You are on page 1of 6

ALLY OMARY CHITANDA

MWENYEKITI WA CHADEMA
MKOA WA LINDI
30/11/2013
KATIBU WA CHADEMA
MKOA WA LINDI

YAH; KUJIUZURU UENYEKITI WA MKOA


Somo la hapo juu lahusika.
Napenda kuchukua nafasi hii kukuarifu kuwa kwa hiari yangu bila ya
kushawishiwa na mtu yeyote, nimeamua kujiuzuru nafasi ya Uenyekiti wa
Mkoa tangu leo tarehe 30/11/2013.
Nashukuru sana kwa ushirikiano wako pamoja na Vionmgozi wote wa
Baraza la Uongozi pamoja na Baraza la Mashauriano la Mkoa, lakini pia
niwashukuru Viongozi wote wa Majimbo naWilaya hasa Nachingwea ambao
kwa kiasi kikubwa, wameniwezesha kufika hapa hasa wakati mgumu wa
Ujenzi wa Chama na kugombea Ubunge 2005 na 2010.Matarajio yangu ya
kuweza kukomboa wanyonge kupitia CHADEMA kwa sasa sioni kama
yanaweza kufikika.
Nitabaki kuwa Mwanachama wa kawaida na ninaahidi kuwa Mwanachama
mwaminifu na pale nitakapohitajika nikotayari kusaidiana na Viongozi
kujenga Chama.Nawataki kazi njema na Ujenzi wa Chama.
Ahsante kwa ushirikiano.
..
A.O. CHITANDA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI YA NDUGU ALLY .O. CHITANDA


MWENYEKITI CHADEMA MKOA LINDI, MJUMBE BARAZA KUU TAIFA NA
MKUTANO MKUU. KATIBU OFISI YA KATIBU MKUU WA CHAMA MAKAO
MAKAUU

NDG: WANA HABARI:


Kwanza kabisa ninawashukuru kwa kuitika wito wangu.
Jina langu naitwa ALLY OMARY CHITANDA,nimejiunga CHADEMA mwaka
2003 nikitokea NCCR MAGEUZI.
Nyadhifa nilizowahi kuzishika na kukitumikia Chama ni:Kuanzia mwaka 2004- Mjumbe wa Baraza kuu Taifa nikiwakilisha vijana
Bara niliendelea kuaminiwa na Chama na kupewa kazi nyingine za kukitumikia
Chama, nimewahi kuwa Afisa wa Vijana Makao Makuu, Afisa wa sheria na Haki
za binadamu Makao Makuu, Katibu wa Kamati ya muda ya Baraza la Vijana
Taifa (BAVICHA) kwa sasa ni Mjumbe wa Mkutano Taifa nawakilisha
Nachingwea, Mwenyekiti wa Mkoa wa Lindi tangu tarehe 26/05/2013.Pia ni
Afisa Mwandamizi Ofisi ya Katibu Mkuu Makao makuu Dsm.
vile vile kwa kipindi kirefu sasa nimekuwa nikifanya shuhuli ya uandishi wa
kumbukumbu za sekretarieti ya chama kama KATIBU WA SEKRETARIETI YA
KAMATI KUU.
Hivyo sasa, pamoja na mambo

mengine yapo masuala nyeti na muhimu

ninayoyafahamu na ikibidi kuwaarifu watanzania kwa njia mbali mbali pindi


itakaponihitaji kufanya hivyo.
Ndugu zangu wanahabari, nimewaita ili kupitia nyinyi niwaambie Watanzania
wenzaqngu juu ya hali ya kisiasa ilivyo hasa ndani ya Chama chetu.
Itakumbukwa kuwa tarehe 20-21/11/2013 Kamati kuu ya Chama ilikaa pamoja na
mambo mengine ilifanya maazimio ya kuwavua nafasi za Uongozi ndani ya
Chama alikuwa Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara Mhe. ZITTO KABWE na

Mjumbe wa Kamati kuu wa kuchaguliwa Mhe. Dr. FITILA MKUMBO, kwa kile
kilichoelezwa kuwa ni kwa sababu:(a) Mhe. ZITTO KABWE (Mb) alishiriki kusaidia Wabunge watatu wa
CCM kupita bila kupingwa kenye Majimbo yao ya Uchaguzi 2010.
(b) Kuandaa mkakati waliouita mabadiliko ya Chama 2013. Mkakati
uliolenga kumuwezesha Mhe. Zitto kushinda nafasi ya Uenyekiti wa
Chama Taifa endapo angekubali kugombea.
(c) Mhe. Zitto alishindwa kutimiza majukumu yake ndani ya Chama kwa
kutoshiriki pamoja na Viongozi wenzake kwenye matukio makubwa
yaliyokikumba Chama kama:(i)

Maandamano ya Arusha.

(ii)

Operesheni zilzofanyika Morogoro na Iringa nk.

MAAMUZI MENGINE YA UBORESHAJI WA MAKAO:


Ni kweli kuwa pamoja na mambo mengine Baraza kuu la Chama iliridhia
pendekezo lililetwa kwake na Kamati Kuu kuhusu jambo hili.Na katika utekelezaji
wake Kamati Kuu ya juzi iliridhia kuwa, uteuzi wa Wakurugenzi watano ambao
ni:1. Mkurugenzi wa Oganaizesheni Mhe. Singo Kigaila Benson.
2. Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano ya ndani Mhe. John
Mnyika (Mb).
3. Mkurugenzi wa Fedha na uwekezaji Mhe. Anthony Komu.
4. Mkurugenzi wa Bunge na Halmashuri Mhe. John Mrema.
5. Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Mhe. Wilfred Lwakatale.
Uteuzi huu hauonyeshi sura ya Kitaifa Wakurugenzi wote watano ni
Wakristo kanakwamba CHADEMA hakuna Waislamu wenye uwezo wa
kushika nafasi hizo.

Lakini pia hauzingatii mgawanyo wa kijamii kwa kuwa kati ya kurugenzi


hizo sita wakurugenzi wanne kati yao wanatokea mkoa mmoja wa
kilimanjaro
Na uteuzi huu unakwenda sambamba na kuboresha maslahi yao kwa kuongeza
posho, -kutoka Tshs. 800,000/= za awali na sasa itakuwa ni kuanzia Tshs.
1,500,000-2,500,000/= kwa Mkurugenzi na kutoka Tshs. 6,800,000/= kwa Afisa
Mwandamizi na sasa ni Tshs.1,000,000-1,500,000/=.
Pamoja na kwamba uboreshaji uliridhiwa, lakini katika mpango ulioridhiwa na
Baraza kuu ni pamoja na kulipa Posho kwa Makatibu wa Wilaya na Mikoa.
Hawa ndio watendaji muhimu katika Ujenzi na Uhai wa Taasisi hii lakini,
hawakuangaliwa wala kuguswa badala yake wanatakiwa kujitolea tu kwa hali na
mali.
Mimi kama nilivyotangulia kusema hapo awali, kuwa niko kwa kwa miaka 10
sasa na nimeshiriki kwa kiasi kikubwa katika Ujenzi wa Chama hiki.Sioni sababu
ya kutoharakisha kulipa posho ya Mkatibu wa Wilya na Mikoa pamoja na
watendaji wengine na badala yake tunaharakisha kujilipa posho nono sisi
watendaji wa Makao Makuu, wakati hawa wa ngazi za chini wanamaeneo
makubwa ya Kiutendaji na wanafanya kazi katika mazingira magumu kwa
kujitolea hata Ofisi zao wanajitolea wenyewe.

MAAMUZI YA KAMATI KUU.


Ningependa kuwaambia wanachadema na watanzania kwa ujumla, maamuzi
haya ya kamati kuu ya kuwavua uongozi zitto kabwe na dkt mkumbo ni maamuzi
ya kijuha na yanayowafanya watanzania sasa waangalie mara mbili mbili kama
hawa watu wapo makini na huo ukombozi wanaousema.
Tumekuwa tukiweka mikakati mbali mbali ya ushindi ili chama kishinde, kwa
mfano, kabla hata ya kifo cha aliyekuwa mbunge wa arumeru mashariki, wakati
tu ilipobainika anaugua, chama kiliandaa mkakati wa kushinda ubunge wa jimbo
hilo na uchaguzi uliporudiwa mkakati ule ulitumika na kushinda.

Nikiwa mtendaji wa ofisi ya katibu mkuu, nimeshiriki pamoja na zitto kabwe na


dkt Slaa kupanga mikakati mbali mbali mizuri na mibaya kwa nchi, lakini
hatukuwahi kuitwa wasaliti, wahaini wala sina lolote baya. Ni fedheha leo mimi
kuwa sehemu ya watu wanaomuita zitto kabwe ni msaliti. Siwezi kuendelea na
ujinga huu na sipo tayari tena.
Si dhambi kumuhukumu mtu kwa kuwa anapanga mipango ya kukushinda
kwenye uchaguzi, dawa ya mpinzani wako ni kumkabili.
Naomba nikiri kwamba nikiwa katibu wa sekretarieti tumekuwa tukilazimishwa
mara kadhaa kuwashawishi wajumbe wengi kutowaunga mkono watu wenye
misimamo thabiti ndani ya chama na badala yake tumekuwa tukitumia rasilimali
za chama kuwajenga wajumbe ndio.
Kwa mfano hivi sasa tunapozungumza, wakati katibu mkuu wa chama anasema
mjadala wa zitto kabwe umefungwa rasmi, amewaagiza wakurugenzi wa chama
kuzunguza nchi nzima kusambaza waraka waliouandaa ukimchafua zitto. Hii si
sawa hata kidogo, si vema kutumia rasilimali za chama kuwanufaisha watu
binafsi kutimiza matakwa yao ya kisiasa.
Nafsi yangu haipo tayari kuendelea kuwa sehemu ya upotoshaji dhidi ya
watanzania wenzangu.
Nafsi

yangu

inanikataza

kabisa

kuendelea

kufumbia

macho

maovu

yanayoendelezwa na chama changu.


Nafsi yangu imechoka kuendelea kushuhudia ubaguzi wa kidini na kikabila
unaofanywa wazi wazi na viongozi wa chama changu.
Nafsi yangu imekataa sasa, haipo tayari tena kuwa kuwadi wa kuwahadaa
Watanzania kuyafikia matarajio tunayowapa ambayo kamwe hayafikiki.

Kwa kuwa siamini kwamba kuvuliwa nyadhifa kwa zitto kabwe na dkt kitila
mkumbo ni kwa sababu ya waraka wa ushindi, bali ninaamini kuvuliwa kwao ni
kutokana na hofu ya uchaguzi, ubaguzi wa kikabila na kikanda.
Hivyo basi, nikiwa na akili timamu kabisa, leo tarehe 30.11.2013 nimeamua
kujivua nyadhifa zangu zote nilizokuwa nazo ndani ya chama.
Sioni tena sababu ya kuendelea kuwa MwanaCHADEMA, sioni tena sababu ya
kuwa mwenyekiti wa CHADEMA MKOA WA LINDI, sioni tena sababu ya kuwa
KATIBU WA SEKRETARIETI YA KAMATI KUU.
Kwa kuwa vipaumbele vya chadema ni kukijenga chama mikoa ya kaskazini.
Basi sisi wananchi wa mkoa wa lindi tunawatakia kila la heri, na kwamba
waendelee kukijenga chama chao huko huko waliko.

Nashukuru wote ambao nilifanya nao kazi pamoja katika kutekeleza majukumu
yangu.
Ahsante Sana
A.O. CHITANDA
0753418510
MWENYEKITI CHADEMA MKOA LINDI
MJUMBE BARAZA KUU TAIFA
KATIBU OFISI YA KATIBU MKUU- SEKRETARIETI

You might also like