikiwa na mpango wa kuongeza vinu vyake vya nishati, nchi hiyo inajiandaa kuingia katika mazungumzo juu ya nishati ya nyuklia na Mataifa sita ambayo ni Marekani, Uingereza, Ufaransa, Urusi, China na Ujerumani Jumanne, baada ya mazungumzo hayo kukwama kwa miezi nane. Akizungumza katika mkutano wa maofisa wa nyuklia jijini Tehran, Saeed Jalili, ambaye ni Osa wa ngazi za juu wa Masuala ya Usalama na mashauriano ya nyuklia, ameyataka mataifa hayo sita kuja na mipango sahihi na yenye hadhi, ambayo haina makosa ya siku za nyuma.
LONDON SHULE za Kiislamu nchini Uingereza, zimetajwa kuwa ni miongoni mwa shule bora kwenye orodha za taasisi za kielimu nchini humo, kufuatia wanafunzi wa shule hizo kufanya vyema kwenye masomo yao. Shirika la Habari za Qurani la Kimataifa IQNA, limemnukuu Hamid Patel, Mkuu wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Tawhidul Islam akisema kuwa, wanafunzi Waislamu nchini Uingereza wanafanya vizuri kwenye masomo yao licha ya kukabiliwa na matatizo mengi. Shule ya sekondari ya wasichana ya Tawhidul Islam, iliyopo katika mji wa Blackburn pamoja na shule nyingine, zimeongoza kwenye orodha ya shule zilizofanya vizuri kimasomo katika mji huo. Takwimu zilizotolewa na Idara ya Elimu ya Uingereza zinaonyesha kuwa, shule hiyo ndio bora zaidi nchini humo katika kuandaa mazingira ya mafanikio kwa mwanafunzi, kufuatia kukosekana kiwango kizuri kwenye shule nyingi za msingi. Mbali na shule ya Tawhidul Islam, zipo shule nyingine kadhaa za Kiislamu nchini humo ambazo wanafunzi wake wamefanya vizuri na kuongoza kwenye taasisi za kielimu nchini humo. Uingereza kuna karibu

KHARTOUM Kiongozi mwandamizi wa harakati ya Ikhwanul Muslimiin nchini Sudan, Ali al Jawish, amesisitiza haja ya kuwepo udharura wa kutekelezwa sheria ya Kiislamu nchini humo. Akizungumza na vyombo vya habari mjini Khartoum, Ali al Jawish, ameongeza kuwa mfumo wa kisekula hauna nafasi yoyote nchini Sudan na kwamba wananchi wa nchi hiyo wanataka sheria za Kiislamu zitekelezwe kwa lengo la kukabiliana na ufisadi, migogoro ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Kiongozi huyo wa

Wasudan wataka sheria za Kiislamu

Waislamu milioni 2.5 mbili kwa mujibu wa takwimu za Baraza la Waislamu nchini humo, ambapo kuna karibu wanafunzi laki nne ambao wanasoma katika shule mbalimbali.

harakati ya Ikhwanul Muslimiin nchini Sudan,

makundi na matabaka yote nchini humo kwa lengo la kukabiliana na njama za dola za kibeberu za Magharibi. Hivi karibuni vyama na makundi ya Kiislamu nchini Sudan, yalitia saini makubaliano yaliyopewa jina la Fajrul Islami, ambayo yametaka kupitishwa katiba ya Kiislamu ambayo marejeo yake ni Qurani Tukufu na Suna za Mtume Muhammad (SAW).

amesema kuwa kuna udharura pia wa kuwepo jitihada za kushirikiana

Makala

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 1 - 7, 2013

AN-NUUR

Uvamizi halisi wa Afrika si habari, leseni ya kusema uwongo ni zawadi ya Hollywood


Na John Pilger maonyesho, zitoe mwavuli wa vita takatifu dhidi ya ukanda wa hatari wa ugaidi wa Kiislamu, usio na tofauti na porojo za hatari nyekundu ya mkakati wa ukomunisti kote duniani. Ikikumbushia vikumbo vilivyopiganwa kugawana Afrika mwisho wa karne ya 19, Kamandi ya Marekani kwa Afrika (Africom) imeunda mtandao wa vibaraka kati ya dola sikivu za Kiafrika zenye uchu wa hongo na silaha za Marekani. Mwaka jana, Africom ilifanya Operesheni Juhudi ya Afrika na majeshi ya nchi 34 za Afrika yakishiriki, yakiamrishwa na jeshi la Marekani. Kaulimbiu ya askari kwa askari ya Africom inaunganisha maofisa wa kijeshi wa Marekani katika kila ngazi ya amri kutoka jenerali hadi osa wa mnazi, saa mkononi. Ni koa za safari za utalii ndizo zinakosekana. Ni kama vile historia ya kujivunia ya ukombozi, kutoka Parrice Lumumba hadi Nelson Mandela, imefukiwa na kusahaliwa na tabaka teule la watu weusi

Januari 31, 2013Mtandao wa kupashana habari UVAMIZI wa jumla wa Afrika umeanza. Marekani inapeleka askari katika nchi 35 za Kiafrika, ukianza na Libya, Sudan, Algeria na Niger. Ikiripotiwa na shirika la Associated Press siku ya Christmas, habari hii haikuonekana katika vituo vya habari vya Marekani na Uingereza. Uvamizi huo hauna uhusiano na kinachoitwa ni harakati ya Uislamu, ila kila upande inahusiana na kushika rasilimali, hasa madini, na ushindani unaoendelea na China. To f a u t i n a C h i n a , Marekani na washirika wake wako tayari kutumia nguvu kwa kiwango kilichoonekana nchini Irak, Afghanistan, P a k i s t a n , Ye m e n n a Palestina. Kama ilivyokuwa wakati wa vita baridi, mgao wa majukumu unahitaji kuwa uandishi wa habari wa nchi za Magharibi na sanaa za

TAI alama ya jeshi la Marekani akitua Jangwani chini ya bwana mkubwa mpya ambao jukumu lao kihistoria, alionya Frantz Fanon nusu karne iliyopita, ni kushabikia ubepari iliojizatiti licha ya kuwa umejicha. Kielelezo kimojawapo cha haja ni Kongo Mashariki, yenye utajiri wa kumwaga wa madini yanye umuhimu mkubwa kimataifa, inayoshikiliwa na kundi katili la M23, ambalo linashikwa na Uganda na Rwanda, ambao ni wasimamiaji wa mahitaji ya Marekani. Ikiwa imepangwa kwa muda mrefu kama jukumu la Nato, bila kutaja Ufaransa yenye shauku kali, ambayo agenda zake za ukoloni zilizoshindwa zipo kando kuinuliwa wakati wowote, vita juu ya Afrika ilifikia kuwa ya haraka mwaka 2011 wakati nchi za Kiarabu zilipoonyesha kujikomboa kutoka kwa kina Mubarak na wateja wengine wa Washington na Ulaya. Mfadhaiko ambao hali hii ilisababisha katika tawala za kibeberu, hauwezi kuongezewa chumvi. Ndege za kuangusha mabomu zilipelekwa siyo Tunis au Cairo ila Libya, ambako Muammar Gadda alikuwa akitawala juu ya hazina kubwa zaidi ya mafuta katika Afrika. Wakati mji wa Sirte nchini Libya ukiwa umebaki magofu, vikosi maalum ya Uingereza vya SAS vilielekeza mgambo waasi katika kile ambacho sasa kimefuchuliwa kama uwagaji damu kwa misingi ya rangi. Wa k a z i a s i l i a w a Sahara. wa-Tuareg ambao wapiganaji wake wa kiBerber Gadda aliwalinda, walikimbilia nyumbani kupitia Algeria na Mali, ambako wa-Tuareg wamekuwa wakitaka nchi yao pekee tangu miaka ya 1960. Kama mdadisi makini Patrick Cockburn anavyoonyesha, ni mzozo huu wa kikanda, siyo Al Qaeda, ambao nchi za Magharibi zinaogopa zaidi katika Afrika KaskaziniMagharibi. Licha ya kuwa maskini, mara nyingi wanaishi juu ya hifadhi kubwa za mafuta, gesi, urani na madini mengine ya thamani kubwa. Ikiwa kwa uhakika ni matokeo ya kushambuliwa na Ufaransa na Marekani kwa Mali hapo Januari 13, kuzingirwa kwa eneo la visima vya gesi nchini Algeria kuliisha kwa umwagaji damu, na kuinua hisia ya ki-Septemba 11 kwa David Cameron. Mpambaji huyo wa zamani wa Carlton TV, alighadhibika kuhusu hatari kwa dunia inapohitaji miongo kadhaa ya mapambano ya nchi za Magharibi (dhidi yake). Alikuwa na maana ya kuingizwa kwa mipango ya biashara ya nchi za Magharibi kwa Afrika, pamoja na ubakaji wa nchi ya Syria yenye tamaduni kadhaa tofauti, na kuanguka kwa Iran iliyo huru. Cameron sasa ameamuru askari wa Uingereza wapelekwe Mali, na kupeleka ndege moja isiyo na rubani ya jeshi la anga la Uingereza, ambayo mkuu wake wa majeshi anayependa kubwabwaja, Jenerali Sir David Richards, amepeleka ujumbe bayana kwa Mujahidina Inaendelea Uk. 7

TANGAZO! TANGAZO! TANGAZO! SHAMBA LINAUZWA


SHAMBA LA EKARI 14 LINAUZWA KWA HARAKA LIPO CHAMAZI-DOVYA DAR ES SALAAM BEI NI MAELEWANO KWA MAWASILIANO: PIGA SIMU: 0754 479783 0784 463207 0756 450425 WAHI MAPEMA BAHATI NI YAKO

Uvamizi halisi wa Afrika si habari, leseni ya kusema uwongo ni zawadi ya Hollywood


Inatoka Uk. 6
kokote duniani: Msikae karibu, kukabiliana nasi. Tutawashughulikia kwa dhati - ambacho hasa ndicho Mujahidina wanataka kusikia. Wa l i k o p i t i a w a h a n g a wa vitendo vya kikatili vya jeshi la Uingereza, wote Waislamu, kuteswa kwao kitaalamu ambako kesi hizo zinapelekwa mahakamani sasa, kunaongeza mzaha usiohitajika katika maneno ya jenerali. Niliwahi kuona kwa karibu njia za dhati za Sir. David nilipomwuliza kama aliwahi kusoma maelezo ya mwanamke mwanaharakati jasiri wa Afghanistan Malalai Joya, akizungumzia hulka za kishenzi za watu wa Magharibi na vibaraka wao nchini kwake. Wewe ni mtetezi wa Taliban ndilo lilikuwa jibu lake. (Baadaye aliomba radhi). Waigizaji haw a w a kukatisha tamaa wanatoka moja kwa moja kwa Evelyn Waugh na kutuwezesha sisi kuhisi upepo baridi wa historia na unafiki. Huo ugaidi wa Kiislamu ambao ndiyo kisingizio chao cha wizi unaodumu w a utajiri w a A frika uliundwa takriban wote na wao. Hakuna haja iliyobaki kumeza mstari wa BBC / CNN na siyo kujua ukweli. Soma kitabu cha Mark Curtis Mambo ya Siri: Ushirikiano wa Uingereza na Uislamu Mujahidina. (Serpents Tail, ambao ni wachapishaji) au cha John Cooley, Vita isiyo takatifu: Afghanistan. Amerika na ugaidi wa kimataifa. (Pluto Press) au Meza kubwa ya chess cha Zbigniew Brzezinski (HarperCollins), ambaye alikuwa mkunga wa kuzaliwa kwa ugaidi wa kimataifa wa siasa kali. Katika hali halisi, Mujahidina wa Al Qaeda na Taliban waliundwa na CIA, shirika dada la Pakistan la ISI (mtandao wa ujasusi wa majeshi yote ya usalama) na MI6 (mtandao wa ujasusi wa jeshi la Uingereza). Brzezinski, aliyekuwa mshauri wa usalama wa taifa wa Rais Jimmy Carter, anaelezea elekezo la siri la Rais la 1979, ambalo lilianzisha kile ambacho kimekuwa vita dhidi ya ugaidi sasa. Kwa miaka 17, Marekani kwa dhamira iliunda, kutoa fedha, silaha na msasa wa propaganda kwa Mujahidina wa siasa kali ambako hulka ya kutwaa silaha ilipenya kizazi chote (cha vijana) cha wakati huo. Ikiwa inaitwa Operesheni Kimbunga, hii ndiyo ilikuwa mchezo mkubwa kuiangusha Urusi lakini uliyaangusha majengo ya minara pacha. Kuanzia wakati huo, habari ambazo watu werevu, waliosoma wanapata na kutumia

Makala

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 1 - 7, 2013

AN-NUUR

zimekuwa uandishi kama sinema, ukiongezewa nguvu kama ilivyo jadi na Hollywood (eneo la kutengeneza lamu nchini Marekani), kuwa na leseni ya kusema uwongo, tena na tena. Kuna sinema inayokuja Dreamworks (kazi za ndoto) kuhusu WikiLeaks (mtandao uliovujisha siri nyingi za jeshi la Marekani na taarifa za kijasusi za Marekani), upikaji habari uliohamasishwa na kitabu cha hujuma cha waandishi wawili wa The Guardian (gazeti la Uingereza) waliojazwa mapesa, na pia kuna Zero Dark Thirty, ambacho kinashabikia utesaji na mauaji, iliyoongozwa na Kathryn Bigelow, m-Leni Riefenstahl wa wakati wetu, kuikuza sauti ya mfadhili wake kama ilivyokuwa kwa mtengenezaji lamu habithi wa Adolf Hitler. Hicho ndicho kioo cha upande mmoja ambako hatupati hata chembe ya picha ya kile ambacho wenye madaraka wanafanya kwa jina letu. www.johnpilger.com

Pichani juu na chini ni washindi wa kuhifadhi Qur'an wakipokea zawadi zao kutoka kwa Sheikh Hijja (wa pili kutoka kushoto) katika Msikiti wa Makukura, Buguruni jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yaliandaliwa na taasisi ya Africa Muslims Agency.

TANGAZO
VITABU VIPYA VYA MIHADHARA, MASWALI NA MAJIBU BAINA YA WAHADHIRI WA KIISLAMU NA WACHUNGAJI, PAMOJA NA MAWAIDHA YA SHEIKH NURDIN KISHKI. VINAPATIKANA MSIKITI WA MTORO (DUKANI KWA SAIMU) KARIAKOO. PIA VINAPATIKA KATIKA MADUKA YOTE YA VITABU VYA DINI JIJINI DAR ES SALAAM, KWA JUMLA NA REJAREJA. PATA NAKALA YAKO SASA. 0713 47 10 90, 0685 47 10 90, 0773 19 46 6.

TANGAZO

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 1 - 7, 2013

AN-NUUR

Makala

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 1 - 7, 2013

AN-NUUR

KUUWAWA kwa kupigwa risasi Padri Evarist Mushi, huko Zanzibar ni lazima kulaaniwe sana na kila mtu anayechukia uhalifu wa aina yeyote ile katika jamii yeyote, hasa ikiwa hapa nyumbani Tanzanaia. Waislam wanafahamu Subhana wa Taala kasema nini kuhusu kutoa roho ya bin Adam bila kuwa na uhalali wowte. Ni wazi kabisa kuwa kutolewa kwa roho ya Padri Mushi, haukuwa na uhalali wowote; kadhulumiwa haki yake ya kuishi. Lakini hapo hapo wananchi watafakari kwamba yeye huyu hayati kuwa ni Mkristo ni matokeo tu. Muhalifu aliyefanya kitendo hicho ni muhalifu. Ikiwa atakishwa mahakamani pakiwa ushahidi wa kutosha, bila shaka atatiwa hatiani na atadhibiwa inavyostahili. Haya bila shaka hayana mjadala kwa vile hoja zote hapa zina mantiki. Lakini kufuatia uhalifu huu kumekuwa na maneno mengi sana ambayo yanaashiria kuwa, wengi wa wale waliotoa maneno hayo bila shaka wamechanganyikiwa. Sababu moja kubwa ya kuwa wamechanganyikiwa ni kuwa, hoja zao zimezingirwa na maslahi binafsi ambayo hasa, hayana uhusiano na uhalifu uliotokea, bali wameweza kuutumia uhalifu huo kwa maslahi yao wenyewe. Kwanza hebu msomaji ukiri tu kidogo, haiwezekani kuwepo muhalifu aliye Muislam na akafanya uhalifu kwa kuwa ni tabia yake ama katumwa. Idadi ya Wananchi wa Zanzibar ni takriban 92% ni Waislam, kwa hiyo kila uhalifu unaotokea humo nchini aliyetenda uhalifu huo kwa 92% atakuwa Muislam. Sasa itakuwa sawa kupiga kelele kuwa kufanya uhalifu kwa sababu ya Uislam wake? Ama Uislam ndio uliomtuma afanye uhalifu huo? Inaelekea kwamba katika hao waliopiga kelele sana juu ya kifo cha Padri Mushi, wamezuka tu kuwa kauawa

Na Khalid S Mtwangi

kwa sababu ya Ukristo wake na aliyemuuwa ni Muislam, na Uislam wake ndio uliomtuma afanye kitendo hicho cha uhalifu wa hali ya juu sana. Inasikitisha sana kuona na kusikia kuwa baadhi ya Masheikh, hasa wa Bara wamelivalia njuga jambo hili na wao kuwa mstari wa mbele kuhusisha mauaji haya na Uislam ,ambao wao wanasema ndio viongozi. Wakristo wamefarijika sana na matendo na maneno ya Masheikh hawa. Inabidi mtu atafakari sana kuwa waliokuwa na kelele nyingi ni Masheikh wa Bara ilihali wale wa Zanzibar kulikotokea mkasa huo wao walijichunga sana na matamshi yao. Viongozi wa Kikristo hasa wale wa Kanisa Katoliki wamejitokeza kwa nguvu na vitisho kuilaumu serekali kwa mauwaji hayo. Hao waliomuuwa mtumishi wa Mungu Padri Mushi, ni wale wanaofanya vitendo vyao vya uhalifu kwa kuvizia na hakuna serekali yeyote ile duniani inayoweza kuzuia kitendo kama hicho kabla hakijatokea. Pamoja na uwezo mkubwa wa pesa na vifaa vya kila aina, Marekani wameshindwa kuwanyamazisha Taliban huko Afghanistan kwa muda wa miaka zaidi ya kumi sasa. Kama inavyofahamika wao wamewaua wananchi wasiokuwa na hatia wa nchi hiyo wengi sana, lakini bado Marekani na washiriki wake wanauawa takriban kila siku na watu ambao kwa kawaida hawana uwezo kama walio nao Marekani na washiriki wake. Sasa kwa hawa viongozi wa Kanisa kutegemea Serikali ya Tanzania iweze mara moja kuzuia uhalifu wa kuvizia ni uonevu mkubwa sana. Hasa kwa vile kumekuwa na rai zikitolewa kuwa, haya yote yanatokea kwa sababu watu wa Zanzibar hawataki muungano na Kanisa ni alama kubwa ya Muungano. Hakika ni lazima ikubalike kuwa Muungano wa Zanzibar na Tanganyika kwa kiasi kikubwa umewezesha Ukristo kushamiri kwa kasi sana huko Visiwani. Kwanza Serikali zenyewe za Zanzibar walikuwa wakijivunia sana kuwa wao ni secular, bila kuwa upande wa dini yeyote. Lakini ukweli ni kwamba Ukristo uliachiwa kutanda kwa marefu na mapana, mpaka wakaweza kutoa maswali sabini na moja yaliyokuwa yakihoji sehemu kubwa za

Masheikh na mauaji huko Zanzibar


Uislam. Inajulikana kuwa wakati Mufti wa Zanzibar alikuwa akiwaruhusu Makanisa kuhubiri kwa marefu na mapana, wakati huo huo Waislam walikuwa wakizuiliwa kuwa na mihadhara ati inakashifu dini zingine. Imetajwa rai ya kutotaka muungano, na kwa vile makanisa ni alama ya muungano, ndio hapo wahalifu wamechukua hatua ya kuondoa alama ya muungano. Hebu tuikubali hoja hii ingawa ni dhaifu kidogo. Ikiwa hivyo ndivyo basi, kiini cha uhalifu huu wa kumuuwa Padri Mushi ni siasa kati ya baadhi ya watu walioko Zanzibar na baadhi ya walioko Tanganyika hasa Makanisa. Uislam unaingiaje hapa? Hebu Masheikh wetu wa Tanganyika watuelimishe. Haiwezekani akatokea muhalifu tu, ambaye ni muhalifu lakini akasema ni muumini wa Kiislam? Sasa inakuwa vipi uhalifu wake unahusishwa na imani yake? Ama damu ya mtu kama Padri Evarist Mushi, ni nzito kuliko ya Sheikh Ali Khamis Ali aliyepigwa mapanga mpaka kufa, ama Sheikh Soraga aliyemwagiwa tindi kali imdhuru na hakukuwa na kelele nyingi, wala haikuonekana kulikuwa na haja ya kuwaita G-Men wenye historia ya ukatili kwa Waislam? Sikumbuki kama kulitokea hata Sheikh mmoja huku Bara aliyejitokeza kwenye television au redio au magazetini kulaani kitendo kile, lakini baada ya kuuawa Padri Mushi, wanaojiita Masheikh kadhaa walihakikisha kuwa wanajitokeza haraka kwenye television waonekane wao ndio Waislam hasa, wanaolaani vitendo vya jinai vinavyotendwa na Waislam kuwatendea wasiokuwa Waislam. Na mpaka wakati huo haijajulikana ni nani kamuuwa Padri Mushi wala sababu iliyomtuma amuuwe binadam mwenzie. Walijuaje kama kitendo kile kilitendwa chini ya mwavuli wa Uislam? I N A S TA A J A B I S H A , INAELEKEA KUWA KWA SABABU YA KITENDO HIKI CHAPADRE KUUAWA NA MTU ASIYEJULIKANA IKAWA HATA VIONGOZI WA KIISLAM KUTOKA

Padri Evarist Mushi N C H I J I R A N I N A O Zanzibar imeendelea vizuri WAALIKWE KUKILAANI sana katika biashara ya utalii; matamshi ya vitisho KITENDO HICHO. Fedha zilizotumika kwa yanaweza kuwa na athari safari za viongozi hao na ya kuwatisha watalii wasite haa iliyofanyika, bila shaka kuamua kuitembelea. Kitendo kama hicho bila ilikuwa ya gharama kubwa. Hivi kweli ilistahili kuwa shaka kinaweza kuathiri hivyo wakati kuna sehemu u c h u m i w a Z a n z i b a r. nyingi sana za Waislam Wasemaji wawe waangalifu nchini wanahitaji misaada, sana na hakika ni kupiga pengine ya kumalizia msikiti zumari kwa sauti ya juu sana, wanaoujenga, ama hata kupiga kelele kuwa ugaidi umeingia Zanzibar. madrasa na shule za Kiislam, Tanzania imewaingiza lakini hawapati misaada t h e F e d e r a l B u r e a u o f hiyo. Investigation (FBI) Wako vijana wengi sana wa kuchunguza mauwaji ya Kiislam ambao wanashindwa Padri Evarist Mushi, kupoteza kuendelea na masomo kwa roho yake ni kuzito kiasi sababu ya uwezo mdogo cha kustahili hatua kama kifedha. Lakini hakuna hiyo. Hawa wanaoitwa Gmasheikha wanaojitokeza men kwa ukatili wao, wako kuwasaidia kwa hilo. Haya tayari kutumia silaha kwa m a p e s a y a l i y o t u m i k a haraka sana, maswali baadae. Waislam wa Iraq, Afghanistan kuwapoza moyo Wakristo na Mashariki ya Kati kwa kwa kuuliwa kiongozi wao jumla wanayafahamu hayo hazingeweza kutumika kwa vizuri sana. maslahi ya Waislam? Mpaka leo wengi ni vilema. Tafadhalini Masheikh Mwanzilishi wa kikosi hicho, wetu, epukeni kutumiwa Edgar Hoover ,aliweka msingi kwa maslahi ya maadui wa wa ukatili huo. Ni matarajio kuwa watu wa Zanzibar Uislam. Lingekuwa ni jambo la watahudumiwa kiasi kwamba labda hawatasahau ujio wa maana sana, kwa wale ambao hawa G-men. wako mstari wa mbele kutoa Ta f a d h a l i M a s h e i k h matamshi ya kila aina kuhusu watuambie nini khatma, mkasa huu, wawe wakikiri ama hukmu ya Muislam kwanza kabla ya kutoa hizo anayeshirikiana na maadui wa nasaha zao. Uislam kuuhujumu Uislam Kudai kuwa kule Zanzibar na kuwahujumu Waislam sasa kuna ugaidi kwa sababu wenzake! Mwenyeezi Mungu Padre ameuawa, bila shaka ni Subhana Wa Taala atunusuru kutia chumvi sana. Itambulike Waislam wa Tanzania na kuwa labda kuliko Bara, mfumo usiowajali wao.

10
MAELFU ya waombolezaji tarehe 25 Februari 2013 walihudhuria maziko ya Arafat Jaradat, ambaye alikufa siku ya Jumamosi akiwa katika gereza la Israel. Jaradat, mwenye miaka 30, alikufa katika jela ya Megiddo wiki moja baada ya kukamatwa na majeshi ya uvamizi ya Israel. Uchunguzi wa mwili wake umeonyesha kuwa alikufa kutokana na kuteswa, wakati wavamizi wa Israel wakidai kuwa eti alikufa kutokana na ugonjwa wa moyo. Takriban wafungwa 3,000 wa kipalestina wanaoshikiliwa bila ya mashtaka wala kuhukumiwa walitangaza kugoma kula kwa muda wa siku moja, kama ishara ya mshikamano wao na hasira zao kwa kifo cha Jaradat. Israel inadai Jaradat alikufa tarehe 23 Februari 2013, kutokana na moyo kusimama. Lakini Wakuu wa Palestina pamoja na familia yake na asasi za haki za binadamu, wote wanadai kuwa kifo chake kilitokana na matendo ya utesaji aliyofanyiwa akiwa kifungoni. Wanasema Arafat hakuwa na udhaifu wa moyo wakati alipokamatwa. Habari za kifo chake zilitangazwa siku moja baada ya Wapalestina 94 kujeruhiwa kutokana na kushambuliwa na majeshi ya Israel, wakati walipokuwa wakiandamana huko Ukingo wa Magharibi wakidai kufunguliwa kwa wafungwa wanne waliogoma kula. Hali duni ya wafungwa wa Kipalestina, hususan wafungwa waliogoma kula imesababisha Wapalestina wengi katika maeneo yaliyovamiwa na Israel kuandamana na ulimwengu umepatwa na wasiwasi. Mamlaka ya Palestina imetangaza siku tatu za maombolezo ili kuomboleza kifo cha Arafat Jaradat. Wa p a l e s t i n a w e n g i wameamua kuandamana katika mitaa ya Ukingo wa Magharibi, wakati hali ya wafungwa ikizidi kuwa duni katika jela za Israel. Zaidi ya Wapalestina 4,500 wamo katika magereza hayo, wengi wao bila ya kuhukumiwa wala kushtakiwa. Aidha haki zao za kimsingi

Makala

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 1 - 7, 2013

AN-NUUR

Mpalestina auawa kwa mateso katika Gereza Israel


zinazidi kudharauliwa, wakiwa wanateswa na kufungwa katika vyumba vya pekee bila ya kuruhusiwa kutoka nje. Arafat Jaradat aliuliwa wakati akihojiwa , alisema Issa Qaraqaa, Waziri wa Palestina anayehusika na masuala ya wafungwa. Tunataka iundwe Tume ya uchunguzi ya kimataifa ili kuchunguza kifo chake, aliongeza. Naye Waziri Mkuu wa Palestina Bw. Salam Fayyad, alielezea jinsi alivyohuzunika na kukasirishwa na kifo cha Jaradat. Alisisitiza kuwa, Israel haiwezi kukwepa lawama kwa vile Jaradat alifariki akiwa katika jela ya Israel. Huu ni uhalifu wa Mkataba wa Nne wa Geneva. Fayyad akaitaka jumuiya ya kimataifa kutekeleza wajibu wake wa kisheria na kimaadili, kwa kuilazimisha Israel itekeleze sheria za kimataifa. Bibi Hanan Ashrawi, mjumbe wa Kamati Kuu ya chama cha ukombozi wa Palestina (PLO), naye alisema Israel inawajibika kwa kifo cha Jaradat, na akaitaka UN na jumuiya ya kimataifa pamoja na mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu kuingilia kati mara moja kwa kufanya uchunguzi wa kifo chake. Bibi Ashrawi, pia alitoa mwito wa kuachiliwa mara moja na bila ya masharti kwa wafungwa wote wa Kipalestina walio katika magereza ya Israel. Kifo cha Jaradat ni ushahidi tosha kuwa hali ya wafungwa hao ni yenye hatari sana kwa maisha yao. Alisema Ashrawi. Arafat Jaradat, alikuwa mkaazi wa Hebron mwenye watoto wawili chini ya miaka mitatu, wakati mkewe ana mimba ya miezi minne Uchunguzi wa maiti umeonyesha kuwa alikufa kutokana na utesaji wa hali ya juu akiwa katika jela ya Israeli, na wala hakufa kutokana na ugonjwa wa moyo kama wanavyosingizia wavamizi wa Israel. Zaidi ya hayo, uchunguzi uliofanywa katika Israel, mbele ya maasa wa Palestina umedhihirisha kuwa Jaradat alikuwa na mifupa sita iliyovunjika katika sehemu za koo, uti wa mgongo, mikono

MMOJA wa Wapelestina waliouawa na majeshi ya Israel hivi karibuni.


na miguu. Aidha alikuwa na majeraha kadha mgongoni mwake na jeraha jingine la duara kifuani. Uchunguzi wote uliofanywa unathibitisha wazi kuwa, Jaradat alikufa kutokana na utesaji, hasa kwa vile ilidhihirika kuwa moyo wake haukuwa na udhaifu wowote. Hii inaonesha kuwa wavamizi wa Kisraeli walikuwa wakidanganya waliposema eti, alikufa kutokana na ugonjwa wa moyo. Kinyume chake, uchunguzi umeonyesha kuwa Jaradat alikuwa ameteswa sana mpaka kupatwa na majeraha makubwa katika sehemu za mabega, mgongo, shingoni, mkononi na kifuani . Rais wa shirika linaloshughulikia wafungwa wa Kipalestina, Bw Qaddura Fares, aliongeza kwa kusema kuwa uchunguzi umeonyesha kuwa Jaradat alikuwa pia na majeraha ndani ya mdomo, usoni na alitokwa na damu puani. Wakili wa Jaradat, Bw. Kameel Sabbagh pia alisema mfungwa huyo aliteswa na wachunguzi wa Kiisraeli. Wakili huyo alikuwepo wakati Jaradat alipokishwa mahakamani siku ya Alkhamisi, wakati Jaji wa Israel alipoahirisha kesi hadi baada siku 12. Nilipoingia mahakamani nilimkuta Jaradat akiwa ameketi juu ya kiti mbele ya Jaji. Mgongo wake ulikuwa umepinda na alionekana akiwa mgonjwa na mdhaifu, alinena Sabbagh. Nilipokaa karibu naye aliniambia alikuwa na maumivu makali mgongoni na sehemu nyingine mwilini mwake, kutokana na kupigwa na kuninginizwa kwa muda wa saa nyingi wakati anapohojiwa Sabbagh alisema Jaradat alionekana kuwa katika hali ya maumivu makali. Hivyo alimueleza Jaji kuwa mfungwa huyo alikuwa akiteswa. Jaji akaagiza kuwa Jaradat achunguzwe na daktari, lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa, aliongeza wakili huyo. Maelfu ya Wapalestina waliandamana wakilaani mauaji hayo katika maeneo ya Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza. Katika maadamano hayo watu wawili walijeruhiwa kwa kupigwa risasi za moto zilizofyatuliwa na majeshi ya Israeli. Mmojawapo alikuwa mtoto wa miaka 13. wengine wengi walijeruhiwa kwa risasi baridi. Nje ya jela kulikwa na askari wengi wa Israel wakijaribu kuwadhibiti Wapalestina waliokuwa wakilaani kufungwa kwa Wapalestina wenzao. Ripoti ya miezi mitatu (Septemba 2012 hadi Januari 2013) iliyotolewa na shirika la misaada kwa wafungwa (Addameer) na Jumuia ya Kutetea Haki za Binadamu, inasema kuna jumla ya wafungwa wa Kipalestina 4,743 katika magereza ya Israel. Ni pamoja na wafungwa 178 wasiohukumiwa, miongoni mwao wakiwemo wabunge 12 wafungwa kumi ni wa kike, pamoja na msichana mmoja chini ya miaka 18. Jumla ya wafungwa watoto ni 193, miongoni mwao 21 wakiwa chini ya miaka 16. Takriban wafungwa 72 wamekuwa kifungoni kwa zaidi ya miaka 20. Ripoti hiyo ya Addameer, inasema kuwa katika muda wa miezi mitatu hakuna hata siku moja iliyopita bila ya mfungwa mmoja wa Kipalestina kugoma kula. Wa f u n g w a w a w i l i wasiohukumiwa, Samer Al Barq na Hassan Safadi, walitangaza mgomo wa kula wakati watawala wa Israel walipokataa kutimiza ahadi yao ya kutorudia tena kifungo baada ya muda wao kumalizika. Mgomo huo uliendelea kupamba moto wakati Ayman Sharawna na Samer Issawi walipopinga amri ya kuwafunga tena bila ya mashtaka, baada ya kuachiliwa katika makubaliano ya kubadilishana wafungwa yaliyofikiwa tarehe 18 Oktoba 2011. Tarek Qaadan, Jafar Azzidine na Yousef Yassin, walikamatwa katika muda huu wa miezi mitatu. Nao walitangaza mgomo wa kutokula mara tu walipopewa amri ya kuwafunga bila ya mashtaka. Kituo cha Habari cha Palestina (Tanzania)

11

Makala

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 1 - 7, 2013

AN-NUUR

Nilivyomjua Sheikh Nassor Bachu


Na Abdulfatah Mussa Iddi, Tehran-Iran
yenyewe. Si tafsiri ya Qurani tu ya Sheikh Nassor iliyoupa moyo na roho yangu hali nyengine, lakini pia qiraa yake ya Qurani katika Sala za jamaa msikitini mle. Katika mazingira ya wakati ule (ambayo yangaliko mpaka leo hii katika baadhi ya misikiti yetu) ya kusomwa Qurani kwa hali ya kuitusi na kuidhalilisha na Maimamu wetu wa sala za jamaa, mtu alikuwa akistaladhi na kuhisi raha isiyo na kifani wakati Sheikh alipokuwa akiisoma Qurani ndani ya Sala. Ningali ninaihisi na kupitikiwa nayo masikioni mwangu sauti yenye mahadhi, yenye mvuto na taathira kubwa ndani ya roho ya qiraa yake, hasa ile ya sehemu za maqraa za mwishoni za Suratul Waaqiah na katikati ya Suratu Haamim Sajdah. Kuna mambo mawili yalikuja kujitokeza wakati ule, ambayo yalibadilisha aina ya mahusiano na maingiliano yangu na Sheikh Nassor. La kwanza ni kwamba siku zile darsa za Sheikh zilikuwa zimestawi hasa. Umma mkubwa wa watu, wazee kwa vijana, kike kiume, wakubwa kwa wadogo, wasomi na watu wa kawaida walikuwa wakihudhuria darsa hizo za Qurani, ambazo mbali na Kikwajuni zilifuatiwa pia na za msikiti wa Rahaleo pamoja na mihadhara katika msikiti wa Magomeni. Ila kulikuwepo na tatizo moja kubwa kuhusiana na uendeshaji wa darsa hizo (pengine kwa zama hizi lingeweza kwa kiasi fulani kutatuliwa japo kwa ujumbe mfupi wa simu ya mkononi) nalo ni kwamba, pale Sheikh alipokuwa akipata udhuru wa kushindwa kuka msikitini siku ya darsa, iwe ni kwa kuumwa au kutokana na udhuru mwengine, ilibidi darsa siku hiyo iakhirishwe. Wakati huo msikiti ulikuwa umefurika, tena basi baadhi ya watu wakiwa wametoka maeneo ya mbali wakija hapo kwa baiskeli au hata kwa miguu (daladala zilikuwa bado). Hali hiyo ilikuwa ikiwatia unyonge waumini waliokuwa wamefika msikitini kwa hamu na shauku kubwa, wakiwa na kiu isiyokwisha ya kutaka kupata

NAKUMBUKA ilikuwa mwaka 1985 wakati najiandaa kuingia Chuo cha Ufundi cha Karume, nilipojuana na Zahor Abdalla, ambaye nijuana naye sahibu yangu huyu na ushawishi wake ndio ulionifanya nitie mkono kizani na kuamua kwenda msikiti wa Kikwajuni kusikiliza darsa za Sheikh Nassor. Nasema hivi kwa sababu siku zile kwenda kwenye msikiti huo wa bida ilikuwa sawa na kutia mguu kanisani! Hali niliyoihisi baada ya kuhudhuria darsa chache tu za Tafsiri ya Qurani ya Sheikh Nassor, sitoisahau hadi mwisho wa uhai wangu. Ni sawa kwamba nilikuwa nimesoma Qurani chuoni kama walivyokuwa watoto na vijana wengi za Kizanzibari. Wakati huo nilikuwa tayari nimebahatika kupata tafsiri ya Kiswahili ya Qurani ya Sheikh Abdulla Saleh Farsy, lakini akili na moyo wangu ulikuwa haujawahi kuhisi adhama ya Qurani na kudiriki walau kwa uchache utukufu na utakatifu wa maneno ya Mwenyezi Mungu kama nilivyohisi katika darsa za Tafsiri ya Qurani iliyokuwa ikisomeshwa na Sheikh Nassor. Kama utaniuliza mimi, kwa uoni wangu Sheikh Nassor alikuwa zaidi ni AnsarulQurani kuliko kuwa AnsaruSunna kutokana na mapinduzi makubwa ya kiimani na kifikra aliyoyaleta kupitia darsa zake, yaliyotufanya vijana wa kawaida kama mimi kuelewa kwamba Qurani kweli ni Katiba na mwongozo wa kivitendo wa maisha ya kila siku ya Muislamu. Nilikuwa nikihisi kama muujiza pale Sheikh alipokuwa akifafanua aya fulani na kujengea hoja za yale yaliyomo ndani ya aya hiyo kwa kudondoa na kunukuu aya nyingine kadha wa kadha za Qurani, ambazo utadhani ziliteremshwa wakati mmoja na aya hiyo. Na alikuwa akilisisitiza jambo hili kwamba mfasiri bora wa Qurani ni Qurani

ALMARHUM Sheikh Nassor Bachu


chakula bora cha roho, yaani maneno ya Allah kutoka kwa mtu aliyetunukiwa na Mola kipaji cha kuwakishia watu wakayafahamu. Minongono iliyokuwa ikijitokeza hapo ni kwamba, kama Sheikh amepata udhuru ingekuwa aula kama angekuwepo mtu wa kutoa walau maa tayassar ili watu waliohudhuria darsa wasirudi majumbani kwao mikono mitupu. Lakini mbali na kuwepo tatizo hilo, itakumbukwa pia kuwa mnamo mwaka 1988 yalifanyika maandamano makubwa mjini Unguja ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, baada ya Sala ya Ijumaa, maandamano ambayo yalianzia msikiti wa Mchangani ya kulaani kauli ya kikafiri aliyotoa Sofia Kawawa, kwenye kikao cha semina ya chama tawala CCM dhidi ya sheria za ndoa na mirathi za dini yetu tukufu ya Uislamu. Maandamano yale yalikabiliwa na ukandamizaji mkubwa wa vyombo vya dola, ambavyo mbali na kusababisha vifo na kuwatia watu vilema, ulisababisha pia wanafunzi kadhaa wa karibu na muhimu wa Sheikh, akiwemo Sheikh Said Suleiman Masoud (Gwiji), U s t a d h K h a m i s Yu s u f , Ustadh Muhammed Suleiman na wengineo kukamatwa, kushtakiwa na kufungwa jela kidhulma kwa sababu ya kushiriki kwao katika maandamano kuonyesha hisia zao za kulaani kitendo kile cha Soa Kawawa. Hali hizo mbili za hitajio la kuwepo mtu au watu wa kushika darsa za Sheikh pale anapokuwa na udhuru, na kuondoka wanafunzi wake muhimu na wa karibu kulimfanya Sheikh aamue kuandaa mkupuo mwengine mpya wa wanafunzi wa kutoa darsa sambamba na kuwapa fursa wanafunzi hao ya kufanya mazoezi ya utoaji darsa na mihadhara msikitini hata katika siku anazokuwepo yeye mwenyewe. Ilikuwa wakati huo ndipo na mimi pia niliposhikwa mkono na kushajiishwa na wenzangu kadhaa tuliokuwa pamoja katika harakati za daawa, niwe miongoni mwa wanafunzi hao. Kwa kuashiria tu niwataje hapa Maustadh (wakati huo) Msellem bin Ali, Ahmad Majid, Muhammed Ahmada, Salum Abdulla, Ali Said na wengineo. Kinyume na nilivyokuwa nikijihisi mimi mwenyewe, wenzangu hao walinipa moyo sana na kuniambia kwamba ninao uwezo mzuri wa kuwa Khatibu. Huo ulikuwa ndio

mwanzo wa kujuana kwa karibu na Sheikh Nassor. Kwa muda mfupi sana nilizoeana na Sheikh. Alianzisha darsa za mazoezi ya uzungumzaji pale Skuli ya Ngambo (Rahaleo) siku za Jumapili asubuhi na tukawa pia na darsa za hifdhi na qhi pale msikiti wa Rahaleo baada ya Sala ya Alfajiri. Kwa kweli Sheikh Nassor alinichunuka sana. Nakumbuka katika mwaka ule ule wa kwanza niliingizwa kwenye orodha ya Maimamu wa Sala za Tarawehe na Witri katika mwezi wa Ramadhani pale msikiti wa Rahaleo. Katika kipindi kile ambapo vitabu vya kidini vya lugha ya Kiarabu vilikuwa adimu mno kupatikana Zanzibar, wakati Sheikh alipoletewa nuksha chache za kitabu cha Fiqhi Sunnah, nilibahatika kuwa miongoni mwa wanafunzi wachache aliowatunukia hidaya ile. Kipindi kile cha kati ya mwaka 1989 na 1990 kilikuwa kipindi cha harakati kubwa za daawa msikiti wa Rahaleo ambapo kwa mara ya kwanza, Sala ya Ijumaa ilianzishwa msikitini hapo na kama ilivyotarajiwa, Khatibu na Imamu wake wa kwanza akawa ni yeye Sheikh Nassor. Nakumbuka yalikuwa ni mazoea yangu kumpitia Sheikh dukani kwake pale Empire ili kumjulia hali, kumuuliza masuali na kupata ushauri wake kuhusu mambo mbalimbali. Siku moja aliniambia katika hali ya kawaida tu kwamba, Abdul, jamaa msikitini wanasema uanze kupanda mimbari pale kwa ajiili ya khutba ya Ijumaa. Na huo ukawa mwanzo wa kupata tauki ya kuwa mmoja wa wanafunzi wake wa mwanzo kusaidiana naye katika kutoa khutba katika Sala ya Ijumaa msikitini pale. Kwa wanaokumbuka, wakati ule Waislamu wa Dar es Salaam walikuwa na kiu kubwa ya kumwona na kumsikia Sheikh Nassor Bachu kwa karibu. Kwa bahati nzuri msikiti wa Qiblatain mjini Dar ulikuwa umeanzisha utaratibu wa kuwaalika Mashekhe kutoka sehemu mbalimbali, kwenda kutoa mihadhara msikitini

Inaendelea Uk. 13

12
TUSOMENI AN-NUUR
WITO leo IKHIWANI, nyote nakutoleeni, Mlo kule VISIWANI, na hapa BARA nyumbani, Lengo tutoke kizani, MIJINI na VIJIJINI, Tusomeni AN-NUUR, kwa HABARI zenye NURU. VYOMBO vingi vya NCHINI, hata vya UGHAIBUNI, VIMEJAA walakini, kwa HABARI ZA KUBUNI, Jambo hili kwa yakini, NATAMKA HADHARANI, Tusomeni AN-NUUR, kwa HABARI zenye NURU. KWA HABARI ZA KUBUNI, DHIDETU VI NAMBA WANI, Siongei kwa kubuni, mithali nitakupeni, SEPTEMBA kumbukeni, MBILI ZIRO ZIRO WANI, Tusomeni AN-NUUR, kwa HABARI zenye NURU. NDIVYO VILOKUITENI, MAGAIDI DUNIANI, VYOTE siyo vya NCHINI, wala vya UGHAIBUNI, Kwa pamoja VILIBUNI, PROPAGANDA ikawini, Tusomeni AN-NUUR, kwa HABARI zenye NURU. Yetu KWAVYO tambueni, i duni sana thamani, Kuenzi yetu thamani, cha kwetu tukithamini, Kulikoni na kwanini, chetu tusikithamini, Tusomeni AN-NUUR, kwa HABARI zenye NURU. ARUSHA nakuiteni, AN-NUUR mada mezani, WITO UZINGATIENI, na MANYARA wajuzeni, KILIMANJARO nendeni, na TANGA uenezeni, Tusomeni AN-NUUR, kwa HABARI zenye NURU. DAR nakujulisheni, AN- NUUR ni namba wani, WITO UZINGATIENI, na MORO wakumbusheni, Muwe pamoja safuni, KWA HABARI ZA YAKINI, Tusomeni AN-NUUR, kwa HABARI zenye NURU. GEITA shikamaneni, AN-NUUR sana someni, WITO UZINGATIENI, SIMIU wabarisheni, SHINYANGA ukisheni, KWA HABARI ZA YAKINI, Tusomeni AN-NUUR, kwa HABARI zenye NURU. IRINGA nakujuzeni, AN-NUUR likamateni, WITO UZINGATIENI, wa MBEYA msiukhini, RUVUMA lipitieni, KWA HABARI ZA YAKINI, Tusomeni AN-NUUR, kwa HABARI zenye NURU. KIGOMA ninaamini, AN-NUUR kwenu si geni, WITO UZINGATIENI, na RUKWA wanasihini, KATAVI lihuisheni, KWA HABARI ZA YAKINI, Tusomeni AN-NUUR, kwa HABARI zenye NURU. LINDI nanyi lisomeni, AN-NUUR kwa umakini, WITO UZINGATIENI, wa MTWARA waumini, Lisiwapite jamani, KWA HABARI ZA YAKINI, Tusomeni AN-NUUR, kwa HABARI zenye NURU. MWANZA wa kwetu jijini, AN-NUUR lienzini, WITO UZINGATIENI, KAGERA kwangu ukweni, MARA wahamasisheni, KWA HABARI ZA YAKINI, Tusomeni AN-NUUR, kwa HABARI zenye NURU. TABORA liperuzini, AN-NUUR kwa undani, WITO UZINGATIENI, SINGIDA lipitieni, Nanyi DOM lisomeni, KWA HABARI ZA YAKINI, Tusomeni AN-NUUR, kwa HABARI zenye NURU. UNGUJA litaliini, AN-NUUR nje-ndani, WITO UZINGATIENI, nanyi PEMBA ikhiwani, Kikoa jumuikeni, KWA HABARI ZA YAKINI, Tusomeni AN-NUUR, kwa HABARI zenye NURU. WITO UZINGATIENI, wa BARA na VISIWANI, AN-NUUR lisomeni, MIJINI na VIJIJINI, Khamsashara mwishoni, kalamu naweka chini, KWA HABARI ZA HAKIKA, TUSOMENI AN-NUUR. ABUU NYAMKOMOGI MWANZA.

Mashairi/Barua

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 1 - 7, 2013

AN-NUUR

Dhambi ya Nyerere yaanza kututafuna


NDUGU Mhariri, naomba wasaa katika gazeti letu tulipendalo la AN-NUUR nami nitoe mchango wangu kutokana na hali tete inayoikabili nchi yetu hivi sasa. Hayati Mwalimu Nyerere alijenga msingi mbovu sana wa nyumba hii iitwayo Tanzania. alikuwa na agenda ya siri ya kuwabana waislamu katika elimu na maendeleo yao kwa ujumla. Baadhi ya waislamu walimshitukia wakamkabili, lakini hakuwajali rejea ni nyingi litoshe tu sakata la East Afrika Muslim Welfere Society. Mwalimu nyerere aliamua kuwashughulikia waislamu na kuwazima. Hata hivyo kilio cha haki siku zote huwa kikali sana na hakizimwi mpaka haki imepatikana. Ndio unaona hata hivi sasa waislamu wamepaza sauti zao zaidi kulalamikia hujuma dhidi yao pale Necta, MoU, Oic uongozi N.K Sidhani kama Tume kuhusu matokeo ya kidato cha Nne 2013 itakuwa na la maana sana kiasi cha kubomoa hiyo ngome ya mfumo Kristo katika elimu. Kwa upande wa Zanzibar, hali ni hiyo kupunguzwa wazanzibar wote viongozi wanasiasa wasomi wafanya biashara na wananchi wa kawaida wamesha gundua kuwa Nyerere aliwazunguka, akawapora nchi yao hawana mamlaka wala sauti juu ya nchi yao. Kila jambo lao, kaburi lake liko CCM Dodoma. Hii ndiyo Sababu wanaona waachwe wapumue. Kutokana na hujuma nzito aliyoifanyia Zanzibar, kamwe nyerere hakuvumilia mtu yeyote ahoji muungano. Siri yake ingejulikana kwa wengi kama ilivyo hivi sasa. Aibu yeyote aliyejaribu kuhoji muungano, alikwenda na maji. Mzee jumbe, Maalimu Seif ni mifano mizuri nyerere hakutoa nafasi kwa mawazo mchanyiko yaendeshe nchi kila jambo aamue yeye na wengine wote wampongeze! Sifa anazopewa ni za bandia watu wawe wakweli. Mungu ndiye fundi Mkuu na Mjuzi, Zama zile zimepita na Nyerere hayupo tena. Waislamu wa Bara na Zanzibar pamoja na wananchi wote kwa ujumla bado tupo Madai yapo pale pale: Necta haki, Usawa na Heshima kwa Zanzibar watu wanataka nchi yao huru kupitia Muungano wa Mkataba. Dhambi kuu ya Nyerere inakuja hivi: Msimamo wake wa kutovumilia maoni, madai na maombi ya Waislamu, Wanzanzibar pamoja na wengineo wenye fikra tofauti na zake unaendelezwa na alichowaaachia dola (Mfumo Kristo) Mpaka sasa, hata kama wanaiona hatari iliyopo machoni pao! Wanaona wakiaddress kiukweli madai ya waislamu na wazanzibar watakuwa wamevunja mfumo wa Nyerere wa kudhibitiwa wananchi hawa wazalendo wa tangu dahari.

serikali iitishe mdahalo huru wa kitaifa, watu wote watoe ya mioyoni, taaluma, falsafa n.k ili tuende sawa kabla ya kuharibikiwa zaidi. Makaburu walikubali tume ya Upatanishi na maridhiano sisi tuliojifanya Bin Adam sana, tunasubiri nini?
Utajiri wetu unanyemelewa na mbweha. Tu k i b a d i l i k a h a r a k a tutanusurika. Wazalendo wa kweli amkeni sasa. Mohamed Mohamed - Dar es salaam

Waona bora washinikize kuletwa FBI ( MOSAD?) kwa mgongo wa Propaganda ya UGAIDI ili wazime madai ya Waislamu, wavuruge kuja dola huru ya Zanzibar na Ikiwezekana katiba Mpya isipatikane kabla 2015. Kina Sheikh Ponda, Azzan, Msellem Ali, Farid. Hawana kosa lolote hawa ni wazalendo wa kiwango cha juu sana kwa wakati huu wa dhulma, ukandamizaji na unaki. Prof. Safari na wachambuzi wote weledi wanatoa wito kwa

VIWANJA VILIVYOPIMWA KONGOWE KIBAHA TOWNSHIP REGISTERED PLAN No. 70995 BLOCK H
PLOT HATUA ENEO MRABA GHARAMA TSH

H1 H2 H3 H4 H5 H6 H7 H8 H9 H10 H11

50 x 29 32 x 32 50 x 30 37 x 30 50 X 45 33 x 37 60 x 45 50 x 40 67 x 50 70 x 45 90 x 50

1341 Sqm 1136 Sqm 1470 Sqm 1115 Sqm 2259 Sqm 1566 Sqm 2423 Sqm 1984 Sqm 3564 Sqm 2842 Sqm 3780 Sqm

4,023,000/= 3408000/= 4410000/= 3345000/= 6750000/= 4695000/= 7269000/= 5952000/= 10692000/= 8526000/= 11340000/=

Vipo Barabara ya Kongowe-Soga Kilomita moja toka barabara ya Morogoro. Simu No.0755 090 754/0715 090 754.

13

MAKALA

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 1 - 7, 2013

AN-NUUR

Nilivyomjua Sheikh Nassor Bachu


Inatoka Uk. 11

pale. Maalim Sheikh Ali Basaleh pamoja na wenzake kadhaa (baadhi yao wameshatangulia mbele ya haki) ndio walioanzisha sunna hiyo njema. Na kwa njia hiyo Sheikh Nassor akawa mmoja wa Mashekhe walioalikwa kwenda kutoa mhadhara Masjidul Qiblatain. Chambilecho Waswahili mchovya asali haonji mara moja, baada ya mwaliko wa kwanza uliotoa msisimko mkubwa kwa Waislamu wa Dar, Sheikh Bassaleh alikuja tena Zanzibar kumwalika Sheikh akatoe mihadhara kwenye misikiti mitatu ya Dar, ambayo ni ya Temeke kituo cha mwisho cha basi, Qiblatain na Idrisa. Kwa kuwa wakati ule Sheikh alikuwa ametingwa na darsa, mihadhara na khutba za Ijumaa alinipendekeza mimi nimwakilishe. Inavyoonekana sikumwangusha Sheikh wangu, kwani baada ya hapo Sheikh Ali Bassaleh alirudi tena Zanzibar kumpa mwaliko Sheikh kwa mnasaba wa kukaribia mwezi wa Ramadhani, ili kwenda kutoa mada Qiblatain kwa mnasaba huo. Sheikh akanipendekeza tena kwa mara ya pili. Na mara ya tatu Maalim Ali Basaleh (Allah amzidishie taufiki ya kuupigania Uislamu) alikuja kunifuata mimi moja kwa moja kwenda kutoa mhadhara msikiti wa Idrisa kwa mnasaba wa Maulidi ya Bwana Mtume SAW. Hiyo ilikuwa ni mwanzoni mwa mwaka 1990. Kwa hakika hisia ambazo nilipata ndani ya moyo wangu katika kipindi hicho kifupi nilichokuwa karibu na Sheikh Nassor, ni kwamba Sheikh alikuwa amejenga imani na matumaini kwangu na hilo likanipa moyo wa kujiamini na kuzidisha mapenzi yangu kwake. Kama mwanafunzi wa Sheikh Nassor, lilikuwa

WAISLAMU wakimswalia Marhuum Sheikh Nassor Bachu, Zanzibar. jambo la fahari kwangu kuweza kuiga fani na staili ya uzungumzaji wake katika darsa na mihadhara niliyokuwa nikitoa. Nakumbuka siku moja nilipokuwa nimetoa darsa jana yake msikiti wa Rahaleo, tulipoonana aliniambia; jamaa jana waliniuliza ulikuwepo Rahaleo? Nikawaambia hapana, nikahisi kwamba kunieleza hivyo ilikuwa ishara ya kupendezwa yeye na suala hilo. Nilivyomjua mimi Sheikh Nassor, alikuwa mtu wa kawaida kabisa katika tabia na mwenendo wake. Hakuwa akijikweza katu wala hakuwa na tabia ya kujitukuza. Nakumbuka siku moja tulipokuwa na darsa ya qhi msikiti wa Rahaleo kabla ya Sala ya Adhuhuri, wakati wa adhana ulipoingia aliinuka yeye mwenyewe kwenda k u a d h i n i . Wa k a t i w a Sala ulipowadia akakimu kisha akaniambia, Abdul ingia. Hili lilikuwa somo la kivitendo kwangu juu ya tawadhuu, kutojikweza na kujenga imani na moyo wa kujiamini kwa wanafunzi, ambalo nilijifunza kwa Sheikh Nassor. Katika kipindi chote cha karibu miaka 22 tangu nilipoondoka Zanzibar sikukata mawasiliano yangu na Sheikh. Wakati wa likizo zangu za kila mwaka nilikuwa nikimpitia kwenda kumjulia hali pale nyumbani kwake M i c h e n z a n i . Wa k a t i mwengine nilikuwa nikizungumza naye kwa simu kutoka huku Iran niliko. Mawasiliano yangu ya mwisho na yeye yalikuwa ya simu miezi michache kabla ya kupata stroke iliyopelekea kutuacha mkono na kurejea kwa Mola. Mnamo mwezi Juni mwaka jana, nilikwenda Dar es Salaam kwenye maziko na mazishi ya mjomba wangu na hiyo ikawa tauki kwangu pia ya kwenda Hospitali ya Muhimbili kumwona na kumwaga kwa mara ya mwisho Sheikh wangu. Sipendi kusimulia hapa lahadha ile ambayo itabakia daima kwenye kumbukumbu zangu. Mimi si mtaalamu wa uandishi wala sina mazoea ya kufanya hivyo. Kwa kawaida hupenda kubainisha hisia zangu kwa njia ya mazungumzo, lakini nimehisi niandike haya machache kumzungumzia al Marhum Sheikh Nassor Abdulla Bachu, Sheikh wangu na mwalimu wangu ili iwe ni tabaruku ya upande wangu ya kumkumbuka na kulienzi jina lake. Na hasa baada ya kukosa bahati adhimu ya kuhudhuria maziko yake kutokana na kuwa mbali na nyumbani. Niseme kwamba ilikuwa taufiki na fahari kubwa kwangu kupata kujuana

na kuwa karibu na Sheikh japokuwa kwa kipindi kifupi, lakini kilichokuwa na mengi. Na nimetaka niyaseme haya hivi sasa baada ya yeye kuondoka duniani nikiamini kwamba huu ndio wakati mwafaka wa kufanya hivyo. Kama alivyo mwana wa Adam yeyote, Sheikh Nassor, naye pia alikuwa na kasoro zake na udhaifu wake. Yeye hakuwa Mtume wala Malaika. Lakini hivi ndivyo unavyotufunza Uislamu, kwamba mwenzetu anapotangulia mbele ya haki tumkumbuke zaidi kwa mema yake. Kwa uoni wangu mdogo wa dini na ufahamu wa masuala ya daawa Zanzibar, katika zama zetu hizi za muongo wa 1980 kujia huku, ninahisi mchango aliotoa Sheikh Nassor kwa Uislamu Zanzibar ni wa nadra kuwahi kushuhudiwa mfano wake. Aliwasha cheche muhimu ya mapinduzi ya kikra na kiimani juu ya Uislamu na Qurani, hasa ndani ya tabaka la vijana, tena basi wake kwa waume. Allah amrehemu huko alikotangulia mbele ya haki, ampe malazi mema katika maisha ya mpito ya Barzakh na amfufue pamoja na Bwana Mtume SAW (ambaye alikuwa na mapenzi naye makubwa) na amsamehe makosa yake, na atupe mema sisi pia tunaofuatia baada yake, Amin.

Imamu apigwa mapanga Zanzibar


Na Mwandishi Wetu, Zbar

Inna lillahi wainna ilayhi rajiuun. Taarifa zilizopatikana mwishoni mwa wiki ni kwamba mtu mmoja anayeitwa Ali Khamis, ambaye ameelezwa kuwa ni Imamu wa Msikiti na Mkaazi wa Mwakaje,

amepigwa mapanga na watu wasiojulikana huko Kidoto mkoa wa Kaskazini Unguja. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ahmada Khamis, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo anasema limetokea majira ya saa 8:00 mchana huko Kitope, wakati Marehemu akiwa

shambani kwake. Kwa mujibu wa taarifa za polisi, inaelezwa kuwa Imamu huyo alipigwa mapanga shingoni na kupoteza damu nyingi, hali iliyosababisha kifo chake wakati akikimbizwa hospitali. Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

14

Dk. Emad Rabie Ahmad Mohamed SHUKURANI zote ni za Mwenyezi Mungu na Rehema na Amani zimkie yule aliyeletwa kuwa ni Rehema kwa viumbe wote, Bwana wetu Muhamad na Jamaa zake na sahaba zake wote. Ama baada ya utangulizi huu, kwa hakika huruma na mapenzi ni alama za Uislamu. Kwa hakika umekuja Uislamu ili kupandikiza kanuni za udugu na kusaidiana watu na ili waeneze huruma na mapenzi kwa viumbe vyote. Ametuonyesha Allah (sw) katika Surat Al Imrami, juu ya neema hii inayojulisha utukufu wa jambo hili la kueneza udugu na huruma, mapenzi na kusogeleana na kuwa karibu badala ya kukimbiana na kunyanya paana na kuchukiana. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, Na

shikamaneni katika kamba ya Mwenyezi Mungu nyote na wala msifarikiane, na zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu kwenu pale mlipokuwa maadui, na akaziunganisha nyoyo zenu na mkawa ndugu, Hadi mwisho wa aya hii amebainisha Mtume (S.A.W) mapenzi ya Muislamu kwa nduguye. Muislamu ni ukamilifu wa imani. Amesema Mtume (S.A.W), haamini mmoja wenu hadi apendelee kwa nduguye lile analolipenda yeye. Na amesema tena Mtume (S.A.W), ogopa yaliyokatazwa utakuwa mcha Mungu, na ridhia kwa alivyokupa Mwenyezi Mungu utakuwa tajiri katika watu. Na Mfanyie mema jirani yako utakuwa mwenye imani na pendelea kwa nduguyo lile unalolipenda wewe utakuwa muislamu. Hebu tusikie neno la mshairi akifafanua sifa za ndugu wa kweli pale aliposema. Hakika ya ndugu yako wa kweli ni yule anayekuwa nawe, na yule aliye kwa muda atakukimbia na hatakusanyika na yanayojulisha juu ya umuhimu wa mapenzi kati

Huruma na mapenzi ni alama za Uislamu


ya Waislamu na nduguye. Kwamba Mtume (S.A.W) amekataza ugomvi na chuki na kununiana Waislamu na kutokuzungumza zaidi ya siku tatu, akasema Mtume (S.A.W) Haifai kwa Muislam kumnunia Muislamu mwenzie zaidi ya siku tatu, na mbora wao ni yule anayemuanza mwenzie kwa salamu. Unahimiza sana Uislamu juu ya kueneza mapenzi na huruma kati ya Waislamu, kwamba Muislamu anapompenda Muislamu mwenzie basi amwambie kuwa ninakupenda kwa ajili ya Mungu. Alikuja mtu mmoja kwa Mtume (S.A.W), anasema ewe Mtume (Mimi ninampenda Fulani, Mtume akasemsa nenda ukamwambaie juu ya mapenzi na huruma hiyo iwe ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa sahihi ya maneno ya Mtume (S.A.W), amesema mambo matatu atakayekuwa nayo, basi amepata utamu wa imani. Awe anawapenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake kuliko vitu vingine na ampende mtu isipokuwa kwa ajili ya mwenyezi Mungu hadi mwisho wa hadithi hii

Makala

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 1 - 7, 2013

AN-NUUR

tukufu. Kama isipokuwa muumini na awachukue waharibifu na mafisadi na waovu na yote hayo ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Na katika hadithi yenye maana hii, yeyote Mwenye kupenda kwa

ajili ya Mwenyezi Mungu na akachukia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na akatoa mali kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na akazuia mali kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwa hakika amekamilika imani.

NAFASI ZA MASOMO YA UALIMU NGAZI YA CHETI 2013/2014


WAISLAMU MNATANGAZIWA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI CHUO CHA UALIMU KIRINJIKO ISLAMIC A. SIFA: Muombaji awe na sifa zifuatazo: (a) Ufaulu wa kidato cha 4 usiopungua alama 27 katika kikao kimoja cha mtihani, asiwe amekaa zaidi ya miaka mitano (5) tangu amalize kidato cha nne. (b) Awe na credits 4 kiwango cha C endapo amekaa mtihani kwa vikao zaidi ya kimoja. (c) Kuhitimu kidato cha 6 ni sifa ya nyongeza. B. MAELEKEZO MUHIMU KWA WAOMBAJI WOTE 1. Fomu ya maombi iambatanishwe na vyeti (leaving and Academic certicates) vya kidato cha 4 pamoja na picha ya hivi karibuni. 2. Fomu irudishwe siku ya kufanyiwa usaili tarehe 8/6/2013 saa 2:00 asubuhi. 3. Vituo vya usaili ni hivi vifuatavyo: (a) Kirinjiko Islamic T.C SAME (b) Ubungo Islamic T.C DSM (c) Nyasaka Islamic S.S. Mwanza 4. Majibu yatatolewa kwa watakaochaguliwa tu. 5. Fomu zinapatikana kwa gharama ya shilingi elfu kumi katika vituo vinavyoonekana ukurasa wa 15 katika tangazo la Shule.

15

TANGAZO

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 1 - 7, 2013

AN-NUUR

NAFASI ZA KIDATO CHA TANO 2013/2014


Waislamu kote nchini mnatangaziwa nafasi za kidato cha Tano kwa shule zifuatazo:

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE


1.

KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL NYASAKA ISLAMIC SECONDARY SCHOOL UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOO L

SAME KILIMANJARO MWANZA DAR ES SALAAM

Shule hizi ni za Kiislamu zenye lengo la kuwapa wanafunzi taaluma ya hali ya juu na malezi bora ya Kiislamu kwa gharama nafuu. Shule hizi ni za mchanganyiko wa wavulana na wasichana na zinapokea wanafunzi wa bweni tu. 2. Masomo yanayofundishwa ni Islamic knowledge, Combinations za SAYANSI, ARTS, BIASHARA pamoja na COMPYUTA. 3. Muombaji awe na Crediti 3 au zaidi na angalau D ya Elimu ya Dini ya Kiislamu katika matokeo ya kidato cha nne. Ikiwa ana F au hakufanya Elimu ya Dini ya Kiislamu, basi awe tayari kusoma programu maalum ya Maarifa ya Uislamu atakapokuwa kidato cha tano. 4. Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni tarehe 18 /05 /2013 5. Fomu za Maombi zinapatikana kwa gharama ya shilingi 10,000/= katika vituo vilivyoorodheshwa hapa chini. 6. Arusha Kilimanjaro Tanga Mwanza Musoma Kagera Shinyanga Osi ya Islamic Education Panel Jambo Plastic Ghorofa ya 2 mkabala na msikiti Mkuu Bondeni - 0763 282 371/ 0784 406 610 Moshi: Msikiti wa Riadha 0654 723 418 Same: Kirinjiko Islamic Secondry School: 0784 296424/0655 697 075 Uongofu Bookshop: - 0784 982525/ Mandia Shop - Lushoto: 0782257533 Nyasaka Islamic Secondary School 0717 417685/0786 417685 Osi ya Islamic Education Panel - Mwanza - Mtaa wa Ruji mkabala na Msikiti Al-Amin 0785 086 770 Duka la Kansolele -Stendi ya zamani sokoni - 0714587193 Bukoba: Alhuda Caf Kwa mzee Kinobe karibu na osi za TRA. - 0688 479 667 Msiikiti wa Majengo-0718866869 Kahama osi ya AN NUUR Karibu na msikiti wa Ibadhi: 0753 993930 Ubungo Islamic High School 0754 260 241/0712033556 Osi ya Islamic Ed. Panel Temeke -Msikiti wa Nurul Yakin 0655144474 Wasiliana na Ramadhani Chale :0715704380 Hijra Islamic Primary School : 0716 544757/0712 325086 Osis ya Islamic Ed. Panel karibu Nuru snack Hotel 0714285465 Babati: Shule ya Msingi Hangoni: 0784 667575 Msikiti wa mwanga Kigoma: 0753 355224 Kibondo Islamic Nursery School: 0784 442860 Kasulu: Murubona Isl.SS. 0714710802 Wapemba Store: 0784 974041/0786 959663 Amana Islamic S.S 0786 729 973 Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa NURU 0715 681701/0716791113 Mkuzo Islamic High School. 0716 791113 Duka la vifaa vya Kiislamu nje ya Msikiti wa Uyole 0713 200209 Rexona Video mkabala na Mbeya RETICO: 0713 200209 Sumbawanga: Masjid TAQWA 0717082 073 Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784 944566 Madrastun Najah: 0714 522 122 Wete: Wete Islamic Education Center: 0777 432331 Madrasatul Fallah: 0777125074Osi ya ust. Yusufu Ally jirani na msikiti mkuu 0653705627

Dar es Salaam Morogoro Dodoma Singida Manyara Kigoma Lindi Mtwara Songea Mbeya Rukwa Tabora Iringa Pemba Unguja Maa -

Pia Fomu zinapatikana kwenye Tovuti: www.ipctz.org. Ikumbukwe kuwa watakaopata fomu kupitia tovuti (download) watatakiwa kuzilipia wakati wa kuzirejesha. USIKOSE NAFASI HII ADHIMU WAHI KUCHUKUA FOMU SASA! Wabillah Tawiq MKURUGENZI

16

AN-NUUR
16
mashta mawili tu, kuwa ni uchochezi na kuhalalisha kuuaa Makari akiwa katika Msikiti wa Thaqib, Jijini Mwanza. Sheikh Katura, alisema kwamba baada ya kusomewa mashtaka, mwendesha mashtaka aliiomba Mahakama kutompatia Imam huyo dhamana kwa madai ya usalama wake. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 3, mwaka 2013. Shkh. Katura, alisema kufuatia hali hiyo wapo katika mchakato wa kumpata wakili atakayesimamia kesi hiyo na masuala mazima ya kisheria juu ya mashtaka hayo. Taarifa zaidi zinasema, kwamba Imam Hamza, alichukuliwa Msikitini hapo, akielezwa kwamba anatakiwa kituo cha Polisi cha kati kwa mahojiano na Polisi. Baada ya waumini kuona Imam huyo harejei, iliundwa kamati chini ya Shkh. Jabiri Katura, aliye Imam Mkuu wa Msikiti wa Ijumaa, Mwanza, kwa lengo la kufatilia Polisi na kujua sababu za kukamatwa kwake.

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 1 - 7, 2013

Usikose nakala yako ya AN-NUUR kila Ijumaa

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA MACHI 1 - 7, 2013

AN-NUUR

Na Bakari Mwakangwale

Imam Hamza akamatwa Mwanza

Mahakama yaombwa kuwaachia huru viongozi wa Uamsho


Alghaithiyyah, Zanzibar

IMAMU wa Masjid Nuru Jijini Mwanza, Hamza Omari, amekamatwa na kufikishwa katika Mahakama Kuu Jijini humo, akikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la uchochezi. Akiongea na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu Jumatano wiki hii kutoka Mwanza, kiongozi wa Kamati Maalumu ya Wa is l am u il iy o t eu l i w a kufatilia tukio hilo, Sheikh J a b i r Yu s u p h K a t u r a , amesema Imam Hamza alikishwa katika Mahakama hiyo na kusomewa mashtaka matatu. Kwamba kabla ya kufikishwa Mahakamani, Imam Hamza alikuwa ameshikiliwa na jeshi la Polisi baada ya kukamatwa siku ya Jumanne wiki hii, akiwa Msikiti wa Ijumaa majira ya asubuhi. Alisema kiongozi huyo wa Waislamu Jijini hapo, alipelekwa Mhakamani siku ya Jumatano wiki hii, kisha kusomewa mashtaka matatu. Hata hivyo alikumbuka

Sheikh Jabir Yusuph Katura

Ni kwa kushindwa kukamilika ushahidi


Mheshimiwa mimi nahisi ni muda mrefu sasa wateja wangu wapo rumande na kesi kila siku upelelezi haujakamilika. Naiomba mahakama yako tukufu iangalie sheria na kanuni ili iweze kuifuta kesi hii, alisema Towk. Kesi hiyo inayowakabili viongozi hao wakiongozwa na Sheikh Farid Hadi Ahmed, ambao wanadaiwa kutenda kosa la uchochezi na kufanya fujo kinyume na kifungu cha 45 (1)(a) na (b) cha sheria namba 6 ya mwaka 2004, walifikishwa tena katika mahakama hiyo mapema wiki hii. Aw a l i u p a n d e w a mashataka uliomba mahakamani hapo muda zaidi wa kuendelea na upelelezi wa kesi hiyo.

MAHAKAMA ya Wilaya ya Mwanakwerekwe imeombwa kuifuta kesi inayowakabili viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI), kutokana na kuchukua muda mrefu bila ya ushahidi wake kukamilika. Wakili wa washitakiwa h a o , S a l u m To u f i k , alimuomba hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Ame Msaraka Pinja, kuwa kutokana na taratibu za kimahakama, hususan katika makosa ya jinai, kesi inapokuwa imekia kuanzia miezi mitatu na kuendelea bila ya upelelezi kukamilika inapaswa kufutwa.

Upande wa mashataka ukiongozwa na Khamis Jafar, umeiomba mahakama kuwapa muda zaidi wa upelelezi baada ya upande wa watetezi kuiomba mahakama hiyo kuifuta kesi hiyo kutokana kwa kuwa kimepita kipindi kirefu pasipo upelelezi kukamilika. Hata hivyo, hakimu wa mahakama hiyo aliiahirisha kesi hiyo hadi Machi 19 mwaka huu, itakapoitishwa kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa kurejeshwa rumande hadi tarehe hiyo. Ukiacha Sheikh Farid Hadi, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mselem Ali, Mussa Juma, Azza Khalid Hamdan, Suleiman Juma, Khamis Ali na Hassan Bakari. Mwendesha mashtaka

alidai mahakamani hapo kuwa washitakiwa hao wakiwa ni wahadhiri kutoka Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu, walitoa matamko ya uchochezi yanayoashiria uvunjifu wa amani na kusasabisha fujo, maafa mbalimbali na mtafaruku kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na uharibifu wa mali za watu na serikali. Wakati huo huo kesi nyingine inayowakabili viongozi wa Jumuiya hiyo, ilitajwa mbele ya hakimu mpya baada ya Hakimu Mohammed Ali Shein kujitoa kuisikiliza. Hakimu Shein alijitoa kusikiliza kesi hiyo ambapo washtakiwa wanatuhumiwa kufanya fujo Desemba 27 mwaka jana. Kesi hiyo inayowakabili Sheikh Farid Hadi na

wenzake sita, ilifunguliwa katika Mahakama ya Mwanakwerekwe mjini Zanzibar. Sasa kesi inasikilizwa na Hakimu wa Wilaya, Khamis Rashid, ambapo washitakiwa wanne wako nje kwa dhamana na watatu bado wako mahabusu kutokana na kesi nyingine inayowakabli. Washitakiwa watatu, yaani Masheikh Farid Hadi, Juma Suleiman na Mussa Juma walipelekwa mahakamani katika kesi hiyo wakitokea mahabusu, kufuatia kukabiliwa na kesi nyingine Mahakama Kuu ya Vuga, ambayo dhamana yao imefungwa. Kesi hiyo ya Mwanakwerekwe inatarajiwa kutajwa Machi 4 na 5 na ile ya Mahakama Kuu itaendelea katika Mahakama ya Vuga Zanzibar.

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

You might also like