You are on page 1of 3

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

TAARIFA KWA UMMA


Tunakanusha taarifa iliyochapishwa na gazeti la The Citizen la
Januari 5, 2016 katika ukurasa wake wa 12 yenye kichwa cha
habari: Umma kununua asilimia 49 ya hisa za Tanesco.
Mwandishi na Mhariri wamejiandikia taarifa hiyo kwa sababu
wanazozijua wao.
Sehemu ya taarifa inasema: Serikali ya Tanzania ina mpango wa
kuuza hisa ya Shirika la Umeme Tanzania kwa umma...
Pia, sehemu nyingine inasema: Waziri wa Nishati na Madini
Sospeter Muhongo aliliambia gazeti la East African kuwa Serikali
itatoa asilimia 49 ya hisa za Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) wakati huo Serikali ikibaki na hisa zingine...
Tungependa wananchi kwa ujumla waelewe kwamba taarifa hiyo si
sahihi na inapotosha umma. Taarifa sahihi kama ifuatavyo:

Kwanza, Waziri Sospeter Muhongo hajafanya mahojiano


yoyote na mwandishi wa gazeti hilo la The East African wala
gazeti la The Citizen.

Pili, Serikali haina mpango wa kuuza hisa za TANESCO kwa


umma.
Mkakati uliopo wa Mageuzi ya kuboresha Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) ujulikanao kama Electricity Supply Industry
Reform Strategy and Roadmap (ESI-RSR) 2014 2025 ni kama
ifuatavyo:

MAELEZO YA MKAKATI NA MWELEKEO WA KUREKEBISHA


SEKTA NDOGO YA UMEME (ESI-RSR)
Mwezi Juni 2014, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ilipitisha na kuchapisha mkakati wa mageuzi wa Electricity Supply
Industry Reform Strategy and Roadmap (ESI-RSR) 2014 2025.
Lengo la msingi wa mkakati huo ni kuboresha mazingira ya
uwekezaji wa sekta binafsi katika nyanja za uzalishaji na
usambazaji, na kuongeza uunganishaji wa umeme katika ngazi
zote.
Utekelezaji wa mpango huo ambao unatarajiwa kutekelezwa katika
kipindi cha miaka kumi na moja (11) umegawanyika katika vipindi
vikuu vitatu ambavyo ni muda mfupi, wa kati na muda mrefu.

Mkakati wa muda mfupi ni kutenganisha shughuli za


Uzalishaji ili zifanywe na Kampuni Tanzu ya TANESCO.
Umiliki wa uzalishaji, usafirishaji na usambazaji chini ya
awamu hii itaendelea kuwa chini ya Serikali, kama mbia
moja.

Mkakati wa muda wa kati unahusu kutenganisha sehemu ya


usambazaji kutoka kwenye usafirishaji. Katika Awamu hii,
Kampuni za uzalishaji, usafirishaji na usambazaji
zitaendelea kuwa chini ya umiliki wa Serikali.

Mkakati wa muda mrefu utahusishaOfisi za Kanda


kujihusisha na usambazaji wa huduma za umeme ambazo pia
zitagawanywa kulingana na uwezo wa kujiendesha. Katika
kipindi hicho cha muda mrefu, kampuni binafsi za
usambazaji umeme zitaendelea kushiriki katika shughuli
za uzalishaji na usambazaji umeme kwa ajili ya kuchochea
ushindani na ufanisi kwenye soko.

Tunawahimiza wadau wote kusoma mkakati wa mageuzi


ujulikanao kama Electricity Supply Industry Reform Strategy and
Roadmap (ESI-RSR) 2014 2025 ambao unapatikana mitandaoni

Aidha, tunawakumbusha Waandishi wa Habari na Wahariri ambao


hawazingatii maadili ya taaluma yao kuandika taarifa sahihi ili
kuepusha upotoshaji kwa umma.
Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
6 Juni, 2015

You might also like