You are on page 1of 1

Kujiunga JWTZ

Uandikishaji
Askari
Mtu yeyote ataandikishwa kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa
sifa zifuatazo: -
Awe raia wa Tanzania
Awe na Elimu ya kidato cha nne na kuendelea na awe amefaulu..
Awe hajaoa/hajaolewa
Awe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25
Awe na tabia na mwenendo mzuri
Awe na akili timamu na afya nzuri
Masharti ya Utumishi
Askari atapewa nambari ya utumishi baada ya kufaulu mafunzo ya awali.
Atalitumikia Jeshi kwa kipindi cha mwanzo cha miaka sita, baada ya hapo atafanya kazi kwa
mkataba wa miaka miwili miwili kwa kibali cha Mkuu wa Majeshi.
Maafisa
Bodi ya Uteuzi wa Maafisa (Officers Selection Board)
huwafanyia usaili askari wenye elimu ya kidato cha sita na kuendelea toka Vikosini na Shule za
askari wapya (Recruitment Schools).
Watakaofaulu masailiano hayo hupewa hadhi ya Afisa Mwanafunzi (Officer Cadet), na
hupelekwa Chuoni (Tanzania Military Academy) kwa mafunzo ya uafisa kwa muda wa mwaka
mmoja.

You might also like