You are on page 1of 1

TAARIFA KWA UMMA

UFAFANUZI JUU YA UVUMI KUHUSU HALI YA MFUKO WA TAIFA WA HIFADHI YA


JAMII (NSSF)
_____________________________

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa mbalimbali zisizo rasmi kuhusu hali na mwenendo wa
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Baadhi ya taarifa hizo zimekuwa zikieleza
kwamba mali za Mfuko huo zimetumiwa vibaya na hivyo kuathiri mafao kwa wanachama.
Taarifa hizi zimesababisha hofu na taharuki miongoni mwa wanachama wa NSSF na wadau
wa Sekta ya Hifadhi ya jamii kwa ujumla kwa kuhofia usalama wa wa fedha na mafao yao.
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) inapenda kuwaondoa
hofu wanachama wote wa Mfuko wa NSSF na Wananchi kwa ujumla na kuwahakikishi
kwamba Mfuko wa NSSF upo katika hali nzuri kifedha na unaendelea kulipa mafao ya
wanachama kama kawaida.

Kama mnavyofahamu, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko

alikwishateuliwa na anaendelea na majukumu ya kusimamia shughuli zote za Mfuko. Vilevile,


taratibu za kupata Bodi mpya ya Wadhamini ya Mfuko huo zipo katika hatua za mwisho.
Aidha, SSRA kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania kwa mamlaka waliyopewa chini ya
Kifungu cha 6(2) (c) cha Sheria Na.8 ya mwaka 2008 ikisomwa pamoja na kifungu cha 40 na
cha 48 wanaendelea kufanya kaguzi za Mifuko yote ukiwemo Mfuko wa NSSF kwa lengo la
kuhakikisha kwamba muda wote Mifuko yote inakuwa katika hali nzuri kwa maslahi ya
wanachama na taifa kwa ujumla.
Mwisho, Mamlaka inapenda kuwaondoa wasiwasi wanachama walioathirika na taarifa hizi
pamoja na wanachama wote wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na kuwahakikishia kwamba fedha
na mafao yao yapo salama na Mamlaka inazifanyia kazi kero zao kwa bidii kubwa.

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano
Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
S.L.P 31846
Tovuti: www.ssra.go.tz
Dar es Salaam
1

You might also like