You are on page 1of 4

Serikali Yaanza Kulipa Deni La Mifuko Ya Hifadhi Ya Jamii

Serikali imevalia njuga swala la deni la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Hadi kufika mwezi
Machi, 2016 tayari Serikali ilikuwa imeshalipa Jumla ya Bilioni 173.11 kwa Mfuko wa
PSPF. Mfuko huo umeweza kulipa Hundi 49,467 ambapo kati ya hizo hundi 46,000 ni
za pensheni za kila mwezi kwa wastaafu na Hundi 3,467 ni za madai mapya ya
Pensheni. Taarifa zinaonesha kwamba Serikali imedhamiria kulipa deni lote la
michango ifikapo June 2016.
Kuhusu hati Fungani (Non cash Bond) taarifa zinaonyesha kwamba mifuko ambayo
ilikuwa bado kuridhia hati ya Makubaliano (deed of settlement) hivi sasa imeridhia.
Serikali inatarajia kutoa Hati Fungani (non-cash bond) ya Shilingi Trilioni 2.6 yenye
riba ya asilimia 6.5 kwenda PSPF. Hati Fungani hii itaiva kwa muda tofauti ili
kuwezesha mfuko kukidhi mahitaji yake ya malipo ya mafao. Hati fungani hizi zitaiva
kwa vipindi tofauti tofauti. Yaani kuna hati fungani za miaka 3, miaka 5, miaka 7, miaka
10 na kuendelea.

MIRADI YA UWEKEZAJI
Mamlaka kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania kwa mujibu wa Kifungu cha 6(2)
(c) cha Sheria Na.8 ya mwaka 2008 ikisomwa pamoja na kifungu cha 40 na kifungu
cha 48 Mamlaka ilikamilisha kaguzi za Mifuko kwa mwaka 2015. Kaguzi hizi
zimepelekea Mamlaka kwa kushirikiana na Benki Kuu kufanya kaguzi maalumu
(Special Inspection) kwenye majengo na milki za Mifuko yote ya Hifadhi ya Jamii ikiwa
ni pamoja na Mfuko wa NSSF. Kaguzi hizi zimeanza toka mwezi Januari 2016. Huu
ni ukaguzi wa kina sana hivyo unatarajiwa kuchukua kati ya miezi 6 hadi 9 kulingana
na upatikanaji wa taarifa zinazohusika. Hata hivyo wakati kaguzi zikiendelea Mifuko
iliyovuka viwango vya uwekezaji tayari imezuiwa kuendelea kuwekeza katika maeneo
hayo. Taarifa ya ukaguzi maalumu, itakapokamilika itasaidia Serikali kuchukua hatua
1

stahiki. Tunaomba kuwaondoa wasiwasi wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii


na kuwahakikishia kwamba michango yao ipo salama na Mamlaka inazifanyia kazi
kero zao kwa bidii kubwa.
Maoni ya wadau kuhusu kuunganisha Mifuko
Mamlaka inaendelea kupokea maoni ya wadau kuhusu namna bora ya kuunganisha
Mifuko. Tayari Mamlaka imeshafanya vikao 6 vya wadau kuhusu swala hilo. Mamlaka
inaendelea na mikutano ya wadau ili kuhakikisha kwamba maamuzi ya jambo hili
pamoja na mengine kama hayo, yanazingatia utaalamu, mapendekezo ya wadau na
hivyo kuwa na mfumo wa Hifadhi ya Jamii wenye tija na Manufaa kwa Wanachama
na Sekta kwa ujumla .
Takwimu za Sekta kwa kipindi kinachoishia Juni 2015

Wanachama milion 2.1

Rasilimali = shilingi Trilioni 8.78

Michango = shilingi Trilioni 1.9

Mafao yaliyolipwa = shilingi Trilioni 1.36

Uwekezaji = shilingi Trilion7.1

Wastaafu = 89, 532

Deni la pensheni limepungua toka asilimia 58 ya pato la Taifa mwaka 2010 hadi
asilimia 25 mwaka 2015.
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii inalipa mafao ya muda mrefu kama vile;- fao la Pensheni
ya Uzee, Mirathi na Ulemavu. Kwa upande wa mafao ya muda mfupi Mifuko inalipa
mafao ya;- Uzazi, Elimu, Afya, Mazishi na Kuumia kazini pamoja na huduma
zingine kama vile Mikopo ya makazi, elimu na mikopo ya kuanza maisha baada ya
kuajiriwa.

UMRI WA KUISHI BAADA YA KUSTAAFU


Umri wa kuishi baada ya kustaafu umeongezeka kufikia miaka 20.8 kwa wanaume,
na miaka 22.2 kwa wanawake. Hali hii itaendelea kuwa nzuri zaidi kadiri ya miaka

inavyoongezeka ambapo kwa kipindi cha miaka 50 ijayo umri wa kuishi baada ya
kustaafu kwa wanaume itakuwa miaka 22.9 na wanawake miaka 24.9.

VIWANGO VYA PENSHENI


Pensheni imeboreshwa kutoka wastani wa asilimia 67 hadi asilimia 72.5. Hata hivyo
kwa Mifuko inayolipa mkupuo wa asilimia 50 viwango vya pensheni kwa mwezi ni
asilimia 27 ya mshahara. Hiki ni kiwango cha chini sana, kiwango kinachotakiwa
kimataifa ni asilimia 40.

UIMARA WA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII


Tathmini inaonesha kwamba Mifuko imeimarika. Mifuko inauwezo kwa kustawi hadi
kufika mwaka 2085 na 2075 kwa mfuko wa NSSF na PPF. Tathmini inaonesha
kwamba Mfuko wa LAPF na GEPF una uwezo wa kufika Zaidi ya mwaka 2058 na
2047. Na iwapo vikokotoo vyao vitarekebishwa Mifuko hii itaweza kufika mwaka 2085.
Hali kadhalika iwapo Mfuko wa PSPF utapokea michango ya kabla ya 1999 na
kufanya marekebisho yanayopendekezwa kwa GEPF na LAPF Mfuko huu utadumu
hadi mwaka 2075. Vilevile Mfuko huu utaimarika iwapo mafao yatarekebishwa au
michango kuongezwa hadi kufika asilimia 28 badala ya asilimia 20. Suala hili
litategemea zaidi utashi wa wadau.

GHARAMA ZA UENDESHAJI MIFUKO.


Kwa ujumla Mifuko imeonekana kuwa na Gharama kubwa ya uendeshaji. Kuwepo
kwa gharama kubwa za uendeshaji kutazorotesha utendaji wa Mifuko. Hivyo kwenye
jambo hili Mamlaka imeandaa kanuni za kushusha gharama za uendeshaji. Mifuko
yote haitaruhusiwa kuwa na gharama inayozidi asilimia 10 kuanzia July 2016. Sheria
zinazoruhusu Mifuko kutumia asilimia 15 zimeingizwa kwenye mchakato wa
marekebisho.

KUINGILIANA KWA MAFAO


Tathimini imeonesha kuwa ukiacha Mafao ya muda mrefu, NSSF wanatoa mafao la
Bima ya Afya pamoja na Fao la Kuumia Kazini wakati uo huo, Mfuko wa Bima ya Afya
ya Taifa (NHIF) hutoa huduma za bima ya afya. Vilevile Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi (WCF) nayo inashughulisha na fao la kuumia kazini. Mamlaka
inashughulikia suala hili ili kupunguza gharama kwa waajiri na kuboresha mafao kwa
wanachama.

UWIANO WA WACHANGIAJI NA WASTAAFU


Tathimini inaonesha kuwa kila mfuko upo katika kiwango chake cha ukuaji. Kiwango
cha idadi ya wanachama kufikia 1.95 milioni wakati idadi ya wanaopokea pensheni
kufikia 97,428. Hii ni uwiano wa wanachama 20 kwa mstaafu mmoja. Hiki ni kiwango
kizuri kwa sekta. Hata hivyo Mifuko yenye wastaafu wengi hasa PSPF na PPF
inapaswa kuongeza wanachama wake mara dufu.
Hitimisho
Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa ushirikiano mkubwa tunaopata toka kwa Serikali
kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye
Ulemavu; Wizara ya Fedha na Uchumi; Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Wzee;
Benki Kuu ya Tanzania; Vyama vya Wafanyakazi; chama cha Waajiri; vyombo vya
habari pamoja na wadau wote kwa ujumla.
Mwisho, Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii inapenda
kuwatoa hofu wanachama na wadau wengine wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwamba
Sekta ipo imara. Iwapo kuna malalamiko, ushauri au maoni yoyote kuhusiana na
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii tafadhali msisite kuwasiliana na Mamlaka ili yapatiwe
ufumbuzi mapema iwezekanavyo.

You might also like