You are on page 1of 3

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


PRESIDENTS OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA
ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.

Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail:
ikulucommpress@googlemail.co
m
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425

Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete amewateua wakuu wa wilaya wapya 13
na kuwahamisha vituo vya kazi wengine saba.
Wakuu wa wilaya 13 walioteuliwa ni Shaaban Athuman
Ntanambe ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mkoa wa
Kagera; Thabisa Mwalapwa ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya
ya Hanang, Mkoa wa Manyara;

Richard Kasesera ambaye

anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mkoa wa Iringa, Ruth


Msafiri ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Mkoa wa
Kigoma na Abdallah Njwayo ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya
ya Kilwa, Mkoa wa Lindi.
Wakuu wa Wilaya wengine wapya ni Asumpta Mshama
ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Wangingombe, Mkoa wa
Njombe; Mohammed Mussa Utaly ambaye anakuwa Mkuu wa
Wilaya ya Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma; Dauda Yasin ambaye
anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Makete, Mkoa wa Njombe;

Honorata Chitanda ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara,


Mkoa wa Kagera; Vita Kawawa ambaye anakuwa Mkuu wa
Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga na Christopher
Ngubyagai ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkalama,
Mkoa wa Singida.
Wakuu wengine wapya ni Hawa Nghumbi ambaye
anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mkoa wa Shinyanga na
Mrisho Gambo ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Uvinza,
Mkoa wa Kigoma.
Wakuu wa wilaya waliohamishwa vituo vya kazi ni Fadhili
Nkurlu ambaye anatoka Mkalama, Mkoa wa Singida kwenda
Wilaya ya Arusha, Mkoa wa Arusha; Wilson E Nkambaku
ambaye anahamishiwa Arumeru, Mkoa wa Arusha kutoka
Kishapu, Mkoa wa Shinyanga; Francis Miti ambaye anahama
Wilaya ya Hanang, Mkoa wa Manyara kwenda Monduli, Mkoa
wa Arusha na Jowika Kasunga ambaye anahamia Wilaya ya
Mufindi, Mkoa wa Iringa kutoka Monduli .
Wengine waliohamishwa ni Muhingo Rweyemamu kutoka
Wilaya ya Makete, Mkoa wa Njombe kwenda Wilaya ya
Morogoro; Hadija Nyembo ambaye anahamia Wilaya ya Kaliua,
Mkoa wa Tabora kutoka Uvinza, Mkoa wa Kigoma na Benson
Mpyesya ambaye anahamia Wilaya ya Songea, Mkoa wa Ruvuma
kutoka Kahama.
Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,


Ikulu,
DAR ES SALAAM.
04 Oktoba, 2015

You might also like