Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Vipande vya Maisha Vilivyopotea
Vipande vya Maisha Vilivyopotea
Vipande vya Maisha Vilivyopotea
Ebook231 pages2 hours

Vipande vya Maisha Vilivyopotea

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Ilikuwa ni mwaka mmoja tangu nikutane na Bahati na Neema, niliposikia simu ya mezani ya ofisini kwangu ikiita. Nilipoinua mkono wa simu nilishtuka kugundua kwamba sauti ya upande wa pili ilikuwa ni ya Rachel, mke wa marehemu Joshua Halimeshi. Nilishtuka kwani haikuwa kawaida ya Rachel kunipigia simu. Mara ya mwisho kuongea naye ilikuwa takribani miaka mitatu kabla ambapo alikuja ofisini kwangu kuulizia deni la R&J Investments. Na siku hiyo alilipa ada ya miaka kumi mbele, zaidi ya deni walilokuwa wanadaiwa.nalo.
“Ndiyo Rachel, habari za siku nyingi?”
“Nzuri tu. Nina shida ya kuonana na wewe ofisini kwako, sijui naweza kuja lini na wakati gani?” Aliuliza Rachel
“Nipo hadi saa sita na nusu, kisha nitakuwepo tena kuanzia saa nane na robo hadi saa kumi na robo jioni.” Nilimweleza.
“Nakuja kabla ya saa sita”
“Karibu Rachel.”
Rachel alikuja ofisini kwangu kwa kutumia gari lake. Alifika saa tano asubuhi. Katika kipindi cha miaka saba ya ujane wake, hakuna siku niliyomuona Rachel amependeza kama siku hiyo. Nilishitushwa sana na uzuri wa Rachel.
Rachel aliniambia kwamba ana maongezi mazito sana yanayohitaji msaada wa kitaalamu. Na alisisitiza kutokana na unyeti wa maongezi hayo, asingependa tuyaongelee pale ofisini na asingependa tuchukue muda mrefu kabla hatujayaongea. Nilimuomba Rachel kwamba, jioni hiyo niende na binti zangu wawili kwani msaidizi wangu wa kazi za nyumbani alikuwa anaumwa. Rachel alikubali. Rachel alishtuka kusikia nina watoto kwani alichojua yeye ni kwamba mke wangu na mtoto walifariki wakati anajifungua. Pamoja na kumbukumbu hiyo, Rachel hakutaka kunihoji sana. Tulikubaliana kwamba mimi ningeenda nyumbani kwa Rachel saa kumi na mbili na nusu jioni ya siku hiyo.
Rachel alimuarifu msaidizi wa wake wa kazi za nyumbani, Kage, juu ya ugeni huo siku hiyo na kwa hiyo alitayarisha vyote alivyopaswa kutayarisha. Muda ulipofika niliingia nyumbani kwa Rachel nikiwa na wanangu. Rachel alishtuka sana alipowaona Neema na Bahati, alihisi maumivu ya siku mwanaye alipotekwa. Alikuwa kama amechanganyikiwa kwa dakika cada. Kage kwa kujua hilo, alimshika Rachel akampeleka kwenye bustani kisha akatukaribisha ndani. Kage aliporudi aliniambia,
“Samahani kaka, dada Rachel bado ana tatizo akiona watoto wa kike ambao anaamini ni umri ambao angekuwa nao Judy; huwa anashtuka sana”.

LanguageKiswahili
PublisherLorna Dadi
Release dateOct 16, 2018
ISBN9789976892345
Vipande vya Maisha Vilivyopotea
Author

Lorna Dadi

Tanzanian Author, Humanitarian and Mindset Stylist Wife and a Mother of two

Related to Vipande vya Maisha Vilivyopotea

Related ebooks

Reviews for Vipande vya Maisha Vilivyopotea

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Vipande vya Maisha Vilivyopotea - Lorna Dadi

    I

    Baada ya miezi miwili tangu Shantali awasili jijini Birmingham nchini Uingereza kutoka Kigali aligundua kwamba alikuwa mjamzito. Usiku wa Jumapili moja alimwambia mumewe Cosmas habari hizo. Mumewe alifurahi sana. Kesho yake alimwita muuguzi aje ampime ili kujiridhisha. Majibu yalionesha alikuwa na ujauzito wa miezi mitatu na nusu. Cosmas alizidisha mapenzi kwa Shantali, akamuongezea hata wahudumu wa kumsaidia kazi za ndani. Shantali hakuruhusiwa kwenda popote kwani hata wauguzi walikuwa wakija kumhudumia nyumbani. Miezi tisa ilipita na siku ya Jumapili ikawadia. Siku ambayo Shantali alijifungua mtoto wa kike ambaye walimpatia majina mawili; Cosmas alitaka mwanae aitwe Doreen na Shantali alitaka aitwe Neria. Doreen alikuwa mzuri sana wa sura na umbile. Alifanana sana na mama yake kwa umbile na sura kidogo. Cosmas alipenda kumwita mwanae Doreen japo kwenye cheti cha kuzaliwa aliandikwa Neria Cosmas Hakizimana. Jina la Doreen lilizoeleka zaidi nyumbani.

    Doreen alilelewa katika malezi mazuri sana hasa na mama yake. Shantali hakutaka mwanae aathirike na utamaduni, mila na desturi za nchi za Magharibi. Baba yake alipenda kumdekeza sana jambo ambalo lilimuudhi sana Shantali. Lakini kwa kuwa muda mrefu Cosmas alikuwa safarini katika biashara zake, Shantali aliweza kumlea mwanae katika malezi aliyoyapenda yeye.

    Alipofikia umri wa kwenda shule, Doreen alianza shule ya awali huko huko Uingereza. Shuleni alitambulika kwa jina la Neria. Alikuwa akifaulu vizuri sana darasani, walimu na hata wanafunzi wenzake walimpenda kutokana na tabia yake nzuri na uchangamfu. Akiwa nyumbani alipenda sana kumuuliza mama yake habari za nyumbani kwao Rwanda na Afrika kwa ujumla. Shantali alijitahidi sana kumweleza mwanae mambo mazuri yaliyopo nyumbani, hasa katika ukanda wa Afrika Mashariki. Akiwa shuleni Doreen alijikuta akipenda sana kusoma na kufuatilia kwa undani somo la Jiografia kwani alitamani kuijua Afrika. Aligundua kwamba Afrika kuna vitu vingi sana vya asili ambavyo sio rahisi kuvipata katika maeneo mengine duniani. Doreen alitamani sana kurudi Afrika ili ajionee mwenyewe lakini baba yake alimwambia angerudi akifikisha umri wa miaka 18.

    Shantali naye hakuwahi kwenda Rwanda tangu atoroshwe na Cosmas. Ila ndugu zake walienda Uingereza kila mwaka wakati wa sikukuu za Krismasi.

    Miaka ikapita Doreen akafikisha umri wa miaka 18 lakini hakuweza kwenda Afrika kama alivyoahidiwa na baba yake kwani alikuwa tayari ameshaanza masomo ya elimu ya juu. Ikatokea akiwa katika likizo moja baba yake alikuwa na safari ya kibiashara kwenda Rwanda na nchi nyingine za Afrika Mashariki. Doreen alimtaka baba yake atimize ahadi yake ya kwamba angempeleka Rwanda akifikisha umri wa miaka 18. Cosmas alikubali; hivyo alisafiri na mwanae hadi Rwanda. Doreen alifurahi sana. Cosmas alimtembeza mwanae kwa ndugu jamaa na marafiki waliokuwa maeneo ya jirani. Watu wengi walimpenda Doreen kwani alikuwa mcheshi na mdadisi. Siku moja walimtembelea dada yake Cosmas mkubwa aliyekuwa anaitwa Eugenia. Kuna wakati Doreen alikuwa nje. Eugenia alimuuliza Cosmas,

    Cosmas mdogo wangu, mbona huyu mtoto hafanani na wewe kabisa?

    Cosmas akashangaa kidogo lakini akamjibu dada yake kwa upole Doreen anafanana sana na mama yake kwa umbile na tabia; kasoro upole wa mama yake tu ndio hakuchukua

    Labda kwa sababu huyo mama yake sijawahi kumuona; inawezekana unachosema ni sahihi. Alijibu dada yake.

    "Dada, kwa nini umeniuliza swali hilo, kwani umeona nini? Alidadisi Cosmas.

    Damu ya kwetu kali sana, mngefanana hata japo sura au angefanana na mtu mwingine wa familia yetu; lakini simuoni akilandana na yeyote huku kwetu. Yaelekea anafanana sana na mama yake. Alizungumza kwa kudadisi.

    Hata mama yake kwao wana damu kali sana, lakini dada hilo sio tatizo kwani hanifanyi mimi nisiwe baba yake. Cosmas alijibu.

    "Hakuna shida Cosmas, nilikuuliza tu. Si unajua shangazi anavyopenda watoto wake warudi nyumbani kukuza ukoo?

    Cosmas akacheka Dada unataka huu ukoo uwe mkubwa vipi? Siku hizi watu wanaoana mchanganyiko sana hata itafika wakati watoto hawatajua makabila wala asili zao. Hata huko kufanana unakokutafuta hutaweza kukuona tena

    Doreen alirudi ndani. Akaongea kidogo na shangazi yake, japo walikuwa hawaelewani sana. Hii ni kwa kuwa Doreen alijua Kiingereza tu wakati Eugenia alijua Kinyarwanda na Kifaransa tu. Eugenia alimpatia Doreen zawadi ya nguo za Kinyarwanda na nyingine ampelekee mama yake Shantali.

    Baada ya kumaliza shughuli zake nchini Rwanda, Cosmas aliamua kutumia usafiri wa barabara kutoka Rwanda kuelekea Kampala, Uganda kisha Dar es Salaam, Tanzania ili mwanae aweze kuyaona vizuri mazingira ya ukanda wa Afrika Mashariki. Alikodi gari kutoka kwenye kampuni moja ya rafiki yake mjini Kigali, ambayo aliitumia katika hiyo safari. Kule Kigali pamoja na mwanae aliondoka pia na mdogo wake mmoja aliyeitwa Deus. Deus ndiye aliyekuwa akisimamia biashara za Cosmas huku Afrika.

    Ilikuwa ni alfajiri ya Jumapili walipokuwa njiani kutokea Kampala kuelekea Dar es Salaam. Wakiwa maeneo ya Gairo mkoani Dodoma, tairi la mbele la gari lao lilipasuka na kusababisha ajali mbaya sana. Doreen aliumia sana kwa sababu alipoingia kwenye gari kuendelea na safari baada ya kupumzika Dodoma mjini, hakukumbuka kufunga mkanda. Deus na Cosmas hawakuumia sana. Watu walifika na kuwatoa kwenye gari. Cosmas alipopata fahamu na kuona hali ya mwanae ilivyo mbaya alichanganyikiwa sana. Lakini alikumbuka kuwapigia simu wafanyabiashara wenzake waliokuwa jijini Dar es Salaam. Miongoni mwao ni Paul na Michael. Marafiki hao waliwasiliana na wenzao wa Dodoma hivyo haraka sana, majeruhi walikimbizwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

    Doreen alikuwa hajitambui. Ili kuokoa maisha yake, Doreen alihitaji kuongezewa damu haraka. Baba yake alikuwa radhi kumuongezea damu lakini ilipopimwa ilionekana haiendani na ya Doreen. Cosmas akashauri itolewe ya Deus ambaye ni baba yake mdogo, lakini nayo ilionekana haiendani. Basi ikabidi wachukue damu kwenye benki ya damu ya pale hospitali. Kitendo cha damu ya Cosmas na ya Deus kuonekana haziendani na Doreen kilileta maswali mengi kichwani mwa Cosmas. Maneno ya dada yake, Eugenia, yalipita akilini mwake. Lakini akaonelea si vyema kujipa maswali mengi hasa wakati huu ambao hali ya mwanae ni mbaya sana. Siku ya Jumanne, akiwa bado hajitambui, madaktari wa Muhimbili walishauri apelekwe nchini India kwa kuwa tatizo lake lilikuwa kubwa sana. Cosmas alifanya mipango yote ya safari ya India, kisha akakubaliana na mkewe Shantali kwamba aende India ili wakutane huko.

    Doreen alisindikizwa na baba yake na wauguzi wawili. Walipofika India matibabu yalianza. Baada ya wiki moja Doreen alianza kupata nafuu kidogo. Siku ya nane tangu Doreen afike India ndiyo siku ambayo Cosmas aliweza kumuelezea Shantali ajali ilivyotokea na jitihada zote za hospitali ya Muhimbili, hadi jinsi ambavyo damu yake na ya Deus ilivyoshindwa kumsaidia Doreen. Shantali alishituka sana baada ya kusikia kwamba damu zao hazikufaa kumsaidia Doreen. Alihisi jambo la hatari. Akili yake ilimhadharisha achukue hatua ya haraka sana kuthibitisha kama kweli Doreen ni mtoto wa Cosmas kwani alimjua mumewe vizuri sana. Alifahamu kwamba Cosmas hataliacha jambo lile liishe hivi hivi tu hewani; alijua iko siku atataka kujua ni kwa nini damu yake na ya Doreen haziendani. Alijua endapo Doreen hatakuwa mtoto wa damu wa Cosmas na Cosmas akagundua hilo basi hatowaacha waishi, angewaua.

    Kesho yake Shantali alimwambia mumewe kwamba ndevu zake zilikuwa na hali ya uchafu na kwamba ingefaa amsafishe. Cosmas alifurahi sana akamruhusu mkewe amnyoe ndevu. Cosmas alijua alifanyiwa vile kwa mapenzi kama ilivyo kawaida lakini Shantali alikuwa na nia nyingine kabisa safari hii. Lengo la Shantali lilikuwa ni kwenda kufanya kipimo cha vina saba ili kujua kama kweli Doreen alikuwa ni mtoto wa Cosmas kabla Cosmas hajaanza kutafuta ukweli.

    Baada ya Cosmas kuridhishwa na maendeleo ya afya ya Doreen aliyoyapata pale hospitalini India kwa muda wa miezi miwili, walikubaliana Cosmas aendelee na safari zake za kibiashara ilhali wao wakiendelea na matibabu. Baada ya Cosmas kurudi Tanzania, Shantali alimuomba daktari mmoja amsaidie kufanya kipimo cha vina saba ili kutaka kujua kama kweli Doreen ni mtoto wa Cosmas. Alimsihi sana yule daktari amsaidie na asimwambie mtu yeyote majibu ya vipimo hivyo. Daktari alikubali kumsaidia Shantali. Majibu ya vipimo yalionesha kwamba Doreen hakuwa mtoto wa Cosmas. Shantali aliogopa sana; alianza kuwaza namna ya kumuokoa mwanae. Moyoni mwake alifahamu mtoto alikuwa ni wa nani. Alipata wakati mgumu sana kwani hakujua angempataje baba yake Doreen kwani ni miaka mingi sasa ilikuwa imepita. Lakini angemwambiaje Doreen kwamba Cosmas hakuwa baba yake halisi? Alijipa moyo kwamba mwanae angemuelewa.

    Wakati Shantali anahangaika na kuthibitisha kama Doreen ni mtoto halisi wa Cosmas nchini India, Cosmas alikuwa tayari jijini Dar es Salaam akiendelea na shughuli zake kama kawaida. Siku moja Jumapili jioni wakiwa wanastarehe kwenye hotel moja maarufu jijini Dar es Salaam pamoja na wamiliki wenzake wa kampuni ya Across Border Company Limited (ABC Limited), ghafla walivamiwa na polisi. Walikuwa wanajua kwamba biashara zao hazikuwa halali hivyo muda wote walikuwa wamejiandaa kwa lolote. Ujio wa wale polisi mahali pale uliwaashiria kwamba walikuwa katika hatari. Hivyo wakataka kuanza kuondoka mmoja mmoja lakini polisi waliwazuia. Katika purukushani na polisi Cosmas alifanikiwa kukimbia. Alipokuwa akikimbia nje ya hoteli hiyo alikuwa akirushiana risasi na polisi. Alipolikaribia gari lake kuna risasi moja ilimpata kichwani akadondoka. Polisi wakakimbia kumchukua ili wampeleke hospitali. Kwa bahati mbaya Cosmas alifia njiani.

    Habari zilienea usiku huo huo kwa kasi sana kwani wamiliki wa makampuni ya ABC Limited walikuwa wanafahamika na kuheshimika sana ndani na nje ya jiji la Dar es Salaam. Kesho yake asubuhi vyombo vyote vya habari nchini Tanzania viliandika na kutangaza juu ya tukio hilo. Hata vyombo vya habari vya kimataifa navyo vilikutangaza tukio hilo.

    Siku mbili zilipita pasipo mawasiliano vaina ya Shantali na mumewe. Kwa Shantali lilikuwa ni jambo zuri kwani alikuwa bado anajipanga jinsi ya kutatua jambo lililokuwa mbele yake. Doreen hakuelewa mama yake alikuwa anapitia wakati gani. Wakiwa wamekaa chumbani pale hospitali, muuguzi mmoja aliingia na kumuomba Shantali amfuate ofisini kwani kulikuwa na dharura. Shantali alikubali. Alipofika ofisini alimkuta daktari na huyo daktari ambaye alimueleza imetangazwa kwenye kituo cha televisheni cha BBC kwamba wamiliki wa kampuni iitwayo Across Borders Company Limited (ABC Limited) yenye makao yake makuu nchini Tanzania na ofisi katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki wamekamatwa na polisi jijini Dar es Salaamna na mmoja kati yao alifariki katika majibizano ya risasi na polisi. Shantali alishtuka sana. Yule daktari aliendelea kumueleza kwamba, mtu aliyeuawa ni mumewe Cosmas na mwili wake upo katika hospital ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

    Shantali hakuweza kujizuia; alilia sana. Alizidi kuumia alipokuwa akiwaza angemwelezaje Doreen. Kwa upande mwingine alishukuru kwa sababu hakuwa na haja ya kuwaza jinsi ya yeye na Doreen kujificha au kumkimbia Cosmas. Baada ya muda alitulia na kujifuta machozi. Akaamua kupiga simu nyumbani kwao Kigali na kuwaeleza yaliyotokea. Wakakubaliana jinsi ya kwenda Tanzania na kufanya taratibu za kuuchukua mwili wa Cosmas kuupeleka Rwanda kwa ajili ya mazishi. Alipomaliza kufanya mawasiliano hayo alienda kumuona Doreen. Alimkuta ameshuka kitandani anafanya mazoezi ya kutembea. Shantali alifurahi sana.

    Jioni wakiwa wameshakula, Shantali alimwelezea Doreen habari za kifo cha baba yake. Alimjua mwanae, Doreen hakupenda kufichwa ukweli hata kama ulikuwa mbaya kiasi gani. Doreen alipoteza fahamu tena. Shantali alikimbia kuwaita wauguzi, wakaja wakampeleka chumba cha wagonjwa mahututi. Kesho yake mchana Doreen alirudishwa wodini. Shantali hakutaka kuongelea habari za Cosmas tena, lakini Doreen alizianzisha. Shantali alimwelezea mwanae jinsi ilivyotokea. Wakachukua kompyuta mpakato wakaingia kwenye mtandao na kuanza kusoma magazeti ya Tanzania yanayoandikwa kwa lugha ya Kiingereza. Doreen hakuamini aliposoma kwamba baba yake alikuwa ni mtu aliyejihusisha na biashara haramu nyingi sana, ikiwemo ya dawa za kulevya na kuuza silaha. Japo alikuwa amekufa Doreen alijikuta akimchukia sana. Shantali alimsihi sana mwanae amsamehe kwani alikuwa baba mzuri kwake, lakini Doreen alisema hawezi kumpenda kama zamani.

    Doreen alimwambia mama yake kuwa ni lazima waende kumzika Cosmas kwa sababu wao ndio walikuwa familia yake pekee. Shantali alisita kwani alimuona mwanae bado hajapona vizuri. Doreen aling’ang’ania kwenda. Wakaongea na daktari wake ambaye alimruhusu kwenda ila kwa masharti fulani ambayo alitakiwa kuyafuata akiwa huko Rwanda. Shantali akapiga simu Rwanda kuwaarifu kwamba wangehudhuria mazishi na kwamba Cosmas asizikwe hadi mwanae afike. Siku ya safari ikafika. Shantali na Doreen wakaenda Rwanda.

    Siku ya mazishi Doreen alilia sana. Hakuamini kuwa Cosmas amefariki. Alitamani ainuke ili amjibu kama ni kweli alijihusisha na biashara haramu. Lakini haikuwezekana. Walipomaliza kuzika, Shantali na mwanae walikaa Kigali kwa wiki moja, kisha wakarudi India kuendelea na matibabu. Walikaa India mwezi mwingine mmoja kisha wakarudi nchini Uingereza na kuendelea na maisha yao.

    **********

    Aliporudi nchini Uingereza kuendelea na masomo, Doreen alijikuta akipenda sana kuwa karibu na wanafunzi ambao walikuwa wametokea ukanda wa Afrika Mashariki. Alipenda kuwa nao karibu ili ajifunze vitu vingi zaidi kuhusu ukanda huo. Katika siku chache alizokaa Kigali na Kampala akiwa na marehemu Cosmas, Doreen aligundua kwamba Waafrika wengi ni wakarimu lakini pia walikuwa na vitu fulani vya asili ambavyo alitamani sana kuvijua. Miongoni mwa marafiki wengi aliokuwa nao alijikuta akiwa karibu zaidi na binti mmoja wa Kitanzania aliyeitwa Namelo. Namelo alikuwa ni Mmasai. Wakati mwingine alipenda kuvaa mavazi ya kiasili ya Wamasai. Hili lilimvutia sana Doreen. Siku moja Doreen alimwalika Namelo nyumbani kwao kwa ajili ya mapumziko ya mwisho wa wiki, yaani kuanzia Ijumaa jioni hadi Jumatatu asubuhi. Jumapili baada ya kumaliza shughuli ndogondogo za nyumbani wakiwa wamekaa sebuleni, Doreen aliwasha televisheni na kukuta kuna habari ambayo ilikuwa inakaribia mwishoni. Habari hiyo ilihusu sehemu moja inayoitwa Olduvai Gorge iliyopo nchini Tanzania. Doreen alitamani kujua zaidi kuhusu sehemu hiyo. Namelo alimweleza kuwa anaijua sehemu hiyo. Akaanza kumuelezea kinagaubaga kuhusu sehemu hiyo. Alimueleza,.

    "Olduvai Gorge ni eneo la kihistoria linalopatikana katika mkoa wa Arusha nchini Tanzania. Bonde hili lipo kati ya maeneo ya hifadhi ya Ngorongoro na Serengeti ambapo ndipo viumbe wa kale wa jamii ya binadamu walisadikiwa kuishi. Katika eneo hili ndipo lilipogunduliwa fuvu la kichwa la kiumbe wa kale wa jamii hiyo ambaye alisadikiwa kuishi miaka milioni mbili au zaidi iliyopita. Pamoja na mabaki ya mifupa ya tembo, kongoo wenye pembe kubwa na mbuni, mwaka 1959 yaligundulia mabaki ya fuvu la kichwa la Zinjanthropus ambalo lipo katika makumbusho ya Dar es Salaam. Huyo anadhaniwa kuwa mtangulizi wa binadamu wa sasa. Karibu na eneo hilo la Olduvai Gorge, eneo la Laitoli ndipo ambapo ziligunduliwa nyayo za mtu wa kale mnamo mwaka 1972"

    Doreen aliduwaa kusikia maelezo hayo. Alitamani kujua zaidi. Namelo kumbe unajua vitu vingi hivi vya kihistoria; sasa naamini maneno ya mama yangu kwani mara nyingi hupenda kuniambia kwamba kwetu Afrika kuna vitu vingi sana vizuri ambavyo nchi nyingine duniani hakuna.

    Ni kweli, japokuwa mimi sijatembea nchi nyingi duniani lakini kwa kusoma vitabu vingi na elimu niliyopata hadi sasa, bado naamini kwamba Afrika tulipendelewa na Mungu kwa kuwa na vivutio vingi vya asili. Kwa mfano, kwetu Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye vivutio vingi sana vya utalii ambavyo huwezi kuvipata nchi nyingine. Tuna mbuga nyingi za wanyama na nyingine zina wanyama ambao huwezi kuwapa sehemu nyingine yoyote ile duniani. Alimjibu Namelo.

    "Unaweza kunitajia baadhi ya mbuga hizo au zote, kama unazifahamu na vivutio vingine? Aliuliza Doreen.

    Namelo alitabasamu na akaanza kumwelezea; "Mbuga ya wanyama ya Serengeti ndiyo kongwe kuliko zote nchini Tanzania na maarufu duniani kote. Natumaini hata wewe ulishawahi kuisikia. Mbuga hii inapakana na nchi ya Kenya na Ziwa Viktoria kwa upande wa magharibi. Mbuga hii ina nyanda, miti, vichaka, mito

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1