You are on page 1of 4

IPTL yakanusha Tuhuma za Rushwa na Taarifa za

Uongo Zilizochapishwa na Gazeti la MwanaHALISI


1.
Makampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL)
na Pan Africa Power Solutions (T) Limited (PAP), tumesononeshwa sana na taarifa
iliyochapishwa na gazeti la kila wiki la MwanaHALISI katika toleo namba 332 la
tarehe 28 Machi 2016 lenye kichwa cha habari, Siri za Kikwete, IPTL zafichuka
; iliyoambatana na nukuu katika ukurasa wake wa mbele inayosomeka hadi
ndani ya jumba jeupe (Ikulu kwenyewe), Singasinga alitembeza
mlungula.
2.
Taarifa hiyo iliyojaa uongo pamoja na kashfa nzito ya rushwa kwa IPTL/PAP na
kwa viongozi waandamizi wa serikali ya awamu ya nne na wengine ambao bado
wamo katika serikali hii ya awamu ya tano, imediriki kudai kwa kunukuu maneno
yafuatayo,.. Sethi alitoa rushwa kila mahali, ikiwamo Ikulu, ili
kufanikisha mpango wake huo.Alihonga kila mtu. Alitoa rushwa kwa kila
aliyeona faili la Escrow. Hadi maofisa wa Ikulu na viongozi waandamizi
kutoka wizara ya fedha..hadi ndani ya jumba jeupe (Ikulu kwenyewe),
Singasinga alitembeza mlungula. Ni BoT pekee, ambako hakuhonga au
kuombwa rushwa.
3.
Tungependa kukanusha taarifa hizi za shutuma ya rushwa ambazo ni za
uongo na uzushi mtupu wenye lengo la kuichafua IPTL na wamiliki wake akiwemo
Mwenyekiti Mtendaji, Bw. Harbinder Singh Sethi. Taarifa hizi zisizo na chembe ya
ukweli ndani yake zinalenga kuchafua sifa ya Ikulu ambayo ni taasisi nyeti hapa
nchini kwa kuihusisha na upokeaji rushwa ambayo ni kosa la jinai kwa mujibu wa
katiba na sheria za nchi yetu.
4.
Isitoshe taarifa hizi zimejaa habari za uongo zilizobuniwa kwa nia na
madhumuni maovu ya kuichafua sifa za kampuni za IPTL/PAP na mwenyekiti wake
Bw. Harbinder Singh Sethi pamoja na kuwachonganisha dhidi ya wananchi wa
Tanzania kwa kuwahadaa na kuwaaminisha Watanzania kuwa IPTL/PAP inaendeshwa
kwa misingi ya rushwa na udanganyifu, hivyo basi haistahili kufanya biashara hapa
nchini.
5.
Awali ya yote, tungependa kuutarifu umma wa Watanzania kwamba tuhuma
za rushwa ni tuhuma nzito na wala siyo za kunyamaziwa kabisa. Rushwa ni moja
kati ya makosa makubwa ya kijinai ambayo vyombo vya dola vinatilia maanani
sana. Hivyo basi, kampuni ya IPTL/PAP haiwezi kukaa kimya wakati tuhuma kama
hizi zikiendelea kuchapishwa dhidi yake, huku ikiwahusisha viongozi waandamizi wa
serikali, bila ya gazeti husika pamoja na mwandishi wa taarifa hizo kutoa udhibitisho
wowote wa tuhuma hizo.
6.
IPTL/PAP tunaamini kwamba taratibu zote za kukabidhiwa kampuni ya IPTL
(ikiwemo mali na madeni halali) zilifuatwa. Tunaamini katika utawala wa sheria
ambayo inazingatia haki za kila mtu. Hivyo basi, haitakuwa busara kuendelea
1

kunyamazia vitendo vya kiovu vya kuichafua kampuni yetu vinavyofanywa na


baadhi ya vyombo vya habari kwa kisingizio cha uhuru wa kutoa maoni au uhuru
wa vyombo vya habari. Kama vyombo vya habari walivyo na uhuru wao, vivyo
hivyo IPTL/PAP kama kampuni ina uhuru wa kufanya shughuli zake kwa mujibu wa
sheria za nchi bila ya kubughudhiwa. Kwa kutuhumu IPTL/PAP au viongozi wake
kutoa rushwa, bila kuthibitisha, ni kuihujumu kampuni ili isiweze kutekeleza
majukumu yake ya kuchangia ukuwaji wa uchumi wa nchi yetu.
7.
Mbali na tuhuma za rushwa, takriban taarifa nzima ya gazeti hilo la
MwanaHALISI imejaa uongo uliokubuhu na uzushi usiokuwa na chembe ya aibu.
Sehemu ya taarifa hiyo ya gazeti la MwanaHALISI inadai na kunukuliwa Kampuni
hiyo binafsi ilidai kuwa gharama za umeme zilikua asilimia 22.3; na
gharama za mtaji asilimia 30 zilikuwa dola za Marekani 38.16 milioni. Hata
hivyo, Mahakama ilithibitisha kuwa gharama halisi za mtaji wa IPTL
zilikuwa chini ya dola za Marekani 1,000. Tunapenda kuwataarifu Watanzania
kuwa hakuna mahakama yoyote duniani iliyothibitisha madai haya na hii ndiyo
sababu kuu ya mwandhishi wa taarifa hii kashindwa kutaja ni mahakama ipi hiyo
iliyothibitisha hayo yanayodaiwa na kunukuliwa.
8.
Sehemu ya taarifa ya gazeti la MwanaHALISI imeendelea kudai na kunukuliwa
Lakini fedha hizo zilichotwa kabla mgogoro huo haujapatiwa ufumbuzi na
katika mazingira ya udaganyifu; na kwa kutumia baadhi ya nyaraka
ambazo ziligundulika kuwa ni za kugushi Hata hivyo Sethi alishindwa
kuweka uthibitisho wowote kuwa kampuni hiyo inamiliki hisa za kampuni
ya Mechmar Limited ya Malaysia ndani ya IPTL.
Kwa yeyote aliyesoma Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) iliyojulikana kama
Taarifa ya Ukaguzi Maalum Kuhusiana na Miamala Iliyofanyika katika Akaunti ya
Escrow ya Tegeta, Pamoja na Umiliki wa Kampuni ya IPTL, anaweza kutambua
kuwa tuhuma na madai yaliyonukuliwa hapo juu ni uongo mtupu. Ripoti hiyo ya
Mkaguzi Mkuu wa Serikali katika ukurasa wake 23 inaeleza kuwa Bw. Harbinder
Singh Sethi aliwasilisha Deed of Assignment of Shares na Mkataba wa Kuuza na
Kununua hisa kati ya PAP na PiperLink Investment kutokana na agizo la kuwasilisha
ushahidi wa kununua asilimia 70 za hisa za Mechmar katika IPTL. Si Mkaguzi Mkuu
wa Serikali wala chombo chochote cha serikali kilichopata kuthibitisha kuwa nyaraka
zilizowasilishwa na Bw. Harbinder Singh Sethi zilikuwa ni za kughushi kama taarifa
ya gazeti la MwanaHALISI ilnavyodai na kunukuliwa hapo juu.
9.
Sehemu ya taarifa ya gazeti la MwanaHALISI imeendelea kudai na kunukuliwa
Malipo hayo kwa PAP yalifanyika bila Waziri wa Nishati, Prof. Sospeter
Muhongo, wala BoT kuhakiki uhamishaji wa hisa kutoka Mechmar kwenda
PAP; bila PAP kusajili hisa zake nchini; bila PAP kuthibitisha kujisajili Kituo
ch Uwekezaji nchini (TIC); na bila kuwa na hati ya mlipa kodi (TIN). Hizi
nazo ni taarifa za uongo zisizokuwa na chembe ya ukweli. Mwandishi amejaribu
kutumia mseto wa hoja zisizokuwa na mshiko ili mradi anajenga taswira kuonyesha
malipo yaliyofanywa kwa PAP yalikuwa ni malipo ya ubabaishaji.
2

10.
Sehemu ya taarifa hiyo ya gazeti la MwanaHALISI imeendelea kudai na
kunukuliwa Serikali ililazimika kukopa kwa siri kiasi hicho cha fedha
kutoka Stanbic kwa kuweka dhamana ya hati fungani, ili kufanikisha
upatikanajiwa fedha za kumlipa Singasinga wa IPTL, ameeleza mmoja wa
maofisa wa Stanbic ambaye ametoka katika benki hiyo hivi karibuni. []
Kigogo huyo anasema, kwa vile wakubwa walishapanga kumlipa Sethi,
kabla ya Desemba 2013, ikabidi wakope benki kwa kuweka dhamana hati
fungani zilizoshushwa bei (discounted treasury bills).
Kwa mujibu wa Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali (iliyotajwa hapo juu) kwenye
ukurasa wake wa 16 inaelezea wazi kabisa kuwa umiliki wa hati fungani
zilizowekezwa na BoT kutokana na fedha zilizokuwa kwenye akaunti ya Escrow ya
Tegeta, ulihamishwa kwenda kwa PAP tarehe 6 Desemba, 2013. Madai ya kuwa
serikali ilikopa kwa kuweka hati fungani zilizoshushwa bei ni uongo na uzushi
usiokuwa na ukweli wowote.
11.
Sehemu ya taarifa hiyo ya gazeti la MwanaHALISI imeendelea kudai na
kunukuliwa Taarifa zinasema, katika kiasi hicho cha dola 180 milioni, dola
takriban 100 milioni, kilitoroshewa nje katika nchi za Falme za Kiarabu,
huko Dubai na Afrika Kusini, kabla ya kuhamishiwa tena nchini Austria.
Nchini Austria, taarifa zinasema, ndiko ambako mtoto wa mmoja wa
waliokuwa viongozi wa juu serikalini, amefungua akaunti. Hizi ni taarifa za
uongo zisizokuwa na chembe ya ukweli na ni tuhuma zisizokuwa na ushahidi
wowote.
12.
Kwa machache haya ya uongo na uzushi tuliyoyanukuu na mengine mengi
ambayo tumeamua kutokuyatolea ufafanuzi kwa nia ya kuiweka taarifa hii kwa
ufupi, tungependa kuomba vyombo husika kuchukua hatua dhidi ya waliohusika na
uenezi wa taarifa hizi za kizushi kwa kuwafikisha mbele ya vyombo vya dola na
kuwahoji ili ukweli wa tuhuma ujulikane. Tunaamini kwamba tabia ya kuikashifu
kampuni yetu na kuwakashifu viongozi wa serikali bila ya kuwa na uthibitisho
isipokomeshwa, basi nchi itajaa waropokaji na heshima ya serikali na vyombo vyake
itaporomoka. Tabia hii isipokomeshwa itaathiri hali ya uwekezaji nchini kwani
itawakatisha tamaa wawekezaji wengine wanaotaka kuwekeza nchini.
13.
Kwa muhtasari, taarifa zilichochapishwa kwenye makala husika ni uzushi
usiokuwa na ukweli wowote. Tungewaomba Watanzania na wote waliosoma au
watakaosoma makala husika wazipuuzie taarifa hizo. Pia tunawataka wahariri na
wachapishaji wa gazeti la MwanaHALISI kuomba radhi kwa taarifa hizo za kizushi
ndani ya siku kumi na nne (14). Kushindwa kufanya hivyo, hatua za kisheria
zitachukuliwa ikiwemo kulifikisha gazeti, wahariri na wachapishaji wake
mahakamani.
14.
IPTL/PAP tuko tayari kutoa ushirikiano kwa mtu yeyote mwenye ushahidi wa
rushwa kufikisha mbele ya vyombo husika na kuhakikisha rushwa inakomeshwa.
3

15.
Tunaomba pia vyombo mbalimbali vinavyohusika na kulinda amani na
utengamano wa nchi yetu ikiwemo jeshi la polisi kuwachukulia hatua mwandishi wa
makala hiyo na wahariri wa gazeti la MwanaHALISI kwa kuvunja sheria za nchi kwa
kuandika habari za uchochezi.
Ahsanteni sana.

Joseph O. R. Makandege (ADVOCATE)


(Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria)
KAIMU MWENYEKITI MTENDAJI
Independent Power Tanzania Limited / Pan African Power Solutions (T)
Limited.

You might also like