You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE LA TANZANIA
Ofisi ya Bunge,
S.L.P. 9133,
DAR ES SALAAM

Simu: +255 022 2112065-7


Fax No. +255 022 2112538
E-mail: info@bunge.go.tz

TAARIFA KWA UMMA


_________
Kufuatia Mabadiliko ya Wajumbe kwenye Kamati za Kudumu za Bunge yaliyofanywa
na Mhe. Job Ndugai (Mb) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana
tarehe 22 Machi, 2016; baadhi ya Vyombo vya Habari na Mitandao ya Kijamii
imenukuliwa ikihusisha mabadiliko hayo kuwa yamefanywa kutokana na tuhuma za
rushwa kwa baadhi ya Kamati za Bunge kufuatia ripoti ya chombo kimoja cha Habari.
Ofisi ya Bunge inapenda kutoa ufafanuzi kuwa madai hayo hayana ukweli wowote,
bali mabadiliko yaliyofanywa na Mhe. Spika ni ya kawaida na wala hayakuanisha
dosari zozote katika Utendaji wa kamati za Kudumu za Bunge. Msingi wa Mabadiliko ya
Wajumbe kwenye kamati, umelenga kuzingatia mahitaji mapya na changamoto
zilizojitokeza baada ya kuunda Kamati hizo mwezi Januari 2016 ambapo alikuwa
ameanza kufanyia kazi mabadiliko hayo tangu mapema mwezi huu.
Waheshimiwa Wabunge wanaosakamwa kwa uvunjifu wa Maadili kupitia Mitandao ya
kijamii na Magazeti, ni budi wakatendewa haki kwa sababu Mhe. Spika anazingatia
sana Utawala wa Sheria na kama kuna Mbunge yoyote anaetuhumiwa kwa makosa
ya Jinai, Mamlaka za kiuchunguzi zinawajibu wa kutekeleza majukumu yao na pale
inapobidi, Bunge lenyewe kupitia kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge
inaweza kufanya uchunguzi kwa Mamlaka ya Spika.
Aidha, ifahamike vyema kuwa, kwa mujibu wa Kanuni ya 116 (3) Mamlaka ya kufanya
mabadiliko kwenye Kamati za Kudumu za Bunge ni ya Spika na anaweza kufanya
hivyo wakati wowote kama alivyofanya mapema mwezi huu ambapo alizingatia
maombi ya baadhi ya Wajumbe 15 kuhamia Kamati nyingine kutokana na sababu
mbalimbali zikiwemo za kiafya kwa baadhi ya Wajumbe na pia kuboresha Utendaji wa
Kamati hizo kama ilivyojitokeza jana kwa wajumbe 27 kuhamishiwa kamati zingine pia.
Mhe. Spika anawasihi Wajumbe wote kuendelea kutekeleza majukumu yao kama
kawaida katika kamati zao.

Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM
23 Machi, 2016.

You might also like