You are on page 1of 8

Balozi mpya wa marekani asifu serikali kupambana na rushwa Uk3

Toleo No.22 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe Juni 27-Julai 3, 2014
Bulletin
News
Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali
kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
au Fika Ofsi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: badra77@yahoo.com
http://www.mem.go.tz
HABARI ZA
NISHATI &MADINI
Canada yaipa
Tanzania
kipaumbele
Soma Tahariri...Uk3
Na Teresia Mhagama
I
meelezwa kuwa Tanza-
nia ni miongoni mwa
nchi 12 barani Afrika zi-
lizo katika mpango maal-
umu unaoainisha nchi
zitakazopewa vipaumbele vya
uwekezaji na biashara utaka-
otekelezwa na Serikali ya Can-
ada katika kipindi cha miaka
mitano ijayo.
Hayo yamesemwa na Wa-
ziri wa Bishara za Kimataifa
wa Canada Bw. Ed Fast aliy-
emtembelea Waziri wa Nishati
na Madini Profesa Sospeter
Muhongo Makao Makuu ya
Wizara ya Nishati na Madini
jijini Dar es Salaam akiwa
ameambatana na ujumbe wa
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter
Muhongo (kulia) akiwa na Waziri wa Biashara za
Kimataifa wa Canada Bw. Ed Fast.
<
2 Bulletin News
http://www.mem.go.tz
Mpango Kabambe wa
Umeme kukamilika 2016
Na Teresia Mhagama
M
pango Kabambe
wa kuboresha zaidi
mfumo wa umeme
nchini unaoandaliwa
na wataalam kutoka Shirika la
Kimataifa la Maendeleo la Japan
(JICA), Shirika la Umeme nchini
(Tanesco) na Wizara ya Nishati na
Madini utakamilika ifikapo mwaka
2016.
Kamishna Msaidizi wa Nishati
anayeshughulikia gesi, Mhandisi
Norbert Kahyoza ameeleza hayo
jijini Dar es Salaam, katika warsha
ya siku moja ya kujadili ripoti ya
mpango huo iliyoshirikisha wadau
mbalimbali ili waweze kutoa maoni
yatakayoboresha mpango huo.
Kamishna Msaidizi amesema
kuwa kukamilika kwa mpango huo
kutakuwa na manufaa makubwa
kwa Tanzania kwani kutapele-
kea kuwapo kwa mfumo mpya
wa umeme hivyo nchi kuwa na
umeme wa uhakika tofauti na sasa
ambapo umeme umekuwa ukika-
tika mara kwa mara au kutowaka
vizuri kutokana na sababu mbalim-
bali ikiwamo nyaya au transfoma
kuchoka.
Mifumo mingi ya kutoa hudu-
ma za umeme nchini na hasa Dar
es Salaam sio mizuri hivyo Waja-
pan kupitia JICA wanasaidia kutoa
utaalam wa kuboresha mfumo huo
kwa kuweka mfumo mpya huku
wakisaidiana na wataalam wetu
hapa nchini Alisema Kahyoza.
Amesema kuwa mradi huu
utanufaisha maeneo ambayo tayari
yana umeme na yale ambayo bado
hayajafikiwa na huduma hiyo na
ukomo wake utakuwa mwaka
2040.
Naye Kamishna Msaidizi wa
Nishati anayeshughulikia Umeme,
Mhandisi Innocent Luoga amese-
ma kuwa mpango kabambe wa
kuboresha mfumo huo wa umeme
utaanza kutekelezwa katika jiji
lote la Dar es salaam na mkoa wa
Pwani katika wilaya za Mkuranga,
Kisarawe na Kibaha na Bagamoyo.
Mpango huu kabambe hauta-
gusa mikoa miwili tu bali utatekele-
zwa nchi nzima ndio maana
warsha hii imehusisha wataalam
wote watakaohusika na utekelezaji
huo zikiwemo Wizara ya Fedha,
Wizara ya Ujenzi, Ofisi ya Rais
ya Uchumi na Mipango, Wizara
ya Viwanda na Biashara, Wizara
ya Ardhi, Ofisi ya Takwimu za
Taifa, na Taasisi mbalimbali zilizo
chini ya Wizara kama Wakala wa
Umeme Vijijini (REA), Shirika la
Umeme (TANESCO) na Shirika
la Maendeleo ya Petroli (TPDC)
na Mamlaka ya Udhibiti wa Maji
na Nishati (Ewura). Alisema
Mhandisi Luoga.
Amesema mpango huo utaku-
wa ni dira ya kuendeleza nishati
ya umeme nchini na kwamba hii
si mara ya kwanza kwa Shirika la
Maendeleo la Japan (JICA) kusaid-
ia kuboresha hali ya umeme nchini
kwani tayari limeshasaidia kubore-
sha miundombinu ya umeme ka-
tika mikoa ya Dar es salaam, Kili-
manjaro na Arusha na sasa hali ya
umeme hasa katika jiji la Dar es
Salaam imeendelea kuimarika.
Naye Mwakilishi Mkazi wa
JICA nchini Tanzania Bw. Yasu-
nori Onishi amesema kuwa serikali
ya Japan kupitia JICA imeamua
kusaidia katika mpango wa kubore-
sha mfumo wa umeme nchini kwa
kuwa sekta ya nishati ni muhimu
kwa maendeleo endelevu ya nchi
na utoaji umeme wa uhakika un-
achangia vitu vingi ikiwamo ukuaji
uchumi na upunguzaji umaskini.
Amesema kuwa mradi huu
ni muhimu sio tu katika kubore-
sha hali ya umeme, nchini bali pia
wataalam wazawa watapata uta-
laam na uzoefu kutoka kwa wen-
zao wa Japan na hii itawawezesha
wazawa hapo baadaye kuandaa mi-
pango hiyo bila kutegemea wataal-
am kutoka nchi za nje.
Utekelezaji wa mpango huo
wa kuboresha mfumo wa umeme
utakaodumu kwa miaka 24 utaan-
za kutekelezwa baada ya kupata
maoni ya wadau, kufahamu ghara-
ma za mpango huo, na upatikanaji
NISHATI/MADINI
MUHONGO ATAKA WAWEKEZAJI MAKINI
Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia gesi, Eng. Norbert Kahyoza (watatu kutoka
kushoto), Mwakilishi Mkazi wa JICA nchini Tanzania Bw. Yasunori Onishi, (wa tatu kutoka
kulia) na Kamishna Msaidizi Nishati anayeshughulikia Umeme, Eng. Innocent Luoga (wa
kwanza kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na watalaam mbalimbali kutoka nchini
Japan na Tanzania kabla ya kuanza kwa warsha ya kujadili ripoti ya mpango kabambe wa
umeme iliyoandaliwa na wataalam kutoka Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Wizara ya
Nishati na Madini na Shirika la Umeme nchini (TANESCO).
Na Veronica Simba
W
aziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Muhongo
amewataka wawekezaji
wenye nia ya kuwekeza ka-
tika miradi inayosimamiwa
na wizara yake kujikita katika eneo mahsusi
wanalodhamiria kuwekeza wakati wanapo-
wasilisha mapendekezo yao ya uwekezaji.
Alitoa wito huo mwishoni mwa wiki
alipokutana na wamiliki wa Kampuni ya
A to Z Investments Corporation Ltd walio-
wasilisha maombi ya kujenga Kiwanda cha
kusafisha mafuta ya Petroli (Petroleum Oil
Refinery) hapa nchini lakini badala ya ku-
jikita kwenye eneo husika, maombi yao ya-
ligusa eneo pana zaidi na hivyo kupunguza
ushawishi.
Profesa Muhongo alimweleza Rais wa
Kampuni hiyo, Zahiir Suleyman kuwa moja
ya vigezo vinavyofanya maombi (proposal)
kuwa na ushawishi ni kujikita katika eneo
mahsusi ambalo mwekezaji analenga ku-
wekeza. Kwenda nje ya mada na kuongelea
mambo mengine inapunguza ushawishi wa
maombi husika, alisisitiza.
Aidha, Waziri Muhongo alitumia fursa
hiyo kuweka bayana kuwa wawekezaji wote
wenye nia ya kufanya kazi na Wizara yake
wanapaswa kujitathmini kama wanavyo vi-
gezo vyote muhimu katika uwekezaji husika
vinginevyo maombi yao hayatakubaliwa.
Hatutaki ubabaishaji. Tunataka ku-
fanya kazi na wawekezaji makini ili tuweze
kufikia malengo, alisisitiza.
Waziri Muhongo amewaagiza wataala-
mu kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli
Tanzania (TPDC) kukutana na Wamiliki
hao kutoka Kampuni ya A-Z Julai 7 mwaka
huu, na kujadili maombi yao ya uwekezaji
kisha waishauri Wizara kuhusiana na
maombi husika.
inatoka Uk1 wataalam kutoka makampuni ya uwekezaji ya nchini
Canada.
Bw. Ed Fast alimweleza Waziri Muhongo kuwa mpango huo
maalum umeainisha sekta zitakazopewa vipaumbele vya uwekezaji
kuwa ni pamoja na madini, miundombinu, nishati jadidifu, usafiri,
elimu, gesi asilia na mafuta.
Waziri huyo wa Biashara wa Canada alisema kuwa ujumbe huo
wa makampuni mbalimbali ya Canada alioambatana nao umefika
wizarani ili kuzifahamu zaidi sekta za nishati madini, hususani nishati
jadidifu, gesi asilia na mafuta ili wataalam hao waweze kupata taarifa
zitakazowasaidia kufanya maamuzi ya uwekezaji nchini.
Naye Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo
ameishukuru Serikali ya Canada kwa kuichagua Tanzania kuwa moja
kati ya nchi 12 barani Afrika zitakazopewa vipaumbele vya uwekezaji
na biashara na nchi hiyo kwa kuwa fursa hiyo itaiwezesha Tanzania
kupiga hatua katika sekta za kiuchumi zilizoainishwa katika mpango
huo.
Amesema kuwa suala la Tanzania kuwa moja ya nchi zitakazo-
pewa kipaumbele na nchi hiyo ya Canada, pia limetokana na nchi hizi
mbili kuwa na historia ya mahusiano mazuri kwa muda wa takribani
miaka 50 hasa zikishirikiana katika masuala ya elimu, na kilimo.
Kuhusu maeneo ya uwekezaji, Waziri Muhongo alimweleza wa-
ziri huyo wa Canada kuwa kwa sasa serikali ya Tanzania inapambana
na vitendo vya rushwa jambo linalomaanisha kuwa muda wa kuwa na
mikataba mibovu kwa sasa hauna nafasi.
Watumishi wa Wizara na Taasisi zake wanaelewa kuwa hata
kama hatuna ushahidi wa mtumishi kupokea rushwa, endapo mfan-
yakazi ataonekana anaendekeza rushwa ataondolewa katika nafasi
aliyopo mara moja.Alisema Profesa Muhongo.
Kuhusu pato la Taifa, Profesa Muhongo amemweleza Waziri
huyo wa Canada kuwa pato la taifa na bajeti ya serikali bado ni ndogo
kuweza kupeleka fedha na teknolojia katika uwekezaji mkubwa kwe-
nye sekta za nishati na madini hivyo, serikali imeamua kufanya kazi
kwa karibu na sekta binafsi ili kuondokana na mazoea kwamba seri-
kali pekee inaweza kuendesha na kufanya mageuzi katika sekta hizo.
Kuhusu suala la uwekezaji katika sekta ya madini, Profesa Muhon-
go alitilia mkazo kuhusu kuwasaidia wachimbaji wadogo hivyo alitoa
mwaliko kwa makampuni madogo madogo kutoka nchini Canada
yanayotaka kufanya kazi na wachimbaji wadogo kuja nchini kushiriki-
ana na wachimbaji hao, kwa kuwa serikali ipo tayari kupata msaada
wa kifedha au mkopo kutoka serikali hiyo ili kusaidia uchimbaji mdo-
go nchini.
Akizungumza kuhusu Shirika la Umeme nchini (TANESCO),
Profesa Muhongo alisema muda wa shirika hilo kuwa ndiye mzal-
ishaji, msambazaji na msafirishaji wa umeme pekee nchini umefika
mwisho kwani katika uzalishaji umeme Tanesco itaendelea kuzalisha
umeme kutoka katika vyanzo inavyomiliki sasa lakini pia serikali ina-
karibisha makampuni binafsi kuzalisha umeme kutoka vyanzo mbal-
imbali.
Ameeleza kuwa ndani ya Tanesco kutakuwa na kampuni ndogon-
dogo zitakazojishughulisha na uzalishaji umeme kutoka vyanzo mbal-
imbali mfano ni kampuni ya umeme unaotokana na Jotoardhi ambayo
itaanza shughuli zake mnamo tarehe 1 Julai 2014, hivyo amekaribisha
kampuni kutoka nchini Canada na kwingineko duniani kuwekeza
kwenye miradi hiyo ya jotoardhi na kwa kushirikiana na kampuni hiyo
ya kitanzania au kwa uwekezaji binafsi.
Vilevile Profesa Muhongo alisema kuwa kutakuwa na kampuni
itakayokuwa ikijishughulisha na masuala ya umeme unaotokana na
upepo na nyingine ikijishughulisha na umeme jua hivyo ameyakari-
bisha makampuni mbalimbali kuwekeza kwenye miradi hiyo na seri-
kali ipo tayari kupata misaada ya kifedha au mkopo kutoka serikali ya
Canada ili kuendeleza miradi hiyo nchini.
Waziri Muhongo amesema kuwa kwa sasa Tanzania inakaribisha
makampuni yenye nia ya dhati kuja kuwekeza nchini na hivyo kuin-
ua uchumi wa nchi ili ifikapo mwaka 2025 watanzania wawe na hali
nzuri ya uchumi tofauti na ilivyo sasa.
Canada yaipa Tanzania kipaumbele
3
Bulletin News
http://www.mem.go.tz
MAONI
Na Veronica Simba
B
alozi mpya wa Mare-
kani hapa nchini
Mhe. Mark Childress
amesifu dhamira ya
dhati na mkakati wa
Serikali kutokomeza rushwa
hususan katika miradi mbalim-
bali ya maendeleo ikiwemo ya
gesi asilia.
Aliyasema hayo hivi ka-
ribuni alipotembelea Makao
Makuu ya Wizara ya Nishati na
Madini jijini Dar es Salaam na
kufanya mazungumzo na Wa-
ziri mwenye dhamana, Profesa
Sospeter Muhongo.
Katika mazungumzo yao,
Balozi Childress aliyeambatana
na Ujumbe wake alipongeza
jitihada zinazofanywa na seri-
kali hususan wizara ya nishati
na madini katika kupambana
na rushwa ili kuhakikisha
pesa zinazotolewa kwa ajili ya
utekelezaji wa miradi mbalim-
bali ya maendeleo zinatumika
kama ilivyopangwa.
Balozi Childress alisema
wazi kuwa ili kutoa misaada ya
maendeleo na kabla ya kuku-
bali kuingia ubia katika miradi
ya maendeleo, rushwa ni mo-
jawapo ya masuala yanayozin-
gatiwa sana na nchi yake.
Rushwa ni kikwazo ki-
kubwa katika utekelezaji wa
miradi hivyo sisi tunalipa suala
hilo umuhimu wa pekee kama
kigezo muhimu cha kufikia
maamuzi ya kusaidia miradi
ya maendeleo au kuingia ubia
katika miradi hiyo, alisisitiza
Balozi Childress.
Aidha, aliahidi nchi yake
kuimarisha ushirikiano na Tan-
zania kwa kuwekeza katika mi-
radi mbalimbali ya maendeleo
hususan katika sekta ya gesi
asilia.
Awali, Profesa Muhongo al-
imweleza Balozi Childress fursa
mbalimbali za uwekezaji zilizo-
po nchini hususan katika sekta
za nishati na madini na kuweka
bayana dhamira ya dhati ya
Serikali kuinua uchumi wa nchi
kupitia sekta husika.
Profesa Muhongo alim-
wambia Balozi Childress na
Ujumbe wake kuwa Serikali
imedhamiria kuwaondolea wa-
nanchi wake umaskini kwa ku-
ingia katika uchumi wa gesi.
Tumedhamiria kuondoa
umaskini Tanzania, na ili tu-
fanye hivyo inabidi tuingie kwe-
nye uchumi wa gesi, alisema
Muhongo.
Waziri Muhongo alitu-
mia fursa hiyo kuwashawishi
Wamarekani kuja kuwekeza
Tanzania katika miradi mbal-
imbali ya nishati na ile ya ma-
dini.
Alisema, Serikali imeweka
mazingira mazuri ya uwekezaji
nchini ikiwa ni pamoja na ku-
weka mikakati ya kutokomeza
kabisa mianya ya rushwa.
Akifafanua zaidi, alisema
kwamba tayari wizara yake ilik-
wishaanza utekelezaji wa mi-
kakati ya kuboresha mazingira
ya uwekezaji na kuhakikisha
wananchi wanapata huduma
sahihi na kwa ubora na kiwan-
go wanachostahili.
Tulidhamiria na kuwaahi-
di wananchi kuwa tutaliunda
upya Shirika la Umeme nchini
(Tanesco), na tayari tumeanza
utekelezaji wake, alisema Pro-
fesa Muhongo na kuongeza
kuwa mabadiliko ya muundo
wa shirika hilo yatatangazwa
rasmi kwa wananchi kufikia
mwishoni mwa mwezi huu.
Aidha, Waziri Muhon-
go alisisitiza kuwa wizara
yake imejipanga kuhakikisha
rushwa haipewi nafasi katika
mradi wowote ulio chini yake
ikiwemo ya gesi asilia na hivyo
kumtaka Balozi na Ujumbe
wake kutokuwa na wasiwasi
kuhusu ufanisi wa miradi wata-
kayoamua kuifadhili au kuingia
ubia na serikali.
Kwa upande wa sekta ya
madini, Profesa Muhongo
alisema wizara imekwishaanza
kuwawezesha wachimbaji wa-
dogo kwa mitaji na mafunzo
ili kuinua kipato chao na hivyo
waweze kuchangia katika kuku-
za uchumi wa taifa.
Alisema, dhamira ya Seri-
kali ni kuhakikisha sekta ya ma-
dini inakuwa na kuchangia sio
chini ya asilimia 10 katika pato
la taifa ifikapo mwaka 2025.
Alifafanua kuwa, Serikali
imelenga kuendeleza sekta ya
madini kwa namna kuu mbili;
kuwainua wachimbaji wadogo
na kuweka mazingira mazuri ya
uwekezaji ili kuvutia wawekeza-
ji kutoka nje. Aliongeza kuwa,
lengo ni kujenga mazingira
wezeshi ya wachimbaji wadogo
kushirikiana na wawekezaji.
Waziri Muhongo alimwam-
bia Balozi Childress kuwa hii
ni fursa nzuri kwa Serikali ya
Marekani kuwekeza Tanzania
katika miradi mbalimbali mi-
kubwa katika sekta za nishati
na madini.
Balozi Mark Childress
alianza kazi rasmi hapa nchini
mwishoni mwa mwezi Mei
mwaka huu.
BALOZI MPYA WA MAREKANI ASIFU
SERIKALI KUPAMBANA NA RUSHWA Tahariri
MEM
Na Badra Masoud
FIVE
PILLARS OF
REFORMS
KWA HABARI PIGA SIMU
KITENGO CHA MAWASILIANO
BODI YA UHARIRI
MHARIRI MKUU: Badra Masoud
MSANIFU: Essy Ogunde
WAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson Mwase
Teresia Mhagama, Nuru Mwasampeta
INCREASE EFFICIENCY
QUALITY DELIVERY
OF GOODS/SERVICE
SATISFACTION OF
THE CLIENT
SATISFACTION OF
BUSINESS PARTNERS
SATISFACTION OF
SHAREHOLDERS
TEL-2110490
FAX-2110389
MOB-0732999263
W
iki hii baadhi ya magazeti yaliandika
kwamba Shirika la Umeme nchini ku-
gawanywa na kuwa Mashirika mawili
baada ya Serikali kupitisha Mkakati wa
mwelekeo wa sekta ndogo ya Umeme
(ESI).
Utekelezaji wa Mpango huo ulielezwa kuanza Agosti
mwaka huu, na lengo likiwa ni kuhakikisha uzalishaji wa
umeme, unaongezeka kutoka megawati 1,583 zinazozal-
ishwa sasa hadi kufikia megawati 10,000 ifikapo mwaka
2025.
Maandalizi ya ugawaji wa TANESCO yataanza rasmi
Julai mwaka huu na utekelezaji wake unatarajiwa kuka-
milika Desemba 2017, ambako yataanzishwa Mashirika
mawili. Shirika moja litakuwa litashughulikia uzalishaji
wa umeme na Shirika jingine litashughulikia Usafirishaji
na Usambazaji Umeme.
Lengo kubwa la Serikali kuigawa TANESCO ni ku-
hakikisha watanzania wanakuwa na uhakika wa upati-
kanaji wa umeme pamoja na kuwapo kwa ufanisi wa hu-
duma kwa Watanzania.
Taarifa hizo zilipokewa kwa furaha kubwa na Watan-
zania wengi ambao baadhi yao walidai kwamba hatua
hiyo ya kuigawanya TANESCO waliisubiri kwa muda
mrefu na hivyo watafuatilia kwa karibu.
lakini pia wapo waliodai kwamba hayo ni maneno ya
serikali ambayo utekelezaji wake huenda utakuwa mgu-
mu.
Napenda kuwahakikishia Watanzania wote kwamba
suala la kuigawa TANESCO linafanyiwa kazi kwa uka-
ribu na umakini mkubwa na linatarajiwa kupitia hatua
moja hadi nyingine hadi itakapofikia hatua ya kuligawa
na kuwa na Mashirika mawili tofauti na lilivyo sasa, am-
bapo Shirika hilo linalosimamia majukumu yote yaani
uzalishaji Umeme, Usafirishaji Umeme na Usambazaji
Umeme.
Wizara ya Nishati na Madini inaendelea kufanya ma-
badiliko mbalimbali kwenye sekta ya Nishati na Madini
ambapo katika Sekta ya Nishati ya umeme imeamua ku-
fanya mabadiliko kadhaa ambayo yameanza kuonekana
miongoni mwa mabadiliko hayo ni kukabiliana na tatizo
la mgawo wa umeme ambapo jambo hilo limefanikiwa na
sasa hakuna mgawo huo.
Halikadhalika, Wizara imefanya mabadiko ya ndani
ya shirika kwa kupeleka madaraka zaidi ya kiutendaji
kati mikoa ya TANESCO pamoja na kuwapa madaraka
makubwa Mameneja waandamizi wa kanda wa Shirika
hilo.
Hayo ni baadhi ya mabadiliko yanayoendelea ndani
ya TANESCO ambayo kwa namna moja ama nyingine
ni uthibitisho wa kutosha kuwa Wizara hii imedhamiria
kwa uhakika kuleta mabadiliko makubwa kwenye sekta
ya umeme ili uchumi ukue na kulifanya taifa la Tanzania
kufikia pato la kati ifikapo mwaka 2025.
Tunawaomba watanzania waungane nasi kwa kutupa
ushirikiano katika utekelezaji wa mpango huo wa kui-
gawa TANESCO.
Watanzania
mtuunge mkono
kuigawa TANESCO!!!
TEL-2110490
FAX-2110389
MOB-0732999263
nAahidi ushirikiano sekta za nishati, madini
4 Bulletin News
http://www.mem.go.tz
NISHATI
Matukio katika picha
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake wakiwa katika picha ya pamoja
baada ya TANESCO kupata kombe la Ushindi katika kipengele cha Taasisi iliyotoa huduma Bora na
Ubunifu wakati wa Maonesho hayo.
http://www.mem.go.tz
Mhandisi Mwandamizi Masoko na Huduma kwa Wateja, Juliana Pallangyo kutoka Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) akimweleza Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue namna mashine ya
Umeme Tayari (UMETA) Ready Board inavyofanya kazi. Anaesikiliza ni Katibu Mkuu Bw. Eliakim
Maswi(wa pili kushoto) na mgeni aliyefika banda la Wizara.
Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzania, Mhe.
Mark Childress akimweleza Waziri wa Nishati
na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo
pichani) utayari wa nchi yake kushirikiana na
Tanzania katika kuendeleza miradi mbalimbali
ya maendeleo hususan katika sekta ya gesi asilia.
Balozi Childress na ujumbe wake walitembelea
Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini jijini
Dar es Salaam ambapo walikutana na kuzungumza
na Waziri Muhongo na Maafisa Waandamizi wa
Wizara pamoja na Taasisi zilizo chini yake.
5
Bulletin News
http://www.mem.go.tz
Tuzo za madini
YALIOJIRI WIKI HII
Baadhi ya wananchi waliotembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini, wakipata
ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusu shughuli za Wizara. Wa kwanza
kushoto ni Mtalaam kutoka Idara ya Madini, Bi.Sijaona Madika akimweleza mwa-
nanchi kuhusu ada mbalimbali za umiliki wa leseni za utafutaji na uchimbaji
madini .
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Maafsa
Waandamizi wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake, wakiwa katika mazung-
umzo na Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Mark Childress na
Ujumbe wake.
Matukio katika picha
Waziri wa Nishati na Madini,
Prof Sospeter Muhongo
(Kushoto) pamoja na
watendaji wa wizara na
taasisi zilizo chini ya wizara
akizungumza na Balozi wa
Tanzania nchini Urusi Luteni
Jenerali, Mathew Kisamba
(Mwenye shati Nyekundu)
aliyefika wizarani kwa lengo
la kupokea mapendekezo ya
maeneo ya ushirikiano wa
kiuchumi atakayowasilisha
nchini Urusi ili kuwezesha
uboreshwaji wa sekta za
nishati na madini.
Na Mwandishi Wetu
M
kutano Mkuu wa 17
wa wanachama wa
Baraza la Habari Tan-
zania (MCT) umem-
chagua tena Bi Badra
Masoud kuwa mjumbe wa bodi wa
baraza hilo kwa kipindi cha miaka
mitatu. Aidha Mkutano huo umem-
chagua Jaji Mstaafu Thomas Mihayo
kuwa Mwenyekiti wa Bodi wa Baraza
hilo akimrithi Jaji Robert Kisanga.
Mkutano huo wa MCT uliofanyika
Jumatano wiki hii Wilayani Bagamoyo
Mkoa wa Pwani pia umemchagua Has-
san Abdallah Mitawi ambaye ni Mku-
rugenzi wa Shirika la Utangazaji Zan-
zibar (ZBC) kuwa mjumbe wa bodi na
Makamu Mwenyekiti wa baraza hilo.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi,
Mwenyekiti wa Uchaguzi katika Mku-
tano huo Bi. Jane Mihanji alisema ka-
tika uchaguzi huo umewarejesha kwe-
nye bodi hiyo ya MCT, Badra Masoud
na Rose Haji, ambaye ni mwandishi
mkongwe, kuendelea na wadhifa wao.
Mihanji alisema kulingana na
Katiba ya MCT, wajumbe hao wawili
waliomaliza muda wao wanaruhusiwa
kuendelea na wadhifa huo kwa kipindi
kingine.
Wajumbe wapya waliochaguliwa
ni Mhariri wa gazeti la Daily News
Bi. Tuma Abdallah, Mhariri wa The
Guardian Bw. Wallace Maugo.
Kutoka kwenye kundi la jamii, wal-
iochaguliwa kuingia kwenye bodi hiyo
ni Prof. Bernadetha Killian, ambaye
ni Mkuu wa chuo Kikuu kishiriki cha
Elimu Mkwawa cha Chuo Kikukuu
cha Dar es Salaam na Alli Mfuruki
ambaye ni Mwenyekiti wa Kampuni
ya Mwananchi Group ya Magazeti ya
Mwananchi na Zuku na mwingine ni
Jaji Mstaafu Juston Mlay.
Tunampongeza Badra Masoud na
kumtakia Kila la Kheri!!
Badra achaguliwa
tena bodi MCT
6 Bulletin News
http://www.mem.go.tz
HABARI/TANGAZO
Na Asteria Muhozya,
Dar es Salaam
W
anafunzi kutoka baadhi
ya Shule za Sekondari ji-
jini Dar es Salaam wame-
tembelea banda la Wizara
ya Nishati na Madini na
Taasisi zilizo chini yake wakati wa Maone-
sho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, kutaka
kufahamu shughuli za nishati na madini zi-
nazosimamiwa na wizara.
Wakati wanafunzi hao walipotembelea
Wizara na Taasisi zake, wameoneshwa ku-
vutiwa na kutaka kufahamu kuhusu namna
shughuli za uchimbaji madini nchini zina-
vyofanyika, kutaka kufahamu aina za ma-
dini yenye thamani kubwa na madini yenye
uzito mkubwa yanayopatikana nchini.
Vilevile, wanafunzi hao wametaka
kuelimishwa kuhusu shughuli za utafiti na
uchimbaji wa gesi zinazofanyika nchini
ikiwa ni pamoja na kutaka kufahamu vyuo
mbalimbali vinavyotoa mafunzo kuhusu
masuala ya gesi, mafuta na madini.
Aidha, wengi wao walipenda kuona
madini ghafi ya Tanzanite yanayopatikana
nchini ikiwa ni pamoja na kufahamu aina
zote za madini yaliyopo nchini. Wanafun-
zi hao wamepata nafasi ya kupata majibu
kuhusu masuala mbalimbali waliyouliza
kutoka kwa waatalamu wa Wizara na
Taasisi waliokuwa kwenye maonesho hayo.
Wanafunzi Dar es Salaam
wavutiwa na Madini/Gesi
Mhandisi wa Nishati kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Robert Dule,
akiwaeleza wanafunzi kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu nishati wakati
wanafunzi hao walipotembelea banda la Wizara.
Na Nuru Mwasampeta,
Dar es Salaam
B
aadhi ya wananchi wa jijini Dar
es Salaam waliofika kutembelea
banda la Wizara ya Nishati na
Madini na Taasisi zake katika
maonesho ya Wiki ya Utrumi-
shi wa Umma wameshauri watumishi wa
Umma kufanya kazi kwa bidii na uadilifu.
Wengi wa wananchi wameeleza kuha-
masika kutembelea Banda la Wizara ili
kupata ufahamu zaidi wa masuala mbalim-
bali yanayohusu sekta za nishati na madini
hususan gesi asilia ambayo wamekuwa wa-
kiyasikia kupitia kwa watu mbalimbali na
vyombo vya habari lakini maonesho hayo
yamewapa fursa ya kuonana moja kwa
moja na wataalam wanaohusika na masu-
ala hayo na hivyo hiyo imekuwa fursa ya
wao kufahamu mambo mengi ya kiutaal-
am.
Mmoja wa wananchi aliyejitambuli-
sha kwa jina la Nubi Mwanzalima kutoka
Tabata Changombe amesema alikuwa
na kiu kubwa ya kukutana na wataalamu
wa Wizara ya Nishati na Madini ili wam-
jibu maswali yake kuhusu namna gesi asilia
itakavyowanufaisha wananchi wa kawaida.
Akijibu swali hilo, Mhandisi Victor La-
baa alisema wananchi watanufaika kwa
namna mbalimbali ikiwemo kutumia fursa
husika kuanzisha biashara mbalimbali ili
kujiongezea kipato na hivyo kukuza uchu-
mi wa mtu mmoja mmoja na wa nchi kwa
ujumla.
Aidha wananchi wengi walionesha ku-
furahishwa zaidi na utendaji wa wizara na
kuitaka wizara kuzidisha juhudi katika ku-
wasaidia watanzania waweze kuondokana
na umaskini pamoja na kukuza kipato cha
taifa kupitia rasilimali za gesi na madini
Katika mchango wake Bw. Salige Musy-
angi mmoja kati ya watanzania waliotem-
belea banda la wizara alisema kazi ni nzuri
inatia matumaini aliongeza kwa kusema
kuwa mti wenye matunda hauachwi ku-
pigwa mawe, endeleeni mbele msikatishwe
tamaa. alisisitiza.
Kwa upande wake Bw. John Bukuku
mwandishi na mmiliki wa mtandao wa
kijamii wa FullShangwe alisema amefura-
hishwa sana na kazi ya Waziri Profesa Sos-
peter Muhongo kwa kusambaza umeme
vijijini, amesema amekuwa akitembelea vi-
jiji vingi na kuona kazi kubwa iliyofanyika.
Aidha ameishauri serikali kujitahidi kutoa
pesa ili miradi iliyopangwa kutekelezwa
ikamilike kwa wakati.
Fanyeni Kazi! Wananchi wanena
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
TAARIFA KWA UMMA
KUANZA KWA UKAGUZI WA UZALISHAJI NA MAUZO YA
MADINI YA UJENZI NA VIWANDANI MKOANI
MOROGORO, TAREHE 01 JULAI, 2014
Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) kwa kushiriki-
ana na Ofsi ya Afsa Madini Mkazi Morogoro unawatangazia
wamiliki wa leseni za uchimbaji pamoja na wafanyabiashara
wa madini ya ujenzi na viwandani (mawe, kotoko, mchanga,
kifusi, chokaa, cheap stone (feldspar na quarts), shaba ghaf
na chuma ghaf) kwamba, utaratibu wa matumizi ya Hati za
Mauzo ya Madini kukagua uzalishaji na mauzo ya madini hayo
mkoani Morogoro utaanza kutumika rasmi kuanzia tarehe 01
Julai, 2014. Wachimbaji wasio na leseni wanahimizwa kufka
Ofsi ya Madini Morogoro iliyopo mtaa wa Kitope jirani na Ofsi
za Hazina Ndogo ili kuomba kupatiwa leseni za uchimbaji. Mfa-
no wa Hati ya Mauzo itakayotumiwa na wamiliki wa leseni za
madini kujaza taarifa za mauzo kila yanapofanyika unaonekana
hapa chini:-
Wanunuzi na wasafrishaji wa madini hayo wanaagizwa kudai
Hati ya Mauzo toka kwa wamiliki wa leseni za uchimbaji ili kue-
puka usumbufu usio wa lazima wakati wa usafrishaji. Kutaku-
wa na vituo vya ukaguzi ambapo wasafrishaji watatakiwa
kusimama ili kukaguliwa na kuacha nakala ya Hati ya Mauzo.
Vitabu vya kutosha vya Hati ya Mauzo ya Madini vitagawiwa
bure kwa wamiliki wote wa leseni za uchimbaji madini husika
kabla ya kuanza kwa zoezi hilo.
IMETOLEWA NA OFISI YA AFISA MADINI MKAZI - MOROGORO
25 JUNI, 2014
7
Bulletin News
http://www.mem.go.tz
MADINI
Kiuchumi bado
tuko vibaya, lakini
bidii na hatua kubwa
inahitajika ili kufkia
Dira ya Maendeleo ya
Taifa ya 2025. Lazima
tuweke mazingira
wezeshi malengo yetu
yatimie
Na Asteria
Muhozya,
Dar es Salaam

UTHAMINI ALMAS
WAMFURAHISHA SEFUE
K
atibu Mkuu Kiongozi, Ba-
lozi Ombeni Sefue ame-
furahishwa na shughuli
za Uthamini Madini ya
Almas unaofanywa na Kitengo cha
Uthamini Madini ya Almas na Vito
(TANSORT), kilicho chini ya Wiz-
ara ya Nishati na Madini.
Balozi Sefue alipata fursa ya
kusikia namna kitengo hicho ki-
navyofanya kazi zake wakati ali-
potembelea banda la Wizara ya Ni-
shati na Madini wakati wa kilele cha
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi
wa Umma, yaliyofanyika katika vi-
wanja vya Mnazi mmoja jijini Dar
es Saalam.
Akitoa ufafanuzi kuhusu shu-
ghuli hizo, Mtaalam wa madini ya
Vito vya Rangi na Almas Bibi Teddy
Goliama, ameeleza kuwa, kitengo
hicho kinatoa huduma ya ushauri
wa masoko ikiwemo ukataji, ukadi-
riaji thamani kwa wachimbaji wa-
dogo na kuongeza kuwa, shughuli
hizo zinafanywa katika kiwango
cha Kimataifa.
Ameongeza kuwa, kitengo hicho
kinahakikisha kuwa, kinapata bei za
madini katika soko la kimataifa na
kuwasiliana na wachimbaji kuwafa-
hamisha kuhusu bei hizo.
Aidha, ameeleza kuwa, mbali
na kufanya utafiti wa masoko na
bei za almas na madini vito, TAN-
SORT inathamini almasi na madini
ya vito kwa lengo la kukokotoa mra-
haba.
Wakati huo huo, Katibu Mkuu
Kiongozi amefahamishwa kuhusu
namna mashine ya Umeme Tayari
(UMETA) Ready Board inavyo-
fanya kazi. Akitoa maelezo namna
kifaa hicho kinavyofanya kazi,
Mhandisi Mwandamizi Masoko
na Huduma kwa Wateja, Juliana
Pallangyo kutoka Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) ameeleza
kuwa, kifaa hicho kinatumika katika
maeneo yasiyohitaji wiring hasa vi-
jijini na kinatolewa bure vijijini.
Katika hatua nyingine, TANE-
SCO limeibuka na ushindi wa kuwa
miongoni mwa taasisi tatu bora
zinazotoa huduma kwa ubunifu
katika kilele cha Maadhimisho ya
Wiki ya Utumishi wa Umma, am-
bapo Wizara ya Nishati na Madini
imekuwa miongoni mwa taasisi 10
zenye mabanda bora katika maone-
sho hayo yaliyofikia kilele tarehe
23 Juni, katika Viwanja vya Mnazi
Mmoja jijini Dar es Salaam.
Akifunga rasmi maonesho hayo,
mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongo-
zi Balozi Ombeni Sefue amesisitiza
watumishi wa umma kuwatumikia
wananchi kwa uadilifu, ukarimu,
upendo, weledi na kwa wakati.
Aidha, amewataka watumishi
kujituma , kufanya kazi kwa bidii
na kuhakikisha wanatimiza wajibu
wao kwa mujibu wa sheria na tarati-
bu za utumishi wa umma bila shurti.
Kiuchumi bado tuko vibaya,
lakini bidii na hatua kubwa inahi-
tajika ili kufikia Dira ya Maendeleo
ya Taifa ya 2025. Lazima tuweke
mazingira wezeshi malengo yetu
yatimie. Amesisitiza Balozi Sefue.
nTANESCO yaibuka Mtoaji Huduma Bora na Ubunifu
nWizara yaingia 10 Bora
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Bw. Eliakim Maswi (kushoto)akimweleza jambo
mgeni aliyefika katika Banda la Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) aliyetaka kufahamu
kuhusu Mradi wa Umeme Vijijini unaosimamiwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA). Wa pili
kulia anayesikiliza ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava
na katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Nishati na Madini Bibi
Badra Masoud.
TUFANYE KAZI KWA UADILIFU, BIDII, WELEDI,
NA USHIRIKIANO BILA KUKATA TAMAA
DAIMA TUSONGE MBELE
KURUDI NYUMA NI MWIKO!!
UJUMBE WA WAZIRI WIKI HII
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Bw. Eliakim Maswi
kulia akimkaribisha katika banda la Wizara, Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alipotembelea banda hilo
wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa
Umma.
.
8 Bulletin News
http://www.mem.go.tz
HABARI
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wasiliana nasi kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
au Fika Ofsi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: badra77@yahoo.com
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
TANZANIA DAIMA LAIKOSEA WIZARA
Benki yaomba kutoa
mikopo miradi ya nishati
Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam
M
akamu wa Rais wa Benki
ya Kifaransa ya BNP Pari-
bas Corporate & Invest-
ment Banking na ujumbe
wake wamekutana na Wa-
ziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Muhongo kwa lengo la kutaka
kufahamu miradi na shughuli mbalimbali zi-
nazotekelezwa katika sekta ya nishati nchini, ili
benki hiyo iweze kutoa mikopo ya masharti
nafuu ya miradi inayotekelezwa na Wizara.
Akizungumza katika kikao hicho, Waziri
wa Nishati na Madini ameeleza kuwa, lengo la
serikali ni kuhakikisha kwamba sekta ya nishati
nchini inachangia kwa kiasi kikubwa katika
kubadilisha hali ya kiuchumi ya Tanzania ili
kuweza kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo
ya Taifa ya 2025.
Hivyo, ameongeza kuwa, serikali iko tayari
kufanya kazi kwa ubia na sekta binafsi ili ku-
weza kufikia malengo iliyojiwekea kupitia sekta
za nishati na madini ya kuhakikisha kuwa, in-
aongeza pato la taifa kupitia rasilimali hizo.
Aidha, ameeleza kuwa, ipo miradi mingi ya
kipaumbele ambayo inahitaji fedha na uwekeza-
ji katika sekta ya nishati ili iweze kutekelezwa
kwa muda uliopangwa na kuitaja miradi hiyo,
ikiwa ni pamoja na Mradi wa Makaa ya Mawe
wa Kiwira, unaosimamiwa na Shirika la Ma-
dini la Taifa (STAMICO) ambao unalenga ku-
zalisha megawati 200 za umeme .
Katika hatua nyingine, Waziri Muhongo
ameeleza kuwa, ili kuhakikisha kwamba len-
go la Wizara la kuondoa tatizo la nishati ya
umeme nchini linafikiwa, tayari maboresho ya-
mefanywa katika Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO), aidha mabadiliko ya kimuundo
yanafanywa katika Shirika la Maendeleo ya
Petroli Tanzania (TPDC) kwa lengo kuweza
kufikia adhma ya serikali ya kuubadilisha uchu-
mi wa Tanzania kupitia rasilimali za nishati na
madini.
Na Malik Munisi

P
amoja na kusimamia
shughuli za utafutaji na
uchimbaji wa Gesi asilia
na mafuta nchini, Shirika
la Maendeleo ya Petroli
Tanzania (TPDC) pia limekuwa liki-
jishughulisha na shughuli za jamii .
Hii imejidhihirisha baada ya
shirika hilo kusaidia kikundi cha
kina mamalishe mkoani Mtwara
jumla ya majiko 25 ya gesi pamoja
na mitungi yake.
Akiongea wakati wa kukabidhi-
wa msaada huo, Katibu wa kikundi
hicho, Bi. Ziha Khalid alieleza ni
kwa namna gani msaada huo uta-
wasaidia katika kuinua kipato chao.
Gharama za uendeshaji wa biasha-
ra zetu zinakuwa kubwa kwasababu
tunatumia zaidi mkaa alisema Bi.
Ziha, kwa ktumia majiko ya gesi,
kwanza tutapunguza gharama za
uendeshaji lakini pia tutapunguza
uharibifu wa mazingira aliongeza
katibu wa kikundi.
Nae Afisa Utumishi mwandam-
izi wa TPDC, Flora Salakana kwa
niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa
TPDC aligawa rasmi majiko hayo
kwa kikundi cha kina Mama na ku-
sisitiza wajasiriamali kufanya kazi
kwa vikundi ili kuongeza nguvu yao.
umoja siku zote ni nguvu, hivyo
nawasisitiza kuendelea kufanya kazi
katika vikundi na kutanua wigo wa
biashara zenu iwe ni zaidi ya kupi-
ka alisema Flora.
Misaada kama hii imekuwa iki-
tolewa na TPDC na washiriki wake
ambao ni makampuni ya Kimataifa
ya Mafuta ikiwa ni dhumuni la Seri-
kali kuhakikisha jamii zinazozun-
guka maeneo yenye ugunduzi wa
rasimali za gesi wanafaidi matunda
ya rasilimali hizo kwa kujenga uw-
ezo wa maisha bora ya baadae. Shu-
ghuli za kusaidia jamii ni kipengele
kinachojitegemea katika Mikataba
ya Uzalishaji wa pamoja (Produc-
tion Sharing Agreement-PSA) na
TPDCinasimamia kuhakikisha
makubaliano hayo yanatekelezwa.
TPDC yagawa majiko kwa Mama Lishe
Baadhi ya wakinamama wa kikundi cha Mama Lishe mkoani Mtwara
wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa kutoka TPDC baada ya ku-
kabidhiwa majiko na mitungi ya gesi .
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiongea jambo wakati wa kikao
kati yake na Makamu wa Rais wa Benki ya Kifaransa ya BNP Paribas Corporate & Investment
Banking na ujumbe wake na baadhi ya watendaji wa Wizara. Anayemwangalia wa kwanza
kulia ni Makamu wa Rais Mwandamizi masuala ya fedha Mashariki ya Kati na Afrika, Bw.
Christopher Serivener.

You might also like