You are on page 1of 37

Jarida la

NCHI YETU
Toleo la 228

Toleo Na. 001

TANZANIA

Toleo Maalum la Mtandaoni, Machi - April, 2016

Toleo Maalum la Mtandaoni

Machi - Aprili, 2016

Aprili 2016

Kaulimbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano ya


Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
HAPA KAZI TU

Government Standing Order Press and Public Relations

GOVERNMENT STANDING
ORDER NO. C. 16
PRESS AND PUBLIC RELATIONS
(a)

The Director of Information Services is the recognized channel for all Government
Information to the Press and Broadcasting Services.

(b)


To enable Regional Administrations, Ministries and Departments to keep the Director of


Information informed, as a matter of routine, of their activities, all Administrative
Secretaries in the regional Administrations, all Permanent Secretaries and Heads of
Departments should appoint an officer at headquarters and/or at such other
offices as may be appropriate to act as liaison officer with the Information Services Division.

Information of a factual nature not connected with major questions of policy and
development, to be given publicity in the local press and the broadcast news service
should be channelled through this officer to the Press Section of the Information
Services Division. Conversely it is to this officer that the officers of the Information
Services Division would first go for any information that they might require.

(c)


Where the information to be given out related to a matter of major importance, the
channel of communication will normally be between the Permanent Secretary Services
concerned and either the Permanent Secretary of the Ministry responsible for
Information and Broadcasting or the Director of Information Services.

(d)

In up-country stations, all material which it is desired to be communicated to the


Press and Broadcasting Services should be submitted to the Regional Information
Officer to pass such a material to the Director of Information Services.

(e)

When an officer is approached by the Press for an eye witness account of any incident,
he will always refer the Press to the Senior Officer present.
This officer will continue himself strictly to a statement of facts and will in no
cirmcustances embark on a discussion of Government policy. Any officer making such
a statement to the press will inform his head of Division immediately of the substance
of his statement and it will be responsibility of the head of Division to pass this
information to the Permanent Secretary of his Ministry and the Director of any
incident likely to by the quickest possible means. This procedure is also to be adopted
for any incident likely to arouse wide public interest or controversy, irrespective of
whether or not Press representatives are present, and/or a statement has been
sought or made.

2016

Nchi Yetu; Tuonavyo Sisi / Yaliyomo

NCHI YETU
TUONAVYO SISI

Heko Rais Magufuli kwa kufichua


Watumishi hewa.
NI miaka 52 ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar ulioizaa Tanzania. Katika kipindi hiki
tumeshuhudia mengi mazuri na chnagamoto
kadha wa kadha. Mafanikio ya Muungano huu
ni pamoja na Amani na Mshikamano baina ya
Watanzania. Kwa kipindi chote hiki tumeishi
kwa kupendana na kuheshimiana kindungu. Licha ya mafanikio haya
miaka 52 inatukuta bado na changamoto kadha ikiwemo rushwa,
madawa ya kulevya na Watumishi hewa. Serikali ya Awamu ya Tano
chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli limetangaziwa vita kali.
Suala la mishahara inayolipwa kwa Watumishi hewa limekuwepo kwa miaka
mingi hapa nchini. Hata hivyo, pamoja na kwamba wizi huu wa fedha za
Serikali ulikuwa unafahamika katika Wizara na Taasisi zake, swali likuwa
ni nani wa kumfunga paka kengele? Tunamshukuru Rais wetu Dkt.
John Pombe Magufuli kwa kulivalia njuga suala hili na sasa limechukua
sura mpya ambapo wahusika wameanza kuchukuliwa hatua za kisheria.
Vita hii imekolezwa na Mheshimiwa Rais ambaye ameonyesha dhahiri
kukerwa na suala la Watumishi hewa na sasa ameamua kufuatilia
kwa karibu zaidi baada ya kuwaagiza Wakuu wa Mikoa kuhakikisha
kwamba hakuna mtumishi hewa katika malipo ya mishahara ya
Watumishi wake. Aliwataka Wakuu hao wa Mikoa kufuata nyayo zake
katika vita hivyo. Katika kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais, hadi sasa
wamegundulika Watumishi hewa 2,700 katika Halmashauri 180 hapa nchini.
Matokeo ya mapambano dhidi ya Watumishi hewa yamedhihirika pale ambapo
Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga wameachishwa
kazi mara moja kutokana na kutokuwa wakweli juu ya kuwepo kwa Watumishi
hewa katika mkoa huo. Tukio hili hakika linaonyesha jinsi Mheshimiwa
Rais alivyodhamiria kupigana hadi kutokomeza suala la Watumishi hewa.

YALIYOMO
Government Standing Order

Kutokana na ushindi wa vita hii Watanzania lazima tuseme heko Rais


Magufuli. Kwa kweli amemfunga paka kengele na hivyo hatunabudi kuungana
naye kwa kuwafichua watumishi hewa. Na kwa waliokuwa wakihusika
na upotevu huu wa fedha sheria haina budi kuchukua mkondo wake.
Heko Rais Magufuli, Hapa Kazi Tu!, unaidhihirisha kwa vitendo. Vita
hii iwe chachu ya mapambano mengine dhidi ya Rushwa na Madawa
ya Kulevya. Tudumishe Muungano kwa kupambana na Watumishi hewa.
Tanzania bila Watumishi hewa inawezekana, tutimize wajibu wetu.

ii

Uk. (i)

Tuonavyo Sisi Uk. (ii)


Uhuru wa Vyombo vya Habari

Uk. 1

Kuapishwa Rais wa Zanzibar

Uk. 4

Mwenge wa Uhuru

Uk. 5

Miaka 50 ya Uhusiano Tanzania na Vietnam Uk. 7


Mikakati ya Serikali katika kilimo

Uk.10

Usafi siku ya Uhuru

Uk.12

Serikali kutoa Hati ya Umiliki Ardhi

Uk. 15

Elimu ya Msingi/Sekondari kutolewa bure

Uk. 16

Wachimbaji Wadogo wa Madini

Uk. 17

Habari picha Uzinduzi wa Daraja la Nyerere Uk. 18


Habari picha Muungano

Uk. 20

Umeme wa REA maeneo ya Vijijini

Uk. 22

Juhudi za Serikali kuboresha Afya nchini

Uk. 24

Maadili na Misingi ya Uwajibikaji

Uk. 26

Umeme wa Jotoardhi

Uk. 27

Mchango wa barabara katika pato la Taifa

Uk. 29

JARIDA HILI HUTOLEWA NA

Hata hivyo, wapo wajanja wachache wenye tamaa na uroho wa fedha


ambao wamekuwa wakitumia majina hayo kufanya malipo ya fedha
za mishahara au kuchukulia mikopo na fedha na kuingiza mifukoni
mwao. Utafiti uliofanyika katika mikoa miwili ya Dodoma na Singida kwa
maelekezo ya Mheshimiwa Rais, unaonyesha kuwa, katika Halmashauri
14 yaligundulika majina ya Watumishi hewa 202. Kati yao sita walikuwa
wameacha kazi, 27 ama wamekufa au wamefungwa, 8 wamefukuzwa
kazi, 158 ni Wastaafu na watatu wako likizo isiyokuwa na malipo.
Mheshimiwa Rais alitolea mfano kwa kusema, tuchukulie hawa watumishi
hewa 2,700 kila mmoja analipwa mshahara wa wastani wa milioni moja kwa
mwezi, ina maana kwa mwezi huo Serikali inapoteza karibu bilioni mbili.
Kwa bilioni mbili ni madawati mangapi yangeweza kununuliwa? Kwa mwaka
mishahara hewa inafikia takribani bilioni 24. Je, vitanda kwenye hospitali
zetu si vingeongezwa na kupunguza adha ya wagonjwa kulala chini?.

2016

Idara ya Habari (MAELEZO)


S.L.P 8031
Dar es Salaam
Faksi: 2122771/3
Barua pepe: maelezo@habari.go.tz
Tovuti: www.habari.go.tz

TUNATOA HUDUMA ZIFUATAZO







Tunasajili Magazeti na Majarida,


Tunauza picha za viongozi wa Kitaifa,
Tunatoa nafasi ya kufanya mikutano,
Tunatoa nafasi ya watu kuzungumza
na wanahabari,
Tunatoa vitambulisho vya Waandishi
wa habari (Press Cards),
Rejea ya magazeti na picha za zamani.

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

2016

Uhuru wa vyombo vya habari nchini


Na Eleuteri Mangi.

anadamu
wameumbwa
kwa
hulka na silika ya kuwa na
uwezo wa kuwasiliana miongoni
mwao, jamii wanamoishi, taifa na hata
ulimwenguni ili waweze kutimiza
nia na azma yao ya kuwasiliana.
Ili
mawasiliano
hayo
yakamilike
ni
lazima
yabebe
ujumbe
unaokusudiwa kufikishwa katika jamii.
Ujumbe huo ili uweze kumfikia mlengwa,
ni lazima iwepo njia ya kuufikisha ujumbe
huo kwa mlengwa ambao huwasilishwa
kwa maandishi (magazeti), sauti (redio)
na picha (TV) pamoja na mitandao
ya kijamii kupitia huduma ya inteneti.
Vyombo hivyo vya habari vinahusisha
wataalamu ambao kazi yao ni
kuhakikisha jamii inapata ujumbe kwa
wakati ili kuweza kujenga, kuboresha
na kuimarisha maisha yao kiuchumi,
kijamii,
kisiasa
na
kiutamaduni.
Vyombo vya habari hakika vimekuwa ndio
macho na masikio ya wananchi ili kufikisha
ujumbe unaohusu mambo mbalimbali
yanayofanyika ndani na nje ya nchi.
Tunapoelekea siku ya maadhimisho ya
uhuru wa vyombo vya habari duniani
ambayo huadhimishwa kila mwaka Mei
2 na 3, maadhimisho hayo mwaka huu
yataadhimishwa nchini Finland, ambapo
wanahabari wote duniani wataungana
kuwakumbuka
wenzao
waliofariki
dunia
walipokuwa
wakitekeleza
majukumu yao na kupanga mipango
mipya ya namna watakavyoboresha
kazi zao ziwe za ufanisi zaidi.
Tanzania ikiwa miongoni mwa mataifa
ya dunia hii, nayo haipo nyuma katika
suala la uwepo wa vyombo vya habari.
Ni dhahiri vyombo vya habari nchini
vimekuwa kiungo muhimu katika

Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa kazini kutekeleza majukumu yao.


kisaidia Serikali kutoa taarifa mbalimbali
na ajira hatua ambayo imesaidia
kupunguza tatizo la ajira nchini.
Ukilinganisha na nchi nyingine za
Afrika Mashariki, Tanzania inayoongoza
kwa kuwa na vyombo vingi vya habari,
hali ambayo ni msingi wa kuajiri
watu wengi zaidi katika tasnia hiyo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Nape Nnauye ambaye ndiye
mwenye dhamana ya habari nchini
anasema Serikali inaunga mkono juhudi
zinazofanywa na vyombo vya habari nchini.
Tulipofika ni pazuri ukilinganisha na
tulipotoka, mengi yamefanyika hasa
ukiangalia idadi ya vyombo vya habari
nchini na uhuru wa waandishi wa habari
wanavyoanadika na wanavyofikisha
ujumbe kwa wasomaji, wasikilizaji
na watazamaji alisema Waziri Nape.
Aidha, Waziri Nape amesema kuwa
bado Serikali inakusudia kuboresha
mazingira ya waandishi wa habari
ili waweze kufanya kazi zao kwa
hali ya uhuru hasa wanapotimiza
majukumu yao ya kiundishi wa habari.
Kwa mujibu wa takwimu za Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

ambacho ni chombo kilichoanzishwa


kisheria
kusimamia
sekta
za
mawasiliano na utangazaji nchini hadi
sasa kuna jumla ya vituo kadhaa vya
radio na televisheni vilivyosajiliwa.
Idadi ya vituo vya redio vilivyosajiliwa
nchini hadi sasa ni 123 ambavyo ni sawa
na asilimia 43.4 katika ukanda wa Afrika
Mashariki huku miongoni mwa vituo
hivyo vinamilikiwa na makampuni binafsi,
taasisi na mashirirka ya dini, jamii na
Serikali ambayo inayomiliki kituo kimoja
cha TBC Taifa inayoendeshwa chini ya
Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC), nchini
Kenya vipo vituo vya redio 118 sawa na
asilimia 41.7, Uganda 37 sawa na asilimia
13.1, Rwanda vituo vitatu sawa na asilimia
1.1 wakati Burundi ina vituo vya redio
viwili ambavyo ni sawa na asilimia 0.7.
Kwa upande wa vituo vya televisheni,
Uganda inaongoza kwa kuwa na vituo
vingi ambavyo idadi yake ni 44 sawa na
asilimia 53.6, ikifuatiwa na Tanzania yenye
vituo 24 sawa na asilimia 29.3, Kenya
vituo 10 sawa na asilimia 12.2, Rwanda
vituo vitatu ambavyo ni sawa na asilimia
3.7 na Burundi ikiwa na kituo kimoja cha
televisheni ambacho ni sawa na asilimia 1.2
Kwa kuzingatia maslahi ya wananchi
na wamiliki wa vyombo vya habari na

Inaendelea Uk. 2

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

2016

Inatoka Uk.1
wanahabari wenyewe, TCRA imekuwa
ikihimiza juu ya ufanisi wa ushindani na
uchumi, kulinda maslahi ya walaji, kulinda
uwezo wa fedha na ufanisi wa wagavi.
Pia inahimiza upatikanaji wa huduma
zinazosimamiwa kisheria kwa walaji
wakiwemo wenye kipato cha chini na
walaji wa vijijini na wa pembezoni,
kukuza mwamko, maarifa na uelewa
wa jamii kuhusu sekta zinazosimamiwa
ikiwemo kuzingatia haja ya kulinda na
kuhifadhi mazingira, haki na wajibu
wa walaji na wagavi wanaosimamiwa.
Katika kuonesha Tanzania inavyosimamia
uhuru wa vyombo vya habari, TCRA ina
jukumu lingine la kusimamia malalamiko
na migogoro inayoweza kujitokeza
miongoni mwa wateja wake wakiwemo
wamiliki wa vyombo vya habari, wananchi
na kupatia ufumbuzi changamoto hizo.
Aidha, hadi Aprili 22, 2016, Tanzania
imekuwa ndio nchi inayoongoza Afrika
Mashariki kwa kuwa na idadi kubwa ya
magazeti yaliyosajiliwa ambapo idadi yake
ni 881 licha ya magazeti na majarida mengi
kusajiliwa, mengi huchapishwa mara
chache na mengine kutokuchapishwa
na kusambazwa baada ya kusajiliwa.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo


mwaka huu inawahimiza wanahabari na
watu wote kutambua Kupata Habari ni
Uhuru wa Kimsingi: Hii ni haki yako!
ikilinganishwa na kauli mbiu ya mwaka
uliyopita ambayo ilisema Achia uwandishi
habari ustawi! Kuelekea upashaji habari
bora, usawa wa jinsia na usalama wa
vyombo vya habari katika enzi ya dijitali.

La Rue anasema Uhuru wa vyombo


vya habari ni muhimu kwa taarifa
muhimu na uwazi ni ambao ni mahitaji
ya jamii ya kidemokrasia. Lakini leo
tunaona ongezeko la ghasia na vitisho
dhidi ya waandishi ambayo mimi
napendekeza nchi zote duniani kuanzisha
utaratibu wa habari na ulinzi kwa ajili
ya usalama wa waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya


habari iliyotolewa na Shirika la Kimataifa la
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
Aprili 8, 2016 imebainisha kuwa katika
maadhimisho ya Siku ya vyombo vya
habari duniani mwaka huu, mwandishi
wa habari za uchunguzi kutoka Azerbaijan
Khadija
Ismayilova
amechaguliwa
kupokea tuzo ya uandishi wa habari
za uchunguzi ijulikanayo Guillermo
Cano inayotolewa na Shirika hilo.

Moja ya changamoto za kuweka


utaratibu wa usalama wa waandishi
wa habari ni idadi ndogo ya mifano
ya taratibu zilizopo ambayo inaweza
kuwa somo ili wengine waweze
kujifunza kutokana na taratibu zilizopo.
Masuala muhimu ya kuzingatiwa
wakati wa kuanzisha utaratibu huo
ni pamoja na kuwepo kwa makundi
matatu ambayo ni wigo wa utaratibu,
ushirikishwaji wa wadau muhimu
pamoja na taasisi kubuni na kutathmini
hatua ambayo itasaidia kufikia malengo
ya kumlinda mwandishi wa habari.

Tuzo hiyo ina thamani ya Dola za


Kimarekani 25,000, na imepoewa jina
hilo kwa heshima ya Guillermo Cano
Isaza, mwandishi wa habari wa Colombia
aliyefariki Desemba 17, 1986 akiwa kazini.

Akizungumzia
maandalizi
ya
maadhimisho kitaifa ya siku ya Uhuru

Kwa idadi ya magazeti nchi za Uganda,


Rwanda na Burundi yapo magazeti
matano yanayotumika katika nchi
hizo wakati Kenya ina magazeti saba
ambayo husomwa na kufikisha ujumbe
kwa walengwa katika mataifa hayo.
Wingi huo wa vyombo vya habari nchini
imekuwa ishara njema ya kujali uhuru wa
kuanzishwa kwa vyombo vya habari kwa
makampuni binafsi, taasisi na mashirika ya
dini pamoja na jamii mbalimbali ili kuweza
kuwa ndio namna yao ya kupata taarifa.
Katika ulimwengu wa leo, uhuru wa
habari ni suala la msingi na lina umuhimu
mkubwa katika kutekeleza haki za
binadamu katika kutafuta, kupata, kupokea
na kutoa habari ambazo ni muhimu kwa
nchi katika kujiletea maendeleo endelevu.

Moja ya mitambo (satellite dish) ya kurushia matangazo ya


Televisheni na redio.
Jukumu la kuenzi na kutoa tuzo ya
heshima kwa waandishi wa habari
duniani linafadhiliwa na taasisi ya
Cano
Foundation
kutoka
nchini
Colombia na Helsingin Sanomat
Foundation kutoka nchini Finland.

wa Vyombo vya habari nchini ambayo


yanafanikia jijini Mwanza Mei 2 na 3,
mwaka huu, Mwenyekiti wa Kamati ya
Maandalizi ya maadhimisho hayo Andrew
Marawiti amesema kuwa yanaendelea
vizuri kulingana na ratiba ilivyopangwa.

Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu wa


Mawasiliano na Habari UNESCO Frank

Katika maadhimisho hayo, Marawiti


amesema kuwa Mgeni Rasmi anatarajiwa

Inaendelea Uk. 3

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

2016

Inatoka Uk. 2
kuwa Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Othman Chande ambapo
wakati wa ufunguzi wa maadhimisho
hayo mada mbalimbali zitawasilishwa
na watoaKuhusu ratiba ya siku mbili za
maadhimisho hayo, Marawiti amesema
kuwa
zitawasilishwa
zikiandamana
na majadiliano kwa washiriki wote.
Miongoni mwa washiriki wanaotarajiwa
kuwepo katika maadhimisho hayo
ni wadau mbalimbali wa habari
wakiwemo
viongozi
wa
Serikali,
Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao
hapa nchini, wawakilishi wa Mashirika
ya Kimataifa, wamiliki wa vyombo vya
habari, waandishi wa habari na wananchi.
Kulingana na takwimu zilizopo, mwandishi
wa habari mkongwe nchini, Mzee Willie
Mbunga amesema kuwa Tanzania ina
vyombo vingi vya habari ikilinganishwa
na hali ilivyokuwa miaka ya nyuma
ambapo kulikuwa vyombo vichache vya
habari ambavyo ni redio Tanzania Dar
es salaam, Tanganyika Standard, Mambo
Leo, Uhuru, Mzalendo na Ngurumo.
Aidha, amesema kuwa changamoto ya
baadhi ya watu kujisahau na kuweka
pembeni maadili ya uandishi wa habari
ni suala ambalo si la kufumbiwa macho,
ni vema litiliwe maanani ili kukiokoa
kizazi cha sasa na kijacho katika
kujenga jamii inayojali na kusimamia
maadili ya taaluma na ya jamii.
Katika
upashanaji
habari,
dunia
sasa imekuwa sawa na kijiji hasa
katika kipindi hiki cha sayansi na
teknolojia
ambapo
mawasiliano
ndio imekuwa nguzo ya kila kitu.

Moja ya studio ya kurusha matangazo ya televisheni


Miongoni mwa mitandao hiyo ya kijamii
ni pamoja na blog ya Serikali, Michuzi,
fullshangwe, bayana, milardayo, mwamba
wa habari, businessmagnetblogs, mpekuzi,
moh Dewji na mitandao mingine.
Mwandishi wa habari Majid Mjengwa
ambaye pia ni mwanzilishi na
mmiliki wa blog ya mjengwa anasema
Mitandao ya kijamii imekuwa ni eneo
la upashanaji habari linalofanya kazi
kama vyombo vingine vya habari.
Ili kufikisha ujumbe kwa jamii, Mjengwa
amesema kuwa watu wote wanaofanya kazi
katika mitandao ya kijamii wanapaswa
kufuata maadili ya taaluma ya habari
pamoja na sheria na taratibu za nchi
husika ili kuondoa mgongano wa maslahi
katika kufikisha ujumbe kwa jamii.

Ni dhahiri haki na wajibu ni vitu


ambavyo haviachani, hivyo ni jukumu la
kila mdau wa habari nchini wakiwemo
Serikali,
waandishi
wa
habari,
wamiliki wa vyombo vya habari na
wananchi kuzingatia sheria, kanuni,
taratibu pamoja na maadili ya jamii.
Hatua hiyo itasaidia kuimarisha na
kuhakikisha wadau hao wanakuwa sehemu
ya kujenga uhuru wa vyombo vya habari
ambavyo vitakuwa chachu ya kujenga taifa
imara lenye uchumi bora kwa manufaa
ya Watanzania ifikapo mwaka 2025.

Awali makala haya yameonesha kuwa


ujumbe katika jamiiulifikishwa kwa
njia ya redio, magazeti na TV, zaidi ya
vyombo hivyo, mitandao ya kijamii
kwa sasa imekuwa nguzo mahiri
na vyanzo vikuu vya habari kwa
waandishi wa habari na wananchi.

Moja ya studio ya kurusha matangazo ya redio.

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

2016

Dkt. Shein aapishwa kuwa Rais wa


Awamu ya Saba wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar.
Na Mwandishi wetu.

ivi karibuni Rais wa Serikali ya


Zanzibar, Mhe. Dkt. Ali Mohamed
Shein aliaapishwa na Jaji Mkuu wa
Zanzibar, Mhe. Jaji, Omary Othman
Makungu kuwa Rais wa Serikali hiyo
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Hatua hiyo ilitokana na ushindi alioupata
kwenye Uchaguzi Mkuu wa marudio,
uliofanyika Machi 20, mwaka 2016 ambao
ulijumuisha vyama vyote vilivyoshiriki
kwenye uchaguzi huo
Oktoba 25,
mwaka 2015 ambapo matokeo yake
yalifutwa na Tume ya Uchaguzi ya
Zanzibar (ZEC) kutokana na ukiukwaji
wa Sheria na taratibu za uchaguzi.
Sherehe hizo za kuapishwa kwa Rais
huyo, zilifanyika Machi, 24, mwaka
2016 katika uwanja wa Amani mjini
Unguja, na kuhudhuriwa na viongozi
mbalimbali, akiwemo Rais
wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Viongozi
wengine
wa
kitaifa
waliohudhuria sherehe hizo ni pamoja
na Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa
na viongozi mbalimbali wastaafu.
Baada ya zoezi hilo la kuapishwa Rais
Shein, viongozi wa dini waliomba dua
wakiongozwa na Kadhi Mkuu wa Zanzibar
Sheikh Khamis Haji Khamis na kufuatiwa
na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki
Jimbo la Zanzibar Mhashamu Augustino
Shayo na Askofu wa Anglikana Dayosisi
ya Zanzibar Padre Michael Henry Hafidh.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali


Mohamed Shein (kushoto) akila kiapo mbele ya Jaji Mkuu, Mhe. Omar Othman
Makungu hivi karibuni mjini Zanzibar.
Akiwahutubia wananchi mara baada ya
kuapishwa, Rais Shein aliahidi kuunda
Serikali makini yenye viongozi wachapa
kazi ambao watatenda haki kwa wananchi
wa Zanzibar bila kujali dini, rangi wala
tofauti za kisiasa na kuwahakikishia
wananchi kuwa ataimarisha ulinzi
wananchi na hatakubali mtu au
kikundi cha watu kuleta vurugu na
kuhatarisha
amani
ya
Zanzibar.
Alisema kuwa uchaguzi umemalizika
kilichopo mbele yao ni kufanyakazi kwa
juhudi na maarifa kama ilivyo kauli ya Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt.Magufuli ya HAPA KAZI TU
ili kuleta maendeleo ya kweli Zanzibar.
Aprili 9, mwaka 2016 baada ya kuingia
Ikulu Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt.
Shein alitangaza Baraza la Mawaziri
lenye Wizara 13, Baraza lilikuwa na
sura mpya nane, zikijumuisha wajumbe
kutoka katika vyama vya siasa vya
upinzani, wanasiasa mashuhuri visiwani
humo, huku naibu mawaziri saba wote
wakiwa wageni katika nafasi hiyo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa


Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali
Mohamed Shein akisaini baada ya
kuapishwa.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa


Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali
Mohamed Shein akikagua gwaride mara
baada ya kuapishwa.

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

2016

Samia: Mwenge wa Uhuru unahitajika


zaidi sasa
Na Benjamin Sawe

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) akiwasha Mwenge wa
Uhuru mkoani Morogoro.
akamu wa Rais wa Jamhuri ya ya changamoto hizo kuwa ni kuanza kutenga maeneo rasmi kwa vijana kwa
Muungano wa Tanzania, Mhe. kujengeka hali ya kudharauliana katika ajili ya kuendesha shughuli za kiuchumi.
Samia Suluhu Hassan, alisema falsafa jamii, kuchukiana na kukatishana tamaa. Alisema wakati taratibu za kutafuta
ya Mwenge wa Uhuru inahitajika Samia alisema kuna haja ya kuzikabili maeneo rasmi zinafanywa, viongozi
zaidi kwa sasa kuliko wakati wowote, changamoto hizo kwa ujasiri wa hao watenge maeneo maalum kwa siku
ili
kukabiliana
na
changamoto hali ya juu kwa malengo yale yale ya za Jumapili na kuwataka vijana walipe
zinazojitokeza za kitaifa na kimataifa. kudumisha amani, upendo, umoja na ushuru, waimarishe usafi na waweke
mshikamano kupitia mbio za mwenge. ulinzi wakati wakiendesha shughuli zao.
Alisema tangu kuanzishwa kwa mbio
za Mwenge wa Uhuru mwaka 1964 Hilo ndilo tunalolifanya viongozi Samia alitumia fursa hiyo pia kuelezea
na kukimbizwa nchini kote, mwenge wenu wa Serikali kitaifa. Hatua zote azma ya Serikali ya kuendelea kupambana
huo umekuwa kichocheo kikubwa tunazozichukua za kutumbua majipu na rushwa na ufisadi kwa lengo la kudhibiti
katika kuhamasisha maendeleo, umoja, ni kurudisha heshima na matumaini mianya ya upotevu wa Mapato ya Serikali
mshikamano na kudumisha amani, kwa wale waliokata tamaa. Serikali na kuboresha uwajibikaji katika usimamizi
ambayo ni tunu pekee ndani ya taifa. inaendeleza falsafa hii, naomba nanyi wa rasilimali na utoaji wa huduma.
mtuunge mkono, alisema Samia.
Akihutubia taifa kwenye uzinduzi
Aliwaasa watumishi wa umma na wa sekta
wa mbio za Mwenge wa Uhuru Pamoja na kusisitiza vijana wapewe binafsi kujiepusha na rushwa na kutekeleza
katika Uwanja wa Jamhuri mkoani elimu na ujuzi wa stadi za kazi, pia alitoa majukumu yao kwa kuzingatia Katiba,
Morogoro, Mhe, Samia alitaja baadhi wito kwa wakuu wa mikoa na wilaya sheria, kanuni, miongozo na taratibu

Inaendelea Uk. 6

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

2016

Inatoka Uk. 5

akamu wa Rais wa Jamhuri ya


Muungano wa Tanzania, Mhe.
Samia Suluhu Hassan, alisema falsafa
ya Mwenge wa Uhuru inahitajika
zaidi kwa sasa kuliko wakati wowote,
ili
kukabiliana
na
changamoto
zinazojitokeza za kitaifa na kimataifa.
Alisema tangu kuanzishwa kwa mbio
za Mwenge wa Uhuru mwaka 1964
na kukimbizwa nchini kote, mwenge
huo umekuwa kichocheo kikubwa
katika kuhamasisha maendeleo, umoja,
mshikamano na kudumisha amani,
ambayo ni tunu pekee ndani ya taifa.
Akihutubia taifa kwenye uzinduzi
wa mbio za Mwenge wa Uhuru
katika Uwanja wa Jamhuri mkoani
Morogoro, Mhe, Samia alitaja baadhi
ya changamoto hizo kuwa ni kuanza
kujengeka hali ya kudharauliana katika
jamii, kuchukiana na kukatishana tamaa.
Samia alisema kuna haja ya kuzikabili
changamoto hizo kwa ujasiri wa
hali ya juu kwa malengo yale yale ya
kudumisha amani, upendo, umoja na
mshikamano kupitia mbio za mwenge.
Hilo ndilo tunalolifanya viongozi
wenu wa Serikali kitaifa. Hatua zote
tunazozichukua za kutumbua majipu
ni kurudisha heshima na matumaini
kwa wale waliokata tamaa. Serikali
inaendeleza falsafa hii, naomba nanyi
mtuunge mkono, alisema Samia.
Pamoja na kusisitiza vijana wapewe
elimu na ujuzi wa stadi za kazi, pia alitoa
wito kwa wakuu wa mikoa na wilaya
kutenga maeneo rasmi kwa vijana kwa
ajili ya kuendesha shughuli za kiuchumi.
Alisema wakati taratibu za kutafuta
maeneo rasmi zinafanywa, viongozi
hao watenge maeneo maalum kwa siku
za Jumapili na kuwataka vijana walipe
ushuru, waimarishe usafi na waweke
ulinzi wakati wakiendesha shughuli zao.
Samia alitumia fursa hiyo pia kuelezea
azma ya Serikali ya kuendelea kupambana
na rushwa na ufisadi kwa lengo la kudhibiti
mianya ya upotevu wa Mapato ya Serikali
na kuboresha uwajibikaji katika usimamizi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia


Suluhu Hassan (kushoto) akipokea Mwenge wa Uhuru toka kwa
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Bw. George Mbijima mkoani Morogoro.
wa rasilimali na utoaji wa huduma.
Aliwaasa watumishi wa umma na wa sekta
binafsi kujiepusha na rushwa na kutekeleza
majukumu yao kwa kuzingatia Katiba,
sheria, kanuni, miongozo na taratibu
zilizowekwa. Alisema mkono wa Serikali
hautamwacha mtu bila kujali hadhi yake.
Anasema Serikali inaendelea kupambana
na malaria, Ukimwi na matumizi
ya dawa za kulevya, hatua ambayo
itawafanya wananchi kuwa wenye afya
bora, nguvu na ari ya kufanya kazi, hivyo
kuongeza tija kwa taifa na kutokomeza
umasikini,
ujinga
na
maradhi.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Walemavu,
Mhe. Jenister Mhagama, alisema
mwenge huo utakimbizwa kwa siku
179 katika mikoa na wilaya zote nchini.
Anasema mbio hizo zimeendelea kueneza
ujumbe wa amani, umoja, mshikamano,
utu, moyo wa uzalendo na kujitolea
miongoni mwa Watanzania. Mambo hayo
yamekuwa tunu zinazoitambulisha nchi
ya Tanzania na watu wake, na ni mambo
yasiyokuwa na chama wala itikadi.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na viongozi
mbalimbali,
wakiwamo
mawaziri,
makatibu wakuu, wakuu wa mikoa na
wilaya kutoka Tanzania Bara na Visiwani.

Ni mara ya pili kwa Mwenge kuwashwa


mkoani humo. Kwa mara ya kwanza
uliwashwa mwaka 1985 eneo la
Wami Sokoine, kabla ya wilaya ya
Morogoro kugawanywa na kuzaliwa
wilaya ya Mvomero. Uliwashwa hapo
kumuenzi Waziri Mkuu hayati Edward
Sokoine aliyekufa kwa ajali ya gari
eneo hilo mwaka Aprili 12, 1984.
Uzinduzi mwingine wa Mwenge wa Uhuru
kitaifa ulifanyika mwaka 2006, uliwashwa
uwanja wa Jamhuri uliopo Manispaa
ya Morogoro. Mkoa huo pia ulipata
heshima nyingine ya kuzima Mwenge wa
Uhuru kitaifa mwaka 1994 katika eneo
la Mazimbu, Manispaa ya Morogoro.
Eneo hilo la Mazimbu, lilitumiwa na
Chama cha African National Congress
(ANC), na yalikuwa ni Makao Makuu
ya ANC katika kuendesha mapambano
dhidi ya makaburu wa Afrika Kusini.
Nae Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mhe.
Dkt. Steven Kebwe alisema Mwenge
wa Uhuru ni urithi aliotuachia Baba
wa Taifa na wananchi wanatambua
kuwa Tanzania imekuwa na utaratibu

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe.


Stephen Kebwe (kulia) akipokea Mwenge
wa Uhuru toka kwa Kiongozi wa Mbio
za Mwenge Bw. George Mbijima mkoani
Morogoro.

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

2016

Miaka Hamsini ya uhusiano kati ya


Tanzania na Vietnam

Na Benedict Liwenga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa


Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli (kushoto) akisalimiana na Rais
wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya
Vietnam, Mhe. Truong Tan
Sang Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Muungano wa Tanzania, Mhe.


Edward Lowassa (2006); na Mhe.
Mizengo Kayanza Pinda (2010).
Mafanikio ya Uchumi ya Vietnam
Vietnam
imefanikiwa
kupunguza
umasikini
wa
wananchi wake kwa asilimia 50.

anzania na Vietnam zimeanza


kuendeleza
ushirikiano
na mahusiano katika maeneo
mbalimbali
ya
kiuchumi
kwa zaidi ya miaka hamsini.
Mahusiano haya yamejengwa na
Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere pamoja na
aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati
Kuu ya Chama cha Kikomunisti
cha Vietnam Hon Chi Minh
mnamo mwaka 1960 na kupelekea
kuanzishwa rasmi kwa mahusiano
ya kidiplomasia mwaka 1965.

ziara za kudumisha mahusiano


ya pamoja ambapo tarehe 25
Septemba 1973, aliyekuwa Rais wa
Vietnam Mhe. Nguyen Huu Tho
alifanya ziara nchini Tanzania.

Kwa upande wa Tanzania, viongozi


waliofanya ziara nchini Vietnam
ni pamoja na Rais wa Awamu ya
Tatu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Benjamin
William Mkapa (2004); Rais wa
Awamu ya Nne wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe.
Jakaya Mrisho Kikwete (2014),
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
Aidha, katika kipindi cha miaka wa Baraza la Mapinduzi Mhe.
50 ya mahusiano ya kidiplomasia Dkt. Ali Mohamed Shein (2012);
baina ya nchi hizi mbili Viongozi Mawaziri Wakuu wa Serikali ya
wa kitaifa wa nchi hizo wamefanya Awamu ya Nne ya Jamhuri ya
7

Vietnam inaongoza ulimwenguni


kwa
kuuza
korosho na
pilipili
manga.
Vilevile,
Vietnam ni miongoni mwa
nchi
zinazoongoza
kwenye
kilimo cha muhogo na mpira.
Biashara kati ya Tanzania na
Vietnam kwa sasa ni zaidi
ya dola milioni 300 ambapo
ndani ya miaka mitano ijayo
inakadiliwa kufikia dola bilioni
moja ifikapo mwaka 2020.
Baadhi ya maeneo ambayo
Tanzania na Vietnam wameonyesha
ushirikiano ni pamoja na uwekezaji
katika kilimo cha mpunga, uvuvi
wa samaki wa ziwani na baharini
pamoja na uanzishwaji wa viwanda
vya kusindika mazao ya biashara.
Kutokana na uhusiano huu baina ya
nchi hizi mbili utasaidia kufungua
mahusiano ya mawasiliano katika
elimu, ambapo kutakua na fursa
Inaendelea Uk. 8

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

Inatoka Uk. 7

kwa wanafunzi wa Kitanzania


kwenda kusoma nchini Vietnam,
na wataalamu wa Vietnam kuja
kufanya kazi pamoja na watanzania.
Mkakati huo unaendana na
utekelezaji wa mpango wa
maendeleo wa nchi hiyo ambao kwa
sasa umelenga kufanya mageuzi
makubwa katika taasisi za kibenki
ili kuwezesha wananchi kupata
mitaji ya kufanya shughuli za
uchumi na maendeleo; na
mageuzi ya makampuni
ya
biashara
ya
Serikali ili yaweze
kushindana
katika uchumi
wa soko ndani
na
nje
ya
nchi
pasipo
kutegemea
ruzuku kutoka
Serikalini.
Katika ziara ya
siku nne nchini,
Rais wa Jamhuri
ya
Kisoshalisti
ya
Vietnam, Mhe. Truong
Tan Sang nchini, aliongozana
na mke wake, Bi. Mai Thi Hanh,
Mawaziri 4 wanaoshughulika
na sekta za Kilimo, Habari
na
Mawasiliano,
Uwekezaji,
Afya,Viwanda na Biashara pamoja
na ujumbe wa wafanyabiashara
30
kutoka
Vietnam.
Madhumuni ya ziara hiyo ilikuwa
ni kukuza uhusiano baina ya
Vietnam na Tanzania mbao
umedumu kwa zaidi ya miaka
hamsini tangu kuanzishwa kwake
8

pamoja kufungua maeneo mapya


ya Ushirikiano wa kiuchumi
baina ya Tanzania na Vietnam.
Hii ilikuwa ni ziara ya kwanza ya
kiongozi huyo Barani Afrika tangu
aingie madarakani mwaka 2011,
ambapo nchi nyingine ambayo
alitembelea
ni
Mozambique.
Katika ziara hiyo, Rais Sang alipata
fursa
ya
kufanya

2016

kuwa nchi hizo zimekuwa na


uhusiano imara wa muda mrefu.
Nakumbuka mwaka 2004 Rais
Mstaafu wa Awamu ya Tatu,
Mhe. Benjamini William Mkapa
alitembelea Vietnam, pia Rais
Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe.
Jakaya Mrisho Kikwete alitembelea
Vietnam mwaka 2014, hivyo
huu ni uhusiano mzuri, na hivyo
kuja kwako hapa ni uthibitisho
tosha namna gani tulivyo na
mahusiano mazuri baina yetu,
alisema
Rais
Magufuli.
Aliongeza
kuwa,
biashara kati ya
Tanzania
na
Vietnam ambayo
kwa
sasa
ni
dola
zipatazo
milioni 300 kwa
mwaka ni kidogo
kulingana
na
uwepo wa fursa
zilizopo
katika
nchi hizo mbili,
hivyo kuna haja ya
kuendeleza mahusiano
ya
kibiashara
ya
pande
zote
mbili.

mazungumzo
Ikulu Jijini Dar es Salaam na
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. John Pombe
Joseph Magufuli ambapo viongozi
hao walisaini mkataba wa
kibiashara baina ya pande mbili.
Rais Magufuli alieleza kuwa ugeni
wa Rais Sang nchini Tanzania
umekuwa wa maana kubwa
kwa Tanzania na kuongeza

Nina furaha kuwa, katika ziara hii


umefuatana na Wafanyabiashara
wakubwa hivyo, mwisho wa ziara
hii ni matumani yangu kuwa
wafanyabishara wetu wa Tanzania
watanufaika kuwa na mahusiano
mazuri ya kibiashara ambayo
yatakuza mahusiano yetu ya
kiuchumi, aliongeza Rais Magufuli.
Kwa upande wake Rais wa Jamhuri
ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe.
Truong Tan Sang anaeleza kuwa, ili
Inaendelea Uk. 9

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni


Inatoka Uk. 8

na Serikali ya Tanzania ya
kidiplomasia ya muda mrefu na
mahusiano hayo na makubaliano hivyo wataendeleza uhusiano
yazidi kuendelea, hakunabudi huo pamoja na kushirikiana ili
kuwa na mawasiliano ya karibu kukuza uchumi wa nchi hizo.
na kukutana mara kwa mara
baina ya watendaji wa Serikali Katika ziara hiyo, Rais wa
hizi mbili ikiwemo kutembeleana Vietnam mbali na kufanya
mara kwa mara kwa lengo la mazungumzo na Rais wa Jamhuri
kukuza maeneo waliyokubaliana. ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
John Pombe Magufuli, alifanya
Waziri wa Mambo ya Nje na pia mazungumzo rasmi na Rais
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe.
Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,
Augustine Mahiga anaeleza kuwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Serikali iliupa uzito wa pekee ugeni Muungano wa Tanzania, Mhe. Job
huo kwa sababu ni ziara ya kwanza Ndugai; Wafanyabiashara kutoka
ya kitaifa katika Awamu ya Tano sekta binafsi na kutembelea eneo
kufanywa na Mkuu wa Nchi hiyo. la uwekezaji la EPZA, lililopo
Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Mhe.
Augustine
Mahiga
anabainisha kuwa mbali na nchi Mikataba ya Mahusiano baina
Tanzania
na
Vietnam.
hiyo kuongoza katika kilimo ya
barani Asia, pia inasifikana Katika jitihada za kuimarisha
duniani kwa kuuza samaki aina mahusiano, mwaka 2001 Tanzania
ya Sato ambao walichukuliwa na Vietnam zilisaini Mkataba wa
kutoka
Ziwa
Victoria. Ushirikiano wa Kuichumi na ufundi.
Aliongeza kuwa, ili Tanzania nayo
ifike ilipo Vietnam hainabudi
kufuata mambo matatu ambayo
Vietnam inayazingatia ikiwemo
kufanya kazi kwa bidii katika
mazingira ya aina zote, utekelezaji
wa maamuzi wanayofanya na
kuwekeza katika mafunzo ya
ufundi, miundombinu kama vile
ya umeme, barabara, reli, bandari
na mabenki kwa ajili ya mitaji
na huduma nyingine za kifedha.
Naye Waziri wa Habari na
Mawasiliano wa Vietnam Mhe.
Nguyen Bal Son anaeleza kuwa
nchi yake ina historia nzuri
ya ushirikiano na mahusiano
9

Mkataba huo uliainisha maeneo


ya
ushirikiano
ikiwemo;
Kubadilishana uzoefu katika
sekta ya kilimo na maendeleo
vijijini; Kubadilishana uzoefu
katika matumizi ya sayansi na
teknolojia katika kuendeleza
kilimo cha umwagiliaji, uvuvi
na misitu; Kupeana taarifa za
fursa za masoko ya bidhaa
za kilimo; Vietnam kuipata
Tanzania utaalam na teknolojia
ya uvunaji na utunzaji wa maji.
Pia mwaka 2014 Tanzania na
Vietnam zilisaini Mkataba wa
ushirikiano katika sekta ya
mawasiliano ambapo kupitia

2016

mkataba huo kampuni ya


Vietel
maarufu kama Halotel
inayomilikiwa na Jeshi la Vietnam
imefanya uwekezaji mkubwa
katika sekta ya mawasiliano
nchini na kuzalisha ajira za
moja kwa moja kwa Watanzania
1600 na fursa za kujiajiri kwa
watanzania
20,000.
Vilevile,
kampuni hiyo kupitia mkataba
uliosainiwa, itatoa huduma za
internet bure kwenye mashule na
mahospitali ya Serikali vijijini.
Ni matumaini makubwa kuwa,
uhusiano huu kati ya Tanzania
na Vietnam uliodumu kwa
miaka zaidi ya hamsini sasa
utaleta
mabadiliko
katika
masuala mbalimbali ili kukuza
mahusiano ya kiuchumi na kuleta
maendeleo baina ya Tanzania.

Mke wa Rais wa Vietnam mama Mai Thi


Hanh (kulia) akimsalimia mcheza ngoma.

Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke


wa Rais wa Vietnam mama Mai Thi Hanh
wakifurahia ngoma.

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

2016

Mikakati ya Serikali katika kukabiliana


na uhaba wa chakula nchini
Na Ismail Ngayonga

atika kukabiliana na uhaba wa chakula


nchini, Serikali imeainisha sekta ya
kilimo kuwa miongoni mwa maeneo sita ya
kitaifa ya kimkakati yaliyo katika mpango
wa matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Chini ya Mpango huo zipo Sekta sita
ambazo zimeainishwa kuwa maeneo
ya
Kipaumbele
Kitaifa
(NKRA)
ili kuhakikisha kwamba Tanzania
inafanikisha malengo yake katika
kuleta maendeleo kwa wananchi na
Taifa kwa ujumla. Sekta hizo ni pamoja
na Kilimo, Elimu, Maji, Uchukuzi,
Nishati na Ukusanyaji wa mapato.
Kuibuliwa kwa Sekta ya kilimo kuwa
miongoni mwa vipaumbele Kitaifa
kunatokana na ukweli kuwa kilimo
kinachangia
asilimia
24
katika
pato la Taifa na kutoa ajira kwa
takribani asilimia 75 ya nguvukazi.
Maeneo
matatu
ya
kipaumbele
yaliyoainishwa kwa upande wa Sekta

10

ya kilimo ni pamoja na kutenga ardhi


kwa ajili ya mashamba makubwa
25 ya uwekezaji, kuwa na skimu za
umwagiliaji 78 za kilimo cha mpunga
na maghala 275 ya kuhifadhia mahindi.
Kiashiria cha Mafanikio ya mpango huo
kinatokana na kuongezeka kwa uzalishaji
wa mpunga kwa zaidi ya mara mbili
kutoka tani 4 hadi 8 kwa hekta ifikapo
mwaka 2016 katika skimu za umwagiliaji.
Kiashiria kingine ni ongezeko la wakulima
wadogo wanaolima mpunga katika skimu
za umwagiliaji zinazoendeshwa kitaalamu.
Lengo ni kuwa na wakulima 29,000 katika
skimu 39 ifikapo mwaka 2016 ambapo kwa
sasa skimu 26 zipo katika marekebisho
ili ziweze kuendeshwa kitaalamu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha
Uwekezaji Tanzania (TIC), Juliet Kairuki
alisema Serikali imeanza zoezi la kuwapata
wawekezaji katika mashamba hayo
limeanza na Hati Miliki za Mashamba

kwa ajili ya wakulima 1,052 zimeandaliwa.


Kati ya hizo hati 185 zimekamilika
kwa ajili ya kuwakabidhi wahusika.
Tathmini ya uzalishaji iliyofanyika
mwezi Agosti 2014 nchini ilibaini
kuwa uzalishaji wa mazao ya chakula
katika msimu wa kilimo wa 2013/2014
ulikuwa tani 16,015,238 zikiwemo
tani 9,828,540 za nafaka na tani
6,186,698 za mazao yasiyo ya nafaka.
Kiasi hicho cha chakula kikilinganishwa
na mahitaji ya chakula ya tani 12,767,879
katika mwaka 2014/2015 kilionesha
kuwepo kwa ziada ya tani 3,247,359 za
chakula, na kulifanya taifa kujitosheleza
kwa chakula kwa asilimia 125.
Aidha, akiba ya nafaka katika Wakala
wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA)
hadi kufikia mwezi Mei 2015 ilikuwa ni
jumla ya tani 422,285.705 zikiwemo tani
413,165.804 za mahindi, tani 5,180.271
za mtama na tani 3,939.630 za mpunga.

Inaendelea Uk. 11

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

Inatoka Uk.10

Taarifa ya mwaka 2015 ya Umoja wa


Mataifa iliyotolewa na Mfuko wa Kimataifa
wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) na
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani
(WFP) inaonyesha takribani watu Milioni
796 wanakabiliwa na njaa duniani.

Vile vile, hadi kufikia Mwezi Mei 2015


Serikali kupitia NFRA ilikuwa imewalipa
wakulima jumla ya Shilingi bilioni 77
zilizotokana na madeni mbalimbali.
Fedha zimegawanywa kwenye vituo,
vikundi na mawakala mbalimbali.
Serikali imeanza uhakiki wa maghala
275 ambapo maghala 113 yapo katika
hali nzuri yakihitaji matengenezo
madogo; maghala 74 yapo katika hali ya
kati yakihitaji marekebisho makubwa
kidogo na maghala 87 yameharibika
na hivyo yanahitaji kujengwa upya.
Aidha Mfuko wa Bill and Melinda
Gates Foundation umeahidi kutoa
dola 750,000 kwa ajili ya matengenezo
na kuyafanya ukarabati wa maghala
30 ili yaanze kazi. Maghala yaliyobaki
yatatengenezwa kwa kutumia fedha
za msaada kutoka Benki ya Dunia.
Kongamano la kilimo na usalama wa
chakula lililofanyika Jijini Washington,
Marekani
mwaka
2012
linaitaja
Tanzania kuwa ni kati ya nchi tatu za
kwanza Barani Afrika zitakazonufaika
na mpango wa pamoja wa kilimo kwa
nia ya kuongeza na kulinda usalama
wa chakula na lishe kwa watu wake.
Nchi nyingine ni Ethiopia na Ghana.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, kati yao watu


milioni 214 wapo katika Bara Afrika
hususani katika eneo la kusini mwa jangwa
la Sahara, na kueleza kuwa katika kila
watu tisa mmoja wao anakabiliwa na njaa.
Akihutubia Kongamano hilo lililofanyika
jijini Washington, Marekani, Rais wa
nchi hiyo Barrack Obama alisema nchi
hizo tatu za kwanza zimechaguliwa
kunufaika na ushirikiano huu kwa
vile
zimeonyesha
kufikia
katika
Kilimo na usalama wa chakula.
Tanzania ilialikwa kuhudhuria kikao
hicho kutokana na mpango wake wa
Kilimo Kwanza, ambapo nchi tajiri
duniani zimeuchukua kama mfano
ambapo juhudi na mikakati iliyomo
katika mpango huo itatumika na
kuendeleza nchi zingine barani Afrika.
Usalama wa chakula, ni suala linalopewa
kipaumbele na Serikali ya Tanzania.
Serikali iliandaa mikakati na programu
ambazo zilizaa mkakati wa Kuendeleza
Sekta ya Kilimo (ASDS). ASDS inasisitiza
sera muafaka na mikakati inayolenga
kuchochea wadau kutoka
sekta ya umma na binafsi
kuwekeza kwenye kilimo.
Mkurugenzi wa Idara ya
Usalama
wa
Chakula,
Wizara ya Kilimo, Mifugo
na Uvuvi Bw. Karim
Mtambo alibainisha kuwa
kwa sasa mikoa yote
nchini ina kiwango cha
chakula kwa asilimia 93.

Mkulima akipalilia shamba kwa


kutumia trekta.

11

2016

Mtambo alisema mavuno


ya mahindi katika nchi za Kusini mwa
Afrika yanatarajiwa kushuka kwa takriban
asilimia 26 ukilinganisha na mwaka 2014,
hali ambayo itasababisha kupanda kwa
bei ya chakula na kutia dosari katika
hali ya sasa ya usalama wa chakula.

Sekta ya kilimo ina dhamana ya kuzalisha


chakula kwa watu zaidi ya billioni
mbili ifikapo mwaka 2050. Jitihada za
kukuza Sekta ya Kilimo ni njia pekee
ya kukabiliana na ongezeko kubwa
la idadi ya watu linalotarajiwa barani
Afrika kwenye kipindi cha miaka ijayo.

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

2016

Watanzania waadhimisha siku ya


Uhuru Kwa kufanya usafi

kufanyika kwa takribani zaidi ya nusu karne


ya uhai wa Tanzania. Tukio hili lina lenga
kuhamisha maadhimisho tuliyozoea ya
kuona gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama
pamoja na halaiki na kushuhudia machepe,
toroli, ndoo, fyekeo na zana nyinginezo za
usafi zikitumika siku hiyo. Ama kweli Dkt.
Magufuli ni kiongozi mwenye uthubutu.

Na Raymond Mushumbusi

Kwa mujibu wa iliyokuwa,Wizara ya


Afya na Ustawi wa Jamii,mlipuko wa
ugonjwa wa kipindupindu umekuwa
ukitokea mara kwa mara hapa nchini na
kusababisha vifo vya Watanzania wengi.
Jitihada nyingi zimefanyika katika kuzuia
na kupambana ugonjwa wa kipindipindu
kupitia vyombo vya habari, lakini
bado tatizo hili limekuwa likiendelea.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli


akizoa takataka katika eneo ambalo alishiriki kufanya usafi siku ya Desemba
9, mwaka 2015 katika maadhimisho ya miaka 54 ya uhuru wa Tanganyika
katika maeneo ya kivukoni jijini Dar es salaam.

fikapo Desemba 9 kila mwaka, Watanzania


kote nchini husheherekea siku ya Uhuru.

Siku hii ni muhimu kwani ndipo Tanganyika


ilipata uhuru wake kutoka kwa wakoloni
kabla ya kuungana na Zanzibar. Hayati Baba
wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere ndiye
alikuwa muhasisi wa kwanza wa Taifa huru
la Tanganyika baada ya kupata uhuru huo.
Kutokana na tukio hilo la kihistoria,
Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere
aliamua kuwa ifikapo Desemba 9, kila
mwaka Watanzania waikumbuke siku
hiyo kwa kufanya sherehe nchi nzima.
Kitaifa,
katika
maadhimisho
hayo
Watanzania
walikuwa
wakishuhudia
maandamano na michezo ya halaiki na
gwaride la majeshi ya ulinzi na usalama.
Katika Awamu Nne za Uongozi wa Serikali
zilizopita, Marais wake waliendeleza
utamaduni wa kusheherekea siku ya Uhuru
hapa nchini ifikapo Desemba 9, kila mwaka.
Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere,
Mhe. Ali Hassan Mwinyi, aliyeongoza
Serikali ya Awamu ya Pili, Mhe. Benjamin
Mkapa aliyeongoza Serikali ya Awamu ya
Tatu na Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
aliyeongoza Serikali ya Awamu ya Nne, wote
walikuwa wakishiriki katika maadhimisho

12

ya siku ya kupata Uhuru wa nchi yetu.


Ilikuwa ni kama ndoto kwa Watanzania
walio wengi na pengine hata nchi jirani
pale ambapo Rais wa Awamu ya Tano Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli alipoagiza
kuwa, katika kusheherekea miaka 54 ya
uhuru ifikapo Desemba 9, 2015, Watanzania
kote nchini wafanye usafi kila mtu
katika eneo lake badala ya kusheherekea
siku ya Uhuru kama ilivyozoeleka.
Akielezea uamuzi wake huo, Dkt. Magufuli
alisema Hatuwezi kufanya sherehe huku
watu wetu bado wanakufa kwa ugonjwa wa
kipindupindu ambao unatokana na uchafu,
badala yake nchi nzima tufanye usafi siku hiyo.
Akitangaza rasmi uamuzi huo wa Dkt.
Magufuli, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi,
Balozi Ombeni Sefue alisema siku ya tarehe
9, Desemba mwaka huu (2015), itakuwa ni siku
ya Uhuru na Kazi. Hivyo basi, maadhimisho
ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanganyika
yatafanyika kwa watu kufanya usafi katika
maeneo yao ikiwa ni jitihada za Serikali za
kuimarisha usafi na kupambana na magonjwa
ya milipuko kama vile Kipindupindu.
Balozi Ombeni aliendelea kufafanua kwa
kusema Kero ya uchafu imemfanya Mhe. Rais
kufanya tendo la kihistoria ambalo halijawahi

Katika kipindi cha miezi nane (8) ambayo


ugonjwa wa kipindupindu umedumu
katika maeneo tofauti nchini na kwa
takwimu zilizopo kuanzia mwezi Augosti
2015 mpaka Aprili 17, 2016 jumla ya
watu 20,882 wameugua ugonjwa huo na
kati yao watu 329 wamepoteza maisha.
Katika kutekeleza agizo hilo, Rais Dkt.
John Magufuli aliongoza kwa vitendo
zoezi la kufanya usafi kama alivyoelekeza.
Dkt. Magufuli na mkewe Mama Janeth
Magufuli walifanya usafi katika maeneo ya
Feri, eneo ambalo liko mita kadhaa kutoka
Ikulu Jijini Dar es Salaam. Naye Makamu
wa Rais, Samia Suluhu alionekana akifanya
usafi katika eneo la ufukwe wa Bahari wa
Coco Beach na baadae kuelekea maeneo
ya Kinondoni Morocco Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa
aliungana na Wananchi kufanya usafi
katika maeneo ya Kariakoo Jijini Dar es
Salaam. Wizara, Taasisi, Idara, Wakala wa
Serikali, mashirika binafsi Asasi zisizo
za kiserikali, mabalozi wanaoziwakilisha
nchi zao walishiriki kufanya usafi
katika
maeneo
mbalimbali
katika
kutimiza agizo la Dkt. John Magufuli.
Kwa kuwa suala la usafi sio kwa Tanzania
Bara pekee, Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.
Ali Mohamed Shein, naye aliungana na
wananchi pamoja na viongozi wengine
wa kitaifa kote nchini kufanya usafi
ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya
miaka 54 ya Uhuru wa Tanganyika.
Dkt. Shein alishirikiana na viongozi

Inaendelea Uk. 13

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

Inatoka Uk. 7
mbalimbali wa Serikali,watumishi wa Idara
maalum za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
(SMZ) na vikosi vya JWTZ kufanya usafi
katika soko la samaki Malindi mjini Unguja.
Akizungumza mara baada ya kufanya
usafi, Dkt. Shein aliwakumbusha wananchi
haja ya kuimarisha usafi ambao umekuwa
ni utamaduni wa watu wa Zanzibar.
Aliwataka wananchi kufanya usafi
katika maeneo yote ya kazi,
makazi pamoja na maeneo
mengine ili kuimarisha usafi
wa mazingira pamoja
na wananchi wenyewe
kwa
kuwa
hatua
hiyo ni kuimarisha
afya
zao
pia.
Alifafanua
kuwa
uamuzi huo ni wa
busara na kitendo
cha
wengine
kufanya usafi na
wengine
kuendelea
na
majukumu
mengine
maofisini,
siku ya leo inadhihirisha
umakini na utekelezaji wa
kauli mbiu ya HAPA KAZI TU.
Kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw.
Alphayo Kidata ambaye pia amewahi
kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi
alisema suala la usafi ni muhimu na sio
la kulazimishwa bali ni lazima kwa kila
Mtanzania katika kuzingatia usafi ili
kuondokana na magonjwa hasa ya mlipuko
yanayosababishwa na hali ya uchafu.
Diwani wa Kawe Mheshimiwa Muta Robert
Rwakatare alimpongeza Mhe. Rais kwa
kufikiria na kutoa uamuzi wa kuwataka
Watanzania kufanya usafi. Alieleza
kwamba tatizo la uchafu limekithiri sana
na kuahidi kushirikiana na Serikali kupitia
Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni
kutafuta njia za kutatua changamoto.
Aliitaja changamoto kubwa iliyopo
ni katika kutekeleza kazi ya kufanya
mazingira
kuwa
safi
ikiwemo
upatikanaji wa magari ya kubebea taka.
Kwa upande wake mkazi wa kata
ya Kawe Bw. Hussein Bana alisema
wamelipokea suala la kufanya usafi katika
maeneo yao sio kila ifikapo Desemba

13

9 pekee, bali wataliendeleza suala hilo


na kuhamasishana hasa vijana kushiriki
katika kufanya usafi kwenye maeneo yao
ili kuondokana na magonjwa hasa ya
mlipuko na kujilinda wao na vijazi vijavyo.
Naibu Waziri wananchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luaga
Mpina alitangaza kuwa kila Jumamosi ya
mwisho wa mwezi itakuwa siku rasmi ya
kufanya usafi
w
a

mazingira
ili
kupambana na magonjwa yanayosababishwa
na uchafu kama vile kipindupindu.
Katika kulilipa nguvu swala kuimarisha
mazingira kwa kuzingatia usafi katika maeneo
mbalimbali,Halmashauri za Majiji ,Wilaya na
Miji Tanzania Bara na Visiwani zilianzisha
faini kupitia sheria ndogo ndogo zilizopo
ili kupambana na uchafuzi wa mazingira
unaofanywa kwa makusudi na baadhi ya watu,
na kwa kuanza Halmashauri ya Manispaa ya
wilaya ya Ilala ilitangaza rasmi kwa yoyote
atakayekamatwa anatupa taka sehemu
isiyostahili atatozwa faini ya shilingi elfu 50
taslimu na kutangaza kutoa nusu ya fedha
ya faini kama zawadi kwa kuwahamasisha
wananchi kutoa taarifa au kufanikisha
kukamatwa kwa mtu atakayevunja Sheria hiyo.
Kamapeni za usafi zilifanyika katika
Mikoa,Wilaya ,Miji na Vijiji nchi kote kwa
wananchi kushirika katika kufanya usafi na
kufanya usafi kuwa ni utamaduni wao na
sio mpaka litolewe tamko juu ya kusafisha
mazingira yanayowazunguka, katika kampeni

2016

hii ya usafi siku ya Desemba 9 ilikubwa


na baadhi ya changamoto ikiwa baadhi ya
wananchi kutoshiriki kampeni hizo katika
maeneo yao na kuwepo kwa uhaba wa
magari ya kuzolea taka katika Halmashauri
za Majiji, Wilaya na Miji iliyosababisha
taka kukaa kwa muda mrefu katika baadhi
ya maeneo lakini juhudi toka Halmashauri
hizo zilifanyika na kuwezesha kuzolewa
na kutupwa katika madampo husika.
Katika kutekeleza suala la kuimarisha usafi
wa mazingira Serikali kupitia Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee
na watoto kupitia Waziri wake Mhe.
Ummy Mwalimu ilitoa tamko la kupiga
marufuku uuzwaji wa vyakula ovyo
katika maeneo yasiyo rasmi na ya wazi
na uzwaji wa matunda yaliyokatwa
ikiwa ni jitihada za Serikali
kupambana na wafanyabiashara
wasiozingatia kanuni za usafi
na Afya ambazo zinaweza
kuhatarisha afya za walaji wa
vyakula hivyo ikiwemo mlipuko
wa magonjwa kama kipindupindu.
Kampeni hizo za usafi siku
hiyo zilileta mafanikio makubwa
katika jamii ya Watanzania hususani
kuhamasisha tabia ya kufanya usafi katika
maeneo yao ili kuweka mazingira safi na pia
kupambana na magonjwa ya mlipuko. Katika
kuweka mazingira safi kampuni mbalimbali
ziliunga mkono agizo la Rais la kufanya usafi
na kushiriki katika maeneo tofauti nchini.
Baadhi ya kampuni zilizoshiriki katika
kufanya usafi siku hiyo ya Uhuru wa
Tanganyika ni pamoja na Clouds Media
Group, Msalaba Mwekundu, Max Malipo,
NSSF, Benki ya Biashara ya Akiba (ACB),
Shirika la Afya Duniani (WHO) na Kliniki
ya Tiba Mbadala ya Ifakara Herbalist
Clinic waliofanya usafi katika soko la
Tandale, wengine ni Mohamed Enterprises
Group MeTL Benki ya FNB waliofanya
usafi ufukwe wa Coco,GEPF na kampuni
ya Saruji ya DANGOTE walifanya usafi
soko la Mbae Mkoani Mtwara, Airtel
Tanzania ilifanya usafi Hospitali ya Wilaya
ya Nzega Tabora, kampuni ya PUMA
ilishiriki na kutoa vifaa vya usafi katika
Manispaa ya Temeke na Azania Bank
nayo ilitoa vifaa vya usafi na kushiriki
usafi katika Halmashauri ya Mji wa Moshi.
Naye Diwani wa Kawe Mhe. Muta Robert
Rwakatare alimpongeza Mhe. Rais kwa
kufikiria na kuleta jambo ambalo ni jema

Inaendelea Uk. 14

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni


Inatoka Uk. 13
kwa Watanzania kwani tatizo la maeneo kuwa
machafu limekithiri kuahidi kushirikiana na
Serikali kupitia halmashauri ya wilaya ya
Kinondoni kutafuta njia za kutatua changamoto
zinazoikabili Manispaa katika kutekeleza kazi
ya kufanya mazingira kuwa safi ikiwemo
upatikanaji wa magari ya kubebea taka.
Kwa upande wake mkazi wa kata ya Kawe
Bw. Hussein Bana alisema wamelipokea sula
la kufanya usafi katika maeneo yao sio kwa
siku ya Desemba 9 ,pekee bali wataliendeleza
suala hilo na kuhamasishana hasa vijana
kushiriki katika kufanya usafi kwenye maeneo
yao ili kuondokana na magonjwa hasa ya
mlipuko na kujilinda wao na vijazi vijavyo.
Juhudi zimefanya Wizara inayohusika na
Mazingira kwa kushirikiana na Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto katika kutoa elimu juu ya
umuhimu wa kufanya usafi katika mazingira
ili kujenga tabia ya kuweka mazingira
safi na kujiweka mbali na magonjwa ya
mlipuko yanayosababishwa na uchafu.
Haya shime Watanzania tumuunge mkono Rais
wetu kwa kuufanya usafi kuwa ni tabia katika
maisha ya kila siku ingawa kuna changamoto
mbalimbali zinazokakabili maeneo yetu
zikiwemo Halmasahuri za Majiji,Wilaya na
Miji katika kutatua changamoto hizo, hivyo
basi hatuna budi kushirikiana na Serikali ya
Rais Magufuli kuboresha mazingira yetu kwa
kufanya usafi kwa faidi yetu na vizazi vyetu
na tudumishe muungano wetu kwa kuzingatia
suala la usafi katika maeneo yetu ili kudumisha
afya na usalama wa familia na vizazi vijavyo.

Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli akishiriki zoezi la kufanya usafi siku
ya kuadhimisha miaka 54 yaUhuru.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu


Hassan (aliyevaa raba) akishiriki zoezi la kufanya usafi siku ya kuadhimisha
Miaka 54 ya Uhuru.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa


Baraza la Mapinduzi,Mhe. Dkt. Ali
Mohamed Shein akizoa taka katika zoezi
usafi wa mazingira katika kuadhimisha
miaka 54 ya Uhuru

14

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznia, Mhe. Kassim Majaliwa


akishiriki zoezi la usafi siku ya kuadhimisha Miaka 54 ya Uhuru.

2016

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

2016

Serikali kutoa Hati ya Kumiliki Ardhi


ndani ya mwezi mmoja

atajua kilichotokea kwa sababu urasimu


umepunguzwa na utaratibu umerahisishwa
zaidi.
Alisema
Waziri
Lukuvi.

Na Eleuteri Mangi

anzania ni miongoni mwa nchi tajiri


wa ardhi katika Ukanda wa Afrika
Mashariki ambayo inaweza kutumika
katika shughuli mbalimbali za maendeleo
ya kijamii na kichumi kama vile makazi,
uhifadhi wa misitu, madini na kilimo
ambazo zinaaminika kuwa ni uti wa mgongo.

Aidha, alieleza kuwa Sera ya Taifa ya


Ardhi ya mwaka 1995, Sheria ya Ardhi
Na. 4 ya mwaka 1999 na Sheria ya Ardhi
ya Vijiji Na. 5 ya mwaka 1999 zinatoa
haki sawa kwa raia wote kumiliki ardhi
sehemu yoyote ya nchi bila kujali jinsia
wala sehemu mwananchi alikozaliwa.

Kwa mujibu wa tarifa ya Idara ya Takwimu ya


Taifa,Tanzania inakadiriwa kuwa na ukubwa
wa kilomita za mraba 945,087 sawa na maili
za mraba 364,087, kati ya hizo Kilometa
885,800 ni ardhi na Kilometa 61,500 ni
bahari, maziwa na mito. Idadi ya Watanzania
inakadiriwa kufikia zaidi ya milioni 51.82,
kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012.

Akizungumzia utaratibu wa utoaji wa


hati hizo, Waziri Lukuvi alisema tayari
maandalizi na maekelezo yametolewa kwa
Makamishina wa Kanda wanaozitoa na
Msajili anayezisajili ili mwananchi yeyote
ambaye ameilipia awe ameipata ndani ya
kipindi hicho. Vifaa vyote vya kutayarishia
ikiwa ni pamoja na karatasi zipo za kutosha
kuweza kutumika mwaka mzima kwa kila
Halmashauri alisisitiza Waziri Lukuvi.

Pamoja na kuwepo na eneo kubwa


la ardhi, wananchi katika maeneo
mbalimbali nchini wanakabiliwa na
migogoro inayotokana na umiliki wa ardhi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi, Mhe. William Lukuvi alisema
kwamba, migogoro mingi imekuwa
ikisababishwa na baadhi ya watendaji wasio
waaminifu ambao kwa makusudi wamekuwa
wakitoa Hati za Kumiliki Ardhi bila kufuata
utaratibu au kuwashirikisha wananchi.
Kutokana na tabia hiyo, wamekuwa
wakisababisha kuwepo kwa migogoro mingi
baina ya wananchi wenyewe, wananchi
na wawekezaji au wakulima na wafugaji
pale inapogundulika kuwa wameingiliana
katika umiliki au matumizi ya ardhi husika.
Waziri Lukuvi alieeleza kuwa, ili kudhibiti
migogoro inayotokea na pia kuwaondolea
wananchi kero na usumbufu wa kupata
hati Serikali sasa imeandaa utaratibu
wa kupima viwanja sehemu mbalimbali
nchini na kuweka muda maalumu ambapo
ndani ya mwezi mmoja mwananchi
ambaye tayari amelipia Hati yake ya
kumiliki ardhi lazima awe ameipata.
Aidha, katika kuhakikisha kwamba dhana
ya uongozi na utawala bora inazingatiwa,
Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa
wananchi wanashirikishwa ipasavyo katika
suala zima la usimamizi wa rasilimali
ardhi kuanzia ngazi ya kijiji hadi Taifa.

15

Muonekano wa Jengo la Nyumba za Shirika


la Nyumba la Taifa (NHC) zilizopo eneo la
Mindu Upanga.
Kwa mujibu wa Waziri Lukuvi, alisema
changamoto iliyopo hivi sasa ni namna ya
kuhakikisha kwamba ardhi yote inapimwa
na kumilikishwa kisheria. Aliongeza kwamba
ili kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali
imeongeza kasi ya kupanga, kupima na
kumilikisha ardhi kwa wananchi kwa ajili
ya shughuli mbalimbali za kiuchumi na
kijamii na hivyo, kuongeza fursa za ajira,
kupunguza umaskini na kukuza pato la Taifa.
Alifafanua kwamba, baada ya Serikali ya
Awamu ya Tano kuingia madarakani wizara
yake imefanikiwa kutoa hati 6,038 na kuzisajili
ikilinganishwa na miezi mitatu kabla ya
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka 2015
ambapo zilitolewa hati 2,000. Hatua hiyo
ya utoaji hati umeongezeka mara tatu zaidi.
Aliongeza kuwa, ongezeko hilo ni sawa na
asilimia 75.1 ikilinganishwa na asilimia 24.9
miezi mitatu kabla ya Uchaguzi Mkuu wa
mwaka jana. Sababu ya kuongezeka kwa utoaji
hati linatokana na kupunguza muda ambao
mwananchi alipaswa kusubiri ili kupata
hati. Muda huo umepunguzwa kutoka miezi
sita na miezi mitatu ya awali, ambapo sasa
mwananchi anatakiwa kusubiri kwa kipindi
cha mwezi moja tangu alipie ada zote za
ardhi katika ofisi yeyote ya ardhi nchi nzima.
Mtu yeyote ambaye atashindwa kupata hati
chini ya mwezi mmoja na amelipa ada yake
kwa Serikali, mkoa na kwa halmashauri
anapaswa kumwandikia barua Waziri

Alizitaja kanda zitakazohusika na utoaji wa


hati ni pamoja na Kanda ya Dar es salaam
inayojumuisha Manispaa za Ilala, Temeke
na Kinondoni, Kanda ya Mashariki ambapo
makao makuu yake yapo Morogoro, Kanda ya
Magharibi makao yake makuu yapo Tabora,
Kanda ya Ziwa makao yake makuu yake yapo
Mwanza na Kanda ya Kaskazini makao yake
makuu yapo Moshi mkoani Kilimanjaro.
Kanda zingine ni Kusini ambayo makao
yake makuu yapo Mtwara, Kusini
Magharibi makao yake makuu yapo
Mbeya na Kanda ya Kati ambayo makao
yake makuu yapo mkoani Dodoma.
Akifafanua juu ya utaratibu wa utoaji ardhi
ya kijiji, Waziri Lukuvi alisema, mauzo ya
eneo linalofikia hadi kiwango cha heka
50 ni lazima yaidhinishwe na Mkutano
Mkuu wa Kijiji ambapo mauzo ya ardhi
ya kijiji yenye heka 50 hadi 150 ni lazima
yaidhinishwe na Mkutano Mkuu wa Kijiji
na kupewa kibali cha Mkurugenzi wa
Wilaya. Mauzo ya ardhi ya kijiji yanayozidi
heka 150 ni lazima pia yaidhinishwe na
Mkutano Mkuu wa Kijiji, Mkurugenzi
wa Wilaya na kisha Kamishna wa Ardhi.
Aidha, pale ambapo kijiji kinataka
kuhamisha ardhi yeyote inayozidi heka 50
kwenda kwa mtu binafsi ni lazima maamuzi
yake yatokane na Mkutano Mkuu wa Kijiji
utakaosimamiwa na Mkuu wa Wilaya.

Inaendelea Uk. 27

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

2016

Elimu ya Msingi na Sekondari kutolewa


bure Nchini
Na Lilian Lundo.

atika Kampeni zake za kugombea Urais


nchini Tanzania, Mgombea kupitia
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli aliwaahidi Watanzania
kwamba akichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania atahakikisha
kuwa Elimu ya Msingi na Sekondari
hadi Kidato cha Nne inatolewa bure.
Ahadi hii imetekelezwa na Dkt. Magufuli
baada ya kushinda nafasi hiyo ya Urais,
katika hotuba yake alipokuwa akifungua
Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania mjini Dodoma ambapo alitangaza
rasmi kuwa elimu hizo sasa zitatolewa bure.
Akifafamua juu ya azma ya Serikali yake
kuamua kutoa elimu hizo, Rais Magufuli
alisema kuwa kumekuwepo na changamoto
nyingi za kushuka kwa kiwango cha elimu
na ufaulu wa wanafunzi nchini. Moja ya
changamoto hizo ni wazazi kushindwa
kulipa ada na michango mbalimbali isiyo
ya lazima wanayotakiwa kutoa shuleni.
Aidha, uchache wa vyumba vya madarasa na
madawati umekuwa ukichangia kutofanya
vizuri wanafunzi wanapofanya mitihani
yao ya mwisho kutokana na kutokuwa na
uelewa wa kutosha kitaaluma kutokana
na mazingira mabaya wanayofundishiwa,
na hivyo kuwafanya washindwe kusikiliza
vema wanapofundishwa na walimu wao.
Rais aliwataka wakuu wa shule kufuta
michango isiyo ya lazima kwa wazazi shuleni
na vile vile kutolipisha mchango wowote kwa
wazazi wanaoandikisha watoto wao shule za
awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mhe. George Simbachawene alieleza kuwa
katika kutekeleza Sera ya Elimu Bila Malipo,
Serikali imeainisha majukumu yake ikiwemo
kutafsiri Sera kwa kutoa nyaraka, miongozo
na kusimamia utekelezaji wake katika ngazi
mbalimbali za kiutawala. Aidha, Serikali
imechukua jukumu la kulipa ada na michango
yote iliyopaswa kulipwa na wazazi shuleni.
Aliongeza
kwamba,
TAMISEMI
kwa
kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi,

16

Teknolojia na Ufundi zimeshatoa miongozo na


nyaraka mbalimbali juu ya utekelezaji wa Sera
ya Elimu Bila Malipo. Miongoni mwa nyaraka
zilizotolewa ni pamoja na Mwongozo wa Utoaji
Elimu ya Msingi Bila Malipo, Mwongozo wa
Uandikishaji Darasa la Kwanza 2016, Maelezo
kwa Wanafunzi Wanaojiunga Kidato cha
Kwanza Mwaka 2016, na Miongozo kuhusu
Matumizi ya Fedha zitakazopelekwa Shuleni.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Msaidizi wa


Idara ya Usimamizi wa Elimu wa TAMISEMI
Paulina Nkwama, moja ya malengo ya dhana
ya elimu bila malipo ni kuongeza ufaulu
kupitia mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu
na wanafunzi katika mchakato wa ufundishaji
na ujifunzaji. Alisema, mafunzo kwa walimu
yanafanyika kwa awamu mbalimbali na
hadi sasa awamu mbili zimeshafanyika.
Awamu ya kwanza jumla ya walimu 4,544
mmoja kwa kila somo katika masomo ya
Kiswahili, Hesabu, Kiingereza, Hisabati
na Baolojia kutoka kwenye kila shule
walitarajiwa kushiriki mafunzo hayo. Katika
awamu ya pili walimu 3,815 waliwezeshwa
kimafunzo, wakiwemo 1,053 wa Kiswahili,
1,041 wa Kiingereza, 829 wa Hisabati na 892
wa Baolojia. Walimu hawa walitoka mikoa
ya Iringa, Pwani, Lindi, Mtwara, Katavi,
Singida, Kagera, Morogoro na Manyara.
Mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha Walimu
kuwatambua wanafunzi wenye uwezo mdogo
kimasomo na kuwapatia mafunzo rekebishi
ili waweze kufanya vizuri katika mtihani
wa Taifa wa kuhitimu elimu ya Sekondari.
Naye Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Ufundi, Stela Manyanya
alifafanua dhana ya elimu bure isichukuliwe
kama sababu ya wazazi na walezi kukwepa
majukumu yao ya msingi ya kuwasimamia
watoto wao kimalezi na kielimu. Aidha
alisema Sera ya elimu bila malipo inalenga
kuwapunguzia mzigo walimu hasa wa
gharama kama ada ambazo awali walikuwa
wakilipa Serikalini. Kauli hii inatoa mwanga
kuhusu mtazamo potofu wa baadhi ya
wazazi waliojitoa kusimamia elimu kwa
watoto wao kwa hoja kuwa huo ni mzigo
unaopaswa kubebwa na Serikali pekee.
Mkurugenzi Msaidizi ufuatiliaji na tathmini
wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na
Mafunzo ya Ufundi Makuru Petro alisema,
ili kuhakikisha Elimu bure inafanikiwa
nchini Serikali imetenga kiasi cha shilingi
131,430,280,000 ambacho kitatumika kuanzia
mwezi Januari hadi June, 2016 fedha ambazo

zimetafutwa nje ya bajeti ya mwaka 2015/16.


Akitoa mgawanyo wa fedha hizo na namna
zitakavyokuwa zikitumwa Makuru alisema
kuwa, kila mwezi Hazina itakuwa ikituma
kiasi cha shilingi 18,775,754,285 kwenda
shule zote za Serikali Tanzania kuanzia
darasa la kwanza mpaka kidato cha nne.
Makuru alisema kuwa katika fedha
hizo shilingi 18,775,754,285, shilingi
15,712,318,571 zitatumwa moja kwa
moja kwenye akaunti za shule na
3,063,435,744 zitatumwa kwa ajili ya
malipo ya mitihani ya kidato Taifa
inayofanyika shule za msingi na sekondari.
Akitolea ufafanuzi wa fedha za mitihani,
Makuru alisema kuwa Serikali imeamua
kuwa inatuma kiasi cha shilingi 3,063,435,744
kila mwezi badala ya kuituma fedha hiyo kwa
mara moja ili kuipunguzia Serikali mzigo wa
kutuma fedha nyingi kwa wakati mmoja.
Elimu bure imepelekea ongezeko kubwa
la uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la
kwanza katika shule nyingi za msingi hapa
nchini ambapo shule hizo zimeandikisha
wanafunzi zaidi ya malengo ambayo shule
ilijiwekea kuwapokea kwa mwaka 2016.
Makuru alisema ongezeko la wanafunzi
limetokana na sera mbili ambazo ni sera
yenyewe ya elimu bure ambayo imepelekea
wanafunzi wengi kuandikishwa kutokana
na kutokuwepo na gharama zozote za
uandikishaji kwa wanafunzi wa darasa
la kwanza. Sababu ya pili ya ongezeko la
wanafunzi shule za msingi ni utekelezaji wa
sera ya kuanza darasa la kwanza kuanzia miaka
6 ambayo imeanza kutekelezwa mwaka huu.
Sera hii imepelekea ongezeko kubwa la
wanafunzi kutokana na wanafunzi waliokuwa
miaka sita kwa mwaka 2015 ambao mwaka
huu wametimiza miaka saba kuandikishwa
pamoja na wanafunzi ambao wana miaka sita
mwaka huu 2016 hivyo kupelekea ongezeko
kubwa la wanafunzi wa darasa la kwanza
mwaka huu 2016. Makuru alisema hadi
sasa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia
imeandikisha
wanafunzi
1,341,589.
Kutokana na ongezeko hilo la wanafunzi,
Serikali ya Awamu ya tano imejizatiti
kukabiliana na tatizo hilo ikiwa ni
pamoja na Mhe. Rais Magufuli kuwataka
mawaziri na manaibu waziri, makatibu
wakuu na manaibu
wao
kuchangia

Inaendelea Uk.17

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

Inatoka Uk. 16
kiasi cha shilingi milioni moja kutoka
katika mishahara yao ya mwezi Februari.
Huku yeye mwenyewe Mhe. Rais, Makamu
wa Rais na Waziri Mkuu wakichangia shilingi
milioni sita kila mmoja ambayo jumla
inaleta shilingi milioni100 zilizopangwa
kujenga shule mpya jijini Dar es Salaam
kwa ajili ya wanafunzi waliongezeka.
Mhe. Rais pia aliwataka Wakuu wa Mikoa,
Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri
kuhakikisha tatizo la madarasa na madawati
linatatuliwa kwenye maeneo yao. Mhe. Rais
alisema kuwa upungufu wa madarasa na
madawati ni kipimo cha kuendelea ama
kutoendelea na wadhifa wa kuwa Mkuu wa
Mkoa, Wilaya au Mkurugenzi wa Halmashauri.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mhe. George Simbachawene alisema agizo
liilotolewa na Mhe. Rais kuwa halina
mjadala na aliwataka wakurugenzi wa
halmashauri kuhakikisha mpaka Juni, 2016
pasiwepo na mwanafunzi anaketi sakafuni
na wakurugenzi watakaoshindwa, watakuwa
wameshindwa kazi na watawajibishwa.
Aidha, Waziri Simbachawene aliwataka
Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao ni
wasimamizi wa rasilimali zilizopo katika
maeneo ya misitu, wasisite kutoa vibali
vya uvunaji wa miti ya kutengeneza
madawati kwenye wilaya zao ili wanafunzi
wote nchini wakae kwenye madawati.
Tamko la Rais kuhusu elimu bure limeleta
mwamko kwa wazazi wengi kuandikisha
watoto wao darasa la kwanza, jambo
ambalo linaonyesha wazazi wengi walikuwa
wanashindwa kuandikisha watoto wao kutokana
na gharama ya uandikishaji na michango
mingine iliyokuwa ikichangishwa shuleni.
Bwana Mussa Hassan ni mkazi wa jiji la
Dar es Salaam, ambaye amepokea kwa
mikono miwili suala la elimu bure huku
akimsifia Rais kwa kufuta ada na michango
kwa shule za msingi na Sekondari.
Bwana Mussa alifafanua kuwa wazazi wengi
walikuwa wanashindwa kuandikisha watoto
wao kutokana na gharama ya uandikishaji
na michango ambayo mzazi anachangishwa
kama michango ya madawati na ulinzi.

17

2016

Serikali yawakopesha
wachimbaji wadogo Sh. 2.5bn
Na Jacquiline Mrisho.
Katika jitihada za kuwajengea uwezo wa
kiuchumi wachimbaji wadogo wadogo, Serikali
imetenga jumla ya Shilingi 2.5b/= kwa ajili ya
mikopo ya masharti nafuu na Shilingi 5.74b/=
kama ruzuku kupitia mradi wa Benki ya dunia.
Aidha, Serikali imetenga kiasi cha Shilingi
bilioni 1.80 kwa ajili ya kununua mitambo
miwili ya uchorongaji miamba ambayo
ingepelekwa katika ofisi za madini za kanda
ya Ziwa (Mwanza) na kanda ya Kusini
Magharibi (Mbeya), ili itumike kwenye
utambuzi wa kiasi cha mashapo yaliyopo
katika maeneo ya wachimbaji wadogo.
Hatua ya Serikali ya kuwawezesha wachimbaji
wadogo wadogo na pia kuwapatia nyenzo
au vitendea kazi inatokana na kilio cha
miaka mingi ambapo wamekuwa wakidai
kuwa Serikali haiwajali na hivyo familia
nyingi kuendelea kuwa masikini zaidi.
Aidha, ilionekana kuwa wachimbaji hao
wadogo wadogo hawakuwa na mchango
wowote katika kuinua uchumi wa Taifa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara
ya Nishati na Madini, katika kipindi cha
mwaka 2010 mpaka 2015 Serikali imejitahidi
kuwakwamua wachimbaji wadogo wadogo kwa
kuanzisha mchakato wa kuwawezesha kupata
maeneo ya uchimbaji, elimu ya uchimbaji, vifaa
na upatikanaji wa soko la madini wanayopata.
Katika mwaka wa fedha 2010/2011 Wizara
hiyo ilianza kutoa mafunzo kwa wachimbaji
wadogo wadogo kuhusu usalama, utunzaji
wa mazingira na biashara ya madini. Aidha,
Wizara iliwapeleka wazalishaji watano wa
chumvi nchini India kwenye mafunzo ya
muda mfupi ya teknolojia bora ya uzalishaji
wa chumvi na kugharamia mafunzo ya
ujasiriamali yaliyofanyika Tanga kwa watu 34.
Katika mwaka wa fedha 2013/2014
Wizara pia kupitia Shirika la Madini la
Taifa (STAMICO) ambalo lina jukumu la
kuratibu shughuli za kuendeleza wachimbaji
wadogo wadogo wa madini lilitenga jumla
ya shilingi bilioni 2.3 kwa ajili ya mfuko
wa mikopo ya kuwaendeleza wachimbaji
wadogo. Pia jumla ya shilingi milioni 880.68
zilitengwa kwa ajili ya mfuko wa ruzuku.

Katika kipindi cha mwaka 2010 hadi


2015 Serikali imejitahidi kuwakwamua
wachimbaji hao kwa kuanzisha mchakato
wa kuwawezesha kupata sehemu za
uchimbaji, elimu ya uchimbaji, vifaa
na upatikanaji wa soko la madini hayo.
Katika mwaka wa fedha 2010/2011 Wizara
ilianza kutoa mafunzo kwa wachimbaji
wadogo wadogo kuhusu usalama, utunzaji wa
mazingira na biashara ya madini na mwaka
huohuo Wizara iliwapeleka wazalishaji watano
wa chumvi nchini India kwenye mafunzo ya
muda mfupi ya teknolojia bora ya uzalishaji
wa chumvi na kugharamia mafunzo ya
ujasiriamali yaliyofanyika Tanga kwa watu 34.
Akiwasilisha makadirio
ya mapato na
matumizi ya bajeti ya Wizara na Taasisi zilizo
chini yake kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015,
aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini
katika Serikali ya Awamu ya Nne na ambaye
pia ni Waziri katika Serikali ya Awamu ya
Tano katika Wizara hiyo hiyo, Mhe. Profesa
Sospeter Muhongo alisema kuwa, Serikali
itaendelea kuwawezesha wachimbaji wadogo
wadogo kupata mitaji na tayari Wizara imetoa
mikopo ya masharti nafuu ya Shilingi milioni
88 kwa vikundi vya wachimbaji wadogo
wadogo 11 kupitia Benki ya Rasilimali.
Kwa miaka mingi sasa wachimbaji wadogo
wadogo nchini wamekuwa wakikabiliwa na
changamoto mbalimbali katika shughuli za
uchimbaji wa madini. Baadhi ya changamoto
hizo ni pamoja na matumizi ya nyenzo
na vifaa duni ambavyo haviwezi kuhimili
kufanya kazi katika maeneo makubwa
ya migodi na hawana mitaji ya kutosha.
Changamoto nyingine ni elimu ndogo ya
uchimbaji, bajeti ndogo inayotolewa na
Serikali kwa ajili yao, kukosekana kwa
vifaa vya kisasa vya uchimbaji na uhaba wa
maeneo ya uchimbaji kwa vile maeneo mengi
yamechukuliwa na wachimbaji wakubwa.
Serikali ya Tanzania imejitahidi kuwasaidia
kwa hali na mali wachimbaji wadogo
wadogo kwa kuweka sera zinazowawezesha
wachimbaji hao kuwa na mazingira rafiki
katika kutekeleza kazi zao za kila siku.

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

UZINDUZI WA DARAJA LA KIGAMBONI KATIKA PICHA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli


(mwenye tai nyekundu) akikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa daraja la Nyerere
lililopo eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Muonekano wa daraja la Nyerere lililopo katika wilaya mpya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

18

2016

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

UZINDUZI WA DARAJA LA KIGAMBONI KATIKA PICHA

Baadhi ya wananchi wakipita katika daraja la Mwalimu Nyerere mara baada ya kuzinduliwa
rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa daraja la Mwalimu Nyerere wakishuhudia tukio hilo katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam.

19

2016

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

PICHA ZA MATUKIO YA MUUNGANO

Mwl. Julius K. Nyerere (katikati) akichanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar huku akishuhudiwa
na Rais Sheikh Abed Amani Karume tarehe 26 Aprili, 1964 Zanzibar.

Mwl. Julius K. Nyerere (aliyekaa kushoto) na Sheikh Abed Amani Karume (aliyekaa kulia) wakisaini
Hati za Makubaliano ya Muungano tarehe 22 Aprili, 1964 Zanzibar.

20

2016

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

PICHA ZA MATUKIO YA MUUNGANO

Sheikh Abed Amani Karume (katikati) akiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano, Mhe. Rashidi Mfaume Kawawa (kulia) pamoja na Kanali Seif Bakari wakiwa
katika moja ya matukio ya Muungano.

21

Mwl. Julius K. Nyerere (kushoto) na Sheikh Abed Amani


Karume (kulia) wakibadilishana Hati za Muungano, 1964
Dar es Salaam.

2016

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

2016

REA yawezesha Wananchi kuanzisha


Miradi ya kiuchumi Vijijini
Na Jovina Bujulu

sambazaji
wa nishati ya umeme
unaofanywa na Wakala wa Nishati
Vijijini (REA) umewezesha wananchi
wengi walioko vijijini kuanzisha miradi
mbalimbali ya kiuchumi na kijamii.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa
REA nchini Dkt. Lutengano Mwakahesya,
nishati bora inachangia ukuaji wa uchumi
wa Taifa jambo ambalo linasaidia kuboresha
hali ya maisha ya Wananchi wengi walio
vijijini. Kwa kutambua umuhimu huo REA
kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali
imeweza kuibua miradi mbalimbali ya nishati
vijijini ili Wananchi waweze kufaidika nayo.
Wadau hao ni pamoja na Shirika la Umeme
Nchini (TANESCO), Mamlaka ya Udhibiti wa
Bei za Bidhaa (EWURA), Wizara ya Nishati
na Madini, Asasi zisizo za Kiserikali (AZISE),
Asasi za Kijamii (AZAKI) na Sekta binafsi.
Dkt. Mwakahesya ameainisha miradi ya nishati
za umeme kuwa ni pamoja na ile inazoyumia
nguvu ya upepo, jua, maji na bayogasi.
Dkt. Lutengano ameeleza kwamba, lengo
kubwa la ushirikiano baina ya REA na Wadau
hao ni kuibua miradi mbalimbali ya nishati,
kutoa ruzuku na kuwezesha upatikanaji wa
ushauri wa kitaaluma kwa waendelezaji wenye
sifa katika masuala ya kiufundi, usimamiaji,

22

uchanganuzi wa kifedha, ugharamiaji wa


miradi na mienendo mizuri ya miradi hiyo.
Alisema,
REA
inahakikisha
kwamba
uendelezaji wa miradi ya nishati vijijini
unazingatia utumiaji wa mazingira ili
kutunza vyanzo vingine vya nishati.
Aliongeza kusema kuwa REA inaongozwa na
Bodi ya Nishati vijijini ambayo husimamia
uendeshaji wa Mfuko wa Nishati vijijini
(REF). Mfuko huu unasaidia kuongeza
kasi ya upatikanaji wa miradi ya nishati.
Serikali kupitia mfuko wa huo, ilifadhili
miradi kabambe ya usambazaji wa
umeme vijijini awamu ya kwanza na ya
pili ambayo inatekelezwa na wakandarasi
binafsi katika mikoa yote ya Tanzania Bara.
Utekelezaji wa mradi huu umekamilika
kwa asilimia 90 na ambapo kilometa
1600 za msongo wa kati na kilometa
97 za msongo mdogo zimejengwa na
vipoza umeme vilifungwa na wateja wa
awali 18,253 wameunganishiwa umeme.
Katika awamu ya pili mradi ulilenga kujenga
vituo 6 vya kuongeza msongo wa (umeme
11/33 KV) katika miji ya Kigoma, Kasulu,
Kibondo, Ngara, Mbinga na Tunduru, ujenzi
wa njia za umeme msongo mdogo na wa kati

na kufunga mashine umba (transfomer)


3100. Mradi ulilenga kuunganisha wateja
225,000 na vijiji 2,500 pindi ukikamlika na
kupeleka umeme makao makuu ya wilaya 13.
Mradi huu uliweza kujenga vituo 6 vya
kuongeza nguvu Kigoma Vijijini, Kasulu,
Kibondo, Ngara, Mbinga na Tunduru.
Aidha mradi ulikamilisha ujenzi wa njia
za msongo mdogo na wa kati,na wateja
61,023 walipatiwa umeme. Jumla ya
vijiji 1,162 viliunganishwa kwenye gridi.
Akielezea juu ya shughuli za kiuchumi
na kijamii zilizoanzishwa vijijini Dkt.
Mwakakahesya alisema, kutokana na
upatikanaji wa nishati ya umeme vijijini
maisha ya wananchi yamekuwa mazuri
kutokana na kuwepo kwa shughuli za
kibiashara kama vile, mashine za kusaga na
kukoboa nafaka, viwanda vya uselemala,
utengenezaji wa milango na madirisha
ya chuma, uuzaji wa vinywaji baridi n.k.
Kwa upaande wa shuhguli za kijamii,
upatikanaji wa nishati wa umeme
umeboresha huduma za hospitali, vituo vya
afya na kumeongezeka kwa ari ya wanafunzi
kujisomea wakati wote na pia matumizi ya
kompyuta mashuleni, Kwa sasa wanawake
wajawazito
wanakwenda
hospitalini

Inaendelea Uk. 23

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

2016

Inatoka Uk. 22
kujifungua bila kulazimika kuchukua koroboi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya
Nishati na Madini, hadi mwaka 2014 kiwango
cha uunganishaji umeme katika Makao
Makuu ya Wilaya na vijijini ulifikia asilimia
24 na kufanya wananchi wanaopata huduma
za umeme kufikia asilimia 36 ya Watanzania
waishio
bara ukilinganisha na mwaka
2005 ambapo kiwango cha uunganishaji
umeme kilikuwa chini ya asilimia 10.

Hadi kufikia Desemba 2015 vijiji 5,009


ambavyo ni sawa na asilimia 33 vilikuwa
vimeunganishwa na huduma za umeme na
miradi inayoendelea itaunganisha vijiji vingine
vipya 1,340 na kufanya jumla ya vijiji 6,349
kupata huduma ya umeme miradi ikikamilika.

kumudu
gharama
za
kuunganishiwa
umeme, upatikanaji wa rasilimali fedha
za kutosha na usalama wa miundombinu
kutokana na uharibifu na vitendo vya
uharibifu vinavyofanywa na wananchi.

Akizungumzia changamoto zinazoikabili


wakala, Rwelengera alisema kuwa ni
pamoja na wananchi wa vijijini kushindwa

Raarifa hiyo inaonesha kwamba ongezeko hilo


linatokana na juhudi mbalimbali za Serikali
ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa Wakala
wa Nishati vijijini (REA) na kupunguza
gharama za kuunganisha umeme wa njia moja
na kuhamasisha wananchi kutumia umeme.
Jumla ya shule za sekondari 1845, zahanati na
vituo vya afya 898 na hospitali 96 zimepatiwa
huduma ya umeme katika maeneo mbalimbali
nchini. Aidha, wakala kwa kushirikiana na
TAZAMA pipeline na Mfuko wa Maendeleo
wa Mafia umewezesha utekelezaji wa
miradi miwili ya kupeleka umeme katika
pampu za kusukuma maji na mafuta za
TAZAMA zilizoko Kisanga (Morogoro).
Akizungumzia mafunzo yanayofadhiliwa na
wakala kwa wananchi, Meneja wa Tathmini na
Ufuatiliaji wa REA , Bw. Vestina Rwelengera
alisema kwamba ni pamoja na kuwapatia
mafunzo yote ya nishati, mfano utunzaji wa
vyakula kwa kutumia nishati ya jua, miradi ya
umwagiliaji, kukausha samaki na mboga mboga.

Moja ya njia kuu kubwa za kusambaza umeme

Alitaja maeneo yaliyonufaika na na mafunzo


hayo kuwa ni Bagamoyo, Mafia na Somanga
Fungu ambapo wananchi walipata mafunzo
ya kutengeneza mkaa kwa kutumia majani
makavu. Pia
wakala kupitia mfuko wa
Nishati Vijijini, ulitoa ruzuku kwa vikundi
vinavyotayarisha maandiko ya miradi ili
kuwawezesha wanavijiji kupata mikopo kutoka
kwenye benki zilizokubaliana na Mfuko huo.
Akizungumzia miradi mingine iliyotekelezwa
na inayoendelea kutekelezwa ya usambazaji wa
umeme vijijini ndugu Vestina aliema kwamba
ni pamoja na mradi wa SAGCOT Cluster ambao
utasambaza umeme kilometa 100 , kujenga
kituo cha kupozea umeme katika mji wa Ifakara
na mradi huu utaunganisha wateja 3,000.
Miradi mingine ni ya Andoya (Mbinga),
Tulila (Songea), Yovi (Kilosa), ambayo
imeanza uzalishaji. Miradi ya Maguta (Kilolo),
Lupali (Njombe), na Isigula (Ludewa)

23

Baadhi ya Mafundi wa Shirika la Ugavi Umeme Tanzania (Tanesco)


wakisimika nguzo ya umeme.

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

2016

Juhudi za Serikali katika kuboresha


huduma ya Afya Nchini
Na Benedict Liwenga

ama ilivyo kwa nchi nyingi zinazoendelea,


huduma ya afya nchini Tanzania
inakabiliwa na changamoto mbalimbali jambo
ambalo wananchi wamekuwa wakiilalamikia
Serikali
kwa
kushindwa
kuboresha
miundombinu na utendaji kazi katika Sekta
ya afya ili iweze kutoa huduma bora zaidi.
Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na
uchache wa majengo yaliyo bora, madaktari
na wauguzi, madawa, vitendea kazi na
utendaji usioridhisha. Aidha, hali mbaya
ya mazingira ya maeneo ya hospitali,
zahanati na vituo vya afya yameelezwa
kuwa ni sehemu ya changamoto hizo.
Inafahamika kwamba, huduma nzuri ya afya
inaanzia na ubora wa hospitali, zahanati au kituo
cha afya, namna mgonjwa anavyopokelewa
na kuhudumiwa na wauguzi pamoja na
waganga na hatimaye kupatiwa dawa. Aidha,
mgonjwa anapotakiwa kulazwa anahitaji
kulala kwenye kitanda chenye shuka nzuri
na huduma ya vyoo na maji safi zinakuwepo.
Kutokana na hospitali, zahanati na vituo
vingi vya afya nchini kushindwa kutoa
huduma bora kwa wagonjwa, kumekuwepo
na malalamiko kutoka kwa wananchi wakidai
kwamba wagonjwa wengi wamekuwa
wakipoteza maisha kutokana na uzembe
wakiwa katika harakati za kupatiwa matibabu.
Rais wa Awamu ya Tano ya Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli ameonyesha kukerwa na tatizo la
huduma mbaya ya afya inayotolewa katika
hospitali, zahanati na vituo vya afya hapa nchini.
Katika jitihada za kulitafutia ufumbuzi
tatizo hili Dkt. Magufuli alifanya ziara ya
kushitukiza katika hospitali ya Rufaa ya
Muhimbili ili kujionea hali halisi ya huduma
ya afya inavyotolewa hospitalini hapo.
Kufuatia ziara hiyo Dkt. Magufuli alionyesha
hali ya kutoridhishwa na utendaji kazi
wa hospitali na hivyo aliamua kuivunja
Bodi iliyokuwa ikisimamia hospitali hiyo.
Baadhi ya wagonjwa walimwambia Dkt.
Magufuli kwamba wamekuwepo hospitalini
hapo kwa muda mrefu wakisubri vipimo
vinavyotumia mashine za MRI na CTScan ambazo zilikuwa hazifanyi kazi huku
wengi wao wakichangia kulala zaidi ya
wagonjwa wawili katika kitanda kimoja.

24

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
(katikati) akipokea vitanda vya vya wagonjwa pamoja na shuka ambavyo vilitolewa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kama
alivyoahidi siku alipozungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam Februari 13, 2016.
Kwa kutambua umuhimu wa huduma ya
afya kwa wananchi ambao ndio wanaotakiwa
kufanya kazi ili kujiletea maendeleo yao
na ya nchi kwa ujumla, Dkt. Magufuli
akiwa mjini Dodoma aliagiza zichukuliwe
fedha kiasi cha Shilingi Milioni 210 kati ya
Shilingi Milioni 225 zilizokuwa zimetengwa
kufanikisha hafla iliyokuwa imeandaliwa
kwa ajili ya Wabunge wapya zipelekwe
Hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kununulia
vitanda na magodoro ya kulalia wagonjwa.
Dkt. Magufuli alisisitiza kuwa kwa
kufanya hivyo tutakua tumejinyima sisi
wenyewe lakini tutakua tumewanufaisha

Nilipoambiwa
kwamba Shilingi
Milioni 225
zimetengwa kwa ajili
ya sherehe, nikasema
fedha hizo zipelekwe
katika hospitali ya
Taifa Muhimbili
zikasaidie kununua
vitanda

wenzetu ambao wana matatizo makubwa


yanayoweza kutatuliwa kwa fedha hizo.
Ili kuhakikisha kuwa agizo hilo linatekelezwa
ipasavyo, fedha hizo ziliweza kutumika
kununulia vitanda 300 pamoja na magodoro
yake, shuka 600, baiskeli za kubebea wagonjwa
pamoja na vifaa vingine ambavyo vilipelekwa
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Sambamba na uboreshaji wa huduma ya
afya katika hospitali, zahanati na vituo
vya afya nchini, Dkt. Magufuli aliiagiza
Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kuhakikisha
inafungua maduka ya madawa katika
hospitali ili wagonjwa waweze kununua
pale watakapoekezwa kufanya hivyo.

Mashine ya CT-Scan iliyonunuliwa na


Serikali ambayo kwa sasa inatumika
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Inaendelea Uk. 25

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

2016

Inatoka Uk. 24
kwa Watanzania kutokana na kasi ya ufanyaji
kazi kwa mashine hiyo kwani ina uwezo wa
kupima kifua na tumbo kwa muda mfupi.
Mashine ya CT-Scan ambayo imefungwa
ina ubora mkubwa na ni ya pili kwa ukubwa
Afrika Mashariki. Kwa sasa tunategemea
kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kutokana
na uwezo uliyonayo na inaweza kufanya
kazi kwa kasi tofauti na mashine iliyokuwa
inatumika hapo awali, alisema Dkt. Flora.
Akielezea zaidi juu ya mashine hizo mpya

Wagonjwa wakiwa wamelala mara baada ya kufungwa kwa vitanda katika


Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
kufanya kazi kwa bidii na kuifanya ionekane
yenye hadhi ya kuwa hospitali ya Taifa.
Kama tunaweza kuwa na huduma nzuri
katika daraja la kwanza (first class) tunaweza
kuwavuta wananchi wengi waje hapa na
waache kwenda hospitali binafsi. Wanatakiwa
kutengewa madaraja ya juu ambayo
huduma zake zinakuwa zimeboreshwa sio
mtu anakuwa daraja la kwanza alafu bado
anachangia choo na wengine au anaye lala
nae hapewi kitanda, alisema Kingwangalla.

Mafundi wakiendelea kufunga vitanda


vilivyotolewa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Magufuli.
Kutokana na kasi ya utendaji wa Serikali
ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Dkt.
Magufuli, Mawaziri na Naibu Mawaziri
wamelazimika kufuata nyanyo zake. Januari
4, 2016 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.
Dkt. Hamisi Kingwangalla naye alifanya
ziara katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mkuu wa Idara ya Mionzi katika hospitali


hiyo, Dkt. Flora Rwakatare ameeleza kuwa,
tangu kuanza kutumika kwa mashine ya
MRI jumla ya wagonjwa 560 walifanyiwa
vipimo ambapo ndani ya siku tatu baada
ya mashine mpya ya CT-Scan kufungwa
jumla ya wagonjwa 26 walipimwa.
Kufungwa kwa mashine ya CT-Scan
kunaonekana kuwepo kwa matumaini mapya

25

Dkt. Flora emesema, zina uwezo mkubwa


wa kupima viungo vya ndani kama moyo,
utumbo, ubongo na kutoa majibu sahihi
ya chunguzi na kwa haraka zaidi. Kati
ya Novemba 26, 2015 hadi Februari 9,
2016 imepima jumla ya wagonjwa 863.
Wakati huo huo, kufuatia agizo la Rais
Magufuli la kuitaka Bohari Kuu ya Madawa
(MSD) kufungua maduka kwenye maeneo ya
hospitali na vituo vya afya nchini, Mkurugenzi
Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu
alibainisha kuwa hadi sasa MSD tayari
imefungua maduka manne katika mikoa ya
Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Mbeya.
Aliongeza kuwas, MSD inafanya mawasiliano
na mikoa mingine ili iweze kufungua
maduka ya dawa katika hospitali, zahanati
na vituo vya afya ambapo MSD itakuwa
inawauzia dawa na kuwawezesha kitaalamu
namna ya kuendesha maduka hayo. Hadi
sasa MSD tayari imefanya mazungumzo
na viongozi wa mikoa ya Ruvuma, Rukwa,
Singida, Dodoma, Geita, Kagera na Iringa.

Baadhi ya idara ambazo, Dkt. Kingwangalla


alitembelea ni pamoja na Kitengo cha dharura,
Chumba cha wagonjwa Mahututi (ICU), Wodi
ya Mwaisela, Duka la dawa la MSD na kukagua
ufanyaji wa kazi wa mashine ya CT-Scan na MRI.
Katika ziara hiyo, Dkt. Kingwangalla
alifurahishwa na mabadiliko ya utoaji wa
huduma katika upimaji kwa kutumia mashine
ya Computerized Tomography Scan (CTScan) na Magnetic Resonance Imaging
(MRI) ambazo awali zilikuwa hazifanyi
kazi. Aliwataka watumishi wa hospitali hiyo

Muuguzi akimfunika mgonjwa kama


inavyoonekana mara baada ya kufungwa vitanda hivyo.

Muuguzi akipandisha Kitanda ili


kiweze kuanza kutumika na mgonjwa.

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

2016

Maadili ni msingi wa uwajibikaji katika


utumishi wa Umma
Na Anitha Jonas

angu enzi za Azimio la Arusha,


suala
la
maadili
limekuwa
likisisitizwa kama kijenzi muhimu cha
ufanisi katika utoaji wa huduma kwa
umma. Lengo lilikuwa ni kuhakakisha
kwamba kila Mtumishi wa Umma
anatekeleza wajibu wake kwa kufuata
sheria, kanuni na miongozo iliyowekwa.
Kutofanikiwa kwa Azimio la Arusha
kulitokana na baadhi ya Viongozi
kujua kwamba utekelezaji wa malengo
ya azimio hilo ungekwamisha nia ovu
waliyokuwanayo kama Watumishi wa
Umma katika kuwahudumia wananchi.
Ndio maana juhudi ya Hayati Baba
wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere za kutaka azimio hilo
liungwe mkono hazikuzaa matunda.
Pamoja na kuwepo sheria, kanuni,
miongozo na mikakati ya kukuza
maadili kwa watumishi wa Sekta ya
Umma na watu binafsi, wananchi bado
wamekuwa
wakilalamika
kuwepo
urasimu usio wa lazima wenye lengo
la kutengeneza mazingira ya rushwa
na huduma zisizoridhisha. Aidha,
wapo baadhi ya wafanyabishara binafsi
wasiozingatia maadili na hata kufikia
hatua ya kuchochea utoaji wa rushwa
au kuzalisha bidhaa zisizo na viwango.
Katika jitihada za kuhakikisha kwamba
Watumishi wa Umma wanakuwa
waadilifu na wanafuata maadili mema,
Serikali ya Awamu ya Nne chini ya
Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete
ilibuni mikakati ya kuwa na utaratibu
mpya kwa viongozi na watumishi wa
Sekta za Umma na Binafsi kusaini
Ahadi ya Uadilifu (Integrity Pledge).
Ahadi ya Uadilifu ni tamko rasmi na
bayana la dhamira ya kuwa na mwenendo
wa kimaadili na kuunga mkono kampeni ya
kitaifa ya maadili na mapambano dhidi ya

26

rushwa. Kwa kusaini tamko hilo, mhusika


au taasisi inakuwa imejipambanua
kwa umma kuwa haitajiingiza katika
masuala yasiyo ya kimaadili katika utoaji
huduma na uendeshaji wa biashara.
Kwa mujibu wa Kamishina wa Maadili
Mhe.Jaji Salome Kaganda, alisema kuna
aina tatu za Hati za Ahadi ya Uadilifu yaani;
Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma,
Watumishi wa Umma na Sekta Binafsi ili
kila kundi liwajibike kwa namna yake.
Akizindua Hati za Uadilifu mwezi agosti
2015, Rais Mstaafu Kikwete alisema,
kuwepo kwa hati hizo ni hatua kubwa
muhimu na ya kihistoria katika safari ya
kuboresha na kuhuisha mifumo ya uadilifu
iliyopo ili iweze kwenda sambamba
na mazingira na nyakati zilizopo.
Dkt.
Kikwete
hakusita
kuelezea
chimbuko la Hati ya Madili kwa kusema,
kwa muda mrefu kumekuwepo na
changamoto kubwa katika kupambana
na rushwa kama moja ya tatizo
kubwa la utovu wa uadilifu nchini.
Tumechukua hatua kadhaa ikiwemo
kutengeneza Mkakati wa Mapambano
Dhidi ya Rushwa na mabadiliko katika
Sheria ambayo ilisaidia kuanzishwa kwa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU). Tumepata mafanikio
makubwa na ya kutia moyo ingawa bado
zipo changamoto na manunguniko
ambayo
hatuwezi
kuyapuuza.
Dkt. Kikwete alifafanua kuwa, kwa
madhumuni ya kuyaongezea mapambano
haya nguvu na kasi, Serikali iliamua
Mpango wa Mapambano dhidi ya Rushwa
uingizwe katika Mpango wa Tekeleza kwa
Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ili kutoa
msukumo wa pekee katika utekelezaji wake.
Akielezea juu ya Mpango wa Tekeleza
kwa Matokeo Makubwa Sasa (BRN),
Mkurugenzi Mtendaji wa BRN Bw.
Omari Issa alisema kwamba Ahadi ya

Uadilifu ni moja ya maeneo 12 yaliyo


katika Mpango wa Mapambano dhidi ya
Rushwa chini ya Mpango wa Tekeleza
kwa Matokeo Makubwa sasa (BRN).
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji
huyo, alisema matokeo ya utafiti
uliofanywa katika kutekeleza mpango huo
imeonekana kwamba moja ya changamoto
iliyoonekana katika eneo la utoaji
huduma na uendeshaji biashara nchini
ni tatizo la rushwa na utovu wa maadili
katika taasisi za umma na binafsi. Hivyo
kulikuwa na haja ya kuweka mikakati
ya uwajibikaji na kufuata maadili katika
Utumishi wa Umma na Sekta Binafsi.
Katika kuweka msisistizo wa suala la
maadili na uwajibikaji kwa Watumishi
wa Umma, Rais wa Awamu ya Tano
Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli alitoa
agizo kwa watumishi wote wa umma
kujaza Hati ya Ahadi ya Uadilifu
(Integrity Pledge) ambayo imeeleza
wazi masharti ya namna Mtumishi
wa Umma anavyopaswa kufanya kazi.
Lengo ni kusaidia kukuza maadili na
mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa
katika Sekta ya Umma na Binafsi kwa kuwa
ahadi au tamko hilo linashawishi viongozi,
Watumishi wa Umma na kampuni binafsi
kuwa tayari kufanya kazi kwa kufuata
misingi ya maadili na kupambana
na rushwa kwa hiari yao wenyewe.
Akiunga mkono juhudi za Dkt.
Magufuli katika kusimamia nidhamu
kwa Watumishi wa Umma, aliyekuwa
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni
Sefue alisema kwamba Hati ya Uadilifu
(Integrity Pledge) itakuwa chachu ya
harakati za kukuza uadilifu na mapambano
dhidi ya rushwa nchini. Ahadi ya
uadilifu itaweka kauli thabiti ya kimaadili
ambayo itaonyesha nia ya kutekeleza
majukumu ya viongozi na watumishi
wa
umma, alisisitiza Balozi Sefue.
Alifafanua kuwa, ujazaji wa hati hiyo

Inaendelea Uk. 27

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

Inatoka Uk. 26
utakuza utamaduni wa viongozi,
watumishi wa umma na sekta binafsi
kwa ujumla kuwa tayari kufanya kazi
kwa kufuata misingi ya maadili na
kupambana na rushwa kwa hiari yao.
Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Utumishi na Utawala Bora Bi.
Angela Kairuki alisema kwamba
mtumishi
wa
umma
anatakiwa
kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu
na uadilifu bila kutoka nje ya mstari.
Mara baada ya kuapishwa kuwa Mkuu
wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri
alisema atasimamia ipasavyo maadili
ya utumishi wa umma hususan katika
kutekeleza miradi ya maendeleo
katika mkoa wake huku akiahidi
kuwawajibisha watumishi watakaokiuka
maadili ya utumishi wa umma.
Tangu achaguliwe kuwa Rais wa
Serikali ya Awamu ya Tano, Dkt. John
Pombe Magufuli amewachukulia hatua
baadhi ya viongozi wa umma kwa
kushindwa kusimamia utekelezaji wa
majukumu waliyopewa. Viongozi hao
ni pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara
ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka,
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari,
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mapato,
Mkurugenzi wa Vitambulisho vya
Taifa na Mkurugenzi wa Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa.

Serikali kutoa Hati ya Tanzania kuzalisha


Kumiliki
umeme unaotumia
Ardhi ndani ya mwezi jotoardhi
mmoja
Inatoka Uk. 10
maamuzi yake yatokane na Mkutano Mkuu
wa kijiji utakaosimamiwa na Mkuu wa Wilaya.
Vile vile, lazima kuwepo na kumbukumbu
za barua ya Mkuu wa Wilaya pamoja
na muhutasari wa Mkutano wa Kijiji
uliosainiwa na kila mtu aliyehudhuria
mkutano huo akiwa na akili timamu.
Katika hotuba yake ya kufungua rasmi Bunge
jipya la 11 la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Novemba 20, 2015 mjini Dodoma,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alisema
kuwa wakati wa kampeni yake, wananchi
wamelalamikia juu ya kuendelea kuwepo
kwa migogoro ya wakulima na wafugaji,
viwanja, kuhodhi maeneo bila kuyaendeleza,
mipango miji na ujenzi katika maeneo ya wazi.
Dkt. Magufuli aliahidi kuwa atashughulikia
kwa nguvu zake zote kuhakikisha kuwa
matatizo hayo yanapatiwa ufumbuzi.

Waziri wa Ardhi na Maendeleo


ya Makazi, Mhe. William Lukuvi
akikagua nyumba za Shirika la Nyumba
la Taifa (NHC) Ubungo.

27

2016

Na Lilian Lundo

anzania ina hifadhi kubwa ya


rasilimali ya Jotoardhi (Geothermal
energy) inayokadiriwa kuwa zaidi ya
megawati 5000 (Mwt), hivyo kuweza
kuzalisha nishati ya umeme kwa
matumizi mbalimbali hapa nchini.
Japokuwa teknolojia ya matumizi
ya rasilimali ya Jotoardhi sio ngeni
duniani, ni nchi chache zilizofanikiwa
kuzalisha nishati ya umeme kwa kutumia
rasilimali hiyo. Jumla ya nchi 21 tu
ikiwemo Marekani zinatumia rasilimali
hiyo kuzalisha nishati ya umeme.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mipango
na Maendeleo ya Biashara wa Kampuni
ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania
(TGDC) Mhandisi Kato Kabaka, alisema
rasilimali hiyo inayotokana na mvuke
wa maji ulio chini ya ardhi inapatikana
pia maeneo ya bonde la ufa (Rift Valley)
na baadhi ya maeneo hapa nchini.
Mhandisi Kabaka, aliyataja maeneo yenye
viashiria vya kuwepo kwa jotoardhi
kuwa ni Ziwa Manyara, Ngorongoro,
Natron, Majimoto Mara, Utete (Pwani),
Kisaki (Morogoro), Luhoi (Pwani),
Ibadakuli
(Shinyanga),
Mtagata
(Kagera), Dodoma, Singida na Tanga.
Amefafanua kuwa, utafiti uliofanyika
unaonyesha kuwa viashiria vingi
vinaonyesha uwepo wa rasilimali ya
jotoardhi katika maeneo ya vijijini
ambako
umeme
bado
haujafika.
Ili kuhakikisha rasilimali hii inaanza
kutumika mapema iwezekanavyo Serikali
ya Tanzania kupitia Shirika la Usambazaji
Umeme Nchini (TANESCO) imesajili
Kampuni ijulikanayo kwa jina la Tanzania
Geothermal Development Company
Limited (TGDC) ambayo ilianza kufanya
kazi Julai, 2014 ili kuendeleza nishati hiyo
huku ikipewa jukumu la kuharakisha
uendelezaji wa nishati ya Jotoardhi nchini.

Inaendelea Uk.28

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

Inatoka Uk. 27
Kampuni imekuwa ikitoa elimu juu ya
faida zitokanazo na nishati ya Jotoardhi
na namna ambavyo nishati hiyo itatoa
fursa kwa wananchi waliopo katika
maeneo ambayo nishati ya jotoardhi
inapatikana pamoja na kuwafanya
wananchi wa maeneo husika kujiona
kuwa na wao ni wamiliki wa miradi
hiyo na sio Serikali peke yake.
Katika mikutano ya uelimishaji juu ya
nishati ya jotoardhi mkoani Morogoro
katika kata ya Kisaki, Mhandisi Kato
Kabaka
aliainisha
fursa
ambazo
wananchi
wa
Kisaki
watazipata.
Alisema wananchi watanufaika na nishati
ya umeme yenye gharama nafuu na yenye
uhakika ukilinganisha na nishati nyingine
ambazo zinategemea maji, mafuta au
gesi ambazo ni ghali na hazina uhakika
kutokana na vyanzo vyake kupungua
au kuisha kabisa baada ya muda fulani.
Nishati
hiyo
pia
inatumika
katika
ufugaji
wa
samaki
kwa
kutumia joto
lizalishwalo
na nishati
y
a
jotoardhi,
s a m a k i
wanakua vizuri
na kuzaliana kwa
wingi katika joto
lisilopungua nyuzi
joto30. Hivyo kwa
kutumia nishati hiyo mfugaji anaweza
kurekebisha joto ndani ya mabwawa kufikia
nyuzi joto 30 kwa kutumia mabomba
ambayo yatakuwa yanapitisha maji moto
ambayo yanakuwa ndani ya mabwawa.
Hivyo basi, uzalishaji wa samaki
unavyokuwa
mkubwa
ndivyo
mwananchi anavyopata fursa ya
kuongeza kipato chake kwa kuuza samaki
ndani na nje ya mkoa na kuongeza kipato
chake pamoja na kuingizia Serikali
fedha kupitia ushuru ambao atakuwa
akilipa katika uuzaji wa samaki hao.

28

Mhandisi Kabaka alitaja faida nyingine


itokanayo na nishati ya jotoardhi ni
uhifadhi wa chakula na mbogamboga kwa
kutumia nishati hiyo. Nishati ya jotoardhi
inaweza kutumika kukausha mazao ya
nafaka au mbogamboga hata kipindi cha
baridi na mvua kwa kupitisha mabomba
ambayo yana maji moto ndani ya chumba
chenye mazao ya nafaka au mbogamboga.
Ikiwa mikoa ambayo inaviashiria
vya nishati ya Jotoardhi itaitumia
vizuri nishati hiyo katika ukaushaji
wa vyakula basi wananchi watasahau
kabisa juu ya janga la njaa katika mikoa
yao. Hii inatokana na kuwa chakula
kilichokaushwa hudumu kwa muda mrefu
bila kuharibika hivyo nishati hiyo itasaidia
utunzaji kwa vyakula kama mbogamboga
ambazo huaribika ndani ya muda mfupi.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo ameiagiza TGDC
kuwa ifikapo June, 2016 iwe imeanza
kuchoronga mashimo kwa ajili ya
uzalishaji wa umeme utokanao
na nishati hiyo kwani
utafiti umekamilika
na joto la maji
ni kubwa
ambalo
n i

230-250C.
Prof. Muhongo amesema Tanzania
haijazalisha hata megawati moja ya nishati
ya jotoardhi wakati Kenya na Ethiopia
wamepiga hatua kubwa katika matumizi
na fursa zitokanazo na nishati hiyo.
Hadi kufikia mwezi Mei mwaka 2014,
Tanzania ilikuwa inategemea uzalishaji
wa umeme kutumia maji kwa asilimia 35,
gesi asilimia 34 na mafuta mzito asilimia
31. TGDC imejipanga kuzalisha megawati
200 (Mwt) za umeme ifikapo mwaka
2020, megawati 500 ifikapo mwaka 2025
na megawati 800 ifikapo mwaka 2033.
Nishati ya Jotoardhi ni nishati ya
uhakika,
inapowashwa
kuzima
kwake kutategemea na urekebishaji
wa mitambo na si kwa sababu ya
kupungua nguvu kwa nishati hiyo.
Mitambo ya kwanza ya Jotoardhi Duniani
ilijengwa katika mji wa Larderello uliopo
Italy mnamo mwaka1911. Mpaka leo
mitambo hiyo
inaendelea
ku z a l i s h a
nishati ya

kilichozalishwa

Watafiti wa nishati ya Jotoardhi wakiwa


kazini katika maeneo yenye viashiria.

2016

umeme
k
w
a
kiwango
k i l e k i l e
mwaka
1911.

Inaendelea Uk. 29

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

2016

Mchango wa barabara katika


kuinua uchumi wa Taifa

Inatoka Uk. 28

Na Beatrice Lyimo na Lorietha Lawrence

Watafiti wa nishati ya Jotoardhi wakiwa


katika moja ya eneo lenye kiashiria cha
nishati ya jotoardhi.

Muonekano wa barabara za jijini Dar es Salaam.

Meneja Shirika la Uendelezaji Jotoardhi


(TGDC). Mhandisi Boniface Njombe
(aliyesimama mbele) akiwaelimisha
wanakijiji mkoani Mbeya kuhusu
umuhimu wa nishati ya jotoardhi kwa
Taifa na wananchi.

atika nchi yeyote ile duniani


miundombinu
ya
barabara
ina mchango mkubwa sana katika
kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi
wa Taifa na maendeleo ya jamii.
Miundombinu
imara
inapunguza
gharama ya usafiri na usafirishaji, inavutia
uwekezaji wa sekta binafsi, utoaji wa
huduma za kijamii, inaunganisha masoko
na kusaidia kuendeleza maisha bora
kupitia mgawanyo bora wa rasilimali.
Vile vile, miundombinu bora inachangia
katika kuongeza mchango wa nyenzo
kuu za uzalishaji mali kwa kuongeza
tija ya nguvukazi na mitaji, kukuza
uzalishaji, faida, mapato na ajira.

Baadhi ya Watendaji wa Shirika la


Uendelezaji Nishati ya Jotoardhi
pamoja na wadau mbalimbali wakiwa
katika moja ya mikutano kujadili
namna ya kuanza utafutaji wa nishati
ya jotoardhi mkoani Mbeya baada
ya tafiti nyingi kufanyika hapo awali
mkoani humo.

29

Inaendelea Uk. 33

Hivyo
basi
Serikali
ni
lazima
ihakikishe
kwamba
miundombinu
ya
barabara
inaimarika.
Kabla hajawa Rais wa Serikali ya Awamu
ya Tano ya Jamhuri ya Mungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli amewahi kuwa Waziri mwenye
dhamana ya masuala yanayohusu Ujenzi,
Mawasiliano na Uchukuzi. Katika kipindi
hicho alisimamia kwa karibu ujenzi wa

miundombinu ya barabara hapa nchini.


Alifanya hivyo kwa kutambua mchango
wa barabara katika kuinua uchumi wa
nchi na maendeleo ya watu wake. Dkt.
Magufuli ameweza kusimamia ujenzi wa
barabara zenye urefu wa kilometa 17,700.
Akifungua rasmi Bunge jipya la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Oktoba 20,
2016 mjini Dodoma, Dkt. John Magufuli
alisema Serikali ya Awamu ya Tano
inaingia madarakani kukiwa na msingi
imara wa kiuchumi uliojengwa katika
Awamu zilizopita. Aliongeza kuwa,
uchumi wa nchi umekuwa ukiimarika
na kukua kwa wastani wa asilimia
7. Fursa mbalimbali za kiuchumi
zilizopo nchini zimezidi kufunguliwa.
Dkt.
Magufuli
alieleza
kwamba
mafanikio haya yametokana na ujenzi
wa miundombinu ya kiuchumi kama
vile barabara, uimarishaji wa bandari,
uimarishaji wa reli, ukuzaji wa sekta za
mawasiliano ya simu na mitandao, ukuzaji
na uongezaji wa uwezo wa kuzalisha
na kusambaza umeme. Alieleleza kuwa
Serikali ya Awamu ya Tano itaendeleza
na kuimarisha ujenzi wa miundombinu
mipya na kuiimarisha iliyopo ili kuvutia na
kushawishi wawekezaji wa ndani na wa nje.

Inaendelea Uk. 30

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

Inatoka Uk. 29
Alifafanua kwamba, miongoni mwa ahadi
alizowaahidi Watanzania ni kuendeleza
ujenzi wa barabara mbalimbali za
kuunganisha miji mikuu ya mikoa na
wilaya; barabara ziendazo kwenye maeneo
muhimu ya kimkakati na kiuchumi;
na upanuaji wa barabara za miji kama
Dar es Salaam kwa kujenga (flyovers),
barabara za pete (ring roads), n.k. Hivyo,
uboreshaji wa barabara na njia nyingine za
uchukuzi na usafirishaji kuingia na kutoka
Dar es Salaam ni muhimu kwa sababu
bandari ya Dar es salaam ni lango kuu
la biashara kwa Tanzania na nchi jirani.
Novemba 30 mwaka jana, Rais Dkt.
John Pombe Magufuli aliagiza kwamba
fedha ambazo zilitengwa kwa ajili ya
sherehe za maadhimisho ya siku ya
Uhuru zinayofanyika ifikapo Desemba
9, kila mwaka, zisitumike kwa shughuli
hiyo. Badala yake alizielekeza fedha hizo
zitumike kwenye ujenzi/upanuzi wa
barabara ya kutoka Moroco hadi Mwenge
jijini Dar es salaam yenye urefu wa kilometa
4.3. Barabara hiyo sasa itakuwa na njia nne
na itaunganisha na ile inayoanzia Mwenge
hadi Tegeta yenye urefu wa Km 12 ambayo
ujenzi wake ulikamilika mwaka 2014.
Uamuzi wa Mhe. Rais ulilenga katika
kuhakikisha kwamba barabara hiyo

ambayo tayari ilikuwa kwenye mipango


ya kujengwa/kupanuliwa na Serikali
kwa gharama ya shilingi Bilioni nne,
inakamilika ili kupunguza msongamano
wa magari na muda mwingi wanaoupoteza
wananchi kwenye foleni wanapoelekea
kwenye shughuli za kijamii na kibiashara
kupitia barabara hiyo. Kwa mujibu wa tafiti
zilizotolewa na Ofisi ya Taifa yaTakwimu
(NBS) ya mwaka 2013, kiasi cha Shilingi
Bilioni 411.55 zilikuwa zikipotea
kutokana na foleni za magari barabarani.
Aidha, Rais Magufuli aliweka jiwe la
msingi la mradi wa ujenzi wa barabara ya
juu (Flyover) katika makutano ya barabara
ya Nyerere na Mandela, eneo la Tazara
jijini Dar Es Salaam ambao utagharamu
kiasi cha takribani Shilingi Bilioni 100.
Kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni 93.44
zitatolewa na Serikali ya Japan kupitia
Shirika lake la Ushirikiano wa Kimataifa
(JICA) na Serikali ya Tanzania itatoa
Shilingi Bilioni 18.3 ambapo ujenzi wake
unatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba
2018. Barabara hiyo itakuwa na njia nne
zenye urefu wa Mita 300 zikitokea katikati
ya jiji la Dar Es Salaam kuelekea Uwanja
wa Kimataifa wa Mwl. Julius K. Nyerere.
Vile vile, Rais Magufuli alizindua daraja

2016

jipya la Kigamboni lenye urefu wa Mita


680 likiwa na jumla ya barabara 6. Kati ya
hizo barabara tatu zinaelekea kigamboni
na nyingine nikielekea katikati ya jiji.
Katika daraja hilo zimetengwa njia za
waenda kwa miguu zikiwa na upana
wa mita 2.5 kila upande. Gharama
ya ujenzi wa daraja hilo ni Dola za
Kmarekani Milioni 135 ambapo asilimia
25 inalipwa kwa fedha Kitanzania
na asilimia 75 kwa fedha za kigeni.
Asilimia 60 ya gharama ya ujenzi wa
daraja hilo imetolewa na Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati
asilimia 40 imetolewa na Serikali.
Gharama nyingine ambazo NSSF
imetumia katika katika mradi huo
ni Shilingi Bilioni 1.61 kwa ajili ya
upembuzi wa awali na upembuzi yakinifu.
Shilingi Bilioni 13.99 ni gharama za
kufidia fidia kwa niaba ya Serikali na
fedha nyingine ambazo ni Shilingi Milioni
525.72 zilikuwa ni gharama kwa ajili ya
Mtaalamu Mwelekezi na fedha mnyingine
Shilingi Bilioni 11.633 ilikuwa ni kwa ajili
ya Mtaalamu Mshauri. Shilingi Milioni
284.5 zilikuwa kwa ajili ya usimamizi
unaofanywa na Wataalamu kutoka
wizara ya Ujenzi,TANROADS na NSSF.
Aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi wakati wa
Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Harrison
Mwakyembe (MB) alisema kwamba

Dara la Mto Malagarasi


(Daraja la Kikwete) lililojengwa kwa
msaada wa Serikali ya Korea likionekana
katika picha. Daraja hili liliwekwa jiwe
la Msingi na Rais Mstaafu wa Awamu ya
Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
mwaka 2011.

Daraja la Umoja(Mtambaswala)
linalounganisha nchi ya
Tanzania na Msumbiji.

Daraja la Umoja(Mtambaswala)
linalounganisha nchi ya
Tanzania na Msumbiji.

30

Inaendelea Uk. 31

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

2016

Inatoka Uk. 30

Moja ya baadhi ya barabara za Tanzania kama inavyoonekana ikiwa imewekwa lami, jambo ambalo linarahisisha
usafiri kwa wananchi kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Sekta ya usafiri na uchukuzi kwa njia
ya barabara imeendelea kuimarika na
kutoa mchango wake katika kutekeleza
shughuli za kiuchumi, kijamii na
kimaendeleo. Hii inatokana na ukweli
kwamba sekta hii imeendelea kuhudumia
zaidi ya asilimia 90 ya mizigo yote
inayosafirishwa nchini ikiwa ni pamoja
na ile inayopitia katika bandari zetu.
Mwakyembe ambaye sasa ni Waziri
wa Sheria na Katiba alieleza kuwa
huduma za usafirishaji kwa njia ya
barabara
zimeendelea
kuimarika
ambapo katika kipindi cha Julai, 2013
hadi Machi, 2014 jumla ya leseni za
malori 47,571 zilitolewa ikilinganishwa
na leseni 44,143 zilizotolewa katika
kipindi kama hicho mwaka 2012/2013.
Aidha, leseni za mabasi 32,387 zilitolewa
katika kipindi hiki ikilinganishwa
na leseni 25,196 zilizotolewa katika
kipindi kama hicho mwaka 2012/2013.
Hata hivyo katika kipindi cha Julai,
2014 hadi Aprili, 2015, mchango wa
sekta binafsi katika ukuaji wa Sekta ya
Usafiri na Uchukuzi kwa njia ya barabara
umeendelea kuongezeka, SUMATRA
ilitoa leseni za usafirishaji 33,415
kwa magari ya mizigo na leseni za
usafirishaji 22,810 kwa magari ya
abiria ongezeko hili ni asilimia 6.6.

31

Waziri wa Uchukuzi wa Serikali ya Awamu


ya Tano Profesa Makame Mbarawa
alisema kwamba Serikali inaendelea na
jitihada za kuhakikisha mikoa mingi
nchini inaunganishwa kwa miundombinu
ya barabara. alifafanua kuwa hivi sasa
barabara zinajengwa sehemu mbalimbali
ikiwa ni pamoja na Magore hadi Turiani
kwa gharama ya Dora za Kimarekani laki
735 na Shilingi za Kitanzania zaidi ya
Milioni 795. Barabara nyingine ni kutoka
Mangaka hadi Mtambaswala yenye
urefu wa Km 62.7, Mangaka-Nakapanya
Km 70.5 na Buliamba-Kisolya Km 51.
Barabara nyingine zinazojengwa ni
za Tankibovu - Goba (Km 9), Goba
Mbezi Mwisho (Km7), Kimara Baruti
Msewe-Chuo Kikuu (Km2.6), Mbezi
Mw i s h o Ma l amb am aw i l i Ki f u r u Kinyerezi (km14), Tabata Dampo-Kigogo
(Km1.6) na Makutano-Nata-Mto wa
Mbu yenye urefu wa km 467.7ambayo
tayari Serikali imeshalipa fedha shilingi
bilioni 8.5. Barabara hiyo ni sehemu ya
barabara ya Nyamuswa-Bunda-KisolyaNansio yenye urefu wa Km 121.9.
Profesa Mbarawa alisema kwamba,
kukamilika kwa barabara ya NyamuswaBunda-Kisolya hadi Nansio yenye urefu
wa Km 121.9 itasaidia kukuza uchumi
wa Wilaya ya Bunda na Ukerewe

kwa kuwa eneo hilo lina shughuli


nyingi za uchumi zinazotokana na
kilimo, ufugaji na uvuvi wa Samaki.
Wananchi wengi wa jiji la Dar Es Salaam
na sehemu nyingine nchini walipokea
kwa furaha uamuzi wa Rais Magufuli wa
kuamuru fedha zilizokuwa zimepangwa
kugharamia sherehe za maadhimisho
ya Siku ya Uhuru Desemba 9 zitumike
kwa ajili ya ujenzi /upanuzi wa barabara
ya kutoka Morocco hadi Mwenge.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti
wananchi hao walisema, ugumu wa
mawasiliano kati ya eneo moja na
jingine kunazorotesha utendaji wa kazi
kama ni kibiashara au za kijamii. Hivyo,
uamuzi huo ni jambo la msingi kwa
kuwa litasaidia kupunguza msongamano
katika barabara hiyo na hivyo kurahisisha
mawasiliano kati ya Mwenge na katikati
ya jiji na pia kuelekea Bagamoyo.
Walifafanua kuwa, miundombinu ya
barabara inawezesha kusafiri kutoka
sehemu moja kwenda nyingine, kwenda
kazini, hospitali, shuleni, viwandani
n.k. Hivyo jukumu la Serikali ni kuona
jitihada kubwa zinafanyika kuhakikisha
kwamba miundhombinu hii inafanya kazi.
Msingi wa kukua kwa uchumi ni
biashara. Watu wanapotaka kufanya

Inaendelea Uk. 32

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni

2016

Inatoka Uk. 31
biashara inawalazimu kusafiri kwenda sehemu

mbalimbali.

Hata wanasiasa wanahitaji barabara kuweza kusafiri maeneo


mbalimbali kukutanana na wananchi na vile vile vyombo vya
usalama pia vinatumia barabara kufanya doria kwa ajili ya usalama
wa wananchi, Alieleza Bw. John Joseph mkazi wa Kinondoni.

Nchi nyingi duniani zina mfumo nzuri wa usafiri ikiwa ni


sehemu ya ulinzi katika jamii na pia unawezesha kuwepo
kwa fursa za ajira kwa mijini na vijijini kwa sababu
inawezesha usafirishaji wa mizigo na huduma katika sekta
zote za kiuchumi zikiwemo wa utalii, elimu, afya na kilimo.

Muonekana wa barabara inayoelekea katika Daraja jipya la Mwalimu Nyerere ambalo limezinduliwa
19 Aprili, 2016 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli

Magari yakipita katika Daraja jipya la Mwalimu Nyerere ambalo limezinduliwa 19 Aprili, 2016 na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Jijini Dar es Salaam.

32

Makala za Habari Maelezo Toleo maalum la Mtandaoni


Inatoka Uk. 29

Mtaalam akiwa na kifaa cha kufanyia utafiti wa jotoardhi kujilikanacho


kama Magnometer

Wataalam kutoka TGDC, GDC pamoja na MEM wakiwa katika majadiliano wakati wa utafiti wa jotoardhi
Mkoani Mbeya.

33

2016

KAMATI YA UHARIRI
Zamaradi Kawawa - Mwenyekiti
Tiganya Vincent - Mjumbe
Jamal Zuber - Mjumbe
Casmir Ndambalilo - Mjumbe
Fabian Rugaimukamu - Mjumbe
Jonas Kamaleki - Mjumbe
John Lukuwi - Mjumbe
MSANIFU JARIDA
Benedict John Liwenga

Vijana ni nguvukazi ya Taifa,


washirikishwe na kuwezeshwa

You might also like