You are on page 1of 8

Toleo No.

24 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - Julai 11-17, 2014
Bulletin
News
Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali
kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
au Fika Ofsi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: badra77@yahoo.com
http://www.mem.go.tz
HABARI ZA
NISHATI &MADINI
Hakuna mizengwe
mkataba Statoil, serikali
nNi kampuni ya Serikali Norway, inaendesha shughuli zake kihalali
nMwananchi, Mtanzania, Nipashe, This day waliandika uongo
Mgodi wa Golden Pride wafungwa rasmiUk 2 Habari Katika Picha Uk4-5
2 Bulletin News
http://www.mem.go.tz
NISHATI/MADINI
Hakuna mizengwe mkataba statoil na serikali
Na Mwandishi Wetu
H
ivi karibuni kumekuwapo na taarifa kwe-
nye baadhi ya magazeti kuhusiana na
Kampuni ya utafutaji wa gesi na Mafuta
ya Statoil inayofanya shughuli zake hapa
nchini kwamba zitaliingizia hasara taifa ya shilingi
trilioni 1.6 kila mwaka.
Kwa nyakati tofauti taarifa hiyo iliandikwa na
magazeti ya Nipashe, Mtanzania, Mwananchi na
This Day ambapo yaliandika taarifa juu ya kam-
puni hiyo ya Statoil kwamba Mkataba wa Utafu-
taji na Ugawanaji Mapato (PSA) kati ya Serikali,
TPDC hauna tija kwa taifa.
Habari hiyo kwenye magazeti hayo ilidai
kwamba Kampuni ya Statoil ya Norway katika ki-
talu Na.2 kwenye Bahari Kuu inapata faida kubwa
lakini inaipatia Serikali mapato kidogo na kuamua
kundika habari hiyo yenye vichwa vya habari to-
fauti visemavyo:- Mapato ya Gesi Asilia Tanza-
nia Kulizwa; Tanzania kupoteza Sh. 1.6 trilioni za
Gesi na Mkataba wa Gesi wavuja
Kwa hakika taarifa hizo hazina ukweli hata ki-
dogo kwani ni za upotoshaji, hazikufanyiwa utafiti
wala uchambuzi wa kina na huenda zilitolewa bila
uelewa wa kutosha kuhusu shughuli za utafutaji
mafuta.
Ni muhimu kutambua kwamba baada ya duru
ya tatu ya Zabuni ya kunadi vitalu kukamilika
Mwaka 2007, Serikali ilisaini Mkataba na Kam-
puni ya Statoil kwa ajili ya kutafuta mafuta katika
kitalu Na. 2 kwenye Bahari kuu. Hii ilikuwa mara
ya kwanza kufanyika utafiti katika Bahari kuu ya
Afrika Mashariki (Somalia, Kenya, Tanzania na
Msumbiji). Aidha, maeneo haya hayakuwa na
ugunduzi wa mafuta. Kwa kuwa utafiti wa aina
hiyo ulikuwa unafanyika kwa mara ya kwanza
nchini, Kampuni ya Statoil ilipendekeza kwenye
zabuni yake 2 kuwa, ikiwa itagundua mafuta ipewe
asilimia 95 ya mgawo wa faida na Serikali asilimia
5 kwa ngazi ya kwanza (first tranch). Chini ya uta-
ratibu wa utafutaji mafuta, Kampuni
hiyo inatakiwa kulipia gharama zote
za utafiti na kubeba risks zote za
kutafuta mafuta kwenye Bahari kuu.
Utaratibu huo pia unaainisha kuwa
kama hakitagundulika kitu chochote,
Serikali haitawajibika kuirudishia
Kampuni hiyo gharama ilizotumia
katika utafiti huo.
Aidha, baada ya majadiliano ya
kitaalamu na kina na kulingana na
mazingira yaliyokuwepo wakati ule,
Serikali kupitia Kamati ya Majadil-
iano (GNT) na kwa kutumia Mkata-
ba wa mfano uliokuwepo wakati ule
(Model Production Sharing Agree-
ment MPSA, 2004) makubaliano
yalifikiwa kwamba, ikiwa mafuta
yatagunduliwa, Kampuni ya Statoil
itapata asilimia 70 kama gawiwo la
faida na Serikali asilimia 30 kwa ngazi
ya kwanza na kwamba Kampuni ital-
ipa kodi asilimia 30% kutoka kwenye
gawio lake.
Hata hivyo, Gawiwo hilo la faida
kwa Serikali halihusishi mapato yato-
kanayo na ulipaji wa mrahaba Roy-
alty (asilimia 5), gawiwo kutokana
na ushiriki wa TPDC - Participating
interest (asilimia 10 ), na ushuru wa
huduma - Service levy (asilimia 0.3).
Aidha, Serikali itapata pia kodi kuto-
kana na gawio la Kampuni kwa kiasi
cha asilimia 30.
Mapato haya yote yanalipwa pa-
sipo Serikali kutakiwa kuwekeza
fedha zozote katika shughuli husika.
Uchambuzi uliofanywa na Serikali na
vyombo mbali mbali vya Kimataifa ni
kwamba mkataba huu wa Statoil utali-
patia Taifa gawio la asilimia zaidi ya
61 na Kampuni yenyewe asilimia 39.
Hivyo, si kweli kwamba Tanzania
italizwa na kupoteza Sh. 1.6 trilioni
kama ambavyo magazeti husika yal-
ivyotaka kuupotosha umma wa Wa-
tanzania.
Aidha, nyongeza ya Mkataba (Gas
Addendum) iliyosainiwa Mwaka 2012
kati ya Serikali na Statoil ilitokana na
Mkataba wa Awali kuwa ulihusu shu-
ghuli za Utafutaji na Ugawanaji wa
Mapato ya Mafuta.
Hata hivyo, kwenye Mkataba huo
kuna kipengele kinachoelekeza kuwa
ikiwa gesi asilia itagundulika badala ya
mafuta, basi pande mbili katika Mka-
taba husika zitajadiliana kuhusu nam-
na ya kuendeleza gesi asilia itakay-
ogundulika ikiwemo uthaminishwaji
wa gesi asilia, viwango vya uzalishaji
na ugawanaji mapato, na ujenzi 3 wa
miundombinu ya kufikisha gesi asilia
kwenye soko la ndani na nje.
Bila kusainiwa kwa Mkataba ka-
tika Kitalu Na. 2 kwenye Bahari kuu
kati ya Serikali na Statoil Mwaka,
2007 ugunduzi mkubwa wa gesi asilia
ambao kwa sasa umefikia takriban futi
za ujazo trilioni 50.5 usingefanyika.
Aidha, kusainiwa kwa mkataba
huo kumefungua maeneo mapya ya
utafutaji mafuta, kumewezesha ku-
patikana kwa takwimu za kitaalamu
ambazo hapo awali hazikuwepo,
kumeiingiza Tanzania kwenye ramani
ya dunia katika masuala ya utafutaji
mafuta na kuharakisha maendeleo ya
utafutaji mafuta na gesi asilia.
Serikali kupitia TPDC itaendelea
kuvutia uwekezaji wa ndani na nje ka-
tika shughuli za utafutaji mafuta kwa
maslahi mapana ya nchi yetu.
Serikali itaendelea kuboresha Mi-
kataba ya Utafutaji na Ugawanaji Ma-
pato ili iendane na mazingira yaliyopo.
Mwisho napenda kuviasa vyombo vya
habari na wenye tovuti za kijamii kuz-
ingatia misingi na miiko ya uandishi
wa habari kwa kutoupotosha umma
kwenye masuala ya msingi kuhusu
mustakabali wa nchi yao.
TPDC itaendelea kutoa elimu
kuhusu tasnia ya mafuta na gesi asilia
na Shirika liko tayari wakati wowote
kutoa maelezo ya kina kwa mwa-
nanchi yeyote mwenye lengo la kutaka
kuielewa Sekta Ndogo ya Mafuta na
Gesi Asilia nchini.
Kwa hakika taarifa
hizo hazina ukweli
hata kidogo kwani
ni za upotoshaji,
hazikufanyiwa utafiti
wala uchambuzi
wa kina na huenda
zilitolewa bila
uelewa wa kutosha
kuhusu shughuli za
utafutaji mafuta.
Mgodi wa Golden Pride wafungwa rasmi

Pic 4: Resolute Process Plant

Na Greyson Mwase,
Dar es Salaam
M
godi wa Golden Pride ul-
iokuwa unamilikiwa na
kampuni ya Resolute Tan-
zania Limited umefungwa
baada ya kumaliza shughuli zake za
uchimbaji na usafirishaji wa madini
aina ya dhahabu. Mgodi huo ulian-
zishwa mwaka 1998 ukiwa na mtaji wa
dola za kimarekani milioni 48
Afisa Habari wa Wakala wa Uk-
aguzi wa Madini Nchini (TMMA), Bw.
Yisambi Shiwa alisema katika kipindi
cha miaka 15 ambapo mgodi huo uli-
kuwa ukifanya kazi, ulifanikiwa ku-
zalisha wakia milioni 2.2 za dhahabu
zenye thamani ya Dola za Marekani
bilioni 1.5 na wakia 207,852 za fedha
zenye thamani ya Dola za Marekani
milioni 2.54
Akizungumzia kodi iliyolipwa na
mgodi huo, Bw. Shiwa alisema kuwa
mgodi ulilipa kodi ya mrabaha Dola za
Marekani 47.29, na kodi ya kampuni
(corporate tax) fedha za kitanzania
shilingi bilioni 100.4
Bw. Shiwa alisema kuwa mgodi
huo ulifanikiwa kuajiri wafanyakazi
wa kitanzania 333 na kuongeza kuwa
mgodi huo ulitumia shilingi bilioni 5.86
kwa ajili ya shughuli za kijamii.
Aidha, juhudi zilizofanywa na mgo-
di huo katika utunzaji wa mazingira Bw.
Shiwa alieleza kuwa wakati wa uhai wa
mgodi huo, ulikuwa ukitunza mazingira
na kusisitiza kuwa maeneo yaliyo ka-
ribu na mgodi yamerudishwa katika hali
yake ya asili.
Mgodi ulianza kurudisha uoto wa
Mgodi wa dhahabu wa Golden Pride unaomilikiwa na kampuni ya Resolute Tanzania Limited.
asili wa maeneo yaliyo karibu kwa kuandaa na kupanda miti
mapema, na mpaka sasa uoto umerudi kabisa hali iliyopele-
kea viumbe hai wa asili kurudi. Alisisitiza Bw. Shiwa
Hata hivyo Bw. Shiwa alisema kuwa changamoto ili-
yopo katika maeneo yaliyorudishiwa katika asili yake ni wa-
nanchi kukata miti hovyo iliyopandwa na mgodi huo.
3
Bulletin News
http://www.mem.go.tz
MAONI
Na Veronica Simba
Aliyekuwa Dodoma
M
aaskofu kutoka Makanisa ya
Kipentekoste nchini (CCT)
wamempongeza Waziri wa
Nishati na Madini Profesa
Sospeter Muhongo kwa kuwaelimisha
kwa kina na kwa ufasaha kuhusiana
na masuala ya mafuta, gesi na madini
na kuahidi kuwa mabalozi wazuri kwa
wananchi ili nao waelewe vema kuhusu
rasilimali hizo muhimu kwa taifa.
Pongezi hizo zimetolewa kufuatia
mada iliyowasilishwa hivi karibuni na
Waziri Muhongo mjini Dodoma, katika
Mkutano Mkuu wa Baraza la Maaskofu
wa CCT kuhusu rasilimali za mafuta na
gesi kwa manufaa ya watanzania wote.
Akitoa neno la shukrani kwa Pro-
fesa Muhongo kwa niaba ya Maaskofu
wenzake, Askofu Dkt. Valentino Mok-
iwa wa Kanisa Anglikana, Dayosisi ya
Dar es Salaam alisema Tunashukuru
kwa maelezo ya kitaalamu sana ya Wa-
ziri. Tumetajirishwa sana na ufafanuzi
wa kina alioutoa na kuanzia sasa tut-
akuwa mabalozi wazuri kwa wananchi
kuhusiana na rasilimali hizi.
Mbali na neno hilo la shukrani ku-
toka kwa Askofu Mokiwa, wengi wa
Maaskofu waliokuwa katika mkutano
huo walizungumzia kuridhishwa na
elimu iliyotolewa na Waziri Muhongo
ambapo Askofu Lucas Mbedule kutoka
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT) Mtwara, alimweleza Waziri
bayana kuwa sijawahi kupata maelezo
mazuri ya gesi na mafuta kama uliyoya-
toa. Nitakuwa Balozi kamili sasa.
Akiwasilisha mada katika mku-
tano huo ambao alialikwa kama Mgeni
Rasmi na mmojawapo wa watoa mada,
Profesa Muhongo alisisitiza kuwa rasili-
mali za mafuta na gesi ni lazima ziwan-
ufaishe watanzania wote na kuongeza
kwamba rasilimali hizo, hususan gesi
asilia lazima zinufaishe kizazi cha sasa
na vizazi vinavyokuja.
Alisema utafutaji mafuta na gesi
hapa nchini umeendelea kufanyika kwa
kasi kubwa na umekuwa na mafanikio
makubwa ambapo hivi sasa, kuna jumla
ya leseni 26 za utafutaji zinazotekele-
zwa na makampuni 18.
Akizungumzia suala la uwazi,
Waziri Muhongo alisema maeneo ya
uwekezaji yanatolewa kwa ushindani
na kwamba wawekezaji wazawa wana-
pewa kipaumbele kwa kuwawezesha
kitaaluma na pia katika elimu ya mi-
radi (investment opportunities).
Aidha, alisema kwamba nia ya
Serikali ni kuhakikisha kuwa rasilima-
li hii adhimu inasimamiwa vizuri kwa
manufaa ya nchi na kwa kuhakikisha
hilo kwa sasa fedha za mapato ya gesi
zinaingia Serikalini ambapo mpango
wa kufungua mfuko maalum na ku-
weka mapato yote ya kodi na mrabaha
yatokanayo na mauzo ya gesi asilia
umeainishwa kwenye Sera ya Gesi
Asilia ya mwaka 2013.
Alisema mapato yake yatatumika
kuendeleza sekta mbalimbali za maen-
deleo na kuhifadhiwa kwa vizazi vi-
javyo hasa ikitiliwa maanani kuwa ra-
silimali hii ya gesi asilia itakuja kuisha.
Msingi mkuu ni kuhakikisha kuwa gesi
inanufaisha kizazi cha sasa na vizazi vi-
takavyokuja, alisisitiza.
Kuhusu suala la ushirikishwaji
wazawa, Profesa Muhongo alisema ni
suala muhimu ambapo wananchi wa-
naweza kushiriki kwa kuwekeza mitaji
kwa kuingia ubia na makampuni ya nje
yenye uwezo na uzoefu. Akitoa mfano,
alitaja kampuni ya Swala Oil and Gas
Tanzania Limited ambayo washiriki
wake ni pamoja na wazawa.
Aidha, alisema wananchi wa-
naweza kushiriki kwa kutoa huduma
mbali mbali muhimu (service indus-
tries) kwenye kampuni za utafutaji
mafuta, kununua hisa za makampuni
yanayofanya kazi katika masoko ya mi-
taji, na kwamba baada ya ugunduzi ku-
fanyika viwanda mbali mbali vinaweza
kuanzishwa na wazawa kutumia gesi
kama nishati rahisi au kama malighafi
kwa kuzalisha umeme, mbolea, plastiki,
kwenye magari, kwenye viwanda na vi-
wanda vya kemikali.
Profesa Muhongo alisema nia ya
Serikali ni kuhakikisha kuwa rasilimali
adhimu ya gesi asilia inasimamiwa vi-
zuri kwa manufaa ya nchi, hivyo Shirika
la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC)
litarekebishwa na vyombo vingine
vitaanzishwa ili kukidhi azma ya usi-
mamizi bora.
Alisema, ili kuhakikisha Serikali
inapata pato sahihi, usimamizi wa
gharama za makampuni utaimarishwa.
Waziri Muhongo alizungumzia su-
ala la maadili katika miradi ya Mafuta
na Gesi na kusisitiza kuwa maadili ni
muhimu ili rasilimali husika ziwe na
manufaa kwa Taifa. Alisema maadili
mema ni pamoja na kuwa na ueledi
katika uendeshaji, uzalendo na mfumo
mzuri.
Ueledi na uzalendo unawezesha
kuweka kipaumbele kwa manufaa ya
Taifa ambapo mfumo bora utatokana
na sera bora, sheria bora, kanuni bora,
mikataba mizuri na taratibu nzuri za
uendeshaji, alifafanua Profesa Muhon-
go na kuongeza kuwa Wizara yake im-
ezingatia hayo yote.
Tahariri
MEM
Na Badra Masoud
FIVE
PILLARS OF
REFORMS
KWA HABARI PIGA SIMU
KITENGO CHA MAWASILIANO
BODI YA UHARIRI
MHARIRI MKUU: Badra Masoud
MSANIFU: Essy Ogunde
WAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson Mwase
Teresia Mhagama, Nuru Mwasampeta
INCREASE EFFICIENCY
QUALITY DELIVERY
OF GOODS/SERVICE
SATISFACTION OF
THE CLIENT
SATISFACTION OF
BUSINESS PARTNERS
SATISFACTION OF
SHAREHOLDERS
TEL-2110490
FAX-2110389
MOB-0732999263
M
iongoni mwa habari kubwa zilizoandikwa
kwenye magazeti ya mwishoni mwa wiki
iliyopita pamoja na wiki hii ni taarifa ya
Kampuni ya utafutaji na uchimbaji wa gesi
na mafuta ya Statoil ya Norway kwamba imeingia mka-
taba unaoigandamiza Tanzania na kueleza kwamba Seri-
kali itakuwa inapoteza sh. Trilioni 1.6 kila mwaka katika
mkataba wa utafutaji na ugawanaji wa mapato (PSA).
Naamini kwamba taarifa hii iliwashtua wengi wanaita-
kia mema Tanzania kwani kwa haraka haraka ukiangalia
kiasi hicho cha fedha kilichotajwa na magazeti hayo ni ki-
kubwa hasa ukizingatia taifa hili bado changa na linahitaji
fedha kuweza kukuza uchumi wake.
Habari hiyo kwenye magazeti hayo ilienda mbali kwa
kudai kwamba Kampuni ya Statoil ya Norway katika kita-
lu Na.2 kwenye Bahari Kuu inapata faida kubwa lakini in-
aipatia Serikali mapato kidogo na kuamua kundika habari
hiyo yenye vichwa vya habari tofauti visemavyo:- Ma-
pato ya Gesi Asilia Tanzania Kulizwa; Tanzania kupoteza
Sh. 1.6 trilioni za Gesi na Mkataba wa Gesi wavuja
Napenda kuwasisitiza Watanzania kuwa makini na
baadhi ya taarifa hizo za upotoshaji zinazotolewa na
baadhi ya watu ambao kwa namna moja au nyingine ha-
wakuzifanyia utafiti na hivyo, si kweli kwamba Tanzania
italizwa na kupoteza Sh. 1.6 trilioni kama ambavyo maga-
zeti husika yalivyotaka kuupotosha umma wa Watanza-
nia.
Naamini wengi watakuwa wamesoma taarifa ya
ufafanuzi iliyotolewa na Shirika la Taifa la Mafuta
(TPDC) au pia kusoma habari kubwa iliyoandikwa kwe-
nye gazeti hili ukurasa wa kwanza.
Kimsingi tunafahamu umuhimu wa vyombo vya habari
katika kuhabarisha, kuelimisha na hata kuburudisha laki-
ni lazima taarifa zake zinazoandikwa ziwe sahihi na zenye
ukweli na usioleta madhara lakini taarifa iliyoandikwa na
magazeti yalitajwa haikuwa na ukweli wowote na kwa
namna moja ama nyingine inaweza ikachochea chuki kati
ya Serikali na Wananchi upande mmoja na upande mwin-
gi inaweza ikawakatisha tamaa wawekezaji na hasa ukiz-
ingatia kampuni hii ni ya Serikali ya Norway.
Kwa wanaofahamu taratibu za nchi za Scandinavia
ikiwemo Norway hawapendi kufanya jambo bila kufuata
taratibu na ndiyo maana uwekezaji katika maeneo nyeti
hufanywa na Serikali na si mtu binafsi mfano mwingine
ni katika Kampuni ya usafirishaji umeme ya STATNETT
ambayo nayo inamilikiwa na Serikali na inafanya vizuri.
Kama alivyosema Waziri wa Nishati na Madini Pro-
fesa Sospeter Muhongo wakati akiwasilisha makadirio ya
bajeti ya Wizara kwamba hakuna kutishwa, hakuna kukata
tamaa tuchape kazi ninasisitiza kusema kwamba Serikali
itaendelea kuboresha Mikataba ya Utafutaji na Ugawanaji
Mapato ili iendane na mazingira yaliyopo.
Mwisho napenda kuviasa vyombo vya habari na kwe-
nye mitandao ya kijamii kuzingatia misingi na miiko ya
uandishi wa habari kwa kutoupotosha umma kwenye
masuala ya msingi kuhusu mustakabali wa nchi yao.
Tuache propaganda
kwenye sekta ya gesi
TEL-2110490
FAX-2110389
MOB-0732999263
Maaskofu wampongeza
Profesa Muhongo
Askofu Dkt. Valentino Mokiwa
wa Kanisa Anglikana Dayo-
sisi ya Dar es Salaam akitoa
neno la shukrani kwa Waziri
wa Nishati na Madini Profesa
Sospeter Muhongo (hayupo
pichani) baada ya Waziri huyo
kuwasilisha mada katika
Mkutano wa Maaskofu wa
Makanisa ya Kipentekoste
nchini (CCT).
nWaahidi kuwa mabalozi mafuta, gesi na madini
Statoil yaingia mkataba halali
4 Bulletin News
http://www.mem.go.tz

Matukio katika picha
Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Leseni za Madini, Mhandisi John Nayopa (pichani kulia) akizungumza na Makamishna Wasaidizi wa Madini na
baadhi ya Maafisa Waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini (waliopo kushoto pichani), katika mafunzo ya uboreshaji Mfumo wa Kielektroniki wa
Utoaji na Usimamizi wa Leseni za Madini ujulikanao kama Mining Cadastre.
http://www.mem.go.tz
Mshauri Mwelekezi na
Mwezeshaji kutoka Kam-
puni ya Spatial Dimension ya
Afrika Kusini, Charles Young
akifafanua jambo wakati wa
mafunzo ya uboreshaji wa
Mfumo wa Kielektroniki wa
Utoaji na Usimamizi wa Leseni
za Madini.
Afisa Habari kutoka Wakala
wa Ukaguzi wa Madini Nchini
(TMAA) Bw. Yisambi Shiwa
(kulia) akizungumza na wana-
chi waliotembelea banda la
wakala huo kwenye maone-
sho ya kimataifa ya Saba Saba
5
Bulletin News
http://www.mem.go.tz
Tuzo za madini

Matukio katika picha
Naibu Katibu Mkuu Wiz-
ara ya Nishati na Madini
Mhandisi Ngosi Mwihava
(kushoto ) akimsikiliza
kwa makini mtaalamu wa
mazingira kutoka Wakala wa
Ukaguzi wa Madini Nchini
(TMAA) Bi. Monica Augus-
tino mara alipotembelea
banda hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika
la Madini la Taifa (STAMICO)
Mhandisi Edward Ngonyani
(katikati) akiangalia sampuli ya
madini aina ya dhahabu kwenye
banda la TMAA mara alipotembe-
lea mabanda ya Wizara ya Nishati
na Madini kwenye maonesho ya
kimataifa ya Saba Saba.
Ujumbe wa Tanzania (kushoto) ukiongozwa
na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa-
Sospeter Muhongo (wa nne kutoka kushoto)
wakiwa katika mkutano wa majadiliano ya
kuanzisha kampuni za Ubia za ujenzi wa mi-
undombinu ya kusambaza umeme na ujenzi
wa Mtambo wa kusindika gesi ya Lique-
fied Petroleum Gas (LPG) ambayo itauzwa
kwa wananchi kwa kutumia mitungi. Walio
upande wa kulia ni Waziri wa Nishati na Mi-
godi wa Algeria, Mhe. Youcef Yousfi, (wanne
kutoka kulia) na ujumbe wake.
Waziri wa Nishati na Madini Mhe.
Profesa Sospeter Muhongo Wa
kwanza kulia), akiongea jambo
na wataalamu wa masuala ya
gesi na umeme wa Algeria waka-
ti walipokwenda kutembelea
Mtambo wa kufua umeme kwa
kutumia gesi asilia wa HAMMA
,Mtambo huo wenye uwezo wa
kuzalisha mewagati za umeme
418 unamilikiwa na Serikali ya
Algeria kwa asilimia 100.
Mtaalamu kutoka Idara
ya Madini Andendekyise
Mbije akitoa elimu kwa
mmoja wa wananchi
waliotembelea banda
la Wizara ya Nishati na
Madini wakati wa ma-
onyesho ya kimataifa ya
Sabasaba.
6 Bulletin News
http://www.mem.go.tz
NISHATI
KITWANGA
TAZAMA lipeni fidia kwa wakulima Malolo - KITWANGA
Na Asteria Muhozya, Kilosa
K
ampuni ya kusafirisha mafuta kwa njia ya bomba
kwa nchi za Tanzania na Zambia (TAZAMA),
imetakiwa kuwalipa fidia ya shilingi milioni 327
wakulima wa kijiji cha Malolo, Wilayani Kilosa,
kutokana na athari walizozipata kupitia bomba la mafuta
la shirika hilo kupasuka na kusababisha athari za kimazin-
gira katika baadhi ya maeneo ya kijiji hicho.
Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Nishati na
Madini anayeshughulikia nishati Mhe. Charles Kitwanga
alipokutana na Kamati ya Uongozi wa kijiji cha Malolo
mwishoni mwa wiki.
Mhe. Kitwanga aliwaagiza TAZAMA na uongozi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kufanya majadiliano kati
ya mwezi Julai na Agosti ya namna ya kulipa fidia hiyo
na ifikapo mwezi Septemba mwaka huu fedha hizo ziwe
zimelipwa.
Nataka tatizo hili tulimalize ndani ya kipindi cha
miezi mitatu (3). Hatuwezi kukaa na mgogoro kwa muda
mrefu, lazima uishe. Amesisitiza Kitwanga.
Aidha, aliagiza kuwa, fedha hizo zilipwe na kampuni
hiyo na si serikali hivyo, amewataka TAZAMA na Hal-
mashauri kuhakiki wananchi walioathirika na tukio hilo
na wanaopaswa wapewe fidia yao.
Katika hatua nyingine, wananchi wa Malolo wame-
oneshwa kufurahishwa kwao kutokana na kitendo cha
Mhe. Kitwanga kuonana na kuzungumza nao kuhusu
mgogoro huo na zaidi aliposisitiza walipwe fidia ya
Sh.327 milioni badala ya Sh. Milioni 50 ambazo zilikuwa
zimepangwa zitolewe awali na kampuni hiyo.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mikumi
Ahmed Nahid alimshukuru Mhe. Kitwanga kwa kukubali
kufika kijijini hapo kuwasikiliza wananchi na kutoa majibu
ambayo yatasaidia kumaliza mgogoro huo.
n Awaagiza walipe ifikapo Septemba, 2014
Ziarani Kilosa
GESI ASILIA KUOKOA BIL .200 KWA MWAKA
Na Veronica Simba
I
meelezwa kuwa Taifa lita-
okoa takribani Shilingi Bil-
ioni 202 za Kitanzania kwa
mwaka endapo mradi wa us-
ambazaji wa gesi asilia katika
jiji la Dar es Salaam utatekelezwa.
Hayo yalibainishwa hivi kar-
ibuni mjini Dodoma katika Mku-
tano wa Maaskofu wa Makanisa
ya Kipentekoste (CCT), wakati
Waziri wa Nishati na Madini, Pro-
fesa Sospeter Muhongo akiwasili-
sha mada iliyohusu rasilimali za
mafuta na gesi kwa manufaa ya
Watanzania wote.
Akielezea mradi husika, Wa-
ziri Muhongo alisema lengo kuu
ni kuweka mtandao wa mabomba
ya kusambaza gesi na vituo vya ku-
jazia gesi magari ambapo ulifany-
iwa upembuzi yakinifu mwaka
2006/2007 na kuhusisha magari
8,000 na makazi yapatayo 30,000.
Profesa Muhongo alisema
ujenzi wa mradi huo unatarajiwa
kuanza Julai 2015 ambapo kwa
sasa zoezi la kumtafuta Mkandar-
asi pamoja na fedha za ujenzi
takribani Dola za Marekani mil-
ioni 76 linaendelea.
Aidha, Waziri Muhongo ali-
zungumzia faida iliyopatikana ki-
taifa kwa kutumia gesi asilia kwa
kipindi cha miaka 10 kutoka mwa-
ka 2004 na kubainisha kuwa Taifa
limepata mapato kiasi cha Dola za
Marekani 235.9 milioni.
Pia, alisema Taifa limeokoa
kiasi cha Dola za Marekani 5.3
bilioni katika kuzalisha umeme na
kiasi cha Dola za Marekani 449.7
milioni katika viwanda.
Manufaa mengine ni pamoja
na Halmashauri husika hupata
Kodi ya Huduma (service levy)
ambayo ni asilimia 0.3 ya mapato
ya mauzo ya gesi. Waziri Muhon-
go alitoa mfano wa mradi wa Son-
goSongo, ambapo Halmashauri ya
Kilwa hupata takribani shilingi za
Tanzania milioni 100 kila baada ya
miezi mitatu.
Akizungumzia faida za bomba
kuu la kusafisha na kusafirishia
gesi asilia ambalo ujenzi wake
unaendelea, alisema mitambo
iliyopo sasa, imesababisha nchi
kupoteza shilingi za Tanzania tril-
ioni 1.6 kwa mwaka kwa kutumia
mafuta kuzalisha umeme badala
ya gesi asilia.
Alisema endapo bomba hili
litatumika katika kiwango chake
cha juu (784 mmscfd), gesi itakay-
osafirishwa kwa kipindi cha miaka
20 ni asilimia 12 tu ya gesi iliyo-
gunduliwa hadi sasa.
Nchi itaokoa Dola za Mare-
kani bilioni moja (sawa na shilin-
gi za Tanzania trilioni 1.6) kwa
mwaka kutokana na mitambo ili-
yopo nchini inayozalisha umeme
kwa kutumia mafuta kuanza ku-
tumia gesi asilia, alisema Waziri
Muhongo.
Aidha, aliongeza kuwa bei ya
uzalishaji umeme itapungua kwa
uniti moja (KWh) ambapo ali-
fafanua kuwa umeme unaofuliwa
kwa dizeli na mafuta ya aina ny-
ingine hugharimu senti za Mareka-
ni 30 hadi 45 wakati bei ya kuzali-
sha uniti moja hiyo hiyo ni senti za
Marekani saba kwa umeme uto-
kanao na gesi asilia.
Alizitaja faida nyingine za
mradi mpya wa bomba la gesi
kuwa ni pamoja na ajira katika
mitambo itakayojengwa Madimba
na SongoSongo kwani kila mtam-
bo utahitaji kiasi cha wafanyakazi
60. Vilevile, alisema mradi utatoa
ajira katika sekta za afya, elimu,
maji usafiri pamoja na huduma
nyingine za kijamii zitakazohita-
jika.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Mhe. Charles Kitwanga, akiongea na wananchi wa kijiji cha Malolo,
Wilayani Kilosa. Mkutano huo uliojadili kuhusu Kampuni ya TAZAMA kuwalipa wakulima wa kijiji hicho fidia ya Sh. milioni 327 ikiwa ni fidia
baada ya bomba la mafuta la shirika hilo kupasuka na kusababisha athari za kimazingira katika kijiji hicho. Anayemsikiliza kushoto kwa Waziri
ni Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Elias Tarimo.
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof. Sospeter Muhongo
7
Bulletin News
http://www.mem.go.tz
NISHATI/MADINI
Mchanga wa dhahabu
wavutia Sabasaba
Na Saidi Mkabakuli
M
amia ya wakazi wa
Jiji la Dar es Salaam
na vitongoji vyake
wamejitokeza kujionea
mchanga wa dhahabu
unaooneshwa kwenye Banda la Waka-
la wa Ukaguzi wa Madini Tanzania
(TMAA) lililopo katika viwanja vya
Maonesho ya Kimataifa vya Mwalimu
Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wakazi hao Bw. Shabaan
Charahani, amesema ameshawishika
kufika ili kujionea mchanga huo na
kupata ukweli juu ya kutoroshwa kama
inavyovumishwa na watu wengi nchini.
Nimekuja kujifunza masuala ya
ukaguzi wa madini na kujua ukweli juu
ya mchanga wa dhahabu unaozalishwa
hapa nchini, alisema Bw. Charahani.
Akitoa maelezo kwa wananchi
hao waliojitokeza bandani hapo, Afisa
Habari wa Wakala huo, Mhandisi
Yisambi Shiwa alisema kuwa mchanga
wa dhahabu ni zao lenye madini ya
shaba na fedha lipatikanalo mara baada
ya kuchenjua mawe yenye dhahabu
kwenye mtambo wa kuchenjulia mawe
hayo uliopo kwenye migodi ya Bulyan-
hulu na Buzwagi.
Aliongeza kuwa kuna mkang-
anyiko wa matumizi sahihi ya neno
mchanga wa dhahabu, ambapo kiusa-
hihi mchanga wa dhahabu ni makinikia
ya shaba (copper concentrate).
Kutokana na madini ya shaba
kuwa mengi kwenye huu mchanga
wa dhahabu kuliko madini mengine,
jina rasmi linalotumika na kutambu-
lisha zao hili ni makinikia ya shaba,
alifafanua.
Kwa mujibu wa Bw. Shiwa, kwa
sasa, uzalishaji wa makinikia ya shaba
unafanyika katika migodi ya Bulyanhu-
lu na Buzwagi tu. Akiitaja sababu ya ku-
wepo na aina ya mashapo ya dhahabu
ya migodi hiyo kuwa na sifa tofauti na
migodi mingine mikubwa ya dhahabu
hapa nchini.
Akitaja sababu za kusafirishwa
nje ya nchi mchanga huo, Bw. Shiwa
alisema kutokuwepo kwa teknolojia ya
kutenganisha madini hayo, pamoja na
gharama kubwa za kuendeshea mtam-
bo wa kufanya kazi hiyo.
Gharama za mtambo wa kuchen-
julia madini hayo ni wastani wa dola za
kimarekani milioni 500. Gharama hizi
ni kubwa ukilinganisha na hali halisi
ya mapato ya migodi ya Bulyanhulu na
Buzwagi yatokanayo na mchanga wa
dhahabu, alisema Mhandisi Shiwa.
Bw. Shiwa aliongeza, kutokuwepo
kwa umeme wa uhakika na uzalishaji
duni wa makinikia hayo ndo sababu
kuu za kutofanyika kwa kazi hiyo hapa
nchini,
Kwa mujibu wa takwimu zilizopo
kiasi cha makinikia kinachozalishwa
hapa nchini ni wastani wa tani 45,000
wakati kiasi kinachotakiwa ni wastani
wa tani 150,000 za makinikia ya shaba.
TMAA ni Wakala wa Serikali ulio-
anzishwa tarehe 2 Novemba, 2009 chini
ya Sheria ya Wakala wa Serikali, Sura
ya 245. Tamko la Waziri la kuanzisha
Wakala lilichapishwa kwenye Gazeti
la Serikali Namba 362 la tarehe 6 No-
vemba, 2009. Lengo la Wakala ni ku-
hakikisha kwamba, Serikali inapata ma-
pato stahiki kutoka kwenye shughuli za
uzalishaji na biashara ya madini nchini
kupitia usimamizi na ukaguzi makini
wa shughuli za uchimbaji, na kuhakiki-
sha kuwa shughuli hizo zinafanyika
kwa kuzingatia uhifadhi na utunzaji
thabiti wa mazingira katika maeneo ya
migodi.
Watumishi wa TMAA wakiwaelimisha wanafunzi waliotembelea Banda lao kwenye viwanja
vya Saba Saba.
KITWANGA
Mianya ya rushwa
kuzibwa sekta ya madini
Na Veronica Simba
Dar es Salaam
M
fumo wa kielektroniki wa utaoji na usimamizi wa leseni
za madini maarufu kama Mining Cadastre unatarajiwa
kuboreshwa zaidi kwa lengo la kuongeza uwazi na ufanisi
ambapo utasaidia pia kuziba mianya ya rushwa.
Kamishna Msaidizi anayeshughulikia leseni za madini,
Mhandisi John Nayopa aliyasema hayo hivi karibuni baada ya
mafunzo juu ya uboreshaji mfumo huo yaliyofanyika kwa Makam-
ishna Wasaidizi wa Madini, Maafisa Madini wa Kanda zote nchi-
ni na baadhi ya maafisa kutoka Idara mbalimbali za Wizara ya
Nishati na Madini.
Akizungumzia maboresho hayo, Kamishna Msaidizi Nayopa
alisema mfumo utaruhusu uwazi zaidi katika kushughulikia leseni
za madini ikiwa ni pamoja na uombaji na utoaji wa leseni hizo.
Wadau wetu watakuwa na uhuru mpana zaidi kwa kuweza
kuona maeneo yaliyo wazi na yale ambayo tayari yanamilikiwa
hivyo kuondoa uwezekano wa mwombaji wa leseni kufanyiwa
udanganyifu wa aina yoyote, alifafanua Nayopa.
Aidha, alisema changamoto iliyopo kwa sasa ni kuhamasisha
na kuwawezesha wachimbaji wadogo wa madini kutumia Mfumo
huo ili waweze kunufaika na huduma hiyo muhimu kama ilivyo
kwa wawekezaji wakubwa.
Awali, wakati wa mafunzo husika, Mwezeshaji ambaye pia
ni Mshauri Mwelekezi, Charles Young kutoka Kampuni ya Spa-
tial Dimension ya Afrika Kusini alisema kuboreshwa kwa mfumo
huo kutarahisisha na kuboresha utendaji kazi na kuongeza kuwa
kutakuza imani ya wawekezaji kwa serikali.
Young alisema Mfumo huo utaondoa utamaduni wa malipo
ya fedha taslim (cash) kwani utawezesha kufanya malipo ya leseni
katika mtandao na kwamba mwombaji ataweza kuhudumiwa ma-
hali popote alipo bila kulazimika kwenda katika Ofisi ya Madini.
Akijibu swali la mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo kuhusu
matumizi ya lugha, Young alisema Mfumo huo utaruhusu mtumi-
aji kuchagua aina ya lugha anayopenda kutumia na kwamba en-
dapo itashauriwa Kiswahili kitumike kama lugha mojawapo ili
kuwanufaisha wadau wengi zaidi hapa nchini, yeye kama Mshauri
Mwelekezi hana pingamizi.
Mfumo huu wa Mining Cadastre ulianza kutumiwa na Wiz-
ara ya Nishati na Madini mwaka 2007 ambapo ni Maafisa Madini
pekee ndiyo walikuwa na uwezo wa kuutumia. Hali itakuwa to-
fauti hivi karibuni baada ya Mfumo huo kuboreshwa na kuruhusu
wadau mbalimbali wa madini kuutumia.
Ugunduzi gesi nchini
wachochea ukuaji uchumi
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
W
aziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah
Kigoda amewataka watanzania kuwa na uja-
siri wa kutumia fursa zilizopo nchini hususani
zinazotokana na ugunduzi wa gesi asili nchini.
Dkt. Kigoda aliyasema hayo wakati akifun-
ga maonesho ya kimataifa ya Saba Saba (Dar es Salaam Inter-
national Trade Fair) yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu
Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Dkt. Kigoda alisema kuwa nchi zilizopiga hatua kimaen-
deleo zilithubutu kutumia rasilimali zake zilizopo pamoja na
kukaribisha wawekezaji kutoka nchi nyingine .
Alisema kuwa matunda ya kugundulika kwa gesi yaliyopele-
kea kuanza kwa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi ji-
jini Dar es Salaam yameanza kuzaa matunda kwani wawekezaji
wameanza kujitokeza katika ujenzi wa viwanda vya sementi vi-
navyojengwa Lindi na Mtwara na vya mbolea vitakavyojengwa
nchini.
Ninawataka watanzania wachangamkie fursa hizi kwa ku-
jiajiri kupitia biashara na kutoa huduma kwa wawekezaji, kuwa
na wataalamu watakaofanya kazi kwenye makampuni hayo
Alisisitiza Dkt. Kigoda
Dkt. Kigoda aliongeza kuwa mara baada ya mradi wa bom-
ba la gesi kukamilika rasmi mwezi Desemba mwaka huu gesi
itakayozalishwa itatumika kuzalisha umeme, kupikia majum-
Profesa Muhongo kuzindua ofisi za LNG
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
W
aziri wa Nishati na Madini Profesa
Sospeter Muhongo anatarajia kuzindua
ofisi za Liquefied Natural Gas LNG
Tanzania mapema wiki ijayo jijini
Dar es Salaam . LNG ni muunganiko
wa makampuni matano ya BG Group, Statoil, Exxon-
Mobil, Ophir na Pavilion kwa ajili ya kufanikisha mi-
pango itakayopelekea ujenzi wa kiwanda cha kuchakata
gesi.
Makampuni hayo yanayounda LNG yatashirikiana
na serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini
(TPDC) na Wizara ya Nishati na Madini.
Hafla ya uzinduzi wa ofisi hiyo pia itahudhuriwa na
Mkurugenzi wa TPDC, viongozi waandamizi kutoka
Wizara ya Nishati na Madini na wadau mbalimbali wa
makampuni ya mafuta.
Mara baada ya kiwanda cha kuchakata gesi kuka-
milika, gesi itakayozalishwa itatumika nchini kuzalisha
umeme wa uhakika utakaopelekea kuongezeka kwa fur-
sa za uwekezaji kwenye viwanda, kilimo na afya.
Kuongezeka kwa viwanda nchini kutapelekea fursa
za ajira kwa wataalamu kuajiriwa katika viwanda hivyo
na wajasiriliamali kutumia nafasi hiyo kuuza bidhaa na
huduma zao kwa wawekezaji hao.
Pamoja na fursa za ajira, wataalamu wa Kitanzania
watapata fursa ya kupata uzoefu kutoka kwa wataalamu
kutoka nje ya nchi na kupelekea kuongezeka kwa wataal-
amu wa gesi nchini.
Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini ilik-
wishaanza mchakato wa kuwapeleka wataalamu wake
nje ya nchi kwa ajili ya kusomea masuala ya gesi kama
njia mojawapo ya kujiandaa na uchumi wa gesi ambao
unategemewa kuiwezesha nchi kupiga hatua hadi kuwa
nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
Gesi ya ziada itauzwa nje ya nchi na kuongeza pato
la taifa ikiwa ni pamoja na kuongeza thamani ya shilingi.
8 Bulletin News
http://www.mem.go.tz
HABARI
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wasiliana nasi kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
au Fika Ofsi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: badra77@yahoo.com
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
TANZANIA DAIMA LAIKOSEA WIZARA
Na Asteria Muhozya
T
anzania na Algeria zinakamilisha
majadiliano ya kuanzisha kampu-
ni ya Ubia itakayohusika na ujenzi
wa miundombinu ya kusambaza
umeme na Kampuni ya Ubia ya
kujenga mtambo wa kusindika gesi ya Liq-
uefied Petroleum Gas (LPG) na kuiuza gesi
kwa wananchi kwa kutumia mitungi.
Makubaliano hayo yamefikiwa katika
ziara ya kikazi ya Waziri wa Nishati na Ma-
dini Profesa Sospeter Muhongo na ujumbe
wake nchini Algeria, ambayo inalenga kufua-
tilia utekelezaji wa makubaliano ya awali ya
kushirikiana katika kubadilishana uzoefu kwe-
nye masuala yanayohusu sekta za Nishati na
Madini kufuatia Mkataba wa Makubaliano ya
ushirikiano wa nchi hizo uliosainiwa tarehe 2
Disemba, 2013 nchini Algeria.
Kwa mujibu wa makubaliano ya mku-
tano baina ya Mawaziri wa Nishati na Ma-
dini wa Tanzania, Profesa Sospeter Muhongo
na Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria
Mhe. Youcef Yousfi, mawaziri hao wamey-
aagiza mashirika ya Umeme ya Tanzania
(TANESCO) na Shirika la Umeme la Algeria
(KAHRIF) kukamilisha majadiliano ya kuan-
zisha kampuni ya ubia ya ujenzi wa miun-
dombinu ya kusambaza umeme.
Mkutano huo wa mawaziri, ulitanguliwa
na kikao cha awali cha wataalamu wa nchi
zote mbili, ambacho kiliongozwa na Kam-
ishna Msaidizi anayeshughulikia masuala
ya Umeme , Wizara ya Nishati na Madini,
Mhandisi Innocent Luoga, ambacho kilijadili
maeneo ya ushirikiano yanayohusu umeme,
mafuta, gesi na madini.
Katika hatua nyingine, Mawaziri hao
wameziagiza kampuni za mafuta na gesi
likiwemo Shirika la Maendeleo ya Petroli
Tanzania (TPDC) na kampuni za mafuta na
gesi za Algeria za NAFTAL na SONATRAC
kukamilisha majadiliano ya kuanzisha kam-
puni ya ubia ya kujenga mtambo wa LPG na
kuuza gesi hiyo kwa wananchi kwa kutumia
mitungi, ambapo kampuni zote za ubia zime-
takiwa kuanza kazi ifikapo Januari, 2015.
Wakati huo huo, Waziri Muhongo ame-
kutana na Waziri wa Viwanda na Migodi wa
Algeria Mhe. Abdessalem BOUCHOAREB
ili kujadili maeneo ya ushirikiano katika sekta
ya Madini ambapo wamezielekeza taasisi zi-
nazohusika na madini za nchi hizo, kuandaa
mpango wa utekelezaji wa ushirikiano ka-
tika kuwajengea uwezo wataalamu wa madini
kubadilishana uzoefu na teknolojia, utafutaji
na uendelezaji wa madini ya dhahabu, chuma,
almasi, phosphates na utunzaji wa taarifa za ji-
olojia na madini (Management of geological
and mining database).
Katika ziara hiyo, Waziri Muhongo na
ujumbe wake wamepata nafasi ya kutembelea
Mtambo wa kufua umeme wa kutumia gesi
asilia wa HAMMA ambao unamilikiwa na
serikali ya nchi hiyo kwa asilimia 100 na una
uwezo wa kuzalisha megawati za umeme
418, na uwezo wa kutumia mafuta ya dizeli na
gesi kwa nyakati tofauti.
Vilevile, ujumbe huo wa Tanzania ume-
pata fursa ya kuona mashine za kuzalisha
umeme zinazotembea (mobile generators)
ambazo hufungwa kwa dharura sehemu in-
apohitajika na kuhamishiwa sehemu nyingine,
ambapo mashine moja ina uwezo wa kuzali-
sha megawati za umeme 20.
Katika ziara hiyo, Mhe. Muhongo
ameongozana na Kamishna Msaidizi wa
Nishati anayeshughulikia masuala ya umeme,
Mhandisi Innocent Luoga na wataalamu
kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST),
TPDC na TANESCO.
Mkataba wa Makubaliano (MoU) ya
ushirikiano wa Tanzania na Algeria, ulisaini-
wa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa
Sospeter Muhongo kwa upande wa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wa-
ziri wa Nishati na Migodi wa Algeria, Mhe.
Youcef Yousfi.
Tanzania, Algeria
kuanzisha kampuni za ubia
TUFANYE KAZI KWA UADILIFU, BIDII, WELEDI,
NA USHIRIKIANO BILA KUKATA TAMAA
DAIMA TUSONGE MBELE
KURUDI NYUMA NI MWIKO!!
UJUMBE WA WAZIRI WIKI HII
n Ni ya ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme
nKujenga mtambo wa kusindika gesi ya LPG, na kuuzwa kwenye mitungi
nSekta ya madini pia yaguswa
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof. Sospeter Muhongo
(Kushoto), akiongea na Waziri wa Viwanda na Migodi wa Algeria,
Mhe. Abdessalem BOUCHOAREB (Kulia). Wakati wakijadiliana
maeneo ya ushirikiano katika sekta ya Madini. Katikakati ni
mkalimani.
By Neema Mbuja
K
ituo cha kuzalisha umeme kwa njia ya maji cha
Mtera kipo njiani kubadili mfumo wa uendeshaji
kutoka analojia kwenda digitali ili kuongeza
ufanisi wa utendaji kazi wa kituo.
Hayo yamewekwa bayana na Kaimu Mhandisi Mkuu
Uendeshaji wa Kituo hicho, Mhandisi Luis Loiloi wakati
wa ziara ya Maafisa Mahusiano wapya wa TANESCO
Makao Makuu.
Mhandisi Loiloi amesema kwamba katika kuhakiki-
sha Kituo cha Mtera kinafikia lengo lake la kuzalisha
umeme wa Megawati 80, Kituo kimepanga kubadili mfu-
mo wa uendeshaji wa mitambo ya uzalishaji ili kuongeza
tija ya utendaji wa mitambo hiyo.
Katika kuhakikisha kuwa tunakuwa na uzalishaji wa
umeme wa uhakika, tumedhamiria kufanya maboresho ka-
tika kituo chetu kutoka mfumo wa analojia kwenda mfumo
wa digitali ili kuongeza kasi ya uzalishaji na kukabiliana na
changamoto mbalimbali zinazosababishwa na uduni wa
teknolojia ya sasa, alisema Mhandisi Loiloi.
Mhandisi Loiloi amesema kuwa mkakati wa kutumia
teknolojia hii ya kisasa ya mitambo ya kuzalisha umeme
kutokana na kwamba hivi sasa baadhi ya teknolojia inay-
otumika ni ya siku nyingi na baadhi ya makampuni ya-
mekwishaacha kutengeneza vipuri vya mashine hizo kwa
sasa sambamba na kutoa mafunzo kwa wafanyakazi juu ya
namna ya kutumia teknolojia mpya za mitambo ya kisasa.
Akizungumzia gharama ya kubadili mfumo huo,
Mhandisi Loiloi amesema kuwa zaidi ya Shilingi Bilioni
tatu zitatumika katika kukamilisha kazi hiyo.
Kazi hii itagharimu takribani Shilingi Bilioni tatu
ambazo zinajumuisha matengenezo na kununulia vipuri
vipya, alisema.
Kwa mujibu wa matengenezo hayo ambayo yanaju-
muisha matengenezo ya jenereta mbili zitakazogharimu
jumla ya fedhas za kitanzania Shilingi 740 milioni, pamoja
kununua mashine mpya inayogharimu shilingi bilioni moja
za kitanzania.
Pia, kiasi cha fedha Shilingi 1.56 bilioni zimetengwa
kwa ajili ya matengenezo na uboreshaji wa kinu cha kufua
umeme.
Mtera ni miongoni mwa vituo muhimu sana kwa uzal-
ishaji wa umeme vinavyoendeshwa na Shirika la Umeme
Nchini (TANESCO). Kituo hiki ni moja ya kituo kinacho-
tumia umeme wa maji ili kuendesha mitambo ya kusukuma
mashine ili kuzalisha umeme. Wataalamu wanasema kuwa
kwa mujibu wa takwimu zilizopo, umeme unaozalishwa
na maji ni umeme nafuu sana ukilinganisha na umeme
unaozalishwa kwa njia ya mafuta, ukifuatiwa na makaa ya
mawe, na kisha gesi.
Kituo cha mtera kilijengwa mwaka 1984 na kukamilika
mwaka 1988 na kiligharimu kiasi cha shilingi milioni 1,580
ambapo kwa wakati huo dola moja ya marekani ilikuwa ni
sawa na shilingi kumi ya kitanzania. Mashine zilizofungwa
katika kituo cha kuzalisha umeme cha Mtera kina uwezo
wa kuzalisha MW 80 ambapo kila mashine moja ina uwezo
wa kuzalisha megawati 40 kwa kila mashine moja.
MTERA YAJIPANGA KUBADILI
MFUMO WA UENDESHAJI

You might also like