You are on page 1of 3

3/06/2015

TAMKO KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA BAJETI YA AFYA, KASMA YA UZAZI WA
MPANGO.
Wito kwa Serikali kuongeza bajeti ya Uzazi wa Mpango kwa ajili ya kutoa Mafunzo
kwa Watoa Huduma ya Uzazi wa Mpango
BAJETI YA UZAZI WA MPANGO
Mahitaji ya kifedha kwa ajili ya kuhakikisha upatikanaji wa huduma na njia za uzazi wa mpango
Tanzania kwa mwaka ni shilingi bilioni 20. Tangu kuanzishwa kwa kasma maalum ya uzazi wa
mpango katika bajeti ya afya, mwaka 20101, mwenendo wa fedha katika eneo hili umekuwa
haukidhi mahitaji halisi. Kwa kiasi kikubwa, wahisani ndio hugharimia sehemu kubwa ya mahitaji
haya. Ili kufikia dhamira ya Tanzania kuongeza upatikanaji na matumizi ya huduma hizi kufikia
asilimia 60 mwaka 2015, ni lazima uzazi wa mpango uwe ni kipaumbele katika sekta ya afya.
Mwaka wa fedha wa 2015/2016, serikali inatarajia kuweka bilioni 1.64 tu katika ununuzi wa njia
za uzazi wa mpango (8.2% ya mahitaji halisi kwa mwaka). Ifahamike pia kuwa nchi
imehakikishiwa upatikanaji wa njia ama dawa za uzazi wa mpango kwa miaka miwili mwaka
2015 na 2016. Lakini kuwa na uhakika huu bila ya kuwekeza pia katika watoa huduma za uzazi wa
mpango ni changamoto inayostahili hatua za haraka.
Kwa mujibu wa Hotuba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Bungeni, 2/06/2015, Tanzania ina
upungufu wa Watoa Huduma za Afya wa asilimia 58. Hali kadhalika, upungufu huu unaonekana
kuwa mkubwa zaidi wanapoangaliwa watoa huduma za uzazi wa mpango. Watoa huduma wenye
ujuzi wa kutoa huduma hizi ni wachache. Dhamira ya serikali kuwa na watoa huduma walau
wawili (2)2 katika kila kituo cha afya bado haijafikiwa, na katika ngazi za zahanati, tatizo ni kubwa
zaidi.
Wakati matumizi ya huduma za uzazi wa mpango (yaani Contraceptive Prevalence Rate)
yakiongezeka kwa takribani asilimia mbili (2) mpaka tatu (3) kila mwaka, umuhimu wa
kuhakikisha Tanzania inao watoa huduma wa kutosha katika njia zote za uzazi wa mpango lazima
utiliwe mkazo. Bila kuhakikisha bajeti ya ununuzi wa dawa ama njia za uzazi wa mpango
vinaendana na kuhakikisha watoa huduma pia wapo kuzifikisha huduma, serikali itaingia hasara
kwa dawa/ njia hizi kupitwa na muda wake wa matumizi (to expire) bila kuwafikia watumiaji.
Tayari Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kupitia Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto
(Reproductive and Child Health Section) wameweka mfumo wa kufuatilia utoaji mafunzo kwa
wahitimu. Wizara, bila kuwategemea wadau, ihakikishe inawatumia ipasavyo wakufunzi wake
katika kutoa matunzo ya kada mbalimbali za watoa huduma ya afya, ili waweze kutoa huduma za
uzazi wa mpango katika ngazi zote. Jambo hili lazima liendane na kuelekeza rasilimali stahiki
katika bajeti ya afya ya 2015/2016.
1

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Fungu no. 52; Kifungu 3001, Idara ya Kinga, Kifungu Kidogo 220408
National Roadmap Strategic Plan to Accelerate Reduction of Maternal, Newborn and Child Deaths in Tanzania
2008 2015 (Sharpened One Plan)
2

Ukurasa | 1
United Nations Association of Tanzania | bringing people closer to the UN

3/06/2015

UMUHIMU WA HUDUMA YA UZAZI WA MPANGO KATIKA AFYA YA MAMA NA MTOTO


Tanzania ni mojawapo ya nchi zenye viwango vikubwa vya vifo vya wanawake vitokanavyo na
uzazi. Utafiti wa Afya na Idadi ya Watu wa mwaka 2010 nchini Tanzania (Tanzania Demographic
and Health Survey DHS 2010) unaonesha kwamba kulikuwa na vifo vya wanawake 454 kwa kila
vizazi hai 100,000 kila mwaka. Kwa wastani, idadi hiyo ilikuwa sawa na takribani vifo:
8,500 kwa mwaka,
708 kwa kila mwezi,
23 kwa kila siku, au
takribani kifo kimoja (1) kwa kila saa.
Kufikia mwaka 2013, vifo hivyo vilipungua kwa kiwango kidogo sana hadi kufikia kiasi cha 410
kwa kila vizazi hai 100,0003 ambayo kwa wastani ilikuwa sawa na vifo:
7,900 kwa mwaka,
658 kwa kila mwezi,
22 kwa kila siku, au
takribani kifo kimoja (1) kwa kila saa.
Wakati huo huo, Tanzania ilikuwa imekusudia kupunguza vifo hivyo kutoka kiwango cha
454/100,000 cha mwaka 2010 hadi kufikia 193/100,000 mwaka 2015 ambayo ingekuwa sawa na
takribani vifo:
2,100 kwa mwaka,
175 kwa kila mwezi,
6 kwa kila siku, au
kifo kimoja (1) kila baada ya saa 4.
Hata hivyo, Tanzania ni mojawapo ya nchi ambazo hazijaweza kuwa na ufanisi wa kuridhisha
katika lengo hili ambalo linaenda sambamba na Lengo la tano (5) la Milenia (MDG 5). Suala ya
uwekezaji wa rasilimali kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango kwa
kila anayezihitaji ni kati ya changamoto zilizochangia kukosekana kwa ufanisi huo. Kwa mfano,
wakati bajeti ya huduma hizo kwa mwaka wa fedha wa 2014/15 ilifikia shilingi Bilioni 4.64 (23.2%
ya mahitaji halisi kwa mwaka), kwa mwaka wa fedha wa 2015/16 serikali inakusudia kuweka
shilingi Bilioni 1.64 (8.2% ya mahitaji halisi). Hatua hii ni ya kushtusha na inarudisha nyuma
matokeo muhimu ya kimaendeleo ambayo nchi ilikuwa imeanza kuyafikia.
United Nations Association of Tanzania na Health Promotion Tanzania kupitia mradi wa Advance
Family Planning (AFP), tunajishughulisha na utetezi kwa lengo la kuchangia katika kupunguza vifo
vya wanawake vitokanavyo na uzazi hapa Tanzania. Mradi huu unaunga mkono juhudi za serikali
pamoja na wadau wengine wa afya juu ya namna ya kufanikisha utekelezaji wa Sera, Mipango, na

World Health Organization (WHO, 2013)

Ukurasa | 2
United Nations Association of Tanzania | bringing people closer to the UN

3/06/2015

Mikakati mbalimbali ya kupunguza vifo hivyo ambayo pia imeainishwa katika Malengo ya Milenia
(MDG 5).
Mipango na Mikakati ya serikali yetu inayohusisha malengo ya kupunguza vifo vya wanawake
vitokanavyo na uzazi ni pamoja na:
Sera ya Afya ya 2007, yaani National Health Policy, 2007,
Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya (HSSP III, 2009 -2015), au Health Sector Strategic Plan
III
Dira ya Taifa ya Kuharakisha Kupunguza Vifo vya Wanawake, Watoto Wachanga, na
Watoto (2008-2015) yaani National Road Map Strategic Plan to Accelerate Reduction of
Maternal, Newborn and Child Deaths in Tanzania, 20082015 (One Plan),
Mpango Uliokasimiwa wa Utekelezaji wa Huduma za Uzazi wa Mpango (2010 2015), au
National Family Planning Costed Implementation Plan (NFPCIP), na
MKUKUTA II (2010-2015) yaani National Strategy for Growth and Reduction of Poverty II
(NSGRP II)
Sera, mipango, na mikakati hii ndiyo inayoainisha lengo la taifa la kupunguza vifo hivyo kwa kuwa
vifo hivyo vinazuilika kwa kuhakikisha upatikanaji wa njia za uzazi wa mpango na dawa za uzazi
salama. Tafiti zinaonyesha kwamba uzazi wa mpango unaweza kuzuia vifo hivyo kwa takribani
44%. Uzazi wa mpango huwasaidia wanawake na familia kupanga wakati, nafasi, na idadi ya
watoto wanaotaka kuwazaa ili kuwapatia malezi bora. Dawa za uzazi salama huwawezesha
wataalamu wa afya kuwapatia wanawake huduma muhimu za kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi
wakati wa kujifungua.
Pamoja na hayo, uzazi wa mpango ni njia ya uhakika ya kutekeleza mipango ya maendeleo kwani
huwezesha taifa kujipanga vema kwa ajili ya kuweka uwiano unaofaa katika muundo wa idadi ya
watu na ukuaji wa uchumi. Si hivyo tu, bali pia uzazi wa mpango husaidia kuokoa gharama za
huduma za jamii kama vile afya na elimu ili kuwekeza katika uzalishaji kwa kupunguza utegemezi,
pamoja na kuliwezesha taifa kunufaika na idadi ya watu wake kwa kuwaandaa vema kuwa nguvu
kazi yenye tija. Kwa ufupi, uzazi wa mpango ndio ufunguo wa kuifikisha Tanzania katika lengo
lake la kuwa taifa la kipato cha kati kama ilivyotokea kwa mataifa ya Kusini-Mashariki mwa Asia
(Asian Tigers) ambayo katika miaka ya 1960 yalikuwa sawa na Tanzania kimaendeleo.

Imetolewa na:

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na:

United Nations Association of Tanzania,


182 Mzinga Way, Oysterbay,
P.O. Box: 9182,
Dar es Salaam, Tanzania

Robert Kasenene,
Katibu Mkuu Msaidizi na Meneja Mradi,
Simu: +255 764 659554
Anuani Pepe: rkasenene@una.or.tz
Tovuti: www.una.or.tz

Ukurasa | 3
United Nations Association of Tanzania | bringing people closer to the UN

You might also like