You are on page 1of 3

Kuwawezesha Wanawake, Kuwezesha Ubinadamu: Pata Picha!

Shindano la Beijing +20 Pata picha!


Je, unaweza kupata picha itakuwaje iwapo usawa wa kijinsia utafikiwa kikamilifu Tanzania? Je,
unaweza kupata picha ya dunia ambapo wanaume na wanawake, wasichana na wavulana
wanapata fursa sawa bila ubaguzi na ambapo haki zao za binadamu zinaheshimiwa kikamilifu?
Katika tukio la miaka ishirini tangu Azimio la kihistoria la Beijing na Jukwaa la Utekelezaji
unakaribishwa kutoa maoni yako au taarifa juu ya usawa wa kijinsia, haki za wanawake na
uwezeshaji wa wanawake Tanzania.
Utafanya hivyo kwa kupiga picha, kuchora au kwa kutengeneza mchoro ambao kwa namna
fulani unahusiana na usawa wa kijinsia, haki za wanawake na / au uwezeshaji wa wanawake
Tanzania, na Jukwaa la Utekelezaji la Beijing.
Mchoro wako / picha utaoneshwa wakati wa mkutano maalum wa washirika wa maendeleo na
wawakilishi wa Umoja wa Mataifa ambao watachagua washindi. Mshindi atapewa kamera.
Mshindi wa pili atapata fursa ya kutembelea Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulilia
masuala ya Wanawake kwa siku moja. Washiriki wote watapata cheti kilichosainiwa na Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa.
Shindano hili ni kwa ajili wanachama wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa, Yuna au UNA katika
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Jinsi ya Kushiriki
Maombi ya kushiriki yanaweza kuwasilishwa kwa:
Baruapepe: info.tanzania@unwomen.org yenye kichwa Shindano la Pata picha
Posta: Kwenda UN Women/UNDP PO Box 9182 Dar es Salaam
Au kwa mkono: Kuwekwa kwenye kasha katika Ofisi za UN Women, UN House, Plot 182
Barabara ya Mzinga, Oyster Bay, Dar es Salaam

Whats App: +255 682 216 486.


Maombi ya kushiriki lazima yapokelewe kufikia saa 10.30 jioni Jumanne tarehe 31 Machi
2015.
Sheria za Shindano
1. Washiriki lazima wawe wanachama wa Klabu ya Umoja wa Mataifa, Chama cha Umoja
wa Mataifa cha Vijana (YUNA) na / au Chama cha Umoja wa Mataifa Tanzania. Iwapo
atashinda mshiriki atatakiwa kuthibitisha uanachama wake.
2. Ushiriki ni mara moja tu kwa mtu.
3. Maombi yote ya ushiriki lazima yaambatane na fomu ya kushiriki au taarifa ifuatayo: jina
kamili, namba ya simu, barua pepe kama inawezekana, maelezo kuhusu kama ni
mwanachama wa Klabu ya Umoja wa Mataifa (yaani), Yuna au UNA, umri, mahali na
maelezo mafupi kuhusu picha zao / mchoro na jinsi inavyohusiana na mada ya
ushindani.
4. Maombi yote lazima yapokelewe kufikia saa 10.30 jioni Jumanne tarehe 31 Machi 2015.
5. Hakuna vikwazo kuhusu ukubwa wa maingizo, hata hivyo lazima ziwe picha, au mchoro
au chapisho. Zinaweza kuchapwa au kutumwa kwa njia ya kieletroniki kama picha
ambazo zinaweza kuchapwa kwenye printa katika ukubwa wa A4. Ukituma picha kwa
njia ya kielektroniki usisahau kuweka jina unaweza pia ukaweka caption au maelezo
mafupi kwamba ulikuwa unaonesha nini.
6. Maingizo yote yatabaki kuwa mali ya Umoja wa Mataifa Tanzania isipokuwa kama
washiriki wataziomba zirejeshwe.
7. Uamuzi wa majaji ni wa mwisho.

Angalia hapa chini fomu ya kujiunga:

Kuwezesha Wanawake, Kuwezesha Ubinadamu: Pata picha!


Shindano la Beijing +20 Pata Picha!
Fomu Rasmi ya Kujiunga

Jina Kamili:
Umri:
Mahali:
Mimi ni mwanachama wa (tafadhali zungushia): Klabu ya Umoja wa Mataifa

Ipi?

YUNA
UNA
Tafadhali toa maelezo mafupi kuhusu jinsi ingizo lako linahusiana na usawa wa kijinsia,
uwezeshaji wa wanawake, haki za wanawake na / au Jukwaa la Utekelezaji la Beijing

Tafadhali weka tiki Nakubalina na sheria za shindano.

You might also like