You are on page 1of 3

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

Kitalu Na. 8, Mtaa wa Luthuli


S.L.P 2643, DAR ES SALAAM
Simu: +255 22 2135747/8; 2137125; 2135222
Faksi: +255 22 2111281
B/Pepe: chragg@chragg.go.tz
Tovuti: www.chragg.go.tz

Mei 31, 2016

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Tamko la THBUB kukemea wimbi la vitendo vya
mauaji vilivyoanza kushamiri nchini
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesikitishwa
kupokea taarifa za vitendo vya mauaji ya kikatili vinavyoendelea kutokea
katika maeneo mbalimbali nchini, hususani kanda ya Ziwa, Mkoa wa
Pwani, na Dar es Salaam.
Wimbi hili la matukio ya vitendo vya mauaji na ukatili uliojitokeza kwa
kufuatana mwezi Mei 2016 yanavunja haki ya kuishi ambayo ndio msingi
wa haki zote za binadamu kwa ujumla wake.
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inalaani vikali mauaji haya
yote na matendo yote ya kikatili dhidi ya mwanadamu yanapotokea popote
nchini.
Baadhi ya matukio hayo kwa mujibu wa taarifa zilizoifikia Tume yametokea
usiku wa Mei 11, 2016 katika kitongoji cha Nyigumba, Kijiji cha Sima
Wilayani Sengerema, Mwanza, ambako watu watano (5) wa familia moja
waliuwawa kwa kukatwa mapanga; Mei 18 watu watatu (3) pia waliuwawa
kwa kukatwa mapanga wakiwa katika nyumba ya ibada, Msikiti wa
Rahman, eneo la Ibanda relini, mtaa wa Utemini, Kata ya Mkolani,Wilaya
ya Nyamagana, Mwanza; Usiku wa Mei 25, mwanamume mmoja na
Page 1 of 3

mkewe waliuwawa kwa kukatwa mapanga kijijini Manzavi, Wilayani


Butiama, Mara.
Aidha, mnamo Mei 22, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Bulale, Kata ya
Buhongwa, Mwanza, Bwana Alphonce Musanyenzi aliuawa. Mauaji
mengine yametokea Mei 18, Mkoani Pwani, Askari Polisi, Sajenti Ally
Salum Kinyogoli alipouwawa kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika.
Mei 23, jijini Dar es Salaam, eneo la Kiwalani, watu wanne (4) waliuawa
kwa kuchomwa moto wakiwa wamelala ndani ya nyumba yao; Mei 26, Bi.
Anathe Msuya aliuawa kwa kuchinjwa akiwa nyumbani kwake Kigamboni,
jijini Dar es Salaam.
Matukio haya ya ukatili yanakiuka haki ya kuishi iliyoainishwa katika ibara
ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977,
Sheria za nchi, matamko na mikataba mbalimbali ya haki za binadamu ya
kikanda na kimataifa.
Kufuatia wimbi hili la mauaji linaloonekana kuendelea nchini, Tume
inalaani na kukemea vikali vitendo hivyo vya kikatili.
Mbali ya ukiukaji mkubwa wa haki ya msingi ya kuishi, mauaji haya na
matukio haya pia ni kinyume na mafundisho ya imani zetu mbalimbali,
hivyo yasifumbiwe macho na kuachwa yaendelee, kwani yanaweza kuleta
mazoea mabaya ya kuona suala la kuuwa ni jambo la kawaida na hivyo
kuhatarisha amani, maisha ya watu na jamii.
Hivyo, Tume inashauri yafuatayo:
1. Serikali kupitia Jeshi la Polisi ichukue hatua mahsusi kuhakikisha ulinzi
wa wananchi dhidi ya mauaji na vitendo hivi, kwani jukumu la kwanza la
kuhakikisha usalama wa wananchi ni jukumu la serikali. Jeshi la Polisi
Page 2 of 3

lihakikishe

watu

wote

waliohusika

kutekeleza

mauaji

haya

wanakamatwa ili sheria ichukue mkondo wake.


2. Tume inawataka pia wananchi wahakikishe wanashirikiana na vyombo
vya dola kufichua maovu na kubaini uvunjifu wowote wa sheria na haki
za binadamu ndani ya jamii, na kutoa taarifa kwa mamlaka husika
kuzuia matukio kama haya kujirudia, au kusaidia upelelezi wa mauaji
haya na matendo mengineyo ya uvunjifu wa sheria.
3. Jamii ijenge utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu.
4. Mamlaka za Serikali za mitaa katika ngazi zote ziwe na mipango
madhubuti ya kuhakikisha ulinzi na usalama katika maeneo yao.
5. Tume inatoa rambirambi kwa ndugu, jamaa na wanafamilia waliopoteza
wapendwa wao katika matukio haya na pole kwa majeruhi.
Jukumu la ulinzi na utetezi wa haki za binadamu ni letu sote!
Imetolewa na:
(SIGNED)
Mhe. Bahame Tom Nyanduga
Mwenyekiti
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
Mei 31, 2016

Page 3 of 3

You might also like