Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali
kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini
Wasiliana nasi Kitengo cha mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofsi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: badra77@yahoo.com Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini Toleo No.19 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Juni 6-12, 2014 Ngonyani Kaimu Mkurugenzi STAMICO uk6 SOMA UK 2 Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia madini Mhe. Stephen Masele Atakayeajiri Watoto migodini kukiona nMasele asisitiza Watoto wakijishughulisha na kazi za madini Soma uk2 2 | MEM News Bulletin NISHATI FIVE PILLARS OF REFORMS TEL 2110490 FAX 2110389 MOB 0732999263 KWA HABARI PIGA SIMU KITENGO CHA MAWASILIANO BODI YA UHARIRI MHARIRI MKUU Badra Masoud MSANIFU Essy Ogunde WAANDISHI Veronica Simba Asteria Muhozya Greyson Mwase Teresia Mhagama Nuru Mwasampeta INCREASE EFFICIENCY QUALITY DELIVERY OF GOODS/SERVICE SATISFICATION OF THE CLIENT SATISFICATION OF BUSINESS PARTNERS SATISFICATION OF SHAREHOLDERS Na Greyson Mwase, Tarime N aibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia ma- dini Stephen Masele amekemea vikali tabia ya wami- liki wa migodi kuajiri watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 kwani inarudisha maende- leo ya watoto hao na jamii kwa ujumla. Waziri Masele ameyasema hayo kwenye ufunguzi wa se- mina iliyoshirikisha wachimbaji wadogo, madiwani, viongozi wa vijiji, wilaya, madiwani pamoja na viongozi wa vyama vya siasa iliyofanyika katika jimbo la Mwibara wilaya ya Bunda mkoani Mara. Masele alisema kuwa kume- kuwepo na tabia ya wamiliki wa migodi, ikiwa ni pamoja na wa- zazi wenye watoto wenye umri chini ya miaka 18 kuruhusu watoto hao kufanya kazi kwenye migodi badala ya kuwahimiza kwenda shule na kupata elimu itakayowasaidia kutoka kwenye giza. Kutokuwapeleka watoto shule na kuwahimiza kushiriki katika shughuli za madini ni kuwaharibu kisaikolojia kwa ku- wakosesha elimu kama haki yao kimsingi, ni kosa kubwa sana. Alisema Waziri Masele Masele alieleza kuwa umefka wakati wa wamiliki wa migodi pamoja na wazazi kuwahimiza watoto kuhudhuria shule ili kuweza kuwa wataalamu wa kutegemewa baadaye katika taifa kama marubani, wahandisi, mawaziri na madaktari. Aliongeza kuwa mkakati wa Serikali ni kuhakikisha kuwa kila sekta inasimamiwa na wata- alamu ambao ni wazawa kwa kuhakikisha inalipa kipaumbele suala la elimu. Inatakiwa pindi migodi mikubwa inapoanzishwa wataal- amu wengi kwenye migodi wawe ni wazawa badala ya kuishia kuwa vibarua na nafasi zao ku- chukuliwa na wataalamu kutoka nje. Alisisitiza Waziri Masele. Aliongeza kuwa ili nchi yeyote iweze kupiga hatua kimaendeleo inahitaji wataalamu katika kada mbalimbali na ku- ongeza kuwa serikali ipo tayari kutoa msaada katika kuzalisha wataalamu hususani katika sekta za nishati na madini. Akielezea mikakati ya serikali katika kuimarisha sekta ya madini Waziri Masele alieleza kuwa serikali kupitia Wizara imeanza kufufua vyama vya uchimbaji madini ikiwa ni pamoja na kuanza kutoa ruzuku kwa wachimbaji wadogo kwani wana mchango mkubwa sana katika pato la taifa. Waziri Masele alieleza kuwa serikali ilianza kutoa ruzuku na itaendelea kutoa ruzuku kwa wachimbaji wadogo watakaot- hibitishwa na chama cha wachimbaji madini kuwa wa- najishughulisha na shughuli za uchimbaji madini lengo likiwa ni kuboresha maisha yao. Alitaja mikakati mingine kuwa ni pamoja na kuende- lea kutoa elimu ya kanuni za uchimbaji bora na salama wa madini kwa kutumia wataalamu wake sehemu zote zenye madini nchini. Akielezea kanuni za uchim- baji salama wa madini Waziri Masele aliwataka wachimbaji wadogo kuachana na matumizi ya zebaki katika uchenjuaji madini kwani zina athari kubwa kiafya na badala yake watumie cyanide. Waziri Masele alisema kuwa matumizi ya zebaki yana athari kubwa kwa mchimbaji madini ikiwa ni pamoja na jamii inayom- zunguka na hata vizazi vijavyo. Alitaja athari za zebaki ni pamoja na magonjwa ya kansa, pamoja na kuwa na kuwa na vizazi vya watoto wenye ulemavu wa mtindio wa ubongo. Unajua athari hizi zinaweza kuonekana hata baaada ya muda mrefu, watu wanaweza kuathirika kwa kula viumbe kama sa- maki vilivyoathiriwa na zebaki iliyotokana na maji yaliyooshea madini hayo kutiririshwa ziwani au kwenye mito. Alisisitiza Waziri Masele. Aliwataka wachimbaji wadogo kufuata kanuni za umi- liki leseni ili kuepuka migogoro inayoweza kujitokeza kati yao na wamiliki wa migodi. Waziri Masele aliongeza kuwa kumiliki ardhi hakutoshi kumpa uhalali mmiliki wa eneo husika kuchimba madini kwani ardhi ni eneo la juu likiwa ni pamoja na mimea na mito na si madini yaliyopo chini yake. Aliwataka wamiliki wa ardhi yenye madini kuomba leseni ya uchimbaji madini ili kuweza kuchimba madini au kuingia ubia na wenye kuhitaji maeneo yao. Ni marufuku kuajiri watoto migodini-Masele Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na mwezeshaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Kungulu Kasongi (hayupo pichani) MEM News Bulletin | 3 MADINI Na Teresia Mhagama S erikali inafanya kila jitihada ili kuhakikisha kuwa mapungufu yaliyojitokeza katika uwekezaji wa sekta ya madini, hayajirudii tena katika sekta ndogo ya gesi asilia. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Elia- kim Maswi wakati akiongea na Waziri wa Nchi katika Jamhuri ya Singapore anayeshughulikia mahusiano ya ndani na nje ya nchi, Bw. Masagos Zulkifi aliyefka Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam ili kuzungumzia fursa za uwekezaji katika gesi asilia na mafuta hasa katika kushauri namna bora ya kutekeleza mradi wa gesi iliyosindikwa (LNG). Katibu Mkuu alimweleza Waziri huyo wa Singapore kuwa serikali hivi sasa inajikita zaidi katika kuhakikisha kuwa miradi mbalimbali ya uwekezaji inayofanyika nchini inawanufaisha wa- nanchi moja kwa moja kuanzia ngazi ya chini ili nao waone matunda ya maliasili ambazo serikali inazisimamia na kuziendeleza. Ili kuhakikisha wananchi wa- nashiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali na wao wafaidike na miradi hii, ni lazima kuwe na uwazi ambao utawafanya washiriki na waelewe nini kinaendelea na wao kujiona ni sehemu ya miradi hiyo.Alisema Katibu Mkuu. Waziri Zulkif ambaye aliambatana na watendaji mbalimbali kutoka baadhi ya makampuni ya serikali na binafsi ameeleza kuwa nchi ya Singapore ina uzoefu na utaalam katika kutoa ushauri wa namna ya kuetekeleza miradi ya gesi iliyosindikwa hasa ujenzi wa nyumba za bei nafuu kwa wananchi wanaopisha miradi ya LNG, ujenzi wa vyuo vya ufundi pamoja na utoaji wa huduma za ulinzi. Ameeleza kuwa ziara hii imefanyika kufuatia ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete aliyeitembelea Singa- Ili kuhakikisha wananchi wanashiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali na wao wafaidike na miradi hii, ni lazima kuwe na uwazi ambao utawafanya washiriki na waelewe nini kinaendelea na wao kujiona ni sehemu ya miradi hiyo < Wadau utafutaji, uzalishaji mafuta, gesi, kutoa maoni Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam W adau wa shu- ghuli za utafut- aji na uzalishaji mafuta, gesi na biashara ya bid- haa za mafuta wanatarajia kutoa maoni kuhusu rasimu ya sera ya Petroli katika warsha itakayowa- kutanisha yenye lengo la kujadili na kupata maoni yao kuhusu sera hiyo, itakayofanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. Akizungumza kuhusu mku- tano huo, Mjiolojia Mwandamizi Wizara ya Nishati na Madini Adam Zuberi ameeleza kuwa, warsha hiyo ni ya pili kufuatia ya kwanza iliyofanyika mwezi Machi, 2014 ambayo ilisam- bazwa kwa wadau muhimu wa sekta hiyo kutoka katika taasisi mbalimbali za serikali na kutoa maoni yaliyowezesha kupatikana kwa rasimu ya sasa ya Sera ya Petroli. Ameongeza kuwa, warsha ya sasa inalenga kuwakutanisha wadau muhimu mbalimbali wanaojishughulisha na shughuli za utafutaji na uzalishaji mafuta, gesi na biashara ya bidhaa za mafuta nchini, ili waweze kupitia kwa pamoja rasimu ya sera hiyo kuweza kupata maoni zaidi yatakayosaidia kuboresha sera hiyo. Zuberi ameeleza kuwa, seri- kali imeona ipo haja ya kuwa na sera mahsusi kwa ajili ya masuala ya petroli nchini kutokana na ugunduzi wa kiasi kikubwa cha gesi katika kina kirefu cha bahari kuu ikiwa ni pamoja na ukuaji wa shughuli za petroli nchini. Pamoja na hayo ameongeza kuwa, sera ya petroli inatarajia kutoa mwelekeo wa namna ambavyo Tanzania na watan- zania watakavyonufaika na sekta ya petroli nchini na namna itakavyochangia katika ukuaji wa kijamii na kiuchumi kwa manufaa ya taifa. Aidha ameogeza kuwa, Serikali ina lenga kuhakikisha kuwa sera hiyo inasaidia kubore- sha maisha ya watanzania kwa miongo mingi kupitia sekta hiyo kwa kuzingatia dira na dhima za sera hiyo. Na Greyson Mwase, Bunda. W achimbaji wadogo wam- etakiwa kujenga utamad- uni wa kupima afya zao mara kwa mara kama njia mojawapo ya kupambana na ugonjwa wa Ukimwi unaoonekana kushambulia hasa wakazi wanaoishi karibu na maeneo ya migodi ya madini Wito huo umetolewa na mhadhiri kutoka ChuoKikuu cha Dar es salaam Dkt. Crispian Kinabo kwenye semina iliyoshirikisha wachimbaji wadogo, wakuu wa vijiji, wakuu wa vyama na madiwani iiliyofanyika huko Mwibara wilayani Bunda, mkoani Mara. Dkt. Kinabo alieleza kuwa takwimu zinaonesha kuwa maeneo ya migodi yanaongoza kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi na kuwataka wachimbaji hao kulinda afya zao pamoja na jamii inayowazunguka. Akizungumia hali ya maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi nchini Dkt. Kinabo alisema kuwa takribani wananchi milioni mbili wanaishi na virusi vya Ukimwi na wananchi 700,000 wamefkia katika kiwango cha kuanza kutumia dawa za kurefusha maisha (ARVs) Dkt. Kinabo aliongeza kuwa kwa ujumla asilimia 5.1 ya watanzania wenye umri kati ya miaka 15 na 49 wanaishi na virusi vya Ukimwi. Aliongeza kuwa ili kukabiliana na ugonjwa wa Ukimwi wachimbaji wadogo wanatakiwa kuwa mfano bora katika jamii inayowazunguka kwa kubadili mienendo yao na kupima afya zao mara kwa mara. Inatakiwa ifke mahali muachane kabisa na michepuko na kubaki njia kuu kwa kuwa waaminifu kwa wenzi wenu. Alisisitiza Dkt. Kinabo. Pimeni afya zenu - Dkt. Kinabo Hatutaki kurudia makosa-Maswi pore mwezi Juni 2013, ziara iliyopele- kea mahusiano mapya ya uendelezaji wa sekta mbalimbali ikiwemo mipango miji, mafunzo ya ufundi, uendelezaji bandari na sekta ya mafuta na gesi asilia. Bw. Zulkifi ameishukuru serikali ya Tanzania kwa ushirikiano alioupata na kueleza kuwa Singapore inahi- taji kushirikiana na Tanzania katika uwekezaji kwa kuwa Tanzania ime- jaliwa kuwa na rasilimali nyingi na Sin- gapore imepiga hatua katika masuala ya kiteknolojia hivyo kwa pamoja nchi hizi zishirikiane kuendeleza rasilimali zilizopo. Naye Katibu Mkuu, Bw. Maswi aliwakaribisha wawekezaji hao na kueleza kuwa serikali bado inakaribisha wawekezaji wa ndani na wa nje ya nchi. Picha ya Juu; Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi (wapili kutoka kushoto) akiongea na Waziri wa Nchi katika Jamhuri ya Singapore anayeshughulikia mahusiano ya ndani na nje ya nchi, Bw. Masagos Zulkifli (wapili kutoka kulia picha ya chini) aliyefika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam 4 | MEM News Bulletin Dodoma B aada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka 2014/2015, Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema sasa ni kazi tu, kwa kuwa watanzania wana matumaini makubwa na Wizara ya Nishati na Madini. Waziri Muhongo aliyasema hayo mara baada ya kukutana na watendaji wa Wizara na Taasisi zake waliokuwepo mjini Dodoma kuhudhuria vikao vya Bunge vilivyokuwa vikijadili makadirio hayo na kuyapitisha. Waziri Muhongo alitumia fursa hiyo kuwaasa wafanyakazi wote wa Wizara na Taasisi zake kuchapa kazi kwa bidii kwa kuwa Wizara ya Nishati na Madini ni moyo wa uchumi kwa kuwa inasimamia sekta muhimu za Nishati na Madini ambazo ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi wa nchi. Profesa Muhongo pia alishukuru uhusiano mzuri wa kazi uliopo kati yake na viongozi wengine wa Wizara pamoja na wafanyakazi wote. Hata hivyo aliwataka wafanyakazi wasio wachapakazi kubadilika na kujituma. Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akinena jambo na Msemaji wa Wizara Bi. Badra Masoud pamoja na Mkurugenzi Mtendaji TANESCO Eng. Felchesmi Mramba. Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi akipongezwa na Wafanyakazi. Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia madini Mhe. Stephen Masele akishukuru kwa ushirikiano mzuri anaopata kutoka kwa viongozi wa wizara pamoja na watumishi. LAZIMA TUFANIKIWE Na Teresia Mhagama, Dodoma Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akipongezwa na wafanyakazi wa Wizara/Taasisi mara baada ya kupitishwa kwa Bajeti ya wizara kwa mwaka 2014/15. MEM News Bulletin | 5 Dodoma Waziri Muhongo ahudhuria kongamano la Nishati Marekani Picha za juu zikimwonyesha Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiwa katika kongamano hilo W aziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ameshiriki kongamano la Umoja wa Mataifa lijulikanalo kama Nishati Endelevu kwa Wote lililofanyika nchini Marekani mnamo tarehe 4-6 Juni 2014. Moja ya mambo yaliyojadiliwa katika kongamano hilo ni pamoja na upatikanaji wa Nishati ya uhakika na salama kwa watu wote ifikapo 2030. Baada ya kongamano hilo Mhe. Waziri pia atakwenda Washington DC kukutana na ``The US Enegy Department pamoja na Wafadhili wa Miradi ya Miradi ya Changamoto za Millenia (MCC) inayoendelea nchini Tanzania . Mtalaamu kutoka Kitengo cha Wachimbaji Wadogo, Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mhandisi Charles Mawala akiwasilisha mada wakati wa semina. Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia madini Mhe. Stephen Masele akifungua mafunzo ya wachimbaji wadogo yaliyofanyika Kibara, mkoani Mara. Semina hiyo ilishirikisha viongozi wa vijiji, vyama pamoja na madiwani lengo likiwa ni kuwapa uelewa wa sheria na kanuni za uchimbaji wa madini. Aliyekaa katikati ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara Mhe. Kangi Lugora. Kushoto ni Kamishna Msaidizi Uendelezaji wa Uchimbaji Mdogo Mhandisi Fredy Mahobe. 6 | MEM News Bulletin Tunalenga kuboresha utendaji na kupunguza hali ya kukosa maelewano katika utekelezaji wa sheria ya madini SHERIA ZA MADINI Masele N aibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia ma- dini, Mhe. Stephen Masele anatarajiwa kufungua mkutano baina ya Wiz- ara, Wakuu wa Mikoa, Wilaya, na Wakurugenzi wa Halmashauri kwa ajili ya kujadili na kujenga uelewa wa pamoja kuhusu utekelezaji wa sheria ya madini. Mkutano huo wa siku moja unafanyika ili kuweka uelewa wa pamoja kuhusu utekelezaji wa sheria hiyo kwa lengo la kuboresha utendaji na kuona namna ya kutatua matatizo yaliyopo katika sekta hiyo. Akizungumza kuhusu mku- tano huo, Kamishna Msaidizi anayeshughulikia wachimbaji wadogo Mhandisi John Nayopa, ameeleza kuwa, serikali inalenga kuweka mazingira ya pamoja katika utekelezaji wa sheria ya madini kutokana na kuwepo malalamiko na mivutano ya namna ya utekelezaji kati yake na serikali za mitaa ili kuwa na sauti moja ambayo itasaidia kuleta matokeo bora na manufaa kwa taifa kupitia sekta ya madini. Tunalenga kuboresha utendaji na kupunguza hali ya kukosa maele- wano katika utekelezaji wa sheria ya madini. Tunataka kujadili jambo hilo ili tuwe na uelewa wa pamoja. Amesisistiza Nayopa. Akieleza zaidi kuhusu mku- tano huo, Kamishna Msaidizi wa Madini, uratibu Mhandisi John Shija, ameeleza kuwa, mkutano huo unatarajia kutoa fursa kwa wizara kuwaelimisha watendaji hao kuhusu majukumu ya wizara hasa juu ya namna ya kusimamia sheria ya madini ikiwa ni pamoja na sekta ndogo ya wachimbaji wadogo. Aidha ameongeza kuwa, mku- tano huo ni muhimu kwa kuwa, unatarajia kujenga na kuimarisha mahusiano na maelewano mazuri baina ya wizara na watendaji hao atika kusimamia shughuli mbalim- bali za miradi ya sekta ya madini jambo ambalo litasaidia kwa kiasi kikubwa kuunganisha shughuli za madini na shughuli nyingine za kiuchumi. Ameongeza kuwa, mada zitaka- zowasilishwa katika mkutano huo zitawasaidia watendaji hao kupata uelewa zaidi kuhusu sekta ya nishati na utekelezaji wa sheria ya madini jambo ambalo litakuwa msaada mkubwa wa utekelezaji wa sekta ya madini kutokana na umuhimu wake kwa maendeleo ya taifa na katika kuwaendeleza wachimbaji wadogo na wadau wote wa sekta hiyo. Wakuu wa Mikoa, Wilaya kujadili Sheria ya Madini Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam Na Issa Mtuwa - Stamico W aziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo amemteua Ka- mishna Msaidizi wa Madini, Mhandisi Edwin Ngonyani (pichani) kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la taifa la Madini (STA- MICO) kuanzia Juni 2, 2014. Ngonyani anachukua nafasi ya Grey Mwakalukwa aliyestaafu kwa mujibu wa sheria. Mara baada ya kuanza kazi katika nafasi hiyo mpya, Ngonyani amehidi kufanya kazi kwa bidii na ufanisi huku akiwataka Wafanyakazi wa STA- MICO kubadilika ili sekta ya madini iweze kuchangia pato la taifa kwa kiasi kikubwa. Hivi sasa tunaingia katika awamu ya kupeleka fedha hazina na si kuchukua fedha hazina. Alisisitiza Ngonyani wakati akizungumza na Wafanyakazi kwa mara ya kwanza. Ngonyani ameeleza kuwa, shirika hilo linatakiwa kuzalisha kwa kiwango cha kutosha na mapato yake kuwasil- ishwa Hazina ili kuchangia katika uchumi wa taifa badala ya kuwa shirika linalokwenda kupiga hodi hazina kuomba fedha za kuliendesha. Hivyo, amewataka kufanya kazi kwa bidii, kuwa wabunifu na kudumisha umoja. Aidha, amemshukuru Waziri wa Nishati na Madini , Profesa Sospeter Muhongo kwa uteuzi huo katika shirika hilo ambalo ni muhimu katika kuchangia uchumi wa taifa na kuhaidi kutomwangusha. Akimkaribisha Kaimu Mkurugen- zi Mtendaji, aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika hilo Gray Mwakalukwa ambaye anastaafu, aliwataka watumishi wa STAMICO kumpa ushirikiano kiongozi huyo ili kuweza kufkia malengo ya shirika hilo kuhakikisha linawavusha watanzania katika hatua nyingine kiuchumi. Aidha, Mwakaluka alitumia fursa hiyo kuwaaga watumishi hao na kuwashukuru kwa ushirikiano walio uonesha katika kipindi chote cha uongozi wake. Kabla ya uteuzi Ngonyani alikuwa ni Kamishna Msaidizi Mkaguzi wa Migodi Wizara ya Nishati na Madini. Aidha, tangu aprili, 2013 alikuwa mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa STAMICO. Mhandisi Ngonyani ateuliwa Kaimu Mkurugenzi STAMICO nAmeahidi kuchapa kazi kwa ufanisi nSTAMICO kuchangia pato la taifa MEM News Bulletin | 7 NISHATI MUHIMU KUZINGATIA UJUMBE WA WAZIRI WIKI HII MARUFUKU MAJADILIANO YA MIKATABA NJE YA NCHI MIKUTANO, MAJADILIANO YA MIKATABA INAYOHUSU RASILIMALI ZETU ZA GESI ASILIA NA MAFUTA NI MARUFUKU KUFANYIKA NJE YA NCHI Na Veronica Simba Z aidi ya Kaya 800 za Watanzania waishio Viji- jini zinatarajiwa kuungan- ishiwa huduma ya umeme katika kipindi cha mwaka mmoja, kuanzia Julai, 2014 kupitia Mradi maalumu wa uunganishaji umeme wa jua (solar energy). Mradi huo wa majaribio una- tokana na jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuhakikisha inawaletea wananchi wake maendeleo, hususan walioko vijijini. Kwa mujibu wa Kamishna Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Nishati Mbadala, Bw. Edward Ishengoma, jumla ya makontena 14 ya umeme jua yanatarajiwa kufungwa katika baadhi ya Vijiji vilivyoko Kongwa-Dodoma, Igalula-Tabora, Katavi na Ruvuma. Kamishna Msaidizi Ishengoma amesema mradi huo utatekelezwa na Kampuni ya Elektro-Merl GmbH kwa gharama ya Euro milioni 5.3 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 13 za Tanzania, kwa mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya Austria kupi- tia benki yake ya UNICREDIT. Akifafanua zaidi, Ishengoma amesema uwezo wa kila Kontena moja ni Kv 13.75 na linaweza kusambaza umeme kwa nyumba/kaya 60. Hata hivyo, amebainisha kwamba mbali na kuunganisha umeme kwe- nye makazi ya watu, Mradi unalenga kuunganisha huduma hiyo kwa waja- siriamali, mashule na vituo vya afya. Vituo vya afya, shule na biashara ndogondogo zinazofanywa na wanan- chi wajasiriamali ni baadhi ya maeneo muhimu yanayohitaji huduma ya umeme; hivyo mbali na kuwapatia wananchi huduma ya umeme majum- bani, tutalenga sehemu hizo muhimu ili kuchangia utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (Mille- nium Development Goals-MDGs) pamoja na mikakati ya maendeleo ya taifa, hususan Mpango wa Maende- leo Makubwa Sasa (Big Results Now-BRN), amesisitiza Kamishna Ishengoma. Amesema, Mradi husika umelenga kuyafkia maeneo ya vijiji, hususan ambavyo havijafkiwa na miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), na kwamba dhamira ya Serikali baada ya Mradi huo wa majaribio ni kusam- baza makontena mengine 600 katika vijiji mbalimbali nchini ili kuwafkia wananchi wengi zaidi. Akielezea maandalizi ya Mradi husika, Kamishna Msaidizi Ishengoma amesema tayari timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini imefanya ziara ya mafunzo katika nchi ambazo zinatekeleza Miradi ya aina hiyo na kuridhishwa na ufanisi wake. Timu ya wataalamu imeridhishwa na ufanisi wa miradi husika katika nchi walizotembe- lea. Taarifa yao imetupa nguvu sisi kuanza utekelezaji wa Mradi huu hivi karibuni kwani maandalizi yote yamekamilika, amesisitiza. Kwa upande wake, mmoja wa wataalamu wa Wizara walioshiriki zi- ara hiyo ya mafunzo, Mhandisi Isdory Fitwangile amesifu ufanisi wa Mradi husika katika nchi walizotembelea na kuongeza kwamba ana uhakika Mradi huo utakuwa wenye mafanikio makubwa hapa nchini. Tofauti na vifaa vya umeme- jua (solar photovoltaic) tulivyozoea kununua hapa nchini, ambavyo kwa kawaida hutumika kuunganisha umeme katika nyumba moja; ma- kontena yatakayotumika katika mradi husika yana uwezo mkubwa kwani kila kontena moja linaweza kutoa hu- duma ya umeme katika kaya/nyumba 60, amefafanua Mhandisi Fitwangile na kuongeza kwamba uunganishwaji wake hutumia distribution line kama zinazotumiwa kuunganisha umeme wa TANESCO (Shirika la Umeme Tanzania.) Nchi ambazo zimetekeleza miradi ya aina hiyo mpaka sasa barani Afrika ni pamoja na Senegal, Mali, Cameroun na Gambia ambayo imeelezwa kuonesha mafanikio makubwa. WATANZANIA VIJIJINI KUNUFAIKA NA MIRADI YA UMEME Moja ya Makontena ya kuunganisha umeme-jua nZaidi ya Kaya 800 kuunganishwa 8 | MEM News Bulletin NISHATI/MADINI Katika ziara hiyo Waziri Masele alikagua miradi ya umeme katika vijiji vya Kibara, Namibu, Kasahunga, Nyamitwebili, Mahyolo, Ka- suguti, Bulamba, Haruzare, Karukekere na Buzimbwe. Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wasiliana nasi kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofsi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: badra77@yahoo.com WIZARA YA NISHATI NA MADINI Serikali yadhamiria kufkisha umeme vijiji vyote nchini Na Greyson Mwase, Bunda W achimbaji wadogo wametakiwa kuendesha shughuli zao za uchimbaji madini kwa kuzingatia malengo waliyojiwekea ili kupiga hatua kubwa kimaendeleo na kujikwamua kiuchumi. Hayo yameelezwa na mtaalamu kutoka Kitengo cha Wachimbaji Wadogo, Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mhandisi Charles Mawala alipokuwa akiwasilisha mada ya ujasiriliamali katika semina ya wachimbaji wadogo, wakuu wa vijiji, viongozi wa vyama na madiwani iiliyofanyika Kibara, wilayani Bunda mkoani Mara. Mhandisi Mawala alisema kuwa ili mchimbaji mdogo aweze kupiga hatua katika shughuli za uchimbaji madini anatakiwa kubaini fursa za mikopo na kuomba kwa kuzingatia masharti yaliyowekwa na kutumia fedha hizo kulingana na malengo aliyojiwekea. Akizungumzia jinsi ya kuweka mipango katika uchimbaji madini Mhandisi Mawala alieleza kuwa wachimbaji wadogo wanatakiwa kutengeneza dhamira ya uchimbaji madini pamoja na kuweka malengo ya muda mfupi na mrefu. Aidha, aliwataka kuhakikisha mipango iliyopangwa inaleta tija katika shughuli za uchimbaji madini. Akizungumzia changamoto katika uombaji wa mikopo kwenye mabenki, Mhandisi Mawala alieleza kuwa biashara nyingi ndogo za uchimbaji madini zimejikita katika sehemu ya chini ya mnyororo wa thamani na hazina mali nyingi inayohitajika na mabenki kama dhamana. Mhandisi Mawala alieleza kuwa mabenki mengi inawawia vigumu kupata taarifa za biashara ndogo kuhusu uwezo wa usimamizi na fursa za uwekezaji za wafanyabiashara na kuongeza kuwa ni gharama sana kwa mabenki kukopesha mikopo midogo ikilinganishwa na mikopo mikubwa. Pamoja na changamoto hizo Mhandisi Mawala aliwataka wachimbaji wadogo kuunda vikundi vya ushirika na kuomba mikopo kwa ajili ya uendeshaji wa uchimbaji madini huku akiwahakikishia kuwa mikopo hiyo inatumika kulingana na malengo waliyojiwekea. Kama mnavyofahamu ujasiriliamali unahitaji kujiamini, na kujipanga kabla ya kuomba mkopo wowote, ni vyema mkahakikisha mmejiwekea malengo ya matumizi ya mikopo mnayoomba na kuhakikisha kuwa matumizi yake yanaendana na malengo mliyojiwekea. Mhandisi Mawala alieleza njia nyingine za kukabiliana na changamoto za upatikanaji wa mikopo kwa wachimbaji wadogo ni pamoja na uhamasishaji wa mitaji ya ubia na uhamasishaji wa ushirikiano katika ununuzi wa malighafi, uzalishaji na uuzaji hasa kwa wachimbaji walio katika eneo moja wanaozalisha madini yanayofanana. Wakati huo huo wachimbaji wadogo waliomba mabenki kulegeza masharti ya dhamana kwa kutumia leseni ya uchimbaji madini au umiliki wa ardhi kama mojawapo ya vielelezo vinavyohitajika wakati wa uombaji wa mikopo. Na Greyson Mwase, Bunda;
S ERIKALI imesema kuwa dhamira yake kubwa ni kuhakikisha vijiji vyote nchini vinapatiwa umeme, ili wananchi waweze kujiletea maendeleo kutokana na nishati hiyo ya umeme. Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia madini Mhe. Stephen Masele, wakati akikagua miradi ya umeme inayotekelezwa katika jimbo la Mwibara, wilay- ani Bunda. Naibu Waziri Masele alisema dhamira ya serikali ni kuhakikisha vijiji vyote hapa nchini vinapata nishati hiyo ya umeme, hali ambayo itaharakisha maendeleo ya wananchi katika maeneo hayo. Katika ziara hiyo Wa- ziri Masele alikagua miradi ya umeme katika vijiji vya Kibara, Namibu, Kasahunga, Nyamit- webili, Mahyolo, Kasuguti, Bulamba, Haruzare, Karukekere na Buzimbwe. Aidha, aliangalia jinsi mradi huo unavyotekelezwa katika jimbo hilo, ambapo mkanda- rasi tayari amekwisha peleka nguzo katika vijiji mbalimbali na kwamba mradi huo kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) unatekelezwa katika vijiji 48 vya jimbo hilo. Alisema kuwa mkandarasi aliyepewa kusambaza umeme katika mkoa wa Mara, amepewa muda wa kumaliza utekelezaji wa mradi huo, ifkapo Juni mwakani. Wachimbaji wadogo watakiwa kuendesha shughuli zao kwa malengo Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini Mhe. Stephen Masele akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachimbaji wadogo mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo. MEM News Bulletin | 9 Imeelezwa kuwa kutokuzingatia kanuni za uchimbaji salama wa madini migodini kunachangia kwa kiasi kikubwa ajali nyingi nchini Hayo yameelezwa na mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Kungulu Kasongi alipokuwa akiwasilisha mada kwenye semina iliyoshirikisha wachimbaji wadogo na viongozi wa serikali za vijiji, wilaya na viongozi wa vyama vya siasa iliyofanyika Kibara, wilayani Bunda mkoani Mara. Mhandisi Kasongi amesema kutokuzingatia kanuni za usalama migodini kumepelekea ajali za mara kwa mara migodini katika kanda ya ziwa kama vile kuangukiwa na vifusi, kugongwa na magari ya vifusi na kukosa hewa. Akielezea athari za ajali migodini kwa wamiliki wa migodi, Mhandisi Kasongi alizitaja athari hizo kuwa ni pamoja na kulipa fidia kwa waathirika, kuharibika kwa mitambo na vifaa, kuharibika kwa miundombinu ya mgodi, kupoteza uzalishaji na kupoteza imani kwa umma na kwa watumishi Mhandisi Kasongi aliendelea kutaja athari za ajali migodini kwa wafanyakazi kuwa ni pamoja na kupoteza kipato, kutumia kipato cha akiba kwa matibabu, kuathirika kiakili na kisaikolojia, kupoteza uwezo wa kufanya kazi kutokufurahia maisha. Akielezea kanuni za afya na usalama migodini Mhandisi Kasongi alieleza kanuni hizo kuwa ni pamoja na kuvaa vifaa maalumu vya kujikinga kama vile kofia ngumu, viatu maalumu, miwani maalumu, gloves; kuweka mgawanyo mzuri wa kazi unaozingatia uwezo wa taaluma; kufanya ukaguzi wa maeneo ya kazi kabla ya kuanza kazi; kufukia mashimo yasiyohitajika na kuzungushia wigo mashimo yanayotumika na kutofanya kazi katika hali ya ulevi na njaa kali au matatizo ya kiafya. Mhandisi Kasongi aliendelea kuelezea kanuni nyingine za usalama migodini ni pamoja na kutofanya kazi katika sehemu zenye vumbi jingi na hewa iliyochanganyika na sumu kwa kuvaa vifaa vya kukinga vumbi na kuvaa vifaa maalumu vya kuzuia makelele kwa sehemu zenye makelele mengi. Aidha, Mhandisi Kasongi aliwataka washiriki hao kutokulundika vifusi vya udongo karibu na mashimo pamoja na kudhibiti kiwango cha hewa chafu au yenye sumu kwa kutumia mashine za kutoa hewa chafu. Pamoja na hayo inashauriwa kutoa taarifa kwa mkaguzi wa migodi juu ya matukio ya hatari au ajali zinazotokea migodini. Alisisitiza Mhandisi Kasongi. Mhandisi Kasongi aliendelea kueleza kuwa kanuni nyingine za kuzingatia katika shughuli za uchimbaji salama wa madini ni pamoja na kutoshirikisha watoto walio chini ya umri wa miaka 18 katika shughuli za uchimbaji madini, vifaa vya huduma ya kwanza kuwekwa mahali pa kazi na kutokufanya kazi ngumu kwa muda mrefu sehemu yenye joto kali. Mhandisi Kasongi aliendela kuelezea kanuni nyingine za usalama migodini ni pamoja na kuepuka kufanya kazi migodini pasipo mwanga kwa kutumia vibatari badala ya tochi maalumu na kutumia njia sahihi kuingia katika mgodi. Si njia sahihi kabisa kuingia au kutoka mgodini bila kutumia ngazi au kamba maalumu. Alisisitiza Mhandisi Kasongi. Akielezea changamoto katika uzingatiaji wa kanuni za usalama migodini Mhandisi Kasongi alieleza kuwa ni pamoja na ukosefu wa vifaa madhubuti na salama vya uchimbaji mdogo wa madini, wafanyakazi migodini kutokuwa na utashi wa kutumia vifaa vya kinga ya mwili, teknolojia duni katika uchimbaji mdogo wa madini, uwezo duni katika kuchunguza matukio na ajali za migodini na usiri katika kutoa taarifa za ajali migodini. Akielezea mikakati ya kupunguza ajali migodini Mhandisi Kasongi alisema ipo haja ya kuendelea kutoa elimu ya uchimbaji salama migodini kupitia semina na vipeperushi, kufanya ukaguzi wa mara kwa mara migodini na wamiliki kuweka mazingira salama ya utendaji kazi migodini na wafanyakazi migodini kuzingatia kanuni za uchimbaji salama. Mhandisi Kasongi aliwataka washiriki kuzingatia usalama kwanza kabla ya kufanya jambo lolote mgodini. Ni imani yangu kuwa iwapo tutazingatia usalama kwanza badala ya faida kwanza kama njia mojawapo ya kuweka usalama kwanza badala ya maslahi basi ajali migodini katika kanda ya Ziwa zitapungua kwa kiwango kikubwa. Alisisitiza Mhandisi Kasongi. Na Greyson Mwase, Bunda Kutokuzingatia kanuni za uchimbaji migodini chanzo cha ajali nyingi Mhandisi Kungulu Kasongi akionesha moja ya vifaa vya kujikinga wakati wa uchimbaji wa madini. 10 | MEM News Bulletin W ananchi wame- aswa kuungana na serikali katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia nishati mbadala kama vile jua, bayogesi, upepo, makaa ya mawe, na gesi asilia ikiwa ni pamoja na kutumia majiko banifu yanayotumia kuni au mkaa mchache ili kupunguza utegemezi kwenye nishati itokan- ayo na maji yaani Hydro power. Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofsi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Mheshimiwa Dkt Binilith Mahenge aliyekuwa Mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa ma- onesho ya Mazingira yaliyofungu- liwa rasmi Juni mosi katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza na kufkia kikomo Juni 5, 2014. Kaulimbiu ya maadhimisho ya siku ya mazingira kimataifa kwa mwaka huu ni Chukua hatua kukabiliana na mabadiliko ya tabi- anchi Ambapo kaulimbiu ya siku hiyo kitaifa ni Tunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi. Kaulimbiu hiyo ilibeba maud- hui yenye lengo la kuelimisha na kuhamasisha wananchi wote vijijini na mijini kuendesha shughuli zao za kiuchumi kwa kuzingatia tarati- bu ambazo hazichangii kuongezeka kwa gesi joto na hazina athari kwa mazingira. Akihojiana na Mwandishi wa Habari hizi Bi Winnifrida Mrema, Afsa Mazingira mwandamizi alisema mwitikio wa wanan- chi ulikuwa mzuri na wananchi wameweza kuelewa madhara na faida wanazoweza kuzipata endapo watafuata taratibu elekezi za uhifa- dhi wa mazingira. Akieleza kuhusu madhara ya mabadiliko ya tabia nchi mabadi- liko ya tabianchi ameyataja kuwa ni pamoja na kukosekana kwa mvua na kuongezeka kwa hali ya ukame yenye athari za moja kwa moja na shughuli za uzalishaji wa umeme unaotokana na uwepo wa maji (Hydro Power). Maonesho hayo ya Mazin- gira yanayofanyika kila mwaka mwezi Juni yamefkia mafanikio makubwa kutokana na wananchi wengi kupata nafasi ya kutembelea mabanda ya maonesho na kujifunza umuhimu wa kuhifadhi mazingira ili waweze kuepukana na mad- hara yatokanayo na uharibifu wa mazingira. Tunza mazingira ukabiliane na mabadiliko ya tabianchi Mtaalamu kotoka kitengo cha Mazingira, Emmanuel shija akimkaribisha mgeni aliyetembelea banda la Wizara katika maadhimisho ya siku ya mazingira jijini Mwanza Baadhi ya wananchi wakiwa katika viwanja vya Furahisha katika maadhimisho ya siku ya mazingira jijini Mwanza Mtaalamu kutoka kitengo cha Mazingira, Winnifrida Mrema akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda la Wizara katika maadhimisho ya siku ya mazingira jijini Mwanza