You are on page 1of 8

Mkakati uboreshaji umeme wakamilika Uk8 Maonesho sabasaba Uk4-5

Toleo No.23 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe Julai 4-10, 2014
Bulletin
News
Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali
kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
au Fika Ofsi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: badra77@yahoo.com
http://www.mem.go.tz
HABARI ZA
NISHATI &MADINI
Bei Poa
WAWEKEZAJI NISHATI KUIUZIA TANESCO UMEME
Waziri wa Nishati na
madini Prof. Sospeter
Muhongo (kulia)
akizungumza na
wawekezaji wa umeme
wa upepo Wind East
Africa unaotarajiwa
kujegwa mjini Singida.
<
2 Bulletin News
http://www.mem.go.tz
NISHATI/MADINI
Wawekezaji nishati kuiuzia Tanesco umeme bei nafuu
Veronica Simba na
Nuru mwasampeta
S
erikali imewataka wawekezaji wote katika
sekta ya nishati nchini kuhakikisha bei zao
za umeme zinakuwa nafuu ili Watanzania
wanufaike ipasavyo na vyanzo vya nishati
hiyo.
Agizo hilo lilitolewa hivi karibuni na Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
alipokuwa akizungumza na wawekezaji wazawa
kutoka Kampuni ya GeoWind Limited, walio-
wasilisha maombi ya kuzalisha umeme wa upepo
mkoani Singida.
Waziri Muhongo alisema Serikali inapaswa
kutimiza ahadi yake iliyoweka kwa Watanzania
ya kuhakikisha wananufaika na vyanzo mbalim-
bali vya nishati vilivyopo nchini, hivyo lengo lake
ni kuhakikisha umeme wa kutosha na wa uhakika
unapatikana na pia bei yake iwe nafuu ili wananchi
waweze kuimudu.
Kampuni yoyote inayodhamiria kuzalisha
umeme kutokana na chanzo chochote hapa nchini,
lazima ihakikishe inapanga bei iliyo chini ya bei ya
Tanesco ya sasa ambayo ni Senti 12.6 vinginevyo
haitapewa nafasi kufanya shughuli za uzalishaji
kwani tutakuwa tunawadanganya Watanzania,
alisisitiza Profesa Muhongo.
Alisema kuwa Tanzania inavyo vyanzo vingi
vya nishati vikiwa ni pamoja na makaa ya mawe,
gesi asilia, jotoardhi, jua, upepo, nishati jadidifu na
maji hivyo hakuna sababu ya kulazimika kuzalisha
umeme wa gharama kubwa kama ilivyo kwa nchi
nyingine ambazo zina vyanzo vichache vya nishati.
Akifafanua kuhusu faida za kuzalisha umeme
wa kutosha, wa uhakika na wenye bei nafuu, Wa-
ziri Muhongo alisema itasaidia kupunguza tatizo
la ajira kwa vijana kwani viwanda vitazalisha zaidi
na hivyo kuongeza ajira na pia wengine wataweza
kujiajiri kupitia miradi mbalimbali.
Aidha, Profesa Muhongo alisema lengo la Seri-
kali ni kuhakikisha Tanesco inaacha-
na na utamaduni wa kupata ruzuku
kutoka serikalini ili fedha hizo ziende
kusaidia wananchi kwenye sekta za
elimu, afya na kilimo.
Kwa upande wake, Mkuu wa
mkoa wa Singida, Dk Parseko Konne
aliafiki msimamo wa Waziri Muhon-
go na kusisitiza kuwa Serikali haiwezi
kukubaliana na wawekezaji wanao-
taka kuzalisha umeme na kuuza kwa
bei zaidi ya ile ya sasa ya Tanesco.
Mnaotaka kuzalisha, hakikisheni
bei yenu inakuwa chini ili Watanza-
nia wanufaike, alisisitiza.
Wawekezaji hao wazawa wali-
kubaliana na maelekezo ya Waziri
Muhongo na Mkuu wa Mkoa Dk
Konne na kuahidi kuyafanyia kazi am-
bapo watawasilisha tena mapendeke-
zo yao ya uwekezaji wizarani, tarehe
23 Julai mwaka huu.
Pamoja na kukutana na wawekeza-
ji wazawa, Profesa Muhongo aliku-
tana na wawekezaji wa kampuni ya
Wind East Africa kujadili namna ya
kutekeleza mradi huo wa umeme wa
upepo kwa wakati kutokana na tara-
tibu za kukamilisha mradi huo ku-
suasua.
Akizungumza wakati wa kikao
hicho Muhongo alisema wahusika
wanaopaswa kukamilisha mradi
huo (Tanesco, Wind East Africa, na
Ewura) wawe na ufanisi kwa kuwapa
watanzania kile wanachokihitaji, yani
umeme wa kutosha na unaopatikana
kwa gharama nafuu.
Aidha Kamishna Msaidizi wa Ni-
shati. Injinia Inocent Luoga alisema
mradi huo wa umeme utakaotekele-
zwa na kampuni ya Wind East Afrika
Utagharimu kiasi cha Dola za kimare-
kani 285 milioni ili kuzalisha umeme
wa kiasi cha Megawati 100.
Kufanyika kwa kikao hicho kume-
pelekea kupatikana kwa ratiba ya
awali itakayofuatwa na Wizara,Taasisi
pamoja na wawekezaji ili kuhakikisha
kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo
ambao utakamilika ifikapo Oktoba
2016.
Kampuni yoyote
inayodhamiria
kuzalisha umeme
kutokana na
chanzo chochote
hapa nchini, lazima
ihakikishe inapanga
bei iliyo chini ya bei
ya Tanesco ya sasa
ambayo ni Senti
12.6 vinginevyo
haitapewa nafasi
kufanya shughuli
za uzalishaji
kwani tutakuwa
tunawadanganya
Watanzania,
Profesa Muhongo.
Muhongo: Fuatilieni mapato ya madini
Waziri wa Nishati na Madini akiwa na watendaji wa wizara ya Nishati na Madini
pamoja na wawekezaji wa mradi wa Wind East Africa walipokuwa wanapanga
mkakati wa namna ya kufanya mradi huo utekelezeke kwa wakati kutokana na
wahusika kupiga danadana katika kuanza utekelezaji wa mradi huo.
Veronica Simba,
Dodoma
Viongozi wa dini nchini wamehama-
sishwa kufuatilia kwa ukaribu matumi-
zi ya fedha zinazotolewa na makampu-
ni ya madini kama ushuru wa huduma
(service levy) kwa halmashauri husika
ili kuhakikisha zinatumika kwa manu-
faa ya wananchi.
Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo ametoa
hamasa hiyo Julai 3 mwaka huu mji-
ni Dodoma, wakati akitoa Mada ya
Manufaa ya Rasilimali za Madini na
Gesi Asilia kwa sasa na kipindi kija-
cho kwa Maaskofu wa Makanisa ya
Kipentekoste nchini, katika mkutano
wao wa mwaka.
Akiwasilisha mada hiyo, Profesa
Muhongo alisema Halmashauri mbal-
imbali nchini zimekwishaanza kupokea
ushuru wa huduma kutoka makampu-
ni ya madini yaliyoko katika maeneo
yao hivyo ni vema mapato hayo pamoja
na matumizi yake yawekwe wazi kwa
wananchi ili waweze kuelewa manufaa
yake kwao.
Alizitaja Halmashauri hizo kuwa
ni pamoja na Geita ambayo mpaka
sasa imekwishapokea jumla ya Dola
za Marekani 1.6 milioni ambazo ni
sawa na shilingi za kitanzania bil-
ioni 2.62. Nyingine ni Kahama am-
bayo imeshapokea Dola za Mare-
kani 2.53 milioni sawa na shilingi
bilioni 4.15 za Tanzania.
Halmashauri nyingine ni Ta-
rime ambayo imeshapokea Dola
za Marekani 2.4 milioni sawa na
shilingi za Tanzania 3.94 bilioni,
Nzega (Dola 3.04 milioni) sawa na
shilingi za Tanzania bilioni 4.99 na
Kishapu ambayo imekwishapokea
Dola za Marekani 202,469 sawa
na shilingi milioni 332.05 za Tan-
zania.
Sasa utasikia watu mbalim-
bali wakilalamika kuwa makam-
puni ya madini hayalipi chochote
jambo ambalo siyo la kweli. Ma-
pato na matumizi yawekwe wazi
kwa wananchi ili waelewe, ali-
sisitiza Waziri Muhongo.
Akifafanua zaidi kuhusu ma-
pato yanayotokana na kodi mbal-
imbali zinazolipwa na makampu-
ni ya madini hapa nchini, Profesa
Muhongo alisema kwa sasa ma-
pato ya kodi yameongezeka kuto-
kana na serikali kuweka usimam-
izi na kuhakikisha makampuni
yote kwa sasa yanalipa kodi ya
kampuni (corporate tax).
Kwa upande wa wachim-
baji wadogo wa madini, Waziri
Muhongo alisema serikali im-
echukua hatua za makusudi ku-
wasaidia ili kuinua kipato chao ili
waweze kuchangia katika kukuza
uchumi wa nchi.
Alisema, kwa mwaka wa
fedha ulioisha Juni 2014, jumla
ya shilingi milioni 880.68 za
Tanzania zilitolewa na serikali
kwa wachimbaji wadogo kama
ruzuku. Aidha, aliongeza kuwa
mwezi huu serikali inatarajia ku-
toa jumla ya shilingi za Tanzania
bilioni 2.3 kama mikopo kwa
vikundi mbalimbali vya wachim-
baji wadogo kupitia Benki ya TIB
(Tanzania Investment Bank).
Profesa Muhongo alisema
kuwa kwa mwaka wa fedha
2014/15, serikali kupitia Wizara
ya Nishati na Madini inatarajia
kutoa mikopo kwa wachimbaji
wadogo yenye jumla ya shilingi
za Tanzania bilioni 2.5 na kwam-
ba jumla ya shilingi bilioni 5.74
kutoka Benki ya Dunia zitatole-
wa kwa wachimbaji hao kama
ruzuku.
Mbali na fedha hizo nilizoz-
itaja, wachimbaji wadogo wata-
patiwa mitambo ya kuchoronga
miamba yenye thamani ya jumla
ya shilingi za Tanzania bilioni
1.80, alisema Waziri Muhongo.
Waziri Muhongo alialikwa
kama Mgeni Rasmi na pia kama
mtoa mada katika Mkutano wa
mwaka wa Maaskofu wa Ma-
kanisa ya Kipentekoste Tanza-
nia (CCT). Katibu Mkuu Kion-
gozi, Balozi Ombeni Sefue pia
alialikwa kutoa mada iliyohusu
masuala ya Matokeo Makubwa
Sasa maarufu kama Big Re-
sults Now.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiwasilisha
mada kuhusu Manufaa ya Rasilimali za Madini na Gesi Asilia kwa
sasa na kipindi kijacho katika Mkutano wa Mwaka wa Maaskofu wa
Makanisa ya Kipentekoste nchini (CCT), uliofanyika mjini Dodoma
Julai 3, mwaka huu.
3
Bulletin News
http://www.mem.go.tz
MAONI
Nuru Mwasampeta
Dar es Salaam
W
anafunzi wana-
osomea lugha
ya Kireno
wamet aki wa
k u o n g e z a
juhudi katika masomo yao ili
kukidhi mahitaji ya kudahiliwa
katika vyuo bora nchini Brazil.
Hayo yamesemwa na Waziri
wa Nishati na Madini Profesa
Sospeter Muhongo alipokuwa
akizungumza na wawekezaji
wa kampuni ya mafuta ya
Petrobras walipofika katika ofisi
yake ili kuzungumzia masuala
mtambuka katika sekta ya gesi
na mafuta na maendeleo ya
uwekezaji wao nchini na bara la
Afrika kwa ujumla.
Muhongo alieleza kuwa
mwezi wa nane mwaka huu
atatembelea nchi ya Brazili
na kueleza kuwa kati ya vitu
atakavyopenda kutembelea na
kuona vifaa vinavyotumika na
kampuni hiyo katika kufanya
shughuli za utafiti pamoja na
kutembelea vyuo vikuu vinne
bora katika kutoa taaluma ya
mafuta na gesi ili kuweza ku-
waombea watanzania nafasi ya
kudahiliwa katika vyuo hivyo.
Akizungumzia hoja hiyo
Samuel Bastos De Miranda
Mtendaji Mkuu wa kampuni
hiyo alisema wanafunzi wa-
takao kuwa na sifa za kuda-
hiliwa katika vyuo bora nchini
Brazil watapata nafasi.
Aidha Samuel amezungum-
zia nia yao ya kurejesha kitalu
namba 5 walichokifanyia utafiti
na kubaini kuwa gharama iliyo-
tumika katika kuchimba kitalu
hicho ni kubwa na hakuna dalili
yeyote ya kupata kile walicho-
tegemea kukipata na hivyo kue-
ndelea na utafiti katika kitalu
namba 6 na namba 8.
Aidha alieleza kwamba wa-
nafanyakazi katika nchi sita ba-
rani Africa ikiwepo Namibia,
Benin, Angola, Nigeria, Tan-
zania na Gabon na kwamba
makao makuu ya uendeshaji
wa biashara yao yapo katika mji
wa Roterdam nchini Uholanzi
kutokana na mji huo kuwa ni
kitovu cha biashara.
Tahariri
MEM
Na Badra Masoud
FIVE
PILLARS OF
REFORMS
KWA HABARI PIGA SIMU
KITENGO CHA MAWASILIANO
BODI YA UHARIRI
MHARIRI MKUU: Badra Masoud
MSANIFU: Essy Ogunde
WAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson Mwase
Teresia Mhagama, Nuru Mwasampeta
INCREASE EFFICIENCY
QUALITY DELIVERY
OF GOODS/SERVICE
SATISFACTION OF
THE CLIENT
SATISFACTION OF
BUSINESS PARTNERS
SATISFACTION OF
SHAREHOLDERS
TEL-2110490
FAX-2110389
MOB-0732999263
W
iki hii katika gazeti letu ukurasa wa kwanza
tuna habari kwamba Waziri wa Nishati na
Madini Mhe. Prof. Sospeter Muhongo ame-
wataka wawezaji wote wa umeme wa ndani
na nje ya nchi kuiuzia TANESCO umeme wa gharama
nafuu ambayo ni ya chini ya bei ya umeme unaouzwa na
Shirika hilo kwa wateja wake.
Prof. Muhongo alienda mbali zaidi kwa kuwataka
EWURA kuandaa kanuni zinazoonyesha bei za umeme
kwa kila chanzo cha umeme utakaouzwa na wazalishaji
binafsi wa umeme kwa TANESCO. Alisema iwapo
mwekezaji atamuuzia TANESCO umeme wa bei ya juu
ya bei ya TANESCO, shirika hilo litauza Shilingi ngapi
kwa wateja wake.
Vyanzo hivyo ni kama umeme wa gesi, jua, jotoardhi,
upepo, mafuta, maji, makaa ya mawe n.k kwamba kila
chanzo kitakuwa na bei yake na iwapo wawekezaji wa-
takaotaka kuwekeza kwenye sekta hiyo itakuwa ni rahisi
kwa wao kuchagua vyanzo wanavyotaka kuwekeza bada-
la ya kutumia muda mrefu wa kujadiliana hasa kwenye
kipengele cha bei ya umeme.
Ninaamini kauli hiyo ya Prof. Muhongo kwa namna
moja ama nyingine imekuja kutokana na baadhi ya miradi
kuchukua muda mrefu kuanza utekelezaji wake na min-
gine imeshindikana kutekelezeka au hata mazungumzo
(negotiation) kuchukua muda mrefu.
Aidha, kuna wengine waliodiriki hata kusema kwam-
ba Serikali, Wizara ya Nishati na Madini au TANESCO
inawakimbiza wawekezaji bila kujua kwamba miongoni
mwa vigezo vikuu vya wawekezaji wa makampuni ya
kuzalisha umeme wanaruhusiwa kufanya biashara hiyo
na TANESCO ni wale wenye gharama nafuu na si vingi-
nevyo.
Kwa hakika, uamuzi huo pamoja na maelekezo ya
Prof. Muhongo lazima tuyaunge mkono juu ya bei hizi za
umeme kutoka kwa wawekezaji binafsi kwa maslahi ya
watanzania na kama tunavyofahamu kwamba iwapo bei
za umeme zitakuwa kubwa kuliko bei ya umeme unauzwa
na TANESCO kwa wateja wake hakuna watakaoumia
zaidi ya Watanzania.
Ni kweli kabisa Serikali na taifa kwa ujumla hatuna
budi kushirikiana na wawekezaji binafsi katika kuongeza
kiwango cha uzalishaji umeme lakini lazima kuwepo
udhibiti wa bei ili kuepukana na bei holela ya umeme.
Pamoja na Tanzania kuwa ndiyo nchi yenye bei ndo-
go ya umeme katika nchi zote za Afrika Mashariki laki-
ni bado Serikali inafanya bidii bei hiyo isiongezeke kwa
namna yoyote ile na wawekezaji binafsi katika uzalishaji
wa umeme wasiuze umeme kwa bei kubwa.
Tunampongeza Waziri Muhongo kwa uamuzi wake
huo na tutamuunga mkono katika kuhakikisha utekelezaji
wa uandaaji wa muongozo utakaotekelezwa na kukami-
lika kwa muda aliouelekeza ili Taifa la Tanzania liwe na
umeme wa kutosha utakaochochea ukuaji wa uchumi.
Tumuunge mkono
Prof. Muhongo kuendeleza
sekta ya umeme!!!
TEL-2110490
FAX-2110389
MOB-0732999263
Watanzania waaswa
kujiendeleza kitaaluma
Profesa Sospeter Muhon-
go kushoto akizungumza
na viongozi wa Kampuni
ya Petrobrass walipom-
tembelea ofisini kwake
kulia kwake ni Mtendaji
Mkuu wa kampuni hiyo
Bw. Samuel Bastos De
Miranda akifuatiwa na
Bw. Paulo Sergio De Sa
Campos Mkurugenzi
Mkuu wa Fedha wa
kampuni hiyo.
4 Bulletin News
http://www.mem.go.tz

Maonyesho ya 38 ya Sabasaba - 2014
Mjiolojia Mkuu kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) Bw. Momburi Philip (kulia) akitoa
elimu kwa mwananchi aliyetembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini.
http://www.mem.go.tz
Mtaalamu kutoka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Bw. Stephen Nyoni Lowoko
akimwonesha Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Wizara ya
Nishati na Madini, Bw. Mrimia Mchomvu mfano wa mashine ya kufua umeme kwa nguvu
ya maji mara alipotembelea banda hilo.
Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Idd akifungua maonesho
ya Kimataifa ya Sabasaba
katika viwanja vya Mwalimu
Nyerere jijini Dar es Salaam.
Greyson Mwase na
Nuru Mwasampeta, Dar es Salaam

W
izara, taasisi na mashirika binafsi yametak-
iwa kutumia maonesho kutangaza fursa za
uwekezaji nchini.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa
maonesho ya kimataifa ya Sabasaba (38 Dar es
Salaam International Trade Fair (DITF) yanayoendelea katika
viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd alisema kuwa idadi
ya washiriki wa maonesho ya Sabasaba imeongezeka kutoka
1601 kwa mwaka 2013 hadi 1690 kwa mwaka 2014
Balozi Idd aliendelea kusema kuwa washiriki ambao ni
makampuni kutoka nje ya nchi wameongezeka kutoka 460 kwa
mwaka 2013 hadi 490 kwa mwaka 2014.
Kuongezeka kwa washiriki ndani na nje ya nchi ni udhi-
hirisho kuwa maonesho haya yanaitangaza Tanzania na rasili-
mali zake ndani na nje ya nchi.
Alisema kuwa mbali na kuonesha mafanikio katika ongeze-
ko la washiriki katika maonesho hayo, washiriki wanatakiwa
kuongeza bidii kutangaza fursa za uwekezaji nchini na kufungua
milango kwa makampuni ya nje kuwekeza zaidi na hivyo ku-
changia katika ukuaji wa uchumi wa nchi.
Balozi Idd alisisitiza kuwa ili nchi yoyote iweze kupiga hatua
ni lazima iwekeze katika sekta ya viwanda na nyinginezo na ku-
karibisha wawekezaji nchini
Tumieni maonesho
kutangaza fursa
za uwekezaji
5
Bulletin News
http://www.mem.go.tz
Tuzo za madini

Maonyesho ya 38 ya Sabasaba - 2014
Mtaalam wa Mazingira
kutoka Wakala wa Ukaguzi
wa Madini Nchini (TMAA)
Bi. Monica Augustino akitoa
maelezo kwa kikundi cha
kinamama wajasiriliamali
kutoka Simanjiro mara wali-
potembelea banda hilo.
Mtaalam kutoka Shirika la
Umeme Nchini (TANESCO)
Mhandisi Juliana Palangyo
akitoa maelezo kwa Mku-
rugenzi Mstaafu wa Shirika
la Madini la Taifa Bw. Gray
Mwakalukwa mara alipo-
tembelea banda hilo.
Mtaalam kutoka Kitengo cha
Uthamini wa Madini ya Almasi
na Vito (TANSORT) Bi. Teddy
Goliama (kulia) akitoa elimu
kwa mwananchi aliyeshika
kinyago kinachotokana na
miamba jinsi shughuli za
uthamini wa madini ya vito
zinavyofanywa na Kitengo
hicho
Meneja Masoko kutoka
Kampuni ya Steps Solar
Limited Bw. Pritesh Chavda
(mwenye Flana) akitoa
maelezo kwa Mkurugenzi
wa Idara ya Utawala na Usi-
mamizi wa Rasilimali Watu
Wizara ya Nishati na Madini,
Bw. Mrimia Mchomvu jinsi
pampu ya maji inayotumia
umeme jua inavyofanya
kazi.
Mjiolojia Mkuu wa Wizara
ya Nishati na Madini Bw.
Mwara Shoo akitoa maelezo
kwa mmoja wa wananchi
waliotembelea banda la
Wizara ya Nishati na Madini
kwenye maonesho ya kima-
taifa ya Saba Saba yanayo-
endelea katika viwanja vya
Mwalimu Nyerere jijini Dar
es Salaam
6 Bulletin News
http://www.mem.go.tz
NISHATI
KITWANGA
Utunzaji Mazingira
wamkuna Kitwanga
Na Asteria Muhozya,
Kidatu/Kihansi
N
aibu Waziri Nishati
na Madini anayeshu-
ghulikia Nishati Mhe.
Charles Kitwanga
amesifu utunzaji wa mazingira
unaofanywa na watumishi wa ma-
bwawa ya uzalishaji umeme ya Ki-
hansi na Kidatu kwa kushirikiana
na wananchi.
Naibu Waziri ameeleza hayo
akiwa katika ziara ya kutembelea
Mabwawa ya kufua umeme ya Ki-
datu na Kihansi ambapo ameleeza
kuwa, utunzaji wa mazingira ni
muhimu kutokana na kuwa na
uhusiano wa moja kwa moja na
vyanzo vya maji ambavyo vina
mchango mkubwa katika kuzali-
sha nishati ya umeme inayotokana
na maji.
Kwa kweli nimefurahishwa
sana na utunzaji wa mazingira.
Tuhakikishe tunaendelea kutunza
vyanzo vyetu vya maji. Tushiriki-
ane na wananchi kulinda vyanzo
hivi. Amesisitiza. Kitwanga.
Katika hatua nyingine
ameeleza kuwa, amefanya ziara
katika mabwawa hayo ili kuona
namna shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) linavyofanya kazi,
kutambua changamoto na kuona
namna ambavyo Shirika hilo li-
taendelea kuzalisha nishati ya ku-
tosha.
Kuhusu uboreshaji wa TANE-
SCO ameeleza kuwa, mabadiliko
yataendelea kufanywa ndani ya
shirika hilo ikiwemo kuboresha mi-
undombinu ili kuongeza uzalishaji
na kuhakikisha kwamba Tanzania
inakuwa na nishati umeme ya ku-
tosha.
Aidha, Kitwanga amesisitiza
kuwepo kwa vyanzo mbadala
vya kuzalisha umeme mbali ya
kutegemea nishati ya gesi na maji.
Lazima tuwe na nishati
mchanganyiko inayotokana na
vyanzo mbalimbali na mpango
uliopo ni kuzalisha megawati za
umeme 10,000 ifikapo mwaka
2025.
Wakati huo huo, Kitwanga
amesifu uwajibikaji wa watumishi
katika Bwawa la kuzalisha umeme
la Kihansi kutokana na jitihada zao
za kurejesha faida kwa wananchi
wanaozunguka eneo hilo ambapo
wananchi wanafaidika moja kwa
moja na huduma muhimu zinazo-
tolewa na shirika hilo ikiwemo za
afya na elimu.
n Apongeza Uwajibikaji wa Tanesco
n Asisitiza nishati mchanganyiko
Kihansi&Kidatu
Kihansi
Kidatu
Mabadiliko menejiment i TANESCO
Na Henry Kilasila
K
ufuatia uteuzi wa
Mhandisi Boniface
S. Njombe kuwa
Meneja Mkuu wa
Kampuni ya Tan-
zania Geothermal Development
Company (TGDLC) Uongozi wa
Shirika la Umeme Tanzania (TA-
NESCO) umemteua Mhandisi
Nazir Kachwamba kuwa Kaimu
Naibu Mkurugenzi Mkuu Uzal-
ishaji Umeme kuazia tarehe
15/06/2014.
Mhandisi Kachwamba aliajiri-
wa rasmi tarehe 01/04/1987 kama
Mhandisi wa Umeme. Imeele-
zwa kwamba Kabla ya uteuzi wa
sasa, Kachamba alikuwa Meneja
Mwandamizi Uzalishaji Umeme
wa Maji.
Mhandisi Nazir Kachwamba
ana Shahada ya Uhandisi wa
Umeme (Electrical Engineering)
kutoka Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam alipohitimu mwaka 1987.
Pia ana Stashahada ya Uzamili
(Postgraduate Diploma in Scien-
tific Computing) kutoka Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam aliyohit-
imu mwaka 2007.
Pamoja na uteuzi wa Mhandisi
Kachamba Shirika hilo limem-
teua Ndugu Godson Makia kuwa
Kaimu Mwanasheria Mkuu
na Katibu wa Shirika baada ya
aliyekuwepo Ndugu Godwin S.
Ngwilimi kuacha kazi, Uongozi
wa Shirika la TANESCO umewe-
ka wazi kuwa Ndugu Makia ame-
kuwa akikaimu nafasi hiyo tangu
mwezi Machi, 2014.
Kabla ya uteuzi huu, Ndugu
Godwin alikuwa Mkuu wa Idara
ya Sheria akishughulikia masuala
ya biashara za Shirika (Legal Man-
ager Commercial Affairs)
Wakili Godson E. Makia ana
Shahada ya Sheria kutoka Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam alipo-
hitimu mwaka 1992. Licha ya
taaluma katika fani ya Sheria, ana
stashahada (Diploma) ya Ualimu
kutoka Chuo cha Ualimu Korog-
we ya mwaka 1985. Hii inamfanya
awe mtu makini wa kuweza ku-
changanua mambo kwa busara na
uadilifu na kusaidia kutoa ushauri
madhubuti katika Shirika.
Makia amelitumikia Shirika la
Umeme (TANESCO) katika nya-
dhifa mbalimbali za uongozi ikiwa
ni pamoja na kukaimu nafasi ya
Katibu wa Shirika, Mshauri wa
Sheria (Legal Counsel), pia am-
etumika kama Mtaalam wa sheria
(Legal Specialist) katika kilichoku-
wa Kitengo cha Ubinafsishaji wa
Shirika (Privatization).
Kutokana na taaluma yake na
uzoefu wa miaka mingi katika ma-
sula ya uzalishaji umeme, Uongozi
wa Shirika una imani na uwezo al-
ionao katika kufanikisha mipango
na malengo kama yalivyoainishwa
katika dira ya Shirika.
Kutokana na taaluma na uzoe-
fu wa miaka mingi katika utendaji
wa shirika la umeme (TANESCO)
Uongozi wa Shirika una imani na
uwezo walionao viongozi hawa
wapya katika kufanikisha mipango
na malengo kama yalivyoainishwa
katika dira ya Shirika.

7
Bulletin News
http://www.mem.go.tz
NISHATI/MADINI
TPDC yaibuka
kidedea kwenye
maonesho ya
Sabasaba
Greyson Mwase
na Malik Munisi
S
hirika la Maendeleo ya
Petroli Nchini (TPDC)
limeibuka kidedea na
kukabidhiwa kikombe
cha ushindi katika
kundi la mashirika ya petroli
na mafuta nchini baada ya
kuyashinda mashirika mengine
yaliyokuwa yanawania kikombe
hicho katika Maonesho ya 38
ya Kimataifa ya Sabasaba ya-
nayofanyika katika viwanja vya
Mwalimu Nyerere vilivyopo ji-
jini Dar es Salaam.
Kikombe hicho kilikabidhi-
wa na mgeni rasmi Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi
Seif Ali Iddi ambapo aliyataka
makampuni mengine kuiga mfa-
no wa TPDC katika uwekezaji
kwa maendeleo ya nchi.
Balozi Iddi alisema ili nchi
yoyote iweze kukua kiuchumi
haina budi kuwekeza kupitia vi-
wanda na kusema kuwa serikali
imeweka mkakati wa kuhakiki-
sha kuwa viwanda vinachangia
kwa kiasi kikubwa katika ukuaji
wa uchumi wa nchi.
Akizungumza mara baada
ya kukabidhiwa kikombe hicho
kwa niaba ya TPDC Msemaji
wa shirika hilo na Msimamizi
wa banda Bw. Sebastian Shana
amesema kuwa ushindi huo
ni faraja kwa shirika hilo na
kuongeza kuwa shirika hilo li-
taendelea kushirikiana na wadau
mbalimbali katika kuchangia
ukuaji wa uchumi kupitia sekta
za gesi na mafuta.
Akizungumzia siri ya mafan-
ikio ya ushindi Shana alisema ni
kuanza kwa maandalizi mape-
ma na kujituma zaidi.
Mikakati ya shirika hilo Bw.
Shana alisema kuwa shirika hilo
limepanga kufanya utafiti zaidi
wa gesi na mafuta kwa kush-
irikiana na wadau mbalimbali ili
kuhakikisha nchi inapiga hatua
kubwa kiuchumi.
Unajua nia ya serikali ni
kuhakikisha kuwa nchi inakuwa
katika kipato cha kati ifikapo
mwaka 2025, na katika kuhakik-
isha serikali inafikia lengo hilo,
TPDC ipo tayari kushirikiana na
wadau wa ndani na nje ya nchi
katika kuendeleza sekta ya gesi
na hivyo kuchangia katika ukua-
ji wa uchumi wa nchi. Alisema
Bw. Shana
Bwana Shana aliendelea
kusema kuwa gesi iliyogunduli-
wa inachangia kwa zaidi ya asil-
imia 50 katika umeme wa gridi
ya taifa na kusisitiza kuwa kama
shirika, wako tayari kuweka ngu-
vu zaidi katika utafutaji na uzal-
ishaji wa gesi ili iweze kuwa na
mchango mkubwa zaidi katika
uzalishaji wa umeme.
Bw. Shana alisema kuwa
TPDC imekuwa ikishirikiana
na wadau wakuu kama Wizara
ya Nishati na Madini ambayo
imelisaidia shirika hilo kupiga
hatua kubwa katika uendelezaji
wa shughuli za utafutaji wa gesi
na mafuta.
Hii ni mara ya saba kwa
shirika hilo kujinyakulia
vikombe kwenye Maonesho ya
Kimataifa ya Sabasaba tangu
lilipoanza kushiriki.
Washiriki kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) wakiwa katika picha ya
pamoja na kikombe cha ushindi mara baada ya kuibuka washindi wa kwanza katika kundi la
makampuni ya mafuta na gesi katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri Nishati
kuongoza ujumbe wa
Tanzania Canada
Teresia Mhagama
Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga, ataongoza
ujumbe wa Tanzania kwenda nchini Canada kwa ajili ya ziara ya
kikazi ambayo inalenga kuiwezesha serikali na watunga sheria
kuongeza uelewa kuhusu namna bora ya uandaaji, usimamizi na
na utekelezaji wa miradi ya Nishati na Madini nchini pamoja na
kupata uelewa wa namna Serikali inavyoweza kuongeza mapato
kupitia miradi ya uziduaji.
Mhe. Kitwanga ataongozana na wajumbe wa Kamati ya Ku-
dumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Naibu katibu Mkuu,Wizara
ya Nishati na Madini, Eng.Ngosi Mwihava na wataalam kutoka
wizarani ambao kwa pamoja watatembelea miradi mbalimbali
ya Nishati na Madini pamoja na Taasisi za elimu ya Juu kuanzia
tarehe 7 hadi 22 Julai 2014.
Kampuni tanzu ya
umeme utokanao na
jotoardhi kuanzishwa
Na Henry Kilasila
Kufuatia uhitaji wa nishati ya umeme nchini Shirika la
Umeme Tanzania limeanzisha Kampuni tanzu itakayojishu-
ghulisha na utafiti na uzalishaji umeme utokanao na joto ar-
dhi, yaani Geothermal Energy. Kampuni hiyo imesajiliwa
rasmi kisheria na kutambuliwa na Serikali.
Kufuatia kuanzishwa kwa Kampuni hiyo Tanzu ya Tan-
zania Geothermal Development Company Limited (TG-
DLC), Mhandisi Boniface Simon Njombe ameteuliwa kuwa
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo kuanzia tarehe 1/6/2014.
Uteuzi huu unalenga kuendeleza tafiti na uzalishaji umeme
wa joto ardhi (Geothermal Energy) nchini kama chanzo
kingine kikubwa cha umeme kwa ajili ya maendeleo ya nchi
yetu.
Tangu alipoajiriwa mwaka 1986, amelitumikia Shirika la
Umeme (TANESCO) katika nyadhifa mbalimbali hadi ku-
fikia ngazi za juu za uongozi. Injinia Njombe ameshika na-
fasi mbali mbali ndani ya Shirika, kama ifuatavyo;
Amewahi kuwa Meneja wa vituo vya Kuzalisha Umeme
wa Maji - Pangani, Mratibu mkuu wa miradi millennia chini
ya ufadhili wa Serikali ya Marekani (Project Coordinator -
MCC ), Meneja wa Mkoa wa Arusha, Kaimu Mkurugenzi
wa Miradi, Mhandisi Mkuu Miradi na mpaka anateuliwa ali-
kuwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia masu-
ala ya Uzalishaji Umeme.
Mhandisi Boniface Njombe ana Shahada ya Uhandisi
kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alipohitimu mwaka
1987 na ni mwenye upeo mkubwa wa masuala mbalimbali
ya kitaifa na kimataifa kuhusiana na masuala ya kiufundi na
ki-uongozi. Hii inatokana na kuwa amehudhuria mafunzo,
makongamano, warsha na semina mbalimbali ndani na nje
ya nchi zilizomfanya kuwa mmoja wa wahandisi mahiri we-
nye uwezo wa kusimamia kampuni mpya iliyoundwa.

Mitambo ya kufua umeme kwa kutumia Methanol nchini Canada
8 Bulletin News
http://www.mem.go.tz
HABARI
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wasiliana nasi kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
au Fika Ofsi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: badra77@yahoo.com
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
TANZANIA DAIMA LAIKOSEA WIZARA
Teresia Mhagama
Dar es Salaam
S
erikali imetangaza kukamilika
na kuanza kwa utekelezaji wa
Mkakati na Mwelekeo wa kubore-
sha Sekta Ndogo ya umeme nchini
ili kuongeza ufanisi, upatikanaji na
ubora wa huduma ya umeme.
Akitangaza mkakati huo mbele ya
waandishi wa habari jijini Dar es salaam,
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini,
EliakimMaswi ameeleza kuwa mkakati
huo ulioanza kutekelezwa Julai mosi
mwaka huu unalenga kulipunguzia mzigo
Shirika la Umeme nchini (TANESCO) wa
kuwa ndilo lililobeba jukumu kuu la uzal-
ishaji, usambazaji na usafirishaji umeme
kwani sasa shirika hilo litagawanywa katika
awamu mbalimbali na wawekezaji binafsi
wataruhusiwa kupeleka huduma hiyo kwa
wananchi.
Alisema kuwa mkakati huo unaainisha
kuwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
utabaki kama ulivyo lakini Wakala huo
utasadia utekelezaji wa majukumu ya ofisi
za kanda za TANESCO ambazo zitaanza
kujitegemea.
Mwongozo wa kutekeleza maboresho
ya sekta ndogo ya umeme umeme uko ka-
tika awamu nne na kuna mambo ambayo
yameanza kutekelezwa ndani ya mwaka
mmoja, ambao ni Julai 2014 hadi 2015,
mengine yatafanyika ndani ya muda mfupi
yani mwaka 2015 hadi 2018, na kuna masu-
ala yatakayotekelezwa katika muda wa kati
ambao ni 2018-2021 na awamu ya mwisho
ya utekelezaji wa mkakati itafanyika mwaka
2021 hadi 2025.Alifafanua Katibu Mkuu
Amesema kuwa mkakati na mwelekeo
wa mwaka mmoja ulioanza kutekelezwa
Julai mosi 2014 na unaotarajiwa kufika
ukomo mwaka 2015, umeainisha masuala
muhimu yanayohitaji kutekelezwa ndani ya
kipindi hicho ili kuboresha sekta ndogo ya
umeme ambayo kuwa ni pamoja na kuima-
risha hali ya kifedha ya Tanesco, kufanya
tathmini ya mali na madeni ya shirika, ku-
fanya tathmini ya mahitaji ya rasilimali
watu, kufanya ukaguzi wa mifumo ya
taarifa za umeme, na kudhibiti upotevu wa
umeme kutoka asilimia 19 hadi 18.
Katibu Mkuu mefafanua kuwa
Mkakati na Mwelekeo huo wa sekta ndogo
ya umeme pia umeainisha masuala yatakay-
ofanyika katika kipindi cha mwaka 2015
hadi 2018 kwamba ifikapo Desemba 2017
itaanzishwa kampuni mpya inayojitegemea
ya uzalishaji umeme, huku shughuli za
usafirishaji na usambazaji umeme zikienda
pamoja.
Tunasema kuwa shughuli za uzal-
ishaji umeme zitakuwa zikijitegemea ifikapo
mkwaka 2017 kwa sababu mpaka mwaka
huo tayari Tanzania itakuwa na umeme wa
kiasi cha megawati 3000 kiwango ambacho
kinaruhusu utenganishaji wa shughuli za
uzalishaji umeme kutoka katika usafirishaji
na usambazaji.Alisisitiza Katibu Mkuu.
Katika kipindi hiki alieleza kuwa sheria
ya umeme ya mwaka 2008 itarekebishwa
hasa kifungu 41 (6) ili kuruhusu wawekezaji
binafsi kuuza umeme moja kwa moja kwa
watumiaji wakubwa.
Kuhusu Ofisi za Tanesco mikoani
kuwa na maamuzi, Katibu Mkuu alieleza
kuwa ifikapo Desemba 2016 maamuzi ya
ununuzi na mipango ya Tanesco itagatuliwa
kutoka makao makuu hivyo watumishi wa
mikoani watakuwa na madaraka kamili ya
kufanya mipango na manunuzi lengo likiwa
ni kuongeza ufanisi katika kanda na mikoa.
Masuala mengine yatakayofanyika
katika kipindi cha mwaka 2015 hadi 2018
ni kudhibiti upotevu wa umeme kutoka
asilimia 18 hadi asilimia 16 ifikapo mwaka
2016 na kuanzisha dawati linaloshughulikia
masuala yote yanayohusu umeme.
Habari njema kwa wawekezaji binafsi
zilizoainishwa katika mkakati na mwele-
keo wa sekta ndogo ya umeme ni kuwa
kuanzia Desemba 2017 wazalishaji bin-
afsi wa umeme watakuwa na mamlaka ya
kuuza umeme moja kwa moja kwa wa-
nanchi badala ya kuiuzia TANESCO tu.
Maswi ameeleza kuwa masuala mengine
yaliyoainishwa ili kutekelezwa katika katika
kipindi cha 2015-2018 ni kuongeza uungan-
ishaji umeme kutoka asilimia 30 hadi 33,
kuanzisha msimamizi huru wa biashara ya
umeme, na kuanzisha msimamizi huru wa
mfumo wa umeme.
Vilevile alitanabaisha kuwa masuala
yanayopaswa kutekelezwa katika kipindi
cha muda wa kati, mwaka 2018 hadi 2021
ni kutenganisha shughuli usambazaji na
usafirishaji umeme hivyo ofisi za kanda
zitakuwa zikijitegemea katika kusambaza
na kusafirisha umeme kwa ushindani, pia
kupunguza upotevu wa umeme kutoka
asilimia 16 hadi 14, kuongeza uunganishaji
umeme kutoka asilimia 33 hadi 39, na ku-
weka kanuni na taratibu za uendeshaji wa
biashara ya uuzaji wa umeme moja kwa
moja kwa watumiaji wadogo.
Kuhusu awamu ya mwisho ya Mkaka-
ti na Mwelekeo wa kuboresha Sekta Ndogo
ya Umeme ambayo itafanyika mwaka
2021 hadi 2025, Katibu Mkuu aliyataja ma-
jukumu yanayopaswa kufanyika kuwa ni
kuanzisha kampuni za usambazaji umeme
zinazojitegemea, kampuni za umeme ku-
jisajili katika Soko la Hisa la Dar es Salaam,
kupunguza upotevu wa umeme kutoka
asilimia 14 hadi 12, kuongeza uunganishaji
umeme kutoka asilimia 39 hadi 50 na ku-
fanya tathmini ya mahitaji ya rasilimali
watu na kuwekeza kwenye rasilimali hiyo.
Katibu Mkuu alidadafua kuwa ili
kutekeleza masuala yote yaliyoainishwa ka-
tika mkakati huo, ni lazima serikali ifanyie
kazi kazi vitu vinavyotishia kukwamisha
ukuaji wa sekta ndogo ya umeme.
Huku akitolea mfano hoja hatarishi ya
kuwa na mwitikio mdogo wa wawekezaji
katika sekta ya umeme kutokana na nchi
kuwa maskini, lakini Katibu Mkuu alieleza
kuwa suala hilo linaweza kutatuliwa kwa
kubadilisha sheria na taratibu zilizopo ili
kurahisisha shughuli za uwekezaji nchini.
Kihatarishi kingine kinachotia
mashaka ni suala la Tanesco kuleta faida
kama tunavyotarajia kwani Shirika hili li-
natumia fedha nyingi kwa ajili ya kuzalisha
umeme, ila serikali inaweza kuondokana
na kihatarishi hiki kwa kuondoa mitambo
ya dharura ambayo inatumia kiasi kikubwa
cha fedha ili kuzalisha umeme, pia serikali
kujikita katika ujenzi wa mitambo ya ku-
zalisha umeme kwa kutumia gesi ambayo
gharama zake ni nafuu na kurekebisha
gharama za bili ya umeme.Alisema Ka-
tibu Mkuu
Aliongeza kuwa ili sekta ndogo ya
umeme ichangie katika kufanya mageuzi
ya kiuchumi, ni lazima nchi iachane na
uzalishaji mdogo wa umeme na hili lita-
fanyika kuanzia mwaka 2017 ambapo
tayari kutakuwa na umeme wa kiasi cha
megawati 3000 huku lengo ni kuwa na
megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025.
Katibu Mkuu alitoa angalizo kuwa
pamoja na serikali kuja na Mkakati na
Mwelekeo mzuri wa sekta ndogo ya
umeme nchini lakini kama watendaji hawa-
tabadilika na kuachana na mawazo mgan-
do mkakati huo utakuwa hauna maana,
hivyo amewataka watendaji kubadilika na
kuwatumikia wananchi kwa ufanisi.
Utekelezaji wa majukumu yaliyopang-
wa kufanyika katika mwaka 2014/15 uta-
gharimu kiasi cha shilingi bilioni 565.771
ambapo fedha hizo zitatolewa na Wizara
ya Nishati na Madini, TANESCO na wa-
shirika wa maendeleo.
Mkakati
umeme
wakamilika
TUFANYE KAZI KWA UADILIFU, BIDII, WELEDI,
NA USHIRIKIANO BILA KUKATA TAMAA
DAIMA TUSONGE MBELE
KURUDI NYUMA NI MWIKO!!
UJUMBE WA WAZIRI WIKI HII
nTANESCO kugawanywa kwa awamu
n2017 wazalishaji binafsi ruksa kuuza umeme
nKutekelezwa 2014-2025
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, EliakimMaswi

You might also like