You are on page 1of 1

United Nations Association of Tanzania | bringing people closer to the UN

Taarifa kwa Vyombo vya Habari; Asasi Zisizo za Serikali


(AZISE) kuandaa ripoti kivuli
Juni 13, 2014 - Dar es Salaam, Tanzania
Asasi ya Umoja wa Mataifa Tanzania (United Nations
Association of Tanzania) inaongoza mchakato wa asasi za
kiraia 25 inaingia kuandaa ripoti kivuli ya Asasi za Kiraia kwa
ajili ya Mkataba wa Kutokomeza Aina Zote za Unyanyasaji
wa Wanawake (Convention on Elimination of All forms of Discrimination Against Women au
CEDAW).
CEDAW ni mkataba wa kimataifa ambao nchi wanachama wa mkataba wamekubaliana
kutokomeza aina zote za unyanyasaji dhidi ya wanawake. Tanzania ilianza utekelezaji wa
mkataba mwezi September 1985. Makubaliano haya yanahitaji nchi wanachama kuwasilisha
ripoti ya utekelezaji Umoja wa Mataifa kwa vipindi maalumu.
Tanzania mara ya mwisho kuwasilisha ripoti ilikuwa mwaka 2008 na mwaka 2014 itawasilisha
tena. Tanzania kama nchi mwanachama inatakiwa kuwasilisha ripoti yake ya utekekelezaji wa
makubaliano kwa kamati ya CEDAW mwezi September 2014.
Ripoti kivuli ya asasi hii pia itawashilishwa Umoja wa Mataifa sambamba na ripoti ya serikali.
Ripoti inayosimamiwa na UNA Tanzania itajikita katika maeneo maalumu tisa ambayo ni Afya,
Elimu, Ukeketaji, Sheria kandamizi dhidi ya wanawake, Mila kandamizi na shurutishi, Ukatili
dhidi ya wanawake, Uelewa wa Mkataba, na Maana ya unyanyasaji wa wanawake katika sheria
za nchi.
Kwa maelezo zaidi, wasiliana na UNA Tanzania kupitia info@una.or.tz
Imetolewa na:
Nancy Kaizilege
Katibu Mkuu
UNA Tanzania

You might also like