You are on page 1of 12

YUSUF MANJI

MGOMBEA UDIWANI - MBAGALA KUU

Miaka kumi iliyopita tulianza safari na katika safari hiyo nilisema,


Kutoa ni moyo na si utajiri na mimi nimetoa moyo wangu kwenu.
Baadhi yenu mnaweza kukumbuka maneno niliyosema kwenye uwanja wa
Mbagala Zakhem mwaka 2005 nilipokuwa na umri wa miaka 29, wakati
nawania kuwa mbunge wa Kigamboni. Mlinikabidhi imani yenu ya dhati
kutoka mioyoni mwenu na kwa kishindo nikashinda kura za chama kupitia
kuwa mgombea mteule wa Ubunge wa Kigamboni tiketi ya CCM.
Nikashauriwa na Wazee wa Chama nisubiri kutokana na umri wangu wa
miaka 29 kuwa mdogo.
Nimesubiri kwa muda wa miaka kumi na sasa nina umri wa miaka 39, na
nimepewa idhini na Chama changu ya kuwania Udiwani wa kata ya Mbagala Kuu. Kama nilivyoahidi kuwapa moyo wangu miaka kumi iliyopita, bado
ninakusudi hilo kwa kupitia thamani ya kura zenu, kuleta maendeleo
ambayo nina amini Kata ya Mbagala Kuu, Wilaya ya Temeke na Mji wa Dar
Es Salaam ulikuwa ukiyangojea.
Katika kipindi chote cha kampeni nimetembelea matawi yote yanayounda
Mbagala Kuu kuanzia Kichemchem Kaskazini hadi Makuka A, Makuka B
mpaka Kizuiani, Kichemchem Kusini, Mbagala Kuu,n.k. ambapo nilipata
nafasi ya kuzungumza na wengi wenu.
MAENDELEO SIO MANENO
1

Nilipoanza kampeni, niliwasikiliza, nikauliza maswali ili kupata uelewa mzuri


wa vikwazo mnavyokumbana navyo na ufumbuzi mnao upendekeza, kwa
kuwa katika mtazamo wangu ninaona ni busara zaidi kuwasikiliza nyinyi
kwanza, kisha tutafakari kabla ya mimi kuwaeleza mipango yangu na ahadi
za safari yetu, ili mpate nafasi ya kuamua kama mimi ninafaa kushiriki
kufikia ndoto mlizonazo juu ya mustakabali wetu na watoto wetu, pia kama
mimi na chama changu tunastahili kura zenu tarehe 25 Oktoba, 2015.
Kwahiyo baada ya kusikiliza kwa umakini na kuhakiki vikwazo vikuu vinayoikumba Kata ya Mbagala Kuu, kupitia Ilani ya Chama changu, kama nikichaguliwa kuwa Diwani, zifuatazo ni hatua nitakazozichukua ili kutatua changamoto zinazoikabili Kata ya Mbagala Kuu:
inatubidi tuelewe mambo makuu mawili;
- Kwanza, tuna uhaba wa ardhi katika kata yetu kukidhi takriban watu
100,000. Kwa hiyo ninacho pendekeza kitawezekana endapo tutasimamia
uhamiaji wa watu kuja katika kata yetu na
- Pili, kujenga daraja la kuleta uwiano katika ugawaji wa rasilimali kukidhi
idadi yetu kubwa.
Kwa
mfano,
tunahitaji
barabara, shule, zahanati,
vituo vya polisi, masoko,
maji n.k. na vyote tunavihitaji kwa wakati mmoja,
kama tukisema tuitegemee
Serikali na Manispaa ya
Temeke kupata huduma
hizo kwa miaka 5, ambapo Serikali pia ina wajibu wa kushughulikia changamoto kama hizo si kwa wilaya ya Temeke pekee bali hata kwa taifa zima.
Hivyo tutapata maendeleo finyu katika barabara, shule, zahanati n.k. (kama
kata zingine) na bado mwisho wa awamu yangu tutajikuta hatujaridhika,
tuna njaa ya mendeleo wakati idadi ya watu itakuwa imeongezeka zaidi na
ardhi yetu kuwa adimu zaidi.

Kwa hiyo, mapendekezo yangu


ni kuwa inatubidi tuendeleze
baadhi ya mambo kupitia rasilimali za sekta binafsi (rasilimali
ambazo mimi ninazo) na
kuruhusu mfuko uliotengwa
kwa ajili ya kata yetu kukidhi
mahitaji ambayo rasilimali za
sekta binafsi hazitaweza au
hazitakuwa tayari kuwekeza.
Zifuatazo ni changamoto na mapendekezo yangu katika kuleta
maendeleo ya Kata ya Mbagala Kuu:

1. Kuunganishwa na maji
Tatizo kubwa linalo tukumba ni k u t o unganishwa na maji kutokana na Kata
yetu kutounganishwa na DAWASCO, hivyo wakazi wanategemea chanzo kimoja tu cha
maji cha Taasisi ya Teknolojia ya Ubelgiji.
Endapo nitachaguliwa, suluhisho langu litakuwa ni kushinikiza moja ya kampuni
zangu kuwekeza katika uchimbaji wa visima virefu vya kutumia umeme ambavyo
vitaanza kazi ndani ya mwaka moja kuanzia siku nitakayo chaguliwa, na kwa gharama
nafuu sana kuruhusu wakazi wa Mbagala Kuu
kuunganishwa na maji, fedha tutakazo
lipia huduma ya maji zitatumika kukidhi gharama za kuendeshea kampuni ili iweze
kuendelea kuwekeza katika sekta ya maji ya taifa.
Pia kulikuwa na mradi wa maji uliopitishwa ambao mpaka sasa haufanyi kazi,
nitafanya uchunguzi ili ifahamike kwanini mradi huo ulikufa na kuwahimiza kutua
mini tena.

2. Huduma za kiafya / zahanati / vyumba vya kuhifadhi maiti:


Hivi sasa, Mbagala Kuu ina zahanati tatu (moja inaendeshwa na Serikali na mbili
ni za mashirika binafsi), pia ipo hospitali moja ya Serikali ambayo inatambulika
kama hospitali ya rufaa ambayo ni kinyume na hali halisi.

Kama nikiteuliwa suluhisho langu


litakuwa ni kushinikiza moja ya
kampuni zangu kuwekeza katika
kuanzisha zahanati 20 zaidi ambazo
zitaanza kazi mwaka moja baada ya
mimi kuchaguliwa na kwa gharama
nafuu sana ili kuwezesha wakazi wa
Mbagala Kuu kupata matibabu.
Uwekezaji huu wa kampuni zangu
utafungua rasilimali kutoka Serikalini
kupandisha daraja hospitali ya Kata
kuwa ya hospitali ya rufaa kwa ajili ya matibabu makubwa
Pia kama sehemu ya mchango kutoka kwa familia yangu kwa kata ya Mbagala Kuu
nitashiriki ujenzi wa vyumba vya kuhifadhia maiti, vitakavyokuwa na uwezo wa
kuhifadhi takriban maiti 15 kwa siku, ujenzi huu utakamilika ndani ya miezi 15.

3. Ajira kwa vijana


Vijana wengi hawana ajira

Endapo nitachaguliwa, suluhisho langu litakuwa ni kushinikiza moja ya kampuni zangu


kuandaa pikipiki imara 3,000 zitumike kama bodaboda ambazo zitauzwa kila mwaka kwa
vijana, ambapo asilimia 70% ya malipo hayo itakuwa kama mkopo wa benki wa miaka
mitatu (ambayo nitashiriki kuwaandalia) na 30% ya bei ya rejareja ya pikipiki itakuwa ni
mchango kutoka kwa kampuni zangu, ili vijana wetu watakao tumia pikipiki hizo wapate
kipato cha kupeleka nyumbani kwa familia zao.
Utekelezaji wa haya utaanza mara tu nitakapo
pata idhini yenu, na kwa njia hiyo ndani ya miaka
5 tutakuwa tumewasaidia vijana 15,000 kupata
ajira, watakao jishughulisha na biashara ya
bodaboda.
Natambua kwamba hii itatatua tatizo la ukosefu
wa ajira kwa wakazi wa kata ya Mbagala Kuu, pia
jitihada nyingine zitabidi zichukuliwe kupitia
vyuo vya ufundi n.k.
Ninaamini kwamba, mchango huu kutoka
kwangu utakuwa na manufaa mengi kwani vijana wetu watakao jishughulisha na biashara
ya bodaboda wataweza kujenga uhitaji wa huduma kwa vijana wenzao ambao watahamasika kuongeza ufundi wao kwa vile kutakuwa na uhitaji wa bidhaa na huduma kata ya Mbagala Kuu.

4. Soko la biashara / Huduma za serikali / Viwanja vya michezo:


Katika kata ya Mbagala Kuu tuna ukosefu wa soko, wakazi wanalazimika kutembea
umbali mrefu kupata huduma kutoka manispaa, na pia vijana wanakosa viwanja vya
michezo.
Endapo nitachaguliwa, ufumbuzi wangu utakuwa ni
kushinikiza moja ya kampuni zangu kuwekeza katika
ujenzi wa soko la kisasa litakalo fanana na jengo letu la
Quality Centre, litakalo kuwa na ukubwa wa mita za mraba
30,000 litakaloanzia viwanja vya Zakhem mpaka uwanja
wa wazi wa Mpakani.
Mjengo huo utakuwa kama ifuatavyo: Kutakuwa na jengo
la ofisi ambalo litakuwa na ofisi za huduma za Serikali ili
wakazi wa Mbagala Kuu tuweze kupata vibali, leseni, vyeti
vya kuzaliwa n.k. na hivyo hakutakuwa na haja ya kwenda
mbali. Ambalo litapangishwa kwa Manispaa ya Temeke.
Pia kutakuwa na benki ambazo zitalipa kodi ya pango kwa
eneo la jengo, ukumbi wa harusi.
Sehemu kubwa ya jengo itakuwa ni kwa
ajili ya Wafanyabiashara
wanaoishi
katika kata ya Mbagala Kuu ambao
wataweza kununua maeneo hayo
kupitia mikopo midogodogo.
Kila mmiliki na mpangaji katika soko
atalipia huduma za uendeshaji kulingana na ukubwa wa eneo lake, makato
hayo ya uendeshaji yatatumika si tu
kutunzia soko bali hata viwanja vya mpira, bustani na viwanja vya michezo ya watoto. Mpago huu utachukua takribani miezi 24 kumalizika

5. Kuunganishwa na Umeme :
Bado kuna uhitaji mkubwa wa kuunganishwa na umeme ambao TANESCO bado
hawajaweza kukidhi mahitaji ya wakazi wa Kata ya Mbagala Kuu.
.

Endapo nikichaguliwa, ufumbuzi wangu utakuwa ni


kushinikiza moja ya kampuni zangu kukopesha kila
nyumba kifaa cha kutumia umeme wa jua kwa kila nyumba
au biashara ambayo watapenda kuunganishwa na umeme
huo wa jua wakati ufumbuzi wa muda mrefu utakuwa ni
kiufuatilia TANESCO na kuhakikisha umeme wa kuaminika
Simu
unaletwa Mbagala Kuu haraka iwezekanavyo. Mpango huu
Feni
wa ukopeshaji wa nyenzo za umeme wa solar utakuwa
tayari siku 60 baada ya mimi kuchaguliwa.
Sola hii i naweza kutumika kwa:
kuchaji simu
kuendesha pangaboi
Kuwasha taa

Taa

6. Vyoo vya umma:


Kwa uelewa wangu kipo choo kimoja tu cha umma katika Kata ya Mbagala Kuu.
Endapo nikichaguliwa ufumbuzi wangu utakuwa ni
kushinikiza moja ya kampuni zangu kuchangia kila
mwaka vyoo 24 kama sehemu ya utumishi wao kwa
jamii na kwa namna hii kutakuwepo na vyoo angalau
100 ndani ya miaka 5.
Vyoo vya kwanza 24 vitakuwa tayari siku 90 baada ya
mimi kuchaguliwa.
-

7. Uwezeshaji wa wanawake kupitia SACCOS, Vijana kupitia


mikopo, na elimu ya Ufundi kwa Vijana:
Kutokana na ukosefu wa ufundi wa aina mbalimbali vijana wanashindwa kuende
sha biashara hata pale wanapokuwa na mitaji.
Endapo nikichaguliwa, nitafanya kazi pamoja na mashirika yasiyo ya Serikali na Benki
ndogo ndogo pamoja na mifuko ya SACCOS kulipia vijana mafunzo ya Ufundi (VETA) ili
wapate mafunzo ya aina mbalimbali. Kwa mwaka takriban wanafunzi 5,000 watapata
nafasi ya kupata mafunzo haya. Baada ya mafunzo haya vijana watawekewa mazingira ya
kupata mikopo kutoka kwenye benki ndogo ndogo pamoja na wanawake. Katika hili
inabidi tusaidiane, kwa kila mmoja kuchukua jukumu la kutekeleza wajibu wake pindi
ambapo amepewa mkopo na kurudisha mkopo huo ili siku nyingine tuaminike kupewa
mikopo zaidi.

8. Vituo vya mabasi / Vivuko vya juu vya barabara ya Kilwa :


Watu wengi wanapoteza maisha wakivuka barabra ya Kilwa, tatizo hili linahitaji
ufumbuzi.
Endapo nikichaguliwa, ufumbuzi
wangu utakuwa ni kushinikiza moja
ya kampuni zangu kuchangia
barabara tatu za juu za watembea
kwa miguu wakati wa kuvuka
barabara ya Kilwa ndani ya miaka
mitatu, ambazo wao watapunguza
gharama kwa kupata faida kupitia
matangazo yatakayo kuwa kwenye
vivuko hivyo. kwa kukadiria kivuko
cha kwanza kitakuwa kimekamilika ndani ya siku 180 na vingine vitakuwa tayari ndani ya
miaka mitatu baada ya mimi kuchaguliwa. Pia nitashughulikia ujenzi wa vituo vya
mabasi katika milango ya kupandia na kushukia vivuko.

9. Mitaro, barabara, taa za mitaani kwa ajili ya ulinzi:


Kata ya Mbagala Kuu inakadiriwa kuwa na barabara ya kilomita 17.7 ambazo haziko
katika hali ya kuridhisha pamoja na mitaro. Hata hivyo inatarajiwa kilometa 5 za barabara
zitatengenezwa kuwa za lami kupitia mpango wa Benki ya Dunia kwa mji wa Dar Es
Salaam.
Endapo nikichaguliwa, nitahakikisha kuwa
barabara zilizopo chini ya mpango wa Mji wa
Dar Es Salaam kwa ajili ya Kata ya Mbagala Kuu,
zinapewa kipaumbele katika ukamilishaji na
kupendekeza kutengewa mipango mingine
kupitia programu za Benki ya Dunia, Manispaa
ya Temeke na Serikali kwa ajili ya mifumo ya
ukusanyaji maji na barabara kama rasilimali
zinazohitajika katika huduma za matibabu,
masoko, kuunganishwa kwa maji, vyoo vya
jamii, n.k. Kama nilivyo onyesha hapo juu mtazamo wangu ni kujenga chini ya Sekta za
Kijamii, Shirikisho la Sekta Binafsi. Ninaamini kuwa ombi la miundombinu bora ya mfumo
wa ukusanyaji maji ni moja kati ya mengi ambayo kata ya Mbagala Kuu inahitaji kutoka
Serikalini na mimi nitakuwa mtu sahihi wa kuyapeleka maombi hayo.

Ili kusaidia barabara ndogondogo za Kata ya Mbagala Kuu kuboreshwa kuwa ya kiwango
cha lami nitatoa greda 5 kwa Manispaa ya Temeke kama mkopo ili kusaidia barabara
ndogo ndogo kuwa za changarawe zitakazoweza kustahimili mabadiliko ya hali ya hewa
ambapo ujenzi huo utaanza ndani ya siku 120 baada ya mimi kuchaguliwa.

10. Utupaji wa Taka:


Kuna tatizo kubwa la utupaji wa taka .
Endapo nikichaguliwa, suluhisho langu
litakuwa ni kushinikiza moja ya
kampuni zangu kukopesha magari 20
kwa Manispaa ya Temeke kwa ajili ya
ukusanyaji wa taka na utupaji kwenye
mahala husika. Mpango huu unakadiriwa kukamilika ndani ya siku 120 baada
ya mimi kuchaguliwa.

11. Wakazi wa maeneo yenye kukumbwa na mafuriko:


Kama nilivyosema awali moja ya tatizo letu kubwa ni upungufu wa ardhi, na hili
limesababisha wakazi kujenga mabondeni. Hakuna suluhisho rahisi la kuongeza
ardhi. Kwa mtazamo wangu suluhisho lipo moja kama ifuatavyo:
Endapo nikichaguliwa, nitamuomba
Mheshimiwa Rais atusaidie kuwaomba
JWTZ wahamishe Maghala yao kwenda
mbali zaidi kutoka maeneo ya makazi ya
watu na kama watakubali, nitahamasisha
moja ya kampuni zangu kujenga ghala la
vifaa vya jeshi vinavyohitajika kwenye
eneo lingine tofauti. Kama fidia ya kuwahamisha, ambapo pia nitawajengea
nyumba za
bei nafuu wale wakazi wanaokaa maeneo ya mabondeni na kuwawekea mazingira
ya kuweza kupata mikopo. Kwa bahati mbaya hili ndio suluhisho pekee ninalo
liona linaloweza kutatua tatizo hili

12. Shule za msingi na sekondari:


Mpaka sasa kuna shule 5 za msingi (Shule ya msingi Kibonde Maji, Shule ya Msingi
Mbagala Kuu, Shule ya Msingi Maendeleo,
Shule ya Msingi Kizuiani na Shule ya Walemavu ya Mbagala Kuu) na ripoti zinaonyesha
kuwa walimu wanao hitajika ni 296 wakati waliopo ni 276 (kuna upungufu wa walimu
20); madarasa yanayo hitajika ni 271 lakini yaliyopo ni 89 (182 yamepungua); madawati
yanayohitajika ni 3779 wakati yaliyopo ni 2277 (yamepungua 1542); vyoo 541 vinahitajika lakini vilivyopo ni 117 (424 vimepungua) viti vya walimu vinavyo hjitajika ni 375
wakati vilivyopo 221 (154 vimepungua); meza za walimu zinazohitajika ni 375 wakati
zilizopo ni 133 (48 zimepungua); makabati ya walimu wanayohitajika ni 20 wakati yaliyopo ni 5 (15 yamepungua) nyumba za walimu 284 wakati zilizopo ni 2 tu (282 zimepungua).
Pia zipo shule 2 tu za Sekondari (Shule ya Sekondari Mbagala Kuu ambayo ina Walimu 48
na Wanafunzi 1,389 wanaolazimika kubanana ndani ya madarasa 16 na kushirikiana
kutumia vyoo 10 tu; nyingine ni Shule ya Sekondari Mbagala ambayo ina Walimu 65, na
Wanafunzi 2,096 wanao lazimika kubanana ndani ya madarasa 27 na kushirikiana
kutumia vyoo 7 tu.
Endapo nikichaguliwa, na kama nilivyo elezea hapo juu mtazamo wangu ni kujenga
Sekta za kijamii, Shirikisho la Sekta Binafsi.
Mahitaji ya Kata ya Mbagala Kuu ni mengi na
hivyo Manispaa ya Temeke haiwezi kukidhi
mahitaji hayo peke yake, ninaamini hakuna
sababu ya kuwaacha Wanafunzi wetu
wakiteseka.
Sitapeleka malalamiko, jitihada zangu zote
kwenda Manispaa ya Temeke kurekebisha
mapungufu yanayo ripotiwa na takwimu kwa
shule za msingi, na kufanya mazingira ya
Wanafunzi wa shule ya
Sekondari kuwa mazuri ili waweze kujifunza kwa amani. Ndani ya miezi 12 baada ya mimi
kuchagukliwa, pia kutoka kwenye rasilimali za familia yangu na marafiki nitakusanya
rasilimali zaidi ambazo:(a) Ndani ya miezi 24 baada ya kuchaguliwa tutakuwa na Shule za Serikali
zenye vifaa bora na
(b) Ndani ya miezi 36 baada ya mimi kuchaguliwa, tutaweza kuvutia walimu bora ili
tujenge Wanafunzi bora si tu kwa Tanzania bali hata kwa Afrika Mashariki
nzima. Nitahakikisha kila mwaka nitachangia si chini ya shilingi milioni 200 kushu
ghulikia hili ndani ya miaka 5.

13. Kusimamia ongezeko la watu:


Nimeeleza kuwa tuna tatizo la idadi ya wakazi, mimi kama Diwani wenu pamoja
na jitihada zote nitakazo weka, tusipo simamia uhamiaji katika kata yetu bado
tutajikuta baada ya miaka 5 hatuoni Maendeleo.
Endapo nitachaguliwa, ndani ya siku 90 nitahakikisha kuwa kuna vitambulisho muhimu
kwa wakazi wote wa sasa wa Mbagala Kuu na Kamati za Ndani zitaanzishwa kusimamia, na
kupitia maombi wa wakazi wapya watakao penda kuhamia katika Kata yetu. Nina amini
kwa dhati kabisa, kwamba ili kuhakikisha maendeleo tunayo yataka tunayafikia ndani ya
miaka mitano inatubidi kusimamia uwiano wa wakazi katika eneo letu maana yake ni
kwamba idadi ya watu wanaohamia katika Kata yetu walingane na wale wanao hama
kutoka kwenye Kata yetu, na pia watu watakao ruhusiwa kuhamia katika Kata yetu waje na
faida kwenye Kata yetu. Pia kuhakikisha watu wanaohamia wanawiana na miundo mbinu
iliyopo katika shule, barabara, maji n.k.

amoja na kwamba mambo niliyoelezea hapo juu


sio matatizo pekee niliyopata malalamiko yake
kutoka Mbagala Kuu, na sio matatizo pekee
Charles Alex Sahim
N12345678
nitakayo yafanyia kazi kwa sababu ninaelewa
0000 0000 0000 0000
shauku ya kutaka kuleta maendeleo kwa watu
wapatao 43,000 itahitaji kupiga mahesabu na
Mtaa: Maturubai , Nyumba No. XX
Madiwani wenzangu kama nikichaguliwa ambapo
MFANYA BIASHARA
nitakuwa katika nafasi nzuri zaidi kuliko kuwapa
mategemeo
matupu.
Mimi nina amini katika uwezeshaji na sio misaada; kwangu mimi wakazi wote wa
Mbagala Kuu wako sawa na sitagawa misaada binafsi, na nawaomba msitegemee
hilo kutoka kwangu, ila badala yake nitatengeneza mfuko wa dharura wa shilingi
milioni 100, na mtu yeyote mwenye dharura ataweza kutuma maombi Kwenda kwa
Uongozi wa mfuko huo.
MBAGALA KUU

KITAMBULISHO CHA MAKAZI

Naomba mkumbuke kwamba ningependa tuwahimize Wabunge wetu watuwakilishe


kuhakikisha tunapata kwenye Kata yetu rasilimali tunazo zihitaji.
Tukumbuke kwamba mshahara na posho anazopata kama Mbunge ni kwa ajili yake
yeye na familia yake. Kama akijitosheleza nyumbani kwake basi hata kuwa na sababu
ya kutokuja katika Kata yetu na kunisaidia kutatua matatizo ya Maendeleo yanayotu
kumba.

10

Jina Langu ni Yusuf Manji,


Ninawaomba kura zenu zenye thamani kubwa
kwenye uchaguzi huu mnichague kama Diwani wenu
wa kata ya Mbagala Kuu, Wilaya ya Temeke,
Dar Es Salaam.

Pia ninawaomba muwapigie kura Madiwani na


Wabunge kupitia tiketi ya CCM sio tu kwa
Dar Es Salaam pekee ambao tutapigiwa kura tarehe 25
Oktoba, 2015 ili na mimi nifanye kazi na viongozi waliochaguliwa
kama timu moja. Kama ilivyo katika mpira mchezaji mmoja sio timu nzima, hivyo tumpigie
kura Mgombea Urais wa chama changu Dr. John Pombe Magufuli, ili nitakapo kutana na
tatizo ndani ya timu ya CCM nitaweza kwenda kwa Rais wangu wa CCM na tukaelewana
kiurahisi zaidi kitu ambacho chama cha upinzani kinaweza kuchukua muda mrefu kuelewa.
Nimekuwa nikisika watu wakisema uchaguzi huu wanataka mabadiliko, na inanifanya
nijiuelize, mabadiliko kutoka wapi kwenda wapi; Tanganyika ilipopata uhuru mwaka 1961
idadi ya wakazi wake ilikuwa nchini ya milioni 10 kutoka makabila mbalimbali, ikiwa na
barabara chache, kiwango cha elimu cha chini ya 20% wakati nchi nyingi za Afrika zikiwa
bado ziko chini ya ukoloni. Ndani ya miaka 50 ambayo CCM imekuwa serikalini, idadi ya
watu imeongezeka na kufikia milioni 55 kutokana na huduma bora za wakina mama
wajawazito, mkoa wa Dar Es Salaam peke yake umekua kutoka wakazi 100,000 kipindi cha
uhuru na sasa kufikia watu zaidi ya milioni 5, shule zikiongeza kiwango cha elimu kwa zaidi
ya 80%, maelfu ya kilomita za barabara, imewakomboa majirani zake wengi kutoka kwenye
ukoloni na kwa wakati huo huo kuondoa ukabila na ubaguzi wa kidini.
Mimi ninavyodhani uchaguzi huu hauhitaji mabadiliko bali unahitaji Maendeleo endelevu
kwa kasi kubwa na ili hilo litendeke tunahitaji timu ya viongozi kuanzia ngazi ya chini ya
Udiwani ambayo mimi ninawania hadi ngazi za juu kabisa zikifanya kazi kuelekea njia moja
ya kuleta Maendeleo ya kasi.
Ninadhamira ya Kata ya Mbagala Kuu kuwa Kata bora kwenye mji wa Dar Es Salaam, Dar Es
Salaam kuwa mji bora Tanzania na Tanzania kuwa nchi bora Afrika na kwa sababu hiyo
ninawaomba kura zenu si tu kwa nafasi yangu kama Diwani, bali kwa timu nzima ya CCM,
kama ilivyo kwenye mpira ushindi wa haraka unakuja kwa kufanya kazi kama timu na si kwa
ushindi wa mchezaji mmoja.

11

TEAM CCM DAR ES SALAAM

Mh. JOHN POMBE MAGUFULI


MGOMBEA URAISI

Mh. IDDI AZZANI


UBUNGE- KINONDONI

Mh. ABBAS MTEMVU


UBUNGE - TEMEKE

Mh. MUSSA ZUNGU


UBUNGE - ILALA

Mh. FAUSTINE NDUNGULILE


UBUNGE - KIGAMBONI

Mh. JERRY SILAA


UBUNGE - UKONGA

Mh. ISSAH MANGUNGU


UBUNGE - MBAGALA

Mh. BONA KALUWA


UBUNGE - KIPAWA

Mh. DIDAS MASABURU


UBUNGE - UBUNGO

Mh. KIPPI WARIOBA


UBUNGE - KAWE

Mh. FENERA MUKANGARA


UBUNGE- KIBAMBA

KINONDONI

Mh. HAMZA ABBAS FARAHANI


MGOMBEA UDIWANI - KINONDONI

Mh. JULIAN R. BUGUJO


MGOMBEA UDIWANI - MAGOMENI

Mh. JOSEPHINA AIDAN WAGE


MGOMBEA UDIWANI - HANANASIFU

Mh. KHERI S. MISSINGA


MGOMBEA UDIWANI - BUNJU

Mh. GODFREY MHELUKA


MGOMBEA UDIWANI - KIMARA

Mh. KEVIN WILIAM MBOGO


MGOMBEA UDIWANI - MBEZI JUU

Mh. SUZAN MASSAWE


MGOMBEA UDIWANI - MABWEPANDE

Mh. MWAKALILA KUMBUKA


MGOMBEA UDIWANI - GOBA

Mh. YUSUPH OMARY YENGA


MGOMBEA UDIWANI - MBURAHATI

Mh. SONGORO HAMIS MNYONGE


MGOMBEA UDIWANI - M/NYAMALA

Mh. MANYAMA GEORGE


MGOMBEA UDIWANI - KIGOGO

Mh. ITEBA WILLIAM CHARLES


MGOMBEA UDIWANI - MAKONGO

Mh. HASHIM M. MBONDE


MGOMBEA UDIWANI - MBWENI

Mh. ANNA JOSEPH LUVANDA


MGOMBEA UDIWANI - WAZO

Mh. RAJAB SULEIMAN HASSAN


MGOMBEA UDIWANI - MAKURUMLA

Mh. HAJI MAKAME MNYAA


MGOMBEA UDIWANI - MAKUMBUSHO

Mh. TAMIM O. TAMIM


MGOMBEA UDIWANI - TANDALE

Mh. BERNARD LWEHABURA ONYERA


MGOMBEA UDIWANI - MIKOCHENI

Mh. THADEY SIMAMAKA MASSAWE


MGOMBEA UDIWANI - NDUGUMBI

Mh. BENJAMIN KAWE SITTA


MGOMBEA UDIWANI - MSASANI

Mh. MDOE HAROUN YUSUF


MGOMBEA UDIWANI - SARANGA

Mh. RAPHAEL NYANGI AWINO


MGOMBEA UDIWANI - SINZA

Mh. KASSIM MHAMADU LEMA


MGOMBEA UDIWANI - MABIBO

Mh. MOHAMED A. CHAMBUSO


MGOMBEA UDIWANI - MZIMUNI

Mh. FRANK KALOKOLA KAMUGISHA


MGOMBEA UDIWANI - KIJITONYAMA

Mh. WILLIAM M. MLEGE


MGOMBEA UDIWANI - UBUNGO

Mh. AYOUB RAMADHAN SEMVUA


MGOMBEA UDIWANI - KIBAMBA

Mh. OLIVERY QUIRINE SHIRIMA


MGOMBEA UDIWANI - MAKUBURI

Mh. ABDULAKARIM RASHID ATIKI


MGOMBEA UDIWANI - MANZESE

Mh. SIRAJU HASSAN MWASHA


MGOMBEA UDIWANI - MSIGANI

Mh. MUTTA ROBERT RWAKATARE


MGOMBEA UDIWANI - KAWE

Mh. MWANASHAHA HASSAN


MGOMBEA UDIWANI - MBEZI

Mh. URION MICHAEL JOSEPHAT


MGOMBEA UDIWANI - KUNDUCHI

Mh. ABEID JUMANNE KOKIOTI


MGOMBEA UDIWANI - KWEMBE

JIMBO LA TEMEKE

Mh. VICTOR M. MWAKASINDILE


MGOMBEA UDIWANI - MAKANGARAWE

Mh. RAPHAEL JAMES LUANDA


MGOMBEA UDIWANI - BUZA

Mh. AMIRI BAKARI SALUM


MGOMBEA UDIWANI - KILAKALA

Mh. KENNY DICKUSI MAKINDA


MGOMBEA UDIWANI - YOMBO VITUKA

Mh. WILFRED MORIS KIMATI


MGOMBEA UDIWANI - KURASINI

Mh. JUDITH BONIFACE MAGEMBE


MGOMBEA UDIWANI - MTONI

Mh. HAMIS ABDALLAH MZUZURI


MGOMBEA UDIWANI - AZIMIO

Mh. FRANCIS SAMSON MTAWA


MGOMBEA UDIWANI - KEKO

Mh. NOEL LUKAS KIPANGULE


MGOMBEA UDIWANI - CHANGOMBE

Mh. FEISAL SALUM HASSAN


MGOMBEA UDIWANI - TEMEKE 14

Mh. ABEL WILBARD TARIMO


MGOMBEA UDIWANI - SANDALI

Mh. RAMADHAN LUKIMANGIZA


MGOMBEA UDIWANI - TANDIKA

Mh. JUMA RAJAB MKENGA


MGOMBEA UDIWANI - MIBURANI

JIMBO LA KIGAMBONI

Mh. DOTTO MSAWA


MGOMBEA UDIWANI - KIGAMBONI

Mh. AMINA ALLY HAMISI


MGOMBEA UDIWANI - TUNGI

Mh. ZACHARIA J. MKUNDI


MGOMBEA UDIWANI - VIJIBWENI

Mh. HENRY LAZARO CHAULA


MGOMBEA UDIWANI - MJIMWEMA

Mh. AMIRI MZURI SAMBO


MGOMBEA UDIWANI - KIBADA

Mh. FRANCIS MASANJA CHICHI


MGOMBEA UDIWANI - SOMANGILE

Mh. ISSA HEMED ZAHORO


MGOMBEA UDIWANI - KISARAWE II

Mh. MAABAD SELEMAN HOJA


MGOMBEA UDIWANI - PEMBA MNAZI

Mh. MUHIDIN SANYA BUHAYA


MGOMBEA UDIWANI - KIMBIJI

JIMBO LA MBAGALA

Mh. MOHAMED SELEMAN MKETO


MGOMBEA UDIWANI - TOANGOMA

Mh. ABDALLAH MTINIKA


MGOMBEA UDIWANI - KIBONDEMAJI

Mh. YUSUF M. MANJI


MGOMBEA UDIWANI - MBAGALA KUU

Mh. ANDERSON SAMWEL CHALE


MGOMBEA UDIWANI - KIJICHI

Mh. HEMED JUMA KARATA


MGOMBEA UDIWANI - CHAMAZI

Mh. SAID FELLA


MGOMBEA UDIWANI - KILUNGULE

Mh. ABDALLAH JAFARI CHAUREMBO


MGOMBEA UDIWANI - CHARAMBE

Mh. TITTO ELIAKIM OSSORO


MGOMBEA UDIWANI - KIBURUGWA

Mh. RAMANDANI ZAME


MGOMBEA UDIWANI - MBAGALA

Mh. SAMINA PATRICK MASHAIRI


MGOMBEA UDIWANI - MIAZINI

JIMBO LA ILALA

Mh. ABDULKARIM SALUM MASAKI


MGOMBEA UDIWANI - KARIAKOO

Mh. TUMIKE MALILO


MGOMBEA UDIWANI - BONYOKWA

Mh. NYASIKA G. MOTEMA


MGOMBEA UDIWANI - KIVULE

Mh. KHERI MOHAMED KESSY


MGOMBEA UDIWANI - KISUTU

Mh. PERFECT EUGEN MASAWE


MGOMBEA UDIWANI - SEGEREA

Mh. MOAHMED R. MSOPHE


MGOMBEA UDIWANI - KIPUNGUNI

Mh. FATUMA A. ALLY


MGOMBEA UDIWANI - GEREZANI

Mh. BATULI M. MZIYA


MGOMBEA UDIWANI - MNYAMANI

Mh. IMELDA T. SAMJELA


MGOMBEA UDIWANI - PUGU

Mh. MARIAM MOHAMED


MGOMBEA UDIWANI - MCHAFUKOGE

Mh. AZIMKHANA A.AZIMKHAN


MGOMBEA UDIWANI - MCHIKICHINI

Mh. SUDI K. SUDI


TABATA

Mh. LUKAS MUNOBI RUTAINURWA


MGOMBEA UDIWANI - GONGO LA MBOTO

Mh. SULTAN A. SALIM


MGOMBEA UDIWANI - UPANGA MASHARIKI

Mh. LEAH B. MGITU


MGOMBEA UDIWANI - KINYEREZI

Mh. TWAHA S. MALATE


MGOMBEA UDIWANI - BUYUNI

Mh. RUKIA MWENGE


MGOMBEA UDIWANI - KIMANGA

Mh. KINGULA M. HASSAN


MGOMBEA UDIWANI - MAJOHE

Mh. SAADY M. KHIMJI


MGOMBEA UDIWANI - ILALA

Mh. ADNAN KONDO


MGOMBEA UDIWANI - UPANGA MAGHARIBI

Mh. GODLISTEN O. MALISA


MGOMBEA UDIWANI - MIREFU

Mh. DEOGLAS O.MASABURI


MGOMBEA UDIWANI - CHANIKA

Mh. BONVENTURE G. MWAIPAJA


MGOMBEA UDIWANI - KIWALANI

Mh. ABDALLAH S. MPATE


MGOMBEA UDIWANI - ZINGIZIWA

Mh. HENRY MASABA


MGOMBEA UDIWANI - KIVUKONI

Mh. YUSUPH M. LIMA


MGOMBEA UDIWANI - KIPAWA

Mh. LUCY J.LUGOME


MGOMBEA UDIWANI - KISUKURU

Mh. MWALILE A. JAFFARI


MGOMBEA UDIWANI - MSOGOLA

Mh. BARUA A. MWAKILANGA


MGOMBEA UDIWANI - BUGURUNI

Mh. JOB I. IBRAHIM


MGOMBEA UDIWANI - MZINGA

Mh. PETER JOSEPH KARIA


MGOMBEA UDIWANI - LIWITI

Mh. EVA M. NYAMOYO


MGOMBEA UDIWANI - KITUNDA

Mh. YOHANA A. NGONGA


MGOMBEA UDIWANI - PUGU STATION

Mh. ASSA S. HAROUN


MGOMBEA UDIWANI - VINGUNGUTI

Mh. HARUNA H. BATENGA


MGOMBEA UDIWANI - UKONGA

Mh. ABDALLAH FARAJI


MGOMBEA UDIWANI - JANGWANI

12

You might also like