You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE LA TANZANIA
Ofisi ya Bunge,
S.L.P. 9133,
DAR ES SALAAM

Simu: +255 022 2112065-7


Fax No. +255 022 2112538
E-mail: info@bunge.go.tz

TAARIFA KWA UMMA


Katika kutekeleza majukumu yake, Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo imepanga
kufanya mikutano ya kusikiliza maoni ya wadau (Public Hearing) kwa mujibu wa Kanuni
ya 117 (9) kuhusiana na Sheria Ndogo zilizowasilishwa na Serikali katika Mkutano wa Pili
wa Bunge uliomalizika Februari 2016.
Mikutano hiyo ya kusikiliza maoni ya wadau kuhusu Sheria Ndogo inatarajiwa
kufanyika Jumatatu tarehe 4 Aprili, 2016 na Jumanne tarehe 5 Aprili, 2016 katika Ukumbi
wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam. Sheria Ndogo
ambazo Kamati inakaribisha wadau na umma kwa ujumla kutoa maoni yao ni pamoja
na zifuatazo:1. The Petroleum (Bulk Procurement) Regulations, 2015
2. The Public Private Partnership Regulations, 2015
3. The Copyright and Neighboring Rights (Copyrighted Works - Communication
to the Public) Regulations, 2015
4. The National Examinations Regulations, 2015
5. The Institute of Judicial Administration Lushoto (Students General Welfare,
Conduct and Disciplinary Matters) Regulations, 2015
6. The Institute of Judicial Administration Lushoto (Students Performance
Assessment) Regulations, 2015
7. The Fire and Rescue Force (Fire Precautions in Buildings) Regulations, 2015
Sheria Ndogo zilizotajwa hapo juu pamoja na nyingine ambazo zinashughulikiwa
na Kamati, zinapatikana kwa kupakua (downloadable) katika tovuti ya Bunge la
Tanzania ya www.parliament.go.tz pamoja na tovuti ya Serikali ya www.tanzania.go.tz
Aidha, maoni ya wadau yanaweza kuwasilishwa kwa njia ya posta au barua
pepe kwa anuani ifuatayo:Katibu wa Bunge,
Ofisi ya Bunge,
S. L. P. 9133,
DAR ES SALAAM
Barua pepe: cna@bunge.go.tz
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM
29 Machi, 2016.

You might also like