You are on page 1of 3

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


JESHI LA POLISI TANZANIA

YAH: TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA DODOMA KWA


VYOMBO VYA HABARI TAREHE 26/09/2015
Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma linamshikilia Mgombea wa
Ubunge kwa tiketi ya Chadema BENSON KIGAILI SINGO na
wenzake kumi (10) kwa tuhuma za KUFANYA MAANDAMANO BILA
KIBALI NA KUZUIA WATUMIAJI WENGINE wa
BARABARA
KUSHINDWA KUENDELEA NA SHUGHULI ZAO, KUMSHAMBULIA
ASKARI,KUFANYA FUJO KITUONI NA KUTUKANA ASKARI.
Matukio hayo yalitokea majira ya saa 18:45 katika barabara
ya Jamatini na Kituo Kikuu cha Polisi baada ya Mgombea huyo
kumaliza mkutano wake wa kampeni katika eneo la stendi kuu ya
Dodoma.
Pamoja na kupewa maelekezo na askari kuacha maandamno
hayo ili watu wengine waweze kuendelea na shughuli zao,
walikaidi na kuanza kutoa matusi na kumshambulia askari kwa
chupa
ya
soda
jambo
ambalo
linaonyesha
walikuwa
wamedhamiria kwa sababu inakuwaje watembee na chupa tupu
za soda. Na kama hiyo haitoshi walipofika kituoni walianza
kufanya fujo na kutoa matusi kwa askari.
Watuhumiwa wanaoshiliwa ni wafuatao:1. BENSON
KIGAILA
SINGO,
MIAKA
46,
Mkazi
wa
Ipagala/Kibakwe.
2. KHADIJA MAULA, MIAKA 40, MFANYABIASHARA WA
NKUHUNGU
3. STELLAH MASSAWE, MIAKA 38, MFANYABIASHARA MKAZI WA
AIRPORT
4. GODFREY CHARLES MANYANYA, MIAKA 29 MWENYEKITI WA
VIJANA CHADEMA MKOA WA DODOMA, MKAZI WA AREA E.

5. HASHIMU SELEMAN KILAINI, MIAKA 45, MFANYABIASHARA


MKAZI WA AIR PORT DODOMA.
6. ALEX NICHOLAUS THOMAS, MIAKA 28, MFANYABISAHARA
MKAZI WA CHAMWINO.
7. PRISCA BAKARI MGAZA, MIAKA 20, MFANYA BIASHARA MKAZI
WA MAKOLE.
8. LUCKYSON KWEKA, MIAKA 28, MWANAFUNZI, MKAZI WA
MAILI MBILI.
9. AISHA MAKWE URIO, MIAKA 22, MWANAFUNZI MKAZI WA
AREA D
10.
POMPEY
MNYALAPE
REMIJO,
MIAKA
40,
MFANYABIASHARA MKAZI WA AREA C.
11.
LAWI NGAMBIE TUMUZA, MIAKA 52, MPIGAPICHA MKAZI
WA AREA E.
Askari aliyeshambuliwa alipelekwa General Hospital kwa
matibabu.
Nitoe wito tena kwa Wagombea wa Vyama vyote na
wananchi wa Dodoma kwa ujumla watii sheria bila shuruti kwani
umaarufu hautafutwi kwa kuvunja sheria na watambue kufanya
hivyo ni kosa la jinai. Watambue hakuna haki isiyokuwa na wajibu.
Pia wanapokwenda na kutoka kwenye mikutano waache
kufanya maandamano na hata watumiapo barabara wazingitie
sheria za usalama barabarani ili watu wengine waweze kuendelea
na shughuli zao bila bughudha au vitisho.
Aidha zipo taarifa kuwa kuna baadhi ya Wanachama na
wafuasi
wa
Chadema
wanapita
sehemu
mbalimbali
wanahamasisha watu kwenda Kituo Kikuu cha Polisi kushinikiza
waliokamatwa waachiliwe kabla ya taratibu za kisheria
hazijakamilishwa. Watambue atakayefanya hivyo ajue atakabiliwa
vilivyo na mkono wa sheria.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma litaendelea kuwachukulia
hatua kali kwa mujibu wa sheria wale wote watakaokiuka sheria
bila kujali ana wadhifa gani.
Imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma
Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi MISIME D.A
(SACP).

You might also like